Iks UDSM
Fasihi Simulizi ni nini?
Wataalamu mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu maana ya FS. Miongoni mwao ni Finnegan (1970), Matteru 1979), Balisidya (1983), Okpewho (1992) na wengineo wengi. Ili kuweza kubaini maana ya FS ni vema kudurusu fasili zilizotolewa na wataalamu hawa. Lengo hasa ni kutaka kufahamu ubora na udhaifu wa fasili zao, hatimaye tuweze kuunda fasili muafaka zaidi kuhusu maana ya FS.
F.S yaweza kuelezwa kwamba, hutegemea msanii ambaye huiumba kwa maneno katika tukio maalum (Finnegan, 1970)
Ni fasihi inayotegemea mdomo ktk kutolewa na kuenezwa kwake,……. (M.LMatteru,
1979)
Ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa waasikilizaji na watumiaji waake (Balisidya, 1983)
F.S humaanisha fasihi itolewayo kwa neno la mdomo…… (Okpewho, 1992)
F.S ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kazi hii ya sanaa huhifadhiwa kwa kichwa na kusambazwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo,….. (M.Msokile, 1992)
Ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia mdomo na vitendo bila kutumia maandishi (Mulokozi, 1996)
Neno F.S linamaanisha hadithi za jadi, nyimbo, mashairi, vitendawili na methali ambavyo hutolewa kwa neno la mdomo (Bukenya na Wenzake, 1997)
Sanaa hii iitwayo Fasihi, inaweza kuhifadhiwa kwa njia kuu mbili: kwa njia ya mdomo na kimaandishi. Aina ya kwanza, ambayo tunajihusisha nayo katika sehemu ya kwanza inajulikana kama F.S (Wamitila, 2003)
1
Fasili hizi hazigusii lolote kuhusu matumizi ya nyenzo za sayansi na teknolojia katika kubuni, kutongoa na kuhifadhi sanaa husika. Nyenzo kama vile, Radio, Video, DVD,
VCD,, Televisheni, Kompyuta na Wavuti….. kwa sasa zinatumika katika kutolea na kurekodia tanzu za F.S kama vile hadithi……
Katika F.S fanani na hadhira huwapo ana kwa ana: dhana ya kuwapo ana kwa ana pia inahitaji mjadala (uwezekano wa kuwa na aina mbalimbali za hadhira)
UAINISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
Utata umekuwa ukijitokeza katika uanishaji na ugawaji wa tanzu na vipera vya FS. Utata huu unatokea kutokana na kutofautiana kwa vigezo vinavyotumiwa na wataalamu mbalimbali katika ugawaji huu, kwani kila mtaalamu hutumia vigezo vyake kulingana na matakwa ama mtazamo wake. Hebu sasa tuwatazame baadhi ya wataalamu ambao wameainisha tanzu za FS, tukiangalia pia udhaifu na ubora wa vigezo walivyotumia
A M .L. BALISIDYA (MATTERU) (1987)
Anagawanya FS katika tanzu tatu ambazo ni NATHARI, USHAIRI na SEMI. Katika kila utanzu kuna vipera vyake mbavyo navyo vina vijipera pia. Uainishaji wake ni kama ifuatavyo:
NATHARI
Ngano
Istiara
Hekaya
Kwanini na kwa namna gani
kharafa
Tarihi
Kumbukumbu
2
Shajara
Hadithi za historia
epiki
Visasili
Kumbukumbu
Tenzi
Kwanini na kwa namna gani
USHAIRI
Nyimbo
Tahlili
Bembea
Tumbuizo
Ngoma
Mwiga
Watoto
kwaya
Maghani
Majigambo
Vijighani
Shajara
tenzi
SEMI
Vitendawili
Kitendawili
Mizimu
mafumbo
3
Methali
Msemo
nahau
Misimu
Utani
Masaguo
soga
Upungufu wa uainishaji huu
Katika uainishaji wake huu, baadhi ya tanzu hazionekani ama tunaweza kusema zimeachwa kabisa. Mfano visakale, ngomezi,
Balisidya anauweka utenzi kuwa ni kipera cha visasili katika kundi la nathari. Hapa anaibua mjadala kwani kama tujuavyo kuwa utenzi katika FS huhusisha uimbaji pia. Hivyo swali la kujiuliza ni je utenzi ni nathari?
Vilevile kuna kuingiliana kwa tanzu. Mfano kumbukumbu na kwanini na kwa namna gani ni tanzu ambazo zinajitokeza katika kundi zaidi ya moja.
M. M MULOKOZI (1989)
Kwa upande wake Mulokozi anaainisha tanzu za FS katika makundi sita ambayo ni MAZUNGUMZO, MASIMULIZI, MAIGIZO, USHAIRI, SEMI, na NGOMEZI.
MAZUNGUMZO
Hotuba
Malumbano ya watani
Ulumbi
Soga
mawaidha
MASIMULIZI
4
Hadithi - Ngano (Istiara, Mbazi, Kisa)
Salua – kisakale, mapisi, tarihi, kumbukumbu, kisasili
MAIGIZO (tanzu zake hutegemea na shabaha na miktadha)
USHAIRI
Nyimbo
Tumbuizo
Bembea
Za dini
Wawe
Tenzi
Tendi
Mbolezi
Kimai
Nyiso
Za vita
Za taifa
Za watoto
Za kazi
Maghani (ya kawaida, ya sifo- kivugo na tondozi) Ghani masimulizi – rara, ngano, sifo, tendi
SEMI
methali
vitendawili
misimu
mafumbo
5
lakabu
NGOMEZI
Za taarifa
Za tahadhali
Za mahusiano k.m mapenzi
Kwa upande wake Okpewho anaeleza kuwa uainishaji wa hadithi/ngano ni tatizo la muda mrefu. Hata hivyo anaeleza kuwa kuna vigezo/njia nne mpaka sasa ambazo zimetumiwa kuainisha hadithi/ngano.
Kwanza, kigezo cha unguli (protagonist of the tale), katika kigezo hiki kunajitokeza ngano zihusuzo wanadamu, ngano za wanyama, ngano za vichimbakazi, na ngano za miungu. Hata hivyo kigezo hiki kinaonyesha kuwa na matatizo.
Matatizo hayo ni pamoja na kufanana kitabia kati ya jamii moja na nyingine. Kwa mfano katika ngano za wanyama, wanyama hupewa uwezo wa kuzungumza, kufikiri, na kutenda kama wanadamu.
Pia kigezo hiki kinapuuza namna mbalimbali katika ngano ambazo vichimbakazi, wanadamu na wanyama huhusiana.
Pili, kigezo cha lengo la ngano husika (purpose of the tale), katika kigezo hiki ngano zinaainishwa kwa kuzingatia lengo la simulizi husika. Hapa panajitokeza ngano za kimaadili, ngano za kuhimiza kazi n.k. Okpewho anaeleza kuwa katika kigezo hiki kundi kubwa la ngano ni zile za kimaadili.
Tatu, kigezo cha sifa ya ubora wa ngano (characteristic quality of the tale), kigezo ambacho ndicho kinaonekana kubeba kundi kubwa la ngano. Katika kigezo hiki kuna ngano ayari (trickster tales)-hizi huambatana na uelevu au ulaghai wa wahusika; ngano za mtanziko (dilemma tales) na ngano za kihistoria ambazo huhusu vita, vizazi, mashujaa, usuli wa kitu/jambo fulani n.k.
6
Nne ni Kigezo cha muktadha wa utendaji wa ngano husika. Katika kigezo hiki kinachoangaliwa ni ngano inatendwa wakati gani na katika mazingira gani. Kwa mfano, kwa kutumia kigezo hiki tunaweza kupata ngano zinazotendwa wakati wa mbalamwezi (moonlight tales), ngano zinazotendwa wakati wa ibada (divination tales), ngano zinazotendwa wakati wa mapumziko ya wawindaji (hunters‟ tales) na nyinginezo.
Kwa ujumla vigezo hivyo vina matatizo kwa sababu kuna uwezakano wa aina moja ya ngano kujitokeza katika vigezo vyote. Kutokana na utata huo, Okpewho anazianisha ngano katika makundi yafuatayo:
Kundi la kwanza ni hekaya (legends). Kundi hili linaelezwa kuwa ndio kundi kubwa kabisa la hadithi na hujumuisha tarihi, ngano za mashujaa, ngano za mapenzi n.k.
Kundi la pili ni ngano fafanuzi (explanatory tales). Hizi hufafanua asili ya kitu au wazo kwa kuzingatia mazingira na tajiriba za jamii. Kundi hili linajumuisha aina mbili kubwa: (1) Ngano zinazoelezea asili ya kuumbwa kwa ulimwengu, (2) Ngano zinazosawiri sifa na tabia za viumbe mbalimbali katika mazingira yao. Aina hii ya pili hujumuisha visasili na visaviini.
Kundi la tatu ni ngano zisizo fafanuzi (fables). Kundi hili hujumuisha hadithi zinazohusu tajiriba zihusuzo wanyama, viongozi wa dini iwe katika ulimwengu au vinginevyo. Katika hadithi hizi msimulizi hatoi maelezo maalumu ni namna gani hadhira iifasili hadithi hiyo.
UFAFANUZI WA TANZU ZA FS NA VIPERA VYAKE
1. SIMULIZI/ HADITHI
Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari fulani (narrate). Ni masimulizi ambayo yanatumiz lugha ya mjazo au nathari na mtiririko wake huwa mwepesi au sahili. Urefu wa hadithi hutofautiana kutoka kitanzu/kipera kimoja hadi kingine. Kwa jumla zipo hadithi ambazo ni za kubuni na zingine za kihistoria. Baadhi ya vipera vya utanzu huu ni;
Ngano
7
Hizi ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu katika kuelezea
au kuonya kuhusu maisha. Utanzu huu unajumuisha fani kadhaa kwa mfano:
Istiara – hadithi ambayo maana yake ya wazi inawakilisha maana nyingine iliyofichika. Yaani hadithi nzima ni kama sitiari.
Mbazi- hadithi fupi yenye mafunzo itolewayo kama kielelezo wakati wa maongezi au wa kumkanya mtu
Kisa- hadithi fupi ya kufurahisha kuhusu tukio la kweli.
Visakale
Masimulizi ya mapokeo juu ya wahenga au mashujaa wa kabila au taifa yenye kuchanganya chuku na historia. Kwa mfano hadithi za Liyongo
Mapisi
Maelezo ya historia bila kutia mambo ya kubuni.
Soga
Ni hadithi ndogo ndogo zinazohusisha utani na ucheshi kwa kiasi fulani. Hizi ni hadithi ambazo
hutambwa katika mtiririko wa matukio ambao huzua kicheko. Soga hudhamiria kuchekesha kwa
kukejeli pia. (wamitila: 2010)
Tarihi
Hizi ni hadithi ambazo husimulia au zimejengwa kwenye matukio ya kihistoria. Inawezekana matukio yanayosimuliwa yakawa ya kweli, yaani yalipata kutokea kihistoria. Hadithi hizi hutokea zaidi katika maandishi, mfano ni tarihi ya Kilwa, tarihi ya Pate n.k.
Visasili
Ni utanzu unaofungamana na imani za dini na mizungu (rituals) ya jamii. Hizi ni hadithi za kale
zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya ulimwengu na
mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe, na maana na shabaha ya maisha yao. Mara nyingi
hadithi hizi huaminiwa kuwa ni kweli tupu, na hutumika kuelezea au kuhalalisha baadhi ya mila
na madhehebu ya jamii inayohusika.
2. SEMI
Semi ni tungo au kauli fupifupi za kisanaa zenye kubeba maana au mafunzo muhimu ya kijamii.
Baadhi ya tanzu katika kundi hili ni;
8
Methali
Methali ni semi fupi fupi zenye kueleza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na uzoefu wa kijamii. Mara nyingi mawazo hayo huelezwa kwa kutumia tamathali hasa sitiari na mafumbo. Methali nyingi huwa na muundo wenye sehemu mbili. Sehemu ya kwanza huanzisha wazo Fulani, na sehemu ya pili hulikanusha au kulikaamilsha wazo hilo. Kwa mfano; haraka haraka haina Baraka, tama mbele mauti nyuma.
Vitendawili
Ni usemi uliofumbwa ambao hutolewa kwa hadhira ili iufumbue. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii hiyo, na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki, mbali na kuwachemsha bongo zao. Vitendawili ni sanaa inayotegemea uwezo wa mtu kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali vilivyomo katika maumbile.
Misimu
Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Msimu ukipataa mashiko ya kutosha katika jamii huweza hatimaye kuingia katika kundi la methali za jamii hiyo.
IV. Mafumbo
Ni semi za maonyo au mawaidha ambazo maana zake za ndani zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa shabaha na hadhira maalum, hivyo ni tofauti na methali au vitendawili ambavyo ni semi za kimapokeo.
Lakabu
Haya ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au kimatendo. Majina haya huwa ni maneno au mafungu yaa maneno yenye maana iliyofumbwa. Mara nyingi majna haya huwa ni sitiari. Baadhi ya majina haya humsifia mhusika, lakini mengine humkosoa au hata kumdhalilisha. Mifano ya lakabu;
Mukwavinyika – mtekaji wa nyika
Baba wa taifa – mwl Nyerere
Simba wa Yuda – Hile Selassie
Mkuki uwakao – Jomo Kenyatta.
9
UTENDAJI SIMULIZI
4.0 Usimulizi wa Hadithi katika Afrika
Okpewho anajadili usimulizi wa hadithi katika Afrika. Anaeleza kuwa msimulizi wa kijadi ni tofauti na msimulizi anayepatikana katika maandishi. Usimulizi katika Afrika unafanyika wakati maalumu hasa wakati wa jioni au usiku watu wanapokuwa katika mapumziko baada ya vipindi maalumu vya kazi.
Usimulizi wa hadithi katika Afrika hufuata fomula maalumu. Usimulizi wa hadithi hizi huwa na mianzo na miisho ya kifomula ingawa mianzo na miisho hiyo hutofautiana toka jamii moja hadi nyingine. Kwa mfano matumizi ya paukwa pakawa, hadithi hadithi n k kutegemeana na utanzu husika.
Pia usimulizi wa hadithi unaambatana na ushiriki wa hadhira ambaye huonyesha kuwa anafuatilia simulizi hiyo.
Kwa jumla, utambaji wa hadithi jukwaani huwa na sifa kadhaa zinazoutambulisha. Sifa hizi huzitenga hadithi za mapokeo na zile tunazozisoma vitabuni. Utendaji huu unaandamana na sifa zifuatazo;
Usemi halisi. msemaji anasema moja kwa moja
Michepuko: msimuliaji hutoa kauli za pembeni au maoni yake. Anaiacha hadithi na kusema mambo ya pembeni au kando kabla ya kuendelea tena kuisimulia. Michepuko hii inaweza kuwa na jukumu la viliwazo hasa katika hadithi za kusikitisha au za kitanzia.
Urudiaji
Matumizi ya wakati uliopo kihistoria/ au uliopita kisimulizi. Utambaji au usimulizi huwa katika wakati uliopita lakini huchanganya pia na sifa zinazohusishwa na wakati uliopo ili kuhakikisha kuwa umbali uliopo kati ya hadhira na hadithi yenyewe umepunguzwa.
