*SOMO LA KWANZA*
MADA: *UCHAPAJI (PRINTING) NA UCHAPISHAJI (PUBLISHING)*
Wapendwa, karibuni sana katika somo letu la kwanza.
Maneno *Uchapaji* na *Uchapishaji* yamekuwa yakiwakanganya waandishi, wachapaji, wachapishaji, wasomaji na wanajamii kwa ujumla.
Katika somo letu hili, tutajitahidi kuona hayo maneno yanamaanisha nini na yanahusiana na kusigana wapi.
A: *Uchapaji au Upigaji chapa*
Hii ni kazi au zoezi la kuuwezesha mswada wa mwandishi kuwa kitabu baada ya kuprintiwa. Zamani, kabla ya teknolojia ya sasa, mwandishi alikuwa anaandika mawazo yake kwa kalamu ya mkono kwenye karatasi. Baada ya hapo, alimtafuta mtu wa kumchapia kwa mashine ya chapa *(taipureta- typewriter)* yale maandishi ya mkono. Huyo aliyechapa maandishi kutoka yale ya mkono, aliitwa *Mpiga Chapa.* Ile kazi iliyotokana na uandishi wa mashine ya chapa, na ile ya mkono, bado iliitwa *mswada au muswada,* ambao baadaye ulikuwa unaprintiwa na kuwa kitabu. Kwa hiyo, mwandishi angeweza kusema, *mswada wangu ulichapwa na mtu fulani.* Huu ni utata mwingine kwa sababu yule aliyeprinti kitabu, naye aliitwa Mpiga Chapa. Leo hii, kama wapo waandishi wanaoanza kuandika vitabu vyao kwa mkono, basi watakuwa wachache sana.
Hivi leo, kutokana na maarifa kuongezeka, na teknolojia kukua, mwandishi anajiandikia mwenyewe kwenye kompyuta. Baada ya hapo, andiko lake kama mswada, humwendea mhariri na baadaye humpelekea mchapaji au mchapishaji wa kitabu. Mchapishaji tutamzungumzia hapo baadaye.
Kwa ufupi kabisa, tuseme hivi, *uchapaji au upigaji chapa* kwa sasa ni kazi au *shughuli inayojihusisha na kuprinti miswada ya waandishi kuwa vitabu.* Mchapaji au Mpiga chapa kwa Kiingereza anaitwa *Printer.* Hata kama mashine ya kuchapia vitabu nayo huitwa Printer kwa Kiingereza, naye *Mchapaji au Mpiga Chapa* huitwa hivyohivyo.
Kiufundi, tunaweza kusema kwamba *Mchapaji ndiye mwenye maarifa ya kuweka mswada wa mwandishi katika karatasi maalumu na kubana (binding) ili kupata KITABU. Huyu hahusiki katika ubora wa maudhui ya kitabu. Mchapaji anachohangaika nacho tu ni kuhakikisha kwamba anaprinti kitabu kwa kufuata maelekezo ya mteja.*
Mchapaji au Mpiga Chapa wa leo tunaweza kumwainisha kwa kusema kwamba ni:
*1. Mtu anayeseti na kuprinti mswada wa mwandishi ili uwe kitabu, kwa kufuata tu maelekezo ya mteja.*
*2. Huyu hajihusishi kabisa na maudhui ya kitabu. Yeye akishaprinti kitabu na kukabidhi aliyempatia kazi basi amemaliza.*
*3. Huyu hahusiki pia na kuuza vitabu. Akimaliza kuprinti anamkabidhi vitabu mteja wake.*
*4. Huyu ndiye mwenye maarifa ya kuendesha na kuseti mashine ya kuprinti vitabu kwa kufuata maelekezo ya wateja wanaomletea miswada.*
Tumalize kwa kufupisha kwamba *Mchapaji au Mpiga Chapa* ni mtu anayeprinti vitabu. Ana maarifa ya kuseti vitabu na kuviprinti. *Huyu anapojitangaza kwenye kitabu cha mteja anatakiwa kuandika, KIMEPIGWA CHAPA NA.....au KIMECHAPWA NA.....*
****************
B: *Uchapishaji wa Vitabu*
Kama tulivyoona hapo awali, neno "uchapishaji" na "uchapaji" huwa yanawakanganya watu. Kwa uchunguzi wangu, huenda maneno haya yanawakanganya watu kwa sababu yote yana kitenzi au nomino *"chapa."* Kwa Kiingereza, neno *uchapaji* ni *printing* na neno *uchapishaji* ni *publishing.* Ni dhahiri kwamba kwa Kiingereza maneno hayo hayawakanganyi watu kama ilivyo katika Kiswahili.
