Monday

USHAIRI WA KISWAHILI NA NADHARIA PDF

0 comments

 

USHAIRI
WA
KISWAHILI

Nadharia, Maendeleo, Mwongozo kwa Walimu wa Kiswahili

na DIWANI YA MEA
Method Samwel (PhD)

Amina J. Seleman

MEVELI PUBLISHERS (MVP) Akech J.Kabiero

2

USHAIRI WA KISWAHILI

Nadharia, Maendeleo, Mwongozo kwa Walimu wa Kiswahili

na DIWANI YA MEA

© MEVELI Publishers & Method Samwel

Toleo la kwanza 2013

Kitabu hiki kinapatikana kwa kuwasiliana moja kwa na waandishi au mchapishaji:

Dkt. Method Samwel

Simu:+255718165528

Baruapepe: method_samwel@yahoo.com

Akech Kabiero

Simu:+255685046179

Baruapepe: akeckabiero@yahoo.com na akabiero@gmail.com

Amina J. Seleman

Baruapepe: aminamikina@yahoo.com

ISBN: 978-9987-9735-0-7

Haki imehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki

kwa jinsi yoyote ile bila idhini ya mchapishaji na Method Samwel. Hata hivyo, inaruhusiwa

kuchukua vipande vifupi vya kitabu hiki kwa minajili ya kufanya marejeo na nukuu au kufanya

mapitio.

3

SHUKRANI

Tunapenda kutumia fursa hii kuwashukuru watu, taasisi na mashirika mbalimbali

ambayo kwa namna moja au nyingine yamechangia katika kukamilika kwa kitabu hiki. Kwanza

tuanze kwa kumshukuru Mungu, ambaye, kwa mtazamo wetu, ndiye huwapa watu afya njema na

mawazo ya nini cha kufanya na nini cha kutofanya. Bila shaka Manani ndiye aliyetupa wazo la

kuandika kitabu hiki na kututia nguvu kulitimiza wazo hilo japo haikuwa kazi rahisi kutimiza

lengo letu kutokana na ugumu wa shughuli nzima ya uchapaji nchini Tanzania. Pia

tunawashukuru wazazi na walezi wetu ambao walitulea na kutusomesha hata tukapata maarifa

haya ambayo leo tunayaweka kitabuni kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Zaidi ya hao, wapo ambao tumetumia maandiko yao katika kujielimisha juu ya ushairi

wa Kiswahili, wale ambao walihariri kazi hii katika ngazi mbalimbali na pia wale waliotoa fedha

kuhakikisha kitabu hiki kinachapishwa na kuwa na muonekano ulionacho. Hivyo tunawashukuru

wanazuoni wote ambao maandiko yao yamenukuliwa katika kitabu hiki. Kwa hakika maandiko

yenu ndiyo yametoa dira ya andiko hili. Tuwataje wachache kati ya hao kuwa ni Maprofesa

Mugyabuso Mlinzi Mulokozi, Kulikoyela Kanalwanda Kahigi, David Massamba, Kyalo

Wamitila, Fikeni Senkoro; washairi Shaaban Robert, Fumo Liyongo, Mwanakupona Binti

Mshamu, Mathias Mnyampala na wengineo mliotangulia mbele za haki. Mlale salama peponi na

Mola awape heri. Wengine tunaowashukuru hapa ni Prof. Yunus Rubanza, Dakta Shani Omari,

Dakta Selemani Sewangi, Dakta Aldin Mutembei na wanazuoni wote wa Taasisi ya Taaluma za

Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hawa ndiyo walitulea tukiwa tunajifunza taaluma

ya Kiswahili, ikiwa ni pamoja na ushairi wake.

Tungependa kumshukuru kipekee Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MEVELI

Publishers, kwa kukubali kuuchapa muswada wetu uliozaa kitabu hiki. Yeye ndiye aliyetoa fedha

za kugharamia hatua kwa hatua uandazi wa kitabu hiki tangu uandishi na upangaji wa muswada,

uhariri na uchapishaji kwa ujumla. Tunakushukuru sana kwa mapenzi yako katika lugha hii. Ni

imani yetu kwamba tumekata kiu yako ya kuhakikisha ujuzi tulionao katika taaluma hii ya ushairi

unawafikia watu wengi.

Mwisho kabisa tuwashukuru wana familia wetu ambao kwa nyakati tofauti walitutia

moyo na kutuvumilia tulipotingwa na kazi hii ya uandishi. Andiko hili liwapoze machungu na

mjisikie kuhusika kipekee katika kuendeleza lugha hii adhimu ya Kiswahili. Tunapenda kusisitiza

kwamba tuliowashukuru hapa hawahusiki na udhaifu wowote utakaoonekana kitabuni. Udhaifu

huo, kama utaonekana, ni wetu wenyewe.

4

DIBAJI

Kitabu hiki kinashughulikia utanzu wa ushairi na hasa ushairi wa Kiswahili uliozagaa

katika nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kinaanza kwa masuala

ya kidhana, kinadharia, historia na maendeleo ya ushairi wa Kiswahili, mbinu za ufundishaji wa

ushairi na Kiswahili kwa ujumla na kisha kumalizia kwa Diwani ya MEA. Katika sehemu ya

kwanza tumechambua kwa kina dhana ya ushairi, nadharia mbalimbali za chimbuko la ushairi,

historia na maendeleo ya ushairi wa Kiswahili na jinsi ya kuufundisha ushairi wa Kiswahili

pamoja na lugha yenyewe kwa ujumla. Tuseme wazi hapa kwamba sehemu hiyo ilikuwa na

changamoto kubwa kwani masuala kama hayo katika taaluma za sayansi ya Jamii, kama

anavyobainisha Madumulla (2009), hayana maelezo ya namna moja. Kuna maelezo mengi

yanayokinzana kuhusu dhana, nadharia na historia na maendeleo ya Kiswahili. Kitabu hiki

kimechunguza maelezo ya wanazuoni waliotangulia na kubainisha udhaifu wa maelezo hayo.

Udhaifu huo ndiyo uliweka misingi ya maelezo yetu katika kitabu hiki tukijaribu kuondoa

udhaifu husika.

Zaidi ya sehemu ya kwanza, kitabu hiki kina sehemu ya pili ambayo imepewa jina

Diwani ya MEA. Katika sehemu ya kwanza tuliyoieleza awali ambayo inaitwa Nadharia,

Maendeleo na Mwongozo kwa Walimu wa Kiswahili, tumetoa tu ufafanuzi wa dhana, nadharia,

historia na mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika katika utunzi na uchambuzi wa mashairi. Ila

katika sehemu ya pili tumepiga hatua na kutunga mashairi kadhaa na Tumeiita Diwani ya MEA.

“Diwani ya MEA” ni kifupi cha “Diwani ya METHOD na AKECH,” waandishi wawili

waliotunga diwani hiyo. Zaidi ya kuwa kifupi cha majina ya waandishi, Diwani ya MEA inapanda

mbegu za mapinduzi katika mioyo ya kila msomaji ili ziweze kumea. Katika diwani hiyo kuna

mashairi mazito na mazuri ambayo yanakusudia kuielimisha na kuiburudisha jamii. Mashairi

hayo yanaakisi masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Aidha,

mashairi hayo yametumia miundo tofauti ikiwa ni mchanganyiko wa muundo wa kimapokeo na

wa kisasa. Kwa kufanya hivyo, sisi waandishi, tunajitambulisha kama wanausasa.

Diwani ya MEA imekusudia kupanda mawazo katika mioyo na vichwa vya wasomaji

wake ili yaweze kumea na hatimaye kuzaa matunda na matunda hayo yakapate kudumu ili

kwamba kila lifanyikalo likumbukwe kwamba linapandwa na litamea. Likishamea litahitaji

mvunaji makini na mwenye utayari ili ayavune na kuyapeleka sokoni kwa mauzo. Kutokana na

sifa hiyo, kitabu hiki kimekuwa cha aina yake katika historia ya ushairi wa Kiswahili. Diwani ya

MEA itamsisimua msomaji huku akipata mafunzo muhimu sana yatakayokuwa taa katika maisha

yake yote. Hata hivyo, diwani hiyo inapaswa kusomwa kwa tafakuri ya kiwango cha juu maana

ukweli kinzani umetumiwa sehemu nyingi.

yaliyomo/ content

Shukrani ................................................................................................................................ 3
Dibaji .................................................................................................................................... 4
Tabaruku ............................................................................................................................... 9
Vifupisho na Akronimu ........................................................................................................ 10
Sehemu ya Kwanza: Nadharia, Maendeleo na Mwongozo kwa Walimu wa .......
Kiswahili ................................................................................................................... 11
Sura ya Kwanza: Utangulizi .......................................................................................... 12
Ushairi kama Utanzu wa Fasihi Simulizi .............................................................................. 12
Uainishaji wa Tanzu za Fasihi Simulizi ................................................................................ 15
Nudhumu Simulizi ............................................................................................................... 20
Nyimbo ............................................................................................................................... 20
Uainishaji wa Utanzu wa Nyimbo kwa Kigezo cha Dhima ................................................... 20
Uainishaji wa Nyimbo Kimaudhui........................................................................................ 22
Uainishaji wa Nyimbo kwa Kifanani/Hadhira ....................................................................... 22
Uainishaji wa Nyimbo Kimuktadha ...................................................................................... 22
Maghani .............................................................................................................................. 22
Uainishaji wa Maghani kwa Kigezo cha Dhima .................................................................... 22
Uainishaji wa Maghani kwa Kigezo cha Utendaji ................................................................. 23
Ushairi kama Utanzu wa Fasihi Andishi ............................................................................... 23
Dhana ya Ushairi Andishi wa Kiswahili ............................................................................... 23
Mkabala wa Kimapokeo Juu ya Dhana ya Ushairi ................................................................ 24
Mkabala wa Kisasa/Kimamboleo Juu ya Dhana ya Ushairi ................................................... 27
Sifa za Jumla za Ushairi ....................................................................................................... 28
Sura ya Pili: Dhima za Ushairi wa Kiswahili .............................................................. 29
Dhima za Ushairi wa Kiswahili Kijamii ............................................................................ 29
Ushairi wa Kiswahili na Uhifadhi wa Historia ...................................................................... 29
Ushairi wa Kiswahili na Kukuza Ushujaa, Ujasiri na Uzalendo ............................................ 32
Ushairi wa Kiswahili na Kuendeleza Matabaka .................................................................... 32
Ushairi wa Kiswahili na Kuhifadhi na Kuendeleza Utamaduni ............................................. 33
Ushairi wa Kiswahili na Kuadilisha na Kuadibisha ............................................................... 34
Ushairi wa Kiswahili na Kuburudisha................................................................................... 35
Dhima za Ushairi wa Kiswahili Katika Fasihi .................................................................. 35
Ushairi wa Kiswahili na Kutambulisha na Kuwajenga Wahusika ......................................... 36
Ushairi wa Kiswahili na Kuhamisha na Kujenga Mbinu za Kifani ........................................ 36
Ushairi wa Kiswahili na Kuibua Maudhui ............................................................................ 37
Ushairi wa Kiswahili na Kukuza Tanzu za Fasihi ................................................................. 38
Sura ya Tatu: Chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ..................................................... 41
Chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni Uislamu/Kiarabu ........................................................ 41
Chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni Ushairi Simulizi wa Kibantu ...................................... 45
Kufanana kwa Ushairi wa Kiswahili na Ushairi Simulizi wa Kibantu ................................... 46
Kufanana Kimaudhui ........................................................................................................... 46
Kufanana kwa Dhima ........................................................................................................... 51
Kufanana Kifani ................................................................................................................... 53
Sura ya Nne: Historia ya Ushairi wa Kiswahili ......................................................... 57
Ushairi Simulizi wa Kiswahili Wakati wa Ujima .................................................................. 57
Ushairi wa Kiswahili katika Karne ya 10 na 16 .................................................................... 58
Mchango wa Waarabu katika Ushairi wa Kiswahili .............................................................. 58
Ushairi wa Kiswahili katika Karne ya 17 na 18 .................................................................... 59
Ushairi wa Kiswahili katika Karne ya 19 .............................................................................. 59
Kuingia kwa Ukoloni na Athari Zake katika Ushairi wa Kiswahili ....................................... 59
Ukoloni wa Wajerumani/Wadachi ........................................................................................ 60
Ukoloni wa Waingereza ....................................................................................................... 60
6
Kupatikana kwa Uhuru na Hali ya Ushairi wa Kiswahili ...................................................... 61
Kipindi cha Uhuru na Azimio la Arusha ............................................................................... 61
Kipindi cha Vita vya Kagera na Ugumu wa Maisha .............................................................. 61
Ushairi wa Kiswahili Kipindi cha Utandawazi ...................................................................... 65
Sura ya Tano: Ushairi wa Bongo Fleva ...................................................................... 66
Dhana ya Muziki wa Bongo Fleva ........................................................................................ 66
Maudhui ya Ushairi wa Bongo Fleva ................................................................................ 67
Maudhui ya Uongozi na Utawala .......................................................................................... 67
Maudhui ya Kiuchumi .......................................................................................................... 67
Maudhui ya Kijamii katika Ushairi wa Bongo Fleva ............................................................. 68
Maudhui ya Kiutamaduni Katika Ushairi wa Bongo Fleva ................................................... 70
Fani ya Ushairi wa Bongo Fleva ........................................................................................ 72
Utungaji wa Ushairi wa Bongo Fleva ................................................................................... 72
Utendaji wa Ushairi wa Bongo Fleva ................................................................................... 77
Mandhari ya Ushairi wa Bongo Fleva ................................................................................... 84
Muundo wa Ushairi wa Bongo Fleva .................................................................................... 84
Mtindo wa Ushairi wa Bongo Fleva ..................................................................................... 88
Wahusika katika Ushairi wa Bongo Fleva .......................................................................... 110
Sura ya Sita: Uainishaji wa Ushairi wa Kiswahili ................................................... 111
Kigezo cha Aina ya Uwasilishaji ........................................................................................ 111
Kigezo cha Umbo ............................................................................................................... 111
Kigezo cha Mbinu za Kisanaa Zinazotumika ...................................................................... 112
Kigezo cha Maudhui Yabebwayo na Shairi ........................................................................ 112
Kigezo cha Idadi ya Mistari ................................................................................................ 113
Kigezo cha Bahari .............................................................................................................. 113
Bahari za Ushairi wa Kimapokeo ....................................................................................... 113
Upungufu wa Kigezo cha Bahari za Ushairi wa Kimapokeo ............................................... 119
Bahari za Ushairi wa Kimapokeo na Kisasa ........................................................................ 120
Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Beti, Mishororo na Vipande .......................................... 120
Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Aina ya Kiishilio ........................................................... 121
Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Urari wa Vina na Mizani ............................................... 121
Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Uradidi ......................................................................... 123
Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Madhumuni ya Utungaji (Lengo) .................................. 123
Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Muundo ........................................................................ 124
Hitimisho kuhusu Bahari za Ushairi ................................................................................... 125
Sura ya Saba: Uchambuzi wa Mashairi .................................................................... 126
Maudhui ............................................................................................................................. 126
Fani ................................................................................................................................. 127
Sura ya Nane: Ufundishaji wa Ushairi ...................................................................... 132
Ushairi kama Mbinu ya Kufundishia Masomo Mbalimbali ................................................. 132
Ushairi wa Kiswahili kama Somo ....................................................................................... 133
Silabasi na Ushairi wa Kiswahili ........................................................................................ 133
Kutafsiri Silabasi kwenye Vitendo...................................................................................... 134
Kufanya Mapitio ya Makusudi ya Ufundishaji wa Ushairi .................................................. 134
Kuchagua na Kupanga Mada za Ushairi Zitakazofundishwa ............................................... 134
Kutambua Vitabu vya Kiada na Kuteua Vitabu vya Ziada .................................................. 135
Kuandaa Mpangokazi wa Ufundishaji ................................................................................ 135
Kuteua na Kuandaa Mbinu ya Kufundishia Ushairi na Maandalizi Yake ............................ 139
Kuandaa Mwongozo wa Ufundishaji wa Ushairi Darasani .................................................. 143
Kuandaa Zana za Kufundishia ............................................................................................ 146
Kuingia Darasani na Kufundisha ........................................................................................ 147
Kufanya Tathmini (Upimaji) ya Ufundishaji wa Ushairi ..................................................... 147
Kutoa Matokeo ya Tathmini na Utoaji wa Motisha ............................................................. 148
7
Upangaji wa Ufundishaji Ujao ............................................................................................ 149
Hitimisho Kuhusu Hatua za Kutafsiri Silabasi kwenye Vitendo .......................................... 150
Sehemu ya Pili:Diwani ya MEA .................................................................................. 151
Lipaka ............................................................................................................................... 152
Hadithi ............................................................................................................................... 152
Mwatulinda? Mwatuua? ..................................................................................................... 154
…………Te. ...................................................................................................................... 154
Te!Te!TeTe! ....................................................................................................................... 155
Madhila Yako..................................................................................................................... 156
Kwaherini .......................................................................................................................... 157
Tangu Atoke Safari ............................................................................................................ 159
Maskini Afrika!! ................................................................................................................ 159

Kisabengo .......................................................................................................................... 161

Chakubimbi ........................................................................................................................ 162

Mchezo wa Maneno ........................................................................................................... 162

Barua Jukwaani .................................................................................................................. 163

Dunia Kambi ...................................................................................................................... 165

Ng’ombe Mmemmaliza ...................................................................................................... 165

Nyathiwa Woung Dala (Mwanetu Ondoka Nyumbani) ....................................................... 166

Naenda Kuitafuta ............................................................................................................... 167

Maji ya Kifo ....................................................................................................................... 170

Ulimi ................................................................................................................................. 171

Tukaogelee! ....................................................................................................................... 171

Akilamba Sabuni ................................................................................................................ 171

Umoja Wetu ....................................................................................................................... 172

Wegesa Mnyamongo (Wege/Penina) .................................................................................. 172

Panya Akimng’ata Chui ..................................................................................................... 173

Hata Kama! ........................................................................................................................ 174

Ksii!! Ksii!! ........................................................................................................................ 175

Mtakosa Kuthaminiana ....................................................................................................... 175

Pamoja Kwamba ................................................................................................................ 176

J.K.Nyerere Baba ............................................................................................................... 177

Sherehe Itakapoisha ............................................................................................................ 178

Rais Awaye Yeye! .............................................................................................................. 179

Barua ya Majibu ................................................................................................................. 180

Ya Nini Lakini? .................................................................................................................. 183

Chuny Piny (Roho Ya Nchi) ............................................................................................... 184

Na Tuvisome Vyote ........................................................................................................... 185

Safari Kuelekea .................................................................................................................. 186

Ndege si Ndege, Mnyama si Mnyama. ............................................................................... 189

Kizungumkuti .................................................................................................................... 190

Bunge la Wahuni. ............................................................................................................... 191

Karibu Mwanangu! ............................................................................................................ 193

Twende Tukawinde ............................................................................................................ 194

Kwa Jirani Yetu! ................................................................................................................ 194

Ni Lini na Wapi? ................................................................................................................ 195

Nyako Ma Ero Ainya ......................................................................................................... 196

Wimbo Ulio Bora ............................................................................................................... 197

Mafamba ............................................................................................................................ 198

Inapotokea .......................................................................................................................... 201

Mwanzo Mwisho ................................................................................................................ 203

Ngao ................................................................................................................................. 204

Tamati! .............................................................................................................................. 204

8

Marejeleo .......................................................................................................................... 205

Faharasa ............................................................................................................................. 211

9

TABARUKU

Tunakitabaruku kitabu hiki kwa washairi wote

waliotangulia mbele ya haki pamoja na marehemu

Prof. Yared Kihore. Mungu awajalie rehema zake na

siku moja tuonane akhera tukiimba na kughani ushairi

wa Kiswahili.

10

VIFUPISHO NA AKRONIMU

a.k.a Anajulikana kama (Also known as)

BAKITA Baraza la Kiswahili la Taifa

CD Compact Disc

CHAKA Chama cha Kiswahili Afrika

CHAKAMA Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki

CHAKITA Chama cha Kiswahili cha Taifa

Dkt. Daktari

DVD Digital Video Disc

EATV East Africa Television

ht. Hakuna tarehe

ITV Independent Television

Khj. Kama hapo juu

PhD Daktari wa Falsafa

p.h.k Pia hujulikana kama

Prof. Profesa

TATAKI Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

TAKILUKI Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni

TUKI Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

TV Television

VCD Video Compact Disc

11

SEHEMU YA KWANZA:

Nadharia, Maendeleo na Mwongozo kwa Walimu wa

Kiswahili

12

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI

Tanzu za lugha ni isimu na fasihi. Katika isimu, kuna tanzu kama vile isimujamii, isimu matamshi

(fonetiki/fonolojia), isimu muundo (Sintaksia), isimu maumbo (mofolojia) n.k. Kwa upande wa fasihi,

kuna aina mbili za fasihi ambazo ni fasihi simulizi na andishi. Ushairi ni utanzu wa fasihi unaopatikana

katika fasihi simulizi na pia andishi. Kitabu hiki kinapitia na kuchambua ushairi kama utanzu wa fasihi

simulizi na pia kama utanzu wa fasihi andishi.

1. USHAIRI KAMA UTANZU WA FASIHI SIMULIZI

Kabla ya kuzama katika kuchunguza ushairi kama utanzu wa fasihi simulizi, ni vema tuchunguze

dhana ya fasihi simulizi. Pamekuwepo na fasili mbalimbali za fasihi simulizi ambapo kila moja ina

jambo la muhimu inayolisisitiza. Suala la utata katika fasili ya fasihi simulizi linabainishwa vizuri na

Akivaga na Odaga (2011:1) wanaposema:

Until recently it was not possible to agree on the definition of oral literature. Different people

have come up with different definitions. Some people have even refused to accept the term “oral

literature,” arguing that it is a contradiction in terms. They argue that literature means the

written word and therefore it can not be oral.

Mpaka hivi karibuni haikuwa rahisi kukubaliana juu ya fasili ya fasihi simulizi. Watu

tofautitofauti wamekuja na fasili tofautitofauti za fasihi simulizi. Wengine wamefikia hatua ya

kuikubali dhana “fasihi simulizi,” kwa madai kwamba ni mkanganyiko wa dhana. Wanadai

kwamba kimsingi fasihi humaanisha maelezo yaliyoandikwa na kwa hiyo hayawezi kamwe kuwa

simulizi (Tafsiri yetu).

Maelezo haya yanatuthibitishia kwamba dhana fasihi simulizi ni yenye mkanganyiko mkubwa na japo

ni muhimu kuielewa kabla ya kuuelewa ushairi simulizi, jambo hilo halimaanishi kwamba litakuwa

rahisi. Ili kuuona ugumu huo unaodokezwa na Akivaga na Odaga (khj.) tuzipitie fasili chache za fasihi

simulizi. Kwa kuanza na Mulokozi (1996:24), tunaona anaiona fasihi simulizi kuwa ni fasihi

inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila

kutumia maandishi. Anaendelea kudai kwamba fasihi simulizi ni tukio linalofungamana na muktadha

(mazingira) fulani ya kijamii na kutawaliwa na mwingiliano wa mambo sita ambayo ni fanani (msanii),

hadhira (msikilizaji), fani inayotendwa, tukio, mahali na wakati. Naye Ngure (2007:1) kwa upande

wake, anasema kwamba fasihi simulizi ni ile ambayo inapitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine

kupitia neno la mdomo. Fasili hizi mbili (ya Mulokozi na ya Ngure), hata hivyo, zinaweka mkazo

katika utungaji na/au uwasilishaji na kupuuza masuala mengine ya kifasihi kama vile uhifadhi na

mabadiliko. Wakati ambapo fasili ya Mulokozi ni bora kuliko ya Ngure kwani inazingatia utungaji na

uwasilishaji, ya Ngure inazingatia tu uwasilishaji. Wamitila (2010a:2-3) anabainisha wazi kwamba

mgawanyo wa fasihi katika makundi (ya fasihi simulizi na andishi) unategemea (a) njia zinazotumiwa

kuhifadhi, kuwasilisha, kupokezana (b) nyenzo yake kuu. Kwa kutumia vigezo hivyo vya uainishaji wa

fasihi, ni wazi kwamba fasili ya Ngure (2007) ina mapungufu makubwa wakati ile ya Mulokozi

inaonekana kutimiza baadhi ya vigezo vya Wamitila. Aidha, fasili hizo mbili (ya Mulokozi, 1996 na

Ngure, 2007) zinachukulia kwamba fasihi simulizi husambazwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo (na

kupuuza nafasi ya mbinu nyinginezo za usambazaji wa fasihi). Mawazo haya yanapingana na halisi.

Wamitila (2001b:13-14) akiandika kwa namna bora zaidi kwa wakati wa sasa anasema kwamba,

“katika tamaduni andishi ambazo zimeathiriwa na mfumo wa kimaandishi, hiyo inayojulikana kama

fasihi simulizi sio simulizi tena (haiwasilishwi kwa njia ya mdomo tu) bali inahifadhiwa kwa njia

mbalimbali kama kwa vinasa sauti, kanda za video na kompyuta” (ufafanuzi ni wetu). Bila shaka

waandishi wengi wa sasa wa fasihi watakubaliana na maelezo haya ya Wamitila na kuyapinga ya

Mulokozi na Ngure. Kutokana na hayo, Wamitila (2010a:3) anasema kwamba tofauti kuu kati ya fasihi

simulizi na andishi ni kwamba fasihi simulizi hutegemea zaidi kauli au usemi kuliko fasihi andishi

ambayo hutegemea maandishi kwa kiasi kikubwa. Wamitila anaendelea kwa kutahadharisha kwamba

“upo uwezekano wa fasihi andishi kupewa sura ya fasihi simulizi na fasihi simulizi kuwasilishwa

kimaandishi.” Hata hivyo, tungependa ieleweke kuwa hatubezi jitihada zilizofanywa na wataalamu wa

awali waliofafanua dhana hizi. Tunatambua kwamba wakati wataalamu wengi wa awali (na hasa

13

walioandika hadi miaka ya 1990) walipokuwa wanaandika juu ya fasihi simulizi, hakukuwa na

maendeleo makubwa ya kuiweka fasihi simulizi katika mbinu mpya za usambazaji kama vile

maandishi, kanda za video na kadhalika kama ilivyo leo. Hivyo, kwa wataalamu wa awali kuchukulia

kuwa fasihi simulizi inasambazwa kwa mdomo bila kutumia maandishi ni dai ambalo labda linatokana

na wakati walipokuwa wakiandika. Msingi wa pili wa dai hilo huweza kuwa sambamba na kile

anachokisema Wamitila (2010a:3) kuwa, fasihi simulizi hutegemea zaidi kauli kuliko maandishi.

Aidha, hata pale fasihi simulizi inapowekwa katika maandishi, bado ukweli unabaki kuwa palepale

kuwa kazi hiyo ilianza kwa kuwasilishwa kwa masimulizi ya mdomo na mbinu zingine za uwasilishaji

zikafuata baadaye. Vilevile, mawazo haya ya wataalamu wa awali huenda yametokana na ukweli

anaouwasilisha Wamitila (2010a:3) kwamba pale fasihi inapohifadhiwa na/au kuwasilishwa kwa njia

zingine ambazo si za kimasimulizi (inapohifadhiwa au kuwasilishwa kwa maandishi) hupoteza sifa

zake za msingi zinazoifanya kazi husika kuwa utanzu wa fasihi simulizi.

Hivyo, bado tusisitize hapa kwamba, fasihi simulizi inazalishwa kichwani mwa binadamu,

inawasilishwa kwa njia za midomo na matendo. Hata pale inapotokea fasihi simulizi ikahifadhiwa kwa

na kuwasilishwa kwa maandishi usimulizi asilia unakuwa ulifanyika katika masimulizi. Kwa mfano,

mtu anapoamua kuandika ngano ya sungura na fisi ina maana kwamba wakati anaandika anakuwa

anasimulia ngano hiyo kwa hadhira dhahania (hadhira ambayo haipo ila itaibuka baadaye na kusoma

kazi husika). Msanii anapoiandika ngano hiyo huwa haitungi maana ilishatungwa zamani, bali

anaisimulia hadhira yake. Aidha, mabadiliko haya ya fasili za fasihi simulizi yanadokeza jinsi

mabadiliko mbalimbali ya kisayansi na kijamii yanavyoweza kubadilisha mitazamo au dhana

mbalimbali za kitaaluma.

Mbali na utata katika suala la nyenzo ya uwasilishaji wa fasihi simulizi, jambo lingine

linaloonekana hapa ni kwamba fasihi simulizi inachukuliwa kuwa ni ile inayorithishwa kutoka kizazi

kimoja hadi kingine kwa njia ya masimulizi ya mdomo na matendo (Finnegan, 1977; Bukenya na

wenzake, 2000; King’ei na Kisovi, 2005; Kimani na wenzake, 2006 kwa kuwataja wachache). Samwel

(2012a) anafafanua kwamba kauli hii inaleta hisia kuwa fasihi simulizi haibadiliki, bali hubaki vile vile

toka kizazi hadi kizazi. Samwel anaendelea kueleza kwamba, kwa kuwa fasihi ni zao la jamii ni wazi

kwamba fasihi simulizi, pamoja na tanzu zake, zinabadilika kulingana na mabadiliko mbalimbali

yanayotokea katika jamii. Samwel (2012a) anamnukuu Rubanza (1994:1) kusisitiza juu ya hilo

anaposema kwamba, “si kweli kuwa fasihi simulizi ni masimulizi tu ya kale yarithishwayo kutoka kizazi

kimoja hadi kingine. Fasihi simulizi ni utanzu wa sanaa ulio hai na ambao hukua na kubadilika

kutokana na mabadiliko ya kiwakati na ya kimfumo jamii.” Aidha, Samwel anamnukuu pia Miller

(1984:151) anayeshadidia kuhusu mabadiliko ya fasihi simulizi kwa kusema kwamba hata idadi na

majina ya tanzu/vipera vya fasihi simulizi yataendelea kubadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea

katika jamii. Hivyo, kuna uwezekano wa tanzu mpya kuzaliwa au tanzu zilizoainishwa awali kupotea.

Hata hivyo Samwel (2012a) akimnukuu Jamieson (1975:414), anasisitiza kwamba fasihi simulizi

inapobadilika na kuibua tanzu mpya, basi tanzu hizo mpya hujengwa katika msingi wa tanzu za awali.

Kutokana na hayo yote, tuseme fasihi simulizi ni nini hasa? Katika kitabu hiki labda tuseme

kwamba fasihi simulizi ni dhana inayochimbuka katika dhana ya Kiingereza “oral literature” ambayo

hasa inamaanisha aina ya fasihi ambayo msingi wake hasa ni masimulizi ya mdomo na matendo, japo

kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, inaweza pia kuhifadhiwa katika maandishi.

Zaidi ya utata katika dhana yenyewe suala lingine lenye utata katika fasihi simulizi ni uainishaji wa

tanzu na vipera vya fasihi simulizi. Uainishaji wa tanzu za fasihi simulizi umekuwa moja ya mambo

magumu sana katika fasihi hiyo. Ugumu wa uainishaji wa tanzu hizo unatokana na mambo kadhaa.

Miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo:

(i) Kuna vigezo vingi vinavyoweza kutumika katika uainishaji wa tanzu hizo. Vigezo hivyo,

hata hivyo, vinatofautiana kutoka mwanazuoni mmoja hadi mwingine. Kwa mfano, tunaona

Wafula na Njogu (2007:13) kwenye kitabu chao Nadharia za Uhakiki wa Fasihi wanabainisha

kwamba vigezo vinavyoweza kutumika katika kuainisha tanzu za fasihi simulizi ni pamoja na:

majina ya tanzu, miundo yake- kwa mfano mianzo na miishio yake, mitindo yake, wahusika

wake, wakati na mahali pa kutambia. Maelezo haya yanatofautiana na ya Mulokozi (1996:34)

katika Fasihi ya Kiswahili ambapo anabainisha kwamba vigezo vinavyoweza kutumika katika

14

kuainisha tanzu za fasihi simulizi ni pamoja na: umbile na tabia ya kazi inayohusika , vipengele

vya ndani na nje mfano lugha iliyotumika kama vile (lugha ya kishairi, kinathari, kimafumbo,

ki-wimbo, kighani, na kadhalika). Anataja vigezo vingine kuwa ni muundo wa fani, wahusika

(kama wapo), muktadha wa uwasilishaji, namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira na dhima ya

fani hiyo katika jamii. Hivyo, vyovyote iwavyo, kutumia vigezo tofauti kutasababisha kuwa na

tanzu tofauti tofauti za fasihi simulizi.

(ii) Tanzu za fasihi simulizi ni nyingi na hutofautiana kati ya jamii na jamii. Kutokana na hili

inakuwa ni vigumu sana kueleza tanzu za fasihi simulizi ni zipi hasa. Kila jamii ina tanzu zake

za fasihi simulizi ambazo zinaweza kuwa tofauti na tanzu za jamii nyingine. Inawezekana tanzu

fulani ikawepo katika jamii fulani lakini isiwepo katika jamii nyingine au ikawepo katika jamii

nyingine lakini ikiwa na sifa tofauti kabisa. Kwa mfano, Samwel (2012a) anawasilisha kwamba

katika jamii za Wahaya na Wasukuma alizozitafiti, zina majigambo ya wanawake. Rejelea

anaposema:

...katika jamii za Kihaya na Kisukuma tulizozitafiti tumebaini kwamba walikuwapo

wanawake ambao walikuwa mashujaa na watawala. Mulokozi (2002:43) akithibitisha

kuwapo kwa mashujaa wa kike katika jamii ya Kihaya anasema kwamba tendi za nanga

zilikuwa za aina tatu, tendi za nanga za mashujaa (enanga z’emanzi), tendi za nanga za

wafalme (enanga z’abakama) na tendi za nanga za mizimu (enanga z’Abachwezi).

Anaendelea kusema kwamba katika tendi za nanga za ushujaa, shujaa kwa kawaida alikuwa

mwanamume jasiri au mwanamke jasiri. Hii ina maana kwamba enanga z’emanzi

zinatambua kuwapo kwa shujaa wa kike katika jamii za Wahaya. Jambo hili si la ajabu

kwani simulizi za Zanzibar pia zinatueleza kwamba Zanzibar hapo awali iliitwa Zinji la

Mwana Aziza ikipata jina hilo kutoka kwa mtawala wa kike aliyeitwa Mwana Aziza. Vivyo

hivyo, simulizi hizo zinatueleza kwamba huko Unguja alipata kuwapo mwanamke jasiri

aliyeitwa Bihole wa Unguja ambaye alimiliki watumwa wengi sana. Hivyo, kama

tunakubaliana kwamba walikuwapo wanawake mashujaa na watawala na kwamba

majigambo ni utanzu ulioghanwa na mashujaa na watawala basi ni wazi kwamba wanawake

mashujaa na watawala nao walikuwa na sababu ya kujigamba.

Hapa Samwel anapingana na dai la Bowra (1952) kwamba wanawake hawakuwa na sababu ya

Kujigamba. Hivyo, anathibitisha bila shaka yoyote kwamba jamii za Wahaya na Wasukuma

zina majigambo hayo ya wanawake. Hata hivyo, aina hii ya majigambo inaonekana kutowepo

katika jamii nyingi za Kitanzania na Afrika kwa ujumla (Taz. Rubanza, 1994; Mulokozi, 1996;

Peek na Kwesi, 2004). Jambo hili linafanya iwe vigumu sana kusema kwamba tuna aina hizi au

zile za tanzu za fasihi simulizi. Tunaweza kufanya hivyo tu kwa kuzingatia jamii moja mahsusi.

(iii) Tanzu hizo huingiliana. Katika fasihi simulizi ni kawaida kwa tanzu kuingiliana; methali

huweza kuwa hadithi na hadithi huweza kuwa methali na kadhalika. Hivyo, inakuwa vigumu

sana kuainisha tanzu. Jambo hili linafafanuliwa kwa kina na Mulokozi (1996) na Samwel

(2012a). Mulokozi (1996:37) anaelezea jinsi methali za Kihaya “obutelagaza bukaisa

Mashanda” (kutokujipangusa mikono kulimponza Mashanda) na ya Kimaragoli “Navolegwa

yita imbogo” (Navolegwa aliua mbogo (nyati)). Mulokozi (khj.) anafafanua kwamba methali ya

kwanza inadokeza hadithi moja ya mtu aliyeitwa Mashanda ambaye alimpa mfalme zawadi ya

buni za kutafuna bila ya kujipangusa mikono kwanza. Mfalme akakasirika na kuamuru auawe

(kwa kumlisha najisi). Methali inayofuata inadokeza hadithi ya Navolegwa ambaye alikuwa

mtu mnyonge sana na dhaifu aliyedharauliwa na kila mtu. Siku moja alikwenda kuwinda,

akamwua nyati, mnyama mkali ambaye hata wawindaji shupavu na wenye nguvu

walimwogopa. Huu ni mfano dhahiri wa kuingiliana kwa utanzu wa methali na hadithi. Samwel

(2012a) naye anatoa mifano iliyo dhahiri ya kuingiliana kwa tanzu ya nyimbo na maigizo (sanaa

za maonyesho) katika muziki wa Bongo Fleva. Katika muziki huu tunaona kwamba kuna

mwingiliano mkubwa baina ya utanzu wa nyimbo na utanzu wa maigizo. Tunaona kwamba

nyimbo za Bongo Fleva zinaporekodiwa katika kanda za video au sidii za kuona (DVD/VCD)

kuna namna fulani ya maigizo ya yale yanayoimbwa. Msanii anapoimba kuhusu kumfumania

mpenzi wake, kwa mfano, tunaona pia anaigiza zoezi zima la kufumaniwa na kuufanya wimbo

15

huo kuwa kama hadithi inayoimbwa. Kuingiliana huku kwa Bongo Fleva na Maigizo ndiko

kulimfanya Mahenge (2012) kuhoji ikiwa muziki wa Bongo Fleva ni utanzu wa nyimbo au

sanaa za maonyesho.

(iv) Tanzu za fasihi simulizi hubadilikabadilika kutegemeana na muktadha wa utendaji na

wakati. Kama tulivyoeleza hapo juu kwamba tanzu za fasihi simulizi hubadilika, tanzu mpya

huweza kuibuka na zamani kufa. Hivyo, ni vigumu kueleza kuna tanzu ngapi za fasihi simulizi

labda pia itajwe uainishaji huo ni kwa wakati gani? Tukitumia andiko la Samwel (2012a)

tunabaini kwamba anashughulikia utanzu wa fasihi simulizi wa nyimbo na kipera cha

majigambo ya Bongo Fleva. Kama anavyobainisha mwenyewe kwamba utanzu huu umeibuka

miaka ya 1980 na kushika kasi miaka ya 1990, hivyo utanzu huu haukuwapo kabla ya mwaka

1980. Kwa hiyo, kama mtu akitumia uanishaji wa tanzu za fasihi simulizi uliofanywa miaka ya

1960 ni wazi kwamba hatakuwa na aina hii ya utanzu maana haikuwapo wakati huo.

Kutokana na sababu hizo, na nyingine nyingi, imekuwa vigumu sana kubainisha tanzu za fasihi

simulizi. Hata hivyo, kwa minajili ya kurahisisha usomaji wa fasihi simulizi kwa wakati wa sasa,

tunachukulia hapa kwamba fasihi simulizi ina tanzu sita ambazo ni kama ifuatavyo:

UAINISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI

1. NUDHUMU

(a) Nyimbo

· Uainishaji wa nyimbo kidhima

i. Tumbuizo

- Bembelezo

- Mbolezo

ii. Tukuzo

iii. Simango

iv. Chapuzo

- Nyimbo za uvuvi na ubaharia (Kimai)

- Nyimbo za makuli

- Nyimbo za kilimo (wawe)

- Nyimbo za kutwangia na kupepetea

- Nyimbo za michezo ya watoto

- Nyimbo za mapigano vitani n.k.

· Uainishaji wa nyimbo kimaudhui

i. Nyimbo za siasa

ii. Nyimbo za dini

iii. Nyimbo za kitamaduni

· Uainishaji wa nyimbo kifanani/hadhira

i. Nyimbo za wazee

ii. Nyimbo za vijana

iii. Nyimbo za watoto

iv. Nyimbo za wanawake

v. Nyimbo za wanaume

· Uainishaji wa nyimbo kimuktadha

i. Nyimbo za jandoni

ii. Nyimbo za unyagoni

iii. Nyimbo za kisimani

iv. Nyimbo za majumba ya ibada

(b) Maghani

· Uainishaji wa maghani kidhima

i. Maghani tumbuizo: haya ni maghani ambayo yanakusudia kutoa burudani kwa hadhira

husika.

16

ii. Maghani tukuzo/sifo: haya ni maghani ambayo dhima yake kuu ni kueleza sifa za mtu

binafsi au za mtu mwingine.

iii.Maghani simango: maghani ambayo dhima yake kuu ni kumsimanga mtu fulani juu ya

mambo aliyoyafanya au anayoaminika kuwa nayo. Kwa kawaida, mambo

anayosimangiwa mtu huwa ni mabaya na hayakubaliki katika jamii husika.

· Uainishaji wa maghani kiutendaji

i. Maghani nafsia

ii. Maghani simulizi

2. NATHARI

(a) Nathari za Kihistoria

i. Visasili: ni hadithi zinazoelezea kwanini viumbe wamekuwa na sifa, tabia au

maumbile ya namna fulani. Kwa mfano, kwanini kobe ana magambamagamba.

ii. Visaviini: ni hadithi zinazoelezea chimbuko la jamii ya watu, kabila, taifa au hata

miungu fulani ya jamii.

iii. Mighani (Visakale)

iv. Mapisi

v. Nasabu/ Shajari

vi. Tarihi

vii. Kumbukumbu

(b) Nathari za Kibunifu

i. Ngano

- Hurafa/ khurafa

- Hekaya

ii. Mbazi

iii. Istiara

iv. Michapo

3. TANZU FUPIFUPI

(i) Methali

(ii) Vitendawili

(iii) Shirikina: ni semi ambazo hutoa onyo kwa jamii juu ya jambo fulani la kiimani.

Hizi hujumuisha marufuku na makatazo ama miiko ya jamii husika. Shirikina

huweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:

- Shirikina za matendo: ukinyoa nywele usiku unakaribisha msiba, ukinyooshea

kidole makaburi kidole kinapinda, kufagia nyumba usiku ni kufukuza baraka,

kuomba chumvi usiku ni kukaribisha misiba n.k.

- Shirikina za wanyama: bundi kulia karibu na nyumba ni ishara ya msiba, kondoo

kuangalia juu ni ishara ya mwisho wa dunia, jogoo kuwika usiku wa manane ni

kukaribisha nuksi n.k.

- Shirikina za jadi: mkono ukiwasha ni ishara kwamba utapokea fedha, macho

yakichezacheza ni ishara kwamba utaona jambo la ajabu sana na nyinginezo.

(iv) Mafumbo

(v) Simo/Misimu

(vi) Vichekesho

(vii) Lakabu

(viii) Misemo

(ix) Vitanza-Ndimi/ Kauli Tauria

4. MAZUNGUMZO

(i) Umbea (fasihi ya wanawake): ni mazungumzo ambayo kwa kawaida huwa ni kati

ya mwanamke na mwenziye yanayohusisha kuwasema watu juu ya mambo mabaya

17

waliyonayo. Mambo hayo huweza kuwa ya kweli au hata ya kubuni lakini pale yanapokuwa

ya kweli huongezewa chuku ndani yake. Kwa kawaida mtu anayesemwa katika

mazungumzo haya huwa hawepo wakati wa mazungumzo.

(ii) Hotuba

i. Hotuba za kimila

- Hotuba za matambiko: hotuba zinazotolewa katika shughuli ya kuwatambikia

mizimu, iwe makaburini, kwenye miti mikubwa au popote pale.

- Hotuba za kuposea: hotuba itolewayo na mshenga wakati wa kuomba kibali

cha kuoa kutoka katika ukoo fulani.

ii. Hotuba za kisiasa

iii. Hotuba za kidini

(iii) Soga

(iv) Mawaidha

(v) Mizaha

(vi) Utani

(vii) Mchongoano

(viii) Maombi

5. DRAMA SIMULIZI

(a) Komedia/Futuhi: ni drama za vichekesho ambapo fanani huiga tabia kadha wa

kadha ili kuichekesha jamii na kuifunza wakati huohuo. Mifano mizuri ya komedia

ni “Ze Orijino Comedy” inayorushwa na kituo cha televisheni cha TBC1, “Futuhi”

inayorushwa na Televisheni ya Star (Star TV) na “Ze Comedy” inayorushwa na

Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) nchini Tanzania. Pia inajumuisha vipindi

vya “Vioja Mahakamani” vinavyorushwa na televisheni mbalimbali nchini Kenya.

(b) Michezo ya Kuigiza

i. Maigizo ya watoto: mfano mzuri wa maigizo ya watoto ni michezo ya “cha

baba na mama” ambapo mtoto mmoja hujifanya baba, mwingine mama na

mwingine jogoo. “Baba” na “mama” huigiza matendo ya baba na mama halisi na

hata wanapoenda kulala, hulala pamoja. Kazi za jogoo huwa ni kuwika pindi

baba na mama wanapolala ili kuwaamsha.

ii. Maigizo ya msibani

iii. Maigizo ya sherehe

iv. Maigizo ya kidini

(c) Miviga

Kumekuwa na utata kuhusiana na ufasihi wa utanzu huu. Utata huo unatokana na

ukweli kwamba kuna baadhi ya mambo yanayotendeka katika miviga si fasihi hasa

bali huweza kuwa sanaa nyingenezo. Ikumbukwe kuwa fasihi ni sanaa itumiayo

lugha (maneno). Hivyo, kinachochukuliwa kuwa fasihi katika miviga ni matini na si

matendo yasiyo na maneno. Katika matambiko, kwa mfano, maneno, manuizo na

nyimbo zinazoambatana na tukio husika ndiyo fasihi simulizi lakini si matendo

yanayotendwa yasiyokuwa na maneno. Katika jando na unyago pia matini na

nyimbo na baadhi ya maigizo yenye maneno ndizo kazi za fasihi. Matendo ambayo

hayana maneno hayawezi kuwa fasihi. Hivyo, vipera vya utanzu huu vinapaswa

kuchunguzwa kwa tahadhari kubwa. Miongoni mwa vipera hivyo ni kama ifuatavyo:

(i) Matambiko

(ii) Jando

(iii) Unyago

(iv) Sherehe za kutolea majina

18

6. FASIHI NGOMA

Utanzu wa fasihi ngoma katika fasihi simulizi unasemwa kuwa ni miongoni mwa tanzu

kongwe sana kwani ulianza sambamba na uumbaji wa dunia. Ushe (2012) akimnukuu Melvin

(1975) anabainisha hili anaposema:

The Talking Drum is the cultural instrument which have endured and survived the test of

time up to the present generation. The history of the Talking Drum is as old as creation

itself. In many parts of Africa, the Talking Drum is used as means of notification,

alertness and entertainment of people in palaces or during ceremonies.

Ngomezi ni zana ya kitamaduni ambayo imepitia vizazi mbalimbali hadi kufikia kizazi

cha sasa. Historia ya ngomezi ni kongwe kama ilivyo historia ya uumbaji wenyewe.

Katika sehemu nyingi za Afrika, ngomezi hutumika kama njia ya mawasiliano, kutoa

tahadhari na kuburudisha watu katika makasri ya Wafalme na watawala au wakati wa

sherehe (Tafsiri yetu).

Nukuu hii inathibitisha kuwa utanzu huu umekuwapo katika jamii za Kiafrika kwa muda mrefu.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, utanzu huu ni mchanga kuliko tanzu nyinginezo za fasihi

simulizi na si utanzu unaoeleweka vizuri sana miongoni mwa wanafunzi wa fasihi. Tunauchukulia

kuwa ni mchanga kutokana na ukweli kuwa ni utanzu ambao haujaanza kubainishwa zamani sana

japo umekuwapo katika jamii mbalimbali kwa muda mrefu. Labda kutotambulika kwake

kulitokana na wanafasihi kusita kuitambua ngoma kama kazi ya fasihi. Ngoma kwa uasili wake

huonekana kama aina ya sanaa za maonesho (Mhando na Balisidya, 1976:7), lakini si fasihi kwa

kuwa fasihi ni sanaa ambayo ni lazima itumie lugha kuwasilisha maudhui kwa jamii lengwa. Kwa

kuwa ngoma katika makabila mengi huwa ni midundo tu isiyokuwa na lugha yoyote itokayo katika

midundo hiyo, wanafasihi wengi waliacha kubainisha uwezekano wa kuwa na fasihi ngoma.

Ukweli ni kuwa upo uwezekano wa kuwa na ngoma ambayo inatoa lugha (maneno). Ngoma hizo

kwa kawaida huwa ni tofauti na ngoma za kawaida na ndiyo maana wanafasihi wengi huziita

ngomezi.

Sababu ya pili iliyosababisha utanzu wa ngoma kuchelewa kubainishwa na wanafasihi ni

kuwa aina hii ya fasihi haipatikani katika jamii nyingi sana kama zilivyo tanzu nyingine za fasihi

simulizi. Utanzu huu unasemwa kuenea sana katika jamii za Afrika Magharibi na tafiti za hivi

karibuni zimejaribu kubainisha kuwa upo uwezekano wa fasihi hii kuwapo katika jamii za Afrika

Mashariki (taz. Mulokozi, 1996).

Utanzu wa fasihi ngoma au ngomezi kama unavyoitwa na wengine, umeelezwa sana na

Kwabena Nketia katika maandiko yake mbalimbali. Nketia ni profesa na mtaalamu wa muziki

aliyefanya tafiti nyingi katika miziki asilia ya Kiafrika na kuandika vitabu mbalimbali kikiwemo

The Music of Africa (1974). Katika utafiti wake kuhusu ngoma, Nketia alibaini kuwa kuna aina

tatu za ngoma. Ambazo ni ngoma za ishara (signal drumming), ngoma za kuchezwa (dance

drumming) na ngoma za kifasihi/ngomezi (talking drums). Uainishaji huu unatupa ufahamu kuwa

si kila aina ya ngoma ni ngoma za kifasihi (ngomezi); zipo ngoma ambazo hazina ufasihi wowote.

Ufasihi wa ngomezi unatokana na ukweli kuwa ni ngoma ambazo hugeza vidatu na toni za lugha

ya mazungumzo. Milio ya ngomezi inaweza kurekebishwa kulingana na jinsi wapigaji

wanavyozipiga na kubadilisha nguvu wanayoitumia katika kupiga. Mapigo hayo, kwa hiyo, hugeza

sauti ya watu wanaoongea na ndiyo maana huitwa ngomezi (Ushe, 2010 na 2012). Fasihi ngoma

hutoa sauti za kimapokeo zilizozoeleka katika jamii kama vile methali au majigambo na hivyo

kueleweka kirahisi miongoni mwa wanajamii. Neno la Kiingereza la utanzu huu “talking drums”

linasawiri uhalisi wa kile ngoma hizi zinachokifanya; ngoma hizi zinaongea. Hivyo, ngomezi ni

tofauti na aina nyingine za ngoma ambazo haziongei bali hutoa midundo tu kwa maksudi maalum

kama vile kuburudisha, kutoa taarifa na kadhalika. Aidha, ngomezi hazikueleweka kwa mtu yeyote

bali kwa watu wenye ujuzi na lugha inayogezwa. Vilevile, ngoma hizi zilipigwa na wapigaji

maarufu waliobobea katika upigaji wake, si kila mtu aliweza kuzipiga ngoma hizi.

Nketia (1963) anabainisha kuwa katika historia ya Afrika, fasihi ngoma imekuwa ikitumika

kwa malengo mbalimbali. Malengo hayo, hata hivyo, yamekuwa yakibadilika kulingana na wakati

19

na jamii husika. Kwa mfano, tunaona anayataja malengo ya fasihi ngoma katika jamii za jadi za

Kiafrika kuwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vijiji vya mbali na kuwaleta watu pamoja kama vile

kuitisha mikutano. Malengo mengine anayoyataja ni kusaidia kusuluhisha migogoro miongoni

mwa wanajamii na kutunza kumbukumbu muhimu za kihistoria na hivyo kuwakumbusha watu

matukio hayo ya kihistoria pindi zinapopigwa. Mbali na matumizi hayo anayoyataja Nketia, Ebeze

(2002) naye kama anavyonukuliwa na Ushe (2012) anabainisha matumizi ya fasihi ngoma katika

jamii nyingine za jadi za Kiafrika kuwa ilitumika pia wakati wa sherehe, kama vile sherehe za

kusimika watawala na machifu, harusi, sherehe za kutoa majina au sherehe za mazishi ya watu

maarufu. Ushe anaendelea kueleza kuwa zilipopigwa wakati wa kusimikwa watawala na machifu,

ngomezi ziliwatahadharisha watawala na machifu hao kutofanya mambo yasiyokubalika

yatakayowafanya wajute. Akizungumzia matumizi ya ngomezi katika jamii za kisasa, Nketia

(1963) anasema kwamba fasihi ngoma inatumika kutukuza au kuwalaani watu wengine na

kuwakaribisha wageni, kuisifu miungu na watu katika jamii, kuita mizimu, wahenga na mizuka,

kusahihisha makosa ya wanajamii, kutoa mazungumzo ya kimethali ili kuwawezesha watu

kuwasiliana na wazee na pia ni sehemu ya sherehe za kifalme au majigambo ya wahenga (maelezo

haya yanabainika pia katika Ushe (2007) na (2012)). Hii inabainisha kuwa malengo na matumizi

ya fasihi ngoma, kama ilivyo kwa tanzu nyingine za fasihi simulizi, ni mambo

yanayobadilikabadilika kulingana na jamii na wakati.

Mbali na matumizi hayo yanayobainishwa na wataalamu hao, matumizi ya fasihi ngoma

yameendelea kupanuka kadri muda unavyozidi kwenda. Kwa mfano, kuanzia karne ya 20

imeshuhudiwa ngomezi zikitumika katika muziki pendwa wa Afrika Magharibi. Fasihi ngoma

imetumika katika aina mojawapo ya muziki wa Senegal uitwao Mbalaksi. Pia imetumika katika

miziki ya Nijeria iitwayo Fuji na Jùjú (katika miziki hiyo ngomezi huitwa dùndún). Aidha,

tunaona wanamuziki wakizitumia ngomezi kwenye miziki yao ya kisasa. Mfano wa wanamuziki

hao ni kama vile Tom Waits ambaye amezitumia ngomezi kwenye wimbo wake uitwao "Trouble's

Braids," iliyo katika albamu iitwayo Swordfishtrombones na Erykah Badu aliyezitumia ngomezi

kwenye wimbo wake "My People," katika albamu iitwayo New Amerykah Part One (4th World

War). Wanamuziki wengine waliotumia ngomezi kwenye miziki yao ya kisasa ni King Crimson

ambaye alizitumia ngomezi kwenye wimbo wake utwao, "The Talking Drum" katika albamu

iliyopewa jina Larks' Tongues in Aspic na mwanamuziki wa Kinijeria anayechukuliwa kuwa

mahiri katika ngomezi Sikiru Adepoju, aliyezitumia ngomezi katika nyimbo zake

alizowashirikisha wasanii maarufu wa Ulaya na Marekani kama vile Stevie Wonder na Carlos

Santana. Mbali na kutumika kwenye miziki ya kisasa, ngomezi pia zimetumika kwenye filamu na

tamthilia. Mfano mzuri wa matumizi haya tunayaona katika filamu ya The Nun's Story iliyotolewa

mwaka 1959.1 Mabadiliko haya ya matumizi ya fasihi ngoma yanaunga mkono madai ya Samwel

(2012a) kuwa si kweli kwamba tanzu za fasihi simulizi hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi

kingine, bali hubadilika kulingana na wakati husika.

Kutokana na maelezo haya tunaungana na Samwel (2012b) kuwa fasihi ngoma huweza

kuainishwa katika aina kama vile fasihi ngoma za Taarifa, fasihi ngoma za Tahadhari, fasihi

ngoma za Uhusiano, fasihi ngoma za Tumbuizo. Fasihi ngoma za taarifa ni zile ambazo hupigwa

kwa lengo la kutoa taarifa fulani muhimu wakati ambapo fasihi ngoma za tahadhari hutoa onyo

kama tulivyoona hapo awali kuwa huweza kuwaonya watawala na machifu juu ya uongozi mbaya.

Aidha, fasihi ngoma za mahusiano ni zile zinazopigwa na vijana ili kuwasiliana na wazee wao

kama tulivyoona hapo awali. Fasihi ngoma za tumbuizo hujumuisha ngomezi zitumikazo katika

miziki na tanzu nyingine kwa lengo la kutoa burudani. Aina nyingine ambayo ni muhimu

kuiongeza hapa ni fasihi ngoma za miungu na mizimu. Hizi ni zile zinazopigwa ili kuwasifu na

kuwaabudu miungu na mizimu.

1 Maelezo haya kuhusiana na matumizi ya ngomezi kwenye tanzu mbalimbali za kisasa yamedondolewa katika mitandao

mbalimbali ikiwa ni pamoja na http://en.wikipedia.org/wiki/File:TalkingDrum.jpg

20

NB: Katika uainishaji huu tumefafanua/tumefasili dhana zile ambazo tunadhani ni ngeni au si maarufu

sana na kuziacha zile maarufu/zilizozoeleka. Aidha, tumefasili pia dhana ambazo uainishaji wetu ni

tofauti sana na uainishaji wa wataalamu mbalimbali waliotangulia na hivyo kama tusipozifafanua

zinaweza kufasiliwa zisivyostahili.

NUDHUMU SIMULIZI

Tanzu nudhumu simulizi ndiyo huitwa na wanafasihi wengine ushairi simulizi kwa kuwa

hapo awali haukuandikwa. Utanzu huu unaainishwa hapa kuwa ni wa kwanza. Tunauchukulia hapa

kuwa ni wa kwanza kwani wanafasihi wengi wanatoa madai ambayo tunayaunga mkono kwamba

ushairi au nudhumu kama tunavyouita hapa, ndiyo utanzu mkongwe zaidi katika historia ya fasihi

simulizi. Utanzu huu ulianza pale mwanadamu alipotoka kwenye uhayawani na kuanza kuzalisha

mali. Ili kuondoa machovu ya kazi, mwanadamu alianza kuimba tungo za kinudhumu ama nyimbo

na huo ndiyo ukawa mwanzo wa utanzu huu (Senkoro, 1988:1-2). Hivyo, nudhumu za kazi ndiyo

huchukuliwa kuwa ushairi wa mwanzo kabisa katika historia ya mwanadamu. Ushairi huu

uliwasilishwa kwa kutumia lugha mbalimbali za jamii husika. Utanzu huu unaonekana kuwa na

vipera viwili ambavyo ni nyimbo na maghani. Tuchambue baadhi ya nudhumu hizi simulizi kama

ifuatavyo:

I. NYIMBO

Nyimbo ni aina ya nudhumu ambayo huwasilishwa kwa toni ya uimbaji. Sauti hii ni tofauti na

vipera vingine vya fasihi simulizi ambavyo huweza kughanwa (maghani/ghani), kutongolewa

(tongozi) au kusemwa (masemezo). Hata hivyo wapo baadhi ya wanafasihi wanaodai kwamba upo

uwezekano wa nyimbo kughanwa, kutongolewa au kusemwa. Jambo hili kama tutalikubali basi

tunapaswa kujiuliza tofauti kati ya nyimbo, maghani na mighani ipo wapi sasa? Katika kitabu hiki

tutazijadili dhana hizo kuwa ni tofauti. Uainishaji wa utanzu wa nyimbo umekuwa na

mkanganyiko mkubwa sana miongoni mwa wanazuoni kwani kila mwanafasihi ameainisha utanzu

huu kwa kutumia mkabala wake. Katika andiko letu tutaainisha utanzu wa nyimbo kwa kutumia

vigezo vikuu vinne: kigezo cha dhima ya nyimbo, kigezo cha maudhui yabebwayo na nyimbo,

kigezo cha mahali/muktadha zinapoimbwa nyimbo na kigezo cha fanani/hadhira ya nyimbo husika.

(a) Uainishaji wa Utanzu wa Nyimbo kwa Kigezo cha Dhima

Dhima, kama inavyochukuliwa hapa, inarejelea kazi au jukumu. Hivyo, katika kigezo hiki

tunaainisha nyimbo kwa kuangalia kigezo cha kazi inayofanywa na nyimbo husika katika jamii.

Nyimbo huweza kuwa na kazi ya kutumbuiza, kutukuza au kuchapuza kazi. Pia nyimbo huweza

kutumika kubembelezea mtu, kuomboleza misiba na majanga mbalimbali na kadhalika. Hivyo,

kwa kutumia kigezo hiki, tuna aina kuu tatu za nyimbo ambazo ni tumbuizo, tukuzo na chapuzo.

(i) Tumbuizo

Neno “tumbuizo” linatokana na neno “tumbuiza.” Kitenzi kinapowekewa mofu “o” huashiria

matokeo kama ilivyo katika “piga” ambacho huzaa “pigo,” “imba” huzaa “wimbo” na kadhalika.

Hivyo, matokeo ya kutumbuiza ni tumbuizo. Tumbuizo ni nyimbo zinazotumbuiza yaani

zinazoburudisha na kusahaulisha machungu yaliyopo kwa wakati husika. Nyimbo hizi hutoa burudani

na kuliwaza. Tumbuizo huwa ni pamoja na bembelezo, yaani nyimbo za kubembelezea watoto na

mbolezo-nyimbo za misibani na katika majanga. Mtoto anapokuwa analia kutokana na sababu

mbalimbali anahitaji kitu cha kumtumbuiza ili aache kulia. Nyimbo huweza kufanya kazi hiyo na hivyo

kumtumbuiza mtoto hadi anyamaze na hata kulala. Vivyo hivyo panapotokea misiba mbalimbali watu

huimba nyimbo za kuliwazana na kujiliwaza ili kujisahaulisha misiba iliyowapata. Nyimbo hizi pia

huweza kutumika kupeana tumaini kwamba msiba uliotokea upo juu ya uwezo wa mwanadamu yeyote

na kwamba zaidi ya msiba husika bado kuna tumaini.

(ii) Tukuzo

Tukuzo ni neno linalotokana na kitenzi “tukuza.” Hivyo, tukuzo ni nyimbo ambazo zinakusudia

kumsifia na kumpa utukufu mtu binafsi au kikundi maalumu cha watu. Nyimbo za tukuzo huweza

21

kuwa zile zinazoimbwa kumsifia Mungu, mke na mume wakati wa ndoa, viongozi wa siasa na vyama

vyao, wapigania uhuru na vyama vyao na pia huweza kujumuisha nyimbo za uzalendo katika taifa

ambazo nyingine husifia taifa husika. Mfano mzuri wa nyimbo za tukuzo ni wimbo ufuatao wa dini ya

Kikristo:

Mwamba wenye imara

Kwako nitajificha

Maji hayo na damu

Yaliyotoka humu

Hunisafi na dhambi

Hunifanya mshindi

Kwa kazi zote pia

Siitimiza sharia

Nijapofanya bidii

Nikilia na kudhii

Hayaishi makosa

Ndiwe wa kuokoa

Sina cha mkononi

Naja msalabani

Nili tupu nivike

Ni mnyonge nishike

Nili mchafu naja

Nioshe nisijafa

Nikungojapo chini

Nakwenda kaburini

Nipaapo mbinguni

Na kukwona enzini

Roho yangu na iwe

Rahani mwako wewe

(Wimbo huu umenukuliwa kutoka katika Musoma Press (1998:58) Tenzi za Rohoni)

Wimbo huu unamtukuza Mungu wa Ukristo, “YEHOVA” kwamba ni Mungu mwenye nguvu. Nguvu

zake zinafananishwa na mwamba. Mwamba ni kitu kigumu ambacho mtu huweza kujificha na

asidhurike na jambo baya. Katika tukuzo hii ya dini tunaona kwamba Mungu anapewa uwezo mkubwa

sana kwamba yeye ndiye anayewasaidia wanadamu kushinda na ndiye mwokozi. Wakati ambapo

Mungu anatukuzwa namna hiyo mwanadamu anajidogosha kabisa na kujifanya kwamba ni kiumbe

kisichokuwa na uwezo wowote. Hii ni kawaida ya tukuzo nyingi, wakati ambapo kitu fulani kinasifiwa

kitu kingine hudogoshwa ili kukifanya kinachotukuzwa kionekane kikubwa zaidi (pawe na

mchomozo2). Hii inatokana na ukweli uliodhahiri katika lugha kwamba vitu vipo katika mfumo. Ili

tukijue kizuri hatuna budi kuwa na kibaya, vivyo hivyo ili tumjue mrefu hatuna budi kumjua mfupi.

Wakati wote tukiambiwa fulani ni mzuri tunajiuliza kuliko nani?

(iii) Simango

Maghani ambayo dhima yake kuu ni kumsimanga mtu fulani juu ya mambo aliyoyafanya au

anayoaminika kuyafanya na sifa alizonazo mtu au anazoaminika kuwa nazo. Kwa kawaida mambo

anayosimangiwa mtu huwa ni mabaya na hayakubaliki katika jamii husika.

(iv) Chapuzo

Chapuzo ni nyimbo zinazochapusha kazi. Aina za nyimbo hizi zilitegemea kazi iliyofanywa

na hivyo tulikuwa na nyimbo za uvuvi na ubaharia (kimai), nyimbo za kutwangia na kupepetea, nyimbo

za mapigano vitani na nyimbo za michezo ya watoto. Nyingine ni nyimbo za kilimo (wawe), nyimbo za

kusukia, nyimbo za upagazi, nyimbo za biashara na uchuuzi na kadhalika. Nyimbo hizi huweza kuwa

nyingi zaidi ya tulivyoziainisha hapa kwani kuna kazi za aina mbalimbali.

2 Mchomozo ni ile hali ya kitu kujitokeza au kujichomoza zaidi ya kitu kingine. Kitu chenye mchomozo huonekana zaidi ya

vingine visivyokuwa na mchomozo.

22

(b) Uainishaji wa Nyimbo Kimaudhui

Katika kigezo cha maudhui, nyimbo huainishwa kwa kuangalia yale yaliyomo ndani ya nyimbo

husika. Tunaangalia ikiwa wimbo husika unabeba maudhui ya kisiasa, kidini, kiuchumi, kijamii au

kiutamaduni. Hivyo, tunaweza kuwa na aina mbalimbali za nyimbo kama vile:

(i) Nyimbo za kisiasa: kama vile nyimbo za kishujaa na kizalendo

(ii) Nyimbo za kiuchumi: kama vile nyimbo za kilimo

(iii)Nyimbo za kijamii: kama vile nyimbo za mapenzi

(iv)Nyimbo za kiutamaduni: kama vile nyimbo za dini

(c) Uainishaji wa Nyimbo kwa Kifanani/Hadhira

Katika kigezo hiki tunaangalia fanani na/au hadhira wa nyimbo husika. Kinachozingatiwa ni

ikiwa fanani na/au hadhira ni wanawake au wanaume, ni vijana, wazee au watoto na kadhalika. Hivyo

kwa kutumia kigezo hiki tunaweza kupata aina zifuatazo za nyimbo:

(i) Nyimbo za wanawake

(ii) Nyimbo za wanaume

(iii)Nyimbo za wazee

(iv)Nyimbo za vijana

(v) Nyimbo za watoto

(d) Uainishaji wa Nyimbo Kimuktadha

Kigezo cha muktadha kinazingatia nyimbo husika huimbwa wapi na kwa ajili gani? Nyimbo

huweza kuimbwa jandoni na unyagoni, katika nyumba za ibada kama vile makanisani na misikitini,

katika harusi, katika tambiko na kadhalika. Hivyo kwa kigezo hiki tunapata aina zifuatazo za nyimbo:

(i) Nyimbo za tohara (nyimbo za jandoni na unyagoni)

(ii) Nyimbo za harusi

(iii) Nyimbo za tambiko

(iv) Nyimbo za kisimani

(v) Nyimbo za majumba ya ibada n.k.

II. MAGHANI

Maghani ni aina ya ushairi inayotumia sauti iliyo kati ya kuimba na kuongea, sauti hiyo huitwa sauti

ya kughani. Tofauti ya nyimbo na maghani ni kwamba wakati nyimbo hutumia sauti ya kuimba,

maghani hutumia sauti ya kughani. Maghani huweza pia kutongolewa. Uainishaji wa maghani

unatumia vigezo vikuu viwili ambavyo ni kigezo cha dhima na kigezo cha utendaji.

(a) Uainishaji wa Maghani kwa Kigezo cha Dhima

Kuainisha maghani kwa kuzingatia dhima ni kama tulivyoainisha nyimbo. Maghani, kama zilivyo

nyimbo, huweza kuwa na dhima ya kutumbuiza, kuburudisha na kadhalika. Hivyo, miongoni mwa aina

za maghani kwa kigezo hiki ni kama ifuatavyo:

(i) Maghani Tumbuizo

Haya ni maghani ambayo hulenga kutoa burudani. Hili ni kundi ambalo huweza kujumuisha pia

aina nyingine za maghani kwani maghani, kama kazi nyingine za fasihi, huwa na dhima kuu mbili

ambazo ni kuelimisha na kuburudisha. Katika kuburudisha ndipo kwenye dhima ya kutumbuiza.

(ii) Maghani Tukuzo/Sifo

Aina hii ya maghani huhusisha tungo ambazo hueleza sifa za mtu binafsi (majigambo) ama

tungo za mtu mwingine (tondozi). Katika majigambo, mjigambi hujitukuza mwenyewe juu ya mambo

mbalimbali ya kishujaa na kijasiri aliyoyafanya au anayoyaamini kuyafanya kwa uwezo wake au kwa

nasaba yake. Tondozi kwa upande mwingine, ni maghani ambazo hutukuza kwa kuelezea sifa za mtu

mwingine, kitu kingine au hata miungu na mizimu.

23

(iii) Maghani Simango

Hii ni aina ya maghani ambayo dhima yake kuu ni kumsimanga mtu fulani juu ya mambo

aliyoyafanya au anayoaminika kuyafanya na juu ya sifa alizonazo mtu au anazoaminika kuwa nazo.

Kwa kawaida, mambo anayosimangiwa mtu huwa ni mabaya na hayakubaliki katika jamii husika.

(b) Uainishaji wa Maghani kwa Kigezo cha Utendaji

Katika kigezo hiki tunaangalia ikiwa fanani anasema na nafsi yake au na nafsi ya mtu mwingine na

ikiwa anawasilisha kwa njia ya kusimulia au nyinginezo. Hivyo, katika kigezo hiki kuna aina kuu mbili

kama ifuatavyo:

(i) Maghani nafsia

(ii) Maghani simulizi

2. USHAIRI KAMA UTANZU WA FASIHI ANDISHI

Zaidi ya ushairi kuwa utanzu wa fasihi simulizi, ushairi pia ni utanzu wa fasihi andishi. Uainishaji

wa tanzu katika fasihi andishi, kama ulivyo katika fasihi simulizi, si suala jepesi. Kimazoea wataalamu

wengi wamekuwa wakidai kwamba fasihi andishi ina tanzu kuu tatu ambazo ni ushairi, tamthilia na

riwaya. Mtazamo huu huenda ndiyo uliowaathiri hata watunga mitaala katika shule na vyuo mbalimbali

nchini Tanzania na ndiyo maana katika nchi hii tanzu za fasihi andishi zinazosomwa katika shule na

vyuo vingi ni ushairi, tamthilia na riwaya. Kwa mfano, katika elimu ya sekondari, katika fasihi andishi

wanafunzi wanafundishwa tanzu hizo tatu. Hali kama hiyo inaonekana pia katika miongozo ya kozi ya

fasihi andishi ya vyuo vingi, ikiwa ni pamoja na chuo kikuu kikongwe kuliko vyote nchini Tanzania,

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo tanzu zinazofundishwa kwa msisitizo zaidi ni tatu tu, ushairi,

tamthilia na riwaya. Hii ina maana kwamba wataalamu hawa hawautambui utanzu wa hadithi fupi.

Aidha, nafasi ya utanzu wa novela katika fasihi andishi haiwekwi wazi, yaani ikiwa ni utanzu

unaojitegemea au ni sehemu ya utanzu wa riwaya. Kutokana na hilo tanzu za novela na hadithi fupi si

tanzu zinazoeleweka sana miongoni mwa watu wengi.

Hivyo, ili kurekebisha kasoro hizo, tunapendekeza kwamba fasihi andishi ichukuliwe kuwa na

tanzu kuu nne ambazo ni ushairi, tamthilia, hadithi fupi na riwaya. Novela tunaichukulia kuwa ni

sehemu ya riwaya. Hata hivyo, katika andiko hili msisitizo wetu ni katika utanzu wa ushairi na

hatutachambua tanzu nyingine za fasihi andishi.

DHANA YA USHAIRI ANDISHI WA KISWAHILI

Kabla ya kuzama katika dhana ya ushairi andishi, kwa kuwa tunashughulikia ushairi andishi wa

Kiswahili, hatuna budi kujiuliza ushairi wa Kiswahili ni upi? Swali hili si rahisi kulijibu kwani

linaturudisha katika swali lilelile la miongo mingi la Mswahili ni nani hasa? Je, Mswahili ni mtu wa

pwani, ni mtu wa Tanzania, ni mtu wa Afrika Mashariki au Mswahili ni nani? Vivyo hivyo katika

mawanda hayo twaweza kujiuliza fasihi ya Kiswahili ni ipi? Je, ni fasihi iliyoandikwa kwa lugha gani?

Je, kila kazi ya fasihi iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ni fasihi ya Kiswahili? Na kama

haijaandikwa kwa lugha ya Kiswahili si fasihi ya Kiswahili? Tukiweza kuyajibu maswali hayo,

tutaweza pia kufafanua ushairi wa Kiswahili ni upi. Ili kukwepa kuurudia mjadala ambao umekufa,

tuchukulie tu kwamba ushairi wa Kiswahili ni ule unaosawiri maisha, mila na utamaduni wa Waswahili

pwani na bara. Mtazamo huo umeathiriwa na fasili ya Senkoro (1988:10-11) katika kitabu chake

Ushairi: Nadharia na Tahakiki kuwa ushairi wa Kiswahili ni ule unaojitambulisha na kujihusisha na

utamaduni wa Waswahili (yaani wananchi wa Afrika Mashariki na kati – pwani na bara). Tukiichukua

fasili hii katika muktadha wa fasihi ya Kiswahili kwa ujumla, tutasema kwamba fasihi ya Kiswahili ni

ile inayojitambulisha na kujihusisha na maisha na utamaduni wa Waswahili. Utamaduni unasemwa

kuwa ni jumla ya mambo yote ya jamii husika. Hivyo, utamaduni wa Waswahili hapa tunahusisha mila

na desturi za Waswahili; Sanaa zao, siasa, sayansi na uchumi wao, na maisha kwa ujumla. Hata hivyo,

Senkoro (khj) anaongezea jambo lingine kwamba ushairi wa Kiswahili unapaswa kuwa katika lugha ya

Kiswahili. Rejelea nukuu hii anaposema:

Zamani sana lugha ya Kiswahili ilikuwa ya watu wa pwani ya Afrika Mashariki tu. Lakini leo

hii hutumika Afrika Mashariki yote pamoja na nchi za jirani kama vile Zaire (sasa Jamhuri ya

24

Kidemokrasia ya Kongo), Burundi, Somalia na Malawi. Kwa hiyo ni wazi kwamba

tukiongelea kuhusu ushairi wa Kiswahili mara nyingi tunamaanisha ule ushairi uliotungwa

kwa lugha ya Kiswahili.... (Ufafanuzi na msisitizo ni wetu).

Hapa tunaona kwamba Senkoro (khj.) anasisitiza kwamba ushairi wa Kiswahili unapaswa kutungwa

katika lugha ya Kiswahili. Hata hivyo tunadhani kwamba jambo hili si wakati wote kwani upo

uwezekano wa ushairi wa Kiswahili (na kwa hiyo fasihi ya Kiswahili) kuandikwa katika lugha

nyinginezo. Hili haliishii tu katika ushairi na fasihi bali pia katika vipengele vingine vya lugha.

Tunalithibitisha hili, kwa mfano, katika andiko la Ashton (1944) ambaye ameandika Swahili Grammar

Including Intonation. Kitabu hiki japokuwa kinaihusu sarufi ya Kiswahili, kimeandikwa kwa kutumia

lugha ya Kiingereza. Kutumia lugha ya Kiingereza hakuipotezei sarufi iliyoandikwa sifa ya kuwa sarufi

ya Kiswahili. Kwa kulifahamu hilo labda ndiyo maana Senkoro hapo juu anasema (... tukiongelea

kuhusu ushairi wa Kiswahili mara nyingi...). Bila shaka anatambua kwamba inaweza kutokea mara

chache ukatungwa kwa lugha nyinginezo. Jambo hili kwa sasa limeongezeka zaidi na kuwa si mara

chache tena bali ni mara nyingi tu inawezekana kuandika ushairi wa Kiswahili kwa lugha nyinginezo au

kuandika ushairi wa lugha nyinginezo kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Hivyo, tuhitimishe kwa kusema kwamba ushairi wa Kiswahili kama unavyochukuliwa hapa ni ule

ambao unahusu utamaduni wa Waswahili bila kujali lugha iliyotumika kuuandika. Jambo la kusisitiza

hapa ni kwamba mambo yanayosawiriwa katika ushairi husika yaihusu jamii ya Waswahili, maisha

yao, falsafa zao na itikadi zao. Dhana ya Waswahili inayotumika hapa inamaanisha watumiaji wa lugha

ya Kiswahili katika shughuli zao za kila siku.

Baada ya kufahamu fasihi ya Kiswahili ni ipi na ushairi wa Kiswahili ni upi sasa turudi kwenye

suala letu la msingi kuhusiana na dhana ya ushairi. Pamekuwapo na fasili mbalimbali juu ya dhana ya

ushairi. Shabaya na wenzake (2009:1) wanatuthibitishia hili kwa kunukuu fasili kadha wa kadha za

ushairi zilizokwisha kutolewa hadi sasa. Baadhi ya fasili wanazozinukuu ni kama ifuatavyo:

· Ushairi ni mfuatano wa hisia nzito zilizokumbukizwa kutokana na utulivu (William

Wordsworth)

· Ushairi ni sauti za lugha ya binadamu katika nyakati ambapo zinakuwa karibu sana na sauti

za malaika na sauti za wanyama (John Wain)

· Ushairi ni maneno bora katika mpangilio bora (Samuel Taylor Coleridge)

· Ushairi ni habari inayobaki kuwa habari (Ezra Pound)

· Ushairi ni ule utungo ambao ni wa kifalsafa zaidi na wa thamani kubwa kuliko historia

(Aristotle)

· Ushairi unaanza kwa uzuri na kuishia kwa busara (Robert Frost)

(Tafsiri zote hapo juu ni zetu)

Hizi ni baadhi tu ya fasili zinazotolewa na Shabaya na wenzake (2009) na hivyo kuthibitisha kwamba

kuna fasili nyingi sana za ushairi. Fasili hizo, hata hivyo, zaidi ya wingi wake, tunazigawa, na ndivyo

zilivyogawiwa pia na wanazuoni wengine, katika mikabala mikuu miwili, mkabala wa kimapokeo na

mkabala wa kimamboleo (Taz. Senkoro, 1988; Mulokozi, 1996 na Githuma, 2010). Dhana “mapokeo”

kama inavyotumika hapa inarejelea ujadi au ukongwe. Hivyo, mkabala wa kimapokeo ni ule ambao

umekuwapo kwa muda mrefu katika historia ya ushairi. Mkabala wa kimamboleo, kwa hiyo, ni ule wa

kisasa. Yaani mkabala ambao umeibuka baada ya mkabala wa kimapokeo.

A. MKABALA WA KIMAPOKEO JUU YA DHANA YA USHAIRI

Mkabala huu ndiyo ulioanza katika kutoa fasili ya ushairi. Unaitwa wa kimapokeo kutokana na

ukweli kwamba wafuasi wa mkabala huu waliupokea kutoka kwa wazee bila kuhoji ikiwa mambo

yanavyoelezwa ndivyo yalivyo au la. Wao waliurithi tu. Dhana hii ya umapokeo ni tafsiri ya ile dhana

ya Kiingereza “traditional approach.” Miongoni mwa wanamapokeo wanaojulikana zaidi ni kama vile

Amri Abedi, Shaaban Robert, Jumanne Mayoka, Amiri A. Sudi (Andanenga), Haji Gora Haji na

wengineo. Wanamapokeo hawa wamewaathiri wengi na hadi sasa pameshakuwapo na wanamapokeo

wengi tu. Hebu tupitie fasili chache za kimapokeo:

Gituma (2010) anafasili shairi kuwa ni mtungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya

mkato katika usemi, maandishi au wimbo unaoelezea wazi juu ya mawazo, hisi au tukio juu ya maisha

na ambao hufuata utaratibu wa urari na muwala maalum uliosheheni kanuni za utunzi wa mashairi…

25

Fasili hii inasisitiza kwamba “shairi ni wimbo, shairi huwa na urari (bila shaka wa vina na mizani),

shairi huwa na kanuni mbalimbali.” Maeneo haya anayoyasisitiza Gituma bila shaka yametokana na

athari za Abedi (1954:1) ambaye imani hiyo ilimfanya kuandika kitabu alichokiita Sheria za Kutunga

Mashairi na Diwani ya Amri. Jambo la dhahiri hapa ni kwamba Amri Abedi, kama alivyo Gituma,

anaamini kwamba utunzi wa mashairi una kanuni maalum. Aidha, wazo la Gituma kwamba shairi ni

wimbo linabainika pia humo katika Amri Abedi na anaongeza kwamba kama shairi haliimbiki basi

halina maana. Mtazamo huu kwamba shairi ni wimbo ndiyo unaotawala sana miongoni mwa

wanamapokeo wengi na tunauona pia kwa Mwaruka (1968) anaposema kwamba:

Mpaka miaka hii ya karibuni watunzi na waimbaji mashairi na tenzi katika nchi yetu

wameongezeka sana. Tena inafurahisha mno kuona kwamba utungaji wa mashairi unafundishwa

katika shule zetu za Tanzania. Kwa hivi, inadhihirika kwamba baada ya miaka michache

Tanzania itakuwa na watungaji na waimbaji wengi zaidi (msisitizo ni wetu).

Katika maelezo haya Mwaruka anasisitiza uimbikaji wa shairi na tenzi. Hii ni kusema kwamba

anachukulia kuwa shairi linatungwa ili liimbwe na hadhira husika. Wazo hili la Mwaruka linapewa

nguvu na fasili ya Uvetie (1976) anaposema kwamba, “napenda kuwafafanulieni kwamba mashairi ni

usemi usemwao kwa namna ya mafumbo, na pia ni nyimbo.” Yeye zaidi ya kusisitiza ushairi kuwa ni

wimbo, anaibua dhana nyingine kwamba shairi lazima liwe fumbo. Hii ni kusema kwamba kama shairi

si fumbo basi si shairi. Aidha, Mnyampala (1964:4) anabainisha kwamba mashairi ni nyimbo zenye

maghani ya mvuto wa madoido na vingorimbo bora. Hapa Mnyampala zaidi ya kuungana na

wanamapokeo wengine kwa kuuona ushairi kuwa ni wimbo, anaongeza suala la mvuto wa madoido na

vingorimbo bora. Anachokisema hapa ni kwamba ushairi lazima utumie lugha tamu yenye madoido.

Dhana ya ushairi kama utamu wa lugha inaonekana pia kwa Uvetie (1976) ambaye anachagua kukiita

kitabu chake cha mashairi Utamu wa Lugha. Anachokionesha hapa ni kwamba ushairi hubeba utamu

wa lugha.

Fasili hizi (za wanamapokeo) zinachukulia kwamba shairi lolote lile lazima liimbike. Fasili hizi

zinaweza kuonekana kuwa sahihi zaidi katika fasihi simulizi ambapo utanzu wa ushairi (na hasa ushairi

simulizi) unachukuliwa kuwa ni wimbo. Kimsingi tunapozungumzia utanzu wa ushairi katika fasihi

simulizi tunazungumzia nyimbo za aina mbalimbali za makabila ya Kiafrika. Hivyo, fasili hii haifai

tunapozungumzia ushairi andishi, ambao ndiyo hasa tunauzungumzia hapa (hata hivyo, dhana ya shairi

kuwa ni wimbo ni muhimu kama tutakavyoijadili hapo baadaye katika sura ya tatu). Ushairi kama

wimbo ulionekana sana katika miaka ya awali ya maendeleo ya taaluma ya ushairi wa Kiswahili (kabla

ya mwaka 1960-1970). Baada ya hapo dhana ya ushairi kama wimbo ilipingwa vikali. Hadi sasa

inakubalika miongoni mwa wanazuoni, na katika fasihi ya Kiswahili kwamba, shairi si lazima liimbike.

Shairi linaweza kughanwa, kutongolewa au hata kusemwa. Kwa kusema kwamba shairi lazima

liimbike, Abedi ana maana kwamba shairi lazima liwe na urari wa vina na mizani. Mashairi

yanayopishana sana vina na mizani ni vigumu sana kuyaimba. Dhana hii ya urari wa vina na mizani

kama sifa kuu ya shairi imepingwa vikali na hatimaye kubainika kwamba shairi linaweza kuwa na urari

wa vina na mizani au lisiwe nao na bado likabaki kuwa shairi. Jambo la kukumbuka ni kwamba shairi

linapokosa urari wa vina na mizani kuna uwezekano mkubwa wa shairi husika kutokuimbika. Hivyo,

dhana ya shairi kama wimbo si ya msingi japo hatuwezi kuipuuza kabisa kwani inajaribu kutupa

upande mmoja wa shilingi wa shairi.

Zaidi ya msisitizo katika kanuni na uimbikaji, fasili nyingine za ushairi zimejikita zaidi katika

dhima ya ushairi. Kwa mfano, tunaona Mnyampala (1975) kwenye dibaji yake anaufasili ushairi kwa

kuzingatia nguvu ya shairi kuiasa, kuiongoza jamii pamoja na uzuri na utamu wa lugha. Anauona

ushairi kuwa ni utungo wenye maneno ya hekima na kwamba ndiyo utungo ulio bora sana katika

maongozi ya dunia. Anaendelea kufafanua kwamba kuna aina tano za mashairi kwa kuzingatia

maongozi na mafunzo yanayotoa. Aina hizo ni mashairi ya kawaida, mashairi ya furaha, mashairi ya

huzuni, mashairi mazito na mashairi ya kuadibu. Mashairi ya kawaida ni yale ambayo yana mawaidha

ya dunia, visa na mikasa ya kawaida na mengine ya aina hiyo wakati mashairi ya furaha hushangilia

tamasha iliyopo, kutakia heri na mafanikio, ombi la kudumisha furaha hiyo na waadhi kwa ajili ya

tafrija hiyo. Kwa upande wa yale yaliyomo katika mashairi ya huzuni Mnyampala anayataja kuwa ni

rambirambi, maombezi kwa Mungu kwa ajili ya marehemu, maombezi kwa wale waliobaki

26

wanaomhusu, historia ya marehemu na kumbukumbu itakiwayo. Nayo mashairi mazito huwa ni

mashairi ya kuzama (kufumba), mashairi ya tambo, pigo kuu la ushairi, furaha ya ushairi na taaluma

zake na kuonyesha mbinu za lugha ya mshairi yule. Aina ya mwisho ambayo ni mashairi ya kuadibu

inajumuisha mashairi ya kumuonya mtu kinagaubaga bila kutumia utusi, kumtanabahisha ya hatima,

mashairi kuhusu maandiko matakatifu na yale yahusuyo uungwana na kadhalika. Tunachokiona hapa ni

kwamba Mnyampala (khj.), zaidi ya kushadidia wazo la wanamapokeo kwamba ushairi ni lazima uwe

na urari wa vina na mizani, anasisitiza kuwa shairi lazima litoe mawazo yenye hekima yenye

kumwongoza mwanadamu. Wakati ambapo tunakubaliana na wazo hili la Mnyampala kuwa shairi

linaweza kumwongoza mwanadamu, tunaona kwamba ushairi unapaswa kufasiliwa kwa kuzingatia

nduni bainifu na si nduni jumuishi kwani tanzu zote za fasihi huwa na jukumu hilo la kumwongoza

mwanadamu. Moja ya dhima kuu za fasihi ni kuelimisha, hivyo ndiyo kusema tanzu zote za fasihi

huweza kuelimisha. Hata hivyo izingatiwe kwamba si kila shairi hubeba mawazo ya hekima na

linakusudia kutoa maongozi kwa jamii. Yapo mashairi mengi ambayo yanapotosha jamii. Fasihi zaidi

ya uwezo wake mkubwa wa kuielimisha jamii, inaweza pia kuipotosha jamii hiyo. Samwel (2012a)

akifafanua jinsi fasihi inavyoweza kupotosha jamii, isipochukuliwa kwa tahadhari, anaonyesha jinsi

ushairi wa Bongo Fleva unavyoweza kuhamasisha ngono na matendo mengine yasiyofaa katika jamii.

Aidha, tukizama zaidi katika uainishaji wa Mnyampala tunabaini kwamba kuna upungufu mkubwa.

Kwa mfano, anaposema kwamba mashairi ya kuadibu ndiyo huwaonya watu na kuwaadibisha juu ya

uungwana na maandiko matakatifu ni kusema kwamba mashairi anayoyaita ya kawaida (na ya aina

nyinginezo anazozianisha) hayamwadibishi hadhira katika maeneo hayo. Jambo hilo kwa hakika

linaweza kupingwa na wengi kwani mashairi ya aina zote anazozianisha Mnyampala yanaweza

kuadibisha juu ya hayo. Kama hiyo haitoshi, majina ya aina za mashairi anayoyatumia ni telezi mno.

Kwa mfano, anapoyaita mashairi mazito twaweza kuhoji uzito huo ni wa nini? Tunaweza pia kuhoji juu

ya mashairi ya furaha kama ni ya furaha kwa kila mtu? Hoja hiyo pia twaweza kuiibua kwenye

mashairi ya huzuni.

Nayo fasili ya Robert (1968), zaidi ya kusisitiza vipengele kama urari wa vina na uimbikaji, inaibua

pia dhana ya ushairi kuwa ni utungo wenye kuvuta moyo kwa namna ya ajabu. Dhana karibu sawa na

hii inaonekana pia katika Mulokozi na Kahigi (1979). Hata hivyo dhana ya ushairi kuvuta moyo kwa

namna ya ajabu (kuburudisha moyo kwa namna ya ajabu, kama inavyodaiwa na wanazuoni wengine) ni

dhana telezi mno na iliyopingwa na wanazuoni wengine. Kwa mfano, Macgoye (2009:2) akipingana na

mtazamo huo anasema kwamba, “Poetry is a human creation. It can be attractive to some people and

repulsive to others. It can be fashionable or unfashionable,” yaani ushairi ni ubunifu wa binadamu.

Unaweza kuwa wa kuvutia kwa watu fulani lakini kuwa wa kuchukiza kwa wengine. Unaweza kuwa

mzuri au mbaya (tafsiri yetu). Hivyo, dhana kwamba ushairi huvuta moyo si sahihi sana na haitusaidii

kuufasili ipasavyo ushairi na labda kuutofautisha na tanzu nyingine maana hata hizo huweza kuwa na

sifa hiyo.

Udhaifu mkubwa unaoonekana katika fasili za wanamapokeo ni kule kudai kwamba shairi bora,

zaidi ya mambo mengine, lazima liwe na urari wa vina na mizani. Jambo hili limesababisha kuibuka

kwa mashairi mengi ambayo japo yanazingatia urari wa vina na mizani bado hayatimizi jukumu la

msingi la fasihi, kuelimisha na kuburudisha. Mashairi mengi hayana maana kabisa. Hoja hii

ilishadokezwa zamani na Abedi katika dibaji ya Akilimali (1971) kwamba:

Watungaji wenye ujuzi mdogo hujipangia tu mashairi muradi vina vipatane, wakaacha

kueleza sababu za mashairi zikifahamika. Lakini mafundi wengi wa mashairi ya

Kiswahili waliopo leo ni watu wanaoeleza falsafa ya maisha na mambo ya hekima sana,

na mahitaji yao…

Hii ina maana kwamba kuna haja ya mashairi kusisitiza maudhui kuliko fani ili ushairi wa Kiswahili

uweze kutimiza jukumu lake la kuielimisha jamii. Hata hivyo ieleweke kuwa hatusemi hapa kwamba

washairi waipuuze fani maana fani na maudhui hutegemeana, hufungamana na kuathiriana.

Tuhitimishe mjadala huu kwa kusema kuwa kwa wanamapokeo ili utungo uitwe shairi hauna budi

kuwa na urari wa vina na mizani na pia uwe unaielimisha jamii kwa namna ambayo hadhira

wanafurahia. Utungo wowote mwingine ambao hauna sifa hizo, kwao wao si ushairi. Japo tumeeleza

udhaifu wa mtazamo huu ieleweke tangu mapema kwamba hii haimaanishi kuwa wanamapokeo

27

hawakuwa na mchango wowote katika kufasili ushairi wa Kiswahili. Walikuwa na mchango mkubwa

na wao ndiyo hasa walioanzisha kutafuta ukweli juu ya ushairi wa Kiswahili hasa ni upi? Aidha,

ieleweke kwamba wanamapokeo wamewaathiri watu wengi na hata leo hii ambapo kuna mtazamo wa

kisasa wa kufasili ushairi (kama tutakavyoona katika sehemu inayofuata) bado watu wengi

wanachukulia kwamba ushairi lazima uende sambamba na urari wa vina na mizani, matumizi ya lugha

isiyokuwa ya kawaida na kuvutia moyo (kama tulivyoona kwa Mulokozi na Kahigi hapo juu). Katika

uzoefu wetu wa ufundishaji wa somo la ushairi, kila tulipowapa wanafunzi nafasi ya kutunga mashairi,

walitunga mashairi yenye urari wa vina na mizani na yenye beti na hivyo kudhihirisha kwamba

wameathiriwa sana na mtazamo huu. Labda kwa kuwa mtazamo huu ndiyo unaoonekana kufundishwa

katika ngazi mbalimbali za elimu ya awali na hasa elimu ya msingi na sekondari kama ilivyodokezwa

hapo awali na Mwaruka (1968).

B. MKABALA WA KISASA/KIMAMBOLEO JUU YA DHANA YA USHAIRI

Mtazamo huu ni wa hivi karibuni, katika miaka ya 1960 na 1970. Wanausasa hutunga mashairi

yanayoitwa masivina, yaani mashairi yasiyokuwa na vina ndiyo maana katika baadhi ya maandiko

mtazamo huu huitwa mkabala wa kimasivina. Wanazuoni wanaoupigia chapuo mkabala huu ni pamoja

na Theobald Mvungi, Fikeni Senkoro, Euphrase Kezilahabi, David Massamba, Kulikoyela Kanalwanda

Kahigi, Mugyabuso Mulokozi na wengineo. Kama tulivyodokeza awali, hawa kwa namna mbalimbali

wameathiriwa na wanamapokeo katika fasili zao na hivyo kimsingi hawatoi fasili tofauti sana na

tulizozipitia awali isipokuwa hawasisitizi urari wa vina na mizani wala uimbikaji wa shairi kama sifa

kuu ya shairi katika lugha ya Kiswahili. Hebu tujivinjari baadhi tu ya fasili za ushairi zinazotolewa na

wanausasa:

Tukianza na Wamitila (2010b:104), tunaona jinsi athari za wanamapokeo zinavyojibainisha kwa

wanausasa. Wamitila, akiathiriwa kwa namna fulani na mkabala wa kimapokeo, anaufasili ushairi kuwa

ni sanaa inayotambulishwa na mpangilio maalum wa sentensi au vifungu; mpangilio ambao una

mdundo maalum au ruwaza fulani inayounda wizani, lugha ya mkato, mafumbo na mpangilio usio wa

kawaida wa vifungu fulani. Fasili hii ya Wamitila, japo ni ya hivi karibuni, lakini bado inashindwa

kutatua matatizo katika fasili ya ushairi yaliyoanzishwa tangu zama za kutamalaki wanamapokeo.

Ingawaje Wamitila amejitahidi sana kubainisha sifa za ushairi (kama vile lugha ya mkato, wizani,

ruwaza n.k.) bado anaibua mjadala katika baadhi ya dhana anazozitumia. Kwa mfano, anaposema

kwamba ushairi una mpangilio usiokuwa wa kawaida wa vifungu fulani, dhana hiyo inaweza ikapingwa

na wengine. Upinzani unaweza kutokana na ukweli kwamba si kila mara sifa hii na hata zile nyingine

alizotangulia kuzitaja zinajitokeza. Au tuseme sifa hizi hazijitokezi katika mashairi yote na hivyo

hatuwezi kuzichukulia kama kigezo cha kutathmini ikiwa utungo fulani ni ushairi ama siyo.

Nao Kanuri na wenzake (2009:32-33) wanafafanua kwamba ushairi hutumia lugha ya mkato,

taswira, ishara na mbinu nyinginezo kuwasilisha maudhui mazito kwa hadhira lengwa. Wakiwa

wanazungumzia zaidi ushairi simulizi, wanasisitiza kwamba ushairi sharti usheheni mafunzo au

mawazo mazito ili msikilizaji aguswe kihisia na kwamba malenga huwa ni mabingwa katika kutoa

maneno ya busara. Kwa hakika fasili hii haitofautiani hata kidogo na ile ya Robert (1968) tuliyoipitia

hapo awali au za wanamapokeo wengine. Tofauti pekee hapa ni kwamba akina Kanuri hawasisitizi

urari wa vina na mizani kama sifa kuu ya ushairi. Suala la malenga kuwa bingwa wa kutumia lugha na

kutoa maneno ya busara linajitokeza pia katika Kezilahabi (1976) ambapo, zaidi ya mambo mengine,

anasisitiza kwamba, ushairi huwa na upangaji mzuri wa maneno ya fasihi yenye mizani kwa kifupi ili

kuonyesha ukweli fulani wa maisha. Dhana ya “upangaji mzuri wa maneno” inamchukulia malenga,

yaani mshairi kuwa mtu mwenye ujuzi mkubwa wa lugha na hivyo hupanga lugha yake vizuri. Hata

hivyo uzuri huu unaoelezwa hapa haupo wazi, uzuri katika nini hasa? Kwamba hatumii lugha mbaya?

Lugha mbaya ni ipi? Au tuseme mpangilio mbaya wa lugha huwaje? Aidha, dhana ya “ukweli”

anayoiibua Kezilahabi pia ina utata mwingi. Ukweli ni nini na ukweli hasa ni upi? Wanafalsafa wengi

wanakiri kwamba kila uongo ni ukweli fulani wa maisha na kwamba ukweli wa mtu mmoja au kundi

moja la watu huweza kuwa uongo kwa mtu au kundi jingine la watu.

Fasili ya Mulokozi na Kahigi (1979:25) haiendi mbali sana na tulizikwisha zipitia. Wao wanasema

kwamba ushairi ni sanaa iliyopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha yenye muwala,

kwa lugha ya mkato, picha, sitiari au ishara, katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuleta

28

wazo au mawazo, kufunza au kueleza jambo au hisi fulani kuhusu maisha na mazingira ya binadamu

kwa njia inayoburudisha na kugusa moyo. Suala la ushairi kuwa na mguso lilishadokezwa zamani na

Mnyampala (1970) anapodai kwamba shairi laweza kumliza mtu akatokwa na machozi kwa ajili ya

mchomo wa hanjari la kuukata moyo na maini kwa ule mchomo na mguso wa maneno ya shairi la

mshairi bora. Mnyampala anaendelea kudai kwamba shairi la mshairi bora linaweza kumfanya mtu

afurahi na kujiona kuwa anayo heri mithili ya mtu aliyeko peponi. Hapa tunaona kwamba zaidi ya

kupingana juu ya ulazima wa shairi bora kuwa na vina na mizani, wanamapokeo (wanaowakilishwa

hapa na Mnyampala) na wanausasa (wanaowakilishwa hapa na Mulokozi na Kahigi) wanakubaliana juu

ya ulazima wa shairi “kuwa na mguso” kwa hadhira yake. Dhana yao ya shairi “kugusa moyo”

tulishaieleza kwa kina wakati twawahakiki wanamapokeo. Hivyo, kuendelea kujitokeza kwa suala hili

kwa wanausasa makini kama Mulokozi na Kahigi tunaweza kuhusianisha na athari za wanamapokeo

katika fasili “bora” za kisasa. Wanaposema kugusa moyo ni kufanyaje hasa? Na je jambo likimgusa

moyo mtu mmoja litamgusa moyo mtu mwingine? bila shaka jibu ni hapana. Ni wazi kwamba hata

uainishaji wa Mnyampala (1970) tulioupitia hapo awali unaonyesha kwamba upo uwezekano mkubwa

wa shairi “kutokuugusa moyo.” Hoja hii imebainishwa kinagaubaga na Macgoye (2009) kwamba yapo

mashairi ambayo hayaburudishi bali yanakasirisha na kukera moyo.

Tuseme tu kwamba mapungufu katika fasili za ushairi yanaonekana tangu katika fasili za

wanazuoni wa zamani sana hadi wa kisasa. Hivyo, tukubaliane tu na Macgoye (2009:2) kwamba

ushairi, sawa na falsafa au dini au nishati au kazi, ni vigumu sana kuufasili kwa kutoa fasili moja fupi.

Labda ni kutokana na ukweli unaobainishwa na Senkoro (1988:3) kwamba [kutokana na ugumu wa

kufasili ushairi] kuwapo kwa pande mbili zinazovutana na kukinzana si jambo geni. Ni dalili ya kukua

kwa fasihi ya jamii inayohusika, pamoja na kupanuka kwa nadharia ya fasihi hiyo (ufafanuzi wetu). Hii

ni kusema kwamba juhudi hizi za kufasili dhana tete ya ushairi ndiyo usomi wenyewe na siku tukikoma

kufanya hivyo ndiyo mwisho wa usomi.

Tuhitimishe kwamba, ili kufasili vizuri dhana ya ushairi ni vema tukichukua vipengele

vinavyojitokeza kwa wanamapokeo na wanamamboleo na kuviunganisha ili kuwa na fasili bora

ambayo labda inaweza kupunguza ukakasi uliopo japo hatusemi kwamba ukakasi huo utakwisha.

Tukichunguza fasili za wanamapokeo na wanamamboleo tunaona kwamba wanakubaliana kuwa ushairi

lazima utumie lugha ya mkato au lugha fupi, mpangilio maalumu, lugha fasaha, lugha ya picha na

ishara na vipengele vingine vya ushairi. Wanachotofautiana hasa ni katika suala la matumizi ya urari

wa mizani na vina. Wakati wanamapokeo wanashikilia kuwa vipengele hivi ni lazima na ndiyo uti wa

mgongo wa ushairi, kama inavyobainika katika Abedi (1954), wanausasa kwa upande wao wanaona

kwamba ushairi unaweza kutumia urari wa vina na mizani au unaweza usitumie na bado ukawa na sifa

ya kuwa ushairi kama inavyobainika katika Mulokozi na Kahigi (1979).

Hivyo, katika andiko hili ushairi tunauchukulia kuwa ni utungo wa kisanaa unaoweza kusimuliwa

au kuandikwa ili kuwasilisha ujumbe fulani kwa jamii kwa kutumia lugha ya picha, mkato, taswira,

ishara na lugha ambayo kimsingi si ya kinathari kama ilivyozoeleka katika tanzu nyinginezo. Ushairi

ulioandikwa kwa maksudi ya kuifurahisha hadhira huweza kuifurahisha hadhira husika na shairi

lililoandikwa kwa maksudi ya kuibua huzuni huweza kuihuzunisha hadhira. Fasili hii inazingatia

ukweli kwamba ushairi huweza kuwa simulizi na pia andishi na kwamba unaweza kutumia vipengele

hivyo au isivitumie vyote kwa pamoja. Aidha, fasili hii inaanza kwa kusisitiza maudhui na kisha fani na

si fani na kisha maudhui kama ilivyofanywa na wengi waliotutangulia. Hata hivyo, hatusemi hapa

kwamba fasili hii ni bora zaidi ya zote zilizotangulia, kila fasili ni bora katika muktadha wake. Hatuna

shaka kwamba kila fasili ni sahihi katika kipindi ambacho ilitolewa ila kwa kuwa ushairi unakua ni

wazi kwamba fasili kadhaa huweza kupitwa na wakati.

SIFA ZA JUMLA ZA USHAIRI

Baada ya kupitia fasili za wanamapokeo na wanamamboleo tunabaini kwamba ushairi una sifa

muhimu kadhaa. Miongoni mwa sifa hizo ni ruwaza katika lugha, uwekevu, ubebaji wa hisia,

huonyesha tajiriba ya maisha, hufikirisha, huweza kuwa na mvuto na huweza kutumia ukiushi wa kaida

za lugha. Sifa nyingine ni zile zinazotajwa na Mulokozi (1996:100-) kuwa ushairi huwa na uteuzi mzuri

wa maneno, huwa na mpangilio maalumu wa maneno, huweza kutumia lugha ya mkato, tamathali za

semi, ishara na mafumbo na mengineyo kadha wa kadha.

29

SURA YA PILI

DHIMA ZA USHAIRI WA KISWAHILI

Neno dhima linatumika hapa kumaanisha kazi, umuhimu au majukumu. Hivyo,

tunapozungumzia dhima za ushairi wa Kiswahili, tunamaanisha kazi, umuhimu au majukumu ya ushairi

wa Kiswahili. Ushairi wa Kiswahili una dhima za namna mbili kuu: dhima za ushairi wa Kiswahili

kwenye jamii/kijamii na dhima za ushairi wa Kiswahili kwenye fasihi/kifasihi. Dhima za ushairi wa

Kiswahili kijamii ni zile kazi mbalimbali za ushairi husika kwenye jamii ya Waswahili. Katika dhima

hii tunaangalia ushairi wa Kiswahili unafanya kazi gani kwa Waswahili? Kwa upande wa dhima za

ushairi wa Kiswahili kifasihi tunazungumzia kazi zinazofanywa na ushairi kwa Kiswahili kwenye

fasihi. Hapa tunaangalia ushairi wa Kiswahili unafanya kazi gani kwenye fasihi ya Kiswahili na labda

kwenye fasihi nyinginezo? Katika sura hii tutafafanua kwa kina dhima hizo na kutoa mifano pale

inapobidi.

I. DHIMA ZA USHAIRI WA KISWAHILI KIJAMII

Ushairi wa Kiswahili una majukumu mengi kwenye jamii ya Waswahili. Miongoni mwa dhima

hizo ni pamoja na kutunza historia ya jamii, kukuza ushujaa, ujasiri na uzalendo na kuendeleza

matabaka. Aidha, ushairi wa Kiswahili huadibisha, huadilisha na pia huhifadhi amali na utamaduni wa

jamii husika. Zaidi ya yote hayo, ushairi wa Kiswahili huburudisha. Kwa ujumla, tunaweza kusema

kwamba, ushairi wa Kiswahili unatimiza dhima kuu mbili za msingi za fasihi ambazo ni kuelimisha na

kuburudisha.

