MISINGI YA TAFSIRI NADHARIA NA MBINU
·
Tafsiri
ni nini?
·
Tafsiri kama Taaluma (somo)
·
Tafsiri kama zao, (kile kinachopatikana baada
ya kutafsiriwa/outcome.
Newmark (1982) Tafsiri ni jaribio la kuwasilisha ujumbe uleule
ulioandikwa katika lugha moja kwa lugha nyingine.
Jaribio kwa sababu si mara zote unaweza kufanya hivyo kwani unaweza
kushindwa au kufaulu.
*
Udhaifu wa Newmark katika fasili yake ni kwamba hakuzingatia umbo la kazi
yenyewe au mtindo wa kazi yenyewe. Mfano; kadi ya mwaliko, barua nk.
Mwansoko na wenzake (2006) Tafsiri ni zoezi la uhawilishaji
(Transferring) wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi lugha
nyingine.
* Ukiangalia wataalamu hawa wawili
utaona kwamba wanafanana; kwani wanaona kuwa tafsiri hufanywa katika maandishi.
Nida na Taber (1969) wanaona kuwa tafsiri hujumuisha upya ujembe wa
lugha chanzi kwa kutumia visawe asilia vya lugha lengwa vinavyokaribiana zaidi
na lugha chanzi, kwanza kimaana na pili kimtindo. Kwa mfano; “Damu nzito kuliko
maji” – "Blood is thinker than water”. Ndugu yako ni muhimu zaidi kuliko
mtu mwingine. “Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni” – “Wonders never end”
* Nida na Tiber wanaona kuwa
katika tafsiri kitu muhimu ni kuzingatia maana na mtindo.
MFASIRI NI NANI?
Ni mtu yeyote anayejishughulisha na kazi za kutafsiri.
Ni mtu mwenye taaluma au ujuzi wa kutafsiri na ambaye anajishughulisha
na kazi hizo (weledi-Professionalism)
MATINI NI NINI?
Ni wazo au mfululizo wa mawazo ambao unajitosheleza kimaana. Matini
inaweza kuwa neno moja, kirai, kishazi, sentensi, aya, kifungu cha habari nk.
AINA ZA MATINI (Text)
Kuna aina mbili za matini ambazo ni Matini Chanzi/Chasili na Matini
Lengwa/matini tafsiri.
· Matini Chanzi/chasili (MC)
“Source Text” ni matini ambayo iko katika lugha yake ya awali au lugha yake
iliyoandikiwa kabla ya mchakato wa kutafsiri.
· Matini Lengwa/tafsiri (ML)
“Target Text” ni matini iliyotafsiriwa kutoka lugha yake iliyoandikiwa.
Lugha Chanzi/Chasili (LC) ni lugha iliyotumika kuandikia matini chanzi
(Source language)
Lugha Lengwa (LL) (Target language) ni lugha iliyotumika kutafsiria matini chanzi au lugha unayoitumia kufanyia
tafsiri.
KISAWE/USAWE (EQUIVALENT/EQUIVALENCY)
Katika muktadha wa tafsiri kisawe ni neno, kirai, kishazi, sentensi au
hata maneno katika lugha lengwa ambayo maana na matumizi yake yanalingana au
kukaribiana na yale ya neno, kirai, kishazi, sentensi au msemo mwingine katika
lugha chanzi
DHIMA / UMUHIMU WA TAFSIRI
· Ni njia ya
mawasiliano/daraja kati ya watu au jamii mbili zinazotumia lugha tofauti.
Mfano; maelezo mbalimbali ya jinsi ya kutumia bidhaa mbalimbali kama vile redio,
simu, kurunzi, dawa, jokofu nk.
· Ni nyenzo ya kuelezea
utamaduni kutoka jamii moja kwenda jamii nyingine. Mfano; kupitia dini –
tafsiri ya Biblia au Kuruani “Koran”, Pia hata katika burudani – tafsiri ya
vitabu mbalimbali ambavyo vina vipengele vingi sana vya utamaduni kama vile
nyimbo nk.
· Ni mbinu ya kujifunzia
au kufundishia lugha kimsamiati na kisarufi.
· Ni kazi ya ajira kama
kazi nyingine, hivyo huweza kumpatia mtu kipato.
· Humliwaza mfasiri; hii
ni baada ya kumaliza kufasiri.
SIFA ZA MFASIRI BORA.
· Awe mahiri wa lugha mbili
zinazohusika; kuwa mahiri katika lugha maana yake nini? Ni kujua vizuri nyanja
mbalimbali za Isimu ya lugha husika kama vile; Fonolojia-Matamshi,
Mofolojia-Maumbo, Sintaksia-Muundo na Semantiki-Maana.
