Kiswahili ni Kibantu
Vipengele vinavyotumika katika kuihalalisha
nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kibantu ni
ushahidi wa ki-Isimu, ushahidi wa ki-Historia na
kuichunguza lugha ya Kiswahili katika mfumo
mzima wa historia ya mgawanyiko wa kusambaa
kwa lugha za ki-Bantu. Wataalamu wa nadharia
hii wanahitimisha kwa kudai kwamba Kiswahili ni
mojawapo kati ya lugha katika jamii kubwa ya
lugha za ki-Bantu.
Baadhi ya wataalamu muhimu wanaoiunga mkono
nadharia hii ni Prof. Malcon Guthrie, Dkt. C.
Meinholf na Dkt. C. Rohl na Prof. Clement
Maganga.
Profesa Malcom Guthrie ni mtaalamu
(mwanaisimu) mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha
London, Uingereza. Alitumia miaka 20
kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha za
Kibantu zilizoko katika eneo lote ambalo hukaliwa
na wabantu. Sehemu hii ni ile ambayo inajulikana
kama Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alifanya uchunguzi wa mashina/mizizi (viini) ya
maneno 22,000 kutoka lugha 200 za Kibantu.
Katika uchunguzi wake alikuta mizizi (mashina)
2,300 imezagaa katika lugha mbalimbali za
Kibantu na Kiswahili kikiwemo. Mashina/mizizi
500 yalilingana katika lugha zote 200.
Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za
Kibantu. Mashina haya yalikuwa ya asili moja.
Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi
Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na
Kikongo kwa asilimia arubaini na nne (44%).
Katika kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina
hayo 500 yaliyomo katika kila lugha, mgawo
uliojitokeza ulikuwa kama ifuatavyo:
Kiwemba kizungumzwacho Zambia -
54%
Kiluba kizungumzwacho Katanga -
51%
**Kikongo kizungumzwacho Zaire -
44%**
**Kiswahili kizungumzwacho Afrika
Mashariki 44%**
Kisukuma kizungumzwacho Tanzania
41%
Kiyao kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji -
35%
Sotho kizungumzwacho Botswana
- 20%
*Kirundi kizungumzwacho Burundi -
43%*
Kinyoro kizungumzwacho Uganda -
37%
Kizulu kizungumzwacho Afrika Kusini -
29%
Baada ya kupata matokeo haya, Profesa Malcom
Guthrie anaiunga mkono nadharia hii ya kwamba
Kiswahili ni ki-Bantu kwa kudai kwamba:
(i) Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa
wageni;
(ii) Anaonyesha kwamba Kiswahili kina
uhusiano mkubwa na lugha za Kibantu;
(iii) Mwisho anasema Kiswahili kilianzia Pwani ya
Afrika Mashariki.
Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl: Wataalamu
hawa wanaamini kwamba:
(i) Wakati wa utawala wa Shirazi katika
upwa wa mashariki ya Afrika kulikuwa na
kabila la Waswahili;
(ii) Kabila hili ni dhuria ya Wazaramo wa
leo.
(iii) Kwa kuwa hawa Wazaramo walikuwa
wamezaliwa katika harakati za kibiashara,
kwa hivyo wakafuata nyayo za wazazi
wao.
(iv) Lugha yao ilikuwa ya aina ya ki-Bantu.
(v) Kwa kuwa Wabantu ni wengi zaidi
kuliko jamii ya makabila mengine, lugha
yao ya Kiswahili ikaanza kutumika na
kuenea katika makabila mengine,
hususan katika ukanda wa pwani ya
Afrika Mashariki.
(vi) Baadaye, Waswahili hawa hawa
wakafanya biashara na wageni waliokuja
kuvinjari Afrika Mashariki, hususan
Waarabu, Washirazi, Wamalaysia, Wahindi
na Wareno ambao tayari walikuwa
wamefurika katika pwani hii ya Afrika
Mashariki miaka kadhaa kabla.