1. Ushairi wa Kiswahili na Uhifadhi wa Historia

Suala la fasihi na uhifadhi wa historia limewashughulisha wanafasihi wengi na kuibua mjadala

mkubwa miongoni mwao. Wapo wanaoona kwamba kazi ya fasihi ipo mbali sana na ukweli wa

kihistoria. Kwa maneno mengine, hawa wanaona kwamba jamii inayosawiriwa na kazi za kifasihi na

jamii halisi ni vitu viwili tofauti kabisa. Dai hili linamaanisha kwamba kazi ya fasihi haibebi historia

halisi ya jamii husika. Wanaounga mkono dai hili wanaongozwa na Lord Raglan na G. Innes kama

inavyoonekana katika Raglan (1956:105-106) na Innes (1974:26). Wengine katika mkondo huu ni

pamoja na Jan Vansina na J.W. Johnson ambao wanaona kwamba historia inayosawiriwa katika kazi za

kifasihi si halisi bali ni historia yenye ukweli pendelevu (history with subjective truth) inayokusudiwa

kutimiza malengo ya jamii husika (Vansina, 1965:102, 160 na Johnson, 1978:193).

Hata hivyo, inakubalika miongoni mwa wanahistoria kwamba ni vigumu kuwa na historia yenye

ukweli thabiti (objective history) kwani kila mwandishi wa historia huweza kuathiriwa na itikadi au

mtazamo fulani anaoupendelea. Kutokana na hilo, wanahistoria wanazigawa kazi zinazohusu historia

katika makundi mbalimbali kulingana na itikadi au mtazamo kazi husika inaouelemea/iliyo athirika

nao. Makundi hayo huitwa mikabala ya uelezaji wa historia ya jamii (historiographies). Kwa mfano,

kuhusu historia ya Afrika kuna makundi mengi ya mikabala ya uelezaji wa historia yaliyobainika.

Miongoni mwa makundi hayo ni mkabala wa Kizungu wa kuieleza historia ya Afrika (Eurocentric

historiography), mkabala wa Kiafrika wa uelezaji wa historia ya Afrika (Africanist/nationalist

historiography), mkabala wa Kimaksi wa uelezaji wa historia ya Afrika (Marxist historiography) na

kadhalika. Mkabala wa Kizungu wa kuieleza historia ya Afrika huitwa pia mkabala wa kikoloni wa

kuelezea historia ya Afrika (Colonialist historiography). Huu ni mkabala unaoielezea historia ya Afrika

kwa kuzingatia mawazo ya Kizungu au ya kikoloni. Wakoloni wa Kizungu walidai kuwa walikuja

Afrika kuzistaarabisha jamii mbalimbali za Kiafrika. Wanafafanua kwamba, Afrika kabla ya ujio wa

Wazungu/wakoloni, ilikuwa haijastaarabika. Hivyo, wanadai kuwa ukoloni ulikuja Afrika ili

kuistaraabisha Afrika. Kutokana na mtazamo huo, vitu vingi vilivyoandikwa na wanahistoria

wanaoelemea mtazamo huu wa Kizungu “viliubeba” na kuusifia ukoloni kuwa ni kitu kilichokuwa na

faida kwa Waafrika. Udhaifu wa mkabala huu ni kuwa unakuza sana nafasi ya Wazungu katika

maendeleo ya Afrika. Aidha, unadogosha na kudunisha sana jamii za Kiafrika tofauti na hali halisi

ilivyokuwa. Pia unaficha ukweli halisi wa sababu za ukoloni Afrika.

Kwa upande wa mkabala wa Kiafrika wa uelezaji wa historia ya Afrika (nationalist

historiography), huu unaelezwa kuibuka ili kuupinga mkabala wa Kizungu/kikoloni. Kinyume na

mkabala wa Kizungu, huu “unawabeba” na kuwasifia Waafrika. Mkabala huu unawaona Waafrika

30

kabla ya ujio wa wakoloni kuwa walikuwa wamestaaribika na kupiga hatua kubwa katika maendeleo.

Aidha, mkabala huu unaulaumu ukoloni kuwa ndiyo chanzo cha umaskini wa Afrika kwani kabla ya

hapo, kiwango cha maendeleo kilichofikiwa na Waafrika kilikuwa kinafanana na kile kilichofikiwa na

Wazungu. Udhaifu mkuu wa mkabala huu ni kuwa unawakuza mno Waafrika na kupinga mchango

wowote wa Wazungu katika maendeleo ya Afrika. Hivyo, mkabala huu, kama ulivyo uliotangulia,

hauelezi ukweli usiokuwa pendelevu.

Mkabala wa tatu ni ule wa Kimaksi wa uelezaji wa historia ya Afrika (Marxist historiography).

Mkabala huu wa uelezaji wa historia ya Afrika unaelemea mawazo ya mwanahistoria aitwaye Karl

Marx. Mawazo ya Karl Marx yameunda kile kinachoitwa mtazamo wa Kimaksi au Umaksi ambao,

mbali na kubainika katika historia, unabainika pia katika nyanja mbalimbali. Kwa kuwa mtazamo huu

unabainika pia katika mawazo ya Fredrick Engles na wengineo waliofuata baadaye, mtazamo wa

Kimaksi huhusu falsafa ya kisiasa na kiuchumi inayohusishwa na Karl Marx (1818-1883) na Fredrick

Engles (1820-1895), pamoja na wafuasi wao. Mkabala huu unachukulia kuwa historia ya jamii imejaa

migogoro na mivutano kati ya matabaka mbalimbali. Mfano mzuri wa migogoro hiyo ni migogoro

baina ya watawala na wataliwa, wafanyakazi na waajiri, na kadhalika. Hivyo, kwa mujibu wa mkabala

wa Kimaksi, historia ya binadamu huwa ni mapambano au harakati za kitabaka. Tabaka ambalo

hudhibiti njia kuu za uzalishaji mali huitawala na kuidhibiti jamii lakini tabaka la wasio nacho

hupambana kuleta mapinduzi. Kwa mujibu wa Wamitila (2003) katika kitabu chake cha Kamusi ya

Fasihi Istilahi na Nadharia, dhana ya Umaksi (pia Umarx) inafafanuliwa kama ifuatavyo:

Umarx ni falsafa ya kipembuzi ambayo inasisitiza jinsi mazingira ya kuishi

yanavyochukua nafasi ya kimsingi yakilinganishwa na mawazo au imani katika maisha

ya binadamu. Umarx unaelekea kuwa na sifa ya umoja (Monism) na inahusu kila kitu

kuanzia uchumi, siasa, historia, jamii na mapinduzi.

Hivyo, tuseme mkabala wa kimaksi katika historia, huelezea historia ya jamii za Kiafrika ukiongozwa

na imani kuwa uchumi (uzalishaji mali) huathiri maisha ya mwanadamu na mtazamo wake kwa ujumla.

Kwa hiyo, historia inayoelezwa na wanaoelemea mkabala huu ni ile ihusuyo njia za uzalishaji mali

pamoja na miundo ya kiuchumi inayoathiri uzalishaji mali na ugawanyaji wa faida (nani anapata nini).

Aidha, historia inayoelezwa inaakisi harakati zinazoendelea baina ya matabaka ya kiuchumi-jamii.

Mabadiliko ya kihistoria yanaelezwa katika msingi wa uzalishaji mali unavyoathiri mabadiliko ya

muundo wa matabaka ya jamii na hivyo kutokeza tabaka tawala na tawaliwa ambayo huwamo katika

mapambano na harakati za kugombea uchumi, siasa na faida za kijamii.

Kutokana na kuwapo kwa mikabala mbalimbali ya kueleza jambo moja tunabaini kuwa ni

vigumu kuwa na historia ambayo haina ukweli pendelevu. Hivyo, tunaweza kudai kwa uhakika kuwa

mawazo ya Raglan (1956:105-106), Innes (1974:26), Vansina (1965:102, 160) na Johnson (1978:193)

kuwa historia inayosawiriwa katika kazi za kifasihi si halisi bali ni historia yenye ukweli pendelevu

(history with subjective truth) inayokusudiwa kutimiza malengo ya jamii husika ni madai ya ukweli

lakini si madai yenye nguvu sana. Hii inatokana na ukweli kuwa historia yoyote ile ni vigumu kuwa na

ukweli usio pendelevu. Aidha, mara nyingi kila jambo, hata mambo ya kawaida yasiyohusiana na

historia, huelezwa kwa mtazamo, imani na falsafa ya mwelezaji. Kwa mfano, inapotokea ajali ya gari

na kukawa na watu watatu, dreva, askari na fundi magari ambao walishuhudia ajali hiyo, kila mmoja

ataielezea ajali hiyo kulingana na mtazamo, imani na falsafa yake. Ni wazi kuwa kila mmoja ataielezea

ajali hiyo kwa kuzingatia taaluma yake. Dreva, kwa mfano, ataeleza jambo linalohusiana na udreva

analohisi kuwa lilisababisha ajali hiyo, polisi ataielezea ajali hiyo kwa mkabala wa kisheria zaidi wakati

ambapo fundi magari atazingatia matatizo ya kiufundi anayoamini ndiyo chanzo cha ajali hiyo. Itakuwa

vigumu kupata maelezo yasiyo na ukweli pendelevu.

Mbali na wataalamu hawa wanaopinga uwezo wa fasihi kusawiri historia, wapo pia wanaoamini

kuwa kazi za kifasihi zinaweza kusawiri historia halisi ya jamii husika. Hawa ni pamoja na Mugyabuso

Mulokozi kama inavyoonekana katika Mulokozi (1986 na 2002) na Samwel (2012a) miongoni mwa

wengi wengineo. Hata hivyo, mawazo haya yalianzishwa na Mwanahistoria Merrick Posnansky

ambaye alieleza kwamba kazi za fasihi zinaweza kuwa chanzo muhimu cha historia ya jamii husika

(Posnansky, 1966 na 1969). Mulokozi (2002:96) anatumia tendi za nanga kushadidia mkondo huu wa

mawazo kwa kusema kwamba:

31

For us, however, the legendary does not negate the historical. On the contrary, in enanga

epic, the two supplement each other and combine with a third element – fiction or artistic

imagination, to create epic…Many enanga epics are historical in the sense that their

heroes are usually based on historical verified prototypes and their episodes revolve

around known historical events…

Kwetu sisi, hata hivyo, usakale haupingani na historia halisi. Katika tendi za nanga ni

kinyume chake, mambo hayo mawili hukamilishana na kuungana na jambo la tatu –

ubunilizi au uumbaji wa kisanii, ili kuunda utendi…tendi nyingi za nanga ni za kihistoria

kwa maana kwamba mashujaa wake kwa kawaida ni wa kihistoria na matukio

yanayowazunguka yalitokea kweli katika historia... (Tafsiri yetu).

Aidha, Mulokozi anatumia tendi za nanga kuonyesha jinsi wahusika wa tendi hizo kama vile

Ruyobya, Mutesa, Kitekere3 na wengineo na matendo yao yanavyoonyesha ukweli wa kihistoria

(2002:98 -102). Jedwali alilolitumia kulinganisha wahusika wa tendi za nanga na uhalisia wao

linathibitisha jinsi fasihi inavyoweza kubeba historia halisi ya jamii husika. Hivyo anahitimisha

kwamba:

A comparison of dramatic personae in Table 12 reveals that there is a complete

agreement between the epic and the historical record on the names and the roles of the

principal personage.

Ulinganisho wa wahusika wa kifasihi katika Jedwali namba 12 unabainisha kwamba

kuna mlingano mkubwa baina ya tendi na kumbukumbu za kihistoria katika majina na

majukumu ya wahusika wakuu (Tafsiri yetu).

Naye Samwel (2012a) anatumia majigambo kushadidia mawazo ya Mulokozi na wengineo

kuwa kazi ya fasihi inaweza kusawiri ukweli wa kihistoria. Samwel (khj.) anaungana na Mulokozi

(2002) kudai kwamba kazi za fasihi, majigambo yakiwamo, hubeba historia ya mtu mmoja mmoja na

jamii kwa ujumla. Samwel katika (2012a:131-152) anatoa mifano ya majigambo mbalimbali ya jamii

za Wahaya na Wasukuma yanavyosawiri ukweli wa historia ya wajigambi wenyewe na jamii zao.

Anabainisha kuwa majigambo hayo yanaeleza mambo mbalimbali ya kihistoria ikiwa ni pamoja na

ukoo wa wajigambi, matukio ya kihistoria yaliyotokea katika jamii kama vile vita, matatizo ya kisiasa,

kiuchumi na masuala mbalimbali ya kiutamaduni. Anatoa mfano wa jigambo linaloelezea kilimo

kinachozingatia viwango vya Nyerere. Samwel anadai kuwa jigambo hilo ni halisi na linataja wahusika

kama Nyerere ambao ni halisi. Anaendelea kufafanua kuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

alikuwa Rais wa Tanganyika na hatimaye Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alihimiza sana

kilimo chenye tija na si kilimo mradi kilimo. Anahitimisha kuwa jigambo hilo pia linaakisi sera za

ujamaa za miaka ya sitini na sabini zilizohimiza kilimo na kupinga ubepari (mirija) ambayo ilipata

kuwapo katika historia ya jamii husika.

Hivyo, tuhitimishe mjadala huu kwa kueleza kuwa ushairi wa Kiswahili, kama zilivyo tanzu

nyingine za fasihi kama vile tendi na majigambo zinazoelezwa na Mulokozi (2002) na Samwel (2012a),

husawiri historia ya jamii husika. Tunaona, kwa mfano, kuna mashairi mengi yanayosawiri historia ya

jamii mbalimbali za Waswahili. Miongoni mwa mashairi hayo ni pamoja na Utenzi wa Uhuru wa

Tanganyika (1967) ulioandikwa na Mwinyihatibu Mohamed Amiri; Utenzi wa Jamhuri ya Tanganyika

(1967) ulioandikwa na Ramadhani Mwaruka; Utenzi wa Uhuru wa Kenya (1972) ulioandikwa na Salim

A. Kibao na Utenzi wa Jamhuri ya Zanzibar. Tenzi hizi zinasawiri matukio ya kihistoria yanayohusiana

na uhuru wa Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Mashairi mengine ni Mashairi ya Azimio la Arusha

(1971) yaliyohaririwa na Grant Kamenju na Farouk Topan na Ngonjera za UKUTA za Mnyampala

1970 ambayo yanasawiri siasa ya Ujamaa na Kujitegemea pamoja na Azimio la Arusha, matukio

ambayo ni ya kihistoria nchini Tanzania. Vilevile kuna Utenzi wa Vita vya Kagera na Anguko la Idd

Amini Dada (1981) ulioandikwa na Henry Muhanika ambao unazungumzia vita baina ya Tanzania na

Uganda iliyotokea kati ya mwaka 1978 na 1979.

3 Ruyobya ni shujaa mpinzani ambaye alikuwa mwana mfalme wa Kiziba. Mutesa alikuwa Kabaka wa Buganda na

Kitekere alikuwa mfalme wa Kyamutwala. Wahusika hawa watatu wanasawiriwa katika Utendi wa Mugangala na pia ni

wahusika ambao waliishi kweli na walikuwa na sifa hizohizo zinazosawiriwa katika utendi husika.

32

2. Ushairi wa Kiswahili na Kukuza Ushujaa, Ujasiri na Uzalendo

Zaidi ya kutunza historia ya jamii husika, ushairi wa Kiswahili pia hukuza ushujaa, ujasiri na

uzalendo miongoni mwa wanajamii. Kwa mfano, mashairi yanayoelezea harakati za kudai uhuru na

jinsi watu walivyojitoa muhanga, kama tulivyoona hapo awali, yanaweza kuwafanya wanajamii kuwa

wazalendo na kuenzi jitihada zilizofanywa na wazee wao katika kuleta uhuru na ukombozi miongoni

mwa jamii za Waswahili. Mashairi na nyimbo pia hutumiwa katika vita, kama inavyobainika katika

nyimbo za wanajeshi (nyimbo za vita) (taz. Samwel, 2012a), na hivyo kukuza ushujaa, ujasiri na

uzalendo. Aidha, yapo pia mashairi yaliyotungwa ambayo yanahimiza ushujaa, ujasiri na uzalendo.

Mfano mzuri wa mashairi ya aina hii ni shairi liitwalo “Upole Wachusha” katika Diwani ya Akilimali.

Katika shairi hilo Akilimali anawaonya wanajamii kutokaa kimya pale wanapoonewa na

kukandamizwa. Anawahimiza wanajamii kuwa mashujaa na majasiri na kupinga vitendo hivyo.

Anasema:

Ulimwengu huu wa leo, wataka kuchangamka

Sikaliye ndio ndio, radae utaumbuka

Si kazi pigwa kibao, ukaselea wacheka

Upole na kimya sana, ulimwengu wachusha

Kimya sana kikizidi, kila jambo kuitikia

Si kazi fanywa kuadi, na vitanda kutandika

Lisilopasa kaidi, ndivyo dunia yataka

Upole na kimya sana, ulimwengu wachusha

3. Ushairi wa Kiswahili na Kuendeleza Matabaka

Uhusiano baina ya fasihi na utawala au matabaka ni jambo lililojadiliwa kwa kina na wataalamu

mbalimbali. Mulokozi (2002), kwa mfano, zaidi ya mambo mengine, anajadili uhusiano uliopo baina ya

tendi za nanga na utawala. Anaeleza kwamba ushairi wa kishujaa, ukiwamo nanga na majigambo,

ulitumika katika jamii za jadi ili kuendeleza tabaka tawala na maslahi yao. Mulokozi (2002:17)

anasema:

These relations of domination and dependence were highly maintained and reproduced

through a superstructure that included a powerful, highly centralized state and

bureaucracy, as well as an ideological apparatus that included royal oriented religious

cults, mythology, heroic poetry, such as enanga epics and praise poetry, and a value

system that upheld the ‘virtues’ of heroism and ‘high birth’, and stressed the superiority

and sanctity of the ruling personages.

Mahusiano haya ya kiutawala na kitegemezi kwa kiasi kikubwa yaliendelezwa na

muundo wa kijamii uliojumuisha matumizi ya nguvu, dola imara na serikali, pamoja na

mbinu za kiitikadi zilizojumuisha mfumo wa dini, imani, ushairi wa kishujaa, kama vile

tendi za nanga na majigambo, na mfumo wa desturi ulioendeleza masuala ya ushujaa na

‘nasaba bora’, na kuhimiza ukuu na utukufu wa tabaka tawala (Tafsiri yetu).

Mtazamo kama huu umebainishwa pia na Vail na White (1984) walipokuwa wanaushughulikia

ushairi wa kusifu (sifo) wa jamii za Wandebele na Hodza na Fortune (1979) walipokuwa

wanashughulikia ushairi kama huo wa jamii za Washona. Hivyo, tunaweza kusema kwa uhakika

kwamba ushairi wa Kiswahili, kama ulivyo ushairi wa jamii nyingine, ni fasihi inayokuza na

kuendeleza tabaka tawala. Aidha, mtazamo huu unabainika pia katika Samwel (2012a)

anapozungumzia ushairi wa majigambo katika jamii mbalimbali za Kitanzania. Samwel (khj.) anadai

kuwa ushairi wa majigambo, zaidi ya dhima nyingine, ulikuwa na dhima hii. Anatoa mfano kuwa,

katika mengi kati ya mashairi ya majigambo ya jadi mjigambi alijikabidhi kwa mtemi, mkuu wa ukoo

au mtu yeyote wa tabaka tawala ambaye majigambo husika yalitendwa mbele yake. Anaendelea

kufafanua kuwa ushairi wa majigambo ulitendwa ili kuonyesha utii kwa tabaka tawala na utayari wa

kulitumikia tabaka hilo. Anahitimisha kuwa wajigambi wa jadi waliona fahari kujinasibisha na tabaka

tawala. Samwel (khj.) anatoa mfano wa ushairi wa majigambo unaokuza na kuendeleza matabaka kwa

kubainisha kuwa wajigambi, katika majigambo ya jadi, wanaanza kwa kutoa heshima kwa mfalme.

Anafafanua kuwa kwa kuanza hivyo, wajigambi walikusudia kusema kwamba “ingawa nitajigamba na

kueleza matendo makuu niliyoyafanya, sistahili heshima bali heshima ni ya mfalme wangu.”

Anabainisha heshima inayotolewa katika moja ya majigambo ambapo mjigambi anasema:

33

Mheshimiwa mtukufu

Akusemaye vibaya hulalia juu ya mwamba

Hujifunika ungo

Nakufananisha na Abahindakazi.

Samwel anaendelea kulifafanua jigambo hilo kuwa hata katika mistari inayofuata mjigambi bado

anaendelea kueleza kwamba ingawa yeye ameelezea matendo makuu aliyoyafanya, hastahili heshima

bali heshima apewe mfalme. Mwisho kabisa mjigambi anamkabidhi mfalme vifaa alivyovitumia

kuwinda, yaani mikuki. Mfalme anaonekana ndiye anayestahili kuvimiliki. Samwel anaendelea

kufafanua kuwa katika majigambo ya aina hii mjigambi hukabidhi pia na mawindo yake kwa mfalme,

na mfalme ndiye aliyemgawia mjigambi kiasi anachostahili kadri mfalme alivyoona inafaa. Aidha,

katika majigambo ya vita, mjigambi hukabidhi silaha za vita na mateka halafu ndipo mfalme

angemzawadia mjigambi sehemu ya ngawira aliyoona inafaa.

Hivyo, kama inavyobainika katika fasihi za jamii nyinginezo na pia katika tanzu nyingine za

fasihi, ushairi wa Kiswahili pia unakuza na kuendelea matabaka. Mashairi na tenzi mbalimbali

tulizozifafanua awali kama vile Utenzi wa Uhuru wa Tanganyika (1967), Utenzi wa Jamhuri ya

Tanganyika (1967), Utenzi wa Uhuru wa Kenya (1972), Utenzi wa Jamhuri ya Zanzibar, Utenzi wa

Vita vya Kagera na Anguko la Idd Amini Dada (1981), Mashairi ya Azimio la Arusha (1971) na

Ngonjera za UKUTA (1970), zaidi ya mambo mengine, yanasifia tabaka tawala na sera zao. Kwa

kufanya hivyo, mashairi na tenzi hizo zinakuza na kuendelea tabaka tawala.

4. Ushairi wa Kiswahili na Kuhifadhi na Kuendeleza Utamaduni

Ushairi wa Kiswahili unahifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii husika. Fasihi ni kioo cha

jamii na hivyo ni sehemu ya utamaduni wa jamii husika. Kwa hiyo, ushairi wa Kiswahili, kama kazi ya

fasihi, hubeba utamaduni wa jamii husika. Ushairi wa Kiswahili unahusu masuala mbalimbali ya

kitamaduni yanaihusu jamii ya Waswahili. Masuala hayo ni kama vile mila na desturi za ndoa, jando,

unyago, na mahusiano ya wanajamii, lugha ya Kiswahili na kadhalika. Mfano mzuri wa hili tunauona

katika shairi la “Utamaduni Kitu Gani” na “Kiingereza Lugha Nzuri?” katika Ngonjera za Ukuta

ambapo mshairi anafafanua dhana ya utamaduni na dhima ya utamaduni wa Kiafrika. Aidha,

anafafanua pia dhima ya lugha ya Kiswahili na kuwaelimisha watu kuwa Kiingereza si lugha nzuri

kuliko Kiswahili kama inavyobainika katika shairi la “Kiingereza Lugha Nzuri?” kama ifuatavyo:

Lo! Hata haya huoni, lugha ngeni kuipenda?

Lugha yao wakoloni, walojiita Kamanda

Tukawekwa utumwani, tukafanywa sisi punda…

Lugha nzuri Kiswahili, tuchezeacho kandanda

Lugha yetu ya asili, ya kunena na kutenda

Ya asili na fasihi, ya taifa twaipenda…

Kiswahili na Kigogo, na lugha nyingi zatanda

Kinyamwezi na kidogo, Kibantu hakina nyonda…

Lugha nzuri Kizaramo, hupendeza kwa Mganda

Huvuta muungurumo, Dogori hupiga panda

Ni wa Kibantu msemo, wananchi waipenda

Lugha nzuri ya kupenda, ni hii ya Kiswahili

Akizungumzia kuuenzi na kuuthamini utamaduni wa Kiafrika, Mnyampala katika shairi la “Utamaduni

Kitu Gani” kama linavyobainika katika Ngonjera za Ukuta. Anasema:

…tamaduni kutukuza, ni mila za kila fani…

Na ufinyanzi wa vyungu, nazo ngoma zetu nchini

Na nyimbo zetu za tangu, na sauti zetu ngomani

Mbali mila za Kizungu, ziwe kwao Uzunguni…

Kazi zetu za asili, silizofanywa zamani

Za mikono na fasili, sidharau tukuzeni…

Za asili zetu kunga. Za unyago na jandoni…

Ndoa zetu za kimila, na shangwe zake nyumbani…

Uchongaji wa sanaa, mapambo yetu nchini

Hadithi zetu zajaa, kuitwa ni utamaduni…

34

5. Ushairi wa Kiswahili na Kuadilisha na Kuadibisha

Kuadilisha ni kumpa mtu maadili wakati ambapo kuadibisha ni kumtia mtu adabu. Ushairi wa

Kiswahili, zaidi ya dhima nyingine, una dhima ya kutoa maadili pamoja na kuadibisha jamii. Tukianza

na kuadibisha tunaona kwamba kupitia ushairi wa Kiswahili, wanajamii hufanywa kuwa na adabu kwa

wakubwa wao, miungu yao, viongozi wao na kadhalika. Katika ushairi wa majigambo, na hasa

majigambo ya ukoo na ya miji na vijiji, kwa mfano, tunaona kwamba wanajamii hufunzwa kuyahusisha

mafanikio yao na vizazi vya ukoo. Samwel (2012a) anabainisha kuwa katika ushairi huo wa majigambo

mjigambi hutaja vizazi vyake vya kuumeni na kukeni na kuyahusisha na mafanikio aliyoyapata.

Wajigambi huona kwamba mafanikio waliyonayo na sifa za kishujaa walizonazo zinatokana na nasaba,

miji na vijiji vyao. Kwa namna hii, wajigambi hujengewa adabu na heshima kwa nasaba, miji na vijiji

vyao. Hivyo, wanajamii huamini kama si ukoo wao pamoja na miji na vijiji walivyotokea, wasingepata

mafanikio waliyonayo yanayowapa haki ya kujigamba. Maelezo haya yanathibitisha sifa za shujaa wa

Kiafrika zilizopendekezwa na Mulokozi (1999 na 2002) kwamba ili mtu awe shujaa katika jamii, zaidi

ya mambo mengine, anapaswa kupata uungwaji mkono kutoka kwa wanajamii wa jamii husika.

Wanajamii hao hupaswa kumsaidia na kumjenga, kinyume chake shujaa huyo ataanguka. Aidha,

mashujaa katika tendi za nanga, kama anavyofafanua Mulokozi, walianguka kutokana na kukosa

uungwaji mkono kutoka kwa wanajamii wa jamii zao. Turejelee Mulokozi (2002: 85-93) anaposema:

This in effect means that the hero needs and must enjoy the support and protection of his

group, which alone knows the source of his occult power, if he is to survive as a fighter.

Group support at the level of kinship and beyond, is obsolutely essential; it is the third

and final heroic trait of the enanga hero.

Hii ilimaanisha kwamba shujaa anahitaji na lazima apate uungwaji mkono na ulinzi

kutoka kwa watu wake, ambao pekee ndio hujua asili ya nguvu zake za ajabu, kama

anahitaji kuendelea kuishi na kushinda. Uungwaji mkono katika ngazi ya wanaukoo na

jamii kwa ujumla ni muhimu sana; ni sifa ya tatu na ya mwisho ya shujaa wa tendi za

nanga (Tafsiri yetu).

Kutokana na hilo, wanajamii walijengewa heshima na adabu kwa wanaukoo, na hasa mababu, na

wanajamii wengine kwa ujumla.

Aidha, yapo pia mashairi mbalimbali yanayowaadilisha watu juu ya mambo mbalimbali. Vile

vile yapo mashairi mengi yanayowaasa watu kuwa na adabu. Mashairi hayo, kwa mfano, huweza

kuwahimiza wanajamii kuwaheshimu wakubwa wao, wake kuwaheshimu waume zao, kuadilishwa juu

ya masuala mbalimbali ya kijamii na kadhalika. Tunaona mfano wa hili katika Diwani ya Akilimali

ambapo kuna mashairi kama vile “Asofunzwa na Wazazi,” “Aringae na Dunia,” “Akiba si Mbaya,”

“Jirani Yako ni Ndugu,” “Kila Mpenda Rushwa,” “Unapokosa Shukuru” na mengine mengi ambayo

huadilisha na kuadibisha. Katika shairi la “Asofunzwa na Wazazi” mshairi anawaonya wanajamii

kuwatii wazazi wao kwani kama hawatawatii na kuwasilikiza basi dunia itawafunza. Aidha, katika

shairi la “Aringae na Dunia” mshairi anawaonya wanajamii kutodharau wengine; katika shairi la

“Akiba si Mbaya” mshairi anahimiza wanajamii kuweka akiba; katika shairi la “Jirani Yako ni Ndugu”

msanii anahimiza wanajamii kupendana na kujaliana na katika shairi la “Kila Mpenda Rushwa” msanii

anaiasa jamii kuichukia rushwa. Tuchunguze ubeti wa kwanza na wa pili wa shairi la “Unapokosa

Shukuru” katika Diwani ya Akilimali kuona jinsi ushairi wa Kiswahili unavyoadilisha jamii kuthamini

kazi na pia kushukuru kwa kile kidogo walichonacho:

Kazi iwayo si mabaya, mabwana tieni nguvu

Kazi yoyote ni niya, bali usiwe mvivu

Mapesa huwa hidaya, hayataki uwerevu

Unapokosa shukuru, kupata kuna Rabuka

Shukuru unachopata, japo ukipata mbovu

Mungu mwenyewe taleta, nzima pasipo nguvu,

Bure pesa hutapata, pasipo uelekevu

Unapokosa shukuru, kupata kuna Rabuka

Mashairi ya kuadilisha na kuadibisha yanaonekana pia katika Malenga wa Mrima cha

Mwinyihatibu Mohamed. Mashairi hayo ni pamoja na “Maovu,” “Ushoga,” “Mmbeya” na mengineyo.

35

Katika shairi la maovu mshairi anawaadilisha wajamii kutambua maovu yao na kuyatubia kabla

hayajawaletea madhara; shairi la “Ushoga” mshairi anaiadilisha jamii kuepukana na tabia ya urafiki wa

kinafiki na katika shairi la “Mmbeya” mshair anaiadilisha jamii kuepukana na tabia ya umbea.

Kwa upande wa Diwani ya Amri tunaona kuna mashairi mengi ambayo yanawaadilisha watu

kuwa wacha Mungu na kuwaadibisha watu kumtii Mungu na wakubwa wao. Mashairi ya kuadilisha na

kuadibisha katika diwani hiyo ni kama vile “Wamchao Rahmani Ndio Wenye Mwisho Mwema,”

“Kheri Nirudi kwa Mola,” “Baba Shika Ushikapo, Muamuzi ni Jalali,” “Mali,” “Maovu Sigeukie” na

“Ahadi ni Deni.” Mashairi ya “Wamchao Rahmani Ndio Wenye Mwisho Mwema” na “Kheri Nirudi

kwa Mola” yanawaadilisha wanajamii kuwa wacha Mungu. Aidha, mashairi hayo yanawaadibisha

wanajamii kumuheshimu Mungu. Pia yanawahimiza wanajamii kuacha maovu na kumrudia Mungu ili

waweze kuishi maisha mazuri duniani na akhera. Shairi la “Baba Shika Ushikapo, Muamuzi ni Jalali”

linawaadibisha wanajamii kuwaheshimu wazazi wao. Mbali na hilo shairi hilo pia linawaadilisha watu

(hasa wazazi) kuheshimu dini za wengine maana mwenye uwezo wa kuhukumu ni Mungu na si

mwanadamu. Vilevile shairi hilo linawaadilisha wazazi kuwapa watoto wao uhuru wa kufanya

maamuzi bila kuingiliwa. Shairi la “Mali” linaiadilisha jamii kufanya kazi kwa bidii ili kupata mali.

Hata hivyo, shairi hilo linawaonya wanajamii kutojali mali kuliko utu. Hivyo, shairi hilo linawataka

wanajamii kuridhika na mali waliyonayo hata kama ni kidogo na kuwataka wasijiingize kwenye

vitendo visivyofaa vya kutafuta mali. Nalo shairi la “Maovu Sigeukie” linawaadilisha wanajamii

kutendeana wema wao kwa wao na kuepukana na maovu. Kwa upande wa shairi la “Ahadi ni Deni”

mshairi anawaasa wanajamii kuheshimu ahadi walizoziweka na kuzitimiza. Turejelee shairi la “Mali”

ili kuona jinsi linavyoadilisha:

Kupenda mno ukwasi, naona nitapotea

Mali ina wasiwasi, sikai nikatulia

Mali huzua maasi, mtu yakampotoa

Mali ni njema hidaya, hili kweli nalijua

Sura yangu iwe mbaya, watu wataisifia

Lakini naona haya, sifa hii kupokea

Mali ni nzuri hidaya, tena ninakariria

Lakini ina hekaya, ngumu kuizingatia

Hususa huwa kayaya, dunia kuizamia

6. Ushairi wa Kiswahili na Kuburudisha

Zaidi ya dhima za kuelimisha, kama vile kuadilisha, kuadibisha, kutunza historia na kadhalika,

ushairi wa Kiswahili, kama kazi zingine za kifasihi, huburudisha. Ushairi wa Kiswahili, na hasa nyimbo

za kazi, huweza kuimbwa wakati wa kazi ngumu na kumburudisha mwimbaji na msikilizaji pia.

Ikumbukwe kuwa nyimbo za kazi ndiyo ushairi wa awali kabisa wa Kiswahili. Ushairi huu ulipunguza

uchovu wa watu hasa katika kazi kama vile kilimo, vita, ufugaji, uwindaji na kadhalika. Vilevile yapo

mashairi andishi ambayo yanaposomwa huweza kumburudisha msomaji. Hii ni kusema kuwa baada ya

kazi nzito za kutafuta kipato watu huweza kusoma mashairi na kuburudika na hata kuwasahaulisha

madhila yao.

II. DHIMA ZA USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA FASIHI

Mbali na dhima za ushairi wa Kiswahili katika jamii, ushairi wa Kiswahili pia una dhima kubwa

katika fasihi, simulizi na andishi. Ushairi wa Kiswahili umetumiwa sana katika tanzu mbalimbali za

fasihi, andishi na simulizi kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano, ushairi wa Kiswahili, na hasa nyimbo,

zimetumiwa sana kwenye riwaya, tamthilia, novela na hata hadithi fupi. Zaidi ya mambo mengine,

matumizi hayo yana dhima kama vile kutambulisha wahusika wa kazi za fasihi, kujenga tamathali za

semi, ishara, taswira, kuweka urari wa vina na mizani na kuonyesha ushiriki wa hadhira katika kazi ya

fasihi. Aidha, dhima nyingine za ushairi wa Kiswahili katika fasihi ni pamoja na kodokeza na kuibua

maudhui na kukuza tanzu za fasihi ya Kiswahili. Katika sehemu hii tutawasilisha maelezo na

uchambuzi wa dhima hizi za majigambo ya jadi katika fasihi.

36

1. Ushairi wa Kiswahili na Kutambulisha na Kuwajenga Wahusika

Kwa kuanza na kutambulisha na kuwajenga wahusika tunaona kwamba ushairi wa Kiswahili

husaidia kujua kazi husika ya fasihi inatumia wahusika wa aina gani na wenye uwezo gani. Dhima hii

huonekana hasa pale ushairi wa Kiswahili unapotumika katika utanzu mwingine. Mulokozi (2002:354)

akielezea hili anabainisha kwamba, ushairi wa majigambo unapotumika katika tendi za nanga,

hutambulisha sifa mbalimbali za shujaa anayesimuliwa, maisha yake, matendo yake, chakula chake,

mavazi yake na kadhalika. Kwa mfano, katika Utendi wa Rukiza tunaona kwa kutumia ushairi wa

majigambo, shujaa anaeleza chakula anachokula, anavyopaswa kuitwa na hata alivyo tayari kufa.

Tuchunguze mstari wa 480-83 anaeleza alivyo tayari kufa.

480. Ndetela n’amata nganywe

481. Nakushohola Ebinyambo bindasha bimbona

obwamba!

482. Ai “Ndetela amajuta nyesiige

483. Nakushohola Ebinyambo bindasha bimbona

obwelu!”

480. Niletee maziwa ninywe

481. Nikitoka Minyambo isinifume mshale na kuona

damu yangu

482. Niletee na mafuta nijipake

483. Nikitoka Minyambo isinifume mshale na kukuta

nimepauka

Chanzo: Mulokozi (2002:354)

Vilevile katika mstari wa 16-18 katika utenzi huohuo wa Rukiza, tunaona kwa kutumia ushairi

wa majigambo, sifa ya shujaa ya kutokula ovyo inabainishwa. Shujaa wa tendi za nanga kama

anavyoeleza Mulokozi (2002:87) hali chochote bali hula chakula maalumu. Sifa hii inasawiriwa katika

utendi kwa njia ya majigambo. Hebu tuangalie, kwa mfano, manju anaposema:

16. Kulya ebyo ntalya nkeita!

17. Kulya omugobe n’eshwiga

18. Ningila eby’abazana bakahomboza!

19. Ai “Mawe Kachenkela”

16. Waama ninahamanika

17. Heri nijiue kuliko kula haramu

18. Kula mboga za majani ya kunde na mnavu (shwiga)

19. Kula takataka zisanywazo na wajakazi!

Chanzo: Mulokozi (2002:322)

Pia Mulokozi (khj.) anabainisha kuwa kwa kutumia ushairi wa majigambo, sifa ya shujaa ya kutoitwa

isivyopaswa inabainishwa. Shujaa anapaswa kuitwa kwa jina la majigambo la Mwinyi/Mheshimiwa

kama inavyobainika katika mistari ya 455-63 hapa chini:

455. Yaija nailuka Kinyampororo

456. Yayema aha nyumanju yamweta

457. Ati “Iwe Rukiza, Rukiza, Rukiza, Rukiza,

Rukiza, iwe kyamawe!

458. Rukiza, Rukiza, Rukiza!

459. [Aho abiita byabanza]

460. Rukiza, Rukiza, Rukiza, Rukiza, Rukiza,

Rukiza, iwe kyamawe!

461. Ai “Katule kalame!

462. Alikunyeta Rukiza nohai?”

463. Ai “Manti inye nkalagwa nyetwa ‘Waitu’?”

464. Ai “Niinye Kinyampororo

455. Kinyampororo akaja anakimbia

456. Akamwita Rukiza kutokea nyuma ya nyumba

457. “Ewe Rukiza, Rukiza, Rukiza, Rukiza, Rukiza, mtoto

wa mama

458. Rukiza, Rukiza, Rukiza!

459. [Hapo vita vimeanza]

460. Ewe Rukiza, Rukiza, Rukiza, Rukiza, Rukiza,

Rukiza, mtoto wa mama

461. Rukiza akaitika, “Na uishi maishi marefu!

462. Ni nani wewe uniitaye ‘Rukiza’?

463. Hujui kuwa mimi huitwa ‘Mwinyi’ (waitu)?

464. Kinyampororo akajibu “Ni mimi Kinyampororo”

Chanzo: Mulokozi (2002:352)

Hivyo, ushairi wa majigambo uliotumika katika mistari hii umesaidia kumtambulisha mhusika kuwa ni

shujaa na pia kutambulisha sifa za shujaa husika.

2. Ushairi wa Kiswahili na Kuhamisha na Kujenga Mbinu za Kifani

Dhima nyingine ya ushairi ni kujenga mbinu mbalimbali za kifani. Hili linathibitisha na

Mulokozi (2002:10) anaposema kwamba tabia ya tendi kutumia au kuazima mbinu za kifani kutoka

katika ushairi wa majigambo huhamisha sitiari na udokezi ambazo hutumiwa sana katika majigambo

kwenda kwenye tendi.

37

The tendency of the epic to incorporate or borrow material from praise poetry transfers a

lot of the rich praise poetry metaphors and allusions into the epics.

Tabia ya tendi kutumia au kuazima matini kutoka katika majigambo huhamisha sitiari na

udokezi ambazo hutumiwa sana katika majigambo kwenda kwenye tendi (Tafsiri na

msisitizo wetu).

Hapa tunaona wazi kwamba pale ushairi wa majigambo unapotumika katika utanzu wa utendi, labda na

tanzu nyinginezo za fasihi simulizi, hujenga mbinu za kifani kwa kuhamisha mbinu zile zinazotumika

katika ushairi wa majigambo na kuzipeleka katika utanzu husika ambao hutumia ushairi huo wa

majigambo. Zaidi ya kuhamisha sitiari na udokezi, ushairi wa majigambo pia huhamisha chuku na

ucheshi, mbinu ambazo hutumika sana katika majigambo. Vivyo hivyo nyimbo, kama ushairi,

zinapotumiwa katika riwaya, tamthilia au utanzu mwingine wowote, huhamisha mbinu za kifani

zilizopo katika wimbo kwenda katika utanzu husika.

Vilevile matumizi ya ushairi katika tanzu nyingine yanasaidia kuibua ushiriki wa hadhira.

Ushiriki wa hadhira ndiyo msingi wa kazi yoyote ya kifasihi simulizi. Sifa hii ni mojawapo ya sifa

zinazoifanya fasihi simulizi kuwa hai. Akielezea jinsi ushairi wa majigambo unavyoweza kuifanya

hadhira ishiriki katika kazi ya fasihi, na hasa tendi, Mulokozi (2002:60) anasema:

Another form of participation occurs when a performance of a given poem is so inciting

that a member of the audience becomes ‘possessed’ by the poetic muse, leaps up, and

begins reciting his ekyebugo ‘self praise’. At that juncture, the bard, pleased by the effect

of his performance on his listerners would usually postpone his singing without breaking

off his instrumental music while the ekyebugo performance lasts.

Namna nyingine ya ushiriki wa hadhira hutokea pindi utendaji wa shairi husika

unapovutia mno kiasi kwamba mmoja wa wasikilizaji (hadhira) huweza “kupagawa” na

munkari wa kishairi, na kuanza kughani majigambo binafsi. Katika hali hii, manju, huku

akifurahia athari ya utendaji wake kwa wasikilizaji wake, kwa kawaida atasimamisha

uimbaji wake bila kusitisha mapigo ya kimuziki wakati utendaji wa majigambo (wa

hadhira iliyogeuka fanani) ukiendelea (Tafsiri yetu).

Hivyo, tunaweza kusema kwamba ushairi wa majigambo na ushairi wa Kiswahili kwa ujumla husaidia

sana katika kuibua ushiriki wa hadhira katika tanzu nyingine za fasihi na hivyo kuzihuisha tanzu hizo.

3. Ushairi wa Kiswahili na Kuibua Maudhui

Kazi ya fasihi hujengwa na maudhui na fani. Kama tulivyofafanua katika sehemu nyingine za

andiko hili, maudhui ni jumla ya mawazo yaliyomo katika kazi ya fasihi wakati fani ni mbinu

zitumikazo kuwasilisha maudhui hayo. Ushairi wa Kiswahili unapotumiwa katika tanzu nyingine za

fasihi huweza kusaidia kuibua au kukazia maudhui yabebwayo na kazi husika ya fasihi. Kwa mfano,

ushairi wa Kiswahili unapotumiwa katika utanzu wa ngano (hadithi), riwaya, tamthilia au hadithi fupi

huweza kusaidia kudokeza au kukazia maudhui yabebwayo na kazi husika ya fasihi. Akifafanua dhima

ya nyimbo, ambao ni kipera cha ushairi, katika hadithi fupi Samwel (2012b:44-46) anaeleza kuwa

waandishi wa hadithi fupi huweza pia kutumia nyimbo. Anafafanua zaidi kuwa matumizi ya nyimbo,

ambacho ni kipera cha ushairi simulizi, katika hadithi fupi, ambacho ni kipera cha fasihi andishi

yanaonyesha jinsi tanzu zinavyoingiliana, kukamilishana na kutegemeana. Samwel (khj.) anaendelea

kueleza kuwa waandishi wa hadithi fupi hutumia mdokezo wa wimbo ili kuibua maudhui

wanayoyakusudia. Anatoa mfano wa matumizi ya nyimbo katika hadithi ya Maeko katika Damu

Nyeusi na Hadithi Nyingine ambapo nyimbo kadhaa zinatumika. Wimbo wa kwanza unatumika kama

kitangulizi cha hadithi hiyo ya Maeko katika ukurasa wa 50. Wimbo huu unaimbwa na Hamduni au

Duni. Huu ni wimbo wa taarabu njia, kwa maana ya kwamba inaimbwa njiani unaoimbwa kama

ifuatavyo:

Wengi wanakuuliza, lililokuweka, oo ‘kuweka

Hutaki kuwaeleza, kuwa meridhika, oo ‘ridhika

Pendo lina miujiza, ya kuajibika, oo ‘ajibika

Ndipo likawashngaza, kwani kunitaka, oo ‘nitaka

38

Samwel (khj.) anaeleza kuwa Duni katika wimbo huo anaangazia ukweli kwamba Jamila ametosheka

na pendo analompa. Pia anabainisha kuwa mapenzi hayo yamewastaajabisha Wanasebleni. Wimbo huu

umerudiwa tena katika ukurasa wa 57 (Takriri ya wimbo).

Samwel anabainisha pia kuwa wimbo wa pili umetumika katika ukurasa wa 51 na mwimbaji ni

yuleyule Hamduni. Katika wimbo huu Duni anamshauri Jamila awaarifu Wanasebleni kwamba

wasimsumbue kimapenzi. Wimbo wa tatu unaobainishwa na Samwel upo katika ukurasa wa 51.

Mwimbaji ni Hamduni vilevile. Katika wimbo huo Duni anamwakilisha mkewe Jamila kuhusu ndoa.

Anakiri kwamba anadumu katika ndoa hiyo kwa sababu ya yale anayofanyiwa na Hamduni. Samwel

anahitimisha kuwa matumizi haya ya nyimbo yana umuhimu mkubwa kwani yanadokeza maudhui.

Aidha, Samwel (khj.) anabainisha kuwa nyimbo zimetumika pia katika hadithi ya Ndoa ya

Samani katika kitabu hichohicho. Samwel anaeleza kuwa hapa nyimbo za harusi zikitumika katika

hadithi fupi. Anatoa mfano wa nyimbo zinazotumika kuwa ni pamoja na wimbo wa bwana arusi

unapoonekana katika uk. 85 kama ifuatavyo:

Yu wapi ee, yu wapi bwana arusi aje hapa!

Tuhangaike naye!

Yu wapi ee, yu wapi bwana arusi aje hapa!

Tuhangaike naye!

Aje hapa!

Tuhangaike naye!

Eeh aje hapa!

Tuhangaike naye!

Anaendelea kufafanua kuwa wimbo huu, zaidi ya mambo mengine, unaonyesha suala la mila na

desturi kwamba arusi ni tukio la shangwe na nderemo ambalo huambatana na nyimbo. Wimbo huu

pia unabeba maudhui yahusuyo majukumu ya ndoa. Unaeleza kwamba maisha ya harusi ni yenye

changamoto nyingi na hujumuisha kuhangaika kwa wanandoa katika kutimiza mahitaji muhimu.

Hivyo, wimbo huu unamjuza bwana arusi ukweli wa mambo.Wimbo wa pili anaoubainisha

Samwel unaonekana katika ukurasa huohuo na una maneno yafutayo:

Hongera mwanangu eeh hongera a!

Name nihongeree hongera!

Mama uchungu mama uchungu

Nyamala mwanangu oyee

Nyamala mwanangu tumbo la uzere linauma mno oyee!

Oyee linauma mno eeh!...

Anabainisha kuwa wimbo huu na unabeba maudhui ya kumpa hongera binti anayeolewa lakini pia

unamweleza matumaini ya jamii juu yake kwamba ndoa huimarika kwa kuzaa watoto. Hata hivyo,

bi arusi anatahadharishwa kwamba kujifungua si kitu rahisi. “Tumbo la uzere” hapa linamaanisha

tumbo la uzazi. Mama ajifunguapo hupongezwa kwa kupata mtoto lakini kuna maumivu ya

uchungu ayapatayo kabla ya kupewa hongera hizo. Suala la uzazi katika ndoa na umuhimu wake

linabeba falsafa halisi ya Kiafrika kwamba ndoa ni watoto (Van Pelt, 1971). Hivyo nyimbo hizi

zinapotumika katika hadithi fupi, hazina budi kuchambuliwa na kuhusishwa na maudhui ya hadithi

yenyewe. Zaidi ya kutumika katika hadithi fupi ushairi wa Kiswahili (nyimbo) huweza kutumiwa

katika riwaya, tamthilia na novela kwa maksudi hayohayo.

4. Ushairi wa Kiswahili na Kukuza Tanzu za Fasihi

Mbali na dhima hiyo ushairi wa Kiswahili, ushairi huo pia huweza kukuza tanzu za fasihi.

Inaelezwa na wataalamu mbalimbali kuwa matumizi ya nyimbo, pamoja na matumizi ya vipengele

vingine vya fasihi simulizi katika fasihi andishi, yanakuza tanzu za fasihi andishi. Matumizi haya ya

vipengele vya fasihi simulizi ndani ya fasihi andishi ambayo hayakuwapo hapo awali katika fasihi

andishi ya Kiswahili, yameibua kile kinachoitwa katika fasihi ya Kiswahili, majaribio katika fasihi na

yameibua dhana ya fasihi ya majaribio (Senkoro, 2011). Hivyo, matumizi haya yameibua riwaya ya

majaribio, tamthilia ya majaribi na kadhalika. Hivyo, matumizi ya tanzu za fasihi simulizi, ikiwa ni

pamoja na ushairi simulizi (nyimbo), yamekuza fasihi andishi ya Kiswahili. Matumizi haya ya nyimbo

katika tanzu za fasihi andishi yanabainishwa pia na Mutembei (2012). Mutembei (khj.) anabainisha

39

kuwa nyimbo zimetumiwa katika tamthilia ya Hatia (Muhando, 1972) ambapo wimbo unaanza katika

onyesho la kwanza kama ifuatavyo:

Sikilizeni, sikilizeni

Hapa si kijijini…ooh

Hapa ni mji mkubwa

tunayaona

Mutembei (2012) anabainisha pia kuwa kuna matumizi ya wimbo kwenye tamthilia ya

Nitaolewa Nikipenda (Ngugi na Ngugi, 1982), Nguzo Mama (Muhando, 1982), Lina Ubani (Muhando,

1984), Mashetani (Hussein, 1971) na Morani (Mbogo, 1993). Mutembei (2012) anaeleza kuwa, zaidi

ya mambo mengine, matumizi haya ya nyimbo hukazia maudhui yabebwayo na tamthilia husika na

kubadilisha mtindo wa uandishi wa tamthilia. Wimbo uliopo katika tamthilia ya Nguzo Mama

unabainisha jinsi jitihada za wanawake kujikomboa zinavyokwamishwa na wanawake wenyewe na pia

wimbo katika tamthilia ya Morani unadokeza maudhui ya uhujumu uchumi. Aidha, matumizi haya ya

nyimbo yanajenga picha, taswira na sitiari katika kazi ya fasihi. Hili linabainika katika wimbo

unaoimbwa kwenye tamthilia ya Lina Ubani, “Ngoma hii siiwezi,” unaibua sitiari ya ngoma katika

tamthilia hii. Ngoma hapa inatumika kumaanisha msiba au majanga.

Tuhitimishe sura hii kwa kufafanua kwamba ushairi wa Kiswahili una dhima kubwa sana kwa

jamii ya Waswahili na pia kwa fasihi yao na ya jamii nyinginezo. Hata hivyo, tuonye hapa kuwa, mbali

na dhima kubwa iliyonayo ushairi wa Kiswahili kwa jamii na fasihi, ushairi wa Kiswahili kama zilivyo

tanzu nyingine za fasihi ya Kiswahili na fasihi ya jamii nyinginezo isipochukuliwa kwa tahadhari

huweza kuipotosha jamii. Samwel (2013) akielezea uwezekano wa fasihi kupotosha jamii anabainisha

kuwa ni ukweli usiopingika kwamba utanzu wowote wa fasihi unaweza kupotosha kama

usipochukuliwa kwa tahadhari au kuzingatia mipaka yake ya utendaji. Katika utanzu wa semi, kwa

mfano, tunabaini wazi kwamba methali zinaelimisha sana. Methali kama vile “aliye juu mngoje chini”;

“sikio halizidi kichwa”; “wa mbili havai moja”; “haraka haraka haina baraka” na nyinginezo nyingi

zinatoa maadili muhimu sana katika jamii.

Samwel (khj.) anaanza na methali “aliye juu mngoje chini” ambapo anabainisha kuwa methali

hiyo inahimiza wanajamii kuwa wavumilivu na kwamba pale wanaponyanyaswa na kuonewa hawana

budi kuwa na subira maana ipo siku wanaowanyanyasa “watashuka chini.” Hata hivyo zaidi ya

kuelimisha huko methali hii inaweza kupotosha. Methali hii, kwa upande mwingine, inawahimiza

wanajamii kutochukua hatua pindi mabaya yanapofanywa katika jamii kwa imani kwamba kuna siku

mambo yatakaa sawa yenyewe. Mwelekeo huu kwa hakika ni wa upotoshaji kwani kama wazee wetu

wangeichukulia methali hiyo kwa mkondo huo hakuna shaka hadi leo ukoloni bado ungekuwa

waendelea kwani wasingepambana nao.

Hali kama hiyo inaonekana katika methali “sikio halizidi kichwa.” Methali hii ni muhimu sana

katika kuadilisha. Inajaribu kutoa onyo kwa watoto kwamba kamwe hawawezi kuwa na hekima kuliko

wazee wao. Hivyo, inahimiza watoto kuwaheshimu wakubwa wao. Hata hivyo, kama methali hii

isipochukuliwa kwa tahadhari inaweza kupotosha jamii. Upotoshaji unaweza kutokana na ufafanuzi

kwamba methali hii inadidimiza juhudi katika maendeleo. Methali hiyo inaweza kuchukuliwa kwamba

inawaonya watoto kutotia bidii katika kazi kwani kama wazazi wao ni maskini wao kamwe hawawezi

kuwa matajiri kuliko wazazi wao. Mtazamo kama huo unabebwa na methali “wa mbili havai moja.”

Kwa upande wa “haraka haraka haina Baraka,” Samwel anaeleza kwamba inafanana na methali

nyingine kama vile “polepole ndiyo mwendo,” “subira yavuta heri” na kadhalika. Methali hizi

zinaionya jamii kutofanya mambo kwa pupa. Kabla ya kufanya jambo lolote lile ni muhimu kutafakari

na kupanga mikakati ya kulifanya jambo husika. Hata hivyo, zaidi ya kuelimisha hii methali hii

inaweza kupotosha na hasa pale inapotumika katika mazingira yasiyofaa. Kwa mfano, kama mtu ana

mgonjwa na akatumia methali hii bila shaka mgonjwa huyo atakufa kwani mgonjwa anahitaji huduma

ya haraka. Vivyo hivyo kama mtu amevamiwa na majambazi au anakabiliwa na hatari na akazitumia

methali hizi hatuna shaka kwamba atapatwa na madhara makubwa kwani katika nyakati za hatari

maamuzi ya haraka huhitajika. Mbali na upotoshaji wote huu bado methali zitabaki kuwa tungo

fupifupi za hekima na za kimapokeo zinazotumika kurithisha falsafa ya jamii kutoka kizazi kimoja hadi

kingine (Mulokozi, 1996; Cuddon, 1998; Senkoro, 2011).

Samwel anaendelea kubainisha kuwa uwezekano wa utanzu fulani kupotosha jamii hauishii tu

katika semi, na hasa methali bali unaonekana pia katika tanzu nyinginezo, ushairi ukiwemo. Hivyo,

40

tuhitimishe kuwa utanzu wowote wa fasihi unatimiza majukumu makuu mawili ya kifasihi ambayo ni

kuelimisha na kuburudisha (Mulokozi, 1996). Katika kuelimisha ndipo tunaona kuna mambo kama

kuadilisha, kuadibisha, kuonya, kukosoa, kuhifadhi amali za jamii, kuendeleza historia na kadhalika.

Mbali na dhima hizo kuu mbili za fasihi, isipochukuliwa kwa tahadhari, fasihi huweza kuipotosha

jamii. Hivyo ni jukumu la wanajamii kuichukulia kazi yoyote ile ya fasihi kwa uangalifu mkubwa ili

iweze kuwafaidisha. Aidha, ni jukumu la washairi wa Kiswahili kuhakikisha kadri inavyowezekana

wanatoa kazi bora za kifasihi ambazo zitatimiza majukumu ya kuelimisha na kuburudisha na

kupunguza uwezekano wa kupotosha jamii.

41

SURA YA TATU

CHIMBUKO LA USHAIRI WA KISWAHILI

Chimbuko, kama tunavyolitumia katika andiko hili, tunamaanisha asili au chanzo cha jambo fulani.

Hivyo, kusema chimbuko la ushairi wa Kiswahili tunamaanisha asili au chanzo cha ushairi wa

Kiswahili. Katika sura hii maneno asili na chanzo yatatumika pia kumaanisha chimbuko.

Chimbuko la ushairi wa Kiswahili, kama ilivyo vipengele vingine tulivyoviangalia hapo awali, ni

suala telezi mno. Utelezi wa suala hilo unatokana na ukweli kwamba kuna nadharia mbalimbali

zinazoelezea chimbuko hilo. Nadharia kuu mbili kati ya hizo, zimeshika mizizi zaidi, kwanza ile

nadharia inayodai kwamba asili ya ushairi wa Kiswahili ni Uislamu na fasihi za Kiarabu na pili, ile

nadharia inayodai kwamba chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni ushairi simulizi wa jamii mbalimbali za

Wabantu. Katika sehemu hii tutachambua nadharia hizi kwa kina na kuona ni ipi inayoweza

kutushawishi kama wanataaluma kukubali chimbuko la ushairi wa Kiswahili.

1. CHIMBUKO LA USHAIRI WA KISWAHILI NI UISLAMU/KIARABU

Dai hili ndilo la awali kabisa na linajibainisha vema katika andiko la Lyndon Harries (1962) liitwalo

Swahili Poetry. Harries anaeleza kuwa, chimbuko au asili ya ushairi wa Kiswahili ni “Uislamu na fasihi

ya Kiarabu.” Anaamini kuwa ushairi wa Kiswahili ulianza karne ya 17 na umetokana na Uislamu na

unafanywa sana na Waislamu. Anaendelea kudai kwamba ushairi wa Kiswahili ulianza pwani ya

kaskazini ya Kenya na hasa Lamu. Wafuasi wa mtazamo huu wa Harries wanauhusisha ushairi wa

Kiswahili na Uislamu na fasihi ya Kiarabu kutokana na mambo kama vile: ushairi wa Kiswahili kuanza

kipindi cha Waarabu, ushairi wa Kiswahili kutumia maneno ya Kiarabu, ushairi wa Kiswahili kubeba

maudhui ya Kiarabu, ushairi wa Kiswahili kuandikwa kwa hati za Kiarabu, ushairi wa Kiswahili

kutungwa sana na Waislamu, ushairi wa Kiswahili kuamini Uislamu na pia ushairi wa Kiswahili

kutumia kanuni za ushairi wa Kiarabu. Tuchunguze kwa makini hoja moja baada ya nyingine kati ya

hizi.

III. Ushairi wa Kiswahili kuanza kipindi cha Waarabu

Hoja ya kwanza inayotumiwa na wafuasi wa nadharia inayodai kwamba ushairi wa Kiswahili

chimbuko lake ni Uislamu ni kwamba ushairi huo ulianza katika kipindi ambacho Waarabu

walitamalaki katika upwa wa Afrika Mashariki. Kipindi kinachodaiwa kuwa ushairi wa Kiswahili

ulianza (karne ya 10-17) ni kipindi ambacho Waarabu walikuwa wameshakuja katika upwa wa Afrika

Mashariki na kufanya biashara na wenyeji. Katika karne ya 17 ndipo Waarabu walipoiteka ngome ya

Yesu kule Mombasa na kuhitimisha utawala wa Wareno waliokuja kuimiliki biashara kati ya Waarabu

na Waswahili (Coupland, 1938). Hivyo, kipindi hicho kiliiamsha upya biashara baina ya Waswahili na

Waarabu na hivyo tunaweza kukiita kuwa ni kipindi cha Waarabu kutamalaki. Kutokana na Waarabu

kutamalaki na kuwa na maendeleo ya kiuchumi, yaliyotokana na biashara mbalimbali walizozifanya,

mamwinyi wao walihitaji kitu cha kuwaliwaza. Hapo ndipo walipoingiza fasihi zao ili kujiliwaza na

ndiyo ukawa mwanzo wa ushairi wa Kiswahili. Uwezekano wa maendeleo ya kiuchumi kuibua kazi ya

fasihi umeelezwa pia na Mulokozi (1996:147) anapozungumzia maendeleo ya riwaya ya Kiswahili.

Anasema:

Kufikia karne ya 16, fani zilizotajwa hapo juu (visakale, visasili, sira n.k.) zilikuwa

zimekwisha enea na kufahamika katika mataifa mengi; kulihitajika tu msukumo wa

kijamii, kiteknolojia, na kiuchumi ili ziweze kuvyaza riwaya…Jambo la kwanza ni ukuaji

mkubwa wa shughuli za kiuchumi huko Ulaya. Ukuaji huo ulifungamana na biashara ya

baharini ya mashariki ya mbali, ‘kuvumbuliwa’ kwa mabara mawili ya Amerika, na

kukua kwa nyenzo za uzalishaji wa viwandani huko Uingereza, hasa viwanda vya nguo.

Malimbikizo ya ziada yaliyotokana na shughuli hizo yalipanda mbegu ya mapinduzi ya

viwanda yaliyotokea karne mbili baadaye. Aidha, mabadiliko haya yalizua tabaka jipya la

mabwenyenye waliohodhi viwanda na nyenzo nyingine za uchumi. Tabaka hilo lilihitaji

fani mpya za fasihi, lilikuwa na wakati wa ziada wa kujisomea, na uwezo wa kifedha wa

kujinunulia vitabu na magazeti.

Japo Mulokozi hakuwa akizungumzia kuhusu kuibuka kwa ushairi wa Kiswahili katika kipindi cha

Waarabu na kwamba yeye si mmoja wa wafuasi wa dai hilo lakini maelezo yake yanatusaidia kueleza

42

kwa nini ushairi wa Kiswahili unadaiwa kuibuka katika kipindi cha kutamalaki kwa Waarabu. Ni kwa

kuwa Waarabu walishajilimbikizia mali na walikuwa na muda wa kusoma na fedha za kujipatia kazi za

kishairi, hivyo kuibuka kwa ushairi wa Kiswahili.

Hata hivyo mtazamo huu kwamba ushairi wa Kiswahili uliibuka wakati wa Waarabu una kasoro.

Kasoro hiyo inatokana na ukweli kwamba ushairi simulizi umekuwapo miongoni mwa wakazi wa upwa

wa Afrika Mashariki na Bara kwa muda mrefu sana, hata kabla ya ujio wa Waarabu. Tukubali tu

kwamba huenda ni kweli kwamba ushairi andishi wa Kiswahili uliibuka baada ya Waarabu kuja,

kuhubiri dini ya Kiislamu na kuwafunza Waswahili hati za maandishi. Baada ya kujifunza hati hizo

ndipo walipoutia ushairi simulizi, uliokuwapo tangu enzi, katika maandishi na kuibua kile

kinachojulikana leo kama ushairi wa Kiswahili. Hivyo dai kwamba ushairi wa Kiswahili unatokana na

Uislamu na fasihi ya Kiarabu, linakosa mashiko.

IV. Ushairi wa Kiswahili uliibuliwa na wafuasi wa Waarabu

Hoja ya pili inayotumika kushadidia kwamba asili ya ushairi wa Kiswahili ni Uislamu na fasihi ya

Kiarabu ni kwamba ushairi huo uliibuliwa na kuenezwa na wafuasi wa Waarabu. Kwa kusema kwamba

ushairi wa Kiswahili uliibuliwa na wafuasi wa Waarabu ina maana kwamba washairi wengi wa

mwanzo wa ushairi wa Kiswahili walikuwa na mahusiano ya karibu na Waarabu. Mahusiano hayo

yanaweza kutokana na unasaba au mambo mengine ya kijamii kama vile dini na ndoa. Inadaiwa

kwamba washairi wengi wa mwanzo wa ushairi wa Kiswahili kama si kuwa na damu ya Kiarabu,

kuzaliwa kutokana na ndoa ya Mwarabu na Mswahili, walikuwa wafuasi wa dini ya Kiislamu au

walikuwa wamehusiana na Waarabu kindoa katika nasaba zao. Uhusiano huo unabainika kwa washairi

hao kuwa Waislamu au kuwa na majina ya Kiarabu. Tunaona, kwa mfano, washairi kama vile Shaaban

Robert, Amri Abedi, Sayyid Abdallah bin Ali, Mohamadi Kijumwa na wengineo wengi ni Waislamu,

wafuasi wa Waarabu kwa dini yao. Kutokana na hilo wafuasi wa nadharia ya Harries wanadai kuwa

hakuna shaka kwamba huenda Waarabu na Uislamu vilikuwa na nafasi katika ushairi wao.

Hata hivyo zaidi ya ukweli ambao unaweza kubebwa na hoja hii ni dhahiri kwamba hoja hii, kama

ile iliyotangulia, ni dhaifu pia. Udhaifu huo unatokana na ukweli tulioudokeza hapo awali kwamba

Waarabu waliwafunza wenyeji hati za maandishi ambazo hatimaye walizitumia kuuweka ushairi

simulizi, uliokuwapo tangu zama, katika maandishi na kuibua kile kilichokuja kuitwa ushairi wa

Kiswahili. Vilevile, zaidi ya kujifunza hati za Kiarabu, washairi hawa walijifunza ushairi wa Kiarabu

kupitia kaswida walizofunzwa katika Uislamu. Kaswida hizi, kwa kuwa nyingi zilikuwa katika

maandishi, ziliwaonyesha haja ya wao pia kuweka ushairi wao katika maandishi. Kutokana na hilo sasa

ushairi wa Kiswahili ukaibuka. Aidha, ifahamike pia kwamba wapo washairi wengine Wakristo

waliokuwapo karibu kipindi sawa na kuwapo kwa washairi wa Kiislamu. Miongoni mwa washairi hao

ni pamoja na Mathias Mnyampala.

V. Ushairi wa mwanzo wa Kiswahili ulihusiana na Dini ya Kiislamu na Uarabu

Jambo lingine linalotumika kushadidia kwamba ushairi wa Kiswahili unachimbuka katika Uislamu

na fasihi ya Kiarabu ni kwamba ushairi wa mwanzo wa Kiswahili ulihusiana sana na dini ya Kiislamu

na Uarabu. Hii ni kusema kwamba mashairi mengi ya mwanzo yalizungumzia Uislamu na Uarabu na

katu hayakuhusiana sana na masuala ya Waswahili. Ushairi mwingi ulioandikwa katika kipindi hiki

ulizungumzia mambo yanayohusiana na dini ya Kiislamu. Kwa mfano, utenzi wa Hamziyya ambao

unahusu maisha ya Mtume Muhamadi, ambaye ndiye mwanzilishi wa Uislamu; utenzi wa Tabuka

ambao unazungumzia juu ya vita kati ya Waislamu wa mwanzo na Mfalme Herekali wa dola ya

Warumi (Mulokozi, 1996:114). Ushairi mwingine wa Kiswahili uliobeba masuala yanayohusiana na

Uislamu na Uarabu ni Utenzi wa Al-Inkishafi na Utenzi wa Mwanakupona. Mulokozi (1999:71)

anabainisha kwa msisitizo kwamba:

Msingi wa maudhui ya Inkishafi ni Kurani Tukufu; mwandishi anachukua mafundisho ya

Kurani kuhusu maisha na mwenendo bora wa muumini, na kuyafafanua kwa vielezo

vinavyotokana na historia na mazingira ya Pate na Afrika Mashariki kwa

ujumla…Dhamira kuu ya Inkishafi ni kufafanua maana ya maisha: Je, maisha ni nini na

yana lengo gani? Maana anayoitoa ni ile ya kidini- ya Kiislamu.

43

Hapa tunabaini wazi kwamba utenzi huu umebeba maudhui mengi yanayohusiana na dini ya Kiislamu.

Tunaona hata maonyo yanayotolewa katika utenzi huu, falsafa ya maisha baada ya kufa inayoelezwa

humo na mengineyo yanaendana na mtazamo wa dini ya Kiislamu. Hali hiyohiyo inaonekana katika

Utenzi wa Mwanakupona ambapo maadili anayopewa binti wa kike ni maadili yanayotokana na Kurani

Tukufu. Ieleweke hapa, hata hivyo, kwamba hatuna kusudi la kudai kwamba tenzi husika ni za kidini

na hazina maana nje ya mpaka ya kidini. Kwa hakika tenzi husika zina maana pia nje ya muktadha wa

kidini kwani mambo mengine yanayoelezwa humo yanafaa katika maisha kwa ujumla wake.

Kama ilivyo kwa hoja zilizotangulia, hoja kuwa ushairi wa Kiswahili unatokana na Uislamu na

fasihi ya Kiarabu kutokana na uhusiano wake na Uislamu na Uarabu haina mashiko ya kitaaluma.

Ukosefu huo wa mashiko unatokana na hoja kwamba, kwa kuwa washairi wengi wa mwanzo (kama

ilivyobainishwa hapo awali) walikuwa Waislamu, hatuna shaka kwamba ingeshangaza sana ikiwa

washairi hao wasingetunga mashairi yanayohusiana na Uislamu. Fasihi ni zao la jamii na hubeba yale

yaliyomo katika jamii na uzoefu wa maisha ya msanii husika (Samwel, 2012a). Hivyo fasihi haiwezi

kujitenga na msanii na jamii yake. Aidha, ni jambo linalopaswa kukumbukwa kwamba wakati huu

ulikuwa ni wakati wa kutamalaki kwa dini ya Kiislamu na Uarabu, hivyo fasihi ilisawiri hali halisi.

Hali hiyo inaonekana pia katika vipindi vingine vya kihistoria miongoni mwa Waswahili ambapo

ushairi, na tanzu nyinginezo, zilisawiri matukio ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni yaliyopo

katika jamii husika. Mulokozi (1996) anaonyesha jinsi ushairi na tanzu nyinginezo za fasihi ya

Kiswahili zilivyosawiri mambo kama ukoloni na harakati za kuuondoa, uhuru, azimio la Arusha, vita

vya Idd Amini na kadhalika.

VI. Ushairi wa Kiswahili ulishamiri sana katika maeneo yaliyokaliwa na Waarabu

Hoja nyingine ya msingi ni kwamba ushairi wa Kiswahili asili yake ni Uislamu na fasihi ya Kiarabu

kwa sababu ushairi huo ulishamiri sana maeneo yaliyokaliwa na Waarabu kama vile Kigoma, Tanga,

Tabora, Lamu, Pate na maeneo mengine. Maeneo haya ndiyo yanayotajwa kuwa njia kuu za biashara ya

Waarabu (Coupland, 1938). Aidha, maeneo haya pia ndiyo ambayo yalishuhudia ustawi mkubwa wa

ustaarabu wa Kiarabu pamoja na dini ya Kiislamu. Mifano ya washairi waliotoka katika maeneo tajwa

inabainishwa hapa chini:

·Kigoma: katika mkoa huu ndipo walipotoka washairi kama vile Amri Abedi, Issa Kitenge na

wengineo

·Tanga: mkoa wa Tanga ulitoa washairi kama vile Shaaban Robert, Hemed bin Abdallah el-

Buhry au maarufu kama Mzee Kibao, Ghulam Mabondo bin Mwinyimatano, Swalehe

Kibwana, Mwinyihatibu Mohamed Amiri n.k.

·Bagamoyo: huku alitoka Mahmoud M. Hamdouny bin Khalfan na wengineo

· Tabora: alikotoka Mwamshamu Yange na wengineo

· Lamu: alikotoka Muhamadi Abubakar Kijumwa, Ahmed Sheikh Nabhany, Zahid bin Mngumi

n.k.

· Pate: alikotoka Sayyid Abdallah bin Ali bin Nasiri, Mwanakupona Binti Mshamu Nabhany,

Fumo Liyongo, Ali Athmani Koti, Mohammad bin Sheikh Mataka n.k..

· Mombasa: huko alitoka Ahmad Nassir bin J. Bhalo n.k.

Historia hii ya washairi na mahali wanapotoka inaelezwa kwa kina katika Mulokozi na Sengo

(1995:28-60). Hivyo, kwa ufafanuzi wa kina kuhusiana na maeneo walikotoka washairi wa mwanzo wa

ushairi wa Kiswahili tazama andiko hilo muhimu.

Kwa ujumla, tuseme kwamba wakati ambapo hatupingi kushamiri kwa ushairi wa Kiswahili katika

maeneo yaliyokaliwa na Waarabu, tunaona kwamba kuchukua hiyo kama hoja ya kuitumainia katika

madai mazito kama haya ni udhaifu mkubwa. Tulishadokeza hapo awali juu ya nafasi ya Waarabu

katika kuibuka kwa ushairi wa Kiswahili, japo tumekanusha kwamba wao si waanzilishi bali wao ni

watia shime tu wa kuibuka kwa ushairi huu. Hoja hiyo pia inafanya kazi hapa.

VII. Ushairi wa Kiswahili kutumia maneno na hati za Kiarabu

Zaidi ya hoja hizo hoja nyingine ni kwamba ushairi wa Kiswahili unatokana na Uislamu na fasihi ya

Kiarabu kwa sababu ushairi wa mwanzo wa Kiswahili (na kwa sehemu hata ushairi wa sasa) unatumia

maneno mengi ya Kiarabu. Mulokozi na Sengo (1995:87), japo wao hawaungi mkono dai kuwa ushairi

44

wa Kiswahili unatokana na Kiarabu, wanabainisha kwamba hata dhana nyingi zinazotumika katika

ushairi wa Kiswahili kama vile shairi, mizani, ubeti, tathlitha, tarbia, takhmisa n.k. zinatokana na lugha

ya Kiarabu. Suala la maneno ya Kiarabu liliibuka pia wakati wa mjadala kuhusiana na chimbuko la

Kiswahili ambapo baadhi ya wanataaluma wakadai kwamba ushairi ni lugha inayotokana na Kiarabu

(Taz. Kitabu cha Historia ya Kiswahili cha Massamba, 2002 kuhusu watu waliotoa madai haya). Hata

hivyo, Massamba (2002) katika kitabu hicho ambacho kwa hakika kimechimba kwa kina anapingana na

madai kwamba Kiswahili ni Kiarabu japo hakanushi juu ya Kiswahili kuwa na maneno mengi ya

Kiarabu. Anasema:

Lakini hata kama ni kweli kwamba katika lugha ya Kiswahili asilimia kubwa ya maneno ya

mkopo ni yale yatokanayo na lugha ya Kiarabu hiyo peke yake haiwezi kuwa sababu ya kutufanya

tutoe kauli kwamba Kiswahili ni Kiarabu. Tunaweza tu kufikia hitimisho kama hilo iwapo

tutathibitisha, kwa kutumia vigezo kuntu, kwamba mfumo mzima wa kiisimu wa lugha hii ya

Kiswahili unashabihiana kabisa au zaidi na mfumo wa Kiisimu wa lugha ya Kiarabu....

(Massamba, 2002:17).

Hapa tunaona wazi kwamba Massamba anapinga madai kwamba Kiswahili ni Kiarabu. Hata hivyo,

anaonekana kukubali kwamba Kiswahili kina maneno ya Kiarabu. Hivyo, tuseme kuwa kwa sababu

lugha ya Kiswahili ina maneno mengi ya Kiarabu na ushairi tunaouzungumzia hapa ni wa Kiswahili,

basi ingeshangaza sana kama ushairi huo usingetumia pia maneno ya Kiarabu. Hata hivyo, matumizi

hayo hayamaanishi kwamba ushairi huo ni wa Kiarabu. Jambo lingine muhimu kujikumbusha hapa

(kama ilivyokwisha daiwa na wanazuoni wengine), Kiswahili hakina maneno ya Kiarabu tu, bali pia

kina maneno ya lugha nyinginezo kama Kiingereza (kwa neno kama shati, sketi, skuli n.k.), Kijerumani

(kwa maneno kama shule toka katika schule) na kadhalika. Inasemwa kuwa ni tabia ya lugha zote

duniani kukopa maneno kutoka katika lugha nyingine. Kukopa huko hakuifanyi lugha kopaji kuwa

lugha kopwaji.

Kuhusiana na matumizi ya hati za Kiarabu katika ushairi wa mwanzo wa Kiswahili pia ni jambo

linaloelezeka na ambalo hatuwezi kulitegemea kuhalalisha kwamba ushairi wa Kiswahili ni Uislamu na

Uarabu. Matumizi ya hati za Kiarabu yanatokana na Waswahili kujifunza hati hizo na kuuweka ushairi

katika maandishi. Matumizi ya lugha fulani hayatoi kibali cha jambo kuwa la lugha hiyo. Kwa mfano,

tulishadokeza awali katika kitabu hiki kwamba kuna vitabu vingi vya Kiswahili vilivyoandikwa kwa

lugha ya Kiingereza. Hata hivyo, matumizi ya lugha ya Kiingereza hayavifanyi vipengele

vilivyoandikwa kuwa vya Kiingereza. Tunaweza pia kutumia lugha ya Kiswahili kuandika ushairi wa

Kiingereza na wa lugha nyinginezo. Akipinga kuuhusisha ushairi wa Kiswahili na Kiarabu kwa

kuegemea katika matumizi ya hati za Kiarabu Mutua (2006:3) anasema:

na ieleweke kuwa Waswahili au herufi za Kiarabu kuliwawezesha washairi (wambuji, malenga,

nguli na manju) wa Uswahilini, kuandika tungo zao wakitumia herufi hizo. Lakini matamshi ya

nyimbo yalikuwa ya Kiswahili. Kuja kwa Wazungu, na mafunzo yao ya herufi za Kilatini

kuliimarisha hifadhi kubwa ya hazina hiyo ya lugha na fasihi ya Kiswahili

Hivyo, Mutua anabainisha wazi kwamba si ujio wa Waarabu wala wa Wazungu unaoweza kuhusishwa

na asili ya ushairi wa Kiswahili. Jambo hili linathibitisha pasipo shaka yoyote kwamba nadharia

inayochukulia kwamba ushairi wa Kiswahili chimbuko lake ni Uislamu na fasihi ya Kiarabu zaidi ya

kuwa na ukweli wa namna fulani ina udhaifu. Ukweli wa nadharia hii unaonekana karibu katika hoja

zote tulizozipitia; hata hivyo, ukweli huo hautoshi kuegemeza madai kwamba ushairi wa Kiswahili ni

Uislamu na fasihi ya Kiarabu. Hata hivyo, ni lazima tukubali kwamba ushairi wa Kiswahili umepiga

hatua kubwa kutokana na mchango mkubwa sana wa Waarabu. Hawa ndiyo walileta hati za Kiarabu

ambazo zilitumika kuuhifadhi ushairi wa Kiswahili katika maandishi. Pia hawa walileta kaswida na

fasihi za Kiarabu ambazo ziliwahimiza Waswahili kuandika kazi za fasihi zao. Zaidi ya hayo, si kweli

kwamba Waarabu ndiyo walioibua ushairi wa Kiswahili. Aidha, mchango mwingine wa nadharia hii

inayodai kuwa ushairi wa Kiswahili unatokana na Waarabu na Uislamu ni kuwa yenyewe ndiyo ya

kwanza katika kuchunguza asili ya ushairi wa Kiswahili. Hivyo, iliweka misingi ya uchunguzi wa

chimbuko la ushairi wa Kiswahili. Hii ina maana kwamba nadharia nyingine zilizofuata ziliibuka

kutokana na udhaifu wa nadharia hii. Vilevile, tuseme hapa kwamba mjadala wa ushairi wa Kiswahili

45

kuibuka kutokana na Uislamu na Uarabu ulianzia katika lugha yenyewe, yaani lugha ya Kiswahili

ambapo pia madai kama hayo yalitolewa kwamba asili ya lugha ya Kiswahili ni Uislamu na Uarabu.

Massamba (2002:18) anapoelezea kasoro iliyopo katika kuihusisha lugha ya Kiswahili na Uislamu

anabainisha kwamba:

Kigezo cha dini ya Kiislamu ndicho kigezo dhaifu zaidi kuliko kile cha kwanza. Si sahihi

kuitumia dini kama kigezo cha kuiainishia lugha ya Kiswahili. Huko ni kuitumia dini mahali

ambapo si pake. Kwa hakika huko ni kushindwa kutofautisha utamaduni wa Kiarabu, Uislamu na

utamaduni wa Kiafrika…

Kama si sahihi kuihusisha dini na lugha, hatuna shaka si sahihi pia kuuhusisha ushairi wa lugha hiyo

na dini ambayo si sehemu ya utamaduni wa jamiilugha inayotumia ushairi huo. Kutokana na upungufu

wa nadharia hii sasa ndipo wataalamu wengine walipoibua nadharia tutakayoipitia katika sehemu

inayofuata.

2. CHIMBUKO LA USHAIRI WA KISWAHILI NI USHAIRI SIMULIZI WA KIBANTU

Mbali na nadharia hiyo, nadharia nyingine inayoelezea chimbuko la Kiswahili ni ile inayodai

kwamba ushairi wa Kiswahili unatokana na ushairi simulizi wa Kibantu, hasa nyimbo za ngoma na

nyinginezo. Nadharia hii inabainika katika maandiko mengi ya wanamapokeo ambao walidai kwamba

ushairi ni wimbo kama tulivyoona katika sura iliyotangulia. Kwa kudai kwamba ushairi ni wimbo, kwa

maneno mengine, walikuwa wanaibua dai kwamba chanzo cha ushairi wa Kiswahili ni nyimbo simulizi

zilizokuwapo tangu zama miongoni mwa jamii za Kiswahili. Wengi wa wanamapokeo tuliowapitia

hawafikii hitimisho hilo moja kwa moja ila Mnyampala (1964:4-7) analisema hilo waziwazi. Anasema:

Mashairi ni nyimbo zenye maghani ya mvuto wa madoido na vingorimbo bora. Aina ya nyimbo

hizo zilianzishwa na mababu au manabii wa zamani za kale, nazo ziliimbwa nyimbo hizo kwa ajili

ya kumtukuza na kumsifu mwenyezi Mungu, kwa masujudu yaliyoimbwa kishairi, haidhuru kwa

kukosana na vina na mizani baina ya mashairi ya leo na hayo.

Hapa Mnyampala anabainisha wazi kwamba anaufasili ushairi kuwa ni wimbo (na kwamba kama

shairi haliimbiki halina maana yoyote) kutokana na hoja kwamba ushairi wa Kiswahili umetokana na

nyimbo simulizi zilizoimbwa na mababu tangu zama za kale. Mnyampala anajenga hoja ambayo

haijengwi na wanamapokeo wengi wanaodai kwamba shairi ni wimbo. Mtazamo huu wa Mnyampala

unashadidiwa pia na Mutua (2006:3) anaposema kuwa mashairi ni tungo zenye kanuni maalumu

ambazo zina asili yake katika nyimbo. Zaidi ya kuungwa mkono, udhaifu wa Mnyampala ni kwamba

anayaona mashairi simulizi (nyimbo) kuwa yalibeba ajenda ya dini kama ajenda kuu. Dini, na hasa

Ukristo na Uislamu anaouzungumzia hapa, zilianza karne ya kwanza na ya sita mtawalia. Hivyo kama

mashairi yanahusiana na dini hizo tu ina maana kwamba mashairi hayo yameletwa na Wakristo na

Waislamu walioleta dini husika. Labda ili kuiboresha hoja hiyo tuseme kwamba mashairi yalikuwapo

hata kabla ya ujio wa dini hizo, wakati huo yakiisifu miungu ya Kiafrika, ambayo inadaiwa kuwapo

mahali pengi (taz. kuhusu miungu na nyimbo za kuwasifu katika Mulokozi, 2002 na Samwel, 2012a).

Hata hivyo, kama tutaliweka dai hilo hivyo, hoja kwamba ushairi chimbuko lake ni kazi na kwamba

binadamu waliimba nyimbo ili kuchapuza kazi, nyimbo ambazo zilizua mashairi itakosa nguvu. Dai

hilo kwa sasa linakubalika miongoni mwa wanafasihi wengi na limekwishafanyiwa tafiti za kina

kulithibitisha (Mulokozi, 1996). Tuseme tu kwamba wazo tunalolichukua kwa Mnyampala kwa sasa ni

kwamba ushairi wa Kiswahili chimbuko lake ni nyimbo. Wazo hilo pia linaonekana katika maandiko

ya wanazuoni na watafiti wa chimbuko la ushairi wa Kiswahili kama vile Chiraghdin (1971:7); Shariff

(1988), Senkoro (1988), Mulokozi (1996), Samwel (2012a) miongoni mwa wengi wengineo.

Wataalamu hawa wanadai kwamba asili ya ushairi wa Kiswahili ni nyimbo simulizi zilizoimbwa na

jamii za Waswahili. Jamii za Waswahili kama inavyochukuliwa hapa ni jamii mbalimbali katika upwa

wa Afrika Mashariki na bara. Jamii hizo hujumuisha watu wa makabila mbalimbali. Nyimbo za

makabila hayo ndizo hatimaye zilizokuja kuvyaza ushairi wa Kiswahili. Nyimbo hizo zilikuwa

zikiimbwa katika shughuli mbalimbali kama vile, wakati wa kufanya kazi, katika sherehe za harusi,

katika jando na unyago, kubembeleza watoto, kuombolezea n.k. na si katika ibada na kuwasifu miungu

tu.

46

Mtazamo kwamba ushairi wa Kiswahili unatokana na tungo simulizi za Waswahili unaonekana

pia katika andiko la Chiraghdin (1977) Malenga wa Mrima: Tungo za Mwinyihatibu Mohamed, la

Knappert (1979) Four Centuries of Swahili Poetry na la Mulokozi na Sengo (1995) History of

Kiswahili Poetry: AD 100-2000. Aidha, mtazamo huu unaonekana pia katika maandiko mengi ya

kisasa na umeshafanyiwa tafiti za kina na kuthibitika kwamba una madai ya msingi. Wanazuoni

mbalimbali wanathibitisha kwamba tungo simulizi za Waswahili zinahusiana sana na ushairi wa kisasa

wa Kiswahili. Mfano mzuri wa wanazuoni waliofanyia utafiti wa kina wa hilo ni Samwel (2012a)

ambaye alifanya utafiti wa kulinganisha na kulinganua ushairi wa Kiswahili wa kisasa wa vijana

(ushairi wa Bongo Fleva) na ushairi simulizi wa jamii ya Wahaya na Wasukuma (majigambo ya jadi).

Matokeo ya utafiti huo yanathibitisha uhusiano wa karibu uliopo baina ya aina hizo mbili za ushairi.

KUFANANA KWA USHAIRI WA KISWAHILI NA USHAIRI SIMULIZI WA KIBANTU

Suala la kufanana kwa ushairi wa Kiswahili na ushairi simulizi wa Kibantu limewashughulisha

wanafasihi mbalimbali. Miongoni mwa wanafasihi hao ni Mmbaga (2004) na Samwel (2012a) kwa

kuwataja wachache. Mmbaga (khj.) analinganisha ushairi wa ngonjera na ushairi simulizi wa kijadi

uliokuwapo katika makabila mbalimbali likiwemo kabila ya Wapare. Anabainisha kuwa ngonjera

zilikuwapo katika jamii mbalimbali za Wabantu tangu kale na kwamba fani inayoibuka katika miaka ya

1960-1970 kama inavyoonekana katika Ngonjera za Ukuta si fani mpya. Naye Samwel (2012a)

anashughulikia kufanana baina ya ushairi simulizi wa Kibantu na ushairi wa kisasa wa Kiswahili.

Anabainisha kuwa ushairi wa majigambo ya Bongo Fleva (ambao anaubainisha kama aina mpya ya

ushairi wa Kiswahili wa kisasa) unafanana sana na ushairi simulizi unaojibainisha katika majigambo ya

jadi ya Wahaya na Wasukuma. Kufanana huko kunabainika kuwapo katika vipengele vyote, yaani

katika maudhui na pia katika fani. Tupitie mfanano huo ili kujenga hoja inayotolewa na nadharia

tunayoishadidia.

I. Kufanana Kimaudhui

Samwel (2012a) anabainisha kwamba ushairi wa majigambo ya jadi na ushairi wa Bongo Fleva

unafanana sana katika dhamira, ujumbe, falsafa, itikadi na mawazo ya kazi ya fasihi kwa jumla. Katika

utafiti wake ilibainika kwamba aina zote mbili za ushairi hubeba maudhui ya kisiasa, kiuchumi, kijamii

na kiutamaduni. Baadhi ya maudhui yanayofanana baina ya majigambo ya jadi na ya Bongo Fleva ni

yahusuyo vita/ushindani, utawala, kazi, mila na desturi, imani za kidini na kadhalika. Tupitie kufanana

huko katika vipengele mahsusi ili kubaini hoja ya msingi:

(a) Kufanana kwa Maudhui ya Kisiasa

Kwa kuanza na maudhui ya kisiasa, tunaona kwamba, ushairi wa Kiswahili na ushairi simulizi

wa Kibantu unabeba maudhui kama vile vita na utawala. Kuhusu maudhui ya vita, tunaona kuwa jamii

za Kibantu za jadi zilihitaji kujipanua, hivyo kukawa na vita vya kugombea ardhi, mifugo, vyakula na

kadhalika. Kutokana na hilo, kukawa na ushairi wa vita. Maudhui haya ya vita yanabebwa pia na

ushairi wa Bongo Fleva. Aidha, tunabaini wazi kwamba katika aina zote mbili za ushairi shujaa ni mtu

muhimu.

Kufanana kwingine anakokubainisha Samwel kupo katika sifa za shujaa. Mbali na shujaa kuwa

mtu muhimu sana katika vita vinavyosawiriwa katika aina zote mbili za ushairi, sifa za shujaa huyo

katika aina zote mbili za ushairi zinafanana. Katika ushairi wa jadi, shujaa ni mtu jasiri, asiye na woga

na anayepambana ili kuilinda jamii yake. Katika ushairi huo, shujaa anakubalika katika jamii na

anaungwa mkono na wanajamii walio wengi katika harakati zake za kuitetea jamii husika. Aidha,

shujaa ni mtu mwenye nguvu nyingi za kimwili na uwezo wa kisihiri na kimiungu. Shujaa huyu pia

huogopa aibu kuliko kifo na rijali kamili. Samwel (2012a) anatoa mfano mzuri wa sifa hizi katika

Utendi wa Rukiza katika mistari ifuatayo kama inavyonukuliwa kwa Mulokozi (2002:87-88):

Waama ninahamanika

Heri nijiue kuliko kula vya haramu

Kula mboga za majani ya kunde na mnavu

Kula takataka zisanywazo na wajakazi!

47

Hapa tunaona Rukiza, ambaye ni shujaa katika utenzi huu, anasawiriwa kwamba hali kitu chochote tu

bali hula vitu vya hadhi ya juu na kwamba yupo tayari kufa kuliko kuaibika kwa kula vitu duni.

Sifa nyingine ya shujaa wa jadi ni kutokuwa mwoga na kuwa rijali kamili. Shujaa huyu hakuwa

anaogopa chochote na hata kifo. Pia alikuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kiwango

kisichokuwa cha kawaida ambacho wanajamii wengine hawawezi. Katika Utendi wa Rukiza, kwa

mfano, tunaona Rukiza anabainishwa kwamba haogopi kifo na ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa

usiku kucha. Katika mstari wa 465-475 wa utendi huo tuliyoinukuu hapa chini tunaliona hili. Tafsiri

yetu ya Kiswahili ya mistari hiyo inasema:

Mteule, mara zote umepigana vita,

Amka upigane vita…

Rukiza akarudi kulala

Kulipopambazuka

Akamwambia Ruhunga wa Nshaiga

Akasema ‘Unajua kukumbatia!

Mke wangu umenikumbatia tangu nilipokuja kulala…

Dondoo hili linatuonyesha kwamba shujaa Rukiza kama kiwakilisha cha shujaa wa jadi hakuogopa

kufa. Hata alipoambiwa maadui wameshafika, yeye akarudi kulala. Aidha, hapa tunaona shujaa huyu

jinsi alivyo rijali kamili kwani amefanya tendo la ndoa na mke wake usiku kucha. Vilevile tunaona

katika utendi huo kwamba shujaa huyu ndiye ambaye mara zote amepigana vita kuitetea jamii yake.

Sifa hizi za shujaa wa jadi zinafanana sana na za shujaa wa kisasa anayesawiriwa katika ushairi

wa Bongo Fleva. Katika ushairi wa Bongo Fleva shujaa anatajwa kuwa mtu asiye na woga na kiongozi

wa wengine katika mapambano ya kuitetea jamii husika. Aidha, shujaa huyo ndiye mtetezi mkuu wa

wanajamii husika, ana uwezo mkubwa wa kimwili na kiakili na rijali kamili. Samwel anatumia wimbo

wa “Mchakamchaka” ulioimbwa na Mr. 2 (Joseph Mbilinyi) ambapo msanii anasawiriwa kuwa ni wa

kwanza na wa mwisho (alfa na omega) na kwamba ndiye kiongozi (kamanda) kwa wenzake. Vilevile

hana uoga, ni mwakilishi wa watu na mtetezi wao (super delegeto, yaani super delegate) na mtu

asiyechoka katika kupambana kama inavyobainika hapa chini:

1. Anha alfa na omega

2. Na ndo maana ni vigumu sana kuiga

3. Kwenye maisha mimi kamanda

4. Sina uoga

5. Na wanga wanavyochonga mimi sipigi nao kelele

6. Zangu mimi ni vita mbele

7. Babu asikwambie mtu kitu

8. Jasho la mtu haliendi bure

9. Na kwenye maiki bado naikamata bongo

10. Yaani mfano wa Koffi anavyoikamata bongo na bolingo

11. Na bado nasaka mingo anha

12. Ni mchakamchaka ni mchakamchaka anha

13. Hakuna kuchoka

14. Mie niite super delegeto ama deiwaka

15. Nalicheza hili gemu nnavyotaka

16. Ni albam ya kumi lakini hasira kama ndo kwanza natoka

17. Maisha ni kama soka kusongana

18. Haitakiwi kuchoka kupambana

19. Na ndo maana kama Sumaye alisoma na utu uzima

20. Basi na mimi ntasoma

21. Najua maisha mazuri

22. Nakataa kurudi nyuma

23. Na maisha ni kujituma anha

Samwel anabainisha nyimbo nyingine zinazosawiri hilo kuwa ni “Moto Chini” na “Veto.”

Hata hivyo, Samwel anabainisha kwamba wakati ambapo katika ushairi simulizi vita

vilivyosawiriwa ni vita baina ya kabila na kabila, jamii moja na nyingine au koo na koo, katika ushairi

wa Bongo Fleva kwa kiasi kikubwa, vita vilivyosawiriwa ni vya mapambano dhidi ya maisha na

ushindani wa kimuziki. Vita katika ushairi wa Bongo Fleva havikuhusisha sana matumizi ya silaha

halisi bali vilikuwa ni vita vya maneno katika kushindania udhibiti wa soko la muziki. Hivyo, katika

ushairi wa Bongo Fleva, vita ni sitiari tu inayotumika kuashiria ushindani.

48

Kufanana kwingine kwa kimaudhui baina ya ushairi simulizi wa Kibantu na ushairi wa kisasa

kunakobainishwa na Samwel (2012a) kunaonekana katika maudhui yahusuyo utawala. Ushairi simulizi

wa Kibantu ulisawiri suala la utawala ambapo wasanii walijibainisha kwamba wao ndiyo viongozi

wanaowaongoza wengine na hawastahili kuongozwa. Samwel ananukuu ushairi wa Kisukuma

ulionukuliwa na Gunderson (2010:175) kama ifuatavyo:

1. Nkanda, ntaale wa Bazinza

2. Basukuma, tumanile

3. Lyene ihanga lya makangi

4. Baluganda lwa Bazinza

5. Hubataale ba Sukuma

1. Nkanda, mtemi wa Bazinza

2. Wasukuma, tunamjua

3. Kwa hakika ni nchi inayotisha

4. Koo za Bazinza

5. (Kwa hakika) ndio viongozi wa Wasukuma

Katika wimbo huu msanii anajibainisha kuwa ametoka katika ukoo wa Bazinza, ambao ni ukoo wa

viongozi bora wa kabila la Wasukuma. Hivyo, anajigamba kwamba ni kiongozi bora.

Maudhui haya ya utawala yanaonekana katika ushairi wa Bongo Fleva pia ambapo washairi

wanajibainisha kwamba wao ni viongozi wa wengine, tena ni viongozi bora. Samwel anatumia mfano

wa wimbo wa “Veto” ambapo Mr. 2 anajibainisha kwamba yeye ndiye rais (president) wa wanamuziki

wa Bongo Fleva na kwamba anatakiwa kutatua matatizo ya wanamuziki wa muziki huu.

(b) Kufanana kwa Maudhui ya Kiuchumi

Zaidi ya kufanana katika maudhui ya kisiasa, kuna kufanana vilevile katika maudhui ya

kiuchumi. Katika ushairi simulizi wa Kibantu tunaona wasanii wakijibainisha juu ya mafanikio katika

kazi. Walibainisha kwamba ni wakulima hodari, wafugaji wazuri na hata wawindaji wazuri. Samwel

(2012a) akimnukuu Songoyi (2005) anatoa mfano wa wimbo wa Kisukuma anaoutafsiri mstari 1-4

kama ifuatavyo:

Sisi ndio tunaozilima nyasi ngumu

Wakulima wa mtama

Wapaliliaji wa palizi

Kwa viwango vya Nyerere.

Katika mistari hii tunaona wazi kwamba msanii anaeleza kwamba wao ndio wakulima wa nyasi ngumu.

Anaendelea kueleza kwamba wao ndio wakulima maarufu wa mtama na wapaliliaji wa mashamba na

kwamba wanalima kwa viwango vya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Huu ni

ushairi wa kazi ya kilimo.

Ushairi wa kazi unaonekana pia katika ushairi wa Bongo Fleva. Samwel anatoa mifano ya

wimbo wa “Mchakamchaka” ambapo Mr 2 (Joseph Mbilinyi) anaelezea juu ya kazi yake kwamba

ndiyo inamjengea heshima (CV) katika jamii na inamwingizia fedha nyingi. Kazi anayojigamba kwayo

ni kazi ya uimbaji kama inavyobainika hapa chini:

1. Anha baada ya dhiki faraja

2. Nimeamini mambo mema

3. Ni kwa yule anayengoja

4. Na wa mbili havai moja anha anha

5. Sasa ni mwendo wa dolali4

6. Ndani ya akaunti mtoni utadhani mtoto wa Balali

7. Sema vijisenti vyangu ni vya halali

8. Bongo mchaka mchaka tu

9. Mafisadi hawalali

10. Nina uhuru wa kusema

11. Na nitasema chochote ntakachoona kinafaa mimi kusema

12. Na nnakuja na falsafa za Obama

13. Tunatakiwa kuchange

14. Tusipochange maisha bora kwetu ndoto kama muafaka wa Zenji anha

15. Wacha niendeleze dozi

16. Maana leo kama balozi

17. Kama kazi ni kazi hakuna ubitozi

18. Na ni upuuzi kusema gemu haliuzi

19. Wakati we unangoja kuuza tepu tu na CD

4 Dolali ni msimu unaotumika kumaanisha dola (za Kimarekani).

49

20. Sisi tunauza mpaka jezi

21. Ni kwa sababu tuna CV

22. Na huu ndo mchakamchaka tunaoutaka

23. Na anha anha hakuna kuchoka

Ushairi huu wa kazi ya uimbaji unaonekana pia katika ushairi simulizi wa Kibantu kama anavyonukuu

wimbo wa Kisukuma kutoka kwa Songoyi (2005) katika mstari wa 1-2 na wa 5-6 anapoutafsiri kama

ifuatavyo:

Ninapokuwa katika uwanja wa ngoma

Mimi ni chifu…

Kwa haya yote nimejiimarisha

Na wachawi

Wamenifanya mkuu.

Katika dondoo hili msanii anaeleza kwamba anapokuwa katika uwanja wa ngoma huimba vizuri kuliko

wengine wote; anaposema yeye ni chifu ana maana kuwa anawaongoza waimbaji wengine. Hapa

tunaona wazi kwamba, maudhui ya ushairi simulizi wa Kibantu na ushairi wa Kiswahili yanafanana.

(c) Kufanana kwa Maudhui ya Kijamii

Vilevile ushairi simulizi wa Kibantu na ushairi wa Kiswahili, na hasa ule wa Bongo Fleva,

unafanana katika maudhui ya kijamii. Tunaona katika ushairi simulizi wa Kibantu kuna ushairi

unaoelezea koo ambapo mtu alielezea ukoo wake. Aidha, washairi katika ushairi huo wa koo walielezea

miji na vijiji walikotoka na kuvinasibisha na mafanikio waliyonayo. Samwel anatoa mfano wa shairi la

majigambo ya Fransisco Lwihula, anayeelezea kuwa ni wa kutoka Kanazi ya Bukiza na kwamba ni wa

ukoo wa Kayango aliyezaliwa na Byorugano anayetokea Kola Omwinoni Onabe. Vilevile msanii

anaelezea vijiji anavyohusiana navyo kama vile Kyanyonyi Kyamwiiga na Kafunjo Kamugoro kama

inavyobainika hapa chini:

1. Naimuka aansi ndi Franscisko eya Lwihula

2. Omuli Kanazi ka Bukiza

3. Naimuka ndi musinjaigulu amuzio rugeju

4. Ndi wa Kayango

5. Ndi wa Byorugana

6. Ndi wa Kola Omwinoni Onabe

7. Ndi wa Kyanyonyi Kyamwigwa

8. Ndi wa Kafunjo Kamugoro

9. Eibanga ntemba Kasiko elipango

10. Ninyija ninzarwamu ta Balingililaki eya Tiinaba

11. Okwo mawe narugayo

1. Nainuka ni miye Fransisko, mtoto wa Lwihula

2. Wa kutoka Kanazi ya Bukiza

3. Nainuka kama shujaa wa mashujaa

4. Ni wa ukoo wa Kayango,

5. Ni wa ukoo wa Byorugana

6. Ni wa kutoka Kola Omwinoni Onabe5,

7. Ni wa kutoka Kyanyonyi Kyamwigwa

8. Ni wa kutoka Kafunjo Kamugoro

9. Hupanda mlima mrefu wa Kasiko

10. Kule nazaliwa na Mzee Balingililaki, mtoto wa Tiinaba.

11. Huo ni ukoo wa mama

Chanzo: Rubanza (1994): (Tafsiri na msisitizo wetu)

Ushairi huo wa koo hautofautiani na ule unaoonekana ushairi wa kisasa wa Bongo Fleva hasa katika

wimbo wa Dogo Janja uitwao “Mtoto wa Uswazi” au wa Prof. Jay (Joseph Haule) uitwao “Ndiyo

Mzee.” Katika ule wa Dogo Janja, msanii anajitambulisha kuwa anaitwa Dogo Janja anayetokea katika

mji wa Arusha (A-Town) ambapo katika wimbo wa Prof. Jay anajitambulisha kuwa anaitwa Joseph

Haule mtoto wa Msolopagazi anayetokea katika nchi iliyopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

MTOTO WA USWAZI wa Dogo Janja Ft Godzilla

KIbwagizo

My name is Dogo Janja a.k.a Forty Seven

A town soldier

Stick to books not drugs

Ubeti wa 1

1. Jua lilipotoka ndo nikawa nimezaliwa

2. Wala sikuwa na nguo nikadhani nimevuliwa

3. Nimezaliwa huko kwenye baridi kali

4. Arusha Tanzania hakuna jua kali

5. Hospitali Mount Meru ndipo nilitokea

6. Thanks mummy and thanx daddy

7. Kila siku nawaombea

5 Kola omwinoni onabe maana yake ni “shika kwenye tope unawe.”

50

8. Muishi pamoja mimi nimewazoea...

9. Muziki nimechagua coz ndo kipaji changu

10. Arusha nitarudi nipo Dar ninatafuta...

11. Waambie walionuna kwamba washachelewa

12. Wape hi Arusha waambie nitakuja

13. Nimekuja kutake over hawa washachuja

14. Hongera mama kwa kunizaa kidume

15. Maisha ya hapo home yananifanya nijitume

16. Najitahidi kwenye mgongo nijikune

17. Na hii ndio sababu ukanizaa mwanamume

NDIYO MZEE wa Prof. Jay

1. Ok ok naitwa Joseph Haule mwana Msolopazi

2. Nadhani nimeletwa kuokoa hiki kizazi

3. Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu

4. Nimeletwa kwenu waungwana niwapunguzie machungu

5. Mimi ni mteule Kusini mwa jangwa la Sahara

6. Ndio maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala

7. Nina hekima kuliko mfalme Sulemani msiwe na wasi

8. Na hii nitadhihirisha pindi mtakaponipa nafasi

9. Actually, nimedhamiria kuwasaidia

10. Taifa lenye nguvu duniani liwe Tanzania

Chanzo: Profesa Jay (2001), Machozi, Jasho na Damu

Katika aina zote mbili za ushairi, ushairi simulizi wa Kibantu na ule wa Kiswahili, wasanii

wananasibisha mafanikio yao na koo zao na mahali walikotoka.

(d) Kufanana kwa Maudhui ya Kiutamaduni

Kufanana kwingine baina ya ushairi simulizi wa Kibantu na ushairi wa Kiswahili upo katika maudhui

ya kiutamaduni. Katika ushairi simulizi kuna suala la imani juu ya kuwapo kwa Mungu. Wasanii wa

ushairi huu, huelezea kwamba wana mafanikio makubwa kwa kuwa wanapendwa na Mungu. Samwel

anatumia mfano wa jigambo liitwalo “Okwebuga kwa Mugasha” (Kujigamba kwa Mugasha)

kubainisha hili:

1. Nayebuga ndi kijuikanila-nda

2. Ky’omwa Lwamula ilembo,

3. Entale Lubologa nsindila omumalungu

4. Ngutula enyama ndaliila

5. Manya bakama bazo tibaija Kyamuyanje

6. Mba kishuma kyo’ Mugasha yahaile

7. Ekiyo mbanda kabugu, Lubaga

8. Nyitila enfulu abutumbi

9. Mba kyegile;

10. Mba lulabyo, ndabiza kabwela

11. Omubanyanga ilala itakamile

12. Abayebembeile nkaita

13. Abasigaile enyuma echuchu

14. Yabaigala amaisho

15. Nikwo kyunyeta eibala lya Tibandekile Lwabukaya

1. Najigamba Kijuikanila-nda

2. Kwa Lwamula ilembo6

3. Simba mkali angurumaye mwituni

4. Hukatakata nyama na kuila

5. Najua wenyewe hawaji Kyamuyanje

6. Mimi ni jizi aliyepewa kisu kikali na Mugasha,7

7. Kisu kitumikacho kuchinja

8. Huulia samaki kilindini

9. Mimi ni mtu asiyeogopa chochote

10. Mimi ni radi, humulika kabwela

11. Kwa wachezaji ngoma

12. Ng’ombe hulala bila kukamuliwa

13. Waliotangulia niliwaua

14. Waliobaki nyuma vumbi liliwaziba macho

15. Ndipo waliponibatiza jina la Tibandekile

Lwabukaya

Chanzo: Rubanza (1994:58-62)

Katika jigambo hili tunaona mshairi akielezea kwamba amefanikiwa kwa kuwa alisaidiwa (alipewa

kisu kikali) na muungu (aitwaye Mugasha). Ushairi wa aina hii, unaonekana katika ushairi wa kisasa

wa Kiswahili ambapo wasanii wanahusisha mafanikio yao na Mungu. Tunaliona hili katika wimbo wa

Bongo Fleva wa Sister P (Happiness Thadei) uitwao “Achana Nao” ambapo katika mstari wa pili wa

wimbo huo msanii anasema “kipawa chatoka kwa Mola wala sijatumia ubani.” Msanii anaamini

mafanikio aliyonayo katika kazi yake ya uimbaji yanatokana na kipawa alichopewa na Mungu kama

inavyobainika hapa chini:

6 Lwamula ilembo ni usemi wa Kihaya ambao unamaanisha mleta baraka

7 Mugasha ni muungu wa Wahaya anayehusika na ziwa. Katika jamii za Wasukuma huitwa Ngassa.

51

1.Nafungua ubongo natoa fikra za utumwa kichwani

2.Kipawa chatoka kwa mola wala sijatumia ubani

3. Sister P kupata chati watu wanadhani rap utani

4. Rap biashara bwana ila angalia usijepata hasara

5.Kuuza vitumbua, pipi maandazi zote biashara

6.Usidharau hizo biashara watu watakuangushia msala.

