Tuesday

KWA SIMBA HII ! MJIPANGE KISAIKOLOJIA BAADA YA KAGERE ANAYEFUATA NI HUYU MNIGERIA

0 comments

Unaweza kusema simba sasa hawataki utani hata Kidogo hii nibaada ya  straika Meddie Kagere aliyetoka Gor Mahia FC kumalizanana mabosi wa Simba baada ya kutua jana nchini, wekundu hao wa Msimbazi wamemshusha mchezaji mwingine kutoka Nigeria, imeelezwa.

Ujio wa Kagere umeambataba na mshambuliaji mwingine kutoka Nigeria, Victor Patrick ambaye amekuja kufanyiwa majaribio na endapo atafuzu ataingia mkataba na klabu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Patrick amewasili kimyakimya nchini na kufichwa na matajiri hao wapya wa jiji la Dar es Salaam katika hotel moja kubwa jijini humo.

Simba wamezidi kuonesha jeuri ya fedha baada ya kumrejesha Pascal Wawa ambaye aliwahi kuichezea Azam FC.

Wakati huo kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani asubuhi ya leo kujiandaa na michuano ya KAGAME inayoanza Juni 29 2018.

No comments:

Post a Comment