Ebora ni moja kati ya virusi 30 vinavyoweza kusababisha homa ya kutokwa na damu. Genusi ya kirusi cha ebola kwa sasa bado kimegawanyika katika makundi matano ambayo ni:
- Sudan Ebolavirus,
- Zaire eboravirus,
- taiforest(ivory coast) eboravirus,
- Reston ebora virus na
- bundibugyo Ebolavirus.
Mlipuko wa ugonjwa wa kirusi cha Ebolavirus mwaka 2014 huko afrika magharibi ilihusisha kirusi cha Zaire Ebolavirus, ulikuwa mlipuko mkubwa sana katika historia ya ugonjwa huu duniani.
NI vema kuangalia magonjwa ya milipuko kabla hujaenda baadhi ya nchi ili kujua hali ya usalama katika nchi hizo nazoenda
Shirika la Chakula na madawa la Us food lilipitisha vipimo viwili vya haraka kwa ajili utambuzi wa kirusi huyu kwenye damu na mkojo kwa mda wa saa moja tu kwenye baadhi ya hospitali na kuzipa uwezo wa kupima kipimo hicho, pia kipimo cha pili ni kile ambacho damu au mkojo hupimwa kwenye maabara maalumu na majibu hutoka kati ya masaa 24 hadi 48
Vihatarishi vya kupata ebola
Aina mbili za kujiweka hatarini kupata maambukizi ya kirusi cha ebora zinatambulika
- Kujiweka hatarini kwa awali ni kwa wale watu wanaoenda kufanya kazi maeneo(nchi) ya ugonjwa huo ulipo
- Kujiweka hatarini kati ya mtu asiye na maambukizi ya ebola na mtu aliye na maambukizi ya ebola mfano(ndugu, dakitari na mgonjwa, wanaoandaa mazikio ya kuzika mgonjwa wa ebora na mtu anayeandaa nyama ya wanyama poli kwa ajiri ya binadamu, mtu anayefanya kazi kwenye wanyama jamii ya nyani)Dalili na ishara za eboraDalili za kuonekana kwa macho hutegemea hatua ya ugonjwa unapoanzakutoa dalili hizo. Kirusi cha ebola cha Afrika hutumia siku 3 hadi 8 kwenye maambukizi ya kwanza na zaidi ya siku hizo kwa maambukizi ya mara ya pili kuonyesha daliliDalili za awali zinaweza kuwa
- Homa
- Tezi koo kuuma au kuvimba(tonsils)
- Dalili kali za ebola
- Harara na vipele( huonekana sana kwa ngozi nyeupe)
- Kuwa na rangi nyekundu kwenye kuta nyeupe za macho au kitaalamu conjunctiva
Dalili baada ya dalili za awali zinaweza kuwa
- Kutokwa na damu kiasi kikubwa unapochomwa sindano kwenye mishipa ya damu na ngozi laini
- Maambukizi ya misuli ya moyo na majikwenye mapafu
- Kwa wagonjwa waofikia hatua ya mwisho, hupata shida ya kupumua, shinikizo la damu kushuka, kupungua sana kwa kiwango cha mkojo, na kuzimia
Kwa wale ambao wamepona kutoka katika maambukizi ya ebola huwa na dalili zifuatazo hapo baadae;
- Maumivu ya misuli
- Kuugua maungio ya mwili yanayohama ungio moja hadi jingine hayatokei kwenye magoti au maungio yanayofanana kwa pamoja
- Maumivu ya kichwa
- Mchoko –kuchoka
- Kula sana au tatizo la ulaji wa chakula (bulimia)
- Kutoona siku (hedhi) kwa wanawake
- Kupoteza usikivu (masikio)
- Makelele kwenye masikio
- Maumivu ya mirija ya tezi mateVipimo
- Kipimo cha damu kutambua jeni zakirusi huyu
- Kipimo cha serology kinachopima kinga zinazopambana na kirusi huyu
