KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI
MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI
I.
Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni
Lengo
kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha
ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza 3.Kusoma 4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni wa lugha
ile
Malengo ya jumla ya kufundisha ili ni
pamoja na:-
1)
Kumwezesha
mwanafunzi ili aweze kumudu lugha.
2)
Kumwezesha
mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha husika
LUGHA YA KWANZA
Stern (1983)
anasema kwamba “lugha ya kwanza lugha ambayo mtoto hupata kutoka kwa mama yake
mzazi angali mchanga.
LUGHA YA PILI
Stern (1983)
anasema kwamba “ lugha ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu aliipata alipoanza
kukua na kupata lugha. Hii ni lugha ya kujifunza,kwa maana ya kwamba mtu huyu
huwa tayari ana lugha nyingine.mfano. hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili
kwa watu wengi
LUGHA YA KIGENI
Ni ile lugha
ambayo unajifunza na kuitumia lakini wazungumzaji wake wako nje ya nchi au
mbali na jamii anapokaa mwanafunzi huyo. Mfn lugha ya kiingereza ni lugha ya
kigeni hapa Tanzania
MALENGO YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA
UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KIGENI
Mara nyingi hii
hutegemea taaasisi yenyewe lakini kuna malengo ambayo ni ya jumla:
1)
Kutaka
kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika
2)
Kujiandaa
kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali
3)
Kwa
ajili ya kufanya biashara
4)
Kukidhi
vigezo vya masomo
5)
Kufanya
utafiti katika taaluma husika
6)
Ili
kupata ajira nchi za ng’ambo
KITU GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA?
Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi
sarufi za lugha hiyo kwanza, utamfundisha ikibidi lakini isiwe kipaumbele chako
W Anza na salamu
za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika ni kitu cha muhimu sana, hivyo
fundisha salamu,maana lengo ni kwamba huyo mtu aweze kuwasiliana.
MALENGO YA UJUMLA YA UFUNDISHAJI LUGHA
YA KISWAHILI KWA WAGENI
a)
Ili mwanafunzi
wa Kiswahili ajue mambo yafuatayo:
i.
Aweze
kumudu lugha ya Kiswahili
ii.
Aweze
kuwasiliana na watumiaji wa lugha ya Kiswahili
iii.
Ili
wanafunzi waweze kung’amua mambo yafuatayo:- Namna ya kusema jambo gani? Mfano
anataka kwenda chooni Asemee wapi? Kwa
nini aseme? Kwa nani aseme? Mazingira gani aseme?
iv.
Ili
kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kujifunza lugha ya Kiswahili. Wanafunzi wafanye
kwa vitendo ili waweze kujichukulia misamiati ya kutosha
v.
Wanafunzi
wang’amue umuhimu wa lugha wanayojifunza
b)
ili wanafunzi
waweze kutimiza malengo haya, mwalimu ni lazima
wape wanafunzi:
kuchunguza®kugundua®kutalii kuhusu lugha ya Kiswahili
c)
wape
uwezo wa kukuza lugha ya Kiswahili kila siku aweze kuongeza msamiati kwa kusoma
vitabu mbalimbali vya hadithi
d)
wape
nafasi kutumia mbinu mbalimbali lugha ili kukuza uelewa wao
e)
wape
uwezo wa kukuza fikra zao na kudadisi
f)
wasaidie
kufanya utumbuizi wa vipengele vya mfumo na utamaduni wa lugha ya Kiswahili
NADHARIA
KUU ZA UJIFUNZAJI LUGHA
Kuna mambo mawili ambayo waalimu
tarajili wanapaswa kujua
1)
mbinu za
kujifunza lugha ya pili ni nyingi
kama ilivyo waalimu wengi
2)
manzingira
halishi wakati wa ujifunzaji. Rogers
(2001) anasema kwamba “ wakati wa ufundishaji wa lugha ya kigeni hutumia
mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wafikie malengo yao”
kuna nadharia
kuu nne (4)za ujifunzaji lugha:
1)
NADHARIA YA UHULKA
ü Mwasisi wake ni Noamy Chomsky (1957)
ü Wazo kuu lake ni kwamba: binadamu huzaliwa akiwa na
uwezo lugha. Yaani kwenye ubongo wake
ana mfumo ambao huzaliwa nao kwa ajili ya kujifunza lugha. Ana kifaa
kinachoitwa LAD (Kifaa cha upataji lugha)
ü Naye Brown (2000) aliunga mkono mawazo haya. Mwingine aliyeunga
mkono niEllis (1997)
walikuwa na hoja kwamba kuna kipindi mtu
akifikia umri Fulani hawezi kupata lugha sawasawa na wazawa wa lugha husika.
Umri huo ni kuanzia 0-miezi 18. Kwa mujibu wa wataalamu hawa mazingira hayana
msaada wowote katika ujifunzaji lugha.
2)
NADHARIA YA UTABIA (BEHAVIORISM)
ü Mwasisi wa nadharia hii ni J.B Watson. Wengine wanaoshadidia
nadharia hii ni Leornald Bloomfied, O.N Mowrer, B.F Skinner na A.W Staats
ü Edward Thorndike (1935) alikuwa wa kwanza kabisa kutafiti zaidi.Kwa
mujibu wa wanatabia ujifunzaji wa lugha ni mwigokwa
maana ya kwamba huiga kile kinachosemwa na watu wanaomzunguka
ü Aliyetafiti zaidi katika nadharia ya ujifunzaji ni BurrhusFrederic(B.F) skinner,
Huyu alikubali ni mwigo lakini akaongeza kuwa ni uimarikaji wa tabia, hivyo mtoto mdogo hazaliwi na lugha bali
huichota kutoka kwa wazazi wake
ü Wilga
Rivers (1968)anasema mtoto
hujifunza kupitia kujaribu na kukosea “trial and error’ huendelea kufanya hivyo
mpaka anapofikia matamshi ya jamii nzima.
ü Nadharia hii inayapa mazingira nafasi kubwa katika
ujifunzaji lugha
ü Je mtu akitengwa na jamii anaweza kuwa na lugha?
3)
NADHARIA YA UTAMBUZI
ü Nadharia hii iliasisiwa na Jean Piaget (1954)
ü Alidai kuwa binadamu anapozaliwa kuna kipindi maalum cha kupata lugha
ü Alidai kuwa kujifunza lugha ni sehemu ya makuzi ya
binadamu, kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyozidi kupata lugha
ü Alidai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa.
ü Arth(2003)anadai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya
kuzaliwa,kuanzia 0-miezi 18
ü Nadharia hii haipingani na umuhimu wa mazingira
katika ujifunzaji lugha
4)
NADHARIA YA UUMBAJI
ü Nadharia hii iliasisiwa na Jerome Brunner
ü Wazo kuu la nadharia hii inasisitiza nafasi ya mama
katika upataji lugha ya kwanza
ü Mtoto hutengeneza lugha kutegemeana na mawasiliano
ambayo mama yake anayatumia
ü Alidai, ili mtoto aweze kupata lugha ni lazima mambo
yafuatayo yatimizwe
·
Muktadha
·
Tajiriba
(experience)
·
Upangilifu
(organization)
·
Kujenga
mazingira ya upekuzi (udadisi_
ü Hukaza zaidi kuhusu mazingira katika ujifunzaji
lugha
ü Mwalimu awatie moyo wanafunzi kugundua mfumo wa
lugha wao wenyewe
ü Mwalimu na wanafunzi wanapaswa kutumia sana
majadiliano
NJIA ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA KISWAHILI
Njia za
ufundishaji Kiswahili ni nyingi kama na waalimu nao walivyo wengi, lakini njia
hizi itatengemea hali ya wanafunzi, hata hivyo njia zifutazo zinapendekezwa
zitumike.
