SAUTI ZA LUGHA ZA BINADAMU
Mchango wa Jan Baudouin de Courtenay, Ferdinand de Saussure na Noam Chomsky kuhusiana na sauti za lugha ya mwanadamu umetusogeza mbele katika kuekewa na kupata maarifa zaidi juu ya sauti za lugha ya binadamu. Kabla ya kuchambua kwa kina kuhusu mchango wa wataalamu hawa ni vema kufafanua baadhi ya dhana muhimi ili kupata uelewa zaidi juu ya lugha ni nini na maana ya sauti za lugha za binadamu. Tukianza na dhana ya lugha: dhana hii imejadiliwa na wataalam mbalimbali kama ifuatavyo;
Massamba (2009) anaeleza kuwa, lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.
Vilevile Habwe na Karanja (2007) wanasema kuwa, lugha ni mfumo wa sauti nasibu na ishara za kisarufi ambazo kwazo watu wa jamii fulani ya lugha huwasiliana na kupokezana utamaduni wao.
Naye Mgullu (1999) akimnukuu Sapir (1921), anasema kuwa, lugha mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilishia mawazo, maono na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari.
Wataalamu hawa wanaonekana kufanana katika kuelezea maana ya lugha, kwani wote wanakubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana zilizokubaliwa na jamii fulani ili zitumike katika mawasiliano miongoni mwao. Mambo muhimi yanayopatikana katika fasili hii ni pamoja na mfumo wa nasibu, wenye maana, kwa lengo la mawasiliano, na hutumiwa na binadamu.
Baada ya kuangalia maana ya lugha kutokana na wataalamu mbalimbali, ufuatao ni ufafanuzi wa maana za sauti za lugha kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.
Habwe na Karanja (wameshatajwa), wanasema sauti za lugha ni zile sauti zinazosaidia kujenga tungo zenye maana katika lugha.
Naye Massamba (kishatajwa) anaeleza kuwa sauti lugha kwa maana ya sauti ya lugha ni sauti yoyote itumikayo katika mfumo wa lugha ya mwanadamu.
Pia Massamba na wenzake (2004) wanasema kuwa sauti za lugha ni sauti zenye kubeba maana na ambazo hutumiwa na jamii fulani ya watu kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. Hii ina maana kuwa sauti za lugha ya binadamu ama zinaweza kufanana sana au kwa kiasi fulani na pia zinaweza zikasigana sana au kwa kiasi fulani tu. Massamba na wenzake wameonekana kuwaunga mkono Habwe na Karanja kwa kueleza namna sauti za lugha zinavyofuata mihimili katika kujenga tungo zenye maana katika lugha. Wao wanadai kuwa kuna uunganishaji wa sauti kuunda silabi au mofimu, uunganisha wa mofimu kuunda maneno na maneno kuunda tungo kubwa zaidi (sentensi). Sauti hizo katika lugha za binadamu kwa ujumla huitwa foni na zile za lugha mahususi huitwa fonimu.
Mtazamo wa wataalam walioorodheshwa hapo juu wanatofautiana katika kuelezea sauti za lugha ya binadamu.
Kwa kuanza na Jan Boudouin de Courtenay: Huyu ni mtaalamu aliyezaliwa mwaka 1845 huko Radzymin nchini Poland. Kwa mujibu wa Jones kama alivyonukuliwa na Massamba (ameshatajwa) anadai kuwa de Courtenay alianza kushughulikia nadharia ya fonimu na mabadiliko ya kifonetiki mwaka 1868. Lengo kubwa la de Courtenay lilikuwa ni kutaka kueleza tofauti kati ya fonimu na ala sauti.
Katika nadharia yake ya fonimu na mabadiliko ya kifonetiki alidai kuwa sauti za lugha ya mwanadamu ni za aina mbili yaani foni na fonimu. Hata hivyo de Courtenay hakutumia istilahi za foni na fonimu kama zinavyotajwa sasa, bali alitumia istilahi za “anthrop phonic” kwa maana ya foni, yaani sauti za kutamkwa tu na “psycho phonetics” kwa maana ya fonimu, yaani sauti za lugha.
Anaendelea kueleza kuwa, foni zipo karibu sana na taaluma ya kumwelewa binadamu pamoja na ala sauti zake ambazo kwa hakika hutofautiana sana na za wanyama wengine. Na kuhusu fonimu alisema kuwa, zinahusu kumwelewa binadamu pamoja na akili zake na namna anavyofikiri katika akili yake. Anadai kuwa mara nyingi binadamu hupokea kinachotamkwa na kufasiliwa.
De Courtenay kama alivyonukiliwa na Mgullu (1999) anadai kuwa, “fonimu ni tukio la akilini ambalo huwa na nia ya mzungumzaji au jinsi msikilizaji anavyomwelewa mzungumzaji au vyote viwili kwa pamoja.” Anaendelea kusema kuwa, “fonimu ni dhana ya kisaikolojia. Ni kipande sauti ambacho picha yake huwa akilini mwa mtu ambaye hukusudia aitoe wakati anapoongea.”
Mtalaam mwingine ni Ferdinand de Saussure (1857-1913). Huyu ni Mswisi ambaye alizaliwa mwaka 1857 huko Geneva. Hujulikana kama baba wa Isimu mamboleo (Muundo).
Moja kati ya mchango wake mkubwa katika taaluma hii ya Isimu ni kwamba aliweza kutofautisha mfumo lugha ambao ni ‘Langue’ na utendaji ambao ndio ‘Parole’. Katika dhana ya kwanza yaani Langue kama mfumo wa lugha mahususi anaueleza kuwa ni uwezo alionao mzungumzaji wa lugha mahususi na kuzungumza na kuelewa matamshi ya mzungumzaji mwingine wa lugha hiyo hiyo. Ni sehemu ya lugha inayowakisha maarifa kati ya sauti na alama, yaani ni mfumo wa alama kwa namna ya kiufundi tu.
Dai lake la msingi ni kwamba alama inategemea vitu viwili yaani kitaja (kiashiria) na kitajwa (kiashiriwa). Kitaja na kitajwa alizieleza kama alama za kiisimu. Kitaja au kiashiria ni umbo fulani la kusema au kuandikwa ambalo huwakilisha dhana fulani. Umbo hilo la kusemwa au kuandikwa ni kitamkwa au sauti ya lugha ya kusemwa na binadamu. Anapoeleza kitajwa au kiashiria ni kitu chenyewe kilichopo katika ulimwengu halisi wa vitu na dhana ambacho huwakilishwa na kiashiria fulani. De Saussure anatumia istilahi za “signify” (kitajwa) na “significant” (kitaja).
