Saturday

PACHA WASAMATTA STAAS KUTUA SIMBA

0 comments



Mbwana Samatta


Kama ulivyosikia, kuwa Simba ipo katika mpango wa kumsajili straika wa Dhofar SC ya Oman, Elias Maguri, lakini kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog  ameomba apewe video zake ili aweze kujiridhisha zaidi.

Simba inataka kumsajili Maguri ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji ili iweze kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu Bara na katika Kombe la Shirikisho la Afrika mwakani.

Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Simba ambaye ameomba kutotajwa jina lake, amebonga na masshele blog 
na kusema baada ya kufanya mazungumzo na Maguri walimpelekea taarifa Omog kuhusiana na mchezaji
huyo lakini akawaambia hamjui vizuri hivyo  wamtafutie video zake ili aweze kuona makali yake uwanjani.

“Kwa hivyo hivi sasa tunatafuta video ili tumpe amwone mchezaji huyo ambaye tunaamini kuwa kama tutamsajili basi anaweza kutusaidia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupambana,” alisema kiongozi huyo.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo aliongeza kuwa: “Ukiachana na suala hilo la Maguri pia kocha ametaka tutafute beki mmoja wa kati, kipa pamoja na winga mmoja, jambo ambalo tutaanza kulifanyia kazi
baada ya mechi yetu dhidi ya Lipuli.”

Alipoulizwa Omog kuhusiana na suala hilo alisema kuwa kwa sasa hawezi kusema chochote kuhusiana na usajili kwani akili yake sasa imetawaliwa na mchezo wa kesho dhidi ya Lipuli.