1.
Njia
ya majadiliano-njia
hii haifai kwa mwanafunzi ambaye ndio kwa mara ya kwanza anasikia Kiswahili.
Lakini ni njia nzuri kwa mwanafunzi ambaye amewahi kusikia habari za Kiswahili
2.
Njia
ya mahojiano.Mfano
mwalimu aandae maswali, awaambie wanafunzi wajipe vyeo mfano mmoja anakuwa
daktari mwingine anakuwa mgonjwa n.k
3.
Mchezo
wa maswali.Kwa
mfano. Kama wewe ungekuwa rais wa marekani ungefanyaje kuhakikisha unakomesha
ugaidi duniani? Watajibu na kujipatia msamiati kibao
4.
Njia
ya uigizaji-mwli
awape wanafunzi mwongozo wa maigizo
5.
Njia
ya maswali ya papo kwa papo(ana kwa ana) mfano: mimi ni Seni, wewe ni nani?
6.
Njia
ya uwandani.
Mfano ukitaka kuwafundisha misamiati ya sokoi wapeleke sokoni.
7.
Njia
ya kutumia mazingira mbalimbali. Mfano kama mwalimu anataka
kuwafundisha michezo wapeleke uwanja wa mpira
8.
Njia
ya usomaji.Mfano
kusoma pande nne za dunia,kuwapa matini mbalimbali wanafunzi
9.
Njia
ya majadiliano funge.Yaani
wanafunzi wanajadili vitu ambavyo vimewekewa mipaka
Angalizo:uteuzi wa njia ipi itumike
itategemea aina ya wanafunzi na kazi zao!
HULKA/TABIA YA UANAFUNZI KUJIFUNZA LUGHA
Wanafunzi
hutofautiana kulingana na hulka zao, mwalimu anahitaji kuangalia mielekeo
ya wanafunzi wake. Baadhi ya tabia zao
ni kama vile: ucheshi, hasira, aibu, hasira za kutojua, hapendi kusahihishwa,
mkimya nk
ATHARI ZA KIJAMII KUHUSU LUGHA/WANALUGHA
Kila jamii ina
mtazamo wake kuhusu ujifunzaji lugha, mtazamo hasi ndio ambao huathiri
ujifunzaji lugha na kupelekea kutopata motisha wa kujifunza lugha. Baadhi ya
mambo yanayoathiri ni kama vile
i.
Nia
au lengo la kujifunza lugha hiyo
ii.
Jinsia;
inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha kuliko wanaume
iii.
Umri;
umri mdogo ni rahisi kupata lugha kuliko umri mdogo
iv.
Mazingira;
mazingira mazuri yanavutia mwanafunzi kujifunza haraka
v.
Umilisi
wa lugha kama akiwa na umilisi mdogo
Malengo ya
mwalimu ni kuhakikisha anafanya mambo yafuatayo:
i.
Kuwatia
motisha wa kujifunza lugha
ii.
Kumsaidia
kuondokana na hasira
iii.
Kuondoa
dhana potofu ya ujifunzaji lugha. Mf. Kuna wanaoamini kwamba Kiswahili ni lugha
ya kiislamu
iv.
Kuondoa
utata katika vipengele vya kisarufi
v.
Kuwaelezea
aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika
Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara
ni muhimu sana kujua ishara zinazotumika katika jamii. Hivyo mwalimu anapaswa
awaeleze mambo yafuatayo;
i.
Baadhi
ya utamaduni huangalia usoni, tabasamu na kujiamini
ii.
Matumizi
ya mkono wa kushoto au wa kulia
iii.
Kuonyesha
vidole-jamii zingine haziruhusu kabisa
iv.
Namna
ya kusimama na kuelezea jambo
Ili kutimiza hayo yote mwalimu
lazima awe na sifa zifuatazo:
i.
Awe
muwasilishaji mzuri
ii.
Awe
na mpangilio mzuri
iii.
Awe
mstahimilivu
iv.
Awe
na ujuzi wa kufundisha
v.
Awe
na uhusiano mzuri na wanafunzi
vi.
Awe
na maarifa ya somo
SIFA
ZA MJIFUNZAJI LUGHA
a)
Awe na utayari wa kujifunza lugha ya Kiswahili bila
kulazimishwa
b)
Afanye mazoezi ya kuitumia lugha hiyo
c)
Atumie akili kupambanua dhana mbalimbali ili
kugundua mambo ambayo jamii Fulani inayafanya
d)
Awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo
e)
Awe na ratiba ya kujifuza
f)
Aweze kulinganua na kulinganisha lugha anayojifunza
g)
Awe na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii
husika
h)
Awe mtendaji
i)
Azingatie ubora ili aweze kujifunza zaidi
MOTISHA
Ni tabia au msukumo
katika kutimiza malengo fulani. TUKI (2004) wanadai kuwa motisha ni kitu kama
fedha inayotolewa ili kumtia mtu hamasa kujifunza jambo.
Hata hivyo, si
lazima umpe kitu bali unamtia moyo mwanafunzi na kumsaidia. Mwalimu anapaswa
kutumia motisha chanya sio hasi.Mfn hutakiwi kuchapa fimbo
Brown (1994) anasema
kuwa motisha;
a)
Ni
kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo unalotaka kufikia
b)
Jitihada
atumiazo mtu kufikia malengo hayo
SKINNER
&WATTSON-hawa
wanaangalia zawadi na uhimizaji kwa wanafunzi pamoja na adhabu ili kufifisha na
kujenga hali fulani
AINA
ZA MOTISHA
1.
Mwamko
wa mjifunzaji mwanyewe
2.
Mazingira
mazuri ya kufundishia Kiswahili mfano, darasa, nje n.k
3.
Jamii
inayomzunguka ni motisha pia
4.
Mwalimu
anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi
5.
Zana/vifaa
vya kujifunzia pia ni motisha
MOTISHA IPO KATIKA MAKUNDI MIWILI
1.
Motisha wa
ndani-
ü Haitegemei vitu
vya nje ya yenyewe
ü Hiki ni kile
kinachoonekana kwa mjifunzaji lugha mwenyewe
ü Hii haibadiliki
kulingana na muktadha wowote ule
2.