Anaendelea kusema kuwa, hakuna uhusiano wowote uliopo kati ya kitaja na kitajwa, uhusiano uliopo ni wa kinasibu tu. Ferdinand de Saussure alionesha uhusiano huu katika mchoro kama ufuatao.
Dhana (dhahania)
Kiashiria .…………………... Kiashiriwa
Mchoro unaonesha kwa mstari uliokatika (…………….) kuwa uhusiano kati ya kiashiria na kiashiriwa si wa moja kwa moja. Hapa tunasema kuwa kitu kinachotajwa kinaweza kuwa ni kilekile lakini kila lugha inaweza kuwa na kiashiria chake cha kukitaja, kwa mfano:
Kiashiriwa: “kiti”. kwa kiswahili ni "kiti" lakini kwa kiingereza ni "chair"
Hivyo ili mawasiliano yafanyike mfumo wa ishara lazima ufahamike na ukubaliwe na wanajamii wote.
Katika dhana ya pili ya ‘Parole’ yaani utendaji anadai kuwa ni ule usemaji wenyewe wa lugha ambao hufanywa na kila mtu. Hili ni tendo la mtu binafsi. Mtu binafsi aghalabu atazingatia mfumo lugha ili aweze kuzungumza kwa usahihi kadiri anavyoweza.
Mtaalamu wa tatu ni Noam Chomsky. Huyu ni mwanaisimu wa Kimarekani anayevuma sana kwa mchango wake katika taaluma ya Isimu kwa ujumla. Dhana za umilisi (competence) na utendaji (performance) zimemfanya awe maarufu ulimwenguni kote.
Chomsky anadai kuwa mtu anapojifunza lugha huanzia na umilisi, umilisi ni ule ujuzi wa lugha ambao wazawa wa lugha fulani huwa wanao. Ujuzi huu ndio huwawezesha wazawa hawa kuzielewa na pia kuzitunga sentensi zote sahihi katika lugha yao pamoja na zile ambazo hawajawahi kuzisikia. Kwa maana hii umilisi ni msimbo (code) uliopo akilini mwa mtu ambao hutumiwa wakati wote mtu anapoongea.
Anaendelea kusema kuwa kwa kiasi kikubwa umilisi (ujuzi) wanaokuwa nao wazawa wa lugha moja hufanana. Utendi ni udhihirishaji wa maarifa ya mtumiaji wa lugha. Hii ndio sababu inayowafanya waelewane katika mazungumzo yao. Mzungumzaji anasema kile anachotaka kusema na msikilizaji anaelewa kile kilichosemwa na mzungumzaji .
Katika sauti za lugha ya mwanadamu anazungumzia fonimu kwa mtazamo wa kisaikolojia, ambapo anadai kuwa fonimu ni tukio la kisaikolojia, hivyo zipo kichwani mwa mzungumzaji wa lugha.
Hivyo tunaweza kusema kuwa, mitazamo ya wataalamu hawa inakaribiana kuhusu sauti za lugha ya mwanadamu. Jan Boudouin de Courtenay na Noam Chomsky wanaona fonimu ni tukio la kisaikolojia kwani zipo kichwani mwa mzungumzaji wa lugha. Pia Ferdinand de Saussure anatumia istilahi za langue na parole zinazokaribiana na istilahi za utendi na umilisi zilizotumiwa na Noam Chomsky. Langue na umilisi zinahusu maarifa ya lugha na parole na utenzi zinahusu udhihirishaji wa maarifa hayo. Wataalamu hawa wamefungua njia kwetu sisi wanataaluma pamoja na wataalamu wengine kuendelea kuchunguza taaluma hii ya sauti za lugha ya mwanadamu kwa kina
KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA FONOLOJIA NA MOFOLOJIA
Katika kujadili swali hili tutaanza kufasili dhana kuu zilizojitokeza ambazo ni fonolojia na mofolojia. Ambapo wataalamu mbalimbali wamefasili dhana hizi huku kila mmoja akitoa fasili yake. Pia tutatalii kwa kina juu ya kuhitilafiana na kufanana kwa fonolojia na mofolojia na mwisho ni hitimisho.Kwa kuanza na mofolojia, wataalamu mbalimbali wamefasili mofolojia kama ifuatavyo,
Massamba na wenzake (2009) wanafasili mofolojia kuwa ni kiwango cha sarufi kinachojishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa maneno katika lugha yaani jinsi maneno ya lugha yoyote iwayo inaundwa.
Besha (2007) anasema mofolojia ni taaluma inayojishughulisha na kuchambua muundo wamaneno katika lugha. Misingi ya wataalamu hawa wawili wanaonekana kuingiliana katika kuonyesha namna ya taaluma ya mofolojia inavyojihusisha na muundo wa maneno katika lugha. Mofimu ndio kipashio cha msingi katika mofolojia.
Pia Rubanza (1996) anaonekana kuungana nao kwa kusema mofolojia kuwa ni taaluma inayoshuhulika na vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji wa maneno.mtaalamu anaongezea namna vipashio vinavyotumika katika kupangilia mfumo wa muundo wa maneno katika lugha. Kipashio cha msingi katika mofolojia ni mofimu.
Hivyo basi fasili ya mofolojia imeonekana kugusia uundaji wa maneno katika lugha kwa mpangilio maalumu. Hivyo mofolojia inaweza kuelezwa kwamba ni taaluma inayoshughulika na uchunguzi na uchambuzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika lugjha.
Baada ya kuangalia taaluma ya mofolojia, kuna wataalamu mbalimbali ambao wamefasili dhana ya fonolojia, wataalamu hao nia kama wafuatao.
Habwe na Karanja (2007) wanafafanua fonolojia kuwa ni taaluma inayoshughulika jinsi sauti zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana. Wanaeleza kuwa sauti hizo zinazotumika katika lugha hiyo mahususi hujulikana kama fonimu.
TUKI (2004) wanaifasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo linajishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha.
Vilevile Kihore ne wenzake (2004) wanafasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo hujishughuliah na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambao hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Katika fonolojia kipashio cha msingi kinachohusika ni fonimu.
