Monday

FONOLOJIA NA FONETIKI

0 comments

 SURA YA KWANZA




1:0 FONOLOJIA NA FONETIKI


1: 1 Fonolojia (Phonology)


Fonolojia ni nini?


Ni tawi mojawapo katika taaluma ya isimu linalojumuisha vipengele vya matamshi, mkazo,kiimbo, lafudhi, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu, mfuatano wa mofimu katika kuunda maneno na tahajia / otografia zake.


Fonolojia ni tawi la taaluma ya isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi, na uanishaji wa sauti pambanuzi katika lugha mahususi. Tawi hili hujishughulisha na sauti ambazo hutumika kutofautisha maana za maneno katika lugha maalum / mahususi. Fonolojia hujihusisha na sheria / kanuni zinazoandamana na utoaji wa sauti pamoja na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi.


Fonolojia imejikita katika lugha maalum ikichunguza namna binadamu anavyotamka sauti na kuziunganisha ili kuleta maana katika lugha maalum inayohusika.



1:2 Fonetiki (Phonetics )


Ni taaluma inayoshughulika na sauti zinazotumika katika lugha mbalimbali duniani. Ni tawi la isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi wa taratibu zote zinazotumika au zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasiri wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla.


Fonetiki huchunguza maumbo mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa au kuzalishwa na alasauti za binadamu. Tawi hili huchunguza namna maumbo hayo yanavyotolewa, yanavyomfikia msikilizaji na jinsi yanavyofasiliwa au yanavyotafsiriwa katika ubongo wa binadamu bila kujali sauti hizo zinatumika katika lugha ipi.


Fonetiki imegawanyika katika matawi manne katika uchunguzi wake wa sauti hizo zinazotolewa na alasauti. Matawi hayo ndiyo yanayokamilisha kazi ya fonetiki katika isimu.


1:2:0 Matawi ya Fonetiki


1:2:1 Fonetiki Matamshi (Articulatory Phonetics )


Hili ni tawi la isimu ambalo linashughulikia jinsi sauti mbalimbali za lugha zinavyotamkwa kwa kutumia alasauti za lugha za binadamu. Tawi hili huchunguza namna utamkaji wa sauti unavyofanyika na mahali pa kutamkia sauti hizo. Mchakato wa tawi hili unaonekana kupitia jedwali la Alfabeti za Kifonetiki la Kimataifa ( International Phonetiki Alphabet <IPA>). Jedwali la konsonanti la alfabeti za kifonetiki la kifamataifa lipo kama ifuatavyo. Thorne (1997).

 




1

 


Kielelezo na: 1


Jedwali la Konsonanti la Alfabeti za Kifonetiki la Kimataifa

JINSI YA

MATAM MAHALI PA KUTAMKIA / MATAMSHI

SHI

Mido Mido Meno,Uf Kipind Kaak Kaak Kaak Kida Mido Mido kishi Korom

mo mo- izi- uka aa aa aa ka mo- mo- mo eo

Meno Meno,Ba gumu gumu laini Tong kaakaa kaakaa

ada ufizi -ufizi e- gumu laini

Kaak

aa

laini

Nazali ɲ ŋ

m ɱ n ɳ N

Vipasuo

p   b t d ʈ ɖ c   ɟ k  g q  ɢ ʔ

Vikwamiz θ ð

i ɸ   β f v s z s ʃ   Ʒ ç   j x   ɤ χ   ᴚ ʍ ħ   ʕ h   ɦ

Vizuio- ɥ

Kwamizi υ ɹ ɻ j ɰ

w

Vitambaz

a-

Kwamizi ɺ ʙ

Vitambaz l ɭ ʎ

a

Vimadend

e r ʀ

Vipigo ɾ ɽ ʀ

Ijektivu ť

Implosivu ɖ ɠ

ɓ

Vidoko- ͽ ʇ c

Kati

Kitambaz ʖ

a-Kidoko





1:2:2 Fonetiki Akustika / Fonetiki Mawimbisauti / Safirishi (Acoustic Phonetics)


Ni tawi ambalo hushughulika zaidi na jinsi ya mawimbi ya sauti za lugha yanavyoweza kusafirisha sauti hizo. Fonetiki Akustika hushughulikia jinsi mawimbi ya sauti yanavyosafirisha sauti kutoka katika kinywa cha msemaji kwenda kwenye sikio la msikilizaji na akili ya msikilizaji na kufanya masikilizano kuwepo.


Sauti husafirishwa na mawimbi kutoka kwa msemaji na kumfikia msikilizaji . Massamba na wenzake (2004)






2

 

1:2:3 Fonetiki Masikizi (Auditory Phonetics)


Ni tawi linaloshughulikia jinsi ya utambuzi wa sauti mbalimbali za lugha unavyofanyika. Fonetiki Masikizi huonesha uhusiano uliopo kati ya sikio, neva masikizi na ubongo. Huchunguza jinsi sikio, neva msikizi na ubongo vinavyohusiana na kufanya kazi katika mchakato wa utambuzi wa sauti Thorne (1997).


Mifano na: 1

Sauti   [b] [a] [r] [g]

[+kons ] [+sil ] [+ghun ] [+ghun ]

[+ghun ] [+ghun ] [+kont ] [+kor ]

[+mid ] [+chin ] [+mad ] [+kons ]

[-kont ] [+son ] [+ant ] [- kont ]





1:2: 4 Fonetiki Tibamatamshi / Majaribio (Experimental Phonetics)


Fonetiki tibamatamshi ni tawi linaloshughulikia matatizo yanayoambatana na usemaji au utamkaji wa sauti na jinsi ya kuyatatua. Mfano tatizo la mtu kuzaliwa na paa la kinywa / kaakaa lililogawanyika ambalo huathiri matamshi katika usemaji wake. Vile vile watu wanaozaliwa na tatizo la mdomo juu kugawanyika hushindwa kutamka vizuri sauti zinazotamkiwa katika midomo.


Lengo kuu la tawi hili ni kujaribu kuchunguza na kutafuta jinsi ya kuwasaidia watu wenye matatizo hayo. Massamba na wenzake (2004)



1: 3 Usuli wa neno Fonetiki (Background of Phonetics)


Fonetiki ni sayansi ya lugha inayoshughulikia sauti za lugha mbalimbali zinazotolewa na kinywa cha binadamu. Tunapozungumzia usuli wa fonetiki tuna maana ya usuli wa jedwali la alfabeti za kifonetiki za kimataifa (International Phonetic Alphabet <IPA>).


Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa (AKK) ni wazo la kuunda alfabeti za kifonetiki ambalo lilifikiwa baada ya kugundua kuwa alfabeti za lugha ya Kirumi zilizotumika kurekodi lugha ya maandishi ya Kiingereza hazikukidhi au hazikuakisi uhalisia wa lugha hiyo. Wanaisimu waliamua kuunda au kutengeneza kielelezo kingine cha alfabeti kiitwacho Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa ambacho kinajaribu kuonesha kila tofauti ya sauti hizo. Kielelezo hicho kilipendekezwa kwa mara ya kwanza na Otto Jespersen kati ya mwaka 1860 – 1943. Mwaka 1886 mchakato wa kuandika kielelezo hicho ulianza. Mwaka 1888 kielelezo cha kwanza cha Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa (AKK) (International Phonetic Alphabet <IPA> ) kilichapishwa.


Lengo la mfumo au mchakato huo lilikuwa ni kuunda maumbo au viwakilishi vya sauti ambavyo vinawakilisha sauti husika. Maumbo hayo ya sauti hutofautiana kutoka sauti moja kwenda sauti nyingine, ambayo pia yataweza kutumika katika lugha yoyote ile ambamo sauti husika inatumika. Thorne (1997)

 




3

 


Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa zimeweza kutumika katika lugha mbalimbali, na matumizi yake kupanuka mara nyingi sana hususani mwaka 1989 katika isimu ya lugha. Hadi hivi sasa bado wanaisimu duniani kote wanatumia kielelezo hiki na ndicho hukubalika zaidi katika miaka ya sasa katika isimu.


Kazi ya kielelezo hiki cha Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa  au IPA ni:

Kupambanua kila sauti kulingana na jinsi inavyotamkwa


Kurekodi sauti za maneno kiuhalisia, kitu ambacho huwasaidia wanaisimu kutofautisha maneno yanayoonekana katika tahajia ya kifonetiki lakini sauti


zinatofautiana


Maneno hupambanuliwa kifonetiki kwa kuyafungia katika mabano ya mraba ili kuonesha kwamba mkazo uko kwenye sauti hizo na jinsi zinavyoundwa wakati wa utamkaji.


Mifano na: 2


Anacheza  [anaʧεza] au [anačεza]

(ii) Ngugu [ndugu  ]


Ghala[ɤala]

(iv) Dawati [dawati ]


Fonetiki kama taaluma ya sayansi inayochunguza namna ya sauti zinavyoweza kuzalishwa kusafirishwa na jinsi zinavyoweza kufasiliwa ama kutafsiriwa kwa kutegemea alasauti za binadamu ambazo ndizo huzalisha sauti hizo. Alasauti hizo ni midomo, meno, ulimi, kaakaa gumu kaakaa laini, ufizi, koromeo, kidaka tonge nakadhalika.



1:4 Alasauti za Lugha.(Speech Organs)


Alasauti za lugha ni viungo mbalimbali maalum vya mwili wa binadamu. Viungo hivi ni muhimu sana katika sayansi ya lugha hususani katika tawi la fonetiki na fonolojia. Viungo hivi hutumika kuunda au kuzalisha sauti mbalimbali ambazo hushughulikiwa katika tawi hili la fonetiki katika isimu ya lugha. Massamba na wenzake (2004)


Alasauti hizi ni mapafu ambayo hufanya kazi ya kuvuta hewa ndani na kutoa nje ya kifua cha binadamu kupitia katika chemba ya kinywa au chemba ya pua. Umio ,koromeo ni aina nyingine ya alasauti ambayo huwa na namna fulani ya kambakamba ya nyama laini zinazoitwa nyuzisauti. Nyuzisauti zina uwazi katikati unaoruhusu hewa kutoka nje ya kifua cha binadamu na kuingia ndani ya mapafu ya binadamu. Nyuzisauti zinapokuwa zimeachana hewa hupita kwa urahisi kwenda nje na hivyo kusababisha sauti zinazotamkwa kutokuwa na mtimbwiliko mfano sauti [t],[p] nakadhalika. Lakini zinapokuwa zimekaribiana au zimegusana hewa kutoka mapafuni hulazimika kuzisukuma ili kuziachanisha na kusababisha sauti zinazotamkwa kuwa na mtimbwiliko mfano sauti [r], [b] nakadhalika.


Alasauti nyingine ni kinywa ambacho kinajumuisha ulimi, kaakaa gumu, kaakaa laini, ufizi, na meno. Ulimi una sehemu kuu tatu; sehemu ya mbele ambayo inajumuisha incha ya ulimi ambayo hukutana na alasauti ama viungo vingine kama meno, ufizi,kaakaa gumu,kaakaa laini ili kutamka sauti [t], [d], [θ], [i] na kadhalika. Kiwiliwili au bapa la

 




4

 


ulimi (ulimi kati), sehemu hii hutusaidia kutamka sauti kama [ɜ:],[ə], [ʌ] na kadhalika katika fonetiki. Shina la ulimi au ulimi nyuma, sehemu hii hutuwezesha kutamka sauti kama [k],[g],[ɑ], [ɒ],[ͻ] na kadhalika ambapo ulimi nyuma huinuka na kukutana na

kaakaa laini kisha sauti kutamkwa.


Katika kaakaa gumu ambalo hufuata mara tu baada ya ufizi, kiungo hiki ndipo sauti [j],[ ɟ], [ɲ], [ʧ],[ʤ] na kadhalika hutamkiwa hapo. Ufizi ni kiungo kingine ambacho kwacho sauti [t], [d],[s],[z],[ɗ],[ɾ] na kadhalika huweza kutamkwa. Ufizi unajumuisha sauti zinazotamkiwa hapo kama [t],[d] pamoja na zile zinazotamkiwa baada ya ufizi kama [r] na kadhalika.


Kaakaa laini ni kiungo ambacho hufuata mara tu baada ya kaakaa gumu. Katika kiungo hiki sauti kama [k], [g], [x], [ ɤ], [ɠ],[ŋ] na nyingine nyingi hutamkiwa hapo. Meno, katika kiungo hiki sauti za [θ],[ð] meno juu na chini yanapokutana, na ncha ya ulimi hupita kati ya meno hayo ya juu na ya chini kwa haraka na kujiburuta kuelekea kwenye ufizi. Kupitia meno hayo hayo ya juu na mdomo chini sauti [f],[v], [υ], na [ɱ] hutamkwa.


Katika viungo hivi midomo kama alasauti huhusika na utamkaji wa sauti za [p], [b], [m], [ɸ], [β], [ɓ] na [w].


Viungo hivi vya binadamu vilivyotajwa hapo juu vina umuhimu sana katika lugha ya binadamu. Binadamu hutegemea uhai wa viungo hivyo ili aweze kuzalisha sauti mbalimbali. Katika fonetiki sauti zote zinazotolewa na kinywa cha binadamu zina sifa nyingi sana kama vile sauti kuwa na msikiko mkubwa au hafifu [+ghun] au [- ghun], sauti kuwa na sifa ya usilabi au la [+sil] au [- sil]. Alama ya [+] ina maana ya sifa hiyo ipo kwa kitamkwa husika na alama ya [-] ina maana ya kutokuwepo kwa sifa hiyo kwa kitamkwa husika.


Mchakato wa kuzibainisha sauti hizi unategemea sifa za sauti hizo. Hebu chunguza


mifano ifuatayo hapa chini;

Mifano  na: 3

[b] [i]

[ +kons ] [+sil ]

[+ghun ] [+juu ]

[+mid ] [+ghun ]

[-sil ] [-kons ]



Baada ya kueleza alasauti za lugha zinazohusika katika utamkaji wa sauti hapo juu hebu sasa angalia na kuchunguza kielelezo cha alasauti kifuatacho hapa chini.

 















5

 

Kielelezo  na: 2


ALASAUTI  ZA LUGHA































Ufunguo wa alasauti Ufunguo wa mahali pa matamshi.

1. Midomo A. Midomo

2. Meno B. Midomo - meno

3. Ufizi C. Meno

4. Ulimi D. Ufizi

5. Kaakaa gumu E. Ufizi – kaakaa gumu

6. Kaakaa laini F. Kaakaa gumu

7. Kidaka tonge G. Kaakaa laini

8. Chemba ya pua H. Glota /Koromeo

Koromeo


Nyuzisauti



Katika kielelezo hicho hapo juu ulimi umegawanywa katika sehemu kuu nne yaani ncha ya ulimi, sehemu ya mbele ya ulimi (ulimi mbele), ulimi kati (kiwiliwili cha ulimi) na ulimi nyuma (shina la ulimi). Kutokana na kielelezo hicho pamoja na ufunguo wake unaweza kupata picha kamili kuhusu alasauti katika mwili wa binadamu, pia unaweza kugundua jinsi viungo hivyo vinavyotenda kazi katika lugha. Kupitia alasauti hizi binadamu ana uwezo wa kuzalisha sauti mbalimbali kama inavyoonekana katika kielelezo namba 1 cha jedwali la Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa (AKK).

 




6

 


Uzalishaji wa sauti hizo hutegemea uhai wa alasauti. Kama alasauti hususani ulimi ukashindwa kufanya kazi, basi mtu wa namna hiyo hawezi kuzalisha sauti za aina yoyote ile kama inavyoonesha katika kielelezo namba 1.


Alasauti za lugha za binadamu zimegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza linajumuisha alasauti kaakaa gumu, ufizi, na meno juu. Alasauti hizi zinaitwa alatuli. Kundi la pili linajumuisha ulimi, midomo, meno chini, kaakaa laini, kidaka tonge na nyuzisauti ambazo huitwa alasogezi.


Alatuli ni alasauti ambazo hufuatwa na alasogezi wakati wa utamkaji wa sauti mbalimbali. Alasogezi ni alasauti ambazo huzifuata alatuli ama hukutana zenyewe kwa zenyewe wakati wa utamkaji wa sauti mbalimbali za lugha za binadamu.


Baada ya kueleza kwa kirefu dhana ya fonetiki na vipengele vyake katika sura hii, sura inayofuata nitaeleleza kwa mawanda mapana dhana ya fonolojia.






Zoezi


Eleza tofauti iliyopo baina ya istilahi “fonetiki” na “fonolojia”. Kwa kuzingatia utendaji kazi wake katika lugha.


Eleza dhima ya Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa katika taaluma ya isimu.


Ni tofaauti gain iliyopo kati ya fonetiki matamshi na fonetiki masikizi?


Kwa kutumia kielelezo namba 1 eleza alasauti zinazohusika katika utamkaji wa sauti zifuatazo: [γ], [x], [ʀ], [ʁ],[ʤ],[ɱ], [ɸ],[β],[ɒ],[ɑ] na[υ].

 






























7

 

SURA YA PILI


2:0 FONOLOJIA


Katika sura iliyopita ya kwanza nimegusia fasili ya fonolojia. Nimeeleza kuwa Fonolojia ni tawi la taaluma ya isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uanishaji wa sauti pambanuzi za lugha maalum au mahususi.


Massamba, D.P.B, Kihore, Y.M na Msanjila, Y. P katika kitabu chao cha Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA) (2004) wanasema;


“ Fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi,uchambuzi, na uanishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu .”


Fonolojia hujishughulisha na sheria ama kanuni zinazoandamana na utoaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi. Fonolojia hujishughulisha na vipengele mbalimbali vinavyohusiana na sauti na mpangilio wake, vipengele hivyo ni lafudhi, matamshi, mfuatano wa sauti hizo katika kuunda silabi, kiimbo, mkazo, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu na maneno pamoja na tahajia za vipashio hivyo.



2:1 Usuli wa Neno Fonolojia


Neno fonolojia (phonology) linatokana na maneno mawili. Maneno hayo ni foni (phone) lenye maana ya sauti na neno logos lenye maana ya neno au maneno.


Kutokana na maneno hayo mawili wanaisimu wakaunda neno fonolojia (phonology) lenye maana ya taaluma inayoshughulikia kanuni zinazoonesha uathiriano wa sauti, mfuatano wa sauti na kutofautiana kwa baadhi ya vitamkwa.


Mfano katika lugha ya Kiswahili mfuatano unaokubalika ni ule wa konsonanti,kiyeyusho na irabu katika maneno kama kwani, upya, bwawa. Lakini mfuatano wa konsonanti tupu haukubaliki katika lugha ya Kiswahili.


Muathiriano wa vitamkwa au sauti tunaangalia au tunachunguza kwa kulinganisha vitamkwa hivyo kutokana na matumizi yake katika lugha maalum ambamo zinatumika sauti hizo ama vitamkwa hivyo. Katika taaluma ya fonolojia kipashio cha msingi kabisa ni fonimu.


Mfano neno baba na bata, sauti zilizoandikwa kwa wino mzito na kupigiwa mstari katika jozi hiyo hapo juu ambazo ni sauti /b/ na /t/ ni fonimu ambazo zinasababisha maana za maneno hayo mawili kutofautiana.



2:2 Historia ya Fonolojia


Taaluma ya fonolojia ilianza mnamo karne ya kumi na tisa baada ya Kristo (19 B.K). Wanaisimu walianza kwa kuichunguza lugha katika tawi hili la fonolojia walichukua sauti kwa kulinganisha ili wautafute mzizi wa lugha. Lengo lao lilikuwa ni kujua mzizi

 



8

 


wa lugha ni upi. Katika uchunguzi au utafiti huo walitumia lugha ya Kiindonesia kama lugha ya utafiti. Katika lugha hiyo waliangalia mfanano na tofauti za sauti ama vitamkwa.


Wanaisimu hawa waligundua kuwa kuna maneno yanayofanana kisauti na yana maana sawa au moja. Mfano lugha ya Kifaransa neno pere lenye maana ya baba ambalo ni sawa na father katika lugha ya Kiingereza ambazo ni lugha za jamii mbili tofauti.


Vile vile lugha za Kirumi na Kijerumani zilifanyiwa utafiti ama uchunguzi. Wanaisimu hawa walifanya uchunguzi katika lugha hizo yaani Kirumi na Kijerumani ili kujua kama kuna mabadiliko yoyote yanayojitokeza au hakuna mabadiliko


yanayojitokeza katika lugha hizo. Fonolojia imeweza kuchunguzwa na wataalam mbalimbali ambao wanajulikana kama waasisi wa fonolojia.





2:3:0 Waasisi wa Fonolojia


Kuna waasisi wengi ambao ndilo chimbuko la taaluma hii ya fonolojia. Kundi hili linajumuisha Baudouin de Courtenay, Ferdinand de Saussure, Nicolai Trubetzkoy, Daniel Jones pamoja na Noam Chomsky na mwenzake Morris Halle.



2:3:1 Baudouin de Courtenay 13 Machi 1845 – 3 Novemba 1929


Huyu ni Mfaransa aliyebainisha taaluma ya foni (phone). Courtenay alibainisha mfumo wa sauti za lugha, katika ubainishaji wake alitumia istilahi za anthropofoniksi (anthropophonics), taaluma inayohusu matamshi yaani fonetiki na saikofoniksi (psychophonics) taaluma inayohusu sauti katika lugha yaani fonolojia. Courtenay alitumia istilahi hizo badala ya istilahi za foni katika taaluma ya fonetiki au kumaanisha fonetiki na fonimu katika taaluma ya fonolojia yaani saikofoniksi ina maana ya fonolojia.


Courtenay alitumia istilahi ya anthropofoniksi kwa sababu istilahi hii inahusika katika kumwelewa binadamu na ni taaluma inayomtofautisha binadamu na wanyama wengine.


Vile vile Baudouin de Courtenay alitumia istilahi saikofoniksi kwa sababu inahusika na saikolojia (akili). Courtenay anasema sauti zinapatikana katika ubongo wa binadamu, hivyo binadamu kile anachofikiri ndicho anachokisema. Baudouin de Courtenay anatoa fasili ya fonimu kama ifuatavyo;


Kisaikofoniksi Courtenay anaifasili fonimu kama hivi,


“Fonimu ni tukio la akilini ambalo huwa na nia ya mzungumzaji au jinsi msikilizaji anavyomwelewa mzungumzaji au vyote viwili kwa pamoja.”


Courtenay anaendelea kusema kuwa hata hivyo ;


“ watumiaji huwa na taswira ya kila fonimu akilini mwao”

 







9

 


Kutokana na maelezo ya Baudouin de Courtenay fonimu inachukuliwa kama taswira iliyoko katika akili ya mtu. Hili analithibitisha katika fasili yake hii.


“ Fonimu ni dhana ya kisaikolojia. Ni kipandesauti ambacho picha yake iko au huwa akilini mwa mtu na hukusudia aitoe anapoongea.”


Hivyo basi kutokana na fasili ya Baudouin de Courtenay fonimu inaweza kufasiliwa kama ni:


“ picha, taswira ya sauti ambayo huwa akilini mwa mtu au watu, wazungumzaji au wasikilizaji wa lugha fulani.”



2:3:2 Ferdinand de Saussure 26 Novemba 1857 – 22 Februari 1913


Huyu ni Mfaransa na mtaalam wa isimu. Saussure anadaiwa kuwa ndiye baba wa isimu ya kisasa (Modern Lingustics) kwa sababu mwanzoni kulikuwa na isimu linganishi tu.


Saussure alingundua kuwa kuna sayansi maalum inayotumika katika lugha. Anadai kuwa sayansi hiyo huthibitika kupitia vitu vikuu viwili ambavyo ni:


langue → Mfumo wa lugha (umilisi) ambao ndiyo fonolojia ya lugha yenyewe.


parole → Utendaji wa lugha ambao ndiyo fonetiki ya lugha.


Saussure anasema kwamba katika lugha, matamshi humfanya mtu asikike au aweze kusikika. Lugha iko ndani na matamshi yako nje.


Saussure anaonesha kuwa katika lugha, akili ya mtu hufikiri kile kinachokusudiwa kuzungumzwa au kusemwa na matamshi hukitoa kile kinachofikiriwa kusemwa akilini mwa binadamu. Hebu angalia kielelezo kifuatacho kinachoonesha mnyororo wa mchakato mzima katika usemaji.


Kielelezo na: 3


A. Kusudio akilini B. Akilini matamshi





D. Embe C. Matamshi ya makusudio


Ferdinand de Saussure ndiye mtu wa kwanza kuleta dhana ya alama katika lugha kwamba kuna vitu vitatu vya msingi katika lugha. Sausssure anasema ni lazima kuwepo na neno ambalo ndiyo alama yenyewe, pia kunakuwa na dhana inayotokana na alama ambayo mtu huiona ama kuisikia pamoja na kitajwa ambacho ni kitu halisi ambacho taswira yake iko akilini mwa binadamu. Saussure alileta dhana hii kwa sababu aliona

 





10

 


hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya matamshi na kitajwa kama itakavyooneshwa kupitia kielelezo hapa chini.


Kielelezo na: 4 Dhana








Neno Kitajwa


Ferdinand de Saussure ana mchango mkubwa sana katika lugha. Katika uanazuoni wake na utaalam wake ametoa mchango mkubwa sana juu ya dhana ya sinkronia (synchrony),na dayakronia (diachrony). Katika upande wa dhana ya sinkronia Saussure anasema :


“Lugha ni mfumo wa ishara ambazo husomwa kama mfumo kamili wa lugha katika kipindi fulani cha muda.”


“Language as a system of signs be studied as a complete system at any given point of time.”


Saussure anasema sinkronia (synchrony) inahusiana na vitu viwili vinavyoshabiana vinavyotumika au vinavyokuwepo kwa wakati mmoja.


Kuhusu  dayakronia (diachrony) Saussure anasema ni:


“ mabadiliko katika maana za maneno kutokana na muda unavyopita” au


“ ni badiliko la maana za maneno kutokana na vipindi mbalimbali vya muda vinavyopita.” Thorne (1999:102)


Uhusiano wa dayakronia ni pale vitu viwili au vinavyoshabihiana kutokea tofauti tofauti kwa muda.


Kutokana na fasili za Saussure kuhusu lugha zinaonesha kwamba lugha inapokea mabadiliko kutokana na muda unavyopita. Lakini pia Saussure anaifasili sauti ama fonimu inatokana na kusudio la mzungumzaji ambalo limo akilini mwake.



2:3:3 Nikolai Trubetzkoy 15 Aprili 1890 - 25 Juni 1939


Nikolai Trubetzkoy ni mtaalam wa isimu katika shule ya Prague- Moscow huko Urusi. Huyu ni mwanzilishi wa taaluma ya fonolojia kwa kutumia misingi ya Ferdinand de Saussure. Trubetzkoy ni wa kwanza kuifasili dhana ya fonimu. Trubetzkoy anasema:


“Fonimu haiwezi kufasiliwa kikamilifu ama kwa kutumia kigezo

 




11

 


cha sifa za kisaikolojia au sifa za kifonetiki bali ni lazima ifasiliwe kwa kutumia sifa za uamilifu wa fonimu hiyo katika mfumo wa fonolojia ya lugha maalum inamotumika.”


Trubetzkoy anaifasili fonimu hivi:


“Fonimu ni jumla ya sifa zote za kifonolojia au za kiuamilifu zinazohusu fonimu Fulani.”


Fasili hii inapatikana katika kitabu chake kiitwacho Principles of Phonology (1939) kinachoeleza maana ya fonimu.


Vile vile Trubetzkoy amebainisha tofauti kati ya fonetiki na fonolojia kwa kueleza dhima ya fonetiki na fonolojia katika lugha ya binadamu. Trubetzkoy anasema:


“ Fonetiki inahusu uzalishaji, mawimbi ya sauti, usafirishaji na upokeaji wa sauti za lugha.”


wakati


“Fonolojia inaeleza au inapambanua jinsi sauti zinavyofanya kazi katika lugha fulani au kupitia lugha ili kutoa maana.”


Kwa ujumla Trubetzkoy anaonesha kuwa fonolojia inahusika na sauti zenye maana tu katika lugha maalum, wakati fonetiki inashughulikia sauti zote katika viwango vya namna sauti hizo zinavyozalishwa au zinavyotamkwa, mawimbi ya sauti yanavyozichukua na kuzisafirisha, na jinsi zinavyopokelewa na kufasiliwa.



2:3:4 Daniel Jones 12 Juni 1881– 04 Desemba 1967


Daniel Jones ni mwanaisimu ambaye ametoa mchango wake mkubwa katika taaluma ya fonolojia. Jones alisoma shahada yake ya kwanza ya hesabu, shahada yake ya pili au ya uzamili alisomea sheria na shahada yake ya tatu au ya uzamivu alisomea lugha.Jones ni mmoja wa waanzilishi wa jedwali la Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa (AKK). Jones ameandika kwa mara ya kwanza nadharia ya fonimu. Mtaalam huyu aliiangalia fonimu katika pande kuu mbili ambazo ni kifizikia na kisaikolojia.


1) Kifizikia


“Fonimu inaonekana kama kitita cha sauti mbalimbali ambazo hutumika kwa lengo moja na kutazamwa kwa maana moja, kama sauti moja.”

Mifano na:1



Fonimu [t] ………………. …..[ṭ]


…………………...[ṱ]

……………………[ț]

 




12

 

Sauti [ț], [ṱ] na [ṭ] ni alofoni za fonimu [t] kifizikia.


Mfano na: 2

Maneno matamshi

1. thelathini [θɛlaθini ]

selasini [sɛlasini  ]


Sauti [θ] na [s] ni alofoni za foninimu [θ]


2. rafiki [rafiki ]


lafiki [lafiki ]


Sauti [r] na [l] ni alofoni za fonimu [r].



Kisaikolojia


“ Sauti iko katika akili ya binadamu, maamuzi katika akili za binadamu. Sauti hizi pia hutokana na makubaliano ya wanajamii katika uteuzi wa sauti za kutumia katika lugha yao.”


Mfano katika lugha ya Kiswahili kuna sauti kama [b], [a],[ɛ], [ɤ], [p],[č] na nyingine nyingi ambazo jumla yake ni thelatini na sita (36).


Kwa mujibu wa Jones fonimu inaonekana kuwa ni zile sauti zote zinazokubaliwa na jamii ya watu ili wazitumie katika lugha yao. Fonimu hizi huwa akilini mwa binadamu ambamo maamuzi ya kuzitumia sauti hizo yamo.



2:3:5 Noam Chomsky 7 Desemba 1928 na Morris Halle 1923


Wataalam hawa wameandika fonolojia zalishi. Chomsky na Halle wanaichukua fonimu kama kitita cha sifa bainifu. Chomsky na Halle wanasema kila sauti ina sifa zake bainifu.


Mifano na: 3

Sauti [i] [b] [m]

[+sil ] [+kons ] [+naz ]

[+ir ] [+mid ] [+kons ]

[+juu ] [+ ghun ] [+ghun ]

[+kont ] [+ant ] [+ant ]

[-kons ] [-kont ] [+mid ]


Baada ya kueleza historia ya fonolojia kwa kirefu na waasisi wake imebainika kuwa waasisi hawa wengi au wote wameshughulikia fonimu ambacho ni kipashio kidogo kabisa katika taaluma ya fonolojia na foni katika taaluma ya fonetiki. Wataalamu hawa wako katika makundi makuu matatu ambayo ni ya kisaikolojia, kifonetiki na kifonolojia.

 





13

 


Courtenay, Saussure na Jones, wao wanaitazama fonimu kama picha ama taswira iliyo katika akili ya binadamu ambamo maamuzi ya kuzitumia fonimu hizo yamo.


Trubetzkoy anaitazama fonimu kifonolojia kwamba fonimu ina sifa za kiuamilifu au za kifonolojia katika mfumo wa lugha maalum. Wakati Chomsky na Halle (1968) wanaitazama fonimu kifonetiki kwamba fonimu ni kipashio chenye kitita cha sifa bainifu. Kwa ujumla wataalam hawa wametupa picha kamili kwamba fonimu ni sauti zinazotumika katika mfumo wa lugha maalum.



2:4 Uhusiano uliopo kati ya Fonetiki na Fonolojia


Fonetiki na fonolojia ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutenganishwa kamwe. Fonetiki ina mchango mkubwa sana katika taaluma ya fonolojia. Kwa maneno mengine naweza kusema kwamba fonolojia ya lugha maalum haiwezi kuwepo endapo fonetiki haitakuwepo. Usemi huu unathibitika katika misingi au kwa sababu zifuatazo:


Sauti zinazoshughulikiwa katika taaluma ya fonolojia zimechotwa au zimechukuliwa kutoka katika taaluma ya fonetiki ndani ya jedwali la alfabeti za kifonetiki za kimataifa (AKK) Thorne(1997) kwa upande wa sauti konsonanti na viyeyusho. Irabu nazo zimechukuliwa kutoka katika kielelezo trapeziam ya irabu msingi, sauti ziitwazo foni. Kwa maana nyingine fonimu zote za lugha ni foni zilizochukuliwa kutoka katika taaluma ya fonetiki. Hivyo basi fonolojia hutegemea sauti zilizoko katika taaluma ya fonetiki ndani ya AKK na Trapeziam ya irabu msingi.


Ubainishaji wa fonimu katika taaluma ya fonolojia hutumia sifa bainifu au pambanuzi zilizoanishwa katika taaluma ya fonetiki, hususani tunapochunguza sifa za fonimu za jinsi ya matamshi, na mahali pa matamshi, mwinuko wa ulimi, sehemu za ulimi na mkao wa midomo wakati wa utamkaji. Ni dhahiri kwamba fonimu zina sifa bainifu za kifonetiki ambazo zinazitofautisha fonimu moja hadi nyingine, lakini ili iitwe fonimu ni lazima iwe na uamilifu katika lugha maalum. Kupitia kielelezo cha trapeziam ya irabu msingi utagundua sehemu za ulimi zinazohusika pamoja na miinuko yake. Hebu chunguza kwa makini kielelezo hicho.


Kielelezo na: 5  Trapeziam ya irabu msingi.

 























14

 


Sifa za fonimu za kifonetiki zinatupatia makundi asilia ya fonimu katika taaluma ya fonolojia. Katika taaluma ya fonolojia ya lugha kuna fonimu ama vitamkwa konsonanti, irabu, na viyeyusho na ndani ya fonimu hizi kuna makundi asilia ya vipasuo,vikwamizi, vilainisho, nazali, irabu pamoja na viyeyusho ambavyo vimegawanywa kwa misingi ya kifonetiki.


Taaluma ya fonetiki inatupatia sifa za msingi za fonimu ambazo ni usonoranti, ukontinuanti, usilabi,unazali, uanteria ukosonanti na kadhalika. Na kutokana na sifa hizi makundi makuu ya fonimu hupatikana. Mfano irabu zote zina sifa ya usilabi.


Kutokana na sifa za kifonetiki bado fonolojia inaangalia uamilifu wa fonimu na mabadiliko yake katika mfumo wa lugha maalum. Vile vile fonolojia hutoa kanuni za kiuandishi na kuonesha umilisi wa lugha na utendaji.



2:5 Tofauti kati Fonetiki na Fonolojia


Fonetiki Fonolojia

1.Ni  taaluma  inayoshughulikia  sauti zote Ni taaluma inayoshughulikia sauti

zinazotolewa na alasauti za binadamu bila zinazotumika  katika  lugha  maalum  au

kujali lugha maalum. mahususi.

2. Kipashio chake cha msingi ni foni. Kipashio chake cha msingi ni fonimu.

3.Fonetiki inahusu sauti zote zinazotolewa Fonolojia inahusu vipashio vyenye maana

au   zinazozalishwa   katika   kinywa   cha katika lugha yaani fonimu, silabi, kiimbo,

binadamu. toni, lafudhi nakadhalika.

4.Fonetiki inaangaliwa kama taaluma Fonolojia inachukuliwa kama umilisi kwa

inayohusu utendaji zaidi, fonetiki maana kwamba ni taaluma inayotoa uwezo

inaangalia namna sauti zinavyoundwa, wa kujua kanuni za sauti za lugha katika

katika kinywa cha binadamu, mfuatano wa kuunda silabi, na kutofautiana

zinavyosafirishwa,zinavyosikika na kwa  fonimu  au  vitamkwa  hivyo  katika

zinavyofasiliwa. lugha maalum.

5.  Fonetiki  inasaidiwa  au  inahusiana  na Fonolojia   inahusiana   na   taaluma   za

taaluma  za  fizikia  na  fiziolojia  (sayansi nyingine za fonetiki, mofolojia,

halisi). sintaksia,semantiki na taaluma ya

saikolojia.



Fonolojia ni taaluma ambayo imejikita katika lugha maalum, ni tawi linaloshughulikia sauti zenye maana katika lugha maalum inayohusika. Katika sura hii tumeweza kuona jinsi wataalam mbalimbali walivyoitazama fonolojia katika mitazamo tofauti tofauti lakini wote wakichunguza sauti au fonimu. Wengine wetumia kigezo cha kisaikolojia ,wengine kigezo cha kifonetiki na wengine kigezo cha kifonolojia lakini wakichunguza sauti zinazotumika katika lugha mbalimbali.


Baada ya kueleza kwa kirefu historia ya fonolojia katika sura hii na kuona jinsi ilivyoshughulikiwa na wataalam mbalimbali na kuitazama fonimu kwa upana tumegundua kuwa fonimu ina alofoni zake kwa mujibu wa Danel Jones(1918). Lakini Noam Chomsky na Morris Halle (1997) wanasema fonimu lazima iwe na sifa bainifu au

 




15

 


pambanuzi. Vile vile Trubetzkoy anasema lazima fonimu iwe na sifa za uamilifu katika lugha inamotumika fonimu husika.


Kwa kuhitimisha sura hii ni kwamba fonolojia inahusika na vipashio vyenye maana tu katika lugha maalum. Kwa sababu hiyo kuna fonolojia mbalimbali za lugha kama vile fonolojia ya Kiswahili, fonolojia ya Kiingereza, fonolojia ya Kifaransa nakadhalika.



Zoezi


1.Fafanua ni kwa namna gani wataalam wafuatao wameifasili fonimu.


 Daniel Jones

 Nikolai Trubetzkoy


 Naom Chomsky na Morris Halle.

Eleza uhusiano na tofauti wa taaluma ya fonolojia na fonetiki kwa mifano hai.

 
















































16

 

SURA YA TATU



3:0 UHUSIANO WA FONOLOJIA NA TAALUMA NYINGINE ZA ISIMU


Fonolojia kama tawi la isimu linahusiana na taaluma au matawi mengine ya isimu ambayo ni mofolojia, sintaksia pamoja na semantiki. Fonolojia inategemeana au inasaidiana na taaluma nyingine za isimu ili kuleta maana katika lugha. Fonolojia ikiwa kama taaluma inayoshughulikia fonimu ambayo ni kipashio kidogo kabisa katika lugha maalum lakini kina uamilifu mkubwa sana. Kipashio fonimu ndicho kitumikacho kama msingi wa muundo wa lugha. Uhusiano wa fonolojia na taaluma nyingine katika isimu nitaueleza kinaganaga kama ifuatavyo hapa chini.



3:1 Uhusiano wa Fonolojia na Mofolojia.


Hapo awali katika sura ya kwanza na ya pili nimeeleza au nimezungumzia juu ya dhana ya fonolojia kwamba ni taaluma inayoshughulika na uchunguzi, uchambuzi na uanishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya lugha za binadamu. Fonolojia inashughulikia sauti zinazotumika kutofautisha maana za maneno katika lugha maalum. Taaluma hii hujishughulisha na mpangilio wa mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu, na mfuatano wa fonimu / sauti au silabi katika kuunda maneno.


Mofolojia ni taaluma inayoshughulikia maumbo mbalimbali ya maneno katika lugha na njia au sheria zinazotumika katika uundaji wa maumbo ya maneno hayo. Mofolojia na fonolojia huhusiana kwa karibu sana. Uhusiano huo unathibitika katika vipengele vifuatavyo:


Kanuni za kifonolojia zinazoongoza uundaji wa vipashio vya taaluma ya mofolojia ambavyo ni mofimu na maneno. Katika uundaji wa mofimu na maneno kanuni za kifonolojia ndizo hutumika kama nyenzo muhimu sana katika mchakato mzima wa uundaji wa silabi ambazo huunda mofimu na maneno. Lakini pia fonimu peke yake huweza kuunda maneno au mofimu ama mofimu huru au tegemezi mfano neno oa limeundwa na fonimu mbili ambazo ni irabu tupu. Kanuni za uundaji wa silabi katika lugha ya Kiswahili inasema silabi ni lazima iwe na irabu ndani yake au iwe imeundwa na nazali silabi kwa maana ya kwamba nazali hiyo ina sifa ya usilabi mfano katika neno nta, mvua mkubwa. Sauti zilizoandikwa kwa wino mzito ni nazali ambazo zina sifa ya usilabi. Kwa ujumla silabi haiwezi kuundwa na konsonanti peke yake isipokuwa nazali silabi, bali ni lazima silabi iwe na irabu au iundwe na irabu peke yake. Muundo unaokubalika ni huu ufuatao:


Konsonanti + irabu (KI)

ma


\

K   I

 







17

 

Konsonanti + konsonanti + irabu  (KKI)

nga


          ȀĀ⤀Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ȁ ȀĀ          Ȁ ⤀Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            Ā ᜀ            │ \

K K I


Konsonanti +kiyeyusho + irabu (KkI)


kwa


│ \ K k I


Irabu peke yake (I)

ita

I

Mifano na: 1

Muundo wa silabi / mofimu / neno Mifano ya silabi/ mofimu / neno

1. II ua oa

/ \ / \

I I I I

2. KI ki ba na

/ \ / \ / \

K I K I K I

3. kI wa ya

/ \ / \

k I k I

4.KKI mba nga nda

/ │ \ / │ \ / │ \

K K I K K I K K I

5.KkI kwa vya

/ │ \ / │ \

K k  I K k I

6.KKkI mbwa ngwa

/ ││ \ /││\

K Kk  I KKk  I

7.KKKI Skru

/││\

KKKI

8.IK al ar

/ \ / \

I  K I K

9. KIK daf ham

/ │ \ / │ \

KI K K I K

 





18

 


Katika mifano iliyomo ndani ya jedwali inaonesha miundo ya silabi, mofimu au maneno ya lugha ya Kiswahili. Miundo iliyo katika namba 1 hadi namba za 8 ni muundo uliotawala katika lugha ya Kiswahili. Utajiuliza mbona mwandishi amesema lugha ya Kiswahili haina muundo wa konsonanti lakini mifano namba 8 na 9 silabi zake zinaishia na sauti konsonanti. Ni kweli lakini ni kwamba ada ya lugha yoyote iliyo hai huchota maneno kutoka katika lugha nyingine ili ikue lugha ya Kiswahili imechota maneno kutoka lugha za kigeni na hivyo kuwa na silabi funge. Lakini pia unachotakiwa kuelewa ni kwamba mbali na kuishia na sauti konsonanti silabi hizo bado zina irabu ndani yake.



Mifano na: 2


Fonolojia Mofolojia

1. /b / a /b / a / → $ba$ba$  → ║baba║ → baba


│││


K IKI

Fonimu silabi mofimu → neno


2. /a/n/c/h/e/z/a/  →$a$na$che$za$→ a+na+chez+a → anacheza


│││││││

IKKKIKI


Fonimu → silabi mofimu neno


Ufunguo:

K─ konsonanti


I ─ irabu

k ─ kiyeyusho


── mpaka wa fonimu $ ─ mpaka wa silabi


║─ mofimu

 ─  mpaka wa mofimu


 alama hii inaonesha uhusiano wa vipashio ↓ alama hii inaonesha aina ya kipashio.


Muathiriano wa sauti katika maneno ambao huleta alomofu. Alomofu ni maumbo tofauti tofauti yanayowakilisha mofimu moja. Mbinu inayotumika katika kubainisha alomofu hizo za mofimu katika taaluma ya mofolojia ni kanuni ya kifonolojia iitwayo mgawo kamilishi (complementary distribution). Kupitia umbo la ndani na la nje alomofu hutokea. Umbo la ndani linahusu umbo la neno kimofolojia na umbo la nje linahusu matamshi ambayo ni kipengele cha fonolojia. Hebu chunguza kwa makini mifano katika jedwali lifuatalo.

 










19

 

Mifano na: 3


Mofolojia Fonolojia

Umbo la  ndani Umbo la nje

(i)  muombezi Mwombezi

(ii)  muuguzi Muuguzi

(iii) mutoto Mtoto

(iv) mualimu Mwalimu

(v)  muembe Mwembe

(vi) muimbaji Mwimbaji


Alomofu ambazo zimepatikana katika maneno hayo hapo juu ni {mw-, mu- na m-} na alomofu hizi zinatokea katika mazingira yaleyale na kuwakilisha mofimu moja ya {mu-}. Alomofu hutokea katika mazingira yaleyale na zikiwakilisha mofimu moja au maana moja. Utokeaji wake unadhibitiwa na kanuni za kifonolojia.


Katika mifano hiyo kuna kanuni ndogondogo za kifonolojia zilizoongoza utokeaji wa alomofu katika taaluma ya mofolojia. Kanuni hizo ni kama ifuatavyo:


Mzizi wa neno unaoanza na fonimu konsonanti hupokea au hubeba alomofu {m-} kama ilivyotokea katika neno mtoto na fonimu irabu / u / imedondoshwa.


Mzizi wa neno unaoanza na fonimu irabu / a /, /ɛ /, /i / na /ͻ / ambazo tahajia zake ni a, e, i, na o, mizizi hiyo hupokea au hubeba alomofu {mw-} na irabu zote za mwanzo wa mzizi hubadika na kuwa kiyeyusho / w / kama inavyoonekana katika maneno ya mwalimu, mwimbaji, mwembe, na mwombezi hapo juu.


Mzizi wa neno unaoanza na fonimu irabu / u /, hupokea au hubeba alomofu {mu-} au hakuna badiliko lolote katika muundo wa nje.


Kanuni ya kifonolojia ya tangamano la irabu hutumika katika mchakato wa kupata alomofu za mofimu ya utendea. Alomofu za mofimu ya utendea zinadhibitiwa na kanuni ya tangamano la irabu, ambapo maumbo (alomofu) hujitokeza katika maumbo mbalimbali yakiwakilisha mofimu ya utendea. Hii inatokana na irabu msingi iliyoko kwenye mzizi wa neno lakini pia mzizi unaishia na aina gani ya sauti ama ni konsonanti au irabu. Lakini hapa jambo la msingi linalozingatiwa ni irabu iliyoko ndani ya mzizi na hiyo ndiyo inayoamua mofimu ya utendea iwe na umbo gani. Iwapo ndani ya mzizi kukawa na irabu a, i, na u lakini unaishia na sauti konsonanti basi umbo la mofimu ya utendea litakuwa i, na kama irabu iliyopo ndani ya mzizi ni e na o na kuishia na konsonanti basi umbo la mofimu litakuwa ni e. Upande wa mizizi inayoishia na sauti irabu a, i, na u, mzizi huo utapokea alomofu li na mizizi inayoishia na irabu e na o, mizizi hiyo hupokea alomofu le. Hebu tuangalie mifano inayoonesha kazi ya fonolojia katika taaluma ya mofolojia. Katika mifano hiyo utaona jinsi kanuni inavyodhibiti utokeaji wa alomofu za mofimu ya utendea.

 












20

 

Mifano na: 4


Neno au shina Kauli ya utendea 1 Kauli ya utendea 2 Alomofu ya utendea

i) paka pak+i+a pakia -i-

ii) toka tok+i+a tokea -e-

iii) kaa ka+li+a kalia -li-

iv) chuma chum+i+a chumia -i-

v) pika pik+i+a pikia -i-

vi) enda end+i+a endea -e-

vii) teka tek+i+a tekea -e-

viii) ona on+i+a onea -e-

ix) imba imb+i+a imbia -i-

x) vua vu+li+a vulia -li-

xi) lia li+li+a Lilia -li-

xii) toa to+li+a tolea -le-

xiii) lea le+li+a lelea -le-

xiv) umba umb+i+a umbia -i-

xv) cheza chez+i+a chezea -e-

xvi) linda lind+i+a lindia -i-


Katika mifano hiyo hapo juu tunaona dhahiri jinsi kanuni ya kifonolojia inavyotawala utokeaji wa alomofu za mofimu ya utendea. Utokeaji wa alomofu hizi umezibitiwa na irabu msingi zilizoko katika mizizi inayohusika. Utokeaji wa alomofu hizo una uchanganuzi ufuatao:


Mizizi yenye irabu msingi a, i, na u au fonimu / a /, / i / na / u / ndani yake na ikiishia na fonimu konsonanti, mizizi hiyo hupokea alomofu ya mofimu ya utendea {-i-} kama ilivyo katika neno chumia, pakia ,imbia, pikia, na umbia. Kanuni ya


alomofu ya mofimu ya utendea {-i} / MZ {a, i, na u}.

I


Mizizi yenye irabu msingi e na o yaani fonimu /ɛ / na /ͻ/ ndani yake na


ikiishia na foniimu konsonanti, mizizi hiyo hupokea alomofu ya mofimu ya utendea {-e-} kama ilivyo katika maneno endea,tokea, chezea, tekea, na onea. Kanuni ya alomofu ya utendea {-e-}/ MZ {e,na o}.


I


Mizizi inayoishia na irabu a, i, u au fonimu /a /, / i / na / u /, mizizi hiyo hupokea alomofu ya mofimu ya utendea {-li-} kama ilivyo katika neno kaa, vulia, na lilia. kanuni ya alomofu ya mofimu {-li-} / MZ {a, i, na u}.


I

Mizizi inayoishia  na irabu e na o au fonimu /ɛ / na /ͻ/, mizizi hiyo hupokea alomofu


ya utendea {-le-} kama ilivyo katika maneno lelea, na tolea. Kanuni ya alomofu ya mofimu ya utendea {-le-} / MZ {e na o}.


I


Kuundwa kwa vipashio vya taaluma ya mofolojia kwa kutumia vipashio vya taaluma ya fonolojia. Vipashio mofimu na neno vya taaluma ya mofolojia huundwa kwa kutumia fonimu na silabi. Taaluma ya mofolojia katika uundaji wa vipashio vyake hutegemea vipashio vya fonolojia, fonimu na silabi. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini

 



21

 

Mifano na: 5

Mofolojia Fonolojia

i) Neno “babu”  limeundwa  na a) fonimu 4 /b/,/a/,/b/na /u/

b) silabi 2 $ba$bu$

c)  mofimu 1  ǁ babu ǁ

ii) Neno “tunaimba” limeundwa na a) fonimu 8 /t/,/u/,/n/,/a/,/i/,/m/,/b/ na /a/


silabi   4 $tu$na$i$mba$

mofimu 4 tu+na+imb+a


iii) Neno “magodoro” limeundwa a) fonimu  8 /m/,/a/,/g/,/ͻ/,/d/,/ͻ/,/r/ na /ͻ/

silabi   4 $ma$gͻ$dͻ$rͻ$


mofimu 2 ma+godoro


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kwamba neno la kwanza limeundwa na fonimu nne (4) ambazo ni sawa na silabi mbili (2), neno la pili limeundwa na fonimu nane (8), ambazo ni sawa na silabi nne (4), na neno la tatu limeundwa na fonimu nane (8) ambazo ni sawa na silabi nne (4).


Wakati huo huo mofimu {babu} imeundwa na fonimu nne ambazo ni sawa na silabi mbili, mofimu {tu-} imeundwa na fonimu mbili au silabi moja, mofimu {-na-} imeundwa na fonimu mbili au silabi moja, mofimu {-imb-} imeundwa na fonimu tatu na mofimu {-a} imeundwa na fonimu moja (kutoka katika neno tunaimba).


Mofimu {ma-} imeundwa na fonimu mbili au silabi moja, wakati mofimu {godoro} imeundwa na fonimu sita au silabi tatu.


Kanuni ya tangamano la irabu inajitokeza pia katika mofimu ya usababishi, kwa maana ya kwamba utokeaji wa alomofu za mofimu ya usababishi au ya utendesha hudhibitiwa na kanuni ya tangamano la irabu. Kwa ufafanuzi zaidi hebu tuchungue mifano ifuatayo.



Mifano na: 6


Neno / shina Kauli  ya  utendesha Kauli  ya  utendesha Alomofu ya

1 2 utendesha

i) enda end+ish+a endesha -esh-

ii)imba imb+ish+a imbisha -ish-

iii)cheza chez-ish+a chezesha -esh-

iv) soma som+ish+a somesha -esh-

v)andika andik+ish+a andikisha -ish-

vi)ruka ruk+ish+a rukisha -ish-

vii)vaa va+lish+a valisha -lish-

viii)toa to+lish+a tolesha -lesh-

ix)chemka chem.+sh+a chemsha -sh-

x)amka am+sh+a amsha -sh-

xi)pambana pamban+ish+a pambanisha -ish-

xii)vua vu+lish+a vulisha -lish-

xiii)lia li+lish+a lilisha -lish-

xiv)noa no+lesh+a nolesha -lesh-

 





22

 


Ukichunguza kwa makini sana katika mifano hiyo hapo juu utangua kuwa alofomu za utendea zimetokea kwa udhibiti wa kanuni ya tangamano la irabu ambapo ilabu iliyoko kwenye mzizi ndiyo inayoamua umbo la mofimu ya utendea iweje. Utokeaji wa alomu hizo nitaufafanua kama ifuatavyo:


Mizizi au mashina yenye irabu msingi a, i, na u au fonimu /a/, /i/ na /u/ na inaishia na sauti konsonanti, mizizi hiyo au mashina hayo hupokea alomofu {-ish-} ya mofimu ya utendesha kama ilivyo katika maneno ya imba, andika, ruka na pambana. Kanunia alomofu ya mofimu ya utendesha {-ish-} / MZ {a,i na u}


I


b) Mizizi au mashina yenye irabu msingi e na o au fonimu /ɛ/ na /ͻ/ na kuishia na sauti konsonanti, mizizi hiyo au mashina hayo hupokea alomofu {-esh-} ya mofimu ya utendesha kama ilivyo katika maneno ya enda,soma na cheza.kanuni ya alomofu ya mofimu ya utendesha {-esh-} / MZ {e, na o}


I


Mizizi au mashina yenye kuishia na irabu a, i, na u au fonimu /a/,/i/ na /u/, mizizi au mashina hayo hupokea alomofu {-lish-} ya mofimu ya utendesha kama ilivyo katika maneno ya vua, vaa na lia. Kanuni ya alomofu ya mofimu ya utendesha {-lish-}/ MZ {a, i, na u}


I


Mizizi au mashina yenye kuishia na irabu e na o au fonimu /ɛ/ na /ͻ/ , mizizi au mashina hayo hupokea alomofu {-lesh-} ya mofimu ya utendesha kama ilivyo katika maneno ya toa na noa. Kanuni ya alomofu ya mofimu ya utendesha {-lesh-}/ MZ {e, na o}


I


Mizizi au mashina yanayoishia na sauti konsonanti lakini yana irabu msingi a, e, i, o na u huku yakiwa yanaingia katika kauli ya utendesha yakitokea katika kauli ya utendeka, mizizi hii au mashina haya hupokea alomofu {-sh-} ya mofimu ya utendesha kama ilivyo katika maneno ya amka na chemka. Hata hivyo utokeaji wa alomofu hii umedhitiwa na utawala wa kimofolojia na si kifonolojia.


Kutokana na mchanganuo huo hapo juu unaonesha dhahiri kwamba mofolojia na fonolojia hutegemeana sana na ni taaluma ambazo haziwezi kutenganishwa. Fonolojia haichunguzi sauti tu bali pia inatoa kanuni au sheria zinazoongoza uundaji wa mofimu na maneno, na kuunda mofimu na maneno kwa kutumia fonimu na silabi.



3:2 Uhusiano wa Fonolojia na Sintaksia


Sintaksia ni taaluma inayoshughulikia miundo mbalimbali ya tungo katika lugha. Tungo ni mpangilio wa vipashio vidogo katika kuunda maneno au mpangilio wa maneno katika kuunda virai, vishazi na sentensi. Tungo hizi katika taaluma ya sintaksia huundwa na maneno ambayo yanafungamana na kanuni za kifonolojia, kwa maana kwamba kanuni zinazotawala katika taaluma ya fonolojia ndizo hutumika pia katika taaluma ya sintaksia. Kanuni hizo ni zile zinazoongoza mpangilio wa vipashio na uundaji wa vipashio hivyo.


Uhusiano wa sintaksia na fonolojia ni mkubwa kama ilivyo kwa taaluma ya mofolojia. Uhusiano huu wa fonolojia umejikita katika kipashio cha msingi cha sintaksia.

 




23

 


Uhusiano huu unathibitika katika maeneo mbalimbali kupitia kipashio tungo neno kama nitavyoeleza hapa chini.


Kipashio cha neno, kipashio hiki huundwa na fonimu au silabi ambavyo ni vipashio vya taaluma ya fonolojia. Vipashio hivi vya kifonolojia yaani fonimu na silabi huunda kipashio cha msingi cha kisintaksia yaani kipashio cha taaluma ya sintaksia kiitwacho tungo neno . Kipashio tungo neno ndicho kidogo kabisa katika taaluma ya sintaksia ambacho huunda vipashio vingine vya kimuundo au kisintaksia kama tungo kirai, tungo kishazi na tugo sentensi. Hebu chungua mifano ifuatayo:



Mifano na: 7


Fonolojia Sintaksia

Fonimu Silabi Neno /maneno Tungo

i) /a/n/a/i/b/a/ $a$na$i$ba$ anaiba Anaiba tungo

neno

ii)/k/a/z/i/ $ka$zi$ kazi Kazi  nyingi –tungo

kirai

iii)/m/t/ͻ/t/ͻ/ $m$tͻ$tͻ$ mtoto Mtoto aliyekuja jana

–kishazi tegemezi

iv)/k/u/w/a/ $ku$wa$ kuwa Kuwa anapika

kishazi tegemezi

v) /n/ɛ/ɛ/m/a/ $nɛ$ɛ$ma$ Neema Neema anacheza

kishazi huru.

vi) /a/n/a/ͻ/m/b/a/ $a$na$ͻ$mba$ anaomba Mama anaomba

sana. –tungo

sentensi sahili

vii)/a/l/i/y/ɛ/p/ͻ/t/ɛ/a $a$li$yɛ$pͻ$tɛ$a$ aliyepotea Mbuzi aliyepotea

jana amepatikana

leo  Katela. –tungo

sentesi changamano

viii) /t/a/n/i/t/a/ $ta$ni$ta$ Tanita Tanita anaimba na

Jester anacheza.

tungo sentensi

ambatano





Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha uhusiano uliopo baina ya fonolojia na sintaksia, vipashio vya kifonolojia huunda kipashio kidogo cha sintaksia cha tungo neno. Maneno huunda tungo kirai, tungo kishazi, na tungo sentensi kama inavyoonekana katika jedwali hapo juu. Ni ukweli usiopingika kwamba fonolojia ni taaluma ya msingi sana katika isimu. Fonolojia inachukuliwa kuwa msingi wa lugha sababu vipashio vikubwa huundwa na vipashio vya kifonolojia.


