TANGAZO
Kozi ya kufundisha Kiswahili wageni
Asasi ya swahilispeaking.co.tz (Dar es Salaam, Tanzania), inayojishughulisha na ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni inatarajia kutoa mafunzo mafupi kwa mtu anayependa kujua namna ya kufundisha wageni. Ni asasi binafsi ya KISWAHILI kwa WAGENI, ni asasi bobevu katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni.
Tunafundisha walimu wa kufundisha wageni na pia tunafundisha wanafunzi wageni. Kwa mtazamo wetu "mzawa" anaweza kuwa "mwalimu wa mgeni" kama atapenda kupata maarifa ya kufundisha, mada za kufundisha, na mbinu za kufundisha. Mgeni ni mtu yeyote ambaye hafahamu Kiswahili na anataka kujua na kukitumia.
*Walimu:*
Tunao walimu waliobobea na wazoefu ambao wamemakinikia katika eneo la ufundishaji Kiswahili kwa wageni. Walimu hawa wana tajiriba na uzoefu mbalimbali wa zaidi ya miongo miwili. Walimu wamefundisha wanafunzi kutoka katika mabara mbalimbali duniani yakiwamo Ulaya, Amerika, Afrika, Australia, na Asia. Gharama zetu ni nafuu sana na tunahakikisha umepikwa na umepikika katika eneo hili la kufundisha wageni.
*Kozi:*
Kozi yetu inatolewa katika sehemu tatu, ambazo ni:
Ngazi ya kwanza,
Ngazi ya pili na
Ngazi ya tatu.
*Ada:*
Kila ngazi ada yake ni shilingi za Tanzania 100,000/= *(Kshs.5,000/=)*
Baada ya kila ngazi utapata cheti cha ushiriki. Kozi nzima ya namna ya kufundisha wageni ni Tsh.300,000/= *(Kshs15,000)*
*Mada*
Mafunzo haya yatajumuisha mada mahususi kwa kila ngazi sambamba na hilo pia watafundishwa mbinu za kutafuta masoko;mbinu za kupata wateja; mbinu za kufundisha wanafunzi wageni kwa kuzingatia viwango vyao; mbinu za kuwafanya wanafunzi wafurahie darasa lako; mbinu za kutathmini wanafunzi wageni kwa kuzingatia viwango vyao.
*Zana za kujifunzia:* Kila mshiriki anayetaka kushiriki mafunzo haya mafupi inatakiwa awe na vitabu viwili: kimoja cha mwalimu na kimoja cha mwanafunzi. Ni muhimu kila mshiriki kuwa na zana hizi kwa kuwa kutakuwa na kazi za nyumbani ambazo kila mshiriki atatakiwa kufanya kazi binafsi na kutoa mrejesho siku inayofuata.
Kila kitabu ndani yake kina mada za kuwafundisha wanafunzi wa ngazi zote, ya kwanza, ya pili, na ya tatu. Kwa hiyo ni kitabu kimoja chenye vitabu vitatu ndani yake.
*Vitabu:*
Kipo kitabu cha mwanafunzi na kitabu cha mwalimu. Kitabu cha mwanafunzi ni Tsh 20,000/= *(Kshs.1,000/=)* kama bei ya punguzo; na kitabu cha mwalimu ni Tsh 20,000/= *(Kshs.1,000/=)* kama bei ya punguzo.
*Lini:*
Mafunzo yatafanyika kwa awamu tatu:
Ngazi ya kwanza ni kuanzia tarehe *8/8/2022 - 12/8/2022*
Ngazi ya pili ni kuanzia tarehe *15/8/2022 - 19/8/2022*
Ngazi ya tatu ni kuanzia tarehe *22/8/2022 - 26/8/2022*
*Muda:*
Kuanzia saa 12:00 jioni (6pm) saa za Afrika Mashariki hadi saa mbili Usiku. Saa moja itakuwa ni ufundishaji wa nadharia; nusu saa itakuwa ni mazoezi kwa vitendo kutoka kwa washiriki; nusu saa ya mwisho ni mawasilisho ya kazi ya nyumbani/kazi binafsi.
*Njia ya ufundishaji:*
Mafunzo yatafundishwa kwa njia ya masafa. Hivyo kila mshiriki ajisajili kwenye akaunti ya Zoom na Google. Mafunzo haya yatafundishwa kupitia njia hizo.
*Vyeti*
Mwisho wa kozi katika kila ngazi mshiriki aliyehitimu atapokezwa cheti.
*Mawasiliano na usajili* :
Kwa yeyote anayependa kujifunza namna ya kuwafundisha wageni atutumie ujumbe kwa nambari +255737872994
Utumapo ujumbe 👆🏾andika taarifa zifuatazo:
1. Jina lako
2. Elimu ya sekondari -Jina la Shule
3.Ufaulu wa somo la Kiswahili sekondari
4. Elimu ya Sekondari ya Juu - jina la shule
5. Mchepuo uliosoma kidato cha tano na sita
6. Diploma uliyosomea, na chuo ulichosoma na mwaka uliohitimu
7. Cheti ulichosomea, mwaka uliomaliza, na chuo ulichosoma
8. Shahada/digrii uliyosoma, programu uliyosoma, na mwaka uliomaliza.
*_TANBIHI:_*
_Hata kama kuna nambari/sehemu hapo juu huhusiki nazo - wewe tutumie sifa zako kwa kuwa ufundishaji wa wageni uko katika ngazi tofauti tofauti_ .
*Muhimu*
Taarifa hizi ni muhimu kwetu kwa kuwa zitatusaidia kupata watu wa kushirikiana nao kuendeleza kazi hii baada ya kuhitimu mafunzo haya.
*KARIBU SANA*
+255737872994