CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

IDARA YA LUGHA YA KISWAHILI NA ISIMU
TAASISI YA TAALUMA ZA KISWAHILI
JINA LA
KOZI: : FALSAFA YA KIAFRIKA NA NADHARIA
YA FASIHI
MSIMBO WA KOZI:
KF 204
SIKU YA KUWASILISHA:
ALHAMISI
NA.
|
JINA
|
NA. USAJILI
|
KOZI
|
SAINI
|
1.
|
Gaspery Emanuele K
|
2016-04-2479
|
BAK
|
EGM
|
SWALI
LA MUHULA:
Kwa mifano bayana taja na kujadili
vipengele vya falsafa ya kiafrika vinavyojitokeza katika riwaya ya Bwana
Myombekere na Bi Bugonoka, juzuu ya kwanza. Vipengele hivyo vinahalisika vipi
katika jamii yako ya leo.
Katika
kujibu swali hili nimeligawa kaitka sehemu tatu ambazo ni utangulizi, kiini na
hitimisho. Katika utangulizi nimeeleza dhana muhimu katika swali, katika kiini
nimeeleza vipengele vya kifalsafa ya
Kiafrka vinavyojitokeza katika riwaya ya Bwana Myombekere na Bi Bugonoka katika
juzuu ya kwanza na uhalisia wa vipengele hivyo katika jamii.
Odera (1990), anasema Falsafa ni taaluma
ambayo kanuni za msingi kuhusu asili, binadamu na jamii huchunguzwa na
kujadiliwa.
vilevile Sodipo (1993), anasema falsafa
ni udadisi unaohusu dhana na kanuni zinazotuongoz kuhusu uzoefu au mazoea
kuhusiana na maadili, dini, sheria, sheria, saikolojia, historia, sayansi ya
jamii na siasa.
Hivyo,
Falsafa ni mawazo ambayo watu katika jamii wanaamini kuwa ni kweli na yanafanya
mawazo hayo kuendelea kutawala misingi ya maisha toka kizazi kimoja hadi
kingine.
Kuhusu falsafa ya Kiafrika wataalamu kama vile
Placide Temples (1959), Oruka (1990) na Mbiti (1990). Wameifafanua dhana hii ya
falsafa ya Kiafrika kuwa ni fikra au mitazamo wanayoishughulikia Waafrika
wenyewe na watu wengine ambao si Waafrika lakini wanakubaliana na mila na desturi za Kiafrika na fasihi simulizi za
Kiafrika. Hivyo falsafa ya Kiafrika ni ile ambayo imejikita katika mifumo ya
kijamii, mila, desturi na fasihi simulizi za Waafrika.
Kwa ujumla falsafa ya Kiafrika ni mawazo ya
Waafrika wenyewe juu ya mambo mbalimbali wanayoyafanya kama vile imani juu ya
maisha, mila, desturi na jinsi ya kushirikiana katika jamii na kutafuta
masuluhisho juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maisha yao ya
kila siku.
Katika
kujibu swali hili riwaya ya ‘‘Bwana Myombekere na Bi Bugonoka’’ hasa juzuu ya
kwanza ndiyo iliyotumika. Riwaya hii imeandikwa na Aniceti Kitereza na
kufasiliwa na Gabriel Rugumbika mwaka (1980). Kwa ujumla riwaya hii
inazungumzia maisha ya Bwana Myombekere na Bi Bugonoka ambayo yamegubikwa na
changamoto za kifamilia kama vile suala la ugumba ambalo Bugonoka alikumbana
nalo huku wakifanya juhudi za kadha wa kadha katika kuondoa tatizo la ugumba
hasa kupitia kwa waganga hadi walipofanikiwa kupata mtoto aliyeitwa Ntulanalwo.
Katika
riwaya hii vipengele mbalimbali vya falsafa ya Kiafrika vimejitokeza, pia ni
vipengele vinavyohalisika katika jamii vipengele hivyo ni kama ifuatavyo;
Falsafa
ya uchawi, mwanafalsafa Placide Temples anasema Waafrika wanategemea sana nguvu
za kichawi. Suala la uchawi limejitokeza katika riwaya ya Bwana Myombekere na
Bi Bugonoka hudhihirika hayo pale mwandishi anaposema,
‘‘........kisa kilichonifanya nikafarakana na mume
wangu
ni
kwa sababu wake wenzangu ndio walinisingizia ya ka
ma mimi
niliwashika ulozi kuwa wao ndio walioua watoto
wangu baba na ndugu zangu wakapata uchungu
sana waka
nena
ondoka twende pamoja, huwezi tena kukaa hapa saba
bu
wachawi hawa wameanza tangu siku nyingi, tazama jinsi
wameharibu
utumbo (kizazi) wako, tumeshuhudia wazi pengi
ne
wasikuue na wewe pia, nasi tukaambulia bure! Wahenga wetu
walisema,
ekilya isoke, kilya n’obwongo ( kilacho nywele kitau
miza
na ubongo. Basi ndivyo hivyo wamenitoa.............................