7.Wasomi wengi wamesoma kwa kutumia hizo biashara

8.Mashairi sibahatishi na nitauza nyingi nakala

9.Na siyo utani nyota kwangu imeonekana biashara

10.Wandago rafiki zangu tena wa kina

11.We uliza maswali mengi majibu mimi sina

12.Nakupa rap shule mashairi yangu yana vina

Vilevile kwa kutambua kuwapo kwa Mungu na uwezo alionao, wasanii katika ushairi simulizi

walijieleza kwamba wao ni wachamungu na washika dini. Wanaeleza kuwa wanatenda mema ili

kumfurahisha Mungu azidi kuwafanikisha. Samwel anatoa mfano wa wimbo wa “Mba Ilungu

Lyobuamila” (Mwito wa Wahamiaji):

1. Naimuka ndi Shelestini

2. Nikwo ichumu ly’obugingo

3. Ndi kalamulila

4. Nindamulila abo nkalala nabo

5. Omukambi ya tata

6. Aikwimka ati munyampara

7. Ii ati mwami

8. Nyowe ntumile, nzagira

9. Ekitebe kilio, omukeka guli ao

10. Enyomyo eyo tata yansigiile empango eliwo

11. Buli muntu nimuwa ekitinwakye

12. Nkokwo nkukiya tata na mae

13. Nti Katonda mbeela

14. Ayandesile abukama

15. Mungu amwebembele

1. Naingia ndimi Selestini

2. Mimi ni mkuki wenye ncha kali

3. Mimi ni msuluhishi

4. Husuluhisha ninaoishi nao

5. Katika kambi ya baba

6. Anayeamka huniita kiongozi

7. Ii asema mwami (mtemi)

8. Mimi nimejivimbisha kwenye kiti

9. Kiti kipo, mkeka upo

10. Nguzo kubwa niliyorithishwa na baba ipo

11. Kila mtu ninampa heshima yake

12. Kama ninavyomuheshimu baba na mama

13. Nasema kuwa Mungu nibariki

14. Aliyenisogeza mbele ya utemi

15. Mungu amwongoze

Chanzo: Rubanza (1994:50-52)

Ushairi wa aina hii wa kujisifia juu ya kutenda mema unaonekana pia katika ushairi wa Bongo Fleva.

Samwel anatoa mfano wa wimbo uitwao “Sisi Tulivyo” ulioimbwa na Sister P ambapo katika mstari wa

1 wa wimbo huo anasema “mimi nilivyo ni mchamungu kuliko ulivyo” na; katika mstari wa 6-7

anasema anapenda sana mambo ya Mungu na kwamba anatenda yote yaliyoandikwa katika biblia bila

kuchagua. Katika mistari mingine anabainisha jinsi alivyo mtenda mema na kwamba anawaheshimu

watu wote hata maadui zake na pia anapenda amani kama inavyobainika hapa chini:

1. Mimi nilivyo ni mchamungu kuliko ulivyo

2. Mimi nilivyo siyo bitozi wa kupenda sana mademu

3. Mimi nilivyo sina habari na adui asemavyo

4. Mimi nilivyo sasa ni peace hakuna uadui

5. Wote rafiki awe msichana awe mvulana

6. Mimi nilivyo napenda sana mambo ya Mungu

7. Sichagui kama inavyosema Biblia

8. Mimi nilivyo sinywi pombe sivuti brother

Chanzo: Omari (2009:295)

II. Kufanana kwa Dhima

Zaidi ya kufanana kwa maudhui kwa ujumla, Samwel (2012a) anabainisha pia kufanana katika

kipengele cha dhima. Anabainisha kwamba aina zote mbili za ushairi zinaweza kuhifadhi historia ya

jamii husika, kukuza ushujaa, ujasiri na uzalendo, kuendeleza matabaka na kuhifadhi na kuendeleza

utamaduni. Kufanana kwingine kwa dhima ni kwamba, aina zote mbili za ushairi zinaadilisha na

kuadibisha na pia zinaburudisha.

Kwa kuanza na dhima ya kuhifadhi historia ya jamii Samwel anabainisha kuwa kuna kufanana

kwingi kidhima. Ushairi simulizi wa Kibantu unaweza kuhifadhi historia ya jamii kuhusu vita,

52

migogoro, maendeleo ya jamii na kadhalika. Anatoa mfano kuwa, ushairi wa vita huweza kusimulia

vita vilikuwa kati ya nani na nani, vilipiganwa wapi na lini na pia nani alishindwa katika vita hivyo.

Ushairi huo ulihifadhi historia ya vita hivyo kwa vizazi vijavyo ambavyo havikuvishuhudia. Vizazi

hivyo vilihabarishwa juu ya vita hivyo kupitia majigambo haya. Anatoa mfano wa ushairi wa aina hii

kutoka katika wimbo wa Kisukuma uitwao “Barugaruga” (Warugaruga) kama unavyonukuliwa hapa

chini:

1. Balugaruga! (x2)

2. Balugaruga! (x2)

3. Tulikapumula nanali kwihala? (x2)

4. Kwihala!

5. Bamashima mashima

6. Ooh, kwihala! (x2)

7. Twiyagalule!

1. Warugaruga (x2)

2. Warugaruga (x2)

3. Tunakwenda lini kulipua kwenye uwanja wa vita?

(x2)

4. Kwenye uwanja wa vita!

5. Sisi watu tunaoheshimika, heshimika

6. Ooh, uwanja wa vita (x2)

7. Tujimwage!

Katika wimbo huo, Warugaruga wanaelezwa kwamba ni mabingwa wa vita na kwamba

wanaheshimika kwa sababu ya ushindi wao vitani. Wimbo huo unatunza historia ya Tanzania kwani

askari hao wa Kirugaruga kweli walikuwapo na walitumiwa na watawala katika vita (Gunderson,

2010).

Ushairi wa Bongo Fleva nao unahifadhi historia ya jamii. Ushairi wa Bongo Fleva kama ulivyo

simulizi wa Kibantu unahifadhi matukio mbalimbali. Katika wimbo wa “Veto” ulioimbwa na Mr. 2

mwanajamii anahabarishwa juu ya ufisadi mkubwa ulioibuka Tanzania miaka ya 2000. Kwa mfano

tunaona katika wimbo huo msanii anataja ufisadi wa EPA ambapo fedha zinazofikia bilioni 133

ziliibwa kutoka katika akaunti ya madeni ya nje. Hili linabainika katika mistari ifuatayo ya wimbo huo:

1. Mi ndo president wa kitambo nishaapa

2. Matatizo ya hili gemu katu siwezi kwepa

3. Kama serikali inavyokwepa ishu ya EPA

4. Hatuogopi kukipaka

5. Hatujali tunachojali ni kuzibana ukweli

Chanzo: Mr. 2 (2009), Veto

Kufanana kwingine katika dhima za ushairi kunaonekana katika dhima ya kukuza ushujaa,

ujasiri na uzalendo. Samwel anabainisha kwamba aina zote mbili za ushairi, zina dhima ya kukuza

ushujaa, ujasiri na uzalendo. Anatoa mfano kuwa katika ushairi wa majigambo ya jadi mjigambi

aliporudi kutoka vitani au katika uwindaji alijigamba na kupewa zawadi mbalimbali zikiwamo

mashamba, mke na mifugo. Waoga walipewa kinyesi wakawape wake zao. Kutokana na hili, wanajamii

wengine walitamani kwenda vitani ili watakaporudi wajigambe. Aidha, wake nao walikuwa

wakiwahimiza waume zao kuwa jasiri ili wasijeleta nyumbani kinyesi. Ushujaa, ujasiri na uzalendo

ulisawiriwa na kusisitizwa pia katika maudhui ya majigambo yenyewe. Ushairi huo ulikidhihaki kifo na

kukifanya kionekane si kitu cha kutisha, kiliudhihaki woga na kuhimiza moyo wa ushujaa.

Aidha, katika dhima ya kuendeleza matabaka ushairi simulizi wa Kibantu na ushairi wa

Kiswahili (Bongo Fleva) unaonekana kufanana. Hii ni kusema kwamba aina zote mbili za ushairi

zinakuza na kuendeleza matabaka katika jamii. Samwel anaeleza kwamba katika ushairi simulizi wa

Kibantu, msanii alikusudia kuonyesha utii kwa watawala waliopo. Ndio maana katika ushairi wa

majigambo tendo la mwisho lilikuwa ni kujikabidhi au kukabidhi mateka kwa mtemi au mkuu wa ukoo.

Hali hii pia inaonekana katika ushairi wa Bongo Fleva ambapo wasanii wake hutumiwa katika kampeni

mbalimbali za urais. Wasanii hawa hulazimika kuwapigia debe wagombea husika bila kujali kufaa na

kukubalika kwao kwa jamii. Kwa kufanya hivyo, majigambo ya Bongo Fleva, kama yalivyo ya jadi,

yanakuza na kuendeleza matabaka.

Kufanana kwingine katika dhima za ushairi kwa jamii ni kwamba aina zote mbili zinaweza

kuhifadhi na kuendeleza utamaduni. Ushairi simulizi wa Kibantu huweza kubeba masuala mbalimbali

ya mila na desturi na umuhimu wake na hivyo kuendeleza mila hizo. Mila kama kufanya zindiko, ibada

ya mizimu na umuhimu wake na mila nyinginezo huweza kusawiriwa katika ushairi simulizi wa

Kibantu. Kwa kufanya hivyo, jamii huweza kukumbushwa juu ya mila zao na jinsi zilivyozisaidia jamii

za jadi. Jambo hili linaweza kuziendeleza mila hizo.

53

Kufanana kwa mwisho kwa dhima baina ya ushairi simulizi wa Kibantu na ushairi wa Kiswahili

na hasa wa Bongo Fleva kupo katika dhima za kuadilisha, kuadibisha na kuburudisha. Samwel

anaendelea kudai kuwa aina zote mbili za ushairi zinatoa maadili, zinatia adabu na pia kumpa mtu

burudani. Anaeleza kuwa katika ushairi simulizi wa Kibantu wanajamii huhimizwa mambo kama

kuwaheshimu wakubwa, kuwaheshimu watawala, kuwaheshimu wazazi na kadhalika. Inaonekana, kwa

mfano, katika ushairi huu msanii hulazimika kuyahusisha mafanikio yake na ukoo wake wa baba na

mama. Ushairi wa aina hii ulikusudia kuadibisha wanajamii kuwaheshimu wazazi. Aidha, inaonekana

kuwa ushairi wa aina hii uliimbwa wakati watu wanaenda vitani au wakati wa vita ili kujiliwaza na

kujipa burudani na kadhalika. Samwel anahitimisha kuwa hali kama hiyo ndiyo iliyoonekana katika

ushairi wa Bongo Fleva ambapo wasanii huwaadilisha, kuwaadibisha na kutoa burudani. Hivyo, hakuna

shaka kwamba aina hizi mbili za ushairi zinafanana sana.

III. Kufanana Kifani

Mbali na kufanana kimaudhui, Samwel (2012a) anabainisha kwamba ushairi simulizi wa

Kibantu na ushairi wa Kiswahili unafanana pia kifani. Kufanana kifani kunaonekana katika utungaji wa

ushairi huo, utendaji, muundo, mtindo, matumizi ya lugha na kadhalika.

(a) Kufanana katika Utungaji

Kwa kuanza na suala la utungaji, Samwel anaeleza kuwa ushairi simulizi wa Kibantu na ule wa

Bongo Fleva, unafanana sana. Aina zote mbili za ushairi ziliweza kutungwa papo kwa papo, bila

kukaririwa wala kuandikwa (Hodza na Fortune, 1979; Mulokozi, 1996; Peek na Kwesi, 2004) na pia

ziliweza kutungwa, kukaririwa na hata kufanyiwa mazoezi kabla ya utendaji wake. Sifa hizi, zinafanana

sana na ushairi wa Bongo Fleva. Kuhusu utungaji wa papo kwa papo wa ushairi wa Bongo Fleva,

wasanii huweza kutunga papo kwa papo wakati wa utendaji. Samwel anaeleza kuwa utungaji huu

unaitwa mtindo huru. Kwa upande wa utungaji wa kabla ya utendaji katika ushairi huu, huchukua

muda. Katika utungaji huu, msanii hukaa na kufikiria jinsi anavyoweza kuliwasilisha wazo alilonalo

kichwani. Muda unaotumika hutegemeana na kipaji cha utunzi alichonacho msanii. Aidha, katika

utungaji huu mtu anaweza kutunga mwenyewe wimbo au kutungiwa na mtu mwingine. Sifa hii, ipo pia

katika ushairi wa Bongo Fleva ambapo msanii huweza kutungiwa na kisha yeye kuyaghani au

kuyaimba. Katika ushairi wa Kiswahili wa kisasa, kuna watu ambao kazi yao ni kutunga mashairi na

kuwauzia wasanii wa Bongo Fleva pamoja na hakimiliki yake. Vilevile wapo wasanii wa Bongo Fleva

ambao kutokana na vipaji walivyonavyo wanawatungia wasanii wengine na kuwapa kutokana na

mahusiano waliyonayo.

(b) Kufanana katika Utendaji

Kipengele cha utendaji kinahusisha fanani (mtendaji) na hadhira (msikilizaji/mshiriki).

Vipengele vingine ni pamoja na mavazi yanayovaliwa katika utendaji wa majigambo pamoja na vifaa,

malipo/zawadi zinazoambatana na utendaji huo, uchezaji na sauti inayotumika katika utendaji wa

majigambo. Samwel (2012a) anabainisha kuwa kuna kufanana kwingi baina ya ushairi simulizi wa

Kibantu na wa Bongo Fleva katika vipengele hivyo vya utendaji.

(i) kufanana kwa Fanani

Fanani ni kipengele cha kwanza kitakachochambuliwa katika kufanana kwa utendaji wa ushairi.

Ushairi simulizi na wa Bongo Fleva unafanana sana katika utendaji na hasa fanani wake. Katika ushairi

simulizi wa Kibantu kuna tanzu za wanawake (sifo), tanzu za wanaume (majigambo) na kadhalika

(Rubanza, 1994; Mulokozi, 1996; Peek na Kwesi, 2004). Katika ushairi wa Kiswahili pia hali ni hiyo

hiyo. Ushairi wa Bongo Fleva, kwa mfano, unaonekana kuwa wa wanaume japo pia wapo wanawake

wachache. Mwanamke anayeimba muziki huu haraka sana huweza kuonekana katika jamii kuwa ni

muhuni.

Kufanana kwingine katika kipengele cha fanani kunatokana na ukweli kwamba ushairi simulizi

wa Kibantu na ule wa Bongo Fleva unaweza kuwa na fanani wa aina mbili: msanii mmoja na kikundi

cha wasanii. Hivyo, Samwel anasema kuwa utendaji wa ushairi kwa jumla, huweza kuwa wa aina

mbili, utendaji wa ushairi wa mtu mmoja mmoja na utendaji wa ushairi wa vikundi.

54

(ii) Kufanana kwa Hadhira

Tukiachana na kipengele cha fanani Samwel anaelezea pia kuwa hadhira ya ushairi simulizi na

ushairi wa Kiswahili inafanana. Katika ushairi simulizi, hadhira ilikuwa ni shirikishi kwa kiasi

kikubwa. Vivyo hivyo hadhira ya ushairi wa kiswahili ni shirikishi. Hata hivyo, hadhira ya aina zote

mbili za ushairi inaweza isiwe shirikishi hasa pale unaporekodiwa kwa kutumia teknolojia mbalimbali

kama vile kanda za kaseti, sidii na kadhalika. Teknolojia hizi hazikutumiwa hapo awali ndio maana

wanafasihi wa awali walidai kwamba majigambo ya jadi ni utanzu simulizi si andishi (Mulokozi, 1996;

Peek na Kwesi, 2004).

(iii) Kufanana kwa Uchezaji

Ushairi simulizi wa Kibantu na ule wa Bongo Fleva unafanana pia katika suala la uchezaji.

Katika ushairi simulizi wa Kibantu, uchezaji ni suala muhimu sana. Katika ushairi wa Bongo Fleva pia,

uchezaji ni mojawapo ya nguzo za muziki huo (Omari, 2009). Aidha, uchezaji katika ushairi simulizi

wa jadi, unaenda sambamba na uigaji wa matendo mbalimbali yanayosimuliwa (Finnegan, 1970;

Mulokozi 1996, Peek na Kwesi 2004:358). Samwel alibaini kwamba, hata ushairi wa Bongo Fleva

unaenda sambamba na matendo ya mwili hasa matumizi ya vidole, mikono, kichwa na kadhalika. Hii

inathibitisha hoja ya msingi kwamba, matendo ni uti wa mgongo wa fasihi simulizi (Finnegan, 1970;

1977 na Mulokozi 1996). Philip na Kwesi (2004:357) wanaeleza kwamba “majigambo (kama ushairi

simulizi wa Kibantu) ni utanzu wa masimulizi na inapotokea ukawekwa katika maandishi, uhai wake

hupotea kutokana na ukweli kwamba matendo ambayo ni uti wa mgongo wa fasihi simulizi hupotea”

(Tafsiri na ufafanuzi wetu). Hali hiyo imeonekana pia katika ushairi wa Bongo Fleva ambapo ili kuuza

kazi zao, wasanii wa ushairi huu wametoa kanda za kaseti na sidii za kusikiliza (audio CD) ambazo

hazioneshi matendo. Ni wazi kwamba sayansi na teknolojia, zaidi ya faida zake, ina athari hasi kwa

maendeleo ya fasihi simulizi.

(iv) Kufanana kwa Sauti

Kufanana kwingine ni katika sauti. Katika ushairi simulizi wa Kibantu kuna tanzu ambazo

zilitumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uongeaji, yaani sauti ya kughani (Ndamugoba, 1987; Rubanza,

1994). Hata hivyo, ushairi simulizi uliojitokeza katika tanzu nyingine kama vile nyimbo za ngoma na

kadhalika, huimbwa (Songoyi, 2005; Gunderson, 2010). Ushairi wa Kiswahili kama unavyoonekana

katika Bongo Fleva pia unaonekana kughanwa na/au kuimbwa. Sauti ya kughani ndiyo ya awali kabisa,

uimbaji katika Bongo Fleva ni dhana iliyokuja hivi karibuni. Hapo awali, muziki unaobeba ushairi huu

(muziki wa Bongo Fleva) uliitwa muziki wa rap, yaani muziki wa kughani (Mwanjoka, 2011). Aidha,

kama ilivyo kwenye ushairi simulizi wa Kibantu ambapo kwa kiasi kikubwa wanawake hutumia sauti

ya kuimba huku wanaume wakighani (Ndamugoba, 1987; Mulokozi, 1996), katika ushairi wa Kiswahili

hasa unaojitokeza katika Bongo Fleva sauti ya kughani hutumiwa zaidi na wanaume kuliko

inavyotumiwa na wanawake. Samwel anamnukuu Suriano (2007:2) kuthibitisha hili anaposema

kwamba, “wanawake katika gemu (muziki wa Bongo Fleva), na hasa wanaoghani, ni wachache…”

(Tafsiri na Ufafanuzi wetu).

(v) Kufanana kwa Mavazi na Vifaa Vinavyotumika

Kufanana kwingine kifani baina ya ushairi simulizi na ushairi wa Kiswahili unaojitokeza katika

muziki wa kizazi kipya, ni matumizi ya ala, mavazi maalumu na vifaa mbalimbali. Rubanza (1994:3) na

Mulokozi (1996:83) wanabainisha kwamba ushairi simulizi wa jadi, na hasa wa kabila la Wahaya, ulienda

sambamba na ngoma zilizoitwa amakondere/omutoro na mavazi maalumu (maleba). Vifaa vingine

vilivyotumika ni pamoja na mikuki, miundu na mapanga. Vifaa vingine vilivyosaidia uwasilishaji wa

ushairi wa jadi ni ngoma, njuga, nanga na vifaa vingine vya jadi. Ala hizi hutofautiana kutoka jamii moja

hadi nyingine. Katika ushairi wa Kiswahili na hasa wa Bongo Fleva, pia suala la vifaa na mavazi maalumu

ni muhimu. Samwel anaeleza kwamba, ingawa kwa sasa hakuna vazi maalumu la ushairi wa Bongo Fleva,

hapo awali yalikuwepo. Aidha, ushairi wa Bongo Fleva nao unatumia vifaa mbalimbali kama gitaa, vinanda,

tumba na kadhalika. Vifaa kama ngoma, nanga, zeze na kadhalika vilivyotumiwa na jamii ya jadi havina

tofauti na vifaa vinavyotumiwa na jamii kwa sasa katika ushairi wa Bongo Fleva. Kwa mfano, gitaa halina

tofauti kubwa na nanga au zeze; pia ngoma hazina tofauti kubwa na tumba. Hivyo, tunaweza kusema

utofauti uliopo ni wa majina na umbile la vifaa, lakini vinatoa sauti zinazofanana. Huu ni uthibitisho

55

kwamba, aina hizi mbili za ushairi zinafanana sana isipokuwa kuna mabadiliko ya aina fulani yaliyotokea

katika utendaji wa majigambo ya jadi yaliyosababishwa na maendeleo ya kiteknolojia na hivyo kuibua aina

mpya ya majigambo, majigambo ya kisasa, yanayotumia vifaa vya kisasa.

(c) Kufanana kwa Mandhari

Kama ilivyo kwa vipengele vingine vilivyotangulia, kipengele cha mandhari pia kina kufanana

baina ya aina hizi mbili za ushairi. Aina zote mbili za ushairi hutendwa katika mandhari yenye watu

(hadhira). Vilevile aina zote mbili za ushairi huweza kutendwa katika kumbi mbalimbali.

(d) Kufanana kwa Wahusika na Mtindo

Vipengele vingine vya kufanana baina ya ushairi wa jadi na wa Bongo Fleva ni wahusika na

mtindo. Ushairi wa jadi na ule wa Bongo Fleva unaonekana kufanana katika vipengele vya wahusika na

mtindo pia. Kwa mfano, katika wahusika tunaona aina zote mbili za ushairi zinatumia wahusika

binadamu, wasio binadamu na hata viumbe wa ajabu. Kuhusu mtindo, tunaona aina zote mbili za

ushairi zina mitindo mbalimbali ukiwemo wa majibizano. Majibizano hayo katika aina zote mbili za

ushairi tunayaona kuanzia katika majina ya wasanii hadi katika ushairi wenyewe. Mfanano mwingine

wa mtindo unaonekana katika vipengele vifuatavyo:

· Kufanana kwa Lugha Inayotumika

Aina zote mbili za ushairi zinaonekana kufanana pia katika lugha inayotumika. Ushairi wa simulizi

hutumia lugha ya picha, ishara na tamathali nyinginezo za usemi (Guma 1967:1-11; Rubanza 1994:22;

Philip na Kwesi 2004:358). Picha na tamathali hizi ndizo zilizojenga mantiki na vielelezo. Tungo hizo

hupewa mapigo maalumu yanayofuatana na kasi ya sauti iendayo kwa mfululizo wa hari (kuonesha ari

na uwezo) ili usimuliaji wake uwe na mori na hamasa (Rubanza, 1994). Baadhi ya picha zenye

kufanana zinazotumika katika ushairi wa jadi na ule wa Bongo Fleva ni pamoja na silaha kama vile

mikuki, mishale na kadhalika; vifaa vya kilimo kama vile jembe; wanyama kama vile dubu, simba,

tembo na kadhalika; watawala wenye nguvu na kadhalika. Picha nyingine zinazotumika ni pamoja na

mawe, majabali na miamba. Mfano wa matumizi haya katika ushairi wa Bongo Fleva unaonekana pale

msanii Inspector Haroun anapojiita Jabali la Rap Katuni na Joh Makini, Mwamba wa Kaskazini.

Matumizi ya dhana ya jabali yanaonekana pia katika wimbo wa “MaDJ” wa Sister P katika mstari wa 3

wa wimbo huo msanii anasema “sasa nije kwa hasira kama vile jabali.”

Kwa upande wa ushairi wa jadi matumizi haya ya lugha ya picha tunayaona katika nyimbo

mbalimbali. Tunaona, kwa mfano, msanii Fransisco Lwihula katika wimbo wake anasema kwamba

anatoka katika miamba ya Ruguta. Dhana ya jabali, mwamba na jiwe inaonekana katika majigambo ya

jadi ya Kisukuma ambapo msanii aitwaye Peter Mlangwa anajiita Jiganga (yaani jiwe). Hapa tunaona

kuna mfanano mkubwa wa falsafa zinazobebwa katika sitiari. Wasanii wa aina zote mbili za ushairi

wanatambua ugumu wa jiwe, mwamba na jabali na ndio maana wanajinasibisha na vitu hiyo.

Kwa upande wa picha ya vifaa vya kazi kama vile jembe, tunaona pia picha hii inatumika katika

aina zote mbili za ushairi. Kwa mfano, katika ushairi wa jadi wa Kihaya msanii Marko Petro

anajifananisha na jembe. Katika mstari wa 5 wa wimbo wake anasema “natonya ndi kafuka mutema

nkeke” yaani “naingia jembe mfyeka magugu.” Ushairi wa Bongo Fleva pia unatumia ishara na picha

kama hii. Msanii Khalid Mohammed au TID anajiita pia Jembe. Naye marehemu Mr. Ebbo alijulikana

kama Jembe la Rap Asili.

Kufanana huku kunaonekana hata katika matumizi ya ishara ya majina ya kiutawala na kishujaa.

Samwel anatoa mfano wa msanii wa ushairi wa jadi wa Kisukuma aitwaye Gumha Mang’ondi

akijitambulisha kwamba yeye ni Kilomanyangaki yaani chifu (Songoyi, 1987:17). Aidha, katika ushairi

wa jadi wa Kisukuma ulionukuliwa na Samwel msanii anasema yeye ni chifu (mstari wa 1-2). Sitiari

hii ya uchifu inatumiwa sana na wasanii wa ushairi wa Bongo Fleva. Miongoni mwao ni pamoja na

Anselm Ngaiza anayetumia jina la majigambo Chifu Rumanyika na Abubakar Katwila anayejulikana

pia kama Q. Chief. Vilevile tunaona msanii wa ushairi wa jadi wa Kisukuma aitwaye Balele Ngoya

akijitambulisha kwa jina la kishujaa la Masahi-o-Mbuga yaani Mmasai wa mbuga. Jina hilo hilo la

Mmasai linatumiwa na msanii wa Bongo Fleva Abel Motika a.k.a Mr. Ebbo kujitambulisha. Picha

nyingine ya kishujaa inayotumiwa pande zote ni picha ya kamanda au jemedari.

56

Kufanana pia kunaonekana katika picha na ishara zinazohusiana na wanyama. Kwa mfano,

tunaona katika shairi la jadi la Kihaya linalonukuliwa na kufafanuliwa katika Rubanza (1994:4-5),

inaelezwa kwamba Mtemi Mutatembwa anafananishwa na Simba wa Mwiko. Picha hii ya simba

inaonekana kutumika pia katika ushairi wa Bongo Fleva ambapo Afande Sele anajitambulisha pia kwa

jina la majigambo Simba Mzee.

Si hivyo tu bali pia kuna kufanana katika tamathali zinazotumika. Kwa mfano, tunaona katika

ushairi wa jadi ulionukuliwa na Samwel, msanii anasema “ninaingia kama radi.” Tamathali hii

inatumika pia katika jigambo la jadi la Kihaya lililonukuliwa na Rubanza (1994:4-5) ambapo zaidi ya

kumfananisha Mtemi Mutatembwa na Simba wa Mwiko anamfananisha pia na Radi Kuu. Tamathali

kama hii inatumika katika ushairi wa Bongo Fleva. Katika wimbo wa MaDJ ulioimbwa na Sister P

tunaliona hili. Katika mstari wa 8 wa wimbo huo msanii anasema “sauti yangu inatambaa kwenye beat

kama radi.” Hii haina tofauti na sitiari “mimi ni radi humulika kabwela” inayobainishwa na Rubanza

(1994) kuwa imetumika katika majigambo ya Kihaya.

· Kufanana kwa Matumizi ya Mapigo, Vina na Mizani

Pia kufanana kwingine kupo katika mapigo na suala la urari wa vina na mizani. Ushairi wa jadi

umebainika kwamba haukufuata kanuni ya urari wa vina na mizani kama sifa yake kuu ingawa ulikuwa

na mapigo. Kwa upande wa ushairi wa Bongo Fleva, ingawa yapo mashairi yanayofuata kanuni ya urari

wa vina na mizani, ushairi wa Bongo Fleva, haulazimiki kufuata kanuni hii. Aidha, ushairi huu nao una

mapigo. Kwa hiyo, tunawasilisha hapa hoja kwamba madai ya walioitwa wanausasa katika mgogoro wa

ushairi kwamba si lazima shairi liwe na urari wa vina na mizani yalikuwa ya msingi kwani yalilenga

kuurejesha ushairi wa jadi wa Kiafrika uliokuwapo tangu enzi katika jamii za Kiafrika katika mifumo

mbalimbali, ukiwamo ushairi wa majigambo. Kwa kuwa ushairi simulizi wa Kibantu haukuwa na urari

wa vina na mizani, hakukuwa na sababu ya kung’ang’aniza kuwapo kwa vina na mizani katika mashairi

yetu.

Samwel (2012a) anahitimisha kwa kusema kwamba, ushairi wa jadi na wa Bongo Fleva, unafanana

sana kifani ingawa pia kuna tofauti ndogondogo. Kufanana huku kifani, na kimaudhui kunaonesha wazi

kwamba ushairi wa Bongo Fleva umejengwa juu ya msingi wa ushairi wa jadi. Kwa maneno mengine

tunaweza kusema, kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni,

utanzu wa ushairi ulilazimika kubadilika ili usipotee. Mabadiliko hayo ndiyo yakaibua ushairi wa

Kiswahili, ushairi unaojitokeza katika miziki mbalimbali ni mifano ya hiyo.

Aidha, anaendelea kudai kwamba kufanana huku ni uthibitisho kwamba wasanii wa ushairi wa

Kisasa wa Kiswahili wamechota mbinu za jadi (kutoka kwenye ushairi simulizi) na kuziingiza katika

ushairi wa kisasa wa Kiswahili. Peek na Kwesi (2004:358) wanaelezea uwezekano wa utanzu mmoja

kuazimwa na kutumiwa katika ushairi wa kisasa. Wanaeleza kwamba hiki si kitu kigeni kwani

kinaonekana katika nchi mbalimbali kama vile Zimbabwe ambapo nyimbo za kwaya za kudai uhuru za

miaka ya 1970 ziliazima na kutumia majigambo ya Nehanda, Kaguvi na Chiminuka ambao walikuwa

mashujaa wa kale. Sifa za mashujaa hao wakapewa wapigania uhuru wa Zimbabwe kama Mugabe,

Chitepo, Takawira na Nkomo. Rubanza (1994:22) akichangia jambo hili anasema:

Majigambo pia yanaweza kutumika katika senema na katika makundi ya maigizo. Vivyo hivyo, majigambo

yanaweza kutumika katika ushairi na riwaya. Matumizi haya yana kasoro zake…Kasoro hizo ni pamoja na

kukosa kuuona utendaji wa mjigambi na/au kundi lake. Kukosa ubora wa muziki unaoambatana na

ujigambi huo na pia kumnyima msikilizaji uwezo wa kushiriki kimatendo. Hata kati ya uchaguzi wa ama

majigambo kutoweka au kurekodiwa ni bora nusu shari kuliko shari kamili. Hivyo, ni vema kuyahifadhi

majigambo na kuyatumia kwa kila njia tutakayoweza.

Dondoo hili linatueleza tanzu zinazoweza kuazima utanzu wa majigambo (kama kielelezo cha ushairi

simulizi wa Kibantu) na kuutumia na pia madhara ya ushairi simulizi (majigambo) kutumika katika

tanzu hizo. Hata hivyo, dondoo hilo linahitimisha kwamba ni muhimu ushairi simulizi (majigambo)

kutumiwa katika tanzu nyingine. Tuhitimishe tu kwamba ushairi wa Kiswahili na ushairi simulizi wa

Kibantu vinahusiana sana na kwamba ushairi simulizi ndiyo umezaa ushairi wa Kiswahili.

57

SURA YA NNE

HISTORIA YA USHAIRI WA KISWAHILI

Ushairi wa Kiswahili una historia ndefu sana. Ushairi simulizi wa Waswahili unasemekana

kwamba ulikuwapo tangu lugha ya Kiswahili ilipoanza kutumika. Mulokozi na Sengo (1995:25)

wanakiri kwamba si rahisi kueleza ni lini hasa ushairi simulizi wa Waswahili ulianza. Kwa upande wa

ushairi andishi wa Kiswahili, ni vigumu pia kueleza ni lini hasa ulianza. Hali hii inatokana na sababu

kuu moja kwamba wataalamu mbalimbali wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya jambo hilo. Mulokozi

na Sengo (1995:25) wanabainisha kuwa wakati Knappert (1979:66) anadai ushairi andishi wa mwanzo

wa Kiswahili ni Hamziyya ulioandikwa mnamo mwaka 1652, Harries (1962:5) anadai ushairi wa

mwanzo wa Kiswahili ni Tambuka (Tabuka) ulioandikwa mwaka 1728. Hata hivyo, utafiti wa

Mulokozi na Sengo unabainisha kwamba huenda wote wawili (Knappert na Harries) wamekosea na

kuwa ushairi andishi wa mwanzo wa Kiswahili umekuwapo tangu wakati wa Fumo Liyongo ambaye

anaaminika kuishi mnamo karne ya 13 huko Pate katika pwani ya Kenya. Aidha, utafiti huo

unabainisha ushairi andishi wa mwanzo wa Kiswahili ni “Swifa kwa Mwana Manga” unajulikana pia

kama “Tumsifu Yanga” ambao unahusianishwa moja kwa moja na Fumo Liyongo. Ushairi huo

umebainika uliandikwa mwaka 1532 B.K. Hata hivyo, Mulokozi na Sengo wanakiri huenda nyaraka

nyingi zitagundulika baadaye ambazo zitatufanya tubaini kwamba ushairi andishi wa Kiswahili

umekuwapo hata kabla ya hapo. Katika andiko hili, tunachukulia kuwa ushairi wa mwanzo wa

Kiswahili ulianza kuandikwa pale tu taaluma ya maandishi ilipoingia.

Tangu kuibuka kwa ushairi wa mwanzo wa Kiswahili hadi sasa, ushairi huo umepitia historia

ndefu sana na vipindi tofauti tofauti vya kihistoria. Tunaweza kuvigawa vipindi hivyo katika makundi

makuu mawili: kipindi cha kabla na wakati wa ukoloni (ushairi wa Kiswahili kabla na wakati wa

ukoloni) na kipindi cha baada ya uhuru (ushairi wa Kiswahili baada ya uhuru). Kipindi cha kabla na

wakati wa ukoloni tunaweza pia kukigawa katika makundi madogomadogo manne. Kundi la kwanza ni

kipindi cha ujima; kundi la pili ni kipindi cha ustawi wa miji, utamaduni na tawala za Waswahili; kundi

la tatu ni kipindi cha utawala wa Wareno na upinzani wa wananchi dhidi yao na; kundi la mwisho ni

kipindi kilichoasisiwa na utawala wa Waarabu wa Omani na kumalizikia na utawala wa Kiingereza na

Kidachi.

Kipindi cha kwanza, kipindi cha ujima kilidumu tangu binadamu alipopata urazini na kutoka

kwenye uhayawani hadi kama mwaka 600. Kipindi cha pili, kipindi cha ustawi wa miji, kilidumu kwa

kama miaka 600 hivi (yaani kuanzia mwaka wa 900 – 1500 BK). Kipindi hiki kilimalizwa na utawala

wa Wareno. Kipindi cha tatu kilianza kwa utawala wa Wareno na hatimaye wananchi wakaanza

kuupinga utawala huo. Kipindi hiki kilikuwa kati ya mwaka 1500 – 1730. Kipindi hiki, kiliishia kwa

kutekwa kwa Ngome ya Yesu (Fort Jesus) na kuingia kwa utawala wa Waarabu wa Oman (kama

mwaka 1730) na kumalizika wakati wa maingilio ya wakoloni wa Kidachi (kama mwaka 1890 baada ya

mkataba wa Berlin na Heligoland) na hatimaye ukoloni wa Kiingereza (kama mwaka 1918, baada ya

Wajerumani kushindwa katika vita kuu vya kwanza vya dunia).

USHAIRI SIMULIZI WA KISWAHILI WAKATI WA UJIMA

Inadaiwa kwamba binadamu anatokana na sokwe na alipitia hatua mbalimbali hadi kufikia

kuwa mtu kamili (homo sapiens). Kipindi cha ujima kinaanza pale binadamu alipopata urazini na

kuanza kuishi kama mtu kamili baada ya kutoka katika katika hali hiyo ya usokwe. Katika hatua za

awali za kipindi cha ujima, binadamu waliishi kwa uwindaji na ukusanyaji wa matunda. Taratibu

binadamu alipiga hatua na kuanza kuyatawala mazingira yake na kuanza kufanya kazi mbalimbali

ikiwemo kazi ya kilimo katika kile kinachoitwa mapinduzi ya kilimo (Neolithic Revolution). Mapinduzi

haya ya kilimo yalisababisha maendeleo makubwa katika maisha ya binadamu na binadamu sasa

wakaanza kuishi pamoja.

Katika kipindi chote hiki cha ujima, mwanadamu alishaibua ushairi kama njia mojawapo ya

kujiliwaza wakati wa kufanya kazi. Hakuna ushahidi kuwa katika kipindi hiki kulikuwa na kazi

nyingine za fasihi bali ushahidi uliopo unaonesha kwamba hiki kilikuwa ni kipindi kilichotawaliwa na

nyimbo za kazi. Hivyo, ushairi wa kazi unachukuliwa kuwa ndiyo ushairi wa mwanzo kabisa (Senkoro,

1988) na pia fasihi ya mwanzo kabisa. Mwanadamu aliimba nyimbo mbalimbali wakati wa shughuli

mbalimbali alizozifanya. Jukumu la nyimbo hizi lilikuwa ni kumliwaza na kumsahaulisha machovu ya

58

kazi husika. Senkoro (1988:2) anasema kuwa ushairi huu wa awali, ambao ulijitokeza zaidi katika

nyimbo za kazi, uliathiri hisia za mwimbaji na kumsukuma kufanya kazi kwa dhati zaidi na

kumsahaulisha ugumu wa kazi ile. Anaendelea kueleza kwamba jukumu hili la nyimbo la kufanya kazi

ngumu na nzito ionekane kutokuwa na hatari yoyote, ndilo linaloonyesha nguvu ya ushairi; na hata

wataalamu wengine wameipa nguvu hii sifa ya UCHAWI na kusema kuwa ushairi umetokana na

uchawi.8 Nyimbo za kazi ziliendelea kudumu kwa muda mrefu na hadi sasa, ingawa kuna mabadiliko

makubwa katika utanzu wa ushairi, nyimbo za kazi (ushairi wa kazi) bado umeendelea kuwa sehemu

muhimu ya ushairi wa Kiswahili.

USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA KARNE YA 10 NA 16

Hiki kilikuwa kipindi cha ustawi wa miji, utamaduni na tawala za Waswahili. Kama tulivyoeleza hapo

awali (katika sura iliyopoita), ushairi wa Kiswahili unatokana na ushairi simulizi wa Kibantu. Ushairi huu

ulihusisha majigambo, tondozi, pembezaji, mbolezi, nyiso, chapuzo, na nyimbo nyinginezo kama vile nyimbo za

kazi na kadhalika. Mulokozi na Sengo (1995:75-76) wanabainisha kwamba kipindi hiki kilitawaliwa na tungo

zilizodaiwa kuwa za Fumo Liyongo. Kutokana na mapokeo tunaambiwa kwamba mshairi wa kale zaidi

anayefahamika ni Fumo Liyongo, ambaye inasemekana kuwa aliishi maeneo ya Shaka, Kipini na Pate huko

pwani ya Kenya katika karne ya 13 au kabla/baadaye. Hakuna hakika kama kweli Liyongo ndiye hasa mtunzi wa

tungo hizo, ila jambo la hakika ni kwamba nyingi zilimuhusu yeye mwenyewe. Iwapo Liyongo ndiye mtunzi,

yaelekea kuwa alitunga mashairi yake kwa ghibu bila kuandika. Tungo zake nyingi zilihifadhiwa kichwani hadi

zilipoandikwa katika miswada karne nyingi baadaye. Utungo wake wa kale zaidi uliotiwa katika maandishi

unaitwa “Swifa ya Mwana Manga” au “Kumsifu Yanga” (Mulokozi na Sengo, khj.; Mulokozi, 1996; Ridhiwani,

1996:22 – 32). Utungo huo unadaiwa kutungwa na Liyongo mwenyewe akimsifia mke wake na ulikuwa simulizi

hadi mwaka 937 H (sawa na mwaka 1531 BM) (Mulokozi, 1999). Kama tulivyoona hapo awali, kuna baadhi ya

wanazuoni, akiwemo Mulokozi na Sengo (1995), wanauchukulia huu kuwa ndiyo utungo wa kwanza wa ushairi

andishi wa Kiswahili.

Ingawa inaaminika kuwa Liyongo aliishi kabla ya karne ya 16, lakini tungo zinazomuhusu (zilizotungwa

na wengine) ambazo tunazo ziliandikwa mwanzoni mwa karne ya 19. Tungo hizo ni “Takhmisa ya Liyongo”

(Sayyid Abdallah bin Ali, kama mwaka 1800 BM) na “Utenzi wa Fumo Liyongo” (Muhamadi Kijumwa, 1913).

Hata hivyo, tungo hizi za baadaye, zilitokana na fasihi simulizi inayomhusu Liyongo na iliyotungwa zama za

Liyongo mwenyewe. Hivyo, kwa kiasi fulani kimaudhui na kihisia zinaakisi kipindi cha 900 – 1500 BK

tunachokizungumzia. Kwa hiyo, Utendi wa Fumo Liyongo ndiyo utenzi wa kale zaidi katika tenzi tatu za kale

(tenzi zingine mbili ni Utenzi wa Mwanakupona na Utenzi wa al-Inkishafi) ingawa umewekwa katika maandishi

karne ya ishirini (taz. Mulokozi (1999) Tenzi Tatu za Kale).

Tungo za Fumo Liyongo zinahusu ustawi wa miji ya pwani. Miji hiyo ni pamoja na Kilwa, Mombasa na

Pate. Miji hii ilisitawi kutokana na biashara ya Bahari ya Hindi (Indian Ocean Slave Trade) iliyoshamiri sana.

Utendi wa Fumo Liyongo, kwa mfano, unaelezea kusitawi kwa mji wa Pate alipoishi Liyongo. Utenzi huu

ulitungwa kutokana na hadithi za kimapokeo kuhusu Fumo Liyongo miongoni mwa Waswahili. Hata hivyo,

masimulizi ya maisha ya Liyongo kama yanavyotokea katika utendi huo si kamili, bali ni simulio mojawapo tu la

maisha yake. Masimulio mengine kama yanavyotokea katika nyimbo zake (zinazomuhusu) yameachwa (taz.

maelezo ya kina ya utenzi wa Fumo Liyongo katika Mulokozi, 1999:1-19).

MCHANGO WA WAARABU KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI

Waarabu ndiyo wageni wa mwanzo kuja katika upwa wa Afrika Mashariki. Hawa walikuja na kuanza

kufanya biashara na wenyeji wa upwa huo ikiwamo biashara ya watumwa. Waarabu pia walileta dini ya

Kiislamu ambayo ilianza kuwa maarufu na watu wakaacha dini yao ya jadi. Aidha, Waarabu walileta hati zao za

Kiarabu. Dini hii na hati za kiarabu, zilikuwa na athari kubwa katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili. Ndipo

hapa sasa hati za Kiarabu zikaanza kutumika kuhifadhi ushairi wa Kiswahili. Aidha, kwa kuwa watunzi wengi

wa mashairi walishabadili dini na kuwa waislamu, hata maudhui ya mashairi yao yalisawiri dini hii. Vilevile,

kutokana na hilo hata aya za Korani na dua za Kiislamu zikaanza kuingizwa katika ushairi wa Kiswahili. Sio

hivyo tu, bali pia hata muundo wa mashairi ya Kiarabu ukaanza kutumika katika mashairi ya Kiswahili. Ndipo

hapa sasa ushairi wenye urari wa vina na mizani ulipoingia. Kasida ni mfano wa ushairi wa kisasa wa Kiarabu

8 Senkoro (1988:11) anafafanua kuwa wazo hili la kuwa ushairi chanzo chake ni uchawi limeelezwa kwa kirefu na George

Thomson katika Studies in Ancient Greek Society: The pre-historic Aegean. Senkoro (khj.) anaendelea kufafanua kuwa

katika Kiswahili, wazo hilo limeendelezwa na K.K. Kahigi katika makala yake, “Ushairi (Mtazamo wa Kisayansi)” katika

Kiswahili, Tol. 411 (Machi 1975). Kwa maelezo ya kina kuhusu haya taz. Senkoro (1988) Ushairi: Nadharia, Tahakiki na

Mifano.

59

ambao una vina na mizani na pia umeanza kutumika hata katika ushairi unaoonekana katika muziki wa Bongo

Fleva ambao katika andiko hili tumechukulia kuwa ni sehemu ya ushairi wa kisasa wa Kiswahili. Aidha, kama

tulivyodokeza katika sura iliyopita tukimnukuu Mulokozi na Sengo (1995:87) hata istilahi kadhaa za kishairi

zilitokana na ujio wa Waarabu. Istilahi hizo ni pamoja na shairi, mizani, ubeti, tathlitha, tarbia na takhmisa.

USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA KARNE YA 17 NA 18

Baada ya kipindi cha ustawi wa miji kilichotokana na biashara baina ya wenyeji na Waarabu, kikaja

kipindi cha pili, kipindi cha uvamizi wa wakoloni wa Kireno. Hawa walikuja kutokana na safari zenye mafanikio

za Dkt. David Livingstone. Wareno walikuja wakiwa na lengo la kudhibiti biashara iliyokuwa inafanywa baina

ya Waswahili na Waarabu. Hivyo, ujio wao uliambatana na vita vya kudhibiti biashara hiyo na kupelekea miji

iliyositawi awali kuporomoka. Miji ya Kilwa, Mombasa na Pate ilipoteza udhibiti wa biashara ya Bahari ya

Hindi na hivyo ikaanza kuporomoka. Biashara hiyo ilichukuliwa na maharamia na wafanyabiashara wa Kireno

na pia ilididimia kutokana na kushambuliwa mara kwa mara na majeshi ya Kireno ambayo yaliwapora mali zao.

Kuporomoka huku kwa miji ndiko kunakosawiriwa katika Utenzi wa al-Inkishafi, utenzi ambao pamoja na

mambo mengine, unazungumzia kuporomoka kwa mji wa Pate (kwa maelezo ya kina ya utenzi huu na utenzi

wenyewe taz. Mulokozi, 1999:63 – 64, 69 -71).

Katika kipindi cha utawala wa Wareno, ushairi kwa kiasi kikubwa ulibaki kuwa simulizi uliokuwa katika

muundo wa nyimbo. Waswahili walitunga mashairi ya kisiasa yaliyowakashifu Wareno na kuibua moyo wa

ushujaa miongoni mwao ili kupambana nao na kuilinda miji yao ya pwani. Mulokozi na Sengo (1995:76)

wanabainisha kwamba kwa bahati mbaya ushairi mwingi simulizi wa kipindi hiki haukuhifadhiwa isipokuwa

vipande vichache kama kile cha Mzungu Migeli wanachokinukuu kama ifuatavyo:

Mzungu Migeli u mwongo

Mato yako yana chongo

Kwani kuwata mpango

Kwenda kibanga uwani?

Wimbo huu unaelezwa kuwahusu Wareno (ambao hapa wanapewa jina la Migeli) ili kuwaonya na vita

vitakavyofuata (Mulokozi, 1982:28 – 29; Mulokozi na Sengo, 1995:76).

Baada ya upinzani wa muda mrefu, hatimaye utawala wa Wareno ulipinduliwa na ndipo kikaanza kipindi

cha tatu, kipindi cha utawala wa Waarabu wa Omani. Katika kipindi hiki Uislamu na ushairi wao ulianza tena

kuwa maarufu na mashairi mengi ya kidini yaliandikwa. Kipindi hiki kilizua tungo nyingi za tendi za kidini

zilizorejelea katika historia ya kuasisiwa kwa Uislamu huko Arabia kama vile Mgeni bin Faqihi, Tabuka,

Hamziyya na Siri ‘lAsirari. Pia kipindi hiki kilishuhudia utendi wa kimawaidha wa Mwanakupona Binti

Mshamu (Utenzi wa Mwanakupona). (Kwa maelezo ya kina kuhusu Utenzi wa Mwanakupona na matini

yenyewe taz. Mulokozi, 1999:107 -109).

USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA KARNE YA 19

Kama tulivyodokeza hapo awali, hiki kilikuwa kipindi cha utawala wa Waarabu wa Omani. Waarabu

hawa walihamisha makao yao toka Omani kuja Afrika Mashariki ambako walifungua mashamba. Aidha, kipindi

hiki pia kilikuwa na uvamizi baina ya miji ya Waswahili ambapo kila mji ulitaka kuutawala mji mwingine.

Utawala wa Waarabu wa Omani ulihusisha pia biashara za watumwa, ufanyaji kazi kwa lazima na kadhalika, na

hivyo, Waswahili wakaanza kuuchukia. Kwa hiyo, upinzani dhidi ya Waarabu hawa ukaanza. Washairi nao

walitunga kazi kuupinga utawala huo wa Waarabu na pia kuhimiza ulinzi wa miji yao dhidi ya uvamizi wa

Waswahili wengine. Mfano mzuri wa mashairi ya wakati huo yanaonekana katika wimbo wa Wakilindi

ulionukuliwa na Mulokozi (1982:33) na Mulokozi na Sengo (1995:76-77). Wimbo huo tunaunukuu pia hapa:

Wakilindi si watu ni pundamilia

Walikuza nti yao kwa reale mia (waliuza nchi yao)

Mulokozi (1982:33) na Mulokozi na Sengo (1995) wanafafanua kwamba wimbo huu unadaiwa kuwa

ulikuwa unawakebehi watu wa Kilindini kwa kuwakaribisha Waarabu katika maeneo yao.

KUINGIA KWA UKOLONI NA ATHARI ZAKE KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI

Kufikia nusu ya pili ya karne ya kumi na tisa ukoloni ulikuwa umeshashika mizizi katika bara la

Afrika, maeneo ya Waswahili yakiwemo. Ukoloni huu unatajwa kusababishwa na maendeleo makubwa

ya viwanda yaliyotokea huko Ulaya kuanzia karne ya kumi na sita na hivyo kusababisha mahitaji

makubwa ya mali ghafi kwa ajili ya viwanda, mahitaji makubwa ya vibarua wa kufanya kazi

60

viwandani, ongezeko kubwa la idadi ya watu na mahitaji makubwa ya soko la kuuzia bidhaa

zilizozalishwa viwandani. Kutokana na hayo, watu kutoka bara Ulaya walikuja Afrika kutafuta mali

ghafi, vibarua, sehemu za kuishi ili kupunguza ongezeko la watu Ulaya na masoko kwa bidhaa zao.

Ukoloni huu ulipitia hatua mbalimbali. Hatua kubwa ya ukoloni ni ile iliyofikiwa baada ya mkataba wa

Berlin mwaka 1884-1885. Wakoloni waliotawala maeneo ya Waswahili ni pamoja na Waarabu,

Wareno, Wadachi na Waingereza. Kwa kuwa tumeshagusia kuingia kwa Waarabu na Wareno na athari

zao katika ushairi wa Kiswahili katika sehemu zilizotangulia, hapa tutajikita zaidi katika ukoloni wa

Wadachi na Waingereza.

1. UKOLONI WA WAJERUMANI/WADACHI

Wakoloni wa mwanzo wanaofahamika zaidi ni Wajerumani ambao wanaitwa pia Wadachi. Ujio wa

wakoloni ulienda sambamba na vita vya upinzani toka kwa Waswahili. Mulokozi na Sengo (1995:77)

wanabainisha kwamba miongoni mwa vita vya upinzani vya Waswahili ni pamoja na Vita vya Witu (1890-94)

vilivyoongozwa na Fumo Bakari na baadaye Fumo Omari; Vita vya Kismayu (1892); Vita vya Takaunga (1895 -

96) vilivyoongozwa na Mazrui na Sheikh Mbaruku Rashid na Mbarak Rashid na; Vita vya Abushiri (1888 –

1889). Aidha, Mulokozi na Sengo (khj.) na Mulokozi (1996) wanaeleza kuwa mashairi mengi yahusuyo vita hivi

hayajakusanywa bado isipokuwa Utenzi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mrima (Hemed Abdalla, 1960) na

Utenzi wa Vita vya Majimaji. Inaelezwa kuwa, Hemed Abdalla aliyetunga Utenzi wa Vita vya Wadachi

Kutamalaki Mrima alishiriki katika vita vya Abushiri vilivyozaa utenzi huo na utenzi wake unabainisha mtazamo

wa Waswahili juu ya vita hivyo. Zaidi ya vita vyote hivi, hatimaye ukoloni ulianza rasmi katika upwa wa Afrika

mashariki.

Ukoloni uliambatana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuanza kutumika kwa hati za Kirumi katika

mashairi, ufunguzi wa shule zilizowaelimisha watu kuhusu ushairi, kuanzishwa kwa magazeti yaliyokuwa na

safu maalumu za ushairi na kadhalika. Washairi wengi wa wakati huu ni wale waliopata elimu katika shule za

kikoloni na pia washairi wengi waliokuja kuwa maarufu kama vile Mathias Mnyampala na Shaaban Robert

waliibuka kupitia utunzi wa mashairi magazetini.

2. UKOLONI WA WAINGEREZA

Ukoloni wa Waingereza ulianza baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu vya kwanza vya

dunia na hivyo makoloni yake kugawanywa miongoni mwa mataifa yaliyoshinda vita. Moja ya mataifa

hayo ni Uingereza. Katika kipindi hiki shule ziliendelea kutoa elimu ya ushairi na pia magazeti

yaliongezeka (kulikuwa na magazeti kama vile Msimulizi, Pwani na Bara na Mambo Leo). Aidha, katika

kipindi hiki palishuhudiwa pia kupiga hatua katika taaluma ya uchapaji wa vitabu. Ushairi wa Kiswahili

ulipiga hatua kubwa katika kipindi hiki na ndipo sheria na kanuni za utunzi wa ushairi zilitungwa na

Amri Abedi mnamo mwaka1954 katika kitabu chake Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri.

Katika kitabu hicho, Amri Abedi anaona kuwa kuenea kwa vitabu na magazeti kumewafanya watu

wengi watake kutunga mashairi. Anadai kuwa mashairi mengi yanayotungwa, yametungwa bila ujuzi

wa kutosha, nayo yanaelekea kupunguza thamani ya mashairi ya Kiswahili mbele ya mashairi ya lugha

nyingine. Hivyo, anaona ni vema kueleza kanuni za kutunga mashairi ili kuwarejesha watungaji katika

mipaka inayotakiwa. Abedi anafasili shairi au utenzi kuwa ni wimbo. Kwa hiyo, kama shairi haliimbiki

halina maana. Pia anaelezea kuwa utenzi ni ushairi wenye mizani chache kuliko kumi na mbili (12),

ambao mara nyingi hauna vina vya kati katika mstari, bali kila ubeti una vina vya namna moja katika

mistari yake isipokuwa mstari wa mwisho katika kila ubeti ambao unaendelea na kina cha namna moja

kinachoitwa bahari. Anaendelea kudai kuwa utenzi wa mizani nane (8) huimbika vizuri. Lakini pia

inawezekana kuwa na tenzi zenye mizani kumi na moja (11) kama vile al- Inkishafi, na pia kuna zenye

mizani sita (6).

Katika andiko hilo, Amri Abedi anabainisha mambo makuu manne ambayo ni muhimu katika

ushairi wa Kiswahili. Mambo hayo ni vina, mizani, kituo na utoshelevu. Abedi anadai kwamba shairi la

Kiswahili halina budi kuwa na urari wa vina na mizani. Anasisitiza kwamba vina na mizani ndiyo uti

wa mgongo wa shairi lolote lile la Kiswahili. Zaidi ya urari wa vina na mizani, anasisitiza umuhimu wa

kituo ambacho anakieleza kuwa ni mstari wa mwisho wa kila ubeti. Huo huwa ama ni kiini cha habari

(haubadiliki) ama kimalizio (hubadilika). Kituo kinapokuwa kimalizio, basi kinabadilikabadilika

ambapo kina cha mwisho huenda kati na cha kati huenda mwisho na kadhalika. Jambo la mwisho

analolisisitiza ni utoshelevu ambapo anadai kwamba kila ubeti ujitosheleze kadiri iwezekanavyo: yaani

61

uwe na maana kamili na maana hiyo isingoje kukamilishwa na ubeti mwingine unaofuata. Mambo

mengine anayoyaeleza Amri Abedi ni kwamba:

i. Kazi iliyo ngumu katika kutunga shairi hasa kwa anayejifunza ni kupata vina vilivyo sawa na

vizuri, vitoavyo maana, vyenye maneno mbalimbali. Kina cha “ni” ni chepesi zaidi. Kupata vina

kwa haraka inabidi ujizoeze kusoma sana mashairi mazuri ya watu mbalimbali.

ii. Watunzi wa mashairi wasiige ovyo bali wakuze vipaji vyao kwa kuwa na shauku ya kutunga na

kusoma mashairi ya watu wengine.

iii. Tunga iwapo haja: tunga shairi kwa jambo linalokusakama sana ndipo mashairi yatapenya

moyo, la sivyo yatakuwa chapwa kama mchuzi wa jogoo.

iv. Tumia lugha nyepesi ukizungumzia mambo ya kawaida. Usitunge mambo ya kihuni bali yale

yawafaayo, yaelimishayo, yafikirishayo, yafurahishayo watu.

v. Tumia lugha ya kizamani (ya wazee) unapotaka kuzungumzia shairi zito la fikra, tumia methali

katika kituo na pia dokeza na mafumbo.

vi. Lugha inayotumiwa na wanawake pia ni safi; huchapusha shairi.

KUPATIKANA KWA UHURU NA HALI YA USHAIRI WA KISWAHILI

Katika wakati wote wa utawala wa wakoloni, Waswahili hawakuwa kimya, bali waliendeleza

mapambano yao ya kutaka kujikomboa na kurudisha heshima yao. Wapo waliotumia njia za amani,

wapo waliotumia vita na mbinu nyinginezo kadha wa kadha. Penye nia pana njia, hatimaye kuanzia

miaka ya 1960 nchi za Afrika Mashariki zikaanza kujipatia uhuru wake. Tanganyika ilipata uhuru wake

1961, Kenya 1962, Zanzibar 1964 na Uganda 1964. Katika kuelezea historia ya Kiswahili baada ya

uhuru, ni vema tukigawe kipindi hicho katika vipindi kadhaa vidogovidogo:

i). KIPINDI CHA UHURU NA AZIMIO LA ARUSHA

Kipindi hiki kinaanza mwaka 1961 na kuishia mwaka 1970. Katika kipindi hiki mashairi mengi

yalikuwa ya kushangilia uhuru na kuwapongeza wapigania uhuru kwa kazi nzito. Mashairi ya aina hiyo

yanaonekana katika mashairi marefu kama vile Utenzi wa Uhuru wa Tanganyika (1967) ulioandikwa na

Mwinyihatibu Mohamed Amiri; Utenzi wa Jamhuri ya Tanganyika (1967) ulioandikwa na Ramadhani

Mwaruka; Utenzi wa Uhuru wa Kenya (1972) ulioandikwa na Salim A. Kibao na Utenzi wa Jamhuri ya

Zanzibar.

Mwaka 1967 Azimio la Arusha lililoambatana na siasa ya ujamaa na kujitegemea lilitangazwa na

hivyo kuleta sura mpya ya ushairi wa Kiswahili. Mashairi ya kijamaa-yaliyosifia Azimio la Arusha na

siasa ya ujamaa na kujitegemea yaliibuka. Miongoni mwa mashairi hayo ni Mashairi ya Azimio la

Arusha (1971) yaliyohaririwa na Grant Kamenju na Farouk Topan. Pia fani/mtindo mpya wa ushairi wa

kimajibizano ulianzishwa ambao ulipewa jina ngonjera. Mfano mzuri wa ushairi huo wa kimajibizano

unaonekana katika Ngonjera za UKUTA za Mnyampala 1970. Ngonjera hizi zilitumiwa sana na

wanasiasa kueneza siasa ya ujamaa na kujitegemea. Hata hivyo, Mbaga katika makala yake iitwayo

“Ngonjera: Historia yake Simulizi hadi Andishi” iliyopo kwenye jarida la Kiswahili na. 67 anaeleza

kuwa fani hii ya ngonjera imekuwepo katika jamii mbalimbali hata kabla ya wakati huo. Dai hili la

Mbaga linathibitisha tu kuwa ushairi andishi wa Kiswahili unachimbuka katika ushairi simulizi wa

Kibantu uliokuwepo tangu kale. Hoja yetu hapa ni kuwa, hata kama ngonjera simulizi zimekuwepo kwa

muda mrefu ngonjera andishi zilianza kuonekana katika wakati huu. Ushairi mwingi wa wakati huu

ulikuwa wa kikasuku. Kasuku ni ndege mwenye tabia ya kuiga kila sauti anayoisikia bila kujua maana

yake na madhara yake. Hivyo, kusema mashairi ya kikasuku tunamaanisha kwamba mashairi

yaliyosifia kila jambo lililosemwa na wanasiasa bila kujiridhisha kufaa kwake.

ii). KIPINDI CHA VITA VYA KAGERA NA UGUMU WA MAISHA

Kipindi hiki kinaanzia mwishoni mwa miaka ya 1960 na kuendelea hadi mwaka 1980. Kipindi hiki

kilishuhudia mambo mengi ikiwa ni pamoja na vita kati ya mataifa ya Waswahili, Tanzania na Uganda,

vita vilivyojulikana kama vita vya Kagera. Kutokana na vita hivi, pakaibuka mashairi yaliyobeba dhana

hiyo ya vita vya Kagera. Mfano mzuri ni Utenzi wa Vita vya Kagera na Anguko la Idd Amini Dada

(1981) ulioandikwa na Henry Muhanika.

62

Katika kipindi hiki palianza kuibuka hali ya kukata tamaa miongoni mwa watu kutokana na

matamanio na matarajio yao baada ya uhuru kutotimizwa. Baada ya uhuru, watu waliamini kwamba

maisha yao yangekuwa mazuri zaidi na kungekuwa na neema zaidi lakini hali haikuwa hivyo. Hapa

ndipo ulipoibuka ushairi wa kihakiki ambao uliikosoa jamii. Ushairi wa kipindi hicho ulionesha hali

halisi ya jamii katika nyanja mbalimbali kama vile hali ya kisiasa, hususani hali ya uongozi mbaya,

ukiritimba, kujilimbikizia mali, uhujumu uchumi na kadhalika. Washairi pia walianza kutathmini upya

kuhusu Azimio la Arusha na siasa ya ujamaa na kujitegemea kama vilikuwa na maana yoyote. Hapa

ndipo palipoibuka mashairi kama Miaka Kumi Baada ya Azimio la Arusha (1977) yaliyohaririwa na

Abdilatif Abdalla. Mashairi hayo yanaonyesha jinsi hali ya kiuchumi na kijamii ilivyokuwa mbaya,

kwa mfano, yanaonyesha jinsi wananchi walivyokuwa wanapata tabu kupata mahitaji muhimu.

Mashairi mengine ya mkondo huu ni ya Kezilahabi (1974) Kichomi na (1988) Karibu Ndani; ya Kahigi

na Mulokozi (1976) Malenga wa Bara na ya Mohamed Seif Khatib (1988) Fungate ya Uhuru.

Waandishi hawa walipendekeza mbinu mbalimbali za kuondokana na matatizo hayo ikiwa ni

pamoja na kuwahimiza wananchi kuungana ili kutatua matatizo yao na kuchukua hatua. Aidha,

yalipendekeza pia viongozi kuwajibika ama kuwajibishwa ili kuepusha matatizo zaidi. Hali hiyo

inaonekana katika mashairi ya Fungate ya Uhuru (1988) na ya Mochiwa (1988) Mvumilivu Hula

Mbovu. Mochiwa anasisitiza kwamba huu si wakati wa wananchi kuwavumilia viongozi wasiofaa

maana mvumilivu hula mbovu. Kwa ujumla, watunzi hawa wanataka Ujenzi wa jamii mpya ambayo

itakuwa na haki, uchumi imara, jamii iliyojikomboa kiutamaduni, yenye watu wazalendo, yenye umoja,

usawa na utu na ambayo ina viongozi bora. Kwa mfano, Kezilahabi katika kitabu cha Karibu Ndani

shairi lake la kwanza kabisa liitwalo “Chai ya Jioni” anabainisha maovu haya ya viongozi. Katika shairi

hili tunaona kuwa mshairi anaonyesha jinsi viongozi wanavyojisahau wakiwa madarakani.

Anawakumbusha kuwa wanapoona mambo yanaenda wajue na muda wa uongozi wao unaisha pia.

Hivyo, anawaasa kuwa ni vema wahakikishe kuwa kabla hawajaondoka madarakani wanafanya mambo

yanayokubalika katika jamii. Mashairi mengine ya mkondo huu katika diwani hii ni pamoja na shairi la

pili kitabuni “Mkesha,” la tatu “Matumaini” na mengineyo mengi. Katika shairi la “Mkesha”

mwandishi anabainisha kwamba wakati watu wanateseka wakisubiri maendeleo viongozi wanaishi

maisha ya kifahari; katika shairi la “Matumaini” mwandishi anabainisha jinsi Waafrika waliokuwa na

matumaini makubwa wakati nchi zao zinapata uhuru kuwa viongozi wa Kiafrika watawaletea

maendeleo, walivyokata tamaa na kukosa matumaini kabisa. Kwa ujumla, mshairi huyu amesawiri sana

hali ya kukata tamaa iliyokuwepo wakati huo. Hata hivyo, izingatiwe kuwa mashairi haya yanaweza

kuchambuliwa kwa namna nyingine na kupewa dhamira nyingine. Kwa mfano, Senkoro anaona kuwa

shairi la “Chai ya Jioni” linahusu mapenzi na wala si siasa kama tunavyodai hapa. Mtazamo huu wa

Senkoro unatuonyesha kuwa kazi ya fasihi huweza kuhakikiwa kwa namna tofautitofauti na kubainika

kuwa na dhamira tofautitofauti kulingana na mhakiki.

Kwa upande wa mashairi yanayohimiza ukombozi wa kiutamaduni yanaonekana katika vitabu

mbalimbali. Kwa mfano, katika Diwani ya Akilimali (1963) cha Akilimali Snow-White na Ngonjera za

Ukuta cha Mathias Mnyampala (1970) mashairi ya aina hii ni mengi sana. Katika Diwani ya Akilimali

tunaona katika shairi la “Kila Mdharau Chake” ambapo msanii anasisitiza watu kudhathamini vya

kwao, ikiwa ni pamoja na utamaduni wao. Aidha, katika Ngonjera za Ukuta msanii ameweka safu

maalumu yenye mashairi yanayohusu elimu na utamaduni. Katika safu hii, ametunga mashairi mengi

ambayo yanahimiza ukombozi wa kiutamaduni. Miongoni mwa mashairi hayo ni pamoja na

“Utamaduni Kitu Gani ” na “Kiingereza Lugha Nzuri?” Katika shairi la “Utamaduni Kitu Gani”

msanii anaielimisha jamii juu ya dhana nzima ya utamaduni wa Kiafrika na kuwataka wauheshimu

utamaduni wao maana ni bora. Katika shairi la “Kiingereza Lugha Nzuri” msanii anahoji uzuri wa

lugha ya Kiingereza. Katika shairi hilo, anawakejeli wanajamii wanaoona kwamba kujua Kiingereza

ndiyo usomi na ujuzi wa mambo na kuwakumbusha kuwa Kiswahili ni lugha inayojitosheleza na lugha

ya usomi pia. Kwa kusema hivyo, msanii alikusudia kuikomboa jamii kutokana na ukoloni wa

kiutamaduni.

KUIBUKA KWA USHAIRI WA KISASA NA MABADILIKO KATIKA USHAIRI

Tumeshuhudia kuwa kumekuwa na mabadiliko katika maudhui ya ushairi wa Kiswahili katika kila

kipindi tulichokieleza. Mbali na mabadiliko hayo ya kimaudhui tuliyoyaeleza katika vipindi

63

mbalimbali, katika kipindi hiki pia palishuhudiwa mabadiliko ya kifani yaliyotokana na kuibuka kwa

ushairi wa kisasa. Mabadiliko haya ndiyo yanayoitwa majaribio katika ushairi. Majaribio yamekuwapo

katika tanzu mbalimbali za fasihi pia. Mabadiliko katika ushairi wa Kiswahili yalianza tangu mwishoni

mwa miaka ya 1960 lakini yakashika kasi sana na kuwa bayana zaidi katika kipindi hiki. Kufikia miaka

ya 1970 kulikuwa na majaribio ya wazi ya kutunga mashairi yasiyozingatia kanuni za awali

zilizopendekezwa na akina Amri Abedi. Mashairi haya yanaonekana kwa wingi katika kazi za E.

Kezilahabi, K. K. Kahigi na M. M. Mulokozi, D.P.B Massamba, S.A Mohamed, M.S. Khatibu,

Mochiwa, Kithaka wa Mberia, F.E.M.K. Senkoro na wengineo. Majaribio haya yalipingwa na washairi

wengine wa kijadi na hapo sasa kile kinachoitwa katika fasihi ya Kiswahili mgogoro wa ushairi

kikaibuka. Wanaujadi wanaojulikana zaidi ni Andanenga, M. Mnyampala, J. Mayoka, S. Robert, Amri

Abedi, Said Karama, Abdilatif Abdala, Ahmad Nassir, Chiraghdin na S. Kandoro. Wanaujadi

wakayaita mashairi ya kisasa kuwa masivina, mapingiti na majina mengine yasiyofaa wakiwa katika

harakati za kuyadhalilisha. Mgogoro huu unafafanuliwa kwa kina na Jumanne Mayoka katika kitabu

chake kiitwacho Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka.

DHANA YA MGOGORO WA USHAIRI NA HALI ILIVYOKUWA

Mgogoro ni hali ya kutokukubaliana au hali ya mvutano baina ya watu wawili au makundi

mawili ya watu. Tunapozungumzia mgogoro wa ushairi tunamaanisha ile hali ya kutokukubaliana na

mvutano baina ya makundi mawili ya washairi na wanafasihi juu ya dhana ya ushairi wa Kiswahili.

Makundi haya yaliyokuwa yanakinzana ni kundi la washairi wakongwe, wanamapokeo, na kundi la

washairi wapya, wanausasa. Wanamapokeo huitwa pia wana ujadi na wanausasa huitwa pia

wanamamboleo. Makundi haya mawili yalihusisha washairi wenyewe pamoja na wataalamu wengine

wa fasihi ambao si washairi. Kila kundi lilikuwa na mtazamo wake juu ya dhana ya ushairi na kuamini

kuwa mtazamo wao ni bora zaidi na hivyo kutokuwa tayari kukubali kubadilika au kuukubali mtazamo

wa kundi lingine.

Mgogoro huu ulijibainisha katika midahalo, vyombo vya habari, mashairi na hata katika

maandiko mengine yasiyokuwa ya kishairi. Kwa mfano, katika midahalo iliyofanyika katika

makongamano mbalimbali mikinzano baina ya makundi hayo ilibainika waziwazi. Mingi ya midahalo

hiyo iliitishwa na idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia kupitia vyombo vya habari

mikinzano hiyo ilijibainisha ambapo washairi hawa walibishana juu ya dhana hasa ya ushairi wa

Kiswahili. Mashairi mengi yaliyoandikwa katika vyombo vya habari vya wakati huo na hasa magazeti

yalikuwa na majibizano baina ya wafuasi wa makundi haya. Aidha, majibizano hayo yalionekana hata

katika mashairi waliyoyatunga vitabuni. Mfano mzuri wa mashairi ya aina hiyo tunayaona katika

Diwani ya Andanenga, Diwani ya Karibu Ndani, Diwani ya Amri miongoni mwa nyingi nyinginezo.

Diwani ya Karibu Ndani ina shairi linalobeba anwani ya diwani hiyo liitwalo “Karibu Ndani” ambalo

linasawiri mgogoro huo wa ushairi. Katika shairi hilo, Kezilahabi anawaeleza wanamapokeo kuwa

ushairi wao unafikia mwisho na aina mpya ya ushairi, ushairi wa kisasa, inashika hatamu. Hili

linabainika katika ubeti wa kwanza anaposema:

Washairi wa mapokeo, sasa wacheza lalasalama

Katika mionzi hafifu, ya jua machweoni

Na mahadhi yagaagaa, juu ya bahari ya utenzi

Yameshindwa chini kuzama, kwenye kina cha urazini

Nao wahenga vibandani, nje tena hawatoki

Hakuna tena ngoma, ya kugeeana kani

Na ushairi umehama, umerudi peponi

Lakini majani makavu, sasa hayatingishiki

Nayo madirisha ya nyumba, imara yamefungwa

Waliomo ndani wahofu, hasira ya mizimu

Aidha, katika ubeti wa mwisho wa shairi hilo, anaufananisha ushairi wa kimapokeo na kibanda

kikuukuu ambacho kinakaribia kuanguka. Hii ina maana kuwa, anauona ushairi huo kuwa umefikia

mwisho na aina mpya ya ushairi, ushairi wa kisasa, unaonekana kutawala. Tazama anasema katika ubeti

huu:

Ni kibanda kikuukuu, kuanguka kimekaribia

Mhimili wake mmoja, umeanza kukatika

64

Nao mchwa walialia, paa si paa tena

Karibu na huu mhimili, katikati ya kibanda

Kuna kigoda kikubwa, ngozi ya chui pambole

Mbele yake pana moto, vijinga vyake mifupa

Mbali na kujibizana kupitia mashairi kwenye diwani zao, walijibizana pia kupitia maandiko

mengine yasiyokuwa ya kishairi. Majibizano ya aina hii yalioneka pia katika tangulizi za vitabu vyao

vya mashairi. Kwa mfano, Abedi (1954) katika dibaji yake anawashambulia washairi wa kisasa na

kuwaeleza kuwa hawajui kutunga mashairi na wanashusha thamani ya ushairi wa Kiswahili. Abedi

anadai kuwa kuenea kwa vitabu (elimu) na magazeti ndicho chanzo cha kuingia kwa fani hiyo mpya,

mashairi ya kisasa, “isiyofaa.” Hebu turejee katika maneno yake anaposema:

Siku hizi kuenea kwa vitabu na magazeti kumewafanya watu wengi watake kutunga mashairi. Mengi mno

katika mashairi yanayotungwa, yametungwa bila ujuzi wa kutosha, nayo yaelekea kupunguza thamani ya

mashairi ya Kiswahili mbele ya mashairi ya lugha nyinginezo…

Chiraghdin (1980:1) naye anatoa maelezo yanayofanana na Abedi (1954). Yeye anasema kuwa

washairi wa kisasa wanauona ushairi kuwa ni mgumu na hivyo hawawezi kutunga mashairi.

Anaendelea kusema kuwa, kwa kuwa hawawezi kutunga mashairi, wanatunga vitu vingine na kudai ni

aina mpya ya ushairi. Kwa maelezo haya Chiraghdin anaonekana wazi hakubaliani na wanausasa na

anauona kuwa ushairi wao si ushairi wa Kiswahili bali wa Kizungu, hasa wa Kiingereza. Hivyo,

Chiraghdin kama ilivyokuwa kwa Abedi (1954) anaonekana kuulaumu ujio wa wakoloni wa Kiingereza

pamoja na elimu kuwa ndiyo chanzo cha “kuharibiwa” kwa ushairi wa Kiswahili. Tazama kwa maneno

yake anaposema:

Hii leo ushairi umekuwa ni taaluma iliyoenezwa tangu mashule hata vyuo vikuu. Lakini mpaka Leo

wanafunzi husikiwa wakilalamika kuwa somo hili ni gumu kwao. Tuseme labda hata hao waliofunzwa

Kiswahili wakakishikilia na kuendelea nacho mpaka daraja za utaalamu wa lugha hii na adabu yake,

wameuona ushairi wa Kiswahili kuwa ni mgumu mno hata wakaona ni heri waukimbie na wakajizibezibe

katika kwapa za kudai kuwa wanauendeleza ushairi huu katika mkondo mpya. Maana kuvyaza kwao si

zaidi ya kufuata vipengee vya Kizungu vya kutunga mashairi kwa njia za nathari, na hali humohumo katika

fasihi za Kizungu, Kiingereza mathalan….

Kwa ujumla, tuseme kuwa, washairi wa wakati huo walikuwa na mgogoro mkubwa kuhusiana

na dhana ya ushairi, ushairi wa Kiswahili ni upi hasa? Ili kupata mwangaza zaidi kuhusiana na mgogoro

huu ni vema tuchambue mawazo ya kila kundi:

MADAI YA WANAMAPOKEO NA WANAUSASA KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI

Dai la msingi la wanamapokeo ni kuwa urari wa vina na mizani ni roho na uti wa mgongo wa ushari

wa Kiswahili. Wengi kati ya wanamapokeo hawakiri kuwa kinachotungwa na wanausasa ni mashairi

(taz. Utangulizi wa Chiraghdin, 1980). Hawa wanauchukulia ushairi wa kisasa kuwa si ushairi bali ni

insha au nathari tu. Kwa upande wa wale wachache wanaokiri kuwa ni ushairi, wanauona kuwa ni

ushairi usio bora na ushairi wa kigeni. Wanauchukulia kuwa ni ushairi uliotokana na kuiga ushairi wa

Kiingereza (taz. Dibaji ya Abedi, 1954). Kwa ujumla, wanamapokeo wanauchukulia ushairi wa kisasa

kuwa ni aina ya uandishi iliyotokana na elimu na ukoloni. Kwa hiyo, tuseme kuwa elimu inaonekana

kwao kuwa na mchango hasi katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili. Aidha, wanawachukulia

wanausasa kuwa ni watu walioshindwa kutunga mashairi ilhali wanatamani kuwa watunzi wa mashairi.

Matokeo yake ni kutunga vitu visivyokuwa mashairi na kudai kuwa ni mashairi ya kisasa jambo ambalo

wao, wanamapokeo hawalikubali.

Kwa upande wao wanausasa wanawalaumu wanamapokeo kwa kuzuia maendeleo ya ushairi wa

Kiswahili kwa kutoutambua ushairi “mpya” ulioibuka. Wanausasa wanabainisha kwamba ushairi

simulizi wa Kibantu, ambao ndiyo chimbuko la ushairi wa Kiswahili, kama wanavyokiri pia

wanamapokeo, haukufuata kanuni za urari wa vina na mizani. Kanuni ya urari wa vina na mizani kama

uti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili wanaiona kuwa ni kanuni iliyotokana na athari za Waarabu

katika ushairi huo na wala si kanuni ya jadi ya ushairi wa Kiswahili. Hivyo, wanausasa nao, kama

ilivyokuwa kwa wanaujadi, wanalaumu ujio wa wageni kama chimbuko la athari mbaya kwa ushairi wa

65

Kiswahili. Wanausasa wanaenda mbali na kukazia kwamba shairi liamuliwe na kufungamana na

mawazo, mtiririko wa hisia na makusudio ya mtunzi na si mbinu za kifani. Hoja ya msingi ya kusisitiza

hapa ni kuwa, wanausasa hawapingi uhalali wa urari wa vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili,

bali wanataka aina “mpya” ya ushairi, ushairi usiofuata urari wa vina na mizani utambuliwe kuwa ni

ushairi wa Kiswahili pia. Kwa hiyo, wanausasa wanatambua mashairi yenye urari wa vina na mizani

kuwa ni mashairi ya Kiswahili lakini hawaoni kuwa huo ndiyo uti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili.

Mashairi ya Kiswahili yanaweza pia kutokuwa na urari wa vina na mizani.

(iii) USHAIRI WA KISWAHILI KIPINDI CHA UTANDAWAZI

Kwa dhana pana, kipindi hiki kinadaiwa kuanza zamani sana tangu ujio wa wakoloni waliovuka

mipaka yao na kuja Afrika. Hata hivyo, maelezo yetu yataelemea katika dhana finyu ambapo

utandawazi unaonekana kuanza miaka ya 1980 na kuendelea hadi sasa. Kipindi hiki kimeshuhudia

maingiliano makubwa baina ya mataifa mbalimbali ulimwenguni na dunia imekuwa kama kijiji kimoja.

Kimekuwa ni kipindi cha kubadilishana na kuathiriana kwa tamaduni baina ya mataifa ulimwenguni.

Maathiriano hayo yamejidhihirisha hata katika fani ya ushairi tunayoishughulikia. Hivyo, kipindi hiki

kimeshuhudia kunawiri kwa ushairi wenye athari kubwa ya kigeni. Kutokana na hali hiyo, ushairi wa

kisasa, ambao hapo awali ulipingwa sana na kuonekana wa kigeni, ukakubalika rasmi kama ushairi wa

Kiswahili, japo bado wapo wachache ambao hawautambui. Aidha, kipindi hiki kimeshuhudia kuingia

kwa aina mpya ya mashairi yanayojitokeza katika miziki mbalimbali kama vile Bongo Fleva, Taarabu

ya Mipasho na muziki wa Dansi. Ushairi huu unasemwa kuwa na athari kubwa ya ushairi wa kigeni.

Athari ya ushairi wa kigeni katika ushairi wa Bongo Fleva inabainishwa vizuri na Omari (2009) na

Samwel (2012a) miongoni mwa wengineo. Ushairi ulioibuka katika kipindi hiki una sifa kuu mbili:

kwanza, umejaa majigambo na pili, unazingatia kanuni za urari wa vina na mizani. Japo yapo pia

mashairi yasiyozingatia urari wa vina na mizani, suala la shairi kuwa na vina linaonekana ni suala

muhimu na ambalo washairi wanajisifia kwalo. Hii ni kusema kuwa, mashairi yasiyokuwa na urari wa

vina na mizani yanapungua thamani yake na kushusha hadhi ya msanii husika. Swali linaweza kuwa je,

msisitizo katika suala la urari wa vina na mizani katika ushairi wa kisasa ni aina mpya au kurejea upya

kwa mgogoro wa ushairi uliokuwapo miaka ya 1960 na 1970? Katika sura inayofuata tutachambua kwa

kina aina hii mpya ya ushairi wa Kiswahili. Kwa kuwa si rahisi kupitia aina zote za ushairi wa wakati

huu, tutajikita katika ushairi wa Bongo Fleva.

66

SURA YA TANO

USHAIRI WA BONGO FLEVA

Dhana ya Muziki wa Bongo Fleva

Ushairi wa Bongo Fleva ni ule unaobebwa na muziki wa Bongo Fleva. Hivyo, ili kuuelewa

ushairi wa Bongo Fleva, hatuna budi kuuelewa muziki wa Bongo Fleva kwa ujumla. Muziki wa Bongo

Fleva umepewa majina mengi sana miongoni mwa wanazuoni na wadau wa muziki huo. Majina hayo

ni pamoja na Bongo Flava na muziki wa kizazi kipya (Suriano 2006:1; 2007:207 na Omari 2009:5;

Samwel, 2012a). Muziki huu unaitwa wa kizazi kipya ikiwa na maana kwamba ni muziki unaopendwa

sana na vijana ambao ndio hasa huonekana kuwa kizazi kipya au kizazi cha leo. Dhana ya muziki wa

Bongo Fleva imekuwa na mkanganyiko mkubwa hasa katika jitihada za kuitofautisha na dhana ya Hip

hop (Suriano, 2006; Omari, 2009; Samwel, 2009; Samwel, 2012a). Wapo wanaouona muziki huu wa

Bongo Fleva kuwa ni aina mojawapo ya muziki wa Hip hop wa Kitanzania (Suriano, 2006:1 na

2007:207). Aidha http://spotistarehe.wordpress.com ikiwa na mtazamo kama huo inaeleza kwamba:

Muziki wa Bongo Flava unatofautiana na Genge (wa Kenya) kwani wao ni Commercial (wa

kibiashara) zaidi wakilenga kuchezesha (kuwaburudisha) watu na wakati mwingine hupati maana

kwenye wimbo mzima hata wakihojiwa wanashindwa kusema muziki ulilenga nini. Tofauti na muziki

wetu (Bongo Fleva) ambao unalenga kutoa ujumbe na kuburudisha na ndio maana utaona kila mtu

anajitahidi kumshirikisha mtu mwingine kwa ajili ya kuleta ladha tofauti ambayo pia inapatikana

kwenye makundi, na utaona nyimbo nyingi ambazo mtu amemshirikisha mwingine zimewatoa sana

(Ufafanuzi wetu).

Maelezo haya yanatudokeza kwamba Hip hop ni kundi kubwa la muziki duniani (universal)

ambapo kila nchi ina mtindo wake, Kenya-Genge, Afrika ya Kusini-Kwaito, Tanzania-Bongo Fleva na

kadhalika.

Aidha, wapo wanaoutofautisha muziki wa Bongo Fleva na Hip hop kwa vigezo vya midundo na

mapigo. Kwa mfano, Ramadhani Mponjika, katika mahojiano yetu, alitueleza kwamba muziki wa

Bongo Fleva ni “kapu” ambamo ndani yake kuna miziki ya aina mbalimbali ikiwemo zouk, rhumba,

reggae, RnB na kadhalika. Anadai kwamba mapigo ya muziki huu huwa ni mepesi, hakuna midundo

mizito (yaani bass). Akiielezea Hip hop anasema ni muziki unaofanana kote duniani na una mapigo

mazito (heavy beats) yanayoambatana na bass. Mawazo kama haya yametolewa pia na Suriano (2006

na 2007) na Omari (2009).

Mtazamo mwingine ni ule unaouona muziki wa Bongo Fleva kuwa ni muziki usio na nguzo

maalum. Muziki huu ni tofauti na muziki wa Hip hop ambao una nguzo zinazofahamika duniani kote.

Nguzo hizo ni pamoja na michoro inayowakilisha maudhui mbalimbali (graffiti), upangaji wa muziki

(deejaying), uchezaji wa kujinyonganyonga (breakdancing), mshereheshaji (MC) na ughani (rap)

(Suriano, 2006, 2007; Omari, 2009). Msanii Happiness Thadei (Sister P) anazitaja nguzo hizo katika

wimbo wake uitwao “MaDJ.” Hebu tuangalie ubeti huu:

1. Nazo nguzo tano za Hip hop weka akilini

2. Kwanza naanza na DJs kuweni makini

3. Pili MC jiheshimu wacha mapepe

4. Usilete mambo ya ajabu kuwafanya watu wacheke

5. Nayo ya tatu tungo zako sharti ujumbe zibebe

6. Zielimishe jamii ili utakacho waelewe

7. Tungo zako zikubalike zitumike hata kwenye mashule

8. Breakdance nayo mtindo wetu wakati ule

9. Hili ndilo darasa nakupa Hip hop shule

10. Hip hop nguzo ya tano michoro

Kundi la mwisho katika mkanganyiko huu ni la watu ambao wanauona muziki wa Bongo Fleva na

Hip hop kuwa ni kitu kimoja. Mtazamo huu unaona hakuna tofauti yoyote kati ya miziki hiyo miwili na

hivyo mwanamuziki fulani anaweza kutambuliwa kama mwanamuziki wa Bongo Fleva na pia anaweza

kutambuliwa kama mwanamuziki wa Hip hop. Mtazamo huu unaonekana hata miongoni mwa wasanii

wenyewe. Hili linathibitishwa na Samwel (2012a) ambaye anasema alipojaribu kuwauliza baadhi ya

wasanii ili kujua mtazamo wao juu ya wasanii fulanifulani kama ni wasanii wa Bongo Fleva au Hip hop

67

alipata majibu ya kutatanisha. Anatoa mfano kuwa, alipouliza kuhusu Joseph Haule (Profesa Jay/Prof.

Jay) na Selemani Msindi (Afande Sele), wengine walimwambia hao ni wanamuziki wa Bongo Fleva

wakati wengine walimwambia ni wasanii wa Hip hop. Samwel (khj.) anafafanua kuwa hii inatupa picha

kwamba muziki wa Bongo Fleva na Hip hop unaonekana kuwa kitu kimoja au kuna kutoelewa upi hasa

mpaka wa miziki hiyo.

Ili kuepuka mkanganyiko usio wa lazima, andiko hili halina lengo la kujiingiza katika mjadala huo

na hivyo katika andiko letu tutachukua mtazamo wa Samwel (2012a) ambaye muziki wa Bongo Fleva

anauita pia muziki wa Hip hop au wa kizazi kipya. Hivyo, katika andiko hili dhana za Bongo Fleva, Hip

hop na muziki wa kizazi kipya zitatumika kama visawe.

1. MAUDHUI YA USHAIRI WA BONGO FLEVA

Ushairi wa Bongo Fleva umebeba maudhui ya siasa, uchumi, utamaduni na maudhui ya kijamii.

Maudhui hayo, kwa hiyo, huhusisha masuala kama utawala, migogoro, kazi na umuhimu wake, dini,

mapenzi na ndoa na kadhalika. Mwanjoka (2011:34), akibainisha utokeaji wa maudhui haya katika

ushairi wa Bongo Fleva, anaeleza kwamba, “ujumbe katika nyimbo nyingi (za Bongo Fleva) za leo

umeegemea sana kwenye mapenzi, siasa, malumbano…” (Ufafanuzi wetu). Hapa tunaona anabainisha

kuwa ushairi wa Bongo Fleva unabeba maudhui ya kiutamaduni na kijamii (mapenzi) na pia kisiasa.

Aidha, Samwel (2012a) anaongezea kuwa ushairi huo huweza pia kubeba maudhui ya kiuchumi. Katika

sehemu ifuatayo tutachambua kwa kina maudhui haya na kuonyesha yanavyojibainisha.

Kwa kuanza na maudhui ya kisiasa tunaona kuwa ushairi wa Bongo Fleva umebeba maudhui

mengi yanayohusiana na siasa. Miongoni mwa maudhui ya mkondo wa kisiasa yanayoonekana katika

ushairi wa Bongo Fleva ni pamoja na maudhui yanayohusu utawala na uongozi.

(a) Maudhui ya Uongozi na Utawala

Uongozi na utawala ni mojawapo ya maudhui yabebwayo na ushairi wa Bongo Fleva. Uongozi

ni moja ya mambo ya msingi katika siasa za jamii yoyote ile. Ushairi wa Bongo Fleva umesawiri sana

maudhui ya kisiasa. Katika mashairi ya mkondo huu, wasanii wa Bongo Fleva wanaimba kuhusu wao

kuwa watawala na/au viongozi. Wasanii wanajipachika au kupachikwa majina kama rais, mfalme,

chifu, mheshimiwa na kadhalika ambayo kimsingi ni majina yanayotumiwa katika medani ya siasa.

Mfano mzuri wa mashairi ya Bongo Fleva yanayohusu siasa ni mashairi yanayoonekana katika

wimbo wa “Muhogo Andazi” wa msanii Rahim Nanji (p.h.k Bob Junior) ambapo msanii anaimba

akijieleza kwamba yeye ndiye rais wa masharobaro. Anafafanua kwamba masharobaro ni watu wasafi

na watanashati. Tunaweza kuthibitisha hili katika kibwagizo hiki anaposema:

1. Mimi ndiye Mr. Chocolate

2. Rais wa masharobaro dunia nzima

3. Ninaposema sharobaro

4. Namaanisha kijana msafi, mtanashati

5. Ninaposema mtoto wa Kitanzania

6. Namaanisha vidole gumba miamia…

7. Ninaposema rais wa wasafi

8. Namaanisha rais wa watanishati

9. Ninaposema sharobaro

10. Namaanisha kijana msafi, mtanashati

Chanzo: Bob Junior (2011), “Muhogo Andazi”

(b) Maudhui ya Kiuchumi

Zaidi ya maudhui yahusuyo siasa, ushairi wa Bongo Fleva umebeba pia maudhui ya kiuchumi.

Ushairi wa Bongo Fleva unaobeba maudhui ya kiuchumi umegawanyika katika makundi makuu

mawili, ushairi unaobeba maudhui ya ushindani na ushairi unaobeba maudhui ya biashara. Tuanze

kuangalia majigambo ya ushindani.

(i) Maudhui ya Ushindani

Ushairi wa muziki wa Bongo Fleva umebeba maudhui ya ushindani. Omari (2009:143) anaeleza

kwamba mashindano ni sifa moja kubwa inayoutambulisha muziki wa kizazi kipya. Mashindano haya

anayaeleza kwamba yamekuwa miongoni mwa wasanii wenyewe, watayarishaji wa muziki,

wasambazaji na hata wadhamini. Anaendelea kufafanua kuwa, mashindano haya yanahusisha kuibiana

68

mashairi, mapigo au mawazo yanayobebwa na nyimbo, kuhama kutoka kundi moja la muziki huu hadi

lingine, kutumia nyimbo za msanii mwingine na hata mapigano halisi baina yao. Ushindani huu na

migogoro inayoambatana nao vimepewa jina la bifu (Omari, 2009:78). Ushindani unaonekana katika

maneno ya wasanii wanapohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari na hata katika mashairi yao.

Omari (2009:79) anabainisha kwamba miongoni mwa mabifu katika muziki wa Bongo Fleva

ambayo yaliwahi kufahamika ni pamoja na bifu baina ya Godfrey Tumaini (Dudu Baya) na Lucas

Mkenda (Mr. Nice); Filipo Nyandindi (O-Ten) na Selemani Msindi (Afande Sele); East Coast Team na

TMK Wanaume Family na bifu kati ya Happiness Thadei (Sister P) na Zainabu Lupangule (Zay B).

Zaidi ya mabifu hayo anayoyataja Omari, mabifu mengine ambayo yaliwahi kubainika ni baina ya

TMK Wanaume Family na TMK wanaume Halisi; Joseph Haule (Prof. Jay) na Selemani Msindi

(Afande Sele); Banana Zoro na Hafsa Kazinja; Naseeb Abdul (Diamond) na Mwingereza Athmani

Mwingereza (Tanzanite) na Naseeb Abdul (Diamond) na Raheem Nanji Rummy Rummy (Bob Junior).

(ii) Maudhui ya Kazi

Aina nyingine ya maudhui ya kiuchumi ya ushairi wa Bongo Fleva ni maudhui ya kazi. Ushairi

wa Bongo Fleva umebeba maudhui ya kazi za aina mbalimbali. Katika muziki wa Bongo Fleva wasanii

wanaelezea juu ya umuhimu wa kufanya kazi na faida zake. Mfano mzuri wa maudhui ya mkondo huu

unaonekana katika wimbo wa Mr. 2 “Mchakamchaka:”

1. Anha baada ya dhiki faraja

2. Nimeamini mambo mema

3. Ni kwa yule anayengoja

4. Na wa mbili havai moja anha anha

5. Sasa ni mwendo wa dolali9

6. Ndani ya akaunti mtoni utadhani mtoto wa Balali

7. Sema vijisenti vyangu ni vya halali

8. Bongo mchaka mchaka tu

9. Mafisadi hawalali

10. Nina uhuru wa kusema

11. Na nitasema chochote ntakachoona kinafaa mimi kusema

12. Na nnakuja na falsafa za Obama

13. Tunatakiwa kuchange

14. Tusipochange maisha bora kwetu ndoto kama muafaka wa Zenji anha

15. Wacha niendeleze dozi

16. Maana leo kama balozi

17. Kama kazi ni kazi hakuna ubitozi

18. Na ni upuuzi kusema gemu haliuzi

19. Wakati we unangoja kuuza tepu tu na CD

20. Sisi tunauza mpaka jezi

21. Ni kwa sababu tuna CV

22. Na huu ndo mchakamchaka tunaoutaka

23. Na anha anha hakuna kuchoka

Chanzo: Mr. 2 (2009), Veto

Hapa msanii anaonesha umuhimu wa kazi ambapo anaeleza kwamba yeye kazi ya muziki inamwingizia

fedha nyingi kama “mtoto wa Balali.” Daudi Balali alikuwa gavana wa Benki kuu ya Tanzania na

alifariki mwaka 2008 huko Marekani alikoenda kutibiwa.10Gavana wa Benki huaminika kuwa na fedha

nyingi sana na hivyo hata watoto wake hunufaika na fedha hizo. Kwa hiyo, msanii hapa anaeleza

kwamba muziki unamwingizia fedha nyingi sawa na anazoingiza gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha, katika mstari wa 17 msanii anasisitiza kazi ni kazi mradi mkono uende kinywani na pia kazi

yoyote lazima ifanywe kwa bidii.

(c) Maudhui ya Kijamii katika Ushairi wa Bongo Fleva

9 Dolali ni msimu unaotumika kumaanisha dola (za Kimarekani).

10 Taarifa hii imesomwa toka katika (http://bongocelebrity.com/2007/12/21/gavana-balali-ajiuzulu) tarehe 24/08/2011

69

Katika uchambuzi wa maudhui kijamii tunaangalia, zaidi ya mambo mengine, mahusiano miongoni

mwa wanajamii. Hivyo, aina kuu ya maudhui ya kijamii tutakayoyachambua hapa ni maudhui ya

mapenzi.

(i) Mapenzi

Mapenzi ni maudhui mengine yanayoonekana katika ushairi wa Bongo Fleva. Mapenzi ndiyo

maudhui yaliyopata umaarufu zaidi katika ushairi wa Bongo Fleva. Mwanjoka (2011:110) akifafanua

mapenzi katika Bongo Fleva, anaeleza kwamba:

Ni ukweli mapenzi huchukua sehemu kubwa ya maisha ya mwanadamu. Na imeandikwa hata

kwenye vitabu vya dini kwamba, (kuna hatua tatu muhimu), moja kuzaliwa, pili mapenzi, tatu ni

kifo. Na vyote hivyo havikwepeki ni lazima mwanadamu avipitie endapo atazaliwa na kuishi

miaka au muda fulani hadi kuja kujitambua. Katika muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) zaidi ya

asilimia hamsini ni nyimbo zinazohusu mapenzi. Na asilimia zinazobaki ni ujumbe mchanganyiko

kama vile siasa na uchumi, majigambo, majibizano, starehe na maisha magumu ya jamii nzima ya

Mtanzania yanayozungumzwa kila kukicha.

Baadhi ya mambo ya mapenzi yanayosawiriwa ni pamoja na kujisifia kuwa na mume/mke bora au

mzuri, kuelezea ujuzi wa kupenda au kuelezea jinsi msanii anavyopendwa na wanawake. Vilevile

maudhui ya mapenzi huweza kuhusu kuelezea jinsi msanii alivyo na maumbile ya siri makubwa (na

hasa wanaume) au anavyojua kumridhisha mwenzi wake kimahaba, anavyochukua wake au wapenzi

wa watu wengine na kadhalika. Mfano wa ushairi wa mapenzi tunauona katika wimbo wa Sugu (Mr. 2)

uitwao “Moto Chini” kama tulivyounukuu hapa chini. Katika wimbo huo msanii anaeleza kwamba ana

mafanikio makubwa katika maisha kutokana na muziki anaoupiga na hivyo anachukua hadi wanawake

(maplayer) wa wenzake (mstari wa 13-14). Msanii anaendelea kudai kuwa anapendwa na wanawake

kutokana na umaarufu na mafanikio yake. Tazama wimbo huo:

1. Nimeshatoa ngoma UK sasa narudi tena

2. Nairobi na Kampala bado nawakilisha kwa sana

3. Maneno bado ni Yes

4. Naona kama hakuna noma

5. Sasa mechi ni international

6. Sugu ni chama kubwa kama Arsenal

7. Bado nipo dimbani

8. Na maiki ipo mkononi

9. Labda huku nilipo nifuateni

10. Maana inaonekana nitachelewa kushuka chini

11. Inashangaza kuona muda unazidi kwenda

12. Na mchezo wa Hip hop ndo kitu nnachokipenda

13. Check maplayer wenu jinsi ninavyowapiga denda

14. Ni VIP kila kiwanja ninachokwenda

15. Kwani hatari kitu gani

16. Kila wakati nipo bwana TBC extra quality

17. Na wachizi wangu wote sasa zidisheni hasira

18. Ni wakati wa kumaliza huu ni utungo wa kibiashara

19. Sasa ni muda mrefu wanatufanya mafara

20. Tunaingiza mabilioni wanahonga mademu vitara

21. Hamuwezi kunitisha

22. Katika kuthibitisha

23. Nawawasha na tafadhali sahauni kuhusu sugu

24. Maana atazidi tu kuleta mavurugu

25. Na kuwanyonga watu simo

26. Labda ganja zamani kidogo nilikuwemo

27. Na ndo mana mpaka leo bado inanipa misimamo

Chanzo: Mr. 2 (2009), Veto

Wimbo mwingine wa Bongo Fleva ambao unabeba maudhui ya mapenzi ni “Ananitesa” ulioimbwa

na Zay B akiwashirikisha Unique Sisters. Tazama mistari ifuatayo:

1. Nakupenda pia nakutaka pia

2. Mwenzio naumia

3. Unanipa machungu moyoni

4. Nikikutazama usoni

70

5. Jinsi ulivyo handsome

6. Nadata ukitabasamu

7. Nakuhusudu si mchezo

8. Ukinikubali utakula vya dezo

9. Usiogope kuitwa binti

10. Nitakutunzia siri

11. Nitakupa offer tutajivinjari

12. Viwanja hatari usione hatari

13. Limekuangukia zali

14. Mimi kwako nimenasa

15. Unanitesa nitajinyonga nikikukosa…

16. Nataka tushinde ndani ya jiji la Makamba

17. Ananitisha na pamba jinsi anavyotoka bomba…

18. Napata wendawazimu mapenzi hayana ugumu

19. Njoo tupate goodtime…

20. Sema unachotaka utapata

21. Ila usilete za kuleta kwangu utapeta

22. Sina ujanja nitakupa hata mkwanja

23. Twenzetu ukaben kiwanja

24. Mi sio mchunaji ukiwa nami utapata ulaji

25. Nina kiasi cha kumwaga tatizo utumiaji

26. Sio kama nachonga wanaume nawahonga

27. Unachotakiwa kwangu kutulia

28. Utakula raha zote za dunia

29. Na maisha utafurahia

Chanzo: Zay B (2002), Mama Afrika

Katika wimbo huu tunaona msanii anaelezea mapenzi ya dhati aliyonayo hata kuwa tayari kujinyonga

kwa sababu ya mapenzi. Anaendelea kueleza kwamba kwa mapenzi aliyonayo atatumia hata fedha zake

na mali nyingi alizonazo kumlisha na kumpa kila kitu mpenzi wake.

Aidha, naye mwanamuziki Bushoke anaelezea mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mpenzi wake na

kwamba bado hajafika mwisho wa kumwonyesha mpenzi wake mapenzi yote. Turejelee wimbo wa

Jackline Ntuyabaliwe (K-Lynn) akimshirikisha Bushoke, uitwao “Machozi ya Furaha.” Tuchunguze

ubeti wa wimbo huo:

1. Na bado na bado sijafika mwisho

2. Na bado na bado sijamaliza kitabu

3. Vumilia maisha yangu, utakula vya kwangu

4. Mimi si wale wanaojisifu kwa ngono

5. Mapenzi si maneno, mapenzi ni vitendo

6. Na bado na bado nimesema bado

Chanzo: K - Lynn (2004), Machozi ya Furaha

Hapa msanii anaeleza kwamba mapenzi ni vitendo na si ya maneno matupu. Katika wimbo huu kama

ilivyo kwa ule wa Zay B msanii anaamini kwamba mapenzi ni kupeana vitu (tazama mstari wa 3).

Mapenzi katika ushairi wa Bongo Fleva yanahusishwa sana na vitu na mali alizonazo mtu.

Ujitokezaji mkubwa wa maudhui ya mapenzi katika nyimbo za Bongo Fleva ndio hutumika

kama kigezo kimojawapo cha kujaribu kuutofautisha muziki wa Bongo Fleva na Hip hop. Hivyo,

muziki wa Bongo Fleva unaonekana kuwa ni ule unaohusu zaidi mapenzi wakati Hip hop hauhusu sana

suala hilo bali mambo mengine “muhimu.” Akithibitisha hili Mwanjoka (2011:111) anaeleza kwamba:

Wapo wasanii wa Hip hop ambao wanaimba nyimbo za mapenzi pia, lakini sio mara kwa mara

kama wasanii wengine wa muziki wa kuimba (Bongo Fleva). Mfumo huu wa kutengeneza nyimbo

za mapenzi kwa wingi umejengeka hata kwa wasanii wapya wanaoanza muziki kwani wengi wao

huanza na nyimbo za mapenzi na wachache ndio huanza na nyimbo za kujisifia (nyimbo za

majigambo) (Ufafanuzi wetu).

(d) Maudhui ya Kiutamaduni Katika Ushairi wa Bongo Fleva

Zaidi ya majigambo ya kijamii, muziki wa Bongo Fleva pia unabeba maudhui ya kiutamaduni.

Miongoni mwa mambo yanayosawiriwa katika ushairi huo ni imani mbalimbali kama vile imani za

waganga na uchawi, masuala ya mila na desturi na kadhalika. Mfano mzuri wa mashairi ya kitamaduni

71

yanayozungumzia masuala ya mila na desturi ni yale yanayoonekana katika wimbo wa Abel Motika

(Mr. Ebbo) uitwao “Mi Mmasai” uliopo katika albamu ya Fahari Yako. Katika shairi hilo msanii

anaelezea mila za Wamasai. Anaeleza kwamba Wamasai wanazishika na kuzifuata mila na desturi za

Kiafrika. Aidha, anaeleza kwamba utamaduni wa Kimasai upo juu kuliko tamaduni zote za Afrika.

Anataja baadhi ya tamaduni hizo kuwa ni pamoja na mavazi ya Kimasai, dawa za asili na kadhalika.

Kujivunia utamaduni wa jamii husika ni moja ya mambo muhimu katika kujenga jamii endelevu (Ayisi,

1972; Mair, 1979).

Aina nyingine ya maudhui ya kiutamaduni ni maudhui ya imani. Wasanii wa ushairi wa Bongo

Fleva wana imani mbalimbali ikiwamo imani kwamba kuna Mungu ambaye ana uwezo wote.

