Thursday

UWAVITA CHAPATA VIONGOZI WAPYA

0 comments

 


Chama Cha umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania (UWAVITA) kilichotamba miaka hiyo na kufariki baadaye Sasa kipo katika mchakato wa uhuishaji ambapo wanachama wake wamechagua viongozi wapya watakao ingiza jahazi la chama hicho, Cha waandishi wa viatabu Tanzania 

Viongozi waliochaguliwa  kwa kupigiwa kura Ni Hawa wafuatao

  1. Mwenyekiti wa uwavita
  2. Makamu mwenyekiti UWAVITA
  3. Katibu mkuu uwavita
  4. Katibu msaidizi UWAVITA
  5. Mhariri mkuu UWAVITA
  6. Mhariri msaidizi UWAVITA
  7. Mweka Hazina UWAVITA
  8. Mwenezi UWAVITA
Ambaoo viongozi Hawa ndio walioshinda kwa idadi ya kura na kutangazwa rasmi kuwa Viongozi wapya wa Uwavita uongozi ambao utadumu kwa miaka mitatu kutoka January 2024.


Profesa Mulokozi , mwandishi, na profesa mstaafu wa Taasisi ya Taaluma za kiswahili TATAKI, pia mwenyekiti wa zamani wa Uwavita atia neno "Hongereni nyote mliochaguliwa kutuongoza. Ni imani yangu kuwa mtaongoza Chama kwa juhudi na maarifa huku mkizingatia Katiba na Kanuni za Chama.  Msisite kuomba ushauri au msaada wakati wowote mtakapouhitaji. Mulokozi"

Profesa Kahigi naye alikuwa na Haya ya kusema " Nami niwapongeze wote kama ifuatavyo:  

1. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Prof. Mulokozi, 
2. Kamati ya Kufufua Chama, 
3. Tume ya Uchaguzi,
4.  Wanachama walioomba kuongoza UWAVITA,
5. Wanachama waliochaguliwa kuongoza UWAVITA, 
6. Wanachama waliopiga kura, 
7. Wanachama ambao wamekuwa mbele katika kuipigania wakati wote (hasa Chama kilipopitia wakati mgumu).

Ninaunga mkono rai ya Prof. Mulokozi kwamba viongozi msisite kuomba ushauri kila mnapouhitaji, kwani baadhi ya viongozi wa zamani bado wapo. 

Mwisho, Mhariri Mkuu anione nimkabidhi baadhi ya nakala za Kijarida cha UWAVITA cha miaka ya nyuma; huenda akajifunza mawili matatu"

Hivyo ndivyo uchaguzi wa chama Cha waandishi wa vitabu Tanzania UWAVITA mpya ulivyokamilika.

No comments:

Post a Comment