Saturday

Karne ya 21 na maajabu yake katika kuikuza Biashara yako.

0 comments



Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) inakua kwa kasi sana ulimwenguni hasa katika karne hii ya 21. Maendeleo haya ya TEHAMA, yamekua chachu ya maendeleo kwawale walio zinduka na kuitumia Teknolojia hii katika kujinufaisha kiuchumi, kisiasa, kitamaduni na kijamii. Na ama kwa hakika mapinduzi ya Teknolojia hii yamewanufaisha wengi, kwa kukuza uchumi wao, na kurahisisha kazi zao na hata nathubutu kusema wanaweza kujiingizia kipato hata wakiwa wamelala au wakiwa wagonjwa.

Swali la kukiuliza wewe mtanzania Teknolojia ya habari na mawasiliano inakusaidiaje katika biashara yako?
Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua kwamba bado wafanyabiashara walio wengi wanaendesha biashara zao kizamani sana, na ndiposa unakuta tunatumia muda mwingi katika kuziendesha biashara hizo bila kuwa na tija. Huku tukiendelea kulalama hali mbaya ya uchumi kilakukicha.


TEHAMA inavyo weza kukusaidia katika biashara zako.
1. Kutafuta Masoko/Wateja. Kwamujibu wa TCRA, watumiaji Wa internet wanaongezeka kila kukicha na takwimu zilizotoka hivi karibuni zinaonesha zaidi ya watanzania milioni 27 wanatumia internet ambayo ndiyo kitovu cha TEHAMA, kumbe basi iwapo utatafuta Wateja kupitia mtandao utakutana na lundo la watu kuliko kujizungusha katika eneo ulilopo ambalo kwahakika hutaweza kukutana na Wateja wapya. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii unaweza kutangaza bidhaa zako na ukapata Wateja wakutosha kulingana na eneo ulilo lenga. Unaweza kutumia WhatsApp businesse, au makundi ya kibiashara ya Facebook au hata kulipia matangazo katika mitandao mbalimbali.( Makala ijayo tutachambua kwa kina namana unavyoa weza kuyafanya haya)


2. Kufanya utafiti kuhusu biashara unayotaka kuianza :
Kupitia Teknolojia hii inakupa fursa kwako wewe mfanyabiashara kung'amua ni biashara gani unayoweza kuifanya kulingana na nchi uliyopo ambayo itazingatia uhitaji hivyo kukurahisishia kupata masoko kwa urahisi na kufanya biashara yenye tija.
Aidha utafiti huu unaweza kuuendesha kupitia online survey na google form ambazo utazitumia kukusanya maoni kuhusu biashara unayotaka kuianza.


3. Kutafuta ujuzi kuhusu biashara yako.
Kupitia maendeleo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano, mfanyabiashara unaweza kujifunza mambo mbalimbali mtandaoni ndiposa, uweze kuiboresha biashara yako.
Ili uweze kuiendesha biashara yako kisasa zaidi hunabudi kutafuta kuhusu biashara yako katika mitandao kama vile youtube.com, na google.com, ambapo utatafuta machapisho yanayoendana na biashara yako mfano kama wewe no mzalishaji na muuzaji Wa sabuni basi unaweza kutafuta namna yakuweza kuzalisha sabuni zenye ubora, vilevile unaweza kutafuta namna ya kupata masoko kiurahisi nambinu nyinginzo za kibiashara ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kuboresha biashara ile unayo ifanya. Kumbuka kuwa biashara yoyote bila maboresho itapoteza mvuto na huweza kupungua Tina ama kufa kabisa hivyo mfanya biashara huna budi kujifunza kila uchao namna ya kuweza kuboresha biashara yako.

4. Kutafuta bidha/kuagiza bidhaa kwaajili ya Wateja wako
Yapo makampuni makubwa ambayo wewe mfanyabiashara unaweza kutafuta kwa kupitia TEHAMA na ukaweza kupata bidhaa za kuwauzia Wateja wako tofauti na ilivyo zoeleka kwa weng mfano mfanyabiashara wa simu za mkononi kusafiri hadi China kufata mzigo, badala ya kuagiza ambapo yapo makampuni kwa ajili ya kazi hizo. Vilevile kama wewe mfanyabiashara unajihusish na utengenezaji Wa bidhaa basi TEHAMA unaweza kukusaidia kutafuta malighafi kwaajili ya utengenezaji huo na kukurahisishia kabisa biashara yako.


5. Kuhifadhi taarifa za Wateja na kuwakumbusha kila bidhaa Mpya zinapo ingia.
Mapinduzi ya TEHAMA tunaweza kusema kuwa yamekuja kuiunganisha jamii pana iliyokuwa imetawanyika na kupitia TEHAMA tunaweza kuungana tena. Mfanyabiashara unaweza kutumia mifumo mbalimbali ya kisasa na kuweza kuifadhi mawasiliano ya Wateja wako kama vile pepe zao, namna zao za simu na masanduku yako ya barua , ambapo unaweza kuwakumbusha kwa kuwaandikia ujumbe kuwa bidhaa Mpya zimeingia na hivyo kuwahamasisha kurudi tena kutafuta bidhaa kwako na hiyo itakutengenezea Wateja wakudumu na wanao kuamini , na kwa mintirafu hiyo unaweza kuuza bidhaa nyingi na biashara yako itakua kwa kasi.

Mwisho mafanikio ya biashara yako katika karne ya 21 yapo katika ubunifu wako na usasa wako.

Endapo utang'ang'ania ukale katika kuendesha biashara zako kila kukicha utasalia kulalama tuu huku ukiwaona kina Jacky Maa wakitusua tu na kufanya biashara zako kuwa za kiulimwengu. Ifike mahali kupitia TEHAMA na sisi watanzainia tuweze kuuza bidhaa zetu popote Duniani. Tukutane katika makala ijayo

Kama unaswali, maoni, unahitaji ushauri, unawazo na hujui pakuanzia tubadilishane mawazo.....
 nitafute katika barua pepe
info.masshele@gmail.com

No comments:

Post a Comment