(vii) Vifaa na majina ya vitu vya biashara
vya wageni hao vikaselelea na kuingizwa
katika mfumo wa lugha hiyo ya Waswahili
ambayo ni ki-Bantu.
Madai ya nadharia hii yakichunguzwa, tunagundua
kwamba inazingatia mitazamo miwili yaani,
mtazamo wa ki-Isimu na mtazamo wa ki-Historia.
Kwa mantiki hii, nadharia hii inaelekea kukubalika
na wataalamu wengi kuwa ndiyo sahihi kuhusu
asili au historia ya Kiswahili.
Profesa C. Maganga, na uthibitisho wake kwamba
Kiswahili ni ki-Bantu. Kama tulivyoona, lugha ya
Kiswahili ilifanyiwa utafiti na uchambuzi na
wanataaluma kadhaa kwa madhumuni ya
kuiainisha kama ilikuwa yenye misingi ya ki-Bantu
au la. Prof. Maganga alifanya uchambuzi wa ki-
Isimu na wa ki-Historia kuhusu lugha hii. Matokeo
ya utafiti wake wa ki-Isimu kuhusu lugha ya
Kiswhili (au lugha kwa ujumla) unadhihirisha
mambo mengi, mojawapo ni asili ya lugha hiyo.
Amethibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya
Kibantu; na kwa hivyo, kuthibitisha kwa ushahidi
thabiti hoja ya Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl
kama tulivyoieleza hapo juu.
(i) Ushahidi wa Kiisimu
(a) Msamiati
Matokeo ya utafiti alioufanya kuhusu msamiati wa
Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote
yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugha
ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% ni
lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za
kigeni kama vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani,
Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chake ni
kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu
hautofautiani.
Mfano:
Kiswahili Kindali Kizigua Kijita
Kikurya Kindendeule
Mtu Umundu Mntu
Omun Omontu Mundu
Maji Amashi Manzi Amanji
Amanche Maache
Moto Umulilo Moto Omulilo
Omoro Mwoto
(b) Tungo (Sentesi) za Kiswahili
Miundo ya tungo (sentesi) za maneno ya Kiswahili
zinafanana sana na miundo ya tungo za maneno
ya ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za
ki-Bantu zina kiima na kiarifu.
Mfano:
Lugha za Kibantu
Kiima kiarifu
Kiswahili
Juma anakula ugali.
Kizigua
Juma adya ugali.
Kisukuma
Juma alelya bugali
Kindali
Juma akulya ubbugali.
Kijita
Juma kalya ubusima.
Kindendeule
Juma ilye ughale.
(c) Ngeli za Majina
Wanataalamu wanakubaliana kuhusu ngeli za
majina kwa mujibu wa:
maumbo ya nomino (umoja na wingi wa majina)
pamoja; na
upatanisho wa kisarufi katika sentesi.
Kigezo cha maumbo ya majina: Kigezo hiki
hufuata maumbo ya umoja na uwingi katika
kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika
lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata
mkondo wa umoja na uwingi. Majina ya lugha ya
Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yana
maumbo dhahiri ya umoja na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu
Umoja Wingi
Kiswahili mtu -
watu
mtoto
- watoto
Kikurya omanto -
banto (abanto)
omona - bana (abana)
Kizigua mntu -
bhantu
mwana
- bhana
Kindali mundu -
bhandu
mwana
- bhana
Kindendeule mundu -
βhandu
mwana
- βhana
Kigezo cha upatanisho wa kisarufi katika sentesi:
Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo
kati ya kiima (jina na viambishi awali vya nafsi)
na vivumishi katika vitenzi vya Kiswahili na ki-
Bantu. Vivumishi, majina pamoja na viambishi
hivyo vya vitenzi hubadilika kutokana na maumbo
ya umoja na uwingi.
