Thursday

MILA NA DESTURI ZA WANGONI:- Upande wa ndoa na kuchumbia

0 comments


Kwanza uchumba halafu harusi/ndoa.
Katika mila za wangoni, hapo zamani kijana na msichana wakikua kufikia umri wa kuoa walioa. Kwa mila za wangoni, mtoto wa kiume hata kama akikua na kuoa halafu hajaenda vitani ilikuwa haionyeshi maana. Wakati wa kupigana vita kijana ilibidi aonyeshe nguvu zake zilivyo. Kijana ambaye bado hajaenda vitani aliitwa (walimwita) ”lijaha” ikiwa na maana ya kijana/mvulana mdogo. Kijana ambaye ametoka vitani walimwita/aliitwa ”lidoda” ikiwa na maana mkubwa . Mke wa kuoa walimtafuta ambaye ni mwenye ukamilifu, anayejua kufanya kazi za nyumbani. Anatafutwa mwanamke anayeweza kuokota kuni, kuchota maji, kutwanga, kupika chakula, kupika pombe na awe mwanamke anayecheka vizuri na watu wote katika mji.

Ndoa haifungwi katika ukoo. Kwa wangoni hawaoi mke au kuolewa na mume mwenye (kibongo) ubini mmoja. Kama watu wakioana katika ukoo, basi wazee wataulizia kwanza kama ukoo huo ni wa karibu au wa mbali. Kama hawa watu walioana katika ukoo wa karibu, basi watawaapizia. Watu wnaogopa kuoana ndani ya ukoo kwasababu wakifanya hivyo watoto watakaozaliwa watakufa. Na pengine watoto hao watapata kifafa au pengine mababu (mahoka) watakasirika.

Mtenga:-
Kwa kingoni cha zamani mtenga ni mtu anayenunua au kuuza kitu. Mtenga anamuuza mototo wa kike. Yeye ndiye atoaye ”Chiyagabuli” yaani mali ya mwanzo na ”Mawolowolo” ikiwa na maana mali yote kwa wenye mtoto wa kike.

Kulonda mdala=Kutafuta mke:-
Wenye mtoto wa kiume wanapotaka kumwoza kijana wao , wazazi wengine walimtafutia mke. Wazazi wengine walimwacha kijana wao atafute mwenyewe mke. amtakaye. Kama walimwona msichana mrembo watamtafuta ndugu yao ambaye watamtaka na kumwelezea habari za ndoa. Na huyu ndiye atakayekuwa MTENGA wao. Mtenga huyu ataanza kuulizia kwa siri mambo ya wazazi wa msichana yule na wanaukoo wake wote na halafu ataenda kuwaeleza wazazi wa kijana. Kama wazazi wataona ya kuwa ni msichana wa hodari, watenga wale wataenda kwa wazazi wa msichana na kuuliza kama wanaruhusiwa kumwoa? Kama wenye binti watakataa, watenga wataombeleza.

Kujitokeza:- Ni lazima wawe na kiulizio , watenga ndio wataenda kuulizia kumwoa mke. Wanapoenda kule , wanachukua kitu fulani ”lukotelu au luhongelu” ni kiulizio , kitu hicho chaweza kuwa nguo, ushanga au hela nk.

Chiyagabuli= Mahari ya mwanzo
Kama wakwe wa pande zote mbili wanakubaliana watoto wao waoane, watenga watapeleka mahari kidogo kwa mama na baba wa binti ambayo ni mahari ya mwanzo. Baada ya muda yatapelekwa tena mahari ya mwanzo yaani kwa mara ya pili itakuwa jembe moja LUSUKA. Kama aina fulani ya jembe "ngwamba" ni jembe lenye tundu pale pmini unapotumbukizwa. Hii itamaanisha binti yao tayari amekwisha poteza ubikira

Kuchicha= kumtembela mchumba
Kuchicha ni kitendo cha msichana aliyechumbiwa kwenda rasmi kumtembelea mchumbake, kimila huyo msichana aliyechumbiwa anaenda na rafiki yake wa kike. Hivyo basi siku hiyo inakuwa ni kama anaenda kuona mazingira atakayokuja kuishi. Kimsingi katika siku ya kuchicha hairuhusiwi kulala pamoja na kufanya mapenzi ndio maana msichana alipaswa kusindikizwa na msichana mwenzake. Lakini basi mara nyingi imekuwa ngumu kujizuia wengi wamekuwa wakiishia kufanya mapenzi, mbaya zaidi unakuta mvulana anaalika na mvulana mwenzake halafu wanagawana hao wasichana waliofika hapo. Lakini pia hilo neno limekuwa likitumika isivyo rasmi kama vile kitendo cha msichana kutongozwa na mvulana wapo walioita kitendo hicho kuchicha na imezoeleka na wengi.

Au pia inakuwa kinyume:- Kijana wa kiume pamoja na vijana wenzake wanaenda rasmi kumtembea mchumba/msichana. Huko anafanya kazi nyingine nyingi. Kwa kufanya hivyo, wakwe watamwona ni kijana /mume wa uhakika, kuwa anaweza kufanya kazi za kianaume, kama anajua/weza kulima kukata matema(kukata miti shambani kwa ajili ya kuandaa shamba), kama ana kaa/ishi vizuri na watu au kama hana haraka ya kula. Muda wote huo wa aliokuwepo, kijana huyu hajionyeshi kwa wakwe zake. Anapotaka kutoka nje ya nyumba alalayo ni lazima ajifunike nguo usoni gubigubi. Kijana atafanya hivyo atakapotaka kumwona mtarajiwa mkewe, hakuna kujionyesha kwa wakwewe mpaka atakapozaa mtoto. Na mwanamke atafanya hivyo kwa wazazi wa mumewe.

Nimefanya utafiti katika kuon au kulipa mahari inaweza kuwa kama ifuatavyoMbuzi 1 dume
Mbuzi 5 dume 1 , majike 4
Sufuria kubwa 1
Mablanket 2
Nguo- kanga doti 2
Nguo vitenge doti 2
Nguo shuka 2
majembe 2
Asante kwakusoma masshele blog ikiwa unahistoria yoyote tuwasiliane katika +255766605392
Itachapishwa hapa