Sunday

MAWAZO NI YA MWANDISHI KITABU NI CHA MHARIRI

0 comments
Machine ya kale ya uchapaji , picha na mtandao
Na
E.Mashele
Ifo.masshele.gmail.com

Karibu ndugu msomaji, leo tutajadili mada hii ambapo mwishoni ninategemea utakuwa na uelewa wakutosha kuhusu nani hasa mmiliki Wa kitabu kati ya mwandishi na mhariri.

Mwandishi ni yule anaye buni wazo, kulifanyia utafiti, kubadili was kuwa mswada, kutafuta kampuni ya kumchapishia na kuchapa kitabu chake, kuingia mkataba, kushirikiana na mhariri katika kuhariri mswada, kupokea mashauri mbalimbali kuhusiana na mswada wake, na kushiriki katika utangazaji na uuzwaji Wa kitabu chake.

Mhariri ni yule mwenye jukumu la kutafuta mswada, kuhariri mswada, kunyoosha lugha, kuandaa mikataba, kuhariri maudhui, kumshauri mwandishi, kuwa kiungo muhimu kati ya mwandishi na kampuni ya uchapishaji  na kupendekeza ikiwa mswada uchapishwe au usichapishwe.
Aidha wakati mwingine mhariri  analo jukukumu la kutafiti masoko.

USHIRIKIANO KATI YA MWANDISHI NA MHARIRI.

Pamoja na majukumu na uwezo mkubwa alionao mhariri katika mswada , mhariri analazimika kushirikiana na mhariri katika kila hatua anayopiga katika mswada.
Mhariri haruhusiwi kuondoa kipengele katika mswada bila kumshirikisha MWANDISHI.

Aidha mhariri anapaswa kuulinda mswada wamhariri na ikitoke mhariri akiupoteza mswada atatakiwa kuingia garama zote za utoaji wa nakala ya mswada mwingine.

KAMA MSWADA UTAKATALIWA.
ikiwa mhariri atapendekeza kutokubaliwa kwa mswada haina maana kuwa mswada huo unaweza kukataliwa katika matlaba au kampuni nyingine ya uchapishaji hivyo mswada unapokataliwa mhariri anapaswa kuurudisha mswada huo kwa mwandishi. Uaminifu, ushirikiano na uwazi ni miongoni mwa mambo yanayotakiwa kuwepo kati ya mhariri na MWANDISHI.

Swali la kujiuliza nikwamba ikiwa mhariri ndiye mwenye jukumu la kupendekeza mswada uwe kitabu au ukataliwe je yeye ndiye awe mmiliki Wa kitabu?

Swali la pili, kama mhariri ndiye atakaye tuhumiwa katika makosa yote yatakayo patikana katika kitabu je yeye ndiye awe mmiliki Wa kitabu?

Swali la tatu, kama kitabu kitakosa soko au kampuni kuingia hasara mhariri ndiye anaye wajibishwa je mhariri ndiye awe mmiliki Wa kitabu?

Swali la nne turejee kwa mwandishi Ngugi amabaye wahariri wengi waliikimbia miswada yake kutokana na hofu ya nguvu ya dola, kwa mintirafu hii nikwamba kama wange kubali kuhariri halafu wakakubali kazi hizo zichapwe wangeanguka mikononi mwa dola je katika hali hii tuwamilikishe wahariri kitabu?

Swali la tano
Wakati mwingine mhariri analo jukumu la kumtafuta mwandishi na kumwambia aandikie jambo ghani kulingana na mahitaji ya kampuni je mhariri amiliki kitabu?


Baada ya kujibu maswali hayo tayari utaweza kuzungumza kitu kulingana na mjadala.

Hitimisho

Kwa ujumla mchakato Wa utoaji wa kitabu unatokana na ushirikiano imara kati ya Mwandishi, Mhariri na kampuni.




No comments:

Post a Comment