Motisha wa nje
ü Ni aina ya
motisha ambayo mwanafunzi hutegema kupewa, kupata, kusikia au kuona
ü Hivi vitamsaidia
katika kujifunza lugha
Mwalimu wasaidie wanafunzi kutumia lugha
kulingana na muktadha. Hapa kuna mambo ya kuzingatia:-
a)
Akili ya mwanafunzi: lazima utambue tofauti zao
katika akili zao ili kujifunza lugha
b)
Kipaji chao-kuna wengine wana vipaji vya kujifunza
lugha
c)
Umri-watu wazima huchelewa kujifunza lugha
d)
Jinsia-inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha
haraka kuliko wanaume
UFUNDISHAJI
LUGHA KIMAWASILIANO
ü Ni muhimu
kuhakikisha kwamba katika kujifunza lugha ufundishaji uwe wa mawasiliano
ü Ni mbinu ya
kufundisha lugha ngeni na lugha ya pili
ü Husisitiza
mwingiliano maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha
KAZI ZA LUGHA
ü Van (1975)anasema kuwa
kazi ya lugha ni:
a)
Kutoa habari
·
Kusimulia
·
Kuuliza
·
Kutoa
taarifa
b)
Kutafuta
taarifa za kitaaluma
c)
Kuelezea
mihemuko na misisimko. Mfno mapenzi, misisimko
d)
Kuelezea
masuala ya uadilifu.mfn kuomba msamaha, ibada etc
e)
Kwenye
mambo ya ushirikiano. Mfn kuamkia watu, kujitambulisha nk
Angalizo: hata kama
mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza lugha hiyo ni lazima umfundishe
umuhimu wa lugha hiyo kulingana na muktadha
MASHARTI
YA KUZINGATIA
a)
Azingatie
majukumu ya kijamii mfn ataanzaje kuzungumza na mtu asiyemjua? Watu wengine ni
wenye mamlaka Fulani, hivyo kuna namna ya kuzungumza nao
b)
Majukumu
ya kisaikolojia-mfano asipendelee upande wowote mfn CHADEMA CUF na CCM
c)
Mazingira
ya lugha ilipo. Je ni lugha ya taifa? Watu wanaokuzunguka wanatumiaje?
Angalizo: lugha sio
sarufi tu au fonolojia bali ni chombo cha mawasiliano, hivyo inahitaji
kufundishwa kimawasiliano zaidi
MUKTADHA WA
UFUNDISHAJI LUGHA
ü Haya ni
mazingira halisi ambapo tukio la ufundishaji lugha hufanyika kwa kuzingatia
wadau wakuu watatu
a)
Mwanafunzi
b)
Mwalimu
c)
Jamii
ü Pamoja na
motisha ufundishaji uzingatie sana mambo yafuatayo:
·
Utoaji
wa kazi na mazoezi mengi
·
Tumia
lugha katika mazingira halisi na yanayostahili ukilenga kwenye stadi nne za
lugha
·
Matumizi
ya lugha kwa kuzingatia muktadha
·
Utumizi
wa mazingira halisi ya darasa.mfn picha, katuni. Nk
·
Himiza
ushirikiano miongoni mwa wanafunzi baina yao na baina yako mwalimu
·
Tumia
mbinu zaidi ya moja. Mfn vikundi, majibizano nk (rejea mbinu)
·
Fafanua
kwa uangalifu masuala ya kisarufi
·
Ajue
maono ya mwanafunzi. Mfn huzuni, ucheshi nk
·
Kuunda
mazingira ya utani darasani
UFUNDISHAJI
WA DARASA MSETO
ü TUKI (2013)
Mseto ni hali ya kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali kutengeneza kitu
fulani
ü Hapa ni
mchanganyiko wa darasa lenye wanafunzi wanaotoka sehemu mbalimbali na wenye
umri tofauti, malengo tofauti nk
ü Hivyo mwalimu
inakubidi utofautishe sana katika ufundishaji wako na uwe makini ili usije
ukawakwaza wanafunzi wengine
NAMNA YA
UFUNDISHAJI DARASA MSETO
a)
Lazima mwalimu uwe na maarifa ya wanajamii mfn
utamaduni wao. Kama ni wazungu, wachina nk jua utamaduni wao
b)
Uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kama ni
Kiswahili basi pendelea kutumia Kiswahili ili usiwakwaze sana. Hata hivyo
lazima wawe na lugha ambayo wewe unaijua
c)
Tumia vitendo halisi, ishara nk
d)
Arika wageni mbalimbali waje waeleze kuhusu lugha na
mazingira
e)
Puuza(ignore) malengo ya wanafunzi
f)
Ufundishaji wa masuala ya utamaduni lazima
ufungamane na muktadha husika
SIFA
ZA MPATAJI LUGHA
Mpataji lugha ni
lazima awe na sifa kuu mbili tu:
1.
Umilisi wa
kiisimu
ü Ni uwezo alio
nao mjifunzaji lugha ambao unamwezesha kutofautisha viambo, miundo tofauti ya
lugha na msamiati wa lugha
ü pia kuweza
kutamka lugha ile.
2.
Umilisi wa
kiisimujamii
ü Ni umilisi ambao
mtumiaji wa lugha hupata lugha inayomwezesha
kujifunza lugha na kuzingatia muktadha
NADHARIA
/MBINU /MIKABALA ZA KUJIFUNZA LUGHA YA KIGENI
ü Nadharia ni
mkondo wa mawazo unaotumika kuelezea jambo
ü Mtesigwa(2009)
anasema “ nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo au vitendo vinavyohusisha
uchunguzi, mpangilio na uchanganuzi wa matukio katika kukabili suala fulani kisayansi
®kuna mambo mawili ambayo lazima
tujikumbushe:
a)
Njia
za ufundishaji lugha ya kigeni ni nyingi kama waalimu walivyo wengi
b)
Kumbuka
hali ya darasa. Tumia njia mbinu zaidi ya moja darasani, usitumie njia moja tu.
ü Rogers&Richards
(2001)wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda kufundisha tunahitaji kujiuliza
maswali yafuatayo:-
a)
Malengo
ya ufundishaji lugha lengwa(LL) ni yapi? Mfano labda lengo lao linaweza kuwa
wanataka kuzungumza tu.
b)
Upi
ni msingi asili wa lugha lengwa na unaathiri vipi njia za kufundisha. Mfn kaida
za lugha ya Kiswahili ni zipi?
c)
Ni
misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?
d)
Ni
misingi ipi ya upangiliaji wa mada. Mfano kwa kuzingatia suala la utamaduni,
mfano salamu nk
e)
Je
lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza lugha? Mfano miundo
ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?
f)
Je
wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha hiyo?
g)
Je
ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya pili (kigeni)?
NADHARIA ZA KUJIFUNZA lugha
1.
Mbinu
ya tafsiri sauti
2.
Mbinu
ya moja kwa moja(direct method
3.
Mbinu
ya usomaji(reading approach method)
4.
Kusikia
na kusimulia (audiolingual method)
5.
Kushirikisha
jamii (community language learning method)
6.
Mbinu
ya ukimya (silence method)
7.
Mbinu
ya mawasiliano (communicative language approach)
8.
Mbinu
ya mwitiko jumuishi(total physical response)
9.
Mbinu
ya utambuzi (communitive code method)
10.
Mbinu
ya upendekezi (suggestopidia method)
1.
Mbinu ya
tafsiri sarufi
ü wakati mwingine
hujulikana kama mbinu ya kimapokeo. Huu ni mkabala ambao ufundishaji wa lugha
ya kigeni umejiegemeza katika sarufi ya lugha ya Kiratini. Iliasisiwa/anzishwa
na Meidinger (1783) na Ploetz (1849) wakati ule iliaminika kwamba lugha ya
kiratini ndiyo lugha pekee.
