Thursday

RIDHIMU NI NINI?

0 comments


©Masshele 2019

Ni mapigo asilia ya sauti
Kila lugha inayo mapigo yake. Mawimbi ya sauti yenye kupanda na kushuka na yanayo fungamana na maana. Ridhimu ya ushairi na muziki hutokana na mlingano wa mapigo ya lugha au sauti.
Asili ya ridhimu ya kishairi ni ridhimu asilia iliyomo katika maumbile mazingira na shughuli za binadamu, kwamfano Nazi, ngoma na nyimbo.  N.k

Ridhimu ya ushairi haina budi kulingana na maudhui ya ushairi husika. Isaidie katika kuyadhihirisha maudhui hayo kihisia, kimtiririko na kimsisitizo.
 Ni chanzo cha ushikamani wa matini na kiungo baina ya sauti na maana.

Ridhimu katika nadhari.

Ridhimu hutokana na kufuata , vikundi vya kimuundo, ambavyo katika mazungumzo, huashiriwa kwa pumziko, na katika maandishi, kwa alama za vituo mbalimbali.
Kikundi au kirai cha kisintaksia chaweza kuchukuliwa kuwa kipashio cha msingi cha ridhimu ya nadhari.

Ridhimu ya ushairi Andishi.
 Hufuata urefu wa mstari ambao ndicho kipashio cha msingi cha ushairi.
Katika mashairi ya kimapokeo, ridhimu imetawaliwa na urari wa vina na mizani.
Katika ushairi wa mtiririko ridhimu imetawaliwa na maudhui na ufundi wa mwandishi.

Maarifa haya yamedondolewa kutoka katika mihadhara ya Dkt J. Bulaya kutoka IKS UDSM.
www.masshele.blogspot.com

No comments:

Post a Comment