· Ajue vizuri utamaduni wa
watu mbalimbali.
· Ajue angalau lugha mbili
· Awe na maarifa ya TEHAMA
(ICT)
· Awafahamu watu, jamii na
utamaduni wao – mitazamo kuhusu watu, mitazamo – kuhusu wanyama.
· Apende kujisomea na
kujiendeleza kulingana na mabadiliko ya jamii. Mfano; kusoma vitabu, majarida,
magazeti mbalimbali kusikiliza redio na kuangalia TV nk.
· Awe mwandishi bora.
MAADILI YA MFASIRI BORA (ETHICS)
· Awe mwaminifu kwa matini na
kwa mwenye matini; yaani asipotoshe habari au kusema uongo.
· Awe mchapakazi
(Kujituma/Bidii katika kazi)
· Awe nadhifu –
Unadhifu-mwonekano wa moyo, asiwe tapeli/laghai
· Aelewe/kuelewa taratibu za
kazi na kuzifuata. Mfano; bei ya kutafsiri kwa ukurasa au kwa maneno.
·Ushirikiano/kushirikiana na watu mbalimbali wa fani mbalimbali, makundi
mbalimbali ikiwa pamoja na wafasiri wenzake.
NADHARIA YA TAFSIRI
Maana; ni maelezo muhimu kuhusu vipengele mbalimbali vya kifasiri
ambavyo vinapaswa kufuatwa au kuzingatiwa na kila mfasiri pindi anapokabiliwa
na kazi ya kufasiri.
Nadharia ya tafsiri ndio nguzo au mhimili muhimu wa shughuli zote za
tafsiri. Vipengele vingine vitakavyojadiliwa katika nadharia ya tafsiri ni
pamoja na taaluma zinazohusiana na tafsiri na dhima ya nadharia ya tafsiri.
Sababu za kuanzishwa kwa nadharia za tafsiri. Newmark (1982), Mwansoko
na wenzake (2006) wanasema kuna mambo matatu yaliyosababisha kuanzishwa kwa
nadharia ya tafsiri ambayo ni:-
i) Wingi wa makosa katika
tafsiri zilizochapishwa awali; ilionekana kwamba, kulikuwa na makosa mbalimbali
kama vile makosa ya kimuundo, kimaumbo, kimsamiati nk. Pia ilikuwa ni
nadra/muhali kupata tafsiri zisizokuwa na makosa.
ii) Kuwepo kwa idadi
kubwa (na inayoongezeka) ya asasi zinazojishughulisha na kazi za tafsiri. Hali
hii ilisababisha kubuniwa kwa nadharia ya tafsiri ili kuwepo kwa misingi
inayokubalika. Mfano; nchini Tanzania peke yake kuna asasi nyingi
zinazojishughulisha na tafsiri kama vile: BAKITA, TATAKI, SHIHATA, WAFASIRI na
vyombo mbalimbali vya habari kwa mfano: TV, Magazeti nk.
iii) Mfumuko wa istilahi
katika taaluma mbalimbali hasa Sayansi na Teknolojia. Hivyo nadharia ya tafsiri
ilianzishwa kwa lengo la kuleta ulinganifu wa istilahi hizo kati ya lugha moja
na nyingine ili kuwe na ufanisi zaidi.
TAALUMA NYINGINE ZINAZOHUSIANA NA
TAFSIRI
Tafsiri inauhusiano mkubwa na taaluma nyingine au vipengele vingine kama
ifuatavyo:
Inauhusiano na isimulinganishi; Isimulinganishi hijishughulisha na
kulinganisha vipengele mbalimbali vya kiisimu vya lugha mbili au zaidi, pamoja
na kuchunguza mbinu za ulinganishi huu. Uhusianao wake na tafsiri;- humsaidia
mfasiri kuelewa mifumo ya lugha mbalimbali na jinsi luhga hizo zinavyotumia
vipengele vyake vya kiisimu kutolea taarifa mbalimbali.
Inahusiana na isimujamii;- Isimujamii inahusika na kuchunguza uhusiano
kati ya lugha fulani na jamii ambayo inatumia lugha hiyo. Rejesta mbalimbali za
kijamii pamoja na maingiliano baina ya lugha. Ujuzi wa isimujamii unamsaidia
mfasiri kufahamu athari zinazotokana na mahusiano baina ya lugha na jamii
husika na kuzingatia mambo mbalimbali katika kutafsiri.