Kubadilisha muundo wa hadithi:mtambaji anauwezo wa kuubadilisha muundo wa hadithi
kwa kuongeza vitushi Fulani, kurudia visa Fulani, kubadilisha msamiati, kurahisisha kisa,
10
kutia ucheshi n.k. Kwa hakika kila utambaji hadithi moja huwa ni tofauti na utambaji wa hadithi hiyo wa mwanzoni yaani inafaraguliwa.
MODULI YA PILI
NADHARIA ZA FASIHI SIMULIZI
Nadharia huchukuliwa kuwa dira ya kumwongoza mtafiti au mchambuzi kulikabili na kulielezea vyema jambo fulani kwa tazamao unaotazamiwa kuwa imara zaidi kuliko ule wa nadharia nyingine. Nadharia hutoa mwongozo katika utatuzi wa jambo fulani ambalo halijaweza kuhakikishwa ukweli wake. Ni mawazo, maelezo au mwongozo uliopangwa ili kusaidia kutatua au kutekeleza jambo fulani, kwa upande wetu jambo la kifasihi simulizi.
HISTORIA YA NADHARIA YA FASIHI SIMULIZI
Historia ya nadharia ya fasihi simulizi ilianza katika elimu ya ushairi, balagha n.k. ya Wagiriki toka karne ya 18. Katika karne ya 20 nadharia hii imekuwa ni mkabala mkubwa katika usomaji wa matini. Kuna nadharia mbalimbali za kifasihi kama vile Umuundo, Umarksi, Ufeministi nk.
Hivyo, tunaweza kujumuisha kuwa nadharia ya fasihi simulizi ni chombo kinachotoa mwongozo kuhusu mwelekeo wa jamii fulani. Hii ina maana kwamba ni mwangaza unaoimulika jamii juu ya mazingira na fikra zake. Kwa hali hiyo basi, nadharia hii haina budi kuzibainisha sifa na ushirikiano wa jamii husika.
Kuingia kwa ukoloni mamboleo kumefanya fikra na maarifa kutoka nje zitukuzwe na kuabudiwa huku fikra za ndani zikidumazwa kila kukicha. Kwa kufanya hivyo nadharia hizi zimeweza kuleta mabadiliko katika nadharia asilia zilizokuwepo. Kwa mfano; utamaduni wetu wa asili kama vile ususi, ufinyanzi, jando na unyago, nk zimebadilika baada ya kuingia kwa ukoloni mamboleo.
11
Hata hivyo, wahakiki wa Magharibi na Kiafrika wameangalia mambo mengi yaliyoikabili fasihi simulizi ya Kiafrika kama tutavyoona katika nadharia za fasihi simulizi tutakazopitia.
Nadharia za Fasihi simulizi tutakazojadili katika kozi hii ni hizi zifuatazo:
Nadharia za kitandawazi
Nadharia ya Ubadilikaji Taratibu( Evolutionalism Theory)
Nadharia ya Msambao (Diffusionism Theory)
Nadharia ya Kisosholojia (Sociological Theory)
Nadharia za kitaifa
Nadharia Hulutishi
Nadharia za Kitandawazi
Ubadilikaji Taratibu “Evolutionalism”
Mfuasi wa nadharia hii ni Charles Darwin (1809-1882) ambapo hoja zake zilikuwa na ushawishi mkubwa kwa wanafunzi waliokuwa wakijifunza kuhusu utamaduni kama vile Edward Burnet Tylor (1832-1917) na James George Frazer (1854-1941). Wote hawa waliamini juu ya misingi anuwai kuhusu kanuni zinazoongoza asili na maendeleo ya utamaduni wa mwanadamu.
Kundi hili liliona kuwa dhana ya ubadilikaji taratibu misingi yake mikuu ni viumbe hai. Wanaona kwamba viumbe hai vyote vinakuwa katika mchakato wa mabadiliko mbalimbali hadi kufikia maumbo vilivyonayo sasa.
Wanaedelea kusema kuwa kuna kanuni ambazo ni muhimu sana zinazochangia makuzi ya kanuni za binadamu. Wakaona kuwa kuna ukoo, akili au asili au jamii moja ambayo imezagaa ulimwenguni kote, na kama uchunguzi utafanywa wa kuchunguza jamii mbili kiutamaduni katika kipindi kilekile cha mabadiliko, itabainika kuwa elimu zao zina tabia zinazofanana.
12
Wanaendelea kusema kwamba, ili kuelewa jamii moja kwa ujumla ni vyema kulinganisha na jamii nyingine ya aina hiyo kwa kipindi kilekile cha ukuaji. Kwa mfano kuchunguza ngano za kijadi katika makabila mbalimbali ya Kusini kama vile uchawi na miviga na kulinganisha na jamii za Kiafrika.
Kwa ujumla katika nadharia hii tunabaini kuwa nadharia hii ilitawaliwa na mbinu linganishi (comparative methods).
Kwa mfano Frazer (kazi yake ni The Golden Bough ambayo ilikuwa katika majuzuu 13), alitafiti sanaa jadi ya Waitalia. Katika utafiti wake yeye alijihusisha na kutafiti chimbuko la matambiko ya uchawi na dini huko Italia. Alichokuwa anataka kuthibitisha kuhusu jamii ya Waitalia ni kwamba asili ya dini inapatikana katika magical rites za mtu wa kale.
Pamoja na watafiti wenzake, walikuja kama watawala na kuchunguza mila na desturi za Kiafrika ili kuzilinganisha na utafiti kama huo aliokuwa akiufanya huko kwao. Walitafiti na kuchunguza jamii ndogo ndogo za Kiafrika na kisha kufanya ulinganishi. Kwa ujumla wataalamu hao walikusanya, walitathimni fani mbalimbali za Kiafrika kama vile ngano, nyimbo, vitendawili, methali na aina nyingine, za FS katika jamii mbalimbali za Kiafrika. Baadhi ya watawala wataaluma wa kikoloni walitafiti kuhusu fasihi simulizi ya Kiafrika chini ya usimamizi wa Frazer ni pamoja na;
John Roscoe ambaye alitafiti jamii ya Baganda- Uganda
Edwin Smith & Andrew Dale ambao walitafiti jamii ya Ila- Zambia
Reverend Henri Junod- Tonga, Afrika Kusini
Robert Rattray- Akan-Ghana, pia Hausa- Nigeria
Amaury Talbot- Ekoi- Nigeria(Southeastern Nigeria)
H. Chatelain- Angola. Chatelain akichunguza kuhusu ngano za Angola na za Afrika kwa jumla, aligundua kuwa ngano za Kiafrika ni tawi toka mti mmoja wa ulimwengu.
13
Mwisho, wote kwa pamoja walihitimisha kuwa watu wa Afrika ni sawa na watu wengine popote
pale ulimwenguni.
CHANGAMOTO
Dhana hii ya ubadilikaji taratibu iliathiri mbinu na matokeo ya utafiti wao kwa njia tofautitofauti
kama vile:
Kila kilichokusanywa katika fasihi simulizi kilihesabika kama masalia ya zamani au mabaki ya fasihi zilizotangulia.
Kadri fani hizo zilivyorithishwa kwa njia ya mdomo toka kizazi kimoja hadi kingine ndivyo zilivyozidi kupoteza sifa mahsusi za ubora, zilichuja na kuchujuka
Chochote kilichosalia lazima kitakuwa na dosari fulani tofauti na kitu halisi cha zamani
Walijihusisha mno na maudhui na kamwe hawakujihusisha na sifa za kifani kama vile miundo na mitindo ya fani husika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba lengo lao lilikuwa
ni kufahamu hali halisi ya utamaduni wa jamii za watu wasiostaarabika na historia yao. Ili kuyafahamu haya waliona kuwa ni bora kupata muhtasari tu wa maudhui yanayojadiliwa ndani ya fasihi simulizi ya jamii husika na sio kujihusisha na fani ya fs hiyo
Hawakuoa umuhimu wa fanani na mtambaji: “ no creator, no author of such tales,…….as a product of joint or communal authorship.
Pia waliziona kazi za fasihi simulizi za Kiafrika kwamba hazina mwenyewe kwa kuwa ni mali ya jamii nzima. Walisema kwamba, ijapokuwa fasihi simulizi ni mali ya jamii,
lakini sio kwa kiwango hicho walichokisema wao. Walisisitiza kuwa si kila mzungumzaji anaweza kuwa fanani wa fasihi simulizi. Wao walilipuuza suala la upekee wa muktadha.
HITIMISHO
Kimsingi, ilikuwa vigumu sana kupata matokeo sahihi katika uchunguzi ulioongozwa na misingi ya kiuibukaji. Hii ni kutokana na mbinu batili zilizotumika pamoja na
14
kuongozwa na malengo muflisi na finyu kuhusu umbile la jamii za Kiafrika kwa jumla. Leo hii nadharia hii haitumiki tena katika mijadala ya fasihi simulizi. Wakoloni waliitumia kama njia ya kuhalalisha suala la uvamizi na ukoloni barani Afrika.
1.2 Nadharia ya Msambao “Diffusionism Theory”
Iliongozwa na mawazo na ushawishi wa Grimms na Thompson
Ni nadharia iliyopingana na nadharia ya ubadilikaji taratibu tuliyoona hapo juu. Wana ubadilikaji taratibu waliamini kuwa;
Ikiwa ngano mbili kutoka katika jamii mbili tofauti zimeonyesha kufanana kwa namna fulani za kimuundo au kimaudui ni kwa sababu wanadamu ulimwenguni kote wanamkondo mmoja wa mawazo na kufikiri kwao ni kwa namna moja, na kwamba ngano hiyo inasawiri hatua sawa za maendeleo ya kiutamaduni katika jamii husika.
Tofauti na wanaubadilikaji, wanamsambao wangeamini kuwa;
Pale ambapo kufanana kwa namna hiyo kutatokea, sababu ya msingi ya kuwapo kwa mfanano huo ni kuwa katika kipindi fulani hapo zamani sana jamii hizo mbili ziliwahi kukutana kwa namna fulani, makutano baina ya jamii hizo yalisababisha hali ya kuazimana kwa baadhi ya mila na tamaduni (mawazo) mojawapo ya jamii husika.
Watafiti hawa waliangalia mila na desturi za jamii zilivyokuwa zikikua na kusema kuwa zilikua kutokana na msukumo wa asili na lugha za Ulaya. Walikubaliana kwa sehemu kubwa kuwa asili ya mila, desturi na aina nyingine za utamaduni zinapatikana India, na walitaka kutafiti ni kwa kiasi gani utamaduni huu wa Indo-European ulikuwa umesambaa duniani.
Wana msambao nao walitumia mbinu ya ulinganishi kama walivyofanya wanaubadilikaji taratibu. Kazi ya utafiti ilihimizwa na wajerumani ambao ni Jacob na Wilhelm Grimm ambao walikusanya ngano nyingi kutoka India na kutoka katika nchi yao.
15
Jacob na Wilhelm Grimm: Walitafiti ngano kutoka India na Afrika, na walihitimisha kwamba, kuna kufanana kwa ngano za India na Ulaya. Wakatoa maamuzi ya kwamba, hadithi za Kiafrika ni chimbuko kutoka kwa wazazi wenye asili na utamaduni wa India na Ulaya. Hivyo, dhana yao hiyo waliifikia kutokana na kuifanyia kazi dhana potofu, kwani kila bara lina utamaduni, mila na desturi zake. Aidha waliliona bara la Afrika kama bara ambalo halijastaarabika.
Stith Thompson: Yeye aliwaunga mkono akina Jacob na Wilhelm. Katika kitabu chake cha The Folktale (1946:438) anapendekeza kuwa panapotokea kufanana kati ya ngano/hadithi za Ulaya na za Afrika, zinaweza kuelezewa kuwa huenda hadithi/ngano hizo zililetwa na Wazungu wakati wa utumwa.
Mawazo yao kwa ujumla ni kuwa;
Utamaduni unaweza kusambaa tu kutoka katika jamii imara na maarufu tena yenye nguvu kuelekea kwenye utamaduni wa jamii
iliyo kinyume chake “from superior to an inferior people)
Ikiwa kulikuwa na kufanana kwa namna yoyote katika ngano zilizopatikana Afrika na Ulaya kwa mfano, lazima moja kati ya
jamii hizo ni dhaifu kuliko nyingine, na jamii dhaifu….Afrika, ilihali jamii imara… ulaya
Yote haya yangeweza kuelezwa tu kwa misingi ya ukweli kuwa jamii za Ulaya zilileta mambo hayo Afrika kutokea Ulaya kipindi
cha biashara ya Watumwa (Thompson 1946:438)
Tafiti ziliendelea kufanyika baada ya Jacob, Grimm na Thompson ambapo bara la Afrika lilionekana kuwa bara lenye giza na hivyo kukaonekana haja ya kuanzisha dini ya Kikristo na teknolojia ya Ulaya barani Afrika ili Afrika iondokane na giza hilo.
Kwahiyo tunaweza kuona namna kila kitu cha Afrika ikiwemo fasihi simulizi yake vilivyodidimizwa na watawala hawa wa kikoloni.
16
Mapungufu
Tunaweza kusema kwamba, ingawa walijitahidi kuipa hadhi fasihi simulizi kwa kusisitiza upekee wa muktadha, hawakuchunguza kwa undani sifa za kisanaa za fasihi simulizi. Pia walijishughulisha na muhtasari tu wa simulizi walizochunguza, na hivyo ni dhahiri kwamba kuna vipengele vingine muhimu ya Fasihi Simulizi ya Kiafrika ambavyo havikutiliwa maanani..
Hitimisho
Bado tafiti za namna hii hapa Afrika zinaendelea lkn mkabala na malengo ni tofauti
Ule upendeleo uliokuwepo hapo zamani sasa umeondoka
Sasa wanajihusisha na kutafiti msambao wa ngano na vipengele (units) vyake ndani ya tamaduni mbalimbali, katika bara la Afrika.
Kama vile asili ya ngano za Kiafrika zinazosimuliwa katika Marekani ya Kusini na Kaskazini
Nadhari ya Sosholojia „Sociological Theory
Mihimili ya Nadharia hii
(a) Umahsusi na sio umajumui
Ilikuwa mahususi zaidi kuliko nadharia zilizotangulia: badala ya kujikita katika taaluma ya sanaa jadi kwa ujumla (maumbile ya mwanadamu na utamaduni wa mwanadamu) kama walivyofanya wanadharia wa zamani, nadharia ya usosholojia ilijikita katika jamii peke yake.
Hii ilikuwa baada ya kugundua dosari zilizofanywa hapo kabla; dosari za kutoa matamko ya juu juu na ya kijumla zaidi
Kauli hizo mara nyingi zilitupilia mbali vipengele fulani vya maisha kmv lugha na mienendo mingine….. hakika viliitofautisha jamii moja dhidi ya nyingine
17
Kwao, tofauti zilizokuwepo baina ya jamii moja na nyingine zilikuwa na maana zaidi kuliko kufanana kulikokuwepo
Kwa hiyo wanasosholojia waliazimia kuchunguza kila jamii kwa wakati na nafasi yake, kwa kurekodi kila kilichopatikana katika jamii husika (sanaa jadi yao).
