Wednesday

MCHICHA WAANGUSHA MBUYU SIMBA WAFA 3-2 TAIFA NA KUFUNGASHIWA VIRAGO KOMBE LA SHIRIKISHO

0 comments


RAUNDI ya tatu, kwa sasa mchezo kati ya Simba na Mashujaa ambao unachezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao ni wa kombe la Shirikisho unaendelea.


Mashujaa wanasawazisha bao la Paul Bukaba dakika ya 48 na kufanya iwe 1-1, Bukaba aliandika bao la kwanza kwa Simba dakika ya 18 baada ya shuti la kona iliyopigwa na Shiza Kichuya kumfikia Said Ndemla aliyepiga shuti kali ambalo mlinda mlango alitema.


Dakika ya 48 Said Hamisi wa Mashujaa anasawazisha bao baada ya Paul Bukaba kuzembea baada ya kumtibulia mipango akaanguka chini.


Dakika ya 57 Jeremia Josephat anaiandikia bao la 2 akitumia makosa yaleyale ya mabeki wa Simba na kuwanyanyua mashabiki wa Mashujaa, Rashidi Athuman anaandika bao la 3 dakika ya 90 akiwa nje ya 18.

Faulo iliyopigwa na Clytous Chama aliyeingia dakika ya 60 akichukua nafasi ya Abdallah Seleman na kufungwa na Paul Bukaba dakika ya 80 na kuweka usawa.

Mlinda mlango wa Mashujaa amekuwa ni shujaa kwa kuokoa mashuti ya washambuliaji wa Simba ambao mpaka sasa wamecheza kona 9, huku mashuti mawili ya Rashid Juma na Mzamiru Yassin yakigoga mwamba.

Kikosi cha Simba kina sura nyingi mpya ambazo zimekuwa hazipati nafasi kwenye kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na kinda Abdallah Seleman, Asante Kwasi, Deogratius Munish huku Chama akiwa benchi kusoma mchezo.