@masshele swahili
.Utangulizi
Kazi hii tutaijadili katika sehemu kuu tatu ambapo sehemu ya kwanza ni utangulizi ambapo tutafasili dhana mbalimbali zilizojitokeza katika swali. Sehemu ya pili ni kiini ambapo tutafafanua dhana ya Lingua franka, Pijini na krioli. Mwisho ni hitimisho la swali.
www.masshele.co.tz
1.1Dhana ya Lingua Franka
Iribemwangi na wenzake (2011), wanafasili kuwa ni dhana inayotumiwa kutajia lugha inayotumiwa na jamii au watu ambao lugha zao za kwanza ni tofauti. Hali hii inaweza kuelezeka kama ile ya lugha kuwaleta pamoja wanajamii fulani husika kimawasiliano. Hivyo basi lingua franka ni lugha unganishi kwa watu ambao hapo awali walikuwa na lugha tofauti tofauti.
Aidha King’ei (2010), anadai kuwa lingua frankani jina linalotokana na lugha iliyoitwa hivyo ambavyo ilitumika katika eneo la Mediterranean katika karne ya 10-15. Lugha hiyo ya kibiashara ilitumika sana katika bandari za bahari hiyo na ilijumuisha maneno na miundo kutoka katika lugha za Kifaransa, Kispaniola, Kigiriki na Kiarabu. Mfano Pamoja na kiswahili ambacho hutumiwa katika maeneo ya Afrika mashariki na kati, kihausa ambacho hutumiwa katika maeneo ya Afrika Magharibi na Kiingereza ambacho hutumika maeneo mengi ya ulimwenguni . Hivyo, Lingua frank ni lugha inayotumika katika kuwaunganisha wati wenye lugha mbili tofauti kwenye mawasiliano.
Kwamujibu wa Onyango (2002) anaeleza kuwa lingua franka ni lugha inayotumiwa na watu walio na lugha tofauti kwaajili ya mawasiliano. Kwamfano lugha ya KKiswahili katika maeneo ya Afrika mashariki.
1.1.1Aina za Lingua Franka
Kwamujibu wa Iribemwangi (2011), ameonesha aina kadhaa za Lingua Franka kama zifuatazo;
a)Kiswahili, ambapo ni lugha inayotumika katika maeneo ya Afrika Mashariki na kati.
b) Kihausa, ambapo hutumiwa katika maeneo ya Afrika Magharibi kama Ghana na Nigeria.
c)Kiingereza, ambacho hutumika katika nchi nyingi ulimwenguni.
d)Kiarabu, Hutumiwa kama lingua franka katika maeneo ya Afrika Kaskazini na pia katika mahubiri ya Dini ya Kiislamu.
e)Kireno, ambapo lugha hii inatumika katika mataifa kama Ureno, Brazili, Macau, Angola, Mozambique, Cape Verde na Umoja wa mataifa.
Mbali na aina hizi za Lingua Franka ( k.h.j),anasema zipo aina nyingine za lingua franka ambazo tunaweza kusema kuwa si halisi nazo ni pamoja na lugha bandya.
1.1.2Sababu za Kuzuka kwa Lingua Franka
Zipo sababu tofauti tofauti, ambapo kwa mujibu wa Iribemwangi (2011), ametoa sababu zifuatazo:
Lingua Franka huibuka kwa sababu ya Hali ya kutaka ushirikiano. Ushirikiano unaotafutwa kupitia Lingua Franka ni ule wa kisiasa, kibiashara, kiutamaduni na kielimu. Mfano Tukirejelea kiswahili lugha hii imetumika katika kujenga, kuendeleza na hata kudumisha uchumi, biashara na umoja miongoni mwa watu wa Afrika Mashariki.
Aidha Lingua franka huzuka kutokanana kuleta umoja miongoni mwa watumiaji wake. Hii humaanisha kuwa miongoni mwa watu walio na utamaduni mbalimbali, lingua franka ndiyo inayotumika kuwaleta pamoja.
1.1.3 Sifa za Lingua Franka
Sifa hizi zinatambulisha na kuzitofautisha na lugha nyinginezo. Iribemwangi (2011) anataja sifa zifuatazo:
Lingua Franka zinamatumizi ya kimawasiliano ambayo huwa ni ya eneo pana la kisiasa na kijamii na ambalo huwa na makabila mbalimbali.
Aidha lingua franka yaweza kuwa lugha ya kwanza ya mzungumzaji au lugha ya pili na kwa wazi wengine lugha ya kigeni.
Hukiuka mipaka ya kiutamaduni.
Hukiuka mipaka ya kimaeneo inaweza kutumiwa katika maeneo mapana.
