Thursday

M-PESA MASTERCARD INAVYOWEZA KUBADILI BIASHARA YAKO

0 comments

-Unaweza kununua bidhaa yeyote mtandaoni ikiwa mahala popote ulimwenguni kwa kupitia M-pesa
-Inakupatia card number pamoja na security code utakazo zitumia kufanya malipo mtandaoni

-Utaweza kuweka fedha katika kadi yako na kufanya miamala kadiri upendavyo

-Ni rahisi kutumia


Hujambo ndugu msomaji,  Karibu tuangazie namna muunganiko wa mpesa na MasterCard unavyo weza kuinufaisha biashara yako. Maendeleo ya kiteknolojia ni ahueni katika nyanja zote, na hii sekta ya biashara haijaachwa nyuma katika suala hilo.

Kupitia Mpesa master card unaweza kulipia na kutangaza bidhaa yako katika mitandao yenye wafikiaji wengi kama vile Facebook na Instagram hivyo itakuongezea Wateja wengi na wapya kutoka sehemu mbalimbali.

Vilevile inakuwezesha kununua bidhaa mbalimbali kutoka maduka ya mtandaoni  ambayo yanapokea malipo ya MasterCard.

Sio hivyo tu bali unaweza kupokea malipo ya bidhaa zako kupitia program hii rahisi. Licha ya hayo program hii ni rahisi sana kutumia, kama ilivyo kufanya malipo ya M - pesa.
Hivyo kwakutumia program hii unaweza kabisa kubadili sura ya biashara yako na ikakuletea faida lukuki.

Kujua namna ya kutumia Mpesa MasterCard bofya HAPA

Tukutane wakati mwingine usisahau kuacha comment yako.

No comments:

Post a Comment