Mfano:
Lugha za Kibantu Umoja -
Wingi
Kiswahili Baba analima -
Baba wanalima
Kindali Utata akulima -
Abbatata bbakulima
Kikurya Tata ararema -
Batata(Tata)bararema
Kijita Tata
kalima - Batata
abalima
Kindendeule Tate ilima -
Akatate βhilima
(d) Vitenzi vya Kiswahili na Kibantu
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya
Kiswahili na vile vya lugha zingine za ki-Bantu.
Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni:
Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na mwanzo au
mwisho wa vitenzi, kama ifuatavyo:
Viambishi: vitenzi vya lugha ya Kiswahili na vya
lugha zingine za ki-Bantu hujengwa na mzizi
(kiini) pamoja na viambishi vyake vya awali na
vya tamati.
Mfano:
Kiswahili - analima = a –
na – lim - a
Kiikuyu - arerema = a
– re – rem–a
Kindali - akulima = a
- ku – lim – a
1 - 2 - 3 - 4
Sherehe:
1 - Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi.
2 - Kiambishi awali cha njeo (wakati uliopo).
3 - Mzizi/Kiini.
4 - Kiambishi tamati.
Mnyambuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko wa vitenzi
vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya
lugha za ki-Bantu.
Mfano:
Kiswahili - kucheka -
kuchekesha - kuchekelea.
Kindali - kuseka -
kusekasha - kusekelela.
Kibena - kuheka -
kuhekesha - kuhekelea.
Kinyamwezi - kuseka -
kusekasha - kusekelela.
Kikagulu - kuseka -
kusekesha - kusekelela
Mwanzo wa vitenzi: Vitenzi vyote vya Kiswahili
na vile vya lugha za ki-Bantu huanza na
viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi, kama
ifuatavyo:
Mfano:
Kiswahili - N i-nakwenda
Kihaya - N i-ngenda
Kiyao - N- gwenda
Kindendeule - Ni- yenda
Mwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-
Bantu na Kiswahili huishia na irabu –a.
Mfano:
Kiswahili kukimbi-a - kuwind-
a - kushuk-a
Kindali kukind-a - kubhing-
a - kukol-a
Kisukuma kupil-a - kuhwim-
a - Kutend-a
Kisunza kwihuk-a - kuhig-
a - kising-a
Kindendeule kuβhutuk-a - kuhwim-a
- kuhuk-a
tafiti wa Prof. Maganga kuhusu ushahidi wa ki-
Isimu wa kuthibitisha kama Kiswahili ni ki-Bantu
au la ungeweza kuelezwa kimuhtasari kwa mifano
mingine ifuatayo:
Mfano wa 1:
Lug
ha
Sentesi
Kisw
ahili
Kipa
re
Kind
amb
a
Kich
aga
Kiha
ya
Kika
guru
Kind
end
eule
Jon
go
Jon
go
Jon
go
Jon
go
Jon
go
Jon
go
Jon
go
anaf
uga
eris
ha
kafu
gha
nao
he
n’af
uga
kach
ima
ifug
a
mbu
zi
mbu
ji
men
e
mbu
ru
emb
uzi
m’
ehe
mbu
hi
kuk
u
nku
ku
ngu
ku
ngu
ku
enk
oko
ngu’
ku
ngu
ku
na
na
na
na
n’
na
na
ng’o
mbe
ng’o
mbe
sen
ga.
umb
e
ente
nn’o
mbe
ng’o
mbe
Katika mfano huu inaonekana kwamba mpangilio
wa maneno katika sentesi una ufanano kwa
sababu katika kila sentesi kuna kiima na kiarifu.
Katika kiima kuna nomino, yaani jina la mtenda
(Jongo) na katika kiarifu kuna kitendo
kinachofanyika na nomino mtendwa. Pia nafasi ya
viunganishi ni ile ile kwa lugha zote
zilizoonyeshwa katika mfano huu.
Kuna mfano mwingine wa ufanano wa mpangilio
huu.