ü Nafasi ya lugha
mama ilipuuzwa kwa kiasi kikubwa na ilijikita katika sarufi ya Kiratini, na
hivyo mwalimu alipaswa kujikita katika kufundisha sarufi ya Kiratini na
vipengele vingine vilipuuzwa
ü Huu ulikuwa ni
mkabala elekezi-yaani unawaelekeza watu namna ya kutumia lugha na sivyo
wanajamii wanavyotumia lugha hiyo
2.
Mbinu ya moja
kwa moja(direct method)
ü
Iliasisiwa
na Gouin(1880)
ü
Nadharia
hii inazingatia uzungumzaji wa lugha husika
ü
Mbinu
zilizopaswa kufundishia ni zile zilizohamasisha wanafunzi kuzungumza. Mfn mbinu
ya majadiliano,uigizaji,maswali katika vikundi
ü
Masomo
yalianza kwa hadithi fupi halafu wanafunzi wanauliza maswali kuhusu hadithi
waliyosimuliwa na mwalimu aliwaambia watoe maoni yao kuhusu hadithi hiyo.
ü
Matumizi
ya vielelezo vilitumika zaidi. Mfano picha, ramani, katuni n.k
ü
Kipengele
vya sarufi kilifungushwa kwa kufuata muktadha halisi ambamo lugha inatumika
ü
Kipengele
cha utamaduni kilifundishwa kwa uchache sana
3.
Mbinu ya usomaji (reading approach method)
ü
Mbinu
hii inatumika kufundishia kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni ambao
hawatarajiwi kutoka nje ya nchi ambapo lugha hiyo inatumika
ü
Malengo
yake huwa kuendeleza uwezo wao wa kusoma ile lugha
ü
Vipengele
vinavyofundishwa ni vile vinavyohusu usomaji, hivyo vipengele vingine
havihusiki. Mkazo wake ni kwamba anayejifunza lugha aweze kusoma vitu vingi kwa
wakati mmoja.
ü
Mbinu
hii haimpi mjifunzaji lugha uwezo wa kuzungumza lugha husika bali ni kuisoma tu.
4.
Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
ü
Nadharia
hii ilitokana na haja ya ukarimani nchini marekani miaka 1940.
ü
Iliasisiwa
na Bloomfield (1942) na Fries (1945)
ü
Msingi
mkubwa wa nadharia hii ni kile kinachosemwa
ü
Maandishi
hayakupewa fursa kubwa bali kile kilichosemwa ndicho kilikuwa cha muhimu sana.
Bloomfield alisema kuwa lugha si katika maandishi bali ni kile ambacho
kinasemwa.
ü
Inahusisha
kusimulia mada mbalimbali na kupima uwezo wa kusikia
ü
Walipenda
sana kutumia miziki, nyimbo, usimulizi na ughanaji
ü
Walisisitiza
stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
ü
Waliongeza
kitu kingine chakuona
5.
Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
ü Iliasisiwa na curran (1976)
ü Dai la nadharia
hii ni lugha ni watu, kwa maana ya kwamba huwezi kutenga jamii na lugha
ü Walidai kwamba
ili uweze kumfundisha mwanafunzi mgeni basi nenda kwenye jamii husika
ü Walidai pia
kwamba kama utaamua kufundishia darasani bali darasa lako lifanye angalau
lifanane fanane na jamii ya lugha husika
ü Ili uweze
kufundisha watu ni lazima ushirikishe watu wanaotumia lugha hiyo.
ü Mwanafunzi
atapata vichocheo vya aina nyingi katika jamii na kubaini ni mambo gani yanafaa
na mambo gani hayafai
ü Nadharia hii
inaipa kipaumbele jamii kama chombo muhimu katika kujifunza lugha
6.
Mbinu ya ukimya (silence method)
ü Nadharia hii
inaamini kwamba kila lugha ina mfumo wake tofauti na lugha nyingine, hivyo
ufundishaji wa lugha ya pili ulenge kumfanya mjifunzaji wa lugha kuwa mmilisi
au kukaribia kuwa mmilisi wa lugha anayojifunza
ü Nadharia hii inadai
kwamba ujifunzaji wa aina yoyote ile unahusisha vitu viwili.
Kichocheo®Mwitikio® mgeuko
(Mwalimu) (mwanafunzi)-(anabadilika)
ü Ili kuweza
kutimiza hili, mwalimu anahitaji kujenga mazingira ya utani katika darasa jambo
ambalo litaleta matokeo mazuri ya umilisi wa lugha husika
ü Nadharia hii
inamhitaji mwalimu kufanya tathimini kwa wanafunzi wake ili kubaini kama kuna
badiliko
7.
MBINU YA UTAMBUZI (COMMUNITIVE CODE METHOD)
ü
Nadharia
hii inatokana na ukosoaji/udhaifu wa nadharia ya mbinu ya sarufi na ile ya moja
kwa moja
ü
Ilianzishwa
mwaka 1970
ü
Wanadai
kwamba mwanafunzi apewe vipengele vyote vya lugha kwa ujumla mwanafunzi kumpa
maarifa mapana kuhusu lugha, kumpakanuni za msingi kuhusu lugha, halafu yeye
mwenyewe kulingana na utambuzi wake aweze kuielewa lugha.
ü
Uwafundishe
kanunu za msingi. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili ni lazima ujue ngeli za
majina-hii itakusaidia kutumia nomino katika mazingira tofauti tofauti,
vitenzi-waeleze namna ambavyo vinaweza kukaa peke yake kama sentensi
8.
Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
ü Nadharia hii pia
hujulikana kama mkabala asilia.
ü Iliasisiwa na James Asher 1969
ü Inatilia mkazo
mfumo na muundo wa lugha.
ü Kama ilivyo
nadharia ya usikizi nadharia hii pia inasisitiza umuhimu wa kumudu mazungumzo
kama sehemu ya umilisi wa lugha
ü Ufundishaji
uhusishe mazoezi ya kurudia rudia ambayo angalau unamfanya mwanafunzi kumudu
anachojifunza
ü Nadharia hii
inasisitiza matumizi ya vitendo na ishara mbalimbali kama nyenzo mojawapo
katika kujifunza lugha.
9.
Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
ü Ilianzishwa na Lonzano georgi (1979)
ü Nadharia hii
inayapa mazingira bora ya ujifunzaji lugha kama nyenzo muhimu mojawapo katika
kujifunza lugha. Hii inamaanisha kwamba mazingira yanayotumika kujifunzia lugha
ni lazima yamkumbushe mwanafunzi kile alichojifunza jana yake
ü Wanaelezea namna
ya mkao wakati wa kufundisha wanafunzi wageni. Mkao katika darasa uwe ni wa
kutazamana, maana yake vikae kwa duara.
ü Wanasisitiza
matumizi ya mziki laini na mziki nyororo
10.
MBINU YA MAWASILIANO (COMMUNICATIVE
LANGUAGE APPROACH)
ü Inasisitiza
maingiliano na maathiriano katika ya mwalimu, mwanafunzi na jamii
ü Wanakaza kwamba
kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.
ü Kujua lugha kwa
hakika sio kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua namna ya kuwasiliana na watu
wa jamii ile kwa kuzingatia mikitadha mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika
ü Ni nadharia
ambayo imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo Noamy Chomsky
ü Hii ndiyo
nadharia ambayo inafaa kutumia kwa ajili ya kujifunza lugha
VIWANGO VYA WANAFUNZI
·
Hapa
inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha Fulani.
