Raundi ya 12 ya ligi kuu soka Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2017/18 inatarajiwa kuanza Ijumaa ya Disemba 29, ambapo mabingwa mara moja wa taji hilo timu ya soka ya Azam FC watawakaribisha Stand United, katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuanza majira ya saa 1:00 jioni, taarifa kutoka katika klabu ya Azam imesema kuwa wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa mchezaji mmoja pekee Mbaraka Yusuph hivyo ni imani yao kuwa mwalimu atakuwa na uwanda mpana wa kupanga kikosi chache.
Akitoa taarifa hiyo Jaffary Idd Maganga ambaye ndiye msemaji wa klabu ya Azam amesema hawatawachukulia poa Stand United na wanachotaka wao ni kuingia kwenye mchezo huo na kupata ushindi ukizingatia mchezo wa mwisho wa ligi walitoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar.
-Ni mchezo mgumu na mchezo ambao unatumia akili nyingi ili kuweza kupata matokeo, niseme tu Mwalimu amepata muda mrefu wa kuiandaa timu, tupo tayari tupo vizuri, majeruhi ni Mbaraka pekee yake wengine wote wapo vizuri, kwa hiyo full squad itakuwepo uwanjani,” Maganga amesema.
Rekodi muhimu kuelekea mchezo huo ni kuwa Azam haijawahi kupoteza mchezo wowote katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Stand United, lakini katika mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu uliopita uliopigwa Kambarage Azam walichezea kichapo cha bao 1-0.
Michezo yao iliyopita.
17 Januari 2015 Stand United 0-1 Azam FC
25 April 2015 Azam FC 4-0 Stand United
16 Septemba 2015 Stand United 0-2 Azam FC
16 Machi 2016 Azam FC 1-0 Stand United
12 Oktoba 2016 Stand United 1-0 Azam FC
04 Machi 2017 Azam 2-0 Stand United