Kwa ujumla fasili zilizoelezwa hapo juu ni za msingi katika taaluma ya fonolojia kwani wataalamu wote wanaelekea kukubaliana kuifasili fonolojia kuwa ni ni uwanja waisimu unaojisgughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa sauti za lugha mahususi.
Kimsingi taaluma ya mofolojia na fonolojia hufanana na kuhitilafiana kwa kiasi kikubwa.
Taaluma hizi zina ufanano kama ifuatavyo; (fonolojia na mofolojia).
Kwanza, vipashio vya kifonolojia ndivyo vinavyouna vipashio vya kimofolojia, kwa kutumia fonimu ambacho ndio kipashio cha msingi katika fonolojia huweza kuunda mofimu ambayo ndiyo kipashio cha msingi cha kimofolojia.
Mfano: /h/,/p/,/t/,/k/,/g/,/m/,/n/,/o/,/u/,/e/,/s/,/a/. fonomu hizo zinzweza kuunda mfuatano wa maneno kama ifuatavyo.
Pat-a =pata
Tak-a =taka
Tes-a =tesa
Maisha Uhusiano mingine ni kuwa kanuni za kifonolojia zaweza kutumika kuelezea maumbo ya kimofolojia Kanuni hizi si kwa kuelezea maumbo tu pia huweza kubadili umbo la neno yaani umbo la ndani na umbo la nje. Kanuni hizo za kifonolojia ni udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuathiri konsonanti, konsonanti kuathiri nazali na tangamano la irabu.
Udondoshaji, kanuni hii inahusu kuachwa kwa sauti fulani katika matamshi wakati mofimu mbili zinapokaribiana yaani katika mazingira hayo hayo ya sauti ambayo ilikuwepo hapo awali hutoweka.hapa kuangalia umbo la ndani la neno na umbo la nje. Umbo la ndani ni jinsi neno lilivyoundwa na mofimu zake mbalimbali na umbo la nje ni jinsi neno lisikikavyo linapotamkwa.
Mfano; umbo la ndani umbo la nje
Muguu mguu
Mutu mtu
Mujapani mjapani
Mara nyingi irabu “u” katika mofimu “mu” ikabilianapo na na mofimu fulani hasa konsonati halisi katika mpaka wa mofimu, irabu “u” hudondoshwa lakini inapokabiliana na irabu inayofanana nayo hubaki kama ilivyo.
Mfano; Muumba- muumba Muumini- muumini Muuguzi-muuguzi Muungwana- muungwana
Uyeyushaji, hii ni kanuni inayohusu ubadilikaji wa irabu fulani kuwa nusu irabu au kama wataalamu wengine waitwavyo “viyteyusho”. Viyeyusho vinavyohusika ni /w/ na /y/. kanuni hii hutokea katika mazingira ambayo irabu “u” hukabiliana na irabu isiyo fanana nayo katika mpaka wa mofimu na kuwa /w/ lakini hubaki kama ilivyo mara ikabilianapo na irabu inayofanana nayo. Pia irabu /i/ katika mofimu inapokabiliana na irabu isiyofanana nayo hubadilika na kuwa /y/ katika mpaka wa mofimu lakini hubaki kama ilivyo inapokabiliana na irabu inayofanana nayo.
Mfano
Mu+ema-----------mwema Vi+ake------------vyake
Mu+ana------------mwana Mu+ako------------mwako
Mu+eupe---------mweupe Vi+ake-------------vyake
Vi+ao--------------vyao Vi+akula----------vyakula
Vi+umb-----------vyumba
Tofauti na
Muuguzi ------ muguzi Muumba ------- muumba
Muungano wa sauti, kanuni hii hutokea pale ambapo irabu ya mofimu moja inapokabiliana na irabu ya mofimu nyingine katika mpaka wamofimu irabu hizo huungana na kuzaa irabu moja.
Mfano;
Umbo la ndani
Umbo la nje
Wa + enya
wenye
Wa + ingi
wengi
Ma + ino
meno
Wa + izi
wezi
Wa + enzi
wenzi
Lakini kanuni hii haifanyi kazi wakati wote kwani kuna mazingira mengine ambayo haifuati hasa katika mofimu mnyambuliko
Mfano:-
Wa + igizi +a +ji - waigizaji
Wa+ingereza - waingereza
Wa +oko+a+ji - waokoaji
Wa+ite - waite
Kanuni ya nazari kuathiri konsonati, kuna baadhi ya sauti ambazo huathiriwa na nazali “n” inapokuwa inaandamia yaani kuna sauti ambazo huathiriwa zinapokaribiana au karibiana moja kwa moja na nazali “n”. mara nyingi hutokea katika maumbo ya umoja na uwingi katika maumbo ya maneno
Mfano:-
Umbo la nje
umbo la ndani
Ulimi
u+limi
Ndimi
u+limi
Urefu
u+refu
Ndefu
n+defu
Kwa hiyo kama vile ulimi mrefu
Ndimi ndefu
Hapa tunaona kwamba sauti [ l ] na [ r ] zinapokaribiana na irabu na irabu haziathiriki lakini zinapokaribiana na nazali “n” hubadilika na kuwa “d”
Kanuni ya konsonati, kuathiri nazali; katika lugha ya Kiswahili sanifu na hakika katika lugha nyingi za kibantu umbo la sauti ya nazali huathiriwa na konsonanti inayoliandamia. Maumbo ya nazali hutokea kutegemeana na konsonanti zinazotamkiwa sehemu moja
Mfano:-
Mbawa
Mbaazi
Mbegu == /m/ na /b/ hutamkiwa mdomoni
Mbuni
Kanuni ya tangamano la irabu, huu ni mchakato wa kifonolojia ambao huhusu athari ya irabu moja kwenye irabu nyingine kiasi cha kuzifanya irabu hizo zielekee kufanana kabisa au kufanana katika sifa zake za kimatamshi. Mabadiliko hayo ya sauti husababishwa na utangamano ambao hujitokeza katika baadhi ya vitamkwa yaani kunakuwa na namna fulani ya kufanana au kukubaliana kwa vitamkwa ambavyo ni jirani.
