Kocha mzoefu na ambaye aliwahi kuichezea timu ya soka ya Simba Sports Club Madaraka Bendela amesema timu hiyo imefanya haraka kuachana na Kocha Joseph Omog kwani bado alikuwa akihitajika katika timu hiyo.
Madaraka ambaye kwa sasa anaishi Jijini Arusha, amesema toka Omog anaingia Simba mwaka jana hadi anaondoka rekodi zake hazikuwa mbaya sana hivyo ilipaswa Simba waendelee kumvumilia na kumpa muda zaidi.
-Omog toka anakuja hadi anaondoka amewaacha Simba wakiwa bado wapo nafasi nzuri, amewaacha wakiwa wanaongoza ligi na kama wangeendelea kumuacha na kumpa muda ukizingatia na usajili ambao wameufanya labda angeweza kupata matunda mazuri kwa hapo baadae," amesema.
Ushauri kwa makocha.
Madaraka ambaye anasifika kwa kuibua vipaji vingi vya soka nchini kikiwemo cha Erasto Nyoni, ametoa ushauri pia kwa makocha wa mpira kujua sehemu wanayoenda kufanya kazi kabla ya kukubali kazi hiyo.
Amesema kila timu inakuwa na falsafa tofauti ya uchezaji mpira hivyo kama mwalimu ukitambua hilo wakati mwingine inakuwa rahisi kwenda sambamba na matakwa ya timu husika.
-Simba Wanastaili yao, wanautamaduni kama timu katika uchezaji, na Omog naye anastaili yake katika ufundishaji tofauti na wanavyotaka Simba, ukiangalia Simba ni ile timu ambayo inataka kuchezea mpira muda wote hawajinyimi kufunguka, lakini Omog anafundisha zaidi namna ya kujilinda," amesema.
Simba iliachana na Kocha Omog Jumamosi ya Disemba 23 baada ya kutolewa mapema kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup na timu ya daraja la pili Green Warriors. Simba walifungwa kwa penati 3-4 baada ya muda wa dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo ambao ulifanyika katika uwanja wa Azam Complex Ijumaa Disemba 22.
Rekodi za Omog.
Mpaka Omog anaondoka Simba alikuwa ameiongoza timu hiyo katika michezo 79 ambapo katika michezo hiyo ameshinda michezo 53, akitoka Sare mechi 16 na kufungwa michezo 10.
Lakini pia alifanikiwa kuipitia timu hiyo ubingwa wa FA, na kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi timu hiyo itashiriki michuano ya kimataifa.