Nadharia ya Upokezi (mwitiko wa msomaji) ambayo husisitiza nguvu ya msomaji. Nadharia ya Upokezi (Reception Theory) iliasisiwa na wahakiki wa waasisi wa Kijerumani mwishoni mwa miaka ya 1960.Miongoni mwa waasisi wa nadharia hii ni Robert C. Holub,Hans Robert Jauss na Wolfagang Isser.Katika kitabu chake Reception Theory (1984), Holub anaelezea nadharia ya Upokezi kuwa ni Mabadiko ya jumla ya umakinikiaji kutoka kwa mwandishi na kazi yake kwenda kwa matini na msomaji”
Nadharia ya upokezi inaakisi mabadiliko ya mbinu katika historia ya fasihi na ilizingatiwa kama jibu kwa jamii,wanazuoni na maendeleo ya fasihi huko Uerumani Magharibi mwishoni mwa miaka ya 1960.Kwa mujibu wa Holub, nadharia ya Upokezi ulikuwa ni njia ya Kimapnduzi kwa wahakiki wa kisasa.
Waitifaki wa nadharia hii wanashiilia msimamo kuwa kazi ya fasihi hupata maana baada ya matini na msomaji kuadhiriana.Msomaji au mpokeaji ndiye huipa maana kazi ya fasih.
Kwani huiona na kuilinganisha na uzoefu wake wa maisha. Kielelezo hiki kipya cha uhakiki hutilia maanani dhima ya msomaji.Hans Robert Jauss katika makala yake “The change in the Paradigm of Literary Scholarship” (1926) ambaye anachukuliwa kama mmoja wa mihimili ya nadharia hii ya Upokezi anaelezea umuhimu wa kuielezea kazi ya Fasihi.Isser anaiona kazi ya Fasihi kama kitu au tukio lililo nje ya muktadha na historia.
Anasema kuwa ili kazi ya fasihi ieleweke ni lazima ushiriki wa msomaji uoane au upatane na maana inayojitokeza katika kazi ya Fasihi.
Kwa hiyo basi , nadharia ya Upokezi hufasili Fasihi kama mchakato wa namna msomaji na wanavyoathiriana.Uzoefu wa maisha wa msomaji unaweza kutoa tafsiri tofauti kwa kazi ya fasihi kutoka msomaji mmoja na mwingine.