Kanuni za kifonolojia, taaluma ya sintaksia inahusiana na fonolojia katika kanuni za uundaji wa maneno. Kanuni za kifonolojia hutumika kufupisha tungo ambazo hufanya

 




24

 


mabadiliko katika lugha husika. Kupitia njia zifuatazo dhana hii huthibitishwa dhahiri. Njia ya udondoshaji, ni mchakato ambao baadhi ya silabi au fonimu huachwa wakati wa utamkaji. Silabi za maneno mawili huweza kuachwa ili kuunda neno lingine, si maneno mawili tu bali hata zaidi na zinapoachwa baadhi ya silabi au fonimu husababisha kutengenezwa kwa maneno mapya. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.



Mifano na: 8


Tungo (sintaksia) Neno (sintaksia) Silabi/fonimu

zilizodondoshwa

i) baba yake babake silabi $ya$

ii)chakula cha jioni chajio silabi $ku$la$cha$ni$

iii)mwana wangu mwanangu silabi $wa$

iv)ntakuja n’takuja fonimu / i /

v)nimeshaondoka n’shaondoka fonimu / i / na silabi $mɛ$

vi)mtu asiye na kwao msikwao silabi $tu$a$yɛ$na$



Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa baadhi ya silabi zimepunguzwa au zimeondolewa kutoka katika tungo virai na kuunda tungo neno kama inavyoonekana hapo juu. Kwa mfano katika tungo kirai namba i) silabi $ya$ imeondoshwa ili kuunda tungo kirai neno babake. Katika mfano namba ii) silabi $ku$ na $la$ zimeondolewa katika neno chakula, neno cha au silabi $ča$ imedondoshwa pamoja na $ni$ katika neno jioni ili kuunda tungo neno chajio hali hii imejitokeza katika mifano yote kama inavyoonekana hapo juu. Lakini mfano wa iv) na v) fonimu /i/ na silabi $mɛ$ katika mfano namba v) hazijaleta mabadiliko makubwa kimuundo tungo hizo bado ziko katika viwango vile vile bali udondoshaji huo umerahisisha matamshi ya maneno hayo.


Njia ya mbadilishano wa fonimu au silabi, kanuni hii inahusu tabia ya fonimu au silabi kubadilishana nafasi. Kubadilishana huko kwa nafasi za fonimu au silabi kunasababisha kuundwa kwa tungo neno nyingine katika taaluma ya sintaksia. Ninaposema mbadilishano wa silabi hupelekea au husababisha kuundwa kwa maneno mengine, ni maneno mapya ambayo maana zake ni tofauti na maana ya awali.


Mifano na: 9


i) toa → ota


Fonimu /t/ na /ͻ/ zimebadilishana nafasi na kuunda neno jipya lenye maana tofauti na neno la awali. Neno toa maana yake ondoa au mpe mtu kitu kama neno la awali wakati neno ota lililotokea baada ya mbadilishano wa nafasi za fonimu lina maana ya kukaa juani /jianika, au mmea kuchipuka / kutokeza aridhini.


ii) ua → au


Fonimu /u/ na /a/ zimebadilishana nafasi na kuunda neno lingine ambalo lina maana tofauti na la kwanza. Neno la kwanza lina maana ya ondoa uhai wa mtu, uzio, sehemu yam mea,au binti wakati nano lililotokea baada ya mbadilishano wa nafasi

 




25

 

za fonimu lina maana ya kwa maana nyingine, jina lingine /mbadala.


iii) taka → kata


Silabi $ta$ na $ka$ au fonimu /k/ na /t/ zimebadilishana nafasi na kuunda neno jipya lenye maana tofauti na neno la awali. Neno la kwanza lina maana ya hitaji au uchafu wakati neno lililotokea baada ya mbadilishano wa nafasi za vipashio hivyo lina maana ya sehemu kijiografia na yenye uongozi kiserikali, tenganisha kitu, chombo cha kutekea maji au kifaa cha kubebea mzigo kichwani.


iv) katiba →  kabati


Silabi $ti$ na $ba$ zimebadilishana nafasi na kuunda neno jipya lenye maana tofauti na neno la awali. Neno la kwanza lina maana ya mwongozo wa nchi lakini lililotokea baada ya mbadilishano wa nafasi za silabi lina maana ya kifaa kitumikacho kuwekea vyombo kama sahani au nguo.


Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha kuwa fonimu na silabi zinapobadilishana nafasi hubadili maana ya maana ya neno lililokuwepo kabla ya mchakato kufanyika. Neno la awali na neno linalotokea baada ya mchakato linakuwa na maana tofauti kabisa na lile la awali.



3:3 Uhusiano wa Fonolojia na Semantiki


Semantiki ni taaluma inayoshughulikia maana za vipashio mbalimbali vya lugha au katika lugha. Semantiki inahusu uhusiano wa mtajo na kitajwa, uhusiano wa sauti na kitajwa, uhusiano wa mtajo na tungo au muundo mzima. Uhusiano wa mtajo na kitajwa ni ile maana ya sauti au neno na kitu chenyewe au kitajwa. Mfano neno “meza”, “duka” , “mtu” nakadhalika.


Uhusiano wa fonolojia na semantiki umejikita katika maana za sauti zinazotumika katika lugha maalum. Ikumbukwe kwamba hapo awali katika sura ya pili nilizungumzia fasili ya fonolojia na kusema kwamba fonolojia inashughulikia sauti zenye maana katika lugha maalum. Kutokana na dhima hizo katika taaluma ya fonolojia na semantiki ndipo tunagundua kuwa fonolojia na semantiki zinahusiana katika sauti zinazotumika katika lugha maalum. Maana ya sauti hupatikana kutokana na matumizi yake katika lugha na unapozungumzia matumizi ya kipashio unazungumzia taaluma ya semantiki. Kupitia mbinu mbalimbali za kifonolojia tunapata maana mbalimbali za maneno. Mbinu hizo ni:


Jozi sahili (minimal pairs /sets) ni mbinu ambayo kwayo maneno mawili au zaidi hufanana sauti isipokuwa sauti moja tu hutofautiana lakini katika nafasi ileile, na ndiyo inayosababisha au hubeba maana ya neno au maneno yanayohusika. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 10


pata ……………………bata

baba……………………bapa

 




26

 

tua……………………...toa

vuka…………………….shuka


pika……………………..paka


Katika jozi hiyo hapo juu kuna fonimu zilizoandikwa kwa wino mzito na kupigiwa mistari, fonimu hizo ndizo zinazotofautisha maana za maneno. Sauti au fonimu zinazotofautisha maana katika mifano namba i) ni /p/ na /b/, katika mfano namba ii) ni fonimu /b/ na /p/, katika mfano namba iii) ni fonimu /u/ na /ͻ/ ambazo tahajia yake ni u na o, mfano namba iv) ni fonimu /v/ na /š/ ambayo tahajia yake ni sh. Mfano wa mwisho namba v) ni fonimu /i/ na /a/.


Fonolojia na semantiki huhusiana pale maana za maneno zinapotofautishwa kutokana na tofauti ya fonimu au sauti katika mazingira yale yale kama inavyoonekana hapo juu.


Sauti kama sauti haina maana mfano [b], [i], sauti hizi zikisimama peke yake hazina maana bali zikiandamana na sauti nyingine kwa mpangilio wa fonolojia yaani konsonanti


irabu au irabu + irabu ambapo muunganiko au mfuatano wa namna hiyo unatupatia maneno yenye maana yenye maana. Kwa mfano fonimu /b/, /i/, /m/, /a/, /u/ na / ͻ/, fonimu hizi zinatupatia maneno yafuatayo:


i)bima ii) oa iii) maua iv) ua  v) imba  vi) bua vii) bia viii) mia  ix)moi


Kutokana na mpangilio maalum wa kifonolojia sematiki huweza kuona neno lina maana au halina maana katika lugha maalum. Naweza kusema kwamba semantiki huweza kushughulikia vipashio vyenye maana lakini ni lazima vipashio hivyo viundwe kwa kanuni maalum za kifonolojia na mpangilio maalum wa taaluma ya fonolojia.


Utumizi wa vitamkwa fulani hutokana na umilisi (kanuni za fonolojia) alionao mtu ambao humwongoza katika kupanga na kupata sauti zenye maana. Kwa maana kwamba mtu mwenye umilisi wa kanuni za kifonolojia atapanga vizuri sauti na atapata maneno yenye maana. Maana sahihi ya neno au sauti hutokana na umilisi ambao hutupatia kanuni ya kupangilia vizuri au kiusahihi vitamkwa kulingana na kanuni za uundaji wa silabi na maneno katika lugha maalum. Hebu chunguza mifano ifuatayo hapa chini:


Mifano na: 11


Kata –fonimu au sauti /p/. /t/ na /a/ zimeunda neno au silabi $ka$ na $ta$ zimeunda neno “kata” lenye maana ya tenganisha kitu, au sehemu kijiografia yenye uongozi kiserikali, chombo cha kutekea maji au kifaa kitumikacho kubebea mzigo kichwani.


Paka – fonimu au sauti /p/, /k/ na /a/ zimeunda neno au silabi $pa$ na $ka$ “paka” lenye maana ama ya kungarisha kitu kama ukuta, au mnyama afugwaye nyumbani.


Mali –fonimu au sauti /m/, /a/, /l/ na /i/ zimeunda neno au silabi $ma$ na $li$ zimeunda neno “mali” lenye maana ya vitu au raslimali.


Vile vile uteuzi wa vitamkwa na mpangilio wa maneno ndiyo unaosababisha kuwepo kwa maana ya sauti hizo au isiwepo. Mpangilio wa sauti au fonimu unaokubalika ni wa konsonanti + irabu ( KI), konsonanti + konsonanti + irabu (KKI), konsonanti + kiyeyusho

 




27

 


+irabu (KkI), kaonsonanti +konsonanti + konsonanti+ irabu (KKKI), konsonanti peke yake (nazali silabi), irabu peke yake (I) au konsonanti + irabu +konsonanti (KIK), muundo wa irabu + konsonanti (IK) na kiyeyusho + irabu (kI). Huu ndiyo mpangilio unaokubalika na kuleta maana katika kuunda silabi pamoja na maneno ambayo huleta maana katika lugha maalum hususani za lugha za Kibantu.


Kutokana na ufafanuzi nilioutoa ukiambatana na mifano dhahiri inaonesha kwamba fonolojia inafanya kazi ndani ya lugha ikishishirikiana au ikifungamana na taaluma nyingine za mofolojia, sintaksia na semantiki. Ni ukweli usiopingika kwamba taaluma hizi hutegemeana yaani lugha yoyote ile msingi wake ni taaluma ya fonolojia. Kwa maana kwamba kipashio fonimu ndicho kidogo kabisa katika taaluma ya isimu lakini ndicho msingi wa vipashio vingine vyote kwa sababu huundwa na kipashio hiki. Kwa msingi huo taaluma ya fonolojia ni ya muhimu sana katika isimu kwa sababu kuwepo kwa taaluma nyingine za isimu kunategemea uwepo wa taaluma ya fonolojia kama yenyewe inavyotegemea kuwepo kwa taaluma ya fonetiki.


Fonimu huunda silabi na mofimu, fonimu na silabi huunda maneno wakati maneno huunda tungo mbalimbali katika taaluma ya sintaksia. Fonimu huunda silabi, maneno, na maneno huunda tungo lakini pia taaluma ya sematiki huingia kwa sababu fonimu, lazima iwe na maana ndipo itumike katika lugha, maneno lazima yawe na maana katika lugha inayohusika. Kwa ujumla tanzu hizi haziwezi kufanya kazi peke yake kila moja bali kwa kutegemeana.



Zoezi

Eleza uhusiano uliopo baina ya


fonolojia na mofolojia

fonolojia na sintaksia


fonolojia na semantiki.

 






























28

 

SURA YA NNE



4: 0 VITAMKWA


Kitamkwa ni sauti dhahiri inayosikika wakati wa utamkaji maneno ambayo huweza kubainishwa kama kitu kimoja ambacho huweza kuwakilishwa kwa kutumia alama zijulikanazo kama kama alfabeti. Massamba na wenzake (2004)


Mfano p,b, t,d, th, dh, k,g nakadhalika.


Swali kubwa tunalojiuliza ni kwamba kipashio kitamkwa kina umuhimu gani katika lugha? Kwa ufupi ni kwamba ni lazima au hatuna budi kujua fasili ya kitamkwa na dhima yake katika lugha. Kitamkwa ni kipashio kinachotumika katika kuunda maneno. Kitamkwa kinajitokeza kama kipandesauti kinachojibainisha kwa dhati yake. Kwa mfano vitamkwa vinavyowakilishwa na maumbo kama p,b,t,d,f,v,m,ŋ nakadhalika. Inaonekana dhahiri kuwa kila kitamkwa kina ubainifu wake ulio wazi. Nikizingatia jinsi vitamkwa hivi vinavyosikika masikioni mwetu vitamkwa p,t, na f vina msikiko hafifu kwa sababu katika nyuzisauti ( vocal cords) hakuna mrindimo au mtimbwiliko. Lakini vitamkwa b, d, v, m, na ŋ vina msikiko mkubwa wakati wa utamkaji kwa sababu katika nyuzisauti kunakuwa na mrindimo au mtimbwiliko unaotokana na hewa ambayo huzisukuma nyuzisauti hizo zinapokuwa zimekaribiana sana. Katika hali ya kutafuta nafasi ya kupita hewa, mtetemeko hutokea katika nyuzisauti hizo zinazolazimika kuachana.


Kipandesauti ni dhana ambayo inajumuisha aina mbalimbali au sauti zote zinazotolewa na alasauti za binadamu. Kwa maneno mengine kipandesauti ni dhana ya kifonetiki wakati kitamkwa ni dhana ya kifonolojia. Kitamkwa kinatumika katika taaluma ya fonolojia.


Kitamkwa hakipo katika tahajia au maandishi bali ni sauti inayosikika na kuhusishwa na maandishi kwa kutumia alfabeti ambazo ni nasibu, yaani alfabeti hizo hazina uhusiano wa moja kwa moja na sauti inayohusika.


Kitamkwa kwa ufafanuzi zaidi kimo ndani ya kipandesauti kwa sababu kipandesauti kinajumuisha au hubeba vitu kama vitamkwa, mkazo, kiimbo, toni, kidatu, nakadhalika.


Vitamkwa vya lugha kwa ujumla hutazamwa kwa namna mbili. Kwanza vitamkwa huweza kuelezwa katika taaluma ya fonetiki na pili huelezwa katika taaluma ya fonolojia. Nitaeleza kinaganaga hapa chini kwa kila mtazamo.



4:1 Vitamkwa vya Kifonetiki


Ikumbukwe kwamba katika sura ya kwanza nilieleza kwamba fonetiki ni tawi la isimu ambalo linashughulikia uchunguzi, uchambuzi, usafirishaji, usikikaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla ( taz. 1:2). Ninaposema utoaji au utamkaji kwa maana kwamba jinsi sauti hizo zinavyotolewa katika kinywa cha binadamu, usafirishaji ni jinsi ambavyo sauti zinalifikia sikio la msikilizaji wakati usikikaji na ufasili wake ni jinsi utambuzi wa sauti mbalimbali unavyofanywa, na uhusiano uliopo baina ya sikio, neva masikizi na ubongo wakati wa masikizi ya sauti au matamshi. Kutokana na fasili hiyo naweza kusema kwamba tunaposhughulikia vitamkwa vya lugha za binadamu katika taaluma ya fonetiki kuna mambo muhimu tunayoyatilia mkazo. Mambo hayo ni kwanza

 




29

 


kitamkwa hicho hakifungamani na lugha yoyote bali hutolewa na alasauti za binadamu. Pili, tunaangalia ule utamkaji wake, usafirishaji wa sauti, usikiaji na ufasili wa vitamkwa hivyo bila kulazimika kuvihusisha na lugha fulani maalum.


Katika taaluma ya fonetiki vitamkwa au sauti huchunguzwa jinsi zinavyoumbwa na kubainisha kila sifa ijengayo sauti husika bila kujali kama sifa hiyo inapatikana katika sauti nyingine kwa mfano sauti inayowakilishwa na umbo θ ni sauti ambayo ina sifa; kikwamizi, inatamkiwa kwenye meno na inatamkwa kwa kubana ncha ya ulimi katikati ya meno ya juu na meno ya chini. Hizi sifa ni halisi za kitamkwa hiki lakini sifa hizi hizi pia zinapatikana katika kitamkwa kinachowakilishwa na umbo ð kama inavyooneshwa katika kielelezo namba 1.


Ufanano huo wa sifa za sauti hizo unathibitisha kwamba vitamkwa vinavyoshughulikiwa katika taaluma ya fonetiki havichunguzwi kama vinatumika kujenga maneno tofauti tofauti katika lugha au la.



4:2 Vitamkwa vya Kifonolojia


Katika sura ya kwanza (taz. 1:0) nilieleza fasili ya istilahi “fonolojia” kuwa ni tawi mojawapo la taaluma ya isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimali ya sauti za lugha za binadamu. Katika taaluma ya fonolojia vitamkwa huchunguzwa katika matumizi yake. Mchakato wa uchunguzi umejikita zaidi katika matumizi ya sauti katika mfumo wa lugha fulani maalum. Vitamkwa huangaliwa kama sauti bainifu katika lugha. “ Sauti bainifu” ina maana ya sauti ambazo huleta tofauti ya maana katika maneno ya lugha fulani maalum.


Kwa ufafanuzi zaidi hebu chungua jozi ya vitamkwa vinavyotofautisha maana za maneno hapa chini vyenye maumbo ya k –g, f –v , m –k , p –t. Vitamkwa hivi huweza kutumika kuunda maneno ya lugha na pia tunaangalia ni kwa namna gani vitamkwa hivi vinatofautisha maana za maneno hayo.


Mifano na: 1

a) pambo b) tambo


c) shoka d) nyoka

e) mamba f) kamba


g) kunia h)gunia


Katika maneno hayo hapo au mifano hiyo hapo juu tunaona dhahiri kwamba vitamkwa vilivyoandikwa kwa wino mzito yaani (p,t, sh, ny, m,k, na g) ndivyo vinavyoleta tofauti ya maana katika jozi nne za maneno nilizozitoa. Jozi hizi ambazo ni a) na b), c) na d), e) na f) pamoja na g) na h). Katika jozi hizo kitamkwa p kikiondolewa katika a) na kuwekwa kitamkwa t badala yake na kupata neno lilelile lililoko b) halikadhalika katika mifano ya jozi ya c) na d), e) na f) pamoja na g) na h). Katika g) tukiondoa kitamkwa k na kuweka kitamkwa g badala yake na kupata neno lilelile lililoko katika h), na kinyume chake pia.


Hapa inaonesha wazi kwamba fonolojia inashughulikia vitamkwa vile tu vinavyotumika katika kuunda maneno yenye maana mbalimbali katika lugha. Vitamkwa

 




30

 


vinajenga maana mbalimbali za maneno kutokana na kubadilishana nafasi. Hebu chungua mifano ifuayo;


Mifano na:2


pika ……………………..kapi


Silabi $pi$ na $ka$ zimebadilishana nafasi na kusababisha maana ya neno la pili kutofautiana na lile la kwanza. Neno la awali “pika” lina maana ya kuuandaa chakula au kuivisha chakula, lakini neno “kapi” lililotokea baada ya mbadilishano wa nafasi za silabi lina maana ya kitu kisichofaa.


choka ………………………kocha


Vitamkwa fonimu /č/,/k/, /ͻ/ na /a/ zimebadilishana nafasi na kutupatia neno lingine lenye maana tofauti na neno la awali. Neno la awali “ choka”lina maana ya nyong’onyea au legea wakati neno “kocha” lililotokea baada ya mbadilishano wa nafasi za fonomu lina maana ya mtu mwenye ujuzi au taaluma ya kuwafundisha namna ya kucheza mfano mpira wa miguu, wa kikapu nakadhalika.


daka ……………………….kada


Silabi $da$ na $ka$ zimebadilishana nafasi na kutupatia neno jipya ambalo lina maana tofauti na lile la awali. Neno la awali lina maana ya kushika kitu ambacho mtu kakurushia wakati neno “kada” lililotokea baada ya mbadilishano wa silabi au fonimu /k/ na /d/ lenye maana ya mfuasi au mshabiki wa kitu fulani au kitengo fulani kikazi kama kada ya ualimu, ya afya na kadhalika.



4: 2:1 Aina za Vitamkwa vya Kifonolojia


Kama ilivyoelezwa hapo juu katika 4:2 kwamba kitamkwa ni sauti zile zote zinazotumika katika kuunda maneno katika lugha maalum. Katika taaluma ya fonolojia vitamkwa vimegawanyika katika makundi mawili. Vitamkwa vinavyotumika katika kuunda maneno katika lugha fulani maalum na vitamkwa vya kimuundo katika taaluma fonolojia hivi huchunguzwa wapi mkazo au shadda,umewekwa, silabi imeundwaje na vingine vingi.



4:2:1:1 Vitamkwa vya Kawaida (Segmental Phonology)


Ninaposema vitamkwa vya kawaida nina maana ya sauti konsonanti, irabu na viyeyusho. Vitamkwa vya kawaida ni vitamkwa ambavyo hutumika katika kuunda maneno. Katika vitamkwa vya kawaida tunachambua fonimu ambazo hujumuisha konsonanti, irabu, na viyeyusho. Vitamkwa vya kawaida hujihusisha na alofoni za fonimu pamoja na njia za kubainisha fonimu hizo pamoja na alofoni zake. Njia hizo ni jozi sahili, ufanano wa kifonetiki, mgawo kamilishi, mpishano huru na usawazisho pamoja na sifa kuu bainifu za fonimu na sifa nyingine kama za usilimisho, udondoshaji,

 





31

 


ukakaishaji na nyingine nyingi. Vitamkwa hivi vitaelezwa kwa undani zaidi katika sura itakayofuata.



4: 2: 1:2 Viarudhi (Supra Segmental Phonology)


Ni vitamkwa vinavyohusisha au vinavyohusu mkazo au shadda, yaani kiwango cha nguvu inayotumika katika utamkaji wa baadhi ya silabi, silabi zinavyoundwa na mkazo unapowekwa wakati wa utamkaji, lafudhi ambayo ni sifa ya kimasikizi (inayohusiana na kusikika kwa sauti wakati wa kutamka) ya matamshi ya mtu binafsi ambayo humpa msemaji utambulisho fulani wa sehemu atokako. Kiimbo ni moja ya viarudhi ambacho kinahusu utaratibu au ni ule utaratibu wa upandaji na ushukaji wa sauti katika usemaji. Katika vitamkwa viarudhi tunashughulikia pia kidatu ambacho ni kiwango cha usemaji ambacho kinaweza kuwa kiwango sha juu, cha kati au cha chini cha usemaji. Katika viarudhi kuna silabi pia, hiki ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za lugha hutamkwa mara moja kama fungu moja la sauti linalojitegemea kimatamshi. Vile vile kipengele cha otografia au tahajia chenye kushughulikia michoro ya maandishi yenye kuwakilisha sauti zisikikazo katika usemaji wa lugha.


Katika sura hii tumeona maana ya vitamkwa, aina za vitamkwa kwa kutumia kigezo cha kifonetiki na kigezo cha kifonolojia. Vitamkwa kwa kutumia kigezo cha kifonolojia na aina zake vitaelezwa zaidi katika sura inayofuata. Ni dhahiri kabisa kuwa kitamkwa ni dhana pana sana hususani tunapokitazama katika mtazamo wa kifonolojia. Katika kitabu hiki nitashughulikia zaidi vitamkwa kwa kutumia kigezo cha fonolojia ya lugha ya Kiswahili.


Zoezi


Eleza dhana ya vitamkwa kwa vitamkwa  kwa mawanda yyake.

Nini maana ya istilahi zifuatayo:


vitamkwa vya kawaida

viarudhi


Toa mifano thabiti kujenga hoja zako.

 























32

 

SURA YA TANO



5: 0 VITAMKWA VYA KAWAIDA (SEGMENTAL PHONOLOGY)


Katika sura ya nne (taz. 4:0) nimezungumzia dhana ya kitamkwa kuwa kitamkwa ni sauti dhahiri inayosikika wakati wa utamkaji wa maneno ambayo huweza kubainishwa kama kitu kimoja ambacho huweza kuwakilishwa kimaandishi kwa kutumia alama maalum zijulikanazo kama herufi za albeti. Kwa mfano th, t, d, g, m nakadhalika. Vile vile nikazungumzia aina ya vitamkwa kwa kutumia kigezo cha kifonolojia kwamba kitamkwa kinatazamwa katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni vitamkwa vya kawaida vinavyojumuisha fonimu, alofoni yaani konsonanti, irabu na viyeyusho, hapa nitaeleza njia ambazo hutuwezesha kuzibainisha fonimu na alofoni zake, pamoja na sifa nyingine za vitamkwa hivyo.


Katika sura hii nitashughulikia fonimu kwa undani zaidi bila kujikita katika lugha ya Kiswahili peke yake bali nitachunguza na kueleza vitamkwa vya lugha ya Kiswahili,Kinyakyusa, Kisafwa pamoja na vya lugha ya Kiingereza. Kundi la pili ni la viarudhi ambalo nitalishughulikia baadaye katika sura zitakazofuata.



5:1 Fonimu


Katika vitamkwa vya kawaida (segmental phonology) nimesema hujumuisha fonimu na alofoni zake. Katika kipengele hiki au sehemu hii nitachunguza fonimu kama kitamkwa cha kawaida kwa kujikita katika dhana ya fonimu. Fonimu ni dhana inayohusu kitamkwa kinachojenga maneno yenye maana katika lugha maalum. Kwa mujibu wa


Massamba, D.P.B, Kihore, Y. M, na Msanjila, Y.P katika katika kitabu chao kiitwacho

Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. (FOKISA) 2004 wanasema:


“ Fonimu ni kitamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalum”


Ubainifu wa kipashio fonimu hautofautiani kutoka lugha moja hadi lugha nyingine. Fonimu hutazamwa kama kipashio kinachotumika katika neno fulani katika lugha maalum.


Fonimu huweza kutazamwa katika mitazamo mitatu; mtazamo wa kifonetiki, mtazamo wa kisaikolojia na mtazamo wa kifonolojia. Kutokana na wanaisimu mbalimbali walioifasili fonimu. Nitaieleza mitazamo hiyo mmoja baada ya mwingine.


5:1:1(a) Mtazamo wa Kifonetiki


Fonimu katika mtazamo wa kifonetiki hutazamwa kama kitita cha sauti au jamii ya sauti zinazofanana kifonetiki, kwa maana ya matamshi yake, namna ya kuzitamka na namna zinavyosikika na jinsi mawimbi ya usafirishaji wa sauti au fonimu husika yalivyo. Fonimu si sauti moja bali ni jamii ya sauti. Ninaposema fonimu ni kitita haina maana kwamba kitita hiki kinaleta tofauti ya maana la hasha. Kitita hiki cha sauti hakileti tofauti ya maana bali maana ile ile.

 




33

 


Mifano na: 1


[p]  ………………[ῤ]

………………[ph]

……………….[p]


[t]  ………………..[ț]


………………..[ṱ]

…………………[t]


[d]………………..[ḑ]


……………….[d]


Sauti [ῤ], [ph] na [p] ni sauti zinazowakilisha fonimu [p] kwa maneno mengine naweza kusema kuwa fonimu [p] ina inawakilisha na maumbo [p], [ῤ] na [ph]. Fonimu [t] inawakilishwa na maumbo ya [t], [ț], na [ṱ]. Na fonimu [d] inawakilishwa na maumbo ya [d] na [ḑ].


Daniel Jones anasema:


“ Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani lenye sauti maalum pamoja na sauti zinazohusiana na sauti hizo ambazo hutumiwa mahali pake”.


Fonimu huwakilisha umbo halisi la kifonetiki yaani sauti zilizoko katika sauti moja huwa na maumbo ya kifonetiki yanayofanana na hutumika katika muktadha maalum. Jones anaeleza haya katika kitabu chake kiitwacho An Outline of Phonetics. (1918)



5:1:1(b) Mtazamo wa Kisaikolojia


Fonimu imefasiliwa kama kitamkwa au kipashio au picha ya sauti iliyochorwa ndani ya akili ya binadamu na picha hii hutofautiana na picha ya fonimu nyingine katika akili ya binadamu kwa mujibu wa mtazamo wa kisaikolojia. Mojawapo ya fonimu hizo ni [b], badala ya [ɓ] au [p] badala ya [ῤ].


Katika mtazamo huu Noam Chomsky, Morris Halle na Boudouin de Courtenay wanasema kwamba:


“ Fonimu ni dhahania inawakilisha kitu unachotakakuzungumza”


Fonimu inaonekana kuwa dhahania kwa sababu lugha yenyewe ni dhahania. Noam Chomsky na Morris Halle katika kitabu chao cha Sound Pattern of English (1968).


Bauduoin de Courtenay anaiona fonimu kama tukio la akilini ambalo huwa na nia ya mzungumzaji au jinsi msikilizaji anavyomwelewa mzungumzaji au vyote viwili kama ilivyoelezwa katika sura ya pili (taz. 2:3: 1). Kwa mujibu wa wataalam hawa fonimu inaonekana kuwa “taswira” ambayo kila fonimu inayo na taswira hizo zimejengeka akilini mwa binadamu. Fonimu ni dhana ya kisaikolojia au kipandesauti




34

 


ambacho picha yake imo akilini mwa binadamu na huikusudia aitoe wakati anapoongea. Kwa ujumla fonimu ni picha au taswira ya sauti ambayo imo akilini mwa mzungumzaji au mzungumzaji pamoja na wasikilizaji wa lugha fulani, Baudouin de Courtenay anasema.


Noam Chomsky na Morris Halle wao wanasema fonimu zina msimbo (code) uliopo akilini mwa mtu ambao hutumiwa wakati wa kuongea . Noam Chomsky katika kitabu chake cha Syntactic Structure (1957) anazungumzia umilisi na utendaji. Umilisi anauzungumzia kuwa ni ule ujuzi wa lugha ambao wazawa wa lugha fulani huwa nao na ndiyo huwawezesha kuzielewa sauti na tungo mbalimbali. Umilisi huu ndiyo huwafanya kuwa na taswira za fonimu mbalimbali katika akili zao na kuzitumia wakati wa kuongea. Noam Chomsky anapozungumzia umilisi anazungumzia kanuni za lugha zinazomwongoza msemaji katika kujua usahihi wa sauti za lugha na miundo ya tungo za lugha hiyo yaani utendaji.


Kutokana na maelezo au ufafanuzi huo ni kwamba wazungumzaji na wasikilizaji wote wana fonimu akilini mwao ambazo zina sifa tofauti tofauti katika lugha zinamotumika.



5: 1:1(c) Mtazamo wa Kifonolojia


Mtazamo huu unawagusa wataalam Nikolai Trubetzkoy na Ferdinand de Saussure. Wao wameitazama fonimu kifonolojia. Trubetzkoy ambaye alitumia misingi ya Saussure katika kitabu chake kiitwacho Principles of Phonology (1939) anasema:


“ Fonimu haiwezi kufasiliwa kikamilifu ama kwa kutumia kigezo cha sifa


za kisaikolojia na sifa za kifonetiki bali ni lazima ifasiliwe kwa kutumia sifa za uamilifu wa fonimu hiyo katika mfumo wa fonolojia ya lugha maalum inamotumika.”


Fonimu kwa ujumla ni jumla ya sifa za kifonolojia au kiuamilifu zinazohusu fonimu fulani.


Kutokana na mitazamo hiyo hapo juu inaonesha dhahiri kwamba fonimu ni kitamkwa chenye sifa bainifu za kiuamilifu katika lugha maalum. Fonimu hizi hujulikana na watumiaji wa lugha hiyo maalum.


Mitazamo hii kwa ujumla wake inaonesha kuwa na manufaa kwa kila mmoja katika kuifasili fonimu. Mtazamo wa kifonetiki unatutaka lazima tujue sifa za fonimu, mtazamo wa kisaikolojia unamtaka mtumiaji wa fonimu lazima ajue sifa na namna ya kuitamka fonimu hiyo kwa sababu fonimu hutamkwa kwa kutegemea akili inavyoiseti fonimu hiyo. Kifonolojia mtumiaji wa fonimu katika lugha yake maalum anapaswa kujua fonimu zinazotumika katika lugha maalum yake, ili kujua fonimu hizo ni lazima awe na umilisi wa lugha hiyo. Mitazamo hii humsaidia msemaji na mwanazuoni wa isimu katika kuchunguza na kuitumia fonimu. Kwa ujumla mitazamo hii hutegemeana na kukamilishana.


Lakini pia mitazamo hii hususani ule wa kisaikolojia na kifonetiki unaleta ugumu kwa mtumia lugha anatakiwa kuwa na umilisi wa kitaaluma kitu ambacho ni kigumu kwa watu wasio wazawa wa lugha husika lakini pia iwapo hana utaalamu na lugha

 




35

 


hiyo. Vilevile si rahisi kwa mgeni kujua fonimu au kuwa na taswira peke yake katika akili yake iwapo hatajua jinsi zinavyotumika katika lugha maalum. Kwa sababu hiyo mtumia lugha na mwanaisimu wanatakiwa kujua sifa zote za fonimu za kifonetiki, kisaikolojia na za kifonolojia.



5:1:2 Sifa za Fonimu


Fonimu kama kitamkwa kina sifa mbalimbali ambazo tunazitazama katika viwango mbalimbali. Fonimu kifonetiki ina sifa pambanuzi ambazo huitambulisha. Mfano fonimu yenye umbo [b] ina sifa ya kutamkiwa kwenye midomo, ni kipasuo kwa sababu hewa huzuiliwa kabisa kwa kutumia midomo ikitokea mapafuni na kuachiwa ghafula wakati wa utamkaji wake. Kitamkwa ama fonimu hii ina sifa ya ughuna kwa sababu katika kisanduku cha nyuzisauti kunakuwa na mtimbwiliko au mrindimo unaotokana na hali ya hewa ya kuzisukuma au kuziachanisha nyuzisauti. Kwa ufafanuzi zaidi chunguza mifano ifuatayo ambapo nitatumia alama ya kujumlisha (+) kwa sifa ambayo ipo na alama ya kutoa (-) kwa upande wa sifa ambayo haipo.


Mifano na: 2


Sauti / fonimu

[b] [ɤ] [ͻ] [ñ] [ɛ ]

[+ghun ] [ +ghun ] [+sil ] [+ghun ] [+sil ]

[+ant ] [+kons ] [+ghun ] [kons ] [+ghun ]

[+mid ] [+kor ] [+kont ] [+naz ] [+kont ]

[+kons ] [+juu ] [+nyum ] [+kor ] [+mbel ]

[-kont ] [ +kont ] [+son ] [+ant ] [+son ]

[-sil ] [+son ] [+kor ] [ +kont ] [+kor ]

[+uviring] [+ utandaz ] [+uviring ] [+msamb] [+utandaz]


Fonimu ina sifa nyingine ya kifonolojia kwamba kila fonimu ina sifa zake za kifonolojia zinazotumika kuipambanua fonimu husika katika lugha maalum. Mfano sauti /ʌ/ ni irabu katika lugha ya Kiingereza hutamkiwa katikati au katika kiwiliwili cha ulimi. Umbo la midomo huwa ni la utandazo wakati wa utamkaji wake. Hutokea katika maneno kama


Mifano na: 3


but   /bʌt/


cup  /kʌp/

come /kʌm/


Vile vile tuna fonimu / ñ /, fonimu au kitamkwa hiki kinapatikana katika lugha ya Kiswahili, hutamkiwa kwenye ufizi na ulimi hujiburuta kuelekea upande wa kushoto wa midomo. Sauti hii hutamkwa nyuzisauti zikiwa zimekaribiana sana au zikiwa pamoja na

 




36

 


hivyo hewa kutoka mapafuni huzisukuma ili kuziachanisha kwa ajili ya kupita. Fonimu hii hupatikana kaatika maneno mengi.


Mifano na 4


a) nyanya /ñaña /

b) nyama /ñama /

c) Nyamagana /ñamagana/


Fonimu kwa kawaida hueleweka na wazungumzaji wa lugha fulani kuwa nisauti za msingi katika lugha yao. Ninaposema fonimu hueleweka na wazungumzaji wote wa lugha fulani kama sauti za msingi nikimaanisha kwamba, wazungumzaji wa lugha hiyo wana taswira au wana picha za fonimu zote za msingi za lugha yao. Mifano wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza wana fonimu zisizopungua arobaini na nne (44) konsonanti na nne 24 na irabu ishirini (20). Fonimu hizi hujulikana na wazawa wote wa lugha ya Kiingereza. Hivyo basi fonimu ni sehemu ya umilisi wao wa lugha.


Vile vile fonimu hutumika kutofautisha maana na maumbo ya maneno fulani katika lugha maalum. Kwa mfano ukikudili fonimu moja katika neno fonimu hiyo hubadili maana ya neno. Mfano neno mama nikiondoa fonimu /m/ ya mwanzoni mwa neno na kuweka fonimu /k/ mwanzoni mwa neno nitapata neno kama na maana ya neno pia itabadilika.


Si hivyo tu, fonimu moja peke yake haina maana yaani ikisimama peke yake. Fonimu huleta maana pale tu inapoandamana na fonimu nyingine kwa kufuata mfumo wa lugha. Fonimu hujenga maana za maneno inapofanya kazi ndani ya mfumo wa lugha maalum huku ikiandamana na fonimu nyingine.


Mifano na: 5


Fonimu zenye kuleta maana kutokana na Fonimu zisizoleta zikisimama peke yake.

mfuatano mzuri

Pata, bata, beba, pete, kibo, sahani, mamba, /p/, /t/,/b/,/a/, /s/, /h/,/i/,/ɛ/, /m/,/g/,/n/ na /u/.

gauni.


Fonimu za upande wa kulia zinaonekana hazina maana lakini upande wakushoto zimepata maana baada ya kuandamana na fonimu nyingine mfano fonimu / p / inafanya kazi ya kulitofautisha neno “pata” na neno “bata” hali kadhalika fonimu /b/.


Fonimu ina tabia ya kubadilisha umbo la neno endapo fonimu zikabadilishana nafasi. Hapa ina maana kwamba kubadili kwa mpangilio wa fonimu maana na umbo la neno hubadilika pia. Mfano baadhi ya maneno, fonimu zake zikibadili mpangilio, hubadili umbo na maana ya maneno hayo.


Mifano na: 6


toa ……………………..ota


au……………………….ua

daka…………………….kada


pete……………………..kete

 




37

 

paka…………………….kapa


Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha mabadiliko katika mpangilio wa fonimu. Katika mfano wa namba i) mpangilio wa fonimu upande wa kwanza au upande wa kushoto unatupatia neno “ toa” lenye maana ya ondoa wakati la upande wa kulia baada ya badiliko kutokea tumepata neno “ota” ambalo limeanza na irabu na kufuatiwa na konsonanti na kisha irabu likiwa na maana ya kitendo cha kukaa karibu na moto au kukaa juani, kitendo cha mbegu kutokeza toka ardhini na kadhalika. Hali hii imejitokeza katika mifano yote yaani mfano namba ii) hadi v).


Kutokana na ufafanuzi huo hapo juu utagundua kuwa fonimu ni kipashio chenye sifa pambanuzi au bainifu zinazoibainisha na kuonesha uamilifu wake katika lugha maalum.



5:1:3 Aina za Fonimu


Katika kipengele cha (5:1) nimeeleza maana ya fonimu kuwa fonimu ni “ kitamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalum.” Fonimu katika lugha inagawanyika katika makundi matatu. Fonimu au vitamkwa hivyo ni konsonanti, irabu na viyeyusho. Vitamkwa hivi ndivyo hutumika katika kuunda maneno ya lugha.



5:1;3:1 Konsonanti


Konsonanti ni aina ya sauti au kitamkwa / fonimu ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondohewa kutoka mapafuni ukipitia ama chemba ya kinywa au chemba ya pua kwenda nje. Uzuiaji wa mkondohewa huo unaweza kuwa wa kubana kabisa na kuachiwa ghafula, kama tunapotamka sauti [p], [t], [b],[d],[k] na [g], unaweza kuwa wa kubana kabisa na kisha ukaachiwa taratibu hususani tunapotamka fonimu yenye umbo la ch [č] na [ɟ]. Unaweza kuwa wa kubana kiasi tu na kuruhusu hewa ipite katika nafasi nyembamba na wakati huo huo sauti hutamkwa, mfano tunapotamka sauti [s], [z],[f],[v],[υ],[ð],[θ],[ɤ] na kadhalika. Uzuiaji pia unaweza kuwa kuwa wa kubana hewa lakini ukiruhusu hewa kupita pembeni mwa ulimi hususani tunapotamka sauti au fonimu


na[ɬ]. Vile vile unaweza kuwa wa kubana kiasi huku ncha ya ulimi ikipigapiga sehemu iliyo baada ya mistari ya ufizi na kutupatia fonimu [r]. Lakini pia unaweza kuwa wa kubana hewa kinywani kwa kushusha kaakaa laini na kidaka tonge na kukutana na ulimi nyuma / shina la ulimi, ambapo huruhusu hewa ipite chemba ya pua kwenda nje ya kifua cha binadamu mfano tunapotamka fonimu [m],[ɱ], [n] [ñ] na [ŋ].


Konsonanti hizi zina sifa mahasusi ambazo huzitambulisha. Katika sura hii nitaeleza sifa za konsonanti kwa ujumla ambazo zinahusu makundi mbalimbali ya konsonanti.



5:1:3:1:1 Sifa Kuu za Konsonanti


Nimekwisha kueleza hapo juu kuwa nitazungumzia sifa za konsonanti zinazohusu makundi mbalimbali ya konsonanti ingawa konsonanti zina sifa nyingi. Katika ufafanuzi wangu nitashughulikia sifa kuu za msingi zinazozibainisha sauti hizi. Katika ubainishaji

 




38

 


wa sifa za konsonanti tunazingatia mambo makuu mawili. Jambo la kwanza ni mahali pa matamshi au sehemu ambayo konsonanti zinatamkiwa. Jambo la pili jinsi konsonanti zinavyotamkwa . Nitaanza kwa kueleza mahali pa mahali matamshi na kisha jinsi konsonanti zinavyotamkwa kwa ujumla wa vitamkwa konsonanti bila kujikita katika lugha fulani maalum.



5:1:3:1:1:1 Sifa za Konsonanti za Mahali pa Matamshi


Sifa za mahali pa matamshi huhusu sehemu mbalimbali za chemba za kinywa ambapo alasogezi na alatuli hugusana au hukaribiana wakati wa utamkaji wa sauti za lugha. Katika utamkaji wa sauti kuna sifa za matamshi yaani. Sehemu au mahali pa matamshi tisa ambazo zinahusu kugusana ama kukaribiana kwa alasogezi na alatuli,au alasogezi tupu. Hapa ni ufafanuzi wa sifa hizo.


Sifa ya kwanza ni ya midomo ambayo kwayo mkondohewa huzuiliwa kwa kuibana mdomo wa juu na mdomo wa chini ( mdomo wa juu na mdomo wa chini hugusana ambayo yote ni alasogezi) kisha hewa huachiwa au hubanwa kwa kuviringa midomo huku ikiwa imeacha upenyo mdogo ambao huwezesha sauti kadhaa kutamkwa au kutolewa. Zifuatazo ni sauti au ni fonimu zinazohusika na sifa hii.


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) b [b] mfano katika neno bakuli

b) p [p] mfano katika neno pahali, pia katika

neno pakyamba kutoka lugha ya

Kinyakyusa lenye maana ya

(mlimani)

c) m [m] mfano katika neno mpishi

d) ph [ɸ] (sauti itokeayo upulizapo kitu)

e) bh [β] mfano katika neno bhandu neno la

lugha ya Kinyakyusa lenye maana ya

(watu)


Sifa ya pili ni midomo –meno, sifa hii inahusu utamkaji wa sauti ambazo kwayo meno ya juu ambayo ni alatuli, hugusana na mdomo wa chini ambao ni alasogezi na wakati huo huo hewa inaruhusiwa kupita kwa kukwamizwakwamizwa katikati ya meno juu na mdomo chini. Hali hii ya kugusana kwa alasauti hizo huwezesha kutamkwa kwa sauti ziitwazo vikwamizi. Zifuatazo ni sauti zinazohusika na sifa hii:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) f [f] mfano katika neno fagia


b) v [v] mfano katika neno vuta

c) m [ɱ] mfano katika neno mvomero


d)vy [υ] mfano katika neno vyura


Sifa ya tatu ni ya meno, sifa hii inahusu utamkaji wa sauti ambazo kwayo ulimi ambao ni alasogezi hugusana na ufizi na meno ambazo ni alatuli. Ncha ya ulimi hugusa ufizi na

 




39

 


kuteleza au kuseleleka kwa haraka na kufika katikati ya meno juu na meno chini ambapo sauti hizo hutamkiwa. Utaratibu huu wa utamkaji unatuwezesha kutamka sauti kama zitakavyooneshwa hapa chini:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) th [θ] mfano katika neno thelath ini


b)dh [ð] mfano katika neno dh ambi


Sifa ya nne ya konsonanti ni ya ufizi ambayo inahusu utamkaji wa sauti ambazo kwayo ulimi ambao ni alasogezi hugusana na ufizi ambao ni alatuli. Kupitia mgusano huu wa alasogezi ulimi na alatuli ufizi huwezesha kutolewa kwa sauti mbalimbali kama ifuatavyo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) t [t] mfano katika neno tano au

la Kiingereza tin

b)d [d] mfano katika neno daka na la

lugha ya Kiingereza dark

c) s [s] mfano katika neno starehe

d) z [z] mfano katika neno zamaradi

e) n [n] mfano katika noa

f) l [l] mfano katika neno  lakini

g) l [ɬ] mfano katika neno matlai


Sifa ya tano ni ya baada ya ufizi ambayo inahusu utamkaji wa sauti ambayo kwayo alasogezi ulimi hugongagonga sehemu iliyo baada ya matuta au mistari ya ufizi ambayo ni alatuli. Kutokana na mgusano huo huwezesha kutamka sauti iitwayo kimadende.


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kawaida

a) r [r]  mfano katika neno rafiki


Sifa ya sita ni ya ufizi –kaakaa gumu ambayo inahusu utamkaji wa sauti ambayo kwayo alasogezi ulimi hugusana na sehemu iliyoko kati ya ufizi na kaakaa gumu ambayo ni alatuli. Kutokana na mgusano huo tunapata sauti zifuatazo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) sh [š] au [ʃ] mfano katika neno sheli

b) zh [ž] au [Ʒ] mfano katika neno la

lugha ya Kiingereza la

“measure


Sifa ya saba ni ya kaakaa gumu ambayo ni inahusu utamkaji wa sauti ambayo kwayo alasogezi ulimi hugusana na kaakaa gumu ambalo ni alatuli. Mgusano wa ulimi na kaakaa gumu hutuwezesha kupata sauti zifuatazo:

 







40

 

Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki


a) j [ɟ] mfano katika neno jalala

b) jh [ј] mfano katika neno jhone ( ni mimi)

kutoka katika lugha ya Kinyakyusa


c) ch [č] mfano katika neno chuma

d) ny [ñ] mfano katika neno nyama


Sifa ya nane ni ya kaakaa laini ambayo inahusu utamkaji wa sauti ambayo huandamana na sehemu ya nyuma ya ulimi ambayo ni alasogezi hugusana na kaakaa laini ambalo pia ni alasogezi. Mgusano huu wa alasogezi hizi huwezesha utamkaji wa sauti zifuatazo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki


a) k [k] mfano katika neno kamba

b) g [g] mfano katika neno gamba


c) gh [ɤ]  mfano katika neno ghala

d) ng’ [ŋ]  mfano katika neno  ng’ombe


Sifa ya tisa ni ya koromeo ambayo inahusu utamkaji wa sauti ambayo inahusisha sehemu ya koromeo. Sifa hii inahusu sauti ifuatayo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) h [h] mfano katika neno haleluya





5:1:3:1:1:2 Sifa za Konsonanti za Jinsi ya Matamshi


Ninaposema sifa za konsonanti za jinsi ya matamshi ninazungumzia namna konsonanti zinavyotamkwa. Kinachoangaliwa hapa ni namna hewa inavyoachiwa wakati wa utamkaji. Mkondohewa huweza kubanwa kabisa au kuzuiliwa kiasi na kuachiwa taratibu kwa kukwamizwakwamizwa. Mkondohewa unaweza kabisa, huachiwa na kupita lakini kwa kugusanisha alasogezi na alasauti nakadhalika. Kutokana na sifa ya jinsi ya matamshi konsonanti hugawanyika katika makundi makubwa sita yaani vipasuo, vizuio kwamizi, vikwamizi, nazali, vitambaza na vimadende.


Kundi la kwanza ni la vipasuo, kundi hili la konsonanti lina sifa kuu pambanuzi ambayo inazipambanua konsonanti hizi. Utamkaji wa konsonanti hizi ni ule wa mkondohewa kubanwa kabisa mahali pa kutamkia sauti au konsonanti hizo na kisha huachiwa ghafula wakati wa kutolewa sauti inayohusika. Konsonanti hizi zimepewa jina hilo kwa sababu ya mkondohewa kuachiwa ghafula na fonimu au sauti itokayo huwa kama ina mlio wa kupasua. Kundi hili linajumuisha sauti zifuatayo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki


a) p [ p] mfano katika neno pamela

b) b [b] mfano katika neno bendera


c) t [t]  mfano katika neno kuta

 




41

 

d) d [d] mfano katika neno daraja

e) k [k] mfano katika neno kamera


f) g [g] mfano katika neno gunia


Sauti hizi zinapotamkwa utahisi utasikia kama mlio wa kitu kilichopasuka, mlio wa kupasua kitu.


Kundi la pili ni vizuio kwamizi, konsonanti hizi zinapotamkwa huruhusu mkondohewa kuzuiliwa na kuachiwa taratibu kwa kukwamizwakwamizwa. Vizuio kwamizi ni kundi lenye vitamkwa fonimu hizi.


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) ch [č] mfano katika neno chuo


b) j [ɟ] mfano katika nneno Jeremia.


Kundi la tatu ni la vikwamizi, hizi ni konsonanti ambazo utamkaji wake hutofautiana na vizuio kwamizi. Mkondohewa huzuiliwa kwa kubana kiasi fulani huku msogeano wa alasauti (alasogezi na alatuli) huwa mwembamba. Hii ina maana kwamba msogeano huo huwa na nafasi nyembamba na kuruhusu hewa ipite katika nafasi hiyo taratibu hadi yote inaisha kutoka mapafuni. Vikwamizi ni sauti ambazo wakati wa utamkaji wake hewa huzuiliwa kiasi na kupenyeza katika nafasi nyembamba sana iliyoko katikati ya alasauti zinazohusika katika utamkaji. Kutokana na msogeano mwembamba wa alasauti na hewa kupenyeza katika nafasi hiyo nyembamba husababisha sauti kutolewa kwa kukwamizwakwamizwa. Kundi hili linajumuisha sauti zifuatavyo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki


a) f [f] mfano katika neno fahamu

b) v [v] mfano katika neno veranda


c) th [θ] mfano katika neno themanini

d) dh [ð] mfano katika neno dhahabu


e) s [s] mfano katika neno samaki

f) z [z] mfano katika neno zabuni


g) sh [š] mfano katika neno shamba

h) zh [ž] au [Ʒ] mfano katika neno la


Kiingereza “leisure”

Ambalo hutamkwa


[leƷə] au [li:Ʒər]

i) h [h] mfano katika neno heko



Kundi la nne ni nazali, ni konsonanti ambazo hutamkwa kwa kuruhusu mkondohewa kupitia chemba ya pua. Sauti hutakwa pale ambapo hewa kutoka mapafuni husafiri inapofika eneo la koromeo kidaka tonge na ulimi nyuma au shina la ulimi hukutana (yaani kidaka tonge hushuka na shina la ulimi huinuka na kukutana) na kuzuia njia ya chemba ya kinywa hivyo hewa hulazimika kupita katika chemba ya pua ili kutoka nje. Kundi hili hujumuisha sauti zifuatavyo:

 





42

 

Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) m [m] mfano katika neno mabaki


b) n [n] mfano katika neno nishai

c) m [ɱ] mfano katika neno mvua


d) ny [ñ] mfano katika neno nyembamba

e) ng’ [ŋ] mfano katika neno ng’ambo


Kundi la tano ni vitambaza, ni konsonanti ambazo hutamkwa kwa kuutandaza ulimi huku ncha ya ulimi ikigusana na ufizi na ambayo ni alatuli na kuruhusu hewa kupita pembeni mwa ulimi. Ulimi unapogusa ufizi hewa hulazimika kupita pembeni mwa ulimi ambamo mna nafasi. Kundi hili linajumuisha sauti zifuatazo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) l [l] mfano katika neno lamba


b) l [ɬ] mfano katika neno matlai


Kundi la sita ni la vimadende, hizi ni konsonanti ambazo hutamkwa kwa kupigapiga au kugongagonga ulimi kwenye sehemu iliyoko baada ya ufizi kwa marudio ya harakaharaka. Hapa ncha ya ulimi hugongagonga mara nyingi kwenye sehemu baada ya ufizi kwa harakaharaka huku hewa ikitoka nje kutoka kwenye chemba ya kinywa. Kundi hili hujumuisha sauti zifuatazo:


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifoneti

a) r [r] mfano katika rehani


Sauti zote zilizoandikwa kwa wino mzito katika kila safu ya vitamkwa/ fonimu upande wa maneno yaliyotolewa kuwa mifano inayobeba fonimu, hayo ndiyo maumbo ya fonimu kitahajia sawa na yale yaliyoko upande wa maandishi ya kawaida.


Kwa ujumla konsonanti hubainishwa kuangalia sifa za matamshi yaani jinsi zinavyotamkwa na mahali zinapotamkiwa. Lakini pia konsonati hutazamwa katika nafasi ya nyuzisauti (hali ya nyuzisauti).



5:1:3:1:1:3 Sifa za Konsonanti za Mtimbwiliko wa nyuzisauti


Konsonanti ni sauti ambazo zina sifa kuu ambazo nimezichunguza hapo juu kuwa zina mahali pa matamshi na namna au jinsi ya kuzitamka. Mbali na sifa hizo konsonanti zina sifa nyingine za mtimbwiliko au mrindimo wa nyuzisauti katika kisanduku cha nyuzisauti wakati utamkaji wake. Kutokana na mtimbwiliko wa nyuzisauti konsonanti zinagawanyika katika makundi mawili. Makundi hayo ni konsonanti ghuna na konsonanti si ghuna.


Kundi la kwanza ni konsonanti ghuna, hizi ni konsonanti ambazo hutamkwa wakati nyuzisauti zikiwa zimekaribiana au zimegusana na hivyo hewa kutoka mapafuni huzisukuma ili ipite. Katika hali ya kuzisukuma nyuzisauti hizi ili kuziachanisha na kupita husababisha nyuzisauti kutetemeka au kutimbwilika, na huo mtimbwiliko huifanya sauti inayotamkwa kuwa na msikiko mkubwa wenye mghuno. Kundi hili linajumuisha

 




43

 


konsonanti hizi; [b], [d],[g] [m][ɱ], [n],[ñ], [ɳ], [ŋ], [v], [ ɤ], [ɦ], [υ], [ð], [θ],[ ɟ],[Ʒ], [ɬ], [l], [r] na kadhalika. Sauti hizi zina mguno wakati zinapotamkwa.


Kundi la pili ni konsonannti sighuna au visoghuna, hizi ni sauti ambazo hutamkwa wakati nyuzisauti zikiwa zimeachana na hivyo hewa hupita kwa urahisi bila kashikashi au usumbufu wowote na kusababisha kutokuwepo kwa mtimbwiliko au hali ya kutimbwilika kwa nyuzisauti. Kundi hili linajumuisha sauti hizi; [p], [t], [k], [f], [s],[θ], [č], [ɸ], [š], [h] na kadhalika. Sauti hizi hutamkwa iwapo uwazi uliopo katikati ya nyuzisauti (yaani aina ya misuli ya kambakamba laini zilizoko katika koromeo) umebaki kama ulivyo.





5:1:3:2 Irabu


Irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasi, bila kuwepo kizuizi chochote katika mkondohewa au hewa itokayo mapafuni ikipitia katika chemba ya kinywa au ya pua iwapo irabu hiyo itasilimishwa. Irabu ziko za aina nyingi lakini mimi nitatumia zaidi irabu za lugha za Kibantu na lugha ya Kiingereza tu. Katika kuainisha sifa za irabu ni lazima kuzingatia lugha ambamo irabu hizo zinatumika, kwa sababu kila lugha huchagua idadi ya irabu kadhaa kutoka katika bohari la sauti kwa kuzingatia irabu msingi ambacho ndicho msingi wa irabu za lugha mbalimbali.


Kuhusu lugha za Kibantu kuna irabu kuu tano ambazo hutumika karibu katika lugha nyingi za Kibantu na lugha ya Kiswahili ikiwemo kama asemavyo Massamba na wenzake (2004). Irabu hizo huwakilishwa kiimaandishi kama ifuatavyo.


Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

a) i [i] mfano katika neno lia, pi ka

b) e [ε] mfano katika neno cheka

c) a [a] mfano katika neno kale

d) o [ɔ] mfano katika neno pokea,bomani

e) u [u] mfano katika neno tume


Irabu hizi katika taaluma ya fonetiki huweza kuoneshwa kwa kutumia kielelezo kiitwacho Trapeziam ya Irabu (The Vowel Trapezium) ambacho kinaonesha mahali pa matamshi pa irabu na kiwango cha mwinuko wa ulimi wakati wa utamkaji wa irabu hizo. Hapa ni kielelezo cha irabu hizo.

