Wednesday

MTIBWA WAPATA KOCHA MPYA

0 comments

  
Klabu ya soka ya Mwadui ‘wachimba Almas’ yenye maskani yake Maganzo mkoani Shinyanga imemtangaza kocha Ali Bizimungu kutoka nchini Rwanda kuwa kocha wao mkuu kusaidiana na kocha Jumanne Ntambi aliyekuwapo tangu kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu.
Akithibitisha taarifa hizo Ramadhan Kilao amesema mabadiliko hayo ya benchi la ufundi yameenda sambasamba na kuongeza wachezaji wawili ambao ni aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Athuman Rajab pamoja na John Kwito anayetokea nchini Burundi.
-Kocha Bizumungu ana leseni A, Jumanne Ntambi yeye ana leseni B hivyo tumemuongeza huyo ili asaidiane na mwenzake kuweza kuisaidia Mwadui, lakini wachezaji wote ambao tumewaongeza ngi wachezaji viungo hilo ndilo lilikuwa pendekezo la mwalimu kwenye ripoti,” Kilao alisema.

Kocha Bizimungu ameshawahi kuzifundisha timu za Bugesera FC, Kiyovu FC, lakini pia aliwahi kuwa kwenye benchi la ufundi la timu ya Rayon Sports ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Rwanda.

Malengo yetu
Kilao ameongeza kuwa matarajio yao msimu huu ni kumaliza katika nafasi za juu, angalau ya sita ama ya tano hivyo mabadiliko hayo ana aamini yataisaidia timu hiyo kufikia malengo yao ambayo wamejiwekea msimu huu.
Mwadui inakibarua kigumu Disemba 23 pale watakapoikaribisha Pepsi FC ya jijini Arusha katika mchezo wa kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup, wakati wakisubiri kucheza na Ruvu Shooting Januari mosi, 2018 katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania Bara.