Inauhusiano na
semantiki/pragmatiki;- Semantiki ni taaluma inayochunguza maana ya maneno
katika upweke na katika makundi/taaluma inayochunguza maana ya maana. Kwa kuwa
kinachotafsiriwa ni mawazo au maana ya matini (siyo neno pwekepweke) basi ujuzi
huu wa semantiki utamwezesha mfasiri kujua au kung’amua kuwa maana ya matini
hiyo haitokani na maana ya neno mojamoja badala yake inatokana na maana ya
kimatumizi kwa ujumla katika mktadha mahususi.
Inauhusiano na elimumitindo (stylistics);- Hii inahusu uainishaji wa
mitindo mbalimbali ya lugha na miktadha ya matumizi yake.
Elimumitindo
Mitindo Mazingira ya kutumia
Uhusiano wake na tafsiri;- Taaluma hii ya elimumitindo itamwezesha
mfasiri kubaini mtindo wa matini chanzi ambao haunabudi kuhamishiwa katika
matini lengwa.
Inauhusiano na mantiki (logic);- Mantiki inahusu ukweli na uhakika au
usahihi wa mambo kama inavyosemwa, kuandikwa au kuaminika kwa watu. Mantiki
humsaidia mfasiri kubaini kauli zisizo dhahiri na zinazokanganya katika matini
chanzi ili azirekebishe kwanza kabla ya kuanza kutafsiri. Kwa mfano; The
current president of United Republic of Tanzania is Mzee Ally Hassan Mwinyi. Je
ni kweli?
NADHARIA YA TAFSIRI
Nadharia ya tafsiri hushughulikia mambo
makubwa manne ambayo ndiyo dhima ya nadharia ya tafsiri.
1. Kubaini na kufasili (define)
tatizo la kifasiri yaani kazi au mlolongo wa shughuli za tafsiri zinazopaswa
kufanywa katika utatuzi wa tatizo la tafsiri lililobainishwa.
2. Kuonesha vipengele vyote
vinavyopaswa kuzingatiwa katika utatuzi wa tatizo la tafsiri lililobainishwa.
3. Kuorodhesha taratibu au njia
zote zinazowezekana kufanikisha tafsiri inayohusika.
4. Kupendekeza taratibu
zinazofaa zaidi katika kutekeleza zoezi la kufasiri pamoja na mbinu za
kutafsiri zilizomuafaka zaidi kwa matini inayohusika.
NADHARIA MAHUSUSI ZA TAFSIRI.
1. Nadharia ya Usawe wa Kimuundo;
nadharia hii inatetewa na mtaalam Catford (1969), Tunapofanya kazi ya kutafsiri
tunatakiwa kuzingatia ulinganifu wa kimuundo kati ya matini chanzi na matini
lengwa, maana yake ni kwamba muundo wa matini chanzi ujitokeze katika matini
lengwa. katika nadharia hii muundo ni muhimu. Pia nadharia hii hutumika zaidi
katika kutafsiri maandiko ya kidini hasa Biblia.
2. Nadharia ya Usawe wa Kidhima;
wa tetezi wa nadharia hii ni pamoja na Nida (1964) na Nida na Taber (1969)
wanaona kuwa usawe wa kidhima ni muhimu zaidi kuliko usawe wa kimuundo.
Wafasiri wanapaswa kuhakikisha kwamba dhima ya matini chanzi pamoja na athari
zake zinajitokeza katika matini lengwa. Yaani kama matini chanzi inawalenga
watoto inapaswa iandikwe kiasi kwamba watoto wataweza kuelewa. Pia kwa
kuzingatia nadharia hii unapaswa kutumia lugha rahisi na inayoeleweka na watu
wote. Vilevile tafsiri yako iwe nzuri kiasi kwamba mtu atakaposoma asiweze
kujua kwamba hii kazi imetafsiriwa.
3. Nadharia ya Usawe wa
Aina-matini; matini yoyote ile ifasiriwe kwa kuzingatia aina yake. Hii inamaana
kwamba kazi itakayotokea itafanana na matini chanzi. Kma matini chanzi ni ya
kisheria itakapotafsiriwa matini lengwa nayo itaonekana kuwa ya kisheria.
Katika nadharia hii kinachozingatiwa ni fani (muundo) na maudhui (dhima/lengo)
ya matini yenyewe inayotafsiriwa. Watetezi wa nadharia hii ni Reiss
(1971), Buhler (1965) na Newmark
(1982/88)
4. Nadharia Changamani (Cross Fertilization theory). Hii ni nadharia
tete iliyoasisiwa na P.S.Malangwa (2010) Ndharia hii inadai kwamba huwezi
kufanya tafsiri kwa kutumia nadharia moja tu, kwa sababu hakuna nadharia
inayojitosheleza yenyewe.