Mfano:-
Umbo la nje
umbo la ndani
Pikia
pik+i+a
Pigia
pig+i+a
Katia
kat+i+a
Endea
end+e+a
Chekea
chek+e+a
Pokea
pok+e+a
Hapa tunaona kwamba kitendea -i- kinawakilishwa na maumbo mawili yaani – I - na – e - hapa tunaona kwamba – I - hujitokeza pale tu ambapo irabu ya mzizi wa neno ni ama o au e kiambishi hiki – I - hubadilika na kuwa – e -. hapa ni wazi kwamba kiambishi cha kutendea huathiriwa na irabu ya mzizi na hii ndiyo tungamano ya irabu.
Zaidi sana mofolojia na fonolojia zote ni nyanja za isimu zinazounda maarifa fulani ya lugha kwa kuchunguza sauti na maumbo ya maneno yatokananyo na sauti za lugha hiyo na mpangilio wake. Nyanja zingine za isimu ni kama fonetiki, sintaksia na semantiki.
Mfano:- Neno
Limia
- Lina sauti tano (5) (kifonolojia) zinazounda
- Mofimu tatu (3) (kimofolojia)
Tembea
- Sauti nne (4)
- Mofimu mbili (2)
Baada ya kuangalia ufanano huo kwa kina, sasa uelezwe utofauti wa taaluma hizo. Tofauti zinazojitokeza ni pamoja na hizi zifuatazo:-
Maana, katika kigezo cha maana inaonekana kwamba fonolojia hujihusisha zaidi na uchambuzi wa sauti za lugha mahususi kwa mfano sauti za lugha ya Kiswahili wakati mofolojia inajikita zaidi katika uchambuzi wa maumbo ya maneno. Hapa fonolojia huangalia kuna sauti ngapi zalizounda au zilizotumika katika neno fulani wakati mofolojia huangalia neno fulani limeundwa kwa vipende vingapi
Mfano:-
Lima - sauti nne (4) /l/, /i/, /m/, /a/ (fonolojia)
- Vipande au mofimu mbili (2) lim – a (mofolojia)
Jamila - sauti sita (6) /j/,/a/,/m/,/i/,/l/,/a/
- Kipande kimoja, jamila
Masikio - sauti saba (7) /m/,/a/,/s/,/i/,/k/,/i/,/o/
- Vipande viwili (2) ma + sikio
Tofauti ya vipashio, kipashio cha msingi cha kifonolojia ni fonimu wakati kipashio cha msingi cha mofolojia ni mofimu.
Mfano:-
Analima - fonimu saba (7) /a/,/n/,/a/,/l/,/i/,/m/,/a/
- Mofimu nne (4) a-na-lim-a
Sema - fonimu nne (4) /s/,/e/,/m/,/a/
- Mofimu mbili (2) sem-a
Baya - fonimu nne (4) /b/,/a/,/y/,/a/
- Mofimu moja
Ukongwe, taaluma ya fonolojia ni kongwe kuliko taaluma ya mofolojia ambayo ilianza baada ya kuibuka taaluma hii ya fonolojia.
Dhima ya vipashio, kipashio cha kimofolojia yaani mofimu kina uamilifu mkubwa sana katika lugha hasa kwa kuangalia mofimu huru ambazo huweza kusimama peke yake na kutoa maana kamili mfano baba, mama, safi, nzuri. Maana ya mofimu huru yaweza kuwa ya kileksika ama kisarufi. Lakini pia mofimu funge huleta utegemezi wenye maana sana katika neno ambapo ni tofauti na kipashio cha kifonolojia yaani fonimu ambayo ikiwa peke yake inakuwa haina maana
Mfano:-
Alilala - kifonolojia /a/, /l/, /i/, /l/, /a/, /l/, /a/
Mofimu hizo hazitakuwa na maana katika muktadha huo, ila tu zitakapoungana kuunda neno.
Alilala – a- mofimu awali ya nafsi ya tatu umoja katika nafasi ya kiima
-li- mofimu awali ya wakati uliopita katika nafasi ya kiima.
-lal- mzizi (mofimu kiini)
-a- kiambishi au mofimu tamati cha maana.
Mwisho vipashio vy akifonolojia hutengwa katika kila umbo la neno baina ya fonimu moja na nyingine wakati si kila kipande au mofimu katika umbo neno hutengwa. Kwa mfano mzizi na mofimu huru daima hazitengwi.
Mfano:-
Sema - /s/,/e/,/m/,/a/
- Sem-a
Juma - /j/, /u/, /m/, /a/
- Juma
Safi - /s/, /a/, /f/, /i/
- Safi
Hivyo basi pamoja na kuwepo tofauti hizo taaluma hizi mbili hukamilishana sana kwani uwepo wa taaluma moja hupelekea kuimarika kwa taaluma nyingine na kutokuwepo kwa taaluma moja hudhoofisha taaluma nyingine. Na hii ndiyo maana hatuwezi kuchunguza sauti za lugha ikiwa lugha hiyo haitakuwa na mfumo na mpangilio maalumu ya maumbo ya maneno na hatutachunguza maneno kama hatutakuwa na sauti zinazopelekea kuundwa kwa maneno hayo.
FONIMU INAVYOWEZA KUVUKA MPAKA WA FONIMU NA KUINGIA KATIKA FONIMU NYINGINE.
Dhana ya fonimu ni dhana ambayo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali wakitumia mitazamo tofauti tofauti. Wataalamu wafuatao wameeleza maana ya fonimu:-
Massamba, (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake. Sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha.
Massamba na wenzake, (2004) wanasema fonimu ni kitamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalumu.
Mgullu, akimnukuu Jones, (1975) anaeleza kuwa Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani, lenye sauti muhimu (phonemes) pamoja na sauti zinazohusiana na ambazo hutumiwa mahali peke katika muktadha maalumu.
Tunaweza kusema kuwa wataalamu hawa wametofautiana katika kuelezea dhana nzima ya fonimu, wakati Massamba (2004), anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha, Jones (1975) akinukuliwa na Mgullu anasema kuwa fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani.
Hivyo tunaweza kusema kuwa fonimu kipashio kidogo cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno katika lugha fulani (mahususi). Kwa mfano pata – baba.
Dhana ya fonimu kuvuka mipaka na kuingia katika fonimu nyingine ni pale fonimu fulani inapoliacha umbo lake la asilia na kuingia katika umbo jingine. Dhana hii imenukuliwa na Massamba (2010) kutoka kwa mtaalamu Bloch (1941).