Wataalamu mbalimbali walioongoza jitihada hizi ni pamoja na hawa wafuatao
Bronislaw Malinowski na A.R. Radcliffe-Brown (Uingereza)
Hawa walichunguza jamii mbalimbali katika Pasifiki, na waliandika mengi kuhusu jamii hizo. Jamii hizo ni pamoja na visiwa vya Trobriand na Andaman mutawalia
Franz Boas (Marekani)
Huyu alichunguza jamii za wenyeji wa Marekani
Wapo pia wataalamu wengi waliofanya utafiti wao, na kuandikia kuhusu jamii za Kiafrika ambao ni pamoja na hawa wafuatao
E.E. Evans-Pritchard………Nuer (Sudani)
Geoffrey Lienhardt……..Dinka (Sudani)
William Boscom…….Yoruba (Nigeria)
S.F. Nadel………..Nupe (Nigeria)
Marcel Griaule……….Dogon (Burkina Faso)
Ingawa hata kabla ya wataalamu hawa, kulikwishakuwepo wataalamu wengine waliotafiti na kuandika kuhusu FS ya kiafrika lakini wataalamu hao waliongozwa na mawazo ya kiubadilikaji taratibu zaidi
(b) Mkazo katika Utendaji
18
-Tofauti na ilivyokuwa kwa wananadharia wa nadharia zilizotangulia ambao hawaku....
“They were not interested in studying the performers of oral tradition” wanasosholojia waliweka msisitizo katika kuchunguza PERFORMERS/watendaji wa fani mbalimbali za FS. Kutokana na msisitizo wao huu imebainika kuwa
*Fanani wa FS wana ujuzi na ustadi wa kiutendaji katika sanaa husika (ubunifu wao ni mkubwa sana). Jambo hili… limetusogeza mbele kidogo ktk kuielewa FS
*Wanasosholia walidiriki na kuthubutu kudokeza kuhusu sifa za ndani za kimtindo katika FS ya kiafrika
Msisitizo juu ya dhima ya Fasihi Simulizi katika jamii
Tofauti na ilivyokuwa imedhaniwa hapo mwanzo kuwa FS ni mabaki tu ya zamani na kwamba hayakuwa na umuhimu wowote katika maisha ya jamii katika zama za kisasa,
wanasosholojia waliamini kuwa uamilifu wa FS uko hai na hauifi na kwamba unabadilika kulingana na maendeleo ya jamii husika. Dhima hizo ni pamoja na “DHIMA ZA
KIJAMII ZA FS…KWA MUJIBU WA WANASOSHOLOJIA”
FS ni kama Encyclopedia ya hekima za jamii husika
Hii ni kwa mujibu wa Bascom 1959 ambaye alifanya utafiti katika Poetry of Divination katika jamii za Wayoruba wa Nigeria
FS ni nyenzo muafaka ya kurekodia hatua mbalimbali za maendeleo ya jamii husika.
Aylward Shorter 1969…..the tales of origin katika jamii ya Wakimbu Tanzania
FS inasaidia na imeendelea kusaidia kuimarisha „authority of statement or a custom in situation kama vile katika mahakama au contests for Chieftaincy. J.C.
Massenger…..Anang of Nigeria 1958, J.B. Christenseu……Fante of Ghana 1958. Hawa walichunguza Methali katika jamii zilizotajwa
CHANGAMOTO ZAKE…….Pamoja na uzuri uliotajwa bado kuna changamoto kadhaa Given far less time to illuminating and analyzing the artistic properties of African OL
19
They have published tale, in flat, unimpressive prose, eliminating features of oral style (repetition and exclamation)
They have done few carefully analyses of techniques of the original language that appealed to the audience of the tale in the first place
The circumstances surrounding the performance of the tale (ushiriki wa hadhira, matumizi ya ala za muziki, nk) not reported
Hata pale ambapo wamejaribu kuuleza vyema muktadha huu, umuhimu na nafasi yake katika kufanikihs au kukwamisha ngano husika haujaelezwa
Ilikuwa vigumu sana kwa kutumia mbinu zao kuona ni kwa vipi ngano kwa mfano inaweza kuwa fasihi
Pia kutokana na mbinu yao ya kusisitiza umuhimu wa FOLKLORE katika utamaduni wa watu, wataalamu kmv BOSCOM NA BEN-AMOS walisisitiza kuwa “Any judgement of
a folk text must be based on the views of the society from which the text come” Wazo hili ni zuri sana lkn, ikiwa kazi za fs ya kiafrika zitaeleza mawazo ya wageni na si ya wenyeji, kmv boscom na amos, ni kwa sababu sanaa hizo zina sifa Fulani fulani ambazo zinaenda na kueleza mambo Fulani yaliyo mbali na dhana ya uzuri kwa waafrika. Mazingira km haya yakitokea, ni jukumu la mwandishi, ikiwa kweli wanaelewa vyea lugha husika, kufafanua sanaa husika na sifa za sanaa hiyo ilimuradi wageni waikubali sanaa husika na waipokee. Kwa hiyo mkabala wa MUKTADHA WA KIJAMII waliokuwa nao wanasosholijia ulikuwa FINYU SANA….. changamoto ya kiuhakiki ktk kazi za kifasihi
HITIMISHO………..Hata kabla ya wataalamu hawa kufanya uchunguzi wa kisosholojia, walishakuwepo wataalamu wa mwanzo kama vile…………………….. ambao walifanya uchunguzi wa kisosholojia.
Tofauti kubwa ni kuwa wale wa mwanzo waliongozwa na mawazo ya kiuibukaji
Waliongozwa na kuhamasishwa na ….kizazi cha Franzer.
20
Hawa wa baadaye walijihusisha na kuhamasika zaidi na “ HISTORIES OF THE
CULTURES THEY STUDIED
PIA waliongozwa na kuhamasishwa na mawazo ya Malinowski
Pia hawa wa baadaye walitilia mkazo matumizi na uamilifu wa sanaa jadi za kiafrika katika jamii “SOCIETAL FUNCTIONS OF OL
Hata hivyo, bado wataalamu hawa hawakufanikiwa au hitimisho lao halikuendana na tathimini ya karibu na kina kuhusu material walizozikusanya. Hii ni kwa sababu
hawakuwa na ujuzi wa kutosha katika lugha za jamii za kiafrika
Hitimisho…………………………
TOFAUTI KATI YA WANASOSHOLOJIA NA WANAUIBUKAJI AU
WATAALAMU WENGINE WA MWANZO
WATAALAMU WA MWANZO They were not interested in studying the performers of oral tradition
Kwa sababu waliamini kuwa watendaji hawa walikariri tu mambo waliyoyapata kutoka kwa mababu zao siku za nyuma na kwamba wao wenyewe hawakuyaelewa mabo hayo,
mengi yao. Hawakuyaelewa
Pia waliamini kwamba, watambaji hawa walikuwa wajinga na washamba kabisa kiasi kwamba hawakuwa na uwezo w kuongeza ubunifu wowote katika sanaa hizo
KWA UPANDE WAO wataalamu hawa waliweka msisitizo katika kuchunguza PERFORMERS wa fani mbalimbali za FS
Kutokana na msisitizo wao huu tumebaini mambo murua yaendanayo na FS
i. Wamebainisha ujuzi na ustadi wa watendaji katika sanaa husika (ubunifu wao ni
mkubwa sana)
21
jambo hili… limetusogeza mbele kidogo ktk kuielewa FS
Nadharia za Kitaifa
2.1 Utangulizi
Je tunakumbuka changamoto za Nadhariaa zilizotangulia? Kwa mfano wanasosholojia?
Hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu lugha za Kiafrika.
Kwa kiwango kikubwa waliathiriwa na dhana za kikoloni na upendeleo wa kibeberu: Afrika ni bara la giza na la washenzi wasiokuwa na aina yoyote ya ustaarabu, na
walistahili kustaarabishwa na Wazungu kupitia mlango wa ukoloni.
Dosari hizi ziliathiri pia uwezo wao katika kuchunguza FS ya Kiafrika
Mara baada ya kutafiti, hawakuwa tayari kuchapisha matokeo halisi ya utafiti wao: waliyahariri
Kwa kutumia msaada wa wenyeji (viongozi na wasomi wa mwanzo) walitafsiri tafiti hizo katika lugha za kigeni
Kila ambacho hawakukielewa, walikifuta kutoka katika data zao
HATIMAYE, sifa na ujumi wa fasihi simulizi ya kiafrika haukudhihirishwa (LITERARY QUALITIES OF AOL WAS NOT APPRECIATED)
Kutokana na dosari hizo, palihitajika kundi la wanazuoni wenye ujuzi na mtazamo mwingine, tofauti na ule wa kikoloni.
Ndipo walipojitokeza wanazuoni wa Kiafrika kmv. S.Adeboye Babalola wa Nigeria, Daniel Kunene wa Basotho, Kofi Awoonor wa Ghana na J.P. Clark wa Nigeria
Lengo na azma yao ilikuwa ni kukosoa mawazo ya wanazuoni wa Kimagharibi. Kwa kweli walifanya hivyo, tena bila kuyatathmini vilivyo
22
Ilifikiriwa kuwa wataalamu hawa walikuwa na sifa maridhawa za kuimarisha uchunguzi katika FS ya Kiafrika. Kwa mfano, mtazamo chanya kuhusu Bara la Afrika, uzoefu wao
kuhusu FS ya Kiafrika na ujuzi wao katika lugha za Kiafrika.
Kwa kutumia nyenzo hizi, walijaribu kuboresha tafiti za zamani za kikoloni katika FS ya Kiafrika. Je waliboreshaje?
Waasisi
S. Adeboye Babalola
Nigeria, aliandika The Content and Form of Yoruba Ijala (1966)
Ijala ni Ushairi wa Wawindaji katika jamii ya Wayoruba
Yaliyomo kwenye kitabu hiki ni yapi
Usuli wa kitamaduni wa utendwaji wa Ijala
Sherehe na matukio mengine ambapo aina hii ya ushairi inatambwa Maudhui ya Ijala
Mafunzo ya Washairi wa Ijala Utendaji wa Ijala
Mbinu za kimtindo katika Ijala (ladha ya Kishairi)
Complex structure of imagery and allusion
The manipulation of sounds and the voice
Linguistic devices.. (poetic diction)
Matini ya Mashairi ya Ijala katika lugha ya Kiyoruba
Tafsiri ya Mashairi katika lugha ya Kingeraza
Tanbihi (Footnote) inayofafanua mambo muhimu katika tafsiri
23
Daniel P. Kunene
- Basotho (1971) Heroic Poetry of the Basotho
Yaliyomo kwenye kitabu cha Kunene
Uchambuzi wa kina kuhusu muundo wa sarufi ya Kisotho
Dhana ya Ushujaa kwa Wasotho
Mbinu zitumikazo kuchagua majina muafaka ya mashujaa
Uchambuzi wa majina ya Sifo… praise Names
Kutathmini ruwaza ya Takriri…..(fomula simulizi)
Kutathmini
njia ambazo mshairi anajenga ishara…
Vitu mbalimbali katika utamaduni unaozunguka
Mazingira
Vitu mbalimbali vinavyosifiwa
Uhusiano kati ya Mtindo wa Kishujaa katika FS na athari yake kwa washairi wa Kisotho katika zama za kisasa
Wanazuoni wa Kimarekani: Milman Parry na Albert Lord
- Harakati za kudai uhuru barani Afrika
Ushairi simulizi wa Kishujaa: mashujaa wa tendi Simulizi
J.P. Clark wa Nigeria
Mhariri wa Ozidi Saga (1977)
Katika Ozidi Saga tunasimuliwa kuwa
24
Ozidi ni hadithi ya Kijadi inayosimuliwa kwa muda wa siku saba
Inasimulia kuhusu mbinu za kivita za kitamaduni za Shujaa Ozidi
Mambo au vitu vinavyoambatana na hadithi kmv
muziki,
nyimbo,
dansi na
uigizaji wa matuko au vitushi muhimu
alirekodi kila kitu kilichowezekana kunaswa na tape recoda
tendo au kauli kutoka kwa mtambaji lililosababisha hadhira kuangua vicheko. Katika hali km hii, fanani alilazimika kufanya uradidi wa kauli au matendo hayo. Hali hii inaonyesha athari ushiriki wa hadhira katika utendaji
matendo au kauli zenye kuibua hali ya mshangao na mshituko kwa hadhira
kauli zilizotolewa na watazamaji ktk hadhira kmv maswali na maoni kuhusu utendaji husika
majibu ya msimuliaji kuhusu kauli hizo
hali ya utendaji ambapo mziki unachezwa na kisha ladha au midundo Fulani ya kimuziki huimbwa na kikundi cha wanamuziki wa fanani
2.2.5 Hitimisho;
Kutokana na yaliyosemmwa na kutendwa na Wananadharia ya Kitaifa, mambo kadhaa
tunaweza kuyasisitiza
Wanazuoni wenyeji walifanikiwa kueleza na kufafanua ufanisi wa mbinu mbalimbali za kimtindo katika FS
25
Wanazuoni wa kiafrika hawakuwa wa mwanzo kufanya uchunguzi wa namna hii, badala yake hata wazungu walikwishajaribu kufanya hivyo, tatizo lilikuwa kwenye mtazamo
(wa kikoloni na wa kitaifa)
Walirekodi hali na muktadha wote wa utendwaji wa FS
Wazungu walikosea kutathmini FS ya kiafrika kwa sababu walitumia vigezo vya FA … yenye misingi na utamaduni wa kimagharibi. Kimsingi, hizi ni Fasihi mbili tofauti, zenye
kutoka katika jamii mbili tofauti, na hivyo zinahitaji vigezo tofauti vya utathmini. Zina michakato tofauti ya kiubunifu.
Nadharia hulutishi / HYBRIDITY THEORY
Iliasisiwa na Wanazuoni wa Kiafrika wenye mtazamo kuwa hata wageni wamechangia sana katika kukuza taaluma ya FS ya Kiafrika. Miongoni mwa waasisi na wafuasi hawa ni pamoja na
M.M.Mulokozi, Johson na Ngungi wa Thiong
Katika nadharia zote zilizotangulia, wakiwemo wana nadharia za Kitaifa kulikuwa na changamoto mbalimbali. Hata hivyo, changamoto hizo zilitofautiana kutoka kundi moja la wananadharia hadi lingine. Kwa kuwa changamoto za nadharia nyingine zilikwisha jadiliwa, hapa tutajadili na kugusia tu zinazohusiana na nadharia za kitaifa
Walipinga kabisa mawazo ya wanazuoni wa Kimagharibi
Walidai kuwa Wananadharia wa Kimagharibi hawakutoa jambo lolote la msingi kuhusu Afrika.
Kimsingi, wazo kuwa Wanazuoni wote na tena mawazo yote yaliyotolewa na Wageni hayafai katika taaluma ya FS ya kiafrika ni batili.
Huu ndio msingi wa kuibuka kwa Nadharia Hulutishi
Nadharia hulutishi zinaleta uwiano wa kitaaluma na kuibua mjadala kuwa
26
Ingawa kwa kiwango kikubwa mawazo ya Wanazuoni wa Kigeni yalitawaliwa na dosari kadhaa, si kila walichokinena kuhusu Afrika, hususani utamaduni na Fasihi ya Kiafrika ni
kibaya.