Wanaoamini hili wanaamini vilevile kuwa kumcha Mungu na kujiepusha na uovu ni jambo la kujivunia

na jambo litakalompeleka mtu mbinguni. Tuthibitishe hili kwa kuangalia mfano kutoka kwa msanii

Sister P katika wimbo wa “Sisi Tulivyo” anapobainisha hili:

1. Mimi nilivyo ni mchamungu kuliko ulivyo

2. Mimi nilivyo siyo bitozi wa kupenda sana mademu

3. Mimi nilivyo sina habari na adui asemavyo

4. Mimi nilivyo sasa ni peace hakuna uadui

5. Wote rafiki awe msichana awe mvulana

6. Mimi nilivyo napenda sana mambo ya Mungu

7. Sichagui kama inavyosema Biblia

8. Mimi nilivyo sinywi pombe sivuti brother

Chanzo: Omari (2009:295)

Katika shairi hilo hapo juu msanii anaelezea jinsi yeye alivyo mchamungu na havuti sigara wala

hapendi ukahaba.

Aidha, wapo wanaoamini nafasi ya Mungu na uganga katika maisha. Wanaamini kwamba

uwezo wa kiganga na Kimungu unaweza kutumika kumwinua mtu na kumpa mafanikio na pia unaweza

kutumika kuwaharibia wengine. Vilevile, wanaonesha imani kwamba msaada kutoka kwa Mungu ndio

upo juu ya msaada mwingine wowote. Tuchunguze wimbo wa “Achana Nao” Sister P anaposema:

1. Kilichotoka kwa Mola kamwe hakitarubuniwa

2. Ni sawa na askari vitani habadili nia

3. Ongeza bidii kwenye steji safisha njia

4. Funga masikio fanya utakavyo Pondela

5. Sikiliza ushauri wa watu panapotakiwa

6. Ufikirie kwa kina kisha utunge ujumbe kwa kina

Chanzo: Omari (2009:292)

Hapa msanii anaonyesha uwezo mkubwa alionao Mungu katika kuwafanikisha wanadamu. Hata hivyo,

msanii anasisitiza nafasi ya juhudi na maarifa ili Mungu aweze kusaidia. Mawazo kama haya

yanaonekana katika ubeti ufuatao:

1. Nafungua ubongo natoa fikra za utumwa kichwani

2. Kipawa chatoka kwa mola wala sijatumia ubani

3. Sister P kupata chati watu wanadhani rap utani

4. Rap biashara bwana ila angalia usijepata hasara

5. Kuuza vitumbua, pipi maandazi zote biashara

6. Usidharau hizo biashara watu watakuangushia msala11.

7. Wasomi wengi wamesoma kwa kutumia hizo biashara

8. Mashairi sibahatishi na nitauza nyingi nakala

9. Na siyo utani nyota kwangu imeonekana biashara

10. Wandago12 rafiki zangu tena wa kina

11. We uliza maswali mengi majibu mimi sina

12. Nakupa rap shule mashairi yangu yana vina

Chanzo: Omari (2009:291)

Katika mstari wa pili (2) wa wimbo huo tuliounukuu anabainisha kwamba mafanikio aliyonayo

hayatokani na uganga bali amepewa na Mungu. “Ubani” hapo unawakilisha uganga kutokana na ukweli

11 Msala ni msimu unaotumika kumaanisha matatizo/kipigo.

12 Wandago anamaanisha Walume Ndago yaani kikundi cha Bongo Fleva cha TMK Wanaume.

72

kwamba ni vitu vinavyotumika sana katika fani hiyo. Hata hivyo, Zay B katika wimbo mwingine

uitwao “Hatari Kitu Gani” anaonesha kuwa Mungu na uganga vinaweza kusaidia tu kama mtu ataweka

juhudi binafsi. Aidha, anabainisha kuwa hata uchawi ukitumika kumkwamisha mtu lakini kama mtu

huyo atakuwa na juhudi, uchawi na uganga huo hautafaa kitu. Tuthibitishe hili katika ubeti huu:

1. Mimi komandoo tena nakuja kwa vishindo

2. Nasema njoo once again nawakilisha Tanzania

3. Wanga mtabana mtaachia lyrics nazidi kuwamiminia

4. Mimi mtaniambia sio kama najifagilia13

5. Mamia kwa mamia wamekiri kama mimi ndio concord…

6. Sauti yangu inasikika dunia nzima

7. Vigumu kuisahau kama Tupac na B.I.G

Chanzo: Omari (2009:342)

Katika wimbo huo msanii anabainisha kwamba zaidi ya “wanga” au wachawi kumbania mtu

(kumroga) bado kuna uwezekano wa mtu husika kufanikiwa. Hapa tunapata picha kwamba “wanga” au

uchawi hauleti maendeleo bali unatumika kuwakwamisha watu. Katika mstari wa tatu anabainisha wazi

kwamba kazi ya wanga ni kubana mafanikio ya watu wengine. Uchawi hapa unawekwa kundi moja na

tabia zenye sifa mbaya kama unafiki, uchoyo, kutopenda mafanikio ya mwingine na kadhalika.

Kutokana na hilo neno “wanga” huweza pia kutumika kumaanisha mtu yeyote asiyependa maendeleo

ya mwingine. Wasanii, kwa hiyo, wanaimba kuelezea jinsi wao wasivyorogeka kwa namna yoyote ile.

Hili linabainika pia katika wimbo “Maisha Uswahilini” wa Sister P:

1. Sister P nakuja wanga sasa mbona mtakwisha...

2. Sina papara katika fani nishatua...

3. Rudi nyuma kumbuka enzi za Mchonga14

4. Watoto wadogo wachawi mpaka skonga15

5. Tunashinda nao maskani nyumbani kwao

6. Tunacheka nao wachawi ni mama zao

7. Amka usiku ndugu zangu muone kazi

8. Walivyo uchi utafikiri radhi

9. Angalia cha moto akifa anavyotapatapa

10. Mchana watu, usiku wamegeuka paka

Chanzo: Omari (2009:303)

Hapa msanii anaonyesha uchawi ni jambo linalomchukiza Mungu, ni dhambi na hivyo mshika dini,

kama yeye, hapaswi kuwa mchawi. Vilevile, anabainisha kuwa uchawi hauwezi kuleta maendeleo bali

unarudisha nyuma maendeleo ya jamii husika. Uchambuzi wa kina juu ya suala la uchawi katika jamii

za Kitanzania na uhusiano wake na Mungu na maadili ya jamii unaonekana katika Mair (1979:218-

232).

2. FANI YA USHAIRI WA BONGO FLEVA

Tumeeleza hapo awali kwamba fani ni jinsi kazi ya kifasihi ilivyoumbwa. Fani hujumuisha

vipengele kama utungaji, muundo, mtindo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha. Katika sehemu

hii tutachambua mbinu mbalimbali za kifani zinazotumika katika ushairi wa Bongo Fleva tukianza na

utungaji.

(a) Utungaji wa Ushairi wa Bongo Fleva

Utungaji wa ushairi wa Bongo Fleva ni wa aina mbili: utungaji wa papo kwa papo na utungaji wa

kabla ya tukio/utendaji. Hebu tuchambue kwa kina aina hizi mbili za utungaji wa ushairi wa Bongo

Fleva.

(i) Utungaji wa Papo kwa Papo katika Ushairi wa Bongo Fleva

Wataalamu mbalimbali wameelezea kuhusu utungaji wa papo kwa papo wa kazi za fasihi.

Maelezo haya yanaonekana katika kile kinachojulikana katika fasihi kama nadharia ya fomula simulizi.

Nadharia hii ilianzishwa na Milman Parry (1928 na 1930) na mwanafunzi wake, Albert Lord (1981).

Parry alianza kwa kujiuliza ni kwa vipi tendi za Homer zilitungwa. Je, zilikuwa simulizi au andishi?

13 Kujifagilia ni msimu unaotumika kumaanisha kujisifia.

14 “Mchonga” hapa linatumika kumaanisha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa sababu alichonga meno. Hivyo hapa

msanii anamaanisha enzi za Nyerere.

15 Skonga ni msimu unaotumika kumaanisha shule. Unatokana na neno la Kiingereza school (skuli)

73

Alihisi kuwa labda zilikuwa simulizi, na kuja kuandikwa baadaye. Ili kuthibitisha nadharia tete hiyo,

alifanya utafiti katika jadi hai ya tendi-simulizi nchini Yugoslavia (miaka ya 1920-1940). Ikumbukwe

kwamba jadi ya Yugoslavia ina uhusiano mkubwa na ile ya Wayunani (Homer). Kabla ya Parry,

wataalamu kama vile Robert Wood (1767) na F.A. Wolf (1775) walikwisha dokeza kuwa huenda tungo

za Homer hazikuandikwa, bali zilikuwa simulizi. Lakini uthibitisho wa kutosha wa dai hili ulikuwa

bado haujatolewa. Kadhalika, wataalamu wa Biblia walikwisha anza kuhisi kuwa huenda hata maelezo

ya Biblia, hasa Agano la Kale; yalikuwa simulizi za mdomo kabla ya kuandikwa.

Parry alianza kwa kuchunguza mishororo ishirini na tano (25) ya mwanzo ya Iliad na Ulisei

(Odyssey) ili kuona ni kwa kiasi gani tungo hizo mbili ni za kifomula. Parry (1971:272) anaielezea

fomula kuwa ni:

A group of words regularly employed under the same metrical conditions to express a given

essential idea.

Kundi la maneno linalotumika katika mazingira ya kinudhumu yanayofanana ili kueleza wazo

fulani mahsusi lililo muhimu (Tafsiri yetu).

Matokeo ya utafiti wake yalimshangaza: Aligundua kuwa takriban 70% ya mistari 27,000 katika

tendi hizo ilikuwa ya ki-fomula. Kutokana na hilo, Parry akahitimisha kwamba tungo hizo ni nudhumu,

ni simulizi (si andishi), na ni za kimapokeo.

Baada ya Parry kufariki mwaka 1935, mwanafunzi wake, Albert Lord, aliuendeleza utafiti wake

na kutoa mchango kubwa. Aliongeza kipengele cha “formulaic expression” – kauli ya kifomula – katika

nadharia ya fomula simulizi. Alisema, mbali na watendi kutumia fomula bila kuzibadilisha, wakati

mwingine huweza kubuni na kutumia kauli zenye muundo wa fomula. Alielezea kauli ya kifomula

kuwa ni “a line or half-line constructed on the pattern of fomula.” (mshororo au kipande chenye umbile

la fomula). Mchango mahsusi wa Lord ni katika kipengele alichokiita “theme.” Kipengele hicho ndicho

kilichokuja kuitwa topos (na kutoholewa kuwa topo kwa Kiswahili) na watafiti wengine. Lord anaeleza

kuwa “theme” ni “repeated incidents and descriptive passages” (Vitushi na vifungu vya maelezo

vinavyorudiwarudiwa). Tofauti na fomula, topo hailazimiki kufuata urari wa mizani, au kujirudia neno

kwa neno, bali huwa na umbo zalishi lenye kubadilika kulingana na mazingira ya usimulizi. Mifano ya

topo inayotolewa ni kupokea barua, kuitisha baraza, hotuba za ufafanuzi, kujibu barua, kujiandaa kwa

vita na kadhalika (taz Mulokozi, 2002, The Epic Contoversy). Topo husaidia kujenga mtiririko wa kazi

ya fasihi simulizi. Kadhalika, humsaidia fanani kuijenga na kuisimulia kazi yake kwa haraka wakati wa

utendaji, maana topo tayari zimo katika jadi na asili yake; anachohitaji ni kuziainisha, kuzirekebisha

kidogo na kuzitumia kulingana na mahitaji (taz. Samwel, 2012a).

Hata hivyo dhana za fomula na topo zikarekebishwa na wataalamu mbalimbali kadri

walivyoona inafaa kulingana na mitazamo yao (taz. Nagler, 1967 na 1974; Johnson, 1978; Okpewho,

1979; na Mulokozi, 2002:132-135). Kwa mfano, Mulokozi (2002:132-135) anaona kwamba maelezo ya

fomula ni bora yaanzie katika ngazi ya maana. Anasema:

Formula as it applies to enanga poetry is ana abstract, traditional recurrent core-idea, serving

primarily as a semantic and structural aid in oral composition-in-performance, and realized

concretely, as a phrase or clause, only in oral performance, and largely through the devices of

verbal repetition, derivation, transformation, and linguistic-contextual association.

Fomula kama inavyotumika katika tendi za nanga ni wazo-kiini radidi la kidhahania la kimapokeo

linalosaidia kuzalisha haraka maana na miundo katika utungaji wa papo kwa wakati wa utambaji,

na ambalo hujidhihirisha tu kama kipashio wakati wa utendaji-simulizi, hususan kwa kutumia

mbinu za uradidi-kauli, unyambuo, ugeuzi, na uhusishi wa kiisimu na/au kimuktadha (Tafsiri

yetu).

Mulokozi anaendelea kwa kusema kwamba fomula hudhihirika kwetu kupitia sura na maumbo

mbalimbali wakati wa uwasilishaji: maumbo hayo anayaita alomofu (< alloform-mulla). Dhana hii ya

fomula kwa mujibu wa Mulokozi, ndiyo iliyotumiwa pia na Samwel (2012a) na ndiyo inayotumiwa pia

katika andiko hili kwani inaboresha ufafanuzi wa awali wa akina Parry. Aidha, Mulokozi (2002:134)

anapendekeza dhana “topos” badala ya dhana “theme” iliyopendekezwa na Parry na Lord. Mulokozi

74

anaona kwamba kwa kuwa dhana ya “theme” tayari inatumika katika fasihi kumaanisha dhamira/wazo

kuu, “theme” katika nadharia ya fomula – simulizi iitwe topo. Anaifasili topo kwa kusema:

A traditional or conventional stock incident or description which is regularly reformulated in

different stories and contexts by the oral bards to build up oral narrative poems during

performance.

Kitushi au sawiri ya kikaida ya kijadi ambayo husimuliwa upya na watendi-simulizi katika hadithi

na miktadha mbalimbali ili kutunga tungo simulizi wakati wa utendaji.

(Tafsiri yetu).

Fasili ya Mulokozi ni bora kwani imeboresha maelezo ya waliomtangulia. Hata hivyo, kwa

kuwa Mulokozi (2002) alikuwa anashughulikia utendi ni wazi kwamba ili tuweze kuitumia fasili yake

katika ushairi wa Bongo Fleva tunaouelezea hapa, tunapaswa kuirekebisha fasili hiyo. Topo, kwa hiyo,

inafasiliwa katika andiko hili kuwa ni kitushi au sawira ya kikaida ya kijadi au kiada ambayo

husimuliwa upya na wasanii wa fasihi simulizi ili kutunga tungo simulizi, ukiwamo ushairi wa Bongo

Fleva, wakati wa utendaji wake. Topo ni moja ya zana zinazozalisha fomula katika usimulizi.

Kwa ujumla, msimamo wa Parry na Lord na wafuasi wao ni kwamba fomula na topo

hazihusishi kukariri. Hii ina maana kwamba kazi za fasihi simulizi, ukiwemo ushairi wa Bongo Fleva,

huweza kutungwa papo kwa papo wakati wa utendaji wake. Huu ndio umekuwa msingi unaotumiwa na

wanafasihi mbalimbali kueleza kwamba tanzu mbalimbali za fasihi simulizi zilitungwa papo kwa papo

wakati wa utendaji wake (taz. Finnegan, 1970; Mulokozi, 1996). Suala hili pia linabainika katika

ushairi wa Bongo Fleva ambapo tunaona kuna wasanii mbalimbali ambao huimba mashairi yao papo

kwa papo.

Baadhi ya wasanii wa ushairi wa Bongo Fleva hutunga mashairi yao wakati wa tukio husika la

utendaji. Wasanii huweza kuwa jukwaani katika maonyesho na baada ya kuimba au kughani nyimbo

zao kadhaa hupandwa na midadi na kuanza kughani au kuimba mashairi mapya papo kwa papo. Wakati

mwingine, huweza kubadilisha maneno ya mashairi ya awali na kuweka maneno mapya

wanayoyatunga papo kwa papo. Mtindo huu ni maarufu kwa jina la free style, yaani mtindo huru.

Profesa Jay katika mahojiano aliyoyafanya katika Samwel (2012a) alimwambia kwamba kuna

wanamuziki wanaojulikana kuwa maarufu kwa mtindo huu wa utungaji. Alimtajia baadhi ya

wanamuziki hao kuwa ni pamoja na Ibrahimu Mohamed (a.k.a Roma), Albert Ngwea (a.k.a Mangwea)

na John Sim Johon Mseke (a.k.a Makini). Kujua mtindo huu kunahusishwa na umahiri katika muziki

wa Bongo Fleva. Afande Sele katika wimbo wake uitwao “Mtazamo” anathibitisha hili anaposema,

“wanaitwa ma MC hawajui mitindo huru, huu mtazamo wangu naona vingi vioja.” Hapa tunaona wazi

kwamba mwanamuziki anayejua mtindo huru ndiye mwanamuziki bora. Hii inaurudisha muziki wa

Bongo Fleva katika sifa za msingi za fasihi simulizi, utendaji wa papo kwa papo.

Utungaji huu, hata hivyo, huongozwa na fomula na topo. Msanii anayetunga papo kwa papo

huongozwa na fomula na hasa ile ya urari wa vina na mizani. Fomula hii humfanya kila mara

kuhakikisha anapachika maneno mapya ambayo yana vina vinavyofanana na mstari uliopita. Kwa

mfano, tulihudhuria maonyesho ya Bob Junior ambaye alighani utungo huu ambao, kwa kuwa haupo

katika nyimbo zake zinazofahamika, tunachukulia kuwa aliutunga papo kwa papo. Hebu tuuangalie

utungo huo:

1. Bob Junior mzee wa mashati

2. Mimi ndiye Rais wa watanashati

3. Sasa naandaa mkakati

4. Mbona mimi mzee wa pati!

5. Sauti ya rojorojo za Chocolate

6. Wale wachawi tuwaweke kati

7. Watalia watajinyonga kwa wakati

Chanzo: Umenukuliwa katika onyesho la Bob Junior lililofanyika Mbeya Tarehe 13/4/2011.

Vivyo hivyo msanii Roma akiwa katika tamasha la Epiq Nation katika jiji la Mwanza alitoa

ghani za papo kwa papo kulingana na muktadha wa tukio lililolokuwa linaendelea. Ghani hizi hazipo

katika wimbo wake wowote na hivyo ni ithibati kwamba alizitunga papo hapo jukwaani. Ghani hizo

zinasema:

75

1. Mwanza, msishindane na mwanamke pedeshee atamuhonga noah16

2. Wanaume mjitahidi ipo siku mtatoboa

3. Mimi ni Rais wa ghetto

4. Sina kabisa mchecheto

5. Na wala sipigi punyeto

6. Namiliki mademu kwa kipato

7. Mwanza, sema oyee kwa Epiq Nation

Chanzo: Umenukuliwa katika onyesho la Epiq Nation Mwanza mwaka 2011.

Fomula hii ya urari wa vina na mizani wakati mwingine huwalazimisha kutumia maneno

ambayo kimantiki hayaendani na yale yaliyotangulia ila kwao lengo la msingi ni urari wa vina na

mizani. Vilevile, hufanya hata mawazo yabebwayo na ushairi husika kuwa hayana ushikamani. Mfano

wa hili tunauona katika wimbo wa Roma uitwao “Mathematics:”

Ubeti 1

1. Nimeshatikisa nyavu mi ndo MVP

2. Wakakimbia depo hapo nipo CCP

3. Niliwapigisha kuruta kwata la JKT

4. Nina kipaji mimi kushinda hata THT

5. Nawapangisha foleni kama benki ya NMB

6. Mi nimesoma PCM siyo PCB

7. So hata tufungwe mimi ni Asernal siyo Man U

8. Kibonde we ni member wa Loan Board au TCU

9. Nchi imeuzwa vigogo wanatuita ATM

10. Tuwakemee mafisadi wote wa CCM

11. Kuvua gamba haiwasafishi mbele ya CUF

12. CHADEMA mwone Makamba, JK kwa TFF

13. Sihitaji dancer wala mapanga yale ya TMK

14. Show zangu siyo longolongo zile za Y2K

15. Na siyo bandia ka Kontena lile la BOT

16. Situkuzi kilicho feki kama TOT

17. Mi ndio Roma ntasimama kama KKT

18. Ahsante Bongo, Macho juu, Nyamongo, TBC

19. Mistari yangu mitamu kama ya TPC

20. Na kwa hizo fomu MC utalazwa KCMC

21. Kodi ya Walalahoi pombe ya TRA

22. Miili yao ndio biashara ndani ya BBA

23. Fataki anatoa mkopo ndani ya TIA

24. Licha ya mimba haina uhakika mpaka DNA

Ubeti wa 2

25. Mwambieni hatukuogopa tabiri za Shekhe Yahaya

26. Mauti yangetufika bila kumpinga Jakaya

27. Sisaliti sirudishi kadi ya chama kama Nakaaya

28. Bado hainiingii akilini hukumu ya Babu Seya

29. (Mgonjwa anakufa mapokezi Doctor anakunywa valuer

30. Wazazi wanakufa labour wengine ICU) x2

31. Waambieni mi mzalendo na hii ndio mbiu ya mgambo

32. TANESCO wakizima umeme upitishe mzigo wa magendo

33. Harakati za Doctor Leakey katika kuinua michezo

34. Mama Terry wamemsaliti Mwasiti wamempa tangazo

35. Lady Pepeta hawavai msema kweli Semunge

36. Mipira hawaitumii eti kwa Babu kuna kikombe

37. Mafuta wanapandisha bei kisa wanaamini misheni

38. Wachina wanapewa tenda si tunanyimwa vibali

39. Gongo la Mboto wanalia misaada wamewatapeli

40. Wandugu bwaga manyama ayaokote Magufuli

41. Pesa za ujenzi wa shule kala na mkewe headmaster

42. Thamani ya mabango ya kampeni somesha watoto VETA

43. Wanajiuliza Doctor Slaa ni wapi anapata data

44. Hata kama nimevaa mlegezo ikulu napiga chata

45. Ikulu imejaa vibaka Manzese wanawakamata

16 Noah ni aina ya basi dogo (minibus) ambazo ni maarufu sana nchini Tanzania. Hutumiwa na watu mbalimbali kama gari

za kutembele. Aina hii ya magari huaminika kuwa ndio yanayotumika zaidi katika kuwahonga wanawake ili watoe penzi.

76

46. Makahaba wanaongezeka boom zinapokata

47. Wanauziana minada mali za serikalini

48. Mhasibu anacheck porno si tumepanga foleni

Ubeti wa 3

49. Ma MC wanapata stress Roma akitua Ubungo

50. Tanga nilifunga tatu nafunga tano hapa Bongo

51. Wanafuga rasta ili wapate mademu wa kizungu

52. We Mchaga kauze mitumba muziki ushakufunga pingu

53. Mistari yako myeusi unaipaka Carolite

54. Katiba siyo msahafu my people need copy...

55. Ndoto zangu kitambo zilikuwa nije kuwa padri

56. Zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa weed

57. Naenda church naanguka tena nasali

58. Na popote utakaponiona shingoni nimevaa rozali

59. Mi natafuta hela ya kula we unamcheck tu Alehandro

60. Unadhani utaandika nini kama siyo hadithi za Kemondo?

61. Kama hauna kipaji kamuone Babu wa Loliondo

Chanzo: Roma (2011), Mathematics

Katika wimbo huu unaoonekana wazi kuwa kabla ya kuurekodi ulitungwa papo kwa papo

kutokana na sifa simulizi zinazobainika, una utata mkubwa kimantiki na kiushikamani. Tunaona visa

anavyovisimulia vimetawanyika na havina ushikamani. Katika ubeti wa kwanza tunaona ni kama visa

hivyo vimepachikwa tu ili kuleta urari wa vina. Kwa mfano, visa vinavyoelezwa katika mstari wa 1-6

havihusiani na kisa kinachoelezwa katika mstari wa 8 na pia visa vyote hivyo havihusiani na kile

kinachoelezwa katika mstari wa 9-12. Pia kinachoelezwa katika mstari wa 9-12 hakina ushikamani

wala uhusiano na kinachoelezwa katika mstari wa 13-20. Hali hiyo inaonekana katika mistari mingine

na beti zingine za wimbo huu.

Mbali na aina hii ya utungaji kuongozwa na fomula na topo, tunaona kuwa hata utungaji wa

nyimbo nyingine zilizorekodiwa, wasanii hawa huongozwa na fomula ambayo huwasaidia kukariri

wakati wa uwasilishaji wa ushairi wao jukwaani. Msanii huweza kuwa na albamu kumi ambapo kila

albamu huwa na nyimbo hadi kumi na mbili lakini huwa na uwezo wa kuziimba nyingi kati ya nyimbo

hizo jukwaani bila kusoma mahali. Katika hali ya kawaida ni vigumu kukariri nyimbo nyingi kiasi

hicho. Vilevile, nyimbo hizo zina marudio mengi hata yasiyo ya lazima wakati mwingine, hivyo

tunadhani kwamba hata utungaji wa nyimbo hizo huongozwa na fomula simulizi. Mfano mzuri wa

nyimbo ambazo tunadhani kwamba zinaongozwa na fomula ni pamoja na wimbo wa Prof. Jay, “Jina

Langu” na wa Sister P “Sisi Tulivyo” kama inavyonukuliwa hapa chini:

WIMBO WA JINA LANGU

1. Jina langu linavuma, kwenye mitaa

2. Jina langu lina uwezo wa kisupastaa

3. Jina langu linaongeza idadi ya maadui

4. Wengine nawatambua wengine siwatambui

5. Jina langu

Chanzo: Prof. Jay (2003), Mapinduzi Halisi

WIMBO WA SISI TULIVYO

1. Sisi tulivyo kama utakavyoniona ndio nilivyo

2. Mimi nilivyo siko sawa na jinsi ulivyo

3. Mimi nilivyo hata unavyodhani sivyo nilivyo

4. Mimi nilivyo huwezi kunitambua jinsi nilivyo

5. Mimi nilivyo na huu ndio ukweli wa jinsi nilivyo

6. Mimi nilivyo siyo sawa na manabii jinsi walivyo

7. Mimi nilivyo nina hekima kuliko mtu mzima alivyo

8. Mimi nilivyo na hadhi zaidi ya wafalme jinsi walivyo

9. Mimi ni mchamungu kuliko ulivyo

10. Mimi nilivyo napenda mademu jinsi walivyo

Chanzo: Omari (2009:295-296)

Katika nyimbo hizo hapo juu tunaona kuwa kuna marudio mengi ambapo maneno, virai, vishazi na

sentensi vimerudiwa, kunyambuliwa au kupinduliwa. Katika wimbo wa “Jina Langu,” kwa mfano,

77

tunaona kirai “jina langu” kimerudiwa sana wakati katika wimbo wa “Sisi Tulivyo” tunaona kirai

“mimi nilivyo” kimerudiwarudiwa sana.

(ii) Utungaji wa Kabla ya Tukio katika Ushairi wa Bongo Fleva

Mbali na utungaji wa papo kwa papo, ushairi wa Bongo Fleva huweza pia kutungwa kabla ya

uwasilishaji wake. Ushairi wa Bongo Fleva huweza kutungwa kabla ya utendaji wake na kukaririwa,

kuandikwa au kurekodiwa. Utungaji huu ndio maarufu zaidi miongoni mwa wasanii wa ushairi huu.

Utungaji huu huchukua muda kutungwa na huandikwa na kukaririwa kabla ya kuimbwa. Kasonga

(2011:10) anabainisha wazi kwamba kutunga mashairi ya Bongo Fleva kunachukua muda mrefu sana

na kunahitaji umakini. Msanii huwa na wazo kichwani, halafu huanza kuliandikia mashairi yake na

hatimaye huyapeleka studio kwa ajili ya kutengenezewa mapigo (beats) na mtayarishaji wa muziki.

Kufikia mwaka 2011, gharama za kutengeneza wimbo studio zilikuwa ni kuanzia laki mbili na

kuendelea kutegemea na aina na ubora wa studio (Mwanjoka, 2011:14). Gharama kama hizi tulitajiwa

pia na Prof. Jay katika mahojiano yetu. Kazi hii ya kutunga mashairi ya Bongo Fleva huchukua muda

kulingana na uwezo wa msanii husika. Kwa mfano, katika mahojiano yetu msanii Kulwa Felician

Pongwa (a.k.a Black wa Uswazi) tuliyoyafanya tarehe 19/05/2011 alitueleza kwamba hutumia kati ya

siku tatu hadi wiki nzima kutunga wimbo ukakamilika. Lakini Adili Nkwera (a.k.a Hisabati) alidai yeye

huchukua kati ya siku moja hadi nne.

Vilevile katika utungaji wa mashairi ya Bongo Fleva kuna wasanii wanaotunga wenyewe na

kuna wale wanaotungiwa na watu wengine halafu wao huyanunua mashairi hayo pamoja na hakimiliki

yake. Ramadhani Mponjika katika mahojiano yetu alituambia kwamba wapo pia wasanii wanaotunga

wenyewe na kujiandalia na mapigo na hivyo kumwelekeza mtayarishaji wa muziki mapigo ya

kuyaweka katika nyimbo hizo. Mwanamuziki Abasi Hamisi (a.k.a Twenty Percent) akihojiwa na

www.Bongo Celebrity.com anathibitisha hili:

Mimi binafsi huwa napenda sana kufanya kazi na producer ambaye ananipa pia muda wa

kuzungumza na kuchangia katika uboreshaji wa kazi nzima kwa sababu mimi ninapotunga wimbo

huwa natunga pia kila kitu mfano beats, chorus, mpangilio wa ala nk. Kwa hiyo huwa napenda

kupata producer ambaye pia ananisikiliza. Nashukuru Mungu kwamba producers wangu

ninaofanya nao kazi tunashirikiana vizuri kabisa katika kuhakikisha kwamba kitu kinachotoka ni

katika kiwango cha kueleweka na kukubalika.

(b) Utendaji wa Ushairi wa Bongo Fleva

Kipengele kingine cha fani ni utendaji. Katika kipengele hiki tutachambua mambo kama fanani wa

ushairi wa Bongo Fleva, hadhira ya ushairi huo, mavazi na vifaa vinavyotumika katika utendaji wa

ushairi huu, malipo ya utendaji na sauti inayotumika katika utendaji wa ushairi wa Bongo Fleva.

Tuanze na kipengele cha kwanza, fanani wa ushairi wa Bongo Fleva.

(i) Fanani wa Ushairi wa Bongo Fleva

Ushairi wa Bongo Fleva huimbwa au kughanwa na wanawake na wanaume. Wasanii wa kike wa

ushairi huu ni pamoja na Happiness Thadei (Sister P), Zainabu Lupangule (Zay B), Judith Wambura

(Lady Jaydee), Estalina Sanga (Lina), Rehema Chalamila (Ray C) na Khadija Shaaban (Keysha) kwa

kuwataja wachache tu. Kwa upande wa wasanii wa kiume kuna Joseph Mbilinyi (Mr. 2), Selemani

Msindi (Afande Sele), Joseph Haule (Prof. Jay), Abdul Sykes (Dully Sykes) na wengineo.

Zaidi ya kubaini kwamba ushairi wa Bongo Fleva hutendwa na wanaume na wanawake, wasanii wa

kiume wanaoimba au kughani mashairi haya ni wengi kuliko wanawake. Kwa mfano, tunaona kuwa

hakuna msanii wa kike hata mmoja ambaye alikuwa maarufu katika muziki huu miaka ya 1990

mwanzoni. Wanamuziki wa kike wa awali walianza kuonekana mwishoni mwa miaka ya 1990 na

mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo tuliona wanamuziki kama vile Zay B, Sister P, Dataz, Lady

Jaydee na Stara Thomas. Idadi hii ni ndogo sana ikilinganishwa na idadi ya wasanii wa kiume katika

kipindi hicho hicho (Mwanjoka, 2011:14).

Uchache wa wanawake katika muziki huu unatokana na ukweli kwamba wanawake

wanakabiliwa na changamoto nyingi ili waweze kudumu katika muziki huu. Katika mahojiano yetu na

msanii aitwaye Ramadhani Mponjika alitufahamisha kwamba kikwazo kikubwa cha wasanii wa kike

kudumu katika muziki huu ni watayarishaji wa muziki na mapromota. Anadai kwamba watayarishaji

78

wa muziki na mapromota huwataka kimapenzi wasanii wa kike ili waweze kuwasaidia kimuziki. Pindi

wanapokataa hufanyiwa fitina na hivyo nyimbo zao kutopigwa redioni na katika televisheni na pia

kutopata maonyesho. Hatimaye wanamuziki hao wa kike hupotea katika muziki. Mawazo kama haya

yametolewa na msanii Vumilia Abrahamu alipohojiwa na Fiesta (2011a:25-27). Anasema, “…wengi

wa wasanii wa kike wanakatishwa tamaa na kazi hii kwa sababu unapoanza muziki kila unayekutana

naye mbele yako anakutaka kimapenzi na kama utakuwa huna msimamo unaweza ukatoa ngono kwa

kila mtu.” Lakini kwa upande wake Vumilia anasema kwamba yeye anakuwa na msimamo, kwa

sababu, anapokwenda studio anakuwa na pesa yake mkononi na mtu anapomwambia suala hilo

anamwambia ukweli kuwa niko kazini sijafuata ngono. Mwanamuziki huyo anasema, “Unapotoa ngono

kwa kila mtu thamani yako inashuka sababu wanapokupata wote wanaenda kukutangaza kuwa wewe

hujatulia.” Zaidi ya kubainisha kuwapo kwa tatizo hilo, msanii huyu anatoa suluhisho kwa wasanii wa

kike kwenda studio wakiwa na hela zao za kurekodia ili kukwepa mtego huo.

Mbali na kikwazo hiki, kipo kikwazo cha kijamii. Wanajamii kwa kiasi kikubwa wanauona

muziki wa Hip hop kuwa ni muziki wa wanaume na hasa wahuni na hivyo mwanamke anapojiingiza

katika muziki huu huanza kuonekana kuwa ni muhuni na asiye na maadili. Kutokana na hilo, wanawake

wengi wenye uwezo na kipaji wameamua kutojiingiza katika muziki huu (Fiesta, 2011a:25-27). Hivyo,

tunaweza kusema kwa hakika hapa kwamba, ingawa kwa kiasi kikubwa fanani wa ushairi wa Bongo

Fleva ni wanaume wapo pia wanawake wachache ambao ni fanani wa ushairi huu.

Mbali na fanani wa kike kuwa wachache, jambo lingine linaloonekana ni kuwa fanani wa ushairi

wa Bongo Fleva anaweza kuwa mtu mmoja au kikundi. Katika sehemu hii tutapitia aina hizi mbili za

fanani wa ushairi wa Bongo Fleva, msanii mmoja kama fanani na kikundi cha wasanii kama fanani.

(ii) Msanii mmoja kama Fanani

Fanani wa ushairi wa Bongo Fleva, kwa kiasi kikubwa, ni msanii mmoja mmoja. Msanii huyo

huweza kutunga nyimbo zote mwenyewe au kutungiwa na watunzi wengine na yeye hununua mashairi

na hivyo hakimiliki ya nyimbo hizo hubaki kwa msanii huyo hadi atakapoamua vinginevyo. Msanii

huyu, kwa kawaida, anatumbuiza kwa mtindo wa kupiga sidii na kuimba kwa kufuatisha (playback).

Wasanii hawa hawawezi kupiga muziki moja kwa moja (live) kwani msanii mmoja hawezi kupiga

kinanda, gitaa, ngoma na vifaa vingine kwa pamoja. Wakati mwingine wasanii hawa hukodisha

wachezaji (dancers/shakers) ambao hucheza pamoja nao. Wengi wa wachezaji hawa si wa kudumu bali

hukodiwa kwa ajili ya shughuli maalumu na kisha kuwalipa. Mchezaji mmoja huweza kukodiwa na

wasanii mbalimbali wa ushairi huu kwa nyakati tofauti.

(iii)Kundi la Wasanii kama Fanani

Zaidi ya fanani wa ushairi wa Bongo Fleva kuwa msanii mmoja, kuna uwezekano wa kundi la

wasanii kuwa fanani. Kundi hili huweza kuwa mkusanyiko tu wa wasanii wanaoimba au kughani

ushairi wa Bongo Fleva kwa pamoja au msanii mmoja aliyeanzisha bendi na kuwakusanya wasanii

mbalimbali na kuwaajiri kama wafanyakazi wake. Miongoni mwa vikundi vya wasanii vilivyopo na

vilivyowahi kuwapo Tanzania ni pamoja na Kwanza Unit, Hard Blasters, Daz Nundaz, East Coast

Team, Wakilisha, Wateule, TMK Wanaume Halisi na TMK Wanaume Family. Vingi kati ya vikundi

hivi vilikufa na wanamuziki kuanza kuimba kwa kujitegemea. Kwa mfano, kuvunjika kwa Hard

Blasters ndiko kulimfanya Prof. Jay kujitegemea. Aidha, kuvunjika kwa Gangwe Mob ndiko

kulikomfanya Inspector Haroun kujitegemea na pia kuvunjika kwa Inafrika Group ndiko kulikowaibua

Banana Zoro, Bob Rudala na Bizman.

Baada ya makundi mengi kati hayo kuvunjika wasanii wakaanza kuimba mmoja mmoja kwa

kujitegemea. Hata hivyo, bado yalibaki makundi machache ambayo, zaidi ya migogoro ya mara kwa

mara miongoni mwa wasanii wake, yameendelea kudumu. Makundi hayo ni pamoja na TMK Wanaume

Family, TMK Wanaume Halisi na Tip Top Connection. Vilevile, wasanii, mbali na kuwa na makundi

yao, huweza kutoa albamu zao kwa kujitegemea. Zaidi ya makundi haya ya wasanii, katika siku za hivi

karibuni kumekuwa na uanzishaji wa bendi za muziki wa kizazi kipya. Miongoni mwa bendi za muziki

wa Bongo Fleva zilizoanzishwa ni kama vile Top Band inayoongozwa na Khalid Mohamed a.k.a TID

(Top In Dar), B-Band inayoongozwa na Banana Zorro na Machozi Band inayoongozwa na Judith

Wambura a.k.a Binti Machozi. Hii ni aina mpya ya fanani wa muziki wa Bongo Fleva ambayo imeanza

79

kuonekana miaka ya 2007 nchini Tanzania. Bendi ya Kwanza kuibuka ni Top Band. Kundi la wasanii

kama fanani wa ushairi wa Bongo Fleva, lina faida moja kubwa kwamba wasanii huweza kubadilishana

uzoefu na kuunganisha juhudi zao na kufanya kazi bora zaidi. Ikifafanua hili

http://spotistarehe.wordpress.com inasema:

Nakubaliana na kila mmoja wao kwenda solo (kuimba kwa kujitegemea) kwani inampa uwanja

mpana zaidi lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa kwenye makundi siku zote kila mmoja ana nafasi

yake, kuna wengine wanajua sana kupanga sauti wengine kupanga vina na wengine kupanga

mpokezano. Mfano kwenye bendi ya Wenge Muzika wakati huo kulikuwa na mtu anaitwa Blaise

Bulla kwenye wimbo utamsikia akiimba verse (mstari) moja tu ila kazi yake kubwa ilikuwa

kupanga sauti na wakati mwingine hata kushauri kuwa beti hii haifai kuimbwa na wewe, ikiimbwa

na fulani italeta mguso zaidi (Ufafanuzi wetu).

Mbali ya kuwa na msanii mmoja au kikundi cha wasanii kama fanani, kwa kiasi kikubwa fanani

wa ushairi wa Bongo Fleva ni vijana. Ushairi huu, na muziki wa Bongo Fleva, kwa ujumla, ni wa

vijana (Suriano, 2006; 2007; Omari, 2009; Mwanjoka, 2011). Akielezea muziki wa Bongo Fleva na

vijana, Mwanjoka (2011:102 -103) anasema:

Muziki huu wa kizazi kipya umefanikiwa kwa kiasi fulani kuwakomboa vijana wengi wa

Tanzania waliokuwa kwenye hali mbaya kimaisha…kabla ya muziki huu vijana wengi walikuwa

hawana kazi na walikuwa wakishinda vijiweni na kupoteza muda wao kwa kuvuta sana

bangi…baada ya muziki huu wa kizazi kipya kushamiri nchini Tanzania …vijana hao waliokuwa

wanakaa mitaani bila ya shughuli maalumu walipata ajira za uhakika.

Kutokana na muziki huu kuwa na fanani vijana ndipo jina la muziki wa kizazi kipya, yaani muziki wa

vijana, lilipopatikana.

(iii) Hadhira ya Ushairi wa Bongo Fleva

Kipengele kingine cha utendaji wa ushairi wa Bongo Fleva ni hadhira. Hadhira ya ushairi wa

Bongo Fleva ni mwanajamii yeyote. Ushairi huu huimbwa au kughanwa katika vituo mbalimbali vya

redio na televisheni nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kupitia kanda na sidii

zilizorekodiwa. Miongoni mwa vituo maarufu vya redio vinavyopiga ushairi huu ni pamoja na vituo

vya redio vilivyopo katika jiji la Dar es Salaam kama vile Clouds Radio, Radio One, East Africa Radio,

Capital Radio, Times Fm, TBC Taifa, TBC Fm na Redio Uhuru. Vingine ni vituo vya redio vilivyopo

katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kama vile Radio Free Africa, Kiss Fm (Mwanza), Bomba Fm

(Mbeya), Kashozi Radio (Bukoba), Aboud Radio (Morogoro) na kadhalika.

Aidha kwa upande wa vituo vya televisheni vinavyopiga muziki huu ni pamoja na vile

vilivyoko Dar es Salaam kama Clouds TV, East Africa TV, Capital TV, ITV, TBC1, C2C, CTN,

Channel Ten na DTV. Vituo vingine vya televisheni ni vilivyoko nje ya Dar es Salaam kama Star TV

(Mwanza), Aboud TV (Morogoro) na kadhalika. Kwa upande wa Kenya, kuna vituo vya televisheni

kama Citizen TV, KTV, KBC na kadhalika ambavyo hupiga muziki huu. Katika nchi ya Uganda na

nchi nyinginezo za Afrika Mashariki na hata nje ya Afrika Mashariki, pia kuna vituo vya redio na

televisheni mbalimbali ambavyo vinapiga muziki huu. Vituo hivi vya redio na televisheni husikika na

kutazamwa katika mahoteli, mabaa, magari ya usafiri kama vile madaladala/matatu na mabasi ya

mikoani na katika maeneo mengine. Kwa hiyo, hadhira ya muziki huu ni pana. Hata hivyo, hadhira hii

si shiriki, ni hadhira mfu. Hadhira ya ushairi wa Bongo Fleva, kwa kiasi kikubwa, haiwezi kushiriki

katika utendaji wa ushairi huo. Hii inatokana na ukweli kwamba kwa kiasi kikubwa ushairi wa Bongo

Fleva umerekodiwa katika kanda na sidii. Hadhira ya ushairi wa Bongo Fleva inaweza kushiriki iwapo

ushairi huo unatendwa katika maonyesho, ambapo mashairi hayo huimbwa au kughanwa katika kumbi

mbalimbali za muziki. Akifafanua juu ya ushiriki wa hadhira katika muziki wa Bongo Fleva, Omari

(2009:82) anasema:

An artist also involves his/her audience in singing or joining in the chorus by pointing out the

microphone to them, or s/he may pause the CD briefly for the audience to sing out loud. The

audience can also be required to jump…

Msanii huweza kuishirikisha hadhira yake katika uimbaji au kwa kuitikia kwa kuielekezea kipaza

sauti, au anaweza kuisimamisha sidii kwa muda mfupi ili hadhira ishiriki kuimba. Pia hadhira

inaweza kutakiwa kucheza... (Tafsiri yetu).

80

Hapa Omari alikuwa anazungumzia jinsi wasanii wa Bongo Fleva wanavyoishirikisha hadhira yao

katika maonyesho ya moja kwa moja (live performance).

(iv) Mavazi katika Utendaji wa Ushairi wa Bongo Fleva

Kipengele kingine muhimu katika ushairi wa Bongo Fleva ni mavazi. Suala la mavazi katika

ushairi wa Bongo Fleva ni jambo ambalo limezua utata mkubwa. Omari (2009:60-62) anaeleza

kwamba muziki wa Bongo Fleva umekuja na mavazi ya aina yake. Hapa anaibua dai kwamba muziki

huu una mavazi maalumu. Anaendelea kudai kwamba, kwa kuwa muziki wa Bongo Fleva unahusisha

zaidi vijana, mavazi yanayovaliwa zaidi ni yale yanayovaliwa na vijana. Anayataja mavazi

yanayovaliwa katika muziki wa Bongo Fleva kuwa ni pamoja na mavazi yanayofanana na yale

yanayovaliwa na wana Hip hop wa Kimarekani. Kwa mujibu wa Omari, mavazi hayo ni yale yenye

nembo mbalimbali kama vile FUBU (For Us By Us), Calvin Clein (CK), Timberland na kadhalika.

Mavazi hayo pia yanajumuisha makoti makubwa na makoti mazito bila kujali hali ya joto iliyopo nchini

Tanzania (Omari, 2009:61). Mavazi mengine yanayovaliwa na wanamuziki wa Bongo Fleva ni suruali

pana za jeans, mashati makubwa, mikufu, hereni, saa kubwa za mkononi, mavazi ya kijeshi, viatu

vikubwa na kadhalika. Zaidi ya mavazi hayo ya kuiga, Omari (2009:65) anabainisha kwamba wapo pia

baadhi ya wasanii ambao huvaa mavazi asilia ya Kitanzania. Anatoa mfano wa wasanii hao kuwa ni

Mr. Ebbo ambaye anavaa mavazi ya Kimasai. Msanii mwingine anayevaa mavazi ya asili ni Mrisho

Mpoto a.k.a Mjomba.

Ingawa imeelezwa kwamba muziki wa Bongo Fleva una mavazi maalumu, hata hivyo, suala

hilo lilikuwa muhimu wakati muziki huu unaanza. Wakati huo wanamuziki wa Bongo Fleva waliiga tu

kutoka nje bila kujua chimbuko la mavazi hayo. Haskins (2000:49) anathibitisha hili kwa kueleza

kwamba wanamuziki wa Bongo Fleva walivaa suruali “mlegezo”17 kutokana na kutojua kwamba uvaaji

huo unatokana na ukweli kwamba wasanii wengi wa Marekani walifungwa jela. Wakiwa magerezani

walivuliwa mikanda na hivyo suruali zao kuanza kushuka mpaka makalioni. Walipotoka jela

walionekana kama “wajanja” na hivyo, ili kujitambulisha kwamba wao ni “wagumu” waliotoka jela,

waliendelea kuvaa mavazi hayo. Baadhi ya wanamuziki wa Bongo Fleva walipobaini hili, uvaaji wa

aina hii ulipungua kutokana na ukweli kwamba kwenda jela si suala la kujivunia nchini Tanzania na

katika nchi nyingine za Afrika Mashariki. Ukweli huu unathibitishwa na msanii Black wa Uswazi

ambaye katika mahojiano yetu alisema:

wanamuziki wengi hawakujua kwamba ile style ya kuvaa mlegezo ilianzia gerezani kule

Marekani. Wanamuziki wengi wa Marekani walianza muziki baada ya kupambana na maisha ya

gerezani kwa kuwa walipotoka walionekana wajanja na wagumu. Walivuliwa mikanda ili

wasijiue. Kwa hiyo ilipojulikana hivyo wengi siku hizi wanaona milege (milegezo) siyo dili

(jambo la maana) (ufafanuzi wa kwetu).

Jambo hili linaonesha kwamba mavazi katika muziki wa Bongo Fleva ni jambo linalobadilika

badilika. Hadi sasa bado kuna wanaovaa mavazi hayo, ingawa tunakubali kwamba uvaaji huo

umepungua sana. Pia wapo wanaovaa mavazi mengine kama suti, nguo za kushona na kadhalika. Kwa

upande wa wanamuziki wa kike, wengi wao huvaa mavazi yanayoacha sehemu kubwa ya maungo yao

ya siri nje (nusu uchi) lakini wapo pia wanaovaa mavazi ya kujisitiri japo ni wachache. Katika

mahojiano yetu na baadhi ya wasanii walitueleza kwamba uvaaji huu hulenga kuwavutia wanaume.

Huu ni uthibitisho kwamba kazi za fasihi hubadilika kulingana na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa,

kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Kwa ujumla, tunaweza kusema kwamba, muziki wa Bongo Fleva

kwa sasa hauna mavazi maalumu. Kila msanii anavaa anavyojisikia, labda pia kulingana na mahali

anapotumbuiza na hadhira iliyohudhuria.

(v) Vifaa vya Utendaji katika Ushairi wa Bongo Fleva

Vifaa ni kipengele kingine muhimu katika ushairi wa Bongo Fleva. Kuna aina mbili za utendaji

wa ushairi wa Bongo Fleva, utendaji wa kufuatisha (playback) na utendaji wa moja kwa moja (live

17 Mlegezo (au kifupi mlege) huitwa pia katakundu (au kifupi kata K). Huu ni mtindo wa uvaaji ambapo suruali huvaliwa

lakini ikiwa inaacha nusu ya matako nje. Hata hivyo matako hayo huweza kusitiriwa na bukta au chupi ambayo huvaliwa

ndani. Katika mtindo huu wa uvaaji chupi au bukta iliyovaliwa ndani huweza kuonekana.

81

performance). Katika utendaji wa kufuatisha kifaa ambacho msanii anahitaji kuwa nacho ni sidii (CD)

tu iliyorekodiwa nyimbo zake. Waandaaji wa matamasha na maonyesho ndio wana jukumu la kuandaa

vifaa vingine kama vipaza sauti, vicheza sidii (CD Players), spika (speakers), amplifaya (amplifiers) na

vifaa vingine vya aina hiyo. Katika utendaji huu msanii huweka sidii katika kicheza sidii na kisha

kuanza kuimba kwa kufuatisha kuimba wimbo ulioimbwa na sidii (Haskins, 2000:110-115; Omari,

2009:80). Kimsingi, sauti inayosikika katika spika ni ile ya sidii iliyorekodiwa na hivyo msanii

anachofanya ni kuigiza kuimba wakati kiuhalisia sauti yake haisikiki. Utendaji huu ndio asilia na

umetumika kwa muda mrefu zaidi. Katika utendaji huu msanii hakuhitaji wasaidizi wengi katika

utendaji wake, mara nyingi mtendaji alikuwa msanii mwenyewe. Haskins (2000:114) na Omari

(2009:80) wanabainisha kwamba utendaji wa aina hii unaufanya muziki wa Bongo Fleva na Hip hop

kuwa muziki wa gharama ndogo katika uzalishaji na uwasilishaji. Jambo hili ndilo limesababisha kuwa

na idadi kubwa ya wanamuziki wa Bongo Fleva kuliko idadi ya wanamuziki katika miziki kama

taarabu na muziki wa dansi. Aidha, jambo hili ndilo limewafanya wanamuziki wapya wa Bongo Fleva

kuibuka kila siku.

Hata hivyo, kutokana na maendeleo, utendaji wa ushairi wa muziki huu ukabadilika na

kumeibuka utendaji wa moja kwa moja (live performance). Ulianza kwa msanii kutengenezewa mapigo

tu na kuingiza sauti moja kwa moja akiwa jukwaani huku akisaidiwa kucheza na wachezaji (dancers)

na kukua hadi uanzishwaji wa bendi. Katika bendi, msanii/wasanii huwa na vyombo mbalimbali vya

muziki kama vile magitaa, vinanda, tumba, matarumbeta na kadhalika ambavyo hutoa mapigo ya

kimuziki na msanii/wasanii kutia sauti wakiwa jukwaani. Aidha, kunakuwa na wachezaji ambao

wananogesha utendaji huo. Utendaji wa moja kwa moja, kwa hiyo, unahitaji vifaa vingi zaidi kuliko

utendaji wa kufuatisha. Utendaji huu ni ghali na unahitaji uwezo mkubwa kifedha na kimuziki. Ili

msanii aweze kuanzisha bendi atahitaji vifaa na wasanii wa kuvipiga vifaa hivyo. Wasanii hawa

atapaswa kuwalipa mishahara ili waweze kuishi. Hii ni tofauti na utendaji wa awali. Hata hivyo, zaidi

ya gharama, utendaji huu ni bora kwani ushiriki wa hadhira ni mkubwa na pia kuna nafasi ya kufanya

mabadiliko kulingana na mazingira.

(vi) Malipo katika Utendaji wa Ushairi wa Bongo Fleva

Kipengele kingine cha utendaji kitakachojadiliwa hapa ni malipo katika utendaji wa ushairi wa

Bongo Fleva. Muziki wa Bongo Fleva umetoa ajira kwa vijana wengi. Vijana wengi wamejiingiza

katika muziki huu ili kupata kipato cha kuwawezesha kuishi (Mwanjoka, 2011:102-104). Kwa hiyo,

suala la malipo ni suala muhimu sana katika ushairi wa Bongo Fleva. Wasanii wa ushairi huu hughani

au kuimba nyimbo zao ili kujiingizia kipato. Hivyo, sehemu kubwa ya malipo wanayoyapata wasanii

hawa ni fedha. Fedha hizo huwawezesha kununua magari ya kifahari, nguo za gharama kubwa, vidani

vya thamani, pombe, madawa ya kulevya na wanawake (mademu) ambavyo vinaonekana kupendwa

sana na wasanii hawa (Omari, 2009; Mwanjoka, 2011).

Hata hivyo, matumizi haya ya vilevi kama pombe na madawa ya kulevya, katika ushairi wa

Bongo Fleva si kitu kigeni. Tunaona hata katika tanzu nyingine za fasihi simulizi na hasa majigambo ya

jadi mjigambi alikunywa pombe kabla ya kujigamba na baada ya kujigamba aliweza kupewa pombe

kama zawadi kwa ujigambi wake. Aidha, suala la wasanii wa Bongo Fleva kutumia fedha wanazozipata

kutafuta wapenzi si geni kwani hata katika majigambo ya jadi, msanii aliyejigamba vizuri aliweza

kupewa mwanamke (Rubanza, 1994; Mulokozi, 1996; Peek na Kwesi, 2004). Tofauti inayoonekana

hapa ni kwamba katika ushairi wa muziki wa Bongo Fleva wasanii wamesahau kunywa kiasi kidogo tu

ili wasiharibu kazi. Wamesahau Amarwa tigombeka,18 yaani pombe haijengi (Alipo, 2011; Musa,

2011).

Mbali na kupata fedha kama malipo ya utendaji wa ushairi wa Bongo Fleva, kuna unyonyaji

mkubwa katika utoaji wa malipo kwa wasanii wa ushairi huu. Mapromota na watayarishaji wa muziki

huwanyonya wasanii na hivyo wasanii wengi kuwa na hali ngumu kiuchumi (Omari, 2009; Abby na

Billy, 2011; Mwanjoka, 2011). Abby na Billy (2011:9) wakithibitisha hili wanasema:

Last week tulieleza jinsi magwiji wa Bongo Fleva walivyokwama nauli ya kurudi Dar wakitokea

Dodoma…..Inatia uchungu kwa sababu magwiji hao wameshafanya kazi kubwa ambayo ingetosha

18 Huu ni usemi maarufu katika majigambo ya Kihaya ambapo zaidi ya wasanii kupewa zawadi ya pombe, walizingatia

kuwa pombe haijengi. Hivyo walikunywa kiasi kidogo tu.

82

kuwapa utajiri na heshima. Walitakiwa kwenda Dom kwa ndege au wangeendesha magari yao,

ingeshindikana wangekodishiwa basi dogo ambalo lingewapeleka na kuwarudisha. Tukasema

muziki hauwalipi wasanii inavyotakiwa ndio maana hali hiyo ilitokea, kwani magwiji hao

wangepata chambi za kutosha hata mapromota uchwara wasingesogea. Mfano ni huyo wa Dom

(wa Dodoma) ambaye alilipa nauli ya kuwapeleka lakini akakosa ya kuwarudisha kwa sababu eti

geti halikutoa mavuno ya kutosha.

Hapa wanathibitisha hali mbaya za wasanii wa ushairi wa Bongo Fleva kiuchumi hadi kufikia kuwa

ombaomba. Hata hivyo, wanaona hali hiyo mbaya imetokana na wasanii kunyonywa na mapromota,

wasambazaji na watayarishaji wa muziki. Wasanii wenyewe wakihojiwa na Abby na Billy wanamtaja

mmoja wa mapromota kuwa mnyonyaji. Wanasema, “anatufanya tufikirie kazi nyingine wakati muziki

ndio ajira yetu. Sisi ndio tumepigana mpaka huu muziki ukawa biashara, sasa inakuwaje huu unyonyaji

uendelee?”

(vii) Uchezaji wa Ushairi wa Bongo Fleva

Kipengele kingine cha utendaji katika ushairi wa Bongo Fleva tutakachokijadili hapa ni

uchezaji. Ushairi wa Bongo Fleva ni utanzu wa fasihi simulizi. Kwa kuwa matendo ndio msingi wa

fasihi simulizi, kama tulivyoona hapo awali, ushairi huu una uchezaji unaoenda sambamba na matendo

ya mwili. Aidha, kama tulivyoeleza hapo awali, muziki wa Hip hop, ambao hapa tumeuchukua kama

sehemu ya Bongo Fleva, una nguzo zake. Mojawapo ya nguzo hizo ni breakdancing, uchezaji wa

kujinyonganyonga ambao huitwa pia kuruka majoka. Katika mtindo huu mchezaji hujinyonganyonga

mikono na miguu huku akifuatisha mapigo ya muziki husika. Mtindo huu umetumiwa sana na

mwanamuziki maarufu wa Pop duniani, marehemu Michael Jackson. Kwa hiyo, uchezaji ni mojawapo

ya nguzo za muziki wa Bongo Fleva. Zaidi ya mtindo wa kuruka majoka mitindo mbalimbali ya

uchezaji imeibuka ambayo inatumiwa pia na wachezaji wa majigambo haya. Miongoni mwa mitindo

hiyo ni ule mtindo wa kurusha miguu juu na kuipiga chini kwa nguvu, maarufu kama mtindo wa

timbatimba ambao ni mtindo wa kikundi cha TMK Majita (Omari, 2009:82). Mtindo huu ulianzishwa

na wasanii wa TMK Wanaume Halisi na kuigwa na wasanii wengine wa muziki wa Bongo Fleva na

hata miziki mingine ukiwamo muziki wa injili. Kwa mfano, msanii wa muziki wa injili aitwaye Rose

Muhando katika wimbo wa “Nibebe” ametumia mtindo huu wa uchezaji. Mtindo mwingine wa

uchezaji ni ule uitwao mapanga shaa (Omari, 2009:82) unaotumiwa na TMK Wanaume Halisi. Mtindo

huu hasa unahusisha uinuaji wa mikono na kuigiza kukata kama panga linavyokata mti huku mchezaji

akiwa amejikunja kulalia nyuma.

Mtindo mwingine ni ule uitwao kiduku ambao suala la mwanzilishi wake limezua mjadala

mkubwa. Wapo wanaomuona msanii wa Bongo Fleva Malima Lawrence (Marlaw) kuwa ndiye

mwanzilishi huku wengine wakimuona msanii wa taarabu ya mipasho, Mzee Yusufu wa kundi la Jahazi

Modern Taarabu, kuwa ndiye mwanzilishi (Mussa, 2010b; Michuzi, 2010). Marlaw anatajwa kuwa

mwanzilishi kwa kuwa katika wimbo wake wa “Pii pii” ndipo mtindo huu ulipoanza kuonekana kwa

watu wengi nchini Tanzania.

Kwa upande wa Mzee Yusufu anatajwa kuwa mwanzilishi wa kiduku kutokana na ukweli

kwamba, wapenzi wa taarabu ya mipasho, ambao ni wengi karibu sawa na wapenzi wa Bongo Fleva,

walianza kuuona mtindo huu kwa mara ya kwanza katika nyimbo zake. Aidha, uchezaji wa kiduku wa

Mzee Yusufu ndio unaonekana kuwa bora na kuwavutia watu wengi kuliko ule wa Marlaw. Katika

kundi la Jahazi Modern Taarabu kiduku huchezwa kwa mtu kuchuchumaa akitetemesha miguu huku

mikono imewekwa kama mtu aendeshaye pikipiki au baiskeli na huweza kushuka hadi akafikia kukaa

chini. Mtindo huu ni tofauti na ule unaoonekana kwa Marlaw ambapo wachezaji huchuchumaa na

kutetemesha miguu huku mikono ikiwekwa kama mtu anayeendesha pikipiki au baiskeli lakini

mchezaji hachuchumai hadi chini.

Hata hivyo, tunaona kwamba mwanzilishi wa mtindo huu ni mwalimu na uchezaji kutoka THT

(Tanzania House of Talent) aitwaye Msami Giovann. Mtazamo huu mpya unatokana na ukweli

kwamba katika mahojiano yetu na Msami tulibaini kwamba amekuwa akiutumia mtindo huu tangu

mwaka 2004. Alitufahamisha kwamba mtindo huu hapo awali ulikuwa unaitwa kidupu na ulikuwa

unatumiwa sana na wavuta bangi wa Temeke. Neno “kidupu” ni msimu ambao maana yake ni bangi.

Aidha, Msami alitueleza kwamba mtindo huu aliuona ukitumika sana kwenye ngoma ya mnanda,

83

mojawapo ya miziki ya jadi ya Kizaramo. Hivyo, Msami anasema aliupenda mtindo huo na akaanza

kuwafundisha wanafunzi wake. Maelezo haya ya Msami, yanafanana na maelezo tuliyopewa na Profesa

Jay alipokuwa anauzungumzia mtindo huu wa uchezaji. Profesa Jay anasema, “unajua mimi

nimeufuatilia sana mtindo huu wa kiduku na kugundua kwamba ulianzia kwa wahuni wa Temeke

kwenye ngoma za mnanda. Wewe waangalie wacheza mnanda utaona wanacheza staili ya kiduku.”

Vilevile Giovann alitufahamisha kwamba mwaka 2008 alikodiwa na Marlaw, pamoja na wachezaji

wengine wa THT, kwenda kucheza katika rekodi ya wimbo wa “Pii pii.” Ni hapo ndipo walipoutumia

mtindo huo, na tangu hapo Marlaw akatajwa kuwa ndiye mwanzilishi wa mtindo huo. Jambo hili

linawezekana kutokana na ukweli kwamba, nafasi ya wachezaji katika umiliki wa wimbo haijulikani.

Mchezaji hukodiwa na kulipwa kwa uchezaji wake na kisha msanii huwa na haki miliki ya wimbo,

mapigo, uchezaji na kila kitu katika wimbo husika. Hivyo, Marlaw kutajwa kuwa mwanzilishi wa

kiduku si kitu cha ajabu kwani wachezaji katika video yake, huonekana kama sehemu ya Marlaw.

Kuhusu uchezaji wa kiduku, Mussa (2010b:15) anasema:

Kiduku ni aina mpya ya uchezaji iliyoenea kwa kasi hivi sasa hapa nchini, hususan katika

vitongoji vya miji mikubwa kama lilivyo jiji la Dar es Salaam. Katika uchezaji wa staili hii,

mchezaji hulazimika kuchuchumaa huku akiwa kasimamia ncha za vidole vya miguu na kucheza

kwa kujitetemesha kiufundi akifuatisha mapigo ya muziki. Inasemekana chimbuko la uchezaji wa

mtindo wa Kiduku ni wa uchochoroni, kutoka kwa baadhi ya vijana wenye umri mdogo

walioamua kujifurahisha kwa kubuni staili hiyo ya uchezaji. Kutokana na ubunifu huo ulivyokuwa

unavutia wengi, makundi ya kushindana baina ya vijana kwa vijana yalianzishwa kwa wingi

ambako hadi sasa karibu kila mtaa kuna kundi la Kiduku. Unaweza kusema vijana wetu

wameharibika kila utakayebahatika kumfuma akinengua katika kipindi hiki ni lazima atakuwa

ananengua kwa namna hiyo tu. Hata hivyo kwa wale wanaomudu vilivyo kunengua katika staili

hiyo ya Kiduku, huonekana kivutio kikubwa kiasi cha watu hulazimika kuacha kazi zao na

kuwatazama. Kwa hakika ni uchezaji unaoonyesha dhahiri kuwa umejaa chembe za ufundi hasa,

kutokana na namna wachezaji wenyewe wanavyojinogesha kwa maringo ya kutupa mikono yao.

Aidha, mara nyingine wachezaji wa mtindo wa Kiduku hupindisha migongo yao pamoja na

kuyumbishayumbisha nyonga zao kiufundi huku shingo zao nazo zikinepa kistadi.

Hapa Mussa zaidi ya kueleza jinsi kiduku kinavyochezwa na kilivyo maarufu miongoni mwa

Watanzania, anatueleza pia mabadiliko mbalimbali ya uchezaji wa kiduku. Akifafanua juu ya

mabadiliko hayo na tofauti iliyopo katika uchezaji wa kiduku baina ya Marlaw na Mzee Yusufu, Msami

Giovann anasema:

Mimi nilipoanzisha kiduku kilikuwa hakichezwi vile. Bali mtu alikuwa anachuchumaa na

kutetemesha miguu huku ncha za vidole zimegusa chini na mikono kama mwendesha baiskeli.

Staili (mtindo) hiyo ilikuwa haimtaki mchezaji kuchuchumaa hadi chini. Kuchuchumaa hadi chini

ni staili (mtindo) mpya kwa kweli.

Kwa ujumla, uchezaji wa ushairi wa Bongo Fleva upo wa namna nyingi ikiwa ni pamoja na

kukata viuno, kurusha miguu, kuruka majoka (breakdancing), timbatimba, mapanga shaa, kiduku na

kadhalika. Hata hivyo, ipo mitindo mingine ya uchezaji ambayo bado haijapewa jina ingawa ni maarufu

katika uchezaji wa ushairi wa Bongo Fleva. Jambo la msingi hapa ni kwamba uchezaji katika ushairi

wa Bongo Fleva huigiza matendo yanayoimbwa katika wimbo husika. Hivyo tunaweza kusema

kwamba, uchezaji katika ushairi wa Bongo Fleva huhusisha matumizi ya viungo vya mwili kuiga

matendo. Hii ni sifa muhimu sana katika fasihi simulizi (Finnegan, 1970; Rubanza, 1994; Mulokozi,

1996). Ushairi wa Bongo Fleva, kwa hiyo, ni fasihi simulizi.

(viii) Sauti katika Utendaji wa Ushairi wa Bongo Fleva

Kipengele cha mwisho katika utendaji wa ushairi wa Bongo Fleva ni sauti inayotumika katika

utendaji. Mwanjoka (2011:51 -52) anaeleza kwamba ushairi wa Bongo Fleva, hasa ulikuwa ushairi wa

kughani. Lakini kutokana na mabadiliko na maendeleo, kwa sasa, kuna aina mbili za sauti zinazotumika

katika ushairi wa Bongo Fleva, sauti ya kughani na sauti ya kuimba. Hivyo, tunaweza kusema ushairi

wa Bongo Fleva umegawanyika katika makundi mawili, ushairi ulioghanwa na ushairi ulioimbwa.

Ushairi ulioimbwa hutendwa zaidi na wanawake wakati ambapo ushairi unaoghanwa hutendwa zaidi na

wanaume. Wanamuziki wa kike wa Bongo Fleva wanaoghani (wanaorap) ni kama vile Sister P, Zay B,

84

Nakaaya Sumari na Sarah Kaisi (Shaa). Wanamuziki wa kiume wanaoghani ni wengi na hawa ni

pamoja na Mr. 2, Prof. Jay, Joh Makini, Kala Jeremiah, TMK Wanaume Family, Afande Sele na

wengineo. Wapo pia wanamuziki ambao wanaimba na kughani kwa pamoja. Ushairi wa Bongo Fleva

wa kughani ndio ushairi asilia ya Bongo Fleva. Wanamuziki wanaoghani wanajiona wao ndio bora

kuliko wanaoimba na wamewapa wanaoimba jina la utani “wabana pua,” kwa maana ya kwamba ni

watu wasiojua kuimba ila wanachojua ni kubana pua tu ili kutoa sauti ya kuvutia. Ushairi wa Bongo

Fleva unaoimbwa na ule wa mchanganyiko wa kuimba na kughani ni wa hivi karibuni na ndio

umetokea kupendwa sana na kuwa na soko kubwa. Ushairi wa awali wa Bongo Fleva, katika miaka ya

1980 na 1990, ulikuwa unaghanwa. Sauti ya uimbaji mara nyingi ilijitokeza katika kiitikio tu.

Tunaweza kuthibitisha hili katika nyimbo za Mr. 2, Prof. Jay na wasanii wengine waliokuwepo wakati

huo. Suala la msingi hapa ni kwamba, aina ya sauti inayotumika hutumiwa pia katika kuitofautisha

Bongo Fleva na Hip hop. Wanaotumia kigezo hiki cha sauti kuitofautisha Bongo Fleva na Hip hop,

wanadai kwamba muziki wa Bongo Fleva hasa ni muziki unaotumia zaidi sauti ya kuimba wakati

muziki wa Hip hop unatumia zaidi sauti ya kughani (Suriano, 2006; Mwanjoka, 2011).

(c) Mandhari ya Ushairi wa Bongo Fleva

Mbali na vipengele vya utendaji tulivyovijadili, kipengele kingine cha kifani kinachojadiliwa hapa

ni mandhari. Utendaji wa ushairi wa muziki wa kizazi kipya kwa kawaida ni katika kumbi za starehe au

mandhari maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo. Katika kumbi hizo, mtazamaji (hadhira)

anapaswa kulipia gharama ya kiingilio mlangoni na ndipo anaweza kushuhudia maonyesho. Miongoni

mwa kumbi hizo jijini Dar es Salaam zinazotumiwa na wasanii hawa ni pamoja na Club Bilicanas, Club

San Sirro, Leaders Club, Maisha Club, Sigara TCC, Equator Grill, Mango Garden, Dar Live, Mango

Garden na kadhalika.

Vilevile muziki huu hutendwa katika hoteli mbalimbali maarufu ambapo wateja wa hoteli hizo

hutumbuizwa wakati wanapata vinywaji na vyakula. Karibu kila hoteli na baa maarufu jijini Dar es

Salaam ina siku maalumu ambapo wasanii wa muziki, wasanii wa Bongo Fleva wakiwamo, hualikwa

na kutoa burudani. Katika burudani hizo, wamiliki wa kumbi husika ndio hulipia maonyesho hayo.

Gharama ya wateja ni kununua kinywaji au chakula tu huku mmiliki wa hoteli au baa akiwalipa wasanii

hao. Kwa mfano, katika baa ya Nyumbani Lounge, Jaydee hutumbuiza kila Jumamosi. Banana Zoro na

Bendi yake ya B-Band hutumbuiza katika ukumbi wa Cine Club kila Jumamosi. Naye Vumilia

hutumbuiza katika ukumbi wa Triz Motel kila Jumapili wakati Top Band imekuwa ikitumbuiza katika

Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Hotel ya Serena, zamani ilijulikana kama Movenpick, kila

Jumamosi na kadhalika. Hata hivyo, hoteli hizo huweza kubadilisha wasanii au hata siku za kuwaleta

wasanii na hivyo si jambo la kudumu.

Si hivyo tu, bali pia ushairi wa Bongo Fleva hutendwa katika mandhari maalumu ambapo kuna

shughuli maalumu. Kwa kawaida sehemu hizi huwa si mahsusi kwa ajili ya shughuli hiyo ila mandhari

ya muda kwa ajili ya kutenda ushairi huu huandaliwa ili kutimiza jukumu hilo. Baadhi ya sehemu hizo

ni viwanja vya mipira na viwanja vya mikutano na hasa wakati wa mabonanza au mikutano maalumu

ya kisiasa ya kuhamasisha vitu kama mapambano dhidi ya magonjwa kama vile UKIMWI na malaria,

kupiga kura, kuienzi amani na kadhalika. Sehemu hizi ni pamoja na viwanja vya Jangwani, Biafra,

uwanja wa Mwembeyanga, uwanja wa taifa na viwanja vya posta katika jiji la Dar es Salaam. Viwanja

hivyo katika miji mingine ni pamoja na CCM Kirumba (Mwanza), Sokoine (Mbeya), Kaitaba

(Bukoba), Jamhuri (Morogoro), Amri Abedi (Arusha) na kadhalika (Mwanjoka, 2011:94).

Pia mashairi ya ushairi wa muziki wa kizazi kipya hurekodiwa na kuhifadhiwa katika kanda za

kaseti, sidii za kusikiliza (audio CD), sidii za kuona (video CD) na hata kuwekwa kwenye simu kama

mlio wa kuitia (ringtones/caller tones). Vilevile, mashairi haya huhifadhiwa katika nakala tepe na

kupigwa kwenye kompyuta, simu za mkononi, magari na hata redio za kisasa ambapo wasanii hawapati

malipo yoyote ingawa waingizaji wa nyimbo kwenye nakala tepe hupata fedha.

(d) Muundo wa Ushairi wa Bongo Fleva

Kipengele kingine cha kifani ni muundo. Ushairi wa muziki wa kizazi kipya hauna muundo

maalumu isipokuwa tu mashairi mengi huwa na muundo wa kishairi wa kuwa na beti na mistari.

Muundo mwingine unaoonekana katika ushairi wa Bongo Fleva ni wa kuwa na beti na kiitikio chake na

85

pia muundo wa simulio. Katika sehemu hii tutachambua miundo hiyo tukianza na muundo wa beti,

mistari na kiitikio.

(i) Muundo wa Beti, Mistari na Kiitikio katika Ushairi wa Bongo Fleva

Matumizi ya istilahi “mistari” katika fasihi simulizi yameleta mkanganyiko mkubwa.

Wanafasihi wanaona matumizi ya neno hilo ni sahihi katika fasihi andishi na si katika fasihi simulizi.

Wanafasihi wengi akiwamo Mulokozi (2002) hawakubaliani na matumizi ya neno mstari katika ushairi

simulizi kwani katika usimulizi hakuna mistari. Wanafasihi wengine, kama Kunene (1971)

wakapendekeza dhana kikundi-mpumuo (breath group). Naye Mulokozi anapendekeza wakaa

(duration) kama kipimo cha urefu wa ushairi. Hata hivyo, kwa kuwa mashairi mengi ya Bongo Fleva

huandikwa kwanza kabla ya kughanwa, na hata pale yanapoghanwa kabla ya kuandikwa hatimaye

huandikwa, katika andiko hili tunaona matumizi ya istilahi mistari katika ushairi wa Bongo Fleva ni

sahihi. Ushairi wa Bongo Fleva unaonekana kuwa na muundo wa beti zanye mistari kadhaa. Idadi ya

mistari katika kila ubeti itategemea uamuzi wa msanii. Wakati mwingine, idadi ya mistari katika beti za

shairi moja hutofautiana. Aidha, mashairi mengi ya Bongo Fleva huwa na kiitikio. Mfano mzuri wa

mashairi ya aina hii unaonekana katika wimbo uitwao “Veto” ulioimbwa na Mr. 2 ambao una muundo

wa ubeti na mistari.

Ubeti wa 1

1. Nakupa kitu cha Veto

2. Muziki sio wa kitoto

3. Natambaa na beat19 nzito

4. Heshima ya huu muziki tunataka kuirudisha

5. Kwenye hili gemu ndo masela tuliobaki

6. Wengine wengi mafeki

7. Huwa wanachange wakikamata vilaki

8. Sie ni masela na zaidi si ndo mabora

9. Ndo mana tunapata mademu wa viwango bora

10. Niko around kitambo kama migomo ya chuo kikuu ah

11. Tukiacha gemu mnalipeleka pabaya

12. Mpaka mnasababisha tunashindwa kuretire

Ubeti wa II

13. Ni nani rapa wa kwanza kuwa na gari?

14. Wa kwanza kwa kila kitu hata kutoka nchi mbalimbali?

15. Na mpaka leo nipo mkali haya ndo maisha yangu

16. Kimbiza kama unaweza spidi yangu ni ya risasi

17. Mizuka ni ile ile ya Bob Marley

Ubeti III

18. Mi ndo president wa kitambo nishaapa

19. Matatizo ya hili gemu katu siwezi kwepa

20. Kama serikali inavyokwepa ishu ya EPA

21. Hatuogopi kukipaka

22. Hatujali tunachojali ni kuzibana ukweli

Chanzo: Mr. 2 (2009), Veto

Katika wimbo huu tunaona kwamba kuna beti tatu. Ubeti wa kwanza una mistari kumi na mbili wakati

ubeti wa pili na wa tatu ina mistari mitano mitano. Shairi hili halina kiitikio. Mfano mwingine ni shairi

la “Kiburi” lililoimbwa na Mr. 2 akimshirikisha Stara Thomas. Turejelee shairi hilo:

Kibwagizo

Sema mama

Anha hawataki

Kiitikio

Wanachotaka wao wewe upate tabu

Raha kidogo tu chuki bila sababu

19 Beat ni neno linalotumiwa na wasanii wa Bongo Fleva kumaanisha mapigo ya muziki.

86

Ubeti wa 1

1. Najua mama hili nitalikubali eh

2. Kwani najua jeuri dawa yake ni kiburi

3. Kwa wanaonijua tangu enzi za Hemenei

4. Au wakati bado mdogo mama aliponiita Mei

5. Miaka chini ya kumi tu nna jina mkali

6. Kila mtu alinijua mimi ni mtoto wa nani

7. Ni hivyohivyo mpaka walimu shuleni

8. Na ndo mana mpaka leo sishangai mimi kushine

9. Nilipoanza muziki sikujua mafanikio yangeambatana na chuki

10. Mara ngapi nachukua nawaita marafiki

11. Sasa nalala macho wanafiki siwataki

12. Maana kila nnachofanya wanaonekana hawataki

13. Anha na sijali wanachosema baba alinifundisha kutazama mbele daima

14. Na moto ni ule ule tu hakuna wa kuuzima

15. Na najua wanachotaka kuona sugu kachoka ili wapate kucheka

16. Watasubiri watachoka watapanda watashuka

17. Mie nabaki vilevile kila siku kila mwaka

18. Na bado nawakilisha chama la deiwaka

19. Mimi ni fighter nafight bila kuchoka

Rudia Kiitikio

Ubeti wa II

20. Kweli jeuri dawa yake kiburi

21. Nami nitabaki mbishi mpaka nilione kaburi

22. Wako wapi walionicheka shuleni nilipofeli

23. Pilika zangu mtaani zimenifikisha mbali

24. Tisini na tatu nipo boda naitafuta South Africa

25. Na kila ninapotaka naenda zangu Amerika

26. Ndivyo maisha yanavyoweza kuchange

27. Leo nipo na terrano kesho VX or range

28. Na bado nikiwa bar nadai chenji

29. Ah pata picha sugu angekuwa ameshachoka

30. Hakika historia ingekuwa imeshafutika

31. Mabwana wadogo wangeongea kuhusu game wanavyotaka

32. Ningeaibika kama wastaafu wa soka

33. Kumbuka niliacha muziki fan wakasema wamenimiss

34. Nimerudi kwa kishindo wengine wanapata stress

35. Wanabaki tu wanasema

36. Nasema waseme watakavyosema

37. Ndivyo watasema mchana na usiku watalala

38. Na wakiamka asubuhi mi naendeleza bakora

Rudia Kiitikio

Ubeti wa III

39. Maisha yangu yote mimi nimepata sana tabu

40. Nashangaa raha kidogo tu chuki bila sababu

41. Sijawafanya madhambi vipi mnataka nitubu

42. Wanasema nikisema wanasema mi nna gubu

43. Najua bado nipo juu kwenye listi

44. Sina mchezo na life ila siogopi kulost

45. Haya siyo maisha yangu ni masuala

46. Haya ni mambo tu ya hela

47. Siku nikikosa mchuma niko ndani ya daladala

48. Hata kama ni kweli mimi sikuzaliwa Gheto

49. Nimekulia street na nimeshazoea misoto20

50. Hadi ndugu zangu machizi waliniita msela ngoto

51. Na kwa DJ sitoi rushwa za kitoto

52. Hata uendelee kubana hautazuia ndoto

53. Au niende PCB21 niwapelekee za moto

20 Misoto ni msimu unaomaanisha matatizo.

87

54. Kama noma na iwe noma na ikibidi iwe kinoma

55. Bora niache muziki ni kwanini nione huruma

Rudia Kiitikio

Chanzo: Mr. 2 (2009), Veto

Katika shairi hili tunaona pia kuna beti tatu zenye kiitikio cha aina moja, kiitikio bahari. Idadi

ya mistari katika beti inatofautiana. Ubeti wa kwanza una mistari 19 wakati ubeti wa pili una mistari 18

na wa tatu mistari 16. Aidha, shairi hili lina kibwagizo ambapo msanii hughani maneno na kuchombeza

ushairi wake kabla ya shairi lenyewe. Hata hivyo, muundo uliozoeleka zaidi katika ushairi wa Bongo

Fleva ni ya kuwa na beti tatu katika shairi. Mashairi ya beti tatu ndiyo mengi zaidi katika muziki wa

Bongo Fleva kuliko aina nyingine za mashairi. Idadi ya beti hizo hufanya nyimbo husika kuwa si fupi

sana kiasi cha kwisha huku hadhira bado inatamani kuusikiliza na si mrefu sana kiasi cha hadhira

kuchoka kusikiliza.

Muundo huu wa beti, mstari na kiitikio katika Bongo Fleva una dhima ya kulifanya shairi

husika liimbike. Vilevile, huweza kuchochea ushiriki wa hadhira ambapo hadhira huweza kushiriki kwa

kuimba kiitikio. Nacho kiitikio bahari huweza kuwa na dhima ya kusisitiza maudhui.

(ii) Muundo wa Simulio katika Ushairi wa Bongo Fleva

Aina ya pili ya muundo wa ushairi wa Bongo Fleva ni muundo wa simulio. Muundo huu

unaonekana kutokea katika mashairi kama yale yanayoonekana katika wimbo wa “Usiniseme”

ulioimbwa na Ali Kiba. Katika wimbo huo msanii anasimulia matatizo mbalimbali aliyoyapata

kutokana na kula kupita kiasi. Katika ubeti ufuatao anasema:

Kibwagizo

Yo lilele yoyo lilele

Ali K, Ali K, Ali Kiba

Yo lilele yoyo lilele

Kiitikio

Usiniseme x3

Usiniseme kama napenda kula

Usinishangae x3

Usinishangae kama napenda kula

Usiniseme x3

Usiniseme kama napenda kula

Usinitenge x3

Usinitenge kama napenda kula

1.Basi hivi juzijuzi

2.Kulikuwa na shughuli

3.Mtaa wa pili tena si mbali

4.Kulikuwa na pilau na wali

5.Basi mimi nikajiunga

6. Palepale kupiga mpunga

7.Watu wakajipanga

8.Nikaanza kwa tonge na nyama

9.Nina matonge x4

10.Mpaka wakanifukuza

11.Nikasema sijali

12.Nikatoa pesa mfukoni

13.Nikanunua mayai

14.Kilichofuata watu hawakai

Rudia kiitikio

21 PCB ni kifupi cha Taasisi ya Kuzuaia Rushwa (Prevention of Corruption Bureau) kwa sasa inaitwa PCCB, Prevention

and Combating of Corruption Bureau (Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa)

88

15. Ilikuwa Jumapili

16. Siku ya watu wenye ufahari

17. Kujirusha sehemu mbalimbali

18. Nami nikasema leo sikubali

19. Wacha niende x3

20. Ila sina pesa nataka nikale

21. Nikapita sokoni

22. Nikaomba embe sokoni

23. Nikaelekea baharini

24. Nikawaona wengi ufukweni

25. Hakika na embe kiutani

26. Nakula ili watamani

27. Mate yaliwajaa midomoni

28. Basi wote wakaanza kuniomba

29. Usiniombe x3

30. Si unasema mimi napenda kula

Rudia kiitiko

Chanzo: Ali Kiba (2010), Mapenzi Yanarun Dunia

Katika wimbo huu msanii anasimulia jinsi alivyokwenda kwenye shughuli/karamu na kula

kupita kawaida na pia alivyokwenda ufukweni. Masimulizi hayo yote yanalenga kujenga majigambo

yake ya yeye kupenda kula kupita kawaida na anawataka watu wasimseme, kumcheka, kumshangaa

wala kumtenga.

Muundo wa simulio unaonekana pia katika nyimbo nyingine za Bongo Fleva kama vile “Tilalila”

wa Mr. Blue na “Mikasi” wa Mangwea. Katika wimbo wa “Tilalila” Mr. Blue anaimba kwa kusimulia

jinsi alivyokwenda baa na kunywa pombe nyingi kiasi cha kulewa kupita kiasi. Msanii katika wimbo

huo, hachukulii kulewa kuwa kitu kibaya bali anaeleza kwamba baada ya kulewa ndipo alipokuwa jasiri

zaidi na alipoweza kufanya mambo ambayo awali hakuweza. Kwa upande wa wimbo wa “Mikasi,”

msanii anaimba kwa kusimulia jinsi alivyokwenda kupata starehe na marafiki zake hata wakatumia

fedha nyingi. Starehe anazoziimba ni kunywa pombe kupita kiasi, kula na kustarehe na wanawake.

(e) Mtindo wa Ushairi wa Bongo Fleva

Zaidi ya muundo, kipengele kingine cha ushairi wa Bongo Fleva kinachojadiliwa hapa ni mtindo.

Cuddon (1998:872) anabainisha kwamba mtindo unajumuisha vipengele vingi ikiwa ni pamoja na

ujitokezaji wa kazi husika ya kifasihi, uteuzi wa maneno, matumizi ya lugha, tamathali za semi, mbinu

za kisanii, muundo wa sentensi, muundo wa aya na kadhalika. Vipengele tutakavyovieleza katika

sehemu hii ni ujitokezaji wa ushairi wa Bongo Fleva, matumizi ya lugha, tamathali za semi, na mbinu

za kisanii. Kipengele cha kwanza tutakachoanza nacho ni ujitokezaji.

I. Ujitokezaji wa Ushairi wa Bongo Fleva

Ushairi wa Bongo Fleva unajitokeza katika majigambo na majibizano. Majigambo na majibizano

haya huonekana katika namna kuu mbili: majigambo na majibizano katika majina ya wasanii na

majigambo na majibizano katika mashairi yao. Hivyo, tunaweza kusema kwamba kuna ushairi wa

majigambo na majibizano ya majina na majigambo na majibizano ya mashairi. Katika sehemu ifuatayo

tutachambua aina hizi za ujitokezaji tukianza na majigambo na majibizano ya majina.

(i) Majigambo ya Majina katika Ushairi wa Bongo Fleva

Mangesho (2003), Omari (2009), (2010) na (2011) wanabainisha kwamba moja ya mitindo ya

Bongo Fleva ni majigambo katika majina ya wasanii. Omari (2009:56) anabainisha wazi kwamba moja

ya sifa muhimu ya muziki wa Bongo Fleva ni matumizi ya majina ya majigambo, majina ya usanii

kama anavyoyaita. Anaendelea kueleza kwamba mengi ya majina haya yana asili ya lugha ya

Kiingereza na yanafanana sana na yale ya wanamuziki wa Hip hop wa nchi za Ulaya na Marekani.

Anatoa ushahidi wa hili katika wimbo ya Prof. Jay uitwao “Bongo Dar es Salaam.” Anasema:

1. Wabongo wanatamani wangezaliwa Brunei wamwage radhi

2. Mabrothermen majina yao ya asili hawayataki

89

3. Bitozi Nyangema anataka aitwe Tupac

Chanzo: Omari (2009:56)

Majina haya ya majigambo yanatumiwa sana na wasanii kiasi cha majina yao rasmi kutojulikana.

Akithibitisha hili, Mtemwa (2011:17) anabainisha kuwa wasanii hawa huweza hata kuyasahau majina

yao rasmi kutokana na kuzoeleka kuitwa kwa majina haya ya majigambo. Akieleza kuhusu msanii John

Simon kusahau jina lake anasema:

Joh Makini ni kichwa kikali (msanii maarufu) cha Hip hop Bongo (Tanzania). Jina lake halisi ni

John Simon a.k.a Joh Makini. Jamaa mmoja aliwahi kukomaa (kuamua) kumuita John lakini

hakugeuka na alipomuita Joh Makini ndipo akashtuka. Hii inatokana na kulizoea zaidi jina hilo

kuliko John (Ufafanuzi wetu).

Nalo Kitangoma (2011c:22) linashadidia hoja hii kwa kusema kwamba “Mwanaisha Said

Nyange ndio jina lake la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Jina lake rasmi), ni msanii wa muziki

wa kizazi kipya japo wengi hawalifahamu, lakini kwa jina lake la kujitafutia mkate wa kila siku (jina

lake la majigambo) anaitwa Dayna” (Ufafanuzi wetu).

Hata hivyo, majina ya majigambo katika muziki wa Bongo Fleva hayaishii tu kwa wasanii bali

huendelea hadi kwa watayarishaji wa muziki, studio na hata watangazaji wanaozipiga nyimbo hizi.

Mfano wa majina hayo ni kama TID (Top in Dar), Studio ya Wasafi (Sharobaro Records), Rais wa

Wasafi, Dhahabu Records, Master J Rercords na kadhalika.

Wasanii wanatumia majina haya ya majigambo ili kuonyesha uwezo wa kimuziki walionao na

ili kujiimarisha kimuziki. Jina lina uwezo mkubwa sana katika muziki na sanaa nyinginezo. Prof. Jay

katika wimbo wake wa “Jina Langu” anathibitisha uwezo wa jina anaposema:

1. Jina langu linavuma, kwenye mitaa

2. Jina langu lina uwezo wa kisupastaa

3. Jina langu linaongeza idadi ya maadui

4. Wengine nawatambua wengine siwatambui

5. Jina langu

Chanzo: Prof. Jay (2003), Mapinduzi Halisi

Majina ya majigambo, au majina ya utani kama yanavyoitwa na wengine, katika fasihi hujulikana

kama lakabu na kwa kawaida huwakilishwa kwa herufi A.K.A, yaani “Anajulikana Kama” (Also

Known As) au P.H.K yaani “Pia Hujulikana Kama.” Mulokozi (1996:42) anafasili lakabu kuwa “ni

majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipatia kutokana na sifa zao za kimwili,

kinasaba, kitabia au kimatendo.” Mwanjoka (2011:14) anaeleza kwamba majina ya majigambo, lakabu,

ya wasanii wa Bongo Fleva yanaonesha mahali atokapo msanii, uwezo wake kimuziki na kadhalika.

Kwa ujumla, majigambo ya majina yanayopatikana katika ushairi wa Bongo Fleva yana nduni

mbalimbali za kimaudhui na kifani.

Tukianza na nduni za kimaudhui, tunaona kwamba majina ya majigambo ya wasanii wa Bongo

Fleva yanaweza kuwa ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni. Miongoni mwa maudhui hayo

ni kama vile utawala na uongozi, utajiri, usomi na heshima. Majina ya majigambo ya Bongo Fleva

yanayobeba maudhui mbalimbali ya kisiasa ni kama yale yanayoonyesha uwezo wa kiutawala. Majina

ya kiutawala kama vile chifu (chief), mfalme (king) na rais (president) yametumika sana katika

majigambo ya majina. Miongoni mwa wanamuziki wanaotumia majina haya ya kiutawala ni pamoja na

mwanamuziki wa kikundi cha kwanza cha muziki wa Hip hop Tanzania, Kwanza Unit¸ Ramadhan

Mponjika ambaye anajulikana kama Chief Rhymson. Wengine ni Anselm Ngaiza anayejulikana kama

Chief Rumanyika na Abubakar Katwila aliyejulikana kama Q. Chief. Wengine ni pamoja na John

Simon Mseke ambaye anajulikana pia kama Mfalme wa Kaskazini na pia mtayarishaji wa muziki wa

Bongo Fleva na promota maarufu Mohamed Abdallah Kiumbe anayejulikana kama Chief Kiumbe

ambaye ni mmiliki wa kampuni ya burudani iitwayo Respect Entertainment. Wengine ni Abdul Nasibu

anayejulikana pia kama Rais wa wasafi na Raheem Nanji anayejulikana pia kama Rais wa

Masharobaro.

Wasanii na watayarishaji wa muziki wanajitambulisha kwa majina ya mkondo huo, kuonyesha

uwezo wa kiuongozi walionao. Wanajitambulisha kwamba katika muziki wa Bongo Fleva, wao ni

watawala wanaowatawala watu wengine (wanamuziki na watayarishaji wengine) (Omari, 2010:4).

90

Tumeeleza hapo awali kuwa machifu ni viongozi wa asili katika jamii nyingi za Kiafrika ambao

walikuwa wanaongoza koo na makabila mbalimbali (Koponen, 1988 na 1995). Aidha, wafalme na

malkia ni watawala wa kijadi katika nchi mbalimbali duniani. Tumetoa mfano wa nchi kama

Uingereza, Saudi Arabia na Jordan ambazo bado zina viongozi wanaotumia vyeo hivyo.

Vilevile, wapo wasanii wa Bongo Fleva wanaojitambulisha kwa majina ya kijeshi. Jeshi ni moja

ya nguzo muhimu ya kiutawala ambayo inatumika kuendeleza tawala mbalimbali. Zipo dola nyingi za

Kiafrika zilizoibuka kutokana na kuwa na jeshi imara (Koponen, 1988; 1995). Kuwa na jeshi dhaifu

kunaweza kusababisha kuanguka kwa utawala (Koponen, 1988:191). Hivyo, watawala katika jamii

mbalimbali na katika vipindi mbalimbali, wamekuwa wakiwaheshimu sana wanajeshi. Wasanii wa

Bongo Fleva wanatumia majina ya kijeshi ili kuonyesha uwezo walionao katika vita (ushindani wa

kimuziki) na pia heshima waliyonayo katika jamii. Kama tulivyotaja hapo awali, miongoni mwa

wanamuziki wanaotumia majina haya ya kijeshi ni pamoja na Afande Sele (Selemani Msindi),

Commander Mullah (Karama Masoud), Inspector Haroun (Haroun Kahena) na Komandoo (Judith

Wambura). Matumizi ya majina haya, yanatupa picha kuwa katika muziki wa Bongo Fleva kuna vita

(ushindani mkubwa) na hivyo ili kuweza kumudu ushindani huo, msanii inampasa kuwa imara kama

mwanajeshi alivyo imara vitani (Omari, 2010, 2011; Mwanjoka, 2011).

Aidha, yapo majina kama “gaidi” na mheshimiwa ambayo yanabeba dhamira ya kisiasa. Katika

miaka ya mwishoni ya 1990 kuliibuka wimbi kubwa la “ugaidi” duniani likiongozwa na Osama bin

Laden na mtandao wa al-Qaeda. Magaidi hawa wameongoza vita dhidi ya nchi za Magharibi na

washirika wao na kusababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na vifo vingi. Tunakumbuka jinsi

“magaidi” walivyolipua jengo la World Trade Centre na Pentagon nchini Marekani tarehe 11/9/2001,

na treni iendayo kasi Uingereza na Hispania na kadhalika. “Magaidi,” kwa hiyo, wanatambulika kwa

kutokuwa na huruma kwa yeyote. Hivyo, msanii kama Zainab Lupangule anapojiita Mwanadada Gaidi

anamaanisha kwamba yeye ni zaidi ya askari na kwamba hana huruma katika vita vya ushindani wa

kimuziki vinavyoendelea. Nalo jina la Mheshimiwa ni jina linalowakilisha kada fulani ya kisiasa kama

vile mbunge, waziri au Rais. Kwa hiyo, kwa wasanii kujitambulisha kuwa waheshimiwa,

wanajitambulisha kwamba ni wanamuziki wa ngazi za juu. Nchini Tanzania, na katika nchi nyingi za

Afrika Mashariki, wanasiasa wanaongoza kwa kulipwa zaidi na hivyo kufanya watu wengi kuacha kazi

zao na kujiingiza katika siasa ili kupata faida kubwa zaidi. Mfano mzuri wa wasanii wanaotumia jina

hili la mheshimiwa ni pamoja na Amani Temba a.k.a Mheshimiwa Temba.

Mbali na maudhui ya kisiasa, majigambo ya majina pia yanabeba maudhui ya kiuchumi.

Wajigambi wanajitambulisha kwamba ni matajiri, watu wa thamani, wenye uchumi uliotengemaa na

wenye uwezo mkubwa kiuchumi. Mfano wa wasanii wanaotumia majina yenye maudhui ya kiuchumi

ni pamoja na Naseeb Abdul anayejulikana kama Diamond (Almasi), Mwingereza Athumani

Mwingereza anayejulikana kama Tanzanite (Tanzanaiti) na Joseph Raymond anayejulikana kama Black

Rhino (Kifaru Mweusi). Almasi ni madini ya thamani sana duniani. Nayo Tanzanaiti ni madini ya

thamani ambayo hupatikana katika nchi ya Tanzania tu. Aidha, kifaru mweusi, zaidi ya nguvu zake, ni

mnyama wa thamani ambaye anatajwa kuwa adimu sana duniani. Hivyo, wasanii hawa kujitambulisha

kwa majina hayo, wanaonyesha kwamba wao ni watu wa thamani sana na adimu duniani.

Wanaonyesha jinsi walivyo ghali katika kukodiwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi walionao.

Aidha, yapo majigambo ya majina yanayobeba maudhui ya kijamii. Kwa mfano, tunaona

wasanii wakijitambulisha kwa majina ya kisomi, yanayoonyesha uwezo wa kitaaluma, kama vile

Daktari (yaani daktari wa falsafa), profesa na mwanafalsafa. Majina haya yanaonekana kwa

wanamuziki John Simba (Doctor John), Hemed Suleiman (PhD, yaani Daktari wa Falsafa), Joseph

Haule (Profesa Jay) na Hamisi Mwinjuma (Mwana FA, yaani mwanafalsafa). Madaktari, maprofesa na

wanafalsafa ni watu wanaoheshimika katika jamii kutokana na ujuzi walionao. Hivyo, wasanii

kujitambulisha kwa majina haya wanataka jamii iwatambue na kuwaheshimu kama inavyowatambua na

kuwaheshimu madaktari, maprofesa na wanafalsafa.

Si hivyo tu, bali pia kuna matumizi ya majina kama CPWAA/C.P, yaani Critical Personmkosoaji

(Illunga Khalifa) na Babu (Haroun Kahena) ambayo pia yanabeba maudhui ya kijamii.

Critical Person ni mtu anayeogopwa katika jamii kutokana na uwezo wake wa kukosoa. Aidha, Babu ni

mtu anayeheshimika kutokana na hekima na busara alizonazo. Katika jamii mbalimbali kuna methali

nyingi zinazowataka watu kuwaheshimu watu wakubwa, kama mababu na mabibi. Kwa mfano,

91

asiyesikia la mkuu huvunjika guu; sikio halizidi kichwa; kuishi kwingi kuona mengi; ukubwa dawa, na

kadhalika. Hivyo, jamii inatambua uzee kuwa chanzo cha hekima na busara. Kwa kujitambulisha kwa

jina la Babu, msanii anataka jamii iamini kwamba yeye ana hekima na busara kama babu alivyo.

Msanii mwingine anayetumia majina ya kizee ni pamoja na Joseph Haule anayeitwa Mzee wa

Mitulinga na Mzee wa Red Carpet; Selemani Msindi anayeitwa Mzee wa Darubini Kali na Abdul

Naseeb anayeitwa Mzee wa Mbagala. Wasanii hawa wamepewa majina hayo kutokana na nyimbo zao

maarufu walizowahi kuzitoa au wenyewe kujitambulisha hivyo. Joseph Haule, kwa mfano, katika

nyimbo zake nyingi anajitambulisha kama J wa Mitulinga, hivyo wanajamii wakampa jina la Mzee wa

Mitulinga. Naye msanii Abdul Nasibu anaitwa hivyo kutokana na wimbo wake maarufu uitwao

“Mbagala.” Selemani Msindi pia anaitwa Mzee wa Darubini Kali kutokana na wimbo wake maarufu wa

“Darubini Kali.”

Aina nyingine ya maudhui yabebwayo na majigambo ya majina ya wasanii wa Bongo Fleva ni

maudhui ya kiutamaduni. Majina ya majigambo yanayobeba dhamira ya kiutamaduni ni pamoja na

TMK Wanaume Family, TMK Wanaume Halisi na Kiuno Bila Mfupa. Jamii ya Kitanzania inatambua

nafasi ya juu aliyonayo mwanamume katika jamii. Kutokana na mfumo dume ulioota mizizi katika

jamii jinsia ya kiume huonekana ndiyo bora zaidi ya jinsia ya kike. Mwanamume anaonekana kuwa

mtu shupavu, shujaa, mwenye nguvu na mvumilivu kuliko mwanamke (Mair, 1979; Basow, 1992). Hii

inathibitika hata katika misemo kama vile “jikaze kiume,” “unalia kama mwanamke” na “uanaume

kazi.” Misemo hii inaonyesha kwamba mwanamume anatakiwa awe mvumilivu kwani kuwa

mwanamume si kazi ndogo. Aidha, msemo “mwanamume suruali” kumaanisha mwanamume

asiyekuwa na kitu unaonyesha jinsi jamii inavyotambua wajibu wa mwanamume kutafuta fedha za

kumlisha mwanamke. Mwanamke asiye na kitu haitwi “mwanamke sketi” kutokana na ukweli kwamba

jamii inaamini kwamba mwanamke anapaswa kuhudumiwa. Hivyo, kwa wasanii hawa kujiita

“Wanaume,” wanataka kutambulika kama watu wavumilivu, watafutaji, watu wa hadhi ya juu na

wajasiri. Vilevile kujitambulisha kama “Wanaume halisi,” maana yake ni kwamba wao ni zaidi ya

wanaume wa kawaida. Mtazamo huu wa udume unaonekana pia katika majina kama Baba Violeth

linalotumiwa na Seif Shaban (Matonya), Baba Willy linalotumiwa na Godfrey Tumaini (Dudu Baya) na

Mr. Chocolate linalotumiwa na Raheem Nanji (Bob Junior). Baba ni kiongozi wa familia mwenye

jukumu la kulea familia na kuwarekebisha watoto wanapokosea. Hivyo, kwa kutumia jina hili bila

shaka wasanii wanakusudia kujitambulisha kwamba wao ndiyo viongozi wa wasanii wengine wa

Bongo Fleva na kwamba wanapaswa kujifunza muziki kwao.

Nalo jina la Kiuno Bila Mfupa ni jina linaloonyesha jamii inavyopendelea wanawake wanaojua

kukata viuno. Katika jamii nyingi za Kitanzania, kukata viuno ni ishara ya umahiri katika tendo la ndoa.

Jamii mbalimbali huwapeleka watoto wao wa kike wa umri fulani unyagoni ili wafundishwe mambo

mbalimbali ya kinyumba, ikiwa ni pamoja na kukata viuno. Pia kuna ngoma kama msondo na sindimba

ambazo hutumiwa kuwafundisha wanawake kukata viuno. Aidha, katika jamii mbalimbali kuna mila ya

wanawake kuwekwa ndani na kufundwa kabla ya kuolewa. Miongoni mwa mambo wanayofundishwa

ni pamoja na kumridhisha mume katika tendo la ndoa na hasa kukata viuno (Mosha, 2010). Hivyo,

kukata viuno ni suala muhimu katika tendo la ndoa. Kwa hiyo, Rehema Chalamila anapojitambulisha

kama Kiuno Bila Mfupa, anajitambulisha kwamba yeye ni mtu aliyehitimu katika mafunzo ya kimila ya

kukata viuno.

Mbali na nduni za kimaudhui za majigambo ya majina, majigambo hayo yana nduni za kifani

pia. Katika kipengele hiki tutawasilisha nduni hizo za kifani. Nduni hizo zimegawanywa katika

vipengele kama vile utungaji, utendaji, wahusika, muundo, mtindo, matumizi ya lugha na kadhalika.

Tuanze kwa kuchambua kipengele cha utungaji wa majigambo ya majina.

· Utungaji wa Majigambo ya Majina

Majigambo ya majina au lakabu kama anavyoyaita Mulokozi (1996:42), huweza kutungwa na

mhusika mwenyewe au mhusika kupewa jina hilo na wanajamii kulingana na sifa zake. Majigambo ya

majina ya wasanii wa Bongo Fleva yanathibitisha maelezo hayo ya Mulokozi kwani nayo hutungwa

kwa namna mbili. Kwanza, msanii mwenyewe huweza kujipa jina, na pili msanii huweza kupewa jina

na wanajamii wanaomzunguka. Alipo (2011:4-7) akithibitisha uwezekano wa mwanamuziki kujipa jina

mwenyewe anasema:

92

...mwenyewe anajiita ‘Heavyweight Mc wa Bongo flava’ Professor Jay ameshinda mtihani wa

kukaa kwenye game la Bongo Flava (muziki wa Bongo Fleva) kwa zaidi ya miaka 10. Prof. Jay

anaweza kuwa mwanamuziki pekee aliyeweza kupindua muono kuhusu muziki huo kwa nyimbo

zake zilizokwenda shule (zilizo bora) kama ‘Bongo Dar es Salaam’ na ‘Ndiyo mzee’ (Msisitizo na

Ufafanuzi ni wetu).

Hapa mwandishi anatambua jina mojawapo la majigambo la msanii Joseph Haule ni Prof. Jay. Hata

hivyo, anatudokeza kwamba mwenyewe anajiita pia “Heavyweight Mc wa Bongoflava.” Jina hili

msanii mwenyewe amejipa ili kujitofautisha na wasanii wengine. Katika jina hilo anajigamba kwamba

yeye ni mshereheshaji (MC) mkuu katika muziki wa Bongo Fleva.

Aidha, Kitangoma (2011b:20) nalo linatupa mfano mwingine wa msanii aliyejipa mwenyewe

jina la majigambo. Linamnukuu msanii Abbas Hamisi (a.k.a Twenty Percent), anasema:

...jina langu halisi ni Abbas Hamis......Hili jina la Twenty Percent nililipata kutokana tu na jinsi

mimi mwenyewe nilivyokuwa najiona (nimejipa mimi mwenyewe kwa jinsi nilivyojiona). Hata

wewe mwenyewe kama utabahatika kusimama na mimi, utajua mimi kweli ni Twenty Percent

kutokana na kimo na maumbile. Halafu pili mimi najitambua kama Twenty Percent kimatendo

kwa sababu, tofauti na labda watu wengine mashuhuri au matajiri duniani ambao wanaishi kwa

kutegemea utajiri waliourithi au akili nyingi walizopewa na Mungu na mambo kama hayo, mimi

natumia akili yangu ndogo kuishi na kufanya mambo yangu kitu ambacho mimi nakiona ni

Twenty Percent, yaani kulinganisha akili yangu na labda za wale manabii wa hapo zamani

(Ufafanuzi wetu).

Hapa tunaona msanii mwenyewe anathibitisha kwamba jina alijipa mwenyewe.

Akizungumzia uwezekano wa msanii kupewa jina na wanajamii, msanii Adili Nkwera a.k.a

Hisabati alipokuwa akihojiwa katika Samwel (2012a) alisema, “Jina la Hisabati nilipewa na mashabiki

kwa kuwa waliona nyimbo zangu zinatungwa kimahesabu zaidi tofauti na wanamuziki wengine.

Nyimbo zangu zina viwango vya hali ya juu.” Naye Profesa Jay akielezea jinsi alivyopewa jina hilo na

wanajamii, alieleza kwamba jina la Prof. Jay alipewa kupitia kipindi cha Radio One ambacho DJ

Dilinga alikuwa anakiongoza. Kupitia kipindi hicho Prof. Jay aliufahamisha umma kwamba anataka

kubadilisha jina la Nigga J na akawaomba wanajamii wampe jina jingine. Hapo ndipo alipopewa jina la

Profesa Jay. Wazo la wasanii wa Bongo Fleva kupewa jina na wanajamii linathibitishwa pia na

Mwanjoka (2011:14) anaposema, “pia wapo waliotungiwa majina na watu kutokana na tabia zao au

aina yao ya kughani...”

