E.Mashele 2019
Je usayansi na usanaa unaotajwa katika utunzi wa kamusi niupi?
karibu katika makala haya twende zote hadi mwisho iliuweze kung'amua usayansi na usanaa uliopo katika utunzi wa kamusi.
Katika makala kadhaa tumekwisha kuona maana ya kamusi, historia ya kamusi, na lexikografia kwa ujumla hivyo mambo hayo hayatajadiliwa hapa sana.
Kwanza tuangalie maana ya dhana hizi mbili ndiposa tuwe na uelewa juu ya dhana hizo.
Dhana yasansi
Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa
Dhana ya sanaa
Sanaa ni ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya akiliyake.
Vilevile sanaa ni uzuri unaojiibua katikaumbo lililosanifiwa.
Kusanifu ni kuumba, kufanya jambo au kitu kwa kutumia ufundi/ustadi ili kiweze kuvutia watu kwa uzuri wake. Mtu hueleza hisia zinazomgusa kwa kutumia umbo fulani ambalo limesanifiwa.
Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemewa ioneshe ufundi wa hali ya juu ili iwe na mvuto kwa hadhira yake.
Tunaweza kuona kazi ya sanaa kupitiatanzu za fasihi, uchoraji, ususi, ufumaji,utarizi, uchongaji, ufinyanzi na kadhalika.
katika kuangalia usayansi na usanaa tutajikita katika mchakato mzima wa kuanza kubuni, kutunga, hadi kutengeneza kamusi. Kwa mintarafu hiyo ndipo tutaweza kung'amua hizo dhana.
USAYANSI KATIKA UTUNGAJI WA KAMUSI
>Ufanyaji utafiti (research)
kuhusiana na fani ya kamusi ambayo mtunga kamusi anayo kusudia au utafiti ilikujua maneno magumu ambayo atayaingiza katika kamusi
> Uingizaji wa taarifa za kiisimu za kidahizo katika kamusi.
> Ufundi wa uundaji wa vidahizo vitakavyo tumika katika kamusi hasa za kisayansi na kiteknolojia rejelea kamusi ya kahigi na wenzake ya teknolojia window PX 2004
> Ukusanyaji wa vidahizo na taarifa nyingine za msingi (data collection)
> Uchunguzaji wa matumizi ya maneno au vidahizo katika jamii.
USANAA KATIKA UTUNGAJI WA KAMUSI.
> Uteuzi wa msamiati wa kamusi. Kuteua msamiati wa kamusi nikuchagua maneno ambayo ama kwa hakika ndiyo mtunga kamusi anamapenzi nayo katika kuyaingiza katika kamusi aliyo kusudia kutunga. Vigezo vya kuteua msamiati wa kamusi hutegemea malengo ya kamusi iliyo tungwa. Katika uteuzi huu mtunga kamusi huteua maneno anayo yapendelea kulingana na kamusi aliyo amua kutunga, hivyo tunaweza kusema maneno anayo amua kuyateua mtunga kamusi yamepata kibali miongoni mwa maneno mengi yaliyopo katika lugha , kwa mintirafu hiyo maneno nayo yamemvutia na ndio usanaa wenyewe.
> Mpangilio wa maneno katika kamusi; hapa ni namna maneno yanavyo orodheshwa katika kamusi. Na huweza kupangwa kwa kuzingatia mpango wa alfabeti au mpango wa kikoa leksimu.
Mpango wa kialfabeti; Maneno yenye kuanza na herufi ya alfabeti ya aina moja hupangwa pamoja kwa utaratibu huu, maneno yote yanayoanza na herufi moja, mathalani herufi A, huwekwa katika orodha moja.
Kikoa leksimu , kikoaleksimu ni kundi la maneno yenye uhusiano wa kimaana.
Kwavipi ni sanaana? Kwasababu huu ni ustadi anaoweza kuuchagua mtunga kamusi kulingana na mapenzi yake kwanamna atakayoonelea itamrahisishia na kumvutia msomaji wa kamusi.
Usanaa mwingine
> matumizi ya rangi
>Matumizi ya picha
>Uteuzi wa jina la kamusi
>uingizaji wa taarifa za kietimolojia na nk.
Mwisho
www.masshele.blogspot.com