Myombekere
akajibu ‘‘Aa! Sivyo, afadhali ingekuwa kama hao wake
wenzako
wangesemwa na watu wengine tuu kwamba wao ndio wachawi
wa
kupindukia hasa, hawalali nyumbani.
(uk-
20)
Yote
haya yanadhihirisha kuwepo kwa falsafa ya kichawi. Pia katika jamii suala la
uchawi ni halisi hasa katika jamii ya Wasukuma ambapo wachawi hutumia nguvu za
kichawi kuua, kuangamiza na kuharibu maendeleo ya watu wengine.
Falsafa
ya nguvu uhai, kipengele hiki kinaelezwa na mwanafalsafa Placide Temples ambapo
anasema Waafrika wanaamini katika nguvu uhai na wanaona kuwa chanzo kikuu cha
nguvu uhai ni Mungu mwenyewe. Nguvu hii upita kwa Wahenga na Mizimu ambapo
hupeleka kwa binadamu na binadamu hupeleka kwa wanyama na mimea. Temples
anaendelea kusema kuwa Waafrika wanaamini nguvu ya waganga na hivyo mganga
anauwezo kubwa wa kupunguza na kuongeza uhai kwa binadamu. Vilevile Temples
anajiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na suala la waganga mfano, dawa
zinawezaje kuponya? Dawa inawezaje kuua
mtu aliye mbali? Ni vipi mtu aliyekufa anaweza kuzaliwa upya, na anasema
kitendo cha kupungukiwa nguvu huitwa ‘‘kufwa’’ na kadhalika katika ‘‘The Bantu Philosophy’’ (uk-22) Temples anasema kuwa majibu ya
maswali yote matatu, ili uweze kuyajibu lazima uwe mshirika wa mambo yote hayo.
Katika riwaya hii suala la nguvu uhai linajitokeza mara nyingi kwani mwandishi
amewaonesha wahusika Bwana Myombekere na Bi Bugonoka wakimtegemea Mungu,
vilevile wakiamini Mungu ndiye mwanye uwezo mkubwa. Pia wakiwatumia waganga
katika kutatua shida zao mfano mwandishi anasema;
‘‘wewe
hutazaa mtoto maishani mwako mpaka kufa! Ijapo nikioa
Wanawake
wengi, nisipojaliwa na Mungu yote hayo ni majivuno
ya
bure’’
(uk-16)
Vilevile
suala hili limejitokeza pale msanii anaposema;
‘‘Myombekere
naye akanena, ‘‘hata mimi, tangu wazee wako
wakuchukue
, huwa natembea kwa watu kuwauliza kama hayo
lakini
nilipofika kwa mwingine, akaniambia hivi, sasa wewe bila
mke
wako nitawezaje kuwaganga? Utarudi siku nyingine na mke
wako
ndipo niwajaribie, kwa sababu aaguae ni maulana.’’
(uk-18)
Maelezo
hayo yanadhihirisha kuwa Waafrika wanaamini kuwa Mungu ndiye mwenye nguvu uhai
kubwa kuliko viumbe wengine. Pia mwandishi ameonesha kuwa Waafrika hawatumii
waganga katika kutatua matatizo yao
kwani uamini kuwa mganga ana nguvu uhai kubwa kudhihirisha hayo mwandishi
anasema;
‘‘Bugonoka hajahesabiwa kuwa mgumba na
mimi hapo niliwaambia
nyinyi mnajua waganga si vizuri zaidi
mngekwenda pamoja nae
,wapate
kumponya? (uk-17)
Vilevile
pale mwandishi anaposema;
‘‘......Kibuguma
akaingia ndani, akamtafutia dawa la kabila jingine
Iliyokuwa
haifanani na ile ya kwanza, akaitia katika kisonzochake
alafu
akamueleza hivi, ‘‘ dawa hii ni sawa na ile niliyoanza kukupa
lakini
hii kazi yake ni kutibu ihuzi (ugonjwa wa mchango) ambao
ndio
unaouwa watoto wako wakiwa bado tumboni mwako.........’’