*Uchapishaji basi ni nini?*
Uchapishaji kwa muktadha wetu huu, ni taaluma inayojihusisha na uzalishaji na usambazaji wa vitabu kwa umma. Ni shughuli ambayo inahusisha michakato mingi sana.
Wakati tunafafanua kuhusu neno "uchapaji" tulisema kwamba uchapaji haujihusishi na maudhui ya vitabu wala soko la vitabu husika. Lakini, *taaluma ya uchapishaji yenyewe inahusika na vyote. Yaani, usimamizi wa wazo la mwandishi kutoka ghafi mpaka kuwa kitabu na kumfikia msomaji kabisa.*
Uchapishaji unawahusisha wafuatao:
*1. Mwandishi (writer/author)* ...ππΏ *uandishi*
*2. Mchapishaji (publisher)*...ππΏ *Uchapishaji*
*3. Mpiga chapa (printer)*... ππΏ *Uchapaji*
*4. Muuza vitabu (seller)* ...ππΏ *usambazaji/uuzaji*
*5. Msomaji (reader) ...ππΏ usomaji*
WAHUSIKA WA MICHAKATO YA UCHAPISHAJI KIMAJUKUMU ππΌππΌππΌ
*1. Mwandishi*
-Huyu ndiye hubuni wazo la kitabu.
-Huandika mswada.
-Hukabidhi mswada kwa mchapishaji.
-Huingia mkataba na mchapishaji na kuutekeleza.
-Hufanya masahihisho yanayoletwa na mchapishaji baada ya wapitiaji wa mswada kupitia na kuleta ripoti.
*2. Mchapishaji*
-Huyu naye anaweza kubuni wazo la kitabu na kumtafuta mwandishi aandike (kwa baadhi tu ya vitabu).
-Hupokea mswada kutoka kwa mwandishi na kuutathmini kama unafaa na kama kitabu chake kinaweza kukidhi vigezo na kuuzika (kwa maana hii, si kila mswada unaowasilishwa utachapishwa).
-Huhariri na kusanifu mswada na kuandaa/kutafuta michoro na vielelezo vinavyohitajika katika kitabu.
-Kuandaa na kusaini Mkataba wa uchapishaji na mwandishi.
-Hutafuta mpiga chapa na kusimamia uchapaji wa mswada kuwa kitabu.
-Hugharimia uhariri, uchapaji na gharama zote za utoaji wa kitabu.
-Huzindua na kutangaza kitabu kwa umma (public).
-Husambaza kitabu kwa wauzaji na kusimamia zoezi na mapato ya uuzaji wa kitabu.
-Hutoa chapa mpya (new print) ya kitabu.
-Humlipa mwandishi mrabaha na haki zake nyinginezo.
-Husimamia na kulinda haki za mwandishi.
*3. Mchapaji au Mpiga Chapa*
-Hupiga chapa na kutengeneza nakala za kitabu kulingana na maagizo ya Mchapishaji.
-Huwa na ufundi wa kuseti kitabu na kuendesha mitambo ya kuprinti vitabu.
*4. Muuza Vitabu*
-Huyu huuza vitabu vya mchapishaji kwa wateja kwa bei za mchapishaji (siku hizi hawa wauzaji hujipangia bei kulingana na mwitiko wa soko).