·
Viwango
hivi viliwekwa na shirika/taasisi moja isiyokuwa ya kibiashara wala kiserikali
liitwalo Interagence Language Round Table (ILRT)
·
Kulingana
na shirika hili wajifunzaji lugha wako katika viwango vitatu
a)
Wanafunzi
wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
b)
Wanafunzi
wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
c)
Wanafunzi
wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level
a)
Wanafunzi
wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
Daraja limegawanyika katika viwango hivi
·
Kiwango
cha 0-®mwanafunzi
hawezi kabisa kuzungumza lugha
·
Kiwango
cha +0-®mwanafunzi
amekaririshwa tu mahitaji muhimu akibadilishiwa tu basi Amepotea
·
Kiwango
cha 1-®mwanafunzi
anaweza kusitahimili mazungumzo ya ana kwa ana ila hawezi kuanzisha mazungumzo
·
Kiwango
cha +1-®huyu anaweza
kuanzisha mazungumzo yeye mwenyewe, hata hivyo ni kwa ajili ya kukidhi
matarajio yake
b)
Wanafunzi wa daraja la kati
(DAKATI)Intermediate Level
·
Daraja
la 2-lugha si kamilifu lakini anaeleweka kwa urahisi
·
Kiwango
cha 3-anaweza kuzungumza lugha kwa muundo sahihi, ana msamiati wa mazingira
fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya kitaaluma
·
Anaweza
kukithi mahitaji ya kitaaluma
·
2+®Lugha yake si kamilifu lakini
anaweza kueleweka kwa urahisi
·
3®mwanafunzi ana uwezo wa kuzungumza
lugha kwa usahihi, ana msamiati toshelevu kwa mazingira fulani fulani tu.
·
3+®mwanafunzi ana uwezo wa
kuzungumza lugha kwa muundo sahihi na ana uwezo wa kukidhi mahitaji ya
kitaaluma
·
4®mwanafunzi ana uwezo wa kutumia
lugha kwa usahihi na ufasaha katika viwango vyote vya lugha. Yaani
fonolojia-matamshi, sintakisia-miundo, mofolojia-maumbo
·
Huweza
kutoa maana ya viambo mbalimbali kulingana na
muktadha
·
4+®uwezo wa mzungumzaji wa kiwango
cha juu kabisa katika mawanda yote lugha: yaani fasihi na isimu
·
Ana
uwezo wa kutumia kwa kuzingatia utamaduni wa lugha husika
·
Anaelekea
kulingana na wazawa wa lugha husika
·
5®usitadi wa lugha alio nao ni wa
kiwango cha mmilisi wa lugha aliyeboboea
·
Ana
sifa za kudhihilisha wakati wa lugha anayojifunza.
TATHMINI YA VITABU VYA
KUFUNDISHIA KISWAHILI KWA WAGENI
Suala
la uteuzi wa vitabu vya kufundishia lina ugumu unaotokana na mambo yafuatayo:
Yaani
malengo tofauti ya:
·
Malengo
tofauti ya wanafunzi
·
Malengo
tofauti ya taasisi
·
Malengo
tofauti ya waajiri
·
Malengo
tofauti ya waalimu
·
Malengo
tofauti ya wazazi/walezi
Tutafafanua utofauti huo kwa namna
ifuatayo:
·
Malengo
tofauti ya mwanafunzi:-mfano viwango tofauti vya wanafunzi
ü kitabia,
kiuchumi, kiuelewa, kiutamaduni,kiumilisi
ü viwango tofauti
za wanafunzi mfano kiwango cha kati,juu nk
·
tofauti
za kimaamzi. Mfano taasisi moja tu ihusike katika uandaaji wa vitabu vya
kufundishia mfano wizara ya elimu
·
uzingatizi
tofauti wa vitabu. Mfano,bei, mwonekano, upatikanaji wake
NAMNA
YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO
·
Malengo
ya kozi inabidi yaangaliwe
·
Wanafunzi
walengwa ni akina nani?
·
Mkabala
utakaotumia kufundishia
·
Stadi
za lugha. Je kitabu kimekidhi stadi zote za lugha?
·
Ubora
wa mazoezi yaliyotolewa ndani ya kitabu
·
Mfuatano
wa masomo/mada. Ngumu? rahisi? Nk
·
Msamiati
·
Hali
ya jumla ya kiisimu jamii. Je kitabu kimetumia lahaja, lugha rasmi, vigezo vya
kiutamaduni
·
Muundo
mzima wa kitabu. Chapa yake ni ndogo au kubwa?
KITABU BORA CHA KUFUNDISHIA
LUGHA KWA WAGENI KIWE NA SIFA ZIFUATAZO
a)
Kila somo/kitabu kiwe na lengo mahususi la kumsaidia
mwanafunzi kuwasiliana
b)
Kila kitabu kiwe na matini ya lugha kama
izungumzwayo na wazawa
c)
Kila kitabu kiwe na kielelezo cha mazingira halisi.
Mfano salamu
d)
Msamiati na sarufi ukidhi matakwa ya wanafunzi
e)
Utumizi wa vilelezo halisi kama vile picha,magazeti,
tangazo, kadi nk
f)
Kila kitabu lazima kiorodheshe sauti zilizo katika
lugha husika ili aweze kuzielewa.
MAELEZO YA MJIFUNZAJI LUGHA
UCHAMBUZI WA DOSARI
Maana yake:
·
Uchambuzi
wa dosari ni njia ya kuainisha, kupambanua na kufafanua dosari mbalimbali za wajifunzaji
wa lugha ya kigeni/lugha ya pili
·
Suala
la uchambuzi wa dosari liliasisiwa na Corder (1967)ambapo yeye anaeleza maana ya dosari
kuwa ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za lugha lengwa
·
Mambo
yanayoshughulikiwa na wanausasanyuzi; wanashughulikia mambo makuu manne
a)
Jinsi
mjifunzaji anavyoilewa lugha ya kigeni anayojifunza
b)
Jinsi
mjifunzaji anavyojifunza lugha ya kigeni/mbinu anazotumia
c)
Matatizo
anayokabiliana nayo wakati anajifunza lugha ya kigeni
d)
Kung’amua
mchakato/kutambua michakato inayotumiwa katika kujifunza lugha ya kigeni
UMUHIMU WA DOSARI/DHIMA YA
DOSARI KWA WAJIFUNZAJI LUGHA YA PILI
·
Dosari
zinazofanywa na wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni hutumiwa kama kioo
kinachoakisi hali halisi iliyofikiwa na wajipatiaji wa lugha ya pili.
·
Dosari
hizi humpatia mwalimu nafasi ya kutathimini jitihada zilizofikiwa na wanafunzi
wake kwa minajili ya kuboresha au kuendeleza mbinu za ujifunzaji lugha na
humsaidia mwalimu kubadilisha vifaa anavyotumia katika ufundishaji.
·
Kwa
ujumla umuhimu wa dosari unaangaliwa katika namna kuu nne
a)
Kwa
upande wa mwalimu
·
Huonyesha
jitihada zilizofikiwa na wanafunzi na kusaidia kuboresha
b)
Kwa
watafiti
·
Huonyesha
jinsi lugha inavyopatikana/inavyoamiliwa
c)
Kwa
mwanafunzi
·
Humsaidia
mwanafunzi kujua ruwaza/partern ya maendeleo ya mwanafunzi alipofikia
d)
Kwa
waandaa mitalaa
·
Huwasaidia
kuboresha uandaaji wa vitabu na machapisho mbalimbali kwa kujifunza
AINA ZA DOSARI
Aina hizi za
dosari zimeainishwa kutokana na mbinu wanazotumia wanafunzi kujifunza lugha.