Kwa mujibu wa Mawazo ya Wananazuoni wa Nadharia Hulutishi, yaliyosemwa na Wageni yanahitaji kuchambuliwa na kufanyiwa ufafanuzi wa kina. Ndani mwake mna
dosari na pia mna uzuri wa namna fulani. hayapaswi kupuuzwa kabisa.
Katika utafiti na uchunguzi wa masuala yanayohusu FS ya kiafrika ni vema kuchanganya
Mbinu bora kutoka kwa kigeni (F ya kigeni na mbinu zao)
Mbinu bora kutoka kwa wenyeji (F ya Kiafrika kwa kutumia mbinu za kiafrika)
Matokeo yake, ilipatikana aina Fulani ya fasihi yenye sifa Mchanganyiko, ndio maana iliitwa nadharia Hulutishi
Mchango wa Wageni ktk FS ya Kiafrika
1. RUTH FINNEGAN
Alifanya utafiti na kuandika mengi kuhusu Afrika
Miongoni mwa kazi zake ni pamoja na Limba Stories & Storytelling (1967), Oral literature in Africa (1970)
Katika kazi zake hizi Finnegan anafanya yafuatayo kuhusu afrika na fasihi yao kwa ujumla
Anaukana muelekeo uliokuwepo wa kulitazama Bara la Afrika na Fasihi yao Kutotilia maanani ubunifu wa fanani wa fs na bara la Afrika kwa ujumla
Anathamini sifa za kiubunifu za FS ya kiafrika
27
Hata hivyo, naye hakusafika sana, kwani pamoja na mchango wake mzuri anatenda makosa kadhaa ya kiufafanuzi na kinadharia. Makosa haya yalileta athari kubwa kwa wanazuoni wa baadaye kuhusu umbo na sura halisi ya FS ya Kiafrika. Makosa ayatendayo ni yapi/
Afrika hakuna tendi
Afrika hakuna Visasili
2 . GORDON INNES
Amechunguza tendi simulizi za jamii ya Wamandinka huko Gambia
Katika uchunguzi wake alihimiza wasifu wa kila msimuliaji, na Muktadha wa utambaji wao, kmv matumizi ya ala za muziki
Kutokana na utafiti wake alithibitisha na kuunga mkono wazo la Finnegan kuwa katika jamii za kiafrika kuna uwezekano kuwa, watambaji au wasimuliaji tofauti wenye kusimulia kisa kimoja kwa namna tofauti tofauti, tofauti hiyo inasababishwa na ujuzi wa mtambaji, uzoefu wa mtambaji na muktadha wa utambaji. Kwa maana hiyo basi, tunapata mawazo kuwa
Innes ana imani kuwa watambaji wa FS kwa kawaida hawana mtindo mmoja wa utambaji. Hii ni kwa sababu kila mmoja ana ustadi wake, uzoefu wake na
muktadha tofauti na mtambaji mwingine.
28
2.5 Hitimisho na Tathmini
Katika hatua za hivi karibuni kumekuwapo na mapinduzi makubwa kuhusu FS ya Kiafrika na Bara la Afrika kwa Ujumla. Huu tunaweza kuiita mueleko mpya ambao “giving greater recognition to the literary qualities of African Oral Literature‟. Swali ni kuwa je, muelekeo huu mpya umesaidia kwa kiasi gani mustakbali wa FS ya Kiafrika?
Kuondolewa na kufutika kwa dhana potofu kuhusu Bara la Afrika
Kukomaa kwa mtazamo chanya kuhusu FS ya kiafrika
Methali na vitendawili “depth of wisdom
Kiwango kikubwa cha ubunifu
Utamaduni ambapo FS hii imechipuka ni changamani sana
Kukua na kukomaa kwa taaluma ya F ya Kisasa ya Kiafrika
Hapo mwanzo F ilitazamwa kama sehemu ya sanaa au tawi la Anthropolojia
Sasa hivi, somo la F linasomwa na kufundishwa katika Vyuo na Taasisi mbalimbali kama somo linalojitegemea. Lina malengo yake, na nadharia zake
Linonyesha uhusiano mkubwa kati Fs ya kijadi na F ya kisasa ya kiafrika
Uzuri na umaridadi wa utamaduni wa Kiafrika sasa hivi unatangazwa kwa njia ya kukusanya na kutafsiri mbinu na tanzu za FS ili kupata F ya kisasa. Katika utunzi mpya,
mbinu za kisasa na za zamani za FS zinachanganywa pamoja
Sasa, maswali mengi ya kiutafiti yamepatiwa ufumbuzi; sisi ni akina nani? Tuko wapi? Tunafanya nini? Kwa nini tuko hapa? Tumefikaje hapa tulipo leo hii? Je, hatua
tuliyofikia inakidhi haja na matakwa ya kijamii katika hali zote (hususani haja ya kisanaa au kiubunifu? Kama haikidhi haja hiyo, tufanyeje ili tusonge mbele?
29
MODULI YA TATU
Uhusiano wa Fasihi Simulizi na fani nyinginezo
Yaliyomo ktk moduli:
Sanaa za Maonesho za jadi/asili
Sanaa za Maonyesho za Kimagharibi
Fasihi Andishi
Fani nyingine zisizo za kifasihi
1. SANAA
Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisi zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum. Kuna aina kuu tatu za sanaa. Kwanza ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. Hizi ni sanaa za uonyesho. Nazo ni kama vile uchoraji, uchoingaji, ufinyanzi, kutarizi n .k. sanaa amabazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo zilizotariziwa, vyungu n.k.
Aina ya pili ya sanaa ni sanaa za ghibu. Hizi ni sanaa ambazo uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali katika umbo linalogusa hisia. Mifano ni kama vile usahiri, uimbaji, upigaji mziki n.k. uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
Aina ya tatu ya sanaa ni sanaa za vitendo. Uzuri wa sanaa za aina hii umo katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika. Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa mwana sanaa na mtazamaji wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja ama sivyo sanaa haikamiliki. Hali hii ndiyo iliyosababisha sanaa hizi za vitendo kuitwa sanaa za maonyesho, kwa sababu lazima wakati zinapotendeka awepo mtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake umo katika vitendo vyenyewe.
30
Sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni:
Dhana inayotendeka
Mtendaji
Uwanja wa kutendea
Watazamaji
MITAZAMO MBALIMBALI JUU YA SANAA ZA MAONYESHO
Wapo baadhi ya wanazuoni wanaoamini kuwa, sanaa za maonyesho ni michezo ya kuigiza, ama ni michezo inayoonyeshwa kwenye jukwaa lenye pazia na mataa mengi ya jadi au ni michezo ya Shakespeare.
Tukizingatia nadharia hii huenda tukaamini kuwa sanaa za maonyesho ni tamthilia tu!!!! Inafahamika kuwa tamthilia ni utanzu ulioletwa na wakoloni hapa Afrika Mashariki. Hivyo basi, kuamini nadharia hii ni sawa na kusema kuwa hakuna sanaa za maonyesho zenye asili ya hapa Tanzania ama Afrika Mashariki.
Au kwa upande mwingine ni sawa na kusema kuwa kabla ya mkoloni kutuletea tamthilia sisi tulikuwa hatuna sanaa za maonyesho zetu wenyewe. Wazo hili si kweli na ni wazo potofu. (Wasome Mhando &Balisidya 1976).
Mtazamo huu unatokana na fasili ya sanaa za maonyesho inayodai kuwa sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa za mchezo, mchezaji, uwanja wa kuchezea na watazamaji.
Ingawaje ufafanuzi huu ni sawa lakini hata hivyo mtazamo huu ni dhaifu kwani ulitokana na watu waliokuwa wakifafanua sanaa za maonyesho wakiegemea zaidi kwa zile za utamaduni wa kizungu.
Ufafanuzi huu haukuzifikiria sanaa za maonyesho zenye ya utamaduni wa Kitanzania.
Dosari kubwa katika ufafanuzi huu imo katika neno mchezo (play). Neno hili lina maana duni likilinganishwa na hali na umuhimu wa sanaa za maonyesho zenye asili ya Kitanzania.
31
Tukichukua kwa mfano unyago, jando, kusalia mizimu, au masimulizi ya hadithi, ambayo ni mifano ya sanaa za maonyesho zenye asili ya Kitanzania, tunakuta zile sifa zote nne zipo. Isipokuwa tunajua kuwa shughuli zote hizi siyo mchezo na umuhimu wao hauruhusu hata kidogo kuingiza neno mchezo. Shughuli hizi zina maana muhimu ambayo inahusu maisha ya binadamu katika jamii yake. Ni shughuli zinazobeba wazo maalum lenye lengo la kujenga utu wa mwanajamii. Basi vipi tuseme shughuli hizi zina sifa ya mchezo?
Wenzetu wazungu wanaridhika na neno hili kwa sababu sanaa za maonyesho za utamaduni wao mara nyingi zinafanywa kwa masihara tu. Sanaa za maonyesho zao zaidi ni kwa madhumuni ya kujiburudisha au pengine kutafuta kipato.
Lakini kila aina ya sanaa za maonyesho ya kitanzania ina dhana fulani ndani yake, kwa mfano dhana kuhusu maana ya maisha, kuhusu utekelezaji wa madaraka ya kiutu uzima, kuhusu ushujaa, mafunzo ya historia ya jamii n.k.
Kwa hiyo basi sanaa za maonyesho za Kiafrika ni dhana zilizo kwenye umbo linalotendeka na siyo mchezo. Kutokana na utamaduni wa Kiafrika tunaweza kusema kuwa: sanaa za maonyesho ni dhana inayotendeka. Na ili dhana hii itendeke anahitajika mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huyu huhutaji uwanja wa kutendea hiyo dhana na wakati akiitenda wamakuwapo watazamaji.
Sanaa za maonyesho ni vichekeso au ni maigizo yanayochekesha.
Wazo hili linatokana na historia ya sanaa za Maonyesho hapa Tanzania. Wakati mkoloni alipotuletea sanaa ya Maonyesho ya kikwao sisi tulishiriki katika
tamthilia za kina Shakespeare kama washiriki au watazamaji tu.
Kwani tamthilia hizi hazikuwa na maana yoyote kwetu kutokana na kuwa zilibeba na ziliongelea utamaduni wa kizungu. Tulifurahishwa na vile vitendo
vilivyofanywa kwenye jukwaa katika tamthilia hizi na hivyo vitendo hivi vilituchekesha tu.
Basi jambo kubwa kwa Mwafrika ikawa ni vile vichekesho na hivyo kudhani kuwa jambo muhimu katika tamthilia ni kule kuchekesha kwake.
32
Sanaa za maonyesho ni maigizo.
Wazo hili limetokana na tafsiri mbovu ya neno play ambalo limetafsiriwa kuwa mchezo wa kuigiza.
Inawezekana aliyetafsiri neno hili alifuata nadharia za zamani sana za drama, ambapo ilidhaniwa kuwa uigizaji (imitation) ndiyo kiini cha drama.
Hata hivyo nadharia hii ilitupiliwa mbali kwa vile haikudhihirisha kiini hasa cha drama.
Tafsiri hii ndiyo imeleta matatizo hapa Tanzania katika kufahamu sanaa za maonyesho. Wengi wamepotoshwa na wazo kuwa uigizaji ndiyo kiini cha sanaa
za maonyesho kama vile neno michezo ya kuigiza linavyoonyesha.
Hivyo, hata katika kutazama sanaa za maonyesho za asili wengi wamekuwa wakitazama iwapo kuna uigizaji. Na hapa wengi wanakwama kwani katika
unyago, jando, kusalia miungu n.k hakuna uigizaji bali wanaoshiriki wanashika nafasi fulanifulani. Hivyo ni bora kutumia neno tamthilia pale tunaporejelea neno plays.
Sababu za kuwepo kwa mitazamo hii ni:
Wakoloni kutokutambua ama kwa makusudi ama kwa kutokuelewa kuwa tulikuwa na sanaa za maonyesho za kwetu, hivyo akatuletea drama kama vile anatuletea sanaa mpya ambayo aina yake haikuwepo hapa kwetu. Hivyo, mkazo wa sanaa za maonyesho ulitiliwa katika drama tu.
Mkoloni alitumia mbinu mbalimbali za kufuta vitendo vyote ambavyo hasa ndiyo sanaa zetu za maonyesho. Mfano alitumia dini ya Kikiristo kupiga vita vitendo kama vile unyago, jando, kusalia mizimu n.k ambavyo viliitwa vya kishenzi.
Tafsiri mbovu zinazofuata nadharia zilizopitwa na wakati kama livyoelezwa hapo juu.
Muhimu
Tukisema sanaa za maonyesho, tunarejelea vitendo maalum vyenye sifa zilizotajwa na kujadiliwa hapo awali. Hata hivyo tutambue kuwa sifa hizi ingawaje ziko sawa lakini kimsingi
33
zinatofautiana katika uzito wake baina ya jamii moja na nyingine. Hatutazamii sanaa za maonyesho za kihindi kuwa sawa kabisa na zile za Kijapani au za kiafrika. Ingawa zote ni sanaa za maonyesho zina misingi tofauti kutokana na tofauti za utamaduni wa jamii husika.
SANAA ZA MAONYESHO ZA ASILI
Kabla ya jamii ya Tanzania kuingiliwa na utamaduni toka nchi za nje, kulikuwa na aina nyingi za sanaa za maonyesho. Kwa vile Tanzania iligawanyika katika makabila mengi, kila kabila lilikuwa na aina zake za sanaa za maonyesho. Lakini kwa ujumla sanaa za maonyesho za asili zinaweza kugawanywa kwenye makundi makubwa matano, ambayo ni;
Sherehe
Ngoma
Masimulizi ya hadithi
Kusalia miungu
Majigambo
Sanaa za maonyesho za makabila mbalimbali zinazoingia kwenye kundi moja zaweza kutofautiana hapa na pale kimtindo lakini kimsingi huwa ziko sawa.
Sherehe
Katika kundi hili sanaa za maonyesho zinahusu kuingizwa kwa mwanajamii kwenye kundi fulani la watu wa aina fulani kutoka kundi la watu wa aina nyingine. Kwa mfano
jando na unyago- ni mtu kutoka kundi la watoto kuingia kundi la watu wazima.
Kutawazwa uchifu- mtu hutoka kundi la raia na kuingia kundi la watawala
Hivyo kundi hili lilijumuisha sherehe mbalimbali katika jamii kama vile , kuoa/kuolew, jando na unyago, tohara, uongozi n;k
34
Ngoma
Neno ngoma lina maana nyingi kama vile;
Ni chombo cha muziki
Ni uchezeshaji wa viungo vya mwili wenye mitindo na miondoko maalum pengine ukiambatana na muziki.
Ngoma pia ni sherehe yote kwa ujumla, iwe ni jambo, harusi, unyago n.k. Tunachorejelea katika mada yetu leo ni ile maana ya pili yaani- uchezeshaji wa viungo vya mwili wenye mitindo na miondoko maalum pengine ukiambatana na muziki.
Masimulizi ya hadithi
Tunazo hadithi za asili kwa maelfu kwani katika jamii ya asili masimulizi ya hadithi yalikuwa ni mojawapo ya mambo ya kila siku. Baada ya kazi nyingi za mchana, wanajamii wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume, walikusanyika majumbani na kusimuliana hadithi kwa lengo la kujipumzisha. Hadithi hizo zilibeba maudhui mazito kulingana na jamii husika pamoja na umri wa waliokuwa wanasimuliwa.