· Muundo wa Majigambo ya Majina

Kipengele kingine cha kifani cha majigambo ya majina ya wasanii wa Bongo Fleva ni muundo.

Majigambo ya majina yana miundo mbalimbali. Mulokozi (1996:42) akifafanua hili anasema kwamba,

“Lakabu ni majina ya kupanga...majina haya huwa ni maneno au mafungu ya maneno...” Hapa

Mulokozi anatudokeza kuwa majina ya majigambo huweza kuwa neno moja au fungu la maneno (kirai,

kishazi na hata sentensi). Hivyo, majina ya majigambo ya Bongo Fleva yana miundo ya neno, kirai,

kishazi na sentensi. Tukianza na majina yenye muundo wa neno moja tunaona majina kama Babu,

Inspector, yaani Inspekta (Haroun Kahena), Diamond, yaani Almasi (Abdul Naseeb), Mfalme (Afande

Sele), Komandoo (Judith Wambura), Mkoloni (Fredrick Mariki) na Sugu (Joseph Mbilinyi).

Kwa upande wa majina yenye muundo wa kirai ni pamoja na TMK Wanaume Halisi, TMK

Wanaume Family, Wachuja Nafaka na Wagosi wa Kaya. Mengine ni Heavyweight MC, Mzee wa

Mitulinga (Joseph Haule), Komando Binti Machozi (Judith Wambura), Mwanadada Gaidi (Zainabu

Lupangule), Mzee wa Misifa (Abdul Sykes) na Kiuno Bila Mfupa (Rehema Chalamila). Aidha, kuhusu

majina ya watayarishaji wa muziki na studio yenye muundo huu ni Master J (Joseph Kimario),

Dhahabu Records (Dully Sykes Records) na Wasafi Records (Sharobaro Records/Raheem Nanji

Rummy Records). Majina yenye muundo wa vishazi na sentensi ni pamoja na jina la Gerald Mwanjoka

anayetumia jina la G SOLO ambalo kwenye jalada la kitabu cha Mwanjoka (2011) anafafanua kuwa ni

kifupi cha vishazi na sentensi zifuatazo: G ni Gerald, S ni Saying, O ni On, L ni Lyrics na O ni Only,

yaani Gerald is Saying On Lyrics Only. Sentensi hii, ingawa inatumia Kiingereza kisicho sahihi,

inamaanisha kuwa Gerald anaongea kupitia mashairi tu. Jina jingine lenye muundo wa sentensi ni Jay

Tunakuzimia linalotumiwa pia na Joseph Haule (Prof. Jay).

93

· Mtindo wa Majigambo ya Majina

Mbali na muundo, kipengele kingine cha kifani ni mtindo. Kama tulivyoeleza hapo awali, mtindo

unajumuisha vipengele vingi. Vipengele vya mtindo vya majigambo ya majina tutakavyovijadili hapa

ni pamoja na matumizi ya mafumbo, taswira na ishara, matumizi ya lugha na tamathali za semi.

Tukianza na matumizi ya mafumbo, ishara na taswira tunabaini kwamba huu ndio mtindo muhimu

uliotumika katika majina ya majigambo. Majina kama vile Afande Sele (Selemani Msindi),

Commander Mullah (Karama Masoud), Inspector Haroun (Haroun Kahena) na Komandoo (Judith

Wambura) ni majina ya kijeshi ambayo yanakusudia kutujengea taswira ya uaskari na kuihusisha na

muziki wa Bongo Fleva. Majina hayo yanatupa taswira kuwa katika ushairi wa Bongo Fleva, wasanii

husika ni mahiri kama walivyo mainspekta, makomandoo na makamanda katika jeshi. Omari (2010:4)

akifafanua hili anasema kwamba sitiari ya majina ya kijeshi inatumiwa na wasanii hawa ili kusawiri

(taswira ya) nguvu za kimwili walizonazo wanajeshi. Omari anafafanua kwamba nguvu hizi zinaashiria

wasanii husika wana uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya ushindani katika soko la muziki kama

wanajeshi wanavyoweza kuhimili mikikimikiki ya vita.

Mfano mwingine, ni majina ya kiutawala kama vile chifu, mfalme na malkia. Miongoni mwa

wanamuziki wa mkondo huu ni pamoja na mwanamuziki wa kikundi cha kwanza cha muziki wa Hip

hop Tanzania, Kwanza Unit¸ Ramadhan Mponjika ambaye alijulikana kama Chief Rhymson, Anselm

Ngaiza aliyejulikana kama Chief Rumanyika na Abubakar Katwila aliyejulikana kama Q. Chief.

Wengine ni pamoja na John Simon ambaye anajulikana kama Mfalme wa Kaskazini na wengineo.

Kama ilivyo kwa majina tuliyoyaeleza hapo awali, haya pia ni ya kitaswira. Majina haya yanaonesha

majigambo kwa njia ya taswira. Omari (2010:4-5), anasema kuwa wasanii wa Bongo Fleva wanatumia

majina haya ili kujitambulisha kwamba wao ni watawala katika muziki huu na wanamuziki wengine ni

raia wa kawaida katika himaya zao za ufalme.

Zaidi ya majina ya kiutawala, wanamuziki wa Bongo Fleva wanajigamba kwa kutumia majina

yanayoonesha uwezo wa kitaaluma (Omari 2010:6) ambayo pia yana taswira. Majina hayo ni pamoja

na Daktari (yaani, daktari wa falsafa), profesa na mwanafalsafa. Majina haya yanaonekana kwa

wanamuziki John Simba (Doctor John), Hemed Suleiman (PhD), Joseph Haule (Profesa Jay) na Hamisi

Mwinjuma (Mwana FA, yaani mwanafalsafa). Omari (khj.) anaeleza kwamba wasanii hawa walitumia

majina haya ili kujitambulisha kwamba ni watu wenye ujuzi wa kutosha katika muziki kama madaktari,

maprofesa na wanafalsafa walivyo na ujuzi mwingi katika taaluma zao. Majina haya yanatuchorea

akilini taswira ya madaktari, maprofesa na wanafalsafa kitaaluma na kuwafananisha na wao.

Aidha, aina nyingine ya majina ya majigambo yanayotumiwa na wasanii wa majigambo ya Bongo

Fleva ni yale yanayoonesha vitu vya thamani katika jamii. Mfano mzuri ni majina kama Naseeb Abdul

anayejulikana kama Almasi (Diamond), Mwingereza Athumani Mwingereza anayejulikana kama

Tanzanaiti (Tanzanite) na Joseph Raymond anayejulikana kama Kifaru Mweusi (Black Rhino). Majina

haya yanatupa taswira ya madini hayo ya thamani na mnyama huyo adimu na kutufanya tuvilingishe na

nyimbo na uwezo wa wasanii husika.

Vilevile, yapo majina ya majigambo yanayotupa taswira ya watu wa kada bora katika jamii.

Miongoni mwa majina hayo ni pamoja na Mheshimiwa Temba, CPWAA/ C.P Critical Person (Illunga

Khalifa) na Babu (Haroun Kahena) kama tulivyokwishaona. Jina la C.P (Critical Person)

linamtambulisha msanii huyu kama mkosoaji na hasa katika mambo yasiyokubalika katika jamii.

Majina mengine ya mkondo huu ni pamoja na jina la Babu linalotumiwa na msanii Haroun Kahena.

Babu ni mzee anayeheshimika katika jamii.

Aidha, kama inavyoelezwa na wataalamu, majigambo yana pande mbili - kusifia na kukashifu (taz.

Rubanza, 1994; Mulokozi, 1996; Samwel, 2012a). Hivyo, zaidi ya majina ya majigambo yanayochora

taswira nzuri ya kusifia, yapo majina yenye kuchora taswira mbaya, inayokashifu. Majina hayo

yanaonekana kubeba taswira mbaya lakini ikiwakilisha uzuri. Miongoni mwa majina ya majigambo ya

mkondo huo ni pamoja na Mzungu Kichaa (Espen Sorensen), Matonya22 (Seif Shaaban), MB Dog

(Mohamed Ali), Dudu Baya (Godfrey Tumaini), Mwanadada Gaidi (Zainabu Lupangule), Crazy G.K.

22 Matonya ni ombaomba maarufu sana aliyepata kuvuma nchini Tanzania miaka ya 2000. Ombaomba huyu, zaidi ya

kurudishwa kwao Dodoma mara kadhaa, alirudi tena Dar es Salaam na kuendelea na kazi yake ya kuombaomba barabarani.

Kazi ya kuombaomba barabarani ni kazi inayodharauliwa sana na ombaomba huonekana kuwa watu duni. Hivyo, msanii

kujiita jina hilo ni namna fulani ya kujikashifu kama upande wa pili wa majigambo yake.

94

(Gwamaka Kihaula) na Mchizi Mox (Taikun Ali). Majina haya kwa hakika hayana sifa nzuri katika

jamii. Jina kama “Kichaa” si zuri, linawakilisha mtu asiyekuwa na akili timamu. Nalo jina la

“Matonya” ni la ombaomba mashuhuri ambaye alikuwa akiomba katika jiji la Dar es Salaam, wakati

MB Dog lina jina “dog’ ambalo lina maana ya mbwa. “Dudu Baya” ni jina linalotupa taswira ya

kiumbe kisichopendeza, kiumbe chenye ubaya wa sura na/au matendo. Nalo jina “mchizi” halina tofauti

na neno kichaa tulilolieleza hapo awali. Majina haya yanatuchorea taswira mbaya kichwani kuwakilisha

kitu kizuri. Majina haya yanatuonyesha upande wa pili wa majigambo, upande wa kukashifu. Zaidi ya

kusifia, majigambo pia huweza kukashifu (Hodza na Fortune, 1979; Rubanza, 1994; Mulokozi, 1996;

na Peek na Kwesi, 2004). Matumizi ya majina haya ya kukashifu yanaonyesha uasi au athari za kigeni.

Kipengele kingine cha kimtindo katika majigambo ya majina ni matumizi ya lugha. Kwa kiasi

kikubwa, majigambo ya majina yanatumia lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa majigambo ya majina ya

wasanii wa Bongo Fleva yanayotumia lugha ya Kiswahili ni pamoja na majina kama Mwanadada

Gaidi, Kiuno Bila Mfupa, Komandoo, Afande Sele, Sam wa Ukweli, Mzee wa Mitulinga, Binti

Machozi, Mchizi Mox, Sugu na Kamanda Mullah. Akizungumzia matumizi ya majina ya majigambo ya

Kiswahili, Mangesho kama anavyonukuliwa na Omari (2009:57) anasema kwamba matumizi haya

yanatokana na majina ya lugha ya Kiingereza yaliyotumika hapo awali kuonekana hayana mantiki

katika muktadha wa Kitanzania. Maelezo haya yanatupa picha kwamba majina ya lugha ya Kiingereza

ndiyo yalianza kutumika. Lakini majina hayo yakabadilika na wasanii wakaanza kutumia majina ya

Kiswahili. Miongoni mwa majina ya majigambo yanayotumia lugha ya Kiingereza ni kama vile King

Crazy G.K., Mr. Ebbo, Mr. Blue, Heavyweight MC, G SOLO (Gerald is Saying On Lyrics Only) na

TID (Top In Dar). Matumizi haya ya majina ya Kiingereza yalianza sambamba na kuibuka kwa muziki

huu. Omari (2009) anaeleza kwamba katika hatua za mwanzo za muziki wa Bongo Fleva, kulikuwa na

athari kubwa za utamaduni wa nje katika muziki wa Bongo Fleva. Matumizi ya majina ya majigambo

yaliyo katika lugha ya Kiingereza, ni moja ya athari hizo. Lakini athari hizi zinaendelea kupungua kadri

muda unavyopita. Mabadiliko haya ndiyo yamesababisha kuwa na matumizi ya majina ya majigambo

yaliyo katika lugha ya Kiswahili. Chachage (2002) anatoa maelezo ya kina ya athari za utamaduni wa

nje, ikiwamo athari ya matumizi ya lugha ya Kiingereza, katika muziki wa Bongo Fleva. Chachage

(2002) anabainisha kwamba matumizi haya yanatokana na athari za utandawazi na yana nafasi kubwa

katika kuleta mgongano wa kitamaduni.

Zaidi ya matumizi ya majina ya majigambo ya Kiswahili na Kiingereza, kuna majigambo ya majina

ambayo yana asili ya lugha za kikabila za Tanzania. Majina hayo ni kama vile Wagosi wa Kaya, na

Mnyalu (Michael Mwakatundu ak.a Mike Tee). “Wagosi” ni neno/jina lenye asili ya Kibondei ambalo

linamaanisha “ndugu,” na “mnyalu” ni neno/jina lenye asili ya kabila la Wahehe (Iringa) ambalo

linamaanisha “mwenyeji” (wa Iringa), au mtu wa kabila la Wahehe/ndugu yao. Jina la Wagosi wa Kaya

ni jina la kikundi cha muziki kinachojumuisha wanamuziki kadhaa ambao wanaishi Tanga. Nalo jina la

Mnyalu linatumiwa na msanii aitwaye Mike Tee. Aidha, yapo majina yenye mchanganyiko wa lugha za

makabila na lugha ya Kiingereza. Jina la Chief Rumanyika ni mchanganyiko wa Kiingereza “Chief”

(chifu) na la Kinyambo, “Rumanyika” (mtu mashuhuri, anayejulikana sana).

Mbali na matumizi hayo ya lugha, majigambo ya majina ya wasanii wa Bongo Fleva hutumia pia

tamathali za semi. Kazi za fasihi hutumia tamathali za usemi ili kuweka mkazo katika maana na mtindo

(Cuddon, 1998; Alembi, 1999; Senkoro, 2011). Miongoni mwa tamathali za usemi zilizotumika katika

majigambo ya majina ni pamoja na sitiari, tashihisi na chuku. Katika sehemu hii tutazipitia tamathali

hizi na kuona jinsi zilivyotumika.

· Sitiari katika Majigambo ya Majina

Tukianza na sitiari tunabaini kwamba majigambo ya majina ya wasanii wa Bongo Fleva yametumia

sana tamathali hii. Hii ndiyo mbinu iliyotumika zaidi katika majigambo ya majina ya Bongo Fleva.

Miongoni mwa majina ya kisitiari ni pamoja na Mwamba wa Kaskazini, Diamond, Tanzanite,

Komandoo, Inspector Haroun, Babu na kadhalika. Katika jina la Mwamba wa Kaskazini, msanii

anakusudia kujilinganisha yeye na mwamba. Mwamba ni jiwe imara ambalo kwa kawaida ni gumu

kuvunjika. Mwamba pia huweza kutumika kuviegemeza vitu vingine dhaifu ili navyo viwe imara.

Msanii, kwa hiyo, anajiona kwamba kwa jinsi alivyoiva katika ushairi huo, yeye ni kama tegemeo la

mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania. Kwa kiasi kikubwa na kwa kipindi kirefu, wasanii wa muziki wa

95

Bongo Fleva wamekuwa wakitokea Dar es Salaam. Aidha, msanii Diamond, anakusudia kujilinganisha

na almasi. Anajiona kwamba ni mwanamuziki wa thamani na ghali kama ambavyo almasi ilivyo ghali

na ya thamani.

Vivyo hivyo kwa jina la Tanzanite, msanii anajitambulisha si tu kwamba ni msanii ghali na wa

thamani, bali anajitambulisha kwamba ni ghali kiasi ambacho hakuna msanii kama yeye duniani.

Madini ya Tanzanaiti yanapatikana katika nchi ya Tanzania tu duniani kote. Matumizi ya sitiari hii

yanaweza pia kumaanisha kwamba msanii anajitambulisha kwamba ni Mtanzania halisi au

anatambulisha chimbuko lake kuwa ni Tanzania. Nalo jina la Komandoo msanii anajilinganisha na

komandoo wa kijeshi. Komandoo katika jeshi huwa ni askari ambaye zaidi ya kupitia mafunzo ya

kawaida ya askari, yeye hupewa mafunzo ya ziada. Huwa ni askari mwenye uwezo mkubwa sana wa

kijeshi na uvumilivu wa hali ya juu pindi anapokutana na mateso. Marekani baada ya kumtafuta gaidi

wa kimataifa kwa miaka zaidi ya kumi bila mafanikio, waliwatuma makomandoo ambao walifanikiwa

kujua alipo na kumuua tarehe 2/5/2011. Kwa hiyo, kwa Judith Wambura kutumia jina hilo,

anamaaniisha kwamba ameiva sana kwenye muziki wa Bongo Fleva na mvumilivu.

Jina la Inspector Haroun, kwa upande mwingine, linamlinganisha msanii na askari polisi mwenye

nyota moja na kuendelea (afisa wa jeshi la polisi). Askari polisi mwenye cheo kama hicho kwa kawaida

hukaa ofisini na ni mara chache hufanya kazi ngumu wanazofanya askari wengine kama makoplo na

kadhalika. Inspekta wa polisi hawezi kwenda doria, na kama akienda atakuwa msimamizi wa askari

wengine, hawezi kwenda lindoni kulinda mabenki, maofisi na kadhalika. Vilevile, hata malipo

(mshahara) ya inspekta wa polisi hutofautiana na polisi wa vyeo vya chini. Kwa hiyo, kwa

kujitambulisha kama inspekta, Haroun Kahena, alikuwa anajigamba kwamba ni askari (msanii)

anayeheshimika miongoni mwa askari wengine (wanamuziki wengine) na kwamba anafanya kazi

ndogo isiyotoa jasho sana lakini kwa malipo makubwa.

· Tashihisi katika Majigambo ya Majina

Mbali na matumizi ya sitiari, majigambo ya majina yanatumia pia tashihisi. Miongoni mwa majina

ya kitashihisi ni Mwamba wa Kaskazini analolitumia John Simon, Diamond, Tanzanaiti na Mbwa. Ni

wazi kwamba mwamba, madini ya Tanzanaiti, almasi na mbwa haviwezi kuimba wala kuongea. Hivyo,

kwa wanamuziki kujipa majina haya, wanavipa uwezo vitu hivyo kuongea na kutenda kama binadamu.

Tamathali hii ndio huitwa tashihisi (Abram, 1981; Akivaga na Odaga, 1998).

· Chuku katika Majigambo ya Majina

Chuku imetumika pia katika majina ya majigambo yanayotumiwa na wasanii wa muziki wa Bongo

Fleva. Majina ya aina hiyo, ni kama vile Profesa Jay, PhD, yaani Daktari wa Falsafa (Hemedi

Suleiman) na Mwana FA. Majina haya ni ya wataalamu waliobobea katika eneo fulani la kitaaluma.

Lissah (2007:7) anabainisha kwamba wasanii wengi wa Bongo Fleva wameacha shule na kujiingiza

katika muziki huu. Kama hivyo ndivyo, ni wazi kwamba wasanii wengi hawana elimu hii

wanayojinasibisha nayo. Utafiti wa Samwel (2012a) unabainisha kuwa wasanii wengi wa Bongo Fleva

wana elimu ya sekondari na wachache sana wamefikia elimu ya Chuo Kikuu na kupata walau digrii

moja. Miongoni mwa wasanii wenye digrii moja ni Roma, mwanaFA na K-Basil. Utafiti wake, kwa

wakati huo, haukumpata msanii hata mmoja mwenye digrii ya uzamili achilia mbali uzamifu (PhD)

wanayojinasibisha nao. Hivyo, majina wanayoyatumia ya Profesa na Daktari wa Falsafa ni chuku.

· Wahusika wa Majigambo ya Majina

Mbali na vipengele hivyo, kipengele kingine cha majigambo ya majina ya wasanii wa Bongo Fleva

ni wahusika. Wahusika wa majigambo ya majina ni kama wahusika wengine wa kifasihi simulizi.

Kama tulivyodokeza hapo awali, wahusika wa fasihi simulizi huweza kuwa watu, wanyama, miti,

mizimu, mahoka na viumbe wengine wasio binadamu. Kwa hiyo, wahusika wa aina hizo pia ndio

wanaotumika katika majigambo ya majina katika Bongo Fleva. Kwa mfano, katika jina la Chief

Rumanyika mhusika hapo ni mzimu/mtu aliyekufa. Omukama Rumanyika aliyekuwa akiitwa Mfalme

Rumanyika Orugundu alikuwa mtawala wa Karagwe nchini Tanzania kati ya mwaka 1853-1879

(Koponen, 1988; 1995). Kwa msanii huyu kujiita Rumanyika, anajitambulisha kwamba yeye ni

marehemu aliyefufuka. Hivyo ni mzimu wa Mfalme Rumanyika.

96

Pia kuna matumizi ya wahusika wasio binadamu. Kwa mfano, jina la “Mwamba wa Kaskazini” ni

matumizi ya jina la kiumbe asiye binadamu. Majina mengine ni kama Diamond (Almasi), Tanzanite

(Tanzanaiti) na mbwa (Mb Dog na Soggy Doggy). Wahusika wengine ni Vichaa (King Crazy GK,

Mchizi Mox, Mzungu Kichaa) na kadhalika.

· Majigambo ya Majibizano katika Bongo Fleva

Zaidi ya mtindo wa majigambo ya majina, mtindo mwingine wa ushairi wa Bongo Fleva ni

majigambo ya majibizano. Omari (2009:195) anabainisha kwamba majibizano au malumbano ni moja

ya sifa muhimu katika muziki wa Bongo Fleva. Majigambo ya majibizano katika muziki wa Bongo

Fleva yanaonekana katika makundi makuu mawili: majibizano katika majigambo ya majina na

majibizano katika mashairi ya majigambo. Katika sehemu inayofuata tutachambua aina hizo mbili za

majigambo ya majibizano tukianza na majibizano yanayojitokeza katika majina ya majigambo ya

wasanii wa Bongo Fleva.

· Majigambo ya Majibizano katika Majina

Majina ya majigambo ya wasanii wa Bongo Fleva wakati mwingi yamekuwa katika hali ya

majibizano – msanii mmoja anatumia jina fulani ili kumjibu msanii mwingine. Kama tulivyoona hapo

awali, wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva wanajipa au kupewa majina ili kujitambulisha

kwamba ni watu wenye uwezo kimuziki, wasanii wanaoongoza katika muziki huu, wasanii wenye

kuhimili ushindani katika soko la muziki, wasanii wenye mashairi yenye hekima na busara na sifa

nyinginezo zinazofanana na hizo. Hata hivyo, imekuwa ni kawaida kwa wasanii kutumia majina ili

kujibu sifa aliyojipa au aliyopewa msanii mwingine. Majibizano hayo yapo katika kila mkondo wa jina

la majigambo, yaani tangu majina ya kijeshi, majina yanayoonesha vitu vya thamani, majina

yanayoonesha utawala na kadhalika.

Kwa kuanza na majina ya majigambo ya kijeshi, tunaona wazi kwamba kuna majibizano baina ya

wasanii. Kijeshi cheo cha Inspekta kinatumiwa na askari polisi wenye kuanzia nyota moja hadi tatu.

Hawa ndio huitwa mainspekta. Mwanamuziki Haroun Kahena anatumia jina la Inspector Haroun

kujitambulisha kwamba yeye katika muziki wa kizazi kipya, ni kama askari polisi mwenye nyota

(mwenye cheo). Haroun Kahena hapa anaufananisha muziki wa Bongo Fleva/Hip hop na jeshi la polisi

lenye askari wasio na vyeo, wenye vyeo vya chini na hata wenye vyeo vya juu. Yeye anajitambulisha

kwamba ni askari mwenye nyota – mwenye cheo cha juu na hivyo anapaswa kuheshimiwa na askari

polisi (wanamuziki) wengine.

Kutokana na ukweli kwamba nchini Tanzania majeshi ya ulinzi yanaheshimika zaidi ya majeshi ya

usalama,23wanamuziki wengine wakajitokeza kumjibu Haroun Kahena (Inspector Haroun).

Wanamuziki hao wakaanza kujitambulisha kwa majina ya vyeo vya majeshi ya ulinzi (JKT na JWTZ).

Kwa mfano, mwanamuziki Karama Bakari anajitambulisha kwa jina la Luteni Karama. Cheo cha

Luteni hutumiwa na askari wa majeshi ya ulinzi. Luteni ni askari jeshi mwenye nyota mbili au moja.

Mwenye nyota moja huitwa luteni usu na mwenye nyota mbili huitwa luteni. Ni wazi kwamba Karama

Bakari anajitambulisha kwamba yeye si polisi bali ni mwanajeshi mwenye nyota.

Aidha, wanamuziki wengine wakiongozwa na Karama Masoud wakajitambulisha kwamba wao ni

Kikosi cha Mizinga. Jeshi la Tanzania linagawanyika katika vikosi mbalimbali na vyenye majukumu

tofauti. Kuna kikosi cha anga, kikosi cha majini, kikosi cha mizinga na kadhalika. Wanamuziki hao

wanajitambulisha kuwa ni kikosi cha jeshi lakini si kikosi cha kawaida bali ni kile cha mizinga

ambacho kina mafunzo ya hali ya juu katika kurusha makombora. Kikosi cha mizinga huwa ni

maalumu kwa ajili ya kushambulia ngome ngumu na kujibu mashambulizi ya silaha nzitonzito. Bila

23 Majeshi ya ulinzi nchini Tanzania yanajumuisha JWTZ (Jeshi la Wananchi wa Tanzania) na JKT (Jeshi la Kujenga Taifa).

Majeshi haya yapo chini ya Wizara ya Ulinzi na jukumu lake kuu ni kulinda usalama wa nchi ikiwamo mipaka. Majeshi ya

usalama ni pamoja na polisi – ambalo ni jeshi linaloshughulikia usalama wa raia na mali zao - na jeshi la magereza. Majeshi

haya yapo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Nchini Tanzania majeshi ya usalama yanaheshimika sana machoni

pa raia na hata machoni pa serikali. Wananchi wengi huwaogopa wanajeshi kuliko wanavyowaogopa polisi au askari

magereza. Mara kadhaa wanajeshi wamewapiga polisi kutokana na mwanajeshi mwenzao kukamatwa au kucheleweshwa na

polisi katika foleni pale ambapo askari polisi wanaongoza magari barabarani. Serikali nayo inatoa mishahara mikubwa kwa

wanajeshi kuliko kwa polisi na magereza.

97

shaka kwa kutumia jina la Kikosi cha Mizinga wanajitambulisha kwamba wana uwezo wa kiwango cha

juu kujibu mapigo pale wanaposhambuliwa. Kwa kuwa moja ya sifa ya muziki wa Bongo Fleva ni vita,

au bifu wanachofanya wanamuziki hawa ni kuwatahadharisha wengine kwamba wao wapo tayari

kujibu mashambulizi.

Majibizano hayaishii hapo, wanamuziki wengine wanajitambulisha kwa majina ya vyeo vya juu

zaidi vya kijeshi kuliko Luteni. Bila shaka wakifahamu kwamba Luteni ni mwanajeshi mwenye nyota

moja au mbili, Mwanamuziki Albert Mangwair katika wimbo wake wa Speed 120 Shaa

anajitambulisha kama Meja Jenerali. Meja Jenerali ni cheo cha juu sana katika Jeshi la Tanzania, ni

askari anayekaribia kufikia cheo cha mwisho kijeshi, Jenerali. Anachokifanya Ngwair hapa ni

kujitambulisha kwamba yeye si tu mwanajeshi bali ni mwanajeshi wa cheo cha juu sana. Bila shaka

anakusudia kuonyesha kwamba yupo juu zaidi ya “wanajeshi” wengine katika muziki wa Bongo Fleva.

Hata hivyo, wanamuziki wengine wakitambua mafunzo ya kiwango cha juu ya kijeshi wanayopata

makomandoo, wanajitambulisha kwa majina hayo ili kuwajibu wenzao. Wanamuziki wanaotumia

majina kama hayo ni pamoja na Judith Wambura anayejiita Komandoo na Karama Masoud anayejiita

Kamanda Mullah.

Majibizano hayapo tu katika majina ya majigambo ya kijeshi bali pia katika majina ya majigambo

ya kiutawala. Wanamuziki wengi wa muziki wa Bongo Fleva hapo mwanzo walijitambulisha kwa jina

la Chief/Chifu. Kama tulivyoeleza hapo awali, machifu walikuwa watawala wa Kiafrika waliotawala

jamii za Kiafrika wakiwasaidia wafalme kabla ya ukoloni kuingia. Katika jamii za Kihaya, kwa mfano,

waliitwa bami b’enshozi (Mulokozi, 2002:17). Kwa hiyo, kwa kutumia jina la Chief/Chifu, wanamuziki

hawa wanajitambulisha kama watawala wa muziki wa Bongo Fleva. Miongoni mwa wanamuziki hao ni

pamoja na Ramadhani Mponjika (Chifu Rhymson), Abubakar Katwila (Q. Chief) na Peter Kiwinga

(Chifu Kiwinga). Lakini, Ansleim Tryphone Ngaiza akijua wapo wanamuziki wanaojiita machifu,

akajiita Chifu Rumanyika. Neno “Rumanyika” ni la Kinyambo lenye maana ya “mtu

maarufu/mashuhuri” au “anayefahamika sana.” Hivyo, msanii kwa kulitumia jina hili, zaidi ya mambo

mengine, alikuwa anawajibu “machifu” waliomtangulia kwamba yeye si tu kwamba ni chifu bali pia ni

chifu anayefahamika zaidi yao.

Hata hivyo, baadhi ya machifu katika jamii za Kiafrika walitumiwa na wakoloni, hasa wa

Kiingereza, kuwatawala Waafrika ukoloni ulipoingia (Koponen, 1988 na 1995; Rubanza, 1995; Omari,

2010). Hivyo, machifu wakaonekana mbele ya wengi kama wasaliti. Si hivyo tu bali pia katika nchi

nyingi za Kiafrika baada ya uhuru machifu na watawala wengi wa kijadi walipoteza mamlaka zao za

asili. Badala yake, uchifu ukabaki kuwa jina tu la kiongozi asiye na mamlaka. Hali ilikuwa hivyo pia

nchini Tanzania (Rubanza, 1994). Ili kuwajibu wanamuziki wenzao waliojiita machifu, wanamuziki

wengine walijigamba kwamba wao ni kiboko cha machifu au ni zaidi ya machifu. Msanii Frederick

Mariki anajitambulisha kwa jina la Mkoloni, hii ikiwa na maana kwamba anawatumia machifu

kutawala kwa niaba yake. Kwa jina hili, Frederick Mariki anajitambulisha kwamba machifu wote wako

chini yake kama machifu wa Kiafrika walivyokuwa chini ya Wakoloni wa Kiingereza. Naye Mr. 2

katika wimbo uitwao “Veto” anajiita Rais (president). Jina la Rais pia linatumiwa na wasanii Diamond

na Bob Junior. Marais wengi ndio walioupiga marufuku utawala wa machifu (Rubanza, 1994:16).

Hivyo, kujitambulisha kama Rais inamaanisha wanatangaza mwisho wa utawala wa machifu katika

Bongo Fleva.

Wanamuziki wengine waliojitokeza kuwajibu wanamuziki waliojiita machifu ni pamoja na John

Simon anayejitambulisha kama Mfalme (King) na Gwamaka Kahaula anayejitambulisha pia kama

King Crazy GK, yaani Mfalme Kichaa GK. Kama tulivyoeleza hapo awali, katika jamii za Kiafrika

kabla ya ukoloni, machifu walikuwa wasaidizi wa wafalme. Kwa kujitambulisha kwa jina la Mfalme,

wasanii hawa wanawajibu wale wanaojiita machifu kuwa wapo chini yao kimuziki. Aidha, kwa upande

wa nje ya Afrika kulikuwa na wafalme. Nchi za Ulaya na Asia ambazo zina maendeleo makubwa,

zilikuwa na zingine bado zina utawala wa kifalme. Kwa wanamuziki hawa kujitambulisha kama

wafalme, kwa upande mwingine, inaweza kuonekana kwamba wanawajibu wale wanaojitambulisha

kama machifu kwamba wanaongoza mataifa tajiri.

Majina mengine ya majigambo yaliyotumiwa na wasanii hawa pia yalikuwa na majibizano. Kwa

mfano, mwanamuziki Tanzanaiti alijipa jina hilo ili kumjibu mwenzake, Diamond (Almasi).

Kinachoonekana hapa, ni kwamba wakati ambapo Diamond ni madini ya thamani sana, Tanzanite ni

98

madini ya thamani zaidi na ambayo hupatikana katika nchi moja tu, Tanzania. Kwa hiyo, msanii huyu

kujiita Tanzanite, alikuwa anamjibu Diamond kwamba yeye si tu ni madini ya thamani bali

yanapatikana katika nchi moja tu, Tanzania.

Hata majina ya majigambo ya kukashifu, yalikuwa na majibizano. Majina kama Gaidi, Dudu Baya

na kadhalika, ni wazi kwamba yalikuwa yanawajibu wasanii wengine. Gaidi ni tishio kwa utawala

wowote ule, uwe wa chifu, mfalme, malkia au hata Rais. Kwa hiyo, kujitambulisha kama Gaidi

kunawaeleza wanamuziki wengine kwamba huyu ni kiboko yao. Hali ni hiyohiyo hata kwa jina Dudu

Baya. Dudu baya linaweza kumshambulia mtawala yeyote, askari yeyote au hata raia mwema. Kwa

kujitambulisha kwa jina hilo kunamaanisha yeye ni kiboko yao.

Majibizano haya ya majina ya majigambo yaliendelea hadi katika mashairi waliyoyatunga. Sister P

na Zay B wametunga mashairi na kujibizana juu ya majina yao. Kwa mfano, katika wimbo wa Zay B

“Gado” anajitambulisha kuwa ni Mwanadada Gaidi. Hili linabainika katika shairi lifuatalo:

1. Zay to the B Mwanadada Gaidi

2. Sitaki ushahidi nini cha ziada

3. Mimi ni danger usinichezee ntakuchinja

4. Niko gado24 tena bado

5. Huwezi kucheza na anga hizi

Chanzo: Omari (2009:333)

Ili kumjibu Zay B, Sister P anajitambulisha kuwa ni “Bush” na Kijukuu cha NATO, kwa hiyo,

hatishiki na Gaidi. Tunaliona hili katika wimbo wake uitwao “Maisha ya Uswahilini:”

1. Sina papara katika fani nishatua

2. Bush nakuja magaidi mtanitambua

3. Mtoto mdogo kifani sasa nishakuwa…

4. Nenda Milembe kawape call machizi

5. Sister P kiburi gaidi kashamdhibiti

6. Kijukuu cha NATO sasa nakula kiulaini

Chanzo: Omari (2009:197)

Hapa Sister P anamwambia Zay B kuwa kama yeye ni gaidi basi yeye ni Bush hivyo ameshamdhibiti.

George W. Bush alikuwa Rais wa Marekani kati ya mwaka 2000-2008 na alikuwa Rais aliyepambana

sana na ugaidi. Huyu ndiye mwanzilishi wa vile vinavyoitwa “Vita vya Ugaidi Duniani” ambapo

aliivamia Afghanstan kwa lengo la kumsaka “gaidi namba moja duniani,” Osama Bin Laden (Wade na

Almir, 2011). Nalo NATO ni Shirika la Kujihami la Mataifa ya Magharibi ambalo nchi wanachama ni

pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Italia. Shirika hilo liko mstari wa mbele

kupambana na “ugaidi” duniani.

Jambo la kukumbuka hapa ni kwamba wasanii wengine wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa

na jina zaidi ya moja la majigambo kwa nyakati mbalimbali au hata kwa wakati mmoja. Kwa mfano,

Joseph Mbilinyi alijitambulisha kwa jina la 2 Proud wakati anaanza muziki, lakini baadaye akabadili

jina na kuitwa Mr. 2 na Sugu ambayo yanatumika kwa pamoja hadi sasa. Vivyo hivyo, Judith Wambura

alitambulika kama Lady Jaydee na kisha Komandoo na Binti Machozi, majina yote hayo yanatumika

hadi sasa. Joseph Haule anatambulika kama Prof. Jay, Jay Arosto, Mzee wa Mitulinga na kadhalika na

Ansleim Ngaiza alijulikana kama Soggy Doggy Hunter na kisha Chief Rumanyika. Naye Abubakar

Katwila alijulikana kama Q. Chief na hatimaye Q. Chila na pia Savimbi. Haroun Kahena

anajitambulisha kama Inspector Haroun, Jabali la Rap Katuni na pia Babu, na Zainab Lipangule

alijulikana kama Zein B lakini akabadilisha na kuitwa Zay B na hatimaye Mwanadada Gaidi (Omari

2010:4, 9). Zaidi ya majina hayo pia tunaweza kuona katika mashairi yake majina mengine aliyowahi

kujipa kama vile Komandoo, Bongo First Lady na Concord. Wengine waliobadilisha majina ni pamoja

na Dudu Baya anayeitwa Dudu Zuri, Hemed Suleiman anayeitwa PhD, TID anayeitwa pia Jembe na

kadhalika. Kubadilisha huku kwa majina au kuongeza jina jipya kuna dhima ya kumpa msanii sifa

mpya ya majigambo anayodhani au ambayo mashabiki wake wanadhani anayo. Kwa mfano, kutokana

na Dudu Baya kuona tabia yake ya ugomvi inahusishwa na jina lake akaamua kubadili jina ili kujaribu

24 Gado ni msimu ambao unamaanisha niko imara.

99

kuwashawishi wapinzani wake kwamba kwa sasa amebadilika na hivyo si Dudu Baya tena bali ni Dudu

Zuri. Hali ni hiyo hiyo kwa Hemed Suleiman ambaye hakuwa na jina la majigambo alipoamua kujiita

PhD ili kuonesha jinsi alivyoiva katika fani ya muziki kwa sasa.

Aidha, wapo baadhi ya wasanii ambao hawana majina ya majigambo. Hawa ni pamoja na Ali

Kiba, Banana Zorro, Ferouz Mrisho, Nakaaya Sumari na Stara Thomas. Wapo walioendelea kutumia

majina yao ya asili kama yalivyo na pia wapo walioyafupisha majina yao ya asilli. Walioyafupisha

majina yao ni kama vile Faridi Kubanda (Fid Q), Ambwene Yesaya (A. Y), Rehema Chalamila (Ray C,

huyu anaitwa pia Kiuno bila Mfupa) (Omari 2010:2-3). Vilevile wapo waliofupisha jina moja kati ya

majina yao. Hawa ni pamoja na Dully Sykes (Abdul Sykes), Angeris Faber a.k.a Angie, Bakari

Abdallah (Beka) na Estalina Sanga (Lina). Majina haya hata hivyo si ya majigambo.

(ii) Majigambo ya Majibizano katika Mashairi ya Bongo Fleva

Mbali na majibizano katika majina yao, wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya walijibizana

katika mashairi ya nyimbo zao. Mambo waliyojibizana, ni ujumbe, anasa, ndoa, dini na kadhalika.

Mfano mzuri wa majibizano ni kati ya msanii Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) na Haroun Kahena

(Inspector Haroun). Mwana FA alitunga wimbo wa “Bado Niponipo Kwanza” ambamo anapinga suala

la ndoa. Turejelee ubeti huu:

1. Japo natokea Tanga mapenzi yalipozaliwa

2. Sijiviki maufundi nikajifanya najua

3.Mi nna akili timamu naona mnavyorukia

4.Ukiniona na demu haimaanishi ndio nitamuoa

5.Napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu

6.Kwani nami nna maumivu yangu nasema tu na moyo wangu

7.Watu wanalalamika wanavyoteswa na ndoa zao

8.Wengine wanaficha wanakufa na maumivu yao

9. Sioi leo sioi kesho kutwa wala mtondogoo

10. Sioi mchana sioi usiku wala majogoo

11. Morali niliyonayo sasa siwezi kukubali kuibiwa

12. Ngoja nizeekezeeke kwanza pengine nitakuja elewa

13. Wengine nifumbe macho, wengine nizibe masikio

14. Nisione wakati naibiwa

15. Hamuwezi kuwa hamjalewa

16. Mi nkiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi

17. So mpaka miaka kadhaa ijayo ndo mniulize naoa lini

Chanzo: Mwana FA (2011), Yalaiti

Katika wimbo huo msanii anajigambo kwamba yeye anatokea Tanga mapenzi yalipozaliwa na

hivyo anajinadi kwamba anajua mapenzi. Zaidi ya ujuzi huu wa mapenzi anaojinasibisha nao

anaonyesha jinsi ndoa inavyoweza kuleta matatizo kwa mtu kutokana na kusalitiwa na ampendaye.

Anabainisha wazi kwamba wanawake katika ndoa si waaminifu na hivyo ili kukwepa matatizo hayo,

msanii anabainisha kwamba ni vema asioe kwa sasa. Akimjibu Mwana FA, Inspector Haroun, ambaye

ameoa, akatunga wimbo wa “Tamu ya Ndoa.” Katika wimbo huo anamjibu Mwana FA kwamba ndoa

ni tamu na ni kitu cha hekima. Inspector anajigamba kwamba anaheshimika kwa kuwa ameoa na

kwamba asiyeoa huonekana muhuni na anayeogopa majukumu.

Aidha, majibizano mengine yanaonekana baina ya Sister P na Zay B. Wasanii hawa kwa muda

mrefu walikuwa kwenye malumbano kutokana na kila mmoja wao kutaka kuonekana ndiye mahiri

katika muziki huu kwa upande wa wanawake. Majibizano kati ya wawili hawa yanabainishwa vizuri na

Omari (2009:195). Kwa mfano, tunaona wanajibizana juu ya suala la biashara. Tuangalie wimbo wa

Zay B uitwao “Mama Afrika”:

1.Msipende kutembea na wazee

2. Fuateni wosia hiyo tabia isiendelee...

3. Tumeumbika ulimwengu mzima tunakubalika...

4.Weusi asilia ndio zetu kujivunia...

5.Watoto wa kike tusikae nyuma na tuzingatie elimu

6.Ukijifanya unajua shauri yako utaishia kuuza vitumbua

Chanzo: Omari (2009:336)

100

Sister P alijibu mashairi hayo katika wimbo uitwao “Achana Nao.” Anasema:

1.Nafungua ubongo natoa fikra za utumwa kichwani

2.Kipawa chatoka kwa Mola wala sijatumia ubani

3. Sister P kupata chati watu wanadhani rap utani

4. Rap biashara bwana ila angalia usijepata hasara

5.Kuuza vitumbua, pipi maandazi zote biashara

6.Usidharau hizo biashara watu watakuangushia msala.

7.Wasomi wengi wamesoma kwa kutumia hizo biashara

8.Mashairi sibahatishi na nitauza nyingi nakala

9.Na siyo utani nyota kwangu imeonekana biashara

10.Wandago rafiki zangu tena wa kina

11.We uliza maswali mengi majibu mimi sina

12.Nakupa rap shule mashairi yangu yana vina

Chanzo: Omari (2009:291)

Vilevile wanajibizana juu ya uwezo wao kimuziki. Rejelea katika wimbo wa “Gado” ulioimbwa na Zay

B:

1. Zay B sasa yuko gado

2.Mashairi yamejaa kisadosado

3.Zay B sasa yuko gado

4.Yote kumi tisa mambo bado bado

Sister P akimjibu katika wimbo wa “MaDJ” anasema,

1.Ya nini visado? Watu tumejaza lumbesa

2.Na bado katika fani tunazidi kutikisa

3. Sister P, Mnyamwezi Hamisi na Prado

4.Hatuogopi vishindo vyenu eti kwamba mko gado

5.Na bado mimi Sister P ni damudamu Thadeo

6. Pumbavu unauliza ningeimba nini Sister P asingekuwepo Zay B...

7. Swali linarudi kwako sasa eh eh

8.Ungeimba nini Mwanafalsafa tusingekuwepo wasanii?

9.Au ungekuwepo wewe bubu katika fani hii?

Chanzo: Omari (2009:196)

Majibizano haya ni aina ya majigambo kwani msanii mmoja anapomjibu mwingine lengo lake hasa

huwa kuionyesha jamii na msanii huyo kwamba msanii anayejibiwa si mwanamuziki aliyebobea na

kwamba anatunga nyimbo ambazo hazina ujumbe mzito unaokubalika katika jamii.

(f) Matumizi ya Lugha katika Ushairi wa Bongo Fleva

Baada ya kuangalia ujitokezaji wa ushairi wa Bongo Fleva kipengele cha kimtindo ni matumizi ya

lugha. Ushairi wa Bongo Fleva, kwa kiasi kikubwa, hutumia lugha ya Kiswahili, ambayo ndio

inaeleweka kwa Watanzania walio wengi. Matumizi haya ya lugha ya Kiswahili huenda

yanasababishwa na ukweli kwamba Kiswahili ndio lugha ya taifa nchini Tanzania na lugha

inayoeleweka kwa wengi. Kwa hiyo, kutumia lugha hii kunatokana na msanii kuilenga hadhira pana

zaidi.

(i) Matumizi ya Lugha Iliyotoholewa

Zaidi ya matumizi ya lugha ya Kiswahili kuna matumizi makubwa ya lugha iliyotoholewa na

kuchanganya lugha hasa Kiingereza na Kiswahili. Majembe (1998), Chachage (2002) na Omari (2009)

wakielezea hili wanasema kwamba muziki wa Bongo Fleva/ Hip hop kwa kiasi kikubwa umeathiriwa

na muziki wa Hip hop wa Kimarekani. Hivyo wanaeleza kwamba kuna mchanganyiko wa lugha ya

Kiswahili na Kiingereza. Lugha ya Kiingereza ndio inayotumiwa na wasanii wa Hip hop wa Marekani.

Mfano mzuri wa nyimbo inayotumia lugha yenye utohozi ni “Mchakamchaka” wa Mr. 2 kama

ifuatavyo:

1. Mie niite super delegeto ama deiwaka

101

2. Nalicheza hili gemu nnavyotaka

3. Ni albam ya kumi lakini hasira kama ndo kwanza natoka

4. Sasa ni mwendo wa dolali

5. Ndani ya akaunti mtoni utadhani mtoto wa Balali

6. Sema vijisenti vyangu ni vya halali

7. Bongo mchakamchaka tu

8. Mafisadi hawalali

9. Nina uhuru wa kusema

10.Na nitasema chochote ntakachoona kinafaa mimi kusema

11.Na nakuja na falsafa za Obama

12.Tunatakiwa kuchange

13.Tusipochange maisha bora kwetu ndoto kama muafaka wa Zenji anha

14.Wacha niendeleze dozi

15.Maana leo kama balozi

16.Kama kazi ni kazi hakuna ubitozi

17.Na ni upuuzi kusema gemu haliuzi

Chanzo: Mr. 2, (2009), Veto

Hapa tunaona anatumia neno super delegeto (super delegate), deiwaka (day worker), gemu (game),

albam (album), dolali (dollar), kuchange (to change), akaunti (account) na dozi (dose). Maneno haya ni

ya Kiingereza yaliyoswahilishwa. Hii inaonesha athari za lugha ya Kiingereza katika Kiswahili na

mchango wake katika kukuza msamiati wa Kiswahili. Aidha, lugha inayotumiwa hapa inasawiri lugha

inayotumiwa na vijana, ambao ndio hasa fanani na hadhira ya ushairi wa Bongo Fleva.

(ii) Matumizi ya Lugha za Mchanganyiko

Mbali na matumizi ya lugha ya Kiswahili na lugha iliyotoholewa, ushairi wa Bongo Fleva unatumia

pia lugha mchanganyiko. Mchanganyiko wa lugha unaotumika ni ule wa Kiswahili na lugha za

makabila na mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza. Katika vipengele vinavyofuata tutaelezea

matumizi haya ya lugha mchanganyiko na kuthibitisha kwa mifano. Tuanze na mchanganyiko wa

Kiswahili na lugha za makabila.

Ushairi wa Bongo Fleva una matumizi ya mchanganyiko wa lugha ya Kiswahili na lugha nyingine

za makabila. Hii inatokana na ukweli kwamba wasanii wa ushairi huu wana makabila yao ambayo

wangependa kujitambulisha kwayo. Uchanganyaji wa aina hii unaonekana katika wimbo wa “Walimu”

ulioimbwa na Wagosi wa Kaya kama unavyonukuliwa katika data namba (106) hapa chini:

1. Goodmorning teacher, goodmorning sir

2. Monika zeze mwalimu hicho ni Kisambaa

3. Nimechanganyikiwa mpaka naongea Kisambaa darasani

4. Na hii ni kwa sababu sina kitu mfukoni

Chanzo: Wagosi wa Kaya (2003), Ripoti Kamili

Hapa tunaona zaidi ya uchanganyaji wa Kiswahili na Kiingereza katika mstari wa 1, kuna

uchanganyaji wa Kisambaa na Kiswahili katika mstari wa 2. Kirai Monika zeze kina maana ya habari za

asubuhi katika lugha ya Kisambaa. Uchanganyaji unaonekana pia katika wimbo wa Suma Lee,

“Hakunaga” ambapo msanii anaanza kwa ghani za kikabila. Aidha, hata neno “hakunaga” analolitumia

mara kwa mara ni neno lenye asili ya lugha za makabila na hasa Kisukuma. Matumizi haya ya lugha za

kikabila yana lengo la kupata soko katika mikoa na maeneo makabila hayo yanamotumika. Sababu

nyingine ya matumizi hayo ya lugha, inaweza kuwa harakati za kujinasua kutoka katika athari za

kutoka nje (ukoloni mamboleo) na hasa athari za kiutamaduni. Likithibitisha haya Fiesta (2011:27)

linasema:

Mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye anatumia lafudhi ya Kimasai katika kuimba nyimbo

zake, Abel Loshilaa Motika maarufu kwa jina la Mr. Ebbo amewataka wanamuziki wa Bongo

Fleva kujivunia lugha yao sio kupenda kutumia lugha za wenzetu katika nyimbo zao.

Akizungumza na Fiesta, mwanamuziki huyo mkongwe katika fani hiyo alisema kuwa utamkuta

mwanamuziki wa Kitanzania anaimba lugha ya kigeni katika nyimbo zetu bila aibu. Msanii huyo

anajivunia kila kilicho chake na pia hapendi kuiga bali anapenda kubuni na anapobuni

anatoka na vitu vya ukweli. Mr. Ebbo anasema tatizo la wasanii wa Bongo Fleva ni kuigana, kila

msanii angekuwa na ubunifu wake basi ingekuwa rahisi kuuzika sokoni lakini wanapoigana

kunakuwa hakuna kitu kipya kwa wasikilizaji (Msisitizo wetu).

102

Katika dondoo hili mwandishi anatueleza kwamba msanii huyu si tu anatumia lugha ya Kimasai, bali

pia anatumia lafudhi ya Kimasai.

Zaidi ya matumizi ya lugha yenye mchanganyiko wa lugha ya Kiswahili na lugha za makabila,

kuna matumizi ya mchanganyiko wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Aina hii ya mchanganyiko wa

lugha, imetumika sana katika ushairi wa Bongo Fleva. Maneno yote tuliyoyawekea hati za mlalo

(italic) katika mashairi ya Bongo Fleva tuliyoyanukuu, yanaonyesha matumizi ya lugha hii

mchanganyiko.

Hata hivyo, kumekuwa na harakati za wasanii kupinga uigaji wa tamaduni za nje yakiwamo

matumizi ya lugha ya Kiingereza katika muziki wa Bongo Fleva. Likisisitiza jinsi matumizi ya lugha

ya Kiingereza katika muziki wa Bongo Fleva yanavyopingwa, Kitangoma (2011a:7) linamnukuu

msanii Dayna anaposema, “ …nawashangaa baadhi ya wasanii wenzetu ambao wamekuwa

wakikimbilia kuimba Kizungu (Kiingereza) na kutukuza lugha za nchi nyingine na kukiacha Kiswahili

ambacho kwa sasa kimeanza kutambulika duniani” (Ufafanuzi wetu).

Matumizi haya ya mchanganyiko wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, ingawa yanaonekana

kupingwa na baadhi ya wasanii na wanajamii, yanaakisi hali halisi ya jamii. Yanaonyesha athari ya

ukoloni mamboleo katika lugha. Mchanganyiko huu wa lugha hauonekani tu katika ushairi wa Bongo

Fleva lakini unaonekana pia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na bungeni na kadhalika.

Hivyo, huu ni uthibitisho kwamba fasihi ni kioo cha jamii husika.

(g) Matumizi ya Tamathali za Semi

Mbali na matumizi ya lugha ya Kiswahili, lugha iliyotoholewa, lugha ya Kiswahili

iliyochanganyika na lugha za makabila na lugha ya Kiswahili iliyochanganyika na lugha ya Kiingereza,

ushairi wa Bongo Fleva unatumia pia tamathali za semi. Baadhi ya tamathali za semi zinazotumika sana

ni sitiari, tashbiha, tashtiti, udokezo na chuku. Katika sehemu inayofuata tutachambua tamathali hizi

kwa kina. Katika kipengele hiki tutapitia tamathali hizo za usemi.

(i) Tashbiha katika Ushairi wa Bongo Fleva

Aina hii ya tamathali imetumika sana katika mashairi mbalimbali ya ushairi wa Bongo Fleva.

Matumizi ya aina hii yanaonekana katika wimbo wa Sister P uitwao “MaDJ” kama inavyonukuliwa

katika ubeti ufuatao:

1.Kwamba mimi sitishiki hata ukishika kisu kikali

2.Nilikutana na Halifani track ya kwanza ilikuwa kali

3. Sasa nije kwa hasira kama vile jabali?

4.Au nije kikakamavu kama vile jemedari?

5.Kutoa vishindo vikuu na sauti za ukali

6. Ili waelewe Bongo Records label yenye nembo kali

7.Najipa cheo kwenye rap mi ni stadi

8. Sauti yangu inatambaa kwenye beat kama radi

9.Usiniulize ovyoovyo jina langu linanipa chart

Chanzo: Omari (2009:190)

Katika ubeti huu tunaona kwamba msanii anatumia tashbiha tatu, “nije kwa hasira kama vile jabali,”

“kikakamavu kama vile jemedari” na ya mwisho “sauti inatambaa kwenye beat kama radi.”

Vilevile, matumizi mengine ya tashbiha yanaonekana katika wimbo wa “Jina Langu”

ulioimbwa na Prof. Jay. Katika ubeti ufuatao mstari wa 5 anatumia tashbiha isemayo “jina langu

mahiri kwenye giza kama kandili.” Turejelee ubeti huo ambapo msanii anasema:

1. Jina langu linavuma kwenye mitaa

2. Jina langu lina hadhi ya kisupa staa

3. Jina langu linaongeza idadi ya maadui

4.Wengine nawajua wengine siwatambui

5. Jina langu mahiri kwenye giza kama kandili

Chanzo: Prof. Jay (2003), Mapinduzi Halisi

103

Matumizi haya ya tashbiha yanaweka msisitizo katika maana inayokusudiwa. Wasanii wanatumia

vitu vilivyozoeleka kufafanua vitu ambavyo wanadhani havifahamiki vema. Kwa mfano, tunaona

msanii Sister P, ili kufafanua ukakamavu alionao, anatumia picha ya jemedari (askari wa jeshi). Katika

jamii majemedari wanafahamika sana kwa ukakamavu wao. Vivyo hivyo anapotaka kufafanua mapigo

(beats) ya nyimbo zake anatumia sauti ya radi ambayo wanajamii wamezoea kuisikia.

Kwa upande wa Prof. Jay, anatumia picha ya mwanga wa taa ya kandili unavyoweza kufukuza

giza hata liwe nene kiasi gani. Hapa anafananisha uwezo wa jina lake na wa taa ya kandili. Picha hii

imezoeleka kwa Watanzania walio wengi kwani wanatumia taa hizo kila siku. Zaidi ya asilimia 80% ya

Watanzania hawapati nishati ya umeme na hivyo taa walizozizoea ni kandili, vibatari na kadhalika.

Akithibitisha hili Msuya (2011:1) anamnukuu Sir George Kahama mmoja wa wanasiasa maarufu

Tanzania anaposema:

Bila kubeza mafanikio makubwa yaliyopatikana, ni vema pia tukiri kwamba, safari yetu ya kufikia

lengo la kuwa na maisha bora kwa kila Matanzania bado ni ndefu. Asilimia 36 ya Watanzania

bado hawajaweza kumudu kupata mahitaji yao ya msingi. Asilimia 86 ya wananchi hawapati

umeme wa gridi ya taifa. Wote tunajua ya kwamba, wananchi wengi bado wanaishi katika nyumba

zilizojengwa kwa kuta za miti, fito na matope na kuezekwa kwa makuti au nyasi.

Hivyo matumizi ya tashbiha yanafanya maudhui kufika kwa njia bora zaidi kuliko kama zisingetumika.

(ii) Sitiari katika Ushairi wa Bongo Fleva

Aina nyingine ya tamathali ya semi iliyotumika kwa kiasi kikubwa katika ushairi wa Bongo

Fleva ni sitiari. Sitiari ni uchoraji wa picha katika akili ya hadhira. Ingawa tashibiha pia huchora picha,

ina tofauti na sitiari kwani sitiari huchora picha kana kwamba ndio ukweli. Sitiari huchora picha kwa

kulinganisha vitu viwili tofauti bila kutumia vifananisho kama: kama, kama vile, mithili ya na

kadhalika. Hivyo, picha inayochorwa huonekana kama ndio uhalisia wenyewe. Mtu anaposema,

“Mariam ana uzuri kama malaika,” anakuwa ametumia tashibiha kuchora picha ya malaika kichwani

mwa hadhira. Watu wengi huamini kwamba malaika ni kiumbe mzuri sana. Hata hivyo, picha hii

huonekana kama mfano tu na si uzuri halisi wa Mariam. Lakini fanani anaposema, “Mariamu kwa uzuri

wake ni malaika” (sitiari), hadhira hupata picha ya uzuri halisi. Picha hii huwa na nguvu na kuaminika

zaidi kuliko ile ya kitashibiha. Hivyo, majigambo ya Bongo Fleva hutumia sitiari ili kujenga picha

halisi na za kuaminika zaidi na hivyo kuweka mkazo katika maana.

Mifano ya matumizi ya sitairi inaonekana katika nyimbo mbili zifuatazo zilizoimbwa na Zay B.

Katika wimbo wa kwanza, “Siwezi Kuacha” anatumia sitiari mbili ambazo ni “mimi ndo Bongo First

Lady” (mstari wa 2) na “wanaotaka ushindani wote takataka” (mstari wa 3) kama inavyojibainisha

katika data ifuatayo:

1.Nacharaza mijeledi na wale wote wapinzani wa jadi

2.Wamekiri mimi ndo Bongo First Lady…

3.Wanaotaka ushindani wote takataka

4.Unanigwaya hatari kuliko miwaya…

5.Katika madada mi kiboko

Chanzo: Omari (2009:348)

Katika wimbo wa pili unaoitwa “Hatari Kitu Gani” msanii anatumia sitiari mbili pia. Sitiari ya

kwanza ni “mimi ni komandoo tena nakuja kwa vishindo” (mstari wa 1) na ya pili ni “mamia kwa

mamia wamekiri kama mimi ndio Concord.” Turejelee ubeti huu:

1.Mimi kamandoo tena nakuja kwa vishindo

2.Nasema njoo once again nawakilisha Tanzania

3.Wanga mtabana mtaachia lyrics nazidi kuwamiminia

4.Mimi mtaniambia sio kama najifagilia

5.Mamia kwa mamia wamekiri kama mimi ndio Concord…

6. Sauti yangu inasikika dunia nzima

7.Vigumu kuisahau kama Tupac na B.I.G

Chanzo: Omari (2009:192)

Katika data namba nyimbo mbili hapo juu tunaona Zay B anafananisha umaarufu wake katika muziki

na umaarufu wa first lady (mke wa Rais) na anawafananisha wapinzani wake na takataka. Vilevile

analinganisha anavyowasumbua wapinzani wake na kuwatesa kama vile mtu anayechapa wengine

104

mijeledi. Pia anajifananisha na komandoo na ndege ya concord. Hapa hatumii vifananisho kama ilivyo

kwenye tashbiha na hivyo anachora picha halisi zaidi na zinazoaminika.

Aidha, zaidi ya kuchora picha za kuaminika na zilizo halisi zaidi, tumeeleza hapo awali kwamba

sitiari ndio huufanya utungo kuwa na sifa ya kishairi kwani ni moja ya sifa muhimu ya utanzu wa

ushairi (Mulokozi, 2002; Songoyi, 2005). Hivyo, tunaweza kusema kwamba matumizi ya sitiari hapa,

zaidi ya mambo mengine, yameyafanya majigambo ya Bongo Fleva kukidhi vigezo vya utanzu wa

ushairi.

(iii) Tashihisi katika Ushairi wa Bongo Fleva

Ushairi wa Bongo Fleva mbali na kutumia tamathali zingine, umetumia tamathali hii ya usemi.

Mfano mzuri ni wimbo uitwao “Nawakilisha” ulioimbwa na Prof. Jay anaposema:

1. Beti kamili zenye mizani thamani zaidi ya madini...

2.Weka mbali malenga mnaosifia huu ubongo ni Shakespeare...

3.Wenyewe mnajuta tena nina uwezo zaidi ya kompyuta

Chanzo: Omari (2009:193)

Katika shairi hili msanii anaupa ubongo wake uwezo wa kuimba na kutunga kazi za kisanii kama

Shakespeare alivyokuwa mahiri katika utunzi. William Shakespeare alikuwa mshairi na mtunzi

maarufu wa mashairi na tamthiliya aliyeisha kati ya mwaka 1564 hadi 1616. Msanii huyu alitunga

mashairi zaidi ya 154 na tamthliya 38 na kazi zake zimetafsiriwa na kutumiwa katika nchi mbalimbali.

Msanii huyu anajulikana kama sheha wa malenga wa taifa la Uingereza (Gibbons, 1980 na 1993;

Grady, 2001a na b). Hivyo, msanii anaufananisha ubongo wake na ule wa Shakespeare. Anachokisema

hapa ni kwamba ubongo wake unaweza kutunga, kuimba na kutenda kama Shakespeare. Katika hali ya

kawaida ubongo hauwezi kutenda hayo.

Tashihisi, kama zilivyo tamathali nyingine, zimetumiwa na wasanii wa ushairi wa Bongo Fleva

ili kukazia maana. Kwa mfano, katika shairi tulilolinukuu msanii anatumia tashihisi ili kuweka mkazo

katika uwezo mkubwa alionao katika ushairi wa Bongo Fleva.

(iv) Udokezi katika Ushairi wa Bongo Fleva

Tamathali nyingine ya usemi ambayo imetumika katika ushairi wa Bongo Fleva ni udokezi.

Tumeeleza hapo awali kwamba udokezi au mdokezo ni tamathali ambayo inatumika katika kazi

mahsusi ya kifasihi ili kurejelea kazi nyingine ya fasihi au ya sanaa, au mtu au hata tukio. Aidha,

tumeona kwamba tamathali hii inatumika katika ushairi wa majigambo kwa dhima ya kuhusianisha kazi

za fasihi, vitu, watu au matukio kwa lengo la kuyapa uzito maudhui ya kazi husika na/au kuupa ushairi

huo upekee (Johnson, 1978: 14; Cuddon, 1998:27). Katika ushairi wa Bongo Fleva udokezi umetumika

sana. Mfano mzuri wa matumizi ya mbinu hii unaonekana katika wimbo wa “Ndiyo Mzee” ulioimbwa

na Profesa Jay ambao tumeunukuu hapa chini.

1. Ok ok naitwa Joseph Haule mwana Msolopazi

2. Nadhani nimeletwa kuokoa hiki kizazi

3. Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu

4. Nimeletwa kwenu waungwana niwapunguzie machungu

5. Mimi ni mteule Kusini mwa jangwa la Sahara

6. Ndio maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala

7. Nina hekima kuliko mfalme Sulemani msiwe na wasi

8. Na hii nitadhihirisha pindi mtakaponipa nafasi

9. Actually, nimedhamiria kuwasaidia

10. Taifa lenye nguvu duniani liwe Tanzania

Chanzo: Profesa Jay (2001), Machozi, Jasho na Damu

Katika mstari wa kwanza wa uberi wa kwanza msanii anasema “ok ok naitwa Joseph Haule

mwana Msolopagazi.” Katika mstari huo msanii anatumia mbinu ya udokezi kwa kuturejesha katika

hadithi za Ridder Haggard za Mashimo ya Mfalme Selemani, na mhusika wake wa Kiafrika aitwaye

Msolopagazi (Umsolopagaas) anayeambatana na wahusika Wazungu, Allan Quarteman, Sir Henry

Curtis na John Good (taz. Haggard, 1885). Hapa msanii, zaidi ya mambo mengine, huenda pia

anakusudia kutuonyesha kwamba yeye ni mwanamuziki wa Kiafrika ambaye hadhi yake ni sawa na ya

105

wanamuziki wa Kizungu na kwamba anawasaidia hata katika tungo zao. Ikumbukwe kwamba kwa

kipindi kirefu muziki wa wanamuziki Wazungu ndio umechukuliwa kuwa bora na wa kiwango cha juu.

Lakini Profesa Jay ameshirikiana kuimba na wanamuziki kadhaa wa nje ya Tanzania wakiwamo

Wazungu. Miongoni mwa alioshirikiana nao ni Jaguar na Amani (kutoka Kenya), Jose Chamellion

(kutoka Uganda), P Square (kutoka Nigeria), Heavy D (kutoka Marekani) na kadhalika.

Udokezi katika wimbo huo unatumika pia katika mstari wa 7 anaposema “nina hekima kuliko

mfalme Sulemani msiwe na wasi.” Hapo anaingiza katika ushairi ngano ya Kiyahudi inayomuhusu

Mfalme Sulemani. Katika ngano hiyo Mfalme Sulemani, ambaye alikuwa mtoto wa Daudi aliyezaliwa

katika ukoo wa Yese, anatajwa kwamba alimpendeza sana Mungu kiasi cha Mungu kumwambia

amuombe chochote atakacho. Ndipo mfalme huyo akaomba hekima. Baada ya kutoa ombi hilo

kinyume na matarajio ya Mungu aliyetegemea angeomba utajiri, Mungu akamwambia atamuongezea

na vingine vyote. Hivyo, Sulemani akawa na hekima kuliko wanadamu wote duniani na hata wafalme

wengine na watawala wa dola nyingine kama vile Malkia wa Sheba wakasafiri umbali mrefu kuja

kushuhudia hekima ya Sulemani (Tanzania Bible Society, 1997:377-379). Udokezi huu unatumiwa na

msanii kwa lengo la kukejeli viongozi wa Kiafrika jinsi wanavyotaka waonekane wana hekima sana

wakati kimsingi hawana hekima yoyote.

(v) Kejeli katika Ushairi wa Bongo Fleva

Zaidi ya kutumia udokezi ushairi wa Bongo Fleva unatumia pia kejeli. Senkoro (2011:13)

anafasili kejeli kuwa ni tamathali ambayo maneno yake huwa kinyume kabisa na maana inayotakiwa

kutolewa. Anaendelea kusema kwamba kejeli huweza kuchanganya tamathali nyingine kama vile

ubeuzi uliofichika, kinyume, tabaini na msisitizo bayani. Nao Kahigi na Mulokozi (1979:37)

wanafafanua kuwa kejeli ni usemi wa kebehi ambamo kisemwacho sicho kikusudiwacho na msemaji,

kisemwacho kumbe ndicho kinachobeuliwa. Tamathali hii imetumika sana katika ushairi wa Bongo

Fleva. Matumizi ya mbinu hii yanaonekana katika wimbo wa “Ndiyo Mzee” tuliounukuu hapo awali.

Wimbo huo umebeba dhana ya unyume. Msanii anawakilisha majigambo ya uongo ya wanasiasa

wakati wa kampeni za uchaguzi. Kwa hiyo, majigambo hayo ni ya kikejeli.

(vi) Chuku katika Ushairi wa Bongo Fleva

Aidha, tunaona matumizi ya chuku katika mashairi ya Bongo Fleva. Mbali na matumizi ya

chuku katika majina ya wasanii wa uushairi wa Bongo Fleva, kama tulivyojadili hapo awali, pia kuna

matumizi ya chuku katika mashairi haya. Kwa mfano, katika wimbo wa Dogo Janja uitwao “Anajua”

tunaona matumizi haya ya chuku. Tunathibitisha hilo katika ubeti ufuatao:

1. Tunainama

2. Tunameza tunatema

3. Mtaipata fresh ya mwaka mpaka mnatetemeka

4. Kuona kwa bei tunamakeup tupo full mzuka...

5. Dogo Janja mimi sirushi ngumi nawachapa tu na ulimi

6. Kwa michano hunichomi

7. Kama ulikuwa hunisomi

8. Nakufunika Ommy

9. Huwezi kukabiliana utemi

10.Dogo Janja sikwami

11.Eh basi nina army

12.Tupo japo hatuvumi

13.A town siyo Miami

14.Dogo Janja kamanda...

Chanzo: Dogo Janja (2009), Ngarenaro

Hapa tunaona msanii anasema hakwami na kwamba ana jeshi (army) na yeye ni kamanda. Katika hali

ya kawaida hakuna binadamu ambaye hakwami. Pia nchini Tanzania hairuhusiwi mtu kuwa na jeshi

lake binafsi. Hivyo, msanii hapa kwa kusema ana jeshi ni chuku zinazotumika kujenga lugha ya picha.

Lugha hii ya picha huwa na mchango mkubwa katika kuweka mkazo katika maudhui. Kwa mfano,

katika shairi hili kwa msanii kusema kwamba ana jeshi anakazia maudhui kwamba yeye hawezekani

maana ana mashabiki wengi wanaomuunga mkono.

106

(vii) Takriri katika Ushairi wa Bongo Fleva

Ushairi wa Bongo Fleva pia unatumia takriri. Takriri ni mbinu iliyotumika zaidi katika ushairi

wa muziki wa kizazi kipya. Dunleavy (1992:23) anaeleza kwamba takriri ni moja ya sifa kuu katika

lugha ya kimuziki na pale takriri zinapotumika, kunakuwa na msisitizo katika maana. Tunaliona hili

anaposema:

We are familiar with the three Rs associated with music – rhythm, rhyme and repetition. When

lyrics are repeated, an idea or concept is reinforced. The repetition of the consonant can

punctuate the rhythm of a piece of music. Letter, words, phrases, lines, refrains, choruses, and

verses can all be repeated.

Tunafahamu kwamba muziki una sifa tatu za msingi ambazo ni mapigo, vina na marudio. Wimbo

unaporudiwa, ujumbe husisitizwa zaidi. Marudio ya konsonanti katika mstari yanaweza kuleta

mapigo ya kimuziki. Herufi, maneno, virai, mishororo, viitikio na hata beti nzima huweza

kurudiwa (Tafsiri yetu).

Katika ushairi wa kizazi kipya, zaidi ya aina nyingine ya takriri, kuna takriri kiitikio. Haya ni marudio

ya kiitikio kizima katika ushairi. Katika muziki wa kizazi kipya marudio ya kiitikio yanaonekana karibu

katika kila wimbo. Tunalithibitisha hilo katika wimbo wa Mr. 2 uitwao “Mchakamchaka,” “Veto” na

ule wimbo uitwao “Moto Chini” ambapo tunaona msanii anarudia kiitikio kizima. (Taz. Nyimbo

mbalimbali tulizozinukuu).

Mbali na takriri kiitikio, pia ushairi wa Bongo Fleva unatumia takriri mstari, takriri neno, takriri

kirai, takriri kishazi, takriri silabi na kadhalika. Kwa mfano, katika wimbo uitwao “Sisi Tulivyo”

ulioimbwa na Sister P:

1. Sisi tulivyo kama utakavyoniona ndio nilivyo

2. Mimi nilivyo siko sawa na jinsi ulivyo

3. Mimi nilivyo hata unavyodhani sivyo nilivyo

4. Mimi nilivyo huwezi kunitambua jinsi nilivyo

5. Mimi nilivyo na huu ndio ukweli wa jinsi nilivyo

6. Mimi nilivyo siyo sawa na manabii jinsi walivyo

7. Mimi nilivyo nina hekima kuliko mtu mzima alivyo

8. Mimi nilivyo na hadhi zaidi ya wafalme jinsi walivyo

9. Mimi ni mchamungu kuliko ulivyo

10.Mimi nilivyo napenda mademu jinsi walivyo

Chanzo: Omari (2009:295-296)

Hapa kuna takriri neno ambapo neno “nilivyo” au sehemu yake limerudiwa karibu wimbo mzima. Pia

kuna marudio ya neno “mimi” (mstari wa 9 na wa 10) na marudio ya kishazi “mimi nilivyo” (mstari wa

2 hadi wa 8). Takriri hii, zaidi ya kukazia maneno yaliyorudiwa, inafanya kazi ya kuleta mapigo katika

ushairi na kushadidia maudhui.

(h) Mbinu za Kisanii

Zaidi ya vipengele hivyo vya mtindo kipengele kingine ni mbinu za kisanii. Kama tulivyomnukuu

Senkoro (2011:25-51) hapo awali mbinu za kisanii tunazozizungumzia hapa ni pamoja na ishara,

picha, ucheshi, vina na mizani, mapigo, methali na, usambamba. Mjadala unaofuata utahusu vipengele

hivi vya kimtindo.

(i) Matumizi ya Picha na Taswira

Picha na taswira zimetumika sana katika ushairi wa Bongo Fleva. Picha na taswira zimetumika

kuanzia katika majina ya wasanii wa ushairi huu, hadi katika mashairi yao. Kwa mfano, majina ya

Komandoo, Chifu na Inspekta ambayo tumeyaeleza matumizi yake huko nyuma, ni majina ya

kitaswira. Maelezo ya kina ya lugha ya ishara na picha tazama kipengele kinachohusu majina ya

wasanii wa ushairi wa Bongo Fleva tulichokieleza hapo awali.

(ii) Ucheshi katika Ushairi wa Bongo Fleva

Mbinu nyingine inayotumika katika ushairi wa Bongo Fleva ni ucheshi. Ucheshi ni mbinu

ambayo hulenga kuchekesha au kuifanya hadhira walau itabasamu (Senkoro, 2011:26). Mbinu hii

huundwa kwa kutumia maneno na sentensi ambazo zinastaajabisha na hivyo kuifanya hadhira ishangae

107

na iishie kucheka au kutabasamu. Pia wakati mwingine msanii huweza kutumia kejeli ili kujenga

ucheshi. Matumizi ya ucheshi katika wimbo wa Bongo Fleva uitwao “Ndiyo Mzee” wa Profesa Jay

kama inavyoonekana katika ubeti ufuatao:

1. Wafanyakazi serikalini nashangaa hamna magari

2. Yaani hata mikweche, ha! ha! ha! hii ni hatari

3. Na nina mpango wa kuongeza mishahara iliyo minono

4. Mara mia moja ya ile ya mwanzo iliyowafanya mfanye migomo

5. Nitawapa nyumba nzuri na magari ya kifahari

6. Watu watashangaa mtakapopita kila mahali

7. Mkulima kila mmoja nitampatia trekta

8. Nadhani hiyo kidogo itasaidia kuinua sekta

9. Mtauza nafaka zenu bilioni kwa mabailioni

10.Watu midomo wazi kama wamekamatwa ugoni

11.Walimu zawadi yenu mh nimezificha moyoni

12.Nadhani mtazimia siku mkizitia machoni

13.We acha tu, mtafurahi nyinyi

14. Ila hapa hapamfai mtu mwingine niwekeni mimi

15. By the way polisi mi nawasifu

16. Jinsi mnavyokwenda sahani moja na wahalifu

17. Sasa kila mmoja nitampatia helkopta

18.Nadhani hiyo ndoto wote hamjawahi kuota

19.Raia wa Tanzania mtalala milango wazi

20. Infact nina uhakika wa kudhibiti ujambazi

21.Nitajenga barabara tano tano juu na chini

22.Nitajenga kumbi nyingi sana za starehe baharini

23.Ninapenda kuitwa mshumaa kumulikia wenzangu

24.Na mtakaoyumba kiuchumi tutagawana vya kwangu

Chanzo: Omari (2009:266 -268)

Katika wimbo huu tunaona msanii anaeleza kwamba ataongeza mishahara ya wafanyakazi mara mia

moja, atawapa wafanyakazi wote magari ya kifahari, atawapa wakulima matrekta na kwamba atajenga

kumbi za starehe baharini. Aidha, msanii anaeleza kwamba kila askari polisi atampatia helkopta na

kadhalika. Mambo haya anayoyasema ni chuku zinazojenga ucheshi kwa hadhira. Hapa msanii

anatumia chuku kujenga kejeli na kejeli hiyo inajenga ucheshi.

(iii)Vina na Mizani katika Majigambo ya Bongo Fleva

Zaidi ya ucheshi mbinu nyingine ya kimtindo inayotumika katika ushairi wa Bongo Fleva ni urari

wa vina na mizani. Katika ushairi wa muziki wa kizazi kipya kuna matumizi makubwa ya vina na

mizani. Utumiaji wa vina na mizani katika muziki huu ndio huonekana kuwa ujuzi wa kuimba na

ubobezi katika fani ya Bongo Fleva. Kwa mfano, katika wimbo uitwao “Nawakilisha” ulioimbwa na

Prof. Jay, msanii anajigamba kwamba mashairi yake yana vina na hivyo yeye amebobea katika muziki

huu. Anasema:

1. Beti kamili zenye mizani thamani zaidi ya madini...

2.Weka mbali malenga mnaosifia huu ubongo ni Shakespeare...

3.Wenyewe mnajuta tena nina uwezo zaidi ya kompyuta

Chanzo: Omari (2009: 193)

Hapa msanii anabainisha kwamba mashairi yenye beti kamili na mizani ndio yenye thamani kubwa

kuliko madini. Kwa maneno mengine, mashairi ambayo hayana sifa hizo hayana thamani yoyote.

Jambo la ajabu ni kwamba, ingawa anajigamba kwamba shairi lake lina urari wa mizani lakini ukweli

ni kwamba shairi hilo, kama yalivyo mengine ya wasanii wa Bongo Fleva, halina urari wa mizani.

Tunaona mstari wa 1 una mizani 20 wakati mstari wa 2 una mizani 25 na mstari wa 3 una mizani 21.

Vilevile tunaona pia msanii Sister P akijigamba kwamba mashairi yake yana urari wa vina. Katika

wimbo wa “Achana Nao” msanii anabainisha hilo kama anavyosema katika ubeti huu:

1. Nafungua ubongo natoa fikra za utumwa kichwani

2. Kipawa chatoka kwa mola wala sijatumia ubani

3. Sister P kupata chati watu wanadhani rap utani

4. Rap biashara bwana ila angalia usijepata hasara

5. Kuuza vitumbua, pipi maandazi zote biashara

108

6. Usidharau hizo biashara watu watakuangushia msala.

7. Wasomi wengi wamesoma kwa kutumia hizo biashara

8. Mashairi sibahatishi na nitauza nyingi nakala

9. Na siyo utani nyota kwangu imeonekana biashara

10. Wandago rafiki zangu tena wa kina

11. We uliza maswali mengi majibu mimi sina

12. Nakupa rap shule mashairi yangu yana vina

Chanzo: Omari (2009:291)

Hapa msanii anabainisha kwamba atauza nakala nyingi na mashairi yake yanakubalika kwa sababu

yana vina (mstari wa 12). Wasanii wengine wanaojigamba kwamba mashairi yao yana vina ni pamoja

na Zay B, Afande Sele, Mr. 2 na Dully Sykes. Hivyo, urari wa vina ni moja ya sifa muhimu

inayoonekana katika mashairi ya Bongo Fleva. Mfano mzuri wa mashairi yenye urari wa vina na

mizani unaonekana katika wimbo uitwao “Moto Chini” ulioimbwa na Mr. 2 kama inavyobainika katika

ubeti ufuatao:

1. Nimeshatoa ngoma UK sasa narudi tena

2. Nairobi na Kampala bado nawakilisha kwa sana

3. Maneno bado ni Yes

4. Naona kama hakuna noma

5. Sasa mechi ni international

6. Sugu ni chama kubwa kama Arsenal

7. Bado nipo dimbani

8. Na maiki ipo mkononi

9. Labda huku nilipo nifuateni

10. Maana inaonekana nitachelewa kushuka chini

11. Inashangaza kuona muda unazidi kwenda

12. Na mchezo wa Hip hop ndo kitu nnachokipenda

13. Check maplayer wenu jinsi ninavyowapiga denda

14. Ni VIP kila kiwanja ninachokwenda

15. Kwani hatari kitu gani

16. Kila wakati nipo bwana TBC extra quality

17. Na wachizi wangu wote sasa zidisheni hasira

18. Ni wakati wa kumaliza huu ni utungo wa kibiashara

19. Sasa ni muda mrefu wanatufanya mafara

20. Tunaingiza mabilioni wanahonga mademu vitara

21. Hamuwezi kunitisha

22. Katika kuthibitisha

23. Nawawasha na tafadhali sahauni kuhusu sugu

24. Maana atazidi tu kuleta mavurugu

25. Na kuwanyonga watu simo

26. Labda ganja zamani kidogo nilikuwemo

27. Na ndo mana mpaka leo bado inanipa misimamo

Ah moto chini

Chanzo: Mr. 2 (2009), Veto

Hapa tunaona msanii anatumia kina cha mwisho -na (mstari wa 1 na wa 2); kina cha mwisho -nal (no)

katika mstari wa 5 na wa 6; kina cha mwisho -ni katika mstari wa 7 hadi wa 10. Vina vingine

vinavyotumika, ni kina cha mwisho -nda katika mstari wa 11 hadi 14; kina cha mwisho -ra katika

mstari wa 17 hadi wa 20; kina cha mwisho -sha katika mstari wa 21 hadi wa 22; -gu katika mstari wa

23 na 24 na kina -mo katika mstari wa 25 hadi wa 27. Hata hivyo, kuna mistari kama vile mstari wa 3

na 4 na mstari wa 15 na 16 ambayo haina urari wa vina. Mistari hii isiyokuwa na urari wa vina

hutumika kama mistari ya mpito inayomwezesha msanii kubadilisha sauti na kuingiza vina vipya

ambavyo ni tofauti na vina vya awali. dhima kubwa ya matumizi haya ya vina ni kwamba yanalifanya

shairi liimbike. Pia vina huweza kuleta mapigo ya kimuziki.

(iv)Matumizi ya Mapigo katika Ushairi wa Bongo Fleva

Aidha, ushairi wa Bongo Fleva unatumia pia mapigo. Mapigo ndio sifa inayoufanya muziki

utofautiane na maongezi mengine ambayo si muziki. Mapigo husababishwa na marudio ya sauti au

sauti zilizopangwa kwa mpangilio maalumu. Dunleavy (1992:9) anaeleza kwamba mapigo ndio msingi

109

wa muziki wowote ule. Ushairi wa Bongo Fleva kwa kuwa ni sehemu ya ushairi nayo yanatumia

mapigo. Mapigo haya zaidi ya kuufanya utungo husika kuweza kuimbika au kughanwa, yanaufanya

utungo huo kutimiza sifa za kuwa ushairi, na hivyo kazi ya fasihi simulizi.

Hata hivyo, kumekuwa na mjadala miongoni mwa wanafasihi kama Bongo Fleva ni ushairi au

sanaa za maonyesho. Mahenge (2009) anaushughulikia kwa kina mjadala huo. Kwa kuwa utafiti huu

hasa unachunguza matini, yaani Bongo Fleva kama ushairi (taz. mawanda ya utafiti katika 3.2.7),

tunaona kwamba Bongo Fleva ni ushairi kama nyimbo za miziki mingine. Hii inatokana na ukweli

kwamba sifa tulizozijadili hapa nyingi zinaufanya uwe na sifa nyingi za kishairi kuliko za sanaa za

maonyesho. Mtazamo huu unaungwa mkono na Omari (2009), Suriano (2006 na 2007) na wasanii

waliohojiwa katika utafiti huu.

(v) Matumizi ya Methali katika Ushairi wa Bongo Fleva

Zaidi ya matumizi ya mapigo, ushairi wa Bongo Fleva unatumia pia methali. Methali kwa mujibu

wa Mulokozi (1996:36) ni usemi mfupi wa kimapokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra na mafunzo

mazito yaliyotokana na tajriba (uzoefu wa maisha) ya jamii husika. Matumizi ya methali katika ushairi

wa Bongo Fleva, yanamaanisha kwamba ushairi huu unakusudia kutoa mafunzo. Maelezo haya

yanaweza kupinga madai yaliyoelezwa hapo awali kwamba ushairi wa Bongo Fleva hupotosha jamii.

Ushairi wa Bongo Fleva, kama tanzu zingine za fasihi simulizi, una dhima ya kuielimisha jamii. Mifano

ya matumizi ya methali yanaonekana katika wimbo wa Zay B uitwao “Siwezi Kuacha.” Anasema:

1.Hii fani jamani haihitaji kiwewe

2.Dua la kuku halimpati mwewe

3.Wacha kupiga mayowe

4.Na kama unaota aliyeko juu mngoje chini

5.Utaingia kaburini bado sijashuka chini

6.Game nalinyaka siyo kama najaribu

7.Vichwa vya kuku hapa mmegonga mwamba

Chanzo: Omari (2009:348)

Methali “dua la kuku halimpati mwewe” na “aliyeko juu mngoje chini” zinasaidia kufikisha maudhui

yake kwa njia. Kwa mfano, katika methali ya kwanza, msanii anaeleza kwamba yeye yupo juu ya

wengine na kwamba wenzake wanamuombea mabaya lakini hayatamfika. Anajifananisha na mwewe na

kuwafananisha adui zake na kuku.

Vilevile matumizi ya methali yanaonekana katika wimbo uitwao “Niko Gado” ulioimbwa na

Zay B. Hebu tuangalie ubeti ufuatao:

1. Domo kama chai jaba makelele mtindo mmoja

2. Mtoto hunyamazi usiniletee pose mambo huyawezi

3. Kama pikipiki basi we batavuzi

4. Kama msichana we kiluzi

5. Huwezi kucheza na anga hizi

6. Kubwa zima kikojozi

7. Ukiulizwa eti oh nilipitiwa na njozi

8. Kumbuka akunyimae mbaazi akupunguzia mashuzi

9. Nakuja live kwako full dose

10.Mimi ndio nyakanga tayari kukupa kozi

11.Bado mpaka mtu atoe machozi

Chanzo: Omari (2009:333)

Kwa kutumia methali “akunyimae mbaazi akupunguzia mashuzi” msanii anakusudia kuwaeleza

wapinzani wake na hasa Sister P ambaye alikuwa anamtenga na kukwepa kushirikiana naye kwamba

anampunguzia “mashuzi.” Methali hii kwa hakika inasaidia kuwasilisha ujumbe wake kwa njia ya

majigambo.

(vi)Matumizi ya Misimu katika Ushairi wa Bongo Fleva

Ushairi wa Bongo Fleva vilevile unatumia kwa kiasi kikubwa lugha za misimu (Omari, 2009:162).

Misimu ni maneno yanayozuka katika kipindi fulani cha kihistoria na kutumiwa na kikundi maalumu

cha watu na hatimaye huweza kupotea. Mulokozi (1996:42) anabainisha kwamba misimu inaweza

kushika mizizi na ikaingizwa katika methali au misemo ya jamii husika. Pia misimu huweza kuingizwa

110

na kuwa msamiati rasmi wa lugha husika. Kuna misimu ya makundi mbalimbali ya wanajamii: misimu

ya wanafunzi, misimu ya wanajeshi, misimu ya madreva, misimu ya wasanii wa Bongo Fleva na

kadhalika. Misimu hii hueleweka na kundi maalumu la watu lakini wakati mwingine huweza

kueleweka kwa jamii pana zaidi.

Ushairi wa muziki wa kizazi kipya umesheheni hazina kubwa ya misimu. Moja ya sababu

zilizoufanya muziki huu hapo awali usikubalike na uonekane wa kihuni ni matumizi ya misimu.

Misimu mingi inayotumika katika muziki huu ni misimu ya vijana ambao wengi wao ndio

wameathirika na suala la ukosefu wa ajira na hivyo kuishia kukaa vijiweni na kutumia madawa ya

kulevya. Aidha, kutokana na ukosefu wa ajira vijana wengi wameishia kuwa wevi, vibaka,

machangudoa, na kujiingiza katika vitendo vingine vinavyoonekana katika jamii kama uhuni. Kutokana

na hili hata misimu inayotumiwa na vijana inaonekana katika jamii kama misimu ya kihuni. Kwa hiyo,

matumizi ya misimu hii yaliufanya muziki huu nao uonekane wa kihuni.

Matumizi ya misimu, hata hivyo, hayapaswi kuchukuliwa kuwa ni kitu hasi bali ni chanya kutokana

na ukweli kwamba misimu ina dhima kubwa katika lugha. Baadhi ya dhima za misimu katika lugha ni

pamoja na kukuza msamiati wa lugha, kupunguza makali ya maneno na kuonesha hisia za watumiaji

wake. Pale misimu inapokua na kusanifiwa, inasaidia kukuza lugha husika. Vilevile matumizi ya

misimu huweza kutunza historia ya jamii husika kutokana na ukweli kwamba misimu husawiri kipindi

cha kihistoria ilipoibuka. Kwa ujumla matumizi ya misimu yanafanya ushairi wa Bongo Fleva kuwa na

dhima kubwa katika jamii. Miongoni mwa misimu iliyotumika katika ushairi wa Bongo Fleva ni

sharobaro (kijana msafi), demu (mpenzi/mwanamke), gemu (muziki), Bongo (Tanzania/Dar es

Salaam), dolali (dola) na kadhalika.

(vii) Usambamba katika Ushairi wa Bongo Fleva

Zaidi ya matumizi ya misimu, ushairi wa Bongo Fleva, hutumia pia usambamba. Kahigi na

Mulokozi (1979:49) wanafasili usambamba kuwa ni takriri ya sentensi au vifungu vya maneno vyenye

kufanana kimaana au kimuundo. Wanaendelea kwa kueleza kwamba usambamba ni sifa muhimu katika

ushairi simulizi. Hivyo, tunaweza kusema kwamba kuna aina mbili za usambamba, usambamba wa

kimuundo na ule wa kisemantiki/kimaana. Matumizi ya usambamba katika fasihi simulizi yanasaidia

kuunda fomula itakayomsaidia fanani kutunga jigambo lake papo kwa papo bila kukariri (Lord,

1981:54). Mfano mzuri wa usambamba tunauona katika wimbo uitwao “Sisi Tulivyo” ulioimbwa na

Sister P:

1. Sisi tulivyo kama utakavyoniona ndio nilivyo

2.Mimi nilivyo siko sawa na jinsi ulivyo

3.Mimi nilivyo hata unavyodhani sivyo nilivyo

4.Mimi nilivyo huwezi kunitambua jinsi nilivyo

5.Mimi nilivyo na huu ndio ukweli wa jinsi nilivyo

6.Mimi nilivyo siyo sawa na manabii jinsi walivyo

7.Mimi nilivyo nina hekima kuliko mtu mzima alivyo

8.Mimi nilivyo na hadhi zaidi ya wafalme jinsi walivyo

9.Mimi ni mchamungu kuliko ulivyo

10.Mimi nilivyo napenda mademu jinsi walivyo

Chanzo: Omari (2009:295-296)

Kutokana na matumizi haya ya usambamba, msanii anawezeshwa kuendelea kuimba ushairi wake bila

kulazimika kukariri shairi zima. Msanii anakariri fomula ya msingi inayojirudiarudia na kisha

kuongezea maneno katika fomula hiyo na hivyo kuunda mstari mpya.

(i) Wahusika katika Ushairi wa Bongo Fleva

Mbali na kipengele cha mtindo, kipengele kingine cha kifani cha ushairi wa Bongo Fleva ambacho ni

muhimu kukijadili hapa ni wahusika. Kama tulivyoona katika majigambo ya majina ya wasanii wa

Bongo Fleva, wahusika wa ushairi wa Bongo Fleva kwa ujumla ni binadamu, wanyama, viumbe wasio

binadamu au hata viumbe wasiokuwa na uhai. Maelezo ya kina kuhusu wahusika wa ushairi wa Bongo

Fleva yametolewa katika kipengele cha majigambo ya majina ya wasanii wa Bongo Fleva hapo awali,

hivyo, hatuna haja ya kukirudia kwa kina hapa.

111

SURA YA SITA

UAINISHAJI WA USHAIRI WA KISWAHILI

Uainishaji ni neno lililozaliwa kutoka katika dhana “aina” yaani namna mbalimbali ya vitu. Hivyo

uainishaji ni kupanga vitu katika aina, namna au makundi. Uainishaji wa ushairi wa Kiswahili pia ni

eneo lingine ambalo ni gumu kulieleza kwa maneno mawili matatu. Ugumu huu unatokana na ukweli

kwamba zipo namna mbalimbali za kueleza aina za ushairi wa Kiswahili. Uainishaji wa awali kabisa

wa ushairi wa Kiswahili ni ule uliofanywa na Mnyampala (1975) ambapo, kama tulivyobainisha awali,

anataja aina tano za mashairi kwa kuzingatia maongozi na mafunzo yanayotoa. Uainishaji kama huu wa

kuzingatia maongozi na mafunzo unaonekana pia kwa El Kaiim (1985:33-44). Yeye anabainisha

kwamba aina za mashairi ni pamoja na mashairi ya kusifu, kutukana, kuomba dua, kutoa shukrani,

kuapiza, kulaumu na kusimanga. Hapa tunabaini jambo moja kwamba El Kaiim anatambua uwezekano

wa shairi kutumia lugha ya utusi ambapo Mnyampala alidai kwamba hauwezi kuitumia. Zaidi ya hawa,

wapo pia wanaoona kwamba kuna aina kuu mbili za ushairi wa Kiswahili ambapo wanaanisha ushairi

wa kimapokeo (huitwa pia ushairi wa jadi) na ushairi wa kisasa (huitwa pia ushairi wa kimamboleo).

Wanazuoni wengine wanaanisha ushairi katika aina kuu tatu ambazo ni mashairi ya simulio, mashairi

ya kidrama na mashairi ya kiwimbo (taz. Shabaya na wenzake, 2009:7).

Jambo moja tunaloliona hapa ni kwamba kila uainishaji unaweza kuwa sahihi kwa namna yake

kwani kila mmoja kati yao ametumia vigezo vyake. Kwa mfano, tunaona uainishaji wa Mnyampala na

El Kaiim unazingatia zaidi kigezo cha dhima ya shairi husika. Kwa namna fulani, Mnyampala pia

anazingatia kigezo cha uhodari na ubora wa shairi husika na hasa anapoainisha aina kama mashairi

mazito, yaani yenye maudhui ya msingi, bila shaka akiyatofautisha na mashairi mepesi, ambayo hayana

maudhui muhimu au ya msingi. Shabaya na wenzake (khj.) wao wanaonekana kuelemea zaidi kigezo

cha mtindo. Hivyo tuhitimishe kwamba kuna vigezo vingi sana vinavyoweza kutumika kuainisha

ushairi na mashairi kwa ujumla. Vifuatavyo ni baadhi ya vigezo vinavyoweza kutumika katika

kuainisha ushairi wa Kiswahili:

· Kigezo cha aina ya uwasilishaji

· Kigezo cha umbo

· Kigezo cha mbinu za kisanaa zinazotumika

· Kigezo cha maudhui yabebwayo na shairi

· Kigezo cha idadi ya mistari

· Kigezo cha bahari

1. Kigezo cha Aina ya Uwasilishaji

Katika kigezo cha uwasilishaji kinachoangaliwa ni jinsi utanzu husika ulivyowasilishwa, yaani

ikiwa umewasilishwa kwa maandishi au kwa masimulizi. Hivyo katika kigezo hiki cha uainishaji kuna

aina kuu mbili za ushairi ambazo ni ushairi simulizi na ushairi andishi. Ushairi simulizi ni ule ambao

unawasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo na mara nyingi huambatana na matendo. Ushairi huu

unahusisha nyimbo mbalimbali kama vile nyimbo za kubembelezea watoto, nyimbo za jandoni na

unyagoni, mbolezi na aina nyinginezo. Aina hii ya ushairi tumeieleza kwa kina katika tanzu za ushairi

wa fasihi simulizi. Aina ya pili ni ushairi andishi. Huu ni ule ushairi ambao unawasilishwa kwa kutumia

hati za maandishi. Mpaka sasa katika lugha ya Kiswahili kuna diwani nyingi zilizokwisha kuandikwa.

Tahadhari haina budi kuchukuliwa hapa kwamba upo uwezekano wa mashairi simulizi kuwekwa katika

maandishi na pia mashairi andishi kusimuliwa. Hata hivyo, mashairi simulizi yanapoandikwa

hayapotezi sifa zake za kisimulizi hali kadhalika na mashairi andishi yanapokuwa simulizi hayapotezi

sifa zake za kuwa andishi.

2. Kigezo cha Umbo

Kigezo cha umbo cha uainishaji wa mashairi kinategemea umbo la shairi husika. Mashairi huweza

kuwa na maumbo mbalimbali ambapo yanaweza kuwa na umbo la kinathari (kisimulizi), umbo la

kitamthilia (kimajibizano) au umbo la kiwimbo. Mashairi ya kisimulizi ni yale yanayosimulia kitu kwa

112

namna ya hadithi. Mashairi haya hufuata kanuni za usimuliaji wa hadithi. Tendi nyingi huwa ni aina hii

ya mashairi maana hubeba hadithi fulani inayosimuliwa.

Zaidi ya aina hiyo, aina nyingine ya ushairi kwa kigezo cha umbo ni ushairi wa kimajibizano.

Ushairi huu huitwa pia ushairi wa kitamthilia au kidrama kwa maana kwamba unafuata kanuni za

kimajibizano. Mashairi haya huwa na wahusika ambao wanajibizana kwa kutumia kauli zao ambazo ni

tofauti na kauli ya mshairi. Wakati mwingine aina hii ya mashairi huweza kuwa na mhusika mmoja tu

ambaye anajibishana na nafsi yake au mhusika anayejibishana na hadhira. Hadhira hiyo inaweza kuwa

dhahiri au ya kufikirika. Sifa kubwa ya mashairi haya ni kuwa na mgogoro, mgogoro ambao unamfanya

mhusika kujibishana na mhusika mwenziye, nafsi yake au hadhira.

Aina ya mwisho ya ushairi kulingana na umbo ni ushairi wa kiwimbo. Ushairi huu huwa na beti na

mistari iliyopangwa vema katika urari wa vina na mizani ili liweze kuimbika. Aina hii ya ushairi ndiyo

iliyokuwa maarufu sana kabla ya kuibuka kwa mashairi ya kisasa miaka ya 1960. Hivyo, hoja ya Amri

Abedi kwamba shairi ni wimbo na kama haliimbiki halina maana yoyote huenda ilitokana na kutawala

kwa aina hii ya mashairi.

3. Kigezo cha Mbinu za Kisanaa Zinazotumika

Kigezo cha tatu cha uanishaji wa ushairi ni kigezo cha kuzingatia mbinu za kisanaa zilizotumika

katika shairi husika. Mbinu za kisanaa tunazozizungumzia hapa ni vina na mizani, miongoni mwa

nyinginezo. Shairi laweza kutungwa kwa kuzingatia urari wa vina na mizani au lisizingatie kanuni hiyo.

Mashairi yanayozingatia kanuni hiyo huitwa ya kimapokeo na mashairi yasiyozingatia huitwa ya

kisasa. Hivyo kwa kutumia kigezo hiki tunapata aina kuu mbili za ushairi: ushairi wa kimapokeo na

ushairi wa kisasa.

Ushairi wa kimapokeo, kama tulivyoeleza awali ni ule wa kijadi, yaani uliokuwapo katika jamii

kwa muda mrefu. Ushairi huu, zaidi ya mambo mengine, unazingatia urari wa vina na mizani kama sifa

yake kuu. Shairi ambalo halizingatii kanuni hiyo huchukuliwa na wanamapokeo kuwa si shairi ama ni

shairi lisilokuwa na ubora wowote. Ushairi wa kisasa kwa upande mwingine ni ule ulioibuka baadaye

na hauzingatii urari wa vina na mizani. Katika aina hii ya ushairi, urari wa vina na mizani si kanuni ya

lazima, shairi laweza kutumia au lisiitumie kanuni hiyo. Kwa kuwa wanausasa hutambua pia mashairi

yenye urari wa vina na mizani kama aina mojawapo ya ushairi wa kisasa, ila si aina pekee, njia bora ya

kumjua mshairi wa kisasa ni kwa kusoma mashairi yake kadhaa na kuona ikiwa yote yanatumia kanuni

hiyo au la. Kama kanuni hiyo haionekani katika mashairi yote basi tunasema kwamba mshairi husika ni

mshairi wa kisasa, lakini kinyume chake tunamchukulia kwamba ni mshairi wa kimapokeo. Mashairi ya

kisasa yasiyozingatia kabisa urari wa vina na mizani huitwa pia mashairi huru, mashairi guni, masivina

na istilahi nyingine kadha wa kadha.

Japokuwa dhana hizi za usasa na umapokeo zimetumika sana katika ushairi wa Kiswahili na kuota

mizizi lakini Samwel (2012a) alihoji usahihi wa dhana hizo ikiwa kweli ni sahihi kuwaita washairi

wanaozingatia kanuni ya urari wa vina na mizani kwamba ni wanamapokeo na wale wasiozingatia

kanuni hiyo wanausasa. Hoja ya Samwel ni kwamba, ushairi usiozingatia urari wa vina na mizani ndiyo

mkongwe kwani hata ushairi simulizi wa Kibantu uliojibainisha katika nyimbo mbalimbali kama vile

mbolezi, nyimbo za jandoni na kadhalika haukuzingatia kanuni hiyo. Hivyo, kwake yeye wanaoitwa

wanamapokeo si wajadi hasa bali ni washairi wa kisasa kwani mtazamo wao si mkongwe bali

ulikuwapo tangu zamani katika jamii mbalimbali. Wanausasa ndiyo wanaostahili kuitwa wanamapokeo

kwani wao wanaturudisha katika ujadi. Mashairi ya Kiswahili yanayozingatia urari wa vina na mizani

uliibuka baada ya Waarabu kuja na kuuathiri ushairi wa Kibantu uliokuwapo. Mtazamo huu wa Samwel

ni muhimu kwani unatoa changamoto kubwa katika mambo ya kinadharia yaliyoonekana kuwa sahihi

kwa muda mrefu.

4. Kigezo cha Maudhui Yabebwayo na Shairi

Kigezo cha maudhui cha uainishaji wa mashairi kinazingatia nyanja ya maisha iliyoangaziwa na

shairi husika. Shairi huweza kubeba maudhui ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Hivyo,

tunaweza kusema kwamba kwa kutumia kigezo hiki kuna aina nne za ushairi ambazo ni ushairi wa

kisiasa, ushairi wa kiuchumi, ushairi wa kijamii na ushairi wa kiutamaduni. Hata hivyo, kigezo hiki ni

telezi mno kwani upo uwezekano wa kuwa na shairi ambalo linasawiri nyanja zaidi ya moja ya maisha.

113

Kwa mfano, shairi laweza kusawiri masuala ya kisiasa lakini wakati huo huo likigusia mambo

mbalimbali ya kijamii na kadhalika.

5. Kigezo cha Idadi ya Mistari

Uainishaji huu huyagawa mashairi katika makundi kulingana na idadi ya mistari katika kila ubeti

wa shairi husika. Shairi huweza kuwa na mstari mmoja katika ubeti hadi mistari kumi na kuendelea,

kila shairi lina jina lake kulingana na idadi ya mistari. Miongoni mwa aina za mashairi tulizonazo kwa

kutumia kigezo hiki ni: tathmina, tathnia, tathlitha, tarbia, takhmisa, tasdisa, tasdia, naudia, telemania

na ukumi.

(i) Tathmina: hili ni shairi lenye mshororo mmoja katika kila ubeti.

(ii) Tathnia: ni shairi lenye mistari miwili katika kila ubeti. Aina hii ya mashairi huitwa pia uwili.

(iii)Tathlitha: aina hii ya ushairi huitwa pia utatu kutokana na ukweli kwamba ni aina ya mashairi

yenye mishororo mitatu katika kila ubeti. Kwa kuwa inadaiwa kwamba bahari ya wimbo huwa

na mistari mitatu kwa kila ubeti mashairi ya utatu huitwa pia wimbo.

(iv)Tarbia: mashairi ya tarbia huitwa pia unne kwa sababu yanakuwa na mistari minne kwa kila

ubeti.

(v) Takhmisa: hili ni shairi lenye mistari mitano katika kila ubeti. Mashairi haya huitwa utano.

(vi)Tasdisa: tasdisa huitwa pia tashilita, sudusia na usita. Haya ni mashairi yenye mishororo sita

katika ubeti.

(vii) Tasadia: ni aina ya mashairi ambayo huwa na mistari saba katika kila ubeti. Hivyo, huitwa pia

usaba.

(viii)Naudia: ni shairi lenye mishororo nane katika ubeti. Huitwa pia unane.

(ix) Telemania: ni shairi lenye mishororo tisa. Huitwa pia utisa.

(x) Ukumi : ni shairi lenye mishoro kumi.

6. Kigezo cha Bahari

Kwa muda mrefu kigezo cha bahari kimetumika kuainisha mashairi ya kimapokeo. Hii inatokana na

ukweli kwamba waandishi wengi wa awali walizingatia kwamba katika kigezo hiki cha uainishaji wa

mashairi kwa kutumia bahari kinachozingatiwa zaidi ni idadi ya mistari iliyopo katika beti na jinsi

mistari hiyo ilivyogawanywa katika vipande. Sifa ya shairi kuwa na beti na mistari inaonekana katika

mashairi ya kimapokeo tu. Kutokana na hilo uainishaji huu kwa muda mrefu umeitwa bahari za

mashairi ya kimapokeo au bahari za mashairi ya kijadi (taz. Mulokozi, 1996:125-135).

BAHARI ZA USHAIRI WA KIMAPOKEO

Kumekuwa na mvutano miongoni mwa wanazuoni na wataalamu wa ushairi juu ya dhana hii ya

bahari na hasa katika kueleza idadi ya bahari zilizopo na bahari hizo ni zipi hasa? Wapo wanaodai

kwamba kuna bahari tatu, wengine tano na kadhalika. Aidha, wapo wanaoona kuwa bahari hizi

zinahusisha aina za mashairi kimuundo kama tulivyoeleza katika kigezo cha idadi ya mstari na wapo

wanaopinga hilo. Kwa mfano, uainishaji wa bahari wa Mutua (2006:18-20) unahusisha pia tathmina,

tathnia, tathlitha, tarbia, takhmisa, tasdisa, kikai, msuko, sarakani na kadhalika. Uainishaji huu unaweka

pamoja uainishaji wa mashairi kwa kuzingatia idadi ya mistari na kwa kuzingatia kile kinachoitwa na

wengine bahari. Lakini bila kujiingiza katika mjadala wa idadi ya bahari na uhakika wa bahari hizo,

tutapitia hapa bahari zote zinazotajwa kuwapo katika ushairi wa kijadi. Kwa kuwa “bahari” za ushairi

kwa kuzingatia idadi ya mistari tumeshazibainisha hapo awali, katika sehemu hii bahari tutakazozipitia

ni shairi, wimbo, utenzi/utendi, ngonjera, kikwamba, zivindo, ukawafi/kawafi, ukara, wajiwaji,

Hamziyya, Mandhuma, msuko, wawe, sarakani, kimai na kikai.

(i) Shairi

Ni utungo wenye mishororo minne kila ubeti na vipande viwili vya mizani nane nane kila kipande.