Pia hutumiwa na watu ambao mama zao ni tofauti.
Kwamujibu wa Onyango (2002) anataja sifa kadhaa za Lingua franka, Baadhi ya sifa hizo ni kama zifuatazo;
Huwa ni lugha ya mawasiliano kati ya watu wenye lugha zaidi ya moja
Huweza kuwa lugha ya kwanza au lugha ya pili ya mzungumzaji na wengine yaweza kuwa lugha ya kigeni.
Huimarika na baadae kuwa lugha ya kimataifa.
Hukutanisha watu wenye asili mbalimbali.
1.1.4Jinsi lingua Franka inavyoenea
Iribemwangi (2011), anaeleza jinsi Lingua Franka inavyoweza kuenea kupitia mambo mbalimbali, baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo;
Vita, mfano kupitia vita lugha ya kigiriki iliweza kuenezwa. Pia Kifaransa kiliweza kuenea hasa enzi ya utawala wa Napoleon Bornaparte. Pia katika lugha ya kiyunani iliweza kuenea kupitia vita, ambapo tawala zilizoshindwa zililazimika kutimia lugha ya mtawala wao mpya. Hivyobasi kupitia vita lingua franka iliweza kuenea maeneo mbalimbali.
Biashara, kupitia njia hii lingua franka huwezwa kuenezwa . Mfano Lugha ya Kiswahili na kihausa zimeweza kuenea kutokana na dhima zao za Kibiashara. Hivyo sio ajabu kupata watafiti kadhaa wakiziita Lingua franka kwa lugha za biashara.
Shughuli za Kikoloni, Lugha za Kifaransa, Kiingereza na Kireno zimeweza kuenea kupitia kwa nyenzo hii ya ukoloni.
Shughuli za Kisiasa, lugha ya luganda nchini uganda imeweza kuenea kutokana na nguvu kisiasa za watu wa Buganda.
Elimu, kama lugha ya kiingereza imeweza kuenea kupitia elimu.Hali hii inawezekana katika maeneo ambapo lugha fulani hutumika katika kutolea mafunzo.
Nguvu ya sayansi na teknolojia, kwa Marekani na Uingereza shughuli za Sayansi na teknolojia zimechangia kuenea kwa lugha ya kiingereza kote ulimwenguni hasa istilahi mpya zinazoibuka kila uchao.
Pijini
Massamba na Wenzake (2009),wanafasili Pijini wakimnukuu Decamp (1971) na Hall (1972), wanasema kuwa ni lugha yenye mfumo uliorahisishwa sana ambao hutumiwa na wazungumzaji wenye lugha tofauti katika mazingira maalum baina yao na kwamba pijini siyo lugha mama kwa mzungumzaji yeyote. Aidha kuhusu mazingira ndiyo kichocheo cha kuzuka kwa lugha za Pijini.
Wanaisimu- jamii wengi wanalubaliana kuwa Pijini ni lugha iliyozuka katika miktadha ya kibiashara na biashara ya Utumwa. Kama asemavyo
Kwa ujumla Pijini ni lugha ambayo huzuka pale ambapo makundi mawili ya watu wenye lugha mbalimbali yanapokutana na haja ya mazungumzo kutokea. Mara nyingi ni lugha zakibiashara hasa.
2.1Asili ya neno Pijini
Wataalamu mbalimbali wamejaribu kueleza Asili ya neno Pijini . Iribemwangi na wenzake (2011) amweleza masuala ya fuatayo
Pijini imetokana na matamshi mabaya ya Kichina kutoka neno la kiingereza “Business” ( biashara), yaani utohozi wa neno business na kuzalisha neno Pidgin kwa hali hii inachukuliwa na kushikiliwa kuwa imetokana na mainhiliano ya kibiashara.
Yapo madai kuwa neno Pijini limetokana na lugha mojawapo ya Marekani Kusini inayojulikana kama “Yayo” ambapo inayo neno Pidian lenye maana ya watu, japo neno hili linakaribiana na neno Pijini lakini si dhahiri katika mfungamano wa maneno haya.
Ipo nadharia tete nyingine kuhusu chanzo cha neno Pijini ambayo inaeleza kuwa linayokana na jina la ndege aitwaye Pigeon.
2.2 Sifa za Pijini
Kwa mujibu wa King’ei (2010) ameeleza sifa za lugha ya Pijini kama zifuatavyo;
Siyo lugha asilia kwa jamii yoyote bali lugha ya mawasiliano kwa jamii zenye lugha zao asilia.
Pijini ni lugha hafifu yenye kujumuisha miundo michache ya sarufi na misamiati kutokana na lugha moja au lugha kadha za jamii zinazoingiliana.