UAINISHAJI WA MTINI
Maana: Kuainisha matini ni kuzigawa
au kuziweka matini katika makundi mbalimbali kwa kuzingatia kufanana kwake.
Sababu: Tunaainisha matini kwa
sababu kila matini inahitaji mbinu maalum ya kuitafsiri.
Mikabala/vigezo vya uainishaji:
Wataalam wengi wanatumia vigezo vitatu ambavyo ni Kigezo cha Mada
(Topic/Field), Kigezo cha Matumizi ya Istilahi, Kigezo cha Dhima kuu za Lugha
1.
Kigezo cha Mada: katika kigezo hiki tunaangalia maudhui ya jumla ya
matini. Tunajiuliza matini hii inahusu uwanja gani hasa katika maisha?Kwa
kutumia kigezo hiki cha mada tunapata aina tatu za matini.
i)Matini za Kifasihi (Literary Text);
hizi ni matini ambazo zinahusu fani mbalimbali za fasihi kama vile riwaya,
tamthilia, ushairi nk.
ii) Matini za Kiasasi
(Institutional Texts); matini hizi ni mtini za kimamlaka kama vile matini za
kisiasa na kiserikali (hotuba, risala, mikataba, vyeti nk).
iii)Matini za Kisayansi (Scientific Texts); matini hizi hujumuisha
masuala yote ya Sayansi na Teknolojia. Kwa mfano; Fizikia, Kemia, Biolojia nk.
2. Kigezo cha matumizi ya
Istilahi: katika kigezo hiki kinachozingatiwa hapa ni kwamba, matini huainishwa
kwa kuangalia wingi au idadi za istilahi-msamiati wa uwanja maalum/husika mf:
sharia nk. Kwa kutumia kigezo hiki tunapata aina tatu za matini:
a) Matini za kiufundi (Technical
Text), matini hizi huwa na idadi kubwa ya istilahi.
b) Matini za kinusu ufundi
(Semi-Techinical Text), matini hizi huwa na idadi ndogo au chache za istilahi.
c) Matini za zisizo za
kiufundi (Non Techinical Text), matini hizi ni zile ambazo hazina kabisa
istilahi bali hutumia maneno ya kawaida kabisa.
3. Kigezo cha Dhima Kuu za Lugha
(Major Language Functions). Buhler (1965) alipendekeza dhima kuu 3 za lugha.
i) Dhima elezi (Expressive Function), katika dhima hii lugha hutumika
kuelezea hisia za mwandishi/mzungumzaji. Anasema, mzungumzaji au mwandishi
hueleza hisia zake bila kumjali msikilizaji au msomaji.
ii) Dhima Arifu (Informative
Function), dhima hii ya lugha hujitokeza
pale ambapo matini au lugha inatumika katika kutoa taarifa kuhusu jambo fulani.
Dhima hii huegemea kwenye ukweli wa mambo.
iii) Dhima amili (Persuasive Function) katika dhima hii lugha hutumika
kuchochea hisia za msikilizaji au msomaji. Kiini cha dhima hii ni hadhira.
Kwa hiyo, kwa kuzingatia dhima hizi tatu “3” tunapata aina kuu tatu za
matini kama ifuatavyo:
1. Matini Elezi (Expressive
Texts); matini hizi huegemea upande wa mwandishi. Mwandishi hutumia matini hizi
kuelezea hisia zake.Mfano, kazi mbalimbali za kifasihi, hotuba, matini
mbalimbali za kimamlaka, matini za kisheria, matini mbalimbali za kitaaluma,
maandishi binafsi nk.
2. Matini Arifu (informative Texts); matini hizi ni zile ambazo zinatoa
taarifa au maarifa kuhusu jambo fulani. Sifa yake ni kuwa zinakuwa na umbo
sanifu au umbo maalum mfano; umbo la jarida, kitabu, ripoti, tasnifu, vitabu
vya taaluma mbalimbali nk.
3. Matini Amili (Persuasive
Texts); matini hizi huegemea upande wa hadhira. Katika matini Amili mwandishi
hujitahidi kadiri awezavyo kuchochea hisia za wasomaji na kuwafanya watende
kama ambavyo mwandishi anataka watende. Hivyo huegemea upande wa msomaji. Mfano
wa matini hizo ni kama vile mialiko mbalimbali, matangazo, maelekezo mbalimbali
nk.
UCHAMBUZI WA MATINI ZA TAFSIRI
Awali ya yote mchambuzi wa matini za tafsiri/mfasiri anapaswa kusoma
matini kwa kina na kuyaelewa kabla ya kuanza zoezi zima la uchambuzi wa
matini.