IV. Kusalia miungu
Katika jamii ya asili watu walielekeza kwa miungu mbalimbali, matatizo ambayo wao, kwa nguvu zao za kibinadamu yaliwashinda. Walipopata tatizo la ukame au waliposhambuliwa na magonjwa ya hatari, walipokabiliwa na wanyama wala watu, walipokosa watoto n.k. Waliikabili miungu yao na kuisalia iwasaidie.
Miungu hiyo ilitofautiana kutokana na imani tofauti. Jamii nyingine zilisalia mizimu ya babu zao, zingine zilisalia miungu ya jua, mito, maziwa au milima.
Mitindo ya kusalia miungu ilitofautiana kutokana na aina ya miungu iliyosaliwa au pengine kutokana na uzito wa tatizo lililoikabili jamii.
Kwa mfano, tatizo la ugonjwa lilipaswa kupelekwa kwa mingu ambayo ilisadikiwa kuwa imekasirika, lakini tatizo la ukame lilipaswa kupelekwa kwa mungu muumba ambaye peke yake ndiye aliyekuwa na uwezo juu ya mvua n.k.
35
Vyovyote vile ilivyokuwa lakini kusalia miungu kulihusu jamii kuiomba miungu iwaondolee matatizo yaliyowakabili.
Na hii ndiyo dhana iliyotendeka, kwani vitendo vyote katika kusalia miungu vilielekea katika jambo hili.
Kutoa sadaka, kuomba kwa maneno, kucheza ngoma, kula na kunywa, vyote vilihusika na kuiomba miungu iondoe tatizo lililoikabili jamii.
Wakati mwingine kusalia miungu ilikuwa ni jambo la kuonyesha kuwa watu waliiacha miungu hii kwa hiyo waliisalia kuonyesha kuwa watu waliiacha miungu hii kwa hivyo iendelee kuwatunza.
Majigambo
Baadhi ya jamii za Tanzania hasa zile zilizoshiriki sana katika vita vya makabila zilikuwa na aina nyingine ya sanaa za maonyesho tunayoiita majigambo.
Majigambo ni masimulizi ya kujigamba kwa mtu kuhusu maisha yakishujaa aliyopata kuyatenda katika maisha yake.
Majigambo haya husimuliwa kwa lugha ya kishairi na masimulizi yake huambatanishwa na vitendo vya mjigambaji mwenyewe.
Mjigambaji akiwa amebeba mkuki na ngao, alitumia vitendo vingi kudhihirisha yale aliyoyafanya hasa matendo ya kishujaa.
Kwa mfano ikiwa anajigamba kuhusu vita fulani alivyopigana, basi atatenda vitendo kuonyesha vile alivyokwenda vitani, alivyokabiliana na adui, alivyomuua adui, au adui alivyokimbia, n.k. na wakati huu wote hutumia zile silaha zake kudhihirisha zaidi vitendo hivi.
Hitimisho
Sanaa za maonyesho zilianza kupuuzwa baada ya ukoloni kuingia barani Afrika. Wakoloni walitumia mbinu mbalimbali kuua sanaa hizi. Lengo likiwa ni kueneza utamaduni wao na hivyo kuwa rahisi kuwatawala Waafrika.
36
MASWALI YA SEMINA
Jadili hali ya sanaa za maonyesho kabla na baada ya ukoloni hapa afrika mashariki, katika mjadala wako onyesha ni mbinu gani zilizotumika wakati wa ukoloni katika kuua ama kufifisha sanaa za maonyesho hapa nchini. Mjadala wako uwe na mifano ya kutosha.
Kwa kutumia mifano kuntu, jadili athari za kimagharibi katika sanaa za maonyesho za kiafrika na fasihi simulizi kwa ujumla. Kisha eleza mchango wa nchi za kimagharibi katika kukuza sanaa za maonyesho/ fasihi simulizi ya kiswahili.
FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI YA KISWAAHILI
UTANZU WA TAMTHILIA
Katika sehemu hii tunabainisha vipengele mbalimbali ambavyo vinachotwa na watunzi wa tamthilia ya Kiswahili, kutoka katika fasihi simulizi na sanaa za Maonesho za Kiafrika.
Harakati za mabadiliko ya utunzi wa tamthilia ya Kiswahili kifani na hata kimaudhui zilianza kujitokeza hasa katika miaka ya 1970, zilipojitokeza tamthilia za kimajaribio.1
Katika miaka hiyo watunzi mbalimbali walianza kujaribu kuchota vipengele fulanifulani vya sanaa za maonesho ya jadi na kuviingiza katika drama ya Kiswahili.
Majaribio hayo ni pamoja na kutumia vipengele kama vile ngoma, nyimbo, utambaji hadithi, na majigambo.
1 Hizi ni tamthilia ambazo zinachota vipengele fulani vya sanaa za maonesho pamoja na vile vya fasihi simulizi.
37
Baadhi ya tamthilia zilizoandikwa kwa kufuata mkondo huu ni pamoja na Nguzo Mama (1982), Lina Ubani (1984) za Penina Muhando; Kinjeketile (1969), Mashetani (1971),
Jogoo Kijijini, na Ngao ya Jadi (1976) za Ebrahim Hussein; Mkutano wa Pili wa Ndege
(1992) ya Amandina Lihamba; na Ngoma ya Ng’wana Malundi (2008), iliyoandikwa na Emanuel Mbogo.
Aidha, majaribio haya yaliifanya tamthilia mpya ya Kiswahili kuwa na upekee wake kiumbo na vilevile kuitofautisha na tamthilia zenye kufuata kanuni za Ki-Aristotle pamoja na kanuni nyingine za Kimagharibi.
Baadhi ya vipengele hivyo vya kimajaribio vinajadiliwa hapa chini kama ifuatavyo:
Kwanza ni matumizi ya wahusika wa kifasihi simulizi. Watunzi mbalimbali wa tamthilia ya Kiswahili wanajenga wahusika wa tamthilia zao katika mwonekano sawa na wahusika waopatikana katika fasihi simulizi. Senkoro (2006:32) anaeleza zaidi kuhusu wahusika katika fasihi simulizi pale anaposema:
Katika fasihi simulizi kuna wahusika wa aina mbalimbali: watu, wanyama, ndege, wadudu, mimea, na hata vitu visivyo na uhai kama vile mawe. Pia wahusika wa kiajabu ajabu wa kuwazika tu kama vile mashetani, hutumiwa katika fasihi hii. Wahusika hawa wote huweza kuingiliana pale ambapo mhusika mtu huweza kukutana na hata kuongea na mhusika asiye mtu kama vile jini, shetani, mti, au hata jiwe. Hali kadhalika, katika ulimwengu wa fasihi simulizi si ajabu kukutana na wanyama, miti, au ndege wanaofanya matendo sawa na ya watu. Si ajabu ndege wakichumbiana, wakioana na kufanya sherehe za harusi kama watu tu.
Hivyo basi, wahusika katika fasihi simulizi wanaweza kuwa ni binadamu, wanyama, wadudu na hata mimea pia; wanaweza kuwa viumbe vyenye uhai au visivyo na uhai.
Si ajabu katika fasihi simulizi kukutana na mhusika kama zimwi, joka, pango, jabali, milima, miti maziwa, mito, misitu, ndege wadudu na wanyama wakisawiri maisha ya wanadamu.
38
Kwa mfano, matumizi ya wahusika ndege katika tamthilia ya Mkutano wa Pili wa Ndege yanatuthibishia nia ya watunzi kubadili mwelekeo wa ujengaji wahusika katika tamthilia zao. Mwandishi Lihamba anatumia wahusika ndege katika kuwakilisha tabia za binadamu.
Mwandishi Ebrahimu Hussein katika tamthilia ya Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi anamtumia mhusika Joka (Sesota) mwenye vchwa sabini, ambaye kimsingi anatumika zaidi katika fasihi simulizi hususani katika utanzu wa ngano na hadithi.. Mwandishi ametumia Joka (Sesota) ambaye anavichwa sabini kama taswira juu ya ukoloni mkongwe na ukoloni mambo leo.
Pia wahusika hawa katika tamthilia ya Kiswahili wanabebeshwa dhima za kiasili na kijadi ambazo hutumika sana katika fasihi simulizi ya Kiafrika.
Hizi ni pamoja na matambiko, nguvu za uganga na uchawi. Kwa mfano katika tamthilia ya Ngoma ya Ng’wanamalundi, mhusika Ng‟wanamalundi ni wa kifasihi simulizi kwani husimuliwa sana katika ngano za kabila la Wasukuma. Emmanuel Mbogo anamtumia mhusika huyu kwa „kumtohoa‟ kutoka katika simulizi hizo za Wasukuma.
Katika tamthilia hii pia, kama ilivyo katika simulizi hizo, mtunzi anamsawiri kuwa na nguvu kubwa za kiuganga na kichawi ambapo shughuli zake hizo anazifanya kupitia matambiko anayoyafanya. (rejea uk wa ……) .
Hivyo matumizi haya ya wahusika wa kingano yanampa mwandishi fursa ya kutumia wahusika wengi na wa aina mbalimbali kwa kadri atakavyo.
Vilevile, matumizi ya takriri au marudiorudio ya kingano ni njia mojawapo katika majaribio haya.
Katika tanzu za fasihi simulizi kuna matumizi ya takriri ya hali ya juu, matumizi haya yana lengo la kusisitiza jambo na wakati mwingine kuonesha urefu wa muda ambao tukio lilitendeka.
39
Kwa mfano, katika usimulizi wa ngano mara nyingi tunakutana na maneno kama haya; „akaenda ..... akaenda …….. akaenda ... akaenda ... akaenda aaa!”
Lengo la msimulizi hapa ni kutuonesha umbali mrefu ambao mhusika huyu alitembea. Katika tamthilia hizi za majaribio mbinu hii inatumiwa sana.
Mwandishi Ebrahim Hussein ameitumia mbinu hii katika uandishi wa Tamthilia ya Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi kwa mfano katika ukurasa wa 14 anasema:
Miaka ikapita
Miaka ikapita
Miaka ikapita
Watu wakaoana
Watu wakazaana
Na kaumu ikazidi
Lengo la mwandishi wa tamthilia hii katika nukuu hapo juu ni kuonesha urefu wa kipindi cha historia ya ukoloni.
Kwa upande wake Penina Mhando naye anatumia sana mbinu hii katika tamthilia zake kama vile Lina Ubani.
Aidha, matumizi ya ngoma katika tamthilia ya Kiswahili ni jambo linalohusishwa na majaribio.
Asili ya jamii nyingi za Kiafrika zilitumia ngoma kama chombo cha mawasiliano. Lengo likiwa ni kuwaarifu watu kukutana kwa ajili ya shughuli fulani ama kuwajulisha kuwepo kwa hatari ili kuchukua tahadhari au hatua ya kuliondoa tatizo.
Mwandishi Penina Mhando katika tamthilia yake ya Nguzo Mama anatumia ngoma ili kutoa taarifa kwa Wanapatata kuhusu kwenda kunyanyua nguzo iliyolala.
Mwandishi ametumia mbinu hii ya ngoma ambacho ni kipengele cha Sanaaa za Maonesho, katika jitihada za kuuondoa umagharibi katika tamthilia ya Kiswahili.
40
Pia ametumia ngoma kwa lengo la kuweka vionjo vya asili katika kuvuta hisia za hadhira yake. Ngoma ni ishara ya kuwaunganisha Wanapatata wote katika kuleta mapinduzi ya kweli ya wanawake na jamii nzima.
Katika jamii mbalimbali za Kiafrika wakati wa utambaji na usimulizi wa tanzu mbalimbali za fasihi simulizi kama vile ngano, hadithi na kadhalika, kuna fomula ambazo huongoza tanzu hizo.
Kwa jumla tunaweza kusema kuwepo kwa mianzo na miisho ya kifomula. Wamitila (2011:29) anafafanua umuhimu wa matumizi ya fomula hizi katika fasihi simulizi kuwa ni njia ya kuwavuta wasikilizaji pamoja yaani kuvuta umakini wa hadhira.
Vilevile hutumiwa pia katika kumtambulisha mtambaji wa hadithi, pia huashiria mwanzo na hata mwisho wa hadithi.
Mathalani katika hadithi maneno kama „Paukwa‟, „pakawa‟, „Hadi Hadithi‟ nakadhalika hutumika kama mianzo ya hadithi za kifasihi simulizi.
Mianzio hii ni tofauti katika tanzu nyingine kwani katika vitendawili mathalani, mianzo inaweza kuwa “kitendawili” na kiitikio “tega” mwishoni mtambaji wa kitendawili anapewa mji.
Waandishi wa tamthilia ya Kiswahili za majaribio wametumia mianzio hii ya kifomula katika kazi zao na hatimaye mwishoni pia wakamaliza kwa fomula kama ilivyo katika hadithi au vitendawili vya fasihi simulizi.
Madhumuni makubwa ni kujenga aina ya tamthilia inayoakisi sanaa za maonyesho za jadi.
Kwa mfano tamthilia ya Nguzo Mama ya Penina Mhando imeanza na mianzo hii ya kifomula (tazama katika uk. 3). Hali kadhalika mianzo na miisho hii ya kifomula inajitokeza pia katika tamthilia za Lina Ubani, Kilio Chetu, Mkutano wa Pili wa Ndege, na Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi.
41
Watunzi wa tamthilia za Kiswahili wanachanganya kazi zao na nyimbo, ambazo ni sehemu ya fasihi simulizi.
Lengo la kufanya hivyo ni kuleta msisitizo wa jambo ambalo mtambaji anaona kuwa lina umuhimu.
Hivyo kupitia wimbo maudhui yaliyokusudiwa hurudiwarudiwa ili kusisitizwa.
Katika fasihi simulizi mtambaji anaweza kuimba wimbo endapo ataona hadhira yake imechoka ama haivutiwi na kile anachosimulia.
Kwa jumla, nyimbo zinaamsha ari, zinachochea hisia za huzuni, furaha, kutia moyo, kuchochea uzalendo na hata kuhimiza mapambano.
Nyimbo pia zinatumika katika kuwaunganisha wanajamii. Penina Muhando katika tamthilia zake anatumia sana nyimbo kwa lengo la kuifanya tamthilia yake kubeba uasili wa sanaa za maonyesho na kuiongezea uhai kiutendaji kwa kugusa hisia za watazamaji na wasikilizaji wake.
Ubunifu huu wa mwandishi wa kuongeza kipengele cha fasihi simulizi katika kazi ya fasihi andishi unathibitisha majaribio tunayoyazungumza katika tamthilia ya Kiswahili.
Hali kadhalika watunzi wengine kama vile Lihamba katika Mkutano wa Pili wa Ndege wanatumia sana mbinu hii.
Aidha hata watunzi wachanga wa tamthilia ya Kiswahili nao wanatumia mbinu hii, mathalani Elizabeth Mahenge katika tamthilia yake ya Changamoto (2010) anatumia nyimbo katika kufikisha ujumbe kwa hadhira yake.
Matumizi ya mbinu hii sasa yanaonekana kuzoeleka na kuwa sehemu ya tamthilia ya Kiswahili. Kwa hivyo basi, nyimbo ni kipengele kimojawapo ambacho kinaweza kutumika katika kubainisha tamthilia ya Kiswahili.
