NADHARIA YA FONIMU
UTANGULIZI,
Dhana ya fonimu inahistoria ndefu sana. Na ilitokana na nadharia ya wanamuundo iliyojulikana kama nadharia ya fonimu.
Asili ya istilahi fonimu.
Ingawa inawezekana kuwa dhana ya fonimu ilikuwamo katika mawazo ya wanaisimu na wanafilolojia wa zama hizo kwa miaka mingi lakini istilahi yake iliundwa baadaye kabisa kama asemavyo Maasamba. Kwamujibu wa Jones (1957) istilahi hii iliundwa na Baudouin de Courtenay, madai hayo ya Jones yanaungwa mkono na Robins (1967:204) ambaye anaeleza kwamba katika kitabu chake cha theory of Phonemes (yaelekea hii ni tafsiri ya baadaye) ambaco kimechapishwa mwaka 1884 ambacho de Courtenay alitumia neno la Ki-Rus fonema kama istilahi,
Hata hivyo Firth (1957:1) anasema kwamba inaelekea de Courtenay aliliazima istilahi hiyo fonema kwa manafunzi wake Kruszewiski ambayo aliitumia katika insha yake iliyokuwa na mada ya “ athari za mkazo katika ubadilishanaji wa irabu katika Rig-Veda insha iliyochapishwa huko Kazan mnamo mwaka 1879.
Hata hivyo wataalamu bado hawakubaliani kuhusu muasisi wa istilahi hiyo kwamfano baadhi ya wataalamu wengine wanadai kuw aistilahi hiyo iliundwa na Dufriche –Desgenettes mnamo mwaka 1873 na kuitumia kama kibadala cha istilahi ya Ki-jerumani Sprachlaut “sauti ya usemaji” hata hivy nilazima tukubaliane kuwa wazo la fonimu nilazima lilikuwamo katika fikra za wanafonetiki na wanaortografia ambao kwa namna Fulani walitumia unukuzi mpana wa sauti.
Kwavyovyote vile kuhusu istilahi fonimu Kramsky (1874) anaelekea kutupa historia ambayo ina muoano mzuri ambapo kwa mujibu wa maelezo yake mwanazuoni wakwanza kabisa kutumia istilahi hii Fonimu alikuwa ni Dufriche Desgenettes katika mkutano wa societe de linguistique de paris (Chama cha isimu cha paris) 24/mei 1873. Alipendekeza kutumia istilahi ya phoneme (fonimu) ukiwa ni utohozi wa Ki-faransa wa neno la Ki-giriki lenye maana ya sauti kama kisawe cha neno la kijerumani sprachlaut.
Kwa mujibu wa kramsky mtu wapili kutumia istilahi hiii alikuwa ni Havet taz (havet “ol et Ul en francais, Romania 1874:321 kwa mujibu wa dondoo la Kramsky . aidha akimdondoa Jakobson (1871:396-397) Kramsky anasema baada ya Havet istilahi hiyo ikatumiwa na De Saussure aliyeitumia istilahi hiyo kwa mtazamo wa kihistoria, kwani kwa mujibu wa de Saussure hilo lilikuwa umbo la kidhahania lakifdonetiki ambalo lilisemekana kujitokeza mara kwa mara katika faridi za kimofolojia za lugha zenye mnasaba mmoja. Umbo ambalo lasemekana kutokana na mame-lugha moja.
Kramsky anadai kwamba baada ya de ssausure istilahi fonimu ikatumiwa na Kruszewski (1851-1887) kruszewski alikiuwa mwanfunzi wa de Courtenay ambapo Kramsky anasema pia katika mwaka 1880 Kruszewski alichapisha tahakiki ya Memoire sur le system primitive des voyelles dans languages indoeuropeennes ambayo ilikuwa imeandikwa na de Saussure katika chapisho lake hilo istilahi fonimu ilitumika kwa mara ya kwanza katika msamiati wa Ki-slavu.
Kwa mujibu wa wa maelezo ya Kramsky, Kruszewski alipotumia istilahi hiyo aliitolea maelezo maalumu yaliyoelekeza kwamba istilahi hiyo ilikuwa na faida ya kutofautisha sauti kama faridi ya kifonetiki na sauti kama tukio la kifiziolojia. Kisha mnamo mwaka 1881 Kruszewski akaeleza wazi kwamba alikuwa napendendekeza kuitumia istilahi fonimu kwa maana ya faridi ya kifonetiki ambayo haiwezi kugawanyika tena pasi na kupoteza uamilifu wake.
Tukizingatia maelezo haya ya Kramsky tutaona kwamba Kruszewski aliichukua istilahi hii katika makala hayo ya Memoire ya de Saussure (siyo katika maandishi ya baadaye ya de Saussure ambamo analitumia neno hilo akimaanisha “sauti za lugha” ) na kulitumia kwa matumizi yake ya wakati huo. Kwahiyo nimuhimu tukasema hapa kwamba ingawa kruszewski hakutoa fasili ya nono hilo lakini angalau alilipa fahiwa mpya.
Kama asemavyo Maasamba akimnukuhu Anderson (1985:67) de Courtney ndiye ambaye angalau alijaribu kufasili dhana ya fonimu. Kwa de Courtney fonimu, za lugha ni, vibadala vya mwisho kabisa vya muundo wa sauti, kisaikofonetiki fasili hii ipo karibu na fasili ya fonimu ilivypochukuliwa baadaye.