Hii ndiyo bahari maarufu zaidi katika utunzi wa mashairi ya Kiswahili na watunzi wengi wa ushairi wa

Kiswahili wamezingatia sifa hii. Mfano ni shairi liitwalo “Tukomesheni Ajira za Watoto” katika Mutua

(2006:32):

Natunga nikiwaasa, watoto kutowajiri

Nawaelezea hasa, ya mambo yalivyojiri

114

Ni kinyume shika sasa, huo ukweli mukiri

Komeni tena komeni, watoto kuwaajiri

Wa ubwana kupigia, nyingi mali kuzalisha

Migongo wamedandia, ya wana kutumikisha

Damuyo kujinyonyea, ili kujitajirisha

Komeni tena komeni watoto kuwaajiri

Katika shairi hili tunaona kuwa kila ubeti una mistari minne iliyogawanyika katika vipande viwili na

kila kipande kina mizani nane (jumla mizani kumi na sita). Kwa mfano, mstari wa kwanza wa ubeti wa

kwanza “Natunga nikiwaasa, watoto kutowajiri,” kipande cha kwanza ni “natunga nikiwaasa” na

kipande cha pili “watoto kutowajiri.” Kipande “natunga nikiwaasa,” kina mizani nane (na-1, tu-2, nga-

3, ni-4, ki-5, wa-6,a-7,sa-8) na kipande “watoto kutowajiri,” kina mizani nane (wa-1, to-2, to-3, ku-4,

to-5, wa-6, ji-7, ri-8)

(ii) Wimbo

Kwa mujibu wa wanamapokeo bahari ya wimbo inahusisha utungo wenye mishororo mitatu katika

kila ubeti. Kila mshororo huwa na vipande viwili. Wimbo unaweza kuwa na vina au la. Bahari hii ni ya

kijadi na imekuwapo kwa muda mrefu sana katika historia ya ushairi wa Kiswahili. Mfano mzuri wa

wimbo tunauona pia katika Mutua (2006:30). Wimbo huo umepewa jina “Haki za Binadamu:”

Kwa jina lake Jalia, muumba wa nchi na mbingu

Aloumba nisia, na wengi viumbe chungu

Rabi mola metimia, kwake hakuna tewengu

(iii) Utendi/Utenzi

Ni shairi refu lenye beti nyingi ambazo zina mizani chache au mishororo mifupi ambayo kwa asili

haina vina vya kati kama yalivyo mashairi ya kawaida. Tenzi/tendi kwa kawaida huwa na maudhui ya

kidini, vita, ushujaa, tukio la kizamani au la historia. Utendi huweza kugusa pia maisha ya mashujaa:

kuzaliwa, shida zao, vita na matendo yao ya kishujaa, vifo vyao, nk. Matukio haya huwa ya kihistoria

ila huweza kuchanganya na visakale na visasili. Mifano mizuri ya tenzi ni: Utenzi wa Nyakiiru Kibi,

Utenzi wa Adamu na Hawaa, Utenzi wa Fumo Liyongo, Utenzi wa Vita vya Maji Maji na Utenzi wa

Vita vya Mau Mau.Kwa mfano, Utenzi wa Nyakiiru Kibi unaelezea historia ya ukoo wa Babito na

kiongozi wao aitwaye Nyakiiru Kibi. Utenzi huu una beti mia nane tisini na mbili (892). Utenzi wa

Adamu na Hawaa ni mrefu pia na unaelezea maudhui ya kidini ambayo pia yanaaminika kuwa ya

kihistoria na kadhalika.

Bahari ya utendi/utenzi imezua mjadala miongoni mwa wanafasihi kwa muda mrefu. Ruth Finnegan

(1970) alidai kwamba utendi haupo katika bara la Afrika. Finnegan alielemea vigezo vikuu vinne vya

utendi Kiaristotle. Sifa hizo ni:

a) Nudhumu (verse): utendi uwe ni utungo wa kishairi na si wa kinathari

b) Urefu (length): ni utungo mrefu wa kutosha

c) Uunganifu (unity): ni utungo wenye visa/hadithi vilivyounganika kimantiki katika mtiririko

na msuko wake wa matukio na si matukio mparaganyiko yasiyohusiana.

d) Maudhui (subject matter): husimulia juu ya maisha na matendo ya kishujaa ya mbabe wa

utendi, kwa mfano kuzaliwa, masaibu yake, safari zake, uongozi wake kwa watu wake na kifo

chake.

Baada ya kuchunguza matini kadhaa zilizodaiwa na wahariri wake kuwa ni tendi akafikia

hitimisho kwamba tendi hazipo katika bara la Afrika kwani hizo si tendi. Nyingi kati ya matini hizo

wahariri wake hawakuzitoa katika muundo wa kishairi hivyo kuishia kuwa masimulizi ya kinathari.

Miongoni mwa matini hizo ni Sundiata, Mugasha na Mwindo. Kauli hii ya Finnegan ilizua mjadala

mzito na kama anavyosema Mulokozi (2002:2) miaka ya 1970 ilichukuliwa kuwa ni ya mjadala wa

kauli hiyo. Hata hivyo, kwa sasa mjadala huu umefikia mwisho kwani wataalamu wanakubaliana

kwamba Afrika ina tendi. Mjadala uliosalia sasa ni tendi hiyo ya Kiafrika ipoje?

Tunaona utendi tuuchukulie kwa Mtazamo wa Mulokozi (2002) kwamba una sifa zifuatazo:

(a) Ni masimulizi

(b) Hutolewa kishairi

(c) Huhusu matukio muhimu ya kihistoria na kijamii

115

(d) Huelezea habari za ushujaa na mashujaa

(e) Huwasilishwa kwa kughanwa (au kuimbwa) pamoja na ala za muziki

(f) Hivyo, utendi hutawaliwa na muktadha wa utungaji na uwasilishaji wake kwa jamii.

Zaidi ya kuchukua mtazamo wa Mulokozi (2002) kuwa ndiyo bora, tunaona sifa moja kati ya saba

alizozitaja hatutaitumia, matini (maneno) yake kwa kawaida hutungwa papo kwa papo, japo kisa au

hadithi yenyewe huwa ya kimapokeo. Sifa hiyo ni ile isemayo, “utendi haukaririwi (hautungwi kabla na

kuhifadhiwa kichwani kwanza ili baadaye utolewe kwa ghibu).” Tunaiacha sifa hii kutokana na ukweli

kwamba kutokana na mtazamo wetu, utendaji wa utendi na fani nyingi za fasihi simulizi (zilizodaiwa

kutendwa papo kwa papo) huhusisha kukariri kwa namna fulani.

Mulokozi (2002:127-170) anabainisha kwamba fanani wa utendi (na tanzu mbalimbali za fasihi

simulizi) hakariri bali hutunga kazi yake papo kwa papo wakati wa utendaji wake, kinachomsaidia

fanani kufanya hivyo ni topo na fomula iliyomo kichwani kwake. Mulokozi (khj.) anadai kwamba

fanani anakariri topo ambazo huzijazia maneno anayoyatunga wakati wa utendaji. Topo hizo huwa ni

hadithi nzima. Hata hivyo, tunaona kwamba topo hizi hukaririwa na hivyo bado kuna kukariri kabla ya

utendaji wake. Hii inatufanya tuone kwamba inaweza isiwe sahihi sana kusema kuwa tendi

hazikukaririwa.

(iv)Ngonjera

Mmbaga (2004:43) anafasili ngonjera kuwa ni utanzu wa ushairi ambamo twakuta mahojiano au

malumbano kati ya mhusika na mhusika, mhusika na wahusika au wahusika kwa wahusika. Hivyo,

twaweza kusema kuwa ngonjera ni ushairi wa majibizano ambao hutolewa baina ya watu wawili au

vikundi viwili vya watu kwa kupokezana. Mmbaga (khj.) anaendelea kubainisha kuwa ngonjera, tofauti

na nyimbo na mashairi, huwa haziimbwi bali husemwa. Katika ngonjera kunakuwa na majibizano

kuhusu mada fulani inayowatatiza wahusika au mmoja wa wahusika katika majibizano hayo na

mhusika mwingine hujaribu kumpa ufafanuzi juu ya mada hiyo. Kwa kawaida majibizano haya huwa ni

ubeti kwa ubeti ambapo mhusika mmoja hutoa ubeti mmoja na mwingine humjibu katika ubeti

unaofuata. Mfano mzuri wa ngonjera za aina hii tunaziona katika Mmbaga (khj.) kama anavyomnukuu

Muyaka:

MDENI

Nilime mnda Ngozini, ule wangu mjuawo

Pata kata ishirini, na mbili zipungushewo

Hawauza hutendani, nionyani zitendwawo

Mke yu ataka nguo, name nawiwa kikanda

RAFIKI

Karejee ngozi mbamba, winike yako mamungo

Mpiga n anti yembe, huinua nililo kongo

Mke mrari au membe, kwa kweli au kwa uwongo

Deni uongeze kiwango, mwenye deni takulinda

Katika ngonjera hii tunaona kuna wahusika wawili ambao wanajibizana juu ya suala la deni. Mmbaga

anaeleza kuwa mtindo huu wa ushairi ni mkongwe zaidi na ulionekana pia kwa malenga wa kale. Mbali

na majibizano kuwa katika ubeti kunaweza kuwa na majibizano katika mistari ambapo mhusika mmoja

anasema mstari mmoja na mwingine kumjibu katika mstari wa pili. Mfano mzuri wa ngonjera hizi pia

tunauona kwa Mmbaga (khj.) anapotoa ngonjera ya jadi ya Kipare:

Msimulizi

Ichua ne mvu velahane

Mvu

Uiao kidoho na singo wesina?

Ichua

Hanini weghereke ghati?

Mvu

Nihala nesila nicho neghereke ghati

Tafsiri:

Msimulizi

Chura na nyigu walishtakiana

Nyigu

116

Unalia bure wala shingo huna

Chura

Mbona wewe u mwembamba kiunoni?

Nyigu

Ni kwa vile mie sili ndio maana ni mwembamba kiunoni

Mifano mingine ya ngonjera tunaiona katika Mnyampala (1970) Ngonjera za UKUTA na Wamitila

(2005) Tamthilia ya Maisha miongoni mwa vingi vingine. Kwa mfano, shairi la “Kuhalalisha Maovu”

katika Wamitila (2005) lililoandikwa na Kineene wa Mutiso ni la kingonjera ambapo kuna majibizano

baina ya tajiri na mnyonge. Katika shairi hilo tunaona kuna majibizano baina ya tajiri na mnyonge

kuhusu utajiri unavyopatikana. Suluhisho la majibizano hayo linapatikana katika ubeti wa mwisho.

(v) Kikwamba

Hii ni bahari ambayo mashairi yake hutumia neno moja mwanzoni mwa kila mshororo. Hii ni

kusema kwamba mashairi haya huanza na neno lilelile katika mistari yake yote. Lengo la msingi la

takriri hii ni kusisitiza na pia kulipendezesha shairi husika kwa kuweka usambamba. Mfano mzuri wa

mashairi ya aina hii tunaona katika Muzale (2009) kwenye shairi la “Kifo” katika Diwani yake iitwayo

Nakuomba. Katika shairi hilo tunaona kuwa mshairi ameanza na neno “kifo” katika mistari yote ya beti

zake zote ishirini na mbili (22). Tazama, kwa mfano, ubeti wa kwanza na wa pili:

Kifo ninakuimbia, sauti kali hewani,

Kifo ninakulilia, chozi hadi miguuni,

Kifo ninakutungia, shairi lenye thamani,

Kifo ninakuinamia, bila kofia kichwani.

Kifo naomba tulia, sikio nalitamani,

Kifo nakusimulia, majonzi ya duniani,

Kifo sote tunalia, huzuni tele rohoni,

Kifo unatusumbua, hatuna tena amani.

(vi)Zivindo

Ni bahari ya kishairi ambayo mashairi hutungwa kwa lengo la kufafanua maana mbalimbali za neno

moja katika lugha ya Kiswahili. Kila lugha duniani, Kiswahili kikiwemo, ina maneno ambayo huwa na

maana mbalimbali. Maneno ya aina hii huweza kuwachanganya watumiaji wa lugha husika. Hivyo,

mashairi haya hukusudia kufafanua maana hizo na kukuza ujuzi wa lugha wa hadhira husika. mfano wa

zivindo tunaziona katika Muzale (2009:74-78) ambapo anafafanua maana za maneno “ulevi” na “utu”

katika mashairi aliyoyaita “Ulevi” na “Utu” mtawalia. Katika shairi la ulevi, mshairi anabainisha kuwa

kuna maana mbalimbali za neon ulevi. Anazitaja maana hizo kuwa ni ulevi wa pombe, bangi na hata

wanawake na kadhalika. Kuhusu utu anafafanua kuwa utu ni mtu kuwa na heshima kwa kusalimia

watu, kuwa na akili timamu, kufanya kazi kwa bidii na kadhalika. Tuchunguze shairi la “Ulevi:”

Kuna wa pombe ulevi, na wengi wake walevi,

Alobobea mlevi, aenda kama kiwavi,

Atalala kwenye jamvi, jamala yake ugomvi,

Hana heshima mlevi, hakosi kuwa mchimvi.

Moshi ulevi wa pili, kazi kuharibu mwili,

Mapafu yakihimili, wavuta bila kujali,

Sigara sumu ya mwili, tumbaku ni sumu kali,

Tumia yako akili, usitafute ajali.

Kulewa televisheni, hiyo nayo ni balaa,

Wanashinda barazani, macho wakiyakodoa,

Kabumbu peke kichwani, mengine wameyaondoa,

Ni ulevi si utani, ushabiki usiofaa.

(vii) Ukawafi au kawafi

Aina hii ya bahari huhusu shairi lenye mistari mitatu au zaidi na wenye vipande vitatu kila

mshororo huku kila kipande kikiwa na kina chake. Katika ushairi vipande hivi vina majina; kipande cha

117

kwanza huitwa ukwapi, cha pili utao na cha tatu mwandamizi. Muundo wa msingi wa bahari hii ya

ushairi huwa kama ifuatavyo:

Ukwapi utao mwandamizi

_________ ___________ ____________

Mfano mzuri wa mashairi yanayoingia katika bahari hii ni shairi la “Biashara” lililopo katika Mbarwa

(2000:11) kama linavyonukuliwa hapa chini:

Biashara ni hasara, huwaka moto, ni kujitolea

Haitaka fikara, ila mvuto, inaweza kolea

Mbiashara busara, impa mapato, na kuendelea

Inahitaji upangaji, ugunduzi, na uvumilivu

Ukaribishaji, utii utumizi, na utulivu

Awe mlipaji, mkakamizi, haitaki ulegevu

(viii) Ukara

Bahari hii mashairi yake huwa na vipande viwili katika kila mshororo, utao na ukwapi, huku

kipande cha pili, ukwapi, kikiwa na vina ambavyo ni irabu. Vina hivyo katika ukwapi, hata hivyo,

hubadilikabadilika katika kila mshororo. Mfano wa kufikirika wa ukara huweza kuwa kama

inavyooneka hapa chini:

Ubeti wa 1: ___________________ni, ________________a

___________________ni, ________________e

___________________ni, ________________i

___________________ni, ________________u

Ubeti wa 2: ___________________ni, ________________u

___________________ni, ________________i

___________________ni,________________e

___________________ni, ________________o

Ubeti wa 3: ___________________ni, _________________o

___________________ni, _________________e

___________________ni, _________________a

___________________ni, _________________u

___________________ni, _________________i

(ix)Wajiwaji au Takhmisa

Hii ni bahari ambayo huwa na mashairi yenye mistari mitano katika kila ubeti. Kutokana na hilo,

mashairi yote yenye mistari mitano huitwa takhmisa. Kwa kawaida mashairi haya huwa na mizani kumi

na tano (15) kila mshororo ambapo si lazima yawe na vina vya kati lakini una vina vya mwishoni.

Mfano mzuri wa aina hii ya mashairi ni “Takhimisa ya Liyongo” ambayo kimsingi yalikuwa yakimsifu

Fumo Liyongo, shujaa wa Kiswahili anayeaminika kuishi huko Pate. Mashairi haya yaitwayo

“Takhmisa ya Liyongo” yalitungwa na Sayid Abdalla Bin Ali bin Nasir. Tazama ubeti ufuatao:

Nabudi kawafi takhmisi kidiriji,

Niwathihishe izagale kama siraji,

Ili kufuasa ya Liongo samba wa miji,

Ai wanji nazawanji kisiza wanji; na

Kadiliza kasiliza, mwanangu mema

Mfano mwingine wa takhmisa unaonekana katika shairi la “Mkulima” katika Mbarwa (2000:36):

Hubarikiwa Mola na jasho lake

Yeye huwa saa zote shambani lake

Hujuwa vizuri ukubwa wa soko lake

118

Amejiajiri tayari shambani lake

Mkulima huwa na bidii na mpango kanuni

Hupata mkopo benkini ya washiriki

Huwa anapo kadri benkini ya ushiriki

Huwapo usahibu na wengine washiriki

Hupatia ananapo misaada na washiriki

Mkulima huwa na bidii na mpango kanuni

(x) Hamziya

Bahari hii ilipewa jina kutokana na utenzi maarufu wa Kiarabu ulioitwa Utenzi wa Hamziyya

ulitungwa na Mmisri Muhammad bin Said Al- Buswiri/al-Busiri ambao ulikuwa ni simulizi ya maisha

ya Mtume Mohammad (S.A.W). Utenzi huo ulipewa jina la Hamziya kutokana na ukweli kuwa ulikuwa

na urefu wa mizani thelathini (30) na uliishia na herufi ya 29 ya lugha ya Kiarabu. Katika herufi za

Kiarabu kuna herufi thelathini na herufi ya 29 huitwa hamza. Hivyo, kwa kuwa utenzi huu uliishia na

herufi ya ishirini na tisa (hamza) ndiyo ukapewa jina kutokana na herufi hiyo. Utenzi huu ulitafsiriwa

katika Kiswahili na Said Aidarus bin Athman kutoka Pate-Kenya mwaka 1652/1749. Hata hivyo,

izingatiwe kuwa tafsiri ya utenzi huo katika Kiswahili, kwa kuwa hautumii herufi za Kiarabu, hauishii

tena na herufi hamza ya Kiarabu (kama ilivyokuwa katika utenzi asilia) (Maelezo mengi kuhusu bahari

hii tumeyadondoa katika Mulokozi, 1996 na Kineene wa Mutiso, 2005). Kwa hiyo, katika Kiswahili

utenzi wowote wenye mizani thelathini, kama ilivyokuwa kwa Utenzi wa Hamziyya, unaingia katika

bahari hii ya ushairi.

(xi)Mandhuma

Mandhuma ni aina ya bahari ambapo mashairi yake huwa na ukwapi na utao isipokuwa ukwapi

hutoa wazo ambalo ni fumbo na kisha fumbo hilo linafumbuliwa katika utao. Mfano mzuri wa shairi

linaloingia kwenye bahari hii ni shairi la “Moyo” lililopo katika Wamitila (2005) Tamthilia ya Maisha

kama linavyonukuliwa katika ubeti ufuatao hapa chini:

Moyo waniambia ota, kuwa mwizi usiote, siwe kaini,

Moyo wanambia kata, mirija yote ikate, mizizini,

Moyo wanambia teta, penye dhuluma patete, andikoni,

Moyo wanambia woga, ndiyo mwanzo wa maafa.

(xii) Msuko

Msuko ni bahari ya ushairi ambayo huwa na kibwagizo, kibwagizo hicho, kwa kawaida huwa ni

kifupi (kina maneno machache) kuliko mishororo mingine katika ubeti husika. Mfano wa msuko

tunauona katika shairi la Mahiri Mwita liitwalo “Nimo” lililomo katika Wamitila (2005). Tazama ubeti

huu:

Nimo ndimo mi nilimo, simo simostahili,

Nimo niwajibikamo, simo mwenye ujahili,

Nimo nikusudiamo, simo wanamodhalili,

Nimo na nitakikamo, simo name kwa thakili,

Nimo kwa kina na kimo, simo mwa wasiobali

Nilimo nimo.

(xiii) Wawe/ Vave

Matamshi tofauti baina ya wawe au vave ni ya kilahaja. Wawe ni bahari ya ushairi inayohusisha

tungo za kishairi ambazo huimbwa wakati wa kufanya kazi, hasa kilimo (kufyeka, kulima, kukata

magugu, kuchoma moto magugu na kadhalika). Tungo hizi zinaweza kuwa na urari wa vina na mizani

au zisiwe nao. Mifano ya tungo hizi inapatikana katika Mulokozi (1996).

(xiv) Sakarani

Bahari hii ni mchanganyiko wa bahari kadhaa katika shairi moja. Hii ni kusema kwamba katika

bahari hii kuna aina mbalimbali za mashairi katika ubeti mmoja au katika shairi moja. Shairi linaweza

kuwa kikwamba na wakati huohuo likawa msuko, au shairi likawa wimbo na wakati huohuo likawa

119

kikwamba na kadhalika. Aidha, shairi moja linaweza kuwa na mashairi ya mistari mitatu, mistari

minne, mistari mitano, mistari sita na kadhalika. Mfano mzuri wa shairi la aina hii ni shairi la Mahiri

Mwita la “Nimo” tulilolinukuu hapo awali. Hebu tuchunguze tena ubeti huu:

Nimo ndimo mi nilimo, simo simostahili,

Nimo niwajibikamo, simo mwenye ujahili,

Nimo nikusudiamo, simo wanamodhalili,

Nimo na nitakikamo, simo name kwa thakili,

Nimo kwa kina na kimo, simo mwa wasiobali

Nilimo nimo.

Kwa hakika ubeti huu unakidhi sifa za kuwa katika bahari ya kikwamba, kwa maana ya kwamba shairi

linaanza na neno moja “nimo” katika kila ubeti, na pia unakidhi sifa za kuwa katika bahari ya msuko,

kwa maana ya kuwa lina kibwagizo kilichofupishwa. Vilevile shairi la Nyambari Nyangwine liitwalo

“Kilio cha Paka” katika Wamitila (2005) linaonekana kuwa na beti mchanganyiko, kuna beti zenye

mistari mitatu, beti zenye mistari mitano, beti zenye mistari sita, beti zenye mistari saba na kadhalika.

(xv) Kimai

Bahari ya kimai inahusu nyimbo zinazoimbwa katika shughuli mbalimbali za baharini. Hizi

hujumuisha nyimbo za mabaharia, wavuvi na wasafiri wa vyombo vya baharini. Nyimbo hizi hazina

idadi kamili ya vina na mizani na pia suala la urari wa vina na mizani si la lazima. Mifano mizuri ya

ushairi unaoingia katika bahari hii tunaiona katika Mulokozi (1996) na King’ei na Kisovi (2005)

miongoni mwa wengi wengineo. Kwa mfano, katika King’ei na Kisovi (2005:145) tunaona wimbo

ufuatao:

Mwana wa maji wa kale, mjuzi wa kazi yangu

Kufa maji nizowele, kufunda kazi yangu

Mwana wa maji na maji, maji yatanitendani?

(xvi) Kikai

Bahari hii, kwa kawaida, huwa na mishororo yenye vipande viwili, ukwapi na utao, ambapo kwa

asili yake huwa na mizani kumi na mbili (12), ambapo ukwapi huwa na mizani nne na utao mizani

nane. Bahari hii pia huhusisha mikondo mingine ya ushairi ikiwa ni pamoja na mashairi yenye mizani

nane kwa sita, nane kwa tatu na tano kwa nane (Mutua, 2009:19). Mutua (khj.) anatoa mfano wa shairi

la bahari hii lenye mizani tano kwenye ukwapi na nane kwenye utao kama ifuatavyo:

Likichomoza, jua liote haraka,

Likiangaza, mapema kazi rauka,

Likikoleza, hifadhi zako nafaka

Likituliza, basi nenda pumzika

UPUNGUFU WA KIGEZO CHA BAHARI ZA USHAIRI ZA KIMAPOKEO

Uainishaji wa ushairi kwa kigezo cha bahari umesemwa kuwa na mapungufu mengi. Mapungufu hayo

yamebainishwa kwa kina na Mulokozi (1996). Katika mjadala wetu tutabainisha udhaifu huo ili tufike

mahali na kuwa na muainisho ambao labda utakuwa bora kiasi cha kuondoa upungufu huo:

1. Kigezo hiki kinatumika kuainisha aina moja tu ya ushairi: ushairi unaoainishwa kwa kigezo

hiki, hadi sasa, ni ushairi wa kimapokeo. Hii ina maana kwamba kwa kutumia kigezo hiki

ushairi wa kisasa hauainishwi. Hii, kwa maana ya urejezi ni kwamba ushairi wa kisasa si ushairi

na hivyo haupaswi kuainishwa.

2. Kigezo hiki kinachanganya sana vigezo vingi vidogovidogo (bila kuvifafanua). Kuna baadhi ya

fasili za bahari ambazo zinatudokeza kwamba kigezo kidogo kilichotumika ni idadi ya mistari

lakini bahari nyingine zinadokeza kigezo cha urefu na aina ya mistari, nyingine ni maudhui,

muktadha na kadhalika. Hivyo, kuna mkanganyiko mkubwa sana hapa.

3. Bahari hizi zina ukomo wake, zipo aina nyingi za ushairi wa kijadi zinazoweza kutungwa

ambazo zinaweza zisiingie katika bahari yoyote kati ya hizo. Hatari iliyopo ni kwamba kuna

120

uwezekano wa ushairi wa aina hiyo kuonekana kuwa si ushairi kwani hauingii katika bahari

yoyote.

Kutokana na upungufu huu tunaona kwamba kuna haja ya kuainisha bahari kwa namna ambayo

itapunguza ama kuondoa kabisa kasoro hizo. Hivyo katika uainishaji wetu tumeainisha bahari kwa

kuzingatia aina zote za mashairi (mashairi ya kimapokeo na kisasa) na kwa kuzingatia vigezo

vilivyobainishwa wazi ili ijulikane wapi tunatumia kigezo gani kupata aina gani ya bahari.

BAHARI ZA USHAIRI WA KIMAPOKEO NA KISASA

Katika andiko letu tunachukulia kwamba uainishaji wa kutumia kigezo cha bahari ni uainishaji wa

ushairi unaoweza kutumika katika aina zote za ushairi. Aidha, tunachukulia kwamba kigezo hiki kina

vigezo vidogo vidogo vingi. Miongoni mwa vigezo hivyo ni kigezo cha vipande vya mishororo, kigezo

cha aina ya kiishilio, kigezo cha urari wa vina na mizani, kigezo cha uradidi, kigezo cha madhumuni ya

utungaji na kigezo cha muundo.

· Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Beti, Mishororo na Vipande

· Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Aina ya Kiishilio

· Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Urari wa Vina na Mizani

· Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Uradidi

· Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Madhumuni ya Utungaji

· Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Muundo

Kwa kuwa katika sehemu iliyopita tulishafafanua kwa kina bahari mbalimbali na kutoa mifano

ilipobidi, katika sehemu hii hatutoa maelezo marefu wala mifano mingi ya bahari hizo, isipokuwa pale

tu kutakapokuwa na haja ya kufanya hivyo.

1. Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Beti, Mishororo na Vipande

Katika kigezo hiki ushairi unaainishwa kwa kuzingatia shairi husika lina mishororo mingapi katika

beti na kila mshororo una vipande vingapi? Kwa kutumia kigezo hiki, kwa hiyo, tunapata aina zifuatazo

za mashairi:

(i) Shairi

Shairi ni dhana pana inayobeba aina nyingine za bahari. Bahari hii inajumuisha tungo zote ambazo

si za kinathari kwa uasili wake. Inajumuisha tungo zenye lugha ya mkato, lugha ya kishairi, na nduni

nyingine bainifu za ushairi kama tulivyobainisha hapo awali. Kwa hiyo, hata wimbo huweza kuwa na

mashairi, utendi huweza kuwa na mashairi na kadhalika.

(ii) Wimbo

Hii ni bahari ambayo inahusisha tungo zenye mishororo katika kila ubeti. Hata hivyo, idadi ya

mishororo katika ubeti inategemea uwezo wa mtunzi husika. Aidha, si lazima idadi ya mishororo katika

kila ubeti wa shairi husika ilingane, inaweza kutofautiana. Kwa kawaida kila mshororo katika bahari hii

huwa na vipande viwili, lakini yapo mazingira ambapo kaida hiyo huweza kukiukwa. Vilevile, wimbo

unaweza kuwa na vina au la.

(iii) Utendi/utenzi

Utendi ni shairi ambalo huwa na kipande kimoja cha mshororo na mizani chache katika mshororo

(kwa kawaida kati ya mizani nne hadi kumi na mbili). Utendi huwa na vina vya mwisho pekee na

huwa ni simulio (hadithi) ndefu kuhusu matukio ya kihistoria, mashujaa, dini na mambo mengineyo

mbalimbali.

(iv)Tumbuizo

Bahari ya tumbuizo huhusu tungo ndefu zenye mishororo mingi lakini si lazima ziwe na urari wa

mizani na vina. Kwa asili yake, tumbuizo zilikuwa na kina kimoja tu cha mwishoni au vina tofauti

katika mistari tofauti.

121

(v) Ukawafi au kawafi

Hii ni aina ya bahari inayojumuisha mashairi yenye mistari mitatu au zaidi na yenye vipande vitatu

kila mshororo huku kila kipande kikiwa na kina chake. Vipande hivyo ni: ukwapi, utao na

mwandamizi. Maudhui ya kawafi nyingi kuhusu dini ingawa zipo chache zizonahusu masuala ya

kidunia.

(vi)Wajiwaji au Takhmisa

Hii ni bahari ambayo huwa na mashairi yenye mistari mitano katika kila ubeti. Kutokana na hilo,

mashairi yote yenye mistari mitano huitwa takhmisa. Kwa kawaida mashairi haya huwa na mizani kumi

na tano (15) kila mshororo ambapo si lazima yawe na vina vya kati lakini una vina vya mwishoni.

(vii) Gungu

Hii ni aina ya ushairi ambao una mizani zaidi ya kumi na mbili katika kila mshororo na hali huwa

hivyo katika mishororo yote. Kwa hakika gungu ni aina mojawapo ya utenzi ila tofauti iliyopo baina ya

tenzi na gungu ni kwamba utenzi huwa na mizani michache katika mshororo wakati katika gungu

mizani huwa mingi zaidi. Tenzi huwa na mizani kati ya 4-12 wakati gungu huwa na mizani 12.

(viii) Mathnawi/ Mathinawi

Mathnawi ni aina ya bahari inayohusu mashairi ambayo kila mshororo huwa na vipande viwili:

ukwapi na utao na kwa hiyo huwa na vina viwili: vya kati na vya mwisho.

Ukwapi utao

____________________na _________________li

____________________na _________________li

____________________na _________________li

(ix)Bantundi

Bahari hii hujumuisha aina ya mashairi ambayo huwa na vipande vinne katika kila mshororo, yaani

ukwapi, utao, mwandamizi na ukingo. Kwa mfano:

Utao ukwapi mwandamizi ukingo

____________lo ______________ma ___________ni _____________mba

2. Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Aina ya Kiishilio

Katika kigezo hiki tunaainisha mashairi kwa kuzingatia kuwapo au kutokuwapo kwa kiishilio

(kituo), urefu au ufupi wa kiishilio na kadhalika. Kiishilio kama kinavyotumika hapa ni mshororo wa

mwisho katika ubeti ambao hujirudiarudia (kituo bahari). Kama mshororo husika haujirudii huitwa

kimalizio. Hivyo, kwa kutumia kigezo hiki tunapata aina zifuatazo za ushairi:

(i) Msuko

Msuko ni aina ya ushairi ambao kiishilio kimefupishwa, yaani kimesukwa kwa namna ambayo

kimekuwa kifupi zaidi kuliko kilivyopaswa kuwa kama kingetumia maneno ya kawaida. Mfano

unaonekana katika shairi la Mahiri Mwita litwalo “Nimo” tulilolinukuu hapo awali.

(ii) Sabilia

Sabilia ni aina ya ushairi ambao kwa kawaida hauna kiishilio bali huwa na kimalizio. Mshororo wa

mwisho katika aina hii ya ushairi huwa hakirudiwi bali kinabadilikabadilika na hivyo huwa kama

kimalizio tu lakini si kiishilio/kituo. Mfano mzuri wa mashairi haya unaonekana katika mashairi mengi

yaliyomo katika sehemu ya pili ya kitabu hiki.

3. Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Urari wa Vina na Mizani

Katika kigezo hiki ushairi huainishwa kwa kuzingatia kuwapo au kutokuwapo kwa urari wa vina,

urari wa mizani au vyote pamoja. Aidha, katika aina hii ya ushairi tunazingatia pia aina ya vina na

122

mizani iliyotumika katika shairi husika pamoja na namna vina na mizani hiyo ilivyopangwa. Kwa

kutumia kigezo hiki tunapata aina zifuatazo za ushairi:

(i) Wajiwaji au Takhmisa

Hii ni bahari ambayo huwa na mashairi yenye mistari mitano katika kila ubeti. Kutokana na hilo,

mashairi yote yenye mistari mitano huitwa takhmisa. Kwa kawaida mashairi haya huwa na mizani kumi

na tano (15) kila mshororo ambapo si lazima yawe na vina vya kati lakini una vina vya mwishoni.

(ii) Wawe/ Vave

Kama tulivyodokeza hapo awali, matamshi tofauti baina ya wawe au vave ni ya kilahaja. Wawe ni

bahari ya ushairi inayohusisha tungo za kishairi ambazo huimbwa wakati wa kufanya kazi, hasa kilimo

(kufyeka, kulima, kukata magugu, kuchoma moto magugu na kadhalika). Tungo hizi zinaweza kuwa na

urari wa vina na mizani au zisiwe nao.

(iii)Kimai

Bahari ya kimai inahusu nyimbo zinazoimbwa katika shughuli mbalimbali za baharini. Hizi

hujumuisha nyimbo za mabaharia, wavuvi na wasafiri wa vyombo vya baharini. Nyimbo hizi hazina

idadi kamili ya vina na mizani na pia suala la urari wa vina na mizani si la lazima.

(iv)Ukara

Hii ni bahari inayohusu mashairi ambayo vina vya kati huwa vinafanana katika mishororo ya beti

zote za shairi husika, huku vina vya nje vikibadilika kutoka mshororo hadi mshororo au ubeti hadi

ubeti. Wakati mwingine mshororo wa mwisho wa kila ubeti huweza kuwa na vina vinavyohitilafiana au

hata kuwa na kituo bahari au kimalizio lakini tu iwe na kina cha kati ambacho ni bahari na kina cha

mwisho kinachobadilikabadilika.

(v) Ukuraguni

Hii ni aina ya mashairi ambapo kuna vina vya kati na vya mwisho vinavyofanana. Hata hivyo vina

hivyo vinabadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine

Ubeti wa 1: ___________________ni, ________________a

___________________ni, ________________a

___________________ni, ________________a

___________________ni, ________________a

Ubeti wa 2: ___________________sa, ________________ma

___________________sa, ________________ma

___________________sa,________________ma

___________________sa, ________________ma

Ubeti wa 3: ___________________po, _________________la

___________________po, _________________la

___________________po, _________________la

___________________po, _________________la

___________________po, _________________la

(vi)Mtiririko

Haya ni aina ya mashairi ambayo kwa kawaida vina vyake vya kati hufanana/hutiririka katika beti

zake zote na pia vina vya mwisho hufanana/hutiririka katika beti zake zote. Kuna baadhi ya maandiko

ambapo dhana ya mashairi ya mtiririko hutumika kumaanisha mashairi yasiyokuwa na urari wa vina na

mizani na ambayo hayana beti bali hutiririka tu mwanzo hadi mwisho. Hata hivyo dhana hiyo siyo

inayotumika hapa.

123

(vii) Masivina

Masivina ni aina ya mashairi ambayo hayana urari wa vina lakini yanaweza kuwa na urari wa

mizani. Neno “masivina” ni kifupi cha “mashairi yasiyokuwa na urari wa vina.” Hii haimaanishi

kwamba ni mashairi yasiyokuwa na urari wa mizani. Kuna baadhi ya wanazuoni huyachukulia

masivina kuwa ni mashairi yasiyokuwa na urari wa vina na mizani, bali dhana hii si sahihi. Masivina

huitwa pia mapingiti, yakitumia dhana kwamba kama ilivyo kwa vipingiti vya vitu mbalimbali kama

vile muwa huweza kufanana lakini si lazima vipingiti vyote vifanane. Vina na mizani hufananishwa na

vipingiti hivyo ambapo katika mashairi haya vina havifanani bali mizani hufanana.

(viii) Kisarambe

Kisarambe ni mashairi yanayokaribiana sana na masivina. Tofauti baina ya masivina na kisarambe

ni kwamba wakati ambapo masivina ni mashairi yasiyokuwa na urari wa vina lakini yanayoweza kuwa

na urari wa mizani, kisarambe ni mashairi ambayo hayana urari wa mizani bali yana urari wa vina.

(ix)Guni

Mashairi guni yanahusiana sana na masivina na kisarambe. Tofauti pekee ni kwamba masivina

hayana urari wa vina bali yanaweza kuwa na urari wa mizani, kisarambe hayana urari wa mizani bali

yana urari wa vina na mashairi guni yenyewe hayana urari wa vina wala mizani. Mashairi haya pamoja

na masivina ndiyo huitwa mashairi ya kisasa.

(x) Upeo

Upeo ni aina ya ushairi wenye idadi tofauti ya mizani katika mishororo ya ubeti mmoja. Hii ina

maana kwamba mshororo wa kwanza unaweza kuwa na mizani kumi na mbili, unaofuata ukawa na

mizani kumi na kadhalika.

(xi)Kikai

Ni aina ya mashairi ambayo huwa na mizani kumi na mbili katika kila mshororo ambapo mizani

nne huwa katika ukwapi na nane katika utao. Hata hivyo bahari hii yaweza kuwa pia na mizani sita au

nane kwa tatu au tano na kwa nane. Jambo la msingi hapa ni kwamba mizani katika upande mmoja wa

mshororo huwa michache sana kuliko katika sehemu nyingine.

4. Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Uradidi

Uradidi ni ile hali ya kujirudiarudia kwa jambo. Uainishaji wa ushairi kwa kutumia kigezo cha

uradidi, kwa hiyo, kinazingatia kurudiarudia kwa neno moja au kifungu cha maneno katika shairi kwa

lengo la kusisitiza wazo au kuweka mkazo katika maana. Kwa kutumia kigezo hiki tunapata aina

zifuatazo za mashairi.

(i) Kikwamba

Kikwamba ni mashairi ambayo neno moja hurudiwarudiwa katika kila mshororo au hata ubeti

mzima. Neno linalorudiwa laweza kuwa lile linaloanza katika kila mshororo au linaweza kujitokeza

katikati ya mshororo. Shairi lililopewa jina “Dini” lililopo katika sehemu ya pili ya andiko hili ni mfano

mzuri wa mashairi ya bahari hii ya kikwamba.

(iii)Pindu

Pindu ni aina ya ushairi ambapo neno au fungu la maneno lililo mwishoni mwa ubeti (linalomalizia

ubeti) linarudiwa kama kianzio cha ubeti unaofuata. Ni mashairi yenye uelekeo wa kitathlitha.

5. Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Madhumuni ya Utungaji (Lengo)

Katika bahari hii uainishaji hufanywa kwa kuzingatia madhumuni ya utungaji wa shairi husika. Kila

mshairi huwa na lengo au madhumuni mahsusi anapotunga shairi lake. Aidha, shairi husika lililotungwa

huwa linatimiza majukumu kadhaa, iwe ni kuelimisha, kuburudisha, kuzindua moyo na kadhalika.

Hivyo, kigezo hiki kinazingatia mambo hayo. Kwa kuzingatia kigezo hiki tunaweza kupata aina

zifuatazo za ushairi:

124

(i) Zivindo

Ni utungo wa kishairi ambapo mshairi hutunga ili kufafanua maana tofauti za neno moja kama vile

paa, kaa, ala, panda, shuka, na kadhalika. Kila mshororo huelezea matumizi au maana tofauti za neno

linalofafanuliwa. Kazi yake ni kufunza lugha kwa kutoa maana tofauti ya neno moja au yenye

matamshi yanayokaribiana.

(ii) Tumbuizo

Ni shairi linaloimbwa au kughanwa ili kutumbuiza na kuwaliwaliza watu. Lengo kuu la utungo huu

ni kutoa burudani.

(iii)Tiyani Fatiha

Ni bahari ya ushairi wa kidini wa kuomba toba. Ni utungo wenye mishororo tisa (9) kila ubeti

ambao una vina vya kati na mwisho. Mbali na uwezekano wa kuwa na urari wa vina vya kati na

mwisho tiyani fatiha huweza pia kakosa sifa hiyo katika baadhi ya mistari.

(iv)Inkishafi/Dura Mandhuma

Bahari hii imepata jina lake kutokana na Utenzi wa al-Inkishafi wa Sayyid Abdalla Bin Ali bin

Nasir (1720-1820) pia kutokana na utungo wa Sheikh Umar bin al-Ahdaly (1798-1869) uitwao Dura

Mandhuma. Ni tungo za kishairi za zamani zilizokuwa na mishororo yenye mizani kumi na moja (11).

Maudhui yake yalikuwa ya kidini, hasa dini ya Kiislamu, na yenye mafunzo ya maadili kama vile

kuusia, kuonya, kufunza mwenendo wa kidini na kuelekeza. Hii ina maana kuwa japo, kwa kiasi

kikubwa bahari hii ilihusu tungo za kidini lakini ilihusu pia tungo zenye maudhui ya kidunia.

(v) Taabali

Ni aina ya ushairi ambao hutungwa ili kuwaenzi marehemu. Utungo huu hukusudiwa kuwasifia

watu walioaga dunia kama njia ya kuwaenzi na kuihamasisha jamii kuwa na matendo mema kama wao

ili watakapokufa na wao wakumbukwe kwa mema.

6. Bahari za Ushairi kwa Kigezo cha Muundo

Kigezo cha muundo kinazingatia umbo la ushairi husika (ikiwa ushairi una umbo la majibizano au

la na kama una majibizano, majibizano hayo yapoje). Kwa kutumia kigezo hiki tunapata aina zifuatazo

za ushairi:

(i) Ngonjera

Haya ni mashairi ya majibizano yanayohusisha fanani wawili au zaidi. Fanani mmoja huimba au

kughani ubeti mmoja au hata mshororo mmoja na wakati mwingine hata kipande kimoja na kisha

fanani mwingine hujibu.

(ii) Sarakani

Sarakani ni aina ya ushairi ambao una muundo wa beti usiolingana, ubeti mmoja unaweza kuwa

na mishoro miwili, unaofuata mitatu na mwingine minne na kadhalika. Aidha, katika bahari hii pia

ubeti wa kwanza huweza kuwa una mishororo mitano, unaofuata minne na kadhalika. Tunaweza

kusema kwamba ushairi wa aina hii unachanganya bahari tofauti tofauti katika beti zake ambapo beti

moja inaweza kuwa utano, nyingine ukumi na kadhalika.

(iii) Mandhuma

Mandhuma ni aina ya shairi ambalo huwa na sehemu mbili, sehemu ya kwanza huwa ni swali na

sehemu ya pili ni jibu. Wakati mwingine sehemu ya kwanza huweza kuwa wazo na sehemu ya pili ni

msisitizo wa wazo husika au ufafanuzi wake. Mgawanyo huu unaweza kuwa baina ya beti moja na

nyingine au hata katika mshororo mmoja ambapo kunakuwa na ukwapi (unaotoa swali) na utao

(unaojibu swali hilo).

125

HITIMISHO KUHUSU BAHARI ZA USHAIRI

Tuhitimishe kwa kusema kwamba uainishaji wa mashairi kwa kuzingatia bahari ni telezi mno na

bado kuna mwingiliano mwingi. Swali la kujiuliza hapa ni je, bahari hizi zipo ngapi hasa na ni lazima

tuainishe mashairi katika bahari mbalimbali? Bila shaka jibu la swali la pili ni rahisi. Ni lazima

tuainishe ushairi katika bahari, kwa uainishaji wa ushairi hurahisisha usomaji wa ushairi na hata

ufafanuzi wake.

126

SURA YA SABA

UCHAMBUZI WA MASHAIRI

Uchambuzi wa mashairi ni uhakiki wa mashairi mbalimbali. Wanafasihi wengi wanabainisha

kwamba uchambuzi wa mashairi huhusisha vipengele vikuu viwili ambavyo ni maudhui na fani. Hata

hivyo kumekuwa na utata wa kipengele gani kinapaswa kuanzwa katika uhakiki wa mashairi na kazi za

wa fasihi kwa ujumla. Wapo wanaoona kwamba uhakiki wa kazi ya fasihi hupaswa kuanza kwa

kuchambua vipengele vya maudhui na pia wapo wanaoshadidia kuanza na vipengele vya kifani. Hata

hivyo katika andiko hili tutaendeleza mkabala unaopigiwa chapuo sana na Samwel katika maandiko

yake kwamba tunapaswa kuanza na uchambuzi wa maudhui na kisha fani. Hoja ya Samwel ambayo

tunakubaliana nayo ni kwamba maudhui ndiyo huanza katika kichwa cha mwanafasihi na kisha

hutafutia fani ya kuyawasilisha maudhui hayo (taz. Samwel, 2012a, Mabadiliko katika Majigambo:

Uchunguzi wa Mabadiliko ya Jadi na Bongo Fleva na Samwel, 2012b, Hadithi Fupi: Nadharia, Mbinu

na Mifano). Hivyo uchambuzi wetu katika sehemu hii utaelemea mkabala huo.

Jambo la msingi la kukumbuka ni kwamba japokuwa katika uhakiki wa kazi za fasihi ukiwemo

ushairi, maudhui na fani hutenganishwa, vipengele hivi ni kitu kimoja. Maudhui na fani huathiriana,

hutegemeana na kukamilishana na hivyo ni vitu ambavyo havipaswi kuchukuliwa kuwa ni tofauti. Kila

mara ni vema kuvihakiki vipengele vya maudhui na kuvihusisha na fani. Maudhui huweza kuathiri fani

na fani kuathiri maudhui. Kwa mfano, pindi mashairi yanapotumia lugha ngumu sana isiyoeleweka

kirahisi hufanya hata maudhui yake yasieleweke. Vivyo hivyo pale mashairi yanapoweka mkazo katika

maudhui na kusahau fani mashairi hayo huweza kuwa chapwa ama yasiyofurahisha kuyasoma na kwa

hivyo maudhui yake kutowafikia wahusika. Hivyo, maudhui na fani ni sawa na sura mbili za sarafu

moja, sura moja inapoharibika sarafu hiyo inapoteza uhalali wake.

1. MAUDHUI

Wanafasihi wengi huyafafanua maudhui kwamba ni umbo la ndani la kazi ya fasihi. Maudhui ni

mawazo yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Ni jumla ya mambo yote yanayobebwa na kazi husika ya

kifasihi. Kwa minajili ya andiko hili, maudhui tuchukulie kuwa ni jumla ya mawazo au mambo

yanayobebwa katika ushairi wa Kiswahili. Maudhui hujumuisha dhamira, ujumbe, migogoro,

masuluhisho, falsafa, fundisho na msimamo.

I. Dhamira

Dhamira ni mada, lengo, kusudi, wazo kuu linalozungumzwa na shairi/kazi ya sanaa. Mashairi

huweza kuwa na dhamira za kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni. Mifano ya baadhi ya

dhamira zinazoonekana katika mashairi ni pamoja na uongozi bora, mapenzi, dini, ndoa, elimu, kazi na

ukombozi. Dhamira hizi huweza kuelezwa kwamba mwandishi anakusudia kuielimisha jamii juu ya

dhana na sifa za kiongozi bora, kuionya jamii juu ya madhara ya mapenzi shuleni, kuielekeza jamii juu

ya umuhimu wa dini katika jamii, kuiasa jamii kuwa na uaminifu katika ndoa na kadhalika.

II. Ujumbe

Ujumbe ni yale mambo ambayo mshairi angependa hadhira ijifunze ili kuweza kufanikisha

misimamo iliyojengwa na msanii huyo. Kwa mfano, kama shairi linahusu mapenzi ujumbe unaweza

kuwa “mapenzi yanaua, mapenzi yanapofanywa shuleni huweza kuathiri ujifunzaji na ufundishaji,

mapenzi huweza kuwa faraja katika kipindi cha matatizo” na kadhalika.

III. Falsafa

Falsafa ni imani ya mshairi. Kipengele hiki huhusisha vipengele vya ujumbe, maadili na

msimamo wa mshairi ambao hutokana na dhamira za kazi hiyo. Mara nyingi falsafa hujitokeza katika

namna mshairi anavyotoa masuluhisho ya migogoro inayojitokeza au mahitimisho anayoyatoa juu ya

masuala mbalimbali. Falsafa inaweza kuwa “pindi wema na ubaya vinapopambana wema hushinda,

malipo ya ubaya ni aibu, tamaa mbele mauti nyuma, asiyesikia la mkuu huvunjika guu, maisha hayana

maana yoyote (kufa leo au kesho vyote ni sawa tu)” na kadhalika.

127

IV. Fundisho

Fundisho huitwa pia mafunzo. Fundisho, kwa hiyo, ni yale mambo ambayo tunajifunza kupitia

shairi husika. Fundisho huhusiana na falsafa na mtazamo wa jamii kwa ujumla jinsi inavyoyaona

mambo. Mara nyingi fundisho huwa ni juu ya mambo mema, hatutarajii mhakiki aseme mshairi

anaifundisha jamii juu ya umuhimu wa wizi katika kipindi cha matatizo. Wizi ni kitu kibaya na katika

jamii hakuna namna ya kuhalalisha wizi. Hivyo, fundisho huweza kuwa, kwa mfano, mwandishi

anaifunza jamii kwamba ni muhimu kuvumilia matatizo kwani mvumilivu hula mbivu.

V. Msimamo

Msimamo wa mshairi huitwa pia mtazamo wa mshairi. Msimamo ni jinsi mshairi

anavyoyachukulia mambo katika ulimwengu au jamii husika anayoisawiri. Msimamo si lazima kila

wakati ukubalike na wanajamii wote japokuwa mafundisho yanayotolewa katika ushairi yanaweza

kukubaliwa na jamii yote. Kwa mfano, msimamo wa Kezilahabi katika kazi zake nyingi ni kwamba

maisha hayana maana yoyote. Msimamo huu unatokana na falsafa ya kidhanaishi inayoaminiwa na

Kezilahabi. Misimamo mingine huweza kuwa “kiongozi mbaya anapaswa kuondolewa kwa nguvu

madarakani na kuuawa, wanyonge wanaokandamizwa watumie vita kujikomboa maana njia ya amani

huchukua muda mrefu, ili kujilinda na UKIMWI wanajamii hawana budi kujiingiza katika dini na

misimamo mingineyo.”

VI. Mgogoro

Mgogoro ni hali ya kutoelewana baina ya watu wawili au makundi mawili ya watu. Kwa mfano,

kunaweza kuwa na mgogoro baina ya wenyenacho na wasionacho ambapo wasionacho wanataka njia

kuu za uchumi zimilikiwe na wote ilhali wenyenacho hawataki hali hiyo. Kunaweza kuwa na mgogoro

baina ya binti na wazazi wake ambapo binti anataka kuolewa na kijana maskini lakini wazazi wake

hawataki na pia kunaweza kuwa na mgogoro baina ya wachungaji na waumini ambapo wachungaji

wanataka waumini watoe sadaka kubwa zaidi ili wao wazitumie katika anasa lakini waumini

wanaamini kwamba kutoa sadaka ni kumpa chochote Mungu ambaye ni tajiri hivyo hata kidogo

chamtosha. Upo pia uwezekano wa mtu mmoja kuwa na mgogoro baina yake na nafsi yake. Mgogoro

huu huitwa mgogoro wa kinafsia na huwa unatokana na mhusika kuwa na mambo mawili

yanayomsonga ambapo kila jambo linamvuta kuliamua. Mhusika huyo, kwa hiyo hujikuta akiwa

kwenye mgogoro ikiwa aamue hili au lile lingine. Kwa mfano, mhusika binti huweza kuwa na mgogoro

nafsia ikiwa ashikilie nia yake ya kuolewa na kijana maskini hata kama wazazi wake wamemkataa ama

akubaliane na wazazi wake na aolewe na kijana tajiri aliyechaguliwa na wazazi wake.

VII. Masuluhisho

Masuluhisho kwa kawaida huenda sambamba na migogoro. Panapotokea mgogoro, msanii

huweza kupendekeza usuluhishi wa mgogoro huo. Kwa mfano, katika mgogoro wa wazazi na binti

mshairi huweza kutoa suluhisho kwamba binti aliolewa na kijana maskini na waliishi kwa amani na

furaha na mwishowe kijana (mume) alikuja kuwa tajiri kuliko tajiri aliyechaguliwa na wazazi wa binti

ili aolewe naye. Hivyo, suluhisho hapa ni kwamba wazazi wawaache watoto wao waolewe na mtu

yeyote wanayempenda maana la msingi katika ndoa ni upendo na amani bali mali hutafutwa. Hata

hivyo mara nyingine washairi huamua kutotoa masuluhisho ya migogoro wanayoiibua na kumwachia

msomaji nafasi ya kuamua lipi linafaa kuwa suluhisho bora.

2. FANI

Fani huelezwa kwamba ni umbo la nje la kazi ya fasihi. Hii ina maana kwamba fani ni mbinu

mbalimbali azitumiazo mshairi katika kuwasilisha fikra na mawazo (maudhui) anayoyakusudia kwa

hadhira lengwa. Vipengele vya fani vilivyozoeleka ni pamoja na muundo, mtindo, matumizi ya lugha,

mandhari na wahusika.

I. Muundo

Muundo hudhihirika kwenye umbo la shairi. Umbo ni sura ya nje ya shairi au kazi ya sanaa, ni jinsi

shairi husika linavyoonekana. Muundo (umbo) la shairi hutegemea na mkabala wa mshairi, ikiwa ni

mwanamapokeo au mwanausasa. Lakini kwa ujumla muundo wa shairi hujumuisha yafuatayo:

128

a) Beti: ni mkusanyiko wa mistari/mishororo na kwa kawaida huwa na wazo moja kamilifu.

Katika uchambuzi, tunaangalia ikiwa shairi husika lina beti au halina na beti hizo zimeundwaje?

b) Mshororo: ni mistari ambayo inapowekwa pamoja huunda beti. Katika kipengele hiki

tunaangalia ikiwa beti za shairi linalochambuliwa zimegawanyika katika mishororo na pia

mishororo hiyo ipoje? Je mishororo imegawanyika katika vipande?

c) Vipande: ni sehemu ya mshororo wa shairi. Mshororo huweza kuwa na sehemu kadhaa,

sehemu hizo ndizo huitwa vipande. Mshororo huweza kugawanyika katika sehemu mbili, tatu

au hata nne na kadhalika. Kipande kikigawanyika katika sehemu mbili sehemu ya kwanza

huitwa ukwapi na ya pili utao; kikigawanyika katika sehemu tatu, sehemu ya kwanza huitwa

ukwapi, ya pili utao na ya tatu mwandamizi; na kikigawanyika katika sehemu nne sehemu ya

kwanza huitwa ukwapi, ya pili utao, ya tatu mwandamizi na ya nne ukingo.

d) Mizani: ni jumla ya salabi katika mshororo mmoja. Kila mshororo huundwa na maneno

yaliyoundwa na silabi. Kila silabi moja ni mizani moja, hivyo, jumla ya silabi katika mshororo

ndizo huunda mizani ya mshororo husika.

e) Vina: ni silabi zinazofanana katika mshororo wa shairi au beti. Kuna aina mbalimbali za vina

ambazo ni pamoja na kina cha kati, kile kinachotokea katika kipande cha mshororo ambacho si

cha mwisho na kina cha mwisho ambacho hujitokeza katika kipande cha mwisho cha mshororo.

f) Kibwagizo: ni mshororo wa mwisho wa ubeti unaorudiwarudiwa, huitwa pia kiitikio.

Kipengele hiki kiliigwa kutoka tungo simulizi. Hasa zenye mwimbaji mkuu mmoja. Kazi ya

kibwagizo katika shairi ni kumalizia ubeti na kushadidia dhamira au wazo la shairi. Upo

uwezekano pia wa kuwa na vibwagizo ambavyo si viitikio. Hivi huwa ni ghani

zinazochomekwa mwanzoni mwa shairi ili kumtambulisha msanii, maudhui yake au shairi

lenyewe. Aina hii ya vibwagizo ni maarufu sana katika ushairi wa Bongo Fleva.

g) Mkarara: ni mshororo wa mwisho ambao unajirudiarudia katika kila ubeti. Neno mkarara

linatokana na dhana ya kukariri, yaani kurudiarudia kwa jambo fulani.

h) Kituo/kimalizio: ni mstari wa mwisho katika ubeti. Iwapo mstari huo unabadilikabadilika

kutoka ubeti mmoja hadi mwingine basi mstari huo ni kimalizio lakini kama mstari huo

haubadiliki basi huitwa kituo (kituo bahari).

II. Mtindo

Mtindo ni upangaji wa fani na maudhui kwa namna ambayo inampambanua mshairi mmoja na

mwingine. Mtindo huhusisha kuchunguza ikiwa shairi ni la tathlitha, tarbia, telemania au mtindo

mwingineo. Mtindo pia huhusisha maneno aliyoyateua mtunzi, je ni magumu au ni rahisi? Ni ya

kilahaja au yanatumia lahaja sanifu? Yanatumia lugha ya wazee, vijana au watoto? Ya wanaume au ya

wanawake? Je mashairi hayo ni ya kimajibizano au ni monolojia? Je, mshairi ametumia lugha ya

Kiswahili pekee au amechanganya lugha? Anatumia lugha fasaha na sanifu au ya mitaani? Mambo

mengine ya mtindo ni pamoja na matumizi ya lugha ya picha, ishara na taswira. Kwa hakika mtindo

hujumuisha pia mambo mengi ikiwa ni pamoja na matumizi ya lugha, lakini ili kurahisisha usomaji na

uchambuzi wa mashairi, matumizi ya lugha hupewa kipengele chake kinachojitegemea.

III. Matumizi ya Lugha

Katika kipengele hiki kinachohusiana sana na mtindo tunaangalia vipengele vile ambavyo

hatujavichambua katika mtindo. Hapa tunaangalia mambo kama vile matumizi ya tamathali za semi,

matumizi ya methali, misemo, misimu, mafumbo na vipengele vingine vya aina hiyo.

129

a) Matumizi ya Tamathali za Semi

Samwel (2012b) anabainisha kwamba dhana ya tamathali za semi imekuwa ikichanganywa sana

na wahakiki pamoja na walimu wengine ambao wamezijumuisha methali, misemo na misimu katika

tamathali za semi (Kanuri na Wenzake, ht.). Uchanganyaji huu unaonekana pia katika Msokile

(1993:60). Samwel anaendelea kubainisha kwamba tamathali za semi, methali, misemo na misimu ni

vitu tofauti. Tamathali za semi ni maneno au miundo inayotumika katika lugha ili kutia msisitizo na

mkazo katika maana, kwa kawaida huwa na idadi kamili na zinajulikana. Tamathali za semi

zinazojulikana kutumika katika ushairi ni pamoja na tashbiha/tashbihi, sitiari, tashihisi, takriri, tasifida,

na chuku. Hata hivyo bado kuna mjadala juu ya tamathali hizi kama itakavyobainishwa katika mjadala

utakaofuata.

(i) Tashbiha: huitwa pia tashibihi au mshabaha. Hii ni aina ya tamathali ambayo hufananisha vitu

viwili tofauti kana kwamba ni kitu kimoja. Tamathali hii hutumia vifananisho kama vile: kama,

kama vile, mfano wa, mithili ya na nyingine za aina hiyo. Mifano ifuatayo itatusaidia kuielewa

dhana hii ya tashbiha:

- Vero ni mrembo kama malaika

- Gilo ni mrefu kama mti wa mwanzi

- Nilimuona kijana mwenye sura mithili ya mwanamke

- Maziwa yana rangi mfano wa chokaa

(ii) Sitiari: huitwa pia istiara, istiari au jazanda. Hii ni tamathali ya usemi (maneno, kirai au

miundo) inayotumika kuumba picha fulani akilini inayotoa athari fulani kwa, au inayoamsha

mwitikio fulani kutoka kwa hadhira. Cuddon (1998:507) anasisitiza kwamba sitiari ni tamathali

muhimu sana katika ushairi. Mifano ya sitiari inaweza kuwa kama ifuatavyo:

- Vero kwa urembo wake ni malaika

- Gilo ana urefu wa mti wa mwanzi

- Asha ana weusi wa mkaa

(iii)Tashihisi: tamathali hii huitwa pia uhaishaji na pia uhuishaji. Kuhaisha ni kuvipa uhai vitu

visivyokuwa na uhai na kuhuisha ni kuvipa hadhi vitu vilivyokuwa duni. Hivyo tunaweza

kusema kwamba tashihisi ni aina ya tamathali ambapo viumbe visivyokuwa na uhai hupewa

uhai (Kahigi na Mulokozi, 1979:33-34; Alembi, 2000:36). Vilevile tashihisi huhusisha viumbe

visivyo binadamu kupewa uwezo wa kiutendaji kama binadamu. Dhana hii ya pili ndiyo

inayobebwa na neno lenyewe “tashihisi” ambalo linamaanisha nafsi. Hivyo, ni mbinu ya kuvipa

nafsi ya binadamu vitu ambavyo havina nafsi hiyo. Cuddon (1998:661) anabainisha kwamba

matumizi ya tamathali hii zaidi ya kuweka mkazo katika maana, inaupa utungo sifa ya kuwa

kazi ya fasihi. Ifuatayo ni mifano ya tashihisi:

- Kiza kinene kilitawala usiku ule kabla mayowe hajaanza kutembea

- Taratibu usingizi ulianza kunichukua huku mawazo yakinibembeleza

- Vumbi lilikimbia njia nzima

(iv)Takriri: huitwa pia inadi au uradidi. Dhana hii inakaribiana sana na dhana ya usambamba.

Kahigi na Mulokozi (1979:40) wanaieleza takriri kuwa ni uradidi, yaani urudiaji wa sauti, neno,

kirai, kishazi na hata sentensi katika kazi ya kifasihi. Takriri hutumika kuweka mkazo katika

maana na pia huleta ushikamani na muunganiko katika ushairi. Katika ushairi kuna aina

mbalimbali za takriri kama vile: takriri irabu, takriri konsonanti, takriri silabi (huitwa pia takriri

mizani), takriri neno, takriri mstari/mshororo, takriri ubeti, takriri vina na takriri kituo na takriri

ridhimu. Takriri pia huweza kuwa katika ngazi ya maudhui ambapo kunakuwa na takriri wazo.

(v) Tasifida: ni aina ya tamathali ambayo inayafanya maneno ambayo hayapaswi kutamkwa

hadharani, kuweza kutamkika kwa mbinu nyingine mbadala (Cuddon, 1998:292; Senkoro,

2011:18).

130

(vi)Udokezi/mdokezo: Cuddon (1998:27) na Mulokozi (2002:187) wanafasili mdokezo kuwa ni

tamathali ambayo inatumika katika kazi mahsusi ya kifasihi ili kurejelea kazi nyingine ya fasihi

au ya sanaa, au mtu au hata tukio.

(vii) Chuku: huitwa pia chukwu au udamisi. Chuku ni mbinu ya kisanii ambapo kitu, mtu au

jambo hukuzwa zaidi ya uwezo wake (Kahigi na Mulokozi, 1979:36; Alembi, 2000:44). Katika

mbinu hii kitu, jambo au mtu anapewa uwezo ambao katika hali ya kawaida hawezi kuwa nao.

Mara nyingi chuku huelezwa kuwa ni kutia chumvi kwa jambo ambako kunaweza kuwa chanya

au hasi.

(viii) Balagha: ni ile hali ya mshairi kuuliza swali ambalo linakuwa la kikejeli kwa kuwa mshairi

anauliza jambo ambalo jibu lake analifahamu fika.

(ix) Ucheshi: Senkoro (2011:26) anafasili ucheshi kuwa ni mbinu ya kifani ambayo wasanii

huitumia katika kazi zao za fasihi kuzichekesha hadhira zao, au walau kuzifanya hadhira hizo

zitabasamu. Lengo la kutumia mbinu hii ili kuwafurahisha wasomaji, wasikilizaji au watazamaji

wa kazi zao, kuiepushia uchovu hadhira ya kazi zao na kujenga kejeli katika kazi zao.

b) Matumizi ya Methali

Methali ni semi fupifupi zinazobeba uzoefu wa jamii kuhusu maisha na hivyo kuadilisha na

kuihekimisha jamii. Kazi kubwa ya methali ni kuitajirisha fani na maudhui ya kazi ya fasihi na

hutumika kama daraja la kupitishia maadili kwa jamii husika. Hivyo, tunaweza kusema kwamba

methali ni tungo za kimapokeo ambazo hubeba falsafa ya maisha katika jamii husika.

c) Matumizi ya Nahau

Nahau ni fungu la maneno ambayo maana yake haipatikani kwa kufasili neno moja moja. Hizi

ni tungo za kimapokeo ambazo maana yake huwa ni tofauti na maana ya neno kwa neno. Samwel

(2012b) anatoa mifano ya nahau kuwa ni kama vile:

- Ana mkono wa birika (mchoyo)

- Ana roho ya korosho (mchoyo)

- Ana mkono mrefu (mwizi)

- Amevunja ungo (amebalehe hasa msichana)

d) Matumizi ya Misimu

Misimu ni maneno yanayoibuka katika kipindi fulani cha kihistoria na huweza kupotea. Wakati

mwingine misimu huweza kusanifiwa na kuwa msamiati. Mifano ya misimu ni kama vile njagu (polisi),

mshkaji (rafiki), changu (kahaba), zali (bahati) na kadhalika.

e) Vipengele Vingine katika Matumizi ya Lugha

Zaidi ya vipengele tulivyovieleza, matumizi ya lugha katika ushairi hujumuisha pia vipengele kama vile

inksari, mazda, tabdili, ritifaa, lugha ya mkato .Ufafanuzi wake ni kama ifuatavyo:

(i) Inksari: kufupisha maneno katka shairi ili kupata ulingano wa vina na hata mizani. Kwa

mfano, aliyekuja ( inafupishwa kuwa alokuja), mwana wako (inafupishwa kuwa

mwanao), mama yako (inafupishwa kuwa mamayo) na kadhalika.

(ii) Mazda: ni kinyume cha inksari. Ni hali ya kurefusha neno kwa nia ya kupata mizani

inayohitajika. Mifano mizuri ya mazda ni kama vile: nenda (inarefushwa kuwa

enenda), ajapo (inarefushwa kuwa anapokuja), nipo (inarefushwa kuwa nimekuwepo)

na kadhalika.

(iii) Tabdili: kubadilisha mpangilio wa herufi au vitamkwa katika neno ili kupata urari

(ufanano) wa vina vinavyotakikana. Mfano mzuri unaweza kuwa kama unataka

131

kutumia kina “hi” bahari (itabadilishwa na kuwa barahi), au kama unataka kutumia

kina “si” basi sukari (itabadilishwa na kuwa karusi).

(iv) Ritifaa: mbinu hii hutumika kwa kuelekeza ujumbe wake kwa kitu kisicho na uhai kama

vile sanamu, maiti. Hutumika kutoa hisi za ndani za huzuni/majonzi makali.

(v) Tanakali Sauti: ni mbinu ambapo mshairi huiga sauti ya kitu halisi kwa kutumia

maneno. Mfano mzuri wa maneno ya ainaa hii ni kama vile churuzika, tiririka,

tetemeka, bandubandu na kadhalika.

(vi) Lugha ya mkato: shairi huzungumza mambo kwa ufupi kwa kutumia taswira na

tamathali

IV. Mandhari

Ni mazingira ya kijamii na kihistoria yaliyozua utungo. Mazingira ambayo kazi ya fasihi imeandikwa.

Mandhari ni dhana inayoonekana rahisi lakini ni pana na yenye mijadala mingi. Kumekuwa na utata juu

ya dhana yenyewe ya mandhari, aina za mandhari zilizopo na hata dhima ya mandhari katika kazi ya

fasihi. Kuna wanafasihi wanaofasili mandhari kwa kuzingatia eneo (mahali) kazi ya fasihi inapotendwa

lakini wapo pia wanaofasili mandhari kwa kuangalia wakati, wengine wanazingatia muktadha na

wengine wanachanganya vyote kwa pamoja.

Wanaofasili mandhari kwa kuzingatia eneo kazi ya fasihi inapotendwa wanajumuisha Msokile (1992),

Njogu na Chimerah (1999), Madumulla (2009) na Samwel (2012b). Kwa upande wa wanaofasili

mandhari kwa kuzingatia wakati na muktadha ni pamoja na Cuddon (1998) na Wamitila (2008). Nao

Sunkuli na Miruka (1990) wanafasili mandhari kwa kuzingatia muktadha. Katika andiko hili, tunaona

kuwa mtazamo bora wa kufasili mandhari ni kwa kuunganisha mitazamo yote. Hivyo, mandhari ni

wakati, mahali na muktadha ambamo kazi ya fasihi inatendwa. Hivyo tuseme ili kufasili mandhari

tunapaswa kujibu maswali yafuatayo: kazi ya fasihi inatendeka wapi? Lini? Inatendwa na nani? Na

inatendwa vipi?

Kuhusu aina za mandhari za kazi za fasihi tunaweza kusema kwamba ni eneo lingine lenye utata

mwingi. Wapo wanafasihi wanaoona kuwa aina za mandhari ni tatu, mandhari ya kijiografia, kijamii na

kihistoria (Sunkuli na Miruka, 1990); wapo pia wanaoona kuwa mandhari ya kifasihi ni ya aina mbili,

halisi na ya kibunifu (Wamitila, 2008; Madumulla, 2009 na Samwel, 2012b). Katika andiko hili

tunaonelea kuwa kuna aina kuu mbili za mandhari, mandhari halisi na ya kibunifu. Mandhari halisi

inajumuisha maeneo ya kweli yanayojulikana katika jamii husika lakini mandhari ya kibunifu

huhusisha maeneo ya kufikirika ambayo hayapo katika ulimwengu halisi. Mandhari pia huweza

kuhusisha wakati halisi uliopo au mwandishi anaweza kurudisha wakati nyuma au kwenda mbele ya

muda. Mwandishi, kwa mfano, anaweza kutunga shairi akielezea hali ilivyo mwaka 2100 kana kwamba

mwaka huo umeshafika.

V. Wahusika

Wahusika ni watu, wanyama au viumbe ambao hutumika katika kazi ya fasihi. Mashairi mengi

hayana wahusika ila mashairi ya masimulizi huwa nao. Mfano mzuri wa hili ni tenzi/tendi mbalimbali

kama inavyobainika katika Utenzi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mrima, Utenzi wa Adamu na

Hawaa ambamo tunaona kuna wahusika. Kwa ujumla, tenzi nyingi hutumia wahusika. Katika uhakiki

wa ushairi tunajiuliza wahusika hao wana tabia/sifa gani? Je, wahusika hao wanaingiliana vipi?

Kutokana na meneno/matendo yao tumepata taswira gani? Je kuna wahusika wengine wa kiishara kama

vile “ua” kumaanisha “mpenzi” na kadhalika? Na je, ipi nafasi ya wahusika hao katika kuibua

maudhui?

132

SURA YA NANE

UFUNDISHAJI WA USHAIRI

Ushairi wa Kiswahili ni moja ya mada za lazima zinazopaswa kufundishwa katika ngazi

mbalimbali za elimu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Katika nchi za Tanzania na Kenya, ushairi wa

Kiswahili unafundishwa katika shule za msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na vyuo vikuu. Katika nchi

nyinginezo za Afrika Mashariki pia Kiswahili kinafundishwa katika ngazi mbalimbali. Vilevile, ushairi

wa Kiswahili unafundishwa katika vyuo mbalimbali ulimwenguni ambavyo vinafundisha lugha ya

Kiswahili na fasihi yake. Kutokana na kupanuka kwa ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili ni muhimu

kupitia namna ushairi wa Kiswahili unavyoweza kufundishwa kwa ufanisi. Hata hivyo, kwa kuwa si

rahisi kupitia ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili katika ngazi zote za elimu katika nchi zote, tutapitia

ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili kwa ujumla bila kuelemea ngazi yoyote mahsusi ingawa tutatumia

mifano ya ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu

katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki.

USHAIRI KAMA MBINU YA KUFUNDISHIA MASOMO MBALIMBALI

Ushairi wa Kiswahili, zaidi ya kuwa somo, ni moja ya mbinu muhimu ambayo inaweza

kutumika kufundishia somo la Kiswahili na masomo mengineyo. Kama mbinu ya kufundishia, ushairi

hujibainisha katika nyimbo zinazotumika kufundishia. Hivyo, mbinu ya nyimbo inahusiana moja kwa

moja na ushairi wa Kiswahili kwani, kama tulivyoeleza hapo awali, nyimbo ni ushairi simulizi wa

Kiswahili. Kwa hiyo, mbinu ya kufundisha kwa kutumia ushairi huitwa pia mbinu ya nyimbo. Katika

mbinu hii, nyimbo hutumiwa kufundisha masomo mbalimbali. Masomo hayo huweza kuwa ya sanaa au

hata ya sayansi. Kwa mfano, wanafunzi wengi wa sayansi nchini Tanzania wanapoanza kujifunza

elementi za kikemia katika somo la kemia hutumia wimbo. Katika shule nyingi nchini Tanzania,

mwanafunzi anapotakiwa kufundishwa elementi hizo, hufundishwa kwa kutumia wimbo maarufu

uitwao “Halo Helena,” ambao kila neno la wimbo husika huwakilisha elementi fulani ya kemia. Wimbo

huo huimbwa kama ifuatavyo:

Halo Helena Lile Beberu Bora Chinja na Ondoa Figo Nene Na yule Mzungu Aliye Simama Pale Serengeti

Club Aende Kwao Canada.

Elementi zinazowakilishwa na kila neno la wimbo huu ni kama ifuatavyo:

Halo (Hydrogen), Helena (Helium), Lile (Lithium), Beberu (Belium), Bora (Boron), Chinja (Carbon), Na

(Nitrojen), Ondoa (Oxygen), Figo (Florin), Nene (Neon), Na (Sodium), Mzungu (Magnesium),

Aliyesimama (Alminium), Simama (Silicon), Pale (Phosphorus), Serengeti (Sulphur), Club (Chloride),

Aende (Algon), Kwao (Potasium), Canada (Calcium)

Mbali na kutumika kufundishia kemia, nyimbo pia hutumika kufundishia kufundishia masomo

ya lugha, ikiwa ni pamoja na Kiswahili na Kiingereza. Kwa mfano, katika shule mbalimbali za

chekechea na shule za msingi katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki, kuna ule wimbo wa “Mabata

Wadogo Wadogo” uimbwao kama ifuatavyo:

Mabata wadogowadogo wanaogelea, wanaogelea

Katika shamba zuri la bustani

Wanapenda kuli kwa kwa kwa kwa kwa kwa, kwa kwa kwa kwa kwa kwa

Katika shamba zuri la bustani

Wimbo huu unawafundisha wanafunzi kutamka konsonanti ambatani kwa ambazo kwa umri wao huwa

ni ngumu sana kuzitamka. Hivyo, hapa wimbo unatumika kama mbinu ya kufundishia muundo KKI

(Konsonanti, Konsonanti, Irabu) wa silabi za Kiswahili. Kwa hiyo, hapa tunaona jinsi ushairi wa

Kiswahili unavyoweza kutumika kama mbinu ya kufundishia masomo mbalimbali. Mbinu hii

inasemwa kuwa, zaidi ya faida nyinginezo, husaidia kuwafanya wanafunzi kuchangamka darasani na

hivyo kuwafanywa wasichoke wakati wa zoezi la kufundisha na kujifunza. Hii ni kutokana na dhima

mojawapo ya ushairi wa Kiswahili ya kuburudisha. Kwa hiyo, somo hueleweka vizuri mbinu hii

inapotumika. Pia, mbinu hii huwasaidia wanafunzi kukariri mambo mbalimbali ambayo wasingeweza

kuyakariri kirahisi kwa namna nyingine.

133

USHAIRI WA KISWAHILI KAMA SOMO

SILABASI NA USHAIRI WA KISWAHILI

Ufundishaji wowote ule huanzia kwenye silabasi na kuongozwa na silabasi hiyo. Tunatumia

neno “silabasi” badala ya neno “muhtasari” ambalo hutumiwa na wengine kwa sababu kuu mbili:

kwanza, neno muhtasari tayari linatumika katika lugha ya Kiswahili kumaanisha ufupisho wa maelezo

fulani. Kanuni ya lugha inasisitiza kuepa matumizi ya maneno ambayo yameshatumika kumaanisha

dhana nyingine. Aidha, dhana ya muhtasari kutumika kumaanisha silabasi inachanganya kwani

inawafanya walimu na wanafunzi kuichukulia silabasi kama ufupisho wa zoezi la ufundishaji. Dhana

hii si sahihi hata kidogo kwani silabasi si ufupisho wa zoezi la ufundishaji. Pili, neno silabasi

linatumika ili kutunza uasili wa dhana yenyewe. Neno silabasi linalotumiwa hapa linatafsiri neno la

Kiingereza syllabus linalotumika kumaanisha mwongozo wa ufundishaji (TUKI, 2001:295 husisha na

TUKI, 2004:896). Hivyo, kulitohoa neno hilo kutalifanya neno silabasi linalozaliwa kuweza kuhifadhi

maana ya msingi ya dhana hiyo kama ilivyorejelewa na walioileta dhana hii kwetu. Wataalamu

wanakubaliana kuwa dhana ya silabasi, kama lilivyo zoezi zima la utoaji wa elimu rasmi (formal

education), ililetwa na wakoloni. Kabla ya ukoloni, sehemu kubwa ya Afrika haikuwa na mfumo rasmi

wa elimu bali mfumo usio rasmi uliojibainisha katika jando na unyago kwa kutaja baadhi tu (Coupland,

1938; Mair, 1964; Van Pelt, 1971; Ayisi, 1972; Rodney, 1975).

Hivyo, silabasi tunaweza kuifasili kuwa ni mwongozo mkuu unaomwelekeza mwalimu namna

ya kufundisha somo husika. Silabasi hii, kwa kawaida, hutokana na malengo na sera za elimu katika

nchi husika. Kila nchi ina malengo yake ya kutoa elimu katika ngazi husika, yaani kila nchi ina

malengo yake ya kutoa elimu ya chekechea, elimu ya msingi, elimu ya sekondari, elimu ya vyuo vya

kati na hata malengo ya elimu ya juu. Wanafunzi katika kila ngazi ya elimu wana mahitaji na matarajio

yao na ya jamii pia. Hivyo, katika kila ngazi kunakuwa na malengo mahsusi ambayo huamua masomo

ya kufundishwa, mada za kufundishwa na mbinu za ufundishaji kulingana na mahitaji na matamanio ya

wanafunzi na jamii. Silabasi hueleza yote hayo ili kuwawezesha walimu kufanya kazi yao ya

kufundisha kwa namna bora. Aidha, zaidi ya hayo, silabasi pia huelezea vitabu vya kiada, ziada na vya

rejea vya kutumika katika kila mada pamoja na zana za kufundishia. Silabasi hubainisha pia namna ya

kumpima mwanafunzi katika kila mada inayofundishwa.

Tangu nchi za Afrika Mashariki, ambazo ndizo hutumia na kufundisha zaidi Kiswahili, zipate

uhuru kumekuwa na silabasi mbalimbali. Wakati wa uhuru nchi hizo zilirithi silabasi za kikoloni

zilizokuwa zinatumika kufundishia shule za kikoloni. Ingawa silabasi hizo zilikusudiwa kutoa elimu

itakayowanufaisha wakoloni na kuendeleza utawala wao, lugha ya Kiswahili pamoja na ushairi wake

pia vilifundishwa (Mulokozi, 1996). Tulieleza katika sura zilizotangulia kuwa wakoloni walikuwa na

nafasi kubwa sana katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili na ushairi wake. Ni kupitia shule hizi za

kikoloni ambapo washairi wengi maarufu wa mwanzo waliibuka. Vilevile, wakoloni waliwafundisha

watu wa Afrika Mashariki ushairi wa nchi nyinginezo ulimwenguni na hivyo kuanza kuchochea

mabadiliko katika ushairi wa Kiswahili. Mabadiliko ambayo hatimaye yaliishia kuibua ushairi wa

kisasa wa Kiswahili, ushairi ambao hauamini kuwa urari wa vina na mizani ndiyo uti wa mgongo wa

mashairi ya Kiswahili. Ushairi ambao unasisitiza maudhui kuliko fani.

Baada ya uhuru, silabasi hizo za kikoloni zilibadilishwa. Tangu wakati huo silabasi zimeendelea

kubadilishwabadilishwa kulingana na mabadiliko ya sera ya elimu pamoja na malengo ya elimu katika

nchi mbalimbali za Afrika Mashariki. Nchini Tanzania, kwa mfano, kumekuwa na mabadiliko katika

sera ya elimu ambapo tangu kupatikana uhuru, sera ya elimu imekuwa ikibadilikabadilika. Sera ya

elimu inayotumika sasa ni ya mwaka 1995 ambayo, hata hivyo, imeonekana kuwa haiendani na

mabadiliko mbalimbali yaliyotokea katika jamii na hivyo kumekuwa na jitihada, ambazo labda zitazaa

matunda karibuni, za kuibadilisha sera hiyo. Kutokana na mabadiliko hayo ya sera ya elimu, hata

silabasi imekuwa ikibadilikabadilika.

Mbali na kubadilika kwa sera ya elimu, sababu nyingine inayoweza kusababisha silabasi

kubadilika ni mabadiliko ya kisiasa. Katika mabadiliko haya, tunazungumzia kubadilika kwa utawala

wa kisiasa katika nchi husika. Utawala unapobadilika, unaweza kuja utawala mpya wenye itikadi

tofauti na ile ya watawala waliotangulia na hivyo kuona kuna haja ya kubadilisha silabasi ili kuisukuma

mbele ajenda ya itikadi wanayoipigia chapuo.

134

Pia, silabasi huweza kubadilika kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Nchi husika

huweza kupiga hatua kubwa kiuchumi kiasi ambacho silabasi iliyopo kuonekana haiwezi kuendana na

maendeleo yaliyofikiwa na nchi husika. Hivyo, kuonekana kuna haja ya kubadilisha silabasi iliyopo ili

iendane na maendeleo hayo.

Kutokana na sababu mbalimbali, kwa mfano, silabasi nchini Tanzania imekuwa

ikibadilishwabadilishwa. Silabasi inayotumiwa sasa katika shule za sekondari ni ya mwaka 2010

ambayo imetokana na kurekebishwa kwa silabasi ya mwaka 2005 ambayo na yenyewe pia ilitokana na

mabadiliko yaliyofanywa katika silabasi ya mwaka 1997.

Silabasi zinazotumika kufundishia hivi sasa katika nchi za Afrika Mashariki katika ngazi

mbalimbali za elimu, zinamtaka mwalimu kufundisha fasihi ya Kiswahili, ushairi ukiwemo. Katika nchi

ya Tanzania, silabasi ya Kiswahili sekondari inamtaka mwalimu kufundisha tanzu tatu za fasihi andishi:

riwaya, tamthilia na ushairi. Nchini Kenya, silabasi ya Kiswahili sekondari inamtaka mwalimu

kufundisha riwaya, tamthilia, hadithi fupi na ushairi. Katika nchi nyinginezo za Afrika Mashariki pia,

ushairi unabainishwa kama mojawapo ya tanzu za fasihi zinazopaswa kufundishwa. Kwa hiyo, silabasi

za Kiswahili zinazotumiwa sasa katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, na kwingineko duniani,

zinabainisha haja ya kufundisha ushairi wa Kiswahili.

KUTAFSIRI SILABASI KWENYE VITENDO

Tunapozungumzia kutafsiri silabasi kwenye vitendo tunamaanisha namna silabasi inavyoweza

kutekelezwa katika zoezi zima la ufundishaji au utumiaji wa silabasi katika ufundishaji. Utafsiri wa

silabasi katika ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili hauna tofauti na utafsiri wa silabasi katika

ufundishaji wa masomo mengine. Kuna hatua kadhaa ambazo mwalimu huzipitia katika kutafsiri

silabasi kwenye vitendo. Hatua zinazofahamika zaidi ni hizi zifuatazo:

1) Kufanya mapitio ya makusudi ya ufundishaji

2) Kuchagua na kupanga mada

3) Kutambua vitabu vya kiada na kuteua vitabu vya ziada vya kuvitumia

4) Kuandaa mpangokazi wa ufundishaji

5) Kuteua na kuandaa mbinu ya kufundishia

6) Kuandaa mwongozo wa ufundishaji darasani

7) Kuandaa zana za kufundishia

8) Kuingia darasani na kufundisha

9) Kufanya tathmini na upimaji

10)Kutoa matokeo ya tathmini na utoaji wa motisha

11)Upangaji wa ufundishaji ujao

Ni vema tuchambue hatua moja baada ya nyingine ili tuone jinsi ambavyo tunaweza kufundisha ushairi

wa Kiswahili kwa mafanikio makubwa na kuufanya utanzu huu kupiga hatua na kurithisha amali kwa

vizazi vijavyo.

1) Kufanya Mapitio ya Makusudi ya Ufundishaji wa Ushairi

Mara baada ya mwalimu kukusudia kufundisha ushairi wa Kiswahili au kupangiwa kufundisha

ushairi wa Kiswahili, anapaswa kuirejelea silabasi na kuona jinsi inavyoelekeza kufundisha ushairi wa

Kiswahili katika ngazi husika. Katika kuirejelea huko, mwalimu anapaswa kufanya mapitio ya

makusudi ya ufundishaji, yaani anapaswa kujua kwa nini ushairi wa Kiswahili unafundishwa katika

ngazi husika (iwe shule za msingi, sekondari au vyuo vya ualimu). Anapaswa kujiridhisha ikiwa

makusudi yanayobainishwa katika silabasi yanaendana na sera ya elimu ya taifa na sera ya elimu ya

ngazi husika (kama ni sera ya elimu ya msingi, sekondari na kadhalika).

2) Kuchagua na Kupanga Mada za Ushairi Zitakazofundishwa

Baada ya kuchambua makusudi ya kufundisha ushairi yanayobainishwa katika silabasi na kuona

kuwa yanaendana na sera ya elimu, hatua inayofuata ni kuchagua mada na kuzipanga. Ni wazi kuwa

uchambuzi wa silabasi ukifanywa kwa makini kuna mada ambazo zitabainika kutofaa, mada hizo, kwa

hiyo, zitaondolewa. Pia, kuna uwezekano wa kubaini kuwa mada zimepangwa katika mpangilio

135

usiokuwa na ushikamani. Hivyo, mada zitapangwa kwa namna ambayo italeta mantiki katika

ufundishaji wake na ina ushikamani. Aidha, kuna uwezekano wa kubainika kuwapo kwa mada radidi na

hivyo kuona haja ya kuondoa uradidi huo. Katika hatua hii, mwalimu atachagua mada zinazofaa

kufundishwa na kisha atazipanga, ipi itaanza kufundishwa na ipi itafuata, kwa namna ambayo anadhani

itawasaidia wanafunzi kuelewa. Njia bora ya upangaji wa maudhui inayopendekezwa zaidi ni kwa

kuanza kufundisha mada nyepesi na kisha kufuatiwa na mada ngumu na pia kufundisha mada

inayojulikana zaidi na kisha isiyojulikana (Samwel, 2012b).

3) Kutambua Vitabu vya Kiada na Kuteua Vitabu vya Ziada

Katika hatua hii mwalimu anapaswa kutambua vitabu vya kiada na kuteua vitabu vya ziada

atakavyovitumia katika ufundishaji wake. Kwa kawaida, vitabu vya kiada huidhinishwa na wizara

inayoshughulikia elimu kupitia taasisi mahsusi zinazohusika na zoezi hilo. Hivyo, mwalimu hana

chaguo katika vitabu hivi. Hata hivyo, mwalimu mzuri husoma na kuelewa mwenyewe kabla ya

kupanga ufundishaji wowote uwao. Hivyo, katika hatua hii mwalimu atasoma mada husika katika

vitabu vya kiada pamoja na vile teule vya ushairi. Vitabu teule vya ushairi hubadilishwa kila baada ya

miaka kadhaa ili kuondoa vitabu vilivyopitwa na wakati na kuingiza vitabu vipya. Pia, vitabu teule

hubadilishwa ili kuingiza vitabu vingine vyenye maudhui yanayopaswa kusisitizwa kwa wakati huo.

Kwa mfano, wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika, vitabu vya ushairi vyenye mrengo huo

vilikuwa muhimu sana, lakini nchi za Afrika zilipopata uhuru, vitabu hivyo vikapungua umuhimu wake

na hivyo kulazimu kubadilishwa na kuingizwa vitabu vingine vinavyobeba maudhui mengine kama vile

ukombozi wa wanawake na kadhalika. Mwalimu anapaswa kuvitambua vitabu hivyo kabla ya kuanza

zoezi la ufundishaji.

Mbali na hilo, mwalimu atachagua na kuvisoma vitabu vya ziada ambavyo atavirejela na kuvitumia.

Jambo la kukumbuka ni kwamba kuna vitabu vingi vinavyoelezea ushairi wa Kiswahili. Vingine ni

dhaifu sana na vimeandikwa bila kufanyika utafiti wa kutosha na vingine hata vina makosa katika

ufafanuzi wa dhana mbalimbali. Kwa hiyo, ni jukumu la mwalimu kutumia vitabu vifaavyo ambavyo,

kadri inavyowezekana, vinawasilisha mawazo sahihi kuhusiana na ushairi wa Kiswahili. Kwa mfano,

kama mwalimu atatumia kitabu cha Harries (1962) Kiswahili Poetry kufundishia chimbuko la ushairi

wa Kiswahili, ni wazi kuwa atawapotosha wanafunzi kwa kuwafundisha kuwa ushairi wa Kiswahili

chimbuko lake ni Uislamu na fasihi ya Kiarabu. Japo kitabu hiki kinasaidia kuelewa chimbuko la

ushairi wa Kiswahili, kinapaswa kutumiwa sambamba na vitabu vingine. Mwalimu, kwa hiyo, hana

budi kusoma vitabu hivi ili kubaini vile vilivyo bora na kuwaongoza wanafunzi kubaini na kuvitumia

vitabu wanavyofaa kuvisoma.

4) Kuandaa Mpangokazi wa Ufundishaji

Baada ya kuchagua mada za kufundisha na kuzipanga ipi itaanza kufundishwa na ipi itafuata na

kusoma vitabu vinavyoelezea mada hizo, hatua inayofuata ni kuandaa mpangokazi wa ufundishaji.

Katika ualimu, mpangokazi wa ufundishaji huitwa azimio la kazi. Azimio la kazi ni mwongozo

ulioandaliwa na mwalimu unaoonesha mpangilio wa mada na mgawanyo wake katika ufundishaji

kwenye muda maalum. Azimio la kazi huandaliwa na mwalimu wa somo husika kama namna ya

kupanga ufundishaji wake utakavyokuwa katika kipindi fulani. Azimio la kazi huweza kuonyesha

ufundishaji katika kipindi cha juma moja, mwezi mmoja, muhula mmoja na kadhalika. Kwa kawaida,

azimio la kazi linaloonyesha ufundishaji katika muhula mmoja ndilo linaloonekana kutumiwa zaidi

kwani linamsaidia mwalimu kupanga ufundishaji utakavyokuwa katika kipindi kirefu. Azimio la kazi la

juma moja halitumiki sana kutokana na ukweli kuwa kama mwalimu atatumia utaratibu huo, atapaswa

kuandaa azimio la kazi kila juma na hivyo kupoteza muda mrefu. Aidha, azimio la kazi la muda mfupi

linaweza kumfanya mwalimu kushindwa kuwa na mipango ya muda mrefu kwa ajili ya darasa lake.

Hata hivyo, azimio la kazi linaloonyesha muda wa zaidi ya mwaka mmoja halifai kutumika kwani, kwa

kawaida, wanafunzi hubadilisha madarasa kila mwaka. Hivyo, azimio la kazi likizidi mwaka mmoja

litakuwa linashughulika na wanafunzi tofauti na labda tuseme haliwezekani kutekelezwa.

Azimio la kazi huwa na vipengele mbalimbali kama vile mwezi mada itakapofundishwa, juma

mada itakapofundishwa, idadi ya vipindi katika juma husika vitakavyotumiwa kufundishia na mada

kuu. Vipengele vingine ni mada ndogo, shughuli za mwalimu zitakazofanywa katika ufundishaji wa

136

mada husika, shughuli za mwanafunzi anazopaswa kuzifanya katika ushiriki wake kwenye zoezi la

kujifunza, vitabu vya rejea vitakavyotumika katika mada husika, vifaa na zana za kufundishia na maoni

yatakayotolewa baada ya zoezi la ufundishaji. Vipengele vyote katika azimio la kazi vinajazwa wakati

wa kuliandaa azimio la kazi husika isipokuwa kipengele cha maoni ambacho kitajazwa mara baada ya

ufundishaji kufanyika. Katika kipengele hicho cha maoni, mwalimu atajaza kile kilichotokea katika

ufundishaji, ikiwa mada imefundishwa kama ilivyopangwa au mada haikufundishwa kutokana na

jambo lolote lililotokea. Miongoni mwa mambo yanayoweza kutokea na yakasababisha wanafunzi

kutofundishwa mada husika katika muda uliopangwa ni kama vile misiba, maafa kama mafuriko na

kadhalika, wanafunzi kuingizwa katika shughuli nyingine badala ya shughuli ya msingi ya kujifunza

kama vile kufyeka, kulima na kadhalika. Kwa ujumla, si kila kilichopangwa na mwalimu katika azimio

la kazi lazima kitokee kwa namna ileile, upo uwezekano wa mambo kutoenda sawa na yalivyopangwa.

Aidha, mwalimu anaweza kubadilisha kipengele chochote kulingana na hali ilivyo wakati wa

ufundishaji. Kwa mfano, mwalimu anaweza kubadilisha shughuli za mwalimu na mwanafunzi

kulingana na hali ilivyo, anaweza kubadilisha kitabu cha rejea kutokana na kupata kitabu bora zaidi cha

rejea, anaweza kubadilisha zana za kufundishia kutokana na kuona kuwa hali ya wanafunzi ilivyo

hairuhusu kutumika kwa zana aliyoibainisha katika azimio la kazi au labda uwezo wa kiuchumi wa

shule kununua zana hiyo ni mdogo na kadhalika. Tunachosema hapa ni kuwa azimio la kazi ni mpango

wa kazi utakavyokuwa na mwalimu anapaswa kujitahidi kadri awezavyo kuutekeleza lakini pale

inapolazimu kubadilisha jambo fulani, mwalimu anaweza kufanya hivyo. Hata hivyo, kwa kuwa azimio

la kazi limeshaandaliwa, mabadiliko yoyote yale hayataingizwa katika azimio la kazi bali mabadiliko

hayo yataonekana katika andalio la somo la siku husika. Katika shule mbalimbali kuna karatasi

maalumu za kuandalia azimio la kazi. Karatasi hizi huwa ni pana zaidi ya karatasi za kawaida. Katika

shule nyingine karatasi hizi hazipo na hivyo ni jukumu la walimu kutafuta karatasi watakazoandalia

azimio la kazi. Mfano wa azimio la kazi unabainishwa hapa chini:

137

SHULE YA SEKONDARI SINGINO

IDARA YA KISWAHILI

AZIMIO LA KAZI LA SOMO LA KISWAHILI KWA MUHULA WA KWANZA, 2013

KIDATO CHA TANO HKL

MWEZI

JUMA

VIPINDI

MADA KUU MADA

NDOGO

SHUGHULI

ZA

MWALIMU

SHUGHULI

ZA

MWANAFUNZI

VITABU VYA

REJEA

VIFAA NA ZANA

ZA KUFUNDISHIA

MAONI

YA MWALIMU

J A N U A R I

1

2 FASIHI KWA

UJUMLA

DHANA ZA

FASIHI

Kuwaongoza

wanafunzi

kuelewa dhana

ya fasihi

ikiwemo

ushairi kwa

kubainisha kazi

mbalimbali za

fasihi

Kushiriki katika

kujifunza kwa

kubainisha dhana za

fasihi kutoka katika

kazi mbalimbali za

fasihi

Samwel

(2012b)

Hadithi

Fupi:

Nadharia ,

Mbinu na

Mifano,

Iringa:

Kasenyenda

Tanzania

Chati za kazi

mbalimbali za fasihi Mada imefundishwa

2 FASIHI KWA

UJUMLA

AINA ZA

FASIHI

Kuwaongoza

wanafunzi

kubaini aina za

fasihi kwa

kutumia kazi

mbalimbali za

fasihi

Kushiriki katika

kujifunza kwa

kubainisha aina za

fasihi kutoka katika

kazi mbalimbali za

fasihi

Mulokozi, M.M.

(1996) Fasihi ya

Kiswahili, Dar es

Salaam: OUT

Chati za kazi

mbalimbali za fasihi

Mada

haikufundishwa

kwani iliingialiana

na michezo ya

UMISSETA. Mada

itarudiwa katika

muda wa ziada

2

2 FASIHI KWA

UJUMLA

DHIMA ZA

FASIHI

Kuwaongoza

wanafunzi

kubaini dhima

za fasihi kwa

kutumia kazi

mbalimbali za

fasihi

Kushiriki katika

kujifunza kwa

kubainisha dhima za

kazi mbalimbali za

fasihi

Mulokozi, M.M.

(1996) Fasihi ya

Kiswahili, Dar es

Salaam: OUT

Chati za kazi

mbalimbali za fasihi

Mada ilifundishwa

ingawa wanafunzi

wachache

walihudhuria.

Wasiohudhuria

walipewa msaada

2 FASIHI KWA

UJUMLA

TANZU ZA

FASIHI

ANDISHI

Kuwaongoza

wanafunzi

kubaini tanzu

za fasihi

andishi

Kushiriki katika

kujifunza kwa

kubainisha tanzu za

fasihi andishi

Mulokozi, M.M.

(1996) Fasihi ya

Kiswahili, Dar es

Salaam: OUT

Chati za ushairi,

riwaya, tamthiliya na

hadithi fupi

Mada ilifundishwa

138

3

4

UCHAMBUZI

WA MASHAIRI

MAUDHUI

YA Diwani

ya MEA

Kuwaongoza

wanafunzi

kusoma na

kubaini

maudhui

yanayojitokeza

katika Diwani

ya MEA

Kushiriki katika

kusoma na

kubainisha maudhui

yanayojitokeza

katika Diwani ya

MEA

Samwel, M. na

Akech, K. (2013)

Diwani ya MEA,

DSM: DZT

Publishers

Chati za ukutani za

mifano ya maudhui ya

kazi za kifasihi

Mada imefundishwa

UCHAMBUZI

WA MASHAIRI

DHAMIRA

ZA

Diwani ya

MEA

Kuwaongoza

wanafunzi

kusoma na

kubaini

dhamira

zinazojitokeza

katika Diwani

ya MEA

Kushiriki katika

kusoma na

kubainisha dhamira

zinazojitokeza

katika Diwani ya

MEA

Samwel, M. na

Akech, K. (2013)

Diwani ya MEA,

DSM: DZT

Publishers

Chati za ukutani za

mifano ya dhamira za

kazi za kifasihi

Mada imefundishwa

4

4

UCHAMBUZI

WA MASHAIRI

FANI YA

Diwani ya

MEA

Kuwaongoza

wanafunzi

kusoma na

kubaini fani

iliyotumika

katika Diwani

ya MEA

Kushiriki katika

kusoma na

kubainisha fani

iliyotumika katika

Diwani ya MEA

Samwel, M. na

Akech, K. (2013)

Diwani ya MEA,

DSM: DZT

Publishers

Chati za ukutani za

mifano ya mbinu za

kifani za kazi za

kifasihi

Mada imefundishwa

UCHAMBUZI

WA MASHAIRI

MATUMIZI

YA LUGHA

KATIKA

Diwani ya

MEA

Kuwaongoza

wanafunzi

kusoma na

kubaini lugha

iliyotumika

katika Diwani

ya MEA

Kushiriki katika

kusoma na

kubainisha lugha

iliyotumika katika

Diwani ya MEA

Samwel, M. na

Akech, K. (2013)

Diwani ya MEA,

DSM: DZT

Publishers

Chati za ukutani za

mifano ya tamathali za

semi

Mada imefundishwa

1 M I T I H A N I Y A N U S U M U H U L A

K U F U N G A S H U L E K W A L I K I Z O Y A N U S U M U H U L A

139

5) Kuteua na Kuandaa Mbinu ya Kufundishia Ushairi na Maandalizi Yake

Baada ya kuandaa azimio la kazi, hatua inayofuata ni kwa mwalimu kuchagua mbinu muafaka

atakayoitumia darasani. Kuna mbinu nyingi ambazo mwalimu anaweza kuzitumia darasani katika

ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili. Kuna mbinu kuu mbili zinazoweza kutumiwa katika ufundishaji

darasani. Mbinu hizo ni mbinu shirikishi na mbinu zisizo shirikishi. Mbinu shirikishi ni zile ambazo

mwalimu anampa mwanafunzi nafasi kubwa ya kutoa mchango wake katika mchakato wa kufundisha

na kujifunza. Katika mbinu hii matakwa na matarajio ya wanafunzi yanazingatiwa na hivyo

mwanafunzi ndiye anakuwa mtendaji mkuu katika mchakato wa kufundisha na kujifunza. Jukumu la

mwalimu katika mbinu hii linakuwa lile la mwezeshaji. Mbinu zisizo shirikishi ni kinyume chake.

Katika mbinu zisizo shirikishi mwalimu huwa ndiye mtendaji mkuu na kwamba zoezi la utoaji wa

maarifa linamilikiwa na mwalimu. Mbinu zisizo shirikishi zina hasara nyingi sana katika matumizi

yake kwani zinamchukulia mwalimu kuwa ndiye mjuzi wa kila kitu na kwamba mwanafunzi hajui

lolote. Mbinu hizi huwanyima wanafunzi nafasi ya kuonesha hisia na uwezo wao. Katika ulimwengu

wa sasa, mbinu shirikishi ndizo zinazopigiwa chapuo zaidi kutokana na ubora wake. Hata zile mbinu

ambazo si shirikishi kwa asili yake, zinashauriwa zirekebishwe katika matumizi yake na kumshirikisha

mwanafunzi kwa kiasi kikubwa ili ziwe shirikishi pia kwa namna fulani. Hivyo, ili kufanikisha

ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili, mbinu shirikishi zinafaa zaidi. Uteuzi wa mbinu ya kufundishia

inategemea mambo kadhaa. Miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo:

(i) Mada: mada itaamua mbinu ya kutumika kufundishia. Kila mada inaweza kufundishika vizuri

kwa kutumia mbinu yake mahsusi na kwamba si kila mbinu inaweza kutumika katika kila mada.

Kwa mfano, itakuwa vigumu sana kutumia mbinu ya nyimbo kufundishia mada ya ushairi

kwani ushairi wenyewe ni nyimbo pia.

(ii) Malengo: uteuzi wa mbinu ya kufundishia pia utategemea malengo mahsusi ambayo mwalimu

anakusudia yatimie katika mada fulani. Kama lengo la mwalimu ni kuwafanya wanafunzi

wakumbuke jambo hilo ni wazi kuwa atatumia mbinu ambayo inaamsha kumbukumbu ya

wanafunzi; kama lengo ni kuwafanya wanafunzi wathamini, au wachanganue au waweze

kufanya kwa vitendo na kadhalika, mbinu inayopaswa kuteuliwa ni ile ambayo inaweza

kutimiza malengo husika.

(iii) Ukubwa wa darasa: kama darasa ni kubwa sana (lina wanafunzi wengi) kuna mbinu hazitafaa

kutumika na pia kama ni dogo sana (lina wanafaunzi wachache) kuna mbinu hazitafaa

kutumika. Kwa mfano, kama darasa ni kubwa sana ni wazi kuwa mbinu ya majadiliano katika

vikundi haitafaa sana kwani makundi hayo hayatapata muda wa kutosha kuwasilisha yote na

yakaisha. Aidha, kuna uwezekano wa kuibuka zogo kubwa sana wakati wa majadiliano.

(iv)Hali ya wanafunzi: wanafunzi wanaweza kuwa katika hali ambayo hairuhusu utumizi wa

mbinu fulani. Kwa mfano, kama wanafunzi wana uwezo mdogo sana kiakili kuna mbinu

hazitafaa kabisa kuzitumia maana zinahitaji wanafunzi wenye uwezo kiasi. Aidha, kama

wanafunzi wamepatwa na msiba wa mwenzao ni wazi kuwa mbinu ambazo si shirikishi

hazitafaa kwani watakuwa wamejaa hofu na huzuni. Njia bora katika mazingira kama hayo ni

mbinu shirikishi ambayo itawashirikisha na wao na hivyo kuwaondolea hofu na mawazo.

(v) Hali ya mwalimu: mwalimu pia anaweza kuathiri uteuzi wa mbinu ya kufundishia. Mbinu

inayoteuliwa inapaswa kuendana na mwalimu, yaani mwalimu awe na umahiri katika kuitumia

ili iweze kuwa na manufaa makubwa. Mwalimu lazima aelewe namna ya kuiandaa mbinu

husika, namna ya kuitumia, faida na hasara zake ili matumizi ya mbinu hiyo yafanikishe somo

lake. Mbinu ambayo mwalimu haimudu vema hapaswi kuitumia. Vilevile, kuna wakati

mwalimu kama binadamu, anaweza kuwa katika hali inayomzuia kutumia mbinu fulani. Labda

hana amani, hana furaha, ana matatizo binafsi na kadhalika. Akiwa katika hali kama hizo ni

dhahiri hataweza kuwa msemaji mkuu darasani. Ni vema msemaji mkuu awe mwanafunzi na

mwalimu awe mwezeshaji tu. Hii ni kusema kuwa katika hali kama hizo, mbinu shirikishi ni

bora zaidi.

(vi)Gharama ya mbinu husika: kila mbinu ina namna yake ya kuiandaa na inahitaji gharama zake.

Kuna mbinu nyingine ni ghali sana na nyingine ni nafuu. Hivyo, uteuzi wa mbinu uzingatie

uwezo wa shule au/na wazazi kuimudu mbinu husika. Mbinu kama ziara, kualika mgeni na

nyinginezo ni gharama sana. Gharama hii huweza kuwa si tu katika fedha bali pia muda.

140

Hivyo tuseme kuwa kuna mbinu nyingi ambazo mwalimu anaweza kuteua kuzitumia katika

ufundishaji, si tu wa ushairi wa Kiswahili bali pia mada nyinginezo. Miongoni mwa mbinu ambazo

mwalimu anaweza kuzitumia ni kama hizi zifuatazo:

a) ZIARA: hii huweza kuwa ziara halisi au ziara zisizo halisi. Ziara zisizo halisi ni zile ambapo

wanafunzi husafirishwa kimawazo kwenda katika maeneo yanayohusu kile kinachofundishwa.

Ziara halisi, kwa upande wake, ni zile ambazo wanafunzi husafiri kwa dhahiri kwenda maeneo

yanayohusu kile kinafundishwa. Ziara zisizo halisi hufanywa sana katika zoezi la kufundisha na

kujifunza kiasi kwamba inapozungumziwa mbinu ya ziara inaonekana ni ziara halisi tu kwani

ziara zisizo halisi ni kitu kilichozoeleka. Katika ziara halisi, wanafunzi wanaweza kuchukuliwa

kupelekwa katika sehemu halisi zinazohusiana na ushairi wa Kiswahili. Kwa mfano,

wanapojifunza kuhusu ushairi simulizi wa Kibantu, wanafunzi wanaweza kusafiri na kwenda

kwenye mikoa ambapo shughuli za jando na unyago hufanyika ili wakajionee utendaji wa

nyimbo za jandoni na unyagoni, ama wanaweza kusafiri kwenda katika jamii ambazo bado

zinatenda majigambo na pia wanafunzi wanaweza kutembelea maeneo waliyoishi wasanii

maarufu wa ushairi wa Kiswahili kama vile Shaaban Robert na kadhalika.

