UTANGULIZI.
Niukweli usiopingika kuwa pamoja na kutofautiana kwa baadhi ya sifa mbalimbali za lugha zipo sifa majumui ambazo huweza kupatikana katika lugha zaidi ya moja
Sifa hizo za lugha huweza kugawanywa katika makundi matatu ambayo ni ,
Sifa majumui halisi za lugha
Sifa majumui pana za lugha
Sifa majumui tabirifu za lugha.
Kwa kuzichanganua zifa hizo nikama ifuatavyo,
SIFA MAJUMUI HALISI ZA LUGHA.
Hizi nizile sifa ambazo ni za kawaida na hupatikana katika lugha zote halisi za binadamu kwamfano katika lugha zote za binadamu huwa na irabu [a] katika orodha ya sauti zake , katika utaratibu wa lugha zote asilia za binadamu huwa na utaratibu wa irabu na konsonanti, ingawa kwa habari ya idadi ya irabu na konsonanti huweza kutofautiana baina ya lugha moja na nyingine. Vilevile katika lugha zote za asilia irabu na konsonati hupangiliwa katika silabi.
SIFA MAJUMUI ZA LUGHA PANA.
Hizi ni zile sifa ambazo hupatikana katika lugha nyingi, ingawa sii zote, kwamfano, wana isimu wanakubaliana kuwa lugha nyingi za binadamu zina angalau irabu tano, pamoja na hayo kuna lugha nyingine zina irabu saba au nane , pia kunalugha nyingine zenye irabu tatu tuu.
SIFA TABIRIFU ZA LUGHA, Hizi nizile sifa ambazo wanaisimu wanakubaliana kuwa , kuna mazingira ambayo kutokea kwa sauti flani katika lugha kunaashiria au kunatabiri kutokea kjwa sauti au irabu nyingine ambazo huambatana pamoja. Huo ndio utabirifu unaotajwa.
Katika fonolojia za lugha nyingi, konsonanti na irabu, ni sifa za msingi, Aidha katika lugha nyingi imedhihirika kwamba kutokea kwa baadhi ya sauti huwa kunaashiria kuwa sauti nyenzie (yani zinazofanana au kuendana nazo) pia zitakuwepo. Mara nyingi hutokea katika katika sauti ambazo zinmasifa za uziada. Kwamfano kama kunasauti [d} yenye sifa ya ziada [+ ghuna] basi kutatabiri uwepo wa sauti ya kinyume cha [t] yenye sifa ya [-sighuna] hata hivyo ieleweke kuwa sio katika lugha zote hali hii hutokea kwani kunalugha nyine kama Ki- fini, kikorea na kipiute ambazo zina konsonanti ambazo si ghuna lakini hazina kinyume chake.
Mfano mwingine tunaweza kuona kuwa lugha zenye toni. Yani tukigundua lugha hiyo ina toni juu, tuna weza kutabiri kuwa lugha hiyo ina sauti za toni chini. Pia tutagundua kuwa lugha hiyo ina toni panda na toni shuka.
Mpaka kufikia hapa naamini kuwa kwa msomaji yeyote Yule makini atakuwa mefahamu kwa undani kuhusu kuwepo kwa sifa majumui za lugha katika fonolojia ya lugha.
Soma zaidi
Chapisho la maasamba fonolojia ya lugha
Emanuel.Gaspa masshele 2022 (mwandishi) wa chapisho hili