Mbegu ambazo zilipelekwa mwezini na chombo cha utafiti wa anga za juu cha Chang'e-4 hatimaye zimechipua, mamlaka jijini Beijing zimethibitisha.
Taarifa hizi ni za kwanza kusikika kuwa mmea wa kibaolojia umechepua mwezini na ni hatua inayofungua njia ya tafiti zaidi za kisayansi mwezini.
Chang'e 4 pia ndiyo chombo cha kwanza kutafiti sehemu ya mbali zaidi ya mwezi ambayo haitazamani na uso wa dunia.
Chombo hicho kilitua mwezini Januari 3 kikiwa kimebeba vifaa vya kuchunguza jiolojia ya eneo hilo.
Hii inafungua milango ya uwezekano wa wanaanga kuweza kuzalisha chakula chao wenyewe wakiwa anga za mbali na kupunguza uhitaji wa kurudi duniani ili kufuata chakula.
Chombo hicho cha China kilibeba udongo wenye mbegu za pamba, viazi na hamira.