Bloch (1941) anashawishi kwa kiasi kikubwa kuwa fonimu kuvuka mipaka ni tukio la kawaida katika lugha ya asili kutokana na ushahidi kuwa alofoni za fonimu moja zinaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kifonetiki. Wakati mwingine zinakuwa na uhusiano na alofoni za fonimu nyingine tofauti na fonimu zilimotokea. Vile vile kifonetiki, sauti fulani inaweza kutokea kuwa katika fonimu mbili au zaidi katika lugha moja. Anaendelea kusema kuwa kuna aina mbili za fonimu kuvuka mipaka ambazo ni:-
Uvukaji mipaka usiokamili, unaamanisha hali ya fonimu ya aina moja kutokea katika fonimu mbili katika mazingira ya hali tofauti.
Kwa mfano:
Udogo Ulimi Loa
Undugu Ndimi Ndoana
Ndugu
Hivyo katika Kiswahili sauti /d/ hujitokeza kama /d/ wakati mwingine huvuka mipaka na kuwa /l/. Sauti /l/ huwa /d/ endapo inatanguliwa na nazali /n/. Endapo tutajikita kifonetiki ni ngumu kutabiri /d/ kama ni alofoni ya fonimu /d/ au fonimu /l/ itakuwa rahisi.
Mfano mwingine wa Kiswahili ni pale:
Ki + ti = ki+eusi (kiti cheusi) katika mifano ya Kiswahili tutaona mabadiliko ya kifonimu yakijitokeza katika mfano wa fonimu /k/ inapofuatiwa na irabu halafu kuwa katika mpaka wa mofimu kisha ikafuatiwa na irabu /e/ hubadilika na kuwa /ch/ yaani (ki+eusi) = cheusi.
Mfano mwingine katika Kiswahili ni:-
N + buzi (mbuzi) /n/ inakuwa /m/ ikifuatiwa na /b/
N+dama (ndama) /n/ inabakia kuwa /n/ ikifuatiwa na /d/
N+gombe (ng’ombe) /n/ inabadilika na kuwa /n’g/
Pia tunaona kuwa nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /b/ hubadilika na kuwa /m/ inapofuatiwa na kitamkwa /d/ hubakia kuwa /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /g/ hubadilika na kuwa [ ŋ ]. Hii inamaana kuwa katika mazingira haya sauti /m/, /n/ na [ŋ] ni alofoni za fonimu /N/
Uvukaji wa mipaka uliokamili. Huu ni uvukaji wa mipaka wa sauti moja kwenda sauti nyingine katika mazingira ya aina moja.
Kwa mfano:-
Katika lugha ya kiingereza uvukaji wa mipaka uliokamili unahusisha fonimu /t/ na /d/ inapotokea katikati ya irabu. Wamarekani hutamka sawa sauti ya ufizi [d].
Mfano:- Butter, Betting, Kitty ukiyatofautisha na Budden, Bedding, Kiddy katika mifano yote hiyo fonimu /t/ na /d/ hutamkwa sawa.
Kwa mfano:- /betting/ - [ beDiŋ] na /bedding/ = [beDiŋ]. Unapotamka haya maneno hautamki moja kwa moja /d/ wala /t/ bali inakuwa sauti katikati ya /t/ na /d/. Kwa msingi huo fonimu /t/ na /d/ hupoteza uhalisia wake katika matamshi. Baada ya ule uhalisia kupotea sauti inayokuja huziwakilisha haizitofautishi sauti /t/ na /d/. aina hii ya uvukaji ndio huitwa uvukaji wa mipaka wa fonimu uliokamili.
Kutokana na mifano tajwa hapo juu ni dhahiri kuwa fonimu inaweza kutokea katika umbo lake asilia na kwenda katika umbo jingine la fonimu au alofoni ambazo hutokana na fonimu moja. Hii husababishwa na mazingira ya utokeaji wake au sifa za kifonolojia
MBINU MBALIMBALI ZA KUBAINI AU KUTAMBUA FONIMU.
Katika kujadili mada hili sehemu ya kwanza tutajikita katika kuangalia maana ya fonolojia na fonimu kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, katika sehemu ya pili tutaangalia mbinu mbalimbali za kubainisha fonimu kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali na sehemu ya tatu tutahitimisha na mwisho marejeo.
Kwa kuanza na maana ya fonolojia imejadiliwa na wataalam mbalimbali kama ifutavyo:-
Massamba, (2004), Habwe na Karanja (2007) kama walivyomnukuu Ladefoged (1975:23) wanaelekea kuwa na fasili zinazokaribiana kuhusu fonolojia. Wanafafanua kuwa fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulika na ufafanuzi , uchunguzi na uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha mahsusi.
Hivyo basi tunaweza kusema fonolojia kwa ujumla tunaweza kufasili kama ni nyanja mojawapo ya isimu inayoshughulika na uchambuzi, uchunguzi wa sauti za lugha mahususi kama vile fonolojia ya Kiswahili, Kingereza, Kisafwa na Kihehe.
Pia dhana ya fonimu imejadiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo;
Massamba (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi za kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake.
Habwe na Karanja, (2007) wanasema kuwa fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha sauti katika lugha kinachokuwa na uwezo wa kubadili maana ya neno.
Massamba na wenzake (2004) wanaema kuwa fonimu ni kipande sauti ambacho hutumika katika kujenga maneno ya lugha, kwa mfano vitamkwa kama /p/,/b/, /u/, /m/, /t/,/d/,/a/,/k/ na /n/ tunaweza kujenga maneno kama tunda, pumba, taka, muda, dunda, kama na kuta.
Hivyo kwa ujumla fonimu tunaweza kufasili kama kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia ambacho huwa na uwezo wa kujenga neno mfano /k/, /a/ na /a/ zinajenga neno “kaa,” /t/,/i/ na /a/-zinajenga neno “tia” au kubadili maana ya neno moja na nyingine mfano pia, bia,tia, kata,pata na bata,hivyo fonimu /p/, /b/, /t/ na /k/ zinabadili maana ya neno moja na jingine.
