Friday

Vin Diesel arejea na filamu ya “Bloodshot” kumbi za sinema

0 comments


Dk Hating endapo Garrison atagundua siri yake na ameshampatia uwezo kana kwamba hata bomu lililomaliza vita ya pili ya dunia haliwezi kumsambaratisha? Picha| Super Hero Hype.

  • Ni filamu inayomchora kama shujaa anayeitwa Bloodshot.
  • Ametengenezwa kana kwamba bomu la atomiki haliwezi kumsambaratisha.
  • Daktari aliyemfanyia matengenezo, anamtumia kulipiza kisasi.

Dar es Salaam. Ni wakati mwingine wa “Action” kwani baada ya kuitazama filamu ya “Ip Man”, burudani ya filamu inakuvuta karibu na muigizaji nguli  Vin Diesel akiigiza pamoja na wababe wengine kwenye kiwanda cha filamu huku wote wakipangwa na kiongozi David Wilson.
Mambo yakoje?
Filamu ya Bloodshot inamzungumzia  Ray Garrison (Vin Diesel) kama shujaa au “Super Hero” ambaye ameongezewa nguvu kwa malengo ya kulipiza kisasi. Kifupi ni kwamba anatumika kufanya hivyo yaani, kulipa kisasi.
Kundi linaloongozwa na Dk Emil Harting (Guy Pearce) linamtengeneza Garrison na kisha kufuta kumbukumbu zake. Wanatumia nafasi hiyo kuendesha kumbukumbu zake kwa kutengeneza zingine ambamo wanaweka wahusika tofauti kila wanapofanya hivyo.
Kwenye kumbukumbu hizo, Garrison ambaye amerejea kutoka vitani na kukutana na mpenzi wake Gina (Talulah Riley) hapati furaha aliyoitarajia kwani Gina anauawa kabla hata hawajalifaidi penzi lao ambalo lilisubirishwa na vita.
Dk Hating anatumia teknolojia kubadilisha sura ya mtu aliyefanya mauaji hayo na kumtumia Garrison ambaye analipiza kisasi akiwa hajua kuwa anatumika.

Ni nini kitampata Dk Hating endapo Garrison atagundua siri yake na ameshampatia uwezo kana kwamba hata bomu lililomaliza vita ya pili ya dunia haliwezi kumsambaratisha?
Tazama filamu hii kwenye kumbi za kuangalizia filamu zikiwemo Mlimani City na Aura Mall huku filamu zingine kama “Bad Boys” na “Onward” zinaendelea kuonyeshwa
Unaachaje kujinyima Sh10,000 kuuona uhondo huu?

No comments:

Post a Comment