Mbinu hii ina ubora na udhaifu wake. Ubora wa mbinu hii ni kama ifuatavyo: kwanza,

inabadilisha mazingira ya kufundisha na kujifunza na hivyo inakuwa na nafasi kubwa ya

kuwasaidia wanafunzi kuelewa. Kwa kawaida, binadamu hupenda mambo tofautitofauti na

hivyo kujifunza katika mazingira yaleyale kila siku miaka nenda rudi kunaweza kumfanya

mwanafunzi kutoelewa somo kutokana na kuyachoka mazingira. Huweza pia kumfanya

mwalimu kutopenda kufundisha kutokana na kuyachoka mazingira. Pili, mbinu hii huweza

kuwafanya wanafunzi kujifunza katika mazingira halisi. Wataalamu wa elimu wanakubaliana

kuwa kujifunza kwa kutumia mazingira halisi husaidia sana wanafunzi kuelewa vizuri somo.

Hivyo, mbinu hii inaweza kuwasaidia wanafunzi kuelewa somo. Tatu, mbinu hii huweza

kusaidia wanafunzi kutunza kumbukumbu. Kwa kuwa wanafunzi wanajifunza katika mazingira

halisi, nafasi ya wanafunzi kukumbuka somo walilojifunza huwa ni kubwa sana.

Mbali na ubora huo mbinu hii ina udhaifu ufuatao: kwanza, mbinu hii ni ya gharama

sana na hivyo haiwezi kutumika katika shule zisizokuwa na uwezo mkubwa kifedha (kama

shule ndiyo hugharamia) au katika jamii ambazo wazazi hawana uwezo mkubwa kifedha (kama

wazazi ndiyo wanagharamia). Kwa kawaida, katika shule nyingi wanafunzi huchangia kiasi cha

fedha kumudu gharama ya usafiri, malazi na chakula wakati wa ziara. Hivyo, wanafunzi ambao

wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia ziara wanaweza kushindwa kushiriki katika

ujifunzaji kwa kutumia mbinu hii. Pili, mbinu hii huweza kuathiri vipindi vya masomo mengine.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa kama ziara inafanyika katika sehemu ya mbali na shuleni,

itahitaji muda zaidi. Jambo hilo litaathiri vipindi vya masomo mengine shuleni. Namna bora ya

kukabiliana na hili ni kwa kufanya ziara katika kipindi cha likizo au wakati wa mapumziko ya

mwisho wa juma. Hata hivyo, changamoto inaweza kuwa kwa mwalimu kuiacha mada husika

hata kama wakati wa kuifundisha umefika hadi likizo itakapofika ili autumie muda huo

kufundisha mada hiyo. Changamoto ya pili ni kuwa muda wa likizo ni kwa ajili ya wanafunzi

kupumzisha akili ili ziweze kurudi katika hali ya kawaida kabla ya kuendelea na ujifunzaji.

Akili ambayo haina muda wa kupumzika hukosa ufanisi katika zoezi la kujifunza. Likizo pia

humsaidia mwalimu kujiandaa kwa ajili ya ufundishaji ujao. Hivyo, kuitumia likizo kwa ajili ya

ziara za kitaaluma kunaweza kuwaathiri wanafunzi na walimu pia.

Udhaifu wa tatu ni kuwa ziara zinaweza kuchochea tabia mbaya miongoni mwa

wanafunzi. Kama shule inahusisha wanafunzi wa kike na kiume waliokwisha kubalehe na

wanafunzi hao wakaruhusiwa kusafiri kwenye gari moja kwenda kwenye eneo la ziara huku

wakiwa wamekaa kiti kimoja kwa muda mrefu usiku na mchana, mahusiano ya kimapenzi

huweza kuibuka. Aidha, ziara zinapofanywa katika maeneo ya miji mikubwa inayowavutia

wengi, wanafunzi huweza kutumia muda huo wa ziara kama sehemu ya matembezi na si kama

sehemu ya kujifunza na hivyo kuathiri maana nzima ya ziara. Ili kudhibiti haya ni jukumu la

mwalimu aliyeambatana na wanafunzi katika ziara kuwaeleza wanafunzi kwa kina dhumuni la

safari yao, yale wanayotarajiwa kuyafanya na yale ambayo hawatarajiwi kuyafanya. Pia, wakati

141

wote wa safari na wakati wa ziara, mwalimu anapaswa kudhibiti mienendo na tabia za

wanafunzi na kuwapanga kwa namna ambayo haitaibua tabia zisizofaa.

b) KUALIKA MGENI: katika mbinu hii mtu ambaye si mwalimu anayefundisha somo hilo kila

siku hukaribishwa ili kuja kutoa mada husika. Mgeni huyu anaweza kuwa mwalimu wa somo la

ushairi wa Kiswahili kutoka darasa lingine la shule hiyo, mwalimu wa ushairi wa shule nyingine

au mtaalamu wa ushairi kutoka taasisi zinazojishughulisha na ushairi na Kiswahili kwa ujumla

kama vile TATAKI, BAKITA, CHAKITA, CHAKAMA, CHAKA, UKUTA na kadhalika. Kwa

kawaida, mgeni husika huandikiwa barua rasmi ya mwaliko na kuelezwa mada na yale

anayokusudiwa kuyafanya. Mwaliko huo lazima uoneshe siku na saa mada hiyo itakapotolewa.

Kwa kawaida, ni jukumu la waalikaji kumgharamia mgeni usafiri, chakula na masuala mengine

muhimu japokuwa zipo baadhi ya taasisi ambazo huweza kuwagharamia wataalamu wao

wanapoalikwa katika shughuli kama hizo. Wakati mgeni anapokuwa anatoa mada husika kwa

wanafunzi, mwalimu lazima awepo ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata kile

alichokikusudia na kwamba wanafunzi wanafuatilia kwa makini mada hiyo.

Ubora wa mbinu hii ni kuwa wanafunzi wanapata nafasi ya kufundishwa na mtu tofauti

na yule anayewafundisha kila siku. Hivyo, kunakuwa na uwezekano wa wanafunzi kuelewa

somo na kuondoa uwezekano wa wanafunzi kumchoka mwalimu wa somo husika. Faida

nyingine ni kuwa kama mgeni atakuwa mbobezi katika mada husika, wanafunzi watakuwa na

uwezekano wa kuelewa zaidi kuliko kama mada hiyo ingefundishwa na mwalimu wa somo.

Zaidi ya ubora huo, mbinu hii ina udhaifu pia. Udhaifu mkuu wa mbinu hii ni gharama.

Mbinu hii ni ghali mno na hasa pale mgeni anapotoka mbali. Pia kama mgeni atakuwa si

mwalimu kuna uwezekano wa kushindwa kuwasaidia wanafunzi kuelewa mada husika.

Walimu, zaidi ya kujua masomo husika, wamefundishwa pia masuala kama saikolojia ya

wanafunzi, mitaala, namna ya kufundisha na kadhalika. Mambo yote kwa ujumla huwasaidia

sana katika kuwasilisha ujuzi walionao. Mtaalamu wa ushairi ambaye si mwalimu atashindwa

kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo binafsi ya kisaikolojia au kitaaluma ambao ili

kuwatambua ni lazima mhusika ajue masuala ya saikolojia na mbinu za ufundishaji.

c) MAJADILIANO: hii ni mbinu ambapo wanafunzi huachwa wajadiliane wao kwa wao juu ya

mada mahsusi. Majadiliano pia huweza kuwa baina ya mwalimu na mwanafunzi. Kuna aina kuu

mbili za majadiliano, majadiliano ya darasa zima na majadiliano katika vikundi vidogo vidogo.

Majadiliano ya darasa zima huhusisha darasa lote juu ya mada fulani ya ushairi. Mbinu hii hufaa

sana kama darasa halina idadi kubwa sana ya wanafunzi, maana darasa likiwa na idadi kubwa

sana mjadala huweza kugeuka na kuwa zogo. Kwa upande wa majadiliano ya vikundi,

wanafunzi hugawanywa katika vikundi vidogovidogo na kuachwa wajadiliane. Katika

majadiliano ya vikundi ni muhimu kuzingatia uwiano wa jinsia kama darasa linahusisha

wanafunzi wa kike na kiume. Si jambo la busara kuwa na kikundi chenye wanafunzi wa kike

pekee au wa kiume pekee; ni vizuri kuwachanganya ili kuwapa uzoefu na kuwafanya wajihisi

kuwa sawa. Pia ni muhimu kuzingatia uwezo wa wanafunzi, si busara kuwa na kikundi chenye

wanafunzi wanaojiweza sana kitaaluma na kuwatenga na wale wasiojiweza. Ni vizuri wanafunzi

kuchanganywachanganywa ili kuwasaidia wale wasiojiweza na kuwafanya wasijisikie vibaya.

Vikundi hivyo pia visiwe vikubwa sana kwani kama wanafunzi wakiwa wengi sana kwenye

kundi kuna uwezekano wa wanafunzi wengine kutoshiriki katika mjadala. Aidha, ni muhimu

kwa kila kikundi kuwa na viongozi kama vile mwenyekiti wa kundi, katibu, mtunza muda,

muhamasishaji na kadhalika. Viongozi hao watasimamia shughuli nzima ya majadiliano na

uwasilishaji wa matokeo ya mjadala wao.

Faida ya mbinu hii ni kuwa wanafunzi wanashiriki katika zoezi la kujifunza na

kufundisha na hivyo ni mbinu bora. Wanafunzi wanaposhiriki katika mchakato wa kujifunza na

kufundisha hujihisi kuwa wamethaminiwa na huongeza uwezekano wa wanafunzi kuelewa.

Faida nyingine ni kuwa mbinu ya majadiliano hupunguza uwezekano wa wanafunzi kuchoka

wakati wa mchakato wa kufundisha na kujifunza na hivyo kuboresha mchakato huo. Vilevile,

142

mbinu hii huwajengea wanafunzi hali ya kujiamini, kushindana kwa hoja na kujenga hoja.

Mambo hayo ni muhimu sana katika maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi.

Kwa upande wa udhaifu wa mbinu hii ni kuwa kama zoezi la kujadiliana

halitasimamiwa vema kuna uwezekano wa kuibua zogo miongoni mwa wanafunzi. Pia

majadiliano huweza kuwafanya wanafunzi kutoka nje ya mada na kuanza kujadiliana mambo

mengine yasiyohusiana na mada. Mijadala kuhusiana na mambo ya michezo kama vile mpira

na kadhalika huweza kuibuka. Vilevile mbinu hii huweza kuwabagua baadhi ya wanafunzi, hasa

wale wenye uwezo mdogo kitaaluma na hivyo kujihisi kama wametengwa na mjadala mzima

kutawaliwa na watu wachache. Mambo haya, hata hivyo, yanaweza kudhibitiwa kwa usimamizi

mzuri wa mwalimu na viongozi wa vikundi.

d) MDAHALO: hii ni mbinu ambapo wanafunzi hugawanywa katika pande mbili na kujibizana

juu ya mada fulani kuhusu ushairi wa Kiswahili. Kwa kawaida pande hizo mbili huwa upande

unaounga mkono na ule unaopinga dai lililotolewa. Mwalimu huandaa mada na kuwaacha

wanafunzi wakijibizana juu ya mada hiyo na wakati huohuo wakijifunza mada fulani ya ushairi

ambayo mwalimu ameikusudia. Kwa mfano, mada inaweza kuwa Vina na Mizani ni Uti wa

Mgongo wa Mashairi ya Kiswahili, Chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni Ushairi wa Kiarabu,

Ushairi wa Bongo Fleva si Ushairi Asilia wa Kiswahili n.k. na wanafunzi wanajibizana,

wengine wakiunga mkono huku wengine wakipinga. Ili mbinu hii ifanikiwe panapaswa kuwa na

viongozi wa mdahalo, yaani mwenyekiti, katibu, mtunza muda na wachangiaji wakuu. Jukumu

la mwenyekiti ni kusimamia zoezi zima la majibizano na ndiye anayetoa nafasi kwa

wachangiaji. Katibu yeye huwa mtunza kumbukumbu na mwandishi wa hoja zinazotolewa.

Naye mtunza muda ana jukumu la kuhakikisha kila mchangiaji anatumia muda uliopangwa na

anayezidisha muda anagongewa kengele ili aweze kukaa chini na kutoa nafasi kwa mchangiaji

mwingine. Nao wachangiaji wakuu hugawanyika katika makundi mawili, wachangiaji wakuu

kwa upande wa utetezi wa mada na wachangiaji wakuu kwa upande wa upinzani. Kwa kawaida

baada ya mwenyekiti kutambulisha mada na kufafanua, wachangiaji wakuu hukaribishwa

kwanza kabla ya wachangiaji wengine. Wachangiaji wakuu hupewa muda mwingi zaidi ya

wachangiaji wa kawaida. Kwa mfano, mchangiaji mkuu anaweza kupewa dakika tano wakati

mchangiaji wa kawaida anapewa dakika tatu na kadhalika. Baada ya mdahalo kwisha hoja

zilizotolewa huhesabiwa na mshindi hutangazwa.

Ubora wa mbinu hii katika ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili ni kuwa wanafunzi

hushiriki katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Pili, mbinu hii huwajengea wanafunzi

hali ya kujiamini, kushindana kwa hoja, upangaji wa hoja na pia uwezo wa kushawishi. Katika

kujiamini tunaona kuwa ili kutoa hoja mwanafunzi lazima asimame mbele ya wenzake inajenga

ile hali ya kujiamini na kuongea mbele za watu. Pia kwa kuwa mdahalo ni kushindana kwa hoja,

wanafunzi wanajengewa uwezo wa kushindana kwa hoja. Vilevile wanafunzi wanawezeshwa

kuweza kupanga hoja za muhimu kwanza na zingine baadaye na uwezo wa kuwashawishi

wenzao kukubali uzito wa hoja wanayoitoa.

Mbali na ubora huo mbinu hii inaweza kuwa na udhaifu. Udhaifu mkuu ni kuwa kama

mdahalo usipodhibitiwa vizuri na wanafunzi kuelezwa kwa kina malengo yake unaweza

kushindwa kutoa maarifa ya mada iliyokusudiwa na kuishia kuwa kama sehemu tu ya

mabishano. Aidha, huweza kuishia katika ugomvi na uhasama wa kudumu miongoni mwa

wanafunzi.

Zaidi ya mbinu hizi tulizozifafanua hapa, mbinu nyingine zinazoweza kutumiwa na

walimu wa ushairi wa Kiswahili ni pamoja na maswali na majibu, igizo na bungua bongo.

Katika maswali na majibu mwalimu huandaa maswali yake ambayo atawauliza wanafunzi

katika kukamilisha ujifunzaji wa mada fulani ya ushairi. Katika igizo, mwalimu huwataka

wanafunzi kuigiza jambo fulani la kishairi. Mbinu hiyo huweza kufaa sana kufundishia ngonjera

ambazo huonekana kuwa na namna fulani ya uigizaji.

143

6) Kuandaa Mwongozo wa Ufundishaji wa Ushairi Darasani

Baada ya mwalimu kuandaa mpangokazi wa ufundishaji (azimio la kazi) unaoonyesha ushairi

utafundishwa lini na kuteua mbinu atakayoitumia katika ufundishaji wa mada anayokusudia

kuifundisha katika siku husika, jambo linalofuata ni kuandaa mwongozo wa ufundishaji wa ushairi

darasani. Mwongozo wa ufundishaji wa darasani huitwa andalio la somo. Andalio la somo ni

mwongozo wa mwalimu juu ya zoezi la ufundishaji darasani. Kwa kawaida, andalio la somo huonyesha

jinsi ufundishaji utakavyokuwa darasani katika kipindi husika. Nchi mbalimbali za Afrika Mashariki

zinatofautiana dakika kwa kila kipindi, na hata shule katika nchi moja huweza kutofautiana katika

dakika kwa kila kipindi. Zipo shule ambazo kipindi kimoja huwa ni dakika arobaini, nyingine ni dakika

arobaini na tano, hamsini na kadhalika. Somo la Kiswahili huweza kuwa na idadi tofautitofauti ya

vipindi katika shule mbalimbali. Zipo shule ambazo Kiswahili hupewa vipindi vitatu kwa wiki, yaani

vipindi viwili kwa pamoja (double periods) na kipindi kimoja (single period). Kwa hiyo mwalimu

katika shule kama hizo atapaswa kuandaa maandalio ya somo mawili, moja kwa ajili ya vipindi viwili

na lingine kwa ajili ya kipindi kimoja. Zipo shule ambazo, kama ilivyo kwa azimio la kazi, zina

madaftari maalumu ya kuandalia maandalio ya somo. Madaftari hayo yamegawanywa katika vipengele

mbalimbali vya andalio la somo na jukumu la mwalimu ni kujaza tu nafasi zilizoachwa katika

vipengele hivyo kulingana na kile anachokusudia kufundisha katika siku husika. Katika shule ambazo

hakuna madaftari ya aina hiyo mwalimu atatakiwa kutafuta karatasi zifaazo na kutengeneza andalio la

somo. Hata hivyo utaratibu wa kuwa na madaftari maalumu ya andalio la somo ni mzuri kwani

unawapunguzia walimu kazi kubwa ya kuandaa andalio la somo na pia husaidia katika kuleta uwiano

miongoni mwa walimu wa shule husika katika sura ya andalio la somo.

Andalio la somo lina vipengele mbalimbali. Vipengele hivyo ni pamoja na tarehe, idadi ya

wanafunzi na jinsi zao, idadi ya vipindi vitakavyotumika kufundisha, mada kuu, ujuzi unaotegemewa

kupatikana, mada ndogo, lengo kuu, malengo mahsusi, vitabu vya kiada, ziada na rejea, zana za

kufundishia, hatua za utoaji wa somo (ufundishaji), shughuli zitakazofanywa na mwalimu na

mwanafunzi, mbinu ya tathmini itakayotumika na maoni ya mwalimu kuhusu ufundishaji husika.

(a) Tarehe: katika kipengele hiki mwalimu atabainisha tarehe atakayofundisha somo husika.

(b) Idadi ya wanafunzi na jinsi zao: katika kipengele hiki mwalimu atabainisha idadi ya

wanafunzi aliowakuta darasani katika ufundishaji wake (waliohudhuria) na pia idadi ya wale

ambao hajawakuta (wasiohudhuria). Mwalimu mzuri atafuatilia idadi ya wanafunzi

wanaohudhuria darasani na wale ambao hawahudhurii ili kubaini tatizo linalowafanya

wengine wasihudhurie na kutafuta namna ya kuwasaidia. Mwanafunzi asiyehudhuria

darasani ana nafasi kubwa ya kushindwa mtihani. Aidha, ni vizuri kujua mahudhurio kwa

jinsi (wanafunzi wa kike na kiume) ili kuweza kubaini matatizo ya kijinsia yanayokwamisha

jinsi fulani kuhudhuria darasani na kutafuta ufumbuzi wake. Kuna baadhi ya jamii katika

nchi za Afrika Mashariki ambazo hazioni umuhimu wa kumpatia mtoto wa kike elimu,

hivyo mtoto wa kike huweza kuachwa nyumbani akifanya shughuli kama vile kupika,

kuchota maji na kadhalika wakati mtoto wa kiume akiwa shule. Kutokana na hilo, ni vizuri

kwa mwalimu kufuatilia mahudhurio kwa jinsi ili kuweza kuyabaini matatizo ya aina hiyo.

(c) Idadi ya vipindi: katika kipengele hiki mwalimu atabainisha kipindi chake ni cha ngapi na

kina muda gani. Muda kipindi kilipopangwa kinaweza kuathiri kueleweka kwa somo. Kwa

mfano, vipindi vingi vilivyo karibu na muda wa mapumziko huathiriwa sana kwani

wanafunzi huwa wanawaza mapumziko na hivyo wakati mwingine kushindwa kuelewa

masomo. Pia vipindi vinavyofuata baada ya chakula huambatana na kulala kwa wanafunzi

wengi kutokana na mchakato wa umeng’enyaji wa chakula. Aidha, idadi ya vipindi

alivyonavyo mwalimu vitaamua uwingi wa mambo atakayoyafundisha mwalimu. Hivyo ni

vema kubainisha idadi ya vipindi ili kupima ikiwa yale anayokusudia kuyafundisha

yatatosha katika muda husika wa kipindi.

(d) Mada kuu na mada ndogo: kwa kawaida mada kuu na ndogo hutoka katika silabasi na

kuchukuliwa katika azimio la kazi. Hata hivyo, mwalimu huweza kuamua mada ndogo

kulingana na muda alionao na upana wa mada husika.

144

(e) Ujuzi: katika kipengele hiki mwalimu anapaswa kubainisha ujuzi anaotaka wanafunzi

husika waupate mara baada ya kumaliza kufundisha na kujifunza mada kuu na mara baada

ya kumaliza kufundisha na kujifunza mada ndogo.

(f) Lengo kuu: hutokana na mada kuu na kwa kawaida huwa ni pana na haliwezi kufikiwa

katika ufundishaji wa kipindi kifupi bali baada ya ufundishaji wa mada nzima. Hivyo, lengo

kuu huwa la jumla na haliwezi kupimwa kirahisi. Maneno yanayotumika katika kuandaa

lengo kuu huwa hayapimiki, ni maneno ya jumla. Maneno hayo huweza kuwa kuelewa,

kujua, kutambua, kufahamu, kuzingatia na kadhalika. Kwa mfano, tunaweza kuwa na lengo

kuu: Kufikia mwisho wa mada wanafunzi waweza kuelewa chimbuko la ushairi wa

Kiswahili. Lengo hili kwa hakika halipimiki. Swali linaweza kuwa je, unawezaje kujua

kuwa wanafunzi wameelewa?

(g) Malengo mahsusi: huitwa pia madhumuni mahsusi. Haya hutokana na mada ndogo na,

kwa kawaida, huweza kupimwa mara baada ya kipindi kwisha. Maneno yanayotumiwa

katika kuandaa malengo mahsusi ni sharti yawe yanayoweza kupimika. Maneno hayo ni

kama vile kutaja, kueleza, kuorodhesha na kadhalika. Hivyo, lengo mahsusi linaweza kuwa:

Kufikia mwisho wa kipindi kila mwanafunzi wa kidato cha tano aweze kueleza kwa usahihi

hoja tatu kati ya tano za Harries zinazoeleza kuwa chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni

Uislamu na fasihi ya Kiarabu. Madhumuni haya ni mahsusi na yanapimika; mwisho wa

kipindi mwalimu anaweza kumwambia mwanafunzi aeleze na akiweza kueleza atajua kuwa

malengo mahsusi ya somo yamefikiwa.

(h) Vitabu vya kiada, ziada na rejea: hivi ni vile vitabu ambavyo mwalimu amevitumia katika

uandaaji wa somo. Mwalimu mzuri ni yule ambaye anasoma kabla ya kuingia katika

ufundishaji darasani. Jambo likieleweka vizuri kwa mwalimu linaweza pia kueleweka kwa

mwanafunzi. Vitabu vya kiada ni vitabu vya lazima katika mada husika, vitabu vya ziada ni

vile ambavyo hutumiwa kuongeza maarifa na vitabu vya rejea ni vitabu vinginevyo

vinavyozungumzia mada husika. Katika kipengele hiki mwalimu anaonyesha mahali

ambapo amejiegemeza katika mada husika.

(i) Zana za kufundishia: kuna tofauti kati ya zana za kufundishia na vifaa vya kufundishia.

Vifaa vya kufundishia ni dhana pana inayojumuisha vitu vyote vinavyoenda sambamba na

zoezi la utekelezaji wa mtaala wowote uwao. Ni vitu vyote vinavyosaidia mchakato wa

kufundisha na kujifunza ikiwa ni pamoja na silabasi, vitabu vya ziada, kiada na rejea, zana

za kufundishia, vifaa kama vile chaki, ubao, hata jengo lenyewe la darasa na kadhalika.

Zana za kufundishia, kwa upande wake, ni vielelezo ambavyo mwalimu ataona vinafaa

kufundishia mada husika ili kumsaidia mwanafunzi kuelewa. Kwa kawaida mwalimu ndiye

huteua zana za kufundishia, huziandaa na kuzitumia darasani katika mchakato wa

kufundisha na kujifunza. Vielelezo hivi huweza kuwa vitu halisi, picha, matukio

yanayosawiri mada na hata sehemu huweza kuwa zana ya kufundishia.

Katika kipengele hiki mwalimu hubainisha zana za kufundishia atakazozitumia. Zana

mbalimbali ambazo mwalimu huzitumia katika ufundishaji wake. Matumizi ya zana za

kufundishia yana dhima kubwa sana katika mchakato wa kufundisha na kujifunza. Miongoni

mwa dhima hizo ni kama ifuatavyo:

· Zana za kufundishia humshirikisha mwanafunzi katika zoezi la ufundishaji na

kujifunza

· Humsaidia mwalimu kulifanya somo kuwa halisi kuliko kuwa la kufikirika

· Humsaidia mwanafunzi kuzingatia anayojifunza

· Husaidia kumbukumbu ya mwanafunzi

· Huchochea udadisi kwa wanafunzi

· Huondoa uchovu kwa wanafunzi

· Husaidia wanafunzi kuelewa mada husika

(j) Hatua za utoaji wa somo: katika kipengele hiki mwalimu atabainisha hatua za ufundishaji

atakazozifuata darasani. Kwa kawaida utoaji wa somo darasani huwa na hatua tano:

utangulizi, utoaji wa maarifa mapya, kukazia maarifa, matumizi na hitimisho la somo.

Katika utangulizi, kwa kawaida mwalimu huwaandaa wanafunzi wake kwa ajili ya mada

145

mpya. Kwanza, mwalimu hupima kumbukumbu ya wanafunzi katika mada iliyopita na kisha

kuhusisha mada iliyopita na mada mpya. Baada ya hapo mwalimu hutaja na kufafanua

malengo mahsusi ya somo. Kumekuwa na mjadala ikiwa malengo ya somo ni kwa ajili ya

mwalimu au mwanafunzi. Hata hivyo, inakubalika kuwa malengo ya somo ni kwa ajili ya

mwalimu na mwanafunzi. Kwa mwalimu, malengo ni muhimu kwani humsaidia kujua nini

akifundishe, akifundisheje na pia atumie mbinu gani kutathmini. Kwa mwanafunzi, malengo

ni muhimu kwani humsaidia kujua kwa nini anafundishwa na ategemee nini na pia mwisho

wa kipindi au mada atatarajiwa kuwa na uwezo wa kufanya nini. Hii humfanya mwanafunzi

wakati wote wa mchakato wa kufundisha na kujifunza awe anatafuta kutimiza malengo

hayo. Kwa kuwa malengo haya ni muhimu kwa mwalimu na mwanafunzi, ni muhimu kwa

mwalimu kuyasoma malengo haya darasani na kuyafafanua kabla ya kuendelea na

ufundishaji wake ili kuwaandaa wanafunzi.

Baada ya utangulizi, hatua inayofuata ni utoaji wa maarifa mapya. Katika hatua hii

mwalimu ataanza utoaji wa maarifa mapya aliyoyakusudia. Hatua zinazofuata ni kukazia

maarifa mapya aliyoyatoa na matumizi ya maarifa hayo mapya. Katika hatua hizi mwalimu

atatumia vifaa na zana mbalimbali za kufundishia kutimiza malengo ya somo husika na

kuwawezesha wanafunzi kuyatumia maarifa hayo. Hatua ya mwisho ni hitimisho. Katika

hatua hiyo, mwalimu atatoa muhtasari wa yale aliyoyafundisha na kisha atapima ikiwa

madhumuni mahsusi ya somo husika yametimizwa. Upimaji wa madhumuni mahsusi ya

somo huenda sambamba na kipengele kinachofuata, upimaji wa kutimia kwa malengo

mahsusi. Katika kipengele hiki cha utoaji wa somo darasani, mwalimu atabainisha kazi

zitakazofanywa na mwalimu na zile zitakazofanywa na mwanafunzi katika kila hatua.

(k) Maoni na tathmini: katika kipengele hiki mwalimu atajipima mwenyewe na ufundishaji

wake kuona ikiwa amefanikiwa au la. Mwalimu katika kipengele hiki atabainisha wanafunzi

wangapi wameelewa na wangapi hawakuelewa na wale ambao hawakuelewa, hata kama ni

wachache, aliwasaidiaje. Katika kipengele hiki mwalimu huweza kuandika, kwa mfano,

mada imefundishwa na kueleweka kwani asimilia tisini ya wanafunzi walipata zaidi ya nusu

katika zoezi nililowapa na wale walioshindwa nilitenga muda wa ziada kuwaelewesha vizuri

zaidi.

(l) Saini ya mwalimu: Katika kipengele hiki mwalimu atapaswa kuweka saini yake ili

kuthibitisha kuwa aliyoyasema huko juu katika vipengele vingine ni kweli. Kipengele hiki

huitwa pia kipengele cha ithibati, yaani kipengele cha kuthibitisha maelezo ya huko juu.

Saini hutumiwa mahali pengi kama njia ya kuthibitisha ukweli wa mambo mbalimbali. Kwa

mfano, saini hutumika benki kuhakikisha kuwa malipo yaliyofanywa ni sahihi, saini

hutumiwa pia katika mikataba na kadhalika.

MFANO WA ANDALIO LA SOMO

SHULE YA SEKONDARI SINGINO

ANDALIO LA SOMO LA KISWAHILI

TAREHE KIDATO VIPINDI MUDA MAHUDHURIO

WALIOFIKA

W/WAKE: 40

W/UME: 20

1/5/2013 V HKL

2

DAKIKA 80

(Saa 6.00-7.20)

WASIOFIKA: 2

MADA KUU: UHAKIKI WA MASHAIRI

MADA NDOGO: DHAMIRA KATIKA DIWANI YA MEA

LENGO KUU: Wanafunzi waweze kutambua dhamira mbalimbali zinazoibuliwa na waandishi wa

Diwani ya MEA.

UJUZI: Wanafunzi waweze kusoma kazi ya fasihi na kubainisha mawazo makuu yaliyomo katika kazi

husika

MADHUMUNI MAHSUSI: Kufikia mwisho wa kipindi cha dakika 80 wanafunzi wa kidato cha tano

146

HKL kwa kutumia Diwani ya MEA waweza kutaja na kuzieleza kwa usahihi dhamira

angalau tano zinazojitokeza katika Diwani ya MEA huku wakitoa mifano katika nchi za

dunia ya tatu.

MAREJEO: Samwel, M. na Akech Kabiero (2013) Diwani ya MEA, Dar es Salaam: DZT Publishers

ZANA ZA KUFUNDISHIA: Chati za ukutani za dhamira za kazi za kifasihi na uhusiano wake na

uhalisia.

UTOAJI WA SOMO:

HATUA

NA

MUDA

SHUGHULI

ZA

MWALIMU

SHUGHULI

ZA

MWANAFUNZI

UTANGULIZI

(Dakika 10)

-Kuwajengea wanafunzi utayari

-Kupima maarifa ya awali juu ya

nadharia ya fasihi

-Kuhusisha nadharia ya fasihi na

uchambuzi wa mashairi

-Kueleza madhumuni mahsusi

ya somo jipya

-Kuwa tayari kwa ajili ya

kujifunza

-Kujibu maswali wanayoulizwa

kuhusiana na maarifa ya awali

-Kuuliza maswali kuhusu

maeneo ambayo hawajayaelewa

vizuri

-Kusikiliza

KIINI (Utoaji wa maarifa

mapya, kukazia maarifa,

matumizi)

(Dakika 60)

-Kuwaongoza wanafunzi

kubainisha dhamira

zinazojitokeza katika Diwani ya

MEA

-Kuwaongoza wanafunzi

kutumia chati za dhamira

kuhusisha dhamira hizo na

uhalisia wake katika dunia ya

tatu

-Kuwashirikisha wanafunzi

katika zoezi zima la kujifunza

-Kushirikiana na mwalimu

katika kubainisha dhamira

zinazojitokeza katika Diwani ya

MEA

-Kutumia chati za ukutani

kubainisha dhamira na kueleza

zinavyohusiana na hali halisi

-Kujibu maswali wanayoulizwa

na mwalimu na wao kuuliza

maswali wasipopaelewa

HITIMISHO

(Dakika 10)

-Kutoa muhtasari wa mambo

muhimu yaliyofundishwa

-Kupima kufikiwa kwa malengo

mahsusi ya somo

-Kusikiliza, kuuliza maswali na

kujibu maswali

-Kufanya zoezi walilopewa ili

kupima kufikiwa kwa malengo

mahsusi ya somo

MAONI NA TATHMINI: Mada imeeleweka kwani wanafunzi wameweza kutaja dhamira kama vile

rushwa, uongozi mbaya n.k. na kuzihusisha na hali halisi. Asimilia 98 ya wanafunzi wamepata

zaidi ya alama 60 kati ya 100 katika zoezi nililowapa. Wachache ambao hawakufanya vizuri

nimepanga kuwasaidia katika muda wa ziada ili kuhakikisha wanaelewa pia.

SAINI YA MWALIMU: Jasinta.

7) Kuandaa Zana za Kufundishia

Baada ya andalio la somo kukamilika, mwalimu anapaswa kuandaa zana za kufundishia mada

husika. Kama tulivyobainisha katika kipengele kilichopita, kwa kawaida, mwalimu hubainisha, katika

andalio la somo, zana za kufundishia mada husika. Baada ya kuzibainisha, hatua inayofuata ni

kuziandaa kwa kuzingatia sifa tulizozieleza hapo awali kwamba zana hizo ni muhimu ziwe zenye

kuvutia, zenye rangi nzuri na pia zinazoonekana vizuri hata kutokea mwisho wa darasa. Aidha, zana za

kufundishia lazima zitumie maandishi makubwa. Maandalizi ya zana hizo hutegemea aina ya zana

husika. Jambo lingine la muhimu ni kuwa zana zinapaswa kuendana na mada husika.

147

8) Kuingia Darasani na Kufundisha

Kuingia darasani na kufundisha huitwa pia ufundishaji halisi darasani. Ufundishaji halisi darasani ni

matokeo ya andalio la somo aliloliandaa mwalimu. Jambo la kukumbuka hapa ni kuwa andalio la somo

ni mwongozo tu ambao mwalimu anautumia na kwamba mwalimu hapaswi kuwa mtumwa wa andalio

la somo. Mwalimu anaweza kurekebisha jambo lolote lililopo katika andalio la somo kulingana na hali

ya wanafunzi au hali halisi aliyoikuta darasani. Kwa mfano, mwalimu anaweza kurekebisha muda

alioutenga kuutumia katika kila kipengele, mwalimu anaweza kurekebisha mbinu ya ufundishaji na

kadhalika. Mfano mzuri ni kuwa kama mwalimu amepanga kutumia dakika kumi katika utangulizi na

akabaini kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi hawako tayari kwa ajili ya maarifa mapya na kwamba

maarifa ya awali hayajaeleweka vema, ni wazi kuwa mwalimu huyo atalazimika kutumia muda mrefu

zaidi katika utangulizi akifafanua maarifa ya awali kabla ya kuanza maarifa mapya. Pia kama mwalimu

amepanga kutumia mbinu ya muhadhara mfupi, kwa mfano, lakini akakuta wanafunzi hawapo katika

hali nzuri kutokana na msiba walioupata ni wazi kuwa mwalimu atalazimika kubadilisha mbinu yake ili

atumie mbinu shirikishi zaidi itakayowafanya wanafunzi kushiriki na kusahau madhila yao. Aidha,

mwalimu hapaswi kila mara kulirejelea andalio la somo kuangalia aliandika katika hatua fulani

atafanya nini. Mwalimu anapaswa kuelewa yale aliyoyaandika katika andalio la somo na kulirejelea

andalio la somo pale tu ambapo ni muhimu kufanya hivyo.

9) Kufanya Tathmini (Upimaji) ya Ufundishaji wa Ushairi

Kuna aina mbili za tathmini zinazoweza kufanywa katika ufundishaji. Kuna tathmini ambayo

mwalimu huifanya wakati zoezi la ufundishaji likiendelea na kuna tathmini ambayo mwalimu huifanya

baada ya ufundishaji kukamilika. Katika tathmini ya wakati zoezi la ufundishaji likiendelea, mwalimu

wakati wote wa ufundishaji wake darasani huuliza maswali mbalimbali kupima uelewa wa wanafunzi

juu ya mambo mbalimbali anayoyafundisha. Wakati wa tathmini hii inashauriwa kwa mwalimu

anayefundisha ushairi wa Kiswahili kuwauliza maswali wanafunzi tofautitofauti na si wanafunzi

wachache tu. Kuna baadhi ya walimu huwa na wanafunzi wao ambao huwauliza maswali mara kwa

mara. Ni vema kuwasaidia hata wanafunzi ambao hawako tayari kujibu maswali haya ili na wao

washiriki kujibu. Pia tathmini hii izingatie jinsi za wanafunzi, mwalimu anapaswa kuwauliza maswali

wanafunzi wa kike na kiume na si wa kiume pekee au wa kike pekee. Kuwauliza maswali wanafunzi

wa jinsi moja inaweza kujenga hisia kuwa mwalimu anaichukia jinsi fulani au mwalimu ana upendeleo.

Aina ya pili ya tathmini, tathmini inayofanywa baada ya kukamilika kwa zoezi la ufundishaji, nayo

imegawanyika katika sehemu kadhaa. Kuna tathmini inayofanywa kama kazi za nyumbani na kuna

tathmini inayofanywa kwa njia ya mitihani, majaribio na mazoezi. Kazi za nyumbani, mara nyingi

hutolewa mara tu baada ya zoezi la ufundishaji kukamilika. Wanafunzi wanapewa kazi ambazo

wanazifanya nyumbani na kuzirudisha shuleni kwa mwalimu siku inayofuata kwa ajili ya usahihishaji.

Mazoezi, majaribio na mitihani hutolewa na walimu katika kipindi fulani. Kwa mfano, kuna mitihani ya

wiki (weekly tests), mitihani ya mwezi (monthly tests), mitihani ya nusu muhula (mid-term tests),

mitihani ya mwisho wa muhula (terminal tests), mitihani ya mwisho wa mwaka (Annual tests) na

mitihani ya taifa (national examinations). Mitihani yote hii ina uzito wake kwa mwanafunzi, mwalimu

na jamii. Kwa kawaida ushairi wa Kiswahili huwa sehemu ya mtihani wa somo la Kiswahili katika

ngazi mbalimbali za elimu. Katika ngazi nyingine mtihani wa ushairi huweza kutenganishwa na

mtihani wa jumla wa Kiswahili na hivyo kuwa somo linalojitegemea au kuwekwa katika mtihani wa

fasihi ya Kiswahili. Kwa kawaida upimaji ni moja ya kipengele kinachobainishwa katika muhtsari na

kuna malengo kadhaa ya kufanya tathmini.

MALENGO YA KUFANYA TATHMINI

(i) Kupima uwezo asilia wa mwanafunzi na uwezo utokanao na kufundishwa na kujifunza

(ii) Kupima maendeleo ya mwanafunzi katika mchakato wa kufundisha na kujifunza kutokana na

malengo mahsusi

(iii) Kupima uwezo wa mwalimu kufundisha na mbinu za ufundishaji anazozitumia

(iv) Kupima ubora wa silabasi inayotumika

(v) Kutathmini ubora wa mazingira mwanafunzi anayojifunza

148

Kutokana na malengo haya ya upimaji tunabaini kuwa zoezi la kufanya tathmini linahusisha

kupima mafanikio ya ufundishaji kwa kuangalia matatizo ya mwanafunzi, mwalimu, silabasi na hata

mazingira ya kujifunzia. Hivyo, kushindwa kwa mwanafunzi katika mtihani ni kushindwa kwa

mwalimu, silabasi na hata mazingira ya kujifunzia japo si wakati wote hali inaweza kuwa hivyo. Kuna

wakati mwanafunzi anaweza kufanya vibaya kwenye mtihani kutokana na uzembe wake lakini mara

nyingi kufanya vibaya kwa mwanafunzi kunatokana na matatizo ya mwalimu, silabasi na hata

mazingira ya kutolea maarifa. Kama mwalimu atakuwa hajafunzwa na kufuzu vema ni wazi kuwa

wanafunzi wake watafanya vibaya maana hata Waswahili husema mwanafunzi hamzidi mwalimu

wake. Hivyo, kuna haja ya kuwekeza kwa walimu kwa kuwapa mafunzo bora na kuhakikisha fani ya

ualimu inatolewa kwa watu waliofanya vizuri na sivyo ilivyo sasa katika baadhi ya nchi za Afrika

Mashariki ambapo kozi ya ualimu (na hasa ualimu wa shule za awali, msingi na sekondari) inatolewa

kwa watu waliopata madaraja ya chini na kwamba ualimu ni fani ya watu walioshindwa kukubalika

katika fani nyinginezo. Kwa hakika, mwalimu anapaswa kuwa mtu aliyepata daraja la juu zaidi

kutokana na umuhimu wake katika jamii. Pia, walimu hao wanapaswa kupewa motisha ambayo itawapa

utulivu katika ufundishaji wao ili kuinua kiwango cha kufaulu. Aidha, mishahara na maslahi mengine

ya walimu hayana budi kuboreshwa. Jambo la kukumbuka ni kuwa kama mwalimu atafundisha akiwa

na furaha na amani, ana nafasi kubwa ya kufanikisha zoezi la utoaji wa maarifa.

Vilevile, hatuna budi kuhakikisha kuwa silabasi unakuwa bora ili kufanikisha zoezi zima la

kujifunza na kufundisha. Zaidi ya yote, wanafunzi wanapaswa kujifunza katika mazingira mazuri yenye

madarasa, viti vya kukalia na kadhalika. Mwanafunzi anayepata elimu chini ya mti ana nafasi kubwa

sana ya kufanya vibaya katika mtihani.

AINA ZA TATHMINI NA UPIMAJI

Kuna aina mbalimbali za tathmini na upimaji zinazoweza kufanywa katika ushairi wa Kiswahili.

Aina hizo za maswali ya kutathmini ufundishaji na kujifunza hujumuisha hizi zifuatazo:

(i) Kuchagua jibu sahihi/sahihi zaidi (multiple choice questions)

(ii) Kweli/Si kweli (True/False questions)

(iii)Kuoanisha (Matching items questions)

(iv)Kujaza nafasi zilizo wazi (Fill in the blanks questions)

(v) Majibu mafupimafupi (Short answers questions)

(vi) Insha (Essay type questions)

10)Kutoa Matokeo ya Tathmini na Utoaji wa Motisha

Baada ya kufanya tathmini, hatua inayofuata ni kutoa matokeo na motisha. Hatua hii ni muhimu

sana lakini walimu na wataalamu wa elimu hawaiwekei mkazo unaostahili. Inapaswa kukumbukwa

kwamba, kama isivyokuwa na maana kupiga kura ya kuchagua viongozi na kutotoa majibu kwa wakati,

ndivyo isivyokuwa na maana kutoa zoezi, kazi ya nyumbani, jaribio, mtihani na kadhalika bila kutoa

matokeo ya upimaji huo (kwa wakati). Wanafunzi wanapofanya zoezi, kazi ya nyumbani, jaribio,

mtihani au aina nyingineyo ya tathmini, hutarajia majibu. Kwa kawaida, wanafunzi (na hata wakati

mwingine wazazi na walezi na jamii kwa ujumla) husubiri kwa shauku kubwa matokeo ya tathmini

iliyofanyika. Mwanafunzi anapofanya mtihani wa taifa, kwa mfano, husubiri kwa hamu majibu hayo ili

(w)ajue ikiwa ataweza kuendelea na ngazi ya elimu inayofuata ama la. Vilevile, tathmini huweza

kumsaidia mwanafunzi, mwalimu, mzazi na jamii kwa ujumla kubaini maendeleo ya elimu kwa mtu

binafsi, shule na hata taifa kwa ujumla. Hivyo, tunaweza kusema kuwa kuna sababu nyingi

zinazosababisha utoaji wa matokeo ya tathmini kuwa muhimu. Miongoni mwa sababu hizo ni:

(a) Kumpa taarifa mwanafunzi juu ya hatua aliyofikia katika kujifunza

(b) Kumweleza mwanafunzi nini anakimudu vema na nini hakimudu vema katika vitu

alivyojifunza

(c)Kuwafahamisha wazazi na walezi maendeleo ya mwanafunzi

(d) Kuweza kuchagua wanafunzi wa kuendelea na ngazi inayofuata ya elimu

(e)Kutoa motisha kwa wanafunzi waliofanya vema na kama ikibidi adhabu/ushauri kwa

waliofanya vibaya.

(f)Kumwezesha mwalimu kujua maeneo ambayo hakuelewa vema wakati wa zoezi la ufundishaji

149

(g) Kuweza kutoa taarifa juu ya kiwango cha elimu kilichofikiwa na shule, wilaya, mkoa hata taifa

kwa ujumla.

(h) Kuweza kuthibitisha usahihi wa maamuzi yaliyofanywa kwa kutumia matokeo hayo. Kwa

mfano, kama mtihani husika ndiyo uliotumiwa kama kigezo cha kuwachagua wanafunzi wa

kuendelea na ngazi nyingine ya elimu au darasa lingine ni vema matokeo ya mitihani hiyo

yakatolewa ili wanafunzi waweze kujua kwa nini walichaguliwa au hawakuchaguliwa.

Kwa kuwa walimu wengi na taasisi zinazohusika na upimaji na tathmini hawaipi hatua hii ya kutoa

matokeo ya tathmini iliyofanyika umuhimu unaostahili, huchukua muda mrefu kwa wanafunzi kupata

matokeo hayo. Wakati mwingine walimu na taasisi zinazohusika na utoaji wa matokeo hutumia muda

mrefu kutoa matokeo hayo na hivyo kuwaweka wanafunzi katika hali ya taharuki kwa muda mrefu. Ni

jambo muhimu sana kusisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kupewa matokeo ya zoezi, kazi ya

nyumbani, jaribio, mtihani au aina nyingineyo yoyote ya upimaji iliyofanyika, mapema kadri

inavyowezekana. Wanafunzi wanapopewa matokeo hayo mapema, kunakuwa na uwezekano wa

kurekebisha makosa yaliyofanywa na mwanafunzi kwani bado mwanafunzi anakuwa anakumbuka

makosa hayo. Matokeo yanapochelewa, mwanafunzi husahau mtihani ulivyokuwa na majibu

anayoyatarajia, kwa hiyo, ni vigumu kuweza kubadilisha tabia ya mwanafunzi. Vilevile, utoaji wa

mapema wa matokeo mapema humwondolea mwanafunzi hofu ambayo huweza kuathiri afya yake.

Aidha, kuna baadhi ya mitihani na tathmini walizopewa wanafunzi hazirudishwi. Kuna baadhi ya

walimu, kwa maksudi kabisa, hawarudishi mitihani ya wanafunzi ingawa kwa mujibu wa taratibu,

walipaswa kuirudisha. Walimu wa aina hii wanadidimiza maendeleo ya elimu kwani wanafunzi

wanakosa fursa ya kutambua makosa yao na kuyarekebisha. Hata hivyo, kuna mitihani ambayo kwa

mujibu wa taratibu, huwa hairudishwi. Mitihani hiyo ni pamoja na mitihani ya kitaifa ya kumaliza

masomo katika ngazi mbalimbali. Ingawa kuna sababu za msingi za kufanya hivyo, tunaona kuwa kuna

haja ya kuwarudishia wanafunzi mitihani hiyo ili waweze kubaini makosa yao. Japokuwa hawawezi

kuyarekebisha makosa hayo katika ngazi husika kwani wanakuwa wameshamaliza masomo, inaweza

kuwasaidia kujirekebisha katika ngazi za mbele kama watabahatika kuendelea na masomo. Aidha,

katika nchi inayozingatia uwazi na ukweli, kurudisha mitihani hiyo linaweza kuwa jambo zuri la

kujenga imani kwa wadau wa elimu na kuwapa fursa ya kutathmini zoezi la usahihishaji lilivyokuwa.

Wasahihishaji, kama binadamu, huweza kufanya makosa. Makosa hayo yanaweza kurekebishwa kwa

wanafunzi kurudishiwa mitihani yao na kuipitia. Tukiri tu hapa kuwa kurudisha mitihani ya namna hiyo

kunaweza kuwa na changamoto na gharama kubwa.

Kwa kawaida, zoezi la kutoa matokeo ya tathmini iliyofanyika huenda sambamba na utoaji wa

motisha kwa waliofanya vizuri au adhabu na ushauri kwa wanafunzi waliofanya vibaya. Mazoezi, kazi

za nyumbani, majaribio, mitihani na aina nyinginezo za tathmini zinazofanywa katika ngazi ya shule au

darasa husika huweza kuwasaidia walimu kutoa motisha kwa wanafunzi waliofanya vizuri. Motisha hii

huweza kuwa zawadi mbalimbali kama vile vitabu, madaftari, kalamu, pesa au zawadi nyinginezo. Hata

kumwandikia mwanafunzi vizuri sana katika daftari la mazoezi ni motisha. Katika ngazi za mitihani ya

kitaifa, motisha hii huweza kuwa kuchaguliwa kwa ajili ya kuingia ngazi nyingine ya elimu au darasa

lingine. Motisha ni muhimu sana katika kukuza ufaulu wa wanafunzi.

11)Upangaji wa Ufundishaji Ujao

Baada ya hatua zote, hatua ya mwisho kabisa katika kutafsiri muhtasari kwenye vitendo ni upangaji

wa ufundishaji ujao. Katika hatua hii mwalimu na shule hufanya tathmini ya zoezi zima la ufundishaji

lilivyokuwa, matokeo ya tathmini yalivyokuwa na sababu za matokeo mazuri au mabaya

yaliyopatikana. Walimu na shule wanapaswa kuyajadili matokeo yaliyotolewa ili kubaini ikiwa kuna

udhaifu wowote. Hilo linaweza pia kuwasaidia kufahamu udhaifu uliobainika umetokana na wanafunzi

wenyewe, mazingira ya kujifunzia, walimu, shule, jamii au sababu nyingineyo. Baada ya sababu

kujulikana, walimu wanapaswa kuandaa mikakati ya kutatua tatizo hilo ili kuhakikisha hali hiyo

haijirudii siku zijazo. Tathmini hii itamsaidia mwalimu kuboresha zana za kufundishia, mbinu za

kufundishia, vitabu na ufundishaji kwa ujumla ili aweze kutoa matokeo bora zaidi katika mwaka

unaofuata. Kwa bahati mbaya sana, kuna shule nyingi ambazo haziweki kipaumbele katika hatua hii.

Shule kama hizo itakuwa vigumu kujinasua kutoka katika ufaulu mdogo waupatao. Shule hazina budi

kukaa na walimu na kuyajadili matokeo na kujua namna ya kufanya. Baada ya hatua hii, mzunguko

150

unaanza tena kwa kurudi katika hatua ya kwanza ya kufanya mapitio ya makusudi ya ufundishaji.

Mapitio ya sasa yatatilia maanani sababu za kufeli na kufaulu zilizobainika kutokana na matokeo ya

tathmini yaliyotolewa.

HITIMISHO KUHUSU HATUA ZA KUTAFSIRI SILABASI KWENYE VITENDO

Hatua hizi ni muhimu sana kwa mwalimu anayetaka kufundisha si tu ushairi wa Kiswahili bali

pia lugha ya Kiswahili kwa ujumla. Hatua hizi hufuatwa pia na walimu wanaofundisha masomo

mengineyo. Hatua hizi zinapaswa kufuatwa na mwalimu anayeanza kufundisha darasa husika kwa mara

ya kwanza. Kwenye baadhi ya shule, mwalimu hupangiwa darasa husika na hulifundisha miaka nenda

miaka rudi. Kwa mfano, mwalimu huweza kupangiwa kufundisha ushairi wa Kiswahili kidato cha nne;

kinachobadilika ni wanafunzi tu wa kidato cha nne ila mwalimu wa ushairi huwa ni yuleyule miaka

yote. Kwa mwalimu wa aina hiyo aliyekwisha kufundisha darasa husika, hatua nyingi huweza kurukwa.

Kwa mwalimu huyo, hakutakuwa na sababu ya kupitia upya makusudi ya kufundisha kwani alishafanya

hivyo mwaka uliopita. Aidha, hatakuwa na sababu ya kuchagua upya vitabu vya kufundishia au

kuandaa mpangokazi wa kufundishia kwani alishafanya mwaka uliopita. Hata hivyo, ni muhimu kwa

mwalimu kujiridhisha ikiwa kweli hakuna haja ya kupitia mojawapo ya hatua hizi hata kama mwalimu

huyo alifundisha somo hilo katika darasa hilohilo mwaka uliopita. Hii ni kwa sababu vitabu vipya

hutungwa kila siku na hivyo kuwa na haja ya kuchagua upya vitabu vya kufundishia ambavyo ni vya

kisasa zaidi na kuachana na baadhi ya vya zamani. Pia, mbinu za ufundishaji hubadilikabadilika

kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa. Mabadiliko haya huweza kuathiri hata muundo wa azimio

la kazi na andalio la somo. Kwa mfano, nchini Tanzania hapo awali, hatua za ufundishaji zilikuwa tatu:

utangulizi wa somo, utoaji wa somo na hitimisho la somo lakini kutokana na tafiti mbalimbali

ikabainika kuwa kuna haja ya kuingiza vipengele vya matumizi na kukazia maarifa na hivyo Serikali

ikaanzisha kile kilichokuja kuitwa muhamo wa ruwaza, yaani kuhama kutoka kwenye muundo wa

zamani wa andalio la somo lenye sehemu tatu hadi muundo mpya wenye sehemu tano.

Vilevile, mapitio haya ni muhimu kwani tathmini iliyofanywa wakati wa hatua ya upangaji wa

ufundishaji ujao inaweza kubainisha kuwa mpangilio wa mada haukuwa mzuri na ndiyo maana

wanafunzi hawakufaulu kwa kiwango kizuri. Aidha, kwa kuwa wanafunzi wanaokuja ni wapya na

wana matamanio tofauti na wale waliopita, mambo mengi huenda yakahitaji kubadilishwa na hivyo

kuwa na haja ya kupitia upya hatua zote hizi.

Jambo la mwisho, ambalo ni muhimu kusema hapa ni kwamba hatua hizi ni muhimu kufuatwa

kwa mwalimu anayeanza na wanafunzi tangu mwanzo wa kuanza darasa husika. Kama mwalimu

anakabidhiwa darasa katikati ya muhula hataweza kupitia hatua hizi. Mwalimu huweza kupewa darasa

katikati ya muhula kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanza kazi kipindi hicho,

mwalimu wa somo kufariki, kuhama au kuacha kazi na sababu nyinginezo. Mwalimu anapokabidhiwa

darasa katikati ya muhula ni imani yetu kuwa mwalimu anayepokelewa alikwisha fuata hatua zote hizo

hapo awali. Hivyo, mwalimu mpokeaji atapaswa kurithi azimio la kazi la mwalimu anayepokelewa.

Anaweza kurithi pia vitabu vilivyokuwa vinatumiwa na mwalimu anayepokelewa kama

vinavyobainishwa kwenye azimio la kazi. Hata hivyo, mwalimu mpya kuanza kufundisha katikati ya

muhula kuna madhara makubwa kwa wanafunzi. Hii inatokana na ukweli kuwa mwalimu husika

hakuhusika kupanga zoezi la ufundishaji na hivyo inakuwa vigumu kufuata mipango ya mtu mwingine,

anaweza akawa hajavisoma vitabu vilivyochaguliwa kutumiwa na mwalimu aliyepokelewa na pia

wanafunzi hupata shida kuzoea mbinu mpya za ufundishaji kutoka kwa mwalimu mpya. Inashauriwa

hapa kuwa, kadri inavyowezekana, walimu wazuiliwe kuliacha darasa katikati ya muhula ili kukwepa

uwezekano wa haja ya kubadilisha mwalimu.

151

SEHEMU YA PILI:

DIWANI YA MEA

152

LIPAKA

Nyauu! Nyauu! Utasikia linalia

Usilijali, usilihangaikie hata likilia

Ni liongo, halifai, huhitaji kulivumilia

Paka yake adabu, kaiweka mkiani

Lipaka hili, lisikupe presha moyoni.

Utu na nidhamu limepungukiwa

Fadhila lifadhili lakini bado litakwibia

Utunze mboga mahala pema likiipata linabwia

Kwa hakika udokozi ndiyo yake tabia

Lipaka mlijue, ni chanzo cha umaskini.

Tazama dharau na masimango yake

Ye’ kuishi ndani awadharau wenzake

Jirani zake mbwa na ng’ombe wakilala nje

Lenyewe lawazomea na kuwaona vibwete

Hili lipaka jamani, liache dharau.

Yote hayamsujudu huyu paka mikasa

Uaminifu, utiifu, wema kwake ni tasa

Ufisadi, wizi, udokozi, kwake layatakasa

Lafuzu zote na sasa laturudisha nyuma kimaisha

Lipaka hili wandugu, haya halioni.

Busara zake ni za kutengeneza

Hazina tija bali ni jeneza

Zinachosha kweli, vema kulipuuza

Panya litakula, samaki litakwibia ukihisi chunguza

Lipaka hili lipige bunduki likafie mbali.

HADITHI

Navuta kiti na meza. Nakaa

Japo hamjanikubalia lakini ntakaa

Hata kwa nguvu ilimradi nimekaa

Kaeni kitako kimakundi na kwa pamoja

Hodi naipiga kila mmoja malangoni pake

Napenda kuileta hadithi hii isiyo ya makeke

Inamhusu yeye, wao na watu wake

Hii ni kwa wote.Waume na wake

Yasikieni mambo haya kwa dhati yote.

Namkumbuka bwana huyu

Kwa zake busara mithili ya mkuyu

Alizozaliwa nazo chini ya mbuyu

Na kupelekea kufahamika kama Kibuyu

Aliipenda sana nchi yake

Ni mzalendo wa kweli

Sikieni sifa za maisha yake

Aliichukia dhambi ya hongo kwa maisha yake

Tangu awali hadi tamati ya uongozi wake

153

Mafisadi kuringa walikoma enzi zake

Walikoma hadi wakaacha makeke

Zavutia sana habari za baba Kibuyu

Zake falsafa, zilivuka ukomo wetu

Aliiona nchi ng’ambo ya mawazo yetu

Kwa kututaka tuwe wazalendo wa taifa letu

Kwa wote waume kwa wake wajifunge mikanda

Tayari kwa vita ya kikamanda.

Taifa kulipigania na kulilinda

Dhidi ya magonjwa, umaskini na ujinga

Ambao ni maadui sugu wa taifa letu changa

Kwa pamoja mapambano walishiriki

Bila hofu wala hamaki

Ilimradi taifa halizimiki

Halifi wala kupotea bila mantiki

Wazawa, wazalendo wakaitikia mikikimikiki

Ya kuwaondoa wasaliti, mafisadi na wazandiki.

Namnukuu alivyosema.“Yatubidi kuukata mbuyu hata kama shetani ni damu na nyama yetu”

Unajua alimaanisha nini?

Alimaanisha hivi fahamu

Sikilizeni kwa zenu timamu

Iwapo ndugu awaye yeye ana hila za kutia sumu

Amani na mustakabali wa taifa si timamu

Hivyo sheria ya nchi ipite katikati ya damu

Iondoe mizizi ya watu hao sumu

Tusikumbatiane sababu sote tuna damu

Taifa likiungua wapi utaitwa binadamu?

Fikara zake ni zaidi za wanadamu.

Ni wajibu wetu kumkumbuka

Shujaa Kibuyu kwa zake hulka

Zilizo amilifu zikachochea kukurika

Taifa likasimama na kuimarika

Uzembe, uongo na ubabe ukatoweka

Tuzienzi jitihada zake si kwa dhihaka.

Yaniuma upepo unapovuma

Taifa liso mhimili sasa limechuchumaa

Maovu yaendeleayo sasa hakika nitasema

Taifa linaumia maumivu yazidi komaa

Wenye dhamana, wasaliti dhamana

Urithi mkuu wa taifa wautia dhahama

Wengi wabakia kurarua ngozi ya mnyama

Wachache wajifungia shingoni nyama

Uchungu huu sasa basi!!

154

MWATULINDA? MWATUUA?

I

Si mnijibu swali hilo…………Alaaaha!

Nawauliza nyie Mabwana Magwanda!

Mnaona aibu kwa vile mnajua uonevu wenu?

Maumivu mwatuachia, familia zetu zaparaganyika

Hivi majuzi mlimpiga hadi kifo rafiki yangu, kosa hatulijui.

II

Haki ya kuishi

Ni haki ya kila kiumbe chenye damu

Kuwa na familia ni msingi wa maendeleo ya kijamii

Furaha ya familia ni uwepo wa ndugu wote ndani yake

Lakini mnavotuua familia hizi mnaziganga vipi na maumivu?

III

Haki yetu kuihoji serikali inapokosea

Haki yetu kuiwajibisha serikali inapobabatiza ukweli

Haki yetu kuandamana kutoa malalamiko yetu kikatiba

Tukifanya hayo mnatujia juu

Na mabomu mazito ya kutishia amani

Tukiomba ushirikiano wenu mnakuwa kizuizi cha hitaji letu

Ngoja niulize, Bwana Magwanda hivi nyie wa akina nani?

IV

Ngoja niwageukie, mna maisha duni kama yetu

Tukipigania ahueni yetu mnatupiga

Mna mishara mibovu twajua

Twakusanya nguvu kuhoji kwa ajili yenu

Mwatusukasuka kwa mabomu na virungu

Mna watoto wenu wanasoma shule hizi za pipijojo

Hawajui kusoma wala kuandika insha, walimu wapo tu

Tukifanya mageuzi ya hali hizo mwatufyatulia mabomu

Hivi nyie ni wa akina nani?

Niambieni nami nijue.

…………TE.

Si haba ila yameshasemwa yote

Hadharani na pengine pote

Wachungaji, maaskofu na mashekhe wote

Si wao tu hata wanasiasa wote

Wamejaribu na watajaribu kote

Kupambana ili kuondoa adha hii kokote

UKIMWI umesambaa pande zote

Hakika ni janga letu sote

Tujihadhari nao na tutapona wote

Hizi ni dalili zake zote

Zitupasazo kuzijua sote

Kuharisha, kutapika kwa mara zote

Kukondeana na kupukutika nywele zote

Baridi kutawala kwa nyakati zote

Si hizo tu nyingine mzitafute

155

Hamu huisha hata ya kumeza mate

Ugonjwa huu si wa nani,ni wetu sote

Utatuua na kututesa sote

Tukiendekeza michezo hatari yote.

Umang’aa na ukahaba upingwe kote

Mahaba nje ya ndoa yatengwe na wote

Heshima na uadilifu uhimizwe kwa wote

Wanandoa, wapenzi heshimianeni pote

Hiyo ndo ngao muishikeni nyote

Vimini na matiti wazi tuzikemee sote

Milegezo na ulevi ni vyanzo vyake vyote

Tukicheka tutateketea sote

Ujane na uyatima vitatawala pote

Si kwa matajiri tu bali kwa watu wote

Masikini na vigogo nao wamo wote

Ni waathirika na tusiaminiane sote

Jiamini wewe kwanza, usimuane yeyote

Tukifanya hayo tutapona siku zote

Lakini yasisahulike na mengine yote

Sindano na mkasi ni hatari zote

Zina ncha kali tukizichangia sote

Ngono zembe iogopwe na watu wote

Na biashara ya uroda itokomezwe kote

Sheria na amri za Mungu tuzikamate zote

Na hizo ndizo hazina za kutuokoa siku zote

Te!Te!TeTe!

Kicheko hiki msikilete

Kimejaa haramu kama ugoro wa mate

Kitatuponza tukikatae sote

Usaliti unapokithiri ni athari kwetu sote

Uzembe, ubadhilifu na uongo ni kansa kwa wote

Wapendeao maendeleo na sio mateteWanasiasa hawa uchwara si budi kuwatema wote

Tuwatemee makohozi wala si mate

Watatuponza na zao zile Disloyalty

Utasikia wakijiita ni watu wa watu wote

Wa matajiri, masikini na wa wengine wote

Lakini cha ajabu hatamu imeenda fungate

Msiba umekuwa mzito kwa makabwela wale wote

Wachangishwa na kukamuliwa kile chao chote

Kidogo wakipatacho kwa mioyo yao yote

Harusi wagharamikia maakuli yao ni mate

Minofu na Michele ya taifa waifungia matete

Ulinzi wauimarisha wazamiaji wasijivute

Kuja kula malipo ya jasho lao lote

Virungu watachezeshewa hadi wakome wote

Shutuma watatupiwa na hukumu iwafuate

Eti kakosa ni kauasi dhidi ya mtawala wa yote

Aaa!Usaliti sasa basi na udhalimu wake wote

156

Miaka mitano nayo ipite

Usaliti wao wapanga eti waufute

Kwa kurudi nyuma na msemate

Wajitetea na kuulaani uchumi kwa yale yote

Eti ndio chanzo cha mambo hayo yote

Kauli zao ni za uoga na zinatishia uhai wa wote

Walowapa dhamana ya miaka mitano wajikitekite

Madarakani wakiwa na dhamira ya awaye yeyote

Sasa tuseme basi juu ya huu umbutete

Na kadhia hii ya nipe nipite

Sasa tunaangalia vipi tumeremete

Tunataka taifa jipya la kwetu sisi sote

La mwalimu kufaidi uchu wa yake mate

La daktari kufanya kazi kwa uledi wake wote

La mkulima kupanda mahindi avune shamba lote

La wanafunzi kusemea jamii msipite

Nje ya ubia wa walalahoi wote

Waliojikota nje ili kuwapa hii mpite

Hili ndilo taifa la ndoto zetu sote

MADHILA YAKO

Magomeni Mwananyamala Tandika nakufuata

Kwa kuikwepa jakala nyumbani nitakukuta

Kabla hata hujalala ili tukaile bata

Asilani naumia na haya madhila yako.

Nakiri nilikusihi, hima ufike nyumbani

Mapema asubuhi ungenikuta uani

Hukuja hata kunisabahi nikavunjika moyoni

Abadani nakusihi jaribu pengine pakufaapo.

Sikia! Sikia mpenzi sikia! Tena sikia

Shida kichwa cha panzi foleni zilinizuia

Sikukusudia habari hizi hata pia kuzinuia

Asilani naumia na haya madhila yako.

Usijitetee hukunijali ulinifanyia hila

Ni heri ungenambia, foleni ipo Mwananyamala?

Ulipita kando ya njia, ukaondoka na vibwambala

Mi nakusibiria, kumbe na mwengine mwagalagala

Asilani nakusihi jaribu pengine pakufaapo.

Umeniacha mimi umempa moyo Kajale

Yeye si kama mimi wasema hana machepele

Mmekula yamini mimi niondoke nikalale

Ulonitendea mimi madhila yako si ya pole

Asilani naumia na haya madhila yako.

Jiheshimu nikuenzi kama wangu wa zamani

Sina tena ncha ya mapenzi kuwa nawe ni msibani

157

Kajale ni wangu mtetezi popote hata vitani

Tafadhari tupe uwazi na huyu wangu mwandani

Asilani nakusihi jaribu pengine pakufaapo.

KWAHERINI

Baba!

Mwanao nakereketwa moyoni

Najua nimevuruga maisha yangu

Lakini uyafanyayo si jema ndani ya taifa

Aibu nimekutia nawe ni rais unapiga kelele

Asubuhi, mchana na usiku

UKIMWI unaua.Jihadhari

Mwanao nimelikwaa gonjwa hilo.

Mi pia ni raia ya nini kunificha ughaibuni?

Kunificha haipaki rangi ukweli huu

Ni aibu kwako na kwa taifa

Lakini usifanye hivyo.

Kifo chaningoja

Kwaheri baba yangu!

Kwaheri mama yangu!

Kwaheri taifa langu!

Kwaheri wanazuoni!

Kwaherini mashekhe na makasisi

Dunia naiacha.

Jamani msiniige mwenzenu

Nilofanya ni tokeo la mimi kuwa kitandani

Mtoko uso pungua na lundo la wasichana

Mapenzi dhaifu bila kinga

Ubabe na dharau zimeniponza

Napandisha kenchi bila mjenzi

Nahara natapika hadi uchu wote

Msijione mkadhani

Gonjwa ni letu sote

La kwenu mbavu za mbwa

La mabosi kizani na vitambi

La kwangu mimi mwana wa Rais

Nawaageni Kwaheri

Tabia isipobadilika hamponi.

Baba najua ntakufa hivi punde

Lakini

Yasikie na ujue mtandao ulivyokuwa

Thabita ni mpenzi wangu

Aliyekuwa kimada wa Mheshimiwa Macheche

Nyuma ya saluni ana kabuzi kake kanafunzi

Usiku Mheshimiwa Macheche hutoka na Zaina

Zaina yasemekana ni kipozeo cha dereva lori

Liendalo nje ya nchi mara mbili

Kwa wiki.

Likifika mpakani dereva ana hawala yake

Ajishughulishaye na kuuza vyakula mpakani

158

Huko ana pedeshee limfanyialo

Mipango ya kuvusha na kuingiza chakula kinyemela

Na baada ya kazi ni dawa. Kazi na dawa

Pedeshee anajishindia gesti naye.

Balaa

Ni kwa Waziri wa Afya na Uhai

Mmiliki wa Kasino nzito jijini

Naye chini ya sakafu habari zaruka

Anakata kiu kwa Zaina.

Mheshimiwa Macheche kuona hayo

Si kagonga hodi kwa mpinzani wake

Kimahaba atoka na Bi Zeituni Masaka

Mke wa Waziri wa Afya na Uhai

Yule mchungaji mseja unamjua

Si naye anamega kwa waziri

Ziara zikianza nyumbani huibukia

Maombezi ndo hoja kumbe

Nyuma anakula asali.

Mtandao ukakua

Hata Dokta Shija alikula kwa Zaina

Siku kadhaa baada ya kumtoa ujauzito

Profesa Kisu si akamvizia Weisiko

Yule binti wa Waziri wa Ujenzi

Miss Chuo Kikuu

Weisiko ni kisu kuliko Profesa Kisu

Nyuma alishadata na pedeshee la mji

Ambaye naye alishafuta jasho kwa Thabita.

Mama!

Nalia siwezi malizia.

Rai yangu baba ni moja

Tangaza hadharani tangu sasa

Nimeukwaa UKIMWI na wote wajue

Usiogope aibu.Aibu ni nguvu ikipita

Usiposema

Orodha hiyo utaificha vipi?

Usiwahukumu bila sheria watakaonong’ona

Mwana wa Rais afariki kwa UKIMWI

Usiwatupe gerezani bali wasifu kwa kuhoji

Gonjwa hili si la wa maskini tu

Si la mapeshee tu

Si la walimu tu

Si la wao tu bali hata mimi

Ni letu sote

Vunja ukimya na sema jambo

Nami ntapumzika kwa amani.

Kwaherini walenga!

Kwaherini wenzangu!

Kwaheri nchi yangu!

159

TANGU ATOKE SAFARI

Mchana homu nimekaa, nikiwa sina hili na lile

Kwa mbali nikasikia simu inaita, furaha ikanijaa kedekede

Mpenzi Nana kuja Daa, kuanzia saa moja mbele

Kan’ita n’ende kumfata, kwa haraka ilioje

Ukweli nilimpenda, hata ninyi muelewe.

Sasa ni mwaka umepita, mpenzi amekuwa mbogo

Nikisema neno pata, ye analeta songombingo

Nakuuliza hivi ni wazimu, mbona hukuwa hivi huko?

Au kuna mme mwenzangu, nieleze ukweli wako

Ukweli nilimpenda, hata ninyi muelewe.

Nahisi nilipenda fuvu, yangu maisha ni udongo

Kuzikwa na sanda langu, wakati mbele ni pigo

Likaushalo damu yangu, nikaja kufa kwa pengo

Kwa hatia ya uchungu, ya kubariki hiki kigongo

Ukweli nilimpenda,hata ninyi muelewe.

Mpenzi umebadilika, tangu utoke safari

Dunia inanicheka, mapenzi yawa lamri

Chini nimeterereka, maumivu yakithiri

Naomi umesimika, kisu bila adhiri

Kiukweli nilikupenda, hata wewe uelewe

Ni heri niwe kapela kuliko huu msumari

Unanigongea bila kuangalia yote mazuri

Nilichimba hata jalala, ili we upate nawe hariri

Nikamkopa hadi Kalala mtaani naitwa taperi

Ukweli nilikupenda, tamaa usaliti vimetawala.

Nenda nenda nakutakia salama mbeleni

Daima nilikupenda weye ukatia kisarani

Umenitenda ukanitenda, sasa nakutupa mgongoni

Nitakiganga kidonda, ili niwe salama salimini

Ukweli nilikupenda, sasa nabwaga manyanga.

MASKINI AFRIKA!!

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio cha ukabila nchini Rwanda

Ya Watutsi na Wahutu mauaji ya Kimbari

Maskini Afrika! Ndugu wakachinjana wao kwa wao.

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu magonjwa ya kutisha Kusini Jangwa la Sahara

UKIMWI, Ebola, Saratani, Maleria na Kifua kikuu

Maskini Afrika! Ni lini tiba zitatosha, magonjwa yasishamiri

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu udini Somalia na Nigeria

Uislamu na Ukristo,vinanyonya amani ya mataifa hayo

Maskini Afrika! Amani yako inadidimizwa kila kukicha.

160

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu maasi ndani ya mataifa

RUF, LRA, M23, Boko Haram na Al-Shabab.

Maskini Afrika! Raia wasio na hatia dhamana yao i’ wapi?

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu ukiukwaji wa demokrasia ya kweli

Ung’ang’anizi wa madaraka na tawala za kimabavu

Maskini Afrika! Mizizi ya udikteta yazidi shamiri.

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu mabadiliko ya sayanasi na teknolojia

Uzinduzi na utengenezaji silaha za kinyuklia

Silaha, Ulaya zizalishwe, yanini Afrika ulingo wa vita?!

Maskini Afrika! Vijana wadogo nao waingizwa vitani.

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu ukiukwaji wa haki za binadamu

Mauji ya Albino, vikongwe na vichanga visivyo na hatia

Maskini Afrika! Imani potofu zachafua taswira ya uzuri wako.

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu majanga ya asili ndani ya mataifa

Mafuriko,baa la njaa na magonjwa ka Ebola.

Maskini Afrika! Wakazi wako walia na kuwa wakimbizi.

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu utitiri wa wakimbizi kila pembe

Mutabila kila mmahali hadi Bonde la Ufa

Maskini Afrika! Sera za uongo majukwaani na ubabe wa wanasiasa pelekeo la ukimbizi.

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu unyonyaji wa rasilimali ya mataifa yetu

Dhahabu, Almasi, Fedha, pembe za ndovu na ardhi ya rutuba

Maskini Afrika! Wazawa wanabakia na kitu gani kujivunia?.

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu sera sirini za uwekezaji

Wazawa wavuurumshwa kupisha uwekezaji, tija hawaioni

Huduma zadorora, malighafi inachotwa, makombo yabakia nchini.

Maskini Afrika! Twajivunia nini kuwa na keki inayoliwa na wageni?

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu uingiliwaji wa kinguvu wa dola za Magharibi

Akina Komesa kimya mwanyamaza,

Uingizaji majeshi hamuhoji,wahanga wananyonywa.

Maskini Afrika! Hujiulizi mbona wao hawakuiti uwaingilie?

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu rushwa, ufisadi na ubadhirifu umeota miguu

Huduma zimepooza hadi chochote kikutoke mfukoni

Wenye nacho wafaidi, wa majalala huzuni tupu maishani

Walalahai uhondo mdomoni, walalahoi miungurumo tumboni

161

Maskini Afrika! Matabaka ya kijamii yazidi kushamiri

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu matumizi ya siasa chafu

Zimetopea chuki, vinyongo, masimango na hongo

Ashindaye si chaguo la wengi

Aliyepaswa kanunuliwa kwa milungula

Wajaleo, waenda leo kutwa kituoni kupiga kura

Huzuni imewaingia kila kukicha

Maskini Afrika! Huruma kwanza kwa mpiga kura wako

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu manyanyaso ya kijinsia

Mikong’oto mizito, mahaba ya nguvu wabinti kuwafanyia

Ukeketaji, maumivu yasoisha mwilini kuwaachia

Msomi wa kike tasa, wa kiume yake ni zalishi

Maskini Afrika! Utu wako umeutundika wapi?

Kilio! Kilio! Kilio barani Afrika!

Kilio chetu utitiri wa magenge na vijiwe vya vijana

Kazi wamekosa, matunda ya elimu yao yaozea jalalani

Bangi wavuta, madawa ya kulevya msimari mtindio’ ubongo

Maskini Afrika! Taifa la kesho linakufa.

KISABENGO

Jogoo hajawika asubuhi

Nyumba ya majirani waibukia

Kwako kumenuna njaa kali

Unaporoja uongo asubuhiasubuhi

Hicho ni kisabengo!

Umeniona na msichana

Koridoni twazungumza

Humjui ni nani na twaongea nini

Unasambaza kwa mwandani wangu

Umefuma koridoni na hawala

Hicho ni kisabengo!

Umekuja kuomba kura yangu

Nakuchagua hutimizi uloniahidi

Unasingizia mtikisiko wa uchumi

Lakini kwako nyumbani na familia yako

Mtikisiko unaouhubiri hakuna!

Hicho ni kisabengo! Adilika.

Unamdharau mama yako

Sababu nawe una matiti

Sababu nawe una sauti nzitonzito

Unamtangaza barabarani kwa mabaya

Hukumbuki alipokutoa

Hicho ni kisabengo! Badilika.

Unawaunganisha watu

162

Mnalenga kuhatarisha amani ya wengi

Mnajua nini thamani ya amani ilivyo

Mnajitia kiburi mnatimiza njama yenu

Usalama unakufa machafuko yanazaliwa

Hicho ni kisabengo! Hatari kinaua.

CHAKUBIMBI

Chakubimbi jamaa mkimuona muogope

Ana meno manne yanauma kotekote

Macho yake tochi mithili ya mtoto wa kenge

Msimualike hata bure kwenye lenu genge

Chakubimbi muone na kumsikia kwa bomba tu.

Muyasemayo yote jueni atayaanzishia kijiwe

Sasa nikumsusia kijiwe hadi akome mwenyewe

Asishiriki hata kukunja nne. Hadi akielewe

Mwaka huu siyo wake tumeijua siriwe

Siri zetu ni zetu na zake akawalishie mwewe

Chakubimbi tumekuzibia hadi ukome kuringa

Kama mkizembea niyasemayo, mtaumia

Sikieni chakubimbi alichonifanyia

Nilimtonya kistaraabu ya kuwa nahamia

Mtaa wa pili toka ule wa Makororo Nehemia

Alaalaa!Si kaanza udaku kusambazia

Mtaani, majirani, mwenye nyumba na kule napohamia

Nyumba nayokaa nikatimuliwa kabla sijajipangia kuhamia

Chakubimbi jamani huna neno moyoni.

Chakubimbi kumbuka urafiki wetu

Haukuchipuka hivihivi bali kwa utatu

Nilikuheshimu na kukujali kama mtu

Wewe si mimi lakini mbona huna utu?

Tabia yako kuniunguzia utambi kwa bosi wetu,

Kazi nimetemwa sasa naishi kwa matumaini tu

Jamani Chakubimbi jua dunia ni mviringo kuna kesho pia.

Hivi majuzi uliyonifanyia nakusamehe bure

Ulinivurugia penzi langu kwa yule wangu wa milele

Ulimpumbaza kwa uongo na chako kijino pembe

Ulimtongoza ukanikandia eti mie nashika pembe

Njiwa wangu ukamrusha na kuniacha mi pekee

Chakumbi nakujua una meno manne unauma kotekote!

MCHEZO WA MANENO

Ni mchezo mzuri kwa vijana na wazee

Namaanisha kwa mtu wa asili-damu pekee

Mchezo huu ni wangu utoto kama kinda pekee

Basi natuuimbe na kucheza wote

Katika maisha haya

Mganga wa jadi anaitwa Kalumanzila

163

La………..Lala salama

Ma……….Mama mzazi

Zi…………Zizi la ng’ombe

Mbe……...Mbele ya nyumba

Mba………Mbali na wewe

We……….Wembe wa kucha

Cha……….Chakula kitamu

Mu…………Mungu mkubwa

Bwa……….Bwawa la samaki

Ki………….Kingi Majuto

To…………Tone la maji

Ji……………Jitu la kale

Le…………Lenye mandevu

Vu…………Vumbua dhahabu

Bu…………Bubu hasemi

Mi…………Mimi mdogo

Go…………Gogo la Mti

Ti………….Tina na Mjuba

Ba………….Baba mkali

Li……….....Taa ya umeme

Me…………Meli imezama

Ma………...Maji mabaya

Ya…………Yai la kuku

Ku…………Kuku mweusi

Si………….Simu inalia

A………….Alimwiba bata

Ta………..Tanzania nchi yangu

Ngu………Ngumi ya Onyango

Ngo……...Ngome ya Yesu

Su………Sungura Mjanja

Nja……..Njaa inauma

Ma……..Mama mzazi

Zi……….Zizi la ng’ombe

Mbe……Mbele ya nyumba

Mba…… Mbali na wewe

We………Wembe wa kucha

Cha……..Chakula kitamu

Mu………Mungu mkubwa

Bwa……..Bwawa la samaki

Ki……….Kiswahili lugha yangu

Najitukuza kujifunza hazina ya lugha hii

Mchezo huu hushitua akili na hata bidii

Kufikiria kwa undani si hayo hata kutalii

Kunako fikra na zile zinazoitwa mvii

Nawasihi watoto rudisheni nyumbani mchezo huu

BARUA JUKWAANI

Pazia nalifungua, jukwaani najivinjali

Kwa manjonjo, madaha na hata sabili

Kuziturufu na hata kuzisoma barua zenu amali

Zichocheazo lakini zichomazo moyo na akili

Basi nami ntazisasambua jukwaani nikitalii

164

Yako barua ni wewe Mashauri Mashishanga

Wa sanduku la barua 111 Mjini Shinyanga

Unasema unataka kupasua jipu hata kwa upanga

Ili ubakie huru na ahueni ije Mjini Shinyanga

Gadhabu yako ni juu ya tabia chafu iliyojivika Shinyanga

Wanaume kupotoka na kufanya ushoga

Kuoa na kuoana wao kwa wao bila uoga

Mji kuuchafua hata aibu kwa wahenga na vitoto vichanga

Japo ni makinda lakini waweza ng’amua huu ujinga

Inakera na kuchukiza nafsi bila kupinga

Unazidi kuhoji juu ya uhalali wa Mji wa Shinyanga

Kuvaa miwani myeusi wakati mji unadokolewa na Kipanga

Unahitimisha kwa kuomba upenyo wa kuvaa gwanda

La ujasiri na uamuzi mgumu ili kuwatilia ngumu na inda

Tabia hii kuimaliza na kuirudisha pahala pake Shinyanga

Kusema hayo nami na kushusha kwa madaha yote

Jukwaani ili ukapumzike na kuujenga upya mjini wenu wote

Nakushukuru kwa barua yako il’ojaa busara potepote

Ni wewe Salome Tainyo wa Temeke, Daresalaama

Sanduku lako la barua ni 099 Daresalaama

Waomba kukwea taratibu vidato ili upande salama

Jukwaani na kuanza kurusha zako hasira na lawama

Juu ya viongozi, wasimamizi na wakazi wa jiji la Daresalaama

Kwa kuzembea na hata kudharua usafi wa jiji la Daresalaama

Unahoji kwa tashtiti iwapo maana halisi ya “Darisalaama

Ni mji wa bandari salama?”

Kama ni hivyo mbona ni aibu na chukizo kwa usalama

Wa raia, wageni na hata wawekazaji wa Daresalaama

Niseme, huenda natoa tu lawama zisizo na mashiko

Lakini zungukia mitaa yote muone vituko

Huko Kariakoo, Tandika, Magomeni, Boko na hata Keko

Kunatisha mithili ya msuguano ulojaa sokomoko

Uchafu, uharibufu na hata magonjwa yamejaa huko

Daresalaama si pepo salama tena ila ni jehanamu ya Kiko

Inacheza mchezo wa uongo na wavutaji wa hiyo Kiko

Wakazi wamefutiwa hisa ya afya njema isiyo na masumbuko

Wanaishi kwa“Angalau ya leo ipite, kesho itakuaje huko?”

Unahitimisha kwa kuzihoji mamlaka husika

“Je wamesau kitu wanachotakiwa kufanya ili kufikika

Kwa maendeleo ya afya ya watu na hata kuimarika

Kwa Mji wa Darisalaama?”

Kusema hayo unaomba nikushushe jukwaani kwa makeke

Nami bila ajizi nakusindikiza hadi chini kwa upweke

Kuifunga barua yako ndo mwanzo wa kufungua nyenzake

Kilio chako kitasikilizwa kote Ilala, kinondoni na pia Temeke

Afya, mazingira safi na uadilifu ni lazima kwa wakazi wake

Viongozi, watendaji na wasimamizi ndivyo inapaswa kieleweke

Barua jukwaani inazidi pasua anga na sasa ni wanawake

We’ hutaji jina na wapi ulipo

Lakini wanivuta shati kwa upepo

165

Unashusha ghadhabu yako kwa mila iliyopo

Hususani barani Afrika huko uishipo

Unasema tabia ya koo kuvunja utu wa mwanamke

Ni unyanyasaji na dhuluma kwa mwanamke

Unahoji mke akiolewa, anaolewa na mume na ndugu zake?

Kwanini mume akifa ndugu purukushani kwa mke wake

Ung’ang’anizi wa mali na hata mke wake

Mwataka kumrithi kikao kikali kumuwekea

Watoto hamkumbuki, mali, mke tu mwaongelea

Unazidi kurusha dongo lako kama tsunami

Unauliza huo ni utu au ufisadi hata wa ndimi

Kaka atafute, afapo chake chenu

Kaka afanye kazi uroho wa mali kwenu

Una hitimisha kwa kusema

Mila hizo zifungwe kwenye dema

Wenye tabia’zo wapelekwe pasipo pema.

Nafunga barua yako nakushusha kwa heshima.

DUNIA KAMBI

Ni kambi ya mkusanyiko wa kila aina

Imekusanya takataka na maua ya kila aina

Tunakaa humo sote kama wakimbizi

Twazikimbia shida lakini kambini napo zipo

Hakika dunia kambi vaa gwanda tayari.

Kambi ya dunia imekusanya wengi

Tunaishi nao ndani ya kambi

Wezi wa mifugo kijijini

Wafitini, wavunja nyumba za watu

Waongo ukweli kwao ni sumu

Wasaliti madhara hawayajui

Dunia kambi vaa shika bunduki mkononi.

Ndani ya kambi kuna mengi

Kuchomeana utambi kazi wafukuzwa

Kusalitiana ndoa inavunjika

Kuasiana taifa linayumba

Kuoneana wasio na hatia waumia

Kunyonyana ukoloni mpya wa Kiafrika

Dunia kambi vaa gwanda tayari.

Hadi sasa kambi ya dunia

Haina kamanda anayetulinda

Kama yupo basi ni dhaifu mithili ya uyoga

Ugomvi unatawala kati yetu hatuongei

Chuki twachukiana hakemei

Uasi twaasiana aunga mkono

Kambi hii ya dunia

Kaa chonjo!

Fumbua macho usijiliwe kekundu!

NG’OMBE MMEMMALIZA

Huruma mmeipeleka likizo nyie wazandiki

166

Mbona mshipa wa aibu mmeuziba kwa matope

Tuliwaamini lakini mmeimeza kwa tindikali imani yetu

Ng’ombe wetu alikuwa mnene na mwenye afya tele

Yako wapi maziwa na nyama zake?

Mmemmaliza halafu mwatuletea makombo!

Hamfai hata bure.

Kila aliyemtegemea ng’ombe huyu sasa analia

Ng’ombe amekamuliwa bila huruma

Usaha wa maumivu yasiyoisha yazidi kumtoka

Yamtoka na kumuachia vidonda visivyopona

Sasa watoto wamegeuka kumlamba vidonda ili apone

Wanawake wamegeuka kuwa waganga wa jadi

Wanalia usiku kucha dawa haipatikani, ngombe anaumia

Kwa hali hii hamfai tena kumfuga ng’ombe wetu

Hivi ndivyo mlivyokuja mkihubiri jukwaani.

Kwa sauti ya ushawishi kisiasa, mkapaza mkisema

“Niaminini mimi kwa mioyo yenu, ng’ombe huyu nitamchunga vizuri na kumfanya anawiri tele. Nyote

mtafaidika kwa maziwa, nyama, na ngozi kupitia kwa watoto wake”

Lakini haijawa hivyo.

Ng’ombe hajazaa sasa yasemekana ni tasa

Ng’ombe hatoi maziwa sasa anatoa usaha wa uongo wenu

Ng’ombe amekonda sasa anaishi kwa matumaini

Ng’ombe amevunjika mguu zizini hatoki tena anasubiri kufa

Ng’ombe ni hazina na rasimali yetu na fanaka kwa wanetu

Lakini sasa ni mwiba na moto moyoni mwetu

Ng’ombe tuliyewapa mmemmaliza pyeee!

Ng’ombe mali ya wazawa wote

Ng’ombe ni rasilimali ya awaye yeyote

NYATHIWA WOUG DALA

(Mwanetu Ondoka Nyumbani)

Okumu mwanetu sasa umekuwa kijana

Umri umekuwa na akili zako zimebeba utimamu sasa

Umejua jema na baya, we si kinda tena

Mimi baba yako na mama yako tuna neno kwako

Lipokee, lifanyie kazi, litakuwa hazina yako maishani.

Tumetafakari kwa kina utukufu wa maisha yako,

Ujenzi wa maisha yako ya sasa na ya baadaye,

Uhalali wa maendeleo yako na neema yako

Hazitoki nyuma ya viganja vyetu bali nje ya dunia yako

Nje ya nyumba ya baba na mama yako.

Kumbuka maandiko na vitabu vitakatifu,

Vya manabii na mitume walivyoandikiwa wanadamu,

Ondoka katika nyumba ya baba yako na uende katika nchi nitakayokuambia……

Kulijua hilo nasi wazazi wako tunakueleza sasa

Umekuwa, nenda ukajijenge uwe baba wa kaya yako

Tena dunia siyo pepo ya amani bali ni jalala la tabu

167

Wanadamu si watu ila usijitenge nao wakujiapo

Tafuta amani ya moyo kwani huko duniani ni kwenu sasa

Washukuru wakusadiao, waombee kwa Mola wakuchukiao

Mwanetu ondoka nyumbani, umekuwa mkubwa sasa

Mimi baba yako sikuwa hivi bila kujituma

Fanya kazi, usidharau kikupacho mkate wako kila siku

Jitenge na magenge hayana tija ni shimo la umaskini

Nilipoyajua hayo nikayamezea moyoni

Sikuwahi kumtemea mtu zaidi yako wewe mwanetu

Nawe yameze hata kama ladha imechujwa kwa teknolojia

Mwanetu kumbuka hili daima

Maisha ni leo tu kesho usiingoje

Ukiisubiri ije mwana hatokua wako tena

Nyumbani usiogope rudi utakapo

Nasi ni lulu yako na wanao ukiwaleta

Mikononi tuwashike mapajani tuwapakate

Mwanetu ondoka nyumbani, umekuwa mkubwa sana.

NAENDA KUITAFUTA

Baba,mama na Mjomba wote nawaiteni jamvini

Msimsahau shangazi,kaka na binamu nao waiteni

Fikeni kwa pamoja jamvini bila kinyongo rohoni

Mwanenu na neno ndani kabisa moyoni

Nataka kuwaageni

Naenda zangu safarini

Mbali kabisa kuitafuta Nyota ile ya Amani

Iloshushwa toka angani na kuzikwa ardhini

Huko nendako mwanenu ni ugenini

Iwe mashariki,magharibi,kusini au kaskazini

Sina ndugu yeyote huko duniani kama nyumbani

Japo ni safari yenye dhoruba,niendapo ntafika kwa imani

Nikifika nitahoji na kujua kulikoni nyota ile ya Amani

Ipotee angani na kuruhusu giza totoro duniani?!

Ni nani haswa aliyeizima nyote ile ya Amani?!

Naam! Ni asubuhi na mapema nipo njiani

Naenda safari ya mbali huko kunakoitwa duniani

Nguvu yangu i moyoni,mlinzi wangu ni yangu imani

Njiani nang’amua wasaliti waliyoishusha nyota angani

Ni dharau ninayemkuta ameketi katikati porini

Amezingirwa na maswahiba wake chuki,uongo na mfitini

Uoga waniteka nyara na kunipokonya ile imani

Najikuta ni mbabe na mwenye kujaa kisirani kichwani

Sikumbuki nilipotoka na safari yangu ni ya ugenini.

Kisirani na ubabe vinanifanya niidondoshe imani

Uongo,usaliti,dharau na majivuno ni adui wa amani

Narithishwa mikoba hiyo katikati safarini

Hata niendako sijapaona nimepokonywa imani

Hazina na mlinzi wangu waliyonipa wazazi nyumbani

168

Imepotea sijijui asilani

Wolololoo! Nakuwa mtumwa njiani wa kuiua imani duniani

Mizimu ya nyumbani mko wapi? Muje munioke utumwani?

Usiku wa siku ya thelathini na dakika ya sitini

Tangu ilipotimia saa sita kamili hapo porini

Najihisi ni mwepesi mithili ya hereni sikioni

Minyororo ya utumwa imenitoka mikononi

Akilini nawa timamu nagundua nimepoteza imani

Mizimu toka nyumbani imenifungua na kunihoji kulikoni

Nashindwa kujitetea.Najikuta natetemeka sana mapajani

Acha usoni,mikononi na hata pia mwilini

Nilikuwa natetemeka hoi bin taabani

Najikusanya upya toka ardhini

Tayari nimeshapoteza ngao yangu ya imani

Ya kunilinda muda wote niwapo safarini

Navuta pumzi nzito yenye muwasho mkali ndani

Naanza safari kulekea mbele zaidi huko duniani

Mizimu inaniacha na kupotelea angani

Najipa moyo nikiamini wapo nami abadani

Hawataniteleza japo nimekosea nikamezwa tena asilani

Nalivuka pori salama bila kadhia njiani

Nafika salama nchi ya watu wa chini

Natangatanga mtaani kutafuta eneo nikajipumzishe chini

Mitaa imechanganyana kila mtu anawaza lake kichwani

Lugha ya mtaani ni kali na inachusha sana moyoni

Matusi,masimango na vijino pembe ni asili ya lugha ya mitaani

Ikichanganyia sana jamii yote hii mashakani

Nalijua hilo na siku zote napita zangu pembeni

Nani atanijua nikijitetea nipo safarini?

Nuru ikiwa haijajizika chini tena ardhini

Pembezoni kabisa mwa nchi hii ya watu wa chini

Katikati ya mji wa Kingelemkeni

Sauti kali mithili ya vurumai inanijia masikioni

Natulia na kutega mlango wa fahamu kwa makini

Kuitambua vema asili ya sauti hiyo Kingelemkeni

Natambua kuwa imejaa ishara kama kitu kimatatani

Naondoka naenda kujionea mwenyewe kulikoni?

Asalale! Macho yangu nchi hii ya ugenini

Watu wamelazwa wakiwa nyang’anyang’a ndivyo natabaini

Wamepewa mkong’oto takatifu-Ondoa mtu duniani

Yasemekana ni majizi tishio Kingelemkeni

Wanakingelemkeni wadai eti tamaa zimewaponza asilani

Navutika kutega matundu yangu ya sikio kwa makini

Kusikiliza madai yao yenye ukali ya kusimumua mwilini

Wazidi kupayuka zaidi bila kusita mioyoni

Walitaka kupokonya akina mama hawa sokoni

Fedha zao,hereni zao na cheni zao shingoni zenye madini

Siyo mara ya kwanza ni wazoefu sana hapa sokoni

169

Wamekubuhu kuliko hata bidhaa za hapa sokoni

Huja na kupokonya tukawajua leo tumewatia mtegoni

Akafunga hotuba yake mzungumzaji huyu makini.

Moyoni nikatamani wasulubiwa wapewe hata ncha ya ahueni

Waitumie kujitetea huenda wanahoja makini

Si mbuzi hawa kana kwamba hawana akili kichwani

Wanayo na wanajua kimbembe cha kutiwa mashakani

Ikigundulika ni kung’atwa na kuondolewa duniani

Huruma chini ya kiatu wanadamu wamevaa miwani

Wanaikanyaga bila kujali,hawaoni kitafuata nini

Jamani hatupendi kuwa hivi ila ni Kingelemkeni

Imetuzaa na kutufanya tuwe na hivi hapa mjini

Tumejitahidi kufanya kazi ila tumetiwa vikwazoni

Tumefanya kazi hali kujipatia kipato mfukoni

Tumeuza mitumba na kuwa machinga hapa mjini

Lakini Kingelemkeni na serikali yake imetuweka vizuizini

Haturuhusiwi kufanya kazi zetu hadi tuhamie eti zizini

Huko ndiko halali kufanyia biashara hadi kileleni

Tumekaa huko wiki inayeyuka hakuna kitu mfukoni

Nami niwaulizeni nani kati yenu anayeenda zizini?

Hamuendi huko kumekufa mithili ya maiti makaburini

Yazikwa kisha waombolezaji watawanyika kurudi nyumbani

Kama ndiyo hivyo tumekosa nini?

Nikashusha pumzi taratibu mithili ya gari mteremkoni

Amejitetea vizuri japo sijui ukweli wa Kingelemkeni

Nikaamini

Kama mimi nawaza jambo akilini

Basi wananchi-vinyongo watakuwa wanawaza makini

Lakini haikuwa hivyo.Nikasikia akisema“wamwagieni mwilini

Astakafili petroli mwilini”

Kiberiti kikawashwa na kudondoshwa chini

Watuhumiwa wao wakaanza teketea chini kwa chini

Moyo ulijikunja kwa huruma nikakumbuka nyumbani

Ya kuwaita mizimu ya ukombozi waje hapa ugenini

Kuwasaidia vijana hawa wanaoteketea ardhini.

Nikajiondokea huku nikimlaumu aliyeishusha nyota ya amani

Yuko wapi Jamani niambieni.

Nikaondoka polepole uchungu ukiwa moyoni

Furaha ikiwa imejizika chini kabisa ardhini

Nikaenda kutafuta nyumba ya kujiegesha wageni

Wawe wasafiri au hata ndugu wa mtaa wa jirani

Huko nikashusha pumzi hofu nikaitia mfukoni

Nikawa mpya kuliko nilivyoingia Kingelemkeni

Namuomba Rabana anijalie bwerere usingizini

Ni saa kumi na moja jogoo aniwikia dirishani

Navuta shuka naamini nimemkwepa asalini

Hiyo haisaidii kwani sauti yake inanizidi usingizini

Kuona hivyo nakoma,naamka nawaza jambo akilini

170

Ni wapi ntafika,nani nimuulize anijibu swali kwa amani

Ni nani aliyeishusha nyota ile ya Amani?

Swali hili nitajibiwa lini?

Kelele inanijia nahisi ni sauti ya wageni

Kusikiliza kwa makini nang’amua ni vurumai chumbani

Sintofahamu inaninyonga ujasiri wangu unapita pembeni

Nafikiria kimapana natafakari akilini

Ni waungwana gani hao,hakujakucha wana yao chumbani

Nifikiriavyo kumbe napotoka wenye mali washikana ugoni

Mume kamsaliti mke bila kujua athari yake ni nini.

Mke naye kamsaliti mume bila kujua balaa lake ni nini

Sasa siwamefumaniana vitaulo viunoni,aibu machoni

Daaa! Duniani jamaa,kuna mengi mengine nyamazeni

Wiki tatu zinayumba nikiwa Kingelemkeni

Kazi niliyoifata kufanya nimeimaliza mimi maskini

Navunja kibubu,basini nakwea narudi nyumbani

Wazazi na ndugu zangu simameni pale barabarani

Mwanenu nimejua nani aliyeishusha nyota ya amani

Kusanyeni kuni baridi ikizidi washeni moto muoteni

Hapo tuchome mahindi,punje tuzirushe mdomoni

Majibu ya kazi yangu nitayatoa kwenye shairi B mbeleni

Tumuombe Mola atutie nguvu zaidi mwilini

Tuonane hapo bila ya vinyongo moyoni.

MAJI YA KIFO

Maji ya kifo hayafai kuoga

Yananyofoa uhai wa mtu

Yanaunguza amani ya mwilini

Yaepuke usiyaoge.

Maji ya kifo

Hayafugi samaki

Yananuka uvundo wa mauti

Yakwepe

Usiyatumie hata kunywa!

Maji ya kifo

Yagadhabisha sana

Yaunguza maua ukiyanyunyiza

Ndege hawayanywi kiu wakiona

Yanatisha!

Yanaogopesha!

Usiyazoee!

Maji ya kifo

Yachemshwe yapoe yachujwe

Hayafai kwa kunywa

Yanavimelea hatarishi

Kioo kikizidi

Vumilia hadi mwisho

Yakwepe kama ukoma.

171

ULIMI

Ulimi nyama laini,sumu iuayo sana

Wengi wako hatarini,amaniyo yagongana

Hofu i tele moyoni,dunia yasalitiana

Ulimi kitu kidogo,chaangusha hata dunia.

Machafuko mitaani,vijana watadundana

Neno lotoka mdomoni,gonjwa linaoteana

Lakomaa hadi ndani,visasi vyazaliana

Ulimi kitu kidogo,chaangusha hata dunia.

Ulimi hata chumbani,wazazi hutifuana

Maneno ya mitaani,yaingiapo chembana

Heshima ’dondoka chini,kwenye ndoa hutengana

Ulimi kitu kidogo,chaangusha hata dunia.

Ulimi nyama laini,laua hata dubwana

Giza tete maishani,amani kama dafina

Imejizika ardhini,magomvi ni yake mnuna

Ulimi ni sumu kali,inayoua taratibu

TUKAOGELEE!

Tukaogelee!

Wapi?! Ndani ya tope zito

Lenye kunatisha nyama ya machungu yetu

Tusivue nguo tukiogelea!

Tuogelee macho wazi mbwa mwitu asijeiba

Tumaini tulolivua kando ya mto

Tukaogelee!

Tukaogelee ndani ya wimbi zito la tafakuri

Lirutubishacho mpito wa kinadharia

Zo dumu zenye utasa ulokubuhu

Manyang’au yatakwama ng’amnoni

Kinani tikielea.

Tukaogelee!

Tukaogelee!

Tukipiga mbizi juu ya ya nyayo ndefu

Katikati ya kina chenye wimbi zito

Pumzi zikichoka

Giza tete la msisitizo bainifu

Litatushukia mbele tukiibuka!

Hekima,busara ni kina cha uvumilivu

Tukishaogelea.

Tukishaogelea!

Tutakuwa?!

Tumeshinda dhoruba ya maisha

Tumechoka tunarudi salama.

AKILAMBA SABUNI

Mate yashamiri ugwadu

172

Radha hufifia mdomoni

Ulimi huteleza pasipo kikomo.

Mbuzi akilamba sabuni!

Utamu huchokocha

Koromeo hukereketa koo hutii

Udenda mzito uso mwisho

Humvuja bila yake hiari.

Kuna wakati nao upo

Binadamu akailamba sabuni.

UMOJA WETU

Kong’ai! Kong’ai!

Ndo yetu dira itupayo nguvu

Isikikapo dunia yatambua moja

Wakuu wa anga hao wakatiza

Furaha yetu safarini kughani

Kong’ai! Kong’ai!

Dhoruba angani nzito ipe moyo

Si wote twafika kwa wakati pangwa

Vunjika mbawa,kosa nguvu ni vikumbo

Hufiki bila kuvikabili na dhati yote.

Akumbwapo mwenzetu si twasonga

Kudra zetu kuziweka kwa kundi la pili lijapo

Nalo hufika kumchota na kumsindikiza nyumbani

Furaha yetu moja

Kughani umoja wetu

Kong’ai! Kong’ai!

Makazi yetu makutini

Minazini kujistiri na baridi kali

Wanana kuwalea na kuwaepushia mbali na dhahama

Tishio mtikisiko wa kimaslahi na ndege wachafu

Bundi na watoao miziki dhalimu

Songombingo!

Minazi kuhimili mikikiki

Maslahi yetu kujilindia

Dira yetu ni moja

Kong’ai! Kong’ai!

WEGESA MNYAMONGO

(Wege/Penina)

Nakueleza kinagaubaga Wegesa Mnyamongo

Kwa beti hili moyoni nakuimbia.Elewa!

Nilidadisapo kutano letu Tarime

Nakiri wazi hata penye mvua pana uwazi

Sitolisahau bali nitalihifadhi kwa pendo kuu

Naamini ni wewe hakika nilofunuliwa na Manani

Nashukuru!

Ni wewe uliye sura ya wanangu

Ukanizalia!

Ni wewe uliye damu na nyama ya wanangu

Ukanilelea!

173

Ni wewe uliye pumziko langu moyoni

Nimetulia!

Kwa hilo nakutabaruku maneno haya

Mapenzi ni mchuzi ulopikwa ukapika

Viungo linganifu ladha yetu tusipoteze.

Nasi tuupike mchuzi wetu juu ya figa letu

Kani ya upepo ni majaribu ya dunia

Mchuzi wetu tukikosa kuunga vyema

Ladha yake ikawa shubiri mioyoni mwetu!

Kumbuka hata wale mbwa mwitu walotupania

Wakakuta kiambaza kikubwa penzi letu ni fupa

La mzimu fisi alisalimu amri na iweje wao?

Nakusihi tusukumize sayari yetu mbele

Lifike salama jalali tunaomba

Hata katika misukosuko ya dhoruba

Agano letu litimie ndoa tuifunge

Na familia yetu isimame kwa jina letu

Nikupendaye ni mimi wengine mafamba.

Moyoni watakutoboa mibani wakikupitisha

Nakuomba yasikie niyasemayo!

Wewe sabuni yangu ya roho!

Penina Mnyamongo!

PANYA AKIMNG’ATA CHUI

Panya akimng’ata chui kilio husikika

Makucha huyatoa kwa sauti huunguruma

Hasira hubeba kisasi hulipiza

Panya na chui si wajamii moja

Urafiki wao ni wa mashaka sana

Chui hujiweka kimbele kama mtawala

Hulinda na kuvizia vitoweo vipitavyo jiraniye

Hajali ujuzi gani atumie kudaka kitoweo hicho

Kukwaruza,kung’ata au hata kunyonya damu

Ubongo wake unajali kitoweo tu na si kingine

Ujane,uyatima na upweke huwatia wenzake

Panya na chui hakika si wa jamii moja

Chui hakumbuki utu na haki za wenzake

Kuwalinda wake na kuwapa ulinzi ndo yake tija

Panya akithubutu kumng’ata kilio utakisikia

Pori litakuwa jehenamu,upende usipende.

Chui akigundua kekiye ipo rehani kuliwa

Huja juu na kumtishia panya

Chuki huionesha ulinzi huimarisha

Kimya hukaa upepo ausome

Hasira zikimzidi pori hulichafua

Panya wote mashakani huishia.

Panya wakikosa umoja wamekufa tayari

Chui hukaa kando kushuhudia vurumai mpya

Paka na panya hii ni vita mpya darini

174

Msako huwa endelevu,chui azidi chekelea

Pori likichafuka mtini hujipandia

Panya akipata mwanya

Humng’ata kwa hasira mkiani

Kilio cha chui utakisikia

Kweli chui na panya si wa jamii moja.