 


















44

 

Kielelezo Na: 6 Trapeziam ya Irabu za Kibantu




















Hizi ni irabu zinazopatikana katika lugha za Kibantu zilizo nyingi. Kiswahili kama lugha yangu ya msingi ambayo ndiyo msingi wa kazi hii nayo ina idadi hiyo ya irabu. Lakini irabu hizi hususani za lugha ya Kiswahili nitazizungumzia zaidi katika sura itakayofuata. Irabu hizi zina sifa zifuatazo:


Irabu sifa za irabu

1. [i] ina sifa za [+juu], [+mbele], [+msamb ] –hali ya midomo ni ya

kutabasamu  au msambao.

2. [ε] ina sifa za [+kati], [+mbele], [+utandaz] –hali ya midomo ni ya kutandaza

au hali isiyo bainifu.

3. [a] ina sifa za [+chini], [+kati], [+utandaz] –hali ya midomo ni ya kutandaza

au hali isiyo bainifu.

4. [ɔ] ina sifa za [+ kati], [+nyuma], [+uviring] –hali ya midomo ni ya

kuviringwa si kwa kufunga kabisa

5: [u] ina sifa za [+juu], [+nyuma], [+uviring] –hali ya midomo ni kuviringwa

kwa kufunga kabisa.


Pia kuna irabu kuu za msingi katika lugha ya Kiingereza Sanifu. Irabu hizi za msingi ziko kumi na mbili zinazotumika katika Kiingereza Sanifu Thorne (1997). Irabu hizi huwakilishwa katika maandishi kama ifuatavyo.



Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki

1. ee, ea, ie [i:] mfano katika neno seen, lead, believe

2. i, e [ɪ] mfano katika neno pit, reply

3. e, a [e] mfano katika neno basin wet, check

4. a [æ] mfano katika man, land, happy

5. a ar [ɑ:] mfano katika neno last, darling,card

6. o [ɒ] mfano katika neno got, contract, pot

7. or, aw,ar [ɔ:] mfano katika neno saw, ward, cord

8. u,oo [ʊ] mfano katika neno put, book, poverty

 




45

 

9. oo,ue,u [u:] mfano katika neno too, cute, blue

10. u [ʌ]  mfano katika neno but, lust, cup

11.ea(r), ir, u(r), er [ɜ:] mfano katika neno heard, bird, fur, person

purpose

12. a, e, o,io [ə] mfano katika neno not, along, barren,

benediction.



Katika maneno hayo hapo juu yaliyotolewa mifano kuna alfabeti nyingine zilizoandikwa kwa wino mzito, alfabeti hizo zinawakisha sauti husika kama inavyoonekana katika safu hiyo ya fonimu irabu za Kiingereza.


Irabu hizi za lugha ya Kiingereza katika taaluma ya fonetiki zinaweza kuoneshwa kwa kutumia kielelezo cha kitaaluma kinachoonesha mwinuko wa ulimi, mahali ambapo pameinuka, mahali ambapo irabu hizo hutamkiwa na sehemu za ulimi. Kielelezo hiki kinaitwa Trapeziam ya irabu za Kiingereza (English trapezium vowel). Hebu chungua kielelezo hicho hapa chini.



Kielelezo  na:7 Trapeziam ya irabu za lugha ya Kiingereza




























Irabu hizi kumi na mbili za lugha ya Kiingereza ndizo irabu za msingi katika lugha hiyo. Irabu hizi zina sifa pambanuzi za msingi kama ifuatavyo;


Sauti /fonimu Sifa za irabu


1. [i:] ina sifa za [+juu],[+mbele], [+msamb] –hali ya midomo ni ya

kutabasamu au msambao,[+wakaa mrefu]

 




46

 

2. [ɪ] ina sifa za [+juu kidogo ya juu kati], [+mbele], [+msamb] – hali ya

midomo ni ya kutabasamu au msambao [+wakaa mfupi]

3. [e] ina sifa za [+ kati ya juu kati na chini kati], [+mbele], [+utandaz] – hali

ya midomo ni ya kutandaza au si bainifu, [+wakaa mfupi]

4. [æ] ina sifa za [+juu kidogo ya chini],[+mbele], [+msamb],

[+wakaa mfupi]

5. [ɑ:] ina sifa za [+chini ], [+nyuma], [+utandaz], [+wakaa mrefu]

6. [ɒ] ina sifa za [+kati ya chini na chini kati], [+nyuma], [+uviring] –hali

ya midomo ni ya kuviringa kana kwamba unabeza [+wakaa mfupi]

7. [ɔ:] ina sifa za [+ kati ya chini kati na juu kati], [+nyuma],[+uviring] –hali

ya midomo huwa ni ya kuviringwa kiasi,[+wakaa mrefu]

8. [ʊ] ina sifa za [+juu kidogo ya juu kati], [+nyuma], [+uviring],

[+wakaa mfupi]

9. [u:] ina sifa za [+juu], [+nyuma], [+uviring] – hali ya midomo ni

ya uviringo wa kubana,[+wakaa mrefu]

10.[ʌ] ina sifa za [+chini ya chini kati],[+kati], [+utandaz],

[+wakaa mfupi]

11.[ɜ:] ina sifa za [+kati ya juu kati na chini kati], [+kati], [+utandaz],

[+wakaa mrefu].

12.[ə] ina sifa za [+ kati ya juu kati na chini kati], [+kati], [+utandaz],

[+wakaa mfupi].





5:1:3:2:1 Sifa Kuu za Irabu


Irabu ni vitamkwa ambavyo vina sifa zake kuu zinazojitokeza katika lugha mbalimbali. Lakini nitajikita katika vipengele muhimu ambavyo hutofautisha fonimu irabu na fonimu konsonanti. Irabu huainishwa kwa kutumia vigezo vikuu vitatu ambavyo ni:

sehemu ya ulimi inayohusika na utamkaji


mwinuko wa ulimi wakati wa utamkaji na

hali ya midomo wakati wa utamkaji


Kigezo cha kwanza ni sehemu ya ulimi inayohusika na utamkaji wakati wa kutamka irabu hizo. Ulimi umegawanyika katika sehemu kuu tatu; mbele ambayo inajumuisha ncha ya ulimi, sehemu ya pili ni kati au bapa la ulimi, na sehemu ya tatu ni nyuma au shina la ulimi. Katika sehemu hizi tunapata sauti irabu mbalimbali kama ifuatavyo:

Sehemu ya mbele ya ulimi hutumika katika utamkaji wa irabu za kibantu za


na [ɛ], na irabu za lugha ya Kiingereza ambazo ni [i:], [e],[ɪ] na [æ]. Irabu hizi hutamkiwa sehemu ya mbele ya ulimi. Irabu hizi zinajulikana kama irabu mbele.


Sehemu ya kati ya ulimi hutumika au huhusika katika utamkaji wa irabu ya kibantu

ijulikanayo irabu kati, na irabu za lugha ya lugha za Kiingereza ambazo ni


[ʌ], [ə] na [ɜ:] ambazo hujulikana kama irabu kati.


Sehemu ya nyuma ya ulimi huhusika katika utamkaji wa irabu [ɔ] na [u] za lugha za Kibantu, vile vile huhusika katika utamkaji wa irabu za Kiingereza ambazo ni


[ɑ:], [ɒ], [ɔ:], [ʊ] na [u:] zijulikanazo kama irabu nyuma.

 




47

 


Kigezo cha pili ni mwinuko wa ulimi ndani ya chemba ya kinywa. Kifonetiki ulimi umegawanyika katika sehemu nne za miinuko ya ulimi. Miinuko hii ni mwinuko juu, mwinuko nusu juu (juu kati), mwinuko nusu chini (chini kati) na mwinuko chini. Katika miinuko hii sauti irabu huweza kuangukia ama kati ya mwinuko chini na nusu chini (chini kati) au chini au juu au kati ya juu na na juu kati au katikati ya juu kati na chini kati.


Mwinuko juu – huu unahusisha utamkaji wa sauti irabu [i] na [u] za lugha za Kibantu na za lugha ya Kiingereza ambazo ni [i:] na [u:] zinazojulikana kama irabu juu.


Mwinuko juu kati – katika utamkaji wa mwinuko huu sauti irabu huangukia eneo


lililoko kati ya juu na juu kati ambapo ulimi huinuka zaidi ya mwinuko juu kati kidogo ambapo tunapata sauti [ɪ] na [ʊ] irabu hizi ziajulikana kama irabu juu kidogo ya juu kati.Wakati sauti irabu za kibantu [ε] na [ɔ] hutamkiwa katika mwinuko wa juu kati. Irabu hizi zinajulikana kama zenye sifa ya kati ya juu kati na chini kati.


Mwinuko chini kati – katika mwinuko huu sauti irabu za lugha za Kibantu ambazo hutamkwa katika mwinuko huo ni [e] na [o] na katika lugha ya Kiingereza


irabu hizi huangukia katikati ya mwinuko juu kati na chini kati. Irabu hizo ni [e], [ɔ:], [ɜ:] na [ə] sauti hizi mwinuko wa ulimi si juu kati wala si chini kati halisi bali uko kati ya juu kati na chini kati.

Mwinuko chini – katika mwinuko huu irabu [a] ya lugha ya Kibantu hutamkiwa


na sauti [ɑ:] ya lugha ya Kiingereza hutamkiwa katika mwinuko huo. Lakini kuna sauti irabu [æ] na [ɒ] za lugha ya Kiingereza hutamkiwa juu kidogo ya mwinuko chini wakati irabu [ʌ] hutamkiwa kati ya mwinuko chini na chini kati (nusu kati) , nayo ni irabu ya lugha ya Kiingereza.


Kigezo cha tatu ni hali ya midomo wakati wa utamkaji wa irabu. Hapa hali ya midomo au umbo la midomo huwa katika hali tatu, uviringo, msambao na utandazo au hali ambayo si bainifu.


Uviringo wa midomo, hali au umbo hili la midomo huhusu utamkaji wa sauti irabu [ɔ] na [u] za lugha za Kibantu wakati huo huo huhusu utamkaji wa irabu


[ɔ:], [ɒ], [ʊ] na [u:] za lugha ya Kiingereza.


Msambao wa midomo, hali au umbo hili la midomo huhusu utamkaji wa irabu [i] ya lugha za Kibantu na irabu [i:], [ɪ] na [æ] za lugha ya Kiingereza. Midomo inapokuwa imesambaa kama kwamba unataka kutabasamu basi sauti au irabu hizi hutamkwa.


Utandazo wa midomo, hali ya midomo inapokuwa si mviringo wala si msambao huitwa hali ya midomo si bainifu au ya utandazo. Umbo hili la midomo huhusu utamkaji au hupelekea kutamkwa kwa sauti irabu [a], [ɛ] na [e] za lugha za Kibantu wakati huo huo irabu [e], [ɑ:], [ʌ], [ɜ:] na [ə] za lugha ya Kiingereza.


Hivyo ndivyo vigezo vyote vya msingi katika kubainisha sifa pambanuzi za irabu zinazozitofautisha irabu moja na irabu nyingine. Kwa mwanafunzi wa somo la fonolojia na mwanaisimu wa lugha lazima azingatie vigezo hivi, vipo katika upambanuzi wa sifa bainifu za irabu.

 




48

 

5: 1:3:3 Viveyusho


Viyeyusho ni aina ya vitamkwa ambavyo si konsonanti wala si irabu. Ni vitamkwa ambavyo huchukuliwa kwamba viko katikati ya irabu na konsonanti. Hii ina maana kwamba kwa kiasi fulani vitamkwa hivi hufanana na sauti konsonanti wakati huo huo kiasi kikubwa hufanana na sauti irabu katika umbile la utamkaji wake. Kwa hakika vitamkwa hivi havina sifa kamili za ukonsonanti na pia havina sifa kamili za uirabu lakini vinaelekea zaidi kufanana na irabu na hivyo wakati mwingine huitwa nusu irabu. Katika lugha mbalimbali za Kibantu pamoja na Kiingereza viyeyusho vipo vya aina mbili.


Lugha za kibantu

Maandishi ya kawaida Maandishi ya kifonetiki


a) y [y] mfano katika neno yenu, yule, yake

b) w [w] mfano katika neno wale, werevu wetu


Lugha ya Kiingereza

Maandishi ya kawaida Maandishi ya  kifonetiki


a) y [j] mfano katika neno you, yawn,

Jerusalem, yes


b) w [w] mfano katika neno wait, wet,


Katika mifano hiyo hapo juu kuna alfabeti zilizoandikwa kwa wino mzito zinawakilisha viyeyusho ambavyo vimeoneshwa katika safu hizo hapo juu.


Viyeyusho kama ilivyo ada ya vitamkwa vyote vya lugha vina sifa kuu zake ambazo hugawanyika katika makundi mawili.



5:1:3:3:1 Sifa za Viyeyusho za Mahali pa Matamshi


Viyeyusho ni vitamkwa ambavyo vina sifa kama fonimu konsonanti na fonimu irabu. Viyeyusho vina sifa za mahali pa matamshi, kwa maana ya mahali ambapo viyeyusho hivyo hutamkiwa. Ninaposema mahali pa matamshi nina maana ya alasauti zinazohusika katika utamkaji wa viyeyusho hivyo.


Kwa upande wa viyeyusho vya lugha za Kibantu zina sifa pambanuzi ziko hivi:


Upande wa mahali pa matamshi, kiyeyusho [w] kina sifa ya kutamkiwa kwenye midomo kwamba alsauti midomo ndiyo huhusika na utamkaji wa kiyeyusho hicho.


Kwa upande wa kiyeyusho [y] kina sifa ya kaakaa gumu. Kiyeyusho hiki kinatamkiwa katika alasauti kaakaa gumu.


Upande wa viyeyusho vya viyeyusho vya lugha ya Kiingereza sifa pambanuzi zake ziko hivi:


Sifa ya mahali pa matamshi ya kiyeyusho [w] ni ya midomo kwa sababu wakati wa utamkaji wake alasauti midomo ndiyo huhusika. Mdomo juu na mdomo chini hukutana.

 







49

 


Kwa upande wa kiyeyusho [j], hiki kina sifa ya kaakaa gumu ya mahali pa matamshi kwa maana kwamba ulimi kati huinuka na kugusana na kaakaa gumu, mgusano huo husababisha kutamkwa kwa kiyeyusho hicho.



5:1:3:3:2 Sifa za Jinsi ya Mahali pa Matamshi


Viyeyusho vina namna au jinsi ya kutamkwa sifa hii inagusa viyeyesho kama ilivyo kwa vitamkwa vilivyotangulia. Viyeyusho vinapotamkwa vina namna ambayo hewa toka mapafuni inavyoachiwa, mkondohewa au hewa haizuiliwi kama konsonanti lakini haipiti kinywani kama ilivyo kwa irabu. Hali ya mkondohewa haifungamani na upande wa irabu yaani kutoka moja kwa moja bila kizuizi au kuwa na kizuizi kikubwa kama ilivyo kwa sauti konsonanti.


Kwa upande wa viyeyusho vya lugha za Kibantu sifa pambanuzi ziko hivi:


Upande wa jinsi au namna ya matamshi ya kiyeyusho [w] , kina sifa ya kuviringa kama kwamba unataka kutamka irabu [ʊ] fupi ya lugha ya Kiingereza, umbo ambalo hudumu kwa muda mfupi tu na kisha hutoweka wakati wa utamkaji wake.


Kwa upande wa kiyeyusho [y], hiki kina sifa ya kusambaza midomo kama kwamba unataka kutamka irabu [ɪ] fupi ya lugha lugha ya Kiingereza umbo


ambalo hudumu kwa muda mfupi.

Upande wa viyeyusho vya lugha ya Kiingereza hakuna tofauti na vile vya lugha za


Kibantu. Viyeyusho vina sifa pambanuzi za jinsi ya matamshi zifuatavyo:


Upande wa jinsi ya matamshi wa kiyeyusho [w], kina sifa ya kuviringa midomo kama kwamba unataka kutamka irabu [ʊ] fupi ya lugha ya Kiingereza, umbo hilo hudumu kwa muda mfupi tu na kisha hutoweka wakati wa utamkaji wa kiyeyusho hicho.


Kwa upande wa kiyeyusho [j] , kina sifa ya kusambaza midomo kama kwamba unataka kutabasamu ili kuunda irabu [ɪ], umbo ambalo hudumu kwa muda mfupi kisha hutoweka wakati wa utamkaji wake.


Kwa ujumla vitamkwa au fonimu zote zina sifa pambanuzi zinzozibainisha na kuzitofautisha viyeyusho hivyo kutoka kiyeyusho kimoja kwenda kiyeyusho kingine. Hivyo basi msikilizaji na mwanazuoni wa lugha anatakiwa kuzingatia sifa hizo kwa sababu ndizo zinazomjengea umilisi wa lugha maalum anayoishughulikia.



5:2 Alofoni


Swali tunalojiuliza akilini mwetu tulio wengi ni juu ya istilahi alofoni kwamba, Je alofoni ni nini? Alofoni zinatofautianaje na fonimu? Ukweli ni huu kwamba alofoni ni dhana inayofungamana na fonimu lakini ni tofauti na fonimu. Kifasili alofoni ni maumbo tofauti tofauti ya sauti zinazowakilisha fonimu moja. Kimsingi alofoni ni sauti ambazo zina sifa za mahali pa matamshi tofauti hali kadhalika sifa za jinsi ya matamshi ni tofauti. Ni mara chache alofoni kufanana kwa baadhi ya sifa hususani za mahali pa matamshi lakini upande wa jinsi ya matamshi naweza kusema kwamba hazifanani kabisa.

 




50

 


Alofoni hazibadili maana ya neno inapojitokeza au inapotumika katika mfumo wa lugha inayohusika. Maana ya neno hubaki kama ilivyo bali umbo hutofautiana na mazingira ya umbo lingine lenye maana sawa na hilo kutokana na athari za kanuni za kifonolojia. Hebu chungua mifano ifuatayo:


a)Mifano kutoka katika lugha ya Kiswahili


Kwa kutumia kigezo cha kifonolojia peke yake. Mifano ya fonimu na: 7


1. fonimu [p] ina alofoni zifuatazo:

[p] ………[p] mfano katika neno “paa”  lenye maana ya kuondoa

Magamba ya samaki.

……….[ph] mfano katika neno “paa” lenye maana ya mnyama

afananaye na swala.



2. fonimu [t] ina alofoni zifuatazo:


[t]……………..[t] mfano katika neno “taa” likiwa na maana ya kifaa

Kitoacho mwanga.

…………….[th] mfano katika neno “taa” likiwa na maana ya aina ya

Samaki wa baharini.


fonimu [č] ina alofoni zifuatazo:


[č]…………….[č] mfano katika neno “čungu” lenye maana ya chombo udongo cha kupikia.


……………[čh] mfano wa neno “č h ungu” lenye maana ya mdudu mdogo afafanaye au jamii ya sisimizi.


Kutokana na mifano hiyo hapo juu tunaona fonimu [p] ina alofoni mbili ambazo ni [p] na [ph], fonimu [t] ina alofoni mbili ambazo ni [t] na [th], na fonimu [č] iliyoko katika mfano wa namba 3 ina alofoni mbili ambazo ni [č] na [čh].


Kwa kutumia kigezo cha mofofonolojia yaani kigezo cha uhusiano baina ya fonolojia na mofonolojia. Hebu chunguza mifano ifuatayo:


Mifano na: 8


Mofimu za neno Matamshi yake

1. ki +ki ki+refu [kiti kirɛfu]

2. ki +ti ki +eusi [kiti čɛusi ] au [kiti cheusi]

3.ki +akula [čakula ] au [chakula   ]


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa fonimu [k] ina alofoni mbili ambazo ni


na [č]. Mazingira ya utokeaji wa alofoni hizo umedhibitiwa na kanuni za kifonolojia au mpangilio wa vipashio fonimu. Mfano alofoni [k] hutokea pale ambapo fonimu [k]

 




51

 


inafuatiwa na irabu [i], halafu mpaka wa mofimu na kufuatiwa na mofimu inayoanza na fonimu konsonanti. Lakini utokeaji wa alofoni [č] ni pale ambapo fonimu [k] inapofuatiwa na irabu [i] halafu mpaka wa fonimu kisha inafuatiwa na mofimu inayoanza na fonimu [a] au [ε] zenye tahajia ya a na e, fonimu [k] hubadilika na kuwa ch yaani fonimu [č] kama ilivyo katika neno ki+eusi →cheusi na neno ki+akula → chakula (taz. Massamba na wenzake 2004:21 – 23).


Mbali na kuwepo kwa kanuni hizo za kifonolojia kudhibiti utokeaji wa alofoni lakini pia ni lazima kujua kuwa kuna baadhi ya maneno ambayo yanayokataa kanuni hizo. Maneno yenye tabia ya namna hiyo huitwa vighairi kwani yanapingana na ruwaza za kifonolojia na hivyo hakuna mabadiliko japokuwa fonimu [k] hufuatiwa na irabu [i] halafu mpaka wa mofimu, na kufuatiwa na irabu [a] lakini hakuna badiliko lolote. Hebu chungua mifano ifuatayo.


Mifano na: 9


Mofimu za neno Matamshi yake


1. ki +azi [kiazi ]

2. ki +atu [kiatu ]


Upande wa lugha ya Kiingereza hali ni hiyo hiyo kwamba fonimu zina alofoni zake.


Alofoni hizi hujitokeza katika kiwango cha fonolojia na cha mofofonoljia.

b)Mifano kutoka katika lugha ya Kiingereza.


i) Kwa kutumia kigezo cha fonolojia.


Mifano na: 10

fonimu [æ] ina alofoni zifuatazo:


………………….[æ] mfano katika neno “and” [ænd] ambalo ni kiunganishi chenye kupewa mkazo wakati


utamkaji wake.

………………….[ə]  mfano katika neno “and” [ənd] lenye maana ya


kiunganishi kisicho na mkazo katika utamkaji

wake


fonimu [ɒ] ina alofoni zifuatazo:


[ɒ]…………………...[ɒ] mfano katika neno “ contract” [kɒntrækt]  lenye

maana ya mkataba na katika kategoria za


manreno ni nomino.

…………………..[ə] mfano katika neno “contract” [kəntrækt] lenye


ingia mkataba au fanya maagano na katika

kategoria za maneno ni kitenzi.


fonimu [ɜ:] ina alofoni zifuatazo:


[ɜ:]………………….[ɜ:] mfano katika neno “permit” [ˈpɜ:mɪt] lenye maana

ruhusa ambalo kategoria yake ni nomino.


………………….[ə]  mfano katika neno “permit” [pəˈmɪt] lenye maana

ya ruhusu,na kategoria yake ni kitenzi.

 




52

 


Kutokana na mifano hiyo hapo juu tunaona kwamba fonimu [æ] ina alofoni mbili ambazo ni [æ] na [ə], ambazo zinaonesha uwekaji wa mkazo katika neno and, fonimu [ɒ] ina alofoni mbili ambazo ni [ɒ] na [ə] ambazo huonesha kategoria za neno contract na fonimu [ɜ:] ina alofoni mbili ambazo ni [ɜ:] na [ə] ambazo nazo huonesha kategoria za neno permit


Kwa kutumia kigezo cha mofofonolojia (uhusiano baina ya fonolojia na mofolojia). Hebu chunguza mifano ifuatayo:


Mifano na: 11


Mofimu za maneno Matamshi yake.


Mofimu ya hali ya mazoea.

1. play + s [pleɪz]


2. look + s [lʊks ]

3. touch +es [tɑʧɪz]


4. go +es [gəʊɪz]

5.lead +s [li:ds  ]


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua fonimu [s] ina alofoni tatu ambazo ni [z], [s] na [ɪz] ambazo utokeaji wake uko kama ifuatavyo:


Maneno yenye mzizi unaoishia na sauti konsonanti au kiyeyusho katika tahajia yake na katika


matamshi yake huishia na irabu au vokali mbili ambazo hutamkwa kamakwamba ni moja, mizizi ya namna hiyo hupokea alofoni [z] katika matamshi yake kama ilivyo katika mfano namba 1.


Maneno yenyemzizi unaoishia ama na konsonanti ghuna au si ghuna katika tahajia yake na


katika matamshi yake huishia na konsonanti kadhalika, mizizi hiyo hupokea alofoni [s] katika matamshi yake kama ilivyo katika mfano namba 2 na namba 5.


Maneno yenye mizizi inayoishia na vizuio kwamizi na irabu katika tahajia na katika matamshi


yake pia mizizi hii hupokea alofoni [ɪz] katika matamshi yake kama ilivyo katika mfano namba 3 na 4.


Tabia hii hujitokeza pia katika njeo wakati uliopita ya lugha ya Kiingereza. Ifuatayo ni mifano:


Mifano na: 12

Mofimu za maneno Matamshi yake

Mofimu ya njeo ya wakati uliopita

1. look +ed [lʊkt  ]

2. train +ed [treɪnd]

3. kill +ed [kɪld  ]

 





53

 

Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha kwamba [d] ina alofoni mbili ambazo ni [t] na

na utokeaji wake uko hivi:


Maneno yenye mizizi inayoishia na konsonati si ghuna maneno hayo hupokea alofoni [t] wakati wa utamkaji wake kama ilivyo katika mfano wa 1


Maneno yenye mizizi inayoishia na konsonanti ghuna maneno hayo hupokea alofoni [d] wakati wa utamkaji wake kama ilivyo katika mfano wa 2 na3.


Katika lugha ya Kiingereza kuna vighairi vingi ambavyo hukiuka ruwaza za kifonolojia kwa kama ilivyo katika maneno ya break –ambalo katika wakati uliopita ni broken, au neno go ambalo wakati uliopita ni gone.


Kutokana na ufafanuzi huo ni dhahiri kwamba mabadiliko ya maumbo hayo ya maumbo ya fonimu hutegemea mahali ambapo fonimu hizi hutokea. Hali hii tumeona inajitokeza katika lugha za Kibantu na za magharibi kama Kiingereza kama ilivyooneshwa katika mifano hiyo hapo juu.


5:3 Uteuzi wa Fonimu na Alofoni


Katika 5;1 nimeeleza maana ya fonimu kuwa ni kitamkwa chenye sifa bainifu za kifonetiki, kisaikolojia na za kifonolojia. Nikitumia kigezo cha fonolojia fonimu inaitazamwa kama kitamkwa chenye uamilifu katika lugha maalum. Fonimu mbali na kuwa na sifa za uamilifu za kifonetiki lakini ni lazima itazamwe katika lugha maalum ambamo ndimo hutumika fonimu hiyo. Kutokana na uamilifu huo wa fonimu ndio maana kila lugha huteua fonimu na alofoni mbalimbali kulingana na asili ya lugha husika. Alofoni ni maumbo mbalimbali tofauti tofauti yanayowakilisha fonimu moja katika lugha maalum. Kwa ujumla ninapozungumzia uteuzi wa fonimu na alofoni nina maana ya uchaguzi wa sauti kutoka katika jedwali la Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa (AKK) na katika trapezium ya irabu msingi.


Uteuzi wa fonimu na alofoni katika lugha yoyote ile hufanywa kwa kutumia mbinu maalum za uteuzi wa fonimu na alofoni. Uteuzi wa fonimu na alofoni, kwa upande mwingine unaweza kuitwa ni utambuzi wa fonimu na alofoni zake.


Kuna mbinu au njia mbalimbali zitumikazo katika kutambua fonimu na alofoni. Njia hizi zinajumuisha jozi sahili, ufanano wa kifonetiki, mgawo kamilishi, mpishano huru na usawazisho wa sauti


Jozi sahili (minimal pairs) ni mbinu ambayo kwayo maneno mawili au zaidi yenye idadi sawa ya vitamkwa na vinavyofanana kimatamshi isipokuwa kitamkwa kimoja hutofautiana. Kitamkwa hiki kinachotofautiana hutokea mazingira yale yale katika maneno na ndicho kinacholeta tofauti ya maana za maneno hayo. Wakati wa utamkaji sauti moja tu ndiyo hutofautiana kutoka neno moja hadi lingine, lakini nyingine hutamkwa sawa au zinafanana kimatamshi katika njia hii ya jozi sahihi. Ifuatayo ni mifano inayodhiririsha kazi ya mbinu ya jozi sahili katika taaluma ya fonolojia.


Mifano na:13


i) bapa  na baba


vitamkwa [p, b] ni fonimu mbili tofauti kwa sababu zinaleta maana tofauti za maneno hayo. Neno la bapa lina maana ya sio badilika au isiyo na miinuko wakati neno baba lina maana ya mzazi wa kiume

 




54

 

pana  na pina


vitamkwa [a, i] ni fonimu mbili tofauti kwa sababu zinaleta tofauti ya maana za maneno hayo. Neno pana lina maana ya ukubwa wakati neno


pina lina mana ya sikio au sehemu ya nje ya sikio.



lafiki na rafiki


sauti [r,l] ni alofoni za fonimu [r] kwa sababu hazileti tofauti ya maana za maneno hayo. Maneno yote mawili yana maana ya mtu wa karibu.


Katika mifano hiyo hapo juu kuna alfabeti zilizoandikwa kwa wino mzito zina wakilisha sauti zilizoko kwenye mabano ya mraba kama inavyoonekana katika mifano hapo juu.


Njia hii ni nzuri sana na hutusaidia kupambanua au kutambua fonimu na alofoni katika lugha maalum. Hata hivyo ina mapungufu yake kwa mchagua fonimu kwa sababu inahitaji umilisi wa kiwango cha juu katika lugha inayohusika. Mtu anayechunguza fonimu na alofoni za lugha maalum hiyo anatakiwa kujua maana za maneno yote ili kujua kama ni fonimu au ni alofoni. Kwa uhakika jambo unalotakiwa kuzingatia unapotumia njia ya jozi sahili ni kwamba maneno unayotumia lazima yawe na idadi sawa ya sauti na yatofautiane sauti moja tu lakini katika mazingira yaleyale.


Njia ya pili ni ufanano wa kifonetiki ambayo kwayo tunaangalia sifa bainifu za fonimu ili kugundua kama sauti iliyotumika ni fonimu au alofoni. Kwa kiasi kikubwa tuapoangalia ufanano wa kifonetiki wa sauti hizo tunakuta kwamba njia hii inatupatia/ hutusaidia katika kupambanua fonimu zaidi kuliko alofoni. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na:14

i) [p] – pata [b] – bata

[-kont ] [-kont ]

[+kons ] [+kons ]

[+ant ] [+ant ]

[-ghun ] [+ghun ]

[-sil ] [-sil ]

[+mid ] [+mid ]

[-kor ] [-kor ]

ii) [a] – lake [ε] –cheka

[+sil ] [+sil ]

[+kont ] [+kont ]

[+ghun ] [+ghun ]

[+kor ] [+kor ]

[+chin ] [+kat ]

[+son ] [+son ]

 







55

 

iii)  [l] –mbele [r] –mbere

[+tamb ] [+mad ]

[+ son ] [+son ]

[+ghun ] [+ghun ]

[+kons ] [+kons ]

[+ant ] [+ ant ]

[+kor ] [+kor ]



Katika maumbo yaliyopo katika maneno yameandikwa kwa wino mzito yanawakilisha sauti zilizomo katika mabano yamraba.


Kutokana na sifa hizo hapo juu za vitamkwa [p], [b],[a] na [ɛ] tunagundua kuwa ni fonimu tofauti tofauti mbali na kwamba zina sifa zinazofanana kwa kiasi kikubwa. Katika mfano i) sauti [p] na[b] ni fonimu mbili tofauti hali kadhalika mfano ii) sauti [a] na [ε] ni fonimu mbili tofauti.


Lakini mfano wa tatu ni tofauti na iliyotangulia kwani sauti [l]  na [r] zinachangia


baadhi ya sifa na baadhi hutofautiana kifonetiki lakini ni maumbo mawili yanayowakilisha sauti [l] kwa maana kwamba sauti [l] na [r] ni alofoni za fonimu [l]


Njia ya tatu ni mgawo kamilishi ambayo kwayo sauti zinagawana mazingira ya utokeaji yaani sauti moja inapotokea nyingine haitokei. Mazingira ya utokeaji hudhibitiwa na kanuni za kifonolojia. Hebu chungua mifano hii.


Mifano na: 15


Data ya lugha ya Kinyakyusa


Mofimu za mneno matamshi ya neno maana ya neno

i) u+ku +bhon+a [ukuβɔna ] lina maana ya “anakuona”

ii) u+ku+mbon+a [ikumbɔna] lina maana ya “ananiona”

iii) ngu+jhobh+a [nguϳɔβa ] lina maana ya “ nasema”

v) a+mbi+kil+e [ambikilε ] lina maana ya “ameniwekea”

vi) a+ku+bhi+kil+e [akuβikilε] lina maana ya “ amekuwekea”


Ukichunguza kwa makini data hii kutoka katika lugha ya Kinyakyusa utagundua kuwa sauti [β] inatokea katika mazingira ambayo inakuwa katikati ya sauti irabu, wakati sauti


hutokea pale inapotanguliwa na sauti aina ya nazali. Sauti au vitamkwa hivi vinategemea mazingira ya utokeaji wake. Katika mazingira ya irabu sauti [β] hutokea na katika mazingira ya nazali sauti [b] hutokea. Kutokana na mazingira hayo ya utokeaji tunagundua kuwa sauti [β] na [b] ni za alofoni za fonimu [β].


Katika lugha ya Kinyakyusa pia kuna sauti nyingine zinazogawana mazingira kutokana na kanuni za kifonolojia zinazodhibiti utokeaji wake. Hebu chunguza data ifuatayo kwa makini hapa chini.

 










56

 

Mifano na: 16

Mofimu za neno matamshi ya neno maana ya neno

i) u+ ku+ndul+a [ukundula ] lina maana ya “ ananisaidia”

ii) u+ku+tul+a [ukutula ] lina maana ya “anakusaidia”

iii) a+ndi+ghil+e [andiɤilε ] lina maana ya “amenikosea”

iv) a+ku+li+ghil+e [akuliɤilε ] lina maana ya “ amekukosea”


Katika data hiyo hapo juu inaonesha wazi kuwa katika lugha ya Kinyakusa sauti zina tabia ya kugawana mazingira ya utokeaji wake. Ukichunguza kwa makini sana utagundua kuwa sauti [d] inatokea katika mazingira ambayo inatanguliwa na sauti aina ya nazali, sauti [t] inatokea katika mazingira ambayo inakuwa katikati ya irabu [u] na sauti [l] hutokea katika mazingira ambayo inakuwa katikati ya irabu [u] na [i]. Kutokana na data hiyo tunagungua kuwa sauti [d] ,[t] na [l] ni alofoni za fonimu [t].


Tabia hii ya sauti kugawana mazingira inajitokeza pia katika lugha ya Kiswahili ambapo ruwaza za kifonolojia zinadhibiti utokeaji wake. Jambo hili linathibitika katika kauli ya utendea ambapo sauti zinaonesha dhana ya utendea huchukua sura mbalimbali za maumbo ya sauti kama inavyoonesha hapa chini.


Mifano na: 17

Data ya lugha ya Kiswahili

Mofimu za neno Matamshi ya neno

i) a+li+ni+pik+i+a [alinipikia ]

ii)  a+me+m+pak+i+a [amεmpakia]

iii) tu+li+m+tek+e+a [tulimtεkεa ]

iv) ni+ta+mw+on+e+a [nitamwɔnεa]

v) a+ta+ni+chum+i+a [ataničumia ]


Katika mifano hiyo hapo juu utagungua kuwa sauti [i] ambayo mi mofimu ya utendea hutokea iwapo mzizi una irabu msingi ya a, u na i, halafu unaishia na konsonanti kama ilivyo katika mfano wa i), ii) na v). Lakini sauti [ε] hutokea katika neno ambalo mzizi wake una irabu e na o, halafu unaishia na sauti konsaonanti kama ilivyo katika mfano wa iii) na iv).


Mchakato huu unatupatia alofoni [i] na alofoni [ε] ambazo hutokea mazingira yale yale lakini zikiwakilisha fonimu moja kwani maana au dhana ni moja ambayo ni ya utendea.


Vile vile katika lugha ya Kiingereza kuna alofoni mbalimbali kwa kuzingatia maumbo mbalimbali ya maneno. Kwa kutumia dhana au taaluma ya mofofonolojia tunapata alofoni mbalimbali. Mfano katika maneno yafuatayo sauti zitakazotokea ni alofoni ambazo zimegawana mazingira ya utokeaji. Hebu chungua mifano hii.

 











57

 

Mifano na:18


Data ya lugha ya Kiingereza


Mofimu za neno matamshi ya neno maana ya neno

i)  boy +s [bɔɪz ] wavulana

ii) bush+es [bʊʃɪz ] brashi

iii)book+s [bʊks ] vitabu

iv)table+ s [teɪbz ] meza

v) baby+es (babies) [beɪbɪz ] watoto

vi) cat +s [kæts ] paka


Katika mifano hiyo hapo juu ina onesha fonimu [s] ina maumbo ya aina tatu. Iwapo mzizi wa neno unaishia na sauti irabu katika utamkaji wake mzizi au neno linaloishia na kiyeyusho kitahajia unapokea alofoni [z] pamoja na mizizi inayoishia na konsonanti ghuna kama ilivyo katika mfano i). Mzizi au neno linaloishia na sauti konsonanti ambayo ni kizuio kwamizi, zinazotamkiwa eneo la ufizi kaakaa gumu na mzizi au neno hilo hupokea alofoni [ɪz] kama ilivyo katika mfano ii) na v) wakati mizizi inayoishia na konsonanti si ghuna na baadhi ya ghuna hupokea alofoni [s] kama ilivyo katika mfano wa


na iv). Kwa asilimia kubwa alofoni [s] hutokea baada ya sauti konsonanti vipasuo.


Hivyo basi kutokana na mchanganuo huo ni dhahiri kwamba sauti [z], [ɪz] na [s] ni alofoni za fonimu [s] kwa sababu hazileti tofauti ya maana bali zote huleta maana moja ya uwingi katika taaluma ya mofolojia.


Njia hii ni nzuri sana lakini kuna sauti nyingine zinagawana mazingira na si alofoni bali ni fonimu mbili tofauti. Hali hii inapotokea sauti hizo huitwa vighairi au hali ya ughairi kwa sababu ni sauti zinazokinzana na ruwaza za kifonolojia. Mfano katika lugha ya Kiingereza sauti [ŋ] haitokei mwanzoni mwa neno na sauti [h] haitokei mwishoni mwa neno. Hizi sauti zimegawana mazingira ya utokeaji lakini ni fonimu. Hebu chungua mifano ifuatayo:


Mifano na: 19


Data ya lugha ya Kiingereza


Mofimu za neno matamshi ya neno maana ya neno

i) sing [sɪŋ ] imba

ii) heart [hɑ:t] moyo


Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha kwana sauti [ŋ] na [h] ni fonimu mbili tofauti kwa sababu zina maana tofauti kabisa, kila moja inasimama peke yake mbali na kwamba zimegawana mazingira.


Njia ya nne ni ya mpishano huru ambayo kwayo sauti hubadilishana nafasi lakini maana ya neno hubaki vile ilivyo. Sauti zinapobadilishana nafasi bila athari yoyote kimaana hupelekea kuwepo kwa alofoni. Hebu chungua mifano ifuatayo ya lugha ya Kiswahili.

 





58

 

Mifano na: 20


Lugha ya Kiswahili


Maneno kiotografia matamshi yake

i) wosia  na wasia [wɔsia] na [wasia]


Sauti [ɔ] na [a] katika maneno hayo juu ni alofoni kwa sababu hazibadili maana za maneno hayo.


ii) shehe na shekhe [šεhε] na [šεkhε]


Sauti [h] na [kh] katika maneno hayo hapo juu ni alofoni kwa sababu zinaleta maana moja ya fonimu [h]


iii) kandamiza na gandamiza [kandamiza] na [gandamiza]

Sauti [k] na[g] ni alofoni mbili za fonimu [k] kwa


sababu hazileti tofauti ya maana za maneno hayo.


iv) heri na kheri [hεri] na [hεri]

Sauti  [h]  na  [kh]  ni  alofoni  za  fonimu  [h]  kwa


sababu

hazileti tofauti ya maana za maneno hayo.


Katika mifano hiyo hapo juu kuna maumbo yameandikwa kwa wino mzito, maumbo hayo yanawakilisha sauti ambazo zimeziita ni alofoni.

 


Mifano na: 21


Lugha ya Kichaga Maneno kiotografia

shadu na shanu


ido  na iro

iii)deda na rera

 







matamshi ya neno maana ya neno

[šadu ] na [šanu] yenye maana ya “viatu”

[idɔ  ] na [irɔ  ] yenye maana ya “kupanda mlima”

[dεda] na [rεra ] yenye maana ya “kuongea”

 


Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha kwamba mpishano huru wa sauti hizo hauleti tofauti ya maana za maneno. Kwa ujumla naweza kusema njia hii ya mpishano huru hutupatia mawanda mapana ya kuelewa fonimu na uamilifu wake. Vitamkwa vilivoandikwa kwa wino mzito katika mifano ya lugha ya Kichaga ni alofoni zenye kuwakilisha fonimu. Mfano namba i) sauti [d, n] ni alofoni zinazowakilisha fonimu [n], mfano wa ii) na iii) sauti [d, r] ni alofoni zinazowakilisha fonimu [r].


Katika mpishano huru sauti zina sifa bainifu za kifonolojia tofauti kabisa na zile sifa bainifu za kifonetiki ni tofauti pia. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba njia hii ni muhimu sana katika kuzielewa fonimu na alofoni. Mbali na kuwa njia au mbinu hii kuwa ni ya muhimu bado kuna utata unaojitokeza katika njia hii kwa sababu mtu asiye na umilisi wa lugha hawezi kutumia njia hii katika kubainisha au kupambanua fonimu na alofoni.

 





59

 


Njia ya tano na ya mwisho ni ya usawazisho wa ambayo kwayo tunaangalia umbo la ndani na umbo la nje la neno. Ni njia inayohusu namna umbo la nje linavyoweza kusaidia kutokana na usawazisho huo tupata alofoni na fonimu. Hebu chungua mifano ifuatayo:


Mifano na: 22

Umbo la ndani neno umbo la nje la neno

i)  ki+atu chakula [čakula]

ii) ki+atu kiatu [kiatu  ]

iii)ki+imba chimba [čimba ]

iv)ki+ imba kimba [kimba ]


Katika mifano hiyo i) hadi iv) sauti [č] na [k] ni fonimu mbili tofauti kwa sababu zinaleta tofauti ya maana. Wakati huo huo maneno hayo yamekula njama kwa sababu yana maumbo ya ndani sawa lakini umbo la nje ni tofauti. Hebu chungua mifano mingine zaidi hapa chini.

 


Mifano na:23


Umbo la ndani la neno


mu+alimu

ma+ino


ki+etu

 





umbo la nje la neno


mwalimu  [mwalimu]

meno [mεnɔ ]


chetu [čεtu ]

 


Katika mifano hiyo hapo juu ukichunguza kwa makini utagundua kuwa katika i) moja kumetokea fonimu [w] kutokana na usawazisho kupitia kanuni ya uyeyushaji. Katika mfano ii) tumepata fonimu [ε] kutokana na usawazisho kupitia kanuni ya uvutano wa irabu, yaani irabu i na a zimevutana na kutengeneza au kuunda sauti [ε] na katika mfano


usawazisho umetupatia fonimu [č] kupitia kanuni ya ukakaishaji, kwamba mofimu ki inapofuatina na irabu hubadilika na kuwa sauti [č] yenye tahajia ch. Mchakato wa umbo la ndani na la nje hutupatia fonimu ndani ya njia iitwayo usawazisho.


Kwa ujumla fonimu zinaweza kupambanuliwa kupitia njia hizi kuu za jozi sahili, mgawo kamilishi au mtoano kamilishi, mpishano huru, ufanano wa Kifonetiki wa sifa za fonimu hizo na usawazisho. Kupitia njia hizi hizi alofoni pia huweza kubainishwa. Hata hivyo ni dhahiri kabisa kwamba mtu mwanaisimu au mtumia lugha ni lazima awe na umilisi wa lugha husika maalum anayoitumia au anayoishughulikia hususani katika taaluma ya fonolojia, fonetiki, semantiki pamoja na mofolojia.


Hata hivyo kwa wanazuoni wengi hutumia njia hizi katika kubainisha idadi ya fonimu pamoja na alofoni za fonimu katika lugha maalum. Njia ni hizi nzuri sana unachotakiwa kukizingatia ni kuwa na umilisi wa lugha fulani maalum unayoishughulikia.

 












60

 

5: 4 Dhima ya Fonimu katika Lugha


Fonimu katika lugha maalum zina dhima kubwa ambazo kwazo lugha maalum huonekana kuwa lugha kamili. Lugha kamili ina maana ya kuwa na mfumo kamili wa mpangilio wa vipashio vyenye kuleta maana katika lugha maalum inayohusika. Dhima ya kwanza ya fonimu katika lugha ni kuunda au kujenga vipashio vikubwa vya lugha. Kwamba fonimu inapoandamana na fonimu nyingine huunda silabi mofimu na maneno, vipashio hivi pia huunda tungo mbalimbali. Mfano fonimu /p/ /a/, /k/ huweza kuunda silabi $pa$ na $ka$, silabi hizi pia huunda maneno paka na kapa.


Dhima nyingine ya fonimu ni kutofautisha maana za maneno. Fonimu inaweza kutofautisha maana za maneno kupitia njia ya jozi sahili ambayo kwayo maneno mawili au zaidi huwa na idadi sawa ya fonimu isipokuwa fonimu moja hutofautiana katika mazingira yale yale. Mfano neno duka na daka yanatofautishwa maana zake kwa fonimu /u/ na /a/.


Fonimu kwa kubadilishana nafasi huweza kuunda maneno mapya katika lugha maalum inayoshughulikiwa. Kimsingi ni kwamba kunakuwa na maneno lakini fonimu zake zinapobadilishana nafasi huweza kuunda maneno mapya kabisa. Mfano ota tunapata neno toa, fonimu /t/ na /ɔ/ zimebadilishana nafasi na kuunda neno jipya la toa lenye maana tofauti na neno la awali.


Kwa ujumla katika sura hii nimeshughulikia fonimu katika mawanda mapana bila kujikita katika lugha maalum. Mbali na hilo nimeeleza sifa zake mbalimbali na dhima zake katika lugha. Si hivyo tu njia maalum zinazotusaidia katika kubainisha au kupambanua fonimu na alofoni katika lugha maalum. Jumla ya yote kinachohitajika ni umilisi wa lugha katika kupambanua fonimu na alofoni zake katika lugha maalum.






Zoezi

1.Fonimu za lugha zinaweza kuchanganuliwa au kupambanuliwa kwa vigezo vifuatavyo:


kigezo cha kifonetiki b)kigezo cha kifonolojia

kigezo cha kisaikolojia

fafanua vigezo au mitazamo hiyo


eleza ubora na udhaifu wa vigezo hivyo.


2.Je kuna umuhimu wowote wa kujifunza fonimu za lugha? Kubali au kataa kwa hoja madhubuti.


3.Fonimu yoyote ile katika lugha maalum ina mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi.


eleza  mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi ya fonimu zifuatazo:

a) /υ/ f) /ñ/


b) /ɱ/ g) /ɤ/

c) /r/ h)/ε/


d) /š/ i) /b/

e) /č/

 




61

 

4.Jadili mambo ya msingi yanayozingatiwa wakati wa upambanuzi wa

konsonanti


irabu

viyeyusho


5.Kwa kutumia mifano dhahiri kutoka katika lugha mbalimbali fafanua mbinu zitumikazo kubainisha fonimu na alofoni katika lugha.

 


























































62

 

SURA YA SITA



6:0 VITAMKWA VYA KAWAIDA VYA KISWAHILI SANIFU


Katika sura ya nne nimezungumzia kwa ujumla vitamkwa vya kifonetiki na vya kifonolojia vya lugha bila kujikita katika lugha maalum. Vile vile katika sura hiyo hiyo nimezungumzia aina ya vitamkwa vya kifonolojia vya kawaida na viarudhi kwa ufupi. Katika sura ya tano nimezungumzia vitamkwa vya kawaida bila kujikita katika lugha maalum, nikieleza dhana ya fonimu, aina za fonimu,yaani konsonanti, irabu, na viyeyusho. Vile vile nikaeleza jinsi ya matamshi na mahali pa matamshi kama sifa kuu za fonimu au vitamkwa hivyo. Si hivyo tu lakini pia nimeeleza sifa kuu za fonimu kwa ujumla na dhana ya alofoni na jinsi ya kutambua fonimu na alofoni kwa kutumia njia za jozi sahili, mpishano huru, ufanano wa kifonetiki, mgawo kamilishi na usawazisho. Katika sura hii nitaeleza vitamkwa vya kawaida vya kifonolojia kwa kujikita katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Sura hii itahusu vitamkwa vya kawaida vya lugha ya Kiswahili Sanifu.



6:1 Aina za Vitamkwa vya Kawaida vya Kawaida Sanifu


Kama nilivyoeleza katika sura ya tano kwamba sauti zinazohusika katika bohari la sauti ni za lugha nyingi ulimwenguni ambazo ni za aina ya konsonanti, irabu na viyeyusho au nusu irabu. Katika lugha ya Kiswahili Sanifu hali ni hiyo hiyo. Kiswahili Sanifu kina aina kuu tatu za vitamkwa au fonimu ambazo ni konsonanti, irabu, na viyeyusho. Ninaposema Kiswahili Sanifu ni lugha ambayo ina ulinganifu mkubwa katika eneo la matamshi, maumbo ya maneno, miundo ya tungo na maana za maneno hayo, wakati huo huo huweza kuwa katika maandishi na matumizi yake ni sahihi. Lugha hii hutumika katika utawala, katika masuala ya elimu hususani katika elimu ya msingi ni lugha ya kufundishia pamoja na vyuo vya ualimu wa tarajali, ni somo katika shule za sekondari na vyuo ya vikuu. Hutumika bungeni kama lugha ya kuendeshea shughuli za kibunge hususani katika vikao vya wabunge na midahalo mbalimbali inayohusu bunge. Si hivyo tu lugha hii husomwa kama somo katika ngazi ya shahada ya kwanza, shahada pili ya uzamili na na ya tatu ya uzamivu. Lugha ya Kiswahili Sanifu pia ni lugha ya taifa la Tanzania na ni lugha ya Kimataifa ambayo inaongoza katika bara la Afrika na inafundishwa katika vyuo mbalimbali ulimwenguni kote.


Kiswahili Sanifu kinatumika katika vyombo vya habari kama redio, luninga na magazeti na katika shughuli za kidini. Vile vile ni lugha inayokubali mabadilko kulingana na mabadiliko ya kisayansi na teknolojia. Kutokana na umuhimu wake kwa watumia lugha, walio wazawa na wageni Kiswahili Sanifu kina sauti zake za msingi au vitamkwa maalum, vinavyotumika katika mfumo wake utumikao katika mawasiliano yake ya kila siku. Wanajamii hawa huzitumia sauti hizo katika kuwasiliana na katika shughuli mbalimbali kama za kiufundi yaani sayansi na teknolojia, taaluma mbalimbali kama somo la Kiswahili, fizikia, jiografia na kadhalika. Vitamkwa hivyo au fonimu hizo ni konsonanti, irabu na viyeyusho kama nilivyotangulia kusema hapo awali. Fonimu hizo ndizo msingi wa lugha ya Kiswahili Sanifu katika kuleta mawasiliano baina ya watumia

 




63

 


lugha ya Kiswahili Sanifu. Katika sura hii nitaelezea sauti au fonimu hizi kwa kuzingatia mfumo wa sauti wa lugha ya Kiswahili.



6:1:1 Konsonanti za Kiswahili Sanifu


Lugha ya Kiswahili Sanifu ina jumla ya konsonanti ishirini na tisa (29) zinazotumika katika mfumo wa lugha wa matamshi na maandishi. Konsonanti hizi za Kiswahili Sanifu zaweza kuoneshwa katika kielelezo. Kielelezo namba 8 kinaonesha orodha ya Konsonanti za Kiswahili Sanifu


Kielelezo na:8. Konsonanti za Kiswahili Sanifu.


Herufi za kawaida Herufi za kifonetiki Herufi za kawaida Herufi za kifonetiki

b [b] n [n]

ch [č] ny [ñ]

ch [čh] ng’ [ŋ]

d [d] p [p]

dh [ð] ph [ph]

f [f] r [r]

g [g] s [s]

gh [ɤ] sh [š]

h [h] t [t]

j [ɟ] th [th]

k [k] th [θ]

kh [kh] v [v]

l [l] vy [υ]

m [m] z [z]

m [ɱ]





6:1:1:1 Sifa za Konsonanti za Kiswahili Sanifu


Konsonanti za lugha yoyote zina sifa kuu zake. Sifa hii zimejikita katika misingi mikuu miwili ambayo ni msingi au kigezo cha mahali pa matamshi na msingi wa jinsi ya matamshi kama ilivyoelezwa katika sura ya tano (taz.5:1:3:1:1:1 na 5:1:3:1:1:2). Konsonanti za Kiswahili Sanifu pamoja na viyeyusho vyake vinaainishwa katika makundi saba ambayo ni vipasuo, vizuio kwamizi, vikwamizi, nazali, vitambaza, vimadende na viyeyusho au nusu irabu. Konsonati za Kiswahili Sanifu si kwamba zina sifa kuu za mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi tu, la hasha zipo nyingi sana kama mtimbwiliko wa nyuzisauti, hali ya midomo, mwinuko wa ulimi, sehemu ya ulimi na mpuo wakati wa utamkajii wake. Lakini katika kueleza kwangu nitaanza kwa kueleza sifa za mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi. Upande wa mahali pa matamshi konsonanti za Kiswahili Sanifu ziko katika makundi nane ambayo ni midomo, midomo –meno, meno, ufizi,baada ya ufizi, kaakaa gumu, kaakaa laini na koromeo.

 



64

 



6:1:1:1:1 Sifa za Mahali pa Matamshi za Konsonanti za Kiswahili Sanifu


Ninaposema sifa za mahali pa matamshi nina maana ya sehemu mbalimbali za chemba za kinywa na pua zinazohusika wakati wa utamkaji wa sauti hizo kama ilivyoelezwa katika sura ya tano (taz.5:1:3:1:1:1). Konsonanti za Kiswahili Sanifu zina sifa nane za mahali pa matamshi ambazo ni midomo, midomo –meno,meno ,ufizi ,baada ya ufizi, kaakaa gumu, kaakaa laini na koromeo. Sifa hizi nitazieleza kama ifuatavyo:


Sifa ya kwanza ni ya midomo ambayo inahusu utamkaji wa vitamkwa ambavyo hutamkwa wakati mkondohewa unapozuiliwa kwa kubana mdomo wa chini na mdomo wa juu huku ikiviringwa (ambayo yote ni alasogezi). Baada ya mkondohewa kubana, huweza kuachiwa au ukabanwa kwa kuviringa midomo huku imeacha upenyo mdogo ambao huwezesha kutolewa kwa sauti kadhaa. Sifa hii inahusisha sauti zifuatazo:

 


Maandishi ya kawaida


a)  b

b) p


c) ph


d) m


e) w

 


maandishi ya kifonetiki


[b]

[p]


[ph]


[m]


[w]  kiyeyusho

 



Sifa ya pili ni ya midomo –meno inayohusu utamkaji wa konsonanti ambazo alasogezi mdomo chini na alatuli meno juu hugusana, wakati huo huo hewa huruhusiwa kupita kwa kukwamizwakwamizwa katikati ya meno juu na mdomo chini. Sifa hii inahusu konsonanti kadhaa za Kiswahili Sanifu. Sauti hizo ni:

 


Maandishi ya kawaida

a) f


b) v

c) m


d) vy

 


maandishi ya kifonetiki

[f]


[v]

[ɱ]


[υ]

 



Sifa ya tatu ni ya meno ambayo inahusu utamkaji wa konsonanti ambazo kwayo ulimi ambao ni alasogezi hugusana na ufizi na meno, hii ina maana ya kwamba ncha ya ulimi hugusa ufizi na kuseleleka kwa haraka sana kufikia kwenye meno( katikati ya meno juu na meno chini) ambapo sauti hizo hutamkiwa. Sifa hii inahusisha sauti zifuatazo:

 


Maandishi ya kawaida

a) th


b) dh

 


maandishi ya kifonetiki

[θ]


[ð]

 








65

 


Sifa ya nne ni ya ufizi ambayo inahusu utamkaji wa konsonanti ambao kwayo ulimi ambayo ni alasogezi hugusana na ufizi (alatuli). Kupitia mgusano wa ncha ya ulimi na ufizi sauti mbalimbali za Kiswahili Sanifu hutolewa au hutamkwa. Sauti hizo ni:


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) t [t]

b) th [th]

c) d [d]

d) s [s]

e) z [z]

f) n [n]

g) l [l]


Sifa ya tano ni ya baada ya ufizi ambayo inahusu utamkaji wa sauti konsonanti moja ya Kiswahili Sanifu ambayo kwayo ulimi (ncha ya ulimi ambayo ni alasogezi) hugongagonga harakaharaka sehemu iliyo baada ya ufizi yaani baada ya mistari ya ufizi ambayo ni alatuli. Kutokana na hali hiyo ya kugongagonga sehemu ya baada ya ufizi hutupatia sauti ya konsonanti hii.


