Tuesday

USIYEMPENDA KAJA

0 comments
.com/proxy/

Beki wa kati wa Simba, Salum Mbonde amerejea uwanjani baada ya kupona majeruhi yake ya goti aliyoyapata muda mrefu katika mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya kuelezwa kuwa Klabu ya Simba imeachana na beki wake mwingine wa kati, Method Mwanjali.
Mbonde ambaye ni beki wa zamani wa Mtibwa Sugar ameeleza kuwa  ushindani uliopo ni mkubwa na ndiyo maana ameamua kwenda kufanya mazoezi ya ziada gym, ili kuongeza nguvu zitakazomwezesha kumudu mapambano na ushindani wa namba uliopo kwenye timu yake.
"Nashukuru nimepona na sasa nipo fiti natarajia kurudi uwanjani wakati ligi itakapoendelea lakini nalazimika kufanya mazoezi ya nguvu ili kujiweka fiti kwa ajili ya kumudu ushindani uliopo,"  amesema Mbonde.
Beki huyo amesema amejipanga kufanya mazoezi hayo kwa wiki nzima ili hadi ligi itakapoanza aweze kuwa fiti na kuendelea na kazi yake ya kulinda lango la Simba ambayo imepania kutwaa ubingwa wa Tanzania bara msimu huu.
Kurejea kwa Mbonde kunapunguza idadi ya majeruhi wa timu hiyo ukiachana na beki Shomari Kapombe na kipa Said Mohamed wanaoendelea na matibabu mpaka sasa.