(uk-159)
Haya
yanadhihirisha uwepo wa nguvu uhai katika riwaya hii ambapo pia suala hili
linadhihirika katika jamii kwani yapo matangazo mengi kuhusu waganga na huduma
wanazotoa kama vile kusafisha nyota, mvuto, kurudisha mpenzi na kutafuta au
kurudisha mali iliyopotea.
Falsafa
ya uduara, Temples anasema kuwa Waafrika hupenda vitu vya umbo la duara kama
vile ngoma, nyumba, sufuria, vyungu na sahani kwani uamini kuwa ni vitu vizuri.
Kipengele cha uduara kimejitokeza katika riwaya hii kwani mwandishi ameonesha
wahusika wakitumia vitu vya duara kama vile ungo, vyungu na mitungi. Mfano
mwandishi anasema;
‘‘
akachukua pembe la mizimu na ungo wake akatoka navyo nje’’
(uk-8)
Vilevile
mwandishi anaposema;
‘‘Basi
walipo kwisha kazi hiyo, ndipo Nkwanzi,akamtuma Barongo, leta kile kibuyu cha kuweka mafuta
na oleabya (chungu cha kuwekea mafuta) tumtilie mafuta (siagi) ili akifika aungie nyama hii waliyo mpa. (Uk 97)
Vilevile
katika kudhihirisha suala la uduara katika riwaya hii mwandishi anaonesha
majina ya watu, vitu pamoja na miezi inayoanza na herufi ‘o’ ambayo ni ya duara mfano anaposema;
‘‘mwezi
wa omwilaguzu (February) ulikuwa ni wa
saba tangu
Bugonoka
atunge mimba’’
(uk-273)
Pia
mwandishi anaonesha pale anaposema;
‘‘mwezi
wa saba (omwerogwechanda) au ikiralya bubezi (julai)’’
(uk-252)
Pia
mwandishi anaonesha tena suala ilo anasema;
‘‘mwenzi
wa tisa 9. Omutagato (Septemba) mambo yaonekanayo
Katika
mwezi huo ni haya’’
(uk-253)
Mambo
hayo yanadhihirisha falsafa ya uduara katika riwaya hii ambayo pia yanahalisika
katika jamii ya Wasukuma ambao hupenda kujenga nyumba zao katika umbo la duara.
Falsafa
ya hofu ya uhai na kifo, Temples anaamini kuwa Waafrika wanahofu juu ya uhai na
kifo kwa kudhihirisha hili unaweza kuangalia salamu zao na pia mtu anapopata na
ugonjwa huhofu kuwa hawezi kupona na kifo kinamsogelea.katika riwaya hii
kipengele hiki kimejitokeza pale mwandishi anaposema;
‘‘baada
ya siku kidogo Yule malkia wa wanawake kule kwake,
alipoona
nyama iliyowindwa na Mbwa wake kabla hawajawatuma
kwa
mfalme wa wanaume ipo karibu kupungua, bila kuona Mbwa
wake,
hapo akatoa tangazo la kuwaalika watu wake wote na
walipo
kutanika Bukimbo akawaambia hivi, sikilizeni wanawake
kumbe
ukarimo uko wa kujiua. Mimi niliona huruma sana nikatoa
mbwa
wangu, wakaenda kwa omukama mwenzangu, kwa sababu
mimi
nilidhani labda hao watarudishwa upesi, kumbe sivyo!
Tazameni
mpaka leo hii hawaonekani na hakuna hata mmoja
Atokaye
kule kuja kutuhakikishia kuwa mbwa walifika ama
Hapana.
Basi nilichowaita ninyi wake wenzangu ni hiki, ninaona
Kuwa
huyo adui njaa tumemjenga kweli msingi wake
na tena
Itakuwa
kweli kutuangamiza sote bila shaka tutakufa tuishe..’’
(uk-198)
Pia
kipengele hiki kinajitokeza pale mwandishi anaposema;
‘‘.............Baada
ya Gwaleba kuondoka, ndipo Bugonoka akaamwa
Mbia
mume wake hivi, mimi nilikuwa nimekwisha kuogopa niki
Dhani
leo tumepata hatia mbaya ya kifo cha mtu mjini mwetu
Mtoto wa watu huyu tumbaku ya chirangi umuuwie hapa
na Watu waje waseme sisi
tumemloga!Myombekere akajibu ndiyo
hata
mimi nimejisemea peke yangu moyoni, toba ya Rabii tumetumwa na nini kumpa kirangi cha tumbako
kali hivi kama akifia mjini mwangu humu itakuwa hatia yangu ya kulipizwa
kisasi.’’ (uk.175)
hoja
hiyo inadhihirisha uwepo wa hofu ya uhai na kifo. Kipengele hiki kinahalisika
katika jamii kwani tunaona kuwa yapo mabango mengi yenye kauli mbiu ya ukimwi
unaua jihadhari nao, vilevile katika jamii watu uamini kifo kinasababishwa na
uchawi.
