Tuesday

UMUHIMU WA MWALIMU KUFAHAMU SHERIA

0 comments

make-d-world-a-beta-placemake-africa-d-sweetest-plc-to-b2.jpg
Kufanya Kilicho Sahihi
Sheria ni nini?
Sheria ni masharti yanayowekwa katika nchi ili kutoa mwongozo wa jinsi ya kufanya mambo kwa usahihi. Sheria lazima zifuatwe na watu wote, na anayevunja sheria huadhibiwa.
Kanuni ni nini?
Kanuni ni maagizo kwa ajili ya asasi kubwa ya umma, zinazoongoza kufanya mambo yaliyo sahihi. Kanuni hizi mara nyingi zinafafanua sheria za nchi.
Taratibu ni nini?
Taratibu ni maelekezo yanayotolewa kwa idara zote za serikali ili kuelekeza kufanya mambo yaliyo sahihi.
1. Mwalimu ni nani katika mazingira yetu ya Tanzania?
Neno “mwalimu” limetafsiriwa kwenye ‘Kamusi ya Kiswahili Sanifu’ TUKI (1981) kwenye ukurasa wa 201 kuwa ni “mtu afundishaye elimu au maarifa Fulani, au mtu anayeonesha wengine”.
Katika Sheria ya Elimu, (sura ya 353 R.E.2002), neon ‘mwalimu’ limepewa maana kwenye fungu la 2 (1) kuwa ni “mtu yeyote aliyesajiliwa kama mwalimu chini ya sheria hii.”
Na fungu la (46) la sheria hii, linaonesha kuwa baada ya mtu kusajiliwa na Kamishna wa Elimu na kupewa cheti, basi mtu huyo anakuwa mwalimu.
2. Umuhimu wa mwalimu kufahamu sheria
Ili mwalimu aweze kutekeleza kwa ufanisi wajibu wake mbele ya umma anapaswa awe na sheria na miongozo ambayo itamsaidia kuelewa vyema utumishi wake kama mtumishi wa umma.
Kanuni za Mpango wa Utumishi wa Umma za mwaka 2005, zilizotolewa kwenye Gazeti la Serikali namba 331 la tarehe 28/10/2005 ambazo zinahusu watumishi wa umma wakiwemo na walimu zinaonesha nyaraka za sheria ambazo mtumishi wa umma anapaswa kuwa nazo.
Kanuni ya 31 (1) ya kanuni hizo inaorodhesha nyaraka hizo kuwa ni;
  1.  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (sura ya 2 R.E. 2002)
  2. Sheria ya Utumishi wa Umma (sura ya 298 R.E. 2002)
  3. Sheria ya Huduma ya Mafao ya Kustaafu (sura ya 371 R.E. 2002
  4. Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Viongozi wa Kisiasa (sura ya 225 R.E.2002)
  5. Sheria ya Huduma ya Umma (chombo cha upatanishi)
  6. Sheria ya Uajiri na Uhusiano wa Kazi (sura ya 366)
  7. Sheria ya Wakala wa Serikali (sura ya 245 R.E. 2002)
  8. Sheria ya Utawala wa Mkoa (sura ya 97 R.E. 2002)
  9. Sheria ya Taasisi za Kazi (sura ya 300)
  10. Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003
  11. Kanuni za Maadili na Tabia za Watumishi wa umma,
  12.  Kanuni mbalimbali za maadili na mwenendo wa wataalam
  13. Kanuni za Serikali kwa ajili ya huduma za Umma
  14. Kanuni za kuajiri wahudumu wa umma
  15. Kanuni za nidhamu ya wahudumu wa umma
  16. Kanuni ya usuluhishi na mapatano ya huduma ya umma
  17. Kanuni za kustaafu na kuachishwa kazi ya huduma ya umma
  18. Kanuni ya sera ya uongozi na uajiri wa huduma ya umma
  19. Sheria nyingine za nyaraka zinazohusika kwa ajili ya marejeo yanayohusika
3. Je, mtumishi wa kawaida anaweza kuzipata wapi hizi sheria na nyaraka anazopaswa kuwa nazo mtumishi wa umma?
Kwa mujibu wa kanuni ya 31 (2) na (3) ya Kanuni za Mpango wa Utumishi wa Umma za mwaka 2005 zinaeleza kuwa, “Kila mwajiri atapaswa kuhakikisha upatikanaji na fursa ya kutumia nyaraka zote anazopaswa kuwa nazo mtumishi aliye chini yake”.
Endapo unahitaji ushauri zaidi kuhusu Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma tafadhali wasiliana na Ofisi ya Raisi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Anuani:
Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
S.L.P. 2483,
Dar es Salaam.
Barua pepepermsec@stabs.go.tz
Simu: 2118531/4
Fax: 2125299