Matibabu ya ebola
Matibabu huwa na mfumo ufuatao
- Kupunguza madhara ya dalili kama vile kuongezewa maji mwilini endapo maji yanapungua sana, kuongezewa madini, chakula na kufarijiwa
- Matibabu hayo hutolewa kwa uangalizi makini na kwa kutengwa kwamgonjwa na watu wengine.maimaji yote kutoka kwa mgonjwa huwa na virusi vinavyoweza mumpata mtu mwingine na hutakiwa kushikiliwa kwa uangalifu sana
- Hakuna dawa inayofahamika kwamba inatibu kwa uhakika ugonjwa huu wa kutokwa na damu
- Hakuna chanjo zinazouzwa kwa ajili ya kirusi cha ebola, ingawa kinga zinazoweza kupunguza mkali ya kirusi huyu bado zipo zinafanyiwa utafiti kutumika kama chanjo
Mpaka sasa hakuna tiba dhidi ya kirusi cha ebola. Dawa ambazo zimefanyiwa uchunguzi na zinatumika katika matibabu na kujikinga na kirusi cha ebola ni kama zifuatazo;
- Ribavarini zimesomwa kwa nyani na zimeshindwa kukinga dhidi ya kirusi cha ebola kwa nyani waliokuwa wameathirika na kirusi huyu
- Nucleoside analogue
- Interferon alpha
- Horseo goat derived immune globurine
- Human dderived immune globurine
- Dawa za jeni
- Protein C
- Dawa zingine za kuzuia damu kutoka
Kwa wagonjwa wanaopona, kupona siku zote huchukua miezi, na baada ya kupona mgonjwa anaweza kupumzika kwa miezi kadhaa ili kurudi kufanya kazi zake za kila siku. uzito kujirudia hali yake na kupata nguvu huwa ni jambo la taratibu.kirusi cha ebola huendelea kuwa katika mfumo wa damu kwa wiki kadhaa baada ya kuondoka kwa dalili za kirusi huyu
Virusi hawa hutunzwa wapi?
Utafiti ulifanyika katika miaka ya 1966 huko DRC kongo na kirusi cha ebola kimeonekana kwa wanyama aina 19 na mimea aina 24. Virusi vya ebola vimeonekana katika matunda yanayoliwa na popo pamoja na popo wenyewe na hujizalia kwenye popo na matunda hayo pasipo kufa.
Kwa jinsi gani husafilishwa.
Virusi vya ebola vya afrika husafilishwa kutoka kwa mtunzaji asiyejulikana (labda popo) kwenda kwa binadamu au mmea na mnyama asiye binadamu. Sana sana kwa kupitia majimaji na damu kutoka kwenye ngozi laini, macho mate na matumbo kwa kupitia michaniko midogo sana katika ngozi na kwa vipimo vya kitaalamu kumeonyesha hata kwa njia ya hewa pia kunaeneza ugonjwa huu.
Mwbwa nao wameonekana kuambukizwa virusi hivi pasipo kuonyesga dalili yoyote, maambukizi haya hutoka katikakinyesi, mkojo au damu kutoka kwa mtunzaji(host) asiyefahamika.
Hatima ya ugonjwa
Hatima ya ugonjwa kwa mwathilika wa kirusi cha ebola ni mbaya. Kwa wale walioishi muda wa wiki mbili baada ya ugonjwa hupona na kurudia kazi zake polepole sana
Ukitoa kirusi wa Reston, maambukizi ya kirusi cha ebola huambatana na vifo na madhara makubwa sana ingawa hutegemea na aina ya kirusi cha ebola. Kirusi cha ebola kinachoua sana ni kile cha aina ya zaile Ebolavirus ambacho kilionekana kuua kwa asilimia 89 kwa waathirika wote. Kirusi cha Sudani ebolavirus kinamauaji kwa asilimia 41 hadi 65.