Mfano wa 2:
Lugha Sentesi
Kiswahili
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kizigua
Sitamkuta kesho
Timushangemu nyenkya
Natusanga intondo
Tumuhanga fadyu
Nesikemkiche yavo
Sirambila luvi
Katika sentensi hizo mpangilio wa maneno una
ufanano kwa sababu kila sentensi ina kiima na
kiarifu chenye kitenzi na kielezi. Pia kiambishi cha
nafsi cha nomino ya mtenda kinajitokeza
mwanzoni mwa neno la kwanza la kila sentesi.
Sitamkuta; Timushangemu; Na tusanga;
Tumuhanga;
Ne sikamkiche; Si tambila.
Viambishi hivyo vya nafsi ya mtenda pia
vinaonyesha hali ya ukanushi katka kila sentesi
na nafasi yake ni ile ile kwa kila sentesi.
Viambishi vya urejeshi navyo vinajitokeza katika
kitenzi cha kila sentesi.
Viambishi {m}, {m}, {ti}, {tu} sita mkuta,
timushangemu, na tu sanga, tumuhanga,
nesikamkiche, na sita mbwila ni vya urejeshi;
vinawakilisha nomino mtendwa.
Kwa hivyo, hali hii inadhihirisha kwamba miundo
ya sentensi hizi inafanana na vitenzi vyake vina
tabia mbalimbali, kama vile:
(i) kubeba viambishi vya nafsi, mtenda na
mtendwa,
(ii) kuonyeshga hali ya ukanushi njeo za
wakati na kitendo kinachofanyika.
Mfano wa 3:
Lugha Sentesi
Kiswahili
Kizigua
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kindendeu
le
Akija mwambie
anifuate
Akeza umugambe
anitimile.
Kalaija
omugambile
ampondele
Ulu nahali
anikubije
Newaja mwele
ang’onge.
Ekiza umti
aniratere
Anda ahikite
n’nongerera
angobhekeraye
Katika sentesi hizo inaonekana kwamba sentesi
zote zinafanana kimpangilio. Pia maneno yake
yanakubali uambishaji, kwa mfano:
(i) Katika maneno ya mwanzo:
akija, akeza. kalaija, akuja, newaja, ekiza,
herufi zilizopigiwa vistari ni viambishi vya
nafsi vinawakilisha dhana ya mtenda.
(ii) Vivyo hivyo katika maneno:
anifuate, ampondele, anitimile, ang’nge,
aniratere, angobhekeraye, viambishi
vilivyoko katika viarifu vya sentesi hizo
vinawakilisha nafsi za watenda.
(iii) Pia vitenzi vya sentesi hizo vina tabia ya
kubeba virejeshi vya nafsi kama ilivyo
katika, mwambie, omu gambile,
na ha li, mbwele na umti, vinaonyesha njeo
na hali ya uyakinifu- hali inayoonyesha
ufanano wa maumbo ya maneno.
(iv) Licha ya kuwa na mpangilio unaofanana
na wa lugha nyingine za kibantu, kwa
mfano, katika mifano tuliyoiona hapo juu,
baadhi ya maneno yanafanana: tazama
maneno:
kafugha (Kindamba); nafuga (Kihaya);
nifuga (Kindendeule); anafuga (Kiswahili).
Pia maneno:
nkuku (Kipare); nguku
(Kindamba);
nguku (Kichaga); enkoko
(Kihaya);
ng’uku (Kikaguru);
nguku(Kindendeule);
nguku (Kindendeule)
Katika mfano wa 3, maneno yafuatayo yana
ufanano:
Akeza (Kizigua); kalaija (Kihaya);
alize (Kisukuma),
newaja (Kinyaturu); ekiza (Kipare);
anda ahikite,... (Kindendeule);
akija, (Kiswahili.)
Pia maneno;
umugambe (Kizigua); omugambile
(Kihaya); unongeraye (Kindendeule); na
mwambie (Kiswahili).
Ufanano huu wa msamiati, maumbo ya maneno
pamoja na wa mpangilio wa maneno katika
sentesi, vyote vinathibistisha kwamba lugha ya
Kiswahili ni ya kibantu kama zilivyo nyingi
nyinginezo.