Friday

Kicheko walaji wa chipsi Njombe, bei ya viazi mviringo ikishuka

0 comments

  • Bei ya chini ya gunia la kilo 100 la viazi mviringo inayotumika leo imeshuka kwa Sh10,000 kutoka Sh45,000 iliyotumika jumatano katika soko la Mwanjela jijini Mbeya. 
  • Bei ya juu ya zao hilo ni Sh120,000 katika Mkoa wa Lindi. 

Dar es Salaam. Walaji wa chipsi katika Mkoa wa Njombe leo watalala na tabasamu tupu, baada ya takwimu za Wizara ya Viwanda na Biashara kuonyesha viazi mviringo vinauzwa kwa bei ya chini kabisa katika mkoa huo ikilinganishwa na mikoa mingine Tanzania. 
Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Machi 6, 2020) na wizara hiyo zinabainisha kuwa gunia moja  la kilo 100 la viazi mviringo linauzwa kwa Sh35,000 bei ambayo ni ya chini kabisa ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.
Zao hilo limekuwa likitumiwa kutengeneza chipsi ambazo ni kivutio kwa watu wengi ambao wanapenda chakula cha haraka na rahisi kutengeneza.
Mazao makuu ya chakula hujumuisha mchele, maharage, viazi mviringo, mahindi, mtama, uwele, ulezi na ngano.
Wakati Njombe wakineemeka na bei ya viazi mviringo, wenzao wa Lindi wanauziwa gunia moja la kilo 100 la zao hilo kwa Sh120.000, bei ambayo ni ya juu kabisa inayotumika sokoni leo. 

Bei hiyo inayotumika Lindi leo ni zaidi ya mara tatu ya ile ya Njombe, jambo ambalo linawafaidisha zaidi wafanyabiashara wanaouza zao hilo katika mkoa huo uliopo kusini mwa Tanzania.
Bei hiyo ya juu inayotumika leo Lindi  imebaki ile ile kama ilivyokuwa jumatano (Machi 4, 2020).
Ifahamike kuwa utaratibu wa kutoa bei za jumla za mazao makuu ya chakula hufanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.
Hata hivyo, bei ya chini ya gunia la kilo 100 la viazi mviringo inayotumika leo imeshuka kwa Sh10,000 kutoka Sh45,000 iliyotumika jumatano katika soko la Mwanjela jijini Mbeya

No comments:

Post a Comment