-Humtumia Mchapishaji mauzo ya kitabu baada ya kukata asilimia yake (kulingana na makubaliano).
*5. Msomaji wa Kitabu*
-Hununua na kusoma kitabu.
-Huhakiki, hukosoa, huchangia
mawazo kuhusu kitabu.
*YATOKANAYO NA SOMO LA KWANZA*
A. Kumbe vitabu vyetu vingi havifuati utaratibu rasmi wa uchapishaji. Si kwamba tunakosea. Ni kwa sababu ya gharama na kuokoa muda. Michakato rasmi ya kuchapisha kitabu mara nyingi huwa zaidi ya miezi 6.
B. Wachapaji sio Wachapishaji bali wanahusika tu katika mchakato wa uchapishaji.
C. Wachapaji wanapewa maelekezo na wachapishaji (au waandishi).
D. Nikiwa na kitabu changu nikakisimamia mwenyewe mpaka kikaprintiwa, maana yake mimi mwandishi nina nafasi mbili. Yaani mimi ni *mwandishi* na *mchapishaji.*
E. Wachapishaji lazima wawe na weledi wa michakato muhimu ya uchapishaji. Lakini, mchapaji yeye anajua zaidi kuseti kitabu na kuseti mashine na kuprinti nakala za vitabu.
F. Maneno Mchapaji na Uchapishaji hutuchanganya mara nyingi kwa sababu wote wawili wanahusika kwenye utoaji wa kitabu.
*HITIMISHO*
1. Wanaoprinti vitabu wanaitwa *Wapiga Chapa* au *Wachapaji.* Hivyo, wakijitangaza kwenye kitabu chako waandike *KIMEPIGWA CHAPA NA..... au KIMECHAPWA NA.....* Kwa hiyo, wale wanaoandika kwamba *Kitabu hiki kimechapishwa na...* huwa wanakosea. Anayetakiwa kuandika hivyo ni *Mchapishaji kama yupo* na siyo Mchapaji.
2. *Kama umeandika na kuprinti kitabu bila kumpelekea Mchapishaji basi wewe ndiye Mchapishaji.* Kitabu chako kikiwa na hali hiyo, basi hakuna haja ya kuandika Mchapishaji ni nani. Ndiyo maana ukienda maktaba kuu kuomba ISBN unaulizwa nani atachapisha kitabu chako. *Ukijibu kwamba utaprinti tu na kuuza kitabu chako, basi huwa wanaandika kwamba wewe pia ni Mchapishaji (Publisher).* Shida kidogo ni kwamba je, utaaminika sokoni kama hauko chini ya Mchapishaji? Lakini, ukiandika mswada na kuupitisha kwenye michakato rasmi ya Uchapishaji, lazima kitabu kioneshe ni Kampuni gani imekichapisha.
3. Mchapishaji akiwa anajiweza kiuchumi, anaweza kuwa na mashine zake za kuprinti vitabu. Akiwa na uwezo huo basi atakuwa ni *Mchapaji na Mchapishaji kwa wakati mmoja.* Hata hivyo, wachapishaji wengi hawana mashine. Hivyo, wanamtegemea Mchapaji awasaidie katika michakato ya kufanikisha upatikanaji wa kitabu.
*MAMBO NI MENGI SANA. HAPA NIMEFUPISHA TU ILI WALAU TUPATE MAARIFA MUHIMU. NIMEKUANDIKIENI KITABU CHA MAMBO HAYA. KITATOKA HIVI KARIBUNI!*
Kama kuna swali lolote naomba niulizwe. Lakini, kabla ya kuuliza hakikisha kwamba umesoma somo vizuri kabisa.
**********
KARIBUNI KWA MJADALA. *BAADA YA KUSOMA SOMO HILI, UMEJIFUNZA NINI?*
*© Leonard Bakize* (09/03/2020)
*(Kwa hisani ya EWCP na Ushirikishanaji Maarifa)*
===================