Wataalamu mbalimbali wamebainisha mbinu mbalimbali za kubainisha fonimu, mbinu hizo ni kama zifuatazo:-
Mgawanyo wa kimtoano au mgawanyo kamilishani, Mgullu (1999) akimnukuu Hyman (1975) anaeleza utoano kuwa ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi za fonimu moja ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa, hii ina maana ya kwamba kila sauti huwa na mazingira yake maalumu ya utokeaji ambayo hayawezi kukaliwa na sauti nyingine,kwa mfano kutoka lugha ya Kiingereza sauti /ph/ yenye mpumuo na /p/ isiyo na mpumuo haziwezi kutokea katika mazingira yanayofanana mfano tunaona kuwa /ph/ yenye mpumuo mara zote hutokea mwanzoni mwa maneno tu kwa mfano /put/, /pin/ na /pen/ na /p/ isiyokuwa na mpumuo hutokea sehemu nyingine yoyote katika neno isipokuwa mwanzoni mwa neno, kwa mfano /spell/na /spin/.
Pia mbinu hii imeungwa mkono na Massamba (2010) akimnukuu Hocket (1958) anasema kwamba sauti mbili zinaweza kuwakilisha fonimu zinazofanana kama zitakua na mazingira tofauti ya utokeaji, sauti zinazotokea katika mgawanyo kamilishani hujulikana kama alofoni za fonimu moja. Mfano kutoka lugha ya Ci-Ruuri:
Imbusi “mbuzi”
Oguβusi “mbuzi mkubwa”
Imbogo “nyati”
oguβogo “nyati kubwa”
Kutokana na mifano ya maneno hayo, tunaona kuwa fonimu /b/ na /β/ hugawana mazingira ya utokeaji, sehemu ambapo /b/ hutokea, /β/ haiwezi kutokea, huwa /β/ hutokea katikati ya irabu na mahala pengine popote, wakati /b/ hutokea tu pale inapokuwa imetanguliwa na nazali kama vile /m/.
Mpishano huru , kwa mujibu wa Mgullu (1999) akimnukuu Martinent anaeleza kuwa dhana ya mpishano huru ni maneno mawili yanayoweza kuwa na tofauti ya fonimu moja tu lakini tunapozitazama fonimu hizo zilizotofauti, tunaona wazi kuwa kwanza fonimu hizo ni tofauti sana Kifonetiki au haziwezi kuwa alofoni za fonimu moja, pia tunaona kwamba fonimu hizo zilizotofauti kifonetiki hazipo katika ule uhusiano wa kimtoano, yaani zote zinaweza kutumika katika mazingira yaleyale kwenye neno lakini fonimu hizo ingawa ni tofauti hazisababishi tofauti za maneno katika maneno zinamotokea yaani kila moja inaweza kutumiwa badala ya nyingine (katika maneno maalumu) bila kubadili maana katika maneno hayo.
Mifano:
Alimradi ilimradi /a/ na /i/
Baibui buibui /a/ na /u/
Amkia amkua /i/ na /u/
Bawabu bawaba /a/ na /u/
Wasia wosia /a/ na /o/
Benua binua /e/ na /i/
Heri kheri /h/ na /kh/ au /x/.
Mfanano wa kifonetiki, Mgullu (1999) akimnukuu Jones (1957) anaeleza kuwa fonimu fulani katika lugha fulani huwa ni ujumuisho wa udhahanishaji wa sauti kadhaa au tuseme kundi la sauti zinazofanana sana kifonetiki ni sauti zilizo na sifa bainifu zinazofanana. Kwa mfano irabu huwa na sifa zake bainifu ambazo ni tofauti na konsonanti, mfano irabu /i/ na /u/ hatuwezi kusema kuwa ni fonimu moja kwa sababu sauti hizi zinatofautiana sana kifonetiki, kwa hiyo hizi ni fonimu mbili tofauti.
Mfano;
/i/ /u/
+ irabu +irabu
+mbele +nyuma
+juu +juu
-mviringo +mviringo
Hivyo irabu /i/ na /u/ zinafanana tu katika sifa mbili ambapo zote ni irabu na zote ni irabu za juu na zinatofautiana katika sifa mbili ambapo irabu /i/ ni irabu ya mbele si viringe na irabu /u/ ni irabu ya nyuma viringe. Hivyo hatuwezi kusema zinafanana kifonetiki kutokana na kutofautian kwa baadhi ya sifa bainifu.
Besha (2007) anasema kuwa uainishaji wa fonimu tunaangalia mfanano wa kifonetiki. Anasema kuchanganua mifumo ya sauti za lugha mbalimbali mfanano wa kifonetiki kati ya sauti ni muhimu sana kwa vile mahusiano ya kifonetiki, kanuni pamoja na minyumbuo yote inategemea katika sifa hii kuainisha sauti za lugha ili kugundua zipi ni fonimu za lugha hiyo pamoja na alofoni zake. Umuhimu huwekwa katika kuangalia uhusiano uliopo katika makundi ya sauti kufuatana na mahali pa kutamkia na namna za utamkaji , makundi makubwa yanayohusiana sana ni matatu ambayo ni Vipasuo, vikwamizi na ving’ong’o,ndani ya makundi haya umuhimu mkubwa huwekwa katika mahali pa kutamkia . Hivyo basi mifano inayotolewa na wataalamu mbalimbali haibainishi mfanano wa kifonetiki kwani sifa za kila sauti zinatofautiana na nyingine, sifa kuu ya mfanano wa kifonetiki ni lazima sauti hizo zifanane kwa sifa zote.
Jozi sahili / jozi ya mlinganuo finyu, kwa mujibu wa mgullu (1999) kama alivyomnukuu Fischer (1975) anasema mlinganuo finyu ni tofauti ndogo kabisa ya kifonolojia iliyopo baina ya maneno fulani,aghalabu maneno hayo huwa yana idadi sawa za fonimu, fonimu zinazofanana isipokuwa fonimu moja na mpangilio wa fonimu ulio sawa.Katika lugha ya kiswahili maneno kama /pia/ na /tia/ ni mfano wa mlinganuo finyu kwa sababu idadi ya fonimu ni sawa, aina ya fonimu zilizopo ni zilezile isipokuwa moja, maneno yote yana /a/ na /i/ isipokua tofauti katika fonimu /p/ na /t/ na mpangilio wa sauti ni sawa ambapo /p/ na /t/ zipo mwanzoni mwa neno zikifatiwa na irabu /a/ na irabu /u/.Pia kutoka lugha ya kiswahili maneno kama
pata na bata
kata na kati
dua na tua
Katika maneno haya fonimu /p/, /b/, /a/, /i/,/d/ na /t/ ndio zinazotofautisha maana za maneno baina ya neno moja na jingine. Mbinu hii pia imeungwa mkono na wataalamu wengine kama Besha (2007) na Massamba (2010) kwani wametoa maelezo yao na mifano inayofanana sana na ya Mgullu (1999) alivyonukuu kutoka kwa Fischer (1975)
Kwa kuhitimisha,ni vigumu kubainisha fonimu kwa kutumia mbinu moja, hivyo basi ni vyema fonimu zikabainishwa kwa kujumuisha mbinu zote kama zilivyobainishwa na wataalam mbalimbali ili kuweza kupata mbinu moja ambayo ni sahihi katika kubaini fonimu.
