Taswira ya Mwonekano itakavyoonekana katika stendi hiyo ikiwemo pia gorofa za hoteli zitakazojengwa eneo hilo.
Mmjoa wa viongoi wa jiji la Dar es Salaam akimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (hayupo pichani) mchoro wa stendi hiyo mpya ya Mbezi-Luis itakavyokuwa.
Makonda na viongozi wengine wakiangalia runinga iliyokuwa ukutani ikionyesha ramani ya ujenzi huo.
Michoro mbalimbali ya stendi hiyo.
STENDI ya Mabasi yaendayo mikoani Ubungo ambayo inahamishiwa Mbezi-Luis jijini Dar es Salaam tayari imetengewa Shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi mwezi ujao, ambapo kituo hicho kitakuwa cha kisasa na chenye huduma mbalimbali za jamii ikiwemo mahoteli.
Makubalino hayo yametolewa na Mkurugenzi Wa jiji lake Spora Liana ambaye amemweleza mkuu wa mkoa mikakati mbalimbali ya manispaa zake zilivyotengewa fedha kutoka ofisi ya Rais Dkt.John Magufuli.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda amesema kuwa manispaa za jiji lake zimetengewa bajeti ya bilioni 250 kutoka mfuko wa Rais ili fedha hizo zitumike kujenga vitega uchumi vilivyo ndani ya manispaa za jiji hilo ili hapo baadaye manispaa zenyewe ziweze kujiendesha kwa mapato zenyewe bila kuhitaji mikopo tena zenye liba kubwa.
Makonda, amesema kuwa wananchi waendelee kumpa ushirikiano Rais Magufuli kwani amedhamiria kwa dhati kuweka mazingira bora kwa wananchi wake.
Amesema Stendi hiyo ya kisasa iliyotengewa bilioni 50 lengo ni Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na kituo bora na kutengeneza ajira kwa vijana pamoja na wageni mbalimbali kuweza kufika kwa ajili ya utalii wa ndani.
Pia soko la kisutu, machinjio ya Vingunguti na mambo mengine yametengewa bajeti kutoka ofisi ya rais tayari kuanza kwa ujenzi ili wakazi wa jiji la Dar waweze kunufaika.
Ameeleza lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na raslimali ya nchi yake japokuwa wapo baadhi ya watu wasioipenda maendeleo ya nchi na kuzungumza mambo yasiyokuwa na manufa kwa Taifa.
Makonda amewataka wakurugenzi kusimamia fedha hizo zilizotolewa na Rais kwani ambaye atakwenda kinyume hatasita kumripoti kwa rais kutokana na kwenda kinyume.