KUNGUNI

Hebu niache ewe kunguni

Usafi nimefanya bado hutaki

Nguo nimefua lakini hutoki

Rangi ukutani nimepaka bado unaning’inia

Kunguni we ni wa aina gani?

Kunguni unaninyonya damu,nakonda!

Unaniaziili hata mbele ya watu

Naonekana mchafu

Tabia gani ulonayo?

Kunguni tafadhali!

Kunguni nakiri nilikukaribisha kwangu

Uishi nami nawe ni kiumbe

Umesahau fadhili zangu

Umekula vyote sasa hadi damu yangu unataka

Kunguni we ni wa aina gani?

Kunguni muda utafika

Kikomo kitashika hatamu

Dawa nitakunyunyizia kwangu unitoke

Niishi kwa amani kama mwanadamu

Kunguni siku itafika!

HATA KAMA!

Hata kama jua litakoma kuangaza leo mchana

Sitagota kuisubiria miale ya penzi lako

Iniangaziayo na kunipa sababu ya furaha moyoni

Hata kama baridi itausukasuka mwili wangu

Sitokufa kwa ganzi maana sauti yako ni koti langu la baridi

Sitoyumba moyo wala kutetemeka meno

Hata kama mawimbi ya bahari yatakoma kuimba

Sitoacha kuwashinikiza ndege na wadudu waimbe badala

Miti na upepo nazo zitaughani wimbo huu wa “Nakupenda”

Hata kama penzi lako litakuwa mwiba kwangu

Nitajifanya siyasikii maumivu yake ili nifike

Nitaliona kama ua zuri la kunidekia machungu hayo

Hata kama mwili wako si blanketi yangu ya baridi

Sitonunua shuka zito kuutelekeza uwepo wako

Nitajikunja hata ngumi kujilinda na baridi kali

Hata kama nikifa kwa kupenda kwa dhati

Pepo haitonifariji kama sauti yako ifanyavyo

Kuzimu haitonitisha kwani sauti yako ni ngao yangu.

Hata kama mvua itaijaza dunia kwa mafuriko

175

Nitajipa moyo kupiga mbizi maana we ni boya langu

Nitaiokoa dunia ili ijue navyokupenda kwa niaba yake

Hata kama kitanda kitanisaliti usiku nikilaliapo

Sitowaza tena,hata chini nitajilaza ukiwa pembeni yangu

Sakafu itanibariki kwa ubaridi mwepesi wa mahaba yako

Tena nawaambia hivi hata kama! Hata kama! Hata kama!

Maswahibu hayataisha,sitakufa moyo

Visa vitazidi,Akech nitavisherehekea

Na hiyo ndiyo fanaka ya pendo langu kwake

Hata kama majangiri yataniwinda usiku kucha

Mwili wangu nautoa rehani kwako

Roho ipumzike kwako

Moyo wangu upoe ndani ya pendo lako

Hata kama! Usipolilea abadani penzi langu!

Nitakupenda!

Ksii!! Ksii!!

Nakupa ujauzito

Twanyofoa mimba

Kiumbe twakinyima uhai

Asubuhi naranda mtaani

Kwa mbali mtu aita simjui

Ksii! Ksii! Ksii

Nageuka nyuma simuoni

Kushoto kulia simuoni

Ksii! Ksii! Aita tena

Natambua ni mwanangu nilemwangamiza

Anililia kwa uchungu!

Namtengeneza mwalimu

Namuajiri vijijini

Maji,umeme hakuna

Nami nalitambua napuuza

Anilalamikia napuuza

Nakunywa chai mjini nasikia

Ksii! Ksiii! Ksiii! Nasimama

Natizama kila kona.Hakuna mtu

Ksii! Ksii! Aita kwa ghamu

Nabaini kwa kina ni mwalimu nilemsaliti

Nakuja kwa wananchi

Naomba kura kwa ghamu nyingi

Naahidi maisha bora

Mwanichagua nashinda

Napuuza jukumu langu kwenu

Nasinzia bungeni.Nasikia

Ksii! Ksii! Nashtuka

Nang’amua ni kilio cha wapiga kura yangu

Wanililia kwa usaliti wangu!

MTAKOSA KUTHAMINIANA

Tabia mliyoanza nasema siyo njema

Kutupiana vijembe mitaani siyo njema

176

Kuchomeana utambi kwa marafiki si njema

Ikikithiri tabia hii

Itatunga mimba ya mauti

Mkizidi kulea hiyo mimba

Mtakosa kuthaminiana

Kamchezo kanakojitokeza si kazuri

Kamchezo ka kujivinjari na wanenu kimahaba

Kamchezo kachohatarisha hadhi zenu

Kaacheni kabla hata jua halijazima

Mkikaendeleza

Mtakosa kuthaminiana!

Mnapotupiana ngumi nanyi mu ndugu haifai

Mnapoingiza ukabila kwenye hakuna mnakosea

Mnapopandikiza udini kwenye hakuna ni dhahama

Tufani likizidi hasara hujitokeza

Mkikomalia hayo

Mtakosa kuthaminiana!

Mnapanga nyumba moja ninyi ni majirani

Shida ya mmoja iwe yenu nyote

Lakini mnapopikiana chokochoko,hafai!

Mnapotupiana tuhuma za kuchafua ujirani,haifai

Msipobadilika!

Mtakosa kuthaminiana!

Mnaponyimana ndani ya nyumba ni laana hiyo

Mliridhiana na kuuvunja umbali ili mfaidiane

Mnapojijengea vikwazo vya uchoyo ikiwa hamu mnayo

Mnapowekeana amri nzito za kukomoana

Mwajikosea wenyewe

Mnajihatarisha wenyewe!

Mtakosa kuthaminiana!

PAMOJA KWAMBA

Pamoja kwamba pendo lako laniacha

Nitalituma langu lilirudishe kwangu

Pamoja kwamba kwaheri inanijongelea

Nitatizama milima,kushindwa kwangu kunatoka wapi?

Anga linafifia na jua halionekani tena

Siku hii ikipambwa na mhemko

Naapia mbingu nitaikabidhi kwako

Ntaisihi mbingu itutakie lakheri hadi dahali.

Najiuliza kama utaondoka tena?

Utarudi lini?

Moyo wangu unazama kwenye zahama

Hofu yangu inazidi kukomaa bila sababu

Pamoja kwamba nimetawaliwa na miujiza

Lakini nyuma ya kumbukumbu zangu

Nakiri sina ujasiri wa kuishi maisha haya bila wewe

Natazama nyuma yako nahisi utakuwa mwisho wetu

Kuonana! Hata kama moyo wangu utapata ganzi

177

Hu,sawa na mshumaa kwenye ukingo

Upulizwao na upepo mkali

Ngoja ya muda mrefu,yanichimbia maumivu yasiyovumilika

Lakini bado…………bado….

Nashauku na wewe kila siku

Hivyo tusitengane turudianapo

Nahitaji pendo lako!

Nakuhitaji!

Nakuhitaji kwa huba lako!

Sina chozi zaidi la kumwaga

Sa tafadhali usiseme kwaheri,usilie bali tabasamu

Sa kwaheri kwa wale waishio gizani kwa upweke

Muda wote nisimamapo kando ya mto ulipo’ndokea

Naikumbuka taswira yako kwa mara nyingine

Nahemka kukukumbatia tena

Nitayaficha machozi yangu katikati ya mvua

Huku nikipunga mkono wangu kwa ukimya

Uendapo na urudipo akutangulie Maulana

Pamoja kwamba! Tunatengana tena.

Bado nakupenda!

J.K.NYERERE BABA

Nyerere baba

Mwana wa Afrika

Mwamba wa mataifa ya Afrika

Twakukumbuka siku zote maishani.

Uliteketeza umimi

Ukavaa uzalendo wa Afrika

Wanyonge ulisimama badala yao daima

Leo haupo nasi

Twakukumbuka siku zote maishani.

Nyerere baba

Kauli zako kali zilileta hamasa

Wezi waliogopa,mafisadi walitetemeka

Hukuwa na mzaha asilani

Leo haupo nasi

Twakukumbuka siku zote maishani.

Ulianzisha umoja wa kitaifa

Ulivunja udini na ukabila kwa maneno

Undugu akauzalisha miongoni mwetu

Thamani ya umoja ilionekana

Leo haupo nasi

Twakukumbuka siku zote maishani.

Hukuwa mchoyo na mroho

Madaraka kuyakumbatia milele

Kwa ridhaa ya moyo wake

Akayakabidhi kwa wananchi

Uamuzi wakauridhia

Nyerere baba!

178

Mfano hai wa kuigwa

Leo haupo nasi

Twakukumbuka siku zote maishani.

SHEREHE ITAKAPOISHA

Sherehe itakapoisha

Tutarudi kwenye msoto

Pesa mpapatiko

Chakula mpapatiko

Maisha thakili

Na gharama za kujikumu

Angani zitapaa.

Sherehe itakapoisha

Kumbukumbu nazo hufifia

Walokufa tunawasahau

Walopigania na kulijenga taifa

Walohatarisha tija ya maisha yao

Tunawafuta pia kumbukubuni

Hakika hatufai!

Thamani ya utu tumeidondoshea kutu.

Sherehe itakapoisha

Fungate litajongea

Ndoa itashika hatamu

Wafadhili wetu watarudi mpapatikoni

Mapesa walitumwagia

Familia zao zapaliwa na ukata.

Sherehe itakapoisha

Taifa litakuwa huru

Makafiri wataishi bwerere

Kwa kidogo chao.Chao na nyumba zao.

Michango ya sherehe zitakoma.

Sherehe itakapoisha

Makinda yatalia sana

Yatakumbuka furaha yaliyoipata

Asalale! Haitojirudia.

Hasira,chuki na vinyongo watazichonga

Kwa wazazi na ndugu.Hasara hawaioni.

Mahusiano yao hatimaye hudidimia.

Sherehe itakapoisha

Ndege angani wata’budu haleluya!

Watarandaranda jalalani kudonoa makombo

Mabaki na makombo ya wahafidhina.

Jasho la makabwela,walilofanyia mafambo

Huzuni tele kwa wakamuliwaji.

Sherehe itakapoisha

Mataji tuliyovishwa tutayavua

179

Sifa tulizovalishwa zitadidimia na sherehe

Maisha yataparara!

Vituko vitakithiri

Utu utatokomea gizani

Mahusiano yatadorora tena nyumbani.

Sherehe itakapoisha

Viziwi watapata kusikia tena

Vipofu watapata kuona tena

Wafu watapata kuishi tena

Wataduwaa kwa maajabu ya sayari hii

Watapinga kuvaa vazi la karne mpya

Uongo ni rangi ya kupendeza

Inatishia uhai wa ukweli

Lakini ukweli ukidhihiri,uongo hujifia.

Sherehe itakapoisha

Maisha yalokuapo yatasonga

Yote yapita,kesho haitokuja

Malengo,maarifa,jitihada na mikakati itatekelezwa

Adha ya kuchangia sherehe zitapotea

Furaha itajipandikiza upya.

RAIS AWAYE YEYE!

Asiwe kipanga

Awe na kauli chanya

Ajue dhamana ya aliyonayo begani

Asijikweze ila atambue makundi yote

Huyo ndiye Rais awaye yeye!

Awe na chachu ya mabadiliko

Asiwe na mgando wa kutambua

Avunje mizizi ya undugu na uswahiba madarakani

Asione aibu kukosoa na kukosolewa

Aseme nipeni ushauri akikwama

Huyo ndiye Rais awaye yeye!

Aishi pamoja na maskini

Ajue ni watu tisa kati ya kumi wanaounda taifa

Awafariji mabalaa yakiwakuta

Machozi awafute asichoke kuwahani

Atatue matatizo na siyo kuyakimbia

Huyo ndiye Rais awaye yeye!

Akemee kwa mshindo mkuu

Azibe mianya rushwa inapotoboa

Amwage razi wasaidizi wake wanapompotosha

Asiwaone haya usoni

Huyo ndiye Rais awaye yeye!

Awe ni sauti ya wengi

Asiwe moyo wa faraja kwa wachache

Azunguke kila kona na ncha ya nchi kuona hali halisi

180

Asiwe wa kuletewe nakala na kupitisha bila kuhoji

Awe ngangari wa uzalendo na si bendera ya uasi

Huyo ndiye Rais awaye yeye!

BARUA YA MAJIBU

Mpenzi!

Udondoshapo macho yako juu ya barua hii

Tambua mimi ni mzima na buheri wa afya.

Nilifurahi,nikaimba,nikatabasamu nilipoisoma

Barua uloniandikia siku ile!

Ni barua nzuri yenye virutubisho vyote

Inanifanya ninenepe kila niisomapo muda nikipata.

Nami usiku huu natembea juu ya kurasa huu mkubwa

Kukuandikia barua.

Barua ya jibu la barua yako!

Ulihoji iwapo nimepata ajira!

Nasikitika kukwambia sijaajiriwa bado

Tangu nihitimu chuo sasa ni miaka miwili

Ofisi zote nilizunguka visigino vikauma

Maajabu nikayaona!

Wapo walioniambia vigezo miaka mitatu ya uzoefu

Jiulize miaka hiyo mitatu nitaipata mimi

Wengine wakadiriki kupinga ufaulu wangu

Eti kwa ufaulu huo,hawawezi kunilipa

Sikutia inda.Nikakata tamaa sasa nimepoa tu

Hakuna kazi! Sina kazi!

Oooh! Kuhusu rafiki yangu K.

Ye’ ameajiriwa sasa ni mwalimu

Huko kijijini nyumba ya kuishi hakuna

Kamshahara kake kaduchu ayavumilia mateso

Marupurupu hakuna

Mazingira ya kazi ni adui wa afya yake

Nawasiliana naye mara kadhaa

Ntamtumia muhtasari wako

Tuliza moyo sasa.

Uliniulizia kuhusu baba!

Ni mzima si kama ulivomuacha

Alilitupa jembe na kutimkia mjini

Kilimo kwake ni sumu-alisema

Huko mjini hana kazi fununu zilisambaa

Aliumizwa na mgambo wa jiji

Alipoanzisha ujasiriamali wa umachinga

Eneo lilipigwa mkasi kumfanyia biashara

Natamani kujua mengi

Nasikitika ni hayo niyajuayo.

Haaa!

Usicheke! Tafadhali nakuomba

X siku hizi ni Mheshimiwa nchini

Unamkumbuka alivyokuwa fakiri?

181

Tulimchagua sababu fakiri huenda angetuona wenzie

Duuu! Uamini usiamini tulichagua msiba

Alifunga ndoa ya mkataba na mzungu pua mbaya

Mkataba wao wa siri wazawa hatuujui

Ndege zatua kila dakika zapakia na kupotea

Malighafi yetu ardhini imenyonywa

Sasa tumebakishwa kabishishi ya mashimo makubwa

Hakuna tunachofaidi!

Ngoja nikutibue moyo

Pili alipokosa kazi japo rushwa aliombwa

Alikataa kutoa,majukumu yakamuandama

Dunia ilipomtelekeza twasikia ana biashara mahsusi

Ana vaa vichupi usiku kwenda kujitafutia chochote

Mtaani aitwa Kahaba machachari

Niliumia,nikasikitika mwisho nikaomboleza

Siku nilipomuona.

Dunia mbaya

Walimwengu nao wachochezi

Tumuombee.

Mpenzi!

Unaikumbuka hospitali yetu takatifu

Si takatifu tena ila ni domo la jehanamu

Kisa kilichotukia hivi majuzi kimetuacha vinywa wazi

Dokta makini,msomi wa nyanja zote

Amfanyia binadamu mwenzie upasuaji

Alipomaliza kamshona kwa nyuzi nzito

Tumboni kamuachia mkasi mgonjwa

Ajabu gani ya dokta huyu msomi?

Tukajua maajabu yameisha hapa duniani

Miezi kadhaa mbele kubwa kuliko likajiri

Mgonjwa wa mguu,mgonjwa wa kichwa!

Aliyepaswa kupasuliwa mguu apasuliwa kichwa

Wa kichwa ye apasuliwa mguu

Tukajiuliza!

Alitaka tibu nini?

Naumwa kichwa watibu mguu

Naumwa mguu watibu kichwa

Akili kweli hiyo?

Dada Aisha uliyemuulizia

Hana raha tena ya maisha baada ya ujauzito

Tabu alizozipata kumzaa mwanae Tabu ni tabu kweli

Alijifungulia chini pamoja na kuwa alikuwa hospitalini.

Mnuna tangu atupokee kwenye unga

Maisha yake ni heri na jehanamu

Ni mlevi amechoka sasa ni teja

Dunia iko kulia,yeye kushoto

Maisha yameganda

Ni huzuni kwetu.

182

Na ukata ule tangu upange kwetu

Amani ya maisha hakuna

Asubuhi njaa! Mchana miayo! Usiku nikulala

Siku zinaenda,zikipita tunasahau

Pesa hakuna! Kazi zimeota mabawa.

Ni kama ulivyotuacha laazizi wangu!

Nimaliziapo kujibu barua hii

Nakiri utakuwa mwendelezo wa barua kadhaa toka kwako

Nipe nikupe,

Uonapo inakidhi nitumie nyingine

Wako katika mapenzi.

Akech!

MKULIMA WA MKONO

Kumekucha!

Kokolikoo!

Jimbi limeshawika

Mkulima damka ukajichimbie shambani

Fanya kazi usikumbuke nyuma

Nyuma.Nyuma kabisa enzi za kampeni

Mwanasiasa alikuambia………..

Mwanasiasa?! Ha! Ha! Ha

Wote ni uchwara tu.

Kheri yako iko kwenye mpini

Uliong’atana na jembe lenye mapengo

Lima asubuhi.Lima mchana.Lima tu

Fanya kazi mavuno yatakufata yenyewe

Ukikumbuka kuna mbolea

Tumia ya ng’ombe wako.

Usisubiri ya siasa.Siasa inachosha subira

Subira nyingi yaumiza moyo

Jua likipoa ardhi imeshika mbolea

Tia mbegu

Palilia shamba

Vuna mwenyewe,usimsubirie mwanasiasa.

Soko lijenge mwenyewe

Soko la serikali ni unyanyasaji

Lina dhamira ya watu wachache.

Nyie wengi umoja wenu ni nguvu

Gumba lenu litamvunja chawa mnyanyasaji

Mkulima wa mkono.Pole sana.

Kumekucha!

Kokolikoo!

Jimbi lawika tena.

Uchaguzi unajivinjari tena

Mwanasiasa mpya na mkongwe wanapigana vikumbo

Wanakujia.Akili yako waiduwaza.

183

Watakupumbaza.“Nipitishe mimi ntakuletea tingatinga la kulimia”

Waongo wakubwa!

Tema ondoka usiwasikilize

Wapaza sauti jukwaani,wakipata ofisini wajichimbia

Ninyi ndugu zangu,

Tena wa damu,

Nilipokuwa navyo,

Niliwasaidia toka moyoni,

Leo nimeishiwa,

Mwanidhihaki,

Wampe ridhaa wewe chini ya jua

Kwenye msururu mrefu wa kupiga kura

Akishinda!

Humuoni tena.Si shambani,jukwaani na wapi……

Amekipata alichokitaka yanini kujisumbua?

Ndiyo falsafa yao mpya

Mpya kabisa nawabainishia.

Miaka mitano unarudi kwenye msoto.

Mkulima wa mkono.Sahau yote

Jua uko mwenyewe bila mkombozi

Jembe lako ndio silaha yako

Imeshasemwa:Jembe halimtupi mkulima.

Lakini:Trekta la mwanasiasa ndio umaskini wako.

Likatae hata bure!

YA NINI LAKINI?

Na kunikejeli,

Ya nini lakini?!

Mwanisomesha nimesoma,

Narudi kwetu nyumbani,

Nyie ni wazazi wangu,

Nanyi ni binadamu,

Mnakosea,mnakandamiza,

Napowakosoa,

Mnanijia juu na kulaani,

Sina nidhamu napotoka!

Ya nini lakini?!

Unatangaza kazini,

Dada yangu anataka kazi,

Anakuja kutafuta,

Unamtongoza na kumlaghai,

Penzi akupe,

Kazi umpe,

Eti mfumo mpya,

Nipe nikupe!

Ya nini lakini?!

Unatuhubiria kanisani,

184

Tutoe tulichonacho,

Twajikamua twatoa,

Sadaka unakula,

Kesho unahubiri tutoe tena,

Tumboni umeshiba,

Umetuibia kidogo chetu!

Ya nini lakini?!

Wanifata haraka,

Wanidokeza lako moyoni,

Wanipenda toka moyoni,

Nakujibu kistaarabu,

Naye wangu wadhati,

Anipenda kwa dhati,

Huamini waning’ang’aniza,

Nimteme nikuchukue weye!

Ya nini lakini?!

Naolewa kwenu

Mume kanitoka

Matanga hayajaanuka

Mmeanza gawana

Mali za ndugu yenu

Watoto hamuwaoni

Uchu wenu ni mali

Mnafikiri nini

Nitaenda wapi mimi?

Ya nini lakini?!

CHUNY PINY

(Roho Ya Nchi)

Ni kiungo laini mwilini mwangu

Kikinikimbia natambua sitoishi

Anajua Manani mwenyewe umbo lake

Aliniwekea mwilini nje ya utambuzi wangu

Naishi sababu ni injini yangu

Je,roho ya nchi nini?

Nchi ni mwili si wa mtu mmoja

Ni mwili wangu,wako,wake na wote

Ni mateso yetu ya nyuma

Adha za utumwa na unyanyasaji tulizovuka

Jana nzima enzi za Berlin

Leo hii twapandikiza roho moja

Nchi inapumua.

Tunaishi kwa furaha

Je,roho ya nchi ni nini?

Amani,umoja,upendo na mshikamano

Ukweli,uadilifu na usawa wa haki

Ndizo zatengeneza mshipa mmoja wa roho ya nchi

Nchi itapumua kwa usawa

Nchi itavuta hewa ya heshima na demokrasi ya kweli

Roho ya nchi,jibu mmeelewa?

185

Rai yangu kwenu wazalendo wa dunia ya tatu

Nchi inapopumua ndo raha yako

Nchi ikifa jua ukimbizi utakuwa subi

Hakuna atakayetupa hifadhi ya maisha

Tumeiua yetu atuamini nani?

Eti yake tutailinda na kuienzi?

Tujiulize hayo bila kudhania.

Roho ya nchi mustakabali wetu.

NA TUVISOME VYOTE

Wosia wangu kwenu

Tuamke twende maktaba tukajisomee

Vitabu ni chemchem ya maarifa isokauka

Vitabu ni dawa ya matatizo yako

Vitakupa nguvu na mwangaza mpya kusoma ukimaliza

Viliandikwa,vimeandikwa na vitaandikwa na wataalamu

Njooni tuvisome vyote,

Hadithi,ushairi na tamthilia

Hadithi!

Mfalme Ndevu na Mmaskini Mkata Kuni

Ya Abdallah Khalfani.

Jipatie elimu juu ya dhuluma,urasimu na tamaa

Ukimaliza kusoma utajihoji mwenyewe

Abed Mehta ni katika Anaona Anasikia

Somo la kujifunza ni athari ya Ukimwi

Ukimwi ni sumu ya maendeleo ya taifa na jamii

Na kitabu cha Mtego Kabambe

Kitakuachia elimu na mafunzo anuani

Kuku Njiwa Kicheche na Hadithi Nyingine

Ya Athumani Abassi.

Ni mahususi kukupa maadili ya kutosha

Chatu cha Bata,A.A

Kinatufundisha thabiti juu ya mapenzi kabla ndoa

Athari zake na ukinzani katika malezi baina-

Ukristo na uislamu

Bwana Jemes, H kupitia Mganga Pazi

Atakuonya juu ya ulaghai katika kupata mali

Balisidya Ndyanayo anasema Ushindi wa Majeruhi

Na Hadithi nyingine

Atakuangazia kwa kina juu ya matatizo

mazitomazito katika maisha

Hao na wengine wengi

Natuitike kuvisoma vyote!

Ushairi!

Zipo tele Kama mvi za babu

Diwani Ya Akilimali cha Akilimali.K.H.A

Chadhamiri kwenye mawaidha mema

Na maadili mbalimbali kama wema na upendo

Utenzi wa Mwanakupona cha Alen .J.W.T

Chenye kudhamiri kwenye maadili mema

186

Na wosia juu ya wanawake-Pwani na Afrika Mashariki

Frenk Wiliam na Diwani Yangu

Mahsusi katika dhamiri ya Mawaidha mbalimbali

Ya kijamii kama siasa safi,adabu,heshima na upendo

Liwazo la ujamaa cha Kandoro,S,A

Chenye dhamiri ya Mapigano dhidi ya unyonyaji,

Na mawaidha juu ya siasa,ujamaa na kujitegemea

Na vingine vingi.

Tamthilia

Ni kama hivi vifuatavyo!

Zimwi la Mrima cha Fawah F

Kinachojadili juu ya dhuluma na uonevu katika jamii

Mashetani cha Hussein E

Kinazungumzia juu ya mapinduzi ya kiafrika

Jitihada za ndani ya bara la Afrika

Kaptula la Marx cha Kezilahabi E

Chazungumzia Utawala wa Kiitikadi hasa wa mafunzo ya Usoshalisti na Ubepari.

Na Mpaka lini? Chake Mariam S M

Alichokiandika kujadili

Madhara ya Rushwa,UKIMWI na Udanganyifu

Naradidi tena na tuvisome vyote

Elimu haina mwisho na ni bahari isokauka

Kujisomea ni chanzo cha maarifa

Ni muda sasa tufunge makazi tukajisomee vitabu

Tusije kuwa vichwa vya wendawazimu

Kwani maono ya vitabu yameandaliwa kwa kina

Twendeni!

Tuvisomeni tusiogope!

SAFARI KUELEKEA

Naitwa Kabiero

Anaitwa Habiba

Namuita Mahabibi!

Ananiita Mahabuba

Raha ya penzi,mpende mpendene.

Na hakika tukashibana mithili ya samaki na maji.

Naivuta taswira nyuma kabisa ya mambo

Ya saa na siku ile

Tulipokutana,tukapanga tarehe ya dibaji yangu

Wazazi na ndugu zake wanitambue

Kisha watutunuku fanaka na ndoa tuifunge

Pingu zituunganishe mwilini hadi moyoni

Si hilo likapita!

Siku ya siku.Ni Jumamosi nifike

Mama mkwe,Habiba na mashemeji wapo CMG Motel

Waningojea

Nimeshavunja kabati suti nyeupe zaningoja

Ngriii! Ngriii! Simu inaita kwa nguvu ikitetemeka

Jina lasomeka-RohoYangu!

187

Napokea.Haloo! Naongea

“Bado upo wapi Laazizi wangu? Mama na ndugu wakutamani.Wahi!”sauti laini ya Habiba yanidekea

Bila kujua hakuna aliye na kesho yake mkononi

Nikajibu kwa mikogo“Nipe lisaa limoja.

Watulize munkari.Aibu sitokutia!”

Laazizi atabasamu kicheko chanitekenya sikio.

Simu nakata.Haraka najivalia viwalo vyangu

Furaha inanisukuma hadi nje

Tabasamu limechanua usoni

Habiba ameamua kunitoa kimasomaso

Kunifungulia hazina ya pendo lake

Halali ya ndoa safi yatoka kwa wazazi

Manani hubarikia wenye malengo yalotimia.

Kisirani ni mjomba wa kiburi.

Najiona nimefika

Furaha imenifura moyoni

Nasahau bado siku haijaisha

Na laiti ningelijua aibu itayonipata ningeihonga

Ikanikalie mbali.

Nisijetoswa majini kwa kumkosa Habiba

Lakini digrii hiyo sina.

Nachunia usafiri wa teksi

Nadandia bodaboda, si nami nionekane nipo.

“Elfu tatu”dereva bodaboda anambia

“Kamua mafuta twende”naamuru kwa mikogo

Safari inazaliwa akilini namuwaza Habiba

CMG Motel ni mita mia saba toka nilipo

Mita mia kabla ya kujivinjari CMG Motel

Bodaboda kajisahau pikipiki kaitumbukiza dimbwini

Yalaa! Maji machafu,mvua ya jana yatwama hapo

Suruali na viatu vyaloa,rangi yabadilika

Balaa gani lanipata mimi.

‘Asalale!’ nang’aka kwa hasira

Pikipiki inakongojwa pembeni

Amani yangu yatumbikia tope la hasira

“We mpumbavu hivi…”najikuta tusi navurumisha

Sijui nifanyeje sasa! Nirudi au niende?

Najipapasa mfukoni kwa hamu simu kuitoa

Taarifa nimjuze Habiba atambue

Napo ndege ni mbaya kwangu

Simu ilishaniponyoka mfukoni

Wazo lanipandia-Imezama majini.

Daaa! Nashtuka kwa ghamu

Jaribu gani lanipata mimi

Mwana wa upendo mjukuu wa amani

Yanibidi kuifata hata kama kuzama dimbwini

Najitosa.Nimekubali hasara sasa.

Kabla sijatia maguu yangu majini

188

Ghafla gari‘Corola’ lilipotoka sijui

Liendapo hata sijichoshi kujua

Lisivyo na utu wala heshima

Lapita kwa kasi dimbwini

Maji machafu lanirushia.Mwili na nguo zalowa

Maji yanikogesha bila kunivua nguo

Sitamaniki.Nipo nyang’anyang’a.

“Kichwa kama gonkone!”namtusi mwenye gari

Uchungu umenikaba.Hasira zimenijaa

Mama mkwe siwezi muona sasa

Mashemaji siwezi waona pia

Ntawajibu nini?

Nitamwambia nini Habiba?

Simu ishapondwapondwa na gari dimbwini

Jameni nambieni.

Aibu hii nimpe nani mimi?

Najiresha nyumbani.Aibu yangu yote

Dunia imenihujumu nisiweze muona Habiba

Wizara ya ujenzi imenitia majaribuni

Halmashauri ya Tarime imedharau utu wangu

Miundo mbinu ya barabara imeraruka

Waona lakini wamejaa porojo kila leo!

Natupa laana yangu kwenu

Mmehujumu dibaja yangu kwa shemeji zangu

Dibaji yangu kwa mama mkwe wangu!

Haipo tena imekufa!

Nimtonye Habiba? Hapana.

Nitamjibu nini? Sijui.

Kesho yake asubuhi si mwenyewe kajivinjari

Kwangu na hasira zimemjaa pomoni

Hataki kunisikiliza

Nilidhamiria kuchuna anasadiki hivyo

Si wake msimamo akaubwaga

“Ni heri kudungwa na mwiba kuliko aibu hii.

Sikutaki tena maishani mwangu”

Hakutia mzaha akatoweka zake………

Zake na kuutupia moyo wangu gizani.

Sasa nalia na moyo!

Nitamuita nani Mahabibi?

Ataniita nani Mahabuba?

Bodaboda amelitia shubiri pendo letu

Amechochea moto penzi letu likateketea

Sina la kumlipa ila namwambia ‘Ahsante’

Wito na rai yangu ni tahadhari

Kinga ni njema tiba usiozee

Usijigambe leo kesho haina jina

Bodaboda ziepukeni japo ni rahisi

Wengi roho zimewatia kapuni

189

Huko kilio kule msiba

Hospitalini walemavu wamiminika

Yote ni kosa la bodaboda

Wilayani kwetu

Wahanga wa pikipiki wamekithiri

Wodi zimefurika wahanga wa bodaboda

Mji unatishika

Taifa linayeyuka nguvu kazi inapotea

Pikipiki inaua kuliko ugonjwa sasa

Tahadhari chukueni vizazi vyote

Kumbukeni usalama kwanza

Mengi tuyape baadaye

Nani atakulindia nyumba ukiondoka?

Nani atamlinda mwanao ukimpa uyatima

Nani atamfariji mkeo ukimuacha mjane?

Nani atamfariji mumeo ukimuacha mgane?

Bodaboda si salama!

Vunjeni chupa ya ukimya mseme!!

NDEGE SI NDEGE,MNYAMA SI MNYAMA.

Enyi wanadamu!

Hamueleweki mnataka nini

Mkipata mnachokitaka

Mwakana mnataka kingine.

Unaitwa kuwa mwalimu

Unafundisha uzalendo toka moyoni

Nasi twakuamini twakuiga

Muda kadhaa twasikia umesaidia kudonoa keki yetu

Sasa tukueleweje?

Unaimba na kughani amani

Unatia mfano unaongoza matembezi marefu

Siku chache jua halijatua

Unakuruta askari wanaingia msituni

Amani unaiua,msiba unabaki kwetu

Sasa tukueleweje?

Twapendana na dunia inajua hilo

Twawekeana viapo kupendana hata kwenye shida

Tunaponda raha pamoja,shida ikijivinjari

Unaruka kimanga,na kuanzisha pendo pengine

Nako unaweka nadhiri

Shida ikiwasili mfumo ni uleule

Unarukaruka kama chura

Sasa tukueleweje?

Kitu kidogo unachukua usiku86

Mchana kweupe waikemea

Tukikuuliza huna la kujibu

190

Unaahidi kuacha kesho unarudia

Sasa tukueleweje?

KIZUNGUMKUTI

Hatari!

Kizungumkuti kwa lidikteta

Alama za nyakati zikitimia

Mvua ya masika ya mabadiliko ikinyesha

Madarakani lafurushwa.

Nchi inazizima.Dunia inafunguka.

Tawala za haki na usawa zinaposimama.

Simanzi!

Jua linapopatwa

Taifa linatikisika,linafifia na linapotea kabisa.

Mfalme anapokufa

Anakufa na utukufu wa taifa lake!

Jaribu!

Umaskini unapokithiri

Maovu hujizalisha

Tufani hutawala nyumbani na mtaani

Wizi unachipuka

Elimu yazalisha wasomi tasa

Ukengeufu unakithiri

Magonjwa yanajitanda majumbani

Jaribu likikomaa laashiria kutoweka.

Furaha!

Miale inapopenyeza

Mabadiliko ya hewa yanaposimama

Upepo unakomba kifusi chote

Taifa jipya linazaliwa

Changa toka tumboni mwa……

Mwa mkulima mnyonge

Mwalimu mla vumbi la chaki

Mstaafu atangishwaye mafao yake

Ni taifa jipya la wazawa!

TUSIRUDI TULIPOTOKA.

Zamani kabla dunia haijaumbwa

Kulikuwa na ombwe kubwa

Hakukua na maisha

Ndipo.

Ndipo dunia ikaumbwa.

Amani ilitawala kila ncha ya nchi

Ustaarabu ulitawala hadi chini ya chupa

Miaka siyohesabika mbele

Tamaa ikatawala

Sisimizi akaingia na kulamba amani yote

Ukoloni ukazaliwa

191

Utumwa ukazaliwa.

Waafrika tukatumikishwa

Tukauzwa kama nyanya sokoni

Tukafungwa minyororo mizito

Mateso yakazidi kikomo

Harakati zikaanza uhuru wetu tukaupigania

Tukapata taifa letu

Leo ni miongo kadhaa imepita

Sisimizi aliyekufa amerudi tena

Anailamba amani taratibu

Matabaka yanajenga tena

Ukoloni umerudi na sura mpya

Ya wenye na wasio nacho

Daraja linakua!

Ukiwa nacho unatawala dunia

Usipokuwa nacho unakoma kuringa

Unamtegemea akuokoe

Anatumia hitaji lako kukukamua

Hali inazidi na mwisho tunarudi dunia ile

Jamani,tusirudi tulipotoka.

BUNGE LA WAHUNI.

Lugha yangu ni Kiswahili

Yataifa yaniunganisha popote niendapo

Lakini hivi majuzi nikajikuta taabani

Mawazoni nikiogelea

Maswali bila majibu

Lugha hii siijui au ni bunge la wahuni?

Bunge la wahuni na wachafuzi wa lugha

Si akaja kijana

Wenzie watano wamekusanyika

Si hapo maajabu nilipoyaona

Akaanza

Masela mishe vipi?

Leo na mchongo mzito nawashushia

Pande zile nazo dozi mimi si msala wa kufa mtu

Shoka likabriki mpini ukastick

Njemba mtoto wa majalala

Si kamlia mingo kinda la kidosi

Madini kamtemea si manzi akaitika.

Huwezi amini,mshua wa demu akazidaka nyeti

Kinda wake anazodolewa na mjalala mmoja hivi

Daaa! Jogoo hajafanya mambo yake

Dingi si akatua geto na mguu wa kuku

Akamsalia mchizi na kumwagia woning’

“Nisikuone wala kusikia unatembea na mwanangu.

Lasivyo nitaitumbukiza risasi moyoni mwako!”

Usiombe mdosho akasepa na kuacha nongwa kitaa!

192

Nikajiuliza alikuwa anongea nini

Si mwenzake akasikika akisema

Chili,chili,nikupe data hizo hizo za mademu

Si unamdaka demu wangu Salome?

Wenzake wakajibu“Sana tu!”

Nikabaki najiuliza ‘sana tu’ nini?

Akaendelea!

Hivi majuzi aliniletea swaga za kijingajinga

Anadai eti nilimpiga upepo

Kitumbo kinamuuma,samaki hawamaindi tena

So anahisi ana kijazuzito

Nikahisi ananichawia tu

Palepale nikabriki karilesheni

Nikamwambia“Kama hutakitoa kijusi hicho.

Sipo tayari kuitwa baba”

Si akatia nyodo na mimi ndiye nguli wake

Nimempiga chini!

Ghafla vicheko vikaripuka

Kila mmoja akamgongea mwenzie mkono

Najikuta naduwaa na kamchezo hako!

Mwingine naye anatema yake

Mazito kuliko hata zege lililolala

Hivi majuzi basi soo likanipenda

Nimedamka mida ya jogoo mfukoni sina kitu

Nikaona isiwe nongwa

Si nikajitupia viwalo hadi mtaa wa kati

Huko kuna kibosile mishe zake si za kuajiri mayanki kupora

Nikafunga mkataba akanipa misheni

Nimuibukie na mguu wa kuku manzi mmoja

Yasemekana alikuwa kipoozeo chake

Nami si nikafanya hivyo

Duu! Manzi mwenyewe wa ukweli

Huwezi amini.Nilipomuona nilipagawa

Nikamdetail eksi wake ameniagiza nimtoe roho

Kusikia hayo Manzi akabwaga chozi

Naye akanijibu“Sema unachotaka nitakupa.

Napenda kuishi.Niachie maisha yangu!”

Akatulia,si akawauliza wenzake swali

Swali ambalo wote walijibu kwa mpigo

“Unajua nilidisaidi nini?

“Kula nyapu!”

Sikutaka kuendelea kukaa hapo tena

Nikaondoka!

Sijui lugha gani haswa waliyokuwa wakitumia

Ni Pijini? Krioli? Au Vizalia?

Haieleweki!

193

Vijana mnafanya nini?

Lugha gani hizo?

Kweli hilo ni bunge la wahuni.

KARIBU MWANANGU!

Karibu sana

Ndani ya ulimwengu huu

Ni chereko nyumbani na moyoni

Twamshukuru Jalali umezaliwa salama

Mimi ndiye baba yako

Huyu ndiye mama yako

Sote tunafuraha isopimika

Twakukaribisha tena nyumbani.

Mwanangu!

Dunia hii ni jino mfupa

Ukiwa tumboni mwa mama yako

Ulikuwa safi

Lakini unapotoka tumboni

Na kuja dunia nyingine

Unatunukiwa hatia usoiona

Tambua hilo.

Yapo mengi mwanangu

Yasikitisha na kuchosha moyo

Duniani tunaishi na majirani wa kutegemewa

Magonjwa,chuki,dharau na masimango

Fitina,uongo,unyonyaji na makandamizo

Lakini!

Unapokuja duniani jua vita tunayo haijaisha

Kila siku twavaa magwanda na silaha mkononi

Amani kuipigania

Usishangae!

Karibu mwanangu.

Chonde chonde mwanangu!

Nje ya nyumba yetu kuna lijinamizi

Linalonyonya na kuacha vipele

Linalolowanisha nywele na kuzipukutisha

Linalonyanyua kenchi za begani

Linalokomba mwili hata damu

Limezalisha wajane kila limvamiaye

Laacha uyatima wazazi wapukutika

Jihadhari!

Halionekani lakini lipo kati yetu

Tiba yake ni moja

Badili tabia na mwenendo!

Mwanangu!

Chapa ya hatia ulotunukiwa unapozaliwa

Haitokutoka hadi mwisho wa dahali

Usijeshangaa ukatupwa jela bila kosa

Kuna wengi twawajua wapo huko

Hawana makosa wanaozea gerezani

194

Wenye hatia warandaranda kama popo

Nikutajie?

Subiri ukue utayaona

Picha zao za udhalimu wao ninazo

Ukiziona na kusihi usiseme kitu

Ila

Chukua hatua thabiti

Chukua mabadiliko ya kujenga

Tafadhari yajue hayo!

TWENDE TUKAWINDE

Tukawinde mbu arukaye kwa roketi

Apigaye mbawa zake kila uwio

Na kutoa mahadhi ya kifu arukapo

Maghorofani azidi kujining’iniza pembeni

Sakafuni ajitundika kutani.Oneni

Ofisini ajibanza kati ya karatasi nzito

Na nyepesi zilizorowa chai ya machozi

Njooni kote tukamwinde.

Huko

Msife moyo!

Milima ni mizito upepo ni kitanzi

Shikeni moyo marungu kuyafumua

Fimbo nzito ziwe mikwaju

Yakujikongojea bahari ya uonevu kuivuka

Jinamizi nyonya jasho na damu yenu

Lipo linajineemesha kwa keki na siagi

Tukilifuma!

Msihoji.Pigieni lipigeni

Life

Lifanyeni mshikaki wa ungaunga

Majivu yake ndo ushindi wetu

Tukirudi salama nyumbani

Silaha msizitupe koridoni

Kesho napo

Kuna lindo la toa roho,fakiri apone

Twendeni tukaliwinde

Dume la nyani lilokubuhu

Kupokonya mahindi yetu shambani

Likicheka pasua kichwa chake

Likinuna kata shingo lake

Likiomba msamaha piga mishale

Onyo na fundisho

Matoto na mate yake yatahama msitu

Ikiwa hivyo

Lindo limefanikiwa!

KWA JIRANI YETU!

Baba amka! Amka!

Mama amka! Amka!

Kaka amka! Amka!

Dada amka! Amka!

Jamani amkeni nawasihi.Amkeni!

195

Kwa jirani kuna balaa limeshika hatamu

Amkeni msikilalie kifo.

Jongeeni dirishani mjionee.

Katikati ya ufinyu huu wa pazia

Kule! Kule kwa Mzee Owadwa

Moshi unarandaranda juu angani

Nyumbani pake pana moto unapikika

Yowee apiga.

Msaada wa moto kuuzima,aomba.

Lakini

Msiende.Mzee Osito sijumuona

Akienda toa msaada nao ni majirani

Wasiwasi wanizonga,begani na mzigo

Mkienda nawaambia:

Mzee Owadwa atafaidika na uingilio wenu

Lawama,shutuma na lalamishi

Atazisukuma kwenu

Mmeenda kumendea mali zake amana

Si kumsaidia moto kuuzima

Unajua kwanini?

Chokochoko za moto kaziwasha mwenyewe

Hamjaona?

Angalieni tu dirishani msiende.

Amkeni!

Kwa Mama Sikitu

Kuna uvamizi wa silaha unafanyika

Msilale sasa vaeni gwanda

Mjomba shika upinde na mshale

Kaka chukua sime

Baba ile bunduki usisahau

Mama nawe chukua kisu

Tunyatie polepole nje tutoke

Majizi ya mali tuyaangamize hadi kifo

Mama Sikutu tumsaidie

Leo Mama Sikitu,kesho kwetu.

Tumlinde mwenzetu lakini

Tusisahau na nyumbani giza ni zito

Macho yetu yasimame

Huku na huko tusijevamiwa.

Jirani ameuguliwa dawa peleka

Jirani amefurukiwa hema peleka

Jirani ana njaa chakula tumpe

Jirani ana kiu maji safi tumpe

Jirani ni jirani mtu wako wa pili

Jirani ni mimi na wewe

Jirani ni nchi nyenzako!

NI LINI NA WAPI?

Najiuliza safari ndefu nendayo

Yenye dhoruba na vingi vijaruba

196

Vunja moyo na simanzi begani

Isoisha kila safari nayopiga

Kutoka hapa kwenda pale

Asipopajua binadamu awaye nani

Ila yeye aliyeziumba na kuzimiliki

Nchi na mbingu na kutia vidole vyake

Ajua fumbo hili

Ni lini na wapi?

Ntafika mimi.

Nainua mikono juu mja wako

Najisalimisha unione kama ulivowaona wale

Unipe leo mkate wangu wa maisha

Tufani ijapo nivuta huko na huku

Mawimbi ya bahari yajapo kisuka chombo

Kwa karima zako utaniweka imara

Nami hujiuliza bila kukoma

Kwani mi ni nani uniangalie?

Kwani mi ni nani nikusahau?

Kwani mi ni nani nijisifu?

Ni we wajua maana uliniumba

Safari ulonianzishia ni we pekee wajua

Ni lini na wapi itaishia!

Kilio changu ni kimoja

Maisha haya ni mazito mno

Kuliko kontena bandarini

Kila kukicha wahesabu tarehe ya maisha

Kila kukicha majanga yazidi niandama

Kila kukicha vilio ni vilevile

Kona yote duniani

Kila kukicha sijui jioni itakuaje

Nipe moyo wa ujasiri

Mapito haya kushinda

Ewe Mola wangu mmiliki wa vyote

Mmiliki wa maisha na kifo cha mwanadamu

Mmiliki wa amani na mfariji mkuu duniani

Nakusifu na kukuheshimu,Amina

Ni we pekee wajua ni lini na wapi

Mimi Akech nitakuwa kesho ikigonga hodiHaleluya!

NYAKO MA ERO AINYA (Msichana Nnayempenda sana)Ni msichana aliyeshushwa toka mbinguni

Mwana wa Adamu aliyetunukiwa shada ya uzuri

Mvuto wa sura na umbo kama la malaika

Atembeapo.Waume kwa wake macho kwake

Mwenye sauti nyororo kama ya kasuku

Anipoozaye moyo maji ya kiu yangu

Ni msichana ninayempenda sana!

Ni msichana anayejua ndugu na wageni

Mkarimu na pambo la nyumba yangu

Aing’arishaye nyota ya uaminifu

197

Machoni nikimuona hana mafamba

Mkweli hata ibilisi anatetemeka akimuona

Ni msichana niyempenda sana.

Ni msichana anayeimiliki dunia

Rafiki yake mkubwa ni amani

Shoga yake mkubwa ni upendo

Shosti yake mkubwa ni uvumilivu

Ajue nilichonacho asinakili nisichonacho

Nalala chini ajue ni mpito tu

Tunakula ugali na dagaa,ajue

Twashiba na bado tunaishi

Ni msichana niyempenda sana.

Ni msichana mwenye macho ya mduara

Madogo mazuri yakuibia hisia

Shingo ndefu kidogo ya pingilipingili

Ngozi laini ya kuishinda sufi

Mwenye pumzi ya moyo wangu

Uwapo jirani nami

Moyo wangu uogelee kwenye maji ya sura yako

Ni msichana ninayempenda sana!

WIMBO ULIO BORA

Wimbo ulio bora

Huimbwa baada ya kazi

Hudunduliza hisia za kweli

Hukonga nyoyo za ushujaa

Ni ule unaochochea badiliko la kweli.

Wimbo ulio bora

Si wa nyokonyoko wala ugeugeu

Si wa kupumbaza wala kughadhabisha

Ni ule unaoparara puya!

Wimbo ulio bora kuimbika

Si ule unaoabudu rushwa na hongo

Si ule unaazima mawazo ya wanyang’anyi

Ni ule unaokidhi shauku ya tahadhari.

Wimbo ulio bora

Haunyofoi furaha ya mafakiri

Walimu,wanafunzi kutandazwa nao barabarani

Kumuimbia mwenye hazina apitaye na gari kwa kasi

Kunakucha,lakini Mheshimiwa akatiza jioni

Ni ule utakaokemea vikali dharau hizo.

Wimbo ulio bora

Si ule unaotukuza taifa kuparaganyika

Si ule unaotukuza maasi barani

Si ule unaosifu ujinga wa watawala

Si ule unaokiuka na kutetea unyanyasaji

Ni ulotukuka kwa tashtiti ya uzalendo,utu na ukemi!

198

Wimbo ulio bora

Si wa kuimbwa na mdomo,bali moyo

Si wa kusemwa na maneno,bali matendo

Si wa kusujudu utumwa,bali uhuru

Si wa sukuma twende,bali wa msimamo kina

Ni ule unaofikia haja ya ndani ya hadhira yake.

MAFAMBA

Wewe ni bosi wa idara

Umepewa dhamana ya rasirimali watu

Unapaswa kuandaa vocha za malipo

Vocha ya malipo ya wafanyakazi wako

Unazilisha majina mengi yasokuwepo

Malipo yanatoka unakula cha hila yako

Hiyo ni mafamba.Acha!

Wewe ni waziri wa nchi

Unaruka na mamilioni yetu kwenda ulaya

Unakunywa chai ya kikombe kidogo hotelini

Unalewa.Unasinzia unasaini mkataba kandamizi

Wazawa wanapokonywa chao

Mwekezaji ananyonya malighafi zetu

Unalijua hilo.Unanyamaza kimya

Unaogopa kuaziliwa kwa chai ulokunywa

Hiyo ni mafamba.Acha!

Wewe ni mzee wa ukoo

Unakosea kama binadamu

Kijana anakurekebisha kiungwana

Unaitisha baraza la wazee

Unatishia kumwagia razi kijana huyo

Eti hana nidhamu kwa wakubwa.

Hiyo ni mafamba.Acha!

Wewe ni kiongozi wa kimila

Unaitisha mjadala wa kimila

Unaamuru kila ukoo ukuletee mfugo mmoja

Unaletwa unachinja

Unakula we na mke wako

Ndugu wakija juu

Unatishia laana itawatandika

Nasaba zao za pili hazitoishi abadani

Hiyo ni mafamba.Jiangalie!

Wewe ni kijana mdogo

Unakaa kijiweni ukivuta bangi

Jua lachomoza,lazama,we na bangi

Kesho unashutumu umerogwa

Unawaona walojituma wakapata,

Ndio wachawi wa maendeleo yako

Hiyo ni mafamba.Acha!

199

Wewe ni mpenzi wangu

Nakupenda sana nawe wajua

Watembea na rafiki yangu mi sijui

Wanisaliti usiku na mchana

Ukiwa nami wajichora kunipenda

Hiyo ni mafamba.Acha!

Wewe ni mke wa mtu

Ndoa ni heshima ya mume na mke

Unarukaruka na vijana wadogowadogo.

Wadogo rika la mdogo wako

Umekosa muhamana wa penzi lenu

Mumeo unampumbaza kumpenda

Hiyo ni mafambo.Acha!

Wewe ni mwanasiasa

Unaporoja jukwaani:Tumaini jema kwa wote

Tunakuchagua ututumikie.

Unatumia vyetu ovyo kutunisha tumbo lako

Tukihoji unapuuza madai yetu

Unatujibu utakavyo.

Hiyo nayo mafamba.Acha!

Wewe ni mwanafunzi

Unakosea unarekebishwa unafyumu

Unachonga kinyongo kikali dhidi ya mwalimu wako

Unamvizia njiani unampiga

Unamuumiza kesho unarudi shule

Hiyo ni mafamba.Acha!

Wewe ni kiongozi wa dini

Una waumini waadilifu

Wanatoa sadaka kujenga hekalu

Usiku unaiba sadaka

Mchana unarudi kuhubiri tena michango

Unawanyonya maskini na wizi wako

Hiyo ni mafamba.Acha!

Wewe ni mwalimu

Unadhamana ya kutoa maarifa

Unatumia chaki yako kupotosha jamii

Uongo unaupaka rangi uwe ukweli

Ukweli unaudidimiza

Unamlindia fulani maslahi

Hiyo mafamba.Acha!

Wewe ni baba mwenye nyumba

Nakulipa kodi yako ipasavyo

Unanipandishia kodi nje ya mkataba

Shutuma ni nyingi zisizo na msingi

Kidogo unajilia familia haijui

Hiyo ni mafamba.Jiangalie!

200

Wewe ni daktari mhodhi wa afya zetu

Dawa zipo hospitalini twajua

Twagonjeka twaja kwako kutibiwa

Unatuandikia vidonge unajua ziliporwa muda

Unatusihi kuzipata duka la tatu

Lenye muamala na wewe

Unadhani hatujui

Hiyo ni mafambo.Badilika!

RAMLI YA TAIFA (Nalipita pembezoni mwa mji)

Moyoni nimechoka kadhia yanilemea

Naliona bango chakavu limetundikwa

Katikati ya miti miwili mikubwa

Najaribu kulisoma!

Mganga wa Jadi mashuhuri yu nchini

Ametua nchini kutatua matatizo yako

Tabu na adha zikupatazo.

Magonjwa anayotibu:

1.Kisukari

2.Kifua kikuu

3.Ukimwi

4.Miguu kujaa maji

5.Surua na pepopunda

6.Magonjwa ya zinaa.

Nafinya macho sielewi kinachotibiwa hapo

Navuta pumzi huenda kadhia yangu

Yanizibia uhuru wa kufahamu tangazo hilo.

Naendelea kusoma.

Matatizo anayotatua

1.Kupendwa

2.Kurudisha mpenzi aliyepotea

3.Kupata pesa haraka

4.Kuondoa mkosi kwenye biashara

6.Kuzindika nyumba.

Najikuta natabasamu sasa

Tabasamu la kusikitikia tangazo hilo

Lenye mvuto lakini la kilaghai

La kuwaibia wazawa hadi kidogo chao!

Mwishoni navutiwa na maneno haya

TUNAPIGA RAMLI UKITAKA!

Navuta usukani najiondoa eneo hilo

Narandaranda barabarani nikiwaza kwa kina

Nawaza.

Kwanini taifa letu tusilipigie ramli?

Ramli isiyo msujudu sangoma

Ramli ya kutatua matatizo majanga nchini

Ramli ya kuvunja visasi

Ramli ya kuagua gonjwa la rushwa

Ramli ya kutokomeza usaliti

201

Ramli ya kusambaratisha matabaka

Ya akina hohehae na ya akina hohihai

Ramli ya kukemea uongo wa viongozi

Ramli ya kuleta umoja wa kitaifa.

Ramli! Ramli! Ramli ya taifa!

Nashtuka!

Nipo katikati ya mji

Natanabahi ramli nayo ni ulaghai

Ulaghai ulosukwa kiustadi na mganga mwenyewe

Daaa! Nang’aka kusadiki nimeokoka

Kutoka kwenye domo la utumwa wa kifikra

Tiba ya taifa langu siyo ramli

Ni umoja wa taifa ndani na nje

Ni mshikamano ndani na nje

Ni uadilifu kazini

Ni ukweli wa tutendayo

Ni kuchukia dhambi ya mirungura toka moyoni

Ni uzalendo wa kufa na kufia nchi

Ni usawa wa watu nchini

Na hizo ndizo ramli aminifu kwa taifa letu.

INAPOTOKEA

De

Degedege likimvagaa mtoto

Wazazi hofu huwatanda

Hospitalini watangatanga

Tiba thabiti kumtafutia

Uchungu mwana kumpoteza,furaha gonjwa likikoma.

Lakini.

Degedege likipenyeza taifani

Wazalendo roho juu juu

Machozi mazito kuwatoka

Watoto huomboleza amani imekufa

Wamama huangua viilo vikali

Wazee hujikunyata.

Lo! Wanasiasa uchwara macho huwatoka

Huajiri hadi ughaibuni,usalama kujiongezea

Familia zao salimini,wazalendo kizaazaa

Tufani ikipumzika,nchini hurejea

Mabavu hutumia madaraka kujitwalia

Degedege lajipenyeza tena taifani!

Mo

Moshi ukifuka,nyumba imeungua

Majirani hujikusanya,maji kumwagia

Mitikisiko ikiendelea,maisha’po rehani

Uchumi gizani,umaskini usukanini

Taifa likisinzia tu

Wazawa kekundu wameshaliwa

Moto ukionekana,amani ishatoweka!

Ila.

202

Moja ikizidi moja,mbili hutokea

Maisha ukiyaanza leo,kesho uwe mwendelezo

Nyuma usigeuke,dahari kuna furaha

Tamaa siisikilize ni mjomba wa poromoko

Bidii ipe mashiko,mafanikio yakujie pekee

Moja ikizidi moja,idadi yaongezeka!

Ki

Kichinjaudhia ikikwama kuponya kichwa

Fikra hugonga mwamba kubaini

Mvua ikishuka bila kikomo kichwa hupoa

Adha za maisha zikitulia loa mafanikio

Ngalawa ya maisha ikusukwasukwa

Kichwa huwanga bila kikomo

La kheri ni kuvaa boya

Mbizi kuipiga hadi pensula ya heri

Lakini.

Kichinjaudhia ikithubutu kuponya kichwa

Kidurango huwa mrefu tena

Mbele hutambua jitihada huamua

Maisha kuyavalia njuga kazi kuifanya

Pepo za kusi zikiyumbisha ngalawa

Machafuko ya bahari hupoa

Kichinjaudhia ikitia nguvu,maisha yanarudia ahueni.

Ra

Radi ikipiga,kifo kimeacha

Tanzia itasikika mtaani kuna msiba

Tukahani kilioni wafiwa tuwafariji

Vurumai yachipuka.Matusi yavurumushwa

Ndugu,majirani washuku radi ni mkono wa mtu

Amani ikitoweka mtaani hapakaliki

Niwinde nikuwinde.Nipe nikupe!

Mfumo mpya wa visasi utatawala,

Ardhi itanyonya damu zisizo na hatia

Radi ikipiga tena.Mvua ya mawe itanyesha

Damu ikichujika udongo utanuka vifo.

Jema ni.

Radi ikipiga,dunia itakoma kuringa

Ngurumo zikitetema ndege watarudi ardhini

Vitoweo bwerere manati haitumiki

Wazalendo watacheka chaguzi zitatii amani

Viongozi watatii jina la demokrasi

Uchumi ukilegea,bolt watakaza

Radi ikitandika.Ukweli utajulikana.

Si

Sibu ya umaskini ikikithiri

Nchi itayumba na kujifia

Mdororo ukizidi kukua

Wenye nacho watageuka miungu watu

Mafukara watalamba michuzi ya chini

Mbwa watagombania kidogo alichotupiwa fakiri

203

Tifu lake litaleta chachu ya maamuzi

Hatimaye.

Sibu ya ukombozi itashika hatamu

Taifa talipigania ili lisipotee

Miungu-watu tutayatwanga shoka ya kichwa

Yakifa huo ukombozi wa kweli

Shuka la tabaka taliteketeza moto

Sote tajifunika blanketi la usawa na undugu

Sibu ya ukombozi ni kuwa na taifa jipya.

MWANZO MWISHO

Unazaliwa

Unakua

Unabalehe/unavunja ungo

Unaoa/unaolewa

Huoi/huolewi

Unazaa/huzai

unazeeka

Unakufa

Unasoma/husomi

Unahitimu/huhimu

Unaajiriwa/huajiriwi

Unastaafu/unaacha kazi

Unaranda mtaani/unapumzika nyumbani

Yote yamekwisha

Unagombea/hugombei

Unachaguliwa/huchaguliwi

Unatimiza wajibu/hutimizi wajibu

Unang’atuka/unavurumshwa

Mageuzi kamili yatokea

Unapenda/hupendwi

Unasaliti/husalitiwi

Unatengana/wasamehe

Unaishi kikapera/unaishi kiseja

Mwakutana tena

Mwasahau na kusameheana

Unacheka/unalia

Unatabasamu/unanuna

Unafurahi/unasikitika

Unalumbana/Una patana

Changamoto za maisha.

DINI

Dini hueleweki! Una matatizo gani hasa?

Dini husitiriki! Umekuwa tuzo duni tasa

Dini hukumbukiki! Umeteta watoto wako!

Dini huchukuliki! Walokuleta wamekukimbia

Dini hukumbuki! Walokupata umewaharibia

Dini hubabaiki! Unatupepeta unatuchafua

204

Dini maaskofu! Wamekutetea umewazingua

Dini waongofu! Wamekulea umewaibia

Dini mashehe! Wamekupigania mama

Dini wahehe! Walikutambua zama

Dini balehe! Umeikosea hama

Dini wazee! Mitini walikuhifadhi

Dini amani! Mjini uligawa ardhi

Dini wa leo! Chupa sawa

Dini kileo! umetupa dawa?

Dini wanasiasa wamekutumia

Dini walimu wamekubabaikia

Dini wakulima wamekupapatikia

Dini madreva wamekupakia

Dini chakula tumekupikia

Dini kijiji umekichafua

Dini wanakijiji umetutifua!

NGAO

Ni ngao vitani vita nyumbani

Vita ya hapa mjini

Vita ya ukapa

Vita iso mipaka

Panya na paka

Wote wanataka

Kukaa jikoni

Kupaa angani

Kukaa kitini

Kiti kile kimoja

Kinamtosha mmoja

Paka anangoja

Panya anangoja

Wanajifanya wana hoja

Wote wakosa

TAMATI!

Tamati!

Kila kitu tamati

Machungu ya maisha tamati

Madhila ya mapenzi tamati

Tamati! Tamati!

Tamati!

Kila kitu chatamatishika

Uongo wa wanasiasa tamati

Dharau na chuki tamati

Maisha yanasimama

Giza linashuka

Kifo! Kifo kila kiumbe duniani

Tamati! Tamati! Tamati

205

MAREJELEO

Abby, C. na Billy Seba (2011) “Kashfa Nzito Part. 2: ni ile ya wasanii wa Bongofleva Kukosa nauli,”

Ijumaa Weekenda, Julai 04, 2011, Dar es Salaam: Global Publishers, uk.9

Abdalla, A. (1973) Sauti ya Dhiki, Nairobi: Oxford University Press.

Abedi, K. A. (1954) Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri, Nairobi: Kenya Literature

Bureau.

Abrams, M. H. (1981) A Glossary of Literary Terms (4 th Ed.), USA: Holt Rinhart na Winston.

Adejeji, J. (1969) "Traditional Yoruba Theatre," African Arts 3.1 (Spring): 60-63

Ajayi, J.F.A. (1999) Historia Kuu ya Afrika: Afrika kwenye Karne ya Kumi na Tisa hadi Miaka ya

1880, Dar es Salaam: TUKI.

Akilimali, K. H. A. (1971) Diwani ya Akilimali, Dar es Salaam, Nairobi na Kampala: East

African Literature Bureau

Akivaga, S. K. na Odaga, A. B. (1998) Oral Literature, Nairobi: Sunlitho Limited.

Alembi, E. B. (2000) Understanding Poetry, Nairobi:Acacia Publishers.

Alipo, J. (2011) “Mitulinga Basi’ Prof. Jay” katika FEMA, July-September, 2011, Dar es Salaam:

FEMINA HIP, Uk. 4 – 6.

Ally, S. (2003) “Wasanii wa Hip hop Wanakaribia Kukitia Mchanga Kitumbua Chao, Nyimbo

Za Mipasho, Majungu Yamezidi, Uwezo Mdogo Roho Mbaya Ndio Chanzo,” Bingwa,

Juni, 3, 2003, Dar es Salaam: Bingwa Newspaper Limited. Uk. 9.

Ayisi, E.O. (1972) An Introduction to the Study of African Culture, Nairobi: East African Educational

Publishers.

Bongo Celebrity (2011) http://www.wahapahapa.com iliyopakuliwa tarehe 22/08/2011

Bowra, C.M. (1952) Heroic Poetry, London: Clarendon Press.

315 – 354.

Bukenya, A. S. na Wenzake (2000) Understanding Oral Literature, Nairobi: Longhorn

Publishers (K) Limited.

Bynoe, Y. (2006) Encyclopedia of Rap and Hip Hop Culture, London: Greenwood Press.

Campbell, L. (1993) Michael Jackson: The King of Pop, New York: Branden.

Chachage, C. S. L. (2002) “Ndani ya Bongo: Utamaduni na Migogoro ya Utamaduni,”

Paper presented at the Tenth Conference on the Political Environment in

Tanzania, 17TH – 18th September, Dar es Salaam.

Chiraghdin, S. (mh.) (1977) Malenga wa Mrima: Tungo za Mwinyi Mohamed, OUP: Nairobi.

Cohen, N. (1993) “Worksongs: A Demonstration Collection of Examples,” katika Archie Green (mh.),

Song About Work: Essays in Occupational Culture, 332 -356, Bloomington: Indiana

University.

Coupland, R. (1938) East Africa and Its Invaders, Oxford: Clarendon Press.

Cuddon, J.A. (1998) Dictionary of Literarry Terms and Literary Theory, Great Britain: Andre

Deutsch.

Curran, J. (2000) Pagan City and Christian Capital, Oxford: Oxford University Press.

Dunleavy, D. (1992) The Language Beat, Ontario: Pembroke Publishing House.

El Kaiim, M. F. S. (1985) Ufasaha wa Ushairi, Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Fiesta (2011a) “Vumilia Abrahamu Braham: Matarajio Yangu ni Kuwa Mwanamuziki Bora Afrika

Nzima,” Aprili – Mei, 2011, Dar es Salaam: Jamana Printers Ltd, Uk. 25 – 27.

________ (2011b) “Mr. Ebbo Alia na Wasanii Wanaopenda Kuiga,” Aprili – Mei, 2011, Dar es

salaam: Jamana Printers Ltd, Uk. 27.

________ (2011c) “H-Baba Aponda,” Aprili – Mei, 2011, Dar es Salaam: Jamana Printers Ltd,

Uk. 27.

Finnegan, R. (1970) Oral Literrature in Africa, Nairobi: Oxford University Press.

________ (1977) Oral Poetry, Its Nature, Significance and Social Context, New

York/Melbourne: Cambridge University Press.

_______(2007) The Oral and Beyond: Doing Things with Words in Africa, Chicago: The University of

Chicago Press

George, V. (2010) “Wamasai Watakiwa Kuacha Ukeketaji,” Mwananchi, Tarehe 24 Novemba,

206

2010, Dar es Salaam: Mwananchi Communicatins Ltd.

Gibbons, B. (1980) Romeo and Juliet. The Arden Shakespeare Second Series, London: Thomson

Learning.

___________ (1993) Shakespeare and Multiplicity, Cambridge: Cambridge University Press.

Goldstein, J. (2005) The Real Price of War: How You Pay for the War on Terror, New York: NYU

Press.

Grady, H. (2001a) "Modernity, Modernism and Postmodernism in the Twentieth Century's

Shakespeare," katika Bristol, Michael; McLuskie, Kathleen, Shakespeare and Modern

Theatre: The Performance of Modernity, New York: Routledge.

___________ (2001b) "Shakespeare Criticism 1600–1900", katika de Grazia, Margreta; Wells,

Stanley, The Cambridge Companion to Shakespeare, Cambridge: Cambridge University Press.

Gunderson, F. (2010) Sukuma Labour Songs from Western Tanzania: We Never Sleep We

Dream of Farming, Leiden/Boston: Brill.

Haggard, H. (1885) King Solomon’s Mines, London: Good Cause.

Harries, L. (1962) Swahili Poetry, London: Oxford University Press.

Haskins, J. (2000) One Nation Under a Groove: Rap Music and its Roots, New York: Hyperion

Books.

Heidegger, M. (1971) Poetry, Language, Thought, New York: Harper & Row Publishers.

Innes, G. (1974) Sunjata: Three Mandinka Versions, Londo: SOAS.

Itandala, A. B. (1983) “A History of the Bazinza of Usukuma, Tanzania,” PhD. Dissertation

(Haijachapishwa), Dalhousie University.

Jamieson, K. M. (1975) "Antecedent Genre as Rhetorical Constraint," Quarterly Journal of

Speech, London: Taylor and Francis Group, 61: 406-415.

Johnson, J.W. (1978) “The Epic of Sunjata: An Attempt to Define the Model for African Epic

Poetry,” PhD Dissertation, in 3 vols., Bloomington: I.U Press

__________(1986) The Epic of Son-Jara, Bloomington: I.U. Press.

Kabuta, N.S. (1997) “Isimu-Ushairi: Muundo wa Majigambo,” katika Nordic Journal of African

Studies 6 (1): 36-60.

Kahigi, K.K & M. M. Mulokozi (1973) Mashairi ya Kisasa, Dar es Salaam: Tanzania Publishing

House.

__________ (1979) Kunga za Ushairi na Diwani Yetu, Dar es Salaam: Tanzania Publishing

House.

Kanuri, J. na wenzake (2008) Mwongozo wa Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine,

Nairobi: NES.

Keyes, C. L. (2002) Rap Music and Street Consciousness, Urbana: University of Illinois Press.

Kezilahabi, E. (1988) Karibu Ndani, Dar es Salaam: DUP.

Kimani, N. na Wenzake (wah.) (2006) Fasihi Simulizi ya Kiswahili, Nairobi: Twaweza

Communications.

King’ei, K. na Catherine Kisovi (2005) Msingi wa Fasihi Simulizi, Nairobi: Kenya Literature

Bureau.

Kisanda, H. (2010) “Wasanii Bongo na Thamani ya Big,” http://www.globalpublishers.info

Iliyopakuliwa tarehe 13/07/2010.

Kisanda, H. na Gladness Mallya (2011) “Bob Junior, Diamond, Wema Vita Nzito,” Amani,

Tarehe 14 April 2011, Dar es Salam: Global Publishers, UK. 9.

Kitangoma (2011a) “Sanaa Imegeuzwa Chombo cha Starehe na Kutukuza Anasa,” Aprili - Mei, 2011,

Dar es Salaam: PrimeTime Promotions Co. Ltd., Uk. 7

___________ (2011b) “20% Sipendi Sifa Bila Ushahidi,” Aprili - Mei, 2011, Dar es Salaam:

PrimeTime Promotions Co. Ltd., Uk. 20-21.

__________ (2011c) “Lugha Yetu ya Taifa ina Vionjo Vingi Wasanii Tuitangaze,” Aprili – Mei,

2011, Dar es Salaam: PrimeTime Promotions Co. Ltd., Uk. 22-23.

__________ (2011d) “Ombaomba ya Wasanii Inatia Kinyaa,” Aprili - Mei, 2011, Dar es

Salaam: PrimeTime Promotions Co. Ltd., Uk. 31.

Koponen, P. (1988) People and Production in Late Pre-colonial Tanzania: History and Structures,

207

Helsinki: Finnish Society for Development Studies.

________ (1995) Development for Exploitation: German Colonial Policies in Mainland Tanzania

1884 – 1914, Helsinki: Finnish Historical Society.

Kineene wa Mutiso (2005) Utenzi wa Hamziyya, Dar es Salaam: TUKI

Lenski, G. (1974) Human Societies: An Introduction to Macrosociology. New York: McGraw- Hill,

Inc.

Little, M. (1987) “Native Development” and Chronic Malnutrition in Sukumaland, Tanganyika 1925

– 1945, PhD Dissertation (Haijachapishwa), University of Minnesota.

Lissah, C. (2007) “Najuta Kuacha Shule-Mr. Blue”, Uwazi, Tarehe 24-30 Aprili 2007, Dar es

Salaam: Global Publishers.

Lo Liyong, T. (1972) Popular Culture of East Africa, Nairobi: Longman Kenya

Lord, A. (1981a) The Singer of Tales, Cambridge: Harvard University Press

____________(1981b) “Memory, Fixty, and Genre in Oral Traditional Literature,” in Foley (mh.):

451 – 61.

Mahenge, E. (2009) “Bongo Fleva ni Uasi au Sanaa za Maonyesho?” Makala Iliyowasilishwa katika

Tamasha la Elimika na Bongo Fleva, Januari 16 – 17, 2010, Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Mair, L. (1964) Primitive Government, London: Penguine Books.

_______(1965) An Introduction to Social Anthropology, Oxford: Clarendon Press.

________(1979) African Societies, Cambridge: Cambridge University Press.

Majembe, A. K. (1998) “Language Use in the Tanzanian Hip hop Scene” Unpublished Research

Paper, UDSM.

Mangesho, P. (2003) “Global Cultural Trends: The Case of Hip hop Music in Dar es Salaam,”

MA Dissertation (Haijachapishwa), University of Dar es Saalam.

Masalu, B. (2011) “Bob Junior: Sitamsamehe Wema”, Ijumaa, Tarehe 4 Mei 2011, Dar es

Salaam: Global Publishers, Uk. 11.

Massamba, D.P.B. (1996) Historia ya Kiswahili: 50 B.K. hadi 1500 B.K., Nairobi: Jomo Kenyatta

Foundation.

_______________(2009) Kiswahili Origins and the Bantu Divergence-Convergence Theory, TUKI:

Dar es Salaam.

Massamba, D. P. B na Wenzake (1999) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA),

Dar es Salaam: TUKI

____________________ (2002) Historia ya Kiswahili: 50 BK Hadi 1500 BK, Nairobi: The Jomo

Kenyatta Foundation.

Mayoka, J. M. (1984) Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka, Dar es Salaam:

Tanzania Publishing House

Mbaga, N.O. (2004) “Ngonjera: Historia yake tangu Simulizi hadi Andishi,” katika Kiswahili Na. 67

Juzuu 67:43-48, Dar es Salaam: TUKI.

Mbarwa, H. (2000) Mashairi Boriti, Nairobi: Eagle H. Publishers.

Mbilinyi, J. (2011) Sugu: The Autobiography, Muziki na Maisha From the Streets to Parliament,

Deiwaka: Dar es Salaam.

Mbunda, M. (1993) Misingi ya Uhakiki wa Fasihi, Nairobi: East African Educational Publishers.

McCall, J. (1995) “Rethinking Ancestors in Africa,” Africa 65 (2), 256 – 270.

Melvin, L.D.F. (1975) Theories of Mass Communication, New York: Longman

Mhando, P. na Ndayanao Balisidya (1976) Fasihi na Sanaa za Maonyesho, Dar es Salaam:

Tanzania Publishing House.

Michuzi, I. (2010) “Mzee Yusufu Ndiye Mwanzilishi wa Kiduku?” katika

http://issamichuzi.blogspot.com/2010/07/mzee-yusuf-ndiye-mwanzilishi-wa-kiduku.html

iliyoangaliwa tarehe 7/10/2010.

Mickys, P. (2010) “Sugu na Ruge Malizeni Tofauti Zenu Kimyakimya,” Spoti Starehe, Tarehe 30,

Juni 2010, Dar es Salaam: Mwananchi Co. Ltd, Uk. 14.

Mihangwa, J. (2009) “Imani za Kishirikina Zinapogubika Chaguzi na Uongozi,” Raia Mwema,

Tarehe 11-17, Septemba, 2009, Uk. 3.

208

Miller, C. (1984) "Genre as Social Action," Quarterly Journal of Speech, 70: 151- 67, London:

Taylor and Francis Group,.

Miller, F, Agnes F. Vandome, John McBrewster (Eds.) (2009) Tanzanian Music, New York:

Amazon Press.

Mnyampala, M. (1970) Diwani ya Mnyampala, Dar es Salaam, Nairobi na Kampala: East

African Literature Bureau.

Msuya, M. (2011), “Maisha Bora kwa Mtanzania Bado,” Sir George Kahama, Mwananchi,

Tarehe 17 Julai, 2011 Uk. 1.

Msongo, B. (2011) “Hata Hicho Kidogo Wananyang’anywa,” Habari Leo, Tarehe 29 Agosti,

2011, Uk. 4.

Mtemwa, I. (2011) “Mastaa 10 Waliosahau Majina Yao,” katika Risasi Jumamosi, Tarehe 20-22,

Agosti, 2011, Dar es Salaam: Imprint Limited, Uk. 17.

Mulokozi, M. M. (1986) “The Nanga Epocs of the Bahaya: A Case Study in African Epic

Characteristics,” PhD Thesis (Unpublished), Dar es Salaam: University of Dar es Salaam.

__________(1996) “Fasihi ya Kiswahili,” Dar es Salaam: OUT.

__________ (1997) Utenzi wa Nyakiiru Kibi, Morogoro: ICOL Publications.

____________(Mh.) (1999) Tenzi Tatu za Kale, Dar es Salaam: TUKI.

__________ (2002) The African Epic Controversy: Historic, Philosophical and Aesthetic

Perspectives on Epic Poetry and Performance, Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers.

Mulokozi, M.M. na T.S.Y Sengo (1995) History of Kiswahili Poetry A.D. 1000-2000,

Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Research.

Musa, M. (2010a) “Keisha Ajitoa Tip Top Connection,” Habari Leo, Tarehe 17 Septemba, 2010,

Dar es Salaam: TSN Publishers, Uk. 16.

______(2010b) “Kiduku Itumike kwenye Dansi,” Tanzania Daima, Tarehe 16, Aprili

2010, Dar es Salaam: Freemedia, Uk. 15.

______(2011) “Nyota wa Bongo Fleva `Aliyeteketea’ kwa Cocaine,” Habari Leo, Tarehe 31,

Julai, 2011, Dar es Salaam: TSN Publishers, Uk. 14.

Musoma Press (1968) Tenzi za Rohoni, Musoma: Musoma Press.

Mutembei, A. (2012) Korasi katika Fasihi: Nadharia Mpya ya Uhakiki wa Fasihi, Dar es Salaam:

TUKI

Mutua, B. F. (2006) Kioo cha Ushairi, Eldoret: Taaluma Publishers

Muzale, H.R.T. (2006) Ikaningabo ya Oruhaya, Dar es Salaam: Mradi wa Lugha Tanzania

_____________ (2009) Diwani ya Nakuomba, Dar es Salaam: Mradi wa Lugha Tanzania.

______________(2011) Kamusi ya Majina na Matumizi ya Mimea kwa Kihaya, Dar es Salaam:

Mradi wa Lugha Tanzania (LOT).

Mwanjoka, G. (2011) Harakati za Bongo Fleva na Mapinduzi, Dodoma: H.M.

Mwaruka, R. (1968) Utenzi wa Jamhuri ya Tanzania, Dar es Salaam, Nairobi na Kampala: East

African Literature Bureau.

Nagler, M.N. (1974) Spontaneity and Tradition: A Study in the Oral Art of Homer, Berkeley:

University of California Press

Nandwa, J. na A. Bukenya (1983) African Oral Literature for Schools. Nairobi: Longman.

Ngure, A. (2003) Fasihi Simulizi kwa Shule za Sekondari, Nairobi: Phonex Publishers.

Njogu, K. na R. Chimerah (2008) Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu, Nairobi: Jomo

Kenyatta Foundation.

Nketia, J.H.K. (1963) Drumming in Akan Communities of Ghana, Accra: Edinburgh: Thomas Nelson.

____________ (1974) The Music of Africa, New York: W.W. Norton Company

Nkwera, F. (1979) Sarufi na Fasihi: Sekondari na Vyuo, Dar es Salaam: Tanzania Publishing

House.

Okpewho, I. (1979) The Epic in Africa, New York: Columbia University Press.

___________(1990) The Oral Performance in Africa, Ibadan: Spectrum Books.

___________ (1992) African Oral Litearature: Backgrounds, Character and Continuity,

Bloomington and Indianapolis: Indiana University Press.

Omari, S. (2006) “Mtindo wa Matumizi ya Lugha katika Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania,”

209

Kiswahili vol. 69, Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Research, 73 – 92.

________ (2009) “Tanzanian Hip hop Poetry as Popular Literature,” PhD Thesis

(Haijachapishwa), Dar es Salaam: University of Dar es Salaam.

_________ (2010) “Call Me Shakespeare: Aliases and Self-Praise in Tanzanian Hip hop

Music,” Unpublished paper.

__________ (2011) “Call Me ‘Top in Dar:’ The Role of Pseudonyms in Bongo Fleva Music,”

Swahili Forum 18 (2011): 69-86.

Parry, M. (1930) “Studies in Epic Techniques of Oral Verse Making II,” HSCP 41:70 – 71.

_______ (1932) “Studies in the Epic Techniques of Oral Verse Making II,” HSCP 43:1 – 50.

Parry, A. (mh.) (1971) The Making of Homeric Verse: The Collected Papers of Milman Parry,

Oxford: Clarendon.

Peek, P. M. na K. Yankah (wah.) (2004) African Folklore: An Encyclopedia, London na

New York: Routledge Taylor and Francis Group.

Perullo, A. (2003) “The Life that I Live: Popular Music, Urban Practises, and Agency in Dar es

Salaam, Tanzania,” Ph. D Dissertation, Indian University.

Posnansky, M. (1966) “Kingship, Archaeology and Historical Myth,” Uganda Journal, 30,1: 1- 12.

___________ (1969) “Bigo Bya Mugenyi,” Uganda Journal, 33, 2:125 – 150.

Raglan, Lord (1956) The Hero, New York: American Library.

1 – 69

Robert, S. (1967) Wasifu wa Siti Binti Saad, Nairobi: Nelson Publishers.

_________(1990) Kusadikika, Nairobi: Evans Africa.

________ (2008) Kufikirika, Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers.

Rodney, W. (1974) How Europe Underdeveloped Africa, Washington, D.C.:Howard University Press.

Roy-Campbell, Z.M. and M.A.S. Qorro (1997) Language Crisis in Tanzania: the Myth of

English vs Education, Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers.

Rubanza, Y. I. (1981) “Dhima ya Fasihi katika Majigambo ya Wahaya,” Makala ya Semina ya

Idara, Idara ya Kiswahili, Cho Kikuu cha Dar es Salaam.

____________(1994) Fasihi Simulizi: Majigambo (Ebyebugo), Dar es Salaam: DUP

Samwel, M. (2010) “Nafasi ya Nyimbo za Mapenzi katika Siasa: Mtazamo wa KiBongo Fleva,”

Makala Iliyowasilishwa katika Tamasha la Elimika na Bongo Fleva, Januari 16 – 17, 2010,

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Samwel, M. (2012a) “Mabadiliko katika Majigambo: Uchunguzi wa Majigambo ya Jadi na Bongo

Fleva,” Tasnifu ya Uzamivu (Haijachapishwa), Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Samwel, M. (2012b) Hadithi Fupi: Nadharia, Mbinu na Mifano, Iringa: Kasenyenda Tanzania.

Samwel, M. (2013) “‘Bongo Fleva Inapotosha Jamii’: Je, ni Dai Jipya katika Maendeleo ya Fasihi ya

Kiswahili?” katika Kioo cha Lugha, Na. 10 Juz. 10, Dar es Salaam: TUKI

Samwel, M. na Wenzake (2012a) Mwongozo wa Mstahiki Meya, Nairobi: NES

_____________ (2012b) Mwongozo wa Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine, Nairobi: NES.

_____________ (2012c) Hadithi Fupi: Nadharia, Mbinu na Mifano, Iringa: Kasenyenda

Tanzania.

Shabaya M. J. na wenzake (2009) Demstifying Poetry, Nairobi: NES

Senkoro, F.E.M.K. (1988) Ushairi: Nadharia na Tahakiki, DUP: Dar es salaa.

______________(2011) Fasihi, Dar es Salaam: KAUTTU LTD.

Shitemi, N.L. (2010), Ushairi wa Kiswahili Kabla ya Karne ya Ishirini, Moi University Press:

Eldoret.

Shija, F. (2009) “Wanandoa Wauawa kwa Mapanga,” Mwananchi, Tarehe 08 November 2010, Uk. 7.

Smith, A. (1776) The Wealth of Nations, Glasglow: Gsm.

Smith, E. W. na A. M. Dale (1920) The Ila Speaking Peoples of Northern Rhodesia, 2 vols,

London: Clarendon

Songoyi, E.M. (2005) “The Form and Content of the Wigashe Dance Songs of the Sukuma,”

Tasnifu ya Uzamivu (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

_________ (1988) “The Artist and the State in Tanzania: Study of Two Singers: Kalikali and

Mwinamila,” Tasnifu ya Uzamili (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

210

Sunkuli, L. O & Miruka, S. O. (1990) A Dictionary of Oral Literature, Nairobi: East Africa

Educational Publishers.

Suriano, M. (2006) “Hip hop and Bongo Flavour music in Contemporary Tanzania: Youths’

Experiences, Agency, Aspirations and Contradictions”, Paper submitted for the conference,

“Youth and the Global South: Religion, Politics and the Making of Youth in Africa, Asia and

the Middle East”, Dakar, 13–15 October 2006.

__________ (2007) “Mimi ni Msanii, Kioo cha Jamii, Urban Youth Culture in Tanzania as Seen

Through Bongo Fleva and Hip- Hop,” Swahili Forum 14 (2007): 207-223.

Tanzania Bible Society (1997) Biblia Takatifu, Dodoma: Tanzania Bible Society.

TUKI (1981) Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Dar es Salaam: TUKI.

Ushe, M.U. (2007) Kpor of Tiv Culture, Enugu: Sam Press.

Ushe, M.U. (2010) The Mortgage Culture of Tiv Death and Burial Rites, Lagos: Vast Publishers.

Ushe, M.U. (2012) “The talking drum: An Inquiry into the Reach of a Traditional Mode of

Communication,” Katika International Journal of Educational Research and Development

Juzuu. 1(2), Uk. 023-028.

Uvetie, E. A. (1976) Utamu wa Lugha, Dar es Salaam, Nairobi na Kampala: East African

Literature Bureau

Vansina, J. (1965) Oral Traditions, Harmondsworth: Penguin.

Wade, M. na Almir Maljevic (Wah.) (2011) A War on Terror?: The European Stance on a New Threat,

Changing Laws and Human Rights Implications, New York: Springer.

Wafula, R.M. na Kimani, N. (2007) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi, Nairobi: Jomo Kenyatta

Foundation.

Wamitila, K. (2005) Tamthilia ya Maisha, Nairobi: Vide Muwa.

__________(2008) Kazi ya Fasihi, Nairobi: Vide Muwa Publishers

__________ (2010) Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi, Nairobi: Focus Books

Wolf, F.A. (1795), Prolegomena (Maelezo mengine ya uchapaji hayapo).

Wood, R. (1767) An Essay on the Origin Genius of and Writings of Homer, New York: Garland

Publishing Inc.

http://en.wikipedia.org/wiki/Clan ilipakuliwa tarehe 12/07/2011

http://spotistarehe.wordpress.com/page/50/

DISKOGRAFIA

Afande Sele (2003) Darubini Kali, Dar es Salaam: GMC Wasanii Promoters.

Bob Junior Ft Nuru (2011) “Muhogo Andazi,” Dar es Salaam: Sharobaro Records.

Dogo Janja (2009) Ngarenaro, Dar es Salaam: GMC Wasanii Promoters.

Lady Jaydee (2007) Shukrani, Dar es Salaam: FKW

Mr. Ebbo (2002) Fahari Yako, Dar es Salaam: FKW

Mr. 2 a.k.a Sugu (2009) Veto, Dar es Salaam: DEIWAKA Entertainment.

Professor Jay (2001) Machozi Jasho na Damu, Dar es Salaam: FKW.

___________ (2003) Mapinduzi Halisi, Dar es Salaam: GMC Wasanii Promoters.

Sister P. (2001) Marekebisho, Dar es Salaam: GMC Wasanii Promoters.

Wagosi wa Kaya (2003) Ripoti Kamili, Dar es Salaam: GMC Wasanii Promoters.

Zay B. (2002) Mama Afrika, Dar es Salaam: GMC Wasanii Promoters.

211

FAHARASA

Abedi, 25, 26, 28, 60, 63, 64, 205

Afrika, 4, 10, 14, 17, 18, 19, 23, 41, 42, 45, 58,

59, 60, 61, 65, 66, 70, 71, 79, 80, 90, 97, 99,

114, 132, 133, 134, 143, 148, 159, 160, 161,

165, 177, 186, 205, 210

Afrika Mashariki, 18, 23, 41, 79, 132, 133, 134

Akilimali, 26, 62, 185, 205

Akivaga na Odaga, 12, 95

Albert Lord, 72, 73

Amri Abedi, 24, 25, 42, 43, 60, 63, 84, 112

Andalio la Somo, 134

Ashton, 24

Azimio la Arusha, 61, 62

Azimio la Kazi, 134, 135

BAHARI ZA USHAIRI WA KIMAPOKEO,

113, 120

Balagha, 130

Bantundi, 121

Bembelezo, 15

Beti, 85, 104, 107, 120, 128

Bongo Fleva, 14, 15, 26, 46, 47, 48, 49, 50, 51,

52, 53, 54, 55, 56, 59, 65, 66, 67, 68, 69, 70,

71, 72, 74, 77, 78, 79, 80, 81, 82, 83, 84, 85,

87, 88, 89, 90, 91, 92, 93, 94, 95, 96, 97, 98,

99, 100, 101, 102, 103, 104, 105, 106, 107,

108, 109, 110, 126, 128, 142, 207, 208, 209,

210

Bowra, 14, 205

Bukenya na wenzake, 13

Chapuzo, 15, 21

CHIMBUKO LA USHAIRI, 41, 45

Chiraghdin, 45, 46, 63, 64, 205

Chuku, 95, 105, 130

Coupland, 41, 43, 205

Dhamira, 42, 126

dhima za ushairi, 52

DHIMA ZA USHAIRI, 29, 35

DRAMA SIMULIZI, 17

Ebeze, 19

Falsafa, 10, 90, 95, 126

fanani, 12, 17, 20, 22, 23, 53, 54, 73, 77, 78, 79,

101, 103, 110, 115, 124

fani, 12, 14, 26, 28, 41, 46, 61, 64, 65, 72, 77,

98, 99, 100, 101, 107, 109, 115, 126, 127,

128, 130, 133, 137, 148

FANI, 72, 127, 137

fasihi, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 22, 23,

24, 25, 26, 27, 28, 41, 42, 43, 44, 46, 54, 57,

58, 62, 63, 64, 72, 73, 74, 80, 81, 82, 83, 85,

89, 94, 95, 102, 104, 109, 110, 111, 115, 126,

127, 129, 130, 131, 132, 134, 137, 144, 145,

146, 147

FASIHI ANDISHI, 23, 137

FASIHI NGOMA, 18

fasihi simulizi, 12, 13, 14, 15, 17, 18, 19, 23,

25, 54, 74, 82, 83, 85

Finnegan, 13, 54, 74, 83, 114, 205

Fuji, 19

Fundisho, 127

Githuma, 24

Gunderson, 48, 52, 54, 206

Gungu, 121

Guni, 123

hadhira, 12, 13, 14, 15, 20, 22, 25, 26, 27, 28,

53, 54, 55, 77, 79, 80, 81, 84, 87, 100, 101,

103, 106, 107, 112, 116, 126, 127, 129, 130,

198

Hamziya, 118

Hamziyya, 42, 57, 59, 113, 118, 207

Harries, 41, 42, 57, 144, 206

hati za Kiarabu, 41, 42, 43, 44, 58

Hekaya, 16

Hip hop, 66, 67, 69, 70, 78, 80, 81, 82, 84, 88,

89, 93, 96, 100, 108, 205, 207, 209, 210

Homer, 72, 208, 210

Hotuba, 17

Hurafa/ khurafa, 16

Inksari, 130

Innes, 29, 30, 206

ishara, 16, 27, 28, 55, 56, 91, 93, 106, 128, 168

Istiara, 16

Jamieson, 13, 206

Jando, 17

Johnson, 29, 30, 73, 104, 206

Jùjú, 19

Kahigi, 3, 26, 27, 28, 58, 62, 63, 105, 110, 129,

130, 206

Kanuri na wenzake, 27

Kejeli, 105

Kezilahabi, 27, 62, 63, 127, 186, 206

Kibwagizo, 85, 87, 128

kiduku, 82, 83, 207

kikai, 113

Kikai, 119, 123

kikwamba, 113, 118, 119, 123

Kikwamba, 116, 123

kimai, 21, 113, 119, 122

Kimai, 15, 119, 122

Kimani na wenzake, 13

King’ei na Kisovi, 13, 119

Kisarambe, 123

Kituo/kimalizio, 128

Knappert, 46, 57

Komedia/Futuhi, 17

212

KUALIKA MGENI, 141

Kumbukumbu, 16, 178

Kwabena Nketia, 18

Lakabu, 16, 92

LENGO KUU, 145

lugha ya mkato, 24, 27, 28, 120, 130

Lugha ya mkato, 131

maandishi, 12, 13, 24, 27, 42, 44, 54, 57, 58,

111

Macgoye, 26, 28

MADHUMUNI MAHSUSI, 145

Mafumbo, 16

Maghani, 15, 16, 21, 22, 23

Mahenge, 15, 109, 207

Maigizo ya kidini, 17

Maigizo ya msibani, 17

Maigizo ya sherehe, 17

maigizo ya watoto, 17

MAJADILIANO, 141

Majigambo ya Majibizano, 96

Majigambo ya Majina, 88, 91, 92, 93, 94, 95

majigambo ya wanawake, 14

malenga, 27, 44, 104, 107, 115

Mandhari, 55, 84, 131

Mandhuma, 113, 118, 124

Maombi, 17

Mapisi, 16

mashairi ya kikasuku, 61

Masivina, 123

Massamba, 3, 27, 44, 45, 63, 207

Masuluhisho, 127

Matambiko, 17

Matumizi ya Lugha, 100, 101, 128, 130, 208

Matumizi ya Mapigo, 56, 108

Matumizi ya Nahau, 130

maudhui, 18, 20, 22, 26, 27, 28, 41, 42, 43, 46,

48, 49, 50, 51, 52, 58, 62, 66, 67, 68, 69, 70,

71, 87, 89, 90, 91, 103, 104, 105, 106, 109,

111, 112, 114, 119, 124, 126, 127, 128, 129,

130, 131, 133, 135, 137

MAUDHUI, 67, 126, 137

Mavazi na Vifaa, 54

Mawaidha, 17, 186

Mazda, 130

MAZUNGUMZO, 16

Mbalaksi, 19

Mbazi, 16

Mbinu ya kufundishia, 139

Mbolezo, 15

Mchongoano, 17

MDAHALO, 142

Melvin, 18, 207

methali, 14, 18, 61, 90, 106, 109, 128, 129, 130

Methali, 14, 16, 109, 130

Mgogoro, 63, 127, 207

MGOGORO WA USHAIRI, 63

Mhando na Balisidya, 18

Michapo, 16

Michezo ya Kuigiza, 17

Mighani (Visakale), 16

Miller, 13, 208

Milman Parry, 72, 209

Misemo, 16, 91

Misimu, 109, 110, 130

Mivigha, 17

Mizaha, 17

Mizani, 128

mkabala wa Kimaksi, 29, 30

Mkarara, 128

Mmbaga, 46, 115

Mnyampala, 3, 25, 28, 31, 33, 42, 45, 60, 61,

62, 63, 111, 116, 208

Mochiwa, 62, 63

Mshororo, 121, 128

Msimamo, 127

msuko, 113, 114, 118, 119

Msuko, 118, 121

Mtindo, 55, 74, 82, 88, 93, 128, 208

Mtiririko, 122

Mugasha, 50, 114

MUHTASARI, 133, 134

muktadha, 12, 14, 15, 20, 22, 23, 28, 43, 74, 94,

115, 119, 131

Mulokozi, 3, 12, 13, 14, 18, 24, 26, 27, 28, 41,

42, 43, 45, 46, 53, 54, 57, 58, 59, 60, 62, 63,

73, 74, 81, 83, 85, 89, 91, 92, 93, 97, 104,

105, 109, 110, 113, 114, 115, 118, 119, 129,

130, 137, 206, 208

Mulokozi na Kahigi, 28

Mulokozi na Sengo, 57, 58, 59, 60

Muundo, 84, 85, 87, 88, 92, 117, 120, 124, 127,

206

Mwanjoka, 54, 67, 69, 70, 77, 79, 81, 83, 84,

89, 90, 92, 208

Mwaruka, 25, 27, 31, 33, 61, 208

Mwindo, 114

Nagler, 73, 208

nanga, 14, 30, 31, 32, 34, 36, 54, 73

NATHARI, 16

Nathari za Kibunifu, 16

Nathari za Kihistoria, 16

Naudia, 113

ngano, 13, 105

Ngano, 16

Ngoma, 18

ngoma za ishara, 18

213

ngoma za kifasihi/ngomezi, 18

ngoma za kuchezwa, 18

Ngomezi, 18

ngonjera, 46, 61, 113, 115, 116, 142

Ngonjera, 31, 33, 46, 61, 62, 115, 116, 124, 207

Nketia, 18, 208

NUDHUMU, 15, 20

nudhumu simulizi, 20

nyimbo, 14, 15, 17, 19, 20, 21, 22, 25, 44, 45,

47, 54, 55, 56, 57, 58, 59, 66, 67, 68, 69, 70,

74, 76, 77, 78, 81, 82, 84, 87, 88, 89, 91, 92,

93, 99, 100, 101, 103, 109, 111, 112, 115,

119, 122, 132, 139, 140

NYIMBO, 20

Okpewho, 73, 208

Omari, 3, 51, 54, 60, 65, 66, 67, 68, 71, 72, 76,

79, 80, 81, 82, 88, 89, 90, 93, 94, 96, 97, 98,

99, 100, 102, 103, 104, 106, 107, 108, 109,

110, 208

Peek na Kwesi, 14, 53, 54, 56, 81, 94

Philip na Kwesi, 54, 55

Picha na Taswira, 106

Pindu, 123

Posnansky, 30, 209

Raglan, 29, 30, 209

Ritifaa, 131

Robert, 3, 24, 26, 27, 42, 43, 60, 63, 73, 140,

209

Rubanza, 3, 13, 14, 49, 50, 51, 53, 54, 55, 56,

81, 83, 93, 97, 209

Sabilia, 121

Sakarani, 118

Samwel, 1, 13, 14, 15, 19, 26, 43, 45, 46, 47,

48, 49, 50, 51, 52, 53, 54, 55, 56, 65, 66, 67,

73, 74, 92, 93, 95, 112, 126, 129, 130, 131,

135, 137, 146, 209

sanaa za maonyesho, 14, 109

sarakani, 113

Sarakani, 124

sayansi na teknolojia, 13, 54

Senkoro, 3, 20, 23, 24, 27, 28, 45, 57, 58, 62,

63, 94, 105, 106, 129, 130, 209

Shabaya na wenzake, 24, 111

shairi, 24, 25, 26, 27, 28, 44, 45, 49, 56, 59, 60,

61, 62, 63, 65, 71, 85, 87, 98, 104, 105, 107,

108, 110, 111, 112, 113, 114, 116, 117, 118,

119, 120, 121, 122, 123, 124, 126, 127, 128,

130, 131, 170

Shairi, 25, 85, 112, 113, 118, 120, 123

Sherehe za kutolea majina, 17

Shirikina, 16

sifo, 16, 22, 53

silabasi, 133, 134, 143, 144, 147, 148, 215

Simango, 15, 21

Simo/Misimu, 16

sitiari, 27, 47, 55, 56, 93, 94, 95, 102, 103, 104,

129

Sitiari, 55, 94, 103, 129

Soga, 17

Songoyi, 48, 49, 54, 55, 104, 209

Sundiata, 114

Suriano, 54, 66, 79, 84, 109, 210

Tabdili, 130

Tabuka, 42, 57, 59

Takhmisa, 58, 113, 117, 121, 122

Takriri, 106, 129

tamathali za semi, 28, 88, 93, 94, 102, 128, 129,

137

Tamathali za Semi, 102, 129

Tanakali Sauti, 131

Tanzu, 12, 14, 15, 20

TANZU FUPIFUPI, 16

tanzu kongwe, 18

Tarbia, 113

Tarihi, 16

Tasadia, 113

Tasdisa, 113

Tashbiha, 102, 129

Tashihisi, 95, 104, 129

Tasifida, 129

Tathlitha, 113

Tathmina, 113

Tathnia, 113

Telemania, 113

Tiyani Fatiha, 124

Tukuzo, 15, 20

Tumbuizo, 15, 19, 20, 120, 124

Uainishaji wa maghani, 15, 16, 22, 23

Uainishaji wa tanzu, 13, 23

UAINISHAJI WA USHAIRI, 111

Ucheshi, 106, 130

Udokezi, 104, 105, 130

UFUNDISHAJI WA USHAIRI, 132

uhakiki wa mashairi, 126

uhifadhi, 12

Uhifadhi wa Historia, 29

Ujumbe, 126

ukara, 113, 117

Ukara, 117, 122

Ukawafi au kawafi, 116, 121

ukawafi/kawafi, 113

ukoloni, 43, 57, 59, 60, 62, 64, 97, 101, 102,

165

UKOLONI WA WAINGEREZA, 60

UKOLONI WA WAJERUMANI, 60

Ukumi, 113

214

Ukuraguni, 122

ukweli wa kihistoria, 29, 31

Umbea, 16

Unyago, 17

Upeo, 123

Usambamba, 110

ushairi simulizi, 12, 20, 25, 27, 41, 42, 45, 46,

47, 48, 49, 50, 51, 52, 53, 54, 56, 57, 58, 61,

64, 85, 110, 111, 112, 132, 140

Ushairisimulizi wa Kibantu, 45, 46

Ushairi wa Bongo Fleva, 66, 67, 72

ushairi wa kazi, 48, 57

USHAIRI WA KISASA, 62

ushairi wa kizazi kipya, 106

Ushe, 18, 19, 210

UTANDAWAZI, 65

Utani, 17

Utendaji, 53, 77, 80, 81, 83, 84

Utendi wa Rukiza, 36, 46, 47

Utendi/utenzi, 114, 120

Utenzi wa Adamu na Hawaa, 114, 131

Utenzi wa al-Inkishafi, 58, 124

Utenzi wa Fumo Liyongo, 58, 114

Utenzi wa Jamhuri ya Tanganyika, 31, 33, 61

Utenzi wa Jamhuri ya Zanzibar., 31, 33, 61

Utenzi wa Mwanakupona, 42, 43, 58, 59, 185

Utenzi wa Nyakiiru Kibi, 114, 208

Utenzi wa Uhuru wa Kenya, 31, 33, 61

Utenzi wa Uhuru wa Tanganyika, 31, 33, 61

Utenzi wa Vita vya Maji Maji, 114

Utenzi wa Vita vya Mau Mau, 114

utenzi/utendi, 113

utoaji wa somo, 143, 144, 145

utungaji, 12, 25, 53, 72, 73, 74, 76, 77, 91, 115,

120, 123

Utungaji wa Kabla ya Tukio, 77

Utungaji wa Papo kwa Papo, 72

Uvetie, 25, 210

uwasilishaji, 12, 13, 14, 54, 73, 76, 77, 81, 111,

115, 141

Vansina, 29, 30, 210

Vichekesho, 16

vigezo, 12, 13, 20, 22, 44, 66, 104, 111, 114,

119, 120, 180

Vina na Mizani, 56, 107, 120, 121, 142

Vipande, 120, 121, 128

vipera vya fasihi, 13

Visasili, 16

Visaviini, 16

Vitabu vya kiada, 144

Vitanza-Ndimi/ Kauli Tauria, 16

Vitendawili, 16

Waarabu, 41, 42, 43, 44, 57, 58, 59, 60, 64, 112

Wafula na Njogu, 13

Wahusika, 55, 95, 96, 110, 131

wajiwaji, 113

Wamitila, 3, 12, 27, 116, 118, 119, 131, 210

wanamapokeo, 24, 25, 26, 27, 28, 45, 63, 64,

112, 114

Wanausasa, 27, 64, 112

Wareno, 41, 57, 59, 60

wawe, 15, 21, 113, 118, 122

Wawe/ Vave, 118, 122

Wimbo, 21, 52, 59, 69, 105, 106, 114, 120, 132,

197, 198

Zana za kufundishia, 144

Ziara, 140

zivindo, 113, 116

Zivindo, 116, 124

215

Ushairi wa Kiswahili umekuwa ukifundishwa katika vyuo mbalimbali katika mahali pengi duniani.

Mbali na kufundishwa huko, hapajakuwa na kitabu kinachofafanua masuala ya kidhana na kinadharia

yanayohusiana na ushairi wa Kiswahili na kuyahusisha na mbinu za ufundishaji wa ushairi na Kiswahili

kwa ujumla. Kitabu hiki kinauvamia mfupa huo. Hivyo, kitabu hiki kinafafanua kwa kina masuala ya

kidhana na kinadharia yanayohusiana na ushairi wa Kiswahili. Kinaelezea, kwa mfano, ushairi ni nini,

ulianzaje, unaainishwaje na unachambuliwaje miongoni mwa mambo mengine. Aidha, kitabu hiki,

tofauti na vingi vilivyotangulia, kinatoa mwongozo kwa walimu juu ya namna ya kufundisha ushairi na

Kiswahili kwa ujumla. Kinafafanua dhana nzima ya ufundishaji wa ushairi na Kiswahili, silabasi ya

Kiswahili ilivyo na nafasi ya ushairi katika silabasi hiyo. Aidha, kinafafanua hatua za kufuata katika

utiaji wa silabasi katika vitendo, uaandaji wa azimio la kazi na andalio la somo pamoja na uteuzi wa

mbinu za kufundishia. Vilevile, kitabu hiki kinafafanua hatua za kufuata katika ufundishaji wa ushairi

darasani na namna ya kutunga mitihani na mazoezi ya ushairi wa Kiswahili na Kiswahili kwa ujumla.

Sehemu ya mwisho ya kitabu hiki inaundwa na Diwani ya MEA ambayo ni kusanyiko wa mashairi

yenye mvuto wa hali ya juu.

Method Samwel ni Mhadhiri wa Isimu na Fasihi katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu Kishiri cha

Elimu Dar es Salaam (DUCE). Ana digrii za BA (Ed.), MA (Linguistics) na PhD (Fasihi ya Kiswahili)

alizozipata katika miaka ya 2006, 2008 na 2012 mtawalia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,

Tanzania. Mwandishi huyu ameshaandika sana katika uwanda wa isimu na fasihi ya Kiswahili na lugha

nyingine za Kibantu. Miongoni mwa vitabu vyake maarufu ni Hadithi Fupi: Nadharia, Mbinu na

Mifano, Mwongozo wa Tamthilia ya Mstahiki Meya na Mwongozo wa Damu Nyeusi na Hadithi

Nyingine. Mbali na uandishi wa vitabu, ameshaandika pia makala mbalimbali katika majarida ya kitaifa

na kimataifa kuhusu lugha, fasihi, muziki na utamaduni.

Amina J. Seleman ni mkufunzi msaidizi katika Idara ya Misingi ya Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki

cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). Ana digrii ya BA (Ed.) (Hons.) (Daraja la Kwanza) kutoka katika

Chuo hichohicho aliyoipata mwaka 2011 akibobea katika Kiswahili na Ualimu. Mwandishi huyu ni

mwanataaluma anayechipukia aliye na utayari wa kujifunza na mwenye bidii kubwa sana katika

kujaribu. Kwa sasa anaendelea na masomo ya digrii ya MA (Ed.) katika Chuo Kikuu cha Dar es

Salaam. Mbali na kufundisha katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam ameshafundisha kwenye

shule mbalimbali za sekondari nchini Tanzania. Hivyo, ni mwalimu mzoefu sana.

Akech Kabiero ni mwandishi maarufu sana wa kazi mbalimbali za fasihi. Yeye huandika mashairi,

riwaya, tamthilia na hadithi fupi. Mpaka sasa ana hazina kubwa ya miswada ya kazi hizo za fasihi

ambazo bado angali anatafuta mchapishaji. Ni mwanafasihi mwenye kipajai cha hali juu. Kabiero

alihitimu digrii ya BA (Ed.) mwaka 2012 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alibobea

katika somo la Kiswahili. Mwandishi huyu zaidi ya kipaji cha utunzi ni mwalimu wa sekondari

aliyebobea.

MEVELI Publishers, Dar es Salaam-Tanzania.

ISBN: 978-9987-9735-0-7

MEVELI PUBLISHERS (MVP)

No comments:

Post a Comment