Mghana James Kotei
KIUNGO mkabaji wa Simba, Mghana James Kotei amefunguka kuwa wameenda kupambana na AS Vita Club kuhakikisha wanaondoka na ushindi.
Kesho Jumamosi, Simba itakuwa ugenini kukipiga dhidi ya wenyeji wao, AS Vita Club ukiwa ni mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi.
Timu hiyo ipo katika Kundi D lenye timu za Al Ahly, JS Saoura na AS Vita Club huku Simba ikiwa ndiyo kinara baada ya kushinda mechi iliyopita kwa idadi kubwa ya mabao.
Kotei ambaye yupo na timu DR Congo kwa sasa, amesema kuwa wamejipanga vyema na wanakwenda kupambana kuona timu hiyo inaibuka na ushindi licha ya kwamba ni ugenini. “Tunajua ni mchezo mgumu lakini tunaenda Congo tukiwa tumejipanga kwenda kusaka pointi muhimu ili kuwa katika nafasi nzuri.
“Lakini tutapambana kwa bidii zote huku tukiamini kile ambacho tunaenda kukipigania tunastahili kukipata na si vinginevyo,” alisema Kotei. Kotei amekuwa chaguo la kwanza katika kikosi hicho kwa msimu huu huku mechi nyingi akicheza nafasi ya kiungo mkabaji.
NA Martha Mboma,