Nadharia
ya vikoa vya maana imeasisiwa na Mjerumani Jost Strier (1930) akiegemea katika
msingi wa kusema kuwa kuna maneno yanayofanana yanaweza kuwekwa pamoja. Mawazo
haya ya Strier, Lyons (1970) anadai kuwa hayakuwa mawazo ya Strier bali
yalikuwa ni ya Mjerumani mwenzake Von Hambolt. Wataalamu wengine waliokubaliana
na mawazo ya Strier ni pamoja na Idsen, Jolls pamoja na Gao na Xu (2013). Hivyo
basi, fasili ya vikoa vya maana imetolewa na wataalamu mbalimbali kama
ifuatavyo:
1.1Fasili yaVikoa vyaMaana
Resani
(2014) anasema vikoa vya maana ni seti au kifungu cha maneno kilicho katika
mpangilio fulani, au ni seti ya maneno yanayowekwa pamoja kwa njia fulani
hususani kwa kuzingatia uhusiano wa kimaana. Kwa mfano, neno mnyamani kikoa cha binadamu, simba, chui, mbwa, nyati, nyani, sungura na wengine wengi. Kutokana na fasili hii inaonesha udhaifu
kwani haioneshi dhahiri mpangilio wa vikoa kwamba ni kikoa kipi kinaanza na
kipi kinafuatia.
Hambwe
na Karanja (2004) wanasema kikoa cha maana ni mahusiano ya kimuundo ambapo kuna
ufinyu na upana wa maana, ambapo neno moja tu hutumika katika lugha fulani
kutaja kitu ambacho hutajwa kwa maneno mawili au zaidi katika lugha nyingine.
Kwa mfano neno Uncle katika lugha ya
Kiingereza ni neno lenye maana pana ambapo ndani yake hujumuisha maneno menengi
kama vile mjomba, baba mdogo na baba mkubwa lakini katika Kiswahili neno hili
lina maana finyu ambalo ni mjomba. Kutokana na fasili hiyo dhana ya ufinyu na
upana wa maana ni katika idadi ya maana zinazopatikana katika vikoa
vinavyoambatana na kikoa hicho.
Kwa
ujumla, vikoa vya maana ni seti za maneno zenye maana zinazohusiana ambazo
maana zake zinategemeana, na kwa pamoja zinatoa dhana ya kimuundo yenye
uhalisia ndani yake. Kwa mfano mitini
kikoa cha maneno mengine kama mchongoma,
mkaratusi, mparachichi, mchungwa, mwembe, na mingine mingi.
1.2 Uhusiano wa Kiwima na Kimlalo
katika Vikoa vya Maana
Kwa
mujibu wa Resani (k.h.j), vikoa vya maana huweza kuwa na mahusiano ya namna
mbili. Mahusiano ya kiulalo na mahusiano ya kiwima. Mahusiano ya kiwima ni
mahusiano yanayoruhusu maneno kubadilishana nafasi na neno jingine hasa yale
yanayokubali kupokea nafasi hiyo huwa ndiyo yenye maana.
Kwa mfano:
Chakula - ugali, kande, ndizi, wali, tambi
Udongo
- mfinyanzi, kichanga, tifutifu.
Vitafunwa
- maandazi, chapati, bajia, vitumbua, sambusa, kachori.
Vilevile
uhusiano wa kiwima yanayotokea katika vipashio vya tungo. Mahusiano haya uhusu
neno kubadilishananafasi ileile na neno jingine katika tungo. Mathalani, katika
tungo nomino inaweza kubadilishana nafasi na nomino ama kiwakilishi kulingana
na sentensi.
Kwa mfano:Mwalimu
anafundisha Kiswahili
Mwanafunzi anafundishwa Kiswahili
Yule anajifunza Kiswahili
Maji anajifunza Kiswahili
yote anajifunza Kiswahili
Katika
mifano hiyo hapo juu, maneno kamamwalimu,
mwanafunzi na yuleyanaweza kuchukuliana nafasi, hivyo yana uhusiano wima, lakini
maneno maji na yote hayawezi kuchukua nafasi ya maneno ya juu, hii ni kwasababu
hayawezi kubadilishana nafasi.
