Chato. Mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Mwekako kata ya Kasenga wilayani Chato mkoani Geita imesababisha vifo vya watoto wawili na kuharibu mali.
Diwani wa kata ya Kasenga wilayani hapa Damian Vilarie amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema mbali na vifo pia mvua imesababisha uharibufu wa miundombinu ya barabara.
Alisema mvua hiyo iliyonyesha kwa masaa matatu jana januar 11 ilisababisha mafuriko yaliyowasomba watoto wawili wa mzee Kurwa waliotoka soko la Igalula kununua bidhaa za nyumbani.
Alisema watoto hao wa mzee Kurwa mmoja anakadiriwa kuwa na miaka 13 na mdogo miaka mawili.
Alisema pia mvua hiyo imebomoa boma la zahanati lenye vyumba 17 ambalo bado lilikua linajengwa.
Alisema kwa sasa uongozi wa kata unapita kwa wananchi kuangalia madhara yaliyojitoleza na kufanya tathmini.