Katika tamthilia ya majaribio ya Kiswahili yapo matumizi pia ya mtambaji wa hadithi.
42
Kwa kawaida mtambaji hujitokeza sana katika fasihi simulizi hususani katika ngano na hadithi.
Mtambaji hadithi huwa ndiye msimulizi mkuu wa hadithi au fanani kama inavyotumika.
Hata hivyo watunzi wa tamthilia ya Kiswahili wanatumia pia mtambaji wa hadithi katika kusimulia matukio ndani ya tamthilia zao.
Dhima ya mtambaji kama inavyojitokeza katika fasihi simulizi inaweza kuwa sawa pia katika tamthilia ya Kiswahili.
Kwani mbali na kuwa mtambaji husimulia hadithi husika katika hali ya utendaji zaidi, vilevile mtambaji mahiri huongeza vionjo vya kiubunifu katika kuvuta hisia za hadhira husika na vilevile katika kuishirikisha hadhira yake.
Kwa mfano nafasi ya mtambaji imeonekana sana katika tamthilia ya Kilio Chetu,
ambapo mtambaji anaonekana kuifahamu vyema hadhira yake na matatizo
yanayoikabili jamii hususani vijana.
Hivyo katika tamthilia hii anatumiwa na mtunzi ili kufikisha maudhui yaliyokusudiwa.
Matumizi ya utambaji yanajitokeza pia katika tamthilia za Jogoo kijijini na Ngao ya Jadi, Mkutano wa Pili wa Ndege, Nguzo Mama, Lina Ubani na kadhalika.
Katika Lina Ubani, mathalani, Penina Mhando anamtumia mhusika Mtambaji katika kutamba hadithi.
Hali kadhalika mhusika Bi Msimulizi anatumiwa katika tamthilia ya Nguzo Mama.
Mbinu hii inasaidia katika kuibua hadithi ndani ya hadithi, kwani huifanya tamthilia wakati mwingine kuwa na muundo wa tamthilia ndani ya tamthilia.
43
UTANZU WA RIWAYA
Mulokozi(1996) katika Utangulizi wa Fasihi anasema, Chimbuko la riwaya ni fani za kijadi za fasihi.
Riwaya haikuzuka hivi hivi tu kutoka katika bongo za watunzi, bali ilitanguliwa na kuathiriwa na fani za masimulizi na sanaa nyingi za kale zilizokuwepo kabla.
Fani hizo zilikuwemo katika fasihi simulizi.
Fani za jadi ambazo huenda zilichangia katika kuchipuza riwaya ni ngano, hekaya, tendi, visakale, historia, sira, masimulizi ya wasafiri, n.k.
Ngano ni hadithi fupi simulizi, na ni fani iliyoenea sana katika fasihi simulizi ya Afrika na
kwingineko.
Ngano zote ni hadithi za kubuni. Nyingi zinahusu wanyama, lakini zipo pia ngano zihusuzo wanadamu, mazimwi, majini na malaika. Nyingi zina msuko sahili ambao
huwasilisha kwa urahisi ujumbe uliokusudiwa. Ngano ni chemchemi isiyokauka ambamo watunzi wa mwanzo wa riwaya waliweza kuchota visa vyao, mbinu za kifani na hata dhamira.
Baadhi ya riwaya ambazo visa vyake ni vya kingano ni S.Robert (Adili na Nduguze 1952), na (Kusadikika 1951), Kiimbila (Lila na Fila 1966) na Ugula (Ufunguo Wenye
Hazina 1969).
Wahusika wa riwaya hizo ni mchanganyiko wa wanyama, mazimwi, majini na wanadamu, na ni bapa wenye kuwakilisha wazo fulani.
Dhamira ni zile zile za kingano, hususani mgongano kati ya wema na uovu, choyo, tamaa nk.
Motifu pia ni zile zile za ngano, kwa mfano motifu ya siri ya hazina iliyofichwa (Ufunguo wenye Hazina), na motifu ya zimwi lafi linaloshindwa kwa msaada wa bibi
kizee(Lila na Fila).
44
Machapisho ya mwanzo ya nathari (za kubuni) katika Kiswahili ni mikusanyo ya ngano iliyohaririwa na Askofu Edward Steere(1866), Specimens of Swahili (Short
Tales)(UMCA), Zanzibar; Hadithi za Unguja (1867); na Swahili Tales as Told by Natives of Zanzibar (1870)
Baadaye yalifuata machapisho mengi, kwa mfano: Hadithi za Esopo (UMCA, London 1890), Visa na Hadithi (1899), Bateman, G. Tales as Told by Natives of Zanzibar of the
East Coast (Chicago 1901); Baskerville, G. Mfalme wa Nyoka na Hadithi Nyingine (Mf. R.K.Watts)(Sheldon, London 1930)
Athari za ngano katika riwaya ya Kiswahili ya leo tunaziona katika muundo wa riwaya (riwaya nyingi zina muundo sahili); wahusika (wengi ni bapa); na lengo (kutoa maadili).
Hekaya ni hadithi ambayo ina visa vya kusisimua, kushangaza ambavyo si vya kawaida.
Ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabu au yasiyokuwa ya kawaida. Mara nyingi masaibu hayo hufungamanishwa na mapenzi.
Hekaya kwa kawaida ni ndefu kiasi, japo si ndefu kama riwaya. Huko Ulaya, hekaya zilichangia katika kuzuka kwa riwaya-chuku ambazo ni kiungo muhimu kati ya hekaya
na riwaya halisi.
Katika jamii ya Waswahili, hekaya zilikuwa zikifahamika tangu zamani. Zilizokuwa mashuhuri
zaidi ni zile za Alfu-Lela-Ulela.
Hadithi za Abunuwas pia zilikuwa zimeenea sana kabla ya ukoloni.
Hekaya mashuhuri zilizochapishwa mwanzo ni Sultan Darai (1884), Kibaraka (1896), Chipande na Broomfield (wah) (1915) Hekaya za Abunuwas na Johnson, F. na Brenn,
E.W. (waf) Alfu-Lela-Ulela (kuanzia 1929).
Baadhi ya riwaya mashuhuri za Kiswahili zilizoathiriwa na hekaya ni S.Robert (Adili na Nduguze 1952); Shariff, O.C.A 1951 Kisa cha Hasan-li-Basir; Amiri A.J. 1972 Nahodha
Fikirini; Kiimbila 1971 Ubeberu Utashindwa
45
Tendi/utendi (simulizi na andishi) ni hadithi ya kishairi inayozungumzia ushujaa/ mambo ya
kishujaa ya kihistoria na ya kubuni, ya jamii au taifa.
Baadhi ya tendi zina sifa za kiriwaya, isipokuwa badala ya kuwa katika umbo la nathari zina umbo la kishairi.
Riwaya pevu, kama tendi, husawiri mawanda mapana ya kijamii na kihistoria, na huzungumzia masuala makuu ya kijamii au kitaifa. Kadhalika riwaya, hasa zile za
kusisimua
Visakale (legends) ni simulizi zinazohusu mambo ya kale.
Baadhi ya mambo ni kweli na baadhi ya mambo yametiwa chumvi. Kwa
mfano Usukumani kuna kisakale cha Ngwanamalundi , Uchagani kuna hadithi ya Mlire. Mfano mwingine ni hadithi ya Liyongo. Hadithi hizo hupatikana katika kila kabila na kila
lugha
Visasili (myths) ni hadithi zinazoelezea asili ya mambo/vitu mbalimbali. Mfano asili ya Kibo na Mawenzi (uchagani), Mumbi wa Gikuyu waliopewa mamlaka na Ngai (Mungu wa Kikuyu) ndipo wakatokea Wakikuyu.
Kisasili ni hadithi ambayo ina uzito kidini na kijamii na inaaminika kuwa ni kweli, mfano hadithi ya Adamu na Hawa
Ni hadithi zinazowakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe, na maana na shabaha ya
maisha yao.
Kisasuli ni hadithi yoyote inayoelezea chimbuko/ asili ya kitu lakini haina uzito wa kisasili. Mfano, Kwanini paka hupenda kukaa mekoni? Watu huwa hawaiamini bali huchukulia kama burudani.
Masimulizi ya historia, Ni masimulizi ya matendo ya mwanadamu katika muktadha na wakati
fulani wa kihistoria.
46
Riwaya nyingi hupata kadhia na visa vyake kutokana na matukio halisi ya historia.
Mfano wa riwaya zilizoathiriwa na fani ya historia ni Uhuru wa Watumwa ya J.Mbotela(1934), Kifo cha Ugenini ya O.Msewa(1977), Kwa Heri Iselamagazi ya
B.Mapalala(1992) na Miradi Bubu ya Wazalendo ya G.Ruhumbika(1992).
Sira hujumuisha wasifu na tawasifu (habari za maisha ya mtu).
Masimulizi ya kisira yalikuweko katika fasihi simulizi, na pia katika maandishi ya Kiswahili tangu zamani. Kabla ya ukoloni yalikuwepo maandishi yaliyohusu maisha ya
mitume na masahaba.
Mwanzoni mwa karne ya 20, Hamed bin Muhammed (1902) aliandika Maisha ya Hamed Bin Muhammed el Murjebi yaani Tippu Tip kwa maneno yake mwenyewe.
S.Robert naye (1949) aliandika Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini.
Baadhi ya riwaya nyingine za kisira katika riwaya ya Kiswahili ni Kurwa na Doto (A.S.Farsy 1960), Rosa Mistika 1971, Kichwamaji 1974, na Dunia Uwanja wa Fujo 1975
(Kezilahabi), Mzishi wa Baba ana Radhi (F.Nkwera 1967), Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka (A. Kitereza) na Kwa Heri Iselamagazi (B.Mapalala 1992).
Motifu ya safari katika ngano za Kiafrika, motifu ya safari hujitokeza sana (ang. F.E.M.K
Senkoro 1996 ktk tasnifu yake ya falsafa ya udaktari “The significance of the Journey Motif in Folktales from Zanzibar”.
Vitabu vya Kiswahili vyenye masimulizi ya kweli ya wasafiri au motifu ya safari ni Safari za Waswahili (cha C.Velten 1901), Maisha ya Hamed bin Muhammed, yaani
Tippu Tip, Mwaka katika Minyororo (cha S.Sehoza) na Tulivyoona na Tulivyofanya Uingereza (cha Martin Kayamba 1932). Uhuru wa Watumwa na Kwa Heri Iselamagazi ni riwaya zilizoathiriwa na visa vya wasafiri.
47
MASWALI YA SEMINA
Kwa kutumia riwaya za NAGONA AU MZINGILE onyesha namna watunzi wa Fasihi ya Kiswahili walivyothubutu kutumia mbinu za kijadi (za kifasihi simulizi) kuelezea maudhui ya jamii zao.
“Riwaya ya Kiswahili inajengwa na fasihi simulizi kifani na kimaudhui”. Jadili kauli hii kwa kutumia riwaya mbili za Shaaban Robert za ADILI NA NDUGUZE NA KUSADIKIKA.
USHAIRI WA KISWAHILI
Baadhi ya wataalamu kama vile Shihabdin Chiraghdin (1975), Mayoka, Sengo, S. Robert, F.E.M.K. Senkoro n .k, wanasema chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni fasihi simulizi, ngoma na sanaa za maonesho za Waswahili na nyimbo. Wanaeleza kuwa ushairi ulianza kwenye shughuli za kijamii kama vile jando na unyago, harusi na gulioni na mahali popote pale ambapo watu walikusanyika.
FASIHI SIMULIZI NA UTENDAJI: (Mihadhara ya 10. 11 na 12)
1.0 Utangulizi
Je tunakumbuka mtazamo wa wachunguzi wa Kikoloni kuhusu Bara la Afrika, husuan kuhusu FS? Hatua na mabadiliko dhidi ya mtazamo huo pia tunapaswa kuzikumbuka. Mafanikio ya nadharia za Kisasa/ mpya/ za kimapinduzi za FS pia tuyakumbuke
Itakumbukwa kwamba kipengele cha utendaji ni miongoni mwa vipengee vilivyopuuzwa sana na watafiti wa awali (wengi wao wakiwa wa kikoloni), na pia kipengele hiki ndicho
kilichotofautisha kwa kiwango kikubwa mawazo ya wanazuoni wa kimagharibi na wanazuoni wa Kiafrika kuhusu FS ya Kiafrika. Isitoshe, kwa sasa hivi, kipengele hiki
ndicho kinachofanyiwa utafiti sana na lindi kubwa la wanazuoni (wachanga, wabobezi,
48
wenyeji na wageni pia). Kasi ya kutafiti na kuchunguza masuala ya kiutendaji inazidi kuwa
kubwa, ingawa haja maridhawa bado haijafikiwa.
Katika moduli hii, tunakijadili kipengele cha utendaji km msingi na uti wa mgongo wa FS. Ili kujadili vyema kipengele hiki hapa kuna masula muhimu kwanza tunapaswa
kuyatanabahi:
dhana ya utendaji, * Nafasi ya Fanani katika utendaji wa FS,* Nafasi ya Hadhira ktk utendaji wa FS, * nyenzo za utendaji na mwisho tutaonyesha namna utendaji unavyojitokeza ktk tanzu mbalimbali za FS. Hatimaye basi, tutahitimisha kuwa Utendaji ndio Uti wa mgongo wa FS kwa vile maana, muundo, mtindo na dhima ya FS imeganda na kugandiana ndani ya dhana nzima ya utendaji.
2.0 Dhana ya UTENDAJI (Utendaji ni nini?)
Wataalamu kadhaa wamewahi kutoa maoni yao kuhusu maana ya utendaji kwa ujumla, na ktk FS. Mioningoni mwao ni M.M.Mulokozi, Okpewho na Wamitila
iii. Mulokozi: Utendaji ni hali ya Fanani na Hadhira kuwasiliana na kushirikiana wakati
wa uwasilishaji wa FS.
iv. Okpewho: “ performance means the total act as well as the context or environment
involved in the delivery of OL”
v. Wamitila: Utendaji ni dhana inayotumiwa kuhusiana na sanaa za maonyesho na
huhusisha uwasilishi wa igizo fulani mbele ya hadhira fulani. Utendaji
huhusisha pia uwasilishi wa tanzu nyinginezo kama FS kwa mfano
nyimbo, ngano n.k mbele ya hadhira yoyote ile. (2003).
vi. Wamitila: Katika FS dhana hii huitwa utendaji katika FS na kuitwa Utendaji
Simulizi…………………………..ambapo anasema kuwa utenfdaji
simulizi ni dhana inayotumiwa kuelezea mtindo wa kuwasilisha tungo
sambamba na kuwepo kwa matendo km uigizaji, kubadilisha sauti,
kutumia ishara-uso nk…..
49
Kutokana na fasili za wataalamu hawa, hususani M.M Mulokozi tunabaini kwamba UTENDAJI huathiriwa na: i. Fanani; ii. Hadhira; iii. Fani inayotendwa; iv. Tukio au shughuli
inayohusika; v. Wakati; vi. Mahali pa kutendea sanaa husika.
Isidore, Okpewho anasena kuwa utendaji wa FS huathiriwa na: umri wa mtendaji, uwezo wa mtendaji, aina ya muktadha/tukio, aina ya jukwaa, muziki na idadi wa watendaji (ama mtu
mmojammoja au kundi la watu zaidi ya mmoja).