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki


a) r [r]


Sifa ya sita ni kaakaa gumu ambayo inahusu utamkaji wa baadhi ya sauti konsonanti za Kiswahili Sanifu. Katika mchakato wa utamkaji huo alasauti ulimi ambayo ni alasogezi hugusana na kaakaa gumu ambalo ni alatuli na kusababisha kutolewa kwa sauti zifuatazo:


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) ch [č]

b) ch [čh]

c) j [ɟ]

d) ny [ñ]

e) sh [š]


f) y [y]  kiyeyusho


Sifa ya saba ni ya kaakaa laini ambayo inahusu utamkaji wa konsonanti ambazo huandamana na sehemu ya nyuma ya ulimi (shina la ulimi au ulimi nyuma) ambapo shina la ulimi hugusana na kaakaa laini ambazo zote ni alasogezi. Mgusano husababisha konsonanti kadhaa za Kiswahili Sanifu. Sauti hizo ni:


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) k [k]

b) kh [kh]

c) g [g]

c) gh [ɤ]


d) ng’ [ŋ]

 




66

 



Sifa ya nane ni ya koromeo ambayo inahusu utamkaji wa konsonanti ya lugha ya Kiswahili Sanifu ambayo utamkaji wake unahusisha sehemu ya koromeo. Sauti hii hutamkiwa eneo la koromeo. Sifa hii inahusu sauti ifuatayo:

 


Maandishi ya kawaida

a) h

 


maandishi ya kifonetiki

[h]

 





6:1:1:1:2 Sifa za Jinsi ya Matamshi za Konsonanti za Kiswahili Sanifu


Konsonanti za lugha ya Kiswahili Sanifu zina sifa za jinsi ya matamshi kwa maana ya jinsi konsonanti hizo zinavyotamkwa. Katika msingi wa jinsi ya matamshi kinachoangaliwa hapa ni jinsi mkondohewa unavyoachiwa wakati wa utamkaji ambapo mkondohewa huweza kubanwa kabisa mahali pa kutamkia sauti na kuachiwa kwa ghafula. Mkondohewa unaweza kuzuiliwa kiasi mahali pa kutamkia sauti na kuachiwa taratibu kwa kukwamizwakwamizwa kupitia nafasi finyu, mkondohewa huweza kubanwa na hewa kupita pembeni mwa ulimi. Vile vile mkondohewa huweza kuzuiliwa kwa kuwepo msogeano wa kubana na ncha ya ulimi kugongagonga sehemu iliyo baada ya ufizi au msogeano wa kubana na hewa kupita katika chemba ya pua. Hapa chini nitaziainisha sifa hizo za jinsi ya matamshi za konsonanti za Kiswahili Sanifu. Kutokana na sifa hizo tunapata makundi yafuatayo:


Kundi la kwanza ni la vipasuo lenye sifa pambanuzi zinazolipambanua kundi hili. Konsonanti za kundi hili zinatamkwa pale ambapo mkondohewa unakuwa umebanwa kabisa mahali pa kutamkia au mahali pa matamshi na kisha huachiwa ghafula wakati wa kutamka sauti hizo. Kundi hili linajumuisha sauti zifuatazo:


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) p [p]

b) ph [ph]

c) b [b]

d) t [t]

e) th [th]

f) d [d]

g) k [k]

h) kh [kh]

i) g [g]



Kundi la pili ni vizuio –kwamizi, kundi hili linahusu konsonanti zinazoruhusu mkondohewa kuzuiliwa na kuachiwa taratibu kwa kukwamizwakwamizwa. Vizuio – kwamizi vinapotamkwa mkondohewa huzuiliwa na taratibu huachiliwa kutoka nje ya kinywa kwa kukwamizwakwamizwa. Kundi hili linahusisha konsonanti za Kiswahili Sanifu zifuatazo:




67

 

Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) ch [č]

b) ch [čh]

c) j [ɟ]



Kundi la tatu ni vikwamizi, hili linahusu konsonanti ambazo utamkaji wake hutofautiana na ule wa vizuio –kwamizi. Mkondohewa huzuiliwa kwa kubana kiasi fulani huku msogeano wa alasogezi na alatuli ukiwa ni mwembamba ( huacha nafasi finyu / nyembamba) na hewa hupita katika nafasi hiyo taratibu mpaka hewa yote iishe kutoka mapafuni. Hizi ni sauti ambazo wakati wa utamkaji wake hewa huzuiliwa kiasi fulani, mzuio huo unaipa hewa mwanya wa kupenyeza katika nafasi nyembamba iliyoko katikati ya alasauti hizo. Kutokana na mchakato huo sauti huweza kutamkwa kwa kukwamizwakwamizwa. Kundi hili linajumuisha sauti zifuatayo:


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) f [f]


b) v [v]

c) vy [υ]


d) th [θ]

e) dh [ð]


f) s [s]

g) z [z]


h) sh [š]


Kundi la nne ni nazali ambalo linahusu konsonanti ambazo zinaruhusu hewa kupita katika chemba ya pua wakati wa utamkaji wake. Sauti hizi hutamkwa pale ambapo hewa kutoka mapafuni husafiri na inapofikia eneo la koromeo kidaka tonge na shina la ulimi hugusana na kufunga njia ya chemba ya kinywa, hivyo hewa hulazimika kupita katika chemba ya pua ili itoke nje. Kundi hili linahusisha sauti hizi:


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) m [m]


b) m [ɱ]

c) n [n]


d) ny [ñ]

e) ng’ [ŋ]


Kundi la tano ni vitambaza ambalo linahusu konsonanti ambazo hutamkwa kwa kuutandaza ulimi ambao ni alasogezi huku ncha ya ulimi ikigusana na ufizi ambao ni alatuli na kuruhusu hewa kupita pembeni mwa ulimi ambamo mna nafasi wazi. Kundi hili linahusu sauti moja ya Kiswahili Sanifu ambayo ni.


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki

a) l [l]

 





68

 


Kundi la sita ni vimadende ambalo linahusu sauti au konsonanti ambazo hutamkwa kwa ncha ya ulimi kupigapiga ulimi mara kadhaa, harakaharaka kwenye eneo lililo baada ya ufizi (baada ya mistari ya ufizi) huku hewa ikitoka nje kupitia chemba ya kinywa. Kundi hili linahusu sauti moja ya lugha ya Kiswahili. Sauti hiyo ni.


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifonetiki


a) r [r]



Katika kuainisha sauti konsonanti tunaangalia vitu vingi kwa sababu sauti hizi zina sifa nyingi mbali na hizo zilizoelezwa hapo juu. Sifa nyingine za konsonanti ni ughuna na usoghuna kwa kushughulikia hali ya nyuzisauti katika kisanduku cha nyuzisauti pamoja na mpumuo.



6:1:1:1:3 Sifa za Konsonanti za Mtimbwiliko wa Nyuzisauti za Kiswahili Sanifu.


Konsonanti za Kiswahili Sanifu mbali na kuwa na sifa za mahali pa matamshi na za jinsi ya matamshi zina sifa nyingine ambazo huzitofautisha sauti hizo. Kwamba kuna konsonanti zenye sifa za ughuna na zisizo na sifa za ughuna.


Sifa ya ughuna inahusu sauti au konsonanti ambazo hutamkwa wakati nyuzisauti zikiwa zimekaribiana au zimegusana na hivyo kuifanya hewa itokayo mapafuni kuzisukuma ili ipate kupita. Katika harakati za hewa kuzisukuma nyuzisauti hizo inapotafuta nafasi ya kupita husababisha nyuzisauti kutimbwilika au kutetemeka, mtimbwiliko huo huifanya sauti inayotamkwa kuwa na msikiko wenye mghuno. Sifa hii inajumuisha sauti konsonanti zifuatazo; [b], [ð], [d], [g], [ɤ], [m],[n], [ñ], [ŋ],[υ],[ ɟ], [v],[l], [z] na [r].


Sifa ya visoghuna au isoghuna inahusu konsonanti ambazo hutamkwa wakati nyuzisauti zikiwa zimeachana au ziko katika hali yake ya kawaida, na hivyo hufanya hewa ipite katikati ya nyuzisauti hizo bila kizuizi chochote na kusababisha kutokuwepo kwa hali ya kutimbwilika. Sifa hii inajumuisha konsonanti hizi; [p], [t], [k], [f], [θ], [s], [č], [š] na [h].



6:1:1:1:4 Sifa za Konsonanti za Mpumuo za Kiswahili Sanifu.


Dhana ya mpumuo kwa mujibu wa Kamusi Sanifu ya Isimu ya Lugha (KSIL) (1990:7) kama ilivyonukuliwa na Massamba na Wenzake katika kitabu chao cha Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA) 2004:42, katika sura ya tatu (3:1:2:1) inafasiri hivi:


“ Mpumuo ni pumzi kali inayojitokeza wakati wa utamkaji wa baadhi ya vitamkwa vinapotamkwa.”


Katika Kiswahili Sanifu kuna baadhi ya sauti ambazo zina mpumuo wakati wa utamkaji wake hususani kwa wazungumza Kiswahili wakaao Pwani ya Afrika Mashariki kwa

 




69

 


maana ya wazaliwa wa pwani ya Afrika Mashariki. Ukweli ni kwamba wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili waliozaliwa bara wanashindwa kutofautisha vitamkwa vyenye mpumuo na visivyo na mpumuo.


Katika matumizi ya kila siku ya Kiswahili Sanifu sauti hizi zenye mpumuo hutumiwa na wazawa wa Pwani ya Afrika Mashariki. Hapo awali ilionekana vitamkwa hivi kutohusishwa ama kutoonekana katika idadi ya vitamkwa vya lugha ya Kiswahili Sanifu. Lakini ni muhimu sana kuvitambua kama fonimu za lugha ya Kiswahili Sanifu kwa sababu zinatumika katika mawasiliano ya kila siku. Kwa sababu hiyo nimeona ni muhimu kabisa kuitambua sifa hii katika konsonanti za lugha ya Kiswahili Sanifu. Si hivyo tu vile vile kutambulika kwa vitamkwa hivi kama ni moja ya vitamkwa vya lugha ya Kiswahili Sanifu. Mpumuo hujitokeza katika utamkaji wa vitamkwa p,t,k,na c.

Hebu chunguza kielelezo kifuatavyo:


Kielelezo na: 9. Vitamkwa vyenye Mpumuo na visivyo na Mpumuo


Maandishi ya Maandishi ya Mifano ya maumbo Maana itokanayo na

kawaida kifonetiki bainifu mifano .

t [p] paa Sehemu ya juu

inayofunika

nyumba.

ph [ph] phaa Mnyama afananaye

na Swala.

t [t] taa Kifaa kitoacho

mwanga

th [th] thaa Aina ya samaki wa

baharini.

k [k] kaa Kipande cha mti

mkavu chenye moto

kh [kh] khaa Mnyama mdogo wa

baharini au mtoni.

ch [č] čungu Chombo cha

udongo cha kupikia

ch [čh] čhungu Mdudu mdogo jamii

ya sisimizi.





Konsonanti za Kiswahili Sanifu zinaweza kuoneshwa katika jedwali. Katika jedwali la konsonanti sifa zote huoneshwa yaani sifa za mahali pa matamshi,jinsi ya matamshi mpumuo na hali ya nyuzisauti (ghuna na visoghuna). Vile vile ndani ya jedwali hilo kuna viyeyusho viwili.


Katika orodha ya vitamkwa nimeongeza vitamkwa viwili vyenye maumbo haya ya kimatamshi [ɱ] na [υ]. Vitamkwa hivi vimekuwa vikitumika katika Kiswahili Sanifu bila kutambuliwa lakini ni fonimu za lugha ya Kiswahili Sanifu. Katika upekee wake na umuhimu wake katika lugha nimeona ni vizuri sasa kuitambua nafasi ya vitamkwa hivi katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Kama kitamkwa [n] kimetofautishwa na kitamkwa [ñ]

 




70

 


chenye tahajia ya ny ipo haja ya kuvitazama kwa upya vitamkwa vya lugha ya Kiswahili. Kitamkwa [ɱ] ni kitamkwa ambacho kina sifa zake bainifu ambacho kina kaida ya kufuatiwa na konsonanti [v]. Lakini pia ni lazima tukubali kwamba yawezekana kitamkwa hiki kimekuwa kikibebwa na kitamkwa [m] jambo ambalo linakidhoofisha kitamkwa hiki. Imefika wakati wa kukitazama kitamkwa hiki kama fonimu ya Kiswahili Sanifu. Kitamkwa hiki kina sifa ya matamshi ambayo ni tofauti kabisa na ya kitamkwa


ambazo zinakibainisha kitamkwa hicho. Kitamkwa hiki kinajitokeza kama ifuatavyo katika Kiswahili Sanifu.


Maandishi ya kawaida matamshi yake

a) mvamizi [ɱvamizi ]

b) mvinza [ɱvinza ]

c) mvomero [ɱvɔmεrɔ ]

d) mvumbuzi [ɱvumbuzi]



Upande wa kitamkwa [υ] nacho kina tabia kama ya kitamkwa [ñ] kwa mantiki ya kimfuatano vina konsonanti na kiyeyusho zinazounda sauti hizo. Si hivyo tu sauti hii ina sifa za mahali pa matamshi zinazokibainisha kama fonimu za lugha maalum kutokana na matumizi yake katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Lakini pia hutumika katika mawasiliano ya watumia lugha ya Kiswahili Sanifu ya kila siku, mfano katika maneno:


Maandishi ya kawaida matamshi yake

a) vyama [υama ]

b) vyenu [υεnu ]

c) vyote [υɔtε ]

d)vyumba [υumba]


Katika jedwali hilo mgawo wa vitamkwa au fonimu uko kama ifuatavyo; upande wa jinsi ya matamshi kuna makundi ya konsonanti sita (6) na la viyeyusho moja (1). Kundi la kwanza hadi la tatu kuna sauti ghuna 9 na visoghuna 9 na sauti mpumuo 4, kundi la nne hadi la sita yana nazali 5 , kitambaza 1 na kimadende 1 na kundi la saba lina viyeyusho viwili ambayo jumla yake ni vitamkwa 31 pamoja na viyeyusho.


Kwa upande wa sifa za mahali pa matamshi, konsonanti za Kiswahili Sanifu zimebainishwa katika makundi nane ambayo ni; midomo, mdomo – meno, meno, ufizi, baada ya ufizi, kaakaa gumu, kaakaa laini na koromeo. Katika sifa za mahali pa matamshi, kundi lenye sifa ya ufizi ndilo lenye vitamkwa vingi zaidi ambavyo viko 7. katika Kiswahili Sanifu kundi lingine linalofuatia baada ya hili ni lile lenye sifa ya kaakaa gumu lenye vitamkwa 6, wakati kundi lenye sifa ya midomo na kaakaa laini yana vitamkwa vitano vitano (5), kundi la mdomo meno lina vitamkwa 4, kundi lenye sifa baada ya ufizi lina kitamkwa 1. Sifa ya meno vitamkwa 2 wakati sifa ya koromeo ina kitamkwa 1.


Mchakato huu wa ubainishaji wa vitamkwa konsonanti na viyeyusho vya lugha ya Kiswahili Sanifu kupitia jedwali unaonesha dhahiri sifa bainifu za msingi za vitamkwa hivyo.upande wa kushoto unaonesha namna vitamkwa hivyo vinavyotamkwa ukiangalia kiwima. Hali kadhalika, kiulalo jedwali linaonesha mahali pa matamshi pa vitamkwa

 




71

 


hivyo. Katika kundi la vikwamizi lenye sifa ya mdomo – meno na ya ughuna kuna vitamkwa viwili ambavyo ni [v] na [υ]. Hebu chunguza kwa makini kielelezo namba 10 ambacho ndiyo jedwali lenyewe.



Kielelezo na: 10. Sifa za Kimatamshi za Konsonanti na Viyeyusho vya Kiswahili Sanifu.




JINSI YA MATAMSHI MAHALI PA MATAMSHI

Baada

Mtimbwiliko Midomo Mdomo Meno Ufizi ya Kaakaa Kaakaa Koromeo

-Meno Ufizi gumu laini

Ghuna b d g

VIPASUO Visoghuna p t k

Mpumuo ph th čh kh

VIZUIO Ghuna ɟ

KWAMIZI

Visoghuna č

VIKWAMIZI Ghuna ð z ɤ

Visoghuna f θ s š h

NAZALI Ghuna m ɱ n ñ ŋ

VITAMBAZA Ghuna l

VIMADENDE Ghuna r

VIYEYUSHO Ghuna w y




6:1:2 Viyeyusho vya Kiswahili Sanifu


Katika sura ya tano (taz. 5:1:3:3) nimeeleza kuwa viyeyusho ni vitamkwa vya lugha ambavyo si konsonanti wala si irabu. Hata hivyo wanafonolojia na wanafonetiki wanaviorodhesha vitamkwa hivi pamoja na konsonanti, kwa maana kwamba viyeyusho huorodhesha vikiwa vimeandamana na orodha ya konsonanti kama inavyoonekana katika kielelezo namba 10. Lugha ya Kiswahili Sanifu ina viyeyusho viwili kama ilivyo katika lugha nyingi za Kibantu na lugha ya Kiingereza. Viyeyusho hivyo ni /w/ na /y/ ambavyo vinaonekana katika jedwali la orodha ya konsonanti za Kiswahili Sanifu hapo juu. Vitamkwa hivi vinadhihirika kama ifuatavyo.


Maandishi ya kawaida maandishi ya kifoetiki


a) w [w] mfano katika neno wenu, wimbo, warembo

b) y [y] mfano katika neno Yerusalemu, yenu, yai





6:1:2:1 Sifa Kuu za Viyeyusho vya Kiswahili Sanifu


Sifa kuu za viyeyusho vya Kiswahili Sanifu ni kama zile nilizoeleza katika sura ya tano. Sifa hizi si tofauti na konsonanti kwa maana kwamba sifa za viyeyusho zimejikita katika misingi ya mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi. Upande wa mahali pa matamshi kiyeyusho / w / hutamkiwa kwenye midomo kwa sababu hiyo kiyeyusho hiki

 



72

 


kina sifa ya midomo, wakati kiyeyusho / y / cha Kiswahili Sanifu hutamkiwa kwenye kaakaa gumu na hivyo kuwa na sifa ya kaakaa gumu ya mahali pa matamshi.


Sifa za jinsi ya matamshi, kiyeyusho / w/ cha Kiswahili Sanifu hutamkwa kwa kuviringa midomo kama kwamba unataka kutamka irabu /ʊ/ fupi ya lugha ya Kiingereza


lakini umbo hili hudumu kwa wakaa mfupi na kutoweka. Upande wa kiyeyusho / y/ kina sifa ya kutandaza midomo wakati huo huo hutengeza umbo kama unataka kutamka irabu / ɪ / ya lugha ya Kiingereza ambalo hudumu kwa wakaa mfupi na kutoweka wakati wa utamkaji wake.





6:1:3 Irabu za Kiswahili Sanifu


Kiswahili Sanifu ni mojawapo ya lugha za Kibantu zenye irabu tano ambazo ni a, e, i, o, na u. Irabu hizi zimepangwa na wataalam wa isimu hususani katika tawi la fonolojia katika mfuatano wa i, e, a,o na u kwa kuangalia sehemu za ulimi zinazohusika na utamkaji wa irabu hizo kupitia kielelezo kiitwacho Trapeziam ya Irabu. Utaratibu huu una maana kwamba katika chemba ya kinywa irabu i yenye msimbo huu kifonetiki


hutamkiwa karibu zaidi na irabu e yenye msimbo wa [ε] kifonetiki kwa sababu zote hutamkiwa sehemu ya mbele ya ulimi ambayo ndiyo huhusika katika utamkaji wake. Irabu o yenye msimbo huu [ɔ] wa kifonetiki na irabu u yenye msimbo wa [u] kifonetiki nazo ziko karibu zaidi kwa sababu zote hutamkiwa sehemu ya nyuma ya ulimi. Lakini irabu a yenye msimbo wa [a] kifonetiki ni tofauti kabisa na irabu nyingine kwa sababu yenyewe hutamkiwa katikati ya ulimi yaani sehemu ya kati ya ulimi ndiyo huhusika na utamkaji. Kwa upande mwingine ni kwamba wakati wa utamkaji wa irabu [i] na [ε] sehemu ya mbele ya ulimi huinuka, utamkaji wa irabu [a] sehemu ya kati ya ulimi huinuka na utamkaji wa irabu [ɔ] na [u] sehemu ya nyuma ya ulimi huinuka. Hebu chunguza kielelezo kifuatacho.



Kielelezo na: 11. Trapeziam ya Irabu za Kiswahili Sanifu.

 

























73

 


Irabu za Kiswahili Sanifu hupambanuliwa kwa kuzingatia vipengele vya msingi vikuu vitatu. Kigezo cha kwanza ni cha sehemu ya ulimi inayohusika wakati wa utamkaji, kigezo cha pili ni mwinuko wa ulimi wakati wa utamkaji na kigezo cha tatu ni hali au umbo la midomo wakati wa utamkaji kama nilivyoeleza katika sura ya tano (5:1:3:2). Sifa hizi nitazieleza kinaganaga kupitia kielelezo kifuatacho.


Kielelezo  na: 12. Sifa Pambanuzi za Irabu za Kiswahili Sanifu


IRABU SIFA PAMBANUZI ZA IRABU

Sehemu ya Mwinuko wa Hali/ umbo la Wakaa wa

ulimi ulimi ndani  ya midomo wakati utamkaji wa

inayohusika. kinywa. wa utamkaji. irabu husika.

[i] Hutamkiwa Ulimi Hali ya Wakaa wake ni

mbele.  Ina sifa huinuliwa midomo ni ya mrefu [+mrefu]

ya [+mbele] katika ulalo wa msambao, hutamkwa kwa

juu  sana, Ina kama muda mrefu.

sifa ya [+juu] unatabasamu,

ina sifa ya

[+msamb]

[ε] Hutamkiwa Ulimi Hali ya Wakaa wake ni

mbele.  Ina sifa huinuliwa midomo ni ya mrefu [+mrefu]

ya [+mbele] katika ulalo wa kutandaza. Ina hutamkwa kwa

kati. Ina sifa ya sifa ya muda mrefu.

[+kati] [+utandaz]

[a] Hutamkiwa Ulimi huwa Hali ya Wakaa wake ni

katikati ya katika ulalo wa midomo ni ya mrefu [+mrefu]

ulimi lakini chini.  Irabu  hii kutandaza. Ina hutamkwa kwa

karibu zaidi na ina sifa ya sifa ya muda mrefu.

nyuma. Ina sifa [+chini] [+utandaz]

[+kat]

[ɔ] Hutamkiwa Ulimi Hali ya Wakaa wake ni

nyuma. Ina sifa huinuliwa midomo ni ya mrefu [+mrefu]

ya [+nyum] katika ulalo wa uviringo usio hutamkwa kwa

kati. Ina sifa ya wa kufunga muda mrefu.

[+kati] kabisa. Ina sifa

ya [+uviring]

[u] Hutamkiwa Ulimi Hali ya Wakaa wake ni

nyuma. Ina sifa huinuliwa kwa midomo ni ya mrefu [+mrefu]

ya [+nyum] ulalo wa juu uviringo wa hutamkwa kwa

sana. Ina sifa ya kufunga muda mrefu.

[+juu] midomo kabisa.

Ina sifa ya

[+uviring]


Katika kielelezo hicho hapo juu nimeonesha sifa pambanuzi zinazozipambanua irabu tano za Kiswahili Sanifu. Maelezo ya sifa hizo bainifu za irabu za Kiswahili Sanifu

 




74

 


yaliyoko katika kielelezo namba 12 yanahusu irabu tano zilizoko ndani ya kielelezo cha namba 11. Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa maelezo yaliyoko katika kielelezo namba 12 yanabainisha sifa mbalimabali za irabu ambazo ziko kwenye kielelezo na 11, ingawa hata ndani ya kielelezo namba 12 irabu hizo zimeoneshwa au zimeandikwa kifonetiki. Sauti au irabu hizi kwa kiasi fulani hutofautiana katika tahajia yake ya kawaida na ya kifonetiki. Hebu chunguza katika kielelezo kifuatacho.


Kielelezo na: 13


Maandishi

ya kawaida i e a o u

Maandishi

ya kifonetiki [i] [ε] [a] [ɔ] [u]



Katika Kiswahili Sanifu irabu zote zina sifa ya wakaa mrefu, ijapokuwa katika lugha nyingine kuna irabu zenye wakaa mrefu na wakaa mfupi kama nilivyoeleza katika sura ya tano (taz. 5:1:3:2) katika lugha ya Kiingereza kuna irabu ndefu, zenye wakaa mrefu katika utamkaji wake na irabu fupi, zenye wakaa mfupi wakati zinapotamkwa. Lugha hutofautiana kutokana na aina ya silabi za lugha fulani maalum. Tukiangalia lugha ya Kiswahili Sanifu ina irabu tano na zote zina sifa wakaa mrefu.


Baada ya kuona vitamkwa au fonimu za Kiswahili Sanifu kwa kuchunguza konsonanti, viyeyusho na irabu umegundua sasa kuwa Kiswahili Sanifu kina jumla ya fonimu 36. Katika jumla ya fonimu hizo au vitamkwa hivyo kuna konsonanti 29, viyeyusho 2 na irabu 5. Ikumbukwe kwamba ninapozungumzia vitamkwa vya Kiswahili Sanifu ninakuwa nazungumzia fonimu za Kiswahili Sanifu.



6:2 Sifa Bainifu za Fonimu za Kiswahili Sanifu


Yapo madai mbalimbali ya wataalam wa taaluma ya fonolojia kuwa fonimu ina sifa kuu bainifu ambazo huibainisha na kuitofautisha na fonimu nyingine. Kwa mfano:


Mgullu (1999) anasema katika kitabu chake kiitwacho Mtaala wa Isimu, Fonetiki na

Fonolojia ya Lugha ya Kiswahili. Anasema kwamba:


“Vitamkwa konsonati vina sifa ya [+kons] wakati vitamkwa irabu vina sifa ya usilabi [+sil] na sifa ya usonoranti [+son].”


Noam Chomsky na Morris Halle (1968) Saund Pattern of English. Wao wanabainisha sifa bainifu za fonimu hivi:


Noam Chomsky anasema kwamba:


“ kuna baadhi ya vitamkwa vina sifa ya ukontinuanti,yaani vifulizwa mfano sauti


[f], vile vile anaeleza kuwa kuna baadhi ya sauti zina wakaa mrefu, nyingine wakaa mfupi na nyingine zina wakaa mrefu zaidi ya kawaida katika utamkaji wake.”

 




75

 


Morris Halle, yeye anazitazama sifa za fonimu kwa kubainisha sifa za konsonanti kwa kuzingatia mahali pa matamshi pa sauti konsonanti, pia anabainisha sifa za sauti husika kwa kuangalia namna ya matamshi mfano sauti [p] ni [+mid] kwamba ina sifa ya kutamkiwa kwenye midomo,vile vile ina sifa ya konsonanti [+kons] sababu wakati wa utamkaji wake kuna mzuio wa mkondohewa ambao ni wa kubana kabisa kisha kuachiwa ghafula.


Kutokana na ubainisho huo uliofanywa na wataalam hawa utagundua kuwa fonimu ina sifa nyingi bainifu. Hata hivyo wataalam hawa wanabainisha sifa kuu tatu za msingi kabisa kisha sifa hizi za jinsi ya matamshi na sifa za mahali pa matamshi. Nitazieleza sifa hizo kwa mawanda yake hapa chini.



6:2:1 Sifa Kuu za Msingi za Fonimu za Kiswahili Sanifu


Katika mchakato wa kubainisha sifa kuu za vitamkwa vya kawaida (fonimu) imegundulika kuwa kuna sifa kuu tatu ambazo zinazitofautisha fonimu hizo. Sifa hizo ni ukonsonanti, usilabi na usonoranti. .


Sifa ya kwanza ni ya ukonsonanti [±kons], sifa hii inahusu sauti ambazo hutamkwa kukiwa na mzuio wa hewa katika mkondohewa. Ninapozungumzia mkondohewa na mzuio wa hewa katika mkondohewa kinachotokea hapa ni kwamba sauti zinagawanyika katika makundi mawili yaani konsonanti na irabu. Sifa ya ukonsonanti inapokuwepo kwa fonimu inayochunguzwa huwekewa alama ya [+kons] kwa maana ya kwamaba sifa ya ukonsonanti ipo katika fonimu husika. Sifa ya ukonsonanti ipo kwa fonimu konsonanti tu ambazo huruhusu mzuio wa hewa katika mkondohewa kwa kutumia alasauti wakati wa utamkaji wake. Fonimu irabu hazina sifa ya ukonsonanti na hivyo hupewa alama ya kutoa konsonanti [-kons] kwa sababu wakati wa utamkaji wake hakuna mzuio wa mkondohewa. Hali hii ya kutokuwepo kwa mzuio katika mkondohewa hujitokeza pia katika vitamkwa viyeyusho pia na hivyo kupewa sifa ya kutoa konsonanti [-kons].


Sifa ya pili ni ya usilabi [±sil], hii inahusu vitamkwa ambavyo vina sifa ya usilabi. Katika sifa hii kundi la irabu ndilo hupewa sifa ya kujumlisha ya usilabi [+sil] kwa sababu zinaweza kusimama kama silabi mfano katika neno “oa”, irabu [ɔ] na irabu [a] zina sifa ya usilabi kwani zinatamkwa kwa mkupuo mmoja wa sauti kila moja kama fungu la sauti linalojitegemea na hivyo kuliona neno “oa” kuundwa silabi mbili. Sifa hii hujitokeza pia katika baadhi ya vitamkwa konsonanti ambazo ni nazali. Nazali ni konsonanti zenye kupewa sifa ya usilabi katika mazingira fulani fulani [+sil], mfano katika maneno yafuatayo:


Mifano na: 1.

a) mbwa → sauti m ina sifa ya [+sil] na [+naz]


b) nje → sautin ina sifa ya [+sil] na [+naz]


m na n maana yake ni konsonanti zenye usilabi. Katika uandishi alama N inatumika kumaanisha nazali au ving’ong’o vyote.







76

 


[m]


[n]

N=[ŋ]


[ñ]


[ɱ]


Sifa ya tatu ni ya usonoranti [±son], hii ni sifa inayoweza kubagua aina ya vitamkwa yaani ving’ong’o ,irabu, na vilainisho. Ni sifa inayohusu vitamkwa vya irabu, vilainisho, viyeyusho, nazali, na konsonanti silabi kwa maana nazali zenye sifa ya usilabi. Lakini kundi la konsonanti halina sifa ya usonoranti,si kwa ujumla wake bali ni kwa vitamkwa konsonanti ambavyo si ghuna. Kwa ujumla usonoranti unahusu vitamkwa vyenye sifa ya ughuna. Hebu chunguza kielelezo kifuatacho kinachoonesha sifa hizo.


Kielelezo na: 14. Sifa Kuu za Fonimu


Sifa  kuu  za Konsonanti Irabu Lainisho Yeyusho Nazali Nazali.

fonimu Silabi

K I L Y N N

Ukonsonanti + + + +

Usilabi + +

Usonoranti + + + + +



Ufafanuzi

[+] → maana yake sifa ipo kwa fonimu au kitamkwa/ kundi husika.


[ ]→ maana yake sifa haipo kwa kitamkwa au fonimu inayohusika / kundi husika.

Lainisho  ni istilahi inayojumuisha vitankwa vimadende na vitambaza.



Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa vigezo hivyo vitatu vina dhana pana sana na hivyo ni vigumu kubainisha sifa bainifu za fonimu au vitamkwa vya lugha husika, kwani kuna sifa nyingine zaidi ya hizo hususani za jinsi ya matamshi na mahali pa matamshi. Wataalam wa taaluma hii ya fonolojia walipoiona dhana hii kuwa na ujumuisho mkubwa wakaamua kuchunguza na kubainisha fonimu kwa kutumia vigezo vya mahali pa matamshi na jinsi ya matamshi. Hapa chini nitaeleza sifa hizo kinaganaga.



6:2:2 Sifa Bainifu za Fonimu za Kiswahili Sanifu za Mahali pa Matamshi


Ni ukweli usioppingika kwamba fonimu au vitamkwa vyovyote vile vina sifa zake mahususi za mahali pa matamshi. Ninaposema sifa za mahali pa matamshi ninazungumzia wapi au mahali gani ambapo sauti hizo zinatamkiwa kila moja kwa nafasi yake. Katika kubainisha sifa za fonimu au vitamkwa kwa kutumia kigezo hiki kuna sifa kadhaa kama nitavyozianisha.




77

 


Sifa ya kwanza ni ukorona [±kor], sifa hii inahusu sauti au fonimu zinazotolewa kwa kutumia bapa la ulimi au ncha ya ulimi kwa kujenga msogeano mwembamba au wa kubana. Sifa hii inahusisha vitamkwa vya meno yaani [θ] na [ð], vitamkwa vya ufizi juu mfano sauti [s], [z], [l], [t], [d], na nyingine nyingi, pamoja na za kaakaa gumu kama vile [č], [š], [ɟ], [ñ] na [y]. Fonimu hizi zina sifa ya ukorona na katika tahajia ya kifonetiki huoneshwa kwa msimbo huu [+kor] wakati sauti zisizo na sifa hii inaoneshwa kwa msimbo huu [ kor].


Sifa ya pili ni uanteria [±ant], sifa hii inahusu fonimu ambazo hutolewa kuanzia kwenye ufizi au mbele ya ufizi yaani midomo, meno, na ufizi juu. Vitamkwa vinavyohusika katika sifa hii ni pamoja na [p], [b], [t], [d], [p h], [t h], [θ], [ð],[s], [z], [f], [v],[ɱ], [υ], [m] [n], [l] na [r]. Fonimu zina sifa hii na katika tahajia ya kifonetiki huoneshwa kwa msimbo huu [+ant] wakati fonimu zisizo na sifa hii huoneshwa kwa msimbo wa [-ant].


Sifa ya tatu ni umeno [±meno], hii inahusu fonimu zenye sifa ya kutamkiwa kwenye meno na zile zisizo na sifa ya kutamkiwa kwenye meno isipokuwa zina sifa ya ukorona. Hapo naweza kusema kwamba fonimu zenye sifa ya ukorona zina sifa ya umeno au la. Kwa mfano fonimu zinazotamkiwa kwenye meno zina sifa ya [+meno] na zile zisizotamkiwa kwenye meno lakini zina sifa ya ukorona zinapewa sifa ya kutoa umeno [-meno].


Mifano na:2


sauti ð [+meno]

sauti z [-meno]


sifa ya nne ni ya uglota [±glot], sifa hii inahusu kitamkwa kimoja tu kinachotamkiwa kwenye glota au koromeo. Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kitamkwa chenye sifa ya uglota ni sauti [h]. Kitamkwa au fonimu hii inapewa sifa ya [+glot] na vile visivyo na sifa hii hupewa au huoneshwa kwa alama ya [-glot].



6:2:3 Sifa za Fonimu za Kiswahili Sanifu za Jinsi ya Matamshi


Ninaposema sifa za fonimu za jinsi ya matamshi ninazungumzia namna hewa inavyotoka wakati wa utamkaji wa fonimu hizo. Katika kigezo hiki tunazingatia msikiko wa sauti na jinsi hewa inavyoachiliwa kutoka katika chemba ya kinywa na chemba ya pua. Kwa kutumia kigezo hiki kuna sifa kadhaa kama nitavyoeleza hapa chini.


Sifa ya kwanza ni ya usilabi [±sil], sifa hii inahusu irabu zote na baadhi ya ving’ong’o ambavyo vyote ni vitamkwa ambavyo hutamkwa kwa mara moja kama fungu moja la sauti linalojitegemea kimatamshi na huwa na msikiko mkubwa zaidi wakati wa utamkaji wake. Kutokana na hali hiyo irabu na ving’ong’o hivyo vimepewa sifa ya [+sil] lakini konsonanti nyingine pamoja na viyeyusho havina sifa ya usilabi hivyo kifonetiki huoneshwa kwa msimbo wa [-sil].


Sifa ya pili ni ya ukontinuanti [±kont], hii ni sifa ambayo inahusu fonimu ambazo wakati wa utamkaji, mkondohewa au hewa hutiririka moja kwa moja bila kuzuiliwa. Fonimu hizo ni irabu, ving’ong’o (nazali), viyeyusho, vilainisho na vikwamizi. Fonimu hizi zina sifa ya ukontinuanti ambayo kifonetiki huandikwa [+kont] lakini kwa upande

 




78

 


wa vitamkwa viitwavyo vipasuo na vipasuo kwamizi au vizuio kwamizi vina sifa kutoa ukontinuanti yaani [-kont].


Sifa ya tatu ni ya mwachio taratibu [±tar], sifa hii inahusu vitamkwa ambavyo wakati wa utamkaji wake mkondohewa huzuiliwa kwa kubanwa kabisa na alasauti zinazohusika na utamkaji wa sauti husika kisha huachiwa taratibu. Vitamkwa vinavyohusika hapa ni


na [ɟ] vina sifa ya [+tar] wakati vingine vyote vina sifa ya [-tar].


Sifa ya nne ni unazali [±naz], ambayo inahusu vitamkwa au fonimu ving’ong’o ambavyo wakati wa utamkaji wake hewa hutolewa nje kupitia chemba ya pua. Sifa hii inahusisha vitamkwa [m],[ɱ], [n], [ñ] na [ŋ]. Sauti hizi zina sifa ya kujumlisha nazali kifonetiki [+naz] na fonimu nyingine zinazobaki zina sifa ya kutoa nazali kifonetiki [-naz].


Sifa ya tano ni ya utambaza [±tamb], ambayo inahusu fonimu ambayo wakati wa utamkaji wake alasauti ulimi huwa katikati huku umetandazwa na ncha yake (ya ulimi) ikigusa ufizi na hewa kupita pembeni mwa ulimi ili kutoka nje ya kinywa. Sifa hii inahusu fonimu [l], hii ina sifa ya [+tamb] na fonimu nyingine zina sifa ya [-tamb].


Sifa ya sita ni ya umadende [±mad], ambayo inahusu fonimu [r], ambayo wakati wa utamkaji wake alasogezi, ncha ya ulimi hugongagonga alatuli, baada ya ufizi kwa harakaharaka mara kadhaa. Sauti [r] ina sifa ya [+mad] na fonimu nyingine zisizo na sifa hizo hubainishwa kifonetiki kwa msimbo wa [-mad].



6:2:4 Sifa za Fonimu za Kiswahili Sanifu za Mtimbwiliko wa Nyuzisauti


Sauti za Kiswahili Sanifu zinabainishwa pia kwa kutumia kigezo cha nyuzisauti. Ninaposema kigezo cha nyuzisauti nina maana kwamba mtimbwiliko wa nyuzisauti katika kisanduku cha nyuzisauti. Kigezo hiki hutupatia makundi mawili ya sauti. Sifa hizi ni:


Sifa ya ughuna [±ghun], sifa hii inahusu fonimu ambazo wakati wa utamkaji wake nyuzisauti hukaribiana sana au hugusana na katika hali hiyo hewa kutoka mapafuni huzisukuma ili ipate nafasi ya kupita. Katika mchakato huo husababisha mtimbwiliko katika nyuzisauti, mtimbwiliko huu husababisha sauti zinazotoka ziwe na mghuno mkubwa. Sifa hii inahusisha sauti hizi [b],[d], [g], [m],[ɱ], [ñ], [ð], [υ], [ɟ], [ɤ], [z], [n],[v], [r],[l], [w], [y], [i], [ε], [a], [ɔ],[u], na [ŋ]. Sauti hizi zina sifa ya ughuna na hivyo kupewa sifa ya kifonetiki kwa msimbo wa [+ghun].


Kundi la pili katika sifa hii ni vitamkwa au fonimu zenye sifa ya [-ghun], vitamkwa vinavyobeba sifa hii utamkaji wake ni ule ambao nyuzisauti huachana au hubaki katika hali yake ya kawaida na hivyo hewa kutoka mapafuni hupita bila kizuizi chochote. Sifa hii inagusa fonimu za [p], [t], [k], [θ], [š], [č], [s] ,[f] na [h]. Sauti hizi kifonetiki zimepewa alama ya [-ghun].



6:2:5 Sifa za Fonimu za Kiswahili Sanifu za Mpumuo


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna fonimu zenye sifa ya mpumuo ambayo kwayo vitamkwa vinavyotamkwa hutamkwa kwa kutumia pumzi kali. Sifa hii hujitokeza katika baadhi ya fonimu za Kiswahili Sanifu kama ifuatavyo:

 




79

 


Sifa ya mpumuo [±mpum] ni sifa ambayo inahusu fonimu ambazo hutamkwa kwa pumzi kali. Fonimu hizo ni [ph], [th], [kh] na [čh], ambazo zina sifa hii ya mpumuo na hupewa sifa ya [+mpum] kifonetiki ambayo nimeona ni muhimu kuitambulisha kama sifa tambulishi ya vitamkwa hivyo ya jinsi ya matamshi.


Upande wa fonimu ambazo hazina sifa hii ya mpumuo hakuna tofauti na zile nilizoeleza katika sifa zilizotangulia. Fonimu hizo zinabainishwa kifonetiki kwa kupewa alama ya kutoa mpumuo [-mpum] katika maandishi ya kifonetiki. Unaweza kuona kuwa kila sifa ina umuhimu mkubwa sana katika kuibainisha fonimu.



6:2:6 Sifa za Fonimu za Kiswahili Sanifu za Ulimi


Katika sifa za fonimu za Kiswahili Sanifu kwa kuzingatia kigezo cha ulimi, tunaangalia mwinuko wa ulimi, sehemu ya ulimi inayoinuka wakati wa utamkaji, kwa maana ya mwinuko wa ulimi ni wa juu, kati au chini na sehemu ya ulimi inayoinuka ni ya mbele, kati au nyuma.


Katika kigezo hiki tunapata sifa kadhaa za fonimu au vitamkwa vya Kiswahili Sanifu, kwa kuzingatia sehemu za ulimi na mwinuko wa ulimi, kwamba mwinuko unaweza kuwa wa juu, kati na chini.


Sifa ya kwanza ni ya ujuu [±juu], ambayo inahusu vitamkwa ambavyo ulimi huinuliwa juu kwenye chemba ya kinywa wakati wa utamkaji wa sauti hizo. Kiwango cha kuinuliwa ni cha juu kabisa na kunuiliwa kwa ulimi huo katika kiwango hicho baadhi ya sauti hutamkwa. Sauti hizo ni kama [i], [u], [ɟ], [ñ], [č], [ŋ] na kadhalika. Zina sifa ya [+juu] na zingine zisizo na sifa hiyo huwekewa alama [-juu].


Sifa ya pili ni ukati [±kati], ambayo inahusu sauti ambazo wakati wa utamkaji wake ulimi huinuliwa katika ulalo wa katikati. Mfano tunapotamka sauti kama [ε], [ɔ], [f], [v] na kadhalika zina sifa ya [+kati]. Sauti zisizo na sifa hii hupewa alama ya [-kati].


Sifa ya tatu ni ya uchini [±chin], ambayo utamkaji wa sauti ambazo ulimi huinuliwa katika ulalo wa chini kabisa katika utamkaji wa sauti hizo. Sauti zinazohusika na sifa hii ni kama [a], [h] na kadhalika ambazo huoneshwa kifonetiki kwa alama ya [+chin] na zisizo na sifa hii hutambulishwa kifonetiki kwa alama ya [-chin].


Sifa ya nne ni ya umbele [±mbel], inahusu sauti ambazo sehemu ya mbele ya ulimi huhusika wakati utamkaji wake. Sifa hii inahusu au inajumuisha sauti zifuatazo; [i], [ε], [t], [d], [v], [m], [υ], [ɱ], [ð] na kadhalika zina sifa ya [+mbel]. Sauti zisizo na sifa hii hubainishwa kwa msimbo huu [-mbel].


Sifa tano ni ya ukati [±kat] ambayo inahusu vitamkwa ama fonimu ambazo katika utamkaji wake sehemu ya kati ya ulimi au kiwiliwili cha ulimi. Vitamkwa hivyo ni [a], [ɟ], [č] na sauti nyingine zina sifa ya kujumlisha ukati kifonetiki,[+kat] na zile zisizo na sifa hii hupewa alama ya kutoa kifonetiki [-kat].


Sifa ya sita ni ya unyuma [±nyum] ambayo inahusu vitamkwa vinavyotamkiwa sehemu ya nyuma ya ulimi katika chemba ya kinywa vikienda sambamba na kaakaa laini. Sifa hii inajumuisha vitamkwa [u], [ɔ],[k], [g], [ŋ], [ɤ] na kadhalika. Vitamkwa hivi vina sifa ya [+nyum] kifonetiki na zisizo na sifa hii hupewa alama ya [-nyum] kifonetiki.

 








80

 

6:2:7 Sifa za Fonimu za Kiswahili Sanifu za Umbo la Midomo


Katika kipengele hiki tunaangalia midomo inakuwa na umbo la namna gani wakati wa utamkaji wa sauti inayohusika. Katika kipengele hiki kuna sifa kuu tatu ambazo ni uviringo, msambao, na utandazo.


Sifa ya kwanza ni ya uviringo [±uviring] ambayo kwayo midomo huviringwa ili kutamka sauti inayohusika. Mtamkaji anapotamka huvuta midomo na kuileta mbele ili kutengeneza umbo la uviringo. Umbo hili linapokuwa limetengeneza husababisha baadhi ya sauti za lugha ya Kiswahili Sanifu kutamkwa. Sifa hii inajumuisha sauti kama [m], [ɱ], [u], [ɔ] na kadhalika ambazo kifonetiki hubainisha kifonetiki kwa alama [+uviring]. Sauti zisizo na sifa hii hutambulishwa kwa msimbo huu [-uviring] wa kifonetiki.


Sifa ya pili ni ya msambao [±msamb] ambayo kwayo hutengeneza umbo la midomo ambalo mtamkaji utafikiri anataka kutabasamu. Midomo husambaa wakati wa utamkaji wa sauti hizo. Sifa hii inahusu sauti kama [i], [f], [v], [υ], [θ], [ð] na kadhalika zina sifa hii ambayo kifonetiki hubainishwa kwa alama ya kujumlisha [+msamb] kifonetiki na sauti zisizo na sifa hiyo hubainishwa kwa alama [-msamb].


Sifa ya tatu ni ya utandazo [±utandaz] ambayo kwayo midomo hutandazwa wakati wa utamkaji wa sauti inayohusika. Sifa hii inahusu vitamkwa kama [t], [d], [s], [z], [a], [ε], [k], [g] na kadhalika. Sifa hii ina idadi kubwa ya fonimu ambazo kifonetiki hubainishwa kwa alama ya [+utandaz] na zile zisizo na sifa hii hubainishwa kifonetiki kwa alama ya [-utandaz].


Kwa ujumla sifa hizo hapo juu zinabainisha fonimu za Kiswahili Sanifu kwa kila moja. Sifa hizi zitaoneshwa dhahiri kwa kila sauti kupitia kielelezo nitachochora hapa chini. Kielelezo hiki kina fonimu thelethini na sita (36) za Kiswahili Sanifu pamoja na sifa zake pambanuzi ambazo zinazipambanua fonimu hizo. Kupitia kielelezo hicho naamini utaelewa utazielewa kwa upana zaidi juu ya sifa pambanuzi za fonimu hizo.

 
































81

 

Kielelezo na: 15



SIFA

BAINIFU FONIMU ZA KISWAHILI SANIFU

N ph th kh čh

a p b t d k g č ɟ f v υ θ ð s z š ɤ h m ɱ n ñ ŋ l r w y i ε a ɔ u

1 Ghun - + - + - + - - - - - + - + + - + - + - + - + + + + + + + + + + + + + +

2 Kont - - - - - - - - - - - - + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

3 Tar - - - - - - - - - + + + - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -

4 Naz - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - + + + + + - - - - - - - - -

5 Tamb - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - + - - - - - - - -

6 Mad - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - + - - - - - - -

7 Kor - - + + - - - + - + + + - - - + + + + - - - + + + + - + + - + + + + - -

8 Ant + + + + - - + + - - - - + + + + + + + - - - + + + - - + + + - + + - - -

9 Meno - - - - - - - - - - - - + + + + + - - - - - - + - - - - - - - - - - - -

10 Glot - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - + - - - - - - - - - - - - - -

11 Juu - - + + + + - + + + + + - - - + + + + + + - - - + + + + + + + + - - - +

12 Kati + + - - - - + - - - - - + + + - - - - - - - + + - - - - - - - - + - + -

13 Chini - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - + - - - - - - - - - - - + - -

14 Mbele + + + + - - + + - - - - + + + + + + + - - - + + + - - + + - - + + - - -

15 Kat - - - - - - - - - + + + - - - - - - - + - - - - - + - - - - + - - + - -

16 Nyum - - - - + + - - + - - - - - - - - - - - + - - - - - + - - + - - - - + +

17 Son - + - + - + - - - - - + - + + - + - + - + - + + + + + + + + + + + + + +

18 Sil - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - + + + + +

19 Kons + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + - - - - - - -

20 Uviring + + - - - - + - - + + + - - - - - - - - - - + + - - - - - + - - - - + +

21 Msamb - - - - - - - - - - - - + + + + + - - - - - - - + + - - - - - + - - - -

22 Utandaz - - + + + + - + + - - - - - - - - + + + + + - - - - + + + - + - + + - -

23 Mid + + - - - - + - - - - - + + + - - - - - - - + + - - - - - + - - - - - -

24 Mpum - - - - - - + + + + - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -









Katika jedwali hilo hapo juu linaonesha sifa bainifu za vitamkwa au fonimu za Kiswahili sanifu amabazo ni sifa za msingi. Alama ya kujumlisha [+] inadhihirisha uwepo wa sifa husika na alama ya kutoa [-] inaonesha kutokuwepo kwa sifa husika. Vile vile katika kielelezo hicho sifa namba 11 – 13 zinahusu mwinuko wa ulimi wakati wa utamkaji wa sauti. Sifa kuanzia namba 14 – 16 zinahusu sehemu za ulimi zinahusika wakati wa utamkaji wa sauti mbalimbali za Kiswahili Sanifu. Na sifa kuanzia namba 20 – 22 zinahusu umbo au hali ya midomo wakati wa utamkaji wa fonimu mbalimbali za Kiswahili Sanifu. Kutokana na sifa zilizoainishwa hapo juu inaonesha kuwa fonimu ina sifa nyingi ambazo huipambanua fonimu husika na kuitofautisha fonimu moja na nyingine.



6:3 Dhana Kuu Katika Ubainishaji wa Sifa Bainifu za Fonimu za Kiswahili Sanifu


Katika ubainishaji wa sifa bainifu za vitamkwa au fonimu za Kiswahili Sanifu kuna dhana kuu mbili ambazo zinatuwezesha kutambua sifa kuu za msingi za fonimu hizo. Dhana hizi hueleza sifa muhimu za fonimu husika au zinazotofautisha fonimu mbili. Katika mchakato huu kuna dhana ya uwekevu na dhana ya uziada ambazo hutusaidia katika kupambanua sifa pambanuzi za fonimu zinazoshughulikiwa. Dhana hizi nitazieleza kwa mawanda mapana hapa chini.

 



82

 

6:3:1 Uwekevu


Dhana ya uwekevu au iktisadi ni dhana ambayo inahusu sifa zote za msingi ambazo huweza kutambulishwa kwa alama ama ya [+] au ya [-] ijapokuwa sifa hizi zimeonekana kuchukua zaidi alama ya kujumlisha kuliko ya kutoa. Sifa hizi huwa ni za msingi kwa kundi fulani la fonimu au vitamkwa. Kwa asilimia kubwa sifa ya uwekevu huonesha uwepo wa sifa fulani au hali fulani kwa fonimu fulani kwa kutumia msimbo wa kifonetiki wa [+] na kwa zile ambazo ni za uwekevu lakini zinaonesha kutokuwepo kwa hali fulani kwa fonimu husika sifa hiyo hutambuliwa kwa msimbo wa [-] kifonetiki. Sifa za uwekevu huweza kutabiri kuwepo au kutokuwepo kwa sifa nyingine fulani kwa fonimu husika.


Sifa za uwekevu kifonetiki zinabainishwa kwa kiasi kikubwa kwa alama ya [+], kwa mfano sifa ya uwekevu ya fonimu [m] ni [+naz] ambayo inatabiri uwepo wa sifa ya [+kons], [+ghun] na [+sil]. Dhana ya uwekevu ni dhana muhimu sana katika ubainishaji wa sifa za msingi ya vitamkwa viwili au zaidi. Lakini pia mfano sifa ya [-kont] ni sifa ya uwekevu kwa vipasuo na vipasuo kwamizi / vizuio kwamizi.


Mifano na: 3

a) [p] [m]

[-kont ] [+naz ]

[+ant ] [+ant ]

[+ mid ] [+mid ]

[+mbel ] [+mbel ]

[-ghun ] [ +ghun]

b) [t] [d]

[- kont ] [- kont ]

[-ghun ] [+ghun ]

[+mbel ] [+mbel ]

[+ant ] [+ant ]

[+kons ] [+kons ]


Katika mifano hiyo hapo juu sauti [p] ina sifa za uwekevu za [-kont] na [-ghun] wakati sauti [m] ina sifa za uwekevu za [+naz] na [+ghun] hizo sifa ndizo zinazitofautisha sauti hizo na sifa zinazobaki ni za uziada kwa sababu vitamkwa vyote vina sifa hizo. Hali hiyo imejitokeza pia katika mfano wa b) sauti hizo zina sifa kuu ya uwekevu ya [-kont] lakini zina sifa ya uwekevu inayozitofautisha sauti hizo ni kwamba sauti [t] ina sifa ya uwekevu ya [-ghun] na sauti [d] ina sifa ya uwekevu [+ghun].


Hata hivyo sifa za uwekevu huenda sambamba na sifa za uziada kwa sababu zote kwa pamoja huweza kuipambanua, na kuitofautisha fonimu moja na fonimu nyingine kwa kutabiri kuwepo au kutokuwepo kwa sifa fulani katika fonimu hiyo.

 











83

 

6:3:2 Uziada


Dhana ya uziada inahusu sifa ambazo huweza kutabirika kupitia sifa za uwekevu. Sifa za uziada huweza kuoneshwa ama kwa alama ya [-] au ya [+] kifonetiki. Sifa ambazo hutabirika kuwepo ama kutokuwepo kutokana na kuwepo kwa sifa moja ya msingi, sifa hizo zinaitwa sifa za uziada. Mfano katika vitamkwa irabu sifa ya [-kons] hutabirika kutokuwepo kwa sababu ya kuwepo kwa sifa ya msingi ya uwekevu ya [+sil], ambayo inatabiri kutokuwepo kwa sifa ya ukonsonanti kwa fonimu.


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu sifa kama ya [+ghun], inaonekana ni ya uziada katika kundi la nazali, vimadende, vitambaza, viyeyusho na irabu kwa sababu kwa asili fonimu hizo ni ghuna. Kwa maana kwamba ukitaja sifa umadende, utambaza, usilabi, unazali, sifa hizi hutabiri uwepo wa sifa ya ughuna kwa fonimu hizo.


Kwa ujumla dhana ya uziada inahusu sifa ambazo huweza kutabirika kuwepo au kutokuwepo kwa sifa fulani kwa fonimu inayoshughulikiwa. Upande wa sifa ya uziada inayooneshwa kwa alama ya kutoa [-] kifonetiki ni kama ifuatavyo.


Mifano na: 4

a)  [a] [k]

[+sil ] [-sil ]

[-kons ] [+kons ]

[-mbel ] [-kat ]

[+kat ] [+nyum]

[+ chin ] [+juu ]

[-juu ] [-chin ]


Katika mifano hiyo ya hapo juu fonimu [a] ina sifa za uziada za [-kons], [-mbel] na [-juu] wakati fonimu [k] ina sifa za uziada za [-sil], [-kat], na [-chin]. Kwa sababu sifa hizi hutabirika kutokuwepo kwake kutokana na uwepo wa sifa za [+sil], [+kat], na [+chin] kwa fonimu [a] na uwepo wa sifa za [+kons], [+nyum] na [+juu] kwa fonimu [k].


Kwa ujumla ama angalizo ni kwamba dhana hizi hufanya kazi kama mapacha lakini kitu cha msingi hapa ni kujua fonimu hizo unazozishughulikia ziko katika kundi gani. Hii ni kwa sababu kila kundi lina sifa yake kuu ya msingi, lakini pia fonimu kama ni za kundi moja huweza kutofautiana mahali pa matamshi na sifa ya nyuzisauti yaani mtimbwiliko. Kupitia sifa hizo unaweza kutambua sifa za uwekevu na za uziada. Kama nilivyoonesha katika mifano namba tatu. Naweka angalizo kwa sababu si wakati wote alama ya [+] hutumika kwa sifa ya uwekevu kama nilivyosema hapo juu hivyo hivyo upande wa alama [-]. Kwa mantiki hiyo ni lazima kuzingatia sifa za msingi za vitamkwa hivyo kwa sababu alama hizi kimatumizi huingiliana.



6: 3:3 Njia au Kanuni za Jumla za Kugundua Uwekevu na Uziada


Sifa za uwekevu na uziada ni za msingi katika kutofautisha fonimu za lugha Fulani maalum katika tawi la fonolojia. Uwekevu na uziada kama sifa zinaweza kutambuliwa au kupambanuliwa kwa kutumia njia mbalimbali. Kanuni za kuweza kubaini mchakato mzima wa sifa za uwekevu na uziada ni za msingi kwa mwanaisimu yeyote

 




84

 


anayeshughulikia sifa bainifu za fonimu za lugha maalum. Katika mchakato huo tuna njia au kanuni zifuatazo:


Kanuni ya kwanza ni ya uwili unaopingana, njia hii inahusu kuwepo kwa sifa mbili zinazopingana, kwa maana kwamba sifa moja ikiwepo nyingine haiwezi kuwepo. Njia hii au kanuni hii hutusaidia sana katika kugundua sifa za uwekevu na sifa za uziada. Hebu angalia na kuchunguza kwa makini mifano ifuatayo:


Mifano na: 5


[+sil]  na  [-kons]


Katika mfano huo hapo juu fonimu inayohusika ina sifa ya uwekevu ya [+sil] na sifa ya uziada ya [-kons].


[-kont] na [ +kons]


Katika mfano huo hapo juu inayohusika na ina sifa ya uwekevu ya [-kont] na sifa ya uziada ya [+kons].


[+juu] na [-chin]


Katika mfano huu fonimu inayohusika hutamkwa wakati ulimi umeinuliwa katika ulalo wa juu kabisa na hivyo kuwa na sifa uwekevu ya [+juu] na kuwa sifa ya uziada ya [-chin].


[+son]  na [+ghun]


Katika mfano huu fonimu inayohusika hapa ina sifa ya uwekevu ya [+son] na sifa ya uziada kwa fonimu hii ni [+ghun].





Kanuni ya pili ni ya ujumisho, kanuni hii inahusu sifa ambayo inajumuisha sifa nyingine ndani yake. Hii ina maana kwamba katika ubainishaji wa sifa bainifu kuna sifa moja inayojumuisha sifa nyingine. Sifa inayojumuisha sifa nyingine ndiyo sifa ya uwekevu na zile zenye kujumuishwa ndani ya sifa hiyo ni sifa za uziada.