Maana: Uchambuzi wa matini unatuwezesha kubaini sifa na vipengele
vinavyojenga matini husika kimuundo, kidhima na kiitikadi.
Hatua/vipengele vya uchambuzi wa matini:
Uchambuzi wa matini unahatua tatu “3” ambazo ni kama ifuatavyo:
1. Kusoma matini yote na
kuielewa vizuri. Hii humsaidia mfasiri kuweza kuandaa marejeleo muafaka,
kuandaa vitabu au machapisho mbalimbali yatayomsaidia katika zoezi zima la
kufasiri matini. Kwa mfano;
- Kuandaa kamusi mbalimbali
kama vile kamusi ya lugha chanzi, kamusi ya lugha lengwa, kamusi ya visawe,
kamusi ya fani maalum.
- Inamsaidia mfasiri kuandaa
orodha ya istilahi.
- Inamsaidia mfasiri kuweza
kugawana sehemu au vipengele vya matini kwa wafasiri wengine.
2. Kuchambua matini yenyewe.
Uchambuzi wa matini hulenga kupata nduni bainifu za matini husika (Distinctive
Features). Kipengele hiki cha pili kina hatua ndogo ndogo tano ambazo ni kama
ifuatavyo:
a)Kubaini lengo la mwandishi wa matini
chanzi. Mfano; malengo ya mwandishi huweza kuwa kukweza, kusifu, kukashfu au
kuarifu jambo.
Kwa kawaida waandishi wa matini chanzi wanakuwa na mitazamo mitatu;
i)Mtazamo hasi kwa mtendwa (biased)
mfano, katika gazeti; “Chelsea yaichabanga Arsenal tatu nunge”
ii)Mtazamo chanya kwa mtendwa (biased)
mfano katika gazeti; “Chelsea yafuta uteja kwa Arsenal”
iii)Mtazamo wa kati (neutral) mfano
katika gazeti; “Chelsea yaifunga Arsenal au Arsenal yafungwa na Chelsea”
b) Kubaini lengo la mfasiri.
Mfasiri anapaswa kujiuliza kwa nini nafasiri kazi hii? Je lengo langu na mimi
ni tofauti na la mwandishi?
- Aepuke upendeleo kwa
hadhira chanzi na hadhira lengwa badala yake ajikite katika ukweli. Hivyo
inafaa awe katika mtazamo wa kati (neutral)
- Kama kuna haja ya kuegemea
upande mmoja basi aegemee kwa hadhira lengwa.
c) Kubaini hadhira na umbo la
matini. Kwa mfano; kama matini chanzi ni kitabu basi matini lengwa nayo iwe
kitabu.
d) Kubaini mtindo wa matini. Hapa
mfasiri ahakikishe kwamba mtindo wa matini chanzi unajitokeza katika matini lengwa.
Mfano; kama kuna monolojia au dayalojia basi na matini lengwa inapaswa kuwa
hivyo.
e)Kubaini ubora na mamlaka ya matini
chanzi. Hapa mfasiri hanabudi kuzingatia ujuzi wa mwandishi katika kutumia zana
za kiisimu/vipengele mbalimbali vya lugha.
Mamlaka hutokana na hadhi au ubobevu wa mwandishi huyo katika taaluma au
fani aliyoandikia. Mfano, kazi ya fasihi ya S. Robert ni bora kuliko
iliyoandikwa na mimi kwa sababu yeye ni mbobevu/galacha katika taaluma hiyo.
3. Kusoma matini kwa mara ya
mwisho. Katika hatua hii ya tatu mfasiri asome tena matini chanzi ili kutoa
taashira (highlight) kuhusu maneno au mambo muhimu.
Mambo muhimu ni: Majina mahususi ya watu, mahali, sehemu au miaka,
maeneo ambayo hayatafsiriki kirahisi ili aweze kuyashughulikia upya hapo
baadaye.
MCHAKATO WA KUTAFSIRI/KUFASIRI
Hatua muhimu katika kutafsiri
Tunapofanya tafsiri kuna hatua muhimu kuu sita kwa mujibu wa Mwansoko na
wenzake (2006). Hatua hizo ni kama ifuatavyo:
1. Hatua ya maandalizi. Hatua
hii inahusisha mambo matatu ambayo ni:
a) Kupitia tena sehemu muhimu za
matini chanzi, kwa mfano; istilahi, majina ya wahusika, majina ya kijiografia,
maeneo au kauli zisizofasirika kirahisi.
b) Kupata marejeleo ili kutafuta
visawe vya kisemantiki
c) Kutafuta na kuandika visawe
hivyo.