Masamba na wenzake (2009) wameeleza sifa zifuatazo;
Asili yake ni mazingira maalumu ya mchanganyiko au mwingiliano wa jamii lugha mbalimbali zisizokuwa na uhusiano wa karibu.
Kutokana na kuishi kwa pamoja kwa jamii hizi kwa muda mrefu, hivyo lugha za Pijini ndio huzuka .
b)Ina mfumo wa lugha sahili
Ina sarufi iliyo sahili, Yaani inatumia maneno machache sana kwa madhumuni ya mawasiliano sahili ile kukidhi haja ya wazungumzaji wa Pijini na Krioli, kwa mfano neno “Spit” kutoka Pijini ya Chinese Pidgin English (CPE) lina maana ya “kutema” au “kutapika” , Metanesian Pidgin English neno “Gras” kutoka Pijini ya (MPE) lina maana ya kitu chochote kinachoota ardhini au kitu chochote kinachoota mwilini mfumo wa MPE ni mfano wa Pijini iliyosanifiwa na ina matumizi mapana , pia huyumika miongoni mwa wanajamii lugha ya New Guinea, kwa kuzingatia hoja kuwa ina maana nyingi za Kikoa , neno Gras lina maana ya majani, mimea, ndevu, au manyoya.
c)Hutumika zaidi katika mawasiliano yasiyo rasmi( Haina matumizi mapana)
Hi ini kwasababu pijini hazijasanifiwa kwa asilimia kubwa , mfano katika shughuli za kibiashara inazokutanisha watu wenye lugha tofauti, kama enzi ya wakoloni biashara kati ya waarabu na waafirika mifano katika sifa za pijini ni pamoja na kwamba Pijini siyo lugha asilia kwa mfano pijini ambayo haitokani na lugha za Ulaya unatoka Indonesia inayoitwa Bazaar ilitokana na lugha za asili za Asia iliyotumiwa zaidi katika masuala ya kibiashara , pia Pijini yenye asili ya Afrika inayoitwa Fanakalo inayotumiwa Afrika ya Kusini mifano hi ni kwa mijibu wa Hall (1982).
Krioli
Kwa mujibu wa Iribemwangi (k.h.j) wanaeleza kuwa mara kwa mara wazungumzaji wa lugha za Pijini huweza kuzitupilia mbali lugha zao asilia na badala yake wao wakazichukua hizo lugha za pijini na kuanza kuzitumia katika kuziendeleza shughuli zao za kila siku, hivyo lugha hiyo ndiyo huitwa Krioli. Krioli ni lugha ni lugha inayotokana na lugha za Pijini yaani hapawezi kamwe kuwa na lugha za Krioli bila kuanza kutanguliwa na lugha za Pijini. De camp na Hall (1982), Krioli ni lugha mama zinazotumiwa na wazungumzaji wazawa ambao kihistoria wametokana na jamii lugha ya pijini. Aidha kuna maneno mengine wazungumzaji wakuu wa lugha za Krioli kama lugha zao za kwanza walizojifunza nyumbani.
Hitimisho
Dhana ya Pijini, Krioli na Lingua Franka zina umuhimu kwani zote kwa pamoja zimeweza kuwa na mchango mkubwa katika lugha ambapo Pijini husaidia wanaisimu jamii kuzielewa jamii lugha hizi katika muktadha wa kihistoria, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Aidha Pijini humwezesha mwana isimu jamii kuchunguza mfumo wa lugha kimofolojia, kimuundo pamoja na msamiati unaotumiwa na wanajamii lugha wenyewe
.
Marejeleo
De camp, D (1971). " Introduction to The Study of Pidgin and Create Language" In D Hymes (eds) Pidginization and Creolization of Language, 13_39. Cambridge : Cambridge University.
Hall, R.A ( 1982). " Pidgin and Creates as a Standard language" In J.B Pride and J.Holmes ( eds) Socio Linguistics. Harmondsworth: Penguin Book ltd.
Hall,R.A (1953). " Haitaian Creole Grammar, Texts Vocabulary" American Anthropological Association Memoic No.74.
King'ei, K ( 2010). Misingi Ya Isimu Jamii. Dar_es_ saalam : Taasisi Ya Taaluma Za Kiswahili.
Massamba na Wenzake ( 2001). Sarufi Miundo Ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo ( SAMAKISA). Dar es saalam: Taasisis ya Uchunguzi Wa Kiswahili .
Mekacha, R.D.K ( 2000). Isimu Jamii: Nadharia na Muktadha Wa Kiswahili. Osake University Of Foreign Studies.
Msanjila, Y.P (1990) " The Role and Status Of Ethnic Group in Tanzania" In Kiswahili. 57.46_ 54
www.masshele.blogspot.com