Wednesday

USAJILI SIMBA: Simba yasisitiza kuwa Mavugo bado ni mchezaji wao, Kwasi mambo bado

0 comments


Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na klabu hiyo ni kuwa kwenye usajili wa dirisha dogo Simba imewaongeza katika kikosi Dayo Antonio wa Ferroviario de Beirra ya Msumbiji na Mghana Asante Kwasi, hivyo kufikisha idadi ya wachezaji saba.
Kwa maana hiyo klabu hiyo ilipaswa kuwaachia wachezaji wawili ambao maoni ya wengi yaliangukia kwa Laudit Mavugo pamoja na Method Mwanjali ambaye tayari ameshaachana na timu hiyo kongwe barani Afrika.
-Hatujasema tumemuacha Mavugo, bado ni mchezaji wetu na ataendelea kuwepo kwenye kikosi chetu, mashabiki wetu wawe na subira siku si nyingi tutatoa ripoti rasmi ya usajili, lakini Mavugo bado tupo naye," alisema bosi huyo wa Simba.
Kwa upande wa Mavugo.
Awali mavugo akizungumza na mtandao huu masshele blog , alisema kuna tatizo moja kwa kuwa hajaachiwa rasmi na Simba ambao walitaka kumtoa kwa mkopo wa miezi sita kwenda AFC Leopards ya Kenya, wakati yeye akisema ingekuwa  bora kama Simba wangemuachia huru asajiliwe na AFC leopards ili kumpatia nafasi kujijenga kisoka.
-Simba hawajaniachia bado wamesema wanaweza wakanitoa kwa mkopo wa miezi sita AFC lakini Mimi ningependa waniachie huru ili niweze kujipanga  japo bado tupo kwenye mazungumzo nao Nataraji tutaongea zaidi nikirejea Dar es Salaam", ameongeza Mavugo.
Ingawa hatma ya Mavugo kubaki Simba kama uongozi unavyosisitiza itategemea na maelewano ya Simba na Lipuli kuhusu usajili wa Kwasi ambaye kama atafanikiwa kujiunga na mabingwa hao wa Kombe la FA basi atafikisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni na Mavugo hatakuwa na nafasi zaidi ya kuondoka Simba.