Timu ya soka ya Singida United imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya mapinduzi Cup inayoendelea huko Unguja Visiwani Zanzibar, baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mlandege FC.
Singida United ambao sasa wanafikisha alama 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu waliyocheza hadi hivi, wamefunga mabao yao matatu kupitia kwa Danny Usengimana ambaye amefunga kwa njia ya penati katika dakika ya 29.
Ilikuwa kama haitoshi Singida United ambao walikuwa wakicheza soka la kushambulia muda wote walipata bao la pili katika dakika ya 37 kupitia shuti kali la guu la kulia la kiungo wa kati Kenny Ally Mwambungu.
Bao la tatu la Singida United ambalo lilikamilisha ndoto yao ya kucheza nusu fainali limefungwa na Lubinda Mundia Mbia katika dakika ya 56 baada ya kufanya jitihada binafsi kuuwahi mpira ambao wengi walidhani kuwa mpira ulikuwa unaenda kutoka na kuuzamisha wavuni.
Bado mechi mbili.
Singida United wanafuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo inatazamiwa kumalizika siku ya Januari 13 wakiwa na michezo miwili mkononi dhidi ya Dar Young Africans Januari 8, na ule dhidi ya JKU Januari 6.