Mifano na: 6

a) [m] b) [u]


[+naz ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun]


[+kons ] [+son ]


Katika mifano hiyo hapo juu kuna sifa za uziada na uwekevu kama hivi; mfano a), sauti


ina sifa ya uwekevu ya [+naz] wakati sifa za [+ghun] na [+kons] ni za uziada kwa sababu ikitajwa sifa ya [+naz] inajumuisha sifa tajwa hapo juu za [+ghun] na [+kons]. Katika mfano b) wenye sauti [u] ambayo ina sifa ya uwekevu ya [+sil] ambayo inajumuisha sifa za uziada za [+son] na [+ghun]. Kwa sababu ukitaja sifa ya [+sil] ni lazima kitamkwa hicho kitakuwa na sifa ya [+son] na [+ghun].

 







85

 


Kanuni ya tatu ni ya mantiki, hii ni kanuni ambayo inahusu uelewa wa mzungumzaji au msikilizaji au msomaji au mwandishi. Uelewa huu ndiyo unamwezesha mtu kujua hii ni sifa ya uwekevu na nyingine ni ya uziada.


Mifano na: 7


[ +mad ] [-naz ] [+ghun ]


Katika mfano huu mtumia lugha atajua kitamkwa au fonimu inayohusika hapa ina sifa ya uwekevu ya [+mad] na haina sifa ya unazali [-naz] na pia ina sifa ya [+ghun] ambazo ni za uziada kwa kitamkwa hiki ambacho ni [r].


b) [+sil ]


[+son ]

[+nyum ]


[+juu ]

[-kons ]


[-chin ]


Katika mfano huu kitamkwa ambacho kinazungumzwa hapo kina sifa za uwekevu za [+sil], [+nyum] na [+juu]. Hii ni kwa sababu sifa ya [+sil] inaitofautisha sauti hii na sauti nyingine ambazo ni konsonanti, sifa ya [+nyum] inaitofautisha na irabu zinazotamkiwa sehemu ya mbele na kati ya ulimi na sifa ya [+juu] inaitofautisha sauti hiyo na irabu zinazotamkiwa katika mwinuko wa chini na kati. Sambamba na hilo sauti hii ina sifa za uziada za [+son] kwa sababu sifa hii inajumuishwa ndani ya sifa ya [+sil] lakini pia ina sifa [-kons] ya uziada ambayo inatabirika kutokuwepo kwa sababu ya uwepo wa sifa ya [+sil].



3: 4 Makundi Asilia ya Kiswahili Sanifu Kutokana na Dhana ya Uwekezaji na Uziada


Dhana ya uwekevu na uziada hutupatia makundi kadhaa asilia ya Kiswahili Sanifu. Ninaposema makundi asilia ya lugha ya Kiswahili Sanifu ni makundi ya konsonanti, irabu pamoja na viyeyusho. Kupitia mchakato huu kuna sauti zote hubainishwa sifa zake kama itakavyoelezwa hapa chini.


Kundi la kwanza ni la vipasuo, hili ni kundi asilia la fonimu za lugha ya Kiswahili Sanifu ambalo lina sifa msingi ya uwekevu moja. Fonimu hizi zinachangia sifa ya uwekevu ya msingi ya [-kont], kwa maana kwamba fonimu hizi hazina hali ya ukontinuanti wakati wa utamkaji wake. Kundi hili lina jumla ya sauti kumi na mbili (12), vipasuo 9 na vizuio /vipasuo kwamizi 3.

 










86

 

1. [p] 2. [b] 3. [t] 4. [d]

[-kont ] [-kont ] [-kont ] [-kont ]

[-ghun ] [+ghun ] [-ghun ] [+ghun ]

[+ant ] [+ant ] [+ant ] [+ant ]

[+mbel ] [+mbel ] [+mbel ] [+mbel ]

[-kor ] [-kor ] [+kor ] [+kor ]

[+mid ] [+mid ] [-mid ] [-mid ]

[+kati ] [+kati ] [+juu ] [+juu ]

5. [k] 6. [g] 7.[ph] 8.[th]

[-kont ] [-kont ] [-kont ] [-kont ]

[-ghun ] [+ghun ] [-ghun ] [-ghun ]

[-ant ] [-ant ] [+ant ] [+ant ]

[+juu ] [+juu ] [+kati ] [+juu ]

[-kor ] [-kor ] [-kor ] [+kor ]

[+nyum ] [+nyum ] [+mbel ] [+mbel ]

[-mpum ] [-mpum ] [+mpum ] [+mpum ]

9. [kh] 10.[čh] 11. [č] 12. [ɟ]

[-kont ] [-kont ] [-kont ] [-kont ]

[-ghun ] [-ghun ] [-ghun ] [+ghun ]

[+juu ] [+juu ] [+juu ] [+juu ]

[-kor ] [+kor ] [+kor ] [+kor ]

[+nyum ] [+kat ] [+kat ] [+kat ]

[+mpum ] [+mpum ] [-mpum ] [-mpum ]

[-ant ] [-ant ] [-ant ] [-ant ]



Kundi la pili ni vikwamizi, hili ni kundi asilia ambalo linachangia sifa ya ukontinuanti katika lugha ya Kiswahili Sanifu yaani sifa ya [+kont]. Katika dhana ya uwekevu ya vitamkwa hivi ambayo inavitofautisha na vitamkwa au fonimu nyingine ni ya [+kont]. Hebu chungua vitamkwa hivi hapa chini ambavyo jumla yake viko kumi.


1. [f] 2.[v] 3.[υ] 4. [θ]

[+kont ] [+kont ] [+kont ] [+kont ]

[-ghun ] [+ghun ] [+ghun ] [-ghun ]

[+meno ] [+meno ] [+meno ] [+meno ]

[-kor ] [-kor ] [-kor ] [+kor ]

[+ant ] [+ant ] [+ant ] [+ant ]

[+mbel ] [+mbel ] [+mbel ] [+mbel ]

 











87

 

5. [ð] 6. [s] 7. [z] 8.[š]

[ +kont ] [+kont ] [+kont ] [+kont ]

[+ghun ] [-ghu ] [+ghun ] [-ghun ]

[+meno ] [-meno ] [-meno ] [-meno ]

[+kor ] [+kor ] [+kor ] [+kor ]

[+ant ] [+ant ] [+ant ] [-ant ]

[+mbel ] [+mbel ] [+mbel ] [+kat ]

[+juu ] [+juu ] [+juu ] [+juu ]

9. [ɤ] 10. [h]

[+kont ] [+kont ]

[+ghun ] [-ghun ]

[+juu ] [+chin ]

[+nyum ] [+nyum ]

[-ant ] [- ant ]

[-glot ] [+glot ]



Kundi la tatu ni la ving’ong’o au nazali, kundi hili asilia la vitamkwa au fonimu linachangia sifa ya unazali katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Kwa maneno mengine ni kwamba kundi hili linachangia sifa msingi ya uwekevu ya [+naz]. Sifa hii ina jumla ya vitamkwa vitano ambavyo ni.


1. [m] 2. [ɱ] 3. [n] 4. [ñ]

[+naz ] [+naz ] [+naz ] [+naz ]

[+ant ] [+ant ] [+ant ] [-ant ]

[+sil ] [+ sil ] [+naz ] [-sil ]

[+ghun ] [+ghun ] [+ghun ] [+ghun ]

[+mbel ] [+mbel ] [+mbel ] [+kat ]

[+mid ] [+meno ] [-meno ] [-meno ]

[+kati ] [+kati ] [+juu ] [+juu ]


[ŋ]

[+naz]


[-ant ] [+ghun ]


[-sil]


[+juu ] [+nyum ]


Kundi la nne ni la irabu, hili ni kundi asilia la fonimu za Kiswahili Sanifu ambalo fonimu zake zinachangia sifa moja kuu ya uwekevu ambayo ni ya usilabi. Sifa hii, katika tahajia ya kifonetiki huoneshwa kwa msimbo wa [+sil]. Kundi hili lina jumla ya fonimu tano ambazo ni:

 







88

 

1. [i] 2. [ε] 3. [a] 4. [ɔ]

[+sil ] [+sil ] [+sil ] [+sil ]

[+juu ] [+ kati ] [+ chin ] [+kati ]

[+msamb ] [+utandaz ] [+utandaz ] [+uviring ]

[+mbel ] [+mbel ] [+kat ] [+nyum ]

[+son ] [+son ] [+son ] [+son ]

[+ant ] [+ant ] [-ant ] [-ant ]

5. [u]

[+sil ]

[+juu ]

[+uviring ]

[+nyum ]

[+son ]

[-ant ]


Kundi lingine la tano ni la vilainisho, kundi hili linahusu vitamkwa ama fonimu za aina mbili. Katika kundi hili asilia kuna kitamkwa kimoja kiitwacho kitambaza ambacho utamkaji wake ulimi hutandazwa katika chemba ya kinywa na hewa hutoka nje kupitia pembeni mwa ulimi. Vile vile linahusisha kitamkwa kimadende ambacho hutamkwa kwa kugongagonga ulimi sehemu iliyo baada ya mistari ya ufizi. Vitamkwa vya kundi hili vinachangia sifa msingi ya uwekevu ya usonoranti [+son]. Vitamkwa hivi viko viwili ambavyo ni .


1. [l] 2. [r]

[+son ] [+son ]

[+tamb ] [+mad ]

[+kor ] [+kor ]

[+ghun ]  Hiki ni kitambaza [+ghun ] Hiki ni kimadende.

[+ant ] [+ant ]

[+mbel ] [+mbel ]

[+juu ] [+juu ]


Kundi la sita na la mwisho ni kundi asilia la viyeyusho la Kiswahili Sanifu. Kundi hili vitamkwa vyake vinachangia sifa kuu tatu za uwekevu ambazo ni kutokuwepo kwa sifa ya usilabi, kukosekana au kutokuwepo kwa sifa ya ukonsonanti na kuwepo kwa sifa ya ujuu. Sifa hizi kifonetiki huoneshwa kwa misimbo hii [-sil], [-kons] na [+juu]. Vitamkwa vya kundi hili viko viwili (2) ambavyo ni;


1. [w] 2. [y]

[-sil ] [-sil ]

[-kons ] [-kons ]

[+juu ] [+juu ]

[+nyum ] [+kat ]

[+mid ] [-mid ]

[+uviring] [+utandaz]

 




89

 


Kwa ujumla unaweza kugundua kuwa dhana za sifa za uwekevu na dhana ya uziada hutusaidia kupata makundi sita hayo hapo juu kama inavyoonekana katika kila safu ya vitamkwa. Kila kundi lina sifa za uwekevu na za uziada. Katika mchakato wa upambanuzi wa sifa bainifu za fonimu za Kiswahili Sanifu utagundua kuwa kundi lina sifa ambayo au ambazo zinajitokeza kwa kila fonimu ya kundi husika. Sifa hizo ndizo ziitwazo sifa za msingi za uwekevu au sifa wekevu msingi.


Sifa ya uwekevu inaweza kujitokeza katika alama ya kujumlisha zaidi kama ilivyo katika kundi la pili, sifa ya [+kont], kundi la tatu lenye sifa ya [+naz], kundi la nne lenye sifa [+sil] na kundi la lenye sifa ya [+son]. Sifa hizo nilizozitaja ni sifa wekevu msingi za makundi hayo. Kupitia makundi hayo pia umegundua kuwa sifa za uwekevu zinaweza kutambulishwa kwa alama ya kutoa kama nilivyosema hapo awali. Hili linadhihirika katika kundi la kwanza lenye sifa wekevu ya [-kont], na kundi la sita lenye sifa ya [-sil] na [-kons].


Kinachotakiwa ni kuzingatia sifa msingi za kila kundi zinazotofautisha makundi hayo pamoja na sifa zile zinazotofautisha fonimu moja na nyingine ambazo ni za kundi moja. Kwa sababu dhana ya uwekevu na uziada hutazamwa na kushughulikiwa katika kiwango cha makundi ya vitamkwa kwa ujumla, lakini pia katika vitamkwa vya kundi moja kwa vipi vinatofautiana na kwa vipi vinachangia baadhi ya sifa. Kutokana na misingi hiyo utaweza kugundua sifa za uwekevu na sifa za uziada za vitamkwa husika.Tunaposhughulikia vitamkwa au fonimu za kundi moja tunachoangalia ni zile sifa zinazozitofautisha fonimu hizo. Kwa mfano sifa za uwekevu za kundi la kwanza ni [+ghun], [-ghun] na [+mpum].


Mifano na: 8 [th]

[p] [b]

[-ghun ] [+ghun ] [-ghun ]

[+mid ] [+mid ] [-mid ]

[-mpum] [-mpum ] [+mpum].



6:4 Dhima ya Sifa Bainifu za Fonimu / Vitamkwa


Swali tunalojiuliza tulio wengi akilini mwetu ni hili; Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kuzijua sifa bainifu za fonimu? Je zina umuhimu wowote kwa mwanaisimu wa lugha anapochunguza fonimu za lugha fulani maalum? Kwa hakika maswali haya ni ya msingi kabisa katika kuyapatia majibu yake. Kimsingi ni muhimu au ni lazima kuzijua sifa hizi bainifu za vitamkwa kwa mwanaisimu na mtumia lugha pia kwa ajili ya kuzipambanua fonimu hizo. Lakini pia sifa hizi zina umuhimu sana katika utambuzi wa fonimu mbalimbali na inatumikaje katika lugha fulani maalum. Sifa hizi bainifu za fonimu zina dhima zifuatazo:


Sifa bainifu za vitamkwa zina dhima ya kupambanua fonimu, hii ni kazi ya msingi ya sifa bainifu kwamba husaidia kupambanua fonimu za lugha maalum kupitia njia mbalimbali za jozi sahili, ufanano wa kifonetiki, mpishano huru, mgawo kamilishi na kadhalika. Sifa hizi hutuwezesha kujua idadi ya fonimu katika lugha fulani maalum. Mtumia lugha au mwanaisimu wa lugha anaweza kujua lugha yake ina fonimu kadhaa mfano lugha ya Kiswahili ina fonimu 36, konsonanti 29, viyeyusho 2 na irabu 5.

 




90

 


Sifa bainifu za vitamkwa zina dhima nyingine ya kuonesha tofauti kati ya fonimu moja na nyingine za lugha moja maalum. Hutofautisha fonimu mbili au zaidi. Hii humsaidia mtumia lugha kujua ni kwa vipi fonimu hizo zinatofautiana.


Mfano na: 9

[b] [p] [m]

[+kons ] [+kons ] [+kons ]

[+ghun ] [-ghun ] [+ghun ]

[+ant ] [+ant ] [+ant ]

[+mbel ] [+mbel ] [+mbel ]

[-kont ] [-kont ] [+naz ]


Sifa bainifu hizo hapo juu zina dhima ya kutofautisha vitamkwa [b], [p] na [m]. Sifa ya ughuna inaitofautisha sauti [b] yenye ughuna na sauti [p] isiyo na sifa ya ughuna. Vile vile sifa ya unazali inaitofautisha sauti [m] yenye sifa ya unazali na sauti [p] na [b] ambazo ni vipasuo au fonimu zisizo na sifa ya ukontinuanti.


Sifa bainifu za fonimu zina dhima ya tatu ambayo ni kutusaidia kuzigawa fonimu katika makundi asilia ya fonimu. Kutokana na sifa bainifu tumezigawa fonimu katika makundi sita ambayo ni vipasuo, vikwamizi, ving’ong’o, irabu, vilainisho pamoja na viyeyusho kama ilivyoelezwa katika 6:3:4.


Sifa bainifu za vitamkwa hurahisisha uandishi wa kanuni ambazo hutumika katika kutaja fonimu husika kwa ufasaha. Kupitia njia ya jozi sahili, mpishano huru, mgawo kamilishi, pamoja na kanuni kama vile usilimisho, tangamano la irabu, ughunishaji, ukakaishaji, unazalishaji pamoja na mvutano wa irabu.


Sifa bainifu za vitamkwa huonesha mwenendo au tabia ya lugha fulani kwa sababu baadhi ya fonimu hubadilika kulingana na mazingira au muktadha. Dhima hii ya tano hupatikana kupitia mbinu ya mgawo kamilishi. Kwa maneno mengine ni kwamba kutokana na sifa bainifu za vitamkwa tunaweza kupata alofoni zinazogawana mazingira na wakati huo huo zikiwakilisha fonimu moja. Pamoja na hayo pia fonimu zinagawana mazingira ya utokeaji wake. Mfano fonimu [ŋ] katika lugha ya Kiingereza haitokei mwanzoni mwa neno na fonimu [h] haitokei mwishoni mwa neno. Katika lugha ya Kiswahili Sanifu sauti [m] yenye sifa ya [+naz], [+sil] hutokea katika muktadha ambamo silabi au mofimu inayoifuata inaanza na konsonati.


Mfano na: 10

Mofimu matamshi

a) mu+tu [mtu   ]

b) mu+toto [mtɔtɔ ]


Sifa bainifu hutusaidia kuonesha umbo la ndani la sauti fulani kwamba ina tahajia yake ya kawaida kupitia tahajia ya kifonetiki au sifa za sauti hiyo (kupitia matamshi). Mfano sauti [ɔ] ambayo ni tahajia ya kifonetiki ambayo hutambulisha umbo la ndani la sauti hiyo kuwa ni o.


Kwa ujumla sifa bainifu za vitamkwa ni za msingi kabisa kuzijua kwani zina dhima mbalimbali katika lugha ya binadamu, kwa mtumiaji wa lugha na mwanaisimu anayeshughulikia lugha fulani maalum.

 




91

 



Zoezi


Taja na fafanua aina za vitamkwa vya lugha ya Kiswahili Sanifu.


Kwa mifano dhahiri eleza dhana zifuatazo:


kikwamizi

baada ya ufizi


kimadende

mpumuo


nazali


Eleza sifa pambanuzi za kifonetiki na kifonolojia za irabu tano za Kiswahili Sanifu


Unaelewa nini kuhusu dhana ya uwekevu na uziada katika taaluma ya fonolojia? Fafanua dhana hizo na dhima zake katika kubainisha vitamkwa.


Jadili  makundi asilia ya vitamkwa vya lugha ya Kiswahili Sanifu.

Eleza dhana zifuatazo kwa mifano dhahiri ya sauti.


ukontinuanti

usonoranti


ujuu

mwachio taratibu


ujumuisho

uwili unaopingana


utandazo.






























92

 

SURA YA SABA



7:0 KANUNI ZA KIFONOLOJIA


Katika lugha yoyote ile kuna kanuni maalum zinazoongoza lugha hiyo. Kanuni ni kaida au mwongozo fulani unaoongoza kitu fulani. Katika lugha kanuni ni kaida au taratibu mbalimbali zinazoongoza utokeaji wa sauti mbalimbali katika mazingira tofauti tofauti. Kabla ya kueleza au kuchunguza kanuni hizi ni muhimu kuelewa kuwa zipo kanuni zinazoongoza lugha maalum lakini pia kuna baadhi ya maneno ambayo hughairi kanuni hizo. Kwa maneno mengine ni kwamba kanuni hizi hufanya kazi mbalimbali lakini zikiwa na vighairi vyake. Jambo la kuwepo kwa vighairi katika kanuni hizo ni la kawaida kwa lugha zote ulimwenguni. Mbali na kuwa na vighairi vyake bado ni muhimu kueleza kanuni hizi kwa sababu kanuni hizi hutumika kwa kiwango kikubwa sana katika lugha. Kanuni hizi wakati mwingine hujulikana kama michakato ya kanuni za kifonolojia.


Katika kueleza na kuchunguza kanuni hizi nitajikita katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Kupitia kanuni hizi za Kifonolojia Noam Chomsky na Morris Halle katika kitabu chao cha Sound Pattern of English (1968) wanabainisha sehemu kuu mbili ambazo ni umbo la nje linaloonekana kulingana na misingi ya fonolojia, na umbo la ndani ambalo huchunguzwa jinsi neno lilivyojengwa kwa misingi ya mofolojia. Katika utambuzi wa umbo la ndani na umbo la nje kuna kanuni maalum hutumika. Ninaposema umbo la nje nina maana ya jinsi neno linavyotamkwa.


Maumbo haya ni maumbo ambayo hupambanuliwa kwa kutumia kanuni zifuatazo; kanuni ya udondoshaji, kanuni ya usilimisho ambayo inajumuisha uyeyushaji, tangamano la irabu, mvutano wa irabu, unazalishaji, na ughunishaji. Michakato hii au kanuni hizihuonesha uathiriano wa sauti katika lugha. Uathiriano huu hudhihirishwa kupitia mofofonolojia kwa kutumia kanuni hizi. Kanuni hizi zimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni usilimisho na si usilimisho. Kanuni hizi nitazieleza moja baada ya nyingine, kwa kuanza na kanuni zinazoangukia katika kundi la usilimisho na baadaye kanuni zisizo za usilimisho.



7:1 Usilimisho


Huu ni mchakato unaohusu kufanana kwa vitamkwa kwa kiasi fulani au kufanana kabisa, au kukaribiana sana katika sifa fulani kutokana na vitamkwa hivyo kufuatana, ukaribu au mfuatano huo unasababisha vitamkwa hivyo kuathiriana. Ninaposema usilimisho nina maana kwamba kitamkwa kimoja hulazimika kuchukua sifa ya kitamkwa kingine kutokana na kufuatana kwa vitamkwa hivyo. Mchakato huu unajumuisha kanuni za unazalishaji, usilimisho wa nazali, ukakaishaji, ughunishaji, tangamano la irabu, na mvutano wa irabu. Nitazieleza kila moja kwa mawanda yake kama ifuatavyo;

 










93

 


7:1:1 Kanuni ya Unazalishaji


Kanuni ya unazalishaji inahusu sauti ambazo zinaingia katika unazali kwa sababu ya kufuatana na nazali japokuwa sauti hizo si nazali. Usilimisho huu hutokea pale vitamkwa hivi visivyo nazali vinapoandamana au vinapofuatana na sauti nazali. Sauti ambazo huwa katikati ya nazali hulazimika kutamkwa kama sauti nazali. Usilimisho huu unajumuisha usilimisho wa irabu yaani irabu kuathiriwa na nazali, nazali kuathiriwa na konsonanti, nazali kuathiri konsonanti, irabu kuathiri kiyeyusho ambacho hugeuka na kuwa nazali, konsonanti kuathiri irabu ambazo hubadilika na kuwa nazali. Kanuni hii nitaieleza katika vipengele vidogo.



7:1:1:1 Nazali Kuathiri Irabu


Usilimisho wa irabu unatokea pale ambapo sauti irabu inakuwa katikati ya sauti nazali. Irabu yoyote ile kwa asili si nazali lakini inapotanguliwa na nazali na kufuatiwa na sauti nazali nyingine au ikatanguliwa na sauti nazali, irabu hiyo hulazimika kutamkwa kama sauti nazali kupitia chemba ya pua. Kwa njia hiyo irabu hupata sifa ya unazali. Vile vile irabu hupata unazali ama inapotanguliwa na nazali au kufuatiwa na nazali.


Mfano na: 1

Neno matamshi

a) mama [mãma  ]

b) nyinyi [ñĩñĩ ]

c)nanasi [nãnãsi ]

d) nyama [ñãma ]

e) Mungu [mũŋũ ]


Sauti [ã] sauti [ĩ] na sauti [ũ] ni irabu zilizonazalishwa katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Kanuni hii ya unazali inajitokeza pia katika lugha ya Kiingereza. Hebu chungua mifano ifuatayo;


Mifano na: 2

Neno matamshi

a) pen [pẽn ]

b) men [mẽn ]

c) bin [bĩn ]



7:1:1:2 Nazali Kuathiri Konsonanti


Kanuni hii inahusu baadhi ya sauti konsonanti kuathiriwa na sauti nazali [n] inapotokea sauti hizo zinaiandamia nazali hiyo. Kwa maneno mengine sauti hizo zinapokaribiana moja kwa moja na sauti nazali [n] huathiriwa nayo. Sauti hizo zinazoathiriwa na nazali

ni kitambaza [l] na kimadende [r] ambazo hubadilika na kuwa kipasuo [d] pale sauti




94

 


hizi zinapotoka katika maneno yaliyo katika umoja na kuingia katika wingi. Katika umoja sauti [l] na [r] husimama kama zilivyo lakini katika wingi sauti hizi hubadilika na kuwa sauti [d].

Tunapoyatazama maneno hayo yanayobeba sauti [l] na [r] katika umoja huwa na sauti


ambayo inasimama kama mofimu ya umoja, lakini maneno hayo yanapoingia katika wingi sauti [n] huhusika na kulazimisha sauti [l] na [r] kubadilika na kuwa sauti [d]. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Kanuni hii kitahajia huwakilishwa hivi;   l, r → d / n

Mifano na: 3

Umoja wingi

Mofimu matamshi mofimu matamshi

1) u+refu [urɛfu ] n+refu [ndɛfu] ndefu

2) u+limi [ulimi ] n+limi [ndimi] ndimi



7:1:1:3 Konsonanti Kuathiri Nazali


Mchakato huu unahusu nazali hususani iliyoko katika ngeli ya 9 ambayo hujitokeza katika maumbo haya [m], [ɱ], [n], [ñ] na [ŋ]. Kanuni hii inahusu namna nazali hii inavyoathiriwa pale nazali hii inapoandamana na konsonanti hizo husababishwa itamkiwe mahali ambapo konsonati hizo hutamkiwa. Hii ni kwamba sauti nazali hizo huathiriwa mahali pa matamshi. Mfano konsonanti ya midomo husababisha nazali inayoandamana nayo iwe ni ya midomo, au itamkiwe kwenye midomo kwa kubana midomo na kuachia hewa ghafula kama kwamba unatamka kipasuo.


Kanuni ya jumla  N → [∞ mahali] au [-kont ]


[+ghun ]

[∞ mahali]


Mifano na:4

1) Kanuni ndogo N → [m] ∕ -b

a) N +boga → mboga  [mbɔga]

b) N +buni → mbuni [mbuni ]

c) N +bali → mbali [mbali ]


Nazali N katika mifano hiyo imebadilika na kuwa [m] katika mazingira ambayo inaandamana au inafuatiwa na konsonati [b] ambayo ni kipasuo.


2) Kanuni ndogo N → [n] / - d


a) N +dizi → ndizi [ndizi ]


b) N +dimu →  ndimu [ndimu]

c) N +dogo → ndogo [ndɔgɔ ]

 



95

 


N katika mifano hiyo imebadilika na kuwa nazali [n] katika mazingira ambayo inafuatiwa au inaandamana na sauti [d] ambayo ni kipasuo

 



3) Kanuni ndogo

 



N → [ŋ] / -g

 


a) N +goma → ngoma b) N +geni → ngeni c) N + gao → ngao

 


[ŋngɔma ]


[ŋngɛni ]

[ŋngaɔ ]

 


N katika mifano hiyo hapo juu imebadilika na kuwa [ŋ] katika mazingira ambayo sauti hii inaandamana na sauti [g] ambayo ni kipasuo.

 


4) Kanuni ndogo

 


N → [ɱ] / -v

 


a) N +vua → mvua [ɱvua ]

 

N +vamizi→  mvamizi [ɱvamizi ]


N +vomero→ mvomero[ɱvɔmɛrɔ]


N katika mifano hiyo hapo juu imebadilika na kuwa nazali [ɱ] katika mazingira ambayo sauti hiyo inafuatiwa na sauti [v] ambayo ni kikwamizi.


Usilimisho wa nazali au kuathiriwa kwa nazali kunatokea pale nazali inapoandamana na vipasuo ghuna pamoja na baadhi ya vikwamizi kama inavyoonesha hapo juu



7:1:1:4 Konsonanti Kuathiri Irabu


Mchakato huu unahusu irabu u ambayo hubadilika na kuwa nazali inapofuatana na konsonanti, hususani maneno hayo yanapotoka katika umoja na kuingia katika wingi. Hebu chungua mifano ifuatayo. Kwa upande mwingine kiufafanuzi ni kwamba katika umoja sauti [u] ndiyo huwakilisha umoja na upande wa wingi nazali N huwakilisha.

 


Kanuni ya jumla

 


U → N / -K au [+sil ]

[+juu ]→N/-K


[+nyum ]

[+uviring]

 


Mifano na:5

1) Kanuni ndogo u → [m] / -b

Umoja wingi

Mofimu matamshi mofimu matamshi

a) u +bale [ubalɛ  ] N+bale → mbale [mbalɛ ]

b) u+bao [ubaɔ ] N+bao → mbao [mbaɔ ]

c) u+bugu [ubugu  ] N+bugu→ mbugu  [mbugu ]




96

 


2) Kanuni ndogo u → [n] / -d

Umoja wingi

Mofimu matamshi mofimu matamshi

a) u +devu [udɛvu ] N+devu  → ndevu  [ndɛvu  ]

3) Kanuni ndogo u → [ŋ] / -g

Umoja wingi

Mofimu matanshi mofimu matamshi

a) u+gowe [ugɔwɛ ] N+gowe → ngowe  [ŋngɔwɛ  ]

b) u+gumbi [ugumbi] N+gumbi→ ngumbi [ŋngumbi ]


Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha dhahiri kwamba irabu u hubadilika na kuwa nazali neno linapoingia kwenye wingi. Irabu u inapoandamana na kipasuo [b] hubadilika na kuwa nazali [m], irabu inapoandamana na kipasuo [d] hubadilika na kuwa nazali [n] na irabu hii inapoandamana na kipasuo [g] hubadilika na kuwa nazali [ŋ].



7:1:1:5 Irabu Kuathiri Kiyeyusho


Mchakato huu unahusu kubadilika kwa kiyeyusho /w/ na kuwa nazali katika mazingira ambayo kinafuatana na irabu. Neno au maneno yanapotoka kwenye umoja na kuingia katika wingi kiyeyusho [w] hubadilika na kuwa nazali. Hebu chunguza mifano ifuatayo:


Kanuni ya jumla w → N / - I au [+mid ]

[-sil ]→N/-I

[-kons ]

Mifano na:6

1) Kanuni ndogo w → [ñ] / - a

Umoja wingi

Mofimu matamshi mofimu matamshi

a) w+araka [waraka ] N+araka  → nyaraka  [ñaraka  ]

2) Kanuni ngogo w → [ñ] / -e

Umoja wingi

Mofimu matamshi mofimu matamshi

a) w+enzo [wɛnzɔ ] N+enzo → nyenzo [ñɛnzɔ ]

b) w+endo [wɛndɔ ] N+endo →nyendo [ñɛndɔ ]










97

 

3) Kanuni ndogo w → [ñ] / -i


Umoja wingi

Mofimu matamshi mofimu matamshi


a) w+imbo [wimbɔ ] N+imbo → nyimbo [ñimbɔ ]


Kutokana na mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa usilimisho wa irabu ni jinsi ya matamshi, usilimisho wa nazali ni wa mahali pa matamshi, usilimisho wa irabu u ni wa mahali pa matamshi. Lakini pia usilimisho wa kiyeyusho [w] ni wa mahali pa matamshi kama inavyoonekana katika mifano iliyopo hapo juu.



7:1:2 Kanuni ya Ukakaishaji


Kanuni hii inahusu sauti ambazo si za kaakaa gumu lakini hulazimika kutamkiwa katika kaakaa gumu kupitia kanuni hii. Mchakato wa kuifanya sauti isiyotamkiwa kwenye kaakaa gumu hutokana na mfuatano wa irabu au hutawaliwa na irabu. Sauti hizi (irabu) katika mchakato wa kutoka katika umbo la ndani kwenda umbo la nje, irabu hizi hupitia mabadiliko ya aina mbili au hatua mbili.


Hatua ya kwanza I → [-kons]


[-sil ] → / -I

[+kat  ]


Hatua ya pili K→ [č] / -y


Kanuni hii ina maana kwamba [y] katika mazingira inamofuatana na irabu, katika mchakato huu huu sauti [k] hubadilika na [č] katika mazingira ambayo inafuatiwa na kiyeyusho [y].


Kanuni ya I → [y] / - I, k → [č] / -y


Mifano na: 7

Umbo la ndani umbo la nje

1) ki+akula kyakula → chakula [čakula ]

2) ki+etu kyetu → chetu [čɛtu ]

3) ki+ao kyao chao [čaɔ ]

4) ki+umba kyumba chumba [čumba  ]

5) ki+imba kyimba chimba  [čimba ]


Katika kanuni hii kuna vighairi au maneno yasiyokubali kanuni hii, maneno hayo hujulikana kama vighairi. Katika Kiswahili Sanifu tuna maneno yenye tabia hiyo kama ifuatavyo:


Mifano na:8

Umbo la ndani umbo la nje

a) ki+azi kiazi  [kiazi  ]

b) ki+mba kimba [kimba ]

 




98

 


Maneno yanayoonekana hapo hapo juu hayakubaliani kabisa na kanuni ya ukakaishaji na hivyo sauti [k] na [i] kubaki kama zilivyo katika umbo la nje. Kwa maneno mengine ni kwamba hakuna mabadiliko yoyote yanayojitokeza kati ya umbo la ndani na umbo la nje.


Si hivyo tu lakini pia kuna maneno mengine ambayo yanakula njama. Kula njama ni pale neno linakuwa na umbo la ndani au mzizi sawa na neno lingine. Maneno hayo huwa na umbo la ndani la mzizi la namna moja lakini umbo la nje au matamshi yake hutofautiana. Hebu chunguza mifano ifuatayo:

 


Mifano na: 9


Umbo la ndani

a) ki+ atu


b) ki+ atu kyatu

 





kiatu →  chatu

 



umbo la nje

[kiatu ]


[čatu ]

 


Neno la b) limepitia mchakato wa ukakaishaji wakati neno la a) halikubaliani na kanuni ya ukakaishaji ijapokuwa mzizi unafanana.



7: 1:3 Kanuni ya Ughunishaji


Ni kanuni inayohusu sauti ambazo si ghuna zinapata sifa ya ughuna zinapoandamana na sauti ghuna au zinapokuwa katikati ya sauti ghuna, aghalabu inapokuwa katikati ya irabu. Kanuni hii inatokana na usilimisho unaotokea katika kisanduku cha nyuzisauti. Kwa maana kwamba sauti ambayo haina mtimbwiliko kwenye nyuzisauti katika utamkaji wake, sauti hiyo hulazimika kutamkwa kwa mtimbwiliko pale inapoanddamana na sauti zenye mtimbwiliko katika kisanduku cha nyuzisauti. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 10

Neno matamshi sauti iliyoghunishwa

1) bapa [bapa ] sauti [p] imeghunishwa

2) bata [bata ] sauti [t] imeghunishwa

3) Lusia [lusia ] sauti [s] imeghunishwa

4) jiko [ɟikɔ ] sauti [k] imeghunishwa

5) lisha [liša ] sauti [š] imeghunishwa


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa sauti [p], [t], [s], [k] na [š] ambazo tahajia zake za kawaida zimeandikwa kwa wino mzito, ni visoghuna lakini kutokana na kuandamana au kutokea katikati ya irabu, sauti hizo zimeghunishwa. Sauti tajwa hapo juu zimekuwa na mtimbwiliko wa nyuzisauti wakati wa utamkaji wake.



7: 1:4 Kanuni ya Tangamano la Irabu


Ni mchakato wa kifonolojia ambao unahusu athari ya irabu moja kwenye irabu nyingine kiasi cha kuzifanya zielekee kufanana kabisa au kwa kiasi fulani katika sifa




99

 


zake za kimatamshi. Hapa ni kwamba irabu fulani hukubali kuandamana na irabu fulani kutokana na mazingira maalum. Tangamano la irabu huchunguzwa katika mofimu za utendea na za utendesha au usababishi, ambapo kupitia mchakato huo tunapata alomofu mbalimbali kutokana na irabu msingi iliyoko kwenye mzizi wa neno. Hebu chungua mifano hapa chini inayodhihirisha kanuni hiyo kwa kutumia umbo la ndani na umbo la nje. Hapa mifano itajikita katika mofimu ya utendea na ya utendesha.


Mifano na:11

a) (i) mofimu ya utendea

umbo la ndani mofimu ya utendea neno umbo la nje

1) lim+i+a -i- limia [limia ]

2) pik+i+a -i- pikia [pikia ]

3) lind+i+a -i- lindia [lindia ]

4) suk+i+a -i- sukia [sukia ]

5) chez+i+a -e- chezea [čɛzɛa ]

6) end+i+a -e- endea [ɛndɛa ]

7) pok+i+a -e- pokea [pɔkɛa ]


Mifano hiyo hapo juu inaonesha kiambishi au mofimu -i- hubakia kama ilivyo pale ambapo irabu msingi iliyoko kwenye mzizi au itokeayo kabla yake ni ama i, a au u. Lakini irabu msingi iliyoko kwenye mzizi wa neno ikiwa ni e au o kiambishi au mofimu ya -i- ya utendea hubadilika na kuwa irabu e. Katika hali hii utagundua kuwa irabu ya mofimu ya utendea hulazimika kufanana na irabu msingi ya mzizi. Athari hii husababisha sauti katika neno kuweza kuathiriana kimatamshi.


a)(ii) mofimu ya utendea

umbo la ndani mofimu ya utendea neno umbo la nje

1) va+li+a -li- valia [valia ]

2) li+li+a -li- lilia [lilia ]

3) fung+li+a -li- fungulia [fungulia ]

4) le+li+a -le- lelea [lɛlɛa ]

5) to+li+a -le- tolea [tɔlɛa ]


Mifano hiyo hapo juu inaonesha kiambishi au mofimu -li- hubakia kama ilivyo pale ambapo mzizi wa neno unaishia na irabu a, i na u au una irabu msingi hizo zikitokea mwishoni mwa mzizi. Lakini kama mzizi unaishia na irabu e au o, mofimu -li- hubadilika na kuwa -le-. Lakini utokeaji wa mofimu hizo hudhibitiwa na irabu msingi zilizoko kwenye mzizi wa neno husika.


b) mofimu ya utendesha

umbo la ndani mofimu ya utendesha neno umbo la nje

1) pik+ish+a -ish- pikisha [pikiša ]

2) ruk+ish+a -ish- rukisha [rukiša ]

3) pang+ish+a -ish- pangisha [pangiša]

4) som+ish+a -esh- somesha [sɔmɛša ]

5) chek+ish+a -esh- chekesha [čɛkɛša ]

 





100

 


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa mofimu -ish- haibadiliki iwapo mzizi wa neno una irabu msingi a, i au u, hubaki kama ilivyo. Lakini kama mzizi una irabu msingi ama e au o, mofimu -ish- hubadilika na kuwa -esh-.





7:1:5 Kanuni ya Muungano wa Irabu


Kanuni ya muungano wa irabu au mvutano wa irabu ni kanuni ambayo kwayo irabu mofimu moja inapokaribiana na irabu ya mofimu nyingine, irabu hizo mbili huungana na kuzaa irabu moja mpya ambayo haifanani na hizo irabu. Kanuni hii hutumika katika baadhi ya maneno. Kanuni hii ya muungano wa irabu hudhihirika katika baadhi ya maneno kama itakavyooneshwa katika mifano itakayofuata hapa chini.


Mifano na: 12

Umbo la ndani umbo la nje

1) wa+izi wezi [wɛzi ]

2) wa+ingi wengi [wɛngi ]

3) ma+ino meno [mɛnɔ ]

4) wa+enzi wenzi [wɛnzi ]

5) pa+ingine pengine [pɛnginɛ ]

6) ma+ingine mengine [mɛnginɛ]


Katika mifano hiyo hapo juu ukichunguza kwa makini utagundua kuwa irabu [+chin],[+kat] ambayo ni [a] na irabu [+juu], [+mbel] ambayo ni [i] huungana na kuunda au kuzaa irabu [ɛ] ambayo ni irabu [+mbel] na [+kati] kama inavyoonekana katika mfano i) hadi vi).


Hata hivyo kanuni hii haifanyi kazi wakati wote, kwa sababu kuna baadhi ya mazingira ambayo kanuni hii hukiukwa. Huu ni ukweli usiopingika kwamba kanuni hii pia ina vighairi ambavyo havikubaliani na kanuni hii japokuwa irabu chini-kat na irabu juu-mbele hufuatana. Ughairi huu hujitokeza pale mofimu inayoiandamia ina mnyumbuliko. Hebu chungua nifano hii.


Mifano na: 13

Umbo la ndani umbo la nje

1) wa+igiz+a+ji waigizaji [waigizaji ]

2) wa+it+e waite [waitɛ ]

3) wa+imb+a+ji waimbaji [waimbaji ]

4) wa+elekez+a+ji waelekezaji [waɛlɛkɛzaji]



7:1:6 Kanuni ya Uyeyushaji


Kanuni ya uyeyushaji inahusu mabadiliko yanayojitokeza katika irabu i na u, fonimu


na [u] hubadilika na kuwa kiyeyusho. Kitamkwa au fonimu irabu [u] hubadilika na kuwa kiyeyusho [w] na hutokea pale ambapo irabu hii inafuatiwa na irabu zisizofanana

 




101

 


nayo. Irabu [i] hubadilika na kuwa kiyeyusho [y] iwapo itafuatiwa na irabu zisizofanana nayo. Uyeyushaji unajitokeza katika mazingira mawili. Hebu chunguza hapa chini.



7:1:6: 1 Uyeyushaji wa Irabu [u]


Uyeyushaji wa irabu [u] unahusu kubadilika kwa irabu u na kuwa kiyeyusho [w] katika mazingira ambayo irabu hii inafuatana na irabu nyingine ambazo hazifanani nayo. Irabu


inapofuatana na irabu hizo katika umbo la neno la ndani, irabu hii hubadilika na kuwa kiyeyusho wakati wa utamkaji ili kurahisisha matamshi umbo la nje la neno.


Kanuni [u] → [w] / - [+sil] (a,e, i na o)


Au [u] → [w] / - I


Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 14

Umbo la ndani umbo la nje

1) mu+ embe mwembe [mwɛmbɛ ]

2) mu+ombezi mwombezi [mwɔmbɛzi ]

3) mu+imbaji mwimbaji [mwimbaji ]

4) mu+alimu mwalimu [mwalimu ]

5) mu+ako mwako [mwakɔ ]

6) mu+ana mwana [mwana ]

7) mu+ingereza Mwingereza [mwingɛrɛza]


Irabu u huweza kubadilika pia na kuwa kiyeyusho [w] katika mazingira ambayo haiandamani au haitanguliwi na sauti nazali [m]. Kwa maneno mengine ni kwamba sauti u inapoanza yenyewe na kufuatiwa na irabu nyingine isipokuwa ikifuatiwa na irabu u, hubadilika na kuwa kiyeyusho. Kanuni hii inadhihirika kama katika mifano ifuatayo;


Mifano na: 15

Umbo la ndani umbo la nje

1) u+end+e wende [wɛndɛ ]

2) u+end+a+ji wendaji [wɛndaji ]

3) u+anda+a+ji wandaaji [wandaaji]

4) u+oko+zi wokozi [wɔkɔzi ]

5) u+imb+a+ji wimbaji [wimbaji ]


Mbali na kwamba kanuni hii inafanya kazi kwa kiasi kikubwa katika lugha lakini bado inakataa katika baadhi ya mazingira fulani. Kwa ujumla ni kwamba kanuni hii ina vighairi vyake, na ughairi hutokea pale irabu u inapofuatiwa na irabu inayofanana nayo


irabu nyuma-juu. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini. Kanuni [u] ≠ - [u]

 







102

 

Mifano na: 16

Umbo la ndani umbo la nje

1) mu+uguzi muuguzi [muuguzi ]

2) mu+ungano muungano [muunganɔ]

3) mu+umba Muumba [muumba ]


Kwa ujumala irabu u huweza kubadilika katika mazingira ambayo inafuatiwa na mofimu ambayo iliyoundwa na irabu isiyofanana nayo. Lakini inapofuatiwa na irabu na mofimu iliyoundwa au inayoanza na irabu inayofanana nayo, yaani irabu [u], irabu u haibadiliki.



7:1:6:2 Uyeyushaji wa Irabu [i]


Ninaposema uyeyushaji wa irabu [i] nina maana ya kwamba irabu hii hubadilika na kuwa kiyeyusho[y] katika mazingira ambayo irabu i inafuatiwa na irabu isiyofanana nayo au mofimu yenye umbo la irabu isiyofanana nayo kiumbo. Katika mchakato huu umbo la nje la irabu hii hubadilika na kuwa kiyeyusho [y] wakati wa utamkaji ili kurahisisha matamshi.


Kanuni [i] → [y] / - [+sil] (a, e,o na u)

Au  [i] → [y] / - I


Hebu chungua kwa makini mifano ifuatayo hapa chini;


Mifano na: 17

Umbo la ndani umbo la nje

1) mi+aka myaka [myaka  ]

2) mi+ongo myongo [myɔngɔ]

3) mi+enge myenge [myɛngɛ]

4) mi+ungu myungu [myungu]


Irabu i huweza pia kubadilika na kuwa kiyeyusho [y] katika tahajia ya kawaida inapotanguliwa na kikwamizi [v] na katika tahajia ya kifonetiki huwa kikwamizi [υ] inapotamkwa ikiwa imeambatana na kikwamizi [v]. Katika mazingira hayo irabu i hubadilika na kuwa na kiyeyusho [y] ambacho kinapoandamiwa na kikwamizi [v] huunda kikwamizi [υ]. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Mifano na: 18

Umbo la ndani umbo la nje.

1) vi+ake vyake [υakɛ ]

2) vi+ote vyote [υɔtɛ ]

3) vi+ungu vyungu [υungu ]

4) vi+etu vyetu [υɛtu ]

5) vi+umba vyumba [υumba ]

6) vi+ao vyao [υaɔ ]

 




103

 


Irabu i huweza kubadilika na kuwa kiyeyusho katika mazingira ambayo haitanguliwi na sauti [m] au [v]. Hii ina maana kwmba katika mazingira ambayo irabu[i] inasimama kama mofimu katika umbo la ndani na kufuatiwa na irabu nyingine isiyofanana nayo ambayo ni mofimu nyingine pia. Mfuatano huu husababisha kuwepo kwa mabadiliko katika irabu i hususani inapokuwa imefuatiwa na irabu zisizofanana nayo. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Mifano na: 19

Umbo la ndani umbo la nje

1) i+etu yetu [yɛtu ]

2) i+ao yao [yaɔ ]

3) i+ote yote [yɔtɛ ]

4) i+ule yule [yulɛ ]

5) i+ai yai [yai ]


Kanuni hii inatumika katika lugha mbalimbali lakini bado ina vighairi vingi kama ilivyo katika kanuni nyingine hususani tulivyoona katika uyeyushaji wa irabu u. Irabu i inapofuatana na irabu inayofanana nayo, irabu hii haibadiliki au hubakia jinsi ilivyo. Kwa maneno mengine, kanuni hii haikubali katika mazingira ambayo irabu i inafuatana na mofimu yenye irabu inayofanana nayo. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Mifano na: 20

Umbo la ndani umbo la nje

1) mi+igo miigo [miigɔ ]

2) mi+iba miiba [miiba ]

3) mi+ili miili [miili ]

4) mi+inuko miinuko [miinukɔ]


Ughairi huu hujitokeza hata pale irabu i inaposimama peke yake kama mofimu bila kutanguliwa na nazali. Irabu hii inaposimama peke yake na kufuatiwa na irabu ana inayofanana nayo au isiyofanana nayo haibadiliki. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Mifano na: 21

Umbo la ndani umbo la nje

1) i+ingie iingie [iingiɛ  ]

2) i+ungue iungue [iunguɛ ]


Katika mifano hiyo yote iliyotolewa inaonesha dhahiri kwamba irabu i ikifuatiwa na irabu inayofanana nayo haibadiliki. Lakini pia katika baadhi ya mazingira haikubali kanuni hiyo ijapokuwa inafuatiwa na irabu isiyofanana nayo kama inavyoonekana katika mfano namba 2. Hali hii inapojitokeza huitwa ughairi au maneno yanayokataa kanuni hizo hujulikana kama vighairi.


Kwa majumuisho ya jumla ya kanuni hii bila kujikita katika ughairi usiofungamana na mfanano wa irabu, naweza kusema kwamba kanuni inasema kuwa; irabu u na i zinapofuatiwa na mofimu yenye umbo la ndani la irabu ni lazima mambo mawili yatazamiwe kutokea.

 




104

 


Iwapo irabu inayofuatiwa na irabu u au i inafanana kabisa na irabu hizo basi irabu u au i hazitabadilika kwa maana ya kubaki kama zilivyo.


Iwapo irabu inayozifuata irabu u na i haifanani nazo kabisa basi irabu hizo hubadilka na kuyeyuka na kupoteza nguvu ya usilabi na kuwa viyeyusho, na katika baadhi ya

mazingira hubakia jinsi zilivyo.


Utokeaji wa jambo la pili hutegemea zaidi jinsi neno linavyotamkwa, mara nyingi likitamkwa taratibu uyeyushaji hautokei lakini kama neno hilo litatamkwa kwa haraka uyeyushaji lazima utatokea.



7:2 Isiyo Usilimisho


Huu ni mchakato unaohusu kanuni moja ya udondoshaji. Mchakato huu hauhusu usilimisho wa vitamkwa bali vitamkwa viwili vinapoandamana vyenye sifa moja ya uwekevu kitamkwa kimoja huondolewa. Kwa misingi hiyo basi tunapozungumzia usiyo usilimisho tunajikita katika dhana ya uondoaji wa baadhi ya sauti wakati wa utamkaji wa sauti hizo.



7:2:1 Kanuni ya Udondoshaji


Kanuni ya udondoshaji ni kanuni ambayo kwayo baadhi ya sauti huondolewa au hudondoshwa wakati wa utamkaji. Kanuni hii hujulikana kama uchopoaji au udondoshaji wa irabu katika taaluma ya mofofonolojia. Labda swali la kujiuliza ni hili; Kwa nini iitwe udondoshaji wa irabu? Hii ni kwa sababu imeonekana zaidi kuwa katika lugha za Kibantu irabu ndizo hudondoshwa katika taaluma ya mofofonolojia. Udondoshaji huu hufanywa ili kurahisisha matamshi katika irabu zilizoandamana. Udondoshaji wa irabu uko zaidi katika makundi haya.



7:2:1:1 (a) Udondoshaji wa rabu [a]


Udondoshaji wa irabu [a] huu hutokea katika mazingira ambayo irabu a hii inaandamana na irabu a nyingine, katika mazingira hayo irabu a moja hudondoshwa ili kurahisisha matamshi. Udondoshaji huu unadhihirika katika lugha ya Kiswahili kupitia maneno mbalimbali kama ifauatavyo:


Kanunia  →Ø / - a

Mifano na: 22

Umbo la ndani umbo la nje

1) wa+angu wangu [wangu ]

2) wa+ake wake [wakɛ ]

3) wa+ako wako [wakɔ ]

4) wa+alimu walimu [walimu ]

5)wa+ana wana [wana ]

 




105

 

7:2:1:1 (b) Udondoshaji wa Irabu [a]


Irabu a huweza kudondoshwa katika mazingira ambayo irabu hii inafuatiwa na irabu e, katika mazingira hayo irabu a hudondoshwa na e ndiyo hubakia wakati wa utamkaji wa maneno hayo. Hebu chungua mifano ifuatayo;


Kanuni a  → Ø /- e

Mifano na:23

Umbo la ndani umbo la nje

1) wa+enyewe wenyewe [wɛñɛwɛ  ]

2) wa+eusi weusi [wɛusi ]

3) wa+ema wema [wɛma ]



7:2:1:2 Udondoshaji wa Irabu [i]


Udondoshaji wa irabu i hutokea katika mazingira ambayo irabu hii inafuatiwa na irabu e. Mazingira haya yanaruhusu irabu i kuondolewa na irabu e kubakia peke yake wakati wa utamkaji wa maneno hayo.


Kanuni  i → Ø / - e

Mifano na: 24

Umbo la ndani umbo la nje

1) zi+etu zetu [zɛtu ]

2) zi+enu zenu [zɛnu ]

3) li+enyewe lenyewe [lɛñɛwɛ ]



7:2:1:3 Udondoshaji wa Irabu [u]


Irabu u pia huweza kudondoshwa katika mazingira ambayo irabu hii inatanguliwa na konsonanti aghalabu nazali [m] na kufuatiwa na mofimu ambayo inaanza na konsonanti. Mazingira haya yanaruhusu konsonanti tangulizi ambayo huwa ni nazali kusimama kama silabi au mofimu na irabu u kuondolewa au kuachwa wakati wa utamkaji wa maneno hayo.


Kanuni   u → Ø / -K-K

Mifano na:25

Umbo la ndani umbo la nje

1) mu+tu mtu [mtu ]

2) mu+toto mtoto [mtɔtɔ ]

3) mu+penzi mpenzi [mpɛnzi ]

4) mu+Kenya Mkenya  [mkɛña ]

 




106

 

5) mu+Tanzania Mtanzania [mtanzania ]

6) mu+nene mnene[mnɛnɛ ]

7) mu+gonjwa mgonjwa [mgɔnjwa ]


Hizi kanuni zilizochunguzwa na kushughulikiwa katika sura hii ni kanuni za msingi kabisa katika lugha mbalimbali za Kibantu na zile za ughaibuni kama Kiingereza. Kama ilivyoelezwa na kuoneshwa dhahiri kwamba kanuni hizi zina vighairi vyake, hilo ni la msingi kulijua kwa sababu si wakati wote kanuni hizi hutumika. Kwa mantiki hiyo mtumia lugha na mwanazuoni atajua mazingira ambayo kanuni hizi hazitumiki kulingana na hulka ya maneno anayoyashughulikia kuwa hayafungamani na kanuni hizo za kifonolojia. Maneno yenye hulka ya namna hiyo yanadhitiwa na mazingira ya kimofolojia.


7:3 Kaida za Uandishi wa Kanuni


Ninaposema kaida za uandishi wa kanuni nina maana ya utaratibu unaotumika katika kuandika kanuni mbalimbali zinazotumika katika lugha. Kanuni zinazoonesha uhusiano baina fonolojia na mofolojia, mofolojia na sintaksia. Ni muhimu kujua alama zinazotumika kuandika au kutambulisha kanuni hizo. Kaida hizi nitazishughulikia kila moja kama ifuatavyo.



7:3:1 Kaida ya [ ]


Kaida hii ya uandishi imejitokeza sana katika uandishi wa kazi mbalimbali za kifonetiki na za kifonolojia. Ukichunguza kwa makini katika kitabu hiki utagundua kuwa alama au kaida hii ya mabano ya mraba imetumika kwa kiasi kikubwa sana. Pengine utajiuliza ni kwa nini mwandishi ametumia kaida hii zaidi katika maandishi yake? Kimsingi kaida hii hutumika kuonesha umbo la nje la sauti pamoja na sifa zake kifonetiki. Ninaposema umbo la nje la sauti nina maana ya kipashio cha kifonetiki kiitwacho foni. Lakini kaida hii huweza kutumika katika kuipambanua sauti inayotumika katika lugha maalum yaani katika taaluma ya fonolojia kama ilivyoitumika katika kazi hii. Hebu chunguza mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na:26

1) Irabu e ina umbo lake la nje ambalo ni [ɛ]


Konsonanti ch ina umbo lake la nje ambalo ni [č]

Konsonanti th ina  umbo lake la nje ambalo ni [θ]


Konsonanti bh ina umbo lake la nje ambalo ni [β]

Konsonanti ph ina umbo lake la nje ambalo ni [ɸ]


Konsonanti dh ina umbo lake la nje ambalo ni [ð]

7) Irabu o ina umbo lake la nje ambalo ni [ɔ]

8) Irabu a ina umbo lake la nje ambalo ni [a]

9) Konsonanti t ina umbo lake la nje ambalo ni [t]

10)Konsonanti g ina umbo lake la nje ambalo ni [g]

 





107

 

7:3:2 Kaida ya / /


Kaida hii ni msingi sana tunapokitazama kitamkwa katika taaluma ya fonolojia ya lugha maalum. Lakini katika uandishi wa kitabu hiki alama hii haijatumika kwa kiasi kikubwa kwa sababu kuu moja kwamba kitamkwa au fonimu ina sifa za kifonolojia na za kifonetiki kwa mantiki hiyo hiyo basi nimetumia kaida ya mabano ya mraba kuonesha sifa za kifonetiki na za kifonolojia za sauti au fonimu husika. Si hivyo tu sifa bainifu za sauti au fonimu za lugha maalum katika fonolojia yoyote ile zinatokana na taaluma ya fonetiki wakati katika taaluma ya fonolojia kinachoangaliwa zaidi ni uamilifu wa fonimu husika. Lakini kaida hii ya alama ya mabano ya mkwaju hutumika katika kuipambanua zaidi fonimu ya lugha maalum kifonolojia. Hebu chungua mifano hii.


Mifano na: 27

pata   na  bata


Katika jozi ya maneno haya kuna fonimu / p / na / b / ambazo zinatofautisha maana za maneno hayo


kamba  na  lamba


Katika jozi hii kuna fonimu / k / na / l / ambazo zinatofautisha maana za maneno hayo


oa  na  ua


Katika jozi hii kuna fonimu / ɔ / na / u / ambazo zinaleta tofauti ya maana za maneno hayo.





7:3:3 Kaida ya ∞


Katika uandishi wa kanuni alama hii ya alfa hutumika ili kuonesha mabadiliko mbalimbali yanayoonesha dhana ya usilimisho wa nazali zinapoathiriwa kimatamshi na vipasuo ghuna. Ni muhimu kutambua kuwa katika kaida hii inaonesha nazali inavyoathiriwa na konsonanti ziitwazo vipasuo ghuna. Alama ya alfa inaonesha mabadiliko yanayotokana na athari ya konsonanti kwa sauti nazali. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Kanuni  N  → [∞ mahali ] [-kont ]

[+ghun ]

[∞ mahali ]

Mifano na:28

1) N+boga  / → mboga [mbɔga  ]

2) N+dogo  / → ndogo [ndɔgɔ ]

3) N+goma /  → ngoma [ŋngɔma ]

4) N+dege  / → ndege [ndɛgɛ ]

 







108

 

7:3:4 Kaida ya →


Alama ya mshale hutumika sana katika kanuni mbalimbali za kifonolojia. Kazi kuu ya alama hii ni kuonesha kuwa kitamkwa fulani hubadilika na kuwa kitamkwa fulani au kitamkwa fulani huwa kapa. Matumizi ya kaida hii yanadhihirika katika kanuni ya unazalishaji, ukakaishaji, uyeyushaji na udondoshaji. Hebu chunguza mifano hii hapa chini.


Mifano na:29

u → [w] / - Imfano.  mu+alimu → mwalimu


au i → [y] /  - I mfano.  i+etu → yetu

2) u → [m] / - b mfano. ubao → mbao

3) u → Ø  / -K-K mfano. mu+tu → mtu



7: 3:5 Kaida ya Ø


Alama ya kapa inahusika katika uandishi wa kanuni hii ambayo imedhihirika katika mchakato wa udondoshaji ambapo sauti moja huachwa au huondolewa. Alama hii huonesha kuwa sauti moja imeondolewa.