1.
Dosari
majumui/majumuisho
»
Hizi
ni dosari ambazo mwanafunzi hutumia kanuni ya jumla ya lugha ya kwanza na
kuitumia katika lugha ya pili. Hii inasabisha kukiuka matumizi ya lugha lengwa.
Mfano katika lugha ya kiingereza vitenzi vingi huongeza “ed” mwanafunzi wamswahili wa kiingereza anaweza kupata shida kwani
anaweza kuwa anaongeza ed katika kila kitenzi jambo ambalo sio sahihi.
2.
Uepukaji/avoidance
»
Ni
ule utaratibu wa mjifunzaji lugha ya kigeni kujaribu kuepuka matumizi ya kanuni/maumbo/miundo
fulani ya lugha. Kwa mfano mwanafunzi anajaribu kuepuka matumizi ya neno fulani
anatajaribu kuliepuka hilo neno na kutumia neno lingine jambo ambalo
litasababisha makosa.
»
Hata
hivyo si rahisi kujua kama mtu fulani amekwepa matumizi ya neno fulani
3.
Urahisishaji
»
Mwanafunzi
anapoamua kurahisisha muundo wa lugha fulani hujikuta katika dosari
4.
Uhawilishaji
»
Uhamishaji
wa miundo na kaida za lugha ya kwanza kwenda lugha ya pili. Miundo hii
inapohamishwa basi hukiuka miundo ya lugha ya pili.
»
Kwa
mfano baadhi ya jamii ya watanzania hukiuka sana kanuni za Kiswahili. Mfano
Wanyakyusa wa hawawezi kusema “chama” bali “kyama” pia Wakinga hawawezi kusema
“viatu” bali wanasema “fyatu”
5.
Utumizi
ziada/over use
»
Ni
kuongeza matumizi yasiyohitajika katika utumizi wa lugha
MISINGI YA UAINISHAJI WA DOSARI
Hapa ni kwa
kuzingatia Nyanja kuu za lugha:
a)
Dosari za kifonolojia/ukiushi wa
matamshi-lugha zingine zina toni zingine hazina.
b)
Dosari
ya kimaumbo/kimsamiati-yaani upangaliaji wa vipashio vinavyounda maneno. Mfano
uwingi wa nomino za kiingereza hupachikwa mwisho tofauti kabisa na lugha ya
Kiswahili ambapo haitabiliki. Mfano pia katika lugha ya Kiswahili neno moja
linaweza kuwa na sifa ya kuwa sentensi, mfano “ninasoma” jambo ambalo kwa
kiingereza haiwezekani kuwa neno moja “ I read”
c)
Dosari
za kimuundo-taratibu tofauti tofauti zinazotumika kuunda vipashio. Kila lugha
ina utaratibu wake. Mfano. My brother-yangu kaka-mfumo huo hauwezekani kuwa
sawa
d)
dosari
za kimaana/kisemantiki- maana huwa ni tofauti tofauti
e)
Dosari
za kipragmatiki-hii ni miktadha mbalimbali mfano sokoni, kanisani
dosari
kulingana na athari za kimawasiliano
Ni
uainishaji wa dosari kulingana na uelewekaji/kutokueleweka kwa ujumbe
uliotolewa na mjifunzaji lugha. Kwa kuzingatia kigezo hiki tunapata aina mbili
za dosari.
1.
Dosari
za kimalimwengu/global errors-ni dosari ambazo zinafanya usemi uliotolewa na
mjifunzaji lugha kutoeleweka kabisa
2.
Dosari
za kienyeji/local errors-ni semi zinazotolewa na mjifunzaji wa lugha ya pili
ambazo haziko sahihi lakini zinaeleweka na msikilizaji. Mfano “I angry”mfano
mwingine ni“ninataka
kura”-akiwa jikoni au akiwa katika jukwaa anasema “ninataka kula”-
hizi zinaeleweka na wasikilizaji japo haziko sahihi.
USHUGHULIKIAJI
WA DOSARI ZA WANAFUNZI
® Kila mwanafunzi
wa lugha ya pili huwa ana dosari katika kujifunza lugha ya pili. Ni jambo la
msingi kushughulikia dosari za
wanafunzi, lakini angalia ni wakati gani ushughulikie dosari hizo, hii ni
kulingana na muktadha wa darasa: aina ya wanafunzi; haiba yao, mihemko, aina ya
dosari, umri n.k. Hata hivyo ikiwezekana dosari hizo ziweze kushughulikiwa ili
kusaidia zisijirudie rudie.
® Wataalamu
wengine wanaona kwamba dosari zisishughulikiwe. Mfano Krashen na Terrell(1983)
husema kuwa mwanafunzi aachwe mwenyewe atazidi kugundua dosari hizo na
atashughulikia mwenyewe.
® Kathleen Bailey
(1985)anapendekeza uamuzi wa aina saba
a)
Puuza
dosari hizo
b)
Dosari
zishughulikiwe papo kwa papo
c)
Kuhusisha
wengine katika kurekebisha dosari hizo. Mfano miongoni mwa wanafunzi hao hao
unaweza kuhusisha na wakakosoana wenyewe
d)
Kuhusisha
wanafunzi mahususi-yaani kumtumia mwanafunzi wa karibu na mwenzake kumsahihisha
mwingine.
e)
Kumrudia mfanyaji dosari/ mfano unaweza kumwambia “unaweza kufikiri zaidi juu ya hilo?”
f)
Kuwaruhusu wanafunzi wengine kutoa tathmini.
g)
Kumpa nafasi ya kujaribu tena na tena mfanyaji wa
dosari baada ya vitendo fulani kufanyika ndani ya darasa.
Mwisho wa yote lazima vitu vifuatavyo viwe
vimejitokeza:-
1.
Usahihi
na uhalali wa dosari uwe umedhihilika
2.
Sehemu
na mahali dosari imefanyika iwe imebainishwa wazi wazi. Mfano kama ni kwenye
neno, tungo nk
3.
Nafasi
ya kurudia na kujirekebisha kwa mfanyaji dosari iwe imetolewa
4.
Mifano
mbalimbali ya dosari na usahihi wa semi uwe umetolewa na kuonyeshwa kwa uwazi
5.
Aina
ya dosari iwe imeonyeshwa. Mfano kama ni dosari ya kimpangilio, kimatamshi nk
6.
Marekebisho
yawe yamefanywa kwa mifano anuai
7.
Mhusika
awe amesifiwa/kama ameepuka hizo dosari
MAMBO YANAYOATHIRI UJIFUNZAJI/UPATAJI
LUGHA YA PILI/KIGENI
Mambo hayo ni
yale ama yanayomwezesha au yanamkwamisha mpataji lugha kupata lugha.
Tutaangalia kwa mujibu wa Martland
(1997)
1.
Umri
® Mtu mwenye umri
mdogo ana ahueni zaidi katika kujifunza lugha kuliko mtu ambaye umri umeenda.