2. Hatua ya pili baada ya
maandalizi ni uhawilishaji (transferring/transference). Katika hatua hii
mfasiri uhawilisha ile taarifa kutoka kwenye matini chanzi kwenda kwenye matini
lengwa, hapa mfasiri anatakiwa kuzingatia sarufi ya lugha lengwa na lugha
chanzi. mfano; “My new car is broken”-langu jipya gari ni vunjika. Tafsiri ya
Kiswahili sanifu inapaswa kuwa “Gari langu jipya limeharibika”
Uhawilishaji maana yake ni kuhamisha maana, ujumbe nk. kutoka lugha
chanzi kwenda lugha lengwa kwa kuzingatia sarufi ya lugha lengwa, lengo la
matini au mwandishi, umbo la matini, mtindo nk.
Mbinu ya tafsiri ambayo inatumika katika hatua hii ya uhawilishaji ni
tafsiri ya neno kwa neno.
3. Hatua ya tatu ni kusawidi
rasimu ya kwanza (drafting). Uhawilishaji wa visawe kutoka lugha chanzi kwenda
lugha lengwa unapokamilika kinachopatikana ni rasimu ya kwanza ya tafsiri.
Rasimu ya kwanza ya tafsiri inakuwa na dosari nyingi na kwa hiyo haifai
kupelekwa kwa mteja au hadhira. Badala yake rasimu ya kwanza lazima ipitiwe
tena upya na kurekebishwa au kudurusiwa/durusu (review) rasimu (draft).
4. Hatua ya nne ni kudurusu
rasimu ya kwanza ili kuunda rasimu ya pili. Mfasiri hupata fursa ya kwanza ya
kuitathimini na kuifanyia marekebisho tafsiri yake mwenyewe. Kazi ya kudurusu
haipaswi kufanywa haraka. Wataalam wengine kama vile Larson (1984) anasema
rasimu ya kwanza ni lazima iachwe kwa muda wa wiki moja.
Udurusu unahusisha shughuli zifuatazo:
·Kusahihisha makosa ya kisarufi, miundo isiyoeleweka vizuri.
·kunyoosha sehemu zenye tafsiri ya mzunguko na zenye matumizi potofu ya
visawe. Mfano; “He rarely visits me these days – Siku hizi ni aghalabu-nadra
sana yeye kunitembelea.”
·Kurekebisha sehemu zenye muunganiko tenge/mbaya ambazo zinazuia
mtiririko mzuri wa matini.
·Kuhakiki usahihi na kukubalika kwa maana zinazowasilishwa katika matini
lengwa. Hapa tunaangalia kama kuna mambo yameongezwa, yamepunguzwa au
yamepotoshwa/kubadilishwa.
·Kuhakiki kukubalika kwa lugha uliyotumia katika tafsiri yako kwa
kuzingatia umbo na mada ya matini chanzi.
·Kuona iwapo mada au ujumbe mkuu wa matini chanzi unajitokeza waziwazi
katika matini lengwa.
5. Hatua ya tano ni kusomwa
rasimu ya pili na mtu mwingine. Msomaji wa rasimu ya pili anaweza kuwa mfasiri
au shabiki wa tafsiri, mhakiki au mhariri wa tafsiri anaweza kuwa mteja wa
tafsiri husika au mtu mwingine yeyote unayemwamini.
Namna ya kumpa mtu akusomee rasimu:
·Kumpa bila kumjulisha kwamba ni tafsiri
·Unampa matini chanzi na matini lengwa ili alinganishe.
Inapendekezwa kwamba mtu huyo asome kwa
sauti ili uweze kubaini mapungufu.
6. Hatua ya sita ni kusawidi
rasimu ya mwisho. Katika hatua hii mfasiri atafanyiakazi maoni na mapendekezo
ya msomaji ambaye alimpa kazi yake. Matokeo ya kufanyiakazi maoni ya mteja
hutupelekea kupata rasimu ya mwisho ambayo ndiyo humfikia mteja, hadhira,
wachapaji nk.
MBINU ZA UUNDAJI WA ISTILAHI
I. Misingi ya kimataifa ya
uundaji wa istilahi
i) Istilahi ziwe fupi
iwezekanavyo ili zieleweke vizuri au kirahisi.
ii) Istilahi zifuate sarufi ya
lugha lengwa.
iii) Tuepuke istilahi za
vifupisho/Akronimu
iv) Tusiunde istilahi kwa
kupanua maana ya istilahi iliyopo.
v) Istilahi zisiwe na
sinonimia au homonimia.
- Kusiwe na maneno kadhaa ambayo yote
yanarejelea kitu kimoja.
