Thursday

MIWASHO UKENI (VAGINAL ITCHING)

0 comments

Miwasho/michomo sehemu za siri/Ukeni huweza kusababisha  kujisikia vibaya na hasa mwanamke akiwa sehemu za watu kwa sababu hushindwa hata kujizuia kujikuna.

Miwasho ukeni huashiria kuna maambukizi au kitu fulani kigeni kimeingia sehemu hizo na hivo lengo la kipengele hiki ni kuzungumzia vitu na maambukizi yanayosababisha miwasho ukeni

Nini husababisha miwasho Ukeni?

Maambukizi mbalimbali yanaweza kusababisha miwasho ukeni kama;
  • maambukizi ya bakiteria
    • maambukizi ya bakiteria maeneo haya huweza kusababisha miwasho pamoja na kuhisi kama unaungua , kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na kutoa uchafu ukeni
  • Magonjwa ya zinaa/sexual transmitted disease (STD)
    • Kisonono, kaswende, trichomoniasis, virusi vya herpes na maoteo sehemu za siri inayosababishwa na  ya virusi vya human papilloma(genital warts)
  • Mambukizi ya fungusi ukeni(yeast infection)- wanawake wa3 kati ya 4 watapata maambukizi haya maishani mwao. Maambukizi haya hutokea pale ambapo wadudu hawa wamekua vihatarishi ni
    • Kufanya mapenzi na mtu mwenye fungasi
    • Ujauzito
    • Kinga ya mwili kuwa chini


Wanawake wote wapo hatarini kupata maambukizi haya kama kinga zao za mwili zipo chini, mbali na kuwasha mgonjwa hutoa majimaji meupe au kama maziwa ukeni
  • Kukoma kwa siku za mwanamke(menopause)- kutokana na mabadiliko katika mfumo wa vichochezi mwili, wanawake waliokoma kuona siku zao mara nyingi kichochezi cha estrogeni huwa chini sana na kusababisha uke kuwa mkavu na kuta kuwa nyembamba na hivo huleta miwasho sehemu hizi- pia kwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wananyonyesha tatizo hili linaweza kutokea pia kwa sababu hizi
  • Kemikali mbalimbali zilizo kwenye sabuni, mafuta ya cream au mafuta mengine , baadhi ya pedi, karatasi za kujifutia unapotoka chooni.

Yapo matibabu  ya miwasho ukeni?

Matibabu ya miwasho ukeni yapo ila hutegemea sababu ni nini, ikiwa umetumia dawa flani au mafuta yanayosababisha miwasho basi ni vema kuiacha, miwasho na miunguzo itaisha yenyewe baada ya siku chache.

Ikiwa miwasho na michomo inaendelea au uchafu unatoka ukeni basi ni vema kuonana na dakitari ili ufanyiwe uchunguzi wa sehemu hizi na upatae matibabu sahisi