Mchezaji wa klabu ya Simba Sc, Said Hamis Ndemla amefanikiwa kufuzu majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya.
Katika klabu ya Eskilstuna ya Sweden. Ndemla aliyekuwa nchini Sweden tangu november 11 kwa majaribio kwenye klabu ya hiyo anayochezea Mtanzania Thomas Ulimwengu wakala wa mchezaji huyo huko sweden amemfahamisha wakala wake Jamal Kasongo na klabu ya simba kuhusu kufuzu kwa Ndemla.
Ndemla anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu novemba 27 na mara baada ya kurejea klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka la kulipwa