Falsafa
ya maisha ya ndoa, katika falsafa hii
Temples anasema Waafrika wanaamini katika ndoa zao na ndoa hizo hudumishwa ili kupata watoto.
Uhai wa bindamu unaanzia kwenye mimba ambayo ni matokeo ya ndoa. Katika riwaya
hii mwandishi anamwonesha mhusika Bi Bugonoka akiangaika kutafuta mtoto ili
kudumisha ndoa yake na Bwana Myombekere. Vilevile mwandishi anaonesha maisha ya
upweke yaliyo na shida kwa kumtumia mhusika Myombekere wakati ambapo Bugonoka
alichukuliwa na wazazi wake, kudhihirisha hayo mwandishi anasema;
‘‘hapo
jamaa wa Myombekere wakaanza kuwaka kwa hasira na kupayuka wakamwambia amkatae
mke wake, wakisema wewe ni ndugu yetu, sasa unakubali kukaa na mke wako huyu
akiwa mgumba hivi uzuri wako wote huu huishie chini! Hivi wewe unadhani
kufufuka hapa duniani ni nini? Sii kuzaa na kuacha mbegu yako hapa duniani
ikiwa hai ndiyo maendeleo ya ukoo wetu.’’ (uk.1)
Falsafa
ya ubuntu; ‘Obuntu ni falsafa ya
Kiafrika inayo sisitiza mahususiano na ushirikiano wa jamii kama misingi ya
maisha bora na amani katika jamii. Neno Ubuntu
linatoka kwenye neno la Kizulu na Kixhosa na jamii nyingi za kiafika. Neno la kihaya Obuntu au kwakiswahili utu linabeba kwa
kiasi fulani maana yaneno utu. Falsafa ya Obuntu inatokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi yajamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi. Msingi wa
falsafa hii ni ‘mtu sii mtu bila watu’ kwa Kizulu ‘‘ Umuntu ngumutu ngabantu’’ kwa Kihaya
‘ ‘Omuntu ti muntu ka ataliho bantu’’. Katika riwaya hii swala la utu
limejitokeza sehemu kadha wakadha mfano pale ambapo Myombekere anapo amua
kwenda kwa wakwe zake kuomba radhi mwandishi anasema ;
‘‘
Basi Myombekere alipo maliza mjini
mwake siku kadha wakadha moyo wake ukazidi kumdunda sana na kumshauri
arudi kwa wakwe zake kuomba radhi.(Uk 40)
Kitendo
cha Myombekere kwenda kuomba radhi ni miongoni mwa matendo ya utu kwa waafrika.
Vilevile kipengele hiki kinajitokeza pale ambapo Myombekere anasaidiwa na watu
ku beba mitungi ya pombe kupeleka kwa wakwe zake. Mwandishi anasema
‘
‘Baada ya kuitoa ile mitungi ya pombe, wakajitwika vichwani. Kila mwanaume
alijitwika mtungi mmoja. Wale wanawake wawili walikwenda wakipokezana
kibuyu cha pombe kinachoitwa engunda
yobukanza bwa ninazara (kibuyu cha machicha cha mama mkwe).
Suala la kushirikiana ni miongoni mwa matendo
ya utu katika falsafa za Kiafrika. Kipengele hiki cha kifalsafa kinajitokeza
katika jamii za leo hasa jamii ya wasukuma ambayo hishirikiana katika mambo
mbalimbali ya kijamii na katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile
shughuli za kilimo. Vilevile ni wakarimu na hushirikiana na kutiana moyo
matatizo yanapotokea
Kuwepo
kwa vipengele hivi vya kifalsafa katika riwaya hii ambayo inaakisi jamii yaa
waakerebe inadhibitisha kuwa waAfrika wana falsafa yao. Na kupinga madai ya
wana magharibi ambao wanadai kuwa Afrika haina falsafa
MAREJELEO
Kitereza,
J. (1980). ‘‘Bwana Myombekere na Bi
Bugonoka’’. Dar es salaam: Tanzania Publishing House.
Mbiti,
J. (1990). African Religion and
Philosophy. New York: praeger Publisher.
Odera,
H.O. (1990). Trend in Contemporary
African Philosophy. Nairobi: Shirikon Publishers.
Sodipo,
J.O. (1993). Foundation of African
Philosophy. Ibadan: Ibadan University Press.
Temples, P. (1959).
‘‘ The Bantu Philosophy’’