Wednesday

ZANZIBAR WACHUKUA UBINGWA MASHINDANO YA VYUO VIKUU

0 comments

Mashindano ya vyuo vikuu (TUSA) kwa mwaka 2017 yamefikia tamati leo huko mjini Dodoma ambapo Chuo kikuu cha Zanzibar kimefanikiwa kuchukua ubingwa kwa upande wa mpira wa miguu baada ya kuitandika St.John magoli 4-2 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa leo.

Mashindano hayo ambayo yalizinduliwa Disemba 14 na waziri wa habari, sanaa,utamaduni na Michezo Dr. Harriso Mwakyembe yamefikia tamati leo huku mgeni rasmi akiwa Naibu waziri wa habari,Juliana Shonza.


 Naibu waziri,Juliana Shonza
Katika hotuba yake waziri Shonza ametoa wito kwa vyuo nchini kutoa ushirikiano kwa wanafunzi wao katika kushiriki michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.