Kanuni ya jumla inasema hivi;


I→  Ø / -K-K au I → Ø / - I


Mifano na:30

zi+etu   →  zetu


mu+ti   →   mti


Hapa irabu i na u zimedondoshwa au zimebadilika na kuwa kapa kwa maana ya kuondolewa katika mazingira yaliyoonehwa hapo juu katika kanuni ya jumla.



7:3:6 Kaida ya K – K


Kaida hii ina maana ya kwamba sauti iko katikati ya konsonanti. Mazingira haya, kwa ujumla yanahusu kanuni ya udondoshaji kama inavyoonekana katika (7:3:5) kwenye mfano wa tatu kwamba;

u → Ø / - K – K au  [+sil ] [+naz ] [-kont  ]


[+juu ]  → Ø / [+mid ]  – [+kons ]

[+nyum] [+sil ] [+ghun]


Mfano na:31


1) mu+tu mtu

2) mu+toto mtoto


mu+Tanzania  →  mtanzania

mu+gonjwa→  mgonjwa

 




109

 


7:3:7 Kaida Nyingine


Kuna kaida nyingi sana katika uandishi wa kanuni, kanuni nyingine nitaziandika kwa kuziorodhesha na kueleza kwa ufupi.

/ ina maana ya katika mazingira ya


$ kaida hii huonesha mpaka wa silabi. Hii itatazamwa zaidi katika sura itakayofuata.

# - kaida hii huonesha  mwanzo wa neno


- # kaida hii huonesha mwisho wa neno

# alama hii huonesha mpaka wa neno. Mfano # kaka # na # dada #.


+ alama hii hutumika kuonesha mpaka wa mofimu

Mfano. a+li+pik+a


7.ǁ ǁ kaida hii inaonesha mofimu.


Kwa ujumla hizo ndizo kaida za msingi zitumikazo kuandika kanuni mbalimbali katika lugha mbalimbali duniani ulimwenguni. Ni muhimu kuzingatia kwamba kaida hizi zinazungumzia uwepo wa kanuni husika lakini pia kuna kanuni nyingine ambayo huonesha ughairi.



7:3:8 Kaida ya Masharti ≠


Kaida hii inahusu maneno ambayo yanakiuka kanuni au yasiyokubali kanuni husika. Kaida hii inapojitokeza inaashiria kuwepo kwa ughairi. Kaida hii inajitokeza katika kanuni ya uyeyushaji na ya ukakaishaji.


Mifano na:32

1) [+sil ] [+sil ]

[+juu ] [+juu ]

[+nyum ] [+nyum ]

Mfano. mu+uguzi [muuguzi ]

2) [+sil ] [+sil ]

[+juu ] [+juu ]

[+mbel ] [+mbel ]

Mfano. mi+igo [miigɔ  ]


Mifano hapo juu inahusu ughairi katika kanuni ya uyeyushaji.


Kwa kuhitimisha sehemu hii au sura hii, ninashauri mtumiaji au msomaji wa kitabu hiki kukumbuka kuwa kaida hizi zinakusaidia kutambua kanuni na vighairi vyake katika lugha maalum unayoishughulikia au unayoichunguza.







110

 

Zoezi


1.Eleza umuhimu wa michakato au kanuni za kifonolojia katika lugha ya Kiswahili Sanifu huku ukitolea mifano hai.


2.Kwa kutumia data ifuatayo tunga kanuni muafaka zinazoakisi mabadiliko ya kifonolojia yanahusu

a)umoja na wingi


umoja wingi

i) ulimi ndimi


ii) waraka nyaraka

iii) ugumbi ngumbi


iv) udevu ndevu

v) ubale mbale


b) (i) mvua


ii) mama

iii)chakula


3.Eleza dhima ya kaida zifuatazo katika lugha.


K – K

[   ]


Ø


$

Toa mifano dhahiri kwa kila kaida.

 
































111

 

SURA YA NANE


8:0 VITAMKWA VIARUDHI (SUPRA SEGMENTAL PHONOLOGY)


Katika sura ya tano nimeeleza vitamkwa vya kawaida kwa ujumla wake. Lakini katika sura hii nitaeleza au nitavichunguza vitamkwa viarudhi. Viarudhi ni vitamkwa vinavyojumuisha dhana ya silabi, utamkaji wa nguvu katika baadhi ya silabi, yaani mkazo au shadda, lafudhi, kiimbo, kidatu, toni na kadhalika. Viarudhi hivi huweza kuchunguzwa katika lugha mbalimbali.


Taaluma ya viarudhi inahusika zaidi na muundo wa vitamkwa hivi pamoja na kazi za vitamkwa hivi wakati wa matamshi au mazungumzo. Vitamkwa hivi vinaitwa viarudhi kwa sababu ni vitamkwa vikubwa zaidi ya fonimu yaani konsonanti, irabu na viyeyusho. Vitamkwa hivi nitavichunguza katika lugha mbalimbali katika sura hii wakati vya Kiswahili Sanifu nitavishugulikia katika sura itayofuata. Nitaeleza kimoja baada ya kingine.



8:1 Silabi


Silabi kama kitamkwa cha kifonolojia kina umuhimu wake mkubwa katika lugha yoyote. Silabi ni kifasili ni kipashio cha neno au ni neno ambacho kina uwezo wa kupokea mkazo au shadda. Silabi inaweza kuwa neno au sehemu ya neno ambayo kutamkwa kwa mkupuo mmoja wa sauti. Kifasili silabi imefasiliwa na wanazuoni mbalimbali kwa namna tofauti tofauti lakini wote wakiwa na dhana ya kuipambanua dhana ya silabi. Wanazuoni hawa wanaifasili hivi.


Maganga, C. (1992) anasema;


“silabi ni kipashio kilicho kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza kutamkika kiurahisi na kwamba huundwa na kitamkwa kimoja au zaidi.”


Hapa Maganga ana maana kwamba silabi ni kipashio kidogo cha kimatamshi ambacho huweza kutambulika kwa urahisi kinapotamkwa katika lugha maalum. Hii ni kwa sababu kitamkwa hiki huweza kupokea mkazo wakati wa utamkaji, lakini pia hutamkwa kama fungu la sauti kwa mkupuo mmoja. Vile vile anaibainisha silabi kuwa huweza kuundwa kwa kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia ambacho ni fonimu, yaweza kuwa moja (yaani irabu peke yake au nazali silabi) au zaidi ya fonimu moja. Kwa mantiki hiyo ni kwamba huweza kuundwa kwa konsonanti na irabu, konsonanti,kiyeyusho na irabu na kadhalika.


Katamba, F (1986) anasema;


“ silabi ni kipashio chenye kiini kimoja chenye usonoranti mkubwa”


Katamba ana maana kwamba silabi yoyote ile ina sauti irabu ndani yake ama imeundwa na irabu yenyewe. Kwa nini Katamba anasema hivyo? Katamba anasema hivyo kwa

 




112

 


sababu sauti yenye usonoranti ina msikiko mkubwa. Vile vile sauti hiyo ndiyo uhai wa silabi husika. Ninasema hivi kwa sababu konsonanti si zote zina usonoranti, japokuwa vilainisho, nazali zenye sifa ya usilabi, nazali pamoja na viyeyusho. Vitamkwa hivi huweza kuunda silabi lakini kwa kuandamana na sauti irabu ambayo ina usonoranti mkubwa zaidi. Ninapozungumzia silabi nina maana ya matamshi pamoja otografia yake.


Massamba D.P.B na Wenzake (2004) wanasema;


“ silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za lugha hutamkwa kwa mara moja kama fungu moja linalojitegemea kimatamshi.”


Wataalam hawa wanaitazama silabi kama fungu la sauti linalojitegemea kimatamshi. Fasili hii inadhihirisha kuwa silabi hutamkwa kwa mkupuo mmoja wa sauti na hivyo silabi kuonekana kama fungu la matamshi. Si hivyo tu wataalam hawa wanaiona silabi kama kipashio kidogo cha kifonolojia, hii haina maana kwamba ni kidogo kuliko fonimu, la hasha! Bali udogo wake ni katika umbo lake katika isimu ya lugha, lakini uamilifu wake ni mkubwa katika taaluma ya isimu ya lugha.


Mgullu, R.S (1999) anasema;


“ silabi ni kipashio cha kifonolojia kilicho kati ya fonimu na neno”


Mgullu anakitazama kitamkwa silabi kuwa kiko kati ya kipashio fonimu na kipashio neno. Hata hivyo silabi inaweza kuwa kubwa kuliko fonimu au ikafanana na fonimu, kwa mantiki kwamba silabi inaweza kuundwa na fonimu moja tu kama inayoundwa na irabu peke yake au nazali yenye sifa ya usilabi peke yake. Vile vile silabi yaweza kuwa ndogo kuliko neno au ikafanana na neno. Mfano silabi $na$, hii ni silabi lakini pia ni aina ya neno ambalo ni kiunganishi kama linavyojitokeza katika tungo hii


Baba na mama.


Kwa ujumla wa fasili hizi tunapata picha kamili kwamba silabi kama kitamkwa kiarudhi kina mambo makuu yafuatayo;


silabi ni kitamkwa kidogo kabisa cha kifonolojia na hutamkwa kwa urahisi huku kikiundwa na sauti moja au zaidi.


silabi ni kipashio chenye kiini kimoja chenye usonoranti mkubwa


silabi ni kipashio cha kifonolojia cha kimatamshi ambacho hutamkwa mara moja kama fungu la sauti


silabi ni kiarudhi kilicho kati ya fonimu na neno.


Kutokana na mambo hayo makuu kuwepo silabi kifasili itafasiliwa kwa mawanda mapana kama hivi:



“ silabi ni kipashio cha kifonolojia ambacho kina kiini kimoja chenye usonoranti mkubwa peke yake au na vitamkwa vingine, kimoja au zaidi ambavyo kwa pamoja hutamkwa kama fungu la sauti mara moja na kwa urahisi.”

 




113

 


Silabi inaweza kuundwa na fonimu peke yake hususani fonimu zenye sifa ya usilabi tu au fonimu zaidi ya moja, kwa sababu hiyo silabi huweza kufanana na fonimu au kipashio kikubwa kuliko fonimu. Vile vile silabi huweza kufanana na neno au kuwa kipashio kidogo kuliko neno.


Silabi huweza kutamkwa kwa mpumuo mmoja wa sauti kwa mara moja tu kama kitita cha sauti. Silabi ni kipashio kinachohusu mfumo au mpangilio maalum wa vitamkwa fonimu vya fonolojia ya lugha maalum. Silabi hupambanuliwa katika taaluma ya fonolojia tukihusianisha na taaluma nyingine katika lugha maalum. Silabi zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni silabi huru na silabi funge.



8:1:1 Aina za Silabi


Silabi katika lugha nyingi za ulimwengu zimegawanyika katika makundi makuu mawili, kundi la kwanza ni la silabi huru ambazo huishia na irabu, sauti ambazo zina usonoranti mkubwa zaidi kuliko konsonanti. Silabi hizi huwa zina usonoranti mkubwa zaidi kwa sababu ya kuishia na irabu, kuundwa na irabu au nazali silabi. Kwa upande wa kundi la pili ambalo ni silabi funge, hizi ni silabi ambazo huishia na konsonanti, sauti ambazo kwa kawaida zina msikiko mdogo au hafifu. Silabi hizi huwa na msikiko mdogo kutokana na kuishia na sauti konsonanti ambazo hazina usonoranti mkubwa sana.



8:1:1:1 Silabi Huru


Silabi huru ni silabi ambazo huishia na sauti irabu. Silabi hizi zina msikiko mkubwa sana kutokana na usonoranti uliomo ndani ya irabu au nazali silabi. Hali hii ya silabi huru kuishia na sauti zenye usonoranti mkubwa zaidi, huifanya silabi hiyo kusikika kwa msikiko mkubwa zaidi na katika baadhi ya lugha silabi hizo hupokea shadda. Ikumbukwe kwamba ninaposema huishia na sauti irabu ni katika matamshi kwa sababu si silabi zote huonekana kuishia na irabu katika tahajia zake. Mfano katika lugha ya Kiingereza, silabi “try” ni silabi ambayo katika matamshi yake huishia na matamshi lakini katika tahajia yake huishia na kiyeyusho. Katika kueleza dhana ya silabi huru nitatumia lugha ya Kiingereza, Kinyakyusa, Kisafwa na Kiswahili. Hebu tuchungue mifano ifuatayo katika lugha hizo nilizozitaja.


Mifano na:1


Lugha ya Kiingereza

i) play $ pleɪ $

ii) no $ nəʊ $

iii) a $ ə $

iv) the $ðɪ$

v) go $ gəʊ $

vi) air $ eə $

vii) boy $ bɔɪ $

viii) try $ traɪ $

 




114

 

ix) buy $ baɪ $

x) toy $ tɔɪ $



Mifano na: 2


Lugha ya Kinyakyusa

i) nu $ nu $

ii) ilopa $ i $ $ lɔ $ $ pa $

iii) ubhumi $ u$ $ βu$ $ mi$

iv) ulutengano $u$ $lu$ $tɛ$ $nga$ $nɔ$

v) ntimi $ n$ $ ti$ $mi$

vi) kyuma $kyu$ $ma$

vii) lughano $lu$ $ɤa$ $nɔ$

viii)syanaloli $sya$ $na$ $lɔ$ $li$

ix) isimbilo $i$ $si$ $mbi$ $lɔ$

x) kyamba $kya$ $mba$



Mifano na: 3


Lugha ya Kisafwa

i) ashila $a$ $ši$ $la$

ii) bhayanga $βa$ $ya$ $nga$

iii) shandabho $ša$ $nda$ $βɔ$

iv) ayinzile $a$ $yi$ $nzi$ $lɛ$

v) minzi $mi$ $nzi$

vi) ifuto $i$ $fu$ $tɔ$

vii) akuga $a$ $ku$ $ga$

viii)ugauli $u$ $ga$ $u$ $li$



Mifano na:4


Lugha ya Kiswahili

i) lakini $la$ $ki$ $ni$

ii) bahari $ba$ $ha$ $ri$

iii) pilipili $pi$ $li$ $pi$ $li$

iv) trekta $trɛ$ $kta$

v) rehani $rɛ$ $ha$ $ni$

vi) ndugu $ndu$ $gu$

vii) mlango $m$ $la$ $ngɔ$

viii)nyumba $ñu$ $mba$

 









maana katika lugha ya Kiswahili

na $na$


damu $da$ $mu$

uzima $u$ $zi$ $ma$


amani $a$ $ma$ $ni$

mchungaji $m$ $ču$ $nga$ $i$


mali $ma$ $li$

upendo $u$ $pɛ$ $ndɔ$


ya kweli $ya$ $kwɛ$ $li$

karamu $ka$ $ra$ $mu$


mlima $m$ $li$ $ma$






maana katika lugha ya Kiswahili

anaenda $a$ $na$ $ɛ$ $nda$

wanaongea $wa$ $na$ $ɔ$ $ngɛ$ $a$


kesho $kɛ$ $šɔ$


amekuja $a$ $mɛ$ $ku$ $ ɟa$

maji $ma$ $ ɟi$

msiba $m$ $si$ $ba$


anaita $a$ $na$ $i$ $ta$


unasemaje $u$ $na$ $sɛ$ $ma$ $ɟɛ$

 


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa katika lugha ya Kiingereza silabi zote ni huru. Vile vile katika lugha ya Kinyakyusa, Kisafwa na Kiswahili. Katika mifano hiyo

 




115

 


hapo juu kuna silabi kama $n$ katika lugha ya Kinyakyusa na $m$ katika lugha ya Kiswahili, ambazo msomaji atajiuliza mbona silabi hizo haziishii na sauti irabu. Lakini kama nilivyotangulia kusema kwamba sauti nazali zina sifa ya usilabi na katika mantiki hiyo basi nazali hizi husimama kama silabi huru. Si hivyo tu nazali hizi zina usonoranti mkubwa. Mbali au sambamba na hilo usilabi wa nazali unatazamwa katika mwathiriano wa vitamkwa. Silabi inayoundwa na sauti nazali peke yake mara nyingi inatokana na nazali hiyo kufuatana na konsonanti au silabi inayoundwa na konsonanti na irabu. Katika mazingira hayo mara nyingi irabu ambayo inaandamana na nazali hiyo hudondoshwa, na nazali husimama kama silabi.


Kwa ujumla nazali [m] na [n] huwa silabi katika lugha za kibantu zilizo nyingi kutokana na kwamba zinapoandamana na konsonanti nyingine zenyewe hutamkwa peke yake kama fungu la sauti na mpumuo wake. Lakini mbali na hayo zina usonoranti wa kutosha.



8:1:1:2 Silabi Funge


Silabi funge ni silabi ambazo huishia na sauti konsonanti, sauti ambazo hazina msikiko mkubwa. Hii inasababisha silabi funge kuwa na msikiko hafifu pia kwa sababu sauti konsonanti hazina usonoranti ijapokuwa kiini chake kina usonoranti, lakini kiini hiki hupungua nguvu yake kutokana na kuwa katikati ya konsonanti au kufuatiwa na konsonanti. Silabi funge hujitokeza zaidi katika lugha ya Kiingereza au lugha za magharibi na Kiswahili, lakini lugha nyingine za Kibantu zinaonekana kutokuwa na silabi funge.


Silabi funge huweza kuundwa na konsonanti, irabu na konsonanti. Kwa maana kwamba silabi hii inakuwa na mwanzo silabi ambao huundwa na sauti konsonanti, kiini silabi ambacho huundwa na sauti irabu na tamati silabi ambayo huundwa na konsonanti. Silabi hizi hujitokeza katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kama nilivyotangulia kusema hapo awali. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Mifano na:5


Lugha ya Kiingereza

i) man $mæn $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

ii) look $ lʊk  $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

iii) pen $ pen $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

iv) street $ strit $ konsonanti tatu mwanzoni na moja mwishoni

v) bag $ bæg $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

vi) pool $ pul $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

vii) like $ laɪk $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

viii)but $ bʌt  $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

ix) love $ lʌv $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

x) grain $greɪn$ konsonanti mbili mwanzoni na moja mwishoni.

 








116

 

Mifano na: 6

Lugha ya Kiswahili

i) halmashauri $ hal $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

ii) daktari $ dak $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

iii) daftari $ daf $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

iv) abdalah $ lah $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

v) ramsa $ ram $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

vi) biblia $ bib $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

vii)  Jehanam $ nam $ konsonsnti moja mwanzoni na moja mwishoni

viii) hosteli $ hɔs $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

ix) mustakabali $ mus  $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni

x) karne $ kar $ konsonanti moja mwanzoni na moja mwishoni



Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa silabi funge zote zimeanza na sauti konsonanti, irabu kisha zikaishia na sauti konsonanti kama inavyoonekana. Tamati silabi umeundwa na konsonanti na mwanzo silabi wake umeundwa na sauti konsonanti.


Silabi funge pia zinaweza kuanza na sauti irabu na kuishia na konsonanti. Silabi funge za namna hii zinapatikana katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili pia. Silabi hizi zina mwanzo silabi kapa, kiini silabi na tamati silabi ambayo ndiyo konsonanti yenyewe. Ifuatayo ni mifano ya silabi hizo.


Mifano na:7


Lugha ya Kiingereza

i) ease $ i:z $ imeishia na konsonanti moja

ii) ark $ ɑ:k $ imeishia na konsonanti moja

iii) and $ ænd$ imeishia na konsonanti mbili

iv) an $ ən $ imeshia na konsonanti moja

Mifano na: 8

Lugha ya Kiswahili

i) alhamisi $ al $ imeshia na konsonanti moja

ii) ankra $ an $ imeishia na konsonanti moja

iii) aprili $ ap $ imeishia na konsonanti moja

iv) ardhi $ ar $ imeishia na konsonanti moja.


Kwa ujumla silabi ni kipashio cha msingi katika kuchunguza mfumo wa lugha fulani maalum. Ni lazima mtumia lugha atambue au azijue silabi huru na silabi funge kwa sababu silabi huru ndizo mara nyingi hupokea mkazo katika lugha nyingi duniani mbali na kwamba hata silabi funge huweza kupokea mkazo katika baadhi ya lugha kama Kiingereza.

 





117

 

8:1:2 Muundo wa Silabi


Silabi kama kipashio kina muundo wa kipekee. Kitahajia huweza kuwakilishwa kwa njia ya matawi, lakini tukijikita katika aina zake kuu mbili. Kimsingi silabi huundwa ama kwa irabu moja, mfano katika lugha nyingi za Kibantu silabi huweza kuundwa kwa irabu peke yake (I), konsonanti + irabu (KI), kiyeyusho+ irabu (kI), konsonanti + konsonanti + irabu (KKI) na kadhalika. Lakini pia lugha nyingi duniani zina muundo wa namna hiyo katika silabi. Hata hivyo kuna baadhi ya lugha ambazo silabi zake kitahajia huweza kuundwa na konsonanti pamoja na viyeyusho lakini katika matamshi yake kuna irabu. Mfano silabi “try” katika lugha ya Kiingereza kitahajia ina konsonanti mbili na kiyeyusho kimoja lakini kimatamshi ina irabu kama hivi $traɪ$. Hivyo basi msomaji wa kitabu hiki asiegamie kutazama tahajia ya silabi bali ajikite katika matamshi, kwa sababu baadhi ya lugha ambazo tahajia ya silabi na matamshi ya silabi ni tofauti.


Muundo wa silabi umeonekana kupitia mabadiliko kadhaa na hivyo kuwagawa wanaisimu katika makundi makuu mawili ambayo ni ya wanamapokeo na wanausasa. Lakini kitu cha msingi hapa cha kukijua ni kwamba wote wanakubali uwepo wa matawi na daraja za silabi. Katika muundo wa silabi kuna mambo makuu yafuatayo;

tawi la kwanza ni la muundo wa silabi yenyewe (syllable).


tawi la pili ni la mwanzo silabi lijulikanalo kama (onsent) pamoja na ukingo silabi (rhyme).


tawi la tatu linazaliwa kutoka kwenye ukingo silabi ambalo hubeba kiini silabi (nucleus) na tamati silabi (coda) kama ipo.


tawi la nne linabeba aina ya vitamkwa yaani konsonanti na irabu.


Hata hivyo ni lazima ikumbukwe kwamba kuna baadhi ya silabi ambazo huundwa na irabu peke yake, silabi za namna hiyo zinakuwa na kiini silabi peke yake.


Katika upande wa darajia za silabi imeonekana kupitia katika mabadiliko kadhaa kama nilivyoeleza hapo awali. Wako wanaodai kuwa silabi ina tia mbili, tia tatu na kadhalika. Upande wa tia za silabi nitazieleza kwa kuwagawa wanaisimu katika makundi mawili kama ifuatavyo.


Upande wa wanamapokeo, wao wanadai kuwa silabi ina tia mbili. Tia ni istilahi inayomaanisha daraja au hatua za kiuchanganuzi za silabi. Kwa maneno mengine ni kwamba wapo wanaisimu wanaosema silabi ina tia au darajia mbili tu. Wataalam hawa ni kama Studdert Kennedy (1967). Kennedy anadai kuwa silabi ina tia mbili, tia ya kwanza ni ya mzizi wa konsonanti na tia ya kiini. Tia ya pili ni ya vitamkwa vyenyewe.


Mifano na:9


Silabi “ba” na “la” zinachanganuliwa kama ifuatavyo:


a)  ba

M K


x x

b a

 










118

 

b) la

M K


x x

l a


M − ni tia ya mzizi wa konsonanti yenye kukazia msukumo wa silabi K − ni tia ya kiini


Mtazamo huu wa kimapokeo una matatizo mengi kwani kiundani ameshindwa kuelezea silabi ambayo zinazoundwa na irabu peke yake, au nazali peke yake pamoja na silabi funge. Ni dhahiri kwamba mtaalam huyu alijikita katika silabi huru peke yake na zenye kuundwa na konsonanti na irabu.


Mtaalam mwingine ni George N. Clements yeye anasema silabi ina tia tatu. George N. Clements anaigawa silabi hivi; kwamba tia ya kwanza ni ya mzizi wa silabi, tia ya pili ni ya konsonanti na irabu na tia ya mwisho au ya tatu ni ya sifa bainifu za vitamkwa. Katika kuchungua hatua za silabi kimuundo Clements anaona kuna hatua tatu au tia tatu. Hebu tuangalie muundo huu katika mifano ifuatayo;


Mifano na:10

a) silabi “na”


………………………………Tia ya kwanza (1)

\


I……………………………Tia ya pili (2)


n a

[+naz  ] [+sil ] ……………………….Tia ya tatu (3)

[+ant ] [+kat ]

[+ghun] [+chin ]

[+juu ] [+ son ]



silabi “nam” katika neno  jehanam


…………………………………….Tia ya kwanza


/ │ \

I   K …………………………………Tia ya pili


│   │

n a m


[+naz ] [+sil]  [+naz ]…………………………Tia ya tatu

[+ghun] [+kat] [+ghun]


[+ant ] [+chin] [+ant  ]

[+kons] [ +son] [+kons]



Silabi inachanganuliwa hivyo kwa misingi ya George N.Clements. Kwa sehemu anakaribia ukweli lakini kwa ujumla silabi haiwezi kutazamwa katika mtazamo wa

 




119

 


Clements peke yake kwa sababu tunapozungumzia tia tuna maana ya ngazi za uchanganuzi wa silabi.


Upande wa wanausasa wao wanaitazama silabi kama kipashio chenye muundo wa kimatawi na tia nne. Hapa tutamwangalia Francis Katamba na Parret Herman. Kabla ya kueleza mawazo ya wataalam hawa nitaeleza kwanza tia za silabi.


Katika muundo wa silabi una vitu vingi kiasi kwamba tia ya kwanza ni mzizi wa silabi yenyewe, mzizi huu hugawanyika katika sehemu mbili. Muundo wa silabi kitia uko hivi;

tia ya kwanza ya mzizi wa silabi yenyewe


tia ya pili ni ya mwanzo silabi na ukingo silabi


mwanzo silabi, hii ni muhimu katika baadhi ya lugha lakini katika lugha nyingine huweza kuwepo au usiwepo kutokana kwamba baadhi ya silabi huundwa na irabu peke yake. Kwa ujumla mwanzo silabi ni konsonanti inayotokea mwanzoni mwa silabi.


ukingo silabi, hujumuisha kiini cha silabi ambayo ni ya lazima katika silabi nyingi za lugha nyingi, na silabi tamati ambayo si lazima sana kuwepo katika katika baadhi ya lugha. Mfano lugha Kiswahili ina tamati silabi kwa silabi funge ambazo ni chache na baadhi ya lugha hazina kabisa mfano lugha za Kibantu.

tia ya tatu ni ya kiini silabi na tamati silabi


kiini silabi, ni sehemu ya silabi ambayo huundwa na sauti irabu na mara nyingi huwa kati ya mwanzo silabi na tamati silabi.


tamati silabi, hii ni konsonanti ambayo hutokea baada ya kiini silabi, hutokea mwishoni mwa silabi.


tia ya nne ni ya konsonanti na irabu


Silabi katika lugha ya Kiingereza huweza kuonesha muundo wake kama ifuatavyo; kwa njia ya matawi na ngoe (tree diagram) kama kielelezo cha muundo wa silabi.


…………………Tia ya kwanza


\

O R …………………Tia ya pili


/  \

N  Ci ……………..Tia ya tatu


│   │

c v ci ……………..Tia ya nne



Ufunguo:


− Tia ya muundo wa silabi au mzizi wa silabi O − Mwanzo silabi (Onsent) tia ya pili


R − Ukingo silabi (Rhyme) tia ya pili

N − Kiini silabi (Nucleus) tia ya tatu


Ci− Tamati silabi (Coda) tia ya tatu

c − Konsonanti Mwanzo  (Onsent) tia ya nne


v − Irabu (Vowel ) tia ya nne

ci − Konsonanti tamati (coda) tia ya nne

 




120

 



Katamba, F (1986)


Mtaalam huyu anaitazama silabi kuwa ina muundo wa tia nne kama kielelezo hapo juu kinavyoonesha, anadai kuwa tia ya kwanza ni ya silabi yenyewe, tia ya pili ni mwanzo silabi na ukingo silabi, tia ya tatu ni ya kiini silabi na tamati silabi na tia ya nne ni ya vitamkwa vilivyoundwa silabi husika. Mfano katika kielelezo hicho hapo juu ni kwamba tia ya nne ina vitamkwa vitatu yaani konsonanti, irabu na konsonanti. Kwa maneno mengine tia hiyo ya nne ina mwanzo silabi, kiini silabi na tamati silabi. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na:11


Lugha ya Kiingereza

Silabi “run”


……………………………….Tia ya kwanza


\

R ……………………………Tia ya pili


/  \

N   Co  …………………….....Tia ya tatu


vc ……………………….Tia ya nne

 


r

 



u

 


n

 





Lugha ya Kiswahili


Silabi “ hal” katika neno halmashauri



………………………………Tia ya kwanza


\

MS US  ………………………….Tia ya pili

/ \

KS TS……………………….Tia ya tatu

K I K ……………………..Tia ya nne

h a l

 





Ufunguo


Lugha ya Kiingereza

σσ − Syllable

 






Lugha ya Kiswahili

σ − Silabi

 




121

 

O − Onsent MS− Mwanzo silabi

R − Rhyme US− Ukingo silabi


N − Nucleus KS− Kiini Silabi

CO− Coda TS− Tamati silabi


C  −  Consonant K  − Konsonanti

V − Vowel I − Irabu


Lugha ya Kinyakyusa


Silabi “nga” katika neno ngatele


…………………………………….Tia ya kwanza

\


MS US  ………………………………Tia ya pili

/ \


│KS ……………………………..Tia ya tatu


KI ………………………………Tia ya nne

n g a





Lugha ya Kisafwa


Silabi “fu” katika neno ifuto


…………………………………..Tia ya kwanza

\


MS US …………………………………Tia ya pili


KS ……………………………….Tia ya tatu



I  …………………………………Tia ya nne

f u


Mifano hiyo hapo juu inadhihirisha wazi kuwa silabi ina matawi na tia kwani vitamkwa vinavyounda silabi husika hupambanuliwa kwa jinsi hiyo kwa mujibu wa wanausasa. Ni vizuri mtumiaji na msomaji wa kitabu hiki kujua mambo yafuatayo: mifano iliyotolewa hapo juu inahusu silabi huru na silabi funge zenye kuundwa na sauti konsonanti na irabu peke yake. Lakini silabi zenye kuundwa na irabu peke yake hazijaoneshwa. Utajiuliza swali kwa nini, lakini mtaalam huyu anaiona silabi ya namna hii haiwezi kuchanganuliwa na kuoneshwa tia zake kama ilivyo katika silabi zenye

 




122

 


kuundwa na konsonanti + irabu. Kwa kumia vigezo vya Katamba silabi ya namna hiyo haiwezi kuchanganuliwa.


Upande wa Parret Herman, yeye anazungumzia uwepo wa silabi za aina mbili ambazo ni silabi nzito na silabi nyepesi. Silabi nzito ni silabi ambazo zina matawi mengi pamoja tia zake. Silabi nzito zinakuwa na ama irabu yenye wakaa mrefu na tamati silabi. Mara nyingi silabi funge ni silabi ziitwazo nzito. Herman anakubaliana na Katamba kuhusu uwepo wa tia za silabi pamoja na matawi isipokuwa yeye anakwenda mbali zaidi kwa kuziona silabi katika makundi mawili ambayo nimeyataja hapo juu.


Hebu chunguza silabi nzito zifuatazo.


Mifano na:12

Lugha ya Kiingereza


Silabi “cat”


………………………………Tia ya kwanza

\


MS US …………………………Tia ya pili

/   \


KS TS ……………………..Tia ya tatu

IK ……………………Tia ya nne.


k æ t



b) silabi “been”


………………………………Tia ya kwanza

\


MS US ………………………….Tia ya pili

/   \


KS TS …………………….Tia ya tatu

K I K  ………………….Tia ya nne

b i n





Silabi za namna hii zinazoishia na konsonanti moja ambazo kwa mujibu wa Herman ni silabi nzito zinapatikana pia katika lugha ya Kiswahili. Silabi za namna hii ziko katika maneno ambayo yamechukuliwa kutoka katika lugha za Kigeni ambayo yameingizwa katika Kiswahili na kutumika kama msamiati wa lugha.

 




123

 



Lugha ya Kiswahili

a)silabi “lum” katika neno maaalum



……………………………Tia ya kwanza

\


/   \


KS TS  ……………………Tia ya tatu

K I K ……………………Tia ya nne

l u m



silabi “dak” katika neno daktari


………………………….Tia ya kwanza


\

MS US ……………………..Tia ya pili

/ \

KS TS …………………..Tia ya tatu

K I K …………………..Tia ya nne

d a k



Silabi ya kwanza inaishia na konsonanti ikiwa na kiini silabi au irabu yenye wakaa mfupi lakini ni imara au ina nguvu katika utamkaji wake. Silabi ya pili ina irabu yenye wakaa mrefu mbali na kuishia na konsonanti. Katika mifano ya silabi za Kiswahili zenyewe zote zina irabu zenye wakaa mrefu na zimeishia na sauti konsonanti. Kwa mantiki hiyo hizi ndizo silabi nzito kwa mujibu wa Parret Herman.


Silabi nzito pia huweza kuundwa na mwanzo silabi, kiini silabi chenye wakaa mfupi lakini ikawa na tamati silabi yenye konsonanti mbili. Silabi za namna hii zinapatikana katika lugha ya Kiingereza kama ifuatavyo;










124

 

Mifano  na: 13

Lugha ya Kiingereza.


a)Silabi “duct” katika neno conduct


……………………………………Tia ya kwanza

\


MS US  ……………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS …………………………..Tia ya tatu

/ \

K I K K  ……………………….Tia ya nne

d ʌ k t






b)silabi “left”


………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………Tia ya pili

/ \

KS TS  ………………………Tia ya tatu

/ \

K I K K  …………………Tia ya nne

l e f t



Upande wa silabi nyepesi, hizi ni silabi ambazo zina wakaa mfupi katika utamkaji wake. Vile vile silabi nyepesi hazina ukingo/ upeo silabi wenye mgawanyiko wa matawi. Silabi nyepesi ni silabi huru yaani zenye kuishia na sauti irabu. Hebu tuchungue mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 14


Lugha ya Kiingereza

Silabi “the” $ðɪ$

 










125

 

………………………………Tia ya kwanza

\


MS US …………………………..Tia ya pili


KS   …………………………Tia ya tatu


K I …………………………..Tia ya nne



ɪ


lugha ya Kiswahili

silabi “ma” katika neno mama


………………………………Tia ya kwanza


\

MS US  …………………………Tia ya pili


KS …………………………Tia ya tatu



K I  ………………………….Tia ya nne


m a


Kutokana na wataalam hawa jinsi walivyoichanganua silabi naweza kusema silabi kama kipashio kina muundo wa kimatawi ambao una hatua nne au tia nne za Kiuchanganuzi. Hatua hizi zijulikanazo kama tia za silabi. Mimi natofautiana kidogo na wataalam hawa kwa kuona uwepo wa tia tano za silabi. Kwa maana kwamba silabi ina hatua tano za kiuchanganuzi. Mchakato huo uko hivi:


tia ya kwanza ni mzizi au muundo wa silabi

tia ya pili ni ya mwanzo silabi na ukingo silabi


tia ya tatu ni ya kiini silabi na tamati silabi (kama ipo)

tia ya nne ni ya aina ya vitamkwa / konsonanti na irabu


tia ya tano ni ya vitamkwa vyenyewe na sifa bainifu zake.



Hebu tuchunguze kwa makini sana mifano ifuatayo hapa chini, kwani ni dhahiri kuwa mtu au mchanganuzi hawezi kuishia tia ya nne bila kuonesha ni konsonanti na irabu gani zilizounda silabi husika.


Mifano na: 15


a) Lugha ya Kiingereza

Silabi “dict” $dɪkt$ katika neno predict

 




126

 


…………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US  ………………………………Tia ya pili

/ \

KS TS  …………………………..Tia ya tatu

/ \

K I K K ………………………Tia ya nne

d ɪ k t  ……………………….Tia ya tano

[+ghun] [+sil ][-ghun ] [-ghun ]

[-kont ] [+mbel][-kont  ] [-kont  ]

[+ant ] [+ juu ][+juu ] [+juu  ]

[+mbel] [+son ][+nyum][+mbel]


Tia ya tano ina vitamkwa vyenyewe na safu ya sifa za vitamkwa hivyo kama inavyoonekana katika ngoe ya silabi. Vitamkwa hivyo vina sifa za uwekevu za [-kont] na [+sil]



Lugha ya Kiswahili

silabi “nga” katika neno nanga


………………………….Tia  ya kwanza


\

MS US …………………….Tia ya pili


/ \

│KS ……………………Tia ya tatu


K K I  …………………….Tia ya nne

n g a ………………Tia ya tano

[+naz ] [-kont ] [+sil ]

[+ant ] [+ghun ] [+chin ]

[+juu ] [+juu ] [+kat ]

[+mbel ] [+nyum ] [+son ]


[+utandaz] [+utandaz] [+utandaz]


Tia ya tano ina vitamkwa vyenyewe ambavyo viko vitatu na sifa bainifu za vitamkwa hivyo, vitamkwa vyenye sifa za uwekevu [+naz], [-kont], na [+sil]




127

 

c) Lugha ya Kinyakyusa

silabi “pya” katika neno ipyana lenye maana ya “upendo”


…………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………….Tia ya pili


/ \

│KS …………………………Tia ya tatu


││

││


K k I  …………………………Tia ya nne

p y a ………………..Tia ya tano

[-kont ] [-sil ] [+sil ]

[+ant ] [-kons ] [+chin ]

[+mid ] [+juu ] [+kat ]

[+uviring] [+utandaz] [+utandaz]

[-kor ] [+kor ] [+kor ]


Tia ya tano inaonesha uwepo wa vitamkwa vitatu pamoja na sifa zake bainifu ambavyo vina sifa za uwekevu za [-kont], [-sil], [-kons] na [+sil]


Lugha ya Kisafwa


silabi “la” katika neno la ashila  lenye maana ya “anaenda”


…………………………….Tia ya kwanza

\


MS US ………………………..Tia ya pili


KS  ……………………….Tia ya tatu


K I  ………………………...Tia ya nne

l a …………………Tia ya tano

[+tamb ]  [+sil ]

[+son ]  [+son ]

[+kor ]  [+chin ]

[+ant ] [+kat ]

[+ghun ]  [+ghun ]


[+utandaz]  [+utandaz ]


Tia ya tano inaonesha ina vitamkwa viwili ambavyo ni [l] na [a] vyenye sifa za uwekevu za [+son], [+tamb] na [+sil]

 




128

 


Kwa ujumla muundo wa silabi tunapoutazama katika kipengele hiki, tunachoangalia zaidi uchanganuzi wa vipashio vinavyounda silabi husika. Utagundua kuwa katika lugha zote silabi zina tia tano pamoja na silabi zinazoundwa na irabu peke yeke. Silabi hizi hazina mwanzo silabi wala tamati silabi. Kwa kawaida huitwa kiini cha silabi kwa maana kwamba mwanzo na kilele au upeo wake hujumuishwa ndani yake. Hata hivyo silabi ya namna hii inachanganuliwa kama silabi nyingine ili kuonesha muundo wake. Uchanganuzi wa silabi ya namna hii uko hivi;


Mfano na: 16

Lugha ya Kiswahili


Silabi “o” katika neno oa


………………………………..Tia ya kwanza (1)

\


MS US ……………………………….Tia ya pili (2)

KS  ……………………………….Tia ya tatu (3)

Ø I  ………………………………...Tia ya nne (4)

Ø ɔ ……………………………Tia ya tano (5)

[+sil ]

[+kati ]

[+nyum ]

[+uviring]

[+son ]


Muundo huu wa silabi zenye kuundwa na irabu peke yake hujitokeza katika lugha nyingi au karibu lugha zote za Kibantu na baadhi ya lugha za magharibi kama Kiingereza. Silabi zote zenye muundo huo huweza kuchanganuliwa kama inavyoonekana hapo juu. Hivyo si kweli kwamba silabi zenye muundo wa namna hiyo haziwezi kuchanganuliwa kimatawi na kuona tia zake.


Kwa ujumla silabi zote zinaweza kuoneshwa katika muundo wake katika njia ya ngoe na tia zake kikamilifu bila kujali ni aina gani ya silabi. Silabi zote zina tia tano kama ilivyooneshwa katika mifano iliyotolewa hapo juu. Msomaji wa kitabu hiki kumbuka kwamba wataalam waliotangulia wanadai kuwepo kwa tia nne za silabi, lakini ni dhahiri kwamba mtu hawezi kuelewa ni kama silabi imebeba vitamkwa gani na vyenye sifa zipi. Ni lazima tia ya tano ieleze vitamkwa vilivyounda silabi husika pamoja na sifa za vitamkwa hivyo. Kwa namna moja au nyingine msomaji wa kitabu hiki atakuwa amepanua dhana ya uchanganuzi wa silabi hizo.

 










129

 

8:2 Kiimbo


Kiimbo katika lugha ya binadamu ni utaratibu maalum wa mpangilio wa mfuatano wa mawimbi ya sauti zake. Kiimbo ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti katika lugha maalum wakati wa usemaji. Kiimbo ni dhana ambayo huaandamana na dhana ya kidatu yaani kiwango cha juu cha sauti, kiwango cha kati cha sauti au kiwango cha chini cha sauti katika usemaji.


Kiimbo ni kule kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti katika lugha maalum wakati wa usemaji, lakini kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti hakuathiri kidatu. Kiimbo kinaweza kuwa cha maelezo, cha kuuliza, cha mshangao, cha kusihi, cha kukejeli au cha amri. Kiimbo huweza kubadilika kulingana na mzungumzaji.



8:3 Kidatu


Swali la kujiuliza ni hili; Je kidatu ni kitu gani katika taaluma ya fonolojia? Lakini kidatu katika lugha ni kitu cha muhimu sana kwa sababu ni moja ya viarudhi katika vitamkwa vyenye kiwango cha juu katika taaluma ya fonolojia. Kidatu ni kiwango cha sauti inayosikika wakati wa utamkaji, chaweza kuwa kiwango cha sauti cha juu, kiwango cha sauti cha katikati au kiwango cha sauti cha chini. Hii ina maana kwamba mtu katika kuzungumza kwake anaweza kupandisha kiwango cha sauti na kuiweka katika kidatu cha juu, au akakishusha kidogo kiwango cha sauti na kuiweka katika kidatu cha kati au akakishusha zaidi na kuiweka sauti katika kidatu cha chini.


Kidatu cha sauti hakiathiriwi na mawimbisauti, kwa maana kwamba kubadilika kwa mawimbi ya sauti hakusababishi kidatu cha sauti kubadilika. Mawimbisauti yanaweza kubadilika lakini kidatu kikabaki vile vile (jinsi kilivyo). Kubadilika kwa kidatu kunatokana na mzungumzaji mwenyewe anavyopenda kuzungumzia jambo analolizungumzia.


Mifano na: 17


Lugha ya Kinyakyusa

a) sokapo (ondoka)


————————————

Kidatu cha juu


————————————


sokapo

—————————————


Kidatu cha kati

—————————————


sokapo


—————————————

Kidatu  cha chini


—————————————

 





130

 


Mifano 17 (a) – (c) inaonesha viwango vya kidatu vya aina tatu; kidatu cha juu, kidatu cha kati na kidatu cha chini katika lugha ya Kinyakyusa. Kidatu huweza kuwakilishwa kwa kumia michoro kama inavyoonekana hapo juu.



8:4 Mkazo


Katika taaluma ya fonolojia dhana ya mkazo huhusu kiwango cha nguvu inayotumika wakati wa utamkaji wa baadhi ya silabi. Mkazo huhusu silabi inayotamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi isiyo na mkazo. Mkazo ni kitu cha muhimu sana katika utamkaji wa maneno katika lugha zinazozingatia matumizi ya mkazo au shadda yaliyo sahihi. Hii ni kwa sababu mkazo huweza kutofautisha kategoria za maneno na maana pia hususani katika maneno ambayo ni tata. Mkazo ukitumiwa na vibaya huweza kuathiri matamshi ya neno au maana ya neno iliyokusudiwa. Hebu tuchungue mifano ifuatayo kutoka katika lugha ya Kiingereza, Kiswahili, Kinyakyusa na Kisafwa. Katika mifano hiyo silabi zitakazopokea mkazo nitaziandika kwa herufi kubwa na mifano hiyo itakuwa katika sehemu mbili ambazo ni A na B.


Mifano na: 18


1. Lugha ya Kiingereza


A B

a) PROduce proDUCE

(zao )  nomino (zalisha)  kitenzi

b) PERmit perMIT

(ruhusa)  nomino (ruhusu)

c) PERfect perFECT

(kamilifu) kivumishi (kuwa kamilifu) kitenzi

d) IMport imPORT

(bidhaa zinazoingizwa) nomino (ingiza bidhaa) kitenzi

e)  CONduct conDUCT

(mwongozo) nomino (ongoza) kitenzi


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua kwamba kubalidilisha mkazo kunaleta tofauti ya maana. Mkazo ukiweka kwenye silabi ya kwanza tunapata maana ambazo ni nomino hususani katika mfano (a), (b),(d) na (e) na kivumishi katika mfano (c). Lakini mkazo ukiwekwa kwenye silabi ya pili tunapata maneno ambayo ni vitenzi, kwa maana yanayozungumzwa ni matendo. Matamshi yaliyoko katika A na B katika lugha ya Kiingereza yote ni sahihi na yanakubalika yote katika lugha hiyo. Kwa sababu mkazo ukiwekwa kwenye silabi ya kwanza tunapata aina ya maneno yaitwayo nomino na kivumishi, wakati mkazo ukiwekwa kwenye silabi ya pili tunapata aina ya maneno yaitwayo vitenzi.

 








131

 


2. Lugha ya Kiswahili

A B

a) ameKUja *aMEkuja

b) ameZIba *aMEziba

c) tunaCHEza *tuNAcheza

d)  baraBAra baRAbara

e) hiviHIvi HIvihivi


Katika mifano 2B kuna alama ya nyota (*) kutoka (a) – (c), alama hii ina maana kwamba usemaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu haukubali kuweka mkazo katika silabi ya pili kutoka kushoto mwa neno. Kwa mantiki hiyo basi maneno yaliyo katika (a) – (c) chini ya sehemu ya B si matamshi sahihi kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu. Lakini matamshi ya mifano iliyoko chini ya A katika (a) – (c) yanakubalika katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Ikumbukwe kwamba kwa kawaida maneno ya lugha ya Kiswahili Sanifu mkazo huwekwa silabi ya pili kutoka mwishoni mwa neno husika. Hata hivyo bado kuna vighairi hususani maneno ambayo yana maana zaidi ya moja na hutofautishwa kwa kutumia mkazo. Kwa maneno mengine maneno ambayo maana zake hutokana na silabi itayopokea mkazo. Hili linathibika katika mifano hiyo hiyo ya Kiswahili Sanifu ambayo iko chini ya A na B katika (d) na (e). Katika (d) chini ya A matamshi yana maana ya njia pana ambayo magari hupita, lakini (d) chini ya B matamshi yana maana ya sawia au murua, katika (e) chini ya A matamshi yake yana maana ya bila sababu wakati


chini ya B matamshi yake yana maana ya kufanana, kutokuwepo kwa badiliko kati ya vitu viwili.


3. Lugha ya Kinyakyusa


A B

a) mbuKIle *MBUkile

(nimeenda)

b) iSIle *Isile

(amekuja)

c) niTIke NItike

(nikubali) (nimekubali)

d) niNGIle NIngile

(niingie) (nimeingia)


Katika mifano hiyo hapo juu utagundua matamshi yaliyoko katika (a) na (b) chini ya B yamewekewa alama ya nyota kuonesha kwamba hayakubaliki katika lugha ya Kinyakyusa lakini yaliyoko chini ya A, hayo ndiyo matamshi sahihi yanayokubalika katika lugha ya Kinyakyusa. Vile vile matamshi yaliyoko katika (c) na (d) chini ya A na B yote yanakubalika lakini maana ya matamshi hayo au maneno hayo ni tofauti kama inavyoonesha katika mifano hiyo na maana za matamshi hayo.







132

 

4. Lugha ya Kisafwa


A B

a) aSHIla *Ashila


(anaenda)

b) bhaYAnga *BHAyanga


(wanaongea)

c) iFUto *Ifuto


(msiba)


Katika mifano hiyo hapo juu umeona kuwa matamshi ya maneno yaliyoko upande wa B yamewekewa alama ya nyota (*) kumaanisha matamshi hayo hayakubaliki katika lugha ya Kisafwa. Lakini matamshi maneno yaliyoko chini ya A ni sahihi na yanakubalika katika lugha ya Kisafwa.


Ni muhimu kujua kuwa katika lugha nyingi za Kibantu zinazotumia mkazo, mkazo huwekwa kwenye silabi ya pili kutoka mwishoni mwa neno kwa kiasi kikubwa. Lakini pia ni vizuri kutambua kuwa kuna lugha ambazo hazitumii mkazo japokuwa ni za Kibantu, lugha za namna hii hutumia toni badala ya mkazo, na kwa mantiki hiyo lugha hizo hazina utaratibu wa mkazo.



8: 5 Lafudhi


Istilahi “lafudhi” ina maana ya sifa ya kimasikizi ya matamshi ya mtu binafsi ambayo humtambulisha msemaji sehemu atokayo kijiografia. Kwa upande mwingine lafudhi hutokana na athari za mazingira ya mtu ya kijamii au kijiografia na lugha mama yake. Lafudhi hutaambuliwa kwa kuoanisha mtu na mazingira aliyomo.


Kwa nini lafudhi huonekana kama utambulisho wa mtu? Nimesema lafudhi huonekana kama utambulisho wa mtu au huweza kumtambulisha mtu kijiografia kwa sababu kwa wazungumzaji wengi ambao ni wa lugha ama ya Kiswahili ama lugha nyingine ni ya pili kwao mara nyingi huathiriwa sana na mazingira yao ya kijiografia na lugha zao za mwanzo au lugha mama zao na jinsi walivyojifunza lugha ya pili kutoka kwa waliowafundisha.


Kwa mfano baadhi ya wasemaji wa lugha ya Kiswahili ni rahisi sana kuwatambua kuwa ni watu wa eneo gani na lugha mama zao ni zipi ijapokuwa wanazungumza Kiswahili. Mzunguzaji huyo anaweza kuwa mwenyeji wa Tanga, mwenyeji wa Mtwara, mwenyeji wa Jamhuri ya Kongo, ni Mmasai, ni Mnyakyusa na kadhalika. Hebu chunguza mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 19


Usiende mbere  ( msemaji atakuwa Mkurya kutoka Mara).

Ngombe anakula mgomba (msemaji atakuwa anatoka Kagera).


Njomba ameleta chamaki (msemaji atakuwa anatoka Mtwara).


Amekuya kutumika fasi ya Waziri Mkuu (msemaji atakuwa anatoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo).


Veve fanya nini hapo? (msemaji atakuwa ni Mhindi).

 




133

 

Wee mitu kabila gani hapana kojoa Mwai Kibaki (msemaji atakuwa ni Mluo).

Kyai hiki kya moto sana  (msemaji atakuwa ni Mnyakyusa kutoka Mbeya).


Nitamyambia baba nikirudi nyumbani (msemaji atakuwa ni Msambaa kutoka Tanga).


Kupitia mifano hiyo hapo juu utagundua kuwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili hushindwa kuzungumza Kiswahili Sanifu, si kwa ujumla wake isipokuwa baadhi yao. Tatizo hili linajitokeza kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza kama lugha yao ya pili au ya tatu, kwani wamekwishaathiriwa na lugha ya Kiswahili Kimatamshi. Kwa mfano asilimia kubwa ya silabi za lugha ya Kiswahili ni silabi huru kwa sababu hiyo basi wazungumzaji hawa hulazimisha silabi funge za Kiingereza kuwa silabi huru. Sambamba na hilo katika lugha ya Kiswahili irabu zote zina wakaa mrefu wakati wa utamkaji wake wakati katika lugha ya Kiingereza kuna irabu zenye wakaa mrefu na mfupi. Wazungumza lugha ya Kiingereza kama lugha ya pili hupata shida ya kutofautisha irabu zenye wakaa mfupi na irabu zenye wakaa mrefu. Hebu chungua mifano ifuatayo;


Mifano na: 20

Lugha ya Kiingereza

Neno matamshi ya Kiingereza matamshi ya Kiswahili

a) but / bʌt / / bati /

b) black / blæk / / blaki /

c) man / mæn / / mani /

d) book / bʊk  / / buku /

e) table / teɪbl / / tɛbɔ /

f) looked / lʊkt / / lukudi /

g) pen / pen / / pɛni /



Kwa ujumla lafudhi mbali na kumtambulisha mtu kijiografia lakini pia huathiri matamshi ya lugha sanifu, kama inavyoonekana kwa baadhi ya wazunguzaji wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiingereza. Wazungumazji hawa wanaziathiri lugha hizo kutokana na kutokuwa na umilisi wa kutosha wa lugha hizo ama inatokana na umilisi wa lugha mama kama ilivyo katika mifano namba 19, hali kadhalika katika mifano namba 20 wazungumzaji wameathiriwa na umilisi wa lugha ya Kiswahili.



8:6 Matamshi


Katika lugha yoyote ile ya ulimwengu hususani yenye mfumo wa sauti zinazotumia hewa itokayo katika mapafu ina matamshi ya sauti hizo. Istilahi “matamshi” lina maana ya sauti zisikikazo wakati wa utamkaji wa maneno yanayotamkwa na mtu fulani. Matamshi yanaweza kuwa mazuri na yenye kujenga na mengine yakawa mabaya na ya kubomoa au kuvunja moyo katika jambo alifanyalo mtu. Kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya kawaida ya neno matamshi linahusu sauti zinazotolewa na binadamu katika

 





134

 


lugha zao. Neno matamshi linatokana na neno “tamka” ambalo maana yake ni kutoa sauti nje ya kinywa au pua ya binadamu wakati wa usemaji au mazungumzo yoyote.


Sauti za lugha za binadamu zina upekee wake kwa sababu zinapotamkwa huleta maana katika mawasiliano ya wanadamu. Kwa sababu hiyo istilahi “matamshi” linaweza kuwa na maana sawa na istilahi “ kauli” kwa maana kwamba huwa na maana fulani katika lugha. Lakini neno matamshi lina maana pana sana kwa mfano likiwa na maana ya kawaida huhusishwa zaidi na mwelekeo hasi. Hivyo neno matamshi kuwa katika taaluma ya lugha lazima litazamwe kwa makini kupitia taaluma ya fonolojia.


Kifonolojia neno matamshi lina maana ya utaratibu utumikao katika utoaji wa sauti ambazo zinajenga maneno ya lugha maalum ya binadamu. Kwa sababu hii dhana ya matamshi inahusu lugha za binadamu peke yake. Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba ninaposema lugha za binadamu ninazungumzia sauti zile tu zitumikazo katika kuunda maneno ya lugha maalum. Sauti kama za vigelegele, chafya, kupiga mluzi, pamoja na kusikitika au kuonea huruma, hizi hazihusiki na dhana ya matamshi. Utaratibu wa matamshi ya sauti za lugha za binadamu huzingatia vitu viwili vya msingi, kwamba ni lazima kuzingatia mahali pa matamshi pa sauti hizo na jinsi ya matamshi ya sauti hizo.


mahali pa matamshi ni kitu cha kwanza kabisa au ni jambo la kwanza ambapo tunaangalia sehemu inayohusika na mkondo wa utamkaji wa sauti mbalimbali ambapo sauti hutamkiwa. Mfano sauti [b] hutamkiwa sehemu ya midomo.


jinsi ya matamshi, hili ni jambo la pili linalozingatiwa, kwa maana kwamba utaratibu wa matamshi huzingatia namna ambavyo sauti fulani hutolewa nje ya kinywa au pua. Mfano sauti [b] hutamkwa kwa kubana mkondohewa kabisa eneo la midomo na kuachilia hewa hiyo ghafula.


Kwa upande wa matamshi katika lugha ya Kiswahili Sanifu nitayaeleza katika sura itakayofuata ya tisa.



8:7 Toni


Katika taaluma ya fonolojia nimesema vitamkwa vinajumuisha vitamkwa vya kawaida na viarudhi. Viarudhi ni vitamkwa ambavyo vinashughulikiwa katika kiwango cha juu. Ndani ya viarudhi kuna toni ambayo katika taaluma ya fonolojia hutazamwa katika kiwango cha silabi. Toni inatumika katika baadhi ya lugha za Kibantu na lugha za magharibi ulimwenguni. Toni inaweza kuwa ya kupanda, kushuka, kupanda – kushuka au kushuka – kupanda au ya katikati.


Toni inaweza kuelezwa kama kiwango cha kupanda ( )kiwango cha kushuka ( ) au kiwango cha kati ( –). Katika maandishi au lugha ya mazungumzo iliyorekodiwa katika maandishi, tofauti za viwango vya toni huoneshwa kwa alama maalum, alama hizo ni ( ) au ( ) au (–) huwekwa na ama juu ya irabu kuu au mwanzoni mwa neno. Katika kueleza dhana hii nitatumia mifano kutoka lugha ya Kiingereza.


Mifano na: 21


a) toni ya kati:  yes au –yes

b) toni ya kushuka: yes au  yes

 




135

 

c) toni ya kupanda: yes au yes


Tofauti ya hizi toni katika usikikaji na utendaji kazi katikaisimu. Iwapo silabi itapokea toni ya kupanda ( ) basi silabi hiyo inahusu kuhakiki au kuchunguza kile kinachosemwa. Vile vile ya kupanda huonesha kinachofuata baada ya kile kilichosemwa.Toni ya kati au ya kawaida (–) hutumika kuweka mipaka ya hali fulani na mara hubeba mawazo au hisia zinazojitokeza mara kwa mara. Mfano kuita majina yaliyo kwenye mlolongo. Kwa upande wa toni ya kushuka ( ) hubeba dhana ya kutoa hitimisho au hukumu ya jambo fulani.