- Au zenye maana
inayokaribiana-homonimia
vi) Istilahi ziweze
kuambatanishwa kuwe na uwezekano wa kupata istilahi mbalimbali ndani ya kikoa
kimoja, mfano; rekodi-rekodiwa nk.
I.
Misingi ya uundaji wa istilahi za Kiswahili
Katika lugha ya Kiswahili kuna misingi
kadhaa ya uundaji wa istilahi za Kiswahili kama ifuatavyo.
i) Istilahi ziakisi
sifa bainifu za dhana zinazolengwa. Mfano; Istilahi kama vile kionambali – hapa
unapata picha ya kile kinachowasilishwa.
ii) Istilahi ambatani
zizingatie mambo yafuatayo:
- Idadi ya maneno yanayounganishwa
yasizidi mawili. Mfano; Mwanajeshi.
- Kama istilahi hizi ni maneno mawili
usitumie kistari (-)
- Zisizidi silabi nane.
iii) Istilahi ziweze
kunyambulika ili kuunda istilahi zaidi za vikoa. (semantiki field) mf; soma,
somea, someana, someaneni, someshanani nk.
iv) Istilahi
ziwetoshelevu/zijitosheleze (precise) na zisiwe ndefu mno. Pia zijitosheleze
kimaana.
v) Ziwe fupi na
zinazoeleweka kirahisi. Mfano; Istilahi “Autumn” – majira ya majani kupukutika
karibu na kipupwe. Hii si Istilahi bali ni ufafanuzi wa istilahi “Autumn.”
vi) Istilahi mahuluti
(blending – mix & combine),finyazo (acronyms) zafaa ziepukwe kwa sababu
etimolojia yake niauvulivuli/haiku dhahiri au haieleweki vizuri.
vii) Upanuzi wa maana
uepukwe kwa sababu huwachanya watumiaji.
viii) Kila dhana iwakilishwe na
istilahi moja tu/yaani kusiwe na maneno mbalimbali yanayorejelea istilahi
ileile.
AINA/MBINU/NJIA YA TAFSIRI/KUFASIRI
Waandishi wengi wanakubaliana kwamba
kuna njia nne zitumikazo katika tafsiri:
Wataalamu wengi wanakubaliana kwamba
kuna aina nyingi za tafsiri kama zilivyo matini nyingi za tafsiri. Kuna mbinu
nyingi za tafsiri kama zinavyobainishwa na wataalam mbalimbali lakini Mwansoko (2006) anasema kuna mbinu kuu nne:
1. Tafsiri ya neno kwa neno
(word for word translation) neno baada ya neno
2. Tafsiri sisisi (literal
translation)
3. Tafsiri ya kisemantiki
(semantic translation)
4. Tafsiri ya kimawasiliano
I.
TAFSIRI YA NENO KWA NENO/NENO BAADA YA NENO.
Tunapotafsiri matini kwa mbinu ya
neno kwa neno, hapo tunafanya tafsiri ya matini chanzi kwa kuzingatia maana za
msingi za maneno katika lugha chanzi na kutafuta maneno hayo katika lugha
lengwa. Katika mbinu hii ya tafsiri maneno na maneno hufasiriwa/hutafsiriwa
yakiwa pwekepweke kwa kuzingatia maana zake za msingi au za
kikamusi bila kujali muktadha wa matumizi. Mpangilio wa maneno katika
matini lengwa(ML) hufuata sarufi ya matini chanzi(MC). Matini lengwa, yaani
tafsiri mara nyingi huandikwa chini ya kila mstari katika matini chanzi. Kwa
mfano:-
“wa-toto wa-dogo wa-na-imba kwa furaha”
(pl)child (pl)small (pl)s.a.m - pre- for happness
Plural subject agreement mark
I like bananas more than oranges
Mimi penda
ndizi-wingi zaidi kuliko chungwa-wingi
Faida ya mbinu
1. Husaidia
kufahamu muundo wa kisarufi wa lugha chanzi
2. Mbinu
hii hutumiwa na wanaisimu katika uchambuzi wa sarufi za lugha mbalimbali
Dosari/upungufu/udhaifu wa mbinu
ü Mbinu
hii si nzuri hasa kwa matini ndefu kwa sababu taarifa inayotolewa haina uangavu
(haijielezi vizuri)
II. TAFSIRI SISISI
Katika tafsiri sisisi maneno hutafsiriwa yakiwa pwekepweke kwa
kuzingatia maana zake za msingi au za kikamusi katika lugha chanzi.Tofauti na
tafsiri ya neno kwa neno tafsiri sisisi hufuata/huzingatia sarufi ya lugha
lengwa
ü
Walimpa
msukumo mkubwa katika biashara yake.