Mambo haya yote yanatawaliwa na MUKTADHA wa kisanaa unaodhibitiwa na Fanani pamoja na Hadhira. Hivyo, inatupasa kutazama kwa undani nafasi ya Fanani na Hadhira katika
utendaji wa FS
3.0 Nafasi ya Fana ni ktk Utendaji wa FS
Fanani ni msanii, mtunzi, msimulizi au msimuliaji, na pia anafahamika kama mtambaji wa sanaa husika anayewasilisha FS au sanaa yoyote kwa hadhira ktk muktadha wa tukio fulani. Fanani ndiye anayeiumba sanaa wkt ule ule au kabla ya kutambwa, kisha huihifadhi kichwani. Ktk FS fanani yuko huru kwani huweza kubadili maneno au kitu chochote ili kukidhi matakwa ya hadhira yake. Jambo moja la msingi ni kuwa mbinu za kisanii za uwasilishaji hutungwa wakt uleule wa uwasilishaji. Kutokana na umuhimu wake Msimulizi/Msimuliaji Mzuri anapaswa
kuwa na sifa bainifu:
Hufanya hadithi upya kila mara anapotamba hadithi au sanaa yake
ili sanaa hiyo ikumbukwe kwa urahisi
upya huo hufanywa kwa kubadili na kuibua vionjo na mbinu za uwasilishaji
Anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja (msanii, mwalimu, mtoa maoni na pia kama mburudishaji).
Anapawa kuwa Mcheshi ili kuwafurahisha na kuwaburudisha hadhira yake
hili lisiwe lengo pekee la usimuliaji wake
yeye mwenyewe anapaswa afurahie kitendo hicho
50
(iv) Anapaswa kuwa mtu mwenye kumbukumbu nzuri
asiwe msahaulifu
pindi anaposahau, aweze kubuni mbinu mpya itakayofidia pengo hilo
(v) Anatakiwa asiwe na aibu
wakati mwingine anatakiwa atumie hata viungo vyake vya mwili ktk kuigiza matukio muhimu
wakati Fulani anatakiwa kutumia lugha Fulani kwenye muktadha mahsusi
Anapaswa kuijua vyema lugha na utamaduni wa hadhira yake
UBUNIFU ndio sifa ya msingi kwa msanii. Kutokana na sifa hii, fanani anawea kufanya na kutenda yanayotakiwa na hadhira yake ipasavyo
4.0 Nafasi ya Hadhira ktk Utendaji wa FS
Hadhira husimama kama wasikilizaji, wahakiki washiriki, watoa maoni kuhsu sanaa husika. Katik FS Hadhira ni kichocheo cha ubunifu kwa msanii. Kimsingi tanzu nyingi za fs haziwezekani bila kuwa na hadhira. Kwa mfano, vitendawili haviwezekani bila kuwepo na hadhira. Kuna aina/ndui kuu mbili za hadhira: Hai na Tuli
Hadhira Hai
-Hii ni hadhira inayoshirikiana kwa kiasi kikubwa na fanani au msimuliaji wkt wote wa utendaji wa FS. Katika hali hii hadhira hushiriki katika utendaji kwa kuonyesha vionjo
vyake kmv
kutoa maoni,
kucheka,
kuuliza maswali,
kuimba,
51
kucheza,
kupiga vigelegele nk..
Nafasi ya hadhira ktk FS inaonekana ktk kipengele hiki.
Aina hii ya hadhira hutupatia utendaji Nyoofu, na mara nyingi hupatikana ktk HADITHI, METHALI, VITENDAWILI, NAHAU na vipera vingine vya FS
4.2 Hadhira Tuli
Husikiliza tu kwa makini uwasilishwaji wa FS
Hadhira haitoi wala haiionyeshi vionjo vyake badala yake hubaki tu km mtazamaji tu
Hutupatia utendaji Changamano na mara nyingi hupatikana ktk tanzu chache za FS kmv USHAIRI.
KWA UJUMLA: Hadhira ndio huipa uhai FS na ndio kichocheo cha ubunifu kwa Msanii au Fanani. Mara nyingi fanani ni mtumwa wa Hadhira kwani hulazimika kufuata matakwa ya hadhira kutegemea na ushiriki wa hadhira husika. Hadhira iliyochangamka, inaweza kuvyaza utendaji thabiti na muruwa ilihali hadira legelege inaweza kuvyaza utendaji uliopwaya na kudoda.
Fikiria ni kwa vipi fani, tukio, wakati na mahali pa kutendea huathiri utendaji wa FS? Kwa msaada zaidi soma Mulokozi 1996
52
Nyenzo za UTENDAJI wa FS
Nyenzo za utendaji ni zana au vifaa vinavyotumiwa na fanani kufanikisha uwasilishaji wa sanaa Fulani mbele ya hadhira.
Nyenzo hizo ni nyingi, hutegemea muktadha wa kiutendaji
Nyenzo hizi huchukua nafasi ya maandishi katika FA
Kuonyesha vituo, vikubwa au vidogo (nukta au koma)
Kuonyesha mshangao
Kuonyesha msisitizo
Kuonyesha dharau
Kuonyesha hisia mbalimbali za fanani pamoja na hadhira.
Mfano wa nyenzo hizo ni pamoja na
Sauti ya Fanani na Hadhira
Toni katika matamshi
Ridhimu
Ala za muziki
Enanga,
Filimbi
Vibuyu
Muziki na dansi
Miondoko na madoido vingine vya fanani
Vichocheo vya hadhira kwa Fanani (kupiga makofi, kushangilia, kuzomea na kupiga vigelegele)
Maleba na mapiku
Nyenzo hizi tunaweza kuziweka katika makundi matatu: nyenzo za kiisimu; nyenzo za kimuziki; nyenzo za kuonekana.
53
5.1 Nyenzo za Kiisimu
Lugha nyingi za kiafrika zinasifa ya utoni. Katika utendaji wa FS, fanani wanatumia sauti zao kuunda midundo mahsusi yenye ladha ya kipekee. Midundi hiyo huzaa ridhimu ya namna fulani.
kwa hiyo kupanda na kushuka kwa sauti, takriri, tanakali sauti ni sehemu ya nyenzo za kiisimu zinazochangia utamu ktk FS.
nyingi ya hizi hujitokeza zaidi ktk USHAIRI, METHALI na NGOMEZI, pia katika
VITENDAWILI
Hapa zinatumika kama kipengele cha kimuundo na kimtindo katika kukamilisha maana ya FS
ni vizuri kuitambua vyema lugha inayotumika katika sanaa ya FS, kwani lugha ni kipengele muhimu cha kimtindo na kimuundo. Kinasaidia kuibua hisia, kujenga picha halisi za dhana inayodhamiriwa.
5.2 Nyenzo za Kimuziki
kundi hili linajumuisha ala za muziki, muziki, ngoma (kifaa). Nyingi ya nyenzo hizi ni za kusikika zaidi, kwa kuwa tunahisi utamu wake kwa njia ya ogani ya masikio yetu. Kwa kiwango kikubwa zinaingiliana na zile za kiisimu.
ala mbalimbali za muziki hutumika kukamilishia na kujalizia mapengo ya namna Fulani ktk fs, kwa mfano tendi za Enanga (Wahaya) zinatumia kifaa kiitwacho Nanga. Ala hizo hutumika kutoa na kutengeneza mdundo muruwa wa kimuziki. Pengine muziki hukamilishwa na upigaji wa ngoma. Kutokana na mdundo wa ala, muziki na ngoma kwa pamoja fanani anaiwasilisha sanaa yake vyema na hadhira pia hupata fursa ya kushiriki kwa kucheza, kufurahia na kushangilia.
fani zinazotumia ala za kimuziki ni pamoja na Tendi Simuilizi, ngoma (kama sanaa), …..
5.3 Nyenzo za Kuonekana
54
Kutabasamu; Kucheka; Kununa; Mavazi (Maleba); Kuigiza (kutembea, kuruka, kukaa, kusimama na matendo mengine); Kupungia mikono; Kupepesa macho; Kubinuabinua
midomo; Kukataa/kukubali jambo kwa ishara
Nyenzo hizi zimesambaa na kuzagaa katika tanzu mbalimbali za FS. Takribani tanzu zote zinaweza kutumia nyenzo hii, kutegemeana na ustadi na matakwa ya Fanani na Hadhira.
Nyenzo zote zafahamika sana, labda tufafanue kidogo kuhusu Maleba
Haya ni mavazi ya kiubunifu yanayovaliwa na watendaji wa FS
Ijapokuwa mavazi hayo ni ya kawaida, lakini yanapotumika kisanaa, huonekana mageni na mapya. Upya huo ni muhimu sana kwani huibua hisia
na kuimarisha dhamira iliyokusudiwa.
Kwa mfano:
Waganga/wauguzi wa Kijadi mara nyingi wana mavazi maalum, je yakoje na yanaathari gani kwa mganga mwenyewe na pia kwa wateja wake?
Katika maigizo mengi (kumbuka sanaa ya uigizaji), kuna mavazi maalum: michezo ya watoto, matanga, majigambo, malumbano ya watani, jando na unyago)…. Kuna mavazi mahsusi. Yakoje, yanaashiria nini na yanaleta athari gani kwa hadhira na kwa fanani
Utendaji imara unazingatia pia ustadi wa Maleba.
Maleba: Wamitila anaihusisha na Sanaa za maonyesho kwa kusema kuwa;
Ni Istilahi inayohusishwa na Sanaa za Maonyesho na Drama
Hutumiwa ktk upana wake kuelezea mavazi, uvaaji, na uwasilishi wake ktk igizo lolote
Huweza kuhusisha vitu kmv mafigu na vinyago
Kimsingi nyenzo hizi tunaweza kuzielewa vyema kwa kurejelea aina mahsusi ya utendaji katika tanzu mahsusi za Fs. Katika kozi hii tutatumia tanzu za ngano (simulizi) mbolezi na Ngomezi. Lengo ni kuonyesha namna utendaji
55
unavyojitokeza, nyenzo mbalimbali za kiutendaji katika tanzu hizo na Umuhimu wa suala zima la kiutendaji katika FS.
6.0 UTENDAJI ktk Tanzu Mbalimbali za FS
Tanzu tutakazojadili katika kozi hii ni Masimulizi (Utambaji wa Hadithi), Nyimbo (Uimbaji), Ngoma (Uchezaji) na Maigizo (Drama/Uigizaji).
6.1 Utendaji katika Masimulizi: Masimulizi ya hadithi ni utanzu mpana wa FS wenye vipera vingi k.m.v. visasili, tarihi, vigano, saga2, kumbukumbu za kihistoria n.k.
Katika moduli hii tutashughulikia Ngano.
Mbali na sifa nyinginezo Ngano ni utanzu wa kinathari ktk FS unaojihusisha na Utambaji au Usimulizi wa Hadithi
Kuna uhusiano mkubwa kati ya utambaji wa hadithi/ngano na utanzu wa FA uitwao Hadithi fupi.
Maoni ya Wataalamu mbalimbali kuhusu Ngano na Utambaji wa Hadithi
Jan Vansina 1985
Usimuliaji wa hadithi ni moja ya utendaji maarufu ktk jamii nyingi za kiafrika
Mara nyingi mtambaji anakaa jioni na kuzungukwa na wasikilizaji
Katika jamii nyingi, utambaji wa hadithi ulifanyika wakati maalum, hasa usiku, kila siku
Lakini kuna baadhi ya hadithi zilitambwa mara baada ya kupita muda mrefu, na sio kila siku. Kwa mfano katka jamii ya Wadogo huko Mali, Usimulizi wa
hadithi ulifanywa kila mara baada ya miaka sita.
2
Saga: Hadithi fupi fupi zinazosimulia mambo ya kishujaa. Ni hadithi fupifupi
lakini zina vitushi vya kishujaa
56
Usimuliaji haukuwa marudio ya matukio bali ulikuwa km uigizaji.
Hadithi inasimuliwa kwa kutumia viungo vya mwili, hata km msimulizi amekaa.
Pia, Fanani anaweza kukaa, kusimama, kutembea, na hatimaye kuigiza vitendo muhimu vya hadithi kwa kutumia viungo vyake vya mwili
Ktk usimulizi huo palikuwepo na historia
Fanani wa hadithi walitofautiana kutoka jamii moja na nyingine. Hivyo, usimuliaji pia hutofautiana … hata ktk mianzo ya hadithi hizo…
Ktk baadhi ya koo ambapo walikuwa na Uchawi, walitumia uchawi wao kusimulia hadithi kwa kuwatoa hadhira ktk ulimwengu halisi na kuwalpeleka
ktk ulimwengu wa kigeni
Hadithi moja ikisimuliwa kwa watu mbalimbali, hata km msimuliaji akiwa yule yule na msuko wa hadithi ukawa mmoja, na miririko…. Hadithi hiyo
huonekana tofauti kabisa
Usimuliaji wa hadithi ktk jamii nyingi Barani Afrika, umebadilika sana. Hii ni kutokana na athari za kielimu, kimazingira, kiuchumi nk… kwa
mfano leo hii, usimuliaji wa hadithi unafanyika hata katika redio, televisheni……….
King ei na Kisovi 1995
Hadithi simulizi huwa fupi fupi
Huwa na mtindo wa moja kwa moja
Hii ni ili kurahisisha utendaji wake
Akivaga na Odaga 1998
Hadithi huweza kusimuliwa baina ya watu wa makundi tofauti: mtu mzima kumsimulia mtu mzima; watoto kwa watoto; ………
57
Usimuliaji wa hadithi hufanyika nyakati za jioni kabla ya kula au baada ya chakula cha jioni/usiku
Mahudhurio si lazima wakti wa usimuliaji
Harold Scheub 1998
Utambaji wa Hadithi ni province ya wanahistoria, wanasheria, wanasaikochanganuzi, na wanafasihi
Hadithi zimekuwa zikitumika kama kiunganishi kati ya zamani na sasa, kuchunguza na kufafanua zamani kwa kutumia muktadha wa kisasa na kinyume chake
Mhimili mkuu wa utambaji wa ngano ni ridhimu: uruwazishaji wa kategoria mahsusi za taswira katika linear movt unaoingiza hadhira katika uzoefu wa sitiari.
Kwa hiyo, taswira ndicho kipengele muhimu zaidi ktk utambaji wa ngano.
Utendaji katika Utambaji wa Ngano
Huu ni utanzu uliosambaa takribani ktk jamii nyingi Barani Afrika.
Unatambwa na watoto, watu wazima, wake na pia wanaume
Mara nyingi, nyakati za jioni kabla au baada ya chakula cha usiku. Baada ya kazi. Ni sehemu ya burudani, watu wanafanya kwa ajili ya kupumzisha miili yao, baada ya kazi ngumu za uzalishaji mali walizofanya mchana kutwa.
huchukua muda mfupi na hufanyika kwa zamu miongoni mwa wahusika
Ktk utambaji wa ngano kuna matumizi makubwa ya innovation na matnipulation
Mara nyingi watambaji wa ngano wanakuwa wanadondoo tu zinazohusu simulizi fulani, na wala sio hadithi nzima
Mtambaji anatarajiwa kufanya adjustment muafaka ktk ngano huska kulingana na matakwa ya hadhira
58
Ili kuufanya utambaji uwe more vivid and convincing, mtambajia analazimika
„kuacompany maneno ya hadithi pamoja na appropriate face anda body movements to illustrate such things as fear, anxiety, delight and the behaviours of characters in the tale
Baadhi ya ngano hutambwa na mtu mmoja mmoja, ilihali wengine wakiwa ni hadhira. Utambaji wa namna hii, mara nyingi hauna ala za muziki, bali kunakuwa na uigizaji, uimbaji na miondoko wa fanani mbele ya hadhira.