Ikumbukwe kwamba hata aina ya tungo pia huweza kutofautishwa kwa kutumia toni hususani katika lugha zinazotumia toni. Kwa mfano tungo aina ya swali hutumia toni ya kupanda wakati tungo elezi hutumia toni ya kushuka. Chunguza mifano ifuatayo;


a) tungo ulizi: Do you want a chair?


b) tungo elezi/arifu: I want a chair.



Vile vile toni ya kupanda na kushuka zinaweza kuwekwa pamoja ili kujenga ugumu fulani wa kile kilichoelezwa. Zinaweza kujitokeza katika namna hizi; shuka – panda ( ) ambayo huelezea mipaka ya makubaliano ya namna fulani,kueleza mshituko au kutoamini. Panda – shuka toni, hii hubeba mawazo makuu, hisia kuu za kuthibitisha au kushangaa kile kinachosemwa.


a) shuka – panda: possibly au possibly


b) panda – shuka: well ^well


Kwa ujumla toni husaidia kutambua hisia za mtu au mzungumzaji na anchokimaanisha katika usemaji wake.



8:8 Otografia


Nimekwishaeleza sauti za lugha ya binadamu ambazo zinatumika kulingana na uhitaji wa lugha husika. Hii ina maana kwamba sauti ni nyingi kiasi kwamba hakuna lugha yoyote duniani inayoweza kuzitumia sauti zote hizo. Kutokana na kuwepo kwa sauti nyingi kila lugha huchagua sauti zake kutoka katika jedwali la Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa (AKK) na katika Trapeziam ya irabu za kutumia katika kujenga maneno ya lugha hiyo. Sauti katika lugha yoyote ile hutumika kwa mawasiliano ya ana kwa ana, yaani pale ambapo wahusika watakuwa pamoja au kupitia vyombo maalum vya kusikilizia sauti hizo kama vile redio, rekoda, luninga na mawasiliano ya simu.


Sauti hizi kiutaalam huweza kuwekwa katika maandishi, kwa sababu si wakati wote watu watawasiliana kwa njia ya mazungumzo au vyombo vya kusafirisha sauti hizo. Taaluma hii ya kutumia maandishi au alama za michoro ya maandishi kuwakilisha sauti zitumikazo katika usemaji wa lugha hujulikana kama otografia. Taaluma hii inahusu herufi maalum ambazo zilibuniwa ili kuwakilisha sauti hizo za lugha fulani maalum.

 





136

 


Neno otografia lina asili ya lugha Kigiriki lenye maana ya “utaratibu wa kutumia alama au michoro ya maandishi kuwakilisha sauti zisikikazo katika usemaji wa lugha” ( taz. Massamba na Wenzake 2004:12). Kwa kawaida kila lugha ina mfumo wake wa sauti na utaratibu wake wa uundaji wa silabi zake ijapokuwa kuna baadhi ya lugha zinazoshabihiana sana katika kuunda silabi. Hii ni sababu kuu sana ya kuiona kila kuwa na utaratibu wake wa uwakilishaji wa maneno yake kimaandishi na kimatamshi.


Hata hivyo kimaandishi kila lugha huweza kubuni utaratibu wake wa kuwakilisha lugha ya mazungumzo, hii ina maana kwamba wataalam wa lugha husika wana kazi ya kubuni utaratibu huo wa kimaandishi ambao utatumika kama mfumo wa maandishi. Mfumo huo wa maandishi unaweza kuwa alama au michoro. Kutokana na msingi huo ni dhahiri kwamba kila lugha ina otografia yake. Mfano lugha ya Kiswahili ina otografia ambayo ni sawa na matamshi, lakini Kiingereza otografia yake ni tofauti na matamshi. Hebu tuchunguze mifano ifuatayo:


Mifano na:22

Lugha ya Kiingereza


Otografia matamshi

a) try / traɪ /


b) rhythm / rɪðɪm/

c) but / bʌt /


Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha dhahiri kuwepo kwa tofauti kati ya otografia yake na matamshi. Hebu sasa tuangalie upande wa lugha ya Kiswahili.


Lugha ya Kiswahili

Otografia matamshi


a) takwimu / takwimu /

b) pete / pɛtɛ /


c) pilipili / pilipili /


Katika mifano hii ya lugha ya Kiswahili utagundua kuwa otografia na matamshi yake ni yanafanana. Huu ni uthibisho tosha kwamba kila lugha ina otografia yake.


Ikumbukwe kwamba ninapozungumzia otografia nina maana ya tahajia ya lugha au maandishi ya lugha fulani maalum. Ni muhimu kujua kuwa neno otografia, maandishi na tahajia vyote vinamaanisha dhana moja ya utaratibu wa kutumia alama au michoro inayowakilisha sauti za lugha fulani maalum.

 


















137

 

Zoezi


1.Eleza kwa mawanda mapana dhana ya vitamkwa viarudhi.


2.Fafanua kauli ifuatayo;


“silabi ni kipashio cha kifonolojia ambacho kina kiini kimoja chenye usonoranti mkubwa peke yake au na vitamkwa vingine, kimoja au zaidi, ambavyo kwa pamoja hutamkwa kama fungu la sauti kwa mara moja na kwa urahisi.”


Eleza aina kuu za silabi katika lugha ya mbalimbali za binadamu huku ukitumia mifano hai.


4.Onesha muundo wa kila silabi katika maneno yafuatayo kwa kutumia tia na matawi yake.

halmashauri


kichaa

simba


5.“Silabi imepitia mabadiliko mengi kiuchanganuzi.”


Hakiki kauli hii na kutoa hitimisho lake kwa kuzingatia tia za silabi.


Unaelewa nini kuhusu dhana za

kidatu


kiimbo

otografia


toni

matamshi


lafudhi

mkazo

 





























138

 

SURA YA TISA



9:0 VITAMKWA VIARUDHI VYA KISWAHILI SANIFU


Katika sura ya nane nimezungumzia dhana ya vitamkwa viarudhi kwa ujumla wake bila kujikita katika lugha maalum. Kwa maneno mengine ni kwamba nimechunguza vitamkwa viarudhi katika lugha zipatazo nne ambazo ni lugha ya Kiingereza, lugha ya Kinyakyusa lugha ya Kisafwa na lugha ya Kiswahili. Vile vile nilizungumzia vipashio vinavyoshughulikiwa katika taaluma ya viarudhi. Viarudhi ni vitamkwa ambavyo vinajumuisha dhana ya silabi, utamkaji wa nguvu katika baadhi ya silabi yaani mkazo au shadda, lafudhi, kiimbo kidatu, matamshi na kadhalika.


Viarudhi kitaalam tunaangalia zaidi muundo wake na utendaji kazi wake katika lugha wakati wa matamshi. Katika sura hii nitachunguza silabi, kidatu, kiimbo, mkazo na lafudhi jinsi vilivyo na jinsi vinavyotumika katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Hapo awali katika sura ya nane nimeeleza kuwa lugha ina namna ya mpangilio wake katika uundaji wa silabi, namna ya kuweka mkazo, na namna vitamkwa vingine vinvyoweza kutumika katika lugha fulani maalum. Hivyo basi katika sura hii nitashughulikia na kuelezea zaidi vitamkwa hivi katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Kama nilivyofanya katika sura ya nane dhana hizi nitazieleza moja baada ya nyingine.



9:1 Silabi za Kiswahili Sanifu


Katika sura iliyotangulia ya nane (taz.8:1) silabi imefafanuliwa kama


“kipashio cha kifonolojia ambacho kina kiini chenye usonoranti mkubwa ama peke yake au na vitatamkwa vingine, kimoja au zaidi, ambavyo vyote kwa pamoja hutamkwa kama fungu la sauti mara moja na kwa urahisi.”


Hii ina maana kwamba silabi hutamkwa kwa mkupuo mmoja wa sauti, vile vile humaanisha kwamba katika mfumo wa lugha maneno ya lugha fulani maalum hutamkwa kwa kufuata utaratibu wa silabi. Si hivyo tu bali pia kuna sifa maalum za utamkaji huo ambazo zinabainisha kipengele cha silabi na vitamkwa vingine kama ilivyooneshwa katika sura ya nane (taz. 8:1:1 na 8:1:2). Ingawa ni kweli kwamba maneno ya lugha hutamkwa kwa kufuata utaratibu wa silabi, lakini namna ya utamkaji hutofautiana kutoka lugha moja hadi lugha nyingine. Tofauti hii inatokana na wakaa wa utamkaji unaotumika kutamka silabi hizo.


Kwa jinsi fonetiki inavyofanya kazi katika kuchunguza wakaa wa utamkaji wa sauti mbalimbali, imedhihirika wazi kuwa kuna baadhi ya sauti zina wakaa mrefu na nyingine zina wakaa mfupi. Kutokana kwamba sauti hizo zinaunda silabi mbalimbali, basi hata silabi hizo huweza kuwa na ama wakaa mrefu au wakaa mfupi katika baadhi ya lugha. Kuna baadhi ya lugha za ulimwengu ambazo wakaa wa utamkaji wa kila silabi katika neno huathiriwa na mkazo unaofungamana nazo. Namna hizi mbili za wakaa wa utamkaji wa silabi ndio hutofautisha makundi ya lugha ulimwenguni. Kwa mfano lugha za Kiingereza, kijerumani na kadhalika, dhana ya wakaa huhusishwa kasi na wizani (mifuatano inayowiana ya mkazo mkali na uhafifu wa sauti) katika utamkaji na kufanya matamshi ya maneno kati ya lugha za kundi moja kutofautiana. Upande wa lugha zenye

 




139

 


kutumia wakaa wa aina moja kundi hili linajumuisha zaidi lugha za Kibantu, Kiswahili Kikiwemo.


Katika sura ya nane (taz. 8:1:1) nimeeleza kuwa katika lugha nyingi za ulimwengu silabi zimegawanyika katika aina kuu mbili ambazo ni silabi huru na silabi funge. Vile vile katika sura hiyo hiyo nimeeleza kuwa silabi huru ni silabi ambazo mara nyingi huishia na sauti irabu katika utamkaji wake, sauti ambazo zina usonoranti mkubwa zaidi na huzifanya silabi hizo kuwa na msikiko mkubwa zaidi. Upande wa silabi funge nikaeleza kuwa ni silabi ambazo zinaishia na sauti konsonanti ambazo hazina usonoranti au zina usonoranti mdogo, na kwa sababu hiyo silabi funge huwa na msikiko hafifu. Aina hizi za silabi zinapatikana pia katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Kiswahili Sanifu kina aina kuu mbili za silabi ambazo ni silabi huru na silabi funge.



9:1:1 Aina za Silabi za Kiswahili Sanifu


Kama ilivyo kwa lugha nyingine za ulimwengu Kiswahili Sanifu nacho ni lugha ambayo ina aina kuu mbili za silabi yaani silabi huru na na silabi funge. Unaweza kujiuliza labda usilabi huru na usilabi funge uliomo ndani ya silabi za lugha ya Kiswahili Sanifu ni tofauti na ule ulimo ndani ya silabi za lugha nyingine, la hasha, hakuna tofauti yoyote. Kitu cha msingi hapa ni ile tahajia na matamshi ya silabi hizo. Kimsingi silabi za Kiswahili Sanifu tahajia zake na matamshi yake vinafanana, tofauti na lugha nyingi magharibi au ulaya.



9:1:1:1 Silabi Huru za Kiwahili Sanifu


Katika sura ya nane nimeeleza dhana ya silabi huru kwamba ni silabi ambazo huishia na sauti irabu zenye usonoranti mkubwa zaidi. Usonoranti huu wa sauti irabu huzifanya silabi huru kuwa na msikiko mkubwa (taz. 8:1:1:1). Upande wa silabi huru za lugha ya Kiwahili Sanifu, hakuna tofauti inayojitokeza kifasili. Silabi huru za Kiswahili Sanifu ni silabi zote ambazo zinaishia na sauti irabu ama kwa kuundwa na sauti irabu peke yake ambazo zina usonoranti mkubwa sana. Usonoranti huu wa sauti irabu huzifanya silabi huru kuwa na msikiko mkubwa zaidi kimasikizi. Silabi huru zinajumuisha silabi zinazoanza na konsonanti ama moja, mbili, tatu, konsonanti moja kiyeyusho au kiyeyusho na kuishia na sauti irabu, zinazoundwa na irabu tu pamoja na zile zinazoundwa na konsonanti nazali zenye sifa ya usilabi.


Vile vile silabi huru za Kiswahili Sanifu zina sifa ya kuwa na tahajia inayofanana na matamshi ya silabi hizo. Kimsingi mfanano huo wa tahajia na matamshi yake hurahisisha ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu kwa wageni au wasio wazawa wa lugha ya Kiswahili Sanifu.



9:1:1:2 Silabi Funge za Kiswahili Sanifu


Kwa upande wa silabi funge nimeeleza kuwa ni silabi ambazo zinaishia na sauti konsonanti, sauti ambazo hazina usonoranti au zina msikiko hafifu. Kutokana na silabi

 




140

 


hizo kuishia na sauti konsonanti zenye msikiko hafifu , silabi hizo pia huwa na msikiko hafifu (taz.8:1:1:2). Je silabi funge za Kiswahili Sanifu zikoje? Silabi funge za lugha ya Kiswahili Sanifu hazina tofauti na silabi funge za lugha nyingine. Silabi funge hizi za Kiswahili Sanifu pia zinaishia na sauti konsonanti ambazo zina msikiko hafifu, kwa sababu ya kuishia na sauti konsonanti zenye msikiko hafifu silabi hizi pia huwa na msikiko hafifu.


Silabi funge za Kiswahili Sanifu kimsingi si za asili ya Kibantu bali ni za asili ya lugha za Kigeni, kwa maana kwamba silabi funge za Kiswahili Sanifu hujitokeza katika maneno yaliyochukuliwa au yaliyochotwa kutoka katika lugha za Kigeni. Unaweza kujiuliza ni kwa nini mwandishi ametumia neno “yaliyochukuliwa” au “yaliyochotwa” kutoka katika lugha za Kigeni na si yaliyokopwa? Sababu kuu ni kwamba nimeona ni maneno yanayoweza kufaa zaidi kuliko neno yaliyokopwa. Kwa sababu unapokopa kitu ni lazima ukirudishe lakini katika taaluma ya lugha tunapochukua maneno hatukusudii kuyarudisha tena katika lugha chansi bali tunayatumia katika lugha lengwa katika maisha yetu yote kama msamiati wa lugha hiyo. Kwa mantiki hiyo tunayatumia maneno hayo katika lugha yetu ambayo huonekana lugha lengwa, lakini pia huendelea kutumika katika lugha chansi.


Baada ya kuona aina hizi mbili za silabi katika lugha ya Kiswahili Sanifu nafikiri sasa ni wakati mzuri wa kueleza miundo ya silabi katika lugha ya Kiswahili Sanifu kwa kuzingatia aina hizo. Mbali na hilo nitajikita katika asili za silabi hizo. Vile vile nitaeleza kwa kuonesha uchanganuzi wake kama ilivyo katika sura ya nane (taz. 8:2) yaani tia za silabi.



9:2 Miundo ya Silabi Huru za Kiswahili Sanifu


Ninaposema miundo ya silabi huru za Kiswahili Sanifu, ni miundo ya silabi zinazotokana na lugha ya Kiswahili Sanifu yenyewe, maneno ya lugha za Kibantu na za maneno yaliyochukuliwa kutoka katika lugha za Kigeni na kuingizwa katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Katika sehemu hii nitaitazama miundo hiyo kwa kuitolea mifano, uchanganuzi wake kimatawai na tia zake.



9:2:1 Muundo wa Silabi ya Irabu Peke Yake (I)


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna silabi zinazoundwa na irabu peke yake kutokana na irabu tano zinazopatikana katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Irabu hizi kila moja huweza kuunda silabi katika baadhi ya miundo ya maneno mbalimbali ya lugha ya Kiswahili Sanifu. Hebu chunguza mifano ifuatayo:


Mifano na: 1


Otografia matamshi

a) iga $ i $ $ga $


b) andika $ a $ $ ndi $ $ ka $

c) koromeo $ kɔ$ $ rɔ $ $ mɛ $ $ ɔ $


d) embe $ ɛ $ mbɛ $

e) umia $ u $ $ mi $ $a$

 




141

 


Uchangauzi wake kimatawi na tia zake ama hatua za uchanganuzi wa silabi. Katika sura ya nane nimeeleza kuwa silabi ya aina yoyote ile ina tia tano. Vile vile nimeeleza kuwa wataalam wengi wa taaluma ya fonolojia wanaziona silabi zinazoundwa na irabu peke yake haziwezi kuchanganuliwa na kuoneshwa tia zake, lakini utagundua kuwa mimi nimetofautiana nao kidogo kwa kuonesha namna silabi hizo zinavyoweza kuchanganuliwa. Hebu chunguza mifano uchanganuzi wa silabi hizo na tia zake. Silabi za asili ya lugha ya kibantu


$ i $


……………………………………..Tia ya kwanza


\

 

MS


 

US ………...........................................Tia ya pili


 


KS ………………………………….Tia ya tatu



I  …………………………………..Tia ya nne

 


 



 

i   ………………………………...Tia ya tano


[+sil ] [+son ] [+mbel ] [+juu ] [+msamb]


S a $


………………………………………..Tia ya kwanza

\

 


MS

 


US

 


…………………………………Tia ya pili

 

 


 


KS  ……………………………….Tia ya tatu


I   …………………………………Tia ya nne



a   ………………………………..Tia ya tano


[+sil ] [+son ]


[+kat ] [+utandaz] [+chin ]




142

 

c) $ ɔ $


………………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US  …………………………………………..Tia ya pili


KS …………………………………………Tia ya tatu

Ø I   ………………………………………....Tia ya nne

Ø ɔ …………………………………………Tia ya tano

[+sil ]

[+son ]

[+nyum ]

[+kati ]


[+uviring]






d) $ ɛ $


…………………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………………….Tia ya pili


KS ……………………………………………Tia ya tatu



Ø I  …………………………………………….Tia ya nne


ɛ  ……………………………………………Tia ya tano


[+sil]


[+son ] [+mbel ]


[+kati ] [+utandaz]

 














143

 

e) $ u $

………………………………………...Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………………..Tia ya pili


KS  …………………………………..Tia ya  tatu



I   …………………………………...Tia ya nne


u   ……………………………………Tia ya tano


[+sil]


[+son ] [+nyum ]


[+juu ] [+uviring ]



Ukichunguza kwa makini sana uchanganuzi wa silabi hizo utagundua kwamba silabi katika tia ya pili ina sehemu mbili yaani mwanzo silabi (MS) na ukingo silabi (US). Katika tia ya nne na ya tano utaona upande kuwa mwanzo silabi hakuna konsonanti inayounda silabi hiyo na badala yake alama kapa (Ø) imewekwa ili kuonesha kutokuwepo kwa konsonanti katika silabi hiyo. Kwa mantiki hiyo, silabi inayohusika imeundwa na irabu peke yake. Lakini si silabi zenye asili ya maneno ya Kibantu na Kiswahili chenyewe tu, pia kuna aina ya silabi za namna hiyo zinazotoka katika maneno yaliyochotwa kutoka katika lugha za Kigeni kama vile maneno yafuatayo:


a) jamaa  $ ɟa$ $ma$ $a$ la Kiarabu


……………………………………Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………..Tia ya pili


KS ………………………………Tia ya tatu


I ………………………………...Tia ya nne


a   ……………………………...Tia ya tano


[+sil]

[+son]


[+kat]


[+chin ] [+utandaz ]

 







144

 

b) aina

……………………………………Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………….Tia ya pili


KS ………………………………..Tia ya tatu



Ø I  …………………………………Tia ya nne

Ø i  ……………………………….Tia ya tano

[+sil ]

[+son ]

[+juu ]

[+mbel ]

[+msamb ]


Katika mifano hiyo hapo juu utaona dhahiri kabisa kwamba silabi zenye muundo wa irabu peke yake zinajitokeza katika maneno ya asili ya lugha ya Kiswahili Sanifu na yale yaliyochotwa au yaliyochukuliwa kutoka katika lugha za Kigeni na kuingizwa katika lugha ya Kiswahili.



9: 2:2 Muundo wa Silabi wa Konsonanti moja na Irabu moja (KI)


Muundo huu wa silabi katika lugha ya Kiswahili Sanifu umeshamiri sana katika maneno mengi ya lugha hii, yale yote yaliyo ya asili ya lugha ya Kiswahili Sanifu pamoja na yale ya asili ya lugha za Kigeni. Muundo huu umeshamiri sana katika lugha nyingi mno kuliko miundo mingine ya silabi. Aina hii ya silabi yenye muundo huu inakuwa na sauti konsonanti mwanzoni na inafuatiwa na sauti irabu yenye usonoranti mkubwa. Hebu chungua mifano ya muundo huu kama ifuatavyo;


Mifano na: 2


Otografia matamshi

a) ruka $ru$ $ka$


b) meno $mɛ$ $nɔ$

c) tibu $ti$ $bu$


d) vyuma $υu$ $ma$


Katika mifano hiyo hapo juu inaonesha dhahiri muundo wa silabi wa konsonanti moja na irabu moja (KI) katika maumbo mbalimbali ya maneno ya lugha ya Kiswahili. Vile vile nitachanganua mifano hii kwa njia ya ngoe na kuonesha tia zake kama ilivyokuwa katika mifano namba 1.

 







145

 

a) (i) $ru$


………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………...Tia ya pili

KS …………………………………Tia ya tatu

K I …………………………………..Tia ya nne

r u ………………………………..Tia ya tano

[+mad ] [+sil ]

[+son ] [+son ]

[+ghun ] [+juu ]

[+juu ] [+nyum ]

[+mbel ] [+uvirng ]

[+utandz ] [+ghun ]







a)(ii) $ka$


………………………………. Tia ya kwanza

\


MS US ……………………………Tia ya pili

KS …………………………..Tia ya tatu

K I  ……………………………Tia ya nne

k a  ……………………………Tia ya tano

[-kons ]  [+sil ]

[+kons ]  [+son ]

[+juu ]  [+chin ]

[+nyum ]  [+kat ]

[+utandaz]  [+utandaz]

 












146

 

b)(i) $mɛ$

……………………………………Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………Tia ya pili

KS  …………………………….Tia ya tatu

K I  ………………………………Tia ya nne

m ɛ ……………………………Tia ya tano

[+naz ] [+sil ]

[+ghun ] [+son ]

[+ant ] [+mbel ]

[+kat ] [+kat ]

[+kons ] [-kons ]

[+uviring ] [+utandaz]







b)(ii)$nɔ$


……………………………………...Tia ya kwanza

\


MS US ………………………………….Tia ya pili

KS  ……………………………….Tia ya tatu

K I  ………………………………….Tia ya nne

n ɔ ……………………………Tia ya tano

[+naz ] [+sil ]

[+ghun ] [+son ]

[+juu ] [+kat ]

[+kons ] [-kons ]

[+ant ] [-ant ]

[+mbel ] [+nyum ]

[+utandaz  ] [+uviring ]

 










147

 

c)(i) $ti $

………………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………….Tia ya pili

KS  ………………………………….Tia ya tatu

K I …………………………………Tia ya nne

t i ………………………………Tia ya tano

[-kont ] [+sil ]

[+kons ] [+son ]

[-ghun ] [+ghun ]

[+juu ] [+juu ]

[+mbel ] [+mbel ]

[+utandaz ] [+msamb  ]

[+ant ] [+ant ]

[+kor ] [+kor ]






c)(ii) $bu$


………………………………………...Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………………Tia ya pili

KS  …………………………………..Tia ya tatu

K I…………………………………..Tia ya nne

b u …………………………………Tia ya tano

[-kont ] [+sil ]

[+ghun ] [+son ]

[+kons ] [+juu ]

[+kati ] [+nyum ]

[+mbel]   [-kons]

[+uviring ] [+uviring  ]

[+ant ] [-ant ]

[+mid ] [-mid ]

 







148

 

d)(i) $ υu$

………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………...Tia ya pili


KS  ………………………………….Tia ya tatu



K I …………………………………Tia ya nne

υ a …………………………….....Tia ya tano

[+mid ] [+sil ]

[+kont ] [+son ]

[+ghun ] [+ghun ]

[+kat ] [+chin ]

[+mbel ] [+kat ]

[+msamb ] [+utandaz  ]

[+kons ] [-kons ]

[+meno ] [-meno ]





d)(ii) $mi$


………………………………………Tia ya kwanza

\


MS US  …………………………………Tia ya pili

KS  ……………………………….Tia ya tatu

K I ……………………………….Tia ya nne

m a …………………………….Tia ya tano

[+naz ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun ]

[+son ] [+son ]

[+kons ] [-kons ]

[+ant ] [-ant ]

[+mid ] [-mid ]

[+mbel ] [+kat ]

[+kat ] [+chin ]

[+uviring ] [+utandaz ]

 







149

 


Katika mifano hiyo hapo juu pamoja na uchanganuzi wake inadhihirisha muundo kamili wa silabi yenye vipashio vidogo viwili vya kifonolojia ambavyo ni konsonanti moja na irabu moja. Uchanganuzi wake una mwanzo silabi ambayo ni konsonanti pamoja na ukingo silabi ambao una kiini silabi yaani irabu kama inavyoonekana kupitia tia zake.



9:2:3 Muundo wa Silabi wa Kiyeyusho kimoja na Irabu moja (kI)


Katika muundo huu silabi huundwa na fonimu ijulikanayo kama kiyeyusho pamoja na fonimu irabu. Ukiangalia katika sura ya sita kielelezo namba 10 yaani jedwali la sauti za Kiswahili Sanifu linaloonesha jinsi ya matamshi na mahali pa matamshi, utagundua kuwa sauti ziitwazo viyeyusho zimejumuishwa ndani ya jedwali la konsonanti za Kiswahili Sanifu. Sauti hizo ni / w / na / y /, mbali na kwamba sauti hizo zimejumuishwa katika kundi la konsonanti lakini bado kuna ulazima wa kuziangalia sauti hizi kipekee kwa upande wake kama sauti muhimu katika uundaji wa silabi za lugha ya Kiswahili Sanifu. Hebu tuchunguze mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 3

Otografia matamshi

a) wa $wa$

b) ya $ya$


Silabi hizi pia huweza kuchanganuliwa kama ilivyo kwa silabi zinazoundwa na irabu peke yake na zile zinazoundwa na konsonanti moja pamoja na irabu. Angalia hapa chini matawi na tia zake.


a) $wa$

σ …………………………………………Tia ya kwanza

/ \

MS US ……………………………………Tia ya pili

KS  …………………………………Tia ya tatu

k I …………………………………Tia ya nne

w a ……………………………….Tia ya tano

[-kons ] [+sil ]

[-sil ] [+son ]

[+juu ] [+chin ]

[+nyum ] [+kat ]

[+kont ] [+kont ]

[+uviring ] [+utandaz]

 







150

 

b) $ya$

……………………………………...Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………….Tia ya pili

KS  ………………………………Tia ya tatu

k I  ………………………………...Tia ya nne

y a ……………………………..Tia ya tano

[-kons ] [+sil ]

[-sil ] [+son ]

[+juu ] [+chin ]

[+kat ] [+kat ]

[+kont ] [+kont ]

[+utandaz] [+utandaz]



Silabi zenye kuundwa na kiyeyusho na irabu huchanganuliwa kama silabi nyingine zenye kuundwa na konsonati moja na irabu au irabu peke yake. Lakini ikumbukwe kwamba mwanzo silabi wa silabi ya aina hii ni kiyeyusho na ukingo silabi wake huwa na kiini silabi peke yake.



9:2:4 Muundo wa Silabi wa Konsonanti moja Kiyeyusho na Irabu (KkI)


Hapa kinachozungumzwa ni kwamba silabi inaundwa na konsonanti moja, kiyeyusho na irabu. Silabi za namna hii si ngeni katika maumbo mengi ya maneno ya Kiswahili Sanifu, kwa maana kwamba ya asili ya Kiswahili Sanifu na yale yatokanayo na lugha za Kibantu, hebu (taz 6:1:2). Silabi hizi hudhihirika katika mifano ifuatayo.


Mifano na: 4

Otografia matamshi

a) kwa $kwa$

b) pya $pya $ katika neno upya

c) mwa $mwa$  katika neno mwaka

d) mya $mya $ katika neno myaka


Silabi hizi huchanganuliwa kimatawi kama silabi zilizotangulia. Tofauti yake ni matawi kuongezeka upande wa mwanzo silabi ambapo huwa na matawi mawili. Uchanganuzi wake huchanganuliwa hivi:

 








151

 

a) $kwa$

σ …………………………Tia ya kwanza

/ \

MS US ………………………Tia ya pili

/ \

KS …………………….Tia ya tatu

K k I ……………………..Tia ya nne

k w a ……………….Tia ya tano

[+kons ] [-kons ] [+sil ]

[-kont ] [-sil ] [+son ]

[+nyum ]  [+nyum ] [+kat ]

[+juu ] [+juu ] [+chin ]

[-ant ] [+ant ] [-ant ]

[+utandaz ] [+uviring ] [+utandaz]

[-mid ] [+mid ] [-mid ]






b) $pya$


…………………………………Tia ya kwanza

\


MS US ………………………………Tia ya pili

/ \


│KS  ……………………………Tia ya tatu

K k I  …………………………….Tia ya nne

p y a ………………………….Tia ya tano

[+kons ] [-kons ] [+sil ]

[-kons ] [-sil ] [+son ]

[+juu ] [+juu ] [+chin ]

[+mbel ] [+kat ]  [+kat ]

[+ant ] [-ant ] [-ant ]

[+mid ] [-mid ] [-mid ]

[+uviring] [+utandaz]  [+utandaz]

 










152

 

c)$ mwa$

……………………………….Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………Tia ya pili


/ \

│KS  …………………………Tia ya tatu


K k I  …………………………..Tia ya nne

m w a …………………….Tia ya tano

[+naz ] [-kons ] [+sil ]

[+ghun ] [-sil ] [+son ]

[+kons ] [+son ] [-kons ]

[+mid ] [+mid ]  [-mid ]

[+kati ] [+juu ]  [+chin ]

[+mbel ] [+nyum ]  [+kat ]

[+uviring] [+uviring]  [+utandaz]





d) $mya$

…………………………….Tia ya kwanza


\

MS US …………………………Tia ya pili


/ \

│KS ………………………..Tia ya tatu


K k I  …………………………Tia ya nne

m y a ………………….Tia ya tano

[+naz ] [-kons ] [+sil ]

[+ghun ] [-sil ] [+son ]

[+kons ] [+son ]  [-kons ]

[+mid ] [-mid ] [-mid ]

[+kati ] [+juu ] [+chin ]

[+mbel ] [+kat ] [+kat ]


[+uviring ] [+utandaz] [+utandaz]



Katika uchanganuzi wa silabi zenye kuundwa na konsonanti moja kiyeyusho na irabu, katika sehemu ya mwanzo silabi huwa na matawi mawili kama nilivyoeleza hapo awali. Tawi la kwanza ni la konsonanti pamoja na tawi la kiyeyusho na kwa upande wa ukingo

 




153

 


silabi tunakuwa na tawi moja tu ambalo ni la kiini silabi. Mifano hii namba 4 inaonesha dhahiri maneno ya Kiswahili Sanifu yenye silabi za muundo huu wa konsonanti moja, kiyeyusho na irabu pamoja na uchanganuzi wa silabi hizo kwa kuzingatia tia zake. Katika miundo ya silabi, muundo huu nao umeshamiri sana katika lugha ya Kiswahili Sanifu kama ilivyokuwa kwa silabi zenye muundo wa konsonanti moja nairabu.



9:2:5 a) Muundo wa Silabi wa Konsonanti mbili na Irabu za Asili ya lugha Kiswahili Sanifu (KKI).


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna muundo mwingine wa silabi ambao unakuwa na vipashio au fonimu konsonanti mbili na irabu. Katika muundo huu wa silabi konsonanti ya mwanzo huwa ni vitamkwa nazali ambazo ni / m / au / n / mara nyingi katika silabi ambazo zinatokana na lugha ya Kiswahili Sanifu na ya asili ya lugha za Kibantu. Labda tujiulize ni kwa nini konsonanti ya kwanza ni nazali? Ukweli ni kwamba hali hii hutokana na uathiriano baina ya sauti nazali na konsonanti pamoja na irabu (taz 7:1:1: 3 na 7:1:1:4). Katika sura ya saba inaonesha dhahiri kanuni zinazopelekea kuwepo kwa silabi za aina hii, na namna zinavyotokea katika lugha. Kwa upande mwingine ni kwamba vitamkwa hivi vinafungamana na konsonanti ya pili au inayoifuata nazali husika. Kwa kawaida kama konsonanti ni ya midomo nazali nayo itakuwa ya midomo. Hebu chungua mifano ifuatayo inayodhihirisha silabi zenye muundo huu katika Kiswahili Sanifu.


Mifano na: 5

Otografia matamshi

a) nda $nda$ katika neno nenda

b) ndo $ndɔ$ katika neno ndoa

c) mba $mba$ katika neno mbali

d) mbe $mbɛ$ katika neno mbegu

e) ngu $ngu$ katika neno ngurumo

f) ngi $ngi$ katika neno ngili



Uchanganuzi wa silabi hizi kimatawi na kitia hautofautiani na ule wa silabi zinazoundwa na konsonanti moja, kiyeyusho na irabu. Hebu tuangalie uchanganuzi wake na tia zake hapa chini.

 


















154

 

a) $nda$


…………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………….Tia ya pili


/ \

│KS  …………………………………...Tia ya tatu


K K I  …………………………………….Tia ya nne

n d a ……………………………….Tia ya tano

[+naz ] [-kont ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun ] [+ghun ]

[+juu ]  [+juu ] [+chin ]

[+mbel ] [+mbel ] [+kat ]

[+ant ] [+ant ] [-ant ]

[+utandaz] [+utandaz] [+utandaz]






b) $ndɔ$

………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………Tia ya pili


/ \

│KS  ………………………………..Tia ya tatu


K K I   …………………………………Tia ya nne

n d ɔ …………………………….Tia ya tano

[+naz ]  [-kont ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun ] [+ghun ]

[+mbel ] [+mbel ] [+kat ]

[+juu ] [+juu ] [+kati ]

[+ant ] [+ant ] [-ant ]

[+utandaz] [+utandaz] [+uviring]

[+kor ] [+kor ] [-kor ]

[+kons ]  [+kons ] [+son ]

 










155

 

c) $mba$

……………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………Tia ya pili


/ \

│KS  ………………………………..Tia ya tatu


││

││


K K I   …………………………………Tia ya nne

m b a ……………………………Tia ya tano

[+naz ] [-kont ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun ] [+ghun ]

[+mbel ] [+mbel ] [+kat ]

[+kati ] [+kati ] [+chin ]

[+ant ] [+ant ] [-ant ]

[+mid ] [+mid ] [-mid ]

[+uviring ] [+uviring] [+utandaz]







d) $mbɛ$


…………………………………………...Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………………..Tia ya pili


/ \

│KS ………………………………………Tia ya tatu


K K I   ………………………………………Tia ya nne

m b ɛ …………………………………Tia ya tano

[+naz ] [-kont ]  [+sil ]

[+ghun ][+ghun ]  [+ghun ]

[+mbel ][+mbel ]  [+mbel ]

[+kati ][+kati ]  [+kati ]

[+mid ][+mid ] [-mid ]

[+ant ][+ant ] [+ant ]


[+uviring][+uviring]  [+utandaz]

 








156

 

e) $ngu$

………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………..Tia ya pili


/ \

│KS  ………………………………..Tia ya tatu


││

││


K K I   …………………………………Tia ya nne

n g u ……………………………..Tia ya tano

[+naz ] [-kont ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun ] [+ghun ]

[+mbel ] [+nyum ] [+nyum ]

[+juu ] [+juu ] [+juu ]

[+ant ] [-ant ] [-ant ]

[+kons ] [+kons ] [-kons ]


[+utandaz] [+utandaz] [+uviring]





f) $ngi$

……………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………..Tia ya pili


/ \

│KS  ………………………………Tia ya tatu


K K I  ………………………………..Tia ya nne

n g i …………………………..Tia ya tano

[+naz ] [-kont ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun ] [+ghun ]

[+mbel ] [+nyum ] [+mbel ]

[+juu ] [+juu ] [+juu ]

[+ant ] [-ant ] [+ant ]

[+utandaz] [+utandaz] [+msamb]



Katika mifano namba 5 silabi zenye muundo wa konsonanti mbili na irabu moja hudhihirishwa kwa upana. Silabi hizi huweza kubeba irabu za aina zote yaani irabu kuu za Kiswahili Sanifu. Silabi hizi pia hujitokeza katikati ya neno au mwishoni mwa neno mfano katika neno pamba silabi $mba$ imejitokeza mwishoni wakati katika neno

 




157

 


pendana silabi $nda$ imejitokeza katikati ya neno. Vile vile umeona uchanganuzi wa silabi hizo kuwa huwa na matawi mawili katika mwanzo silabi kama ilivyo kwa silabi zenye kuundwa na konsonanti moja, kiyeyusho na irabu. Silabi hizo hapo juu zinajitokeza katika maneno yenye asili ya lugha ya Kiswahili na lugha za Kibantu kama ilivyoelezwa hapo awali. Vile vile muundo huu wa silabi hujitokeza katika maneno ya lugha ya Kiswahili Sanifu yaliyochukuliwa kutoka lugha za Kigeni.





9:2:5(b) Muundo wa Silabi wa Konsonanti mbili na Irabu katika Maneno ya Kiswahili Sanifu yaliyochukuliwa kutoka lugha za Kigeni (KKI).


Katika silabi za Kiswahili Sanifu zilizo katika maneno yaliyochotwa kutoka lugha za Kigeni kuna muundo wa konsonanti mbili na irabu (KKI). Silabi za muundo huu zimejitokeza katika maneno mengi yanayotumika katika lugha ya Kiswahili Sanifu lakini asili yake ni lugha mbalimbali za Kigeni. Maneno haya yenye silabi za namna hii mengi yamechotwa kutoka katika lugha za Kiarabu, Kiajemi, Kihindi, Kiingereza, Kijerumani, Kireno na kadhalika.


Muundo wa silabi wa konsonanti mbili na irabu, silabi zilizo ndani ya maneno yaliyochukuliwa kutoka lugha za Kigeni ni tofauti na zile zenye asili ya lugha ya Kiswahili au lugha za Kibantu kwa sababu zifuatazo:


Katika silabi za asili ya Kiswahili Sanifu, konsonanti za kwanza huwa ni nazali. Lakini silabi za maneno ya Kigeni, yaliyoingizwa katika Kiswahili Sanifu konsonanti zake za kwanza si nazali.


Katika silabi za Kiswahili Sanifu za asili ya Kiswahili za muundo huu konsonanti ya pili hufanana na konsonanti ya kwanza mahali pa matamshi kwa maana kwamba kama konsonanti ya kwanza ni ya midomo basi na konsonanti ya pili pia huwa ya midomo. Lakini upande wa silabi za muundo huu zinazotokana na maneno yenye asili ya lugha za Kigeni, konsonanti ya kwanza na ya pili hutofautiana mahali pa matamshi.


Katika silabi za Kiswahili Sanifu zenye asili ya Kiswahili, konsonanti zote mbili zinazounda silabi husika ni ghuna. Lakini silabi zinazotokana na maneno yenye asili


ya lugha za Kigeni zinaweza zote kuwa ni ghuna au zote ni visoghuna.


Baada ya kuona tofauti zinazotofautisha silabi za asili ya lugha ya Kiswahili na zenye asili ya Kigeni, sasa ni wakati mzuri wa kuchunguza silabi hizo. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 6

Otografia matamshi

a) bda $bda$ katika neno labda (kutoka lugha ya Kiajemi)

b) bla $bla$ katika neno kabla (kutoka lugha ya Kiarabu)

c) ksi $ksi$ katika neno faksi (kutoka lugha ya Kiingereza)

d) fta $fta$ katika neno daftari (kutoka lugha ya Kiarabu)

e) kta $kta$ katika neno sekta (kutoka lugha ya Kiingereza)

 







158

 


Silabi hizo hapo juu utagundua kuwa zimeundwa kwa konsonanti mbili na irabu. Katika mifano a) na b) silabi hizo zimeundwa na konsonanti ghuna na irabu, wakati silabi zilizoko katika mfano c) hadi e) zimeundwa na konsonanti si ghuna mbili na irabu kila moja. Lakini pia silabi hizi huchanganuliwa kama zile zilizoko katika (9:2:4 na 9:2:5a ) katika maana ya mgawanyo wa matawi. Hebu chungua uchanganuzi na tia zake.


a) $bda$

……………………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………………….Tia ya pili


/ \

│KS  ……………………………………….Tia ya tatu


K K I   ………………………………………..Tia ya nne

b d a ………………………………….Tia ya tano

[-kont ] [-kont ] [+sil ]

[+ghun ] [+ghun ][+son ]

[+kons ] [+kons ] [-kons ]

[+mid ] [-mid ] [-mid ]

[+ant ][+ant ] [-ant ]

[+mbel ][+mbel ] [+kat ]

[+kati ][+juu ] [+chin ]

[+uviring ][+utandaz] [+utandaz]


b) $bla$


…………………………………………...Tia ya kwanza

\


MS US ……………………………………..Tia ya pili

/ \


│KS ……………………………………Tia ya tatu

K K I  ……………………………………Tia ya nne

b l a ……………………………..Tia ya tano

[-kont ] [+tamb ][+sil ]

[+ghun ] [+ghun ][+son ]

[+mid ] [-mid ][-mid ]

[+ant ][+ant ][-ant ]

[+mbel ][+mbel ][+kat ]

[+kati ][+juu ][+chin ]

[+uviring][+utandaz][+utandaz]

 




159

 

[-kor ][+son ][-kons ]

c) $ksi$


…………………………………………Tia ya kwanza

\


MS US ……………………………………Tia ya tatu

/ \


│KS  ………………………………….Tia ya tatu

K K I  ……………………………………Tia ya nne

k s i ……………………………Tia ya tano

[-kont ] [+kont ][+sil ]

[-ghun ] [-ghun ][+ghun ]

[+nyum ] [+mbel ][+mbel ]

[+juu ] [+juu ][+juu ]

[-son ] [-son ][+son ]

[+utandaz][+utandaz][+msamb]

[-ant ] [+ant ][+ant ]






d) $fta$


…………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………………...Tia ya pili


/ \

│KS …………………………………….Tia ya tatu


K K I  ………………………………………Tia ya nne

f t a ………………………………..Tia ya tano

[- kont ][-kont ][+sil ]

[-ghun ][-ghun ][+ghun ]

[-son][-son ][+son ]

[+meno ][-meno ][-ghun ]

[+mbel ][+mbel ][+kat ]

[+kati ][+juu ][+chin ]

[+uviring][+utandaz][+utandaz]

[+ant ][+ant ][-ant ]

 







160

 

e) $kta$

………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US  ………………………………….Tia ya pili


/ \

│KS …………………………………Tia ya tatu



KI …………………………………..Tia ya nne

k t a ………………………….Tia ya tano

[-kont ][-kont ][+sil ]

[-ghun ][-ghun ][+ghun ]

[+kons ][+kons ][-kons ]

[+nyum ][+mbel ][+kat ]

[+juu ][+juu ][+chin ]

[-ant ][+ant ][-ant ]


[+utandaz][+utandaz][+utandaz]



Mifano hiyo hapo juu inadhihirisha tofauti iliopo baina ya silabi zinazoundwa na konsonanti mbili na irabu za asili ya Kiswahili Sanifu au Kibantu, na silabi zenye muundo huo huo lakini zinatokana na maneno yenye asili ya lugha ya Kigeni.



9:2:6 Muundo wa Silabi wa Konsonanti mbili, Kiyeyusho na Irabu (KKkI)


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna silabi za asili ya lugha Kiswahili Sanifu yenyewe na za Kibantu zenye muundo wa konsonanti mbili, kiyeyusho na irabu. Hapa nina maana kwamba maneno ya asili ya Kiswahili Sanifu, na yale yaliyomo katika Kiswahili Sanifu lakini yanatokana na lugha za asili yana silabi zenye muundo wa kuwa na konsonanti mbili zikifuatiwa na kiyeyusho pamoja na irabu. Ifuatayo ni mifano inayodhihirisha muundo huo wa silabi katika lugha ya Kiswahili.

 


Mifano na:7


Otografia matamshi

a) ngwa $ngwa$


b)mbwa $mbwa$

c) ndwi $ndwi$

 





katika neno chungwa


katika neno mbwa


katika neno hupendwi

 


Silabi hizi huchanganuliwa kama silabi nyingine zilizotanguliwa isipokuwa mwanzo silabi huwa na matawi matatu. Hebu chungua uchanganuzi huo hapa chini.ambapo nitaonesha matawi hayo na tia zake

 







161

 

a) $ngwa$


…………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………..Tia ya pili

/ / \

KS  …………………………..Tia ya tatu

K K k I  ……………………………Tia ya nne

n g w a ………………………Tia ya tano


[+naz ][-kont  ][-sil ][+sil ]

[+ghun ][+ghun ][+ghun ][+son ]

[+mbel ][+nyum][+nyum][+kat ]

[+juu ][+juu ][+juu ][+chin ]

[+ant ][-ant ][+ant ][-ant   ]

[+kons ][+kons ][-kons ][-kons ]







b)  $mbwa$


……………………………………….Tia ya kwanza

\


MS US ………………………………..Tia ya pili

/ /   \

KS  ……………………………...Tia ya tatu

K K k I  ………………………………..Tia ya nne

m b w a …………………………Tia ya tano

[+naz ][-kont ][-sil][+sil]

[+ghun ][+ghun ][+ghun ][+son ]

[+mbel ][+mbel ][+nyum][+kat ]

[+kati ][+kati ][+juu ][+chin ]

[+ant ][+ant ][+ant ][-ant ]

[+kons ][+kons ][-kons  ][-kons  ]

[+mid   ][+mid ][+mid ][-mid ]

[+kor ][+kor ][-kor ][+kor ]

 








162

 

c) $ndwi$

………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………Tia ya pili


/ / \

│   │KS  ………………………………Tia ya tatu



K   kI  ………………………………..Tia ya nne

n d w a …………………………..Tia ya tano

[+naz ][-kont ][-sil ][+sil ]

[+ghun ][+ghun][+ghun ][+son ]

[+mbel ][+mbel][+nyum][+kat ]

[+juu ][+juu ][+juu ][+chin ]

[+ant ][+ant ][-ant ][-ant ]

[+kons ][+kons ][-kons ][-kons ]





Katika mifano hiyo hapo juu utagungua kwamba yote imebeba konsonanti mbili na kiyeyusho / w / na irabu. Ukweli ni kwamba silabi za namna hii zimeonekana kuundwa na konsonanti mbili na kiyeyusho kimoja cha midomo ambacho ni / w / wakati zile zenye kuundwa na kosonanti moja na kiyeyusho na irabu, hizi hubeba viyeyusho vyote viwili kama inavyoonekana katika 9:2:4.





9:2:7 Muundo wa Silabi wa Konsonanti tatu na Irabu (KKKI)


Katika miundo mbalimbali ya silabi za Kiswahili Sanifu mingi imejitokeza katika maneno ya asili ya Kiswahili Sanifu, na maneno yaliyochotwa kutoka lugha za Kibantu na kuingizwa katika lugha ya Kiswahili isipokuwa mifano iliyopo katika 9:2:5b). Katika kipengele hiki nitazungumzia zaidi silabi zinazoundwa na konsonanti tatu na irabu (KKKI). Muundo huu unajitokeza katika silabi za maneno ya Kiswahili Sanifu ambayo yamechotwa kutoka katika lugha za Kigeni na kuingizwa katika lugha ya Kiswahili Sanifu hususani kutoka lugha ya Kiingereza.


Mifano na: 8

Otografia matamshi

a) skru $skru$ katika neno skrubu kutoka lugha ya Kiingereza (screw)

b) spri $spri$ katika neno springi kutoka lugha ya Kiingereza (spring)

c) skri $skri$ katika neno skrini kutoka lugha ya Kiingereza  (screen)

 







163

 


Uchanganuzi wa silabi hizi kitia na kimatawi hazina tofauti na zile zilizoko katika kipengele kilichotangulia cha (9:2:6). Silabi hizi pia huwa na matawi matatu katika mwanzo silabi.


a) $skru$

σ


\

MS US

/ / \

KS

K K K I

s k r u


[+kont ][-kont  ][+mad ][+sil ]

[-ghun ][-ghun ][+ghun][+son ]

[+kons ][+kons ][+kons][-kons ]

[+juu ][+juu ][+juu ][+juu ]


[+mbel ][+mbel ][+mbel][+nyum]

[+ant ][+ant ][+ant ][-ant ]


[+kor ][-kor ][+kor ][-kor ]



b)$spri$


…………………………………………..Tia ya kwanza

\


MS US ……………………………………..Tia ya pili

/ / \

KS  …………………………………..Tia ya tatu

K K K I  ……………………………………Tia ya nne

s p r i …………………………….Tia ya tano

[+kont ][-kont ][+mad ][+sil ]

[-ghun ][-ghun ][+ghun ][+son ]

[+kons  ][+kons ][+kons  ][-kons  ]


[+juu ][+kati ][+juu ][+juu ]

[+mbel ][+mbel ][+mbel ][+mbel ]


[+ant ][+ant ][+ant ][+ant ]

[+kor ][-kor ][+kor ][+kor ]

 







164

 

c)$skri$

……………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………..Tia ya pili

/ / \

KS  ……………………………..Tia ya tatu

K K K I  ……………………………….Tia ya nne

s k r i ………………………….Tia ya tano

[+kont ][-kont ][+mad  ][+sil ]

[-ghun ][-ghun ][+ghun ][+son ]

[+kons ][+kons ][+kons ][-kons ]

[+juu ][+juu ][+juu ][+juu ]

[+mbel][+nyum][+mbel ][+mbel ]

[+ant ][-ant ][+ant ][+ant ]

[+kor ][-kor ][+kor ][+kor ]



Katika mifano hiyo hapo juu umeona kuwa mwanzo silabi katika uchanganuzi una matawi matatu kama ilivyo kwa silabi zenye kuundwa na konsonanti mbili, kiyeyusho na irabu. Lakini ukichunguza kwa makini katika silabi hizo utagundua kuwa konsonanti ya kwanza ni kikwamizi kisoghuna, konsonanti ya pili ni kipasuo kisoghuna na konsonanti ya tatu ni kimadende ambacho ni ghuna katika silabi zote zilizoshughulikiwa katika kipengele hiki.



9:2:8 Muundo wa Silabi wa Nazali peke yake (N)


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna silabi ambazo zinaundwa na sauti nazali peke yake. Muundo huu unahusisha vitamkwa / m /, / ɱ / na / n / katika lugha ya Kiswahili. Kiundani silabi za namna hii zinatokana na mwathiriano baina ya taaluma ya fonolojia (matamshi) na taaluma ya mofolojia (maumbo) kwa kiasi kikubwa. Kutokana na mwathiriano huu ambao kitaalum hujulikana kama mofofonolojia baadhi ya sauti katika mofimu ambazo ni sehemu ya silabi hudondoshwa. Udondoshaji huu unasababisha kimatamshi sauti nazali kusimama peke yake kama silabi. Hapa ni lazima nieleze kwamba katika lugha ya Kiswahili Sanifu, vitamkwa vya aina hii huwa silabi pale tu vinapokaribiana na konsonanti nyingine au inapofuatiwa na konsonanti nyingine katika mpaka wa mofimu. Kwa maneno mengine, kiumbo mofimu hii ambayo ni silabi $mu$ sauti irabu hudondoshwa iwapo mofimu au silabi inayofuata inaanza na sauti konsonanti. Hebu rejea sura ya saba (7:2:1:3). Lakini upande wa /ɱ/ yenyewe husimama kama silabi inapofuatiwa na kikwamizi / v / katika mpaka wa mofimu. Upande wa sauti / n / yenyewe hujitokeza kwa kudondosha zaidi sauti /i/ mbali na kwamba kuna vighairi vingi vinavyokiuka kanuni hizo.

 




165

 


Silabi hizi huweza kutokea mwanzoni mwa neno, katikati ya neno. Hebu tuchungue muundo huu katika mifano ya maneno ifuatayo hapa chini.


Mifano na:9

Otografia matamshi

a) m $m$ katika maneno ya mrefu, mshindi, mcheshi, alimpiga, namna nk.

b) m $ɱ$ katika maneno ya mvua, mvomero, mvamizi, mvinza nk.

c) n $n$  katika maneno ya nne, nta, nchi nk.


Kama tulivyoona katika silabi nyingine, silabi hizi pia huweza kuchanganuliwa kimatawi kama ifuatayo:


a) $m$

σ ………………………………...Tia ya kwanza


/ \

MS US ……………………………Tia ya pili


KS………………………….Tia ya tatu


K Ø ………………………….Tia ya nne


m Ø


[+naz ]………………………………….......Tia ya tano

[+ghun ]


[+kati ]

[+mid ]


[+mbel ]

[+ant ]


[+sil ]


b) $ɱ$

……………………………………Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………Tia ya pili


KS……………………………..Tia ya tatu


K Ø ……………………………..Tia ya nne


Ø


[+naz ]………………………………………..Tia ya tano

[+sil ]


[+kati ]

[+mid ]


[+meno ]

[+mbel ]

 




166

 

c)$n$

………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………….Tia ya pili


KS ………………………………..Tia ya tatu



K Ø ………………………………....Tia ya nne


n Ø


[+naz ]………………………………………….Tia ya tano

[+ghun ]


[+juu ]

[+mbel ]


[+ant ]

[+sil ]


[+utandaz]


Katika uchanganuzi huu utagundua kuwa silabi hizi kitia zinafanana na silabi nyingine. Vile vile zimegawanyika katika sehemu kuu mbili kimatawi. Upande wa mwanzo silabi kuna konsonanti lakini upande wa ukingo silabi hakuna kipashio fonimu dhahiri kwa maana kwamba kiini silabi hakipo katika umbo dhahiri na alama kapa (Ø) imewekwa badala yake ili kuoneha kutokuwepo kwa umbo dhahiri la irabu. Katika silabi za muundo wa nazali peke yake alama (Ø) hutumika kuonesha kutokuwepo kwa umbo dhahiri la irabu au haipo fonimu irabu. Wakati katika silabi zenye muundo wa irabu peke yake alama kapa (Ø) hutumika kuonesha kutokuwepo kwa umbo dhahiri la fonimu konsonanti au huonesha hakuna konsonanti katika mwanzo silabi.


Baada ya kuona silabi huru za lugha ya Kiswahili Sanifu kama ilivyooneshwa katika miundo mbalimbali na uchanganuzi wake kitia na kimatawi. Katika kipengele kinachofuata nitashughulikia miundo mbalimbali ya silabi funge za Kiswahili Sanifu kwa kuzingatia zaidi ukingo wa silabi hizo.



9:3 Miundo ya Silabi Funge za Kiswahili Sanifu


Kiswahili kama lugha nyingine ina tabia ya kuchota msamiati kutoka lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu. Kutokana na uchukuaji au uchotaji wa maneno hayo kutoka lugha za Kigeni, lugha ya Kiswahili imejikuta ikiwa na silabi funge. Silabi funge ni silabi ambazo huishia na konsonanti. Sauti ambazo zina msikiko hafifu, na kwa sababu hiyo husababisha silabi funge pia kuwa na msikiko hafifu kama nilivyoeleza hapo awali katika sura ya nane (taz.8:1:1:2). Lugha ya Kiswahili ina silabi za namna hii na huweza kuchanganuliwa kimatawi na kuoneshwa tia zake. Nitazishughulikia silabi hizi kwa kuzingatia vipengele viwili vya msingi ambavyo ni konsonanti tamati na mwanzo silabi.

 




167

 

9:3:1 Muundo wa Silabi wa Irabu na Konsonanti (IK)


Ninaposema silabi funge zenye muundo wa irabu na konsonanti, nina maana kwamba silabi hiyo / hizo zinaanza na irabu na kuishia au kumalizikia na konsonanti. Katika kundi hili nitazingatia sauti ishilizi/ nitazishughulikia kwa kujikita katika sauti inayohusika na tamati silabi.



9:3:1:1 Silabi zinazoanza na Irabu na kuishia na Konsonanti / k /


Hizi ni silabi ambazo huanza na irabu na kuishia na konsonanti pasuo / k / kama tamati silabi yake. Silabi hizi zipo katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Hebu tuchungue mfano huu hapa chini.


Mfano na:10

Otografia matamshi

a)ik $ik$  katika neno iktisadi


Uchanganuzi wake uko hivi:

$ik$


…………………………………………Tia ya kwanza

\


MS US …………………………………...Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………..Tia ya tatu

IK …………………………….Tia ya nne


Ø i k ………………………….Tia ya tano

[+sil ][-kont ]

[+son ][-ghun ]

[+juu ][+juu ]

[+mbel ][+nyum ]

[+ant ][-ant ]


[+msamb ][+utandaz]





9:3:1:2 Silabi zinazoanza na Irabu na kuishia na Konsonanti / l /


Hizi ni silabi ambazo ukingo wake au tamati silabi yake huwa ni sauti konsonanti / l /.

Silabi hii hujitokeza katika lugha ya Kiswahili Sanifu kama hivi:

 







168

 

Mifano na:11

Otografia matamshi

a)al $al$  katika maneno almasi, Alhamisi, alfajiri, alhaji na kadhalika.


Uchanganuzi wake

$al$


…………………………………………Tia ya kwanza

\


MS US ……………………………………Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………….Tia ya tatu

IK ……………………………….Tia ya nne


Ø a l …………………………..Tia ya tano

[+sil ][+tamb ]

[+son ][+son ]

[+chin ][+juu ]

[+kat ][+nyum ]

[-kons ][+kons ]

[-ant ][+ant ]

[+utandaz][+utandaz]



9:3:1: 3 Silabi zinazoanza na Irabu na kuishia na Konsonanti / n /


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna silabi funge ambazo zinaishia na sauti konsonanti / n / kama tamati silabi yake. Mfano katika neno ankra.


Mfano na: 13


Otografia matamshi

a) an $an$ katika neno ankra


Uchanganuzi wake.

