Tuesday

Maana ya Ujumi- Ujumi wa mwafrika, ujumi mweusi

0 comments

-maana ya ujumi
-faida za ujumi
-misingi ya ujumi


UJUMI (AESTHETICS)


Ujumi ni nini?

Ujumi ni tawi la falsafa linaloshughulika na uzuri, ubaya, ladha, n.k.

 AU

Ujumi ni elimu ya sheria na kanuni za sanaa.

Neno ujumi kwa kiingereza linajulikana kama “Aesthetics”. Neno hili limetoholewa kutoka katika lugha ya kigiriki “Ais  -  thesis”, likiwa na maana ya “Hisia” (Feelings), hasa hisia za akilini (Mental perception).

Alexander Gottlieb Baumgarten (mjerumani) ni miongoni mwa wanafalsafa yalioshungulikia kwa kina juu ya falsafa hii ya Ujumi. Baumgarten alidokoa baadhi ya mawazo fasaha kutoka kwa Leibniz. Leibniz alizungumzia mambo makubwa mawili amabayo ni LOGOS na ETHOS. 



LOGOS, ni mantiki itokanayo na neno la maharifa au sababu ipelekeayo uwelewa mpya au kuyachekecha mawazo makuukuu na kupata neno lenye kuchukua mkondo mpya.

ETHOS, ni desturi ama mguso, tabia ama kaida Fulani ndani ya jamii ambazo hufanya matakwa yahusuyo jamii Fulani tu.

Baumgarten, alikiendeleza kipengele cha mguso na hisia na neno “Aesthetics” likaanzishwa.
Kabla falsafa mpya ya Aesthetics haijachukua kasi yake, hapo awali masuala ya hisia yaliwekwa chini ya nadharia ya hisia za akili (mental perception). Dhana ya ujumi ilitoka kwenye nadharia ya hisia za akili katika karne ya 18 na kuitwa “Falsafa ya uzuri” au “Falsafa ya sanaa” au yote mawili kwa pamoja.  Baadaye ujumi uliachana na falsafa na kuwa tawi linalojitegemea la elimu.

Kabla ya Baumgarten, ushairi na sanaa kwa ujumla ilijadiliwa kitaalamu katika kapumoja. Hii inamaana kwamba ushairi haukutofautishwa na muziki au uchoraji ama ususi, vyote vilielezwa kwa pamoja.
Baumgarten akaigawa dhana hii katika maeneo mawili ambayo ni uzuri na sanaa.

1.       UZURI (The good or the truth).

Uzuri ni ukamilifu wa hisia za akili unaoleta kulitazama jambo au mambo Fulani katika mtazamo chanya, haijalishi, kwani mwingine anaweza kulichukulia jambo hilo kimtazamo hasi lakini mtazamo wake hauondoi uzuri wa chanya kwa atazamaye chanya.

2.       SANAA


Sanaa ni ufundi wa kuunda jambo. Twaweza kuueleza uzuri kupitia sanaa. Sanaa yaweza kuupambanua uzuri kwa viwango vya juu zaidi kuliko jambo lolote lile.

No comments:

Post a Comment