Vilevile,
mahusiano ya kimlalo ni yale ambayo vipashio huwa nayo kwa kutokea pamoja na
vipashio vingine. Mahusiano haya ni ya kimfuatano au namna yanavyopangana katika
tungo.
Mfano1: Mwanafunzi amechelewa shuleni.
Katikamfano
huo kuna uhusiano kati ya‘mwanafunzi
na mrefu’, ‘chelewa na shule’, ‘mwanafunzi na kuchelewa’.
Mfano 2: Msichana mzuri ameolewa na
mwanaume tajiri.
Katika
mfano huo, mahusiano yaliyojitokeza ni kati ya ‘msichana na mzuri’, ‘msichana na olewa’, ‘olewa na tajiri’.
1.3 Sifa za Vikoa vya Maana
Vikoa
vya maana vina sifa zifuatazo. Kila kikoa kinaweza kuzaa vikoa vingine vidogo
vidogo ndani yake kwa mfano, majira -
vuli,kipupwe,masika,kiangazi. Pia
hakuna kanuni wala mpangilio maalumu wa kupanga vikoa vya maana, yaani
kubainisha ni kikoa kipi kinaanza na kipi kinafuata, kwa mfano; rangi - nyekundu, kijani, blu, njano, nyeusi. Japokuwa kuna vikoa vighahiri ambavyo huenda katika
mpangilio maalumu wa kimfuatano kwa mfano namba, siku miezi na vipimo.
Aidha vikoa vya maana huwa na sifa ya
kuhusiana kwa msingi wa usiganifu yaani maneno huwa na ufanano lakini pia
huweza kuwa na tofauti kwa mfano katika kikoa cha ndege – kuku, kunguru, njiwa,
mwewe.ndege hawa wanasifa zinzofanana [+ndege] lakini wanatofautiana katika
sifa ya [+kufugwa] na [-kufugwa].
2.0 Kiini
Katika
kiini ufafanuzi juu ya umuhimu wa vikoa vya maana umetolewa kama ifuatavyo:
2.1 UmuhimuwaVikoavyaMaana katika
Taaluma ya Maana
Mosi,
Mdee (2010) anaeleza kuwa vikoa vya maana husaidia katika utunzi wa kamusi,
Massamba (2004) kamusi ni kitabu cha orodha ya maneno katika lugha yaliyopangwa
kwa utaratibu maalumu pamoja na maana au fasili zake. Hivyo, kikoa cha maana
kinapoingizwa katika kamusi hutolewa maana kama kidahizo na kuonesha uhusiano
na vikoa vingine vya maana kwa mfano, ndege
ni kikoa cha maana kilichoingizwa kama kidahizo katika kamusi kisha kutolewa
maana na mifano inayohusiana na kikoa hicho, na mifano hiyo huwa ni sehemu ya
vikoa vya ndege na vikoa hivyo huweza kusimama kama vidahizo. Mathalani, katika
TUKI (2004).
Kukunm
ndege anayefugwa na anayefanana sana na kware mkubwa.
Kurumbizanm ndege
mdogo mwenye kichwa cheusi, mgogo na mbawa za.
kahawia,
rangi iliyoiva kifuani na tumboni.
Pili, husaidia kuonesha uhusiano wa
maneno wenye sifa sawa au zinazoelekeana kimaana. Resana (k.h.j), katika kuweka
vikoa vya maana ndani ya kikoa kikuu kimoja kunahitaji kubainisha kama sifa za
kikoa hicho kinaendana na vikoa vinavyoambatana navyo pamoja na maana. Hivyo
basi, vikoa vidogovidogo vya maana vinavyotokana na kikoa kimoja kikuu huwa na
sifa zinazofanana au zinazoelekeana. Kwa
mfano, lazima ujue sifa za kikoa kikuu ni zipi, ambacho ni mti ndipo uweze kutaja au kuorodhesha miti inayojenga kikoa hicho
kama vile mchongoma, mkaratusi, mchungwamzambarau. Kwa ujumla vikoa hivi huchangia sifa
zinazofanana au kuelekeana ambazo ni:


+matawi
+mizizi
+shina
+maua
Tatu,
husaidia kurahisisha mawasiliano, katika mawasiliano matumiaizi ya neno moja
pana linalorejelea maana nyingine ndogondogo, husaidia kuokoa muda baina ya
wazungumzaji.