Michakato ya
kiusilimisho katika fonolojia.
Katika kujadili mada hii tutalenga kuangalia michakato ya kiusilimisho namna inavyotumika katika kuyakokotoa maumbo ya ndani kwenda maumbo ya nje katika lugha ya Kiswahili. Lakini kabla ya kuonesha ukokotozi huo ni vyema kwanza tuangalie maana ya mchakato, maana ya usilimisho, umbo la ndani na nje, kisha tutaelekea kwenye hitimisho pamoja na marejeo.
Tuki (2004) inaeleza kuwa mchakato ni mfululizo wa shughuli unaosababisha kitu fulani kufikiwa.
Hivyo katika uwanja huu wa fonolojia tunaweza kusema kuwa mchakato utakuwa unafanyika pale ambapo mofimu mbili zinapokutanishwa huweza kutokeza mabadiliko fulani katika mofimu mojawapo au kutotokea badiliko lolote. Mfano viungu hubadilikia kuwa vyungu,kietu hubadilika kuwa chetu hapa tunaona kuwa mabadiliko yametokea lakini miti hubakia kuwa miti, kiti hubakia kuwa kiti na hapa tunaona kuwa hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea.
Massamba (2011) anaeleza kuwa kuna aina mbili za michakato asilia yaani mchakato usilimisho na mchakato sio-usilimisho. Lakini katika mjadala huu tutajikita kwa kuangalia mchakato mmoja tu yaani ule wa kiusilimisho, ambao Massamba anasema muwa usilimisho ni pale ambapo kitamkwa kimoja hufanywa kifananefanane na kitamkwa kilicho jirani yake kwa maana kwamba hupata baadhi ya sifa za kipande sauti chenziye kilicho jirani. Kwa mfano, konsonanti inaweza kupata baadhi ya sifa za irabu au irabu ikapata baadhi ya sifa za konsonanti, na konsonanti moja huweza kuathiri konsonanti nyenziye au irabu moja huweza kuathiri irabu nyenziye. Pia anaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha michakato kadhaa kama vile,unazalishaji wa irabu, utamkiaji pamwe wa nazali, ukaakaishaji, ughunishaji kati irabu, uhafifishaji kati irabu, tangamano la irabu, ughunishaji konsonanti shadda, muungano.
Habwe na Karanja (2004), wanaeleza kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kikamilifu kutokana na kuathiriana. Hapa sauti jirani katika neno huathiriana kiasi kwamba fonimu hupokea ama kupoteza sifa za kifonetiki kwa fonimu jirani, na matokeo yakiwa kuwa fonimu hizi hukabiliana sana katika kufanana. Pia wanaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha kuimarika, kodhoofika, kuingizwa, kudondoshwa, au kuungana kwa fonimu katika neno.
Hivyo tunaweza kusema kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kiukamilifu kutokana na kuathiriana kwake kunakosababishwa na fonimu iliyo jirani.
Baada ya kuangalia utangulizi huo sasa ni wakati wa kukokotoa michakato hiyo ya kiusilimisho kutoka umbo la ndani kwenda la nje.
Lakini kabla ya kukokotoa kwanza tuangalie umbo la ndani kuwa ni namna umbo lenyewe linavyoumbwa na mofimu zake au tunaweza kusema kuwa ni umbo la neno ambalo halijafanyiwa michakato yoyote ya mabadiliko. Na umbo la nje ni lile lililofanyiwa mabadiliko au michakato na mara nyingi huakisi umbo la ndani. Michakato itakayooneshwa ni ile ambayo imeorodheshwa na wataalamu lakini ambayo inahusiana na lugha ya Kiswahili tu kwani mingine inahusiana na lugha zingine kwa mfano michakato ya Massamba ameingiza michakato miwili inayohusiana na lugha za kigeni ambayo ni ughunishaji kati irabu na uhafifishaji kati irabu, hivyo hiyo hatajadiliwa.
Unazalishaji wa irabu
Massamba (2011) anadai kuwa unazalishaji wa irabu ni aina ya usilimisho ambao irabu hupata sifa ya unazali kutokana na irabu yenyewe kutangamana na konsonanti ambayo ni nazali. Hivyo irabu nyingi hupewa sifa za unazali kutokana na ama kufuatiwa kwa nazali ama kutanguliwa na nazali. Na alama inayowakilisha unazalishaji ni alama ya kiwimbi [ ̴ ] ,zaidi tuangalie mifano ifuatayo.
Mifano
umbo la ndani
umbo la nje
/nondo/
[nondo]
/penya/
[penya]
/mama/
[mama]
/ngambo/
[ ambo]
/nyumba/
[ umba]
/muwa/
[muwa]
Hivyo sauti zote zilizowekewa alama ya kiwimbi ( ̴ ) zina unazali kwa sababu zimefuatana na nazali na hivyo zimefanywa kuwa unazali.
Kanuni katika Kiswahili
I I N
Kanuni ya jumla.
+sila
+kons +naz -kos
+naz
+kons
+naz
Ukaakaishaji
Mgullu (1999) akimnukuu Les (1984), anadai kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea ambapo fonimu zisizo za kaakagumu zinapobadilika na kuwa za kaakagumu. Yeye anadai kuwa katika Kiswahili sauti za kaakagumu zipo mbili tu yaani /ɟ/ na /ʧ/ ambazo ni vizuiwa kwamizwa. Anamalizia kwa kusema kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu zisizo vizuiwa kwamizi hubadilika na kuwa vizuiwa kwamizwa. Hii katika ukokotozi wake unakuwa kama ifuatavyo.
umbo la ndani
umbo la nje
umbo la nje
/ki+enu/
[kjenui]
[ enu]
/ki+eusi/
[kjeusi]
[ eusi]
/ki+ombo/
[kjombo]
[ ombo]
/ki+umba/
[kjumba]
[ umba]
/ambaki+o/
[ambakjo]
[amba o]
Hapa tunaona kwamba kipasuo cha kaakaalaini /k/ hubadili mahali pa matamshi na kuwa kizuiwa kwamizi /ʧ/ cha kaakaagumu katika mazingira ya kufuatiwa na sauti /ϳ/.