They gave him/her a big push in his/her
business
They
gave him/her a big push in his/her business
ü
One
day my dreams will come true
Moja siku
angu ndoto (w.ujao)
kuja kweli
Siku moja ndoto zangu zitakuja kweli
Faida za mbinu
Husaidia
kufasiri dhana au matini zisizotafsirika kirahisi.Mfano; majina/maandishi ya
kanga, misemo, nahau nk.
Hasara/udhaifu wa mbinu
Si
mbinu nzuri kutafsiri matini ndefu ingawa ni mbinu bora ikilinganishwa na mbinu
ya neno kwa neno.
III. TAFSIRI YA KISEMANTIKI/WAZI
ü
Huegemea
zaidi upande wa mwandishi au upande wa matini chanzi
ü
Hulenga
kufasiri kila kipengele katika matini chanzi.
ü
Huzingatia sarufi ya lugha lengwa
ü Huzingatia zaidi
maana ya matini chanzi kiasi kwamba huwa na mwelekeo wa kuwa fafanuzi kwa
sababu inataka kufasiri kila kipengele
kilicho kwenye matini chanzi. Kwa mfano;
® Tanzania Electric Supply Company Limited
Kampuni tanzu ya ugavi wa umeme Tanzania
® Alikwenda mpaka nyumbani kwake
She/he went up to her/his home
®
Wonders never end
Maajabu kamwe hayaishi
Faida ya mbinu hii: -
ü
Husaidia
sana kufasiri matini elezi
ü
Husaidia
kuitajirisha lugha lengwa kwa misemo au semi mbalimbali kutoka katika matini
chanzi.mfano
·
Yote
kwa yote (All in all)
·
Natambua
uwepo wako (I acknowledge your presence)
·
Haijalishi
(It doesn’t matter)
·
Mwisho
wa siku (At end of the day)
·
Mwisho
lakini si kwa umuhimu (Last but not least)
·
Mabibi
na mabwana (ladies and gentileman)
·
Mwisho
lakini si kwa umuhimu (last but not least)
Hasara
ya mbinu hii:
ü
Hukosa
vionjo (haivutii) na kumfikirisha sana msomaji
ü
Mbinu hii huwa ni ya mzunguko na ya kifafanuzi
mno. Mfano; Tafsiri ya neno Autumn
IV.
FAFSIRI YA MAWASILIANO/KIMAWASILIANO AU TAFSIRI HURU
ü
Mbinu
hii huegemea zaidi upande wa hadhira lengwa
ü
Mbinu
hii huzingatia utamaduni,itikadi,mazingiranahistoria ya jamii lengwa.
ü
Hulenga msomaji wa matini lengwa apate athari
ileile kama aipatayo msomaji wa matini chanzi.
®®
Hii ndiyo mbinu ya tafsiri inayotumika kutafsiria matini nyingi zaidi kuliko
mbinu zilizotangulia na kwa sababu hii ndiyo mbinu bora zaidi ya nyingine mbinu
hii hufaa zaidi kufasiria matini Arifu na Amili.
®©
Katika mbinu hii mfasiri hutafuta visawe katika lugha lengwa kama vile misemo
na methali ambazo maana zake na mikitadha yake ya kimatumizi hufanana na
maana ya lugha chanzi au matini chanzi. Kwa mfano;
a)
Walimpa msukumo mkubwa katika biashara yake
®They gave him a big support in his business
®They helped him a lot in his great deal/in his
business
® They asisisted him/her a great deal in his/her
business
b)
Tanzania National Electric Supply Company Limited
®Shirika la Umeme Tanzania
c)
Wonder never end
®Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni
d) Christmas comes but once a year
®Mtumaini cha
nduguye hufa masikini
e) A stich in time saves nine.
MAZOEZI
YA KUTAFSIRI
1. Tanzania
investment bank
a) Kisisisi-benki ya uwekezaji Tanzania
Uwekezaji benki Tanzania
b) Kimawasiliano-Benki ya Rasilimali Tanzania
®®tafsiri ya
kimawasiliano ni lazima ujiulize katika jamii hiyo jambo hilo husemwaje? Je
watu wanalijuaje?
2.
The
prime minister condemned commercial sex workers
1)
Kisisisi-Waziri Mkuu aliwalaumu wafanyabiashara wa
ngono
2)
Kimawasiliano-Waziri Mkuu alikemea biashara ya ngono
3.
Mkuki
kwa nguruwe kwa binadamu mchungu(ugumuupo katika kutafsiri)