Baraza la kiswahili la taifai (BAKITA)
Chombo hiki kiliundwa kwa sheria ya bunge na 27 ya mwaka 1967. madhumuni ya kuunda bakita ni pamoja na,
kukuza maendeleo na matumizi ya kiswahili fasaha katika wizara mbalimbali na kwa watu binafsi.
kushirikiana na vyama navyuo katika nchi yetu vinavyohusika na ukuzaji wa kiswahili.
kutoa jarida la kiswahili litakaloongoza matamshi sahihi ya maneno
kulinda na kutoa tafsiri sahihi za maneno ya kiswahili
kuisaidia serikali na mashirika yake kwa haja watakazotaka watendewe pamoja na kusaidia wenye nia katika kutunga vitabu vya kiswahili kwa mujibu wa lugha ya kiswahili.
Kujihusisha na ukuzaji wa misamiati
kuendesha mijadala kuhusu matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili
kufanya uchunguzi kuhusu matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili
Kudhibitisha usahihi wa lugha ya kiswahili katika miswada mbalimbali inayotarajiwa kuwa vitabu vya lugha hiyo vitakavyotumika shuleni
Hata hoivyo bakita bado inakumbana na changamoto mbalimbali kama vile uhaba wa fedha kwa kutochukuliwa kwa umuhimu kama taasisi ya serikali
ukosefu wa miundombinu ya kisasa