Wednesday

Taaluma ya Tafsiri na sifa za mfasiri bora na mbinu za tafsiri

0 comments





Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu nne, sehemu ya kwanza ni utangulizi ambapo dhana ya tafsiri na mfasiri zitafafanuliwa kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, sehemu ya pili ni kiini cha swali ambapo sifa za mfasiri bora zitafafanuliwa na sehemu ya tatu ni hitimisho na sehemu ya nne ni marejeleo.
Tafsiri imefasiliwa kuwa, ni kutoa mawazo kutoka katika lugha moja kwenda lugha nyingine bila ya kubadilisha maana. (TUKI 2002). Ikiwa Mwansoko na wenzake (2006), wanafasili tafsiri kuwa ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja(lugha chanzi) kwenda lugha  nyingine (lugha lengwa). Hivyo ili kufanikisha shughuli ya tafsiri ni lazima mambo mawili muhimu yazingatiwe. i, Mawazo yanayoshughulikiwa ni sharti yawe katika maandishi na si vinginevyo. ii, Mawazo kati ya lugha chanzi na lugha lengwa  sharti yalingane. Kwa ujumla tafsiri huweza kufafanuliwa kama zoezi la uhamishaji wa ujumbe ulio katika maandishi toka lugha moja kwenda lugha nyingine.
Mfasiri ni nani? Ni mtu yeyote anayejishughulisha na kazi za kutafsiri. Ni mtu mwenye taaluma au ujuzi wa kutafsiri na ambaye anajishughulisha na kazi hizo (weledi-Professionalism). Katika mchakato mzima wa kutafsiri ni lazima awepo mfasiri ambaye hubeba sifa muhumi ambazo humwezesha kufanikisha mchakato wa kutafsiri. Hivyo mfasiri bora anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
  Awe mahiri wa lugha husika, hii ina maana kuwa awe anajua kwa ufasaha lugha zote mbili, yaani lugha chanzi na lugha lengwa. Hii ni kujua vizuri nyanja mbalimbali za Isimu ya lugha husika kama vile; Fonolojia-{Matamshi}, Mofolojia-{Maumbo}, Sintaksia-{Muundo} na Semantiki-{Maana}. Kwa mfano mfasiri anayetaka kufasiri ujumbe ulio katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili hana budi kuzifahamu vema lugha hizi katika Nyanja na taaluma mbalimbali, jambo ambalo litasaidia kuzalisha ujumbe ulio bora  na wenye kujitosheleza katika maumbo yote.
  Awe na ufahamu mkamilifu wa ujumbe au mada iliyoandikwa katika matini chanzi na uwezo au jinsi ya kuelezea ujumbe au mada hiyo kwa ufasaha katika lugha lengwa. Mtesigwa (2006) anaeleza kuwa sifa hii itamsaidia mfasiri kuifanya kazi kwa kujiamini Zaidi na kwa kuichanganua kwa kila kiwango mada anayoshughulikia. Hivyo ni vema mfasiri aielewe vema mada anayokwenda kuifanyia kazi.
  Awe mjuzi wa TEHAMA. Kutokana na mbadiliko ya sayansi na teknolojia, mfasiri hupaswa kubadilika kulingana na mabadiliko hayo yanayoendele katika jamii. Taaluma ya tafsiri hubadilika pia kulingana na maendeleo ya teknolojia katika jamii, huvyo mfasiri akiwa mjuzi katika taaluma ya teknolojia, habari na michezo atarahisisha zoezi zima la kuafsiri matini mbalimbali.
  Awe na tajiriba kubwa ya usomaji wa aina mbalimbali za tafsiri na kujiendeleza kulingana na mabadiliko ya kijamii. Mfasiri akiwa na tajiriba kubwa kyuhusiana na taaluma ya tafsiri ndani nan je ya nchi itapelekea kuongezeka kwa ujuzi katika ufanisi wa kazi zake za tafsiri. Usomaji wa kazi mbalimbali za tafsiri husaidia kuona mapungufu na kuyarekebisha. Hivyo jambo hili hupeleka uzalishaji wa mfasiri bora ndani ya jamii.
Mfasiri pia hana budi  kufahamu vizuri watu, jamii na utamaduni wa watumiaji wa lugha chanzi na lugha lengwa. Kuifahamu vema jamii ambayo kwayo mfasiri anafanya kazi yake kutasaidia kubaini taratibu za jamii hizo na kutafuta mbinu bora ya kufasiri kazi endapo kutakuwa na tofauti mbalimbali za kiisimu ambazo zinaweza kujitokeza wakati mfasiri anapofanya kazi yake.
Vilevile mfasiri bora hana budi kuwa mwaminifu, Mwansoko (2006) anasema kuwa, japo tafsiri hufanywa  na mfasiri lakini bado kazi itakayomfikia msomaji inapaswa iwe kazi ya mwandishi. Mfasiri amemsaidia mwandishi kuufikisha ujumbe wake kwa kutumia lugha aliyochagua mfasiri. Maudhui yaliyomo katika mada pamoja na uzito na mpango vinapaswa vifasiriwe kama mwandishi alivyoviandika.
Kwa ujumla mchakato wa kutaafsiri hauwezi kukamilishwa pasipo kuwa na mfasiri bora ambaye ana sifa ambazo zimekwisha kujadiliwaqa katika kiini cha swali. Hivyo basi mfasiri hana budi kuongeza maarifa katika taaluma ambayo anaifanyia kazi kwa lengo la kupata kazi iliyobora ndani ya jamii, kurahisisha mawasiliano, kukuza lugha na kuburudisha jami.




MAREJELEO
Mwansoko H. J. M (20O6) Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na Mbinu. Dar es Salaam:
                                             Taasisi   ya Uchunguzi  Wa Kiswahili
TUKI (2012) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam



No comments:

Post a Comment