Mtoto ambaye hajabalehe mfano miaka kabla ya tisa (9). Hii inatokana na kwamba
mtu mzima tayari anakuwa na lugha nyingine ambayo inasigana na lugha
anayojifunza
2.
Hali
ya kiuchumi ya mjifunzaji lugha:
® Mtu wa tabaka la
chini hawezi kutumia vitu vya kisasa ili kupata lugha, maana vifaa hivyo ni vya
gharama kubwa.
3.
Hali
ya darasa:
® Darasa ambalo
limejengewa mazingira ya utani, wanafunzi wanamudu haraka sana kupata lugha.
® Hii inajumuisha
michezo mbalimbali katika darasa hilo
4.
Msaada
wa kifamilia/community support:
® Ikiwa mwanafunzi
lugha anayojifunza inatumika ndani ya jamii hiyo, atapata haraka sana lugha
kuliko mwanafunzi ambaye anajifunza lugha ambayo wazungumzaji wake hawako hapo.
® Mfano: Mtanzania
anayetaka kujifunza kiingereza anapata shida kwa sababu wazungumzaji wake wako
nje ya nchi
5.
Motisha:
® Motisha ni
kipengele muhimu sana katika ujifunzaji lugha
® Mwanafunzi aliye
na motisha ya ndani atapata lugha haraka kuliko anayepata motisha ya nje. Ref. motisha
6.
Kiwango
cha elimu:
® Mtu mwenye
kiwango kikubwa cha elimu ana uwezo mkubwa sana wa kupata lugha kuliko mtu
ambaye hana elimu kabisa.
7.
Matarajio:
® Kama mjifunzaji
lugha ana lengo la kufanya utafiti sehemu fulani, matarajio yake ni kujifunza
lugha na kuimudu ili akafanye kazi yake.
® Kama mwanafunzi
hana matarajio yoyote basi itakuwa ngumu kupata lugha.
8.
Haiba
® Wanafunzi
wacheshi hupata lugha haraka kuliko wanafunzi ambao sio wacheshi.
® Wachesi hupenda
kujichanganya sana.
9.
Mtazamo
wa utamaduni wa ujifunzaji lugha ya kigeni/pili.
® Mwanafunzi kama
ana mtazamo hasi na lugha anayojifunza basi itakuwa ngumu sana kupata lugha.
® Mtazamo chanya
ndio utakaomsaidia mjifunzaji lugha kupata lugha.
10.
Uwezo
wa kumudu lugha ya kwanza:
® Uwezo wa lugha
ya kwanza una kawaida ya kuathiri umuduji wa lugha ya pili, hasa inapotokea
kwamba lugha ya kwanza ni tofauti kabisa na mfumo wa lugha ya pili. (Nozalle
(2012)
11.
Viigwa
(role models in the community)
® Hii ni kwamba
kuna mtu gani katika jamii ambaye ni mtu maarufu unataka uzungumze kama yeye?
Hii itakusaidia kwa sababu mjifunzaji lugha atajaribu kujitahidi azungumze kama
mtu huyo.
12.
Muktadha/mazingira
® Mazingira ni
muhimu katika upataji lugha
TOFAUTI ZA UPATAJI WA LUGHA YA KWANZA NA
LUGHA YA PILI/KIGENI
Kuna tofauti
kubwa kati ya upataji wa lugha ya kwanza na lugha ya pili. Kila mtu ana lugha
ya kwanza. Wataalam wanaokuwepo hapa kushadidia hili niEllis (1994) na Bley Vroman (1988)
Hawa
wanabainisha hoja tisa, kama ifuatavyo:
1.
Mafanikio
kwa ujumla: mtoto anapopata lugha ya kwanza huipata lugha ile kwa usahihi
katika Nyanja zote, japo anaweza asiweze kutofautisha uchambuzi kiisimu lakini
wapataji lugha ya pili hupata mafaniko katika maeneo fulani fulani tu katika
lugha wajifunzayo.
2.
Kushindwa(failure):
katika upataji wa lugha ya kwanza kushindwa hakupo labda kama ana ulemavu
fulani lakini kwa wapataji lugha ya pili kushindwa ni jambo la kawaida
3.
Utofauti
baina ya wajifunzaji/wapataji lugha (variation): wajipatiaji wa lugha ya kwanza
hawana tofauti yoyote katika upataji lugha, yaani wakifikia umri fulani labda
kama miaka 3 hivi wote watakuwa wamepata, kama atakuwa hajapata lugha mpaka
miaka 9 basi huyo atakuwa na matatizo (msukuku-kukoma kujifunza lugha
(fossilization )lakini lakini wajifunzaji wa lugha ya pili kuna
tofauti kubwa sana, utakuta mwishoni mwa kozi mmoja amemudu na mwingine bado
4.
Malengo/goals:
lengo la mjipatiaji lugha ya kwanza ni umili wa lugha hiyo katika viwango vyote
lakini lengo la mjipatiaji lugha ya pili ni kupata maudhui na umilisi
kidogo
5.
Usukuku(ukakamaaji):
suala la usukuku halipo kwa mtoto anayejipatia lugha ya kwanza lakini kwa mjipatiaji lugha ya
pili hii ni hali ya kawaida kabisa(soma Han1998-2013).
6.
Uvumbuzi/ughamuzi:
wajipatiaji wa lugha ya kwanza huendelea kujipatia lugha ya kwanza katika ughamzibwete
(kujisahihisaha dosari pasipo kujua) lakini mpataji lugha ya pili huwa
katika ughamzi tambuzi.
7.
Maelekezo/instruction:
ujipatiaji wa lugha ya kwanza hauhitaji maelekezo, labda kidogo kwa ajili ya kuchochea lakini
mjipatiaji wa lugha ya pili anahitaji maelekezo ya kina na sahihi na kwa
utaratibu maalumu.
8.
Uthibitisho
hasi:katika ujipatiaji wa lugha ya kwanza usahihishaji wa dosari haumsaidii
mpataji wa lugha ya kwanza kupata lugha ile lakini katika upataji wa
lugha ya pili ni muhimu kufanya masahihisho ili kumpa mwelekeo sahihi.
9.
Athari
hisivu (affective factor): mjipatiaji wa lugha ya kwanza hakuna kitu
kinachomwathiri kujipatia lugha ya kwanza, mfano hafikilii kwamba atakosea,
atachekwa bali yeye hutamka tu lakini katika ujipatiaji wa lugha ya pili
athari hisivu zina msaada sana katika kupata lugha. Mfano mwanafunzi mcheshi,
hucheka atapata lugha haraka kuliko mkimya.
10.
Muda:
mtoto huchukua muda mfupi kati ya miezi 36 anakuwa mmilisi wa lugha lakini
mjipatiaji wa lugha ya pili hutumia muda mrefu sana. Inachukua miaka kama tisa
UTAYARISHAJI WA
MBINU ZA UFUNDISHAJI
A.
UTAYARISHAJI WA SOMO:
®
Hapa
tunaangalia muundo wa andalio la somo (lesson plan) unahitaji kuangalia mambo
haya:
1.
Muda
2.
Mada
3.
Malengo-ie
kitu gani kitokee katika somo hilo. Mfano mwisho wa somo mwanafunzi aweze
kutaja aina ya ‘nomino’
4.
Mazingira/muktadha-darasa,
aina ya wanafunzi.