Mfano 1: mtu anapoandikiwa dawa
na daktari hawezi kuambiwa “nenda ukachukue, paracetamol, albendazol, mucolin, flagil”lakini husema kwa ujumla “nenda ukachukue dawa dirishani”.
Hivyo, dawa imetumika kama kikoa
kikuu chenya vikoa vingine ndani yake vinavyoweza kurahisisha mawasiliano.
Mfano 2: “mama alienda sokoni kununua: vikombe, sahani, bakuli, ndoo, jaginasufuria”, lakini
likitumika neno vyomboambavyo ndiyo
kikoa kikuu, linarahisisha mawasiliano kwa kujumuisha vitu vyote vilivyotajwa.
Nne,
huwasaidia wanaisimu kujua sifa mbalimbali za maneno yanayosigana kimana. Katika
lugha kuna maneno yanayoandikwa sawa na kutamkwa sawa lakini yana maana
tofauti. Hivyo vikoa vya maana vinaweza kumsaidia mwanaisimu kubaini sifa za
maneno hayo na uhusiano wake na vikoa vingine vinavyo husiana navyo.
Kwa mfano maneno yenye utata
kama vile: pamba
kata
kaa
mbuzi
Maneno
hayo huwezwa kuwekwa katika kikoa fulani kwa kuzingatia sifa za kikoa hicho.
Mathalani, ili kujua mbuzi yupo
katika kikoa cha wanyama ni lazima kujua sifa bainifu za mbuzi anayezungumziwa.
Tano,
husaidia kupata kamusi zenye makundi
maalumu. Kikoa cha maana kimoja chenye
maana pana kinaweza kusaidia kupata kamusi mbalimbali kama vile, kamusi ya
wanyama, kamusi ya mavazi, kamusi za vyakula, kamusi tiba ya magonjwa, kamusi
ya misuko ya nywele. Kwani kikoa kimoja cha maana huwa na vikoa vidogovodogo
ndani yake na vikoa hivyo huwa na vikoa vingine.
Sita, hurahisisha michakato ya ujifunzaji
lugha, vikoa vya maana husaidia kumuelekeza mjifunzaji lugha, ili kujua vitu
mbalimbali vilivyowekwa katika kundi fulani. Kwa mfano mjifunzaji lugha huweza
kujifunza kuwa dhana ya neno nafaka
hurejelea, mahindi, uwele, mtama, maharagenangano. Hivyo mjifunzaji lugha
anapotajiwa miongoni mwa vitu vilivyo orodheshwa hapo juu atajua kuwa ninafaka.
3.0 Hitimisho
Kwa
ujumla, dhana ya vikoa vya maana vina changamoto mbalimbali. Kama vile, kuna
baadhi ya vikoa vya maana vina maana zaidi ya moja mfano ndege, kuna ndege kiumbe hai na ndege chombo cha usafiri. Hivyo
kumfanya mtumiaji wa lugha kupata utata wakati wa uainishaji wake hasa muktadha
wa utumizi usipowekwa wazi. Kwahiyo, ili kuondoa changamoto ya upangaji wa
vikoa vya maana ni vyema kujua sifa na uhusiano wa maneno katika lugha.
MAREJELEO
Habwe
J na Karanje P, (2004), MisingiyaSarufiyaKiswahili.
Phoenix Publishers Ltd.
Nairobi kenya
Massamba,
D.P.B (2004) KamusiyaIsimunaFalsafayaLugha,
Taasisi ya Uchunguzi
wa
Kiswahili (TUKI): Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mdee
J. S (2010) NadharianaHistoriayaLeksikografia
TUKI: Dar es Salaam
Resani
M (2014) SemantikinaPragmatikiyaKiswahili.
Karljamer Print Technology:
Dar es Salaam, Tanzania