Tuesday

UDHAIFU WA KUFASILI KISHAZI KAMA KUNDI LA MANENO LENYE KIIMA NA KIARIFU

0 comments


Kishazi kama kundi lenye kiima na kiarifu ni fasili iliyo tolewa na massamba 2004. Hatahivyo fasili hii  inamapungufu kadha Wa kadha kwani kusema kishazi kina muundo Wa kiima na kiarifu ni sawa na kusema kishazi ni sawa na sentensi.
Je nikweli kubwa kishazi kina hadhi ya kubwa sentensi?
Hapana hata hivyo kishazi Huru pekee ndicho chenye hadhi ya kuwa sentensi sahili. Vipi kuhusu kishazi tegemezi?

Labda tungepitia kwa kina maana ya kiima na kiarifu

Kwa ufupi kiima  ni sehemu katika sentensi inayo kaliwa na nomino ya mtenda au ni sehemu ya kwanza ya sentensi

Kiarifu ni sehemu ya pili katika sentensi inayo arifu kuhusu kiima na hukaliwa na kirai kitenzi.


Embu tuchunguze hiki kishazi tegemezi

1. Iwapo utanipigia magoti

Je kiima chake ni kipi?

2. Baada ya kumaliza kusali
Je kiima na kiarifu utazigawaje?

Na je iwapo sentensi inavishazi viwili mfano
 Habiba ameanza kuimba baada ya kumaliza kuswali.

Habiba ameanza kuimba ni Kishazi cha kwanza

Baada ya kumaliza kusali ni Kishazi cha pili , je katika tungo hiyo kwa mkabala huo ingepaswa kuwa na viima viwili na kiarifu viwili katika sentensi moja kitu ambacho sio sahihi.

mjadala utaendelea
Niandikie kupitia info.masshele@gmail.com

No comments:

Post a Comment