 


















169

 

$an$

……………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US  ………………………………...Tia ya pili


/ \

KS TS  ……………………………Tia ya tatu


IK ……………………………Tia ya nne


Ø a n ………………………..Tia ya tano

[+sil ] [+naz ]

[+son ] [+ghun ]

[+chin ] [+juu ]

[+kat ] [+mbel ]


[+utandaz] [+utandaz]



9:3:1:4 Silabi zinazoanza na Irabu na kuishia na Konsonanti / p /


Vile vile katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna baadhi ya silabi funge zenye ukingo wa sauti konsonanti / p / kama tamati silabi yake. Kwa upande wa uchanganuzi wake silabi ya namna hii haina tofauti na zilizochanganuliwa katika 9:3:1:1 na 9:3:1:2. Hebu tuangalie na kuuchunguza mfano ufuatao


Mfano na:12

Otografia matamshi

a) ap $ap$  katika neno Aprili


Uchanganuzi wake.

$ap$


……………………………….Tia ya kwanza

\


MS US …………………………...Tia ya pili

/ \

KS TS ………………………Tia ya tatu

IK ………………………Tia ya nne


Ø a p …………………Tia ya tano

[+sil ][-kont ]

[+son ][+kons ]

[+chin ][+kati ]

[+kat ][+mbel ]

[+utandaz][+uviring]

 




170

 

9:3:1:5 Silabi zinazoanza na Irabu na kuishia na Konsonanti / r /


Wakati mwingine silabi funge huwa na ukingo silabi wenye tamati silabi ya sauti konsonanti / r /. Silabi hii huweza kujitokeza katika neno ardhi.


Mfano na:14


Otografia matamshi

a) ar $ar$ katika neno ardhi


Uchanganuzi wake


$ar$

…………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS  ………………………………..Tia ya tatu


IK ………………………………..Tia ya nne

Ø a r ……………………………Tia ya tano

[+sil ][+mad ]

[+son ][+son ]

[+chin ][+juu ]

[+kat ][+mbel ]

[+utandaz][+utandaz]

[-ant ][+ant ]

[-kons ][+kons ]



9:3:1:6 Silabi zinazoanza na Irabu na kuishia na Konsonanti / s /


Hizi ni silabi funge ambazo ukingo silabi wake una sauti konsonanti / s / kwa maana kwamba kimuundo tamati silabi yake ni sauti konsonanti / s /. Silabi za aina hii hujitokeza katika maneno ya askari, askofu, istilahi na kadhalika.


Mifano na: 15


Otografia matamshi

a) as $ as $ katika neno askari, askofu


b) is $ is $ katika neno istilahi


Silabi hizi pia huweza kuchanganuliwa kama silabi funge za muundo huu zilizotangulia. Silabi hizi huwa na matawi matatu, moja upande wa mwanzo silabi ambalo hubeba alama ya kapa kuonesha hakuna konsonanti dhahiri na upande wa ukingo silabi kuna matawi mawili la kiini silabi na tamati silabi. Hebu chungua mifano ifuatayo.

 




171

 

a)$ as $

………………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US   …………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………….Tia ya tatu


IK ………………………………Tia ya nne

Ø a s ………………………….Tia ya tano

[+sil ][+kont ]

[+son ][-ghun ]

[+chin ][+juu ]

[+kat ][+mbel ]

[-ant ][+ant ]

[+utandaz ][+utandaz ]






b)$ is $

………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS  …………………………….Tia ya tatu

Ø I K …………………………….Tia ya nne

Ø i s …………………………Tia ya tano

[+sil ][+kont ]

[+son ][-ghun ]

[+juu ][+juu ]

[+mbel ][+mbel ]

[+ant ][+ant ]

[+msamb  ][+utandaz ]

[+kor ][+kor ]


Baada ya kuona silabi funge zinazoanza na irabu na kuishia na konsonanti mbalimbali kama vile sauti / k /, / l /, / n /, / p /, / r / pamoja na sauti / s /. Vile vile umeweza kuona uchanganuzi wake kimatawi na tia zake kama ilivyo kwa silabi zilizotangulia yaani silabi huru za Kiswahili Sanifu. Tofauti inayojitokeza hapa kati ya silabi funge na silabi huru ni

 




172

 


kwamba ukingo wa silabi huru haugawanyika au hakuna tamati silabi bali hubeba kiini silabi tu. Lakini upande wa silabi funge ukingo silabi hugawanyika katika matawi mawili ambapo kunakuwa na kiini silabi na tamati silabi.


Katika kipengele kinachofuata nitazichunguza silabi funge zinazoanza na sauti konsonanti na kuishia na konsonanti pamoja na uchanganuzi wake.



9:3:2 Muundo wa Silabi wa Konsonanti, Irabu na Konsonanti (KIK)


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna silabi funge ambazo muundo wake ni wa konsonanti, irabu na konsonanti. Utajiuliza mbona lugha za Kibantu hazina silabi funge? Ni kweli kabisa kwa asili lugha za Kibantu na Kiswahili kikiwemo hazina silabi funge, lakini kutokana na tabia ya lugha yoyote iliyo hai ya kuchota maneno kutoka lugha nyingine na kuyafanya sehemu ya msamiati wake, lugha ya Kiswahili imejikuta ikiwa na silabi funge kutokana na kuchota maneno ya lugha za Kigeni kama nilivyokwisha kusema hapo awali. Silabi hizi ni zile nilizozichunguza katika 9:3:1 na hizi nitakazozichunguza hapa chini. Silabi hizi nitazichunguza kwa kuegamia katika silabi tamati husika, kwa maana ya konsonanti ya mwisho katika silabi.



9:3:2:1 Silabi zinazoishia na Konsonati / b / na Konsonanti / f /


Hizi ni silabi funge za Kiswahili Sanifu zenye tamati silabi za sauti konsonanti / b / na


f /. Katika lugha ya Kiswahili Sanifu si maneno mengi yenye sifa ya kuwa na silabi zenye tamati silabi ya konsonanti za aina hii. Hebu tuchungue mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 16

Otografia matamshi

a) bib $ bib $ katika neno biblia

b) daf $ daf $ katika neno daftari


Uchanganuzi wake hautofautiani na silabi nyingine zilizotangulia. Silabi hizi zina tia tano, tawi moja upande wa mwanzo silabi, na matawi mawili upande wa tamati silabi.

 





















173

 

a) $ bib $

………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US  …………………………………Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………Tia ya tatu

K I K ……………………………Tia ya nne

b i b ………………………….Tia ya tano

[-kont ][+sil ][-kont ]

[+ghun ][+son ][+ghun ]

[+ant ][+ant ][+ant ]

[+kati ][+juu ][+kati ]

[+mbel ][+mbel ][+mbel ]

[+uviring ][+msamb ][+uviring ]



b)  $ daf $

………………………………………...Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………..Tia ya pili

/\

KS TS  ……………………………..Tia ya tatu

K I K ……………………………..Tia ya nne

d a f …………………………Tia ya tano

[-kont ][+sil ][+kont ]

[+ghun ][+son ][-ghun ]

[+ant ][-ant ][+ant ]

[+juu ][+chin ][+kati ]

[+mbel ][+kat ][+mbel ]

[+utandaz][+utandaz ][+uviring ]





9:3:3:2 Silabi zinazoishia na Konsonanti / h /


Kutokana na lugha ya Kiswahili Sanifu kuchukua maneno au kutohoa maneno kutoka lugha za Kigeni imejikuta ina silabi funge nyingi ambazo mojawapo ni hizi zinazoishia

 





174

 


na konsonanti /h/. Silabi hii hujitokeza katika maneno ya alhamdulilah, inshaalah na kadhalika


Mifano na: 17


Otografia matamshi

a) lah $ lah $ katika maneno ya alhamdulilah, inshaalah


Uchanganuzi wake


$lah $

………………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………….Tia ya pili

/ \

KS TS ……………………………….Tia ya tatu

K I K ………………………………Tia ya nne

l a h ………………………….Tia ya tano

[+tamb ][+sil ][+glot ]

[+ghun ][+son ][-ghun ]

[+juu ][+chin ][+chin ]

[+mbel ][+nyum   ][+nyum ]

[+ant ][-ant ][-ant ]

[+utandaz ][+utandaz ][+utandaz]

[+kons ][-kons ][+kons ]






9:3:2:3 Silabi zinazoishia na Konsonanti / k /


Hizi ni silabi zinazoanza na konsonanti yoyote ile lakini zinaishia na sauti konsonanti


k /. Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna silabi nyingi za namna hii. Hebu tuchungue mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na:18

Otografia matamshi

a) dak $ dak $ katika neno daktari

b) nuk $ nuk $ katika neno nukta

c) bak $ bak $ katika neno bakshishi

 










175

 

Uchanganuzi wa silabi hizi uko hivi:


a) $ dak $

……………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………….Tia ya pili

/ \

KS TS  …………………………….Tia ya tatu

K I K  ……………………………Tia ya nne

d a k …………………………Tia ya tano

[-kont ][+sil ][-kont ]

[+ghun ][+son ][-kons ]

[+juu ][+chin ][+juu ]

[+mbel ][+kat ][+nyum ]

[+ant ][-ant ][-ant ]

[+utandaz][+utandaz][+utandaz]

[+kons ][-kons ][+kons ]







b) $ nuk $


………………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………….Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………….Tia ya tatu

K I K   ……………………………..Tia ya nne

n u k ……………………………Tia ya tano

[+naz ][+sil ][-kont ]

[+ghun ][+son ][-ghun ]

[+juu ][+juu ][+juu ]

[+mbel ][+nyum ][+nyum ]

[+ant ][-ant ][-ant ]

[+utandaz][+uviring][+utandaz]

[+kons ][-kons ][+kons ]

 





176

 

c) $ bak $

…………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………………Tia ya pili

/ \

KS TS ………………………………..Tia ya tatu

K I K ………………………………..Tia yanne

b a k …………………………..Tia ya tano

[-kont ][+sil ][-kons ]

[+ghun ][+son ][-ghun ]

[+kati ][+chin ][+juu ]

[+mbel ][+kat ][+nyum ]

[+ant ][-ant ][-ant ]

[+uviring ][+utandaz][+utandaz]

[+kons ][-kons ][+kons ]






9:3:2:4 Silabi zinazoishia na Konsonant / l /


Hizi ni silabi funge ambazo zinaishia na sauti konsonanti / l / katika muundo wake. Hii ina maana kwamba silabi hizo zinaanza na konsonanti, zikifuatiwa na irabu kisha konsonanti / l /. Silabi hii inajitokeza katika baadhi ya maneno ya lugha ya Kiswahili Sanifu. Hebu tuchungue mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na:19

Otografia matamshi

a) bal $ bal $ katika neno balbu

b) fal $ fal $ katika neno mfalme au falme

c) hal $ hal $ katika neno halmashauri





Uchanganuzi wa silabi hizi hauna tofauti na silabi zilizochanganuliwa hapo juu kwamba upande wa ukingo silabi kuna matawi mawili ambayo ni ya kiini silabi na tamati silabi. Wakati upande wa mwanzo silabi una tawi moja.

 











177

 

a) $ bal $

………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US  …………………………………Tia pili

/ \

KS TS  …………………………….Tia ya tatu

K I K  ……………………………Tia ya nne

b a l ……………………….. Tia ya tano

[-kont ][+sil ][+tamb ]

[+ghun ][+son ][+ghun ]

[+mbel ][+kat ][+mbel ]

[+kati ][+chin ][+juu ]

[+uviring][+utandaz][+utandaz]

[+ant ][-ant ][+ant ]

[+kons ][-kons ][+kons ]





b) $ fal $


………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US  ………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………Tia ya tatu

K I K  …………………………..Tia ya nne

f a l ……………………….Tia ya tano

[+kont ][+sil ][+tamb ]

[-ghun ][+son ][+ghun ]

[+kati ][+chin ][+juu ]

[+mbel ][+kat ][+mbel ]

[+uviring ][+utandaz][+utandaz]

[+ant ][-ant ][+ant ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[+meno ][-meno ][-meno ]

[+mid ][-mid ][-mid ]

 








178

 

c) $ hal $

…………………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US ……………………………………….Tia ya pili

/ \

KS TS  ………………………………….Tia ya tatu

K I K ………………………………….Tia ya nne

h a l ……………………………..Tia ya tano

[+glot ][+sil ][+tamb ]

[-ghun ][+son ][+ghun ]

[+chin ][+chin ][+juu ]

[+nyum ][+kat ][+mbel ]

[+utandaz ][+utandaz][+utanda  ]

[-ant ][-ant ][+ant ]

[+kons ][-kons ][+kons ]






9:3:2:5 Silabi zinazoishia na Konsonanti / m /


Hizi ni silabi funge ambazo zinaishia na kitamkwa nazali / m / katika muundo wake, kwa maana kwamba silabi za namna hii huanza na konsonanti nyingine na kuishia na konsonanti nazali. Huweza kuanza na konsonanti nazali, kimadende, vikwamizi na kadhalika zikifuatiwa na irabu na mwisho konsonanti nazali / m / ambayo ni tamati silabi. Silabi zenye tamati silabi ya aina ya nazali / m / ziko nyingi katika maneno ya lugha ya Kiswahili Sanifu. Ifuatayo ni mifano ya silabi hizo.


Mifano na:20

Otografia matamshi

a) ham $ ham $ katika neno hamsa, alhamdulilah

b) nam $ nam $ katika neno Jehanam

c) ram $ ram $ katika neno ramsa

d) mem $ mɛm $ katika neno memsahib, MEMKWA



Uchunganuzi wa silabi hizi katika lugha ya Kiswahili Sanifu uko kama ifuatavyo:

 











179

 

a)$ ham $

……………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………Tia ya tatu

K I K …………………………..Tia ya nne

h a m ………………………..Tia ya tano

[+glot ][+sil ][+naz ]

[-ghun ][+son ][+ghun ]

[+chin ][+chin ][+kati ]

[+nyum ][+kat ][+mbel ]

[+utandaz][+utandaz][+uviring ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[-ant ][-ant ][+ant ]

[-mid ][-mid ][+mid ]





b)$ nam $


…………………………………….....Tia ya kwanza

\


MS US  ………………………………...Tia ya pili

/ \

KS TS  …………………………...Tia ya tatu

K I K   …………………………..Tia ya nne

n a m ………………………Tia ya tano

[+naz ][+sil ][+naz ]

[+ghun ][+son ][+ghun ]

[+juu ][+chin ][+kat ]

[+mbel ][+kat ][+mbel ]

[+utandaz ][+utandaz ][+uviring ]

[+ant ][-ant ][+ant ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[-mid ][-mid ][+mid ]

 








180

 

c) $ ram $

…………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………….Tia ya pili

/ \

KS TS  ………………………………..Tia ya tatu

K I K……………………………..Tia ya nne

r a m …………………………Tia ya tano

[+mad ][+sil ][+naz ]

[+ghun ][+son ][+ghun ]

[+juu ][+chin ][+kati ]

[+mbel ][+kat ][+mbel ]

[+utandaz ][+utandaz][+uviring ]

[+ant ][-ant ][+ant ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[-mid ][-mid ][+mid ]







d) $ mɛm $


…………………………………………….Tia ya kwanza

\


MS US ……………………………………….Tia ya pili

/ \

KS TS  …………………………………Tia ya tatu

K I K  ………………………………..Tia ya nne

m ɛ m ……………………………..Tia ya tano

[+naz ][+sil ][+naz ]

[+ghun ][+son ][+ghun ]

[+kati ][+kati ][+kati ]

[+mbel ][+mbel ][+mbel ]

[+mid ][-mid ][+mid ]

[+uviring ][+utandaz ][+uviring ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[+ant ][+ant ][+ant ]

 





181

 

9:3:2:6 Silabi zinazoishia na Konsonanti / r /


Lugha ya Kiswahili Sanifu ina silabi funge ambazo ukingo silabi wenye tamati silabi sauti konsonanti / r /. Kwa upande wa mneno yenye silabi ya muundo huu si mengi katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Hebu tuchungue mifano ifuatayo ya maneno yanayodhihirisha uwepo wa silabi hii.


Mifano na:21


Otografia matamshi

a) kar $ kar $ katika neno karne, karlini


Uchanganuzi wake kimatawi na tia zake.


a) $ kar $

…………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US  …………………………………...Tia ya pili


/ \

KS TS  ………………………………Tia ya tatu

K I K  ……………………………..Tia ya nne

k a r ………………………Tia ya tano

[-kont ][+sil ][+mad ]

[-ghun ][+son ][+ghun ]

[+juu ][+chin ][+juu ]

[+nyum ][+kat ][+mbel ]

[-ant][-ant ][+ant ]

[+utandaz][+utandaz][+utandaz]

[+kons ][-kons ][+kons ]





9:3:2:7 Silabi zinazoishia na Konsonanti / s /

 


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu kuna konsonanti, irabu na konsonanti tamati silabi silabi / s / ziko nyingi katika lugha ya inayodhihirisha uwepo wa silabi hizo.

 


silabi funge ambazo zina muundo wa


s /. Silabi zenye ukingo wenye tamati Kiswahili Sanifu. Ifuatayo ni mifano

 


Mifano na: 22

Otografia matamshi

a) des $ dɛs $ katika neno desturi

b) was $ was$ katika neno wastani

c) mus $ mus$ katika neno mustarehe, mustakabali

 




182

 

d) hos $ hɔs $ katika neno hospitali

e) ras $ ras $ katika neno rasmi

f) tas $ tas $ katika neno taslim


Uchanganuzi wake kimatawi na kitia.


a) $ dɛs $

……………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US  ………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………Tia ya tatu

K I K   …………………………Tia ya nne

d ɛ s ………………………Tia ya tano

[-kont ][+sil ][+kont ]

[+ghun ][+son ][-ghun ]

[+juu ][+kati ][+juu ]

[+mbel ][+mbel ][+mbel ]

[+ant ][+ant ][+ant ]

[+utandaz][+utandaz][+utandaz]

[+kons ][-kons ][++kons ]

[+kor ][+kor ][+kor ]


b) $ was $


……………………………………..Tia ya kwanza

\


MS US …………………………………Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………Tia ya tatu

K I K  …………………………...Tia ya nne

w a s ………………………Tia ya tano

[-sil ][+sil ][+kont ]

[-kons   ][-kons ][+kons ]

[+juu][+chin ][+juu ]

[+nyum ][+kat ][+mbel ]

[+son ][+son ][-son ]

[+mid ][-mid ][-mid ]

[+ant ][-ant ][+ant ]

 




183

 

c) $ mus $

……………………………………….Tia ya kwanza


\

MS US ………………………………...Tia ya pili


/ \

KS TS  …………………………….Tia ya tatu

K I K …………………………….Tia ya nne

m u s ……………………….Tia ya tano

[+naz ][+sil ][+kont ]

[+ghun ][+son ][-ghun ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[+kati ][+juu ][+juu ]

[+mbel ][+nyum ][+mbel ]

[+ant ][-ant ][+ant ]

[+uviring ][+uviring ][+utandaz]

[+mid][-mid ][-mid ]






d) $ hɔs $


………………………………………..Tia ya kwanza


\

MS US  …………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS  ………………………………Tia ya tatu

K I K  ……………………………..Tia ya nne

h ɔ s ……………………….Tia ya tano


[+glot ][+sil ][+kont ]

[-ghun ][+son ][-ghun ]

[+chin ][+kati ][+juu ]

[+nyum ][+nyum ][+mbel ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[+utandaz ][+uviring ][+utandaz ]

[-ant ][-ant ][+ant ]

 








184

 

e) $ ras $


…………………………………………Tia ya kwanza


\

MS US …………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS  ……………………………..Tia ya tatu


IK  ……………………………Tia ya nne

r a s ………………………Tia ya tano

[+mad ][+sil ][+kont ]

[+ghun ][+son ][-ghun ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[+juu ][+chin ][+juu ]

[+mbel ][+nyum ][+mbel ]

[+utandaz][+utandaz][+utandaz]

[+ant ][ -ant ][+ant ]





f) $ tas $

σ  ……………………………………………Tia ya kwanza

/ \

MS US ……………………………………..Tia ya pili

/ \

KS TS …………………………………Tia ya tatu

K I K  ………………………………Tia ya nne

t a s …………………………Tia ya tano

[-kont ][+sil ][+kont ]

[-ghun ][+son ][+ghun ]

[+juu ][+chin ][+juu ]

[+mbel ][+kat ][+mbel ]

[+kons ][-kons ][+kons ]

[+utandaz][+utandaz][+utandaz]

[+ant ][-ant ][+ant ]

 











185

 


Katika kuitazama silabi kimuundo utagundua kuwa silabi za Kiswahili Sanifu zipo za miundo mbalimbali. Upande wa silabi huru umeona kuwa kuna silabi za muundo wa irabu peke yake (I), konsonanti na irabu (KI), kiyeyusho na irabu (kI), konsonanti, kiyeyusho na irabu (KkI), konsonanti, konsonanti na irabu (KKI), konsonanti,konsonanti kiyeyusho na irabu (KKkI), konsonanti, konsonanti, konsonanti na irabu (KKKI) na nazali peke yake (N). Upande wa silabi funge umeona zinaanza na irabu kisha konsonanti (IK) pamoja na zenye kuanza na konsonanti,ikifuatiwa na irabu kisha konsonanti (KIK).


Vile vile umeweza kuona namna silabi hizo zinavyochanganuliwa kimatawi na kuonesha tia zake. Kimsingi silabi zote huweza kuchanganuliwa kimatawi na kuonesha tia zake bila kujali ni aina gani ya silabi. Tofauti iliyopo baina ya silabi huru zenye konsonanti nyingi na viyeyusho na silabi funge ni utokeaji wa matawi. Silabi huru zenye konsonanti nyingi pamoja na viyeyusho mwanzo silabi wake huweza kugawanyika katika matawi mawili au matatu, wakati silabi funge ukingo silabi wake ndiyo hugawanyika katika matawi mawili tu katika lugha ya Kiswahili Sanifu.


Hata hivyo ni muhimu kutambua kwamba katika lugha ya Kiswahili kuna baadhi ya silabi ambazo kiotografia hazionekani dhahiri hususani tunapoitazama silabi katika taaluma au kipengele cha mofofonolojia. Lakini kwa kuwa silabi inahusika na matamshi basi niseme kwamba silabi hizi zinaweza kuoneshwa kitahajia kupitia matamshi yake. Hii ina maana kwamba katika umbo la ndani umbo dhahiri la silabi hiyo halionekani lakini katika umbo la nje la silabi hiyo umbo dhahiri linaloonekana. Mfano mzuri katika lugha ya Kiswahili Sanifu ni silabi nazali ambazo wakati mwingine kitahajia hazionekani mathalani zinapotazamwa katika umbo la ndani. Ninasema hivyo kwa sababu silabi za namna hii katika baadhi ya mazingira huwa na umbo dhahiri katika umbo la nje isipokuwa katika mazingira mengine hazionekani. Hata hivyo maneno ambayo silabi hizi kwayo hazina umbo dhahiri la ndani, silabi hizi hudhihirika wazi katika umbo la nje la maneno hayo. Hebu chungua mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 23


Otografia matamshi

a) nje $ n $ $ nje $


b) mbwa $ m $ $ mbwa $

c) mbale $ m $ $ mba $ $ lɛ$



Katika mifano hiyo hapo juu katika 23 a) – c), silabi nazali $ n$ na $ m $ hazionekani katika otografia ya maneno hayo ya maumbo ya ndani ( ya kimofolojia) lakini katika otografia ya matamshi ya maneno hayo ya maumbo nje (ya kifonolojia) yanaonekana. Sababu kuu inayosababisha hali kama hii kuwepo ni kutokana na kuwa karibu au katika mpaka wa silabi, sauti nazali hizo zinafuatiwa na sauti zinazofanana nazo, hivyo silabi hizo hulazimika kuondolewa katika tahajia maumbo ya maneno hayo ya ndani (ya kimofolojia).

 











186

 

9:3:3 Dhima ya Silabi katika Lugha


Silabi kama kiashio cha uamilifua katika lugha kina umuhimu mkubwa sana katika lugha maalum. Kama ilivyo kwa vitamkwa vingine vina dhima kubwa sana katika lugha maalum kwa kila kimoja kwa nafasi yake ndivyo ilivyo hata kwa kipashio silabi. Dhima za silabi katika lugha ni kama ifuatavyo:


Kwanza kabisa silabi ina dhima ya Kifonetaktiki, kwa maana kwamba kipashio hiki kina kanuni maalum inayomruhusu mtumiaji wa lugha kutumia mfuatano maalum wa mfumo wa lugha unaokubalika katika kuunda silabi. Hii ina maana kwamba mfuatano maalum wa fonimu na kumkataza kutumia mfuatano wa fonimu usiokubalika. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili Sanifu mfuatano wa konsonanti tupu haukubaliki bali mfuatano uliooneshwa katika vipengele 9:3:1:1,2,3,4,5,6,7 na 9:3:2:1,2,3,4,5,6, na 7 ndiyo inayokubalika. Kwa kutumia miundo mbalimbali ya silabi tunaweza kutambua mfuatano wa vitamkwa unaofaa na usiofaa.


Dhima ya pili ni kwamba silabi inatumika kama mawanda ya kanuni za kifonolojia. Kwa maana kwamba hatushughulikii silabi za lugha tu bali tunangalia au tunashughulikia matumizi yake katika lugha. Silabi kama nilivyokwisha kusema hapo awali kuwa ni kipashio kinachohusika katika matamshi ya lugha, hivyo ni lazima pia kujua kuwa silabi ina dhima kuu ya kuunda maneno mbalimbali ya lugha.


Silabi zina dhima nyingine, kwamba silabi ni kipashio chenye muundo wa kipandesauti changamano (structure of complex segment) ambao hudhibiti sifa pambanuzi ambazo hubainisha vitamkwa. Vile vile huonesha muundo wa ndani wa vitamkwa au fonimu zinazounda silabi hizo. Hii inadhihirishwa katika uchanganuzi wa silabi kupitia zile tia tano na matawi yake.


Mwisho, silabi ni kipashio ambacho hutumika kuunda vipashio vikubwa zaidi katika taaluma ya mofolojia na sintaksia. Vile vile huonesha maana ya neno kupitia mkazo unaowekwa katika baadhi ya silabi.





9:4 Kiimbo


Katika sura ya nane (taz. 8:2) kiimbo kimeelezwa kuwa ni utaratibu maalum wa mpangilio wa mfuatano wa mawimbi ya sauti au utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti katika lugha maalum wakati wa usemaji. Kama nilivyoeleza hapo awali katika 8:2 kwamba kila lugha ina utaratibu wake maalum unaotumika katika upandishaji na ushushaji wa mawimbi ya sauti. Kiimbo katika lugha kinasaidia kubainisha lengo la usemaji lililokusudiwa na mzungumzaji wa lugha husika. Katika usemaji wa watu tunaweza kutambua kama mzungumzaji anatoa maelezo, anauliza swali au anatoa amri. Tofauti hiyo inatokana na kiimbo kinavyobadilikabadilika. Katika lugha nyingi pamoja na Kiswahili Sanifu kiimbo kimegawanyika katika aina kuu nne ambazo ni kiimbo cha mshangao, maelezo, amri na maulizo au swali.

 










187

 

9:4:1 Aina za Viimbo


Katika lugha ya Kiswahili Sanifu tuna viimbo vya aina kuu nne kutokana na mabadiliko yanayojitokeza wakati wa usemaji. Lengo au maana ya msemaji ndiyo inasababisha kuwepo kwa aina hizo kuu za viimbo . Viimbo hivyo ni cha maelezo, amri, maulizo / swali pamoja na cha mshangao.



9:4:1:1 Kiimbo cha Maelezo


Kiimbo cha maelezo ni kiimbo ambacho kwa kawaida msemaji wa lugha akiwa katika kidatu chochote kile mawimbi ya sauti katika usemaji wake yanakuwa katika msitari ulionyooka. Lakini hata hivyo maelezo hutofautiana kimaana kwani kuna maelezo ya kusimulia moja kwa moja, maelezo ya kuagiza, maelezo ya kutisha na maelezo ya kumshangaza msikilizaji. Kutokana na tofauti hizo hata kiimbo kinachotumika katika aina hizo za maelezo hutofautiana pia kwa kiasi fulani. Hebu chungua mifano ifuatayo.


Mifano na:24


a). Ataingia kesho jioni.

——————————————


——————————————


Wanaenda Kyejo


——————————————


——————————————


Ameitwa na mwalimu.

——————————————


——————————————



9:4:1:2 Kiimbo cha Kuuliza / Swali


Hiki ni kiimbo kinachojitokeza kwa kutumia viwango tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa. Kimsingi msemaji anapofikia mwisho wa usemi hupandisha kidatu na kumalizia kwa kukishusha. Hebu chungua mifano ifuatayo.


Mifano na: 25

Mama  anarudi lini?


———————————


———————————

 





188

 

Unaniita  nani?

—————————


—————————


Kwa  lipi ?


—————————


—————————


Kwa kawaida ni vigumu sana kuvibainisha viwango hivi kwa usahihi sana bila kuwa na umilisi kuhusu fonetiki akustika (fonetiki mawimbisauti). Ubainishaji huu wa viwango vya kidatu vinavyoandamana na mawimbisauti unafanywa na vifaa maalum vya kimaabara. Lakini mifano iliyopo hapo juu inakidhi kiwango kilichokusudiwa.



9:4:1:3 Kiimbo cha Amri


Kiimbo hiki cha amri kinashabihiana sana na kiimbo cha swali. Uchunguzi wa kifonetiki unaonesha kuwa katika utoaji wa amri msemaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko katika kiimbo cha maelezo. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Mifano na: 26

Ondokeni


————————


————————


Njooni hapa

————————


————————


Toka  nje


————————


————————


Katika mifano 26(a) – (c), mzungumzaji anatumia kidatu cha juu anapotoa amri kwa wasikilizaji wake. Hali hii hujitokeza hata pale tamko la maelezo kama amri. Katika kubaini kiimbo alama ya nukta–mkia hutumika kubaini mwelekeo wa kiimbo. Nukta– mkia ikipanda kwenda (yaani mkia ukipanda juu ) mstari wa juu unaonesha kiimbo kimepanda na kama mkia utashuka kwenda mstari wa chini basi kiimbo kitakuwa kimeshuka.

 







189

 

9:4:1:4 Kiimbo cha Mshangao


Kiimbo cha mshangao hutolewa kwa kuambatanisha mawimbisauti katika kiwango cha kupanda, kushuka na kupandisha kidatu cha silabi za mwishoni mwa neno. Hebu chunguza mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 27

a) Aloo! Alaa!

————— —————

————— —————

b) Kumbe! Naam!

————— —————

————— —————

c) Ahaa! Mungu  wangu!

————— ————————

————— ————————


Mifano hiyo hapo juu inahusu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu tu. Hii ina maana kwamba katika usemaji wao huweza kutumia viimbo vya aina hizo katika utumiaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu.



9:5 Kidatu


Katika sura ya nane (taz. 8:3) nimeeleza kuwa kidatu ni kiwango cha sauti inayosikika wakati wa utamkaji, chaweza kuwa kiwango cha sauti cha juu, cha katikati au cha chini. Kwa maana kwamba mzungumzaji wa lugha anaweza kupandisha kiwango cha sauti na kuiweka katika kidatu cha juu, au akakishusha kidogo na kuiweka katika kidatu cha kati au akakishusha zaidi na kuiweka sauti katika kidatu cha chini.


Hata hivyo kidatu hakiathiriwi na mawimbi ya sauti kwa maana kwamba kubadilika kwa mawimbisauti hakusababishi kidatu kubadilika. Mawimbisauti yanapobadilika kidatu hubaki vile vile.


Kidatu huweza kuwakilishwa kwa mistari miwili iliyokaa sambamba ambapo ndani ya mistari hiyo huwekwa alama ya nukta – mkia ambayo hufanana na alama ya mkato [ ], mkia wake unaweza kuelekea juu au chini. Alama hii huonesha kidatu cha sauti. Alama hiyo ya nukta – mkia ikiwa karibu na mstari wa juu ina maana sauti iko katika kidatu cha juu, inapokuwa iko katikati ya mistari miwili ina maana sauti iko katika kidatu cha kati na ikiwa alama nukta – mkia iko karibu na mstari wa chini ina maana kwamba sauti iko katika kidatu cha chini. Hebu chunguza mifano ifuatayo hapa chini.

 







190

 

Mifano na: 28

Nenda  haraka sokoni


————————————

Kidatu cha juu


————————————


Nenda  haraka  sokoni

————————————


Kidatu cha kati

————————————


Nenda  haraka  sokoni


————————————

Kidatu cha chini


————————————


Mifano 28(a) – (c) inaonesha viwango vya kidatu vya aina tatu yaani kidatu cha juu, kidatu cha kati na kidatu cha chini katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Ni dhahiri kuwa mtumiaji wa lugha huweza kutumia vidatu hivyo kutokana na kile anachokimaanisha



9:6 Mkazo


Kama nilivyoeleza katika sura ya nane (taz.8:4) kuwa, mkazo huhusu kiwango cha nguvu inayotumika wakati wa utamkaji wa baadhi ya silabi. Mkazo ni utamkaji wa nguvu zaidi katika sehemu ya neno au katika fungu la maneno, kwa kawaida huwekwa kwenye silabi. Silabi yenye kutamkwa kwa mkazo ina msikiko mkubwa zaidi kuliko silabi nyingine za neno husika. Lugha nyingi ulimwenguni hutumia mkazo ijapokuwa si zote. Kiswahili Sanifu ni mojawapo ya lugha zinazotumia mkazo wakati wa utamkaji. Kwa upande wa Kiswahili dhana ya mkazo hujitokeza katika viwango viwili yaani kiwango cha neno na kiwango cha sentensi. Uchunguzi wa kifonolojia unaonesha kuwa maneno yanayotokea peke yake, au mkazo katika kiwango cha neno katika lugha ya Kiswahili Sanifu huwekwa katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno (kutoka kulia mwa neno). Mkazo katika tungo za lugha ya Kiswahili Sanifu maneno yenye kubeba maana au dhamira ya msemaji ndiyo hupokea mkazo. Mfano wa maneno hayo ni nomino, vitenzi, vivumishi, vielezi na viunganishi katika baadhi ya mazingira. Mkazo huoneshwa ama kwa kutumia herufi kubwa (silabi inayopokea mkazo huandikwa kwa herufi kubwa taz.8.4), au kwa kutumia alama ya [ ' ] mbele ya irabu ya silabi inayohusika au mbele ya


konsonanti nazali / m /, /ɱ / na / n /.


Katika mifano nitakayoitoa hapa chini nitatumia alama ya [ ' ] kuonesha mkazo katika maneno hayo. Hebu chunguza mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na:29

Otografia matamshi


a) ameondoka [anaɔndɔ'ka]

b) mhandisi [mhandi'si]

 




191

 

c) nta [n'ta]

d) mti [m'ti]


e) ubaya [uba'ya]


Katika usemaji mkazo huweza kuwekwa kama ilivyo hapo juu kuonesha usemaji wa kawaida. Vile vile mkazo huweza kutumika kuonesha dhima ya msisitizo na ubainishaji wa maana za maneno. Msemaji anapotaka kusisitiza jambo fulani analolizungumza huweka mkazo katika silabi ya kwanza ya neno. Hebu chunguza mifano ifuatayo.


Mifano na:30

Kawaida Msisitizo

Otografia matamshi otografia matamshi

a) hapahapa [hapaha'pa ] hapahapa [ha'pahapa ]

b) sawasawa [sawasa'wa] sawasawa [sa'wasawa]

c) polepole [pɔlɛpɔ'lɛ ] polepole [pɔ'lɛpɔl ]


Mifano hiyo hapo juu katika 30(a) – (c) hususani iliyoko upande wa kulia inaonesha dhana ya msisitizo katika usemaji. Vile vile mkazo unaoonesha msisitizo hujitokeza katika maneno rudufu yaani maneno yenye maumbo yanayorudiwarudiwa.


Mkazo pia katika Kiswahili Sanifu una dhima ya kutofautisha maana za maneno ambayo yana maana zaidi ya moja. Wataalam wengine wanadai kuwa ni maneno ambayo yanafanana kimaumbo lakini hutofautishwa kwa kutumia mkazo. Hebu chungua mifano ifuatayo kwa ufafanuzi zaidi.


Mifano na:31

Otografia matamshi maana

a) barabara [baraba'ra ] njia kuu ambayo magari,pikipiki hupita humo.

b) barabara [bara'bara ] sawasawa

c) katakata [kataka'ta ] kugawa kitu katika vipande vipande

d) katakata [ka'takata ] kabisa kabisa

e) hivihivi [hivihi'vi ] bila sababu

f) hivihivi [hi'vihivi ] kufanana, kutokuwepo kwa badiliko


Katika mifano hiyo utagundua kuwa mkazo unapohamishwa na kuwekwa kwenye silabi nyingine maana ya neno pia hubadilika. Hata hivyo lugha ya Kiswahili Sanifu kuna maneno machache sana yenye kaida ya namna hii ikilinganisha na lugha nyingine kama lugha ya Kiingereza.



9:7 Lafudhi


Lafudhi ni dhana ambayo nimeieleza kwa kirefu katika sura ya nane (taz. 8:5). Lafudhi ni sifa ya kimasikizi ya matamshi ya mtu binafsi ambayo humtambulisha msemaji sehemu atokako kijiografia au kijamii. Lafudhi hutokana na athari za mazingira ya mtu kijamii au kijiografia na lugha mama yake. Lafudhi hutambuliwa kwa kuoanisha mtu na mazingira yake.

 




192

 


Wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kwa upande wa Tanzania, utagundua kuwa wasemaji wa Kiswahili wana lafudhi tofauti, kwa maana kwamba watu wa Pwani wana lafudhi yao tofauti na watu wa Tanzani bara. Tofauti iliyopo baina ya watu wa Pwani, Zanzibar na Tanzania Bara inatokana na lugha mama zao. Kwa upande wa wazungumzaji wengi wa Bara Kiswahili kwao ni lugha ya pili na ndiyo sababu wengi wao hutamka maneno ya lugha ya Kiswahili kama wanavyotamka katika lugha mama zao. Tofauti hii ya uzungumzaji huleta tofauti katika usemaji wa Kiswahili na kupelekea kuwepo kwa lafudhi mbalimbali kama vile Kiswahili cha Pwani, Kiswahili cha Bara, Kiswahili cha Kusini, Kiswahili cha Wapare na kadhalika. Hebu chunguza kwa makini mifano ifuatayo hapa chini.


Mifano na: 32


Ntoto ndogo analia. (msemaji ni Mmakonde)

Tunaendaga sokoni. (msemaji ni Mnyakyusa)


Nitamyambia baba. (msemaji ni Msambaa)

Angesema mimi. (msemaji ni Msambaa )


Tumbo zinaniuma . (msemaji ni Mchaga)

Kyai kya rangi. (msemaji wa Mnyakyusa)


Thatha ni wakati wa kula. (msemaji ni Mpare)


Mifano katika 32(a) – (g) hapo juu kuna wasemaji watano wenye lafudhi tofauti. Msemaji wa mfano wa 32(a) ameathiriwa na lugha ya Kimakonde, badala ya kutamka [mtɔtɔ mdɔgɔ] kama inavyotakiwa katika Kiswahili Sanifu, yeye anasema [ntɔtɔ ndɔgɔ] sawa na lugha ya Kimakonde). Msemaji wa pili katika mfano wa 32(b) na (f) ameathiriwa na lugha ya Kinyakyusa, badala ya kusema b) [huwa tunaɛnda sɔkɔni] na


[čai ya rangi] msemaji anasema [tunaɛndaga sɔkɔni] na [kyai kya rangi] . Msemaji wa tatu ameathiriwa na lugha ya Kisambaa, badala ya kusema c)[nitamwambia baba] na d)


[ningɛsɛma mimi] bali anasema c) [nitamyambia baba] na d)[angɛsɛma mimi]. Msemaji wa nne ameathiriwa na lugha ya Kichaga, badala ya kusema e)[tumbɔ linaniuma] anasema [tumbɔ zinaniuma], hali kadhalika msemaji wa tano ameathiriwa na lugha ya


Kipare badala ya kusema g) [sasa ni wakati wa kula] anasema [θaθa  ni wakati wa kula].


Lakini lafudhi ya Kiswahili Sanifu haimtambulishi mtu kijiografia au kijamii. Msemaji wa Kiswahili Sanifu hutamka na kuzungumza Kiswahili kilichosanifiwa na kukubalika kitumike rasmi na mamlaka husika. Msemaji wa Kiswahili Sanifu aliye na umilisi wa lugha na utendaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu haathiriwi na mazingira wala lugha mama yake katika usemaji wake. Hii ina maana kwamba hafungamani na lafudhi yoyote ya kieneo au kijamii. Wasemaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu wanatamka na kuzungumza Kiswahili kilichosanifiwa na kwa lafudhi moja. Ili kubaini au kutambua lafudhi ya Kiswahili Sanifu ni lazima mkazo uzingatiwe mahali unapostahili kuwekwa. Katika Kiswahili Sanifu katika maneno mengi mkazo huwekwa katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno (kutoka kulia mwa neno).

 











193

 

Zoezi

1.Jadili aina za silabi za Kiswahili Sanifu


2.“Silabi ina muundo wa kimatawi na kitia.” Thibitisha kauli hii kwa kutumia aina za silabi zifuatazo:

muundo wa irabu peke yake


konsonanti, kiyeyusho na irabu

konsonanti, konsonanti na irabu


konsonanti,irabu na konsonanti

nazali


Eleza dhima ya silabi katika lugha ya lugha Kiswahili Sanifu


Eleza dhana zifuatazo huku ukitoa mifano dhahiri


kiimbo

kidatu


mkazo

d)lafudhi

 











































194

 

MSAMIATI





AKK Alfabeti za Kifonetiki za Kimataifa ni jedwali ambalo


lina jumla ya sauti zote zinazotolewa na alasauti za binadamu.



Alasauti viungo mbalimbali maalum vya mwili wa binadamu

vinavyotumika katika utoaji wa sauti za lugha.


Alasogezi alasauti ambazo zina uwezo wa kujongea wakati wa


utamkaji wa sauti za lugha kama ulimi, meno chini, midomo, kaakaa laini.


Alatuli alasauti ambazo hazina uwezo wa kujongea wakati wa


utamkaji wa sauti za lugha kama ufizi, meno juu na kaakaa gumu.


Alofoni maumbo tofauti tofauti ya sauti yanayowakilisha fonimu


moja.


Alomofu maumbo tofauti tofauti au umbo jingine linalowakilisha

mofimu ile ile.


Fonetiki tawi la isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi wa


taratibu zinazohusika katika utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla.


Fonetiki Akustika tawi la fonetiki linaloshughulikia jinsi mawimbi ya sauti


za lugha yanavyoweza kusafirisha sauti kutoka kwa msemaji hadi kwenye sikio la msikilizaji.


Fonetiki Masikizi tawi la fonetiki linaloshughulikia jinsi utambuzi wa sauti

mbalimbali za lugha unavyofanyika.


Fonetiki Matamshi tawi la fonetiki linaloshughulikia jinsi sauti mbalimbali za


lugha za binadamu zinavyotamkwa kwa kutumia alasauti.


Fonetiki Tibamatamshi tawi la fonetiki linaloshughulikia matatizo


yanayoambatana na utamkaji wa sauti na jinsi ya kuyatatua.


Foni vitamkwa ambavyo vinashughulikiwa katika taaluma ya

fonetiki au (ni kipashio kidogo cha kifonetiki) bila

 




195

 

kujikita katika lugha maalum.


Fonimu kitamkwa chenye sifa bainifu za kiuamilifu na kilicho

kidogo kabisa katika lugha maalum kijengacho


maneno yenye maana tofauti tofauti na huweza kubadili

maana za maneno.


Fonolojia tawi la isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi na


uainishaji wa sauti pambanuzi katika lugha maalum.


Jozi Sahili mbinu ambayo hutumika kubainisha fonimu na alofoni


ambayo kwayo idadi ya vitamkwa katika maneno mawili au zaidi huwa sawa, isipokuwa kitamkwa kimoja hutofautiana kimatamshi.


Kidatu kiwango cha juu, cha kati au cha chini cha msikiko wa sauti


katika usemaji.


Kiimbo upandishaji na ushushaji wa mawimbi ya sauti katika

usemaji wa lugha za binadamu.


Kiini Silabi sehemu ya silabi ambayo huundwa na sauti irabu.


Kikwamizi konsonanti ambayo / ambazo hutamkwa kwa kuachia hewa


ipite katikati ya alasogezi na alatuli zinazogusanishwa kiasi cha kuifanya hewa itoke kwa kukwamizwakwamizwa lakini kwa mfululizo.


Kimadende konsonanti ambayo hutamkwa kwa kupigapiga ulimi


kwenye sehemu iliyo baada ya ufizi kwa marudio ya harakaharaka.


Kipandesauti aina yoyote ya sauti inayoweza kutolewa na alasauti za


matamshi, ni dhana ya jumla inayobeba vitu kama vitamkwa, lafudhi, kiimbo, silabi, toni na kadhalika.


Kipasuo konsonanti ambayo/ ambazo hutamkwa kwa kuibana kabisa

hewa na kisha kuachiwa ghafla.


Kitambaza konsonanti ambayo hutamkwa kwa kuutandaza ulimi na


kuruhusu hewa ipitie pembeni mwa ulimi.


Kitamkwa sauti dhahiri inayosikika wakati wa utamkaji wa maneno

na ambayo huweza kuwakilishwa kimaandishi.


Kiyeyusho sauti ambayo hutamkwa bila kubana au kuachia

 




196

 

mkondohewa, ni sauti ambayo si irabu wala konsonanti.


Kizuio Kikwamizi konsonanti ambayo hutamkwa kwa kuibana kabisa hewa na

kisha kuiachia taratibu ili itoke kwa mwendo wa


kukwamizwa.


Konsonanti sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondohewa kutoka


mapafuni kwenda nje ukipitia ama chemba ya kinywa au chemba ya pua.


Lafudhi sifa ya msikiko wa sauti ya msemaji ambayo humpa mtu

utambulisho fulani katika jamii au eneo kijiografia.


Matamshi sauti zinazosikika wakati wa utamkaji wa maneno


yanayotamkwa na mtu fulani.


Mgawo Kamilishi mbinu ambayo kwayo sauti zinagawana mazingira ya

utokeaji.


Mkazo kiwango cha nguvu itumikayo wakati wa utamkaji wa


baadhi ya silabi.


Mofimu kipashio kidogo kabisa cha lugha kilicho katika


umbo la neno au neno lenyewe chenye uamilifu ama wa kisarufi au kileksika.

Mofolojia tawi la isimu linaloshughulikia uchambuzi, uchanganuzi na


uanishaji wa maneno katika lugha.


Mpishano Huru mbinu ambayo kwayo sauti hubadilishana nafasi lakini

maana  haibadiliki.


Mpumuo sifa ya vitamkwa ambayo inahusu pumzi kali inayojitokeza


wakati baadhi ya vitamkwa vinapotamkwa.


Mwanzo Silabi konsonanti au konsonanti kapa inayotokea / zinazotokea

kabla ya kiini silabi katika muundo wa silabi.


Nazali konsonanti ambayo hutamkwa kwa kuruhusu mkondohewa


kupitia puani.


Otografia mfumo wa maandishi unaotumiwa katika lugha fulani

unaweza kuwa wa alama au michoro.


Semantiki tawi la isimu linaloshughulikia maana za vipashio


mbalimbali katika lugha.

Silabi kipashio cha kifonolojia ambacho kina kiini kimoja chenye

 




197

 

usonoranti mkubwa peke yake au na vitamkwa vingine,

kimoja au zaidi ambavyo kwa pamoja hutamkwa kama


fungu moja la sauti mara moja na kwa urahisi.


Silabi Funge silabi ambayo / ambazo huishia na sauti konsonanti na

haina mvumo wa sauti.


Silabi Huru silabi ambayo / ambazo aghalabu huishia na irabu,au huwa


irabu peke yake au konsonanti silabi peke yake (nazali silabi) yenye msikiko mkubwa na mvumo wa sauti.


Sintaksia tawi la isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi na


uanishaji wa miundo mbalimbali ya tungo katika lugha.


Tia hatua za uchanganuzi wa silabi katika njia ya matawi.


Toni kiwango cha kupanda, cha kati, cha kushuka, cha

panda – shuka au shuka – panda katika usemaji.


Ufanano wa Kifonetiki ufanano wa sifa bainifu za sauti au fonimu katika lugha.


Usawazisho mbinu ambayo inahusu umbo la ndani na umbo la nje


yanavyoweza kubainisha fonimu na alofoni.


Uwili Unaopingana kanuni inayohusu kuwepo kwa sifa mbili zinazopingana,

moja ikiwepo nyingine haiwezi kuwepo.


Uwekevu sifa za msingi za vitamkwa zinazovitofautisha vitamkwa


vya kundi moja na lingine.


Uziada sifa za ziada za vitamkwa au fonimu ambazo hutabirika

kuwepo au kutokuwepo kutokana na sifa wekevu.


Wakaa muda utumikao katika kutamka sauti yoyote ile.

 





















198

 

MAREJEO



Chomsky, N. na Morris Halle (1968) Sound Pattern of English. New York Harper & Row.


Chomsky, N (1957) Syntactic Structure. New York, Harper & Row.


Clements , G.N(1983) CV Phonology: Generative Theory of the Syllable. MIT Press, Combridge Mar



De Cortenay,  B (1895)Versuch einer Theorie Phonetischer Alternationen.Ein Kapitel ausder Psychophotek. StruBhury.LING PSYC.


Herman, P (1976) History of Linguistic Thought and Contemporary Linguistics.

Walter De Gruyter Inc. Switzerland.


Jones, D (1918) An Outline of English Phonetics. New Delhi, Kalyani Publishers. Katamba , F (1986) An Introduction to Phonology. New York, Longman Publishers Kennedy, M. S (1967) Perception of the Speech Code. University of Toronto Press.


Kihore, Y.M, Massamba ,D.P.B na Msanjila, Y.P (2003) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Sekondari na Vyuo. Dar es salaam. TUKI


Massamba,D.P.B, Kihore,Y.M na Msanjila,Y.P(2004) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Sekondari naVyuo. Dar es salaam. TUKI


Mgullu, R. S (1999) Mtalaa wa Isimu, Fonetiki na Fonolojia ya Lugha ya Kiswahili. Nairobi. Longhorn Publishers


Thorne, S (1997) Mastering Advanced  English Language. Macmillan Press Ltd.

London.


Trubetzkoy, N (1939) Principle of Phonology. University of Carifonia Press.


TUKI (1981) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press.

 















199

 

Dibaji



Azma yangu kuu ni kuandika na kuchapisha vitabu vinavyohusu uwanja wa isimu ili kukidhi haja ya wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu. Kwa mara ya kwanza kabisa nimeandika na kukikamilisha kitabu hiki kiitwacho Fonetiki na Fonolojia ya Lugha ya Kiswahili Sanifu (FOFOLUKISA). Kitabu hiki kinachambua fonolojia ya lugha ya Kiswahili Sanifu kwa mawanda mapana sana kutokana na uchambuzi yakinifu nilioufanya.


Kitabu hiki nimekiandika kutokana na kuwepo kwa uhaba mkubwa wa vitabu vya isimu ya lugha ya Kiswahili hususani katika uwanja wa fonolojia. Kwa kuanza nimeona ni muhimu kuanza na kitabu kinachohusu taaluma ya fonolojia katika lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kitakidhi haja ya wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu katika taaluma au kozi ya fonolojia. Katika kitabu hiki nimeweza kueleza vipengele mbalimbali vya taaluma ya fonolojia kwa namna nilivyofikiri kwamba itaeleweka vema kwa wahusika wa ngazi ya elimu iliyolengwa. Nimevichambua vipengele hivyo kwa kina na kutoa mifano ya kutosha.


Katika kitabu hiki dhana ya muundo wa silabi imeelezwa kwa mawanda mapana zaidi. Uchanganuzi wa silabi hizo umefanywa ili kuonesha vipashio au fonimu zinazounda silabi husika kwa kuzingatia tia na matawi ya silabi husika kimuundo.


Msomaji ataelewa vizuri miundo ya silabi kupitia uchanganuzi huo.


Ninatarajia kwamba kuchapishwa kwa kitabu hiki kutawasaidia sana wanafunzi katika kuisoma kozi ya fonolojia ya Kiswahili. Vile vile kitawasaidia wahadhiri katika kuifundisha kozi ya fonolojia ya Kiswahili. Kwa kiasi kikubwa kumekuwepo na uhaba wa vitabu vya fonolojia ya Kiswahili na hivyo kuwafanya wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu kulazimika kutumia muda mwingi kusoma vitabu vya fonolojia ya Kiingereza na kutafsiri kwenda lugha lengwa Kiswahili. Kutokana na tatizo hilo nimeazimu kuandika kitabu hiki na vingine vya sarufi ya Kiswahili Mungu akinijalia uzima.


Kwa ujumla naweza kusema kwamba kitabu hiki kimeandikwa kwa kuilenga taaluma ya fonolojia na wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi pamoja na wahadhiri wa vyuo hivyo. Kutokana na hali hii ni matarajio yangu kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watafaidika sana kwa kusoma kitabu hiki.


Mwisho napenda kusema kwamba matokeo ya kitabu hiki ni changamoto zilizonikuta nilipokuwa nikisoma shahada yangu ya kwanza katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Nawashukuru wahadhiri wote wa idara ya Kiswahili wa chuo kikuu cha Dar es salaam kwa dhati kabisa, hawa ndiyo chachu kubwa ya azma yangu ya kuandika kitabu hiki. Natoa shukrani zangu kwa wadau mbalimbali wa Kiswahili walionipa ushauri ambao umenisaidia kukamilisha kitabu hiki.



Shida .B. Masuba


Mwandishi

 








200

 

Utangulizi



Hiki ni kitabu kipya ambacho kitawsaidia wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu wa idara ya Kiswahili. Baada ya kuona vitabu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeweza kukidhi haja ya wanafunzi lakini bado nimeona kuna umuhimu wa kuandika kitabu kitakachoendana na kozi ya fonolojia katika vyuo vikuu.


Kutokana na kuliona hilo baada ya uchunguzi wa kina nikaamua kuandika kitabu hiki ambacho kitakidhi haja ya wanafunzi wa vyuo vikuu wa kozi ya fonolojia na wahadhiri pia.


Kitabu hiki kinaendana na kozi ya fonolojia kwa ujumla wake. Ni tarajio langu kuwa wanafunzi, wanazuoni na wahadhiri watafarijika kukipata kitabu hiki ambacho kitasogeza gurudumu la kuondoa adha ya vitabu vya taaluma ya fonolojia ya Kiswahili. Kutokana na mada zilizoshughulikiwa katika kitabu hiki naamini kitawasaidia sana wasomaji wa taaluma ya fonolojia ya Kiswahili.


Kitabu cha Fonetiki na Fonolojia ya Lugha ya Kiswahili Sanifu (FOFOLUKISA) kina vipengele vyote ambavyo mwanafunzi wa taaluma ya fonolojia anavyotakiwa kuvisoma. Lengo la kitabu hiki ni kuwasaidia wanafunzi, wahadhiri pamoja na wanazuoni wa lugha ya Kiswahili kutohangaika katika kuisoma au kujifunza, kuifundisha, na kuichunguza taaluma ya fonolojia ya lugha ya Kiswahili.


Kitabu hiki kina sehemu kuu zifuatavyo: sura ya kwanza ambayo inahusu fonetiki kifasili, matawi ya fonetiki na jinsi yanavyohusika katika lugha ya binadamu. Lakini pia sura hii inaeleza usuli wa fonetiki.


Sura ya pili ya kitabu hiki inahusu fonolojia kama tawi la isimu ya lugha. Inaeleza usuli wa fonolojia na waasisi wa taaluma ya fonolojia. Vile vile inaeleza uhusiano wa taaluma ya fonolojia na taaluma ya fonetiki na jinsi zinavyotofautiana.


Sura ya tatu inahusu uhusiano wa taaluma ya fonolojia na taaluma nyingine. Katika sura hii uhusiano wa taaluma ya fonolojia umeoneshwa na taaluma za mofolojia, sintaksia na taaluma ya semantiki. Kwa ujumla wake umeonesha jinsi taaluma hizi zinavyathiriana katika vipashio vyake.


Sura ya nne inahusu dhana nzima ya vitamkwa katika lugha. Katika sura hii vitamkwa vimetazamwa katika mitazamo miwili kifonetiki na kifonolojia. Vile vile aina za vitamkwa vya lugha zimeainishwa mbili ambazo ni vitamkwa vya kawaida na vitamkwa viarudhi.


Sura ya tano inahusu vitamkwa vya kawaida kwa ujumla wake katika lugha mbalimbali. Sehemu hii ya kitabu inajumuisha fonimu, alofoni na sifa zake. Mbali na hilo sura hii inaeleza mbinu zinazotumika katika uteuzi wa fonimu na alofoni.


Sura ya sita inahusu vitamkwa vya kawaida vya Kiswahili Sanifu ambavyo ni fonimu (konsonanti, irabu na viyeyusho). Sifa pambanuzi za vitamkwa hivyo, dhana ya uwekevu na uziada katika ubainishaji wa sifa pambanuzi za vitamkwa. Vile vile makundi asilia ya vitamkwa vya Kiswahili Sanifu yameelezwa, dhima ya sifa bainifu za vitamkwa na dhima ya fonimu katika lugha.


Sura ya saba inaeleza kanuni mbalimbali za kifonolojia na michakato ya kifonolojia katika taaluma ya fonolojia. Michakato hiyo ni ya usilimisho inayojumuisha kanuni za tangamano la irabu, unazalishaji, ughunishaji, muungano wa irabu na uyeyushaji.

 





201

 


Mchakato usiyo ya usilimisho ni udondoshaji. Vile vile inaeleza uandishi wa kaida au kanuni hizo za kifonolojia.


Sura ya nane inahusu vitamkwa viarudhi vya lugha kwa ujumla. Vitamkwa hivi vimechunguzwa katika lugha mbalimbali. Vitamkwa viarudhi silabi, lafudhi, kiimbo, kidatu, mkazo, matamshi,otografia na toni katika lugha mbalimbali.


Sura ya tisa na ya mwisho inahusu vitamkwa viarudhi vya Kiswahili Sanifu.Katika sura hii miundo mbalimbali ya silabi imeelezwa pamoja na uchanganuzi wake.Dhana ya mkazo,kidatu,kiimbo,lafudhi,na kadhalika vimeelezwa kwa upana wake.


Kutokana na mada au vipengele vya fonolojia vilivyoshughulikiwa na kuelezwa katika kitabu hiki,ninaamini kuwa kitabu hiki kitakuwa msaada kwa wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu.

 




















































202


No comments:

Post a Comment