Kanuni yake /i/ [ ] I =
kisha inabadilika kuwa
/k/ [ ] /i/
Kanuni ya jumla.
+kons
-sila +stn’d +sila
+juu + juu -kons
+nyuma +k’gumu -nyuma
-fulizwa +juu
-ghuna
Uyeyushaji
Uyeyushaji, wataalamu wengine huita irabu kuwa nusu irabu Mgullu (1999). Huu ni mchakato ambapo irabu irabu za juu /u/ na /i/ hubadlika na kuwa /w/ au / j/ katika mazingira ya kufuatiwa na irabu zisizofana nazo. Kwa kifupi ni kwamba /u/ inapofuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika kuwa [w] na /i/ ikifuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika na kuwa [j].
Hivyo tunaweza kusema kuwa uyeyushaji ni kanuni inayoelezea mabadiliko ya sauti (irabu) na kuwa kiyeyusho aidha [w] au [j] hii ni kwa irabu zote za juu zinapofuatana na sauti zingine zisizofanana nazo. Na sauti hizo hubadilika katika mazingira ya /u/ hubadilika kuwa [w] inapofuatana na irabu nyingine isiyofanana nayo na / i/ inabadilika na kuwa [ϳ] pia inapofuatana na irabu isiyofanana nayo.
Mfano wa /u/
umbo la ndani
umbo la nje
/mu+aminifu/
[mwe:mbamba]
/ku+enu/
[kwe:nu]
/mu+ anafunzi/
[mwa:nafunzi]
/mu+eupe/
[mwe:upe]
/mu+embe/
[mwe:mbe]
Hivyo tunaona wazi kabisa kuwa irabu ya juu nyuma /u/ imebadilika na kuwa kiyeyusho [w] katika mazingira ya kuatiwa na irabu isiyofanana nayo ambayo ni /a/ na /e/ kwa hapo juu lakini hata ikiwa ni /o/ huweza kubadilisha.
Kanuni /u/ [w] I = u
Mfano wa irabu /i/
/umbo la ndani/
[umbo la nje]
/mi+embe/
[mje:mbe]
/mi+endo/
[mje:ndo]
/mi+ezi/
[mje:zi]
/mi+anzo/
[mja:nzo]
/mi+eusi/
[mwe:usi]
/mi+oyo/
[mjo:jo]
Hivyo tunaona kuwa irabu ya juu mbele /i/ hubadilika na kuwa [j] inapofuatana na irabu nyingine isiyofanana nayo ambayo ni /e,a na o/.
Kanuni yake /i/ [j] I/= i
Kanuni ya jumla.
+sila -kons
+juu -sila +sila
+mbele + juu +juu
I = +mbele
+sila -kons +sila
+juu -sila +juu
+nyuma +juu +nyuma
+nyuma
Tangamano la irabu (usilimisho wa irabu pekee)
Huu ni mchakato wa kiusilimisho baina ya irabu na irabu katika kuathiriana kiasi kwamba hulazimika kufuatana. Katika mchakato huu kinachotokea ni kwamba, kama irabu ya mzizi ni /i, u au a/ basi irabu ya kiambishi cha utendea lazima kiwe ni [i] , wakati irabu ya mzizi ikiwa ni/ e au o/ katika hali ya utendea kiambishi chake kitakuwa ni [e]. Mfano.
umbo la ndani
umbo la nje
/imb+a/
[Imb-i-a]
/andik+a/
[andik-i-a]
/dak+a/
[dak-i-a]
/chun+a/
[ un-i-a]
/og+a/
[og-e-a]
/ ez+a/
[ ez-e-a]
/kom+a/
[kom-e-a]
Hapa tumeona kuwa mofimu ya utendea ina alomofu mbili ambazo ni /i/ na /e/ ambapo alomofu /i/ tunaona inatokea pale ambapo irabu ya mzizi inakuwa na /i,u na a/ wakati ambapo alomofu /e/ inatokea wakati irabu ya mzizi ikiwa ni /e na o/. kinachoonekana hapa ni kwamba irabu zinatangamana kwa kufuata mahali pa matamshi. Kwa mfano kama irabu ya mzizi ni ya juu basi irabu ya utendea pia itakuwa ni ya juu, na irabu ya mzizi ikiwa ni ya kati basi irabu ya utendea pia itakuwa ya kati,na irabu ya chini siku zote inaonekana kuwa ni ya juu.
Kanuni.
+sila +juu +sila
-kons -nyuma -kati
-juu +K
-nyuma +sila
- chini -juu
-chini
Utamkaji pamwe wa nazali.
Huu ni mchakato ambapo katika mkururo wa nazali na konsonanti hupelekea nazali kuathiriwa na konsonanti inayofuatana nayo. Usilimisho huu hutokea pale ambapo nazali hufuata mahali pa matamshi pa konsonanti inayofuatana nayo. Mifano yake ni kama ifuatayo;
umbo la ndani
umbo la nje
/n+buzi/
[mbuzi]
/n+bwa/
[mbwa]
/n+bu/
[mbu]
/n+gongo/
[mgo go]
/n+gozi/
[ gozi]
/n+vua/
[ vua]
Hivyo katika mifano hii tunaona kuwa nazali zimebadilika kwa kufuata mahali pa matamshi pa konsonanti zilizokaribiana nazo. Mfano /n+gozi/ imebadilika kuwa [ɳgozi] ambayo huweza kuoneshwa kwa kanuni ifuatayo;
/n / [ ] /g/
Kanuni ya jumla.
+kons +kons
-sila [ mahali] -sila
+naz mahali
Kwa kuhitimisha tunaona kuwa michakato ya kiusilimisho katika lugha ya Kiswahili ipo na inatumika kukokotoa umbo la ndani kwenda umbo la nje. Huweza kufanya mabadiliko ya karibu au moja kwa moja kuliko michakato isiyo ya kiusilimisho ambayo haionyeshi mabadiliko ya moja kwa moja.