Tuesday

LAHAJA ZA KISWAHILI

0 comments


TUKI (2004), wanadai kwamba lahaja ni tofauti katika matamshi, maumbo na matumizi ya maneno katika maeneo mbalimbali kwa lugha yenye asili moja.

Aidha Msanjila na wenzake (2009), wanadai kuwa lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi huesabiwa kuwa ni lugha isipokuwa inatofautiana katika baadhi ya vipengele mbalimbali kama vile lafudhi, fonolojia, miundo. Lakini fasili hii inaibua utata ambao ni lugha, wanatumia istilahi lugha kufasili lahaja, kwani lahaja ni sehemu ya lugha.

Kwa ujumla, lahaja ni tofauti ndogondogo za kiusemaji zinazojitokeza katika lugha moja. 

Lugha ya kiswahili ina lahaja nyingi na kiswahili sanifu ni mojawapo ya lahaja hizo, katika lugha ya kiswahili uainishaji wa lahaja umezingatia utengano wa kijiografia. Mfano pemba- kipemba, unguja – kiunguja, kipate- pate, kimakunduchi- makunduchi. Aidha lahaja nyingi zinapatikana katika upwa wa Afrika mashariki.

Wataalamu kama Nurse na Spear (1985), wanagawa lahaja za kiswahili katika makundi mawili, lahaja za kaskazini na kusini, lahaja za kaskazini ni Chimiini, kibajuni, kipate, kiamu, kimvita, kijomvu, chichifundi na lahaja za kusini kuna kitumbatu, kimakunduchi, kipemba, kiunguja, kimtang’ata , kivumba, kimafia, kimgao, kimakunduchi.

Aidha Iribemwangi na Mukhawa (2010), wanazigawa lahaja katika makundi mawili ambayo ni lahaja za kijamii ambazo tunapata lahaja kama vile lahaja za kijinsia, lahaja za kidini, lahaja za kitabaka, na lahaja za kiuchumi, pili ni lahaja za kijiografia hapa wanataja mfano wa lahaja hizo kama vile lahaja ya kipemba, kiunguja, kiamu, kipate hizi zinatengwa kutokana na mahali zinapotumika, tatu ni lahaja za kihistoria ambapo wanaeleza kwamba hapa tunapata lahaja kutokana na historia, mfano wa lahaja hizo ni lahaja ya kingozi. Lahaja za kiswahili zinatofautiana kati ya sehemu na sehemu katika vipengele tofauti tofauti kama vile;

Msamiati, TUKI (1990), wanadai kwamba msamiati ni jumla ya maneno yanayotumika katika lugha fulani, baadhi ya lahaja za kiswahili zinatofautiana katika kipengele cha msamiati usio kuwa wa msingi,

                      Mfano

                       Chimbalazi                                          kimvita

                       Chala- kidole                                     chanda-kidole                                                                     

                       Kingare                                                  kimvita

                       Biti – bichi                                           danga- bichi

    

Aidha, lahaja za kiswahili hutofautiana katika kipengele cha semantiki, Richards (1985), wanadai kwamba semantiki ni stadi ya maana.

               Mfano,

                       Kimakunduchi                                      kiunguja

                       Bonge- mwanamke                                mtu mnene

                       Asa- kuacha ziwa                                   kutoa onyo  

                       Tembo- uchi wa mwanamke                  Mnyama

Hivyo, kutokana na data hiyo ni wazi kwamba maana ya maneno kati ya lahaja moja na lahaja nyingine unatofautiana.   

Aidha utofauti mwingine upo katika kipengele cha mofolojia kati ya lahaja moja na nyingine Aurbach (1971), anadai kuwa mofolojia ni neno linalotumiwa kuainisha utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa maneno.

                                    Kivumba                                Kiunguja

                                  Wampigani                             wamempiga nani

                                  Nyumba yani                          nyumba ya nani

Hivyo kutokana na mifano hapo juu ni dhahiri kwamba lahaja ya kivumba inayozungumzwa sehemu ya wasini na vanga  inatofautiana na lahaja ya kiunguja kimaumbo.

Pia , fonolojia kati ya lahaja moja na nyingine zinatofautiana. chunguza mifano kutoka lahaja ya kivumba

                                     Lahaja ya kivumba                     Kiunguja

                                               Wera                                        waita

Katika mfano hapo juu tunaona kwamba lahaja ya kivumba inayozungumzwa vanga inatofautiana na kiswahili sanifu.

Aidha lahaja hutofautiana na kiswahili sanifu katika kipengele cha msamiati kama vile

                                   Mfano,

                                           kipemba                                    kiswahili sanifu

                                             Mfereji                                       bomba 

Aidha lahaja za Kiswahili zinatofautiana katika kipengele cha semantiki,

                              mfano        

                                           Kimakunduchi                          kiswahili sanifu

                                            Bonge-mwanamke                       mtu mnene

                                            Asa- kuacha ziwa                         kutoa onyo

Pia lahaja hutofautiana na kiswahili sanifu katika kipengele cha mofolojia.

                                    Mfano                                                                                                            

                                            Kingazija                                   kiswahili sanifu

                                               Soha                                                  shoka

                                               Hari                                                   kati

Aidha lahaja nilizozitumia katika kazi hii ni lahaja za kijiografia kwa kuzingatia namna ambavyo zilivyoainishwa katika maeneo tofauti, aidha Nurse na Spear (1985), anazigawa lahaja za kiswahili katika makundi mawili lahaja za kaskazini ni kama vile Chimiini, kibajuni, kipate, kiamu, kimvita, kijomvu, chichifundi na lahaja za kusini kuna kitumbatu, kimakunduchi, kipemba, kiunguja, kimtang’ata , kivumba, kimafia, kimgao, kimakunduchi.

Kwa ujumla, lahaja za Kiswahili sanifu huweza kutambuliwa kwa kipengele cha msamiati wa msingi ingawa kuna vipengele vingine kama vile lafudhi, mofolojia , semantiki, fonolojia, pia lahaja zimesaidia sana katika Kiswahili sanifu.                                                                



































                                                                  MAREJELEO

Aubach, et al (1971) Transformational Grammar : A Guide for Teachers. Research Associates                                        Inc Washngton

Habwe J & Karanja P (2007) Misingi ya sarufi ya Kiswahili: Nairobi: phoenix publishers

Iribemwangi, P.I & Mukhwana A (2010) Isimu jamii: Kenya: focus publishers ltd.

Massamba, D. Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) Isimu jamii sekondari na vyuo. TUKI.

Nurse, D na Spear (1985) The Swahili Reconstructing the History and Language of an African

                                   society. Philadelphia University of Pennsy Ivania.

Richard et al (1985) Dictionary of applied linguistics. Longman: harlow.

TUKI (2013) Kamusi ya Kiswahili sanifu: Dar es salaam: Oxford University Press.

                 

No comments:

Post a Comment