Mbwa mmoja nchini Kaskazini mwa Thailand amemuokoa mtoto mchanga aliyekuwa amezaliwa baada ya kuzikwa hai anayedaiwa kuzikwa na mwanamke mwenye umri mdogo.
Mwili wa mtoto huyo mchanga wa kiume unasemekana ulikuwa umezikwa na mama mwenye umri wa miaka 15, ambaye alikuwa amewaficha wazazi wake ujauzito.
Mbwa kwa jina Ping Pong alionekana akiwa anabweka na kuchimba ardhini kwenye shamba katika kijiji cha Ban Nong Kham.
Mmiliki wake anasema aliposogelea mahali alipokuwa ndipo alipoona mguu wa mtoto mchanga ukitokezea juu ya ardhi.
Wanakijiji walimkimbiza mtoto hospitalini ambako madaktari walimuogesha na kutangaza kuwa alikuwa mzima wa afya.