®
Shajala
®
Logbook
®
Mhitasali
MUUNDO WA ANDALIO LA SOMO
Andalio
la somo linatakiwa kuwa na mambo yafuatayo
1.
Malengo
ya jumla (main objective)-haya ni mabadiliko ya muda mrefu yanayotakiwa kutokea
kwa muda mrefu. mfanoMwanafunzi aweze
kutathimini….mwanafunzi aweze kufahamu…
·
Mara
nyingi malengo haya hayabadiliki
2.
Malengo
mahusus/malengo wezeshi
·
Haya
ni malengo ya muda mfupi
·
Haya
ni malengo ambalo ni la kudumu lakini lengo lake ni kusaidia lengo la jumla
·
Tofauti
kati ya malengo mahusus na malengo ya jumla ni kwamba malengo ya jumla
hayapimiki ilhali malengo mahusus yanaweza kupimika
·
Malengo
mahususi ni mabadiliko ya muda mfupi ilhali malengo ya jumla ni mabadiliko ya
muda mrefu
Mwanafunzi
aweze kutaja viungo vya binadamu
vilivyo katika kichwa…mwanafunzi aweze kulinganisha
na kulinganua
Mwanafunzi
aweze kuonyesha viungo vya mwili..
Kubainisha
viungo vya mwili
3.
Mada
kuu.
·
Kila
unapoenda kufundisha lazima kunakuwa na maada. Mfano wa mada ni Usafiri wa Anga
4.
Mada
ndogo:
·
Kama
mada yako itakuwa hapo juu, mfano Usafiri wa Anga, mada ndogo inaweza
kuwa,kuwasili
kwa ndege, kukata tiketi, kufika uwanja wa ndege, mahali uwanja wa ndege ulipo,
hali ya miundombinu kwenda uwanja wa ndege nk
·
Kama
ikiwa mada kuu ni familia: basi mada ndogo yaweza kuwa aina za familia
5.
Zaka
za kufundishia
·
Hakuna
somo lisilo na zana za kufundishia. Mfano kama ni usafiri wa anga. Unaweza
kuchora picha ya mwanza, kuwapa ramani nk.
6.
Utaratibu
wa somo/yaani darasani
·
Somo
lolote linakuwa na:
a)
Utangulizi-tanguliza
somo lako, kama sio mara ya kwanza wape chemsha bongo, kama ni kwa mara ya
kwanza unaweza kuanza na hadithi. Hii itakusaidia kuvuta usikivu wa wanafunzi.
Pia unaweza kuwaruhusu wanafunzi wakuulize maswali kuhusu wanaelewa nini kuhusu
kile unachoenda kukifundisha
b)
Uwasilishaji
wa kiini cha somo:- unaweza kuandaa maswali, unaweza kuandaa makundi ya
wanafunzi wachache wachache.
c)
Utumizi/utendaji
wa wanafunzi. Hapa mwalimu unategeneza mazoezi, kazi binafsi, mazoezi mengine
ambayo watafanya wenyewe, maswali ya papo kwa papo au mazungumzo
7.
Kazi
ya nyumbani
·
Haifai
hata kidogo kuwafundisha wanafunzi wageni kumaliza kuwafundisha na kuwaacha bila
kuwapa zoezi lolote la kufanya
·
Zoezi
hilo lihusishe vile ambavyo mwanfunzi amesoma darasani.
·
Mfano
wa zoezi: Mtafute mtu yeyote kule mitaani
muulize maswali haya. Wewe ni nani, unasoma? Umeoa? Je unapenda nini? Nk
·
Hii
itakusaidia sana kujua wapi palipo na udhaifu ili uwee kuwasaidia wanafunzi
kama hajaelewa.
8.
Tathmini/
·
Ni
lazima kujitathimini wenyewe kama wameelewa au la.
UONGOZI WA DARASA/UTHIBITI WA DARASA
1. Upangaji wa darasa/ je darasa
limepangiliwaje? Je watu wote wako sana?
2. Mbinu za ufundishaji/mbinu
zinazopendekezwa ili uweze kulitawala darasa ni mbinu shirikishi. Usiwe
mwongeaje tu wewe mwenyewe. Pia tumia mbinu za kuona.
3. Uimara wa mwalimu/lazima mwalimu
ujiamini katika ufundishaji wako. Usionyeshe kuyumba hata kidogo, kumbuka mara
utakapoyumba hawatakuamini tena hata kama ukifundisha vizuri. Kama wakikuuliza
swali ambalo hulijui jaribu kuwashirikisha, kama na wao hawajui basi waambie
utawapata jibu siku nyingine. Unahitaji kuwa msafi. Uwe mbunifu.
4. Mwonekano wa darasa/ lazima
darasa liwe linaonekana. Kusiwepo na sauti nyingine inayoingia ndani
5. Matumizi ya ubao au power point.
Vionekane vizuri
6. Sauti ya mwalimu-je sauti yako
inasikika vizuri? Hakikisha sauti yako inasikika kwa wanafunzi wote. Uwe na
uwezo wa kuimudu lugha vizuri.
7. Ukubalifu wa mambo ambayo
hukufundisha/hukupanga kuyafundisha..kama wanafunzi wakitaka kufundishwa kitu
Fulani ambacho wewe hukujiandaa kuwafundisha, itategemea hali ya darasa
UTAYARISHAJI WA MITIHANI
Huu
ni mchakato wa upimaji wa maarifa/ujuzi ambao wanafunzi wameupata tangu mwanzo
wa kozi hadi mwisho wa kozi. Kipengele hiki ni cha muhimu sana hivyo lazima
lifanyike kwa ustadi na ubunifu mkubwa.
Malengo
ya mitihani lazima yalenge kupima mambo manne
1. Ulenge kupima maarifa na ujuzi
aliyopata mjifunzaji lugha.
2. Kupima mbinu mbalimbali
alizotumia mwalimu kufundishia kama zimeeleweka au la.
3. Mitihani imelenga kupima mitaala
4. Mitihani inapima uwezo wa
kuchochea kujifunza maarifa mapya.
AINA
ZA UPIMAJI
1. Upimaji rasmi-huu ni upimaji
unaofanyika mwisho mwa kozi na hufanyika mara moja tu. Hupima viwango vyote
ambavyo alijifunza mwanafunzi.
2. Upimaji usio rasmi-mwanafunzi
anapimwa wakati somo linaendelea,mfano mazoezi, mitihani nk. Mara nyingine
upimaji huu huitwa upimaji umbaji
KANUNI ZA UPIMAJI
1. Kuwapa wanafunzi muda wa
kujiandaa-wape muundo wa mtihani ulivyo
2. Hakikisha jaribio lako linapima
wanafunzi kitu walichojifunza
3. Hakikisha kwamba jaribio lako
lina uhalisia/reality
4. Hakikisha kwamba jaribio
lako/mtihani wako linachochea utendaji
***ili kutimiza haya, unapaswa
1.
Hakikisha
unaondoa utata katika mtihani huo/maswali yawe bayana/yawe wazi.
2.
Muda
wa kufanya mtihani huo uzingatie
3.
Kuwepo
na umakini katika uandishi/ avoid typing errors.
4.
Hakikisha
haurudii majaribio
5.
Hakikisha
wanafunzi wako hawaibii/kuangaliziana katika mtihani/cheating