Thursday

MAANA YA MCHOMOZO/ UCHIMUZI

0 comments

©masshele 2019
Ni dhana ya muhimu katika taaluma ya elimu-mitindo.
Hujidhihirisha katika viwango vyote vya uchambuzi.

Ni mbinu ya kuyadokeza mambo fulani au sifa fulani katika kazi za kifasihi kwa namna ya wazi wazi na kuyafanya yajitokeze wazi ukilinganisha na mambo mengine (wamitila 2002)
Hii ni mbinu inayotumiwa kusizitiza mambo fulani yanayoonekana kuwa ni ya muhimu na yenye uzito katika kazi fulani ya kifasihi.

Ni ujitokezaji wa wingi/ uchache/kapa kulinganishwa na kaida zilivyo wa vipengele vya lugha katika muktadha mahususi. Ujitokezaji huu huzingatia kaida maalumu.
Huhusiana na kuingiliana sana na takriri.
Maranyingi MCHOMOZO ndio unao amua kama takriri ya kipengele fulani ni yamuhimu au laa kwani si kila takriri huiga au kudokeza maana .

Maarifa haya yamenykuliwa katika mihadhara ya Dkt Bulaya kutoka IKS UDSM
www.masshele.blogspot.com

No comments:

Post a Comment