Pia kuna hadithi nyingine hutambwa na kundi la watu zaidi mtu mmoja. Kwa mfano ktk hadithi ya Ozidi. Katika hadithi za namna hii,: * kuna watu wanaosaidiana na mtambaji kuiumba hadithi * kuna muziki * kuna ala za muziki * hutambwa kwa muda wa siku saba
kuna uchezaji * pia kuna uigizaji wa matukio na vitushi muhimu ktk ngano/saga * kuna
vichocheo vingi kutoka kwa hadhira kmv MASWALI, KUSHANGAA, VICHEKO,
MAONI……pia majibu ya fanani kwa hadhira yake.
Kwa kiwango kikubwa utendaji wa hadithi za namna hii umeathiriwa na hadhira husika
UTENDAJI katika Nyimbo
6.2.1 Nadharia ya Nyimbo: Maana, chimbuko na dhima yake ktk jamii
Dhana ya Nyimbo
Matteru:
Nyimbo ni tungo za kishairi zenye kutumia mahadhi, melodia, mkongosio, mapigo na muwala
Pia huweza kuimbwa na mtu mmoja pekee, mtu mmoja pamoja na wazumi wake na kundi la waimbaji pamoja na wazumi wao.
Dhima ya wazumi ni kuitikia mkarara.
Mulokozi:
(i) Kila kinachoimbwa
59
(ii) Nyimbo hutambulishwa na: * muziki wa sauti ya waimbaji au muimbaji, * muziki wa ala (km ipo), * matini/ maneno yanayoimbwa, * hadhira (km ipo), * muktadha (unaofungamana na wimbo huo…. Sherehe, ibada, msiba.. nk). NYIMBO za maombolezo….. katika misiba ili kuwaliwaza wafiwa.
(iii) Kuna makundi 15 ya nyimbo (tumbuizo, Bembea, Kongozi, za kidini, wawe, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso,za vitani, uwindaji, za taifa, za watoto na za kazi).
Kwa ujumla: Nyimbo ni tungo zenye mahadhi ya sauti yaliyopangiliwa kwa sauti zenye kupanda na kushuka kwa uwiano maalum. Tungo hizi zinaundwa kwa lugha ya mkato, mpangilio wa silabi na ala (ngoma, marimba, pembe, kinanda, zeze,- ingawa sio lazima).
Chanzo cha Nyimbo ktk jamii
Freuchen (1962)….. nyimbo ni mawazo yanayoimbwa na watu baada ya kusukumwa na nguvu maalum. Mawazo hayo hayawezi kutolewa kwa hadhira ktk mazungumzo ya kawaida yakaeleweka, ama kuleta athari iliyokusufiwa. Kumbe mawazo ya wanadamu yanasukumwa na nguvu maalum…. Furaha, hofu, uchungu
Nguvu hizi, huzua msongamano wa mawazo katika kichwa cha mwanadamu, huzidi kiasi kwamba mwanadamu anashindwa kupumua vizuri, anapatwa na mashaka na moyo humdunda. Mapigo ya moyo huongezeka,
Athari hii huzua matukio mapya, na kunakuwapo na haja ya kupatikana kwa maneno ya kutuliza hali hiyo, au kulieleza jambo hilo vyema. Maneno hayo yatajitokeza yenyewe, na kwamba ndiyo yanayounda wimbo, tena wimbo mpya
Kimsingi … mazingira. Mazingira humfanya mtu awaze na kuwazua. Katika kuwaza na kuwazua hisia muafaka hupatikana, kisha mawazo hurejea tena katika hali ya kawaida. Hapa, mwanadamu anawaza tu pasipo kuwazua.
Nyimbo zinabeba mawazo na ujumbe mzito ktk jamiiunaokusudiwa kuonyesha uhusiano wa kijamii, migogoro, kejeli, kuliwaza, kubembeleza, kutumbuiza na kuburudisha. Kimsingi,
60
shughuli zote zinazofanywa na mwanadamu (kulima, kuwinda, kufuga, kuchunga, kutwanga, kusuka, kufua……) huenda sambamba na uimbaji wa nyimbo
6.2.2 Suala la Utendaji ktk Nyimbo
Kutokana na upana wake, nyimbo hujitokeza kama
sanaa inayojitegemea
(rejea nyimbo zinazoimbwa katika jamii mbalimbali kukidhi mahitaji anuwai)
pia kama kijalizo cha sanaa nyingine
(kwa mfano ktk FS…..kmv utambaji wa ngano)
Kama sanaa inayojitegemea nyimbo zinakidhi dhima mbalkimbali katika jamii kmv
Ni mojawapo ya zana ama vyombo muhimu vya utamaduni
Huelekeza wanajamii kuhusu mienendo bora ya maisha
Hufichua yaliyofichikana ktk jamii
Huelimisha,
Huburudisha
Kuliwaza na kuhuzunisha
Kama kijalizo cha sanaa nyingine, nyimbo hutumika kwa minajili ya:
Kusisitiza kiini/wazo kuu ktk simulizi
Kushirikisha hadhira
Kuchangamsha hsdhira
Kuiliwaza hadhira
Kuwazindua hadhira na kuwafanya wawe makini zaidi
Kupambanua wahusika na matukio muhimu ktk fs
Kuipa uhai sanaa inayotendwa
Kutokana na dhana na dhima au nafasi ya nyimbo ktk jamii, Msanii wa nyimbo anapaswa;
61
Kuielewa vyema hadhira yake
Kuielewa vyema lugha yake
Azingatie muktadha wa jamii na tukio husika, kmv masikitiko, huzuni, chuki, upendo, uaguzi, imani, uzalendo….azingatie ufasaha na ukweli unaoendana na muktadha husika
Kuzingatia mabadiliko ktk jamii kmv siasa, uchumi, utamaduni. Anapaswa asiwe pembezoni mwa wanajamii, ili ayajue mapya na ayatengenezee nyimbo, kwani nyimbi zapaswa kwenda sambamba na mabadiliko yanayjitokeza ktk jamii.
Utendaji ktk Maigizo
6.4.1 Nadharia ya Sanaa ya Maigizo: Dhana, aina na dhima yake ktk jamii
Istilahi na Fasili ya Maigizo
drama, michezo ya kuigiza, sanaa za maonyesho, tamthiliya na thieta
Maneno au majina haya mara kwa mara yanatumika kwa kubadilishana nafasi, ili mradi si rahisi sana kuyatofautisha, inagalau tunafahamu wazi
kuwa hizi ni Istilahi tofauti enye kuwakilisha dhana tofauti
hata hivyo, dhana kuu inayojitokeza ktk sanaa hii ni Uigizaji
Kwa hiyo tunaweza kufasili maigizo katika FS kama ni sanaa inayohusisha uigaji wa tabia na matendo ya watu au viumbe wengine ili kuburudisha na
kutoa ujumbe fulani.
Uigizaji huo huweza kuwa wa sauti, miondoko, mavazi (maleba).
Historia ya Maigizo Afrika
Saifu D. Kiango 1973
62
Ameeleza kwa kirefu maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili upande wa Michezo ya kuigiza. Katika makala yake hii tunabaini kuwa:
Kuna maigizo yaliyoandikwa (ya kisasa) na yasiyoandikwa (ya zamani zaidi)
Yasiyoandikwa :
Haya ni ya zamani sana na yalikuwepo Afrika hata kabla ya ukoloni. Yalijumisha fani nyingi Barani Afrika kmv.
Ngoma za makabila mbalimbali Afrika
Michezo ya watoto
Yaliyoandikwa
ya Kishairi kwa mfano tenzi na ngonjera za watunzi mbalimbali. Kazi za M.Mnyampala (Ngonjera za Ukuta), E.Kezilahabi (Dakika 15 za Uzalendo),
Ahmad Nassir (Tumsihi). Pia tenzi za Fumo Lyongo na Maisha ya Adam na Hawaa. Kazi hizi zina masimulizi na majibizano yanayofaa kuigizika. Kwa hiyo ni sehemu ya sanaa za Maigizo zilizotumia mbinu za kiuandishi, kitenzi na kingonjera.
yasiyo ya kishairi kwa mfano tamthiliya mbalimbali kmv Mgeni Karibu,
Afadhali Mchawi na Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi. Zipo kazi nyingi sana za namna hii. Kazi hizi zimeandikwa kwa kutumia lugha ya mazungumzo ya kawaida, lakini katika mtindo unaowezekana kuigizika.
M.M Mulokozi
Anaelekea kukubaliana na Kiango
Anaongeza kuwa mara nyingi drama za Kiafrika huambatana na NGOMA3, UTAMBAJI WA HADITHI, NYIMBO, MATAMBIKO NA SHEREHE ZA KIJADI
3
Kwa Waafika Ngoma ina dhana tatu: kama sherehe kubwa ya kijamii (mivigha na matambiko), kifaa/ala
ya kutolea muziki na km kitendo cha kuchezesha viungo vya mwili huambatana na miondoko ya kimuziki. Hapa ni uchezeshaji wa viungo. (Balisidya na Mhando).
63
Kutokana na mawazo ya wataalmu hawa:
Maigizio ni sanaa pana yenye vipera mbalimbali kmv;
Maigizo ktk michezo ya watoto
Maigizo ya misibani (Matanga)
Maigizo ya sherehe za kuzaliwa kwa watoto, jando, na unyago
Maigizo ya kidini
Hata ktk majigambo na malumbano ya watani
Pia ktk shughuli za kijamii kmv uwindaji na kilimo
Sanaa ya Maigizo inaingiliana sana na sanaa nyinginezo za FS, husuani Ngoma
Licha ya mabadiliko makubwa yaliyojitokeza katika sanaa hii, tangu enzi za Kikoloni bado sanaa hii ni hai na ina upekee wa aina yake
Upekee wake unajidhihirisha ktk utendaji wake
Katika utendaji wake tunabaini vionjo kadhaa vya kiubunifu kmv
uigaji wa tabia, mienendo……
mavazi maalum ya kisanii/maleba
jukwaa/uwanja wa kutendea sanaa husika
nyenzo za kisanaa kmv njuga, filimbi, vinanda, silaha za jadi
kiwango kikubwa cha ushirikishwaji wa hadhira
6.3 Utendaji katika Ngomezi
Hii ni sanaa inayotumia ngoma kuwasilisha taarifa kwa jamii. Baadhi ya makabila huweza kusambaza habari za kijamii (matukio ya dharura, mf. Vita, msaragambo, pia habari kuhusu kazi za kijamii kmv usafi wa mazingira na ujenzi wa barabara) kwa njia ya ngoma. Mahala pengine ngoma hutumika sambamba na sana nyingine kmv hadithi, jando na unyago
64
Ktk Ngomezi kunakuwa na midundo Fulani ya ngoma yenye kuwasilisha kauli mahsusi ktk lugha ya kabila husika. Mara nyingi kauli hizo ni kishairi na zenye mafumbo. Akifafanua zaidi kuhusu sanaa ya ngomezi J.R. Nketia 1963:174 anaelezeaa namna tatu za upigaji wa ngoma:
Mdundo-ishara
Mdundo-kalima
Mdundo-dansa
Mdundo unaoshughulikiwa hapa ni ule wa upigaji ngoma wa kalmia yaani mdundo wa ngoma wenye kutoa maana na ujumbe Fulani
Naye R.Finnegan 1970:483-4 anafafanua kuwa katika ngomezi lugha hufuata kanuni za lugha ya kawaida (hususani toni na mawimbi ya sauti). Kwa hiyo lugha ya ngoma ni aina ya uandishi: kwa maneno mengine ni aina ya ishara zinazowakilisha maana unaoana vizuri na lugha zenye toni
Kwa ujumla, sanaa ya ngoma hutumia fomula na kauli za kimapokeo (uimbaji, uchezaji, uigizaji wa matukio na mambo anuwai yanyofahamika ktk jamii husika)
Kauli hizo zinafahamika na watu wengi ktk jamii inayohusika
Zinatumiwa kutoa, kuhifadhi, au kupeleka ujumbe toka sehemu moja hadi nyingine
Huchukua umbo la lugha ya kishairi na kimafumbo (ujumbe na fani yake pia)
Hitimisho
Swali la msingi tulilopaswa kujibu katika moduli hii ni “Je, UTENDAJI una nafasi gani katika
FS? Katika kujibu swali hili Finnegan aliwahi kusema kuwa;
“ORAL LIT. is by definition dependent on a performer who formulates it in words in a specific occasion- there is no other way in which it can be realized as a literary product” …. P.2
4
Mtaalamu mashuhuri wa muziki kutoka Afrika Magharibi
65
Kutokana na dondoo hii, tunapata kutanabahi umuhimu na nafasi ya UTENDWAJI katika FS.
Tunakubaliana na wazo kuwa UTENDWAJI NDIO UTI WA MGONGO WA FS. Umuhimu
na nafasi ya UTENDWAJI ktk FS tunaupata…..
Tunapodiriki kufasili maana ya FS tunapaswa tuzingatie kuwa umbo halisi la FS ni la kiutendaji
Hata tunapogawa FS ktk tanzu mbalimbali yatupasa tuzingatie hali ya kiutendaji
Uumbaji wa sanaa mbalimbali za Fs umefungamana na suala la usambazwaji wa sanaa husika. Hakuna mpaka kati ya mchakato wa uumbaji, uwasilishwaji na uwepo wa sanaa
husika
Hatuwezi hata kutambua athari ya au nafasi ya aina mahsusi ya fani za FS bila kuchambua utendwaji wa sanaa husika.
Kipengele chochote cha FS (kifani na kimuundo au cha kimaudhui……) havina maana yoyote km havitendwi. Katika muktadha wa kiutendwaji, ndimo tunapa kufahamu maana
na umuhimu wa vipengele hivyo katika fs na ktk jamii.
Hata pale itakapolazimika fs kuandikwa au kuhifadhiwa kwa njia nyingine yoyote ya kidijitali, bado fani hiyo itakayokuwa imehifadhiwa haitakuwa halisi, bali itakuwa ni
kivuli tu fani husika km kipengele cha kiubunifu wa fanani, na hadhira.
Kwa kuhitimisha, nadharia ya utendaji katika FS ina mchango mkubwa sana ktk taaluma ya FS. Imesaidia kujibu mwaswali ya msingi kuhusu FS kwa ujumla, hususani FS ya Kiafrika, isitoshe, imechochea masuala nyeti ya kiudadisi kuhusu taaluma hii. Masuala hayo kimsingi ndio yanatufanya tukiri kuwa UTENDWAJI NI UTI WA MGONGO WA FS.
Tangazo Michezo yakubet
KUJIUNGA NA PARMACH TZ NA KUPAKUA PARMACH APK
BOFYA >>>HAPA>>> kisha jaza taarifa zako udeposit kupokea bonasi
- 22bet tanzania app jisajili na upakue kwa kubofya >>HAPA>>