Tuesday

WAALIMU 8 WATIMULIWA KISA Q-NET

0 comments

 



WALIMU wanane wilayani Geita mkoani Geita wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za utoro uliotokana na kujikita kwenye shughuli za Kampuni ya Mtandao wa Biashara maarufu kama Q-NET na hivo kutelekeza majukumu yao ya msingi.

-

Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Geita, Sitta Mussanga amewaambia waandishi wa habari kuwa uamuzi huo umefikiwa na Kamati ya Tume hiyo baada ya kufuatilia na kujiridhisha utoro wa walimu hao ulitokana na wao kuacha kazi na kwenda Q-NET ambako waliamini kuna maslahi mazuri zaidi ya wajibu wao darasani.

-

Walimu waliofukuzwa ni Kalokola Hurbano na Critus Mkombozi kutoka shule ya sekondari Kivukoni, Stella Ernest wa shule ya msingi Kivukoni, Revocatus Kimasa wa Shule ya msingi Mkoani, Aneth Bikombo wa shule ya msingi Nyantorotoro.

-

Wengine ni Mahemba Peter kutoka shule ya msingi Bukayaga, Benjamin Petrus kutoka shule ya msingi Mtakuja pamoja na Jijaga Galima wa Shule ya msingi Lubanda ambao walishatakiwa na mtuhumiwa kwa nyakati tofauti.

-

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Wilayani Geita, Samwel Dotto amekiri taarifa za kamati ya nidhamu ya Tume ya Utumishi ya Walimu kuwafuta kazi walimu waliorubuniwa na Q-NET ambapo aliiomba serikali